Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1462 | 1463 | (Page 1464) | 1465 | 1466 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mradi wa Little Hearts wa nchini Saudi Arabia ambao ni moja ya mradi wa Afya ulioko ndani ya Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao Makuu yake mjini London nchini Uingereza zimefanya uchunguzi kwa watoto 131.

  Uchunguzi huo umefanyika katika kambi maalum ya siku sita ya matibabu ya moyo kwa watoto wenye umri wa kuanzia mwaka mmoja hadi miaka kumi na nne ilianza tarehe 10/12/2017 na kumalizika leo tarehe 15/12/2017.

  Kati ya watoto waliofanyiwa uchunguzi watoto 54 wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na 28 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na hali zao zinaendelea vizuri. Kupitia kipimo cha kuangalia mtoto aliyepo tumboni kama anatatizo la moyo au (Fetal Echocardiography) tulimpima mama mwenye ujauzito wa miezi minne na kugundua kuwa mishipa ya damu ya mtoto imepishana. Mama huyu yuko chini ya uangalizi wetu hadi pale atakapojifungua.

  Watoto waliofanyiwa uchunguzi na kufanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo. Mioyo ya watoto hao ina matundu na mishipa ya damu ya moyo haipitishi damu vizuri.Changamoto kubwa tuliyokabiliana nazo katika kambi hii ni upatikanaji wa damu na ufinyu wa chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwa wagonjwa ambao wanatoka katika chumba cha upasuaji.

  Tunawaomba wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi kuchangia damu. Mgonjwa anayefanyiwa upasuaji wa moyo anatumia kati ya chupa sita hadi saba za damu. Hivyo mahitaji ya damu ni makubwa kwa mgonjwa anayefanyiwa upasuaji wa Moyo.

  Kwa upande wa wazazi na walezi wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha Hospitali na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulika mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.Kwa wamama wajawazito wafanye uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya moyo.

  Tunawashauri watu wazima kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na hivyo kupata tiba kwa wakati. Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo katika matibabu ya wagonjwa wetu ni wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri.

  Taasisi inawashukuru sana wenzetu hawa wa Taasisi ya Msaada ya Muntada katika mradi wake wa afya wa Little Hearts kupitia Taasisi ya Kiislamu ya DHI NUREIN yenye makao yake Makuu mkoani Iringa kwa kutuwezesha kutoa huduma ya matibabu kwa watoto wetu. Hii ni mara ya nne kwa wenzetu hawa kuja katika Taasisi yetu na kutoa huduma tangu mwaka 2015 tulipoanza kufanya matibabu ya pamoja kwa watoto.

  Kwa mwaka huu wa 2017 hii ni kambi ya 15 na ni ya mwisho kufanyika. Tumefanya matibabu ya pamoja na washirika wetu kutoka mabara ya Asia, Australia, Ulaya na Amerika. Katika kambi zote hizo kambi za watoto ni tano na kambi za watu wazima ni 10. Jumla ya wagonjwa 120 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua kati ya hao watoto ni 80 na watu wazima ni 40.

  Aidha wagonjwa 169 walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Kati ya hawa watoto ni 93 na watu wazima 76.

  Kwa wagonjwa wote hawa 289 kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua hapa nchini Taasisi imeweza kuokoa zaidi ya bilioni 7 (Tshs. 7,225,000,000/=) ambazo Serikali ingezilipa kama wagonjwa hawa wangetibiwa nje ya nchi. Gharama za mgonjwa mmoja anayetibiwa nje ya nchi ugonjwa wa moyo ni zaidi ya milioni 25.

  Kwa namna ya kipeke tunaishukuru sana Serikali kwa kuhakikisha tunafanya kambi maalum za matibabu ya moyo katika Taasisi yetu na hivyo wagonjwa kupata huduma za matibabu kwa wingi. Licha ya wagonjwa kupata matibabu wataalam wetu wa afya wamekuwa wakijifunza mambo mbalimbali katika kambi hizi hii ikiwa ni pamoja na kubadilishana ujuzi wa kazi.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo, MAELEZO-DODOMA

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehamia rasmi Makao Makuu ya Nchi Dodoma leo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli alililitoa tarehe 25, Ju.

  Akizungumza wakati wa halfa ya kumkaribisha, Makamu wa Rais amesema kuwa mpaka sasa ni mwaka mmoja na nusu tangu tamko la kuhamia Dodoma litolewe hivyo Serikali ipo na inatekeleza majukumu yake.

  “Siku ya leo ilikuwa mawazoni mwangu, ninafurahi imefika na pia ninamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa maandalizi mazuri ya kunipokea ” Alisisitiza Mhe. Samia.Aidha, Mhe. Samia amesema kuwa Ofisi yake imekuja na agenda ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani hivyo wameandaa programu mbalimbali ikiwemo ya upandaji miti .

  “Tarehe 21, Disemba mwaka huu kutakuwa na shughuli ya upandaji miti hivyo tunaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma kutuunga mkono ili kuweza kutimiza azma hii” ameongeza Mhe. Samia.Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Baba wa Taifa aliweka nia ya Serikali kuhamia Dodoma tangu mwaka 1973 na leo Serikali ya Awamu ya Tano imetimiza ndoto hiyo.

  “Tunaendelea kuamini kwamba tamko la Rais linatekelezeka ambapo mpaka sasa watumishi 2816 tayari wameshahamia Dodoma na wanaendelea kutoa huduma za Serikali na kuanzia Februari mwaka 2018 tunaendelea kupokea watumishi wengine” amefafanua Waziri Mkuu.

  Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Pancras Ndejembi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza historia ya Mwalimu Nyerere ya Dodoma kuwa Makao Makuu.

  “Sikuwaza kama kuna siku Makao Makuu yatakuwa Dodoma kwa sababu siku nyingi mambo haya yanazungumzwa sasa yamekamilika kwa vitendo, leo nina furaha sana kuona ndoto ya tangu mimi kijana imetimia” ameongeza Mzee Ndejembi.

  Kwa upande wake Balozi Job Lusinde amesema kuwa “leo Makamu wa Rais anahamia Dodoma, kweli Mungu hupanga na Mungu huweka wakati wake, leo imekuwa”.

  Mbali na hayo Balozi Job Lusinde amesema kuwa Makamu wa Rai amekuja kipindi ambacho Mkoa wa Dodoma unaanza kuandaa mashamba kwa ajili ya kulima, hivyo kumpatia jina la kabila hilo “Mbeleje” likimaanisha kipindi cha kuandaa mashamba.
  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiwa na na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Januari Makamba wakicheza ngoma ya Mwinamila wakati wa Makaribisho ya Makamu wa Rais Mkoani Dodoma leo Desemba 15,2017.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

  0 0


  Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia-TBL, Bw. Roberto Jarrin ambaye ameahidi kuwa kampuni yake itajenga kiwanda kikubwa cha bia kitakachogharibu takriban dola milioni 100 za Marekani, mkoani Dodoma.

  Jarrin ameeleza kuwa hatua hiyo inalengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.Amesema kuwa mafanikio makubwa ambayo kampuni yake imeyapata hapa nchini hasa baada ya kubadilisha ujazo wa kinywaji chake kimoja umeifanya Kampuni yake ifikirie kuongeza uzalishaji kwa kuongeza kiwanda kingine mkoani humo.

  Bw. Jarrin amebainisha kuwa upanuaji wa huduma zake nchini utakwenda sambamba na kuendeleza kilimo cha mazao yanayotumika kutengenezea vinywaji hususan shayiri ama ngano hatua ambayo itawanufaisha wakulima nchini.Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameuelezea mpango huo wa TBL kwamba utachochea ukuaji wa uchumi na ajira kwa wananchi.

  “Tunataka kujenga Tanzania ya viwanda, na TBL ni kiwanda ambacho kitanipa ajira kwa Watanzania, kitanipa kipato zaidi, lakini pia nataka Dodoma iwe kitovu kingine cha uchumi kwa kutupatia mapato kama ilivyo Dar es Salaam inayochangia zaidi ya asilimia 80 ya mapato ya Serikali” alisema Dkt. Mpango.Ameunda timu ya wataalamu itakayopitia na kuchambua masuala mbalimbali ya kikodi na kisera yaliyowasilishwa na kampuni hiyo ili yafanyiwekazi haraka kwa manufaa ya pande hizo mbili.

  “Ameahidi kuwekeza kiwanda chenye thamani ya Dola milioni 100 na ili aweze kufanya hivyo amehitaji ajue msimamo wa Serikali kuhusu kupunguza gharama za uendeshaji ikiwemo kodi na mambo mengine ambayo tutayafanyiakazi” Alisisitiza Dkt. Mpango

  Dkt. Mpango amesema kuwa ameweka utaratibu wa kukutana na wawekezaji wengine wanaozalisha vinywaji baridi na vikali ili kufungua wigo zaidi wa majadiliano ili kukuza uwekezaji hapa nchini kwa kuangalia na kujadiliana kuhusu vikwazo na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin, alipokuwa anamueleza nia ya Kampuni hiyo kuwekeza mkoani Dodoma, alipomtembelea Dkt. Mpango ofisini kwake mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akimsikiliza Kamishna Msaidizi-Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi akifafanua jambo wakati Waziri Mpango, alipokutana na kufaya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bw. Roberto Jarrin, uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin, akifafanua jambo wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.


  Watumishi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakichukua kumbukumbu wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin (hawapo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bw. Roberto Jarrin (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania-TBL, Bw. Roberto Jarrin, (katikati) akifafanua jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango


  ………..

  0 0  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi Ikulu ya Kilimani, mjini Dodoma. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati akiwasili kwenye hafla fupi ya kumkaribisha kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba wakati akiwasili kwenye hafla fupi ya kumkaribisha kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akicheza ngoma ya Kigogo pamoja na wasanii wa kikundi cha Hiari ya Moyo Mwinamila wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitamka kukubali karibu ya kuhamia Dodoma akishuhudiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa picha ya pamoja na ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya kuhamia kwenye makazi yake mapya Kilimani, mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa picha ya pamoja na ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya kuhamia kwenye makazi yake mapya Kilimani, mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin, alipokuwa anamueleza nia ya Kampuni hiyo kuwekeza mkoani Dodoma, alipomtembelea Dkt. Mpango ofisini kwake mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akimsikiliza Kamishna Msaidizi-Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi akifafanua jambo wakati Waziri Mpango, alipokutana na kufaya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bw. Roberto Jarrin, uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin, akifafanua jambo wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.


  Watumishi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakichukua kumbukumbu wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin (hawapo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bw. Roberto Jarrin (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania-TBL, Bw. Roberto Jarrin, (katikati) akifafanua jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango


  ………..


  Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma


  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia-TBL, Bw. Roberto Jarrin ambaye ameahidi kuwa kampuni yake itajenga kiwanda kikubwa cha bia kitakachogharibu takriban dola milioni 100 za Marekani, mkoani Dodoma.

  Jarrin ameeleza kuwa hatua hiyo inalengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.Amesema kuwa mafanikio makubwa ambayo kampuni yake imeyapata hapa nchini hasa baada ya kubadilisha ujazo wa kinywaji chake kimoja umeifanya Kampuni yake ifikirie kuongeza uzalishaji kwa kuongeza kiwanda kingine mkoani humo.

  Bw. Jarrin amebainisha kuwa upanuaji wa huduma zake nchini utakwenda sambamba na kuendeleza kilimo cha mazao yanayotumika kutengenezea vinywaji hususan shayiri ama ngano hatua ambayo itawanufaisha wakulima nchini.Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameuelezea mpango huo wa TBL kwamba utachochea ukuaji wa uchumi na ajira kwa wananchi.

  “Tunataka kujenga Tanzania ya viwanda, na TBL ni kiwanda ambacho kitanipa ajira kwa Watanzania, kitanipa kipato zaidi, lakini pia nataka Dodoma iwe kitovu kingine cha uchumi kwa kutupatia mapato kama ilivyo Dar es Salaam inayochangia zaidi ya asilimia 80 ya mapato ya Serikali” alisema Dkt. Mpango.Ameunda timu ya wataalamu itakayopitia na kuchambua masuala mbalimbali ya kikodi na kisera yaliyowasilishwa na kampuni hiyo ili yafanyiwekazi haraka kwa manufaa ya pande hizo mbili.

  “Ameahidi kuwekeza kiwanda chenye thamani ya Dola milioni 100 na ili aweze kufanya hivyo amehitaji ajue msimamo wa Serikali kuhusu kupunguza gharama za uendeshaji ikiwemo kodi na mambo mengine ambayo tutayafanyiakazi” Alisisitiza Dkt. Mpango

  Dkt. Mpango amesema kuwa ameweka utaratibu wa kukutana na wawekezaji wengine wanaozalisha vinywaji baridi na vikali ili kufungua wigo zaidi wa majadiliano ili kukuza uwekezaji hapa nchini kwa kuangalia na kujadiliana kuhusu vikwazo na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

  0 0


  0 0


  Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla Ulega jana amekamata samaki aina ya sangara wachanga na wazazi tani 11 waliokuwa wakitoroshwa kwenda nchi jirani ya DRC kwa kukwepa kulipa kodi.

  Samaki hao tani 11 walitakiwa kulipiwa ushuru wenye thamani ya Tsh.99,000,000, badala yake wafanyabiashara hao wa kikongo walikwepa kulipa ushuru huo kwa kuchukua kibali kinachoonesha samaki hao wanaenda kuuzwa Tunduru mkoani Ruvuma

  Akizungumza na uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mhe Ulega amesema kuwa watumishi wa serikali watangulize Uzalendo katika nafasi zao wanazozitumikia kuliko kuendekeza rushwa."Jamani naombeni sana msimamieni sheria Ili kulinda Rasilimali zetu zisitoroshwe kwenda nje bila kulipiwa Kodi,tumuunge Mkono Rais wetu John Pombe Magufuli katika kuhakikisha Rasilimali hizi zinawanufaisha wananchi na sio watu wachache"alisema.

  Ulega aliesma ni kinyume cha sheria kuvua samaki wachanga na wazazi, na ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Ilemela kwa kupitia Mkurugenzi wake kuhakikisha wanasimamia sheria ipasavyo na hakuna samaki wachanga na Wazazi kuvuliwa.

  "Ikitokea wakati wa ukaguzi wenu mmekamata samaki wachanga au wazazi taifisheni na sheria ichukue mkondo wake kwa yoyote anayehusika au anayevunja sheria kwa kujua au kutokujua"alisema Ulega.Katika hatua nyingine Mhe. Naibu Waziri Abdalla Ulega alipata fursa ya kuhutubia wafanyabishara katika soko hilo,mara nyingi Naibu Waziri alikatishwa hotuba yake kwa kushangiliwa na umati mkubwa wa wafanyabiashara waliokusanyika sokoni hapo.

  Aidha wafanyabiashara hao walimweleza Naibu Waziri changamoto wanazokumbana nazo hapo sokoni ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maji safi na salama na ubovu wa miundombinu ya vyoo katika soko hilo.

  Mhe.Ulega amempa siku tatu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bw.John Wanga kuhakikisha maji na miundombinu ya vyoo sokoni hapo inashugulikiwa ndani ya siku tatu."Mkurugenzi nakuagiza kufikia Jumatatu Decemba 18 changamoto ya maji safi na Salama na Miundombinu yote ya vyoo vya soko hili viwe vimepatiwa Ufumbuzi".Alisema Ulega.
   .Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi, Abdalla Ulega akipima ulefu mmoja wa Samaki waliokamatwa tani 11 wakisafirishwa kinyume na taratibu mkonani katika soko la Samaki la Kimataifa (Mwaloni-Kirumba) jijini Mwanza.
   Naibu Waziri wa  Mifugo na  Uvuvi, Abdalla Ulega akifafanua jambo mbele ya watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
   Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi, Abdalla Ulega akizungumza na wafanya biashara wa katika  soko la Samaki la Kimataifa (Mwaloni-Kirumba) jijini Mwanza.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akiwa akisalimiana na wafanyabiashara katika soko hilo. Picha  zote  na Emmanuel Massaka,MMG Mwanza.

  .Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akikagua miundo mbinu ya maji katika soko hilo na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bw.John Wanga kufikia Jumatatu Decemba 18 changamoto ya maji safi na Salama na Miundombinu yote ya vyoo vya soko hilo viwe vimepatiwa Ufumbuzi

  0 0

  Jengo la shule ya wavulana Bwiru baada ya kufanyiwa ukarabati.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ukarabati wa shule ya sekondari Ngaza mkoani Mwanza.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza na walimu wa shule ya Ngaza.
  Wanafunzi wa shule ya Ngaza wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo ya ujenzi wa jengo jipya katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana.
  Mafundi wakijenga jengo la Hospitali ya wilaya ya Nyamagana.


  Zoezi la ukarabati wa shule kongwe 89 hapa nchini limeonyesha kupandisha hamasa ya wanafunzi kimasomo kutokana na kubadilika kwa mazingira ya kujifunzia kuwa bora zaidi ikilinganisha hali ya awali kabla ya ukarabati huo ulipokuwa haujaanza.

  Hali hiyo imebainika wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipotembelea shule ya wavulana Bwiru pamoja na shule ya Ngaza zilizopo mkoani mwanza. 

  Katika ziara hiyo ,Jafo amepata nafasi ya kuongea na wanafunzi wa Ngaza ambao walimhakikishia Waziri Jafo kwamba watafanya vizuri zaidi katika mitihani yao kwani kwasasa wamepata amani kubwa na hamasa tele.

  Ukarabati wa shule hizo umehusisha ukarabati wa madarasa, mabweni, vyoo, bwalo za chakula, maktaba, maabara, pamoja na mifumo ya maji na umeme.Katika hatua nyingine,Waziri Jafo amepongeza jiji la Mwanza kwa kuanza ujenzi wa jengo la ghorofa kwa ajili ya wodi ya wanaume katika hospitali ya wilaya ya Ngamagana.

  Ujenzi wa jengo hilo umeanza kwa kutumia mapato ya ndani ya jiji hilo na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai 2018.Jengo hilo linajengwa na mkandarasi Mzinga Company ambapo mpaka sasa ujenzi huo unaenda vizuri.

  Katika mradi huo, Jafo amezitaka Halmashauri zingine kuiga mfano huo ili kupunguza changamoto za miundombinu katika hospitali za wilaya.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde amewataka vijana wasomi wa nchi kuwa mstari wa mbele kuunga mkono kazi nzuri na kubwa anayofanya Rais John Magufuli katika kupambana na Rushwa, Ufisadi na Udhalimu.

  Mavunde ameyasema hayo jana katika ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre-Dar es salaam wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya Viongozi wa Vyuo vikuu nchini juu ya masuala ya Maadili ya viongozi na rushwa.

  Amehimiza Vijana wasomi kutambua nafasi yao katika Jamii na kutambua kwamba Taifa hili linawategemea kwa ustawi wake hivyo lazima wawe mstari wa mbele kuhakikisha kwamba tunajenga Taifa la Vijana wenye maadili lakini pia Vijana ambao watakuwa mstari wa mbele katika kupambana na Rushwa na aina yoyote ya udhalimu.

  Aidha,Mwenyekiti wa Tahliso Stanslaus Peter Kaduguze amewashukuru Taasisi ya Uongozi kwa kufanikisha mafunzo hayo ambayo anaamini yamebadilisha fikra na mtizamo wa Vijana wengi wasomi juu ya masuala ya Maadili na Vita dhidi ya rushwa.

  0 0  Wafanyakazi wa hoteli ya Southern Sun wakishiriki michezo na wazazi wa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs) 
  Father Christmas akitoa zawadi mmoja wa wazazi wa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. 
  Father Christmas akitoa mhudumu wa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. 
  Father Christmas akitoa zawadi mmoja wa wazazi wa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. 
  Father Christmas akitoa zawadi mmoja mfanyakazi wa kujitolea kutoka nchini Marekani, Christine Corcoran katika hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na wafanyakazi wa Hoteli ya Southern Sun kwa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. 
  Father Christmas akitoa zawadi mmoja wa wazazi wa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. 
  Father Christmas akitoa zawadi mmoja wa wazazi wa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. 
  Father Christmas akitoa zawadi kwa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. 
  Father Christmas akitoa zawadi mmoja wa wazazi wa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. 
  Father Christmas akitoa zawadi mmoja wa wazazi wa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. 
  Wafanyakazi wa hoteli ya Southern Sun wakishiriki michezo na wazazi wa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. 
  Wafanyakazi wa hoteli ya Southern Sun wakishiriki michezo na wazazi wa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. 
  Wafanyakazi wa hoteli ya Southern Sun wakishiriki michezo na wazazi wa watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. 
  Wafanyakazi wa hoteli ya Southern Sun wakiwahudumia chakula watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, Disemba 15 2017. 
  Mfanyakazi wa hoteli ya Southern Sun wakiwahudumia chakula watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, Disemba 15 2017. 
  Wafanyakazi wa hoteli ya Southern Sun wakiwahudumia chakula watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, Disemba 15 2017. 
  Wafanyakazi wa hoteli ya Southern Sun wakiwapatia zawadi watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, Disemba 15 2017. 


  Wafanyakazi wa hoteli ya Southern Sun wakiwahudumia chakula watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, Disemba 15 2017. 


  Father Christmas akitoa zawadi mmoja wa wafanyakazi wa wa kujitolea kwenye watoto wenye saratani wanaopata matibabu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania jijini Dar es Salaam leo, baada ya kupata mlo wa mchana. (Kuhusu Tumaini la maisha Tanzania, link www.wearetlm.org
  0 0

  Na Judith Mhina - MAELEZO

  Mojawapo ya sababu zinazowakosesha Wakulima kupata mazao mengi shambani ni viumbe hai waharibifu ambao hushambulia mbegu au mazao yenyewe kabla na baada ya kuvunwa. 

  Kutokana na hali hii uzalishaji wa mazao shambani unapungua na pia kiasi kidogo kinachopatikana baada ya kuvuna nacho hupungua kutokana na viumbe hao waharibifu kuendelea kuharibu kikiwa ghalani. Aidha, hali hii kuwakosesha Wakulima kipato chao na Taifa kwa ujumla.

  Kwa mujibu wa mtafiti kutoka Kituo cha Viumbe Hai Waharibifu wa Mazao na Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - SUA, Dkt. Christopher Sabuni, aliyenukuliwa kupitia kipindi cha "Ukulima Bora" kinachorushwa na TBC FM, viumbe hai waaribifu wa mazao wapo wengi na wamegawanyika katika makundi tofauti kama vile wanyama, wadudu, na ndege.

  Amewataja viumbe hai waharibifu katika mazao ya kilimo wanaotambulika sana na wakulima hapa nchini ni pamoja na panya, kupe, dumuzi, mdudu Cytophilus au tembo, viroboto, kupe, mmbu na wengineo.Amesema, jukumu la Kituo cha Viumbe Hai Waharibifu wa Mazao ni pamoja na kufanya tafiti mbalimbali zitakazosaidia kuokoa mazao ya wakulima yasiharibiwe na wadudu ili kumwezesha mkulima kupata mazao mengi zaidi.

  Kutokana na jukumu hilo, Kituo hicho kimefanya utafili wa kudhibiti panya waharibifu wa mazao ambapo kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo asilimia 40 ya mazao mashambani yataokolewa. Dkt. Sabuni amesema utafiti huu una manufaa mengi kwa mkulima ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya ufundishaji na udhibiti wa uharibifu wa mazao. 

  "Hata hivyo, tunalenga kutoa elimu kwa mkulima ni kwa jinsi gani anaweza kupunguza hasara ili aweze kufaidika na nguvu zake kwa kuvuna chakula kingi iwezekanavyo,"amesema.

  Akifafanua zaidi kuhusu wanyama waharibifu amesema, kuna aina 2276 za panya ambao hupatikana karibu sehemu nyingi duniani. Hawa ni wanyama ambao hunyonyesha isipokuwa aina chache sana ambao hazipatikani maeneo mengine. Panya wenye kutia hasara ni wale wanaokula nafaka, matunda na mazao aina ya mizizi kama mihogo, viazi nk.

  Panya wenye kutia hasara kubwa barani Afrika hususani kusini mwa Jangwa la Sahara ni wale wanaokula nafaka, viazi na pamba. Panya hawa hujulikana kwa jina la Shambarat au mutmanitret. Aidha, panya hawa wana matiti mengi na ustawi sana mashambani na kwenye mapori. Wana uwezo wa kuzaa watoto 20 kwa wakati mmmoja na huongezeka kwa wingi.
  Kutokana na wingi wao wanao uwezo wa kula mbegu zikiwa shambani wakati wa kupanda maana zinatoa harufu na kuwa kichocheo kinachowafanya kufuatilia na pia zinapokuwa zimehifadhifa ghalani. 

  Aina nyingine ya panya ni wale wanaoishi majumbani katika paa la nyumba ambao hujulikana kwa jina la Roofrat. Aina nyingine ya panya wa ndani ni Ratus ratus wanaoishi ghalani lakini pia huweza kutoka nje na kula lakini mara nyingi hukaa ndani. 
  Fuko ni aina nyingine ya panya anayeshinda kwenye mashimo na kula mazao ya mizizi kama vile mihogo, viazi na mizizi mingine ya porini. Panya huyu ambaye haoni anatumia sana kunusa kuweza kutambua chakula. Akitoka nje ya shimo inakuwa vigumu kutembea kutokana kuwa katika mazingira mageni. Fuko anatofautiana na panya wengine kwani ni mkubwa kwa umbo. 

  Aina nyingine ya panya ni wale wenye rangi mweupe ambao mara nyingi wanatumiwa katika maabara. Panya hawa ambao ni wadogo ukilinganisha na wengine wanakosa rangi ya asili huzalishwa kwa wingi kwa ajili ya kutumika katika tafiti mbalimbali. 

  Panya wengi wanatofautiana kwa maumbile na maeneo wanayoishi. Panya mkubwa zaidi ana uzito wa kilo 25 na hupatikana nchini Australia, mdogo ana gram 4. 


  Udhibiti wa panya

  Kwa mujibu wa Dkt Christopher Sabuni, kuna aina mbalimbali za kuweza kudhibiti panya waharibifu. Njia ya kwanza ni kuhakikisha kwamba shamba linakuwa safi. Fanya usafi mita 10 kutoka katika shamba lako ili panya wakose eneo la kujificha kutoka katika mpaka wa shamba. Kutokana na usafi huu shamba lako linakuwa vigumu kuvamiwa na panya kwa sababu watakosa sehemu ya kujificha, kuzaliana na kutengeneza makao.

  Pili, kutumia viatilifu ambavyo vinanyunyuziwa kwenye mashamba. Hata hivyo utafiti unaendelea kuweza kupata viatilifu vitakavyolenga kuangamiza panya tu. Kwa sasa viatilifu vilivyopo vinaua hata wale wasio waharibifu. Vile vile, utafiti huo unalenga kupata viatilifu ambavyo havitakuwa na madhara kwa binadamu.

  Tatu, utafiti huo umegundua matumizi ya vidonge vya uzazi kwa panya waaribifu wa mazao. Vidonge hivyo vyenye harufu ya kuwavutia huwekwa katika maeneo ambayo yataonekana kuwa ni makazi yao na hivyo watakapokula watakuwa wamepunguzwa uwezo wa kuzaana.

  Nne, matumizi ya mifuko sahihi isiyopitisha hewa na kufanya mazao kuwa salama unapohifadhi nafaka iitwayo Hemetic Bags. Mifuko hiyo imetengenezwa bila kutumia dawa ya aina yeyote. Unapoweka nafaka ndani ya mfuko na kuufunga bila ya kupitisha hewa, harufu ya nafaka haitoki na hivyo panya wanashindwa kujua kama kuna nafaka ndani yake na kushambulia mfuko.

  Mifuko hiyo ambayo inatengenezwa mkoani Tanga imeanza kutumiwa na wakulima wa mikoa ya Njombe, Morogoro, Mbeya na Iringa. Aidha, wajasiriamali wanaagiza mifuko hiyo kupitia Halmashauri zao kulingana na mahitaji yao.

  Tano, udhibiti wa panya hufanywa kwa kutumia mtego aina ya Treebit Beilar System - TBS. Mtego huu unaotoa harufu inayowavutia huwekwa katika eneo dogo la shamba lililopandwa mazao kama sehemu ya kuwatega na kuwakamata (catching point). Unapoona idadi ya panya imepungua sasa unaweza kupanda shamba zima uliloliandaa.

  Kwa mujibu wa utafiti wa Kituo cha Viumbe Hai Waharibifu wa Mazao, pia wapo panya ambao wanakula majani tu. Panya hao ni waharibifu kwenye bustani za makazi ya watu au bustani. Mkulima anayezingatia na kutumia mbinu zilizoelezewa na Kituo hiki, atafaidika katika kuokoa asilimia 40 ya mazao yake ambayo yangepotea na kujiongezea kipato cha familia yake na Taifa kwa ujumla.

  0 0

  Na Mathias Canal, Kilimanjaro

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya serikali iliyopewa jukumu la Kusimamia sekta ya Kahawa nchini Ndg Primus Kimaryo ameagizwa kusimamia na kuwalipa haraka wakulima malipo mara baada ya kukusanya mazao yao kwani kufanya hivyo kutawezesha mazingira mazuri ya biashara na kuwanufaisha wakulima kutokana na kilimo hicho.

  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ametoa agizo hilo jana Disemba 15, 2017 alipotembelea Ofisi za Bodi ya Kahawa akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Kilimanjaro.Mhe Mwanjelwa alisema kuwa pamoja na wakulima kuuza kahawa kwa bei ya shilingi 5000 kwa kilo katika msimu wa mwaka 2016/2017 lakini bado changamoto ni kubwa ya ucheleweshaji wa malipo kwa wananchi jambo ambalo linarudisha nyuma ufanisi wa zao.

  Alisema miongoni mwa kazi kubwa ya Bodi ya Kahawa nchini ni pamoja na kulinda maslahi ya wakulima dhidi ya makundi mbalimbali yanayofanya biashara ya zao la kahawa hivyo kucheleweshwa kulipwa malipo yao ni ishara ya Bodi hiyo kutotekeleza majukumu yake ipasavyo.Aidha, Kaimu Mkurugenzi huyo wa Bodi ya Kahawa ametakiwa kuwa na mikakati imara na yenye tija itakayolifanya zao la kahawa kuwa na ubora zaidi Duniani kwa kwa kuliongezea thamani.

  Katika ziara hiyo pia Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alitembelea chuo cha mafunzo ya Kilimo Cha Kilimajanro (KATC-Kilimanjaro Agricultural Training College) ambapo ameupongeza uongozi wa Chuo hicho kwa kuwawezesha zaidi ya wakulima 7000 katika skimu zaidi ya 100 kuboresha kilimo cha mpunga na mazao mengine hivyo kupata ongezeko kubwa la mazao.

  Sambamba na pongezi hizo pia amewataka kuongeza ufanisi katika utendaji ili kuunga mkono kwa vitendo serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii, ufanisi, na ubunifu.

  Aliwasisitiza wananchi hao kutofanya kazi kwa mazoea badala yake kuwa wabunifu katika kazi ikiwa ni pamoja na kuzikabili changamoto na kuzigeuza kuwa fursa.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikaanga kahawa mara baada ya kutembelea Kitengo cha kukaanga Kahawa katika Ofisi za Bodi ya Kahawa akiwa ziarani Mkoani kilimanjaro, Jana 15 Disemba 2017. Picha Zote na Mathias Canal
  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua namna kahawa zinazohifadhiwa mara baada ya kutembelea Maabara ya kuandaa kahawa kwa ajili ya wanunuzi katika Ofisi za Bodi ya Kahawa akiwa ziarani Mkoani kilimanjaro, Jana 15 Disemba 2017
  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kuhusu uendeshaji wa mnada wa kahawa kwa mfumo wa kisasa Kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Ndg Primus Kimaryo alipotembelea Ofisi za Bodi ya Kahawa akiwa ziarani Mkoani kilimanjaro, Jana 15 Disemba 2017
  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwasili katika chuo cha mafunzo ya Kilimo Kilimajaro (KATC) wakati wa ziara ya kikazi Mkoani humo, Jana 15 Disemba 2017.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua miongoni mwa mashamba ya kufundishia kilimo cha mpunga mara baada ya kikao na watumishi wa chuo cha mafunzo ya Kilimo Kilimajaro (KATC) wakati wa ziara ya kikazi Mkoani humo, Jana 15 Disemba 2017

  0 0

   Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile aliyevaa shati la drafti akikagua na kutoa maelekezo juu ya upatikanaji wa dawa katika baadhi ya vituo vya afya katika Wilaya ya Meru wakati wa ziara yake mkoani Arusha. 
  Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile aliyevaa shati la drafti akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa katika vituo vya afya katika Wilaya ya Meru wakati wa ziara yake mkoani Arusha.
  Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa pili kulia akisikiliza maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meru Dkt. Cosmas Kilasara wa kwanza kulia kwenye moja ya jengo la Hospitali ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha.PICHA NA ALLY DAUD-WIZARA YA AFYA MERU ARUSHA


  Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru TICD wakitoa chngamoto na maswali kwa Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati alipotembelea chuo hiko katika ziara yake mkoani Arusha. 
  Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya mtumishi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii cha Tengeru (TICD) wakati alipotembelea chuo hiko katika ziara yake mkoani arusha.
  Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati akionyeshwa mpaka wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru TICD wakati alipotembelea chuo hiko katika ziara yake mkoani Arusha
  Baadhi ya Watumishi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru TICD wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati alipotembelea chuo hiko katika ziara yake mkoani Arusha.

  0 0

   
  Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta mabadiliko hayo ikiwemo ujenzi na ukarabati wa choo na jengo hilo,kama jengo lionekanavyo pichani juu na juu  Waziri Ummy akikagua choo hicho
  Waziri Ummy Mwalimu akipokea mabango kutoka kwa wananchi yenye jumbe mbalimbali kuhusiana na changamoto za Afya, wakati alipokuwa akitembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika mikoa nane nchini.
   Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akimwelekeza mmoja wa Wazee waliopata vitambulisho vya Matibabu bure kwa Wazee wakati wa tukio hilo mapema leo Wilayani Rufiji.
    Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akimkabidhi mmoja wa Wazee kitambulisho cha Matibabu bure kwa Wazee wakati wa tukio hilo mapema leo Wilayani Rufiji.
    Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwakabidhi baadhi ya Wazee vitambulisho vya Matibabu bure kwa Wazee wakati wa tukio hilo mapema leo Wilayani Rufiji.

     Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akishangiliwa vilivyo na Wananchi wa Rufiji .
  Na.WAMJW-Rufiji.

  Utekelezaji wa mpango wa malipo kwa ufanisi(RBF) Wilayani Rufiji umeleta mabadiliko makubwa katika Vituo vya afya na Zahanati kwa uboreshaji wa miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa muhimu

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika mikoa nane nchini

  Waziri Ummy alisema mabadiliko hayo katika sekta ya afya yamefanyika katika maeneo ya utoaji huduma,Uongozi na Utawala,Rasilimali watu,Mifumo ya usimamizi wa utoaji taarifa za afya,madawa na teknolojia ya afya ambapo mfumo huo umesaidia maboresho, uwajibikaji,ufanisi na usawa kwani dhana hiyo inamfanya mtoa huduma kulipwa kulingana na matokeo ya kazi yake ambayo amehakikiwa na hivyo kufanya vituo hivyo kuongeza hali ya upatikanaji wa dawa na kuboresha miundombinu ya vituo hivyo

  "Tumeanza mpango huu katika mikoa 8,tumefanya tathimini kwenye vituo vya afya na zahanati zote za Mkoa wa Pwani ikiwemo Wilaya ya Rufiji,tukabaini vituo vya afya na zahanati hazikuwa na viwango vya ubora unaotakiwa, tukaona tuwapatie  shilingi milioni 10 kila kituo vilivyokidhi kwa ajili ya kuboresha miundombinu"alisema Waziri ummy.

  Hata hivvyo aliipongeza kamati ya afya ya kijiji cha Nyamwage kwa kutumia ipasavyo shilingi milioni 10 kwa kuongeza urefu wa paa na kupaua,kuweka malumaru na kuongeza matundu ya choo pamoja na tundu moja la choo kwa ajili ya walemavu"nikupongeze mganga mfawidhi kwa kuboresha zahanati hii kwakweli unapaswa kupongezwa kwani umefanya vizuri ila badilika lugha chafu kwa wananchi haitakiwi,nakupa mwezi mmoja ila kwa upande huu mwingine umenifurahisa,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni"

  Aidha ,alitoa wito kwa wanawake  kuhudhuria kliniki pale wanapohisi kuwa wajawazito na hasa mahudhurio yote manne ili kuweza kujua hali zao kiafya na kuweza kupata matibabu pale wanapogundulika na matatizo na kujifungua salama"hatutaki kuona mwanamke mjamzito anafariki wakati wa kujifungua,ndiyo maana serikali ya awamu ya tano imeboresha huduma za afya na tumeanza ujenzi wa vyumba vya upasuaji wa dharura kwa mwanamke atakayepata uzazi pingamizi,kujifungua salama ni haki ya kila mwanamke mjamzito

  Akisoma taarifa ya  Wilaya,Mkuu wa Wilaya ya Rufiji  Mhe.Juma Njwayo alisema mpango wa malipo kwa ufanisi umeongeza idadi ya akina mama wanaojifungulia kwenye zahanati na kutoka 3,382 mwaka 2016 hadi kufikia 4,086 mwaka 2017 na wanawake wanaohudhuria mahudhurio  manne kliniki wamefikia 3,955 mwaka 2017 kutoka 1,906 mwaka 2016.

  "Hali ya upatikanaji dawa muhimu hivi sasa ni asilimia 91 na dawa zingine ni zaidi ya asilimia 50 na hii inachangiwa na mpango huu"alisema Mhe. Njwayo.

  Malipo kwa ufanisi (RBF) wilayani Rufiji ulianza kutekelezwa mwaka 2016 kwa kupatiwa shilingi milioni 240 kutoka wizara ya afya na kila kituo cha afya ama zahanati kilipatiwa shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuboresha miundombinu na inatekelezwa kwenye vituo kumi na mbili ambavyo vilikidhi vigezo vya mpango huo.

  0 0

  Msimamizi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Pangani kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Mahenda S. Mahenda (kulia) akitoa maelezo kuhusu uzalishaji wa umeme katika kituo hicho kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) katika ziara aliyoifanya mapema leo tarehe 15 Desemba, 2017 katika kituo hicho.
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Pangani mapema leo tarehe 15 Desemba, 2017
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ( wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika ziara hiyo.


  Na Greyson Mwase, Tanga

  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka wakandarasi wanaojenga miundombinu ya usambazaji wa umeme vijijini chini ya Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kuongeza kasi ili miradi yote iweze kukamilika ifikapo mwaka 2019.

  Mgalu aliyasema hayo mapema leo tarehe 15 Desemba, 2017 katika ziara yake aliyoifanya katika kijiji cha Bwitini wilayani Korogwe mkoani Tanga, lengo likiwa ni kukagua hatua ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini iliyopo chini ya REA Awamu ya Tatu na kutorishishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo.

  Katika ziara hiyo Naibu Waziri Mgalu aliambatana na watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

  Alisema kuwa, Serikali ilikwishawalipa wakandarasi wote malipo ya awali na kuwataka kuanza kazi mara moja lakini wamekuwa wakifanya katika kasi ndogo hususan katika hatua ya upembuzi yakinifu.

  “ Wakandarasi wengi wamekuwa wakichukua muda mrefu kutekeleza miradi kwa kisingizio cha kufanya upembuzi yakinifu wakati fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi zimekwishatolewa, nichukue fursa hii kuwatangazia wakandarasi wote nchini kuanza kazi mara moja,” alisema Mgalu

  Aliendelea kusema kuwa mkandarasi yeyote atakayefanya kazi kwa kiwango kisichoridhisha atanyang’anywa kazi na kupewa mkandarasi mwingine mwenye uwezo wa kufanya kazi kulingana na kasi inayotakiwa na Serikali.

  Alisema kuwa wananchi wengi kwa sasa hususan walipo katika maeneo ya vijijini wanahitaji nishati ya umeme kwa gharama nafuu, hivyo wamechoka na masuala ya michakato.

  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Mgalu aliwataka wakandarasi wote nchini kununua vifaa kutoka ndani ya nchi hususan transfoma na nguzo badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi kama ilivyoagizwa awali.

  Akielezea mikakati ya serikali katika uboreshaji wa upatikanaji wa umeme wa uhakika na kwa gharama nafuu, Mgalu alisema kuwa serikali kupitia REA Awamu ya Tatu inasambaza umeme katika vijiji vyote nchini ambapo ifikapo mwaka 2019 karibia vijiji vote vitakuwa na umeme wa uhakika.

  Aliendelea kuelezea mikakati mingine kuwa ni pamoja na matumizi ya nishati jadidifu kama vile jua hususan katika maeneo yasiyofikiwa na umeme kutoka Gridi ya Taifa, ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji wa Stieglers Gorge na mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa Kinyerezi I na Kinyerezi II.

  Alisisitiza kuwa serikali imeweka mkakati wa kufufua mkoa wa Tanga kiuchumi hivyo kuwataka wawekezaji ndani ya nchi kuwekeza kwenye viwanda katika mkoa huo.

  Alieleza kuwa kutokana na uwepo wa mradi mkubwa wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika mkoa wa Tanga, mahitaji ya umeme yatakuwa makubwa hivyo Wizara ya Nishati imejipanga katika kuhakikisha kuwa nishati ya uhakika inapatikana.

  Wakati huo huo Naibu Waziri Mgalu aliwataka wananchi wa Tanga kutoharibu vyanzo vya maji katika Bonde la Mto Pangani yanayotumiwa katika uzalishaji wa umeme katika kituo cha kufua umeme cha Hale ili kutoathiri uzalishaji wa umeme katika mkoa huo.

  Alisisitiza kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua hali za kisheria wananchi watakaobainika wanaharibu mazingira.

  0 0

  Serikali imeiagiza Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Shanta Mining Limited inayofanya shughuli zake Mkoani Singida kuharakisha ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha maeneo yao ili shughuli za uchimbaji zianze mara moja. 

  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alitoa agizo hilo Desemba 12, 2017 wakati wa ziara yake ya kutembelea migodi ya dhahabu katika wilaya za Ikungi na Manyoni ili kujionea shughuli zinazoendelea pamoja na kuzungumza na wachimbaji wa madini.

  “Mchakato wa fidia ufanyike haraka na mgodi uanze shughuli zake za uchimbaji mapema,” aliagiza Naibu Waziri Nyongo. 

  Akiwa njiani kuelekea kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Elizabeth Shango uliopo katika Kijiji cha Sambaru, msafara wake ulisimamishwa na wananchi katika Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi ambao walilalamika kuzuiwa kuendeleza maeneo yao na kampuni hiyo na huku wakicheleweshewa kulipwa fidia. 

  Walisema kuwa tayari wameachia maeneo waliyokuwa wakimiliki kwa kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kilimo na uchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu ili kupisha shughuli za uchimbaji mkubwa lakini Kampuni hiyo ya Shanta bado haijakamilisha ulipaji wa fidia.
   Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi waliosimamisha msafara wake (hawapo pichani) 
   Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani). 
   Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mbele katikati) akiwa nyumbani kwa Mzee Bastan Mtundwi (mbele kulia) na mkewe Esta Mtundwi ambao walijengewa Nyumba na Kampuni ya Shanta ikiwa ni fidia ya kupisha eneo.
   Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.


  0 0

  Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, akizungumza na wajumbe wa bodi mpya ya Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC), (hawapo pichani), wakati akiizindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam jana.
  Wajumbe wa bodi hiyo wakiwa katika hafla ya uzinduzi.
  Mwenyekiti wa bodi hiyo, Profesa, Egid Mbofu, akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Meneja Mkuu wa TFC, Salum Mkumba.
  Wajumbe wa bodi hiyo wakiwa bize kuchukua maagizo ya Waziri Mwijage.
  Waziri Mwijage akisisitiza jambo katika uzinduzi huo.
  Hapa ni kalamu zikizungumza katika uzinduzi huo wakati Waziri Mwijage alipokuwa akiipa majukumu bodi hiyo mpya ya TFC.
  Uzinduzi ukiendelea.
  Waziri Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi hiyo.


  Na Dotto Mwaibale


  WAZIRI wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, ameitaka Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) kubadilisha mfumo wa utendaji ikiwa ni pamoja na kutoingia mikataba inayoweza kuisababishia serikali hasara, badala yake kuangalia wabia wanaoweza kuisaidia kujipanua na kupata faida kubwa zaidi.

  Waziri Mwijage, aliyasema hayo juzi wakati akiizindua bodi mpya ya Wakurugenzi ya TFC, na kuongeza kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli, haiko tayari kuona taasisi zake za umma zikiingizwa katika mikataba mibovu na isiyokuwa na tija.

  Pia aliagiza kwamba, baada ya kuizindua bodi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Egid Mbofu na wajumbe wake, waanze kazi mara moja na moja ya majukumu yao ya awali ni kuangalia ama kuipitia upya miokataba ambayo awalo iliingiwa na TFC.

  Alisema TFC ikifanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kujielekeza kwenye kazi zenye faida kubwa, itaweza kusaidia kasi ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini, na kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya Taifa la uchumi wa kati na wa Viwanda.

  "Tunatambua sekta ya kilimo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uchumi wa TANZANIA, lakini haiwezi kuleta mafanikio makubwa kwa jamii, ikiwa TFC haitaweza kupewa uwezo na kuwafikia wakulima wengi zaidi", alisema Waziri Mwijage.

  Aliongeza kusema kwamba, mazingira ya sasa ya kilimo kwa Tanzania, yanahitaji umakini katika uagizaji wa mbolea zinazotumiwa na wakulima wengi ambao malengo yao ni kupata faida, lakini wamekuwa wakiangushwa na baadhi ya wafanyaviashara wanaoagiza mbolea feki.

  TFC ni mtoto wa serikal, hivyo nimeagizwa na mheshimiwa Rais, kuwaonoa hofu na kwamba tunahitaji kuiongezea uwezo ili Taifa liweze kufikia malengo ya uzalishaji mkubwa wa chakula pamoja na mazao mengine yanayohitajika kama malghafi katika viwanda.

  Kwa upande wake Profesa Mbofu, alimshukuru Waziri Mwijage na kumuahidi kwamba, wako tayari kwa kazi hiyo lakini pia akasema wamfikishie Rais shukrani zao kwa uaminifu wake kwao.

  "Ninaomba kwa niaba ya wajumbe wa bodi hii, menejimenti ya TFC kukushukuru kwa kazi hii nzuri na maagizo yako yote kwetu, tunakuahidi kuifanya kazi hii kwa uaminifu na uadilofu mkubwa na tutaendelea kuomba ushauri wako kila tunapohitaji kufanya hivyo kama njia ya kupata miongozo zaidi," alisema Profesa Mbofu.

  Meneja Mkuu (GM), Salum Mkumba, alimhakikishia Waziri Mwijage, kwamba TFC iko tayari kwa mabadiliko ya aina yeyote na wafanyakazi wako tayari kwa kusimamia maagizo kwa ajili ya kuendana na Tanzania ya Viwanda kulingana na sera na miongozo ya serikali ya awamu ya tano.

  Pia GM Mkumba, alisema TFC ni miongoni mwa taasisi za umma zilizo chini ya wizara ya Viwabda na Uwekezaji, ambazo tayari zilianzisha mabaraza ya wafanyakazi kwa ajili ya kuwashirikisha wafanyakazi na kuwajengea uwezo wa kushauri kasi ya maendeleo kwenye kampuni hiyo ya umma.

  0 0

  . Sekta ya utalii nchini Tanzania imetakiwa kukubali kuendana na mifumo mipya inayotokana na maendeleo ya TEHAMA katika uendeshaji wa huduma zao na kuwahudumia wateja ili kujiongezea thamani na kuleta tija zaidi kwenye biashara zao.
  Akizungumzia juu ya maendeleo ya mifumo ya kiteknolojia kwenye sekta ya utalii, Meneja Mkazi wa Jumia Travel Tanzania, ambayo ni kampuni inayojihusisha na huduma za hoteli kwa njia ya mtandao Afrika amebainisha kuwa tabia za wateja zinabadilika kwa kasi na zinachochewa na maendeleo ya tekinolojia duniani.

  “Hapo nyuma kidogo hoteli zilikuwa ni sehemu za malazi ambazo watu walikuwa wanakwenda kupumzika tofauti na mahali wanapoishi. Lakini sasa hivi mambo yamebadilika na kutoa wigo mpana kwani wateja hawaendi kwenye hoteli kupumzika tu bali kuwezeshwa kuendelea na shughuli zao kama kawaida. Shughuli hizo zinaweza kutegemea tekinolojia moja kwa moja au zisitegemee, kitu ambacho kimeifanya TEHAMA kuwa na umuhimu mkubwa kwa mameneja wa hoteli na kuwapatia uzoefu wateja juu ya huduma mbalimbali,” alisema Bw. Gerniers.

  “Karibu ujihudumie. Leo hii, wateja wengi hupendelea zaidi kutumia tekinolojia kujihudumia wenyewe na mambo madogomadogo kuliko kukutana na wahudumu hotelini moja kwa moja. Zipo huduma kadhaa zinazopendekezwa na wateja ambazo zinaweza kuwekwa kwenye mifumo ya kitekinolojia na kujiendesha zenyewe. Hii itaweza kusaidia kuwapunguzia mzigo wa kazi mameneja na wahudumu wa hoteli na kuwaacha wateja wajihudumie wenyewe,” aliongezea.

  Akifafanua zaidi namna Jumia Travel inavyosaidia kurahisisha uendeshaji wa huduma za hoteli kwa mameneja, Meneja Mkazi huyo amesema kuwa, “Tumeutambulisha mfumo rahisi wa uendeshaji wa shughuli za hoteli unaojulikana kama Extranet. Tekinolojia hii ya kisasa inayotumika duniani kote humpatia fursa meneja uwezo wa kusimamia shughuli mbalimbali kama vile; kujulishwa mteja anapotaka huduma mara moja; kupitia taarifa za huduma iliyoombwa na mteja; kuperuzi au kutafuta huduma zilizoombwa; na kuthibitisha au kukataa ombi la mteja papo hapo,” alisema na kuhitimisha, “Kwa kuongezea, meneja anaweza kubadili au kurekebisha bei za vyumba na upatikanaji wake katika siku husika au zijazo pia. Lakini kupitia mfumo huu ni rahisi kuelewa tabia za wateja kama vile; kujulisha mara mteja anapotembelea na kutathmini hoteli yako; kujifunza kilichowavutia wateja na wanachofikiria nini kiboreshwe; na kupata takwimu za utendaji wa hoteli kwenye mtandao wa Jumia Travel kupitia idadi ya wanaotembelea, kuomba na kutumia huduma.”
  Naye kwa upande wake Mshauri wa Huduma kwa Wateja kwenye kampuni hiyo, Flora Rwehumbiza ameongezea kwa kutoa maoni yake kwamba bado sekta ya hoteli nchini Tanzania inakumbwa na changamoto katika kupokea mabadiliko kwa upande wa kitekinolojia.

  “Mbali na Jumia Travel kutoa fursa kwa mameneja wa hoteli na wateja kujiendesha wenyewe na kujihudumia mtandaoni, pia tuna dawati la huduma kwa wateja linalofanya kazi masaa 24. Dawati hili ni mbadala wa pale kunapotekea changamoto mbalimbali lakini pia kutoa msaada pale unapohitajika. Asilimia kubwa ya wateja wanajitahidi kufanya kila kitu wao wenyewe kwenye mtandao wetu lakini changamoto huja kwa upande wa hoteli,” alisema.


  “Unakuta mara nyingi kuna masuala rahisi ambayo yanaweza kufanywa na mameneja lakini hayafanywi mpaka tuwapigie simu na kuwakumbusha mara kadhaa. Kwa mfano, mfumo wetu wa ‘Extranet’ umerahisisha huduma kama vile kuona maombi ya huduma za vyumba hotelini, kukubali au kukataa pamoja na kubadili bei za vyumba au upatikanaji wake kwa siku husika au ndani ya muda fulani ujao. Lakini mameneja hawafanyi hivyo mpaka tuwakumbushe kwa kuwapigia simu kitu ambacho huwa kinaleta mkanganyiko baina yetu, wateja na hoteli,” alihitimisha Bi. Rwehumbiza.

  Kuhusu Jumia Travel


  Jumia Travel (www.travel.jumia.com) ni kampuni nambari moja barani Afrika katika utoaji wa huduma za usafiri mtandaoni, inarahisisha huduma za usafiri kwa kumpatia uzoefu mtumiaji kwa kulinganisha bei na huduma zinazopatikana kwa njia ya haraka na salama zaidi.

  Ikiwa ina hoteli zaidi ya 30,000 Afrika (na zaidi ya hoteli 300,000 duniani) na makampuni ya ndege zaidi ya mia moja kama washirika wake, Jumia Travel inalenga kutoa uhuru wa kusafiri kupitia kupunguza gharama za kusafiri, kutoa orodha kubwa ya hoteli na kuwezesha huduma bora na zenye viwango vya juu kwenye kila nchi husika ili kuwa mojawapo ya sehemu ambayo mteja atakidhi haja zake zote za kiusafiri barani.
  Jumia Travel inafanya shughuli zake katika nchi zaidi ya 40 za Afrika, ikiwa na ofisi kwenye nchi 10 miongoni mwake, na wataalamu wa masuala ya kusafiri zaidi ya 400 ambao wapo tayari kuwahudumia wateja wakati wowote. Ofisi zetu kuu zinapatikana Lagos (Nigeria), Accra (Ghana), Dakar (Sénégal), Abidjan (Ivory Coast), Algiers (Algeria), Douala (Cameroon), Kampala (Uganda), Dar Es Salaam (Tanzania), Nairobi (Kenya) na Addis Ababa (Ethiopia). Kabla ya mwezi Juni 2016, Jumia Travel ilikuwa ikijulikana kama Jovago. Ilianzishwa 2013 na Jumia huku ikiendeshwa kwa ushirikiano wa MTN, Rocket Internet, Millicom, Orange, Axas na washirika wengine.

  0 0

  Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibok akizungumza katika hafla fupi ya kuagwa kwa wazelendo 47 waliopanda mlima Kilimanjaro.
  Baadhi ya Washiriki katika changamoto ya kupanda Kilimanjaro kwa ajili ya kutangaza Utalii wa Ndani na utunzaji wa Mazingira.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza katika hafla ya kuwaaga washiriki wa changamoto ya upandaji wa mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kutangaza Utalii wa ndani na Utunzaji wa Mazingira.
  Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii Tanzania ,Balozi Charles Sanga (kulia) alikua ni miongoni mwa Wazalendo walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimajaro.
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara anayeshiriki zoezi la kupanda  Mlima Kilimanjaro kwa mara ya 10 sasa akazungumza na washiriki wa zoezi hilo kabla ya kuianza safari.
  Mkuu wa wilaya ya Rombo ,Agness Hokororo ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuwaaga Wazalendo 47 kupanda mlima Kilimanjaro. 
  Mkuu wa Wilaya ya Rombo ,Agnes Hokororo akimkabidhi Bendera ya taifa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,Jenerali George Waitara kabla ya kuanza kwa safari hiyo.
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,Jenerali George Waitara akikabidhi Bendera kwa Mkuu wa kamandi ya Brigedi ya Magharibi,Brigedia Jenerali Mkumbo aliyekuwa mkuu wa Msafara wa Wazalendo 47 waloshiriki kupanda Mlima Kilimanjaro.
  Wazalendo 47 walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Rombo .Agness Hokororo.
  Safari katika siku ya kwanza ya kuelekea kilele cha Uhuru ikaanza ,Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali ,Georg Waitara akiongoza.
  Kundi la Wanahabri lilikua na kazi ya kuchukua taswira za safari nzima ya kulekea kileleni. 
  Uzalendo wa kuifikisha Bendera ya Taifa katika kilele cha Uhuru ndio uliongeza morali kwa washiriki ya kuendelea na safari . 
  Wazalendo walipata mapumziko katika eneo la Nusu njia lijulikanalo kama Kisambioni na baadae kuendelea na safari.
  Licha ya kuwepo kwa mvua ,bado safari ya Wazalendo 47 iliendelea.
  Wengine walipatiwa msaada pindi walipohitaji ili mradi safari iwe rahisi.
  Safari ya Wazalendo haikuwacha nyuma ,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro ,Betrita Loibook na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete .walitembea licha ya kunyeshwa na mvua.
  Wenye kiu walipata maji na baadae kuendelea na sfari. 
  Hatimae safari katika siku ya kwanza kwa Wazalendo 47 kuelekea kilele cha Uhuru ikakamilika mara baada ya kuwasili kituo cha mapumziko cha Mandara.

  Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,aliyekuwa katika safari hiyo

older | 1 | .... | 1462 | 1463 | (Page 1464) | 1465 | 1466 | .... | 1897 | newer