Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

VIJUSO VYA MAGAZETI YA IJUMAA LEO DECEMBER 15,2017


NAIBU WAZIRI AWESO ATEMBELEA MAMLAKA YA MAJI TANGA UWASA

$
0
0

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa ziara hiyo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi anayefuatia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Phares Aram

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Phares Aram akizungumza wakati wa ziara hiyo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na watumishi wa mamlaka hiyo

Afisa Rasilimali watu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa),Haika Ndalama akizungumza wakati wa ziara hiyo wa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso

Sehemu ya watumishi wa mamlaka hiyo wakifuatilia nasaha za Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka hiyo
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga,Phares Aram wakati alipotembelea mradi wa mfumo wa uboreshaji wa Maji
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso katikati akimsikiliza kwa umakini Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga,Phares Aram wakati alipotembelea mradi wa mfumo wa uboreshaji wa Maji (Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo akimueleza jambo kwenye ziara hiyo ya Naibu Waziri
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akichimba mtaro katika eneo la Mikanjuni Jijini Tanga wakati alipotembelea mradi wa mfumo wa uboreshaji wa Maji Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akichimba mtaro katika eneo la Mikanjuni Jijini Tanga wakati alipotembelea mradi wa mfumo wa uboreshaji wa Maji
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akitoa mchanga kwenye mtaro huo mara baada ya kuuchimba na sururu wakati wa ziara yake ya kutembelea mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga,Phares Aram akichimba mtaro huo katikati anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akisalimiana na Afisa Rasilimali watu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa),Haika Ndalama mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya kuitembelea mamlaka hiyo

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akisalimiana na Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya kuitembelea mamlaka hiyo kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Mhandisi Phares Aram

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Phares Aram wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo kwa ajili ya kumpatia taarifa wakati wa ziara yake.

TADB PAYS A FAREWELL TO MIVARF’S RAVI MALIK

$
0
0
TADB’s Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (left) talks during the farewell ceremony for Mr. Ravi Malik (not in picture), the outgoing Technical Adviser (Rural Finance) to Marketing Infrastructure, Value Addition and Rural Finance (MIVARF). Others in picture are some the senior management of the Bank
TADB’s Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (right) gives souvenirs to the outgoing Technical Adviser (Rural Finance) to Marketing Infrastructure, Value Addition and Rural Finance (MIVARF), Mr. Ravi Malik (left). Mr. Malik has been in Tanzania since 15 February 2014.

The outgoing Technical Adviser (Rural Finance) to Marketing Infrastructure, Value Addition and Rural Finance (MIVARF), Mr. Ravi Malik (left) chats with TADB’s Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (right) after a farewell ceremony held at TADB’s premises.


By Our Reporter,

The sole agricultural bank in in the country, Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) has paid a farewell to the Technical Adviser (Rural Finance) to Marketing Infrastructure, Value Addition and Rural Finance (MIVARF) Support Programme.

MIVARF is a project under the Prime Minister’s Office. The program aims to reduce rural poverty and accelerate economic growth on a sustainable basis. The Programme Development Objective is to enhance incomes and food security of the target group on a sustainable basis.

Speaking during the farewell meeting at TADB’s premises, the Acting Managing Director of the Bank, Mr. Francis Assenga said the Bank will remember Mr. Malik’s contribution toward establishment of Smallholder Credit Guarantee Scheme (SCGS) and Management of Rural Innovation Fund (RIF) under custodian of TADB.

“Your contribution toward establishment of Credit Guarantee Scheme and Rural Innovation Fund is remarkable, we will forever remember you for making these two prestigious projects under TADB to happen,” he said.

An Indian born, Mr. Malik has been in Tanzania since 15 February 2014 where he was assisting MIVARF to meet its twin objectives. Firstly, to collaborate with and support Bank of Tanzania, Ministry of Finance and the Ministry of Agriculture, Food Security & Cooperatives and the Networks, with a view to facilitating formulation of a suitable policy/institutional framework (including enactment of a legislation) for the orderly growth and regulation & supervision of rural finance sector in Tanzania, including the Micro Finance (MF) sector.

Secondly, to help a few partner institutions, (the Community/Cooperative Banks and MF Institutions (MFIs), to extend their outreach in rural areas, so as to bring five hundred thousand additional rural households under the ambit of the formal financial system by 2017.

According to the recently issued statement by African Development Bank MIVARF has successfully achieved its development objectives in increasing the percentage of all-year passable rural roads and decrease in the number of households located more than 10kms from passable roads; increased volume of goods moved within and out of the focal areas and access of farmers’ produce to markets; and increased price of farmers produce and districts’ revenue collection.

UNHCR: YAELEZA NAMNA INAVYOFANYA SHUGHULI ZAKE KWA WANA HABARI WALIOTEMBELEA KAMBI ZA NDUTA NA MTENDELI

$
0
0
 Ofisa wa Masuala ya Maji na Usafi wa Mazingira  kutoka Shirika la  Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR), Nosakhare Boadi akizungumza wakati  wa Mkutano wa kutoa maelezo kwa ufupi kwa Ujumbe wa Waandishi wa Habari watano kutoka Vyombo mbalimbali nchini Tanzania.
 Mtaalamu wa Masuala ya Ukatili wa Kijinsia na Ustawi wa Jamii Kutoka Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),Rehema Katyega akizungumza na ujumbe wa Waandishi wa Habari waliotembelea Kambi za Nduta na Mtendeli Mkoani Kigoma.
 Sehemu ya Ujumbe wa Waandishi wa habari waliotembelea Kambi za Wakimbizi za Mtendeli na Nduta Mkoani Kigoma kujionea shughuli zinazotekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la  Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) pamoja na Wadau mbalimbali .
 Wafanyakazi wa  Ofisi ndogo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la  Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) Kibondo mkoani Kigoma  wakifatilia kwa karibu mkutano wa maelezo  mafupi juu utekelezaji wa shughuli  mbalimbali za shirika hilo katika kambi za Wakimbizi  za Nduta na Mtendeli
Sehemu ya  Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la  Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) wakiwa katika mkutano huo

IGP SIRRO, AZINDUA ZAHANATI NA KUSHIRIKI MAZOEZI YA UTAYARI MKOA WA KATAVI

$
0
0
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa pili kulia akiwa na maafisa wa Jeshi la Polisi wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Mkoa wa Katavi leo katika ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani humo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) kulia kwake ni Meja Jenerali Mstafu Rafael Muhuga, wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Katavi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wanne kutoka kulia akiwa katika mazoezi ya utayari na Askari waliokuwa wakifanya maonyesho ya utayari Mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake.Picha na Jeshi la Polisi.

RAIS DKT. MAGUFULI ATEKELEZA AHADI YAKE YA SH. MILIONI 60 KWA WAJUMBE WA CHAMA CHA WALIMU PAMOJA NA WANAFUNZI WA UDOM WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO CWT

$
0
0
Katibu wa Rais Ngusa Samike akikabidhi kiasi cha Shilingi milioni 60 kwa Kaimu Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Leah Ulaya kutekeleza ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa hapo jana mara baada ya kuendesha harambee ya papo kwa papo ambapo kiasi hicho cha fedha kilipatikana.
Katibu wa Rais Ngusa Samike akizungumza mara baada ya kukabidhi kiasi hicho cha Shilingi milioni 60 kwa Kaimu rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Leah Ulaya. Katika fedha hizo, kiasi cha Shilingi milioni 50 zitagawiwa kwa wajumbe wote wa CWT waliopo mkutanoni na kiasi cha Shilingi milioni 10 ni kwa ajili ya wanafunzi Tarajali wa UDOM waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo.
Fedha hizo kiasi cha Shilingi milioni 60 zilizo kabidhiwa kwa CWT ambazo Rais Dkt. John Pombe Magufuli alizichangisha kwa viongozi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano wa CWT siku ya jana. Katika fedha hizo Rais Dkt. Magufuli alitoa kiasi cha Tsh. Milioni 10 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa kiasi cha Sh. Milioni 10 pia na zilizobaki zilichangwa na viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo.

PICHA NA IKULU

POLISI TAZARA WATOA ONYO KWA WAHALIFU

$
0
0

Na. Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi nchini limewaonya badhi ya watumishi wasio waaminifu wanaofanya kazi katika Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya wizi wa mafuta na miundombinu mbalimbali ya shirika hilo kuacha mara moja.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi Mwandamizi PATRICK BYATAO wakati wa hafla fupi ya kuwatunukia zawadi baadhi ya Askari waliofanya vizuri katika kuhakikisha usalama wa miundombinu ya shirika hilo ambapo baadhi yao walifanikiwa kuwakamata watumishi wa shirika hilo wakiiba mafuta.

Amesema katika siku za karibuni kumekuwa na matukio kadhaa ya watumishi wa shirika hilo wasio waaminifu ambapo wamekuwa wakilitia hasara shirika hilo jambo ambalo amesema wanaendelea kuimarisha usalama ili kuhakikisha kuwa wanawadhibiti.

BYATAO amesema Kikosi hicho kitaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha wanakomesha tabia hiyo ambayo imekuwa ikidhoofisha utendaji wa TAZARA pamoja na kuitia hasara Serikali.

Akizungumzia utoaji wa Zawadi hizo BYATAO amesema askari hao kumi wamefanya vizuri kwa kujituma katika kipindi cha mwaka 2017 hivyo kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Polisi ni vyema kuwazawadia ili kuongeza morali yao ya kazi na kuwafanya wengine kuendelea kujituma zaidi.

Kwa upande wake mmoja wa Askari waliopata zawadi baada ya kufanya vizuri WP NINA DACHI amewaasa askari wenzanke kuendelea kufanya kazi kwa umakini ili kuhakikisha kuwa miundominu ya shirika hilo inakuwa salama wakati wote.
 Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi cheti cha utendaji bora WP Nina Dachi wa kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi cheti cha utendaji bora mmoja wa askari wa kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi zawadi ya jiko la gesi mmoja wa askari wa  kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akikagua gwaride wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku askari waliofanya vizuri kwa mwaka 2017 katika kikosi hicho ambapo kwa kiasi kikubwa wamezuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA.Picha na Jeshi la Polisi

WANAZUSHA TUU LAKINI MIE NIKO FITI KABISA-LIPUMBA

$
0
0
Na Baba Feilsal.

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi(CUF) Ibrahimu Lipumba amesema afya yake iko imara na hana tatizo lolote kiafya.

Ametoa kauli hiyo  muda huu wakati akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu ambapo amesema anashangazwa na taarifa ambazo zipo kwenye baadhi ya mitandao kuwa anaumwa na amelazwa Hospitali ya Agha Khan.

"Nimeshangaa sana kusikia eti kuna taarifa zinadai nimepatwa na nshtuko, taarifa hizo si za kweli na ndio hizo hizo zinaitwa feck news.Nipo imara na najiandaa kwenda msikiti na baada ya hapo nitakwenda makao makuu ya chama kwa ajili ya kusimamia kikao," amesema Prof Lipumba.

Amefafanua hakuwa anajua kinachoendelea mtandaoni kuhusu yeye kwani anapoingia kwenye mtandao ni kwa ajili ya kuangalia tafiti mbalimbali na si taarifa za kuzusha.

Amesema alishangaa kuona anapigiwa simu na watu mbalimbali wakimpa pole ya ugonjwa ndipo aliposhangaa na kuanza kufuatilia chanzo cha hiyo taarifa.

Nimepata fursa ya kuzungunza kwa kirefu na prof lipumba yupo bukheri wa afya njema  na ameshangazwa na uzushi kuwa ameptwa na mshutuko.

WAZIRI LUKUVI AMALIZA MGOGORO WA ARDHI ULIODUMU MIAKA 10 CHAMWINO DODOMA

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza wakati wa Mkutano wa Hadhara katika Kata ya Membe Wilayani Chamwino jana ambapo alitoa uamuzi wa kuirudisha kwa Wananchi wa Vijiji vya Membe na Mlimwa ardhi yenye ukubwa wa ekari 1756 aliyepewa mwekezaji Davidi Mazoya Poli ( aliyesimama kushoto) kinyume cha taratibu miaka 10 iliyopita.


Baadhi ya wakazi wa Kata ya Membe wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipofanya ziara katika Kata hiyo jana.


Baadhi ya wakazi wa Kata ya Membe wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipofanya ziara katika Kata hiyo jana.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Membe wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipofanya ziara katika Kata hiyo jana.


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi amefuta uamuzi wa viongozi wa Vijiji vya Membe na Mlimwa vilivyopo Kata ya Membe Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma wa kumpatia ardhi yenye ukubwa wa ekari 1756 mwekezaji David Mazoya Poli takribani miaka 10 iliyopita hali iliyosababisha mgogoro wa ardhi na kuhatarisha amani katika Kata hiyo.

Hali ya sintofahamu iliwagubika wakazi wa Kata hiyo kwani licha ya kukataa kutoa ardhi yao kwa mwekezaji huyo kupitia mikutano mikuu ya Vijiji, viongozi wao walimmilikisha Mwekezaji huyo ardhi hiyo ikiwemo ekari 100 alizopewa na Kijiji cha Membe kwa makubaliano kuwa atawajengea Ofisi ya Serikali ya Kijiji ahadi ambayo hata hivyo hajaitekeleza.

Akizungumza na wakazi wa Kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara jana, Waziri Lukuvi alisema kuwa amefuta maamuzi yote yaliyofanywa na Serikali za Vijiji hivyo kwani yalikiuka Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999 inayotoa mamlaka kwa Vijiji kumilikisha ardhi isiyozidi ekari 50 tu na sio vinginevyo.

“Kuanzia leo nimefuta maamuzi yote yaliyofanywa na viongozi wa Vijiji hivi kumpa mwekezaji huyu ardhi yenye ukubwa wa ekari 1756 kwani ni kinyume cha Sheria ya Vijiji…hata kama Vijiji vitakubali kutoa ardhi kupitia mikutano mikuu ya Vijiji bado maamuzi hayo hayatakuwa halali endapo ardhi inayotolewa itazidi ukubwa wa ekari 50” alifafanua Waziri Lukuvi.

Alimtaka Mwekezaji huyo ambaye alifika katika mkutano huo, kufuata taratibu za kumilikishwa ardhi inayozidi ukubwa wa ekari 50 endapo ana nia ya kuendelea kuwekeza katika Kata hiyo, ikiwa ni kuomba ardhi katika Vijiji hivyo na endapo vitaridhia, vitapendekeza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye mwenye Mamlaka ya kumilikisha ardhi inayozidi ekari 50 baada ya ardhi hiyo kuhama kutoka katika Mamlaka ya Vijiji.

Wakazi wa Kata hiyo walimshukuru Waziri Lukuvi kwa uamuzi huo wa Serikali kwa madai kwamba wameteseka kwa kipindi kirefu ikiwa ni pampoja na kukosa maeneo ya kulima na malisho kwa ajili ya mifugo yao.

KATIBU MKUU WA CCM KOMREDI KINANA AWAASA WANA CCM KUMUUNGA MKONO MWENYEKITI WAO,RAIS DKT MAGUFULI KATIKA VITA YA KUPAMBANA NA RUSHWA PAMOJA UFISADI

$
0
0
 Katibu MKuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mjumbe wa kamati kuu ya siasa ya Mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi jana mara baada ya kuwasili katika Kata ya Ilongero,Singida vijijini katika jimbo la Singida la Kaskazini,ambapo Chama cha Mapinduzi jana kilikuwa kinapiga kura za maoni kumchagu Mbunge atakaekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA.
 Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Singida Vijijini wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahamani Kinana alipokuwa akizungumza nao kabla ya kupiga kura ya kumchagua atakaewawakilisha katika nafasi ya Ubunge,na hatimaye kugombea katika uchaguzi mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika jimboni humo hivi karibuni.
Mjumbe wa kamati kuu ya siasa ya Mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi akizungumza mapema jana kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya Wilaya uliokuwa ukifanyika jana katika kata ya Ilongero,Singida vijijini katika jimbo la Singida la Kaskazini,ambapo Chama cha Mapinduzi kinamtafuta Mbunge atakaekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA. 
 Katibu MKuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mapema jana kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya Wilaya uliokuwa ukifanyika jana katika kata ya Ilongero,Singida vijijini katika jimbo la Singida Kaskazini,ambapo Chama cha Mapinduzi kilikuwa kikipiga kura kutafuta Mbunge atakaekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA.Ndugu Kinana aliwaasa Wajumbe hao kumchagua mtua anaefaa na atakawasaidia na kuwasemea matatizo yao,na atakae kuwa tayari kuwaletea maendeleo.
Wajumbe wakimsikiliza Ndugu Kinana kwa umakini kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wananchi waliovutiwa na hotuba ya Katibu Mkuu Ndugu Kinana,ilibidi wasogee zaidi na kuendelea kusikiliza

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida Ndugu Juma Kilimba akimkaribisha Mgeni rasmi,Katiibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyepita kuwasalimia na kuona wamejiandaaje na uchaguzi wao wa kura za maoni kwa ajili ya kumchagu Mtu atakaewawakilisha katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA.Ndugu Kinana aliwaasa Wajumbe hao kumchagua mtua anaefaa na atakawasaidia na kuwasemea matatizo yao,na atakae kuwa tayari kuwaletea maendeleo.

KWA UFUPI YALIYOJIRI WAKATI WA MKUTANO WA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI DKT. HASSAN ABBASI NA WAANDISHI WA HABARI DODOMA LEO

$
0
0

  Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt Hassan Abbasi akifafanua jambo kwa msisitizo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo kwenye ofisi za Idara ya Habari MAELEZO mjini Dodoma,mambo mbalimbali ikiwemo na kuwakaribisha rasmi katika ukumbi mpya wa MAELEZO hapa Dodoma,kwamba Idara imeshahamia rasmi Dodoma na huduma zote zitakuwa zikitolewa hapo.
 Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo kwenye ofisi za Idara ya Habari MAELEZO mjini Dodoma,mambo mbalimbali ikiwemo na kuwakaribisha rasmi katika ukumbi mpya wa MAELEZO hapa Dodoma,kwamba Idara imeshahamia rasmi Dodoma na huduma zote zitakuwa zikitolewa hapo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza  Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt Hassan Abbasi alipokuwa akitolea ufafanuzi mambo mbali ikiwemo ripoti ya IMF mapema leo kwenye ofisi za Idara ya Habari MAELEZO mjini Dodoma,pamoja na kuwakaribisha rasmi Wanahabari hao katika ukumbi mpya wa MAELEZO hapa mjini Dodoma,kwamba Idara imeshahamia rasmi Dodoma na huduma zote zitakuwa zikitolewa hapo.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA.

#Nawashukuru wanahabari wote kwa kushiriki vyema katika sherehe za miaka 56 ya Uhuru;

#Napenda kuwakaribisha rasmi katika ukumbi mpya wa MAELEZO hapa Dodoma.Idara imeshahamia Dodoma na  huduma zote zinatolewa hapa;

#Nawakumbusha press card zinamalizika muda wake Disemba 2017 hivyo wanahabari wanapaswa kuanzia Januari kuwahi kupata vitambulisho vipya kwa haraka kwani baada ya muda hakuna mwandishi ataruhusiwa kushiriki matukio makubwa bila press card.

#Nizungumzie pia taarifa ya IMF ambayo wataalamu wake wamekamilisha kazi hapa nchini juzi kama ambavyo pia wamekamilisha tathmini kama hizo Afrika na kwingineko;

#Ripoti yao ni nzuri na imebainisha mambo mazuri ambayo nchi imepiga hatua na changamoto ambazo tunaendelea kuzifanyiakazi;

#Lakini kama kawaida kuna wanasiasa "vyuma vimekaza"-hawana ajenda bali kutafuta matukio na mwanya wa pa kusemea  ili kuropokaropoka;

#Sasa ngoja niwape mambo ya hakika kuhusu walichosema wataalamu hao. Ripoti yao imeonesha uchumi wa Tanzania upo imara, unakuwa kwa asilimia 6.8 kwa maana ya kuelekea nusu ya mwaka huu na mfumuko wa bei upo chini ya asilimia 5 tofauti na nchi nyingine zilizofanyiwa tathmini.

#Katika nchi ambazo zimefanyiwa tathimini kuanzia Novemba hadi Desemba mwaka huu Tanzania ipo juu kwa maana ya ukuaji kuna nchi moja ya Afrika wataalam hao wameeleza uchumi wake unakua kwa asiliamia 1.1 na huenda mwakani ukawa -1.

#Taarifa ya IMF imeonesha nchi yetu imepata daraja ya juu kwamba imetekeleza vyema ushauri wa kitaalam iloyopewa maana mradi huu haukuwa wa fedha bali ushauri wa kitaalam;

#Sisi kama nchi tumeridhishwa na maoni ya wataalam wa IMF na kwenye changamoto tutaendelea kuzifanyia kazi.

#Niwapongeze wakulima kwani taarifa inaonesha mavuno mazuri ya mazao katika mwanzo wa mwaka huu yamesaidia sana upatikanaji wa chakula cha kutosha na hivyo kushusha bei za chakula.Tuendelee na kazi kubww mashambani na viwandani;

#Taarifa za IFM zinaonesha mfumuko wa bei ya chakula ulishuka hadi kufikia asilimia 4.4 Novemba mwaka huu ikiwa ni chini ya lengo ambalo IFM ilidhani mfumuko ungekuwa asilimia 5 na zaidi.

#Benki nyingi za Tanzania bado zina mitaji ya kutosha wameeleza wataalam hao na masuala ya changamoto za kushuka mikopo yanashughulikiwa lakini watanzania ni vyema wakajifunza kukopa na kulipa; 

#Zoezi la kuhuisha takwimu za kiuchumi (Debasing) ni la kawaida chini ya mifumo ya upimaji uchumi duniani kwa lengo la kuongeza shughuli mpya za kiuchumi tofauti na anavyopotosha mwanasiasa mmoja ambaye ni dhahiri "vyuma vimekaza" hana tena ajenda anarukiarukia matukio na kuokoteza vitakwimu;

#Zoezi hili la kuhuisha takwimu linaendelea katila nchi zote za EAC na Tanzaniq hii ni marq ya 5 kufanyika na matokeo yatatangazwa mwishoni mwa Disemba hii ili kuingiza mchango wa shughuli mpya za kiuchumi kama gesi, viwanda vipya n.k;

#IMF wamesifu pia  makusanyo yetu kutokana na utekelezaji wa sera.Ndio maana makusanyo ya Serikali yameongezeka kutoka tril. 9.9 mwaka 2015 hadi Tril 14 mwaka 2017 kwa wastani wa mwaka;

#Wametusifu pia kuwa Serikali yetu inajitahidi kulipa madeni na kama mlivyosikia juzi Rais amesema katika miaka miwili hii ameshalipa madeni ya zaidi ya TZS bilioni  900 na nyingine uhakiki unaendelea na atalipa fedha hizo zipo hakuna shida;

#Tufike hatua kama watanzania katika kujenga nchi yetu kwenye kufikia Tanzania tunayoitaka, tujue sio kila kitu ni siasa kuna mambo ni uchumi wa nchi na kuna mambo ni maendeleo hayapaswi kufanyiwa tashtiti;

#Katika tathmini hizi ambazo pia zimefanyika nchi mbalimbali ipo nchi moja kubwa tu ya Ulaya imeelezwa kuwa na changamoto nyingi za kiuchumi katika tathmini ya uoande wa nchi zilizokopeshwa fedha.

Sisi tupo vizuri na tunafanyiakazi changamoto zilizoainishwa kama vile mikopo chechefu na kuendelea kukusanya kodi na kuboresha sekta binafsi.

Asanteni kwa kunisikiliza.

Imeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

SBL yazindua kampeni ya kuitangaza Whisky ya Johnnie Walker Black Label

$
0
0



Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Cesear Mloka Akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema jana katika uzinduzi wa kampeni ya kuitangaza Whisky ya Johnie Walker Black label ambayo inaambatana na maadhimisho ya miaka 20 ya Kampuni mama ya Diageo.Pembeni yake ni Meneja Masoko Nicholaus Machugu.


wadau wakionja ladha ya Whisky ya Johnnie Walker Black Label mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya kuitangaza mapema jana .
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Cesear Mloka Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana katika uzinduzi wa kampeni ya kuitangaza Whisky ya Johnie Walker Black label ambayo inaambatana na maadhimisho ya miaka 20 ya Kampuni mama ya Diageo.



Ni katika kuadhimisha miaka 20 ya Kampuni mama ya Diageo

Dar es Salaam, Desemba 14, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya pombe kali aina ya Johnnie Walker (JW) Black Label inayojulikana kama, ‘JW Paints Tanzania Black’.

Katika kampeni hii, shughuli mbali mbali zitafanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni mama ya Diageo yatakayofanyika tarehe 15/12/2017. Diageo ndiyo mwana hisa mkubwa kwenye kampuni ya SBL.

Ikiwa inatengenezwa na kampuni ya Diageo na kusambazwa na SBL kwa hapa Tanzania, Johnnie Walker Black Label ambayo ni Whisky ya Kiskoti inachukuliwa na wataalamu kama ndiyo whisky bora zaidi duniani huku ikijali thamani ya pesa kwa watumiaji wake.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Cesear Mloka, kampeni hiyo itaanza kwa programu ya kuongezewa maarifa kwa wafanyakazi wa SBL ambayo itakwenda hadi katika ngazi ya marafiki, wanafamilia pamoja na wadau wa biashara.

“Tunatarajia kuwa na tukio la kufurahisha litakaloongozwa na wafanyakazi wetu ambao wataelezea ufahamu wao pamoja na mapenzi yao kwa Johnnie Walker kwa watumiaji wa kinywaji hicho kwenye sehemu mbali mbali kinapouzwa hapa nchini kama Bella Whispes, The Great, KB Tabata,Green Palm, Lachaz, MK, TIPS, Kuringe, Triple A, Front View, Dodoma Carnival na Golden Crest.

Tukio hili halitafanyika hapa Tanzania peke yake, bali linafanyika siku hiyo hiyo katika nchi 180 ambako Diageo inafanya biashara zake na ambako Johnnie Walker Black Label inapatikana. Tanzania ni sehemu ya kampeni ya kidunia ya JW inayojulikana kama ‘Paint the World Black’ kuadhimisha shughuli hii yenye mafanikio makubwa,” alisema Mloka wakati wa uzinduzi uliofanyika Dar es Salaam.

Mloka aliongeza kuwa, kampeni hiyo itatangazwa kwenye magazeti, radio na televisheni, mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya mawasiliano ya ndani ya kampuni.

Kampuni ya SBL pia imezindua maeneo maalum ya kufanya manunuzi ya whisky ya Johnnie Walker Black Label mpaka mwishoni mwa mwezi Disemba katika maduka ya vileo yaliyopo Dar es Salaam ya Kibong'oto, Lamana, Master Liquor, Madeira & Herera pamoja na Arusha ya New Open Center & Chware Stores. Johnnie Walker Black Label iliyoyachanganywa ina umri wa miaka 12 na Ilitengenezwa wakati Johnnie Walker ikitimiza miaka 100 tangu ilipotengenezwa kwa mara ya kwanza mwaka 1909. Ladha yake ni mchanganyiko wa kipekee wa kimea, matunda, cocoa pamoja na vanilla. 

Ikiwa inauzwa takribani kila nchi duniani, ni whisky ya Kiskoti inayosambazwa zaidi duniani.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA MAPOKEZI YA MAKAMU WA RAIS KUHAMIA MKOANI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongaza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dodoma katika mapokezi rasmi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan baada ya kuhamia Mkoani Dodoma leo Desemba 15, 2017. kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa salamu za kumkaribisha Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan aliyehamia rasmi Mkoani Dodoma leo Desemba 15, 2017.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Januari Makamba wakicheza ngoma ya Mwinamila wakati wa Makaribisho ya Makamu wa Rais Mkoani Dodoma leo Desemba 15, 2017.
Balozi Job Lusinde akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa Dodoma kwakuhamia Makamu wa Rais Mkoani Dodoma.

Na Beatrice Lyimo, MAELEZO-DODOMA

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehamia rasmi Makao Makuu ya Nchi Dodoma leo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli alililitoa tarehe 25, Ju.

 Akizungumza wakati wa halfa ya kumkaribisha, Makamu wa Rais amesema kuwa mpaka sasa ni mwaka mmoja na nusu tangu tamko la kuhamia Dodoma litolewe hivyo Serikali ipo na inatekeleza majukumu yake.

“Siku ya leo ilikuwa mawazoni mwangu, ninafurahi imefika na pia ninamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa maandalizi mazuri ya kunipokea ” Alisisitiza Mhe. Samia

Aidha, Mhe. Samia amesema kuwa Ofisi yake imekuja na agenda ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani hivyo  wameandaa programu mbalimbali ikiwemo ya upandaji miti .

“Tarehe 21, Disemba mwaka huu kutakuwa na shughuli ya upandaji miti hivyo tunaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma kutuunga mkono ili kuweza kutimiza azma hii” ameongeza Mhe. Samia.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Baba wa Taifa aliweka nia ya Serikali kuhamia Dodoma tangu mwaka 1973 na leo Serikali ya Awamu ya Tano imetimiza ndoto hiyo.

“Tunaendelea kuamini kwamba tamko la Rais linatekelezeka ambapo mpaka sasa watumishi 2816 tayari wameshahamia Dodoma na wanaendelea kutoa huduma za Serikali na  kuanzia Februari mwaka 2018 tunaendelea kupokea watumishi wengine” amefafanua Waziri Mkuu.

Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Pancras Ndejembi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza historia ya Mwalimu Nyerere ya Dodoma kuwa Makao Makuu.

“Sikuwaza kama kuna siku Makao Makuu yatakuwa Dodoma kwa sababu siku nyingi mambo haya yanazungumzwa sasa yamekamilika kwa vitendo, leo nina furaha sana kuona ndoto ya tangu mimi kijana imetimia” ameongeza Mzee Ndejembi.

Kwa upande wake Balozi Job Lusinde amesema kuwa “leo Makamu wa Rais anahamia Dodoma, kweli Mungu hupanga na Mungu huweka wakati wake, leo imekuwa”.

Mbali na hayo Balozi Job Lusinde amesema kuwa Makamu wa Rai amekuja kipindi ambacho Mkoa wa Dodoma unaanza kuandaa mashamba kwa ajili ya kulima, hivyo kumpatia jina la kabila hilo “Mbeleje” likimaanisha kipindi cha kuandaa mashamba.

Uchumi wa Nchi Uko Imara - Dkt. Hassan Abbas

$
0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Serikali kupitia Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan imesema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Fedha Duniani  (IMF) uchumi wa nchi uko imara ukilinganisha na nchi zilizofanyiwa tathimini.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akiongea na vyombo vya habari juu ya maoni ya wataalam wa uchumi kutoka IMF ambao wamemaliza ziara yao hapa nchini Desemba 12, 2017.
 
"Ripoti ya IMF inaonesha katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017 uchumi umekua kwa asilimia 6.8 takwimu ambazo ni za juu katika chumi zinazokua kwa kasi na ikizidi nchi kadhaa zilizofanyiwa tathmini mwaka 2017 zikiwemo za Ulaya," amefafanua Dkt. Abba.

Ameendelea kusema, mapato ya nchi yameongezeka kutoka Shilingi Trilioni 9.9 mwaka 2015 kufikia Shilingi Trilioni 14 mwaka 2017.Aidha, kutokana na usambazaji mzuri wa chakula mfumuko wa bei ya chakula ulishuka hadi kufikia asilimia 4.4 ikiwa ni chini ya lengo ambalo IMF ilitabiri mfumuko ungekuwa asilimia 5.

Aidha amesema, Serikali imeendelea kulipa madeni ya ndani ambapo mpaka sasa Shilingi bilioni 900 zimeshalipwa na shilingi bilioni 37 zimelipa madeni ya watumishi wa Serikali.Vile vile Serikali imefanikiwa kufufua viwanda vipya 17  kupitia ofisi ya Msajili wa Hazina ambavyo vilikuwa vimekufa na viwanda vingine vipya zaidi ya 500 vimeanzishwa ambavyo na kuhesabika kuwa kigezo kipya cha uchumi kutokana na kutoa ajira kwa watanzania pamoja na kulipa kodi kwa Serikali.

Msemaji wa Serikali ameeleza kuwa kwa kawaida uchumi wa nchi hausimami na kwamba kuna shughuli nyingine mpya zinaingia katika uchumi na kutumika kama kigezo cha kukua kwa uchumi.Timu hiyo ya  wataalamu kutoka IMF iliongozwa na Bw. Mauricio Villafuerte ambapo walifanya ziara juu ya tathimini ya uchumi katika nchi Saba Afrika ikiwemo Tanzania pamoja na Msumbiji, Rwanda, Nigeria, Uganda, Senegari na Cape Verde.

Dkt KALEMANI aendelea na ziara ya Kukagua Maendeleo ya Miradi ya Umeme

$
0
0
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ameendelea na ziara ya kukagua hatua iliyofikiwa katika ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na njia ya kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea.

Lengo la ziara hiyo ni kukagua uimara wa mitambo ili Serikali kupitia TANESCO iweze kujipanga vizuri kwa kuwa na umeme wa uhakika.
Waziri wa Nishati Dkt MEDARD KALEMANI akiwa kwenye ziara ya Kukagua hatua iliyofikiwa katika ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na njia ya kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea.

"Kama ilivyo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda, tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika". Alisema Dkt. Kalemani. Habari Wakuu naomba Mpokee Codes kwa ajili ya Kuhabarisha Umma.....Natanguliza Shukrani Katika ziara hiyo pia amekagua miradi ya umeme Vijijini Awamu ya Tatu inayoendelea katika Mikoa hiyo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati. Akikagua mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 220 kutoka Makambako hadi Songea, Dkt. Kalemani alisema mradi huo utaiunganisha Mkoa wa Ruvuma katika Gridi ya Taifa. Pia, kukamilika kwa miradi hiyo kutaipunguzia gharama Serikali kwa kuondokana na mitambo ya mafuta.
Pichani ni Baadhi ya vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na njia ya kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea.

DC MCHEMBE AZINDUA KAMPENI YA KUPANDA MITI WILAYA YA GAIRO KATA KWA KATA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe amezindua kampeni ya kupanda miti Kata kwa Kata. Akizungumza jana wakati akizindua kampeni hiyo iliyofanyika katika tarafa la Nongwe kata ya Chanjale, alisema kuwa wananchi ni lazima waheshimu kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti na si kuikata ovyo. 

Katika kampeni hiyo Mhe. Siriel aliambatana na Meneja wa Misitu Wilaya Bw. David Maiba waliweza kuwahamasisha wananchi kupenda mazingira maana ndiyo yamekuwa yakisababisha wao kupata nvua. "Nawaomba wananchi mpende kuhifadhi mazingira maana ndiyo uhai wetu ambao unasababisdha hata mvua kupatikana, sehemu ikiwa jangwa hamuwezi pata hata maji, niwaombe sana mtunze mazingira kwa ukaribu sana," alisema mhe. Siriel. Kampeni hiyo imeanzia Tarafa ya Nongwe Kata ya Chanjale. Tarafa hii ipo uwanda wa juu ambapo mvua tayari zimeanza. 

Viongozi wengine ambao aliambatana nao ni Diwani wa Chanjale Mhe. Maswaga Malima, Mtendaji Kata Bi. Stella Ngomano, Wenyeviti wa Vijiji, Watendaji wa Kata, Wazee Maarufu, Viingozi wa Dini na wananchi kwa ujumla. Kata ya Chanjale ina Misitu ya Hifadhi yenye ukubwa wa ekari 3,000. Aliongeza kuwa upandaji wa miti utakuwa ni zoezi endelevu na ameshaagiza kila kijiji kiwe na kitalu cha kuzalisha miti japo changamoto inayowakabili ni viriba, ambapo wanahitaji viriba zaidi ya milioni moja kwa Wilaya yote ya Gairo.
 Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akizungumza machache na wananchi waliofika katika uzinduzi huo. 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akipanda miti kuashiria uzinduzi wa kampeni hiyo. 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akielekea eneo la tukio na wananchi eneo la tukio.

DKT. MWAKYEMBE : MICHEZO YA VYUO VIKUU INATOA FURSA YAKUBAINI VIPAJI VIPYA

Mabondia Francis Cheka na Shabani Kaoneka wapima uzito leo,kuzichapa kesho uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara

$
0
0
Mabondia Francis Cheka na Shabani Kaoneka, wamepima uzito leo tayari kwa pambano lao linalotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi katika uwanja wa Umoja  Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara, ambapo Francis Cheka anatetea mkanda wake wa IBO Africa

Zoezi la upimaji Uzito likiwa linaendelea na kusimamiwa na Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi wa Ngumi za Kulipwa Tanzania Ally Bakari na kuthibitisha Ulinganifu wa Uzito.

Mara baada ya zoezi Hilo Franciss Cheka ambaye anatetea Mkanda IBO Afrika amewaomba mashabiki wa ngumi Mkoa wa Mtwara Kuweza kujitokeza kwa wingi na tayari amefanya mazoezs ya kutosha Kuweza kushinda

Pambano hilo la round Kumi, litasindikizwa na mapambano ya utangulizi yatakayowahusisha mabondia wa Mtwara dhidi ya mabondia kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Tanga sambamba na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii Sholo Mwamba na 20 Percent.
 
 

TAARIFA YA KUFUNGA MWISHO WA MWAKA KWA WANA TASNIA YA HABARI

MADAKTARI NA WATOA HUDUMA ZA AFYA WATAKIWA KUFANYA TATHMINI YA MFANYAKAZI ALIYEUMIA MAHALA PA KAZI KWA UFANISI NA WELEDI

$
0
0
Madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya nyanda za juu Kusini, waliokuwa wakishiriki mafunzo ya wiki moja ya kufanya tathmini kwa mfanyakazi aliyeumia mahala pa kazi, wakionyesha stika watakazobandika maofisini kwao, zikionyesha ofisi ya mtoa huduma, mwishoni mwa mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF na kufanyika jijini Mbeya Desemba 15, 2017. 
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said


KAIMU Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Yahya Msuya, (pichani juu), amewatakamadaktari na watoa huduma za afya, waliokuwa wakishiriki mafunzo ya wiki mojaya kufanya tathmini ya ulemavu kwa wafanyakazi watakaoumia au kuugua kutokanana kazi zao, kutumia elimu waliyoipata kwa ufanisi na weledi.


Akifungamafunzo hayo ya siku tano yaliyoratiubiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ilikuwajengea uwezo wataalamu hao wa afya, Dkt. Msuya alisema, ni ukweli kwambaMfuko wa WCF hauna muda mrefu tangu uanzishwe na serikali na kwa mantiki hiyo,mkakati wa mafunzo ni muhimu ili kuhakikisha kwamba wadau wote wanaonufaikaau kuwajibika na Mfuko kuelewa shughuli zake na kuhakikisha kwamba lengo lakuanzishwa kwa Mfuko huo linatimia.


“Nahakikakatika kipindi hiki mlichokuwepo hapa mtakuwa mmejifunza mambo mengi mapya nakuwapa ujuzi ambao huenda hamkuwa nao wakati mnakuja hapa.” Alsiema Dkt. Msuya.


Kwaupande wake, Mratibu wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tiba na
Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, alisema, lengo kuu ni kuwaelimisha
madaktari kufanya tathmini ya ulemavu kwa wafanyakazi watakaoumia au kuugua
kutokana na kazi zao kwenye maeneo yao ya kazi ili kutoa mapendekezo kwa Mfuko
kwa ajili ya uamuzi wa mwisho wa kutoa fidia. “Washiriki 85 kutoka mikoa ya
kanda ya nyanda za juu kusini wameshiriki na tuna hakika pamoja na elimu waliyoipata lakini pia watakuwa mabalozi wetuwazuri watakaporejea kwenye maeneo yao ya kazi.” Alisema Dkt. Omar.

NayeMkuu wa Kitengo cha Mawasiliano WCF, Bi. Laura Kunenge, amesema, kila mshiriki
amepatiwa cheti cha ushiriki na stika atakayokwenda kuibandika kwenye ofisi
yake kwa nia ya utambuzi wa mtoa huduma ya tathmini.

“Stikahizi zinamuelekea mteja kuwa ofisi hiyo anapatikana daktari aliyepatiwa mafunzo
ya kufanya tathmini ya mfanyakazi aliyeumia au kupata maradhi mahala pa
kazi.”Alifafanua Bi. Laura.Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Dkt. Mertson Mgomale, amesema, binafsi amepata faida kubwa kwani sasa anaelewa kutofautisha kiwango cha madhara aliyoyapata mfanyakazi aliyeumia kutokana na tathmini atakayomfanyia. “tulikuwa tunampima mgonjwa kama wagonjwa wengine, lakini kuchunguza viwango vya kuumia hiyo haikuwepo lakini kwa mafunzo haya sasa nimeelewa ni jinsi gani naweza kumfanyia tathmini mfanyakazi aliyeumia wakati akitekeleza wajibu wake kazini.” Alisema mshiriki huyo.

Mafunzohayo ni mkakati wa Mfuko kupanua mtandao wa watoa huduma ya tathmini nchi nzimaili hatimaye Mfanyakazi aliyeumia aqweze kuhudumiwa kwa kufanyiwa tathminiiliyo sahihi kwa mafao ya fidia sahihi. Hadi sasa ukiachilia mbali madaktari
hao 85 wakiwemo watoa huduma za afya, jumla ya madaktari 504 kutoka mikoa yote
Tanzania Bara wamepatiwa mafunzo hayo.
Mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Yahya Msuya, (wapili kulia), akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt. Rehema Mwanga. wanaoshuhudia ni Mratibu wa mafunzo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kulia), na kiongozi wa timu ya wawezeshaji, Daktarin bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina.
Washiriki wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasilianoi WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki, Dkt. Gloria Mbwile, ambaye ni mganga mfawidhi hospitali ya mkoa wa Mbeya.
Dkt. Ali Mtulia kutoka WCF akitoa mada mwishoni mwa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki.
Baadhi ya washiriki.
Mgeni rasmi, Kaimu Mganga Mkuu, Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Yahya Msuya, (katikati), Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini, WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kulia) na Mkuu wa timu ya wawezeshaji wa mafunzo hayo, Daktari bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina.
Mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Yahya Msuya, (wapili kulia), akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt. Hassan Y. Lumbe. wanaoshuhudia ni Mratibu wa mafunzo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kulia), na kiongozi wa timu ya wawezeshaji, Daktarin bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina.
Mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Yahya Msuya(wapili kushoto), akiongozana kutoka kushoto, Dkt. Mhina, Dk. Hussein, na Dkt. Omar.
Picha ya pamoja kundi la kwanza
Picha ya pamoja kundi la pili.
Dkt. Msuya akiagana na Dkt. Omar baada ya shughuli hiyo. Kulia mni Dkt. Mhina.
Dkt. Msuya akiagana na Dkt. Mtulia baada ya shughuli hiyo. Katikati ni Dkt. Omar.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images