Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1474 | 1475 | (Page 1476) | 1477 | 1478 | .... | 1896 | newer

  0 0


  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akisaini cha wageni kata ya Songea alipokuwa na mkutano wa hadhara na wananchi wakati wa ziara yake
  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akimwaga mchanga kwa ajili ya mradi huo


  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua mradi huo wa maji
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimuagiza Mkandarasi wa Maji mbele ya Wananchi wa Tunduma kuhakikisha mradi wa maji unakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma za maji .  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema hatasita kumchukulia hatua mkandarasi yoyote ambaye atashindwa kukamilisha kwa wakati miradi ya maji waliopewa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kuwasimamisha.

  Lakini pia ametoa wito pia wakandarasi wa magengeni kuacha kutumiwa kwenye maeneo mbalimbali kwani wamekuwa ndio chanzo cha kupelekea miradi mingi kushindwa kukamilika kwa wakati hali inayosababisha adha kubwa kwa wananchi.

  Aliyasema hayo baada ya kukagua mradi wa maji wa eneo Songea katika mji mdogo wa Tundyma wilaya ya Momba mkoani Songwe ambao unatekelezwa na Mkandarasi wa Kampuni ya Best One Company ambapo aliwataka kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa waledi mkubwa ili uweze kuwa chachu ya mafanikio kwa wananchi hao.Katika mradi huo Serikali imetolea fedha bilioni moja kwa ajili ya mradi huo ambapo Naibu Waziri huyo alizitaka zitumike kwa uangalifu mkubwa ili kuweza kuukamilisha kwa lengo la kuondoa kero kwa wananchi .

  Hata hivyo alisema iwapo mradi huo utashindwa kukamilika kwa wakati hawasita kumchukulia hatua ikiwamo kumsimamisha kazi kwani hawako tayari kuona uzembe unafanyika wakati wananchi wana uhitaji mkubwa wa huduma hiyo.“Labda niwaambie kwamba sisi kama serikali nia yetu kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi kwenye maeneo yao lakini niwaambie kuwa pia hatutamvumilia Mkandarasi yoyote ambaye akishindwa kukamilisha mradi huo kwa wakati hasa huyo ambaye anatekeleza eneo hili “Alisema Naibu Waziri Aweso.

  Naye kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Momba,Juma Irando ameitaka idara ya maji wilayani humo kutowapa tenda wakandarasi wanaotuhumiwa kukwamisha juhudi za serikali za kukabiliana na tatizo la maji kuhakikisha linakwisha.Hata hivyo alisema inadaiwa kuwa baadhi ya miradi ya maji wilayani humo inashindwa kukamilika kwa wakati kutokana na uwezo mdogo kitaalamu walionao baadhi ya wakandarasi ambao wanakabidhi miradi (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0  0 0

  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipewa maelezo ya ujenzi wa maabara katika kituo cha afya Nkowe na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ruangwa, Waziri Mkuu yupo Wilayani Ruangwa kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka ambapo aliamua kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake. Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa na mganga mkuu wa kituo cha afya Nkowe Dk. Paul Mbinga,wakati akikagua ujenzi wa nyumba ya daktari, Waziri Mkuu yupo Wilayani Ruangwa kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka ambapo aliamua kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake. Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Nkowe,baada ya kutembelea na kukagua kituo cha afya Nkowe Wilayani Ruangwa,. Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea wanachama wapya 60 wa Kata ya Nkowe Wilayani Ruangwa, kutoka Chama cha Wananchi (CUF) ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM). Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Sister Nelly Membe wa Shirika la Bikira Maria Msaada wa Wakristu la Ndanda,katika Kata ya Nkowe Wilayani Ruangwa, Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Sister Mfurahishi Choaji wa Shirika la Bikira Maria Msaada wa Wakristu la Ndanda,katika Kata ya Nkowe Wilayani Ruangwa, Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akifungua Tawi la vijana wakereketwa wa CCM la Majaliwa Camp,katika Kata ya Nkowe Wilayani Ruangwa, Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na waumini wengine wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay wakishiriki Ibada ya jumapili ya Familia Takatifu katika Kanisa hilo la jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru mara baada ya kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya Jumapili ya Familia Takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitakiana Heri na Masista walioshiriki katika Ibada ya jumapili ya Familia Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Fr. Asis Mendokta mara baada ya Ibada ya jumapili ya Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada ya jumapili ya Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

  0 0

   Msafara wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa ukitoka Korogwe mjini kuelekea Kata ya Kwagunda Jimbo la Korogwe Vijijini kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni za udiwani wa Kata hiyo ambapo Dkt Mndolwa alikuwa mgeni ramsi  gari yaa mbele inayongoza msafara huo ni ya Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu
   Msafara wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa ukiwasili eneo la Kijiji cha Mkokola Kata ya Kwagunda ambapo kulifanyika uzinduzi wa kampeni za udiwani wa kata hiyo baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo kufariki dunia
   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mkokola Kata ya Kwagunda mara baada ya kuwasili kuzindua kampeni za udiwani kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Korogwe Vijijini
   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akisaliana na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni hizo mara baada ya kuwasili kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi

   Meza kuu katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akiangalia vikundi vilivyokuwa vikitoa burudani wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Korogwe Mjini,Charles Emanuel na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu na MNEC na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa
   Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu na MNEC na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa akiangalia taarifa mbalimbali kabla ya kuanza kwa uzinduzi wa kampeni hizo
   Sehemu ya wana CCM na wananchi wa Kijiji cha Mkokola wakifuatilia uzinduzi huo aliyevaa shati katika ni Diwani wa Kata ya Majengo(CCM) Mustapha
   Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu na MNEC na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa kushoto akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa wakati wa uzinduzi huo katika ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Korogwe mjini,Charles Emanuel
   Vikundi vya burudani vikiendelea kutoa burudaani wakati wa uzinduzi huo
   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa mbele akiwa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini na MNEC na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu wakitunza kikundi cha maigizo wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi
  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini na MNEC na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu wakitunza kikundi cha maigizo wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo
   Katibu wa CCM Korogwe mjini,Ally Issa akitunza kikundi cha maigizo katika uizunduzi huo
   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa wa tatu kutoka kushoto akifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi huo wa pili ni Mwenyekiti wa CCM Korogwe mjini,Emanuel Charles na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu
   Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi kushoto akicheza wimbo na Msanii Dkt Njau wakati wa uzunduzi wa kampeni hizo
   Msanii wa Singeli akitumbuiza katika kampeni hizo
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akizugumza katika uzinduzi wa kampeni hizo ambapo aliwataka wananchi aliwataka kumchangua mgombea wa CCM kwani anafahamu changamoto zao na hivyo itakuwa rahisi kuweza kuzipatia ufumbuzi
  Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo akiwataka wananchi kumpa kura za kishindo mgombea wa CCM kama walivyofanya kwenye chaguzi zilizopita ili waweze kushirikiana na viongozi wengine kuwapa maendeleo

  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu (MNEC) na Mjumbe wa baraza Kuu la wazazi Taifa  akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hizo ambapo aliwataka wananchi kumuunga mkono mgombea wa CCM kwa kumpa kura za kishindo
   Mwenyekiti wa CCM Korogwe mjini,Emanuel Charles akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo
   Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akiinguruma katika kampeni hizo ambapo aliwataka wananchi kumchangua mgombe wa CCM ili waweze kushirikiana nae kuwapa maendeleo
   Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akiinguruma katika kampeni hizo ambapo aliwataka wananchi kumchangua mgombe wa CCM ili waweze kushirikiana nae kuwapa maendeleo
   Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akiinguruma katika kampeni hizo ambapo aliwataka wananchi kumchangua mgombe wa CCM ili waweze kushirikiana nae kuwapa maendeleo
   Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu (MNEC) na Mjumbe wa baraza Kuu la wazazi Taifa kushoto akimnada mgombea udiwani kata ya Kwagunda
   Diwani wa Kata ya Majengo (CCM) Mustapha akiwasalimia wananchi katika uzinduzi huo
   Msanii Dkt Njau akisailimia wananchi
   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akimnadi Mgombea udiwani wa Kata ya Kwagunda Saidi Shenkawa wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa kulia akiwa na Katibu wa CCM mkoa wa Tanga,Allan Kingazi kushoto wakiondoka eneo la mkutano mara baada ya kumalizika(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  Watalii wakiwasili uwanja mdogo wa ndege wa Seronera wilayani Serengeti mkoa wa Mara uliopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti(Senapa) kwaajili ya kutembelea vivutio vya kitalii wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka.
  Watalii wakiwasili uwanja mdogo wa ndege wa Seronera wilayani Serengeti mkoa wa Mara ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,kukamilika kwa jengo la wageni wanaowasili na wanaondoka kumerahisisha huduma za usafiri ndani ya hifadhi hiyo.
  Afisa Utalii Mwandamizi wa Hifadhi ya Taifa Serengeti mkoa
  wa Mara,Susuma Kusekwa akizungumza na watalii waliotembelea hifadhi hiyo.
  Watalii wakimsikiliza Zacharia Mathayo ambaye ni mwongoza watalii wakati akitoa maelezo kuhusu uhamaji wa wanayamapori aina ya Nyumbu kutoka Kaskazini mwa Hifadhi ya Taifa Serengeti hadi Kusini.
  Watalii hufurahia kuona wanyama wakubwa wakiwemo Tembo na wengine wanaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti.
  Tembo ni mojawapo ya kivutio kikubwa kwa watalii wanaotembelea hifadhi hiyo.
  Wanyama wadogo aina ya Pimbi ni sehemu ya vivutio utakavyokutana navyo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
  Wanyama wadogo aina ya Pimbi ni sehemu ya vivutio utakavyokutana navyo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imefanikiwa kutangaza vivutio vyake kikamilifu sio kwa watalii wanaotoka mataifa ya Ulaya,Asia na Amerika pekee bali pia watalii wa ndani ni sehemu ya wageni wanaotembelea hifadhi hiyo.
  Makundi makubwa ya Simba kama hili utayaona ndani ya hifadhi hiyo.

  Serengeti.Idadi ya watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa
  ya Serengeti(Senapa) imeongezeka katika siku za hivi karibuni kutokana na sekta ya utalii kukua huku miundombinu ya barabara na viwanja vidogo vya ndege vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo kufanya kazi vizuri.

  Afisa Utalii wa Senapa,Evance Magomba alisema kuwa
  baada ya kujengwa jengo dogo la wageni wanaowasili na wanaoondoka katika uwanja mdogo wa ndege wa Seronera idadi ya wageni imeongezeka huku wakala wa makampuni ya ndege wakiweka wawakilishi wao katika uwanja huo.

  Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa katika kipindi cha
  Januari hadi Septemba mwaka huu kumekua na safari za ndege 3,724 katika uwanja  wa Seronera huku uwanja wa Lobo katika kipindi hicho ni safari 349 na uwanja wa Kogatende safari 564.

  Alisema ndani ya hifadhi hiyo kuna viwanja vidogo vya ndege saba kikiwemo cha Seronera ambacho ni kikubwa zaidi chenye uwezo wa kupokea ndege
  kubwa yenye uwezo wa kubeba abiria 60 ikiwemo ya shirika la Precision
  Air inayofanya kazi mara nne kwa wiki.

  “Miaka miwili iliyopita hatukua na jengo hili la abiria naamini pamoja na sababu nyingine limekua kishawishi  kwa wageni kuongezeka kwani linawawezesha kuwa na sehemu nzuri ya kupumzika kabla ya kuanza safari zao,”alisema Magomba

  Alisema kutokana na ukubwa wa hifadhi hiyo wanavyo viwanja vingine vilivyosambaa maeneo mbalimbali ili kutoa huduma kwa urahisi na
  kuwawezesha watalii kupata muda mzuri wa kutembelea vivutio zaidi.

  Magomba alivitaja viwanja vingine kuwa ni  ogatenda,Lobo,Ndutu,Kirawira ,Fort Ikoma na Lamai ambavyo hutumika kwa malengo ya kurahisisha kufika eneo husika na kulingana na watalii wanapenda kuona
  vivutio maalumu.

  “Hifadhi ya Serengeti ina uwezo wa kupokea wageni wa aina
  zote na zipo huduma za malazi zikiwemo hoteli saba,makambi ya kudumu sita na makambi ya muda zaidi 140 yaliyosambaa na kipekee tuwakaribishe wananchi kutembelea hifadhi zetu kwasababu zipo bei maalumu kwaajili yao,”alisema Magomba

  Dereva wa kampuni ya kitalii ya Micato Safaris,Emmanuel Lema alisema huduma za kitaalii nchi zimekua kwa kasi baada ya serikali kupitia Bodi ya Utalii(TTB),shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) na wadau wengine wa utalii kutangaza kwa kiwango kikubwa sekta ya utalii.

  Alishauri Tanapa kuongeza ukubwa wa jengo la wanaowasili
  na kuondoka na huduma zingine muhimu ili kuwawezesha watumiaji wa jengo hilo kupata huduma za kiwango cha juu hasa wakati wa msimu wa utalii.

  Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

  0 0  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) amekabidhi hundi ya shilingi Milioni 6.8 ( 6,830,000/=) kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi katika zahanati ya kijiji cha Solwa kilichopo kata ya Solwa jimbo la Solwa mkoani Shinyanga.
  Akizungumza leo Jumamosi Desemba 30,2017 wakati wa kukabidhi hundi hiyo kwa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo,Mheshimiwa Azza alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa alipotembelea zanahati hiyo mwezi Mei mwaka huu na kukuta changamoto ya uhaba wa vyumba vya kutolea huduma za afya ikiwemo wodi ya watoto na akina mama.
  “Nilifanya ziara katika zanahati hii mwezi Mei mwaka huu wakati natoa vitanda vya kujifungulia na viti vya wagonjwa,baada ya kuingia katika chumba cha akina mama nilikuta vitanda vitatu,niliguswa na jinsi akina mama walivyokuwa wanahangaika,lakini nikaambiwa wananchi wana mpango wa kujenga wodi ya watoto na akina mama,nikaahidi kuchangia mabati 20 pindi majengo yatakapofikia hatua ya upauaji”,alieleza mbunge huyo.
  “Mwezi Septemba mwaka huu,Diwani wa kata ya Solwa alinitumia picha za majengo mawili yakiwa tayari kwa upauaji,nikawaza kuhusu mabati yangu 20,nikaona hayatoshi,ndipo nikaamua kuanza kutafuta watu wa kunisaidia,juzi nikapokea ujumbe kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF kuwa wamekubali ombi langu na wameamua kutoa shilingi 6,830,000/= kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo moja”,alieleza mheshimiwa Azza Hilal Hamad.
  Alisema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kununua mabati na mbao pamoja shughuli zingine katika kukamilisha ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa iliyojengwa kwa michango ya wananchi wa kijiji cha Solwa.
  “Niwapongeze sana watu wa Solwa kwa kuamua kuchangishana na kuanza ujenzi,Solwa itajengwa na Wana Solwa,hili ni jibu tosha kabisa kwamba kila kilio kina mwenyewe,mlichokifanya kinapaswa kuigwa katika maeneo mengine,niwashukuru sana pia NSSF kwa kunishika mkono ili kuokoa maisha ya akina mama na watoto”,aliongeza Azza Hilal Hamad.
  Hata hivyo aliwataka wananchi wa Solwa kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili iwe na manufaa kwa wananchi.
  Mbunge huyo alitumia fursa hiyo pia kuwakumbusha wazazi na walezi kupeleka watoto shule badala ya kuwaozesha wangali wadogo kwa tamaa ya mali huku akisisitiza kuwa urithi mzuri kwa mtoto ni elimu pekee.
  “Ni marufuku kuozesha watoto wa kike wanafunzi,matokeo ya darasa saba yametoka,wote waliofaulu wapelekwe shule,waliofeli nao watafutieni kazi zingine za kufanya siyo kuwaozesha,kufeli shule siyo kufeli maisha”,aliongeza.
  Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji Solwa,George Bushiya alisema baada ya wananchi kukerwa na adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya walikubaliana kuchangishana fedha ili kujenga majengo ya wodi ya watoto na akina mama ambapo zaidi ya shilingi milioni 36 zimetumika mpaka sasa.
  Naye Diwani wa kata ya Solwa Awadhi Mbaraka (CCM) alimshukuru mbunge huyo kwa misaada mbalimbali ambayo amekuwa akiitoa katika kata hiyo ikiwemo vitanda vya kujifungulia kwa akina mama na ujenzi wa jengo la zahanati ya Solwa.
  “Huyu mbunge amekuwa nasi tangu mwanzo kabisa tunaanza ujenzi huu,ametuletea vitanda,viti vya wagonjwa,pia amemsaidia mtoto Salawa Mihangwa (03) aliyekuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo,sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji jijini Dar es salaam,na leo katuletea pesa kumalizia ujenzi wa wodi,mungu akubariki sana ndugu yetu Azza”,aliongeza Mbaraka.
  Kaimu Mganga Mkuu wa halmashauri ya Shinyanga,Dk. Salim Matondo alimshukuru mbunge huyo kwa kusaidia ujenzi wa wodi ya akina mama ambapo pindi ujenzi utakapokamilika itasaidia kupunguza adha ya akina mama kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya katika hospitali ya Nindo na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga. 
  Baada ya Mheshimiwa Azza Hilal Hamad kukabidhi hundi ya shilingi milioni 6.8,wananchi waliohudhuria kikao hicho kifupi waliamua kutoa michango ya papo kwa papo kumuunga mkono mbunge wao ambapo zaidi ya shilingi Milioni 3 zilipatikana huku ahadi ya mifuko ya saruji,tripu za mchanga na moram nayo ikitolewa ili kuhakikisha ujenzi wa wodi hizo mbili unakamilika haraka iwezekavyo.
  ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
  Muonekano wa majengo mawili yaliyojengwa na wananchi wa kijiji cha Solwa yatakayotumika kama wodi ya watoto na akina mama katika zahanati ya Solwa iliyopo katika kijiji cha Solwa,kata ya Solwa,jimbo la Solwa mkoani Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Muonekano wa majengo hayo mpaka leo Jumamosi Desemba 30,2017
  Muonekano wa majengo hayo mawili
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa kukabidhi hundi ya shilingi Milioni 6.8 ( 6,830,000/=) kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi katika zahanati ya kijiji cha Solwa kilichopo kata ya Solwa jimbo la Solwa mkoani Shinyanga.
  Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akielezea kuhusu namna alivyopata shilingi 6,830,000/= kutoka mfuko wa hifadhi ya Jamii NSSF kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa
  Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa ameshikilia hundi ya shilingi Milioni 6.8 kabla ya kuikabidhi wa wajumbe wa kamati ya ujenzi wa majengo ya zanahati ya Solwa
  Hundi iliyokabidhiwa
  Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi hundi ya shilingi 6,830,000/= kwa wajumbe wa kamati ya ujenzi.Kulia ni mwenyekiti wa kamati hiyo Mussa Shibina.
  Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi hundi ya shilingi 6,830,000/= kwa wajumbe wa kamati ya ujenzi
  Mheshimiwa Azza Hilal Hamad na viongozi mbalimbali wa kijiji na kata ya Solwa wakiingia katika jengo la wodi ya akina mama ambalo ndiyo pesa iliyotolewa itatumika kukamilisha ujenzi( kuweka mbao na mabati)
  Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa ndani ya jengo la wodi ya akina mama
  Kulia ni Muuguzi msaidizi katika zahanati ya Solwa,Dk.  Mehrab Nyato akitoa maelezo kwa mbunge Azza Hilal kuhusu vyumba katika jengo hilo
  Mheshimiwa Azza Hilal akisikiliza maelezo kutoka  Dk.  Mehrab Nyato
  Mheshimiwa Azza Hilal akiuliza jambo 
  Mheshimiwa Azza akiendelea kutembelea majengo hayo
  Diwani wa kata ya Solwa Awadh Mbaraka akizungumza wakati wa kikao cha makabidhiano ya hundi
  Mwenyekiti wa CCM kata ya Solwa Leonard Malando akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema kazi anazofanya mbunge Azza Hilal zinasaidia kupunguza maswali ya kwamba viongozi wa CCM wanafanya nini katika kata hiyo
  Kaimu Mganga Mkuu wa halmashauri ya Shinyanga,Dk. Salim Matondo akizungumza katika kikao hicho
  Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi Mussa Shibina akizungumza katika kikao hicho
  Afisa Mtendaji wa kijiji Solwa,George Bushiya akizungumza katika kikao hicho
  Mzee Mwinamila Kibiongo akiimba shairi la kupongeza kazi za Mheshimiwa Azza Hilal
  Mbunge Azza Hilal akicheza muziki na mmoja wa wananchi wa kijiji cha Solwa ambaye alioma awekewe wimbo wa Mama Ushauri unaomhusu Mbunge Azza Hilal
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akimsalimia mama aliyejifungua mtoto wa kike mara baada tu ya mbunge kufika katika zanahati hiyo.Mama huyo alikuwa amepewa rufaa ya kwenda kujifungulia katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga,lakini kutokana na Kaimu Mganga Mkuu wa halmashauri ya Shinyanga,Dk. Salim Matondo kuhudhurika kikao cha mbunge,ndiyo ikawa fursa nzuri kwa mama huyo kupewa huduma na Daktari huyo
  Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa amembeba mtoto aliyepewa jina la "Azza"
  Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akifurahia jambo baada ya kumpatia zawadi ya vitenge mama aliyejifungua mtoto wa kike katika zahanati ya Solwa.
  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akimsajili mmoja wa Wananchi wa Kata ya Kahama Mjini aliyejitokeza kusajiliwa wakati zoezi la usajili likiendelea kwenye Kata hiyo.
  Mkusanyiko wa wananchi wa Kata ya mjini Wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakisubiri huduma ya usajili Vitambulisho vya Taifa, zoezi linaloendelea katika Wilaya hiyo na kuhusisha Kata ya Mjini na mitaa yake.

  Mkusanyiko wa wananchi wa Kata ya mjini Wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakisubiri huduma ya usajili Vitambulisho vya Taifa, zoezi linaloendelea katika Wilaya hiyo na kuhusisha Kata ya Mjini na mitaa yake.  Mmoja wa wananchi wa Kahama akisajiliwa na kujaziwa fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa na Mtendaji wa Mtaa wa Kahama kabla ya kusajiliwa.

  ……………………………………………………………………………….

  Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa 16 ya Tanzania ambayo zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa linaendelea huku mamia ya wananchi wakionekana kuhamasika na zoezi hilo kwa kujitokeza kwa wingi kwenye vituo ambavyo usajili umekuwa ukiendelea.

  Akizungumzia zoezi hilo Afisa Usajili wa Wilaya ya Kahama bwana Ibrahim amesema mwitikio mkubwa wa watu katika vituo vya usajili ni kiashiria kwamba uelewa wa wananchi ni mkubwa na kwamba wanatambua vitakavyowasaidia katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

  Akizungumzia gharama za zoezi afisa huyo ameeleza zoezi ni BURE na kwamba mwananchi hapaswi kutozwa kiasi chochote cha fedha zaidi ya kufika na nakala (photocopy) za nyaraka/viambatanisho muhimu vya kuweza kumtambulisha uraia wake, umri na makazi. Mfano wa nyaraka hizo ni; Kadi ya mpiga kura, cheti cha kuzaliwa, leseni ya udereva, ID ya Mzanzibar mkazi, TIN, Pasi ya kusafiria, vyeti vya elimu nk.

  Mbali na Shinyanya mikoa mingine ambayo NIDA inaendesha zoezi ni Iringa, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Songwe, Njombe, Singida, Manyara, Mwanza, Simiyu, Mara, Geita, Lindi, Mtwara na Ruvuma.

  0 0

  Waziri wa mambo ya Ndani Mhe.Dkt Mwigulu  Nchemba akikagua baadhi ya Vitambulisho 3470 ambavyo watagawiwa wananchi wa Kata ya Songea ambao Usajili wao umekamilika kufuatia zoezi la Usajili Vitambulisho kuwa kufanyika katika Kata za karibu kabla ya kuanza Usajili wa Umma. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme na Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida Ndugu Andrew W. Massawe.

  Mhe Waziri akimkabidhi Kitambulisho chake mmoja wa wananchi wa Kata ya Songea Bwana Hassan Ally Shomari wakati wa zoezi la ugawaji Vitambulisho kwenye sherehe za uzinduzi wa zoezi la Usajili kwa mkoa wa Ruvuma. Jumla ya Vitambulisho 3470 viligawanywa kwa wanachi wakati wa sherehe hizo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt Mwigulu L.Nchemba akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Ndugu Andrew W. Massawe wakiwasili kwenye viwanja vya Lisaboni –Songea kushiriki sherehe za uzinduzi wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa mkoa wa Ruvuma.

  kikundi cha burudani za asili maarufu kama wana Lizombe wakitumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa zoezi la Usajili kwa mkoa wa Ruvuma.

  ……………………………………………………………………………………

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Ndg Andrew W. Massawe ameitaja mikoa ya Mara, Arusha, Iringa, Geita, Lindi, Simiyu, Mbeya na Songwe kuwa mikoa inayoongoza katika zoezi la kuwasajili wananchi kupata Vitambulisho vya Taifa; huku mikoa mingine ikiwa nyuma kiusajili kulinganisha na malengo waliyowekewa.

  Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa zoezi la usajili kwa mkoa wa Ruvuma lilofanyika katika viwanja vya Lisaboni-Songea, Ndugu Massawe amemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba kusaidia kuweka msukumo kwa viongozi na wananchi kwenye mikoa ambayo haifanyi vizuri ili iongeze kasi ya usajili kwa lengo la kukamilisha usajili kwenye mikoa yao kwa muda uliopangwa.

  Akihutubia wananchi wa Ruvuma waliofurika kwenye viwanja vya Lisaboni vilivyopo nje kidogo ya mji wa Songea, Waziri wa Mambo wa Ndani ya Nchi Mhe.Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amewasisitizia wananchi kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kwani kuwa na kitambulisho cha Taifa siyo suala la hiyari ni wajibu kwa kila Mtanzania mwenye sifa kuwa nacho.

  “ Mhe. Rais wetu ametoa hela za kuwasajili, zoezi ni bure bado kujisajiliwa kwenda kupigwa picha na kuchuliwa alama za vidole ikushinde?” aliuliza Waziri huyo mwenye dhamana kubwa katika kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo.

  Aidha amewataka viongozi wa Mikoa na wote wenye dhamana katika kusimamia zoezi hili kuhakikisha wanashirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika kuhakikisha wananchi wenye sifa wanasajiliwa na kamwe pasiwepo wageni watakaojipenyeza kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa kama raia.

  “Kwakuwa NIDA inatoa vitambulisho vya aina tatu, cha Raia, Mgeni na Mkimbizi basi niwaombe wageni badala ya kufanya udanganyifu wajisajili kwa hadhi yao kwani siyo dhamira ya Serikali kumfukuza yeyote lakini kuwatambua Raia wake kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani” alisema

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme amemhakikishia Mhe. Waziri mkoa wake uko tayari kusimamia na kuhakikisha wananchi wote wenye sifa wanasajiliwa na kupata Vitambulisho ndani ya muda uliopangwa na kwamba kamwe hata mvumilia mtu yeyote ambaye atakuwa kikwazo katika utekelezaji wa zoezi hilo kwa wananchi; akiwakemea wanasiasa kuingiza siasa kwenye zoezi la Usajili wananchi vitambulisho vya Taifa.

  Mkoa wa Ruvuma wenye Wilaya 5 unakisiwa utawasajili zaidi ya wananchi 900,000 katika zoezi lililopangwa kumalizika ndani ya miezi mitatu. Tayari NIDA imekamilisha usambazaji wa vifaa na kutoa mafunzo kwa maafisa ambao watatumika kuwasajili wananchi wa Ruvuma na viunga vyake.

  Mikoa mingine inayoendelea na Usajili kwa sasa ni Iringa, Mbeya, Njombe, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Songwe, Lindi na Mtwara.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mima.


  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amezitaka Ofisi za wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya nchini kuteua wauguzi kati ya wawili hadi wanne kwa kuwapeleka kwenye mafunzo maalum ya dawa za usingizi ili waweze kutoa huduma hiyo wakati wa upasuaji kwenye vituo vya afya.

  Waziri Jafo ametoa maelekezo hayo ya serikali leo alipokuwa anakagua uboreshaji wa kituo cha Afya Mima kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

  Amesema mafunzo hayo yawe ya muda mfupi na muda mrefu ili kujiweka tayari katika kuwahudumia wananchi ipasavyo kwenye huduma za upasuaji kutokana na serikali ya awamu ya tano kwasasa inaboresha vituo vya afya nchini kwa kuvijengea vyumba vya upasuaji na miundombinu mbalimbali.

  “Wakati tunaendelea kuboresha vituo vya afya hapa nchini niwatake wakurungezi wa halmashauri na waganga wakuu wa wilaya zote kuwawezesha wauguzi wenu katika fani za dawa za usingizi kwa kutumia chuo cha Muhimbili, KCMC, na vyuo vingine hapa nchini ili kazi hii ya ujenzi inapokamilika na vifaa vya upasuaji vitakapoweka ninyi muwe mmejiandaa na sio kubweteka mnasubiri kila jambo muelekezwe,”Amesema Jafo

  Ameongeza “Nataka mujiongeze kwani japo serikali tunaendelea kuajiri madaktari na wauguzi lakini nyinyi mnapaswa pia kujiongeza kwenye hili ili wananchi wetu waweze kupata huduma bora,”.

  Katika ziara yake wilayani Mpwapwa, Waziri Jafo amefanikiwa kukagua miradi mingine ya ujenzi ikiwemo barabara za lami zinazojengwa na Wakala wa barabara mijini na vijijini(Tarura) katika mji wa Mpwapwa na mradi wa maji wa kijiji cha Mima.

  0 0
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mh Godfrey Zambi alipokuwa akimueleza jambo wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Upandaji mikorosho Bora na mipya Million10 iliyofanyika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisikiliza Maelezo toka kwa Afisa Ubanguaji Toka Bodi ya Korosho Tanzania CBT Domina Mkangara wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Upandaji mikorosho Bora na mipya Million10 iliyofanyika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.


  0 0

   Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba Ndugu Nyakia Ally Chirukile akichangia damu baada ya kushiriki zoezi la Usafi wa kila jumamosi ya mwisho wa Mwezi,zoezi ambalo lilikwenda sambamba na upandaji wa miti zaidi ya 2000 pembezoni mwa barabara ya Dodoma -Babati kuanzia Kidoka mpaka  Kilema.

  Akizungumza baada ya shughuli nzima,Ndugu Nyakia aliwaomba wananchi wa wilaya ya Chemba na mkoa wa Dodoma kwa ujumla,kuunga mkono juhudi za Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassani katika suala zima la uhamasishaji wa kupanda miti na kuhakikisha mkoa huo unakuwa wa kijani .
  Baada ya kufanyika shughuli ya uchangiaji Damu,pia kulifanyika tukio la usafi na upandaji wa miti zaidi ya 2000 pembezoni mwa barabara ya Dodoma -Babati kuanzia Kidoka mpaka  Kilema,kuhakikisha mkoa wa Dodoma unakuwa wa kijani,kufuatia kampeni maalum ya upandaji miti iliozinduliwa hivi karibuni na Makamu wa Rais,Mama Samia Suluhu Hassan mkoani humo na kushirikisha viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Wadau wengine wa Mazingira.
    Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba Ndugu Nyakia Ally Chirukile akishiriki shughuli ya  upandaji wa miti zaidi ya 2000 pembezoni mwa barabara ya Dodoma -Babati kuanzia Kidoka mpaka  Kilema,baada ya zoezi hio Ndugu Nyakia pia alishiriki tukio la Usafi na uchangiaji wa Damu.

  0 0
  Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule (kushoto) akionyesha moya ya mashine ya kufulia iliyotolewa na Same Kaya Saccos kwa kituo cha afya cha Hedaru, Kilimanjaro.  
  Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule akiwa amenyanyua mikono mara baada ya kukata upete wa kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la SACCOS kata ya Hedaru, Kilimanjaro.


  Watoto yatima na wa mazingira magumu Hedaru wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Rosemary Senyamule mara baada ya kupatiwa zawadi ya madaftali.


  Mhe. Rosemary Senyamule akipanda mti wakati wa hafla hiyo.
  Mhe. Rosemary Senyamule akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Same Kaya Saccos.

  Same Kaya Saccos yashika nafasi ya pili Mkoa wa Kilimanjaro 2017 kwa kufanya vizuri katika nyanja zote. Hayo yamebainika mwishoni mwa wiki hii wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la SACCOS kata ya Hedaru ambalo ni tawi la 2 ukiacha ofisi ya makao makuu Same. A
   
  kizungumza wakati hafla hiyo fupi iliyofanyika Hedaru, Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Bw. Kisimbo alisema kuwa kwa sasa wametimiza miaka 15 na tayari wameshapata tuzo siku ya SACCOS dunia mwezi Oktoba 2017. 
   
  "Kwa muda ambao tumekuwa tukiwahudumia wanachama wetu tumeweza kupata mafanikio mengi likiwemo la kupata tuzo siku ya SACCOS duniani Mwezi Octoba, 2017," alisema Kisimbo. 
   
  Kwa upande wake Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule aliwapongeza kwa juhudi ambazo wamekuwa wakizifanya na pia aliwaomba kuendelea kuongeza wanachama wawe wengi zaidi. 
   
  Mhe. Rosemary Senyamule aliwaomba wanachama waendelee kuwa waaminifu kwa kulipa madeni yao kwa wakati, wananchi wengi kujiunga na SACCOS hiyo iliyoonyesha mfano mzuri wa kutunza fedha za wanachama wake.

  0 0

  Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akikagua fomu ya tamko la rasilimali na madeni iliyowasilishwa na mmoja wa viongozi wa umma katika ofisi za Sekretarieti hiyo Jijini Dar es Salaam leo. . Leo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo ambapo kila kiongozi aliyetajwa katika sheria husika analazimika kuwa amewasilisha fomu yake.(Picha na: Frank Shija -MAELEZO)
  Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akimuelekeza jambo mmoja wa viongozi wa umma aliyefika katika ofisi za Sekretarieti hiyo kwa ajili ya kuwasilisha fomu yake ya tamko la rasilimali na madeni leo Jijini Dar es Salaam. . Leo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo ambapo kila kiongozi aliyetajwa katika sheria husika analazimika kuwa amewasilisha fomu yake.
  Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akikagua fomu ya tamko la rasilimali na madeni iliyowasilishwa na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Omary Mkumba katika ofisi za Sekretarieti hiyo Jijini Dar es Salaam leo. . Leo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo ambapo kila kiongozi aliyetajwa katika sheria husika analazimika kuwa amewasilisha fomu yake.(Picha na: Frank Shija -MAELEZO)
  Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Omary Mkumba akisaini fomu yake ya tamko la rasilimali na madeni mara baada ya kuwasilisha na kukaguliwa na Afisa wa Sektretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Leo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo ambapo kila kiongozi aliyetajwa katika sheria husika analazimika kuwa amewasilisha fomu yake. (Picha na: Frank Shija -MAELEZO)

  0 0

  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiangalia Mche Mpya wa Korosho, wakati akikagua kitalu cha miche hiyo, katika kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Desemba 31, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipata ufafanuzi wa Miche Mipya ya Korosho kutoka kwa Afisa Ubanguaji Bodi ya Korosho Tanzania, Domina Mkangara, wakati akikagua kitalu cha miche hiyo, katika kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Desemba 31, 2017. 
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Hassan Jarufu, wakati akikagua kitalu cha miche mipya ya korosho, katika kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Desemba 31, 2017. Katikati ni Afisa Ubanguaji Bodi ya Korosho Domina Mkangara 
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ruangwa wakati wa kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipanda mche mpya wa korosho mara baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.
  aziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimwagilia maji mche mpya wa korosho aliyoupanda, baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimkabidhi mche mpya wa mkorosho Bi. Mwanahamisi Saidi, mkazi wa Kilimahewa, baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.Desemba 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  “Maafisa kilimo na maafisa ushirika mkisimamiwa na Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, mshirikiane na kusimamia kwa umakini upatikanaji wa takwimu za wakulima na maeneo yanayolimwa, haiwezekani kila mwaka takwimu ziwe ni zilezile tu,” alisema.

  “Afisa kilimo wa wilaya lazima ujue una wakulima wangapi, je hao wakulima wako, kila mmoja analima ekari ngapi? Na katika ekari hizo, ana miche mingapi, na je ana mahitaji ya pembejeo kiasi gani?” alisema.

  “Pia nilikwishawaagiza maafisa ushirika na viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) mpaka chama kikuu cha ushirika, kuwa kila mmoja anapaswa atambue ana wanachama wangapi katika chama chake. Hili litawezekana pia kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji wa Kata au Mwenyekiti wa Kijiji, kwa sababu wao wana idadi kamili za watu wanaowaongoza,” alisema.

  “Ninaamini tukifanya hilo tutamaliza tatizo la takwimu na Serikali itakuwa na uwezo mkubwa wa kuwahudumia wakulima wake, na tutaweza kuweka bajeti ya kutosha kuhudumia mahitaji yao,” alisisitiza.

  Waziri Mkuu alipanda mche mpya wa korosho ili kuanzisha zoezi la upandaji miche hiyo na kisha akagawa miche kwa wakulima 10 kutoka vijiji vya Likunja, Kitandi, Kilimahewa na Nachingwea ambao waliwawakilisha wenzao.

  Mapema, kabla ya kuzungumza na wananchi Waziri Mkuu alikagua vitalu vya miche ya mikorosho vilivyopandwa na Halmashauri ya Ruangwa na kuelezwa kuwa miche hiyo ipo ya aina mbili ambapo aina ya kwanza ni ile iliyotokana na mbegu na ya pili ni ile iliyotokana na vikonyo (grafting).

  Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka jimboni kwake.

  Sherehe hizo zilihudhuriwa na wakuu wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na wajumbe wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT). Wakuu wa Wilaya na wataalamu kutoka kituo cha utafiti cha Naliendele walishiriki zoezi hilo.

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiagana na Kiongozi Mkuu wa kimila kabila la Wasafa lililopo Mkoani Mbeya, Rocket Mwashinga mara baada ya mazungumzo mafupi walipokutana katika viwanja vya Magereza Mkoani Mbeya, leo Desemba 31, 2017. Kamishna Jenerali wa Magereza nchini yupo Jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambapo hadi jana amefanya ukaguzi katika Magereza ya Ruanda, Kyela, Tukuyu pamoja na Chuo cha Mafunzo ya Magereza, Kiwira kilichopo Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kimila Mkoani Mbeya(kushoto) ni Kiongozi Mkuu wa kimila kabila la Wasafa lililopo Mkoani Mbeya, Rocket Mwashinga(kulia) ni Kiongozi wa Pili wa Wasafa Mkoani Mbeya, George Joto mara baada ya mazungumzo mafupi na Kamishna Jenerali wa Magereza walipokutana katika viwanja vya Magereza Mkoani Mbeya, leo Desemba 31, 2017(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizingumza na wananchi wa kijiji cha Kiziko alipofanya ziara katika jimbo la Mkuranga.
  Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mkuranga, Juma Abeid akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kiziko juu ya mikakati ya Halmashauri katika uboreshaji wa sekta mbalimbali.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwasili katika kijiji cha cha Kitonga katika ziara ya vijiji jimbo la Mkuranga. 


  Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii.

  NAIBU waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mbunge) wa Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdalla Ulega ametoa agizo kwa Watendaji wa vijiji na Wenyeviti kuwasomea mapato na matumizi wananchi wao ili kuepuka kurudisha nyumba uchangiaji wa shughili za maendeleo.

  Naibu waziri huyo ametoa agizo hilo wilayani humo akiwa katika mwendelezo wa ziara za vijijini ambapo akiwa katika kijiji cha Kiziko, kilichopo Kata ya Mwarusembe baada ya kupokea malalamiko ya wananchi juu ya viongozi wao ngazi ya kijiji kushindwa kusoma taarifa ya mapato na matumizi.

  Alisema kushindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi kunachangia kwa asilimia kubwa wananchi kushindwa kuchangia maendeleo katika maeneo hayo hivyo lazima wananchi wajulishe kinachoingia na kinavyotumika.

  "Natoa agizo hili kwa watendaji na wenyeviti kusoma mapato na mapato na matumizi na hapa naagizi mtendaji wa Kata ya Mwarusembe kuhakikisha hadi kufika Januari 2 ,2018 niwe nimepata taarifa za kushindwa kusoma mapato na matumizi katika kijiji hiki cha kiziko. "alisema Ulega

  Alisema wananchi wanatamani kujitolea kwa lengo la kuchangia maendeleo lakni wanavunjwa moyo viongozi hao huku akisisitiza kupewa ifika January 2 awe amepata taarifa nakuhaidi kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu zaidi.

  Pia akiwa katika kijiji hicho cha alitoa mifuko 50 ya saruji pamoja na shilingi laki tano kwa ajili kuchangia ujenzi ya serikali ya kijiji hicho ikiwa pamoja na matundu ya vyoo katika shule ya msingi kiziko huku akitoa ahadi ya shilingi tisa. Kwa ajili ya kuchangia vikundi tisa vya Vikoba.

  Awali wakitoa kero zao kwa Mbunge huyo walisama wamakerwa sana na kukithiri kwa mifugo aina ya ng'ombe hali inayosababisha umasikini na njaa kwa wananchi hao kutokana na mazao yao.Pia walilalamikia kukosekana kwa barabara, inayounganisha kijiji hicho cha kiziko na vijiji vingine pamoja na Daraja linalounganisha vitongoji vya Gwanzo, Chakande vyenye wakazi wengi zaidi.

  "kwakweli tuna kero nyingi mno hapa kijijini kwetu kwani mbali na barabara na Daraja lakini pia tunakero ya kukosa Daktari kwenye Zahanati hii yetu hali inayosababisha wananchi kukosa kupatiwa huduma stahiki. "alisisitiza Mojamed Ally mjumbe wa serikali ya kijiji.

  Naye Ofisa Kilimo wa Kijiji hicho... Alisema wananchi hao ambao waliowengi ni wakulima lakini wanakosa dhana za kisasa za kilimo pamoja na ukosefu wa gereta ili kusikuma maji kwenye kisima cha maji kilichopo shule ya msingi kiziko ili wanafunzi na raia wengine wapate maji.

  Mbali na kijiji hicho pia Naibu waziri Ulega aliendelea na ziara katika kijiji cha Kitonga kata hiyo ya Mwarusembe ambapo pia alipokea kero ya kuvamiwa na ng'ombe kwenye mashamba ya wananchi huku wakimtaka kumaliza kero hiyo.

  Wakati huohuo wananchi hao walilalamika kwa Kiongozi wao huyo juu ya kutoridhishwa na huduma zinazotolewa katika Hospitali ya wilaya hiyo nakudai kwamba wakinana mama wanapohitaji kujifungua kuambiwa wabebe vifaa vya uzazi mbali Serikali kusema huduma hiyo bure.

  "Naibu waziri kwakweli wananchi wako sisi tunaumia. Pale Hospitali ya Wilaya ya mkuranga ni tatizo bado panafigisu na kona kona nyingi tunaomba tusaidie. "alisema mmoja wa wananchi katika mkutano huo.

  0 0

  MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, ambae pia ni mkuu wa Mkoa huo, mhandisi Evarist Ndikilo , akizungumza na baadhi ya wakulima wa korosho wakati alipotembelea ghala moja lililopo wilayani Mkuranga.Picha na Mwamvua Mwinyi  Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga

  MKOA wa Pwani ,tayari umeuza tani 19,815 ambazo zimeingiza zaidi ya bilioni 39 tofauti na msimu uliopita ambapo uliuza tani 13,000 na kupata bilioni 33.##

  Mkoa huo umejiwekea lengo la kuuza tani 25,000 hadi 30,000 kwa msimu huu ambao minada yake ya korosho ikiwa bado inaendelea .Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,aliyasema hayo Mkuranga ,wakati akizungumzia changamoto na mafanikio waliyoyapata msimu wa korosho 2017/2018 .

  Alieleza ,mbali ya hayo wakulima wa korosho mkoani Pwani wakiwa bado wanadai zaidi ya bilioni tano.Mhandisi Ndikilo alisema ,kuuza tani 19,815 hadi sasa ni mwanzo mzuri wa kufikia malengo yao waliyojiwekea msimu huu.Alisema ,hatua hiyo imetokana na serikali kutoa pembejeo bure katika msimu huu na mfumo wa stakabadhi ghalani.

  Alibainisha ,licha ya mafanikio hayo lakini kuna changamoto zimejitokeza tangu kuanza kwa minada mwaka huu ikiwemo uhaba wa magunia .Kero nyingine ni ile iliyojitokeza sasa ya kuchakachua ubora wa korosho unaofanywa na baadhi ya vyama vya msingi vya ushirika (Amcos).

  “Changamoto ya magunia inaweza kuwa historia endapo tutakubaliana kwa kukaa na mikoa ya Lindi na Mtwara ili kuhamasisha wawekezaji waje wawekeze kiwanda cha magunia lengo likiwa ni kukabiliana na tatizo hili” alifafanua .Akizungumzia kuhusu tatizo la ubora wa korosho, mhandisi Ndikilo ,alisema baadhi ya Amcos zimejiingiza kwenye kuhujumu minada hiyo kwani baadhi yao wameweka michanga na mawe kwenye magunia ya korosho .

  Alisema huo ni wizi,uhujumu uchumi na kuaibisha sifa ya nchi ya Tanzania nje ya nchi kwani magunia hayo yangefika India na nchi nyingine ingekuwa aibu na fedheha.Kutokana na upuuzi huo ndio maana nimeamua kutoa maagizo kuwa Amcos 10 zilizojihusisha na ubabaishaji huo viongozi wake wakamatwe na kuhojiwa.

  Kwa mujibu wa mhandisi Ndikilo ,kuwepo kwa maghala makubwa itainua soko la korosho msimu ujao na kuondoa ubabaishaji wa maghala ya vichochoroni yanayoleta dosari .Alisema mfumo wa stakabadhi ghalani ni mkombozi kwa wakulima hivyo anawashangaa wale wanaobeza na kuyumbisha mfumo huo.

  Mhandisi Ndikilo ,aliwataka wakulima wa korosho kuacha kukubali kurubuniwa na madalali ama wanunuzi wachache hali inayosababisha kukosa mapato kulingana na korosho zao.Serikali mkoani humo imewatoa shaka wakulima wa korosho ambao bado hawajalipwa fedha zao na kudai itasimamia makampuni na wanunuzi kulipa kwa wakati na changamoto zinazojitokeza

  0 0


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akishiriki katika zoezi la Usafi wa Mazingira katika eneo la Nyumba za Wazee Sebleni na kujumuika na Wananchi katika zoezi hilo, kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika Nyumba za Wazee Sebleni Unguja, kulia Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe. Maudline Cyrus Castico.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wazee wanaoishi Nyumba za Wazee Sebleni alipofika katika viwanja hivyo kwa ajili ya Uzinduzi wa Usafi wa Mazingira katika eneo hilo
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Vifaa vya Usafi Katibu wa Baraza la Vijana Wilaya ya Magharibi A Unguja Farida Juma, kwa ajili ya zoezi la Usafi katika Wilaya yao, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Nyumba za Wazee Sebleni wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Usafi
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa meza kuu wakiwa wamesimama kwa dakika moja kuwakumbuka Wazee waliotangulia mbele ya haki.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Usafi wa Mazingira katika viwanja vya Sebleni Unguja
  BAADHI ya Vijana wanaoshiriki katika zoezi la Usafi wa Mazingira katika eneo la Sebleni Nyumba za Wazee wakifanya usafi
  WAZEE wa Sebleni wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa usafi wa mazingira katika maeneo ya nyumba za wazee sebleni Unguja.
  VIJANA wa Mabaraza ya Vijana ya Mkoa wa Mjini Magharibi na Wananchi wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa usafi wa mazingira katika eneo la Nyumba za Wazee Sebleni, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla hiyo
  KATIBU Tawala wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Hamida Mussa Khamis akisoma risala ya Mkoa wakati wa Uzinduzi wa Usafi wa Mazingira katika viwanja vya Nyumba za Wazee Sebleni Unguja.
  MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuzungumza na Wananchi walioshiriki kazi ya Usafi wa Mazingira katika viwanja vya Nyumba za Wazee Sebleni.
  Picha na Ikulu

  0 0


  Baadhi ya wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida kaskazini wakiwa kwenye viwanja vya mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mtinko,singida vijijini juzi.
  Baadhi ya wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida kaskazini wakiwa kwenye viwanja vya mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mtinko,singida vijijini juzi.
  Naibu katibu Mkuu wa CCM Tanzania bara,Rodrick Mpogolo akizindua kampeni za uchaguzi mdogo wa CCM katika jimbo la Singida kaskazini zilizofanyika juzi katika Kijiji cha Mtinko,singida vijijini. 
  Mgombea wa kiti cha ubunge wa jimbo la Singida kaskazini,Justine Monko akiwa tayari amepokea ilani ya chama kwa ajili ya kutekeleza yaliyoainishwa ndani ya ilani hiyo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)  Na,Jumbe Ismailly SINGIDA 

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kimezindua kampeni zake za uchaguzi mdogo katika jimbo la Singida Kaskazini na kusisitiza juu ya kudumisha amani,utulivu na mshikamano uliopo hapa nchini.

  Akizindua kampeni hizo zilizofanyika katika Kijiji cha Mtinko,Singida Vijijini,kwa niaba ya Katibu mkuu wa CCM taifa,Naibu katibu mkuu wa CCM,Tanzania bara,Rodrick Mpogolo alisema idadi kubwa ya wananchi wameendelea kukichagua chama cha mapinduzi kutokana na kuwa na mipango mizuri ya maendeleo.

  Alizitaja sababu zingine kuwa ni chama chenye historian a pia kina awamu tano za uongozi na kwamba ni chama kilichokomaa na endapo kitakabidhiwa nchi au ukikabidhi madaraka,watakuwa na uhakika kwamba madaraka hayo yameshikwa na watu waliokomaa.

  Kwa mujibu wa Naibu katibu mkuu huyo wakati wote CCM imekuwa ikishughulikia kero za watu na kwa hivi sasa inayo matumaini makubwa ya kubadilisha maendeleo ya nchi na kwamba hivi sasa rais wan chi amekwisha hamisha makao makuu ya serikali yake Mkoani Dodoma,jirani kabisa na Mkoa wa Singida.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi pamoja na kuwashawishi wananchi wa jimbo la Singida kaskazini kumchagua mgombe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini hakusita pia kutaja utekelezaji unaofanya na serikali ya chama hicho kwa hivi sasa.

  Dk.Nchimbi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Singida aliweka bayana kwamba mradi wa usambazaji umeme vijijini awamu ya pili nay a tatu umeshaanza na tayari zaidi ya shilingi bilioni 71.3 zinatarajiwa kutumika kusambaza nishati hiyo katika vijiji vyote.

  “Kwa hivyo nawaombeni wananchi wa jimbo la Singida kaskazini mchagueni mgombea wa CCM kwani mkimleta mtu mwingine haijui ataanza kwanza kujifunzafunza atatuchelewesha,kwa hiyo mleteni Monko ili aendeleze utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)”alisisitiza Dk.Nchimbi.

  Akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,Juma Hassani Kilimba alisema kutokana na wingi wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo,unadhihirisha wazi kwamba wao tayari kumchagua mgombea huyo wa CCM ifikapo jan,13,mwaka ujao.

  Hata hivyo Kilimba alisisitiza huku akijinasibu kwamba chama hicho hakina wasiwasi juu ya kushinda katika uchaguzi huo mdogo kutokana na serikali ya chama hicho kujishusha kwa wananchi wa ngazi za chini.Naye mgombea wa chama hicho Justine Monko kwa upande wake amewahakikishia wakazi wa jimbo hilo kwamba hataweza kuwaangusha endapo watampa ridhaa ya kuwa mbunge wao kwa kumchagua kwa kura za kutosha na za kishindo na hatasita kuwatumikia kwa weledi wa hali ya juu.

  “Namshukuru sana Rais wetu Dk.John Pombe Magufuli kwa kuniteua kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Liwale,kanipa nafasi hiyo nimejifunza mengi sana pamoja na namna bora ya kuwatumikia wananchi”alisisitiza Monko.

older | 1 | .... | 1474 | 1475 | (Page 1476) | 1477 | 1478 | .... | 1896 | newer