Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1473 | 1474 | (Page 1475) | 1476 | 1477 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Uturuki nchini, Mhe.Ali Dovutoglu. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Desemba 2017.
  Mhe. Waziri Mahiga akizungumza na Mhe. Dovitoglu ambapo alimuhakikishia kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake pamoja na kumpongeza kwa kuteuliwa kwake kwa awamu nyingine kuiwakilisha Jamhuri ya Uturuki nchini.

  0 0

  Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde akimkabidhi fimbo mwenyekiti wa chama cha wasioona mkoa wa Dodoma Omari Lubuva ikiwa ni msaada uliotolewa na Next Generation Microfinance.
  Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde akiwa na baadhi ya viongozi wa chama cha wasioona mkoa wa Dodoma na meneja wa Next Generation Microfinance wakijaribu kutumia fimbo zilizotolewa na taasisi hiyo kwa ajili ya watu wasioona mkoa wa Dodoma.
  Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kukabidhi fimbo kwa ajili ya watu wasioona mjini Dodoma,kushoto kwake ni mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma Neema Majule na kulia kwake ni meneja wa Next Generation Microfinance Sospeter Kansapa.
  Katibu wa chama cha wasioona(TLB)mkoa wa Dodoma Enock Mbawa akizungumza wakati wa kupokea msaada wa fimbo kwa ajili ya watu wasioona,kushoto kwake ni meneja wa Next Generation Microfinance Sospeter Kansapa na kulia kwake ni mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dodoma Bill Chidabwa.
  Meneja wa Next Generation Microfinance Sospeter Kansapa akizungumza wakati wa kukabidhi fimbo kwa ajili ya watu wasioona mkoa wa Dodoma.
  Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa jumuiya za CCM mkoa wa Dodoma na wafanyakazi wa Next Generation Microfinance baada ya kukabidhi fimbo kwa ajili ya watu wasioona wa mkoa wa Dodoma.  ……………..

  NAIBU waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde leo amekabidhi msaada wa fimbo za kisasa thelathini (30)kwa ajili ya watu wasioona wa mkoa wa Dodoma huku akitoa rai kwa taasisi binafsi na jamii kuweka utaratibu wa kusaidia makundi yenye mahitaji.

  Msaada huo umetolewa na taasisi inayojishughulisha na kutoa huduma ya mikopo(NEXT GENERATION MICROFINANCE).

  Akikabidhi msaada huo Mavunde ambaye ni mbunge wa Dodoma mjini ameipongeza taasisi hiyo kwa kutumia faida waliyoipata kusaidia watu wenye mahitaji maalum jambo ambalo linapaswa kuwa chachu kwa taasisi nyingine pia.

  “Ndugu zanguni mlichokifanya leo kina maana kubwa sio duniani tu bali hata mbinguni,mmeona ni busara kutumia faida mliyoipata kwa ajili ya kusaidia wenzetu wenye mahitaji badala ya kutumia kufanya party,naomba utaratibu huu usiishie leo tu bali muendelee kugusa na makundi mengine yenye uhitaji,”alisema Mavunde.

  Katika kusaidia makundi hayo ameiomba pia taasisi hiyo kusaidia chama cha waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma ili waweze kuwa na ofisi yao inayoendana na hadhi ya makao makuu.Ametoa rai pia kwa viongozi wa chama cha wasioona mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanagawa fimbo hizo kwa walengwa bila ya upendeleo wowote.

  Akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada huo katibu wa chama cha wasioona(TLB)mkoa wa Dodoma Enock Mbawa ameishukuru taasisi hiyo kwa kusaidia serikali kupunguza changamoto walizonazo na kuahidi kuhakikisha fimbo hizo zinafika kwa walengwa waliokusudiwa.

  Awali akimkaribisha mgeni rasmi meneja wa Next Generation Microfinance Sospeter Kansapa amesema wameamua kuitikia wito wa rais John Magufuli wa kuwataka wadau wa maendeleo kote nchini kujitokeza kutoa mchango katika ustawi wa Taifa wakiamini kuwa fimbo hizo zitakuwa chachu katika kuleta maendeleo ya Taifa.

  0 0


  Tofauti na taarifa zilizochapishwa zinadozai kuwa Tigo ndio mtandao wenye gharama kubwa zaidi, Tigo ingependa kuwataarifu kuwa wateja wetu wanafurahia mojawapo ya gharama nafuu zaidi nchini.

  Bando zetu zinaanzia TZS 500; hakika wateja wa Tigo wanaonunua bando ya sauti ya TZS 500 kupitia menu yetu mpya ya 147*00 wanapata dakika 16. Pamoja na hili, wateja wa Tigo wanaonunua bando hii wanapokea bonasi ya dakika tano (5) BURE kila mara wanaponunua bando hii kupitia promosheni ya TUMEKUSOMA ambayo inawapa jumla ya dakika 21. Kwa hiyo kwa bando la TZS 500, bei zinaweza kufikia TZS 17.2 kwa dakika bila kujumuisha kodi.

  Bando ya TZS 1000 inayonunuliwa kupitia *147*00# inawapa wateja wetu dakika 55, ambapo pia wanapokea bonasi ya dakika 30 BURE kupitia promosheni ya TUMEKUSOMA. Hii inawapa jumla ya dakika 85; kwa hiyo bei inaweza kufikia TZS 8.5 kwa dakika bila kujumuisha kodi.

  Tigo inajulikana kwa promosheni kabambe na ubunifu wa ofa. Tigo pia imejijengea jina kama mtandao unaowaelewa zaidi wateja wake na kuwapa bidhaa zinazoendana na mahitaji ya soko.

  Wateja wa Tigo ndio watumiaji wa simu pekee wanaopokea bonasi za bure kwa kila bando wanayonunua, hivyo kuhakikisha kuwa wateja wa Tigo wanafurahia huduma bora zaidi kwa viwango bora na nafuu nchini.

  Kupitia huduma zake za kipekee za sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi ya juu ya 4G na huduma za kifedha kupitia simu za mikononi, Tigo inaongoza kwa ubunifu wa kidigitali ikiwemo;
  • Tigo Halichachi ndio bando ya kwanza iliyowezesha wateja wa simu nchini kutumia bando zao za simu bila muda wa ukomo wa matumizi.
  • Kuwa kampuni ya kwanza ya simu kuzindua simu za Smartphone zenye lugha ya Kiswahili
  • Kuwa kampuni ya kwanza ya simu kuzindua Facebook ya bure kwa lugha ya Kiswahili
  • Kampuni ya kwanza ya simu kuzindua huduma za fedha kupita smart apps
  • Huduma ya kwanza yenye uwezo wa kubadili thamani ya fedha kwa sarafu ya nchi husika Afrika Mashariki iliyowezesha wateja kufanya miamala ya uhakika ya fedha kupitia simu za mkononi kwenda nje ya nchi.     
  Tigo pia inajivunia mtandao mpana, wa uhakika zaidi wa 4G nchini, uliosambaa katika miji 24 Tanzania, hivyo kuwawezesha wateja kufurahia maisha ya kidigitali.

  Kwa miaka mitatu mfululizo, Tigo ndio kampuni ya simu inayokuwa kwa kasi zaidi nchini, na hivyo kuwa kampuni ya pili kwa ukubwa nchini na wateja zaidi ya 11 milioni.  0 0

  VIONGOZI wa Vitongoji na Vijiji vilivyopo kwenye mipaka mkoani Tanga wameonywa kuacha tabia ya kuuza ardhi kwa wageni wanaofika kwenye maeneo yao badala yake hakikishe wanatoa taarifa wanapowaona watu wasiowajua ili kuweza kukomesha vitendo vya wahamiaji haramu.

  Hayo yalisemwa na Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga Crispian Ngony’ani wakati akizungumza na vyombo habari ambapo alisema viongozi hao wamekuwa ni tatizo kubwa badala ya kukemea vitendo vya wahamiaji haramu lakini wamekuwa wakiwakumbatia kwa kuwapatia ardhi jambo ambalo ni kosa kisheria.

  Alisema utafiti walioufanya mpakani mwa Kenya na Tanzania Horohoro wamebaini idadi kubwa ya wakenywa wameuziwa ardhi katika maeneo hayo na wanaishi nchini kinyume cha sheria huku akiwataka viongozi hao kuachana na vitendo hivyo kabla hawajakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya dola.

  “Tatizo kubwa viongozi wa vitongoji na vijiji badala ya kumemea uuzaji wa ardhi kinyemele hivyo napenda kutoa onyo kwao kuacha tabia hiyo kwani sisi kama idara ya uhamiaji tupo macho kuhakikisha wale wote wanaohusika na vitendo hivyo tunawachukulia hatua “Alisema.

  Alisema viongozi hao badala ya kukemea uzaji wa haramu ardhi kwa wageni wao wamekuwa mstari wa mbele kuwakarabisha kwenye maeneo hayo bila kutambua kufanya hivyo ni makosa kisheria hivyo kuwaonya kuacha vitendo vya namna hiyo mara moja.

  “Pindi wanapomuona mgeni au raia anauza ardhi watoe taarifa kwenye vyombo vinavyo husika ikiwemo idara ya uhamiaji tukishirikiana kwa mtindi huo tutaweza  kukomesha vitendo vya watu kuvamia ardhi yetu na kuishi kinyume cha sheria tu “Alisema Ofisa Uhamiaji huyo.

  Wakati huo huo,Ofisa Uhamiaji huo alisema katika kipindi cha mwaka 2017 wamekamatwa watanzania 61 kwa kuvunja sheria za uhamiaji ambapo kosa kubwa ni kushiriki vitendo viovu vya kuwasafirisha wahamiaji hao katika maeneo mbalimbali na kuwaingiza nchini.

  Alisema hasa wahamiaji ambao ni raia kutoka nchini Ethiophia
  wanaonekana wana biashara kubwa sana kwa baadhi ya watu mkoani Tanga kwa kwenda nchini Kenya  kuwachukua kwa kufanya udalali na kuwapitisha kwenye njia za panya hadi kwenye maeneo wanayotaka kufika.

  Aidha alisema kutokana na hali hiyo idara hiyo imeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha wanakomesha vitendo vya namna hiyo kwa kuongeza udhibiti wa watu wanaoingia nchini kwa kushirikiana na vyombo vya vyengine vya dola.

  Hata hivyo alisema katika kipindi hicho kesi 28 zimefunguliwa ambazo zilikuwa zinawahusu watanzania na zilizokuwa zikiendelea ni 10,nne zilikwisha,mbili zilifutwa na moja iko kwa wakili wa serikali na nyengine moja ipo uhamiaji.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0


  0 0


  Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Rajab AbdulKahal maarufu Harmonize ametoa Msada wa Fimbo30 kwa Chama cha Wasioona Kilichopo Mkoa wa Mtwara Zenye Thaman ya Shilingi Million1 na Laki8 kama njia mojawapo ya kuwafariji walemavu wa macho katika kipindi hiki cha Sikukuu.

  Katika Salam zake Hamornize amesema alipata taarifa ya kuwa chama Hicho kinauhitaji wa Fimbo kwa ajili ya Matumizi ya Kutembelea hivyo kuamua Kuleta Fimbo hizo ambapo Mahitaji ya Fimbo kwa kiasi kikubwa yanahitajika.

  Aidha amewaomba baadhi ya Wadau wenye uwezo kujitokeza na kutoa Msaada ili kupunguza changamoto ambazo zinawakabili watu wenye ulemavu wa Macho.

  Akizungumzia Kuhusiana na ziara yake Mkoani Mtwara Harmonize anasema bado Ataendelea Kutoa Msaada kulingana na anachopata na ataendelea kutembea asasi mbalimbali zenye mahitaji maalum ili kuweza Kusaidi.
  Msanii wa Muziki wa kizazi Kipya Harmonize akimkabidhi Fimbo 30  katibu wa chama cha Wasioona Mkoani Mtwara Ally Ismail.

   Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Harmonize katika Picha ya Pamoja na chama cha watu Wasioona Mkoani Mtwara Mara baada ya kukabidhi Msaada wa Fimbo kwa walemavu wa Macho Mkoani Mtwara.
   Harmonize akimuongoza Kushuka Ngazi katibu wa Chama cha Wasioona Ally Ismail katika Makabidhiano ya Msaada wa Fimbo za kutembelea kwa watu wenye Ulemavu.


   Harmonize akiwa na Rafiki yake Sarah Akiongea na Wanachama wa Chama cha watu Wasioona kabla ya Kukabidhi Fimbo30 kwa ajili ya kutembelea.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 ambapo alitoa agizo kwa vyombo vya ulinzi kuwakamata wanaowalazimisha watanzania kufanya malipo kwa Dola badala ya Shilingi, mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akitoa maelekezo kwa Benki nchini kuangalia namna ya kupunguza riba kwa wakopaji na pia kufuata vigezo stahiki kwa mkopaji ili kuondoa mikopo chechefu wakati wa mkutano kati yake na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (mbele) akiwa katika Mkutano na waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Susana Mkapa na Afisa Mwandamizi wa Wizara hiyo Bw. John Sausi wakizungumza jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na Waandishi wa Habari kuhusu Hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Maafisa Waandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifurahia jambo wakati Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo aliangazia suala la hali ya Uchumi na kubainisha kuwa ni imara ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaabani (kushoto) akizungumza na wadau waliohudhuria Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kulia.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)


  Na. Paschal Dotto.

  Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imewatoa hofu wananchi kuhusu uvumi wa kuongezeka kwa deni la Taifa kwamba deni hilo ni himilivu na liko chini ya ukomo wa hatari.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philipo Mpango wakati akitoa mwenendo wa hali ya uchumi na utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 .

  Dkt. Mpango alisema kuwa katika tathimini iliyofanyika mwezi Novemba mwaka huu inaonesha kuwa uwiano wa deni hilo na pato la Taifa ni asilimia 32.5 likilinganishwa na ukomo wa asilimia 56.

  “Katika kuangalia ukomo wa deni hili ambao uko chini, inaonesha kuwa deni hili ni himilivu katika kipindi cha muda wa kati na muda mrefu”, alisema Dkt. Mpango.Akieleza takwimu hizo, Waziri Mpango amesema kuwa mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, deni la Taifa lilifikia shilingi bilioni 47,823.1 ikilinganishwa na bilioni 42,552.4 katika kipindi kama hicho mwaka 2016 ambapo kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 13,417.5 ni deni la ndani sawa na asilimia 28.1 na shilingi bilioni 34,405.6 ni deni la nje ambalo ni sawa na asilimia 71.9.

  Dkt. Mpango alisisitiza kuwa ongezeko hilo lilitokana na kupatikana kwa mikopo mipya ya nje na ndani ya nchi kwa ajili ya kugharamia miradi ya maeneeleo.Aliitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa mradi wa umeme Kiwira (Kiwira Coal Mine), miradi ya uboreshaji wa huduma za maji kwa jamii, mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa kinyerezi na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege ambapo miradi hiyo itawezesha watanzania kufika uchumi wa kati wenye viwanda.

  “Mambo muhimu ya kujiridhisha nayo ni kwamba mikopo inayokopwa itumike katika kujenga uwezo zaidi wa kuzalisha mali na huduma nzuri kwa watanzania”, alisisitiza Dkt. Mpango.

  Aidha Waziri Mpango amesema kuwa kufuatia hatua zinazochukuliwa na Serikali, ukwasi kwenye benki za biashara uliongezeka na kusaidia kupungua kwa riba ya mikopo baina ya mabenki na kufikia wastani wa asilimia 3.53 mwezi Novemba mwaka huu kutoka wastani wa asilimia 14.93 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2016/2017.Vilevile riba za dhamana za Serikali zilishuka kutoka wastani wa asilimia 15.56 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016/2017 hadi asilimia 8.76 mwezi Novemba, 2017 na kuongeza kuwa Serikali inatarajia kasi ya ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi itaanza kuimarika.

  Aidha, Dkt. Mpango amewaonya watu wanaotoa takwimu za uongo kuacha mara moja kwani wanaipotosha jamii, huku akiwataka waandishi wa habari kupata takwimu maalumu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kuweka takwimu sahihi.

  0 0


  Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Phillip Mpango akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hali ya uchumi kwa mwaka 2017 leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Khatib M. Kazungu.


  Na. Paschal Dotto.


  Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imewatoa hofu wananchi kuhusu uvumi wa kuongezeka kwa deni la Taifa kwamba deni hilo ni himilivu na liko chini ya ukomo wa hatari.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philipo Mpango wakati akitoa mwenendo wa hali ya uchumi na utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 .

  Dkt. Mpango alisema kuwa katika tathimini iliyofanyika mwezi Novemba mwaka huu inaonesha kuwa uwiano wa deni hilo na pato la Taifa ni asilimia 32.5 likilinganishwa na ukomo wa asilimia 56.

  “Katika kuangalia ukomo wa deni hili ambao uko chini, inaonesha kuwa deni hili ni himilivu katika kipindi cha muda wa kati na muda mrefu”, alisema Dkt. Mpango.

  Akieleza takwimu hizo, Waziri Mpango amesema kuwa mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, deni la Taifa lilifikia shilingi bilioni 47,823.1 ikilinganishwa na bilioni 42,552.4 katika kipindi kama hicho mwaka 2016 ambapo kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 13,417.5 ni deni la ndani sawa na asilimia 28.1 na shilingi bilioni 34,405.6 ni deni la nje ambalo ni sawa na asilimia 71.9.

  Dkt. Mpango alisisitiza kuwa ongezeko hilo lilitokana na kupatikana kwa mikopo mipya ya nje na ndani ya nchi kwa ajili ya kugharamia miradi ya maeneeleo.

  Aliitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa mradi wa umeme Kiwira (Kiwira Coal Mine), miradi ya uboreshaji wa huduma za maji kwa jamii, mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa kinyerezi na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege ambapo miradi hiyo itawezesha watanzania kufika uchumi wa kati wenye viwanda.

  “Mambo muhimu ya kujiridhisha nayo ni kwamba mikopo inayokopwa itumike katika kujenga uwezo zaidi wa kuzalisha mali na huduma nzuri kwa watanzania”, alisisitiza Dkt. Mpango.

  Aidha Waziri Mpango amesema kuwa kufuatia hatua zinazochukuliwa na Serikali, ukwasi kwenye benki za biashara uliongezeka na kusaidia kupungua kwa riba ya mikopo baina ya mabenki na kufikia wastani wa asilimia 3.53 mwezi Novemba mwaka huu kutoka wastani wa asilimia 14.93 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2016/2017.

  Vilevile riba za dhamana za Serikali zilishuka kutoka wastani wa asilimia 15.56 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016/2017 hadi asilimia 8.76 mwezi Novemba, 2017 na kuongeza kuwa Serikali inatarajia kasi ya ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi itaanza kuimarika.Aidha, Dkt. Mpango amewaonya watu wanaotoa takwimu za uongo kuacha mara moja kwani wanaipotosha jamii, huku akiwataka waandishi wa habari kupata takwimu maalumu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kuweka takwimu sahihi.

  0 0

  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akionyesha barua  aliyopokea kutoka kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,wakati akizungumza na waandishi wa habari kijijini kwake Namahema ‘A’ wilayani Ruangwa mkoani Lindi leo jioni Ijumaa, Desemba 29, 2017.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema amekwishawasilisha tamko la maadili ya viongozi wa umma kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma tangu jana (Alhamisi Desemba 28, 2017).
  Akizungumza na waandishi wa habari kijijini kwake Namahema ‘A’ wilayani Ruangwa mkoani Lindi leo jioni (Ijumaa, Desemba 29, 2017), Waziri Mkuu amesema fomu hizo zilipokelewa jana na amekwishapatiwa barua ya kupokea tamko hilo.
  “Nimewaita hapa ili kuthibitisha kuwa nimetekeleza takwa hilo la kisheria na tayari Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi ya Umma imekiri kupokea tamko langu kwa barua hii hapa,” alisema Waziri Mkuu huku akionyesha barua hiyo ambayo ilisainiwa na Jaji Harold Nsekela, Desemba 28, 2017.
  “Kwa kuzingatia mfano ulioonyesha na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ninawaagiza viongozi wote wanaotakiwa kujaza fomu hizo kwa mujibu wa sheria wafanye hivyo na kuziwasilisha ifikapo tarehe 31 Desemba, 2017 saa 10 jioni,” alisisitiza Waziri Mkuu.
  Alisema anawakumbusha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu wote na viongozi wote walioko kwenye ngazi za uteuzi wahakikishe wanatimiza takwa ambalo liko kwa mujibu wa kifungu cha 9 na cha 11 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya Mwaka 1995.
  Wakati huohuo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwatakia Watanzania wote heri wakati wanaposubiri kumaliza mwaka 2017 na kuwatakia heri na fanaka katika maeneo waliyopo wanapojiandaa kuupokea mwaka 2018.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  IJUMAA, DESEMBA 29, 2017.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo itakayojengwa eneo la Kijiji cha Lusanga wilayani humo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Like Gugu wakishuhudia tukio hilo


  Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu akichimba mtaro kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo eneo la Lusanga wilayani humo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo,Like Gugu
  Sehemu ya wananchi wakishiriki katika uchumbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Muheza Mkoani Tanga 

  Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu akishiriki kubeba tofali kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali itakayojengwa eneo la Kijiji cha Lusanga wilayani Muheza   Sehemu ya wadau wa maendeleo wilayani Muheza wakishiriki kwenye zoezi la ubebaji wa matofali wilayani humo
  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa tatu kutoka kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu wa pili kutoka kulia wakipokea mifuko 600 ya saruji kutoka kwa kampuni ya Lucky Cement ya Kisarawe Mkoani Pwani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu
  Sehemu ya shehena ya saruji ambayo ilishushwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza
  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kupokea saruji hiyo ambapo aliishurku kampuni hiyo huku akiyataka makampuni mengine yaliyopo mkoani hapa kuunga mkono jitihada hizo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu 
  Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu akizungumza katika halfa hiyo ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kuamua kuwasaidia ujenzi huo huku akiyataka makampuni mengine kuiga mfano huo
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Lucky Cement iliyopo Kisarawe,Emanuel Muya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu azma yao ya kusaidia mifuko ya saruji 600 kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya wilaya ya Muheza kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu 


  MKUU wa wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo,Mbunge wa Jimbo hilo,Balozi Adadi Rajab na wakazi wa wilaya hiyo wakishirikiana kwa pamoja wameanza kuchimba msingi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya katika Kijiji cha Lusanga Kata ya Lusanga ambayo itasaidia kuondoa changamoto ya kutokuwepo kwa kipindi cha miaka 37.

  Hatua ya viongozi hao ina lengo la kuandika historia tokea wilaya hiyo ilipoanzishwa mwaka 1974 ambapo wananchi walikuwa wakitegemea kupata huduma za matibabu kwenye hospitali ya Teule Muheza kutoka maeneo mbalimbali kabla ya kufikiria kuanzishwa kwa hospitali hiyo ambayo itakayogharimu zaidi ya bilioni 11.

  Akizungumza wakati akishiriki zoezi la uchimbaji wa mtaro wa Hospitali hiyo na kupokea mifuko ya saruji 600 ya Lucky kutoka kwa Kampuni ya kuzalisha Saruji ya Kisarawe, Mhandisi Mwanasha alisema waliamua kufanya hivyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya huduma ya afya ambayo ilimlazimu wakati ameteuliwa kuiongozi wilaya hiyo kukutana na wadau kuweza kuona namna ya kuweka mikakati ya kupatikana kwake.

  Aidha kutokana na kuwepo kwa hospitali ya wilaya walikuwa wakilazimika kutimia hospitali ya teule Muheza tokea ilipoanzishwa lakini imeonekana kuzidiwa na watu wanaohitaji huduma hasa ukizingatia pia zahanati na vituo vya afya vipo vichache huku wananchi wakiongezeka.

  “Nilibaini changamoto ya hospitali ya wilaya wakati nilipokuwa nikifanya vikao kwa kuzunguka kata zote nikaona tatizo la huduma ya afya ni kubwa sana na hivyo kuonekana kuna haja ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza lakini hata kwenye baraza la madiwani suala hilo lilizungumzwa”Alisema

  Mkuu huyo wa wilaya alisema baada ya kufikiria wazo hilo la ujenzi wa hospitali hiyo waliona wafanya mazungumzo na Agro Tan ambao wanamiliki Shamba la Muheza Estate ambao walikubali kutoa eneo lao la ekari 100 kwa ajili ya ujenzi huo.

  Awali akizungumza katika eneo hilo,Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema juzi ilikuwa ni siku muhimu sana kwao kutokana na wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye msaragambo kwa nia ya kujengwa hospitali ya wilaya ambacho kilikuwa kilio chao kwa muda mrefu.

  Alisema waliamua kuanzisha mchakato wa ujenzi wa hospitali hiyo baada ya kuona huduma ambazo zilikuwa zikitolewa katika hospitali ya Teule Muheza kuelemewa kutokana na watu kuongezeka huku maradhi yakiwa mengi kila wakati na ndio walipoamua kuchukua uamuzi huo.

  Mbunge huyo alisema wananchi wa wilaya hiyo waliposikia mipango ya kuwepo kwa ujenzi huo walianza kujitolea fedha kiasi cha elfu mbili ikiwemo kushiriki kwenye uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa hospitali hiyo tokea alfajiri wakiunga mkono juhudi za serikali. 

  “Lakini pia nisema tunawashukuru kampuni ya Lucky Cement kwa kutukabidhi mifuko 600 ya saruji na tunategemea pia kuvitumia viwanda vilivyopo mkoani Tanga kwa lengo la kuongeza nguvu katika ujenzi wa hospitali ya wilaya yetu tunavifaa vya kutosha vya kuanzia tutaanza na baadae wataingiza kwenye bajeti kuiomba serikali iwasaidie”Alisema Mbunge huyo

  Kwa upande wake,Meneja Masoko wa Kampuni ya Lucky Cement iliyopo Kisarawe,Emanuel Muya alisema wao kama wadau wa maendeleo waliguswa na kuamua kuchangia ujenzi wa hospitali hiyo ili kuwasaidia wananchi kuondokana na changamoto za huduma ya afya katika wilaya hiyo.

  Alisema kwa kutambua thamani ya maendeleo katika nchi ndio sababu kubwa iliyowasukuma kuamua kusaidia saruji hiyo kwa ajili ya kuanza mchakato wa ujenzi wa hospitali hiyo ambapo itakapokamilika itawasaidia kuwaondolea changamoto wananchi.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa na diwani wa kata ya Mapanda Obed Kalenga na mwenyekiti wa kijijicha Ihimbo wakati wa kueleza vitu gani ambavyo amevifanya kwenye kata hii kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa kata ya Mapanda 
  Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa kwenye moja ya darasa ambalo litakarabatiwa kutumia mfuko wake wa jimbo ili liwe kwenye kiwango kinachotakiwa 
  Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua majengo ya shule na kuangalia majengo yapi yanastahili kukarabatiwa
  Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa kwenye moja ya zahati ambayo inatakiwa kufanyiwa ukarabati ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa kata ya Mapanda  Na Fredy Mgunda,Mufindi.

  Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa amekabidhi jumla ya mifuko ya saruji 400 na bati 150 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule za msingi pamoja na zahati za Kata ya Mapanda kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, alisema kuwa niliomba kuwa mbunge kwa lengo la kuwatumikia wananchi hivyo najitahidi huku na kule kuhakikisha natimiza azma yangu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini.

  “Nimetoa jumla ya mifuko ya saruji 400 na bati 150 kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi na ukarabati wa madarasa katika shule na zahati za kata hii ikiwa ni mwamzo tu nitaendelea kutoa saruji nyingine na bati hata vitu vingine ili kulifanya jimbo la Mufindi Kaskazini kupata maendeleo kwa kasi” alisema Mgimwa

  Mgimwa alisema kuwa halmashauri ya Mufindi imeshaanda mpango kabambe ambao utakuwa msaada mkubwa kuchochoe maendeleo kwa kasi huku serikali ikiendelea kufanya jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata maji ya kutosha na kuitumia vizuri ardhi ya halmashauri hiyo kwa kufanya maendeleo.

  “mimi lengo langu inapofika kipindi cha uchaguzi ninakuwa nimetatua kero zote za wananchi na kujihakikishia napewa ridha ya kuongoza kipindi kingine kwa maendeleo ya wananchi wa jimbo la mufindi kaskazini na kuongeza kuwa hatakusikia kuwa kuna kitu kinasababisha migogoro ya kugombea ardhi katika jimbo hili la Mufindi Kaskazini” alisema Mgimwa

  Aidha Mgimwa alisema kuwa shule na zahanati zilizopata saruji na mabati ni shule za kijiji cha Mapanda,shule ya kijiji cha Uhafiwa,Ukama,Ihimbo na Chogo lengo ni kuchochoe kuleta maendeleo kwa wananchi.

  Mgimwa amewapongeza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kata na ametoa ahadi ya kuendelea kushirikiana kwa kuchangia ujenzi wa shule zote za jimbo la Mufindi Kaskazini na kutatua kero nyingine za wananchi wa jimbo hilo.Obedi Madembo, Peter Kaguo, Kristopher Ngunda,Thobias Luvinga na Fransisco Mfaume ni wenyeviti wa vijiji vya kata ya Mapanda walimpongeza mbunge huyo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatafutia wananchi mandeleo kwa kutumia nguvu zake zote.

  “Hata ukiangalia mwandishi utagundua gharama alizozitumia mbunge zimewaondolea wananchi kuchangia kabisa hivyo bila mbunge huyu mzigo wote huu ulikuwa unawaangukia wananchi wa vijiji vyote vya kata ya Mapanda” walisema wenyeviti wa vijiji vya kata ya Mapanda

  Kwa upande wake diwani kata ya Mapanda Obed Kalenga alimshukuru kwa kazi kubwa aliyoifanya na kuwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono mbunge huyo ili andelee kufanya kazi ya kuwatafutia maendeleo wananchi wa kata ya Mapanda na jimbo la Mufindi Kaskazini kwa ujumla.

  “Wananchi kweli wananjitoa sana kufanya kazi za kuleta mandeleo hiyo wanapoona kuwa mbunge naye anatumia nguvu kubwa kufanya maendeleo kutaongeza chachu ya kufanya kazi kwa kujitolea kwenye shughuli za kimaendeleo hata mchakato ulivyokuwa hadi kupelekea kushirikiana na wananchi kuanzisha ujenzi na ukarabati wa shule na zahati ili kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa kata hiyo na kupatikana kwa huduma za afya bora kwa wananchi wote” alisema Kalenga.

  0 0

  Msanii Nyota wa Bongofleva Afrika Mashariki na kwingineko Diamond Platnum akimkabidhi mmoja wa masahabiki wake baada ya kujishindia manukato (pafyume) ya CHIBU,mara baada ya kushiriki promosheni ya 'nogewa ushinde' inayoendelea kuchezeshwa kupitia bidhaa yake ya Karanga,ambayo pakiti yako moja huuzwa shilingi 300/= tu . 
  Msanii Nyota wa Bongofleva Afrika Mashariki na kwingineko Diamond Platnum akimkabidhi mmoja wa masahabiki wake baada ya kujishindia simu ya mkunoni aina Samsung J7,mara baada ya kushiriki promosheni ya 'nogewa ushinde' inayoendelea kuchezeshwa kupitia bidhaa yake ya Karanga,ambayo pakiti yako moja huuzwa shilingi 300/= tu . 
  Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya aka Bongofleva hapa nchini Abdull Nassib almaarufu kwa jina la Diamond Plutnum akiwataja washindi mbalimbali waliojinyakulia zawadi kupitia promosheni ya karanga zake iitwayo 'Nogewa Ushinde',hafla hiyo imefanyika mapema leo jijini dar na kuhudhuriwa na mashabiki wake lukuki.
  Msanii Nyota wa Bongofleva Afrika Mashariki na kwingineko Diamond Platnum akimkabidhi ufunguo mmoja wa masahabiki wake baada ya kujishindia piki piki mara baada ya kushiriki promosheni ya 'nogewa ushinde' inayoendelea kuchezeshwa kupitia bidhaa yake ya Karanga,ambayo pakiti yako moja huuzwa shilingi 300/= tu . 
  Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya aka Bongofleva Abdull Nassib almaarufu kwa jina la Diamond platnumz akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mapema leo jijini Dar,mara baada ya kugawa zawadi mbalimbali kwa washindi wa promosheni inayoendeshwa kupitia karanga zake (diamondkaranga) inayoitwa 'nogewa ushinde',Diamond Platnumz amemwaga zawadi hizo kede kede kwa washindi wa promosheni hiyo zaidi ya 30,zikiwemo  piki piki,Manukato (pafyumu ya CHIBU),simu mbalimbali

  0 0


  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akikagua mbegu zilizohifadhiwa ghalani kabla ya kuanza kusambazwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge (Kulia) na Meneja uzalishaji Wakala wa Mbegu Ndg Charles Levi (Kushoto). Picha Zote Na Mathias Canal
  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo baada ya kukagua baadhi ya mashine za mbegu alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua namna mbegu za mazao mbalimbali zilivyohifadhiwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017.  Na Mathias Canal, Morogoro

  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa leo Disemba 29, 2017 amewaagiza wafanyabiashara wa mbolea kote nchini walioweka mgomo wa kupeleka mbolea kwa wakulima kufikia 30 Disemba 2017 wawe wamefungua maghala yao kwa ajili ya kuwauzia mbolea wakulima.

  Alisema endapo wafanyabiashara hao wasipofanya hivyo serikali itawanyang'anya leseni zao haraka iwezekanavyo ili kuruhusu wafanyabiashara wenye uwezo wa kufanya jukumu hilo pasina kuwaumiza wakulima kutokana na bei ghali ya mbolea.

  Mhe Mwanjelwa ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) Mara Baada ya kubaini kuwa kuna wafanyabiashara ambao wameanza kufunga maghala kwa madai ya kupanda kwa mbolea katika soko la Dunia.

  Alisema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria na kuijaribu serikali kwani malalamiko yao ya kupanda kwa bei katika soko la Dunia hayana tija kwani mbolea zote zilipo nchini tayari wakishanunua kipindi soko likiwa kwenye unafuu mkubwa.

  Alisema kuwa serikali ilitoa bei elekezi katika mbolea ya kukuzia na kupandia ikifahamu fikra kuwa kupitia gharama hiyo wakulima watanufaika lakini pia wafanyabiashara watanufaika kutokana na faida wanayoipata lakini wameamua kubadili utaratibu wa kutaka kupata faida kubwa zaidi pasina kujali wakulima wataumizwa na bei hiyo kwa kiasi gani.

  Mhe Mwanjelwa ameitaka kampuni ya Premium ambayo ni moja ya kampuni zilizogoma kufungua maghala na kupeleka mbolea kwa wakulima kwa bei elekezi iliyotolewa na serikali.

  Alisema kuwa wafanyabiashara hao kwa makusudi wameamua kufifisha juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ya kuwakomboa wakulima kupitia gharama nafuu ya mbolea hivyo kufikia kesho wasipofungua maghala hayo watanyang'anywa leseni zao ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa sheria.

  0 0


  0 0

   Askari wa wanyama pori wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha Ndg. Majid Kijaji (kushoto) akimfafanulia   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wa kwanza kulia) kuhusu fuvu la Fisi alipotembelea hifadhi hiyo iliyoko mkoani Arusha leo tarehe 29/12/2017 kama juhudi za kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
  Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha Bi. Mery Kirombo (wa kwanza kulia) akimpatia maelezo mafupi kuhusu hifadhi hiyo  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) muda mfupi kabla ya kuanza kwa safari ya kuhamsisha utalii katika hidadhi hiyo leo tarehe 29/12/2017 mkoani Arusha. Katikati  ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Ndg. Godifrey Mngereza. Safari hiyo iliandaliawa na Taasisi ya Mtandao wa Wasanii wa  Musiki wa Njili hapa Nchini (TAGOANE)
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wa pili kulia waliokaa nyuma)  akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Tengeru English Medium katika eneo la Ngurudoto Crater  alipotembelea  hifadhi ya Taifa  ya Arusha (Arusha National Park) iliyoko mkoani Arusha leo tarehe 29/12/2017. Kushoto kwake ni msanii wa maigizo Kingwnedu na kulia kwake ni Rais wa TAGOANE Dkt. Godwin Maimu , taasisi ya TAGOANE ndiyo iliyo ratibu safari hiyo ya siku moja ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
   Afisa Utalii na Masoko wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha Ndg.  Nicholaus Mahimbi (kulia) akimfafanulia  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) kuhusu mabaki ya fuvu la Nyati lililopo katika eneo la Ziwa Dogo la Momella wakati Mhe. Shonza alipotembela hifadhi hiyo iliyoko mkoani Arusha leo tarehe 29/12/2017 kama juhudi za kuhamasisha utalii wa ndani nchini. 
   Askari wa wanyama pori wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha Ndg. Agustino Kombwa (wa kwanza kulia) akimpa maelekezo ya namna ya kupanda mlima Meru  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wa kwanza kushoto)alipotembela hifadhi hiyo iliyoko mkoani Arusha leo tarehe 29/12/2017 kama juhudi za kuhaasisha utalii wa ndani nchini.Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Ndg. Godfrey Mngereza na Dkt. Godwin Maimu Rais wa taasisi ya TOGOANE. Taasisi ya TAGOANE ndiyo iliyo ratibu safari hiyo.
  PICHA NA OCTAVIAN KIMARIO-WHUSM.


  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akioneshwa ramani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani na Mwakilishi wa Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Vitalis Kuluka huku akishirikiana kuonesha eneo hilo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo,Erica Yigella ( wa pili kulia) mahali kilipo Kitongoji cha Uvinje ambapo wakazi wa eneo hilo wamegoma kuhama ndani ya hifadhi hiyo na wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea hifadhi hiyo jana. Wa kwanza kulia ni Afisa Wanyamapori, Godfrey Maro na Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani, Stephano Msumi na pande wa kulia nyuma ya Katibu Tawala ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Fredrick Mofulu 
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa pili kulia ) akizungumza na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani , Stephano Msumi ( katikati) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kujionea changamoto mbalimbali zinazoikabili . Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Erica Yigella, Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Vitalis Kuluka, wa tatu kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Fredrick Mofulu 
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza jana na Wananchi wa Kitongoji cha Uvinje ambao wamegoma kuhama ndani ya hifadhi hiyo, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea kwa ajili ya kuzungumza nao ili kujua ukubwa tatizo la mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 10 sasa .
  Bango lililopo katika geti la Gama linalokuelekeza sheria na taratibu ukiwa unaingia katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( kushoto ) akipatiwa maelezo na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani , Stephano Msumi ( katikati) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kujionea changamoto mbalimbali zinazoikabili .Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa, Vitalis Kuluka, nyuma ya Mhifadhi wa Saadani ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Fredrick Mofulu
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( mbele ) akiwa na baadhi ya viongozi wa Hifadhi za Taifa pamoja kamati ya ulinzi na usalama kutoka Wilayani Bagamoyo akiongoza kwenda kuangalia sehemu kunakofanyika utalii wa boti katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kujionea changamoto mbalimbali zinazoikabili .
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kulia) akipatiwa maelezo na Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Fredrick Mofulu ( wali kushoto) kuhusiana na sehemu kunakofanyika utalii wa boti katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani . Wengine ni baadhi ya viongozi wa Hifadhi za Taifa pamoja na kamati ya ulinzi kutoka Wilayani Bagamoyo . 
  Picha na Lusungu Helela  Wananchi wa Kitongoji cha Uvinje kilichomo ndani Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyopo wilayani Bagamoyo Mkoani wa Pwani wamesema hawapo tayari kuhama wala kulipwa fidia ili kupisha hifadhi hiyo.

  Kitongoji hicho, ambacho ni kati ya vitongoji nane vya Kijiji cha Saadani, kilitakiwa kiondolewe tangu mwaka 2005 baada ya hifadhi hiyo kupandishwa daraja kutoka pori la akiba na kuwa hifadhi kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Namba 281 la Septemba 16, 2005.

  Akizungumza mbele ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Bagamoyo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati alipofanya ziara jana katika kijiji hicho aliwambia wananchi hao kuwa lengo la ziara yake ni kutaka kuwasikiliza juu mgogoro huo na sio kuwahamisha.

  ‘Mimi ni mgeni kidogo kwenye Wizara hii, Nimekuja kuangalia sio kuwahamisha kwa kuwa sijui eneo hili lina ukubwa kiasi na lina kaya ngapi lakini nimekuja kutembelea hifadhi na maeneo yote yenye changamoto. ‘’ alisema.Alisema amefika kwa ajili ya kuwasikiliza ili aweze kujua jinsi mgogoro ulivyo kwa sababu hakutaka kusikia upande mmoja wa TANAPA pekee.

  Naye , Kaimu Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Hassan Akida alisema wakazi wa eneo hilo hawapo tayari kuhama na wala kulipwa fidia kwa vile ni ardhi yao tokea enzi za mababu zao.’‘Tumesema hapa ndo kwetu mnataka kutuhamisha mtupeleke wapi wakati sisi tumezoea maisha yetu hapa’’ alisema Akida.

  Aliongeza kuwa kitongoji hicho kimekuwapo kwa muda mrefu na waliishi bila shida hadi pale pori hilo lilipobadilishwa na kuwa Hifadhi ya Taifa.“Wakati hili ni pori la akiba tuliishi vizuri tu na wazazi wetu walikuwa ni wafanyakazi wa pori. Lakini tangu iwe hifadhi imekuwa taabu. Sasa tunafukuzwa wakati tumezaliwa hapa na wazazi wetu wamezikwa hapa hapa,” anasema Hassan Akida. 

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Saadani, Adam Mwandosi alisema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na umekuwa ukileta chuki kati ya Serikali na wananchi.Amesema wananchi wa eneo hilo muda mwingine wamekuwa wakimuona hata yeye Mwenyekiti wao kama anawasaliti kwa vile tokea mgogoro huo ulipoanza viongozi wengi wamekuwa wakifika hapo lakini wamekuwa hawana majibu ya kumaliza mgogoro huo.

  Mhifadhi Mkuu wa Saadani, Stepahano Msumi amesisitiza kuwa kitongoji hicho kimo ndani ya hifadhi kinyume cha sheria.Alisisitiza kuwa sheria za hifadhi za Taifa haziruhusu makazi ya watu ndani yake.

  “Kwa ufupi tu ukiangalia GN (Tangazo la Serikali) linaonyesha kuwa eneo lote la kitongoji cha Uvinje liko ndani ya hifadhi. Ni kweli lilikuwa eneo la watu ambao walikuwa watumishi wa pori la akiba tangu lilipoanzishwa mwaka 1968. Waliombwa kuondoka lakini waliendelea kuongezeka,” anasema.

  Anasema katika makubaliano, iliamuliwa kuwa walipwe fidia kwa taratibu lakini hata hivyo licha ya kutekeleza utaratibu wa fidia bado wamegoma kuipokea mbali ya wachache kujitokeza.

  Ikumbukwe kuwa, Saadani ni hifadhi pekee ya Taifa nchini na Afrika Mashariki yenye fukwe za bahari na inayotazamana na Bahari ya Hindi na fukwe zake zinakutana na uoto wa asili wa nchi kavu.

  Inapatikana katika mikoa ya Tanga na Pwani. Uwepo wake ni matokeo ya pori la akiba la Saadani, ranchi ya Mkwaja na sehemu ya kaskazini, sambamba na akiba ya msitu wa asili wa Zaraninge.

  0 0

  NA VICTOR MASANGU, MKURANGA 

  MAMLAKA ya mapato (TRA) Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani imefanikiwa kukamata tani 26 za mizigo ya aina mbali mbali ambayo ilikuwa imepakizwa katika malori mawili ya magari ikisafirishwa kinyemela kutokea kariakoo Jijini Dar es Salaam kuelekea mikoa ya kusini bila ya kuwa na risiti halali kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi.

  Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa TRA Wilaya ya Mkuranga Amosie Ernest alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa baada ya kuyakamata malori hayo walipoyapekuwa waliweza kubaini kuwa yamesheheni bidhaa nyingi ambazo hazijakatiwa risiti kwa mfumo wa mashine ya kielectroniki (EFD), hivyo walikuwa wanakwepa kulipa kodi.

  “Ni kweli kwa sasa tupo katika msako mkali kwa ajili ya kuweza kugagua magari yote ambayo yanabeba miigo bila ya kuwa na risiti, na katika zoezi hili tumefanikiwa kuyakamata magari mawili makubwa ambayo yalikuwa yamebebeba mzigo ambao ulikuwa na bidhaa mbali mbali na baada ya kufanya uchunguzi tuliweza kuona kuwa kuna mapungufu makubwa kutokana na wahusika kutokuwa na risiti hivyo magari tumeyakamata yote,”alisema Ernest.

  Pia alisema kwamba mizigo hiyo ambayo ilikuwa inasafirishwa kutokea maeneo ya kariakoo Jijijini Dar es Salaam kuelekea mikoa ya kusini ilikuwa na mapungufu makubwa kutokana na baadhi ya mizigo mingine ilikuwa haina risiti kabisa na baadhi ya mingine ilikuwa imekatiwa risiti kwa gharama ambayo ni ndogo ukilinganisha na bei iliyonunuliwa dukani.

  Kwa upande wake Afisa elimu na huduma kwa mlipa kodi wa TRA Mkoa wa Pwani Kapera Bakari amebainisha kuwa thamani ya awali ambayo wameifanya wamebaini mizigo hiyo ambayo ina jumla ya thamani ya shilingi milioni 84 imekwepa kulipiwa kodi kihalali ni zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 16 ambazo zilitakiwa kuingia serikalini.

  Aidha Kapera alibainisha kuwa serikali ya awamu ya tano kwa sasa ipo macho katika kuhakikisha inakusanya mapato yake hivyo amewaasa wafanyabiashara wote Mkoa wa pwani kuachana na tabia ya kununua mizigo dukani bila ya kuwa na risiti ya aina yoyote kwani kufanya hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa kupoteza mapato kutokana na tabia ya ukwepaji wa kulipa kodi kwa kutumia mashine za EFD.

  Mmoja wa madereva ambaye amekamatwa kutokana na kuhusika na tukio hilo ajulikanaye kwa jina la Hamis Abibu amesema kwamba mizigo ambayo alikuwa ameipakia katika gari yake akutambua lolote kama imenunuliwa bila ya kuwa na risiti ambazo zinastahili.

  Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga Sevelini Lalika ambaye nae alifika katika eneo la tukio ameipongeza TRA kwa juhudi wanazozifanya za kumuunga Rais wa awamu ya tano Dk,John Pombe Mgaufuli katika kuhakikisha wanakusanya kodi ipasavyo na kuwabana wale wote wenye tabia ya kukwepa kulipa kodi ya serikali kwa makusudi.

  MALORI hayo mawili ya magari ambayo yamekamatwa na TRA yamekutwa yamesheheni bidha mbali mbali zikiwemo mikeka, viatu, mashuka, baiskeli,sabuni, spea mbali mbali za pikipiki, zimeingiza hasara ya zaidi ya kisi cha shiingi milini 16 kutokana na kukwepa kulipa kodi kihalali.

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewataka maafisa maendeleo kutembelea vijijini ili kuhamasisha maendeleo katika kaya za vijiji kutokana baadhi vijiji kuwa nyuma kimaendeleo.

  Kutofika kwa watendaji kuhamasisha maendeleo kunasababisha wananchi kuona serikali haifanyi kazi. Amesema kuwa vijiji vikiwezeshwa vitaleta maendeleo kwa haraka kwani serikali ya awamu ya tano inaitaji kusonga mbele bila kumwacha mwananchi yeyote nyuma katika ukuaji wa uchumi.

  Akizungumza katika kijiji cha nyangunguti na Mkenge Kata ya Beta wilayani Mkurunga ,amesema maofisa wa maendeleo wanatakiwa kukimbizana na kasi ya maendeleo kwani muda wa kukaa ofisini umekwisha.

  Amesema ili kuimarisha serikali na kumsaidia Rais Dk.John Pombe Magufuli ,watendaji wawe chachu ya maendeo kwa kuwafikia wananchi moja kwa moja. Kwa upade wa wananchi wa kijiji cha Nyangunguti wamemuomba Naibu Waziri huyo kuendelea kuhamasisha maendeleo ili vijiji vikue kwa kasi

  Katika ziara ya Vijiji hivyo ameahidi kutoa Mifuko 130 ya saruji ,Mifuko 100 ikiwa ni sehemu ya kuchangia ujenzi wa shule mpya na 30 katika kijiji cha Mkenge kwa ajili sakafu ya shule ya kijiji hicho. Aidha ametoa fedha tasilimu sh.100000 kwa ajili wanafunzi yatima wa kijiji cha Nyangunguti.


  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Nyangunguti.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akisalimina na mmoja wa watoa huduma mara baada ya kuwasili katika Zahanati ya kijiji cha Mkenge Mkoa wa Pwani.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akionesha karatasi namna ya udanganyifu wa Korosho unaosababisha soko la zao hilo kuwa na tatizo.
  Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri Ulega .Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  0 0


  Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Capt Mstaaf George Mkuchika  amewataka Wabunge,madiwani na Viongozi wa Una wanaojihusisha na Biashara Na Halmashauri Kuacha Mara moja kutokana na Kwenda Kinyume na Sheria ya Viongozi Na watumishi wa Uma.

  Mkuchika Ameyasema hayo wakati akirejesha taarifa form za Rasilimali na Madeni katika Ofisi ya sekretarieti ya maadili ya Uma Kanda ya Kusini Iliyopo Mkoani Mtwara.

  Mpaka Kufikia Sasa Jumla ya Viongozi 794 ndio wamerejesha fomu za Rasilimali na Madeni kati ya Viongozi 1246 ambao wanatakiwa kuwasilisha.

  Aidha Ofisi Hiyo imetenga Siku ya Jumapili tareh 31 kuanzia Mchana mpaka Jioni Kupokea Taarifa kwa Viongozi ambao hawajawasilisha.
  Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Capt Mstafu George Mkuchika Akikabidhi Form za Rasilimali na Madeni kwa Katibu Msaidizi wa Tume ya serkretariet ya Maadili ya Utumishi wa Uma Kanda ya Kusini Mayina Henjewele.
  2.Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Capt Mstaafu George Mkuchika akionesha Form Mara baada ya kukabidhi Form zake na Kuhakikiwa.

  0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


   
   

  TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA KIGENI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa maagizo kuhusu matumizi ya fedha za kigeni katika  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusisitiza kuwa utekelezaji wake uanze  tarehe 1 Januari, 2018.  Maagizo hayo ni kama ifuatavyo: -

           i.            Bei zote hapa nchini zitangazwe kwa shilingi ya Tanzania. Bei hizi zinajumuisha kodi ya nyumba za kuishi na maofisi, bei ya ardhi, gharama za elimu na afya, bei za vyombo vya usafiri na vifaa vya kielektroniki.

         ii.            Bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au wateja wasio wakazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni. Bei hizi zinajumuisha gharama za usafirishaji kwenda nchi za nje kupitia Tanzania, gharama za mizigo bandarini kwenda nchi za nje, gharama za viwanja vya ndege na viza kwa wageni, na gharama za hoteli kwa watalii kutoka nje ya nchi. Walipaji wanaotumia fedha za kigeni watambuliwe kwa vitambulisho vyao kama pasi za kusafiria na nyaraka za usajili kwa makampuni.

        iii.            Viwango vya kubadilishana fedha vitakavyotumika katika kuweka hizo bei katika sarafu mbili viwekwe wazi na visizidi vile vya soko. Ifahamike wazi kuwa ni mabenki na maduka ya fedha za kigeni tu yanayoruhusiwa kupanga viwango vya kubadilisha fedha kutokana na ushindani katika soko la fedha za kigeni.

      iv.            Mkazi yeyote wa Tanzania asilazimishwe kulipia bidhaa au huduma yeyote hapa nchini kwa fedha za kigeni.

  Aidha Dkt. Mpango ameviagiza vyombo vya dola viwachukulie hatua za kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo haya ya Serikali.


  IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
  WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

older | 1 | .... | 1473 | 1474 | (Page 1475) | 1476 | 1477 | .... | 1897 | newer