Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1460 | 1461 | (Page 1462) | 1463 | 1464 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg:Kheri D James (katikati) akiwasili Ofisi za Makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa kushoto kwake ni Ndg Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka.
  Ndg:Rodrick Mpogolo Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi akimpokea Mwenyekit wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi alipowasili Makao makuu ya chama cha mapinduzi.
  Mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Dodoma akiwasilisha salamu za vijana wa mkoa wake kwa mwenyekiti wa umoja wa vijana Taifa.
  Kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ndg:Shaka Hamdu Shaka akizungumza.
  Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi ndg:Thabia Mwita akizungumza na vijana wa Umoja wa Vijana wa chama cha mapinduzi katika viwanja vya makao makuu ya ccm dodoma.
  Kikundi cha chipukizi kikitoa burudani
  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ndg:Kheri D James akipokea wanachama wapya 200 toka vyama mbalimbali vya upinzani pichani ni alie kuwa katibu wa chama cha ACT WAZALENDO mkoa wa Mwanza ndg:gwanchele.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ndg:Kheri D James akizungumza na Vijana wa mkoa wa dodoma katika hafla ya kumkaribisha iliofanyika makao makuu ya CCM DODOMA.

   Meza kuu
  Vijana wakisikiliza kwa umakini hotuba ya mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ndg:Kheri D James.
  PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa askari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  (JWTZ) waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC, kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JWTZ, Upanga jijini Dar es salaam akimwakilisha Rais John Pombe Magufuli, Desemba 14, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017  alikomwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini, Jenerali Venance Mabeyo baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,. Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo  baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete  baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Susan Kolimba baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. Katikati ni Rais Mstaafu wa Awamu wa Nne, Jakaya Mrisho Kikwete na kushoto Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika - SADC.  
   Askari wa Jeshi  la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba miili ya askari 14 wa JWTZ waliouwa wakiwa kwenye operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo -  DRC,`kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JWTZ Upanga jijini Dar es salaam  Desemba 14, 2017.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari hao.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wafiwa baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wanachama wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kabla ya kufungua mkutano huo  Mkuu wa (CWT )katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma. Wanachama hao wa CWT walisimama na kushangilia  mara baada ya ahadi ya Rais Dkt. Magufuli kuwaahidi kuendelea kutatua kero zao mbalimbali.
   Mamia ya Wajumbe wa Chama cha Walimu(CWT) wakishangilia ndani ya ukumbi wa Chimwaga wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akijibu kero zao mbalimbali walizoziwasilisha.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya wajumbe wa Chama cha Walimu CWT mara baada ya kuwahutubia katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa muda wa  CWT, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Spika wa Bunge Job Ndugai, pamoja na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakiimba wimbo wa mshikamano pamoja na Wajumbe wote wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
   Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakiwa wameshikana mikono wakati wakiimba wimbo wa mshikamano kabla ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhutubia na kufungua mkutano huo wa CWT katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wajumbe wa CWT katika ukumbi wa Chimwaga.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza viongozi wa muda wa Chama cha Walimu Tanzania walipokuwa wakiwasilisha hoja zao mbalimbali zinazo wakabili walimu nchini katika mkutano mkuu wa CWT uliofanyika katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma. PICHA NA IKULU

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taaasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Mkurugenzi wa Taasisi ya kifedha ya Tanzania Mortage Refinance Company(TMRC) Oscar Mgaya wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye matatizo ya Moyo na wazazi wao wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mfano wa hundi ya shilingi milioni nane ambayo wamezitoa kwa ajili ya matibabu ya watoto hao.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya kifedha ya Tanzania Mortage Refinance Company(TMRC) Oscar Mgaya akiwakabidhi wazazi wa watoto wenye matatizo ya Moyo mfano wa hundi ya shilingi milioni nane ambazo zimetolea na Taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu ya watoto wanne.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taaasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Mkurugenzi wa Taasisi ya kifedha ya Tanzania Mortage Refinance (TMRC) Oscar Mgaya wakizungumza baada ya kumaliza makabidhiano ya hundi ya shilingi million nane kwa ajili ya kuwezesha matibabu ya moyo kwa watoto wanne .Picha na JKCI  Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kifedha ya Tanzania Mortage Refinance Company (TMRC) imekabidhi msaada wa shilingi milioni nane kwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuwezesha matibabu ya moyo kwa watoto wanne.

  Watoto hao watafanyiwa upasuaji wa moyo wa kuziba matundu na wengine kutibiwa mishipa ya damu ambayo haipitishi damu vizuri katika moyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi wa TMRC Oscar Mgaya alisema wameguswa kuchangia fedha hizo ili kuokoa maisha ya watoto hao wenye matatzo ya moyo ambao ni Taifa la kesho.

  “Tumetoa shilingi millioni nane kwa ajili ya upasuaji wa kutibu magonjwa ya moyo kwa watoto wanne, tumeguswa kutoa fedha hizi ikizingatiwa watoto wengi ni wadogo hawajafikisha hata miaka mitano na watalaam wanaeleza ikiwa hawatapatiwa matibabu hasa ya upasuaji kwa wakati muafaka wataweza kupoteza maisha”,.

  “Moyo ni kiungo cha muhimu sana katika mwili wa binadamu, unaweza kukosa mguu au mkono ukaishi lakini siyo moyo, binadamu akikosa moyo hawezi kuishi”, alisema.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi aliishukuru Taasisi ya TMRC kwa kutoa fedha hizo ambazo zitaokoa maisha ya watoto wanne wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo.

  Prof. Janabi alitoa rai kwa Taasisi zingine kuiga mfano na kuendelea kujitokeza kufadhili matibabu ya watoto ambao bado wanasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo.

  0 0


  Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) David Nzarigo akipandishwa kwenye gari ya Polisi Baada ya agizo la Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola akipokea taarifa ya shughuli zinazofanywa na Mgodi huo.
  Mganga Mkuu wa Mgodi ambaye pia anasimamia kitengo cha mazingira Mgodini wa Dhahabu wa Geita(GGM)akitoa taarifa ya namna ambavyo mgodi umekuwa ukihifadhi mazingira.
  Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akitazama baadhi ya nyaraka wakati ambapo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola.
  Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo akipelekwa kwenye gari la polisi na askali baada ya agizo la Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola.
  Moja kati ya Nyumba ambayo hipo ndani ya eneo la Mgodi.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola akikagua madarasa ambayo yanaonekana kuharibiwa na mipasuko.


  Na Joel Maduka,Geita

  Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo amekamatwa na serikali baada ya kudaiwa kukutwa na nyaraka za serikali .

  Mwanasheria huyo amekamatwa kwa amri ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola alipotembelea Mgodi huo ambapo pamoja na mambo mengine amebaini mgodi huo kuwa unaendesha shughuli zake bila kufuata sheria ya mazingira .

  Akiwa katika katika ziara ya kikazi ya siku mbili Wilayani Geita,Mhe.Kangi Lugola ameagiza kukamatwa kwa mwanasheria huyo baada ya kudaiwa kukutwa na nyaraka za serikali ambazo hazijawa rasmi kutumika kutoka taasisi ya wakala wa utafiti wa jiolojia Tanzania(GST).

  Hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida na bila kutarajiwa.Mwanasheria huyo aliyekuwa akiukingia kifua mgodi huo ili usikumbane na rungu la fidia ya uharibifu wa kimazingira kama sheria inavyotamka, alijikuta akimweleza Naibu Waziri kuwa anayo ripoti ya GST aliyodai haijaeleza iwapo mgodi huo unahusika moja kwa moja kwenye uharibifu hivyo mgodi huo usibebeshwe mzigo huo.

  Kutokana na hali hiyo,Naibu Waziri Lugola aliomba apatiwe ripoti hiyo ili ajiridhishe,lakini mwanasheria huyo akijibu kwa kujiamnini alimtaka kiongozi huyo wa juu kutumia mbinu zake kuipata Serikalini, lakini yeye hawezi kutoa nyaraka ya serikali, jambo lililomkasirisha Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira na kutoa agizo la kukamatwa mara moja.

  Diwani wa kata ya mtakuja Constatine Morandi ameelezea kuwa wananchi wamekuwa wakisumbuliwa muda mrefu na mgodi bila ya kupatiwa fidia na kwamba kutokana na wao kuwa ndani ya bikoni kumesababisha kutokupatiwa huduma mbali mbali za kijamii hivyo ni vyema kwa serikali wakaweka nguvu kuwasaidia wananchi hao.

  Bw Abdallah Omary-Mkazi Nyamalembo alimweleza Naibu waziri kwamba wamekuwa wakiishi maisha ya mashaka kutokana na hali ilivyo ya maeneo hayo ya mgodini na kwamba mgodi ulikwisha wai kuwapatia fidia ya shilingi elfu ishirini jambo ambalo limeonekana kuwa ni udhalilishaji kwani pesa hiyo ni ndogo.

  Kwa upande wake Makamu wa Rais wa mgodi huo Saimon Shayo,alisema kuwa eneo ambalo wananchi wamekuwa wakilalamika kuhusu suala la fidia hadi sasa kuna nyumba mbili na kwamba fidia ya kwanza walilipa kiasi cha sh,Bilion Moja na waliipatia serikali iweze kuwafidia wananchi

  0 0


  Meneja wa Njia Kuu za Umeme,Mhandisi Amos Kaihula akitoa mada katika mkutano wa wanakijiji cha Misigiri mkoani Singida
  Mkuu wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida,Emanuel Luhahula akizungumza
  Meneja wa Njia Kuu za Umeme,Mhandisi Amos Kaihula akizungumza na waandishi wa habari


  Meneja wa Njia Kuu za Umeme,Mhandisi Amos Kaihula akisisitiza jambo kwenye mkutano huo

  WANANCHI wa kijiji cha Misigiri mkoani Singida wakifuatilia mkutano huo
  Mmoja kati wa wananchi akiuliza swali katika mkutano huo


  Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Misigiri mkoani Singida wakifuatilia mkutano huo


  WANANCHI wametakiwa kuithamini na kuitunza miundombinu ya umeme ambayo imewekezwa kwa fedha nyingi ili kuhakikisha wanapata wanapata uhakika wa huduma ya umeme katika maeneo yao yanayowazunguka.

  Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida Emanuel Luhahula ambapo amesema kumekuwa na viashiria vya baadhi ya watu kuihujumu miundombinu ya umeme kwa maslahi binafasi jambo ambalo kufanya hivyo kunaathiri upatikanaji wa hudumaa hizo kwa wananchi.

  “Lakini wanafanya hivyo bila kuthamini jitihada kubwa zinazofanywa na serikali …Hawa ni wanaoihujumu miundombinu ya umeme hawatavumiliwa hata kidogo kwa maana wanarudisha nyuma jitihada za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais JPM ambayo malengo yake makubwa ni kuinua uchumi wa wananchi kupitia viwanda ”Alisema.

  Alisema viwanda hivyo vinategemea umeme na ndio maana serikali imeamua kuwekea kwenye nishati ya umeme hivyo watakaobainika wamehusika kuharibu miundombinu watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.

  Aidha aliwaomba wananchi kushirikiana na serikali ikiwemo shirika la Tanesco kuhakikisha miundombinu ya umeme iliyopo kwenye maeneo yao inatunzwa sanjari na kuwafichua watu wote wenye nia ovu ya kurudisha nyuma maendeleo kwa kuihujumu.

  Awali akizungumza Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Polisi (OCD) Bw Kimolo alisema kuwa kosa la uharibifu wa miundombinu ya umme ni sawa na lile la kuhujumu uchumi hivyo wananchi wasilichukulie kama jambo la mzaha.Alisema uhujumu uchumi ni kosa kisheria hivyo wananchi wanapaswa kujihadhari na vitendo vya uvunjifu wa sheria kwani serikali ipo macho kwa kushirikiana na wananchi ili kuwafichua uhalifu huo.

  Kwa upande wake akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Misigiri Mkoani Singida,Meneja wa Njia kuu za Umeme Mhandisi Amosi Kaihula alisisitiza suala la utunzaji wa miundombinu kuwa ni jukumu wananchi wanaoishi kwenye maeneo iliyopo kwani ni mali ya umma na shirika hilo limepewa dhamana ya kuisimamia.

  Ubadhirifu wa miundombinu hii una madhara makubwa ikiwemo kusababisha nchi kukosa umeme lakini pia kupelekea matatizo ya kukatikakatika kwa huduma hiyo kwenye baadhi ya maeneo jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya Taifa”Alisema.liongeza licha ya kurudisha nyuma maendeleo lakini pia kusababisha kukosekana kwa huduma za kitabibu na kusimama kwa shughuli za viwanda unaosababishwa na ukosefu wa umeme baada ya miundombinu kuhujumiwa.

  Hata hivyo aliwataka wananchi kushirikiana kuitunza miundombuni ya umeme ikiwemo kuachana na tabia za kufanya shughuli za uchumi karibu na miundombinu ya umeme lakini wahakikishe wanachukua tahadhari wanapoona nyaya za umeme zimeanguka au kuwepo kwa hitilafu yoyote ili kuepuka ajali za umeme.


  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro akikagua ajali iliyotokea kati ya roli aina ya fuso na basi la kampuni ya Adventure lenye no T 186 AKX, iliyokuwa ikitokea mkoani katavi kwenda mkoa wa Kigoma, ajali hiyo imetokea eneo la Mishamo barabara ya Kigoma – Mpanda mkoani Katavi wakati akitokea mkoa wa Kigoma alipokuwa na ziara ya kikazi siku mbili.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro wa kwanza mkono wa kulia akiangalia ajali iliyotokea kati ya roli aina ya fuso na basi la kampuni ya Adventure lenye no T 186 AKX iliyokuwa ikitokea mkoani katavi kwenda Mkoa wa Kigoma, ajali hiyo imetokea eneo la Mishamo barabara ya Kigoma – Mpanda mkoani Katavi wakati akitokea mkoa wa Kigoma alipokuwa na ziara ya kikazi siku mbili.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, alievaa nguo ya kijani akishilikiana na wananchi kupata ufumbuzi wa magari yaliokuwa yamepata ajali kati ya roli aina ya fuso na basi la kampuni ya Adventure lenye no T 186 AKX iliyokuwa ikitokea mkoani katavi kwenda mkoa wa Kigoma, ajali hiyo imetokea eneo la Mishamo barabara ya Kigoma – Mpanda mkoani Katavi wakati akitokea mkoa wa Kigoma alipokuwa na ziara ya kikazi siku mbili.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, akipokelewa na maafisa wa Jeshi la Polisi mkoani katavi baada ya kuwasili mkoani humo.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro akiagana na wananchi waliokuwa wamepa ajali baada ya kuhakikisha ufumbuzi wao wa kuondoka umepatikana, ajali hiyo iliyotokea kati ya roli aina ya fuso na basi la kampuni ya Adventure lenye no T 186 AKX iliyokuwa ikitokea mkoani katavi kwenda mkoa wa Kigoma, ajali hiyo imetokea eneo la Mishamo barabara ya Kigoma – Mpanda mkoani Katavi wakati akitokea mkoa wa Kigoma alipokuwa na ziara ya kikazi siku mbili.Picha Na Jeshi La Polisi

  0 0

   Maofisa wa NBC wakiendesha droo ya pili ya Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Humudi Semvua kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Meneja Masoko wa NBC, Alina  Kimaryo, Meneja Amana za Wateja, Dorothea Mabonye na Meneja Maendeleo ya Biashara wa NBC, Amos lyimo. Jumla ya washindi 12 wakijishindiaa kila mmoja shs milioni 1.
   Meneja Masoko wa NBC, Alina Kimaryo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uchezeshaji wa droo ya pili ya Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana ambapo washindi 12 walijishindia kila mmoja shs milioni 1. Katikati ni Meneja Amana za Wateja wa NBC, Dorothea Mabonye na Meneja Maendeleo ya Biashara wa NBC, Amos Lyimo.
  Meneja Maendeleo ya Biashara wa NBC, Amos Lyimo (kulia) akipiga simu kwa mmoja wa washindi  wakati wa droo ya pili ya Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humudi Semvua, Meneja Masoko wa NBC, Alina Kimaryo na Meneja wa Amana za Wateja, Dorothea Mabonye. Washindi 12 walijishindia shs milioni 1 kila mmoja.


  0 0

  CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimewataka viongozi wake wote waliochaguliwa hivi karibuni katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanawatumikia wanachama na wasio wanachama kwa uadilifu na uzalendo ili kuendelea kukijengea imani Chama hicho kwa watu wote. 

  Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Nzega na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati anakabidhi vitendea kazi (pikipiki 19) kwa viongozi na watendaji wa Chama hicho katika Jimbo la Nzega vijijini vilivyotolewa na Mbunge wao na kuweka jiwe la Msingi kwenye Kitega Uchumi CCM wilaya ya Nzega.
  Alisema kuwa uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kwa viongozi wapya walichaguliwa kuwatumikia wanachama wote waliowachagua na ambao hawakuwachagua ili kuendelea kukiimarisha Chama chao. 

  Kinana alisema kuwa uchaguzi umekwisha kinachofuata ni kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2015 hadi 2020, ahadi za Mgombe wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizitoa wakati akiomba kura na zile zilizotolewa na Wabunge ambazo hakuwa katika Ilani. Alisema kuwa ni muhimu kwa MwanaCCM na watumishi wa umma na wananchi wengine kuhakikisha wanatekeleza Ilani ya Chama hicho ambacho kiko madarakani. 

  Aidha Kinana aliwataka viongozi na watendaji waliopatiwa vifaa hivyo kuvitumia kwa ajili ya shughuli za kukiimarisha zaidi Chama na sio kwa ajili ya mambo mengi ambayo sio malengo yake. 

  Naye Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala alisema kuwa uchanguzi umekwisha ni vema wakawa wamoja kwa ajili ya kuendelea kujenga Chama chao. 

  Alisema kuwa ataendelea kushirikiana na wanachama wote walioshinda na walioshindwa kwa ajili ya kuimarisha mshikamano ndani ya CCM na kwa ajili kuendelea kukipa matokeo mazuri katika chaguzi mbalimbali zijazo. 
  Dkt. Kigwangala alisema kuwa pikipiki 19 ni za CCM na sio ya watu waliokabidhiwa na hivyo viongozi na watendaji wa Chama waliopata wanatakiwa kuzitumia katika kuimarisha Chama hicho kwenye maeneo yao ya kazi. Alisema kuwa Jimbo la Nzega Vijiji ni kubwa kwa hiyo usafiri huo utawasaidia kuwafikia wanachama na watu wengi na hivyo kukijenga Chama hicho.

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Dkt. Edmund Bernard Mndolwa ametengua ushindi wa Ndg. Ngingite Nassoro Mohamed ambaye alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia Jumuiya ya Wazazi (Bara) baada ya kubaini uwepo wa kasoro kubwa katika uhesabuji wa kura wakati wa uchaguzi.

  Kufuatia uamuzi huo Dkt. Edmund Mohamed Mndolwa amemtangaza Ndg. Kitwala Erick Komanya kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia Jumuiya ya Wazazi (Bara) .
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Edmund Benard Mndolwa akizungumzia kuhusu kutengua ushindi wa mjumbe mmoja aliyechaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi kwa upande wa Tanzania bara. 

  0 0

  Mtaalamu wa Masuala ya Ukatili wa Kijinsia na Ustawi wa Jamii kutoka Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Ofisi ndogo ya Kibondo akizungumza na Wanawake wakimbizi wa Kambi ya Mtendeli iliyopo katika Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma juu ya Biashara ya ufumaji wa bidhaa kwa wanawake hao waishio ndani ya kambi hiyo na kupatiwa ujuzi wa kuweza kujiongezea kipato.
  Muwezeshaji wa Wanawake wa kutoka Shirika la IRC linalofadhiliwa na UNHCR,Beatrice Emmanuel akitoa maelezo namna kikundi cha wanawake wafumaji wanavyoweza kujiongezea kipato katika familia zao kwa kutengeneza na kuuza bidhaa zao katika soko la pamoja linalojumuisha wakimbizi na Watanzania wanaoishi katika vijiji vya jirani na eneo la kambi ya wakimbizi ya Mtendeli. Pia wageni mbalimbali wanaowatembelea eneo la kambi kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali ikiwemo wahisani na wadau mbalimbali. lengo la mradi huu wa ufumaji ni kuwawezesha wanawake kupata ujuzi utaowawezesha kujiongezea kipato ili pindi watakaporejea  nchini mwao kila mwanamke aweze kuwa na shughuli inayoweza kumuingizia kipato
   Afisa Uzalishaji kutoka IRC, Foibe Julius, akitoa maelekezo ya namna ya kusuka vikapu  kwa mmoja wa Mwanamke Mkimbizi anayeishi katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli iliyopo katika Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma 
  Msaidizi Mkuu wa Makazi katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli- Lulu Malima akiangalia moja ya Bidhaa zilizofumwa na Wanawake wakimbizi wa kambi hiyo ambao wameweza kuuza na kujiongezea kipato ili kuweza kujikimu katika maisha yao.
  Wanawake wanaoishi katika kambi ya Wakaimbizi ya Mtendeli ya Wilaya ya Kakonko mkoa wa Kigoma wakipanga bidhaa zao katika hali ya usafi ili kuwawezesha wanunuzikuziona kwa urahisi katika eneo lao na kununua.
  Mmoja ya Wanawake kutoka kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli Wilaya ya Kakonko akifuma  kikapu katika eneo la mafunzo linalofadhiliwa na UNHCR kupitia shirika la IRC
   Wanawakewaishio katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli wakifuma  vikapu katika eneo la mafunzo linalofadhiliwa na UNHCR kupitia shirika la IRC
   Wanawake waishio katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli Wilaya ya Kakonko Wakifuma  Vikapu katika eneo la mafunzo linalofadhiliwa na UNHCR kupitia shirika la IRC

  0 0


  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameagiza taasisi zote zinazohusika na udhibiti wa maudhui ya luninga nchini kubuni mkakati wa pamoja wa kuboresha udhibiti.

  Dk Mwakyembe ametoa rai hiyo baada ya kuzikutanisha taasisi hizo za udhibiti leo jijini Dar Es Salaam.

  "Nyinyi nyote ni taasisi za Serikali, hivyo tengenezeni mkakati wa kufanya kazi kwa pamoja kudhibiti maudhui mabovu ili kulinda  maadili ya jamii yetu," alisema.Waziri Mwakyembe alifanya mkutano wa pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

  "Kuna hitaji za kuongeza uwezo wa kufuatilia maudhui ya luninga ikiwa ni pamoja na filamu zote ili kubaini maudhui hasi kwa jamii yetu na kuzishughulikia ipasavyo kabla hazijaleta madhara kwa jamii," alisema.

  Alisema changamoto za ongezeko la mahitaji ya jamii zinazidi kukua kwa haraka kutokana na kasi ya maendeleo hivyo ni vizuri kuhakikisha  kuwa majawabu yake yanapatikana.

  Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi Susan Mlawi, alisema Wizara itaangalia jinsi ya kuunganisha majukumu ya taasisi zinazosimamia maudhui ya vyombo vya utangazaji nchini ili kuimarisha udhibiti wa pamoja. 

  Akiongea katika mkutano wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dodoma mapema wiki hii, Rais John Pombe Magufuli aliiagiza Wizara ya Habari na TCRA kutosita kuvichukulia hatua vyombo vya utangazaji zinavyokiuka kanuni za utangazaji nchini.
   Dk Mwakyembe akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA,Bi.Valerie Msoka,
   Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi Suzan Mlawi, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Eng James Kilaba na Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Chief Fredrick Ntobi.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deo Ndejembi, leo ameendelea na ziara katika kata ya Hogoro na vijiji vyote vitano vya Kata hiyo ambavyo ni Mkutani, Banyibanyi, Nyerere, Hogoro na Chamae. Hogoro ni kata ya 11 kati ya kata 22.

  Mpaka sasa DC Ndejembi amefanya ziara katika vijiji 44 kati ya 87 na Kata 11 kati ya 22. Lengo la ziara hii ni muendelezo wa kampeni yake ya Ondoa Njaa Kongwa( ONJAKO) iliyozinduliwa msimu huu wa Kilimo inayohimiza kilimo cha Mtama na Uwele ili kuhakikisha kuna usalama wa chakula wilayani. 
  Vile vile akiwa katika vijiji hivyo DC Ndejembi husikiliza kero mbali mbali za wananchi na kutoa maagizo na maelekezo yenye kulenga kutatua kero hizo.Katika majukumu yake DC Ndejembi alikwisha tembelea kata zote 22, ila kwa sasa atatembelea Vijiji vyote 87 katika Wilaya ya Kongwa.
  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deo Ndejembi, leo akizungumza na baadhi ya wananchi wa kata ya Hogoro,wilayani humo.Mh Deo ameendelea na ziara yake katika kata ya Hogoro na vijiji vyote vitano vya Kata hiyo ambavyo ni Mkutani, Banyibanyi, Nyerere, Hogoro na Chamae. Hogoro ni kata ya 11 kati ya kata 22.
  Baadhi ya wananchi wakimsikilia Mkuu wa wilaya ya Kongwa,Mh Deo alipofanya  ziara katika kata ya Hogoro na vijiji vyote vitano vya Kata hiyo ambavyo ni Mkutani, Banyibanyi, Nyerere, Hogoro na Chamae. Hogoro ni kata ya 11 kati ya kata 22.


  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua hospitali ya wilaya ya Misungwi.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata taarifa ya miradi ya elimu kutoka kwa viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa maabara katika sekondari ya Misasi.


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo ametilia shaka makusanyo katika hospitali ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na kuagiza kusimamiwa vyema ukusanyaji mapato.

  Jafo ameyasema hayo katika ziara yake ya kikazi ndani ya Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo alisema amegundua kuna kila dalili kwamba mapato ya hospitali hiyo yanavuja kutokana na taarifa nyingi za fedha za Malipo ya wagonjwa kutoingizwa kwenye mfumo wa kielekroniki hivyo kusababisha kukusanya wastani wa Sh.milioni 4 kwa mwezi. 

  Katika ziara hiyo, Jafo amezungumza na watumishi wa Halmashauri ya Misungwi ambapo amewasisitiza watumishi na viongozi kuwa na mahusiano mema ili waweze kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo.

  Jafo amesisitiza kwamba kila mmoja anapasa kumthamini mwenzake na kushirikiana katika kazi ili kuwaletea wananchi maendeleo.

  Aidha Jafo amewapongeza walimu wa shule ya sekondari Misasi kwa kufanya vyema sana kwani wamefanikiwa kupeleka watoto 45 kidato cha tano kati ya wanafunzi 100 waliomaliza kudato cha nne mwaka jana.

  Baada ya ziara hiyo waziri Jafo ameendelea na ziara yake wilayani sengerema mkoani Mwanza

  0 0


  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe leo Jijini Dar es Salaam kuashiria uzinduzi wa Mfumo wa MaxBurudani ulioandaliwa na Kampuni ya MaxMalipo wenye lengo la kusambaza kazi za wasanii.
  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) pamoja na viongozi wa Kampuni ya MaxMalipo wakionyesha baadhi ya kazi za wasanii zitakazosambazwa na Kampuni hiyo kupitia mfumo wa MaxBurudani leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mfumo huo.  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Wasanii (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa MaxBurudani ulioandaliwa na Kampuni ya MaxMalipo wenye lengo la kusambaza kazi za wasanii.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya MaxMalipo Afrika Mhandisi James Kasati akizungumza na Wasanii (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa MaxBurudani ulioandaliwa na Kampuni hiyo wenye lengo la kusambaza kazi za wasanii.
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na wasanii mbalimbali (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Mfumo wa MaxBurudani ulioandaliwa na Kampuni ya MaxMalipo wenye lengo la kusambaza kazi za wasanii.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Bw. Godfrey Muingereza akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na wasanii mbalimbali (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Mfumo wa MaxBurudani ulioandaliwa na Kampuni ya MaxMalipo wenye lengo la kusambaza kazi za wasanii.
  Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Niki wa Pili akizungumza kwa niaba ya wasanii wezake baada ya uzinduzi wa wa Mfumo wa MaxBurudani ulioandaliwa na Kampuni ya MaxMalipo wenye lengo la kusambaza kazi za wasanii.

  …………………………………………………………………………………

  Na Shamimu Nyaki – WHUSM.

  Serikali imewataka wasanii kutengeneza kazi nzuri zenye ubora zinazozingatia maadili ya Kitanzania ili kuwavutia wawekezaji wengi wanaotaka kudhamini kazi hizo katika kuziandaa na kuzisambaza.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati akizindua Mfumo wa MaxBurudani ulioandaliwa na Kampuni ya MaxMalipo ambapo ameishukuru Kampuni hiyo kwa kuamua kuchukua dhamana ya kusambaza kazi za wasanii ili kuondoa kero ya muda mrefu ya wizi wa kazi za wasanii hao kupitia njia mbalimbali walizokuwa wanatumia wasanii hao ambazo zilikua zikiwalipa kiasi kidogo.

  “Nimefurahishwa sana na Mfumo huu namna ambavyo utaweza kutatua changamoto ya wizi wa kazi za wasanii wetu kwa vile umeonyesha wazi namna ambavyo msanii anaweza kunufaika na kazi yake kuanzia idadi ya kazi zake zilizoenda sokoni,asilimia anazopata kwa kazi yake ambayo ni kuanzia 40-50 pamoja na kumuwezesha kutouza Haki Miliki yake kama walivyokuwa wanafanya hapo awali.”Alisema Mhe.Mwakyembe.

  Aidha amewataka Wasanii kutengeneza kazi zenye ubora ambazo zitakidhi vigezo vyinavyotakiwa na Kampuni hiyo ambapo pia ameiagiza Kampuni hiyo kutochukua kazi yeyote ambayo itakuwa haina ubora wala kuwa na maadili.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mhandisi James Kasati amesema kuwa Mfumo wa MaxBurudani inalengo la kuhakikisha wasanii wananufaika na kazi zao kwa kuwa ndio kundi lililoajiri vijana wengi hapa nchini.

  Mhandisi Kasasi ameongeza kuwa Mfumo huu utatumia mawakala wa Max Malipo katika kusambaza kazi hizo ambapo Msanii atatakiwa kupeleka kazi ambayo itakuwa imekidhi vigezo vya kusmbazwa na Kampuni hiyo ndani na nje ya nchi kwa zile nchi ambazo Kampuni hiyo ina matawi.

  “Mfumo huu utatumia teknolojia katika kusambaza kazi za wasanii,kulinda Haki Miliki za Wasanii lakini pia msanii kujua takwimu sahihi za mchanganuo wa kazi yake pamoja na namna ambavyo anaweza kulipa kodi kwa Serikali”.Alisema Mhandisi Kisati.

  Naye Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi.Joyce Fissoo amesema kuwa Bodi yake inapokea Kampuni au mtu yeyote ambae anataka kusambaza kazi za wasanii endapo tu atakuwa anawalipa Wasanii hao kile wanachostahili kupata kupitia kazi hizo.

  Aidha Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Muingereza mbali na kuipongeza Kampuni hiyo kwa Wazo zuri lakini pia ameishauri kuona ambavyo inaweza kuwasadia wasanii hao kupata mikopo itakayowasaidia kuandaa na kutengeneza kazi nzuri.

  Mfumo huo tayari umeanza kupokea baadhi ya kazi za wasanii tayari kwa kuzisambaza ambazo ni Filamu ya Kampuni ya J For Life, Albamu ya Fiesta pamoja na Albamu ya Msanii wa Nyimbo za Injili Bw. Godluck Gosbert.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akihutubia katika mkutano maalum wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, uliofanyika mjini Dodoma ili kujadili masuala ya Mitaji na Mpango wa Kuziunganisha Benki za Wananchi Tanzania.
  Washiriki wa mkutano maalum wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mkutano huo uliofunguliwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Mjini Dodoma.
  Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Benard Kibesse (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Benki za Wananchi –COBAT, Bw. Rukwaro Senkoro, wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), mijini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akifurahia jambo na Mbunge wa Mtwara Vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia baada ya kufungua mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, uliofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa Nne kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, Bw. Rukwaro Senkoro, nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
  Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),(kulia), anaeshughulikia masuala ya kibenki Bw. Kened Nyoni na Kaimu Kamishna Msaidizi Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Michael Nyagoga (Kushoto) wakifuatalia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi (COBAT), uliofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
  Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania (COBAT), Bw. Mugwagi Stephen akizungumza katika mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi uliofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma. Kulia kwake ni Mweyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mhe. Hawa Ghasia na Kushoto kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
  Mbunge wa Mtwara Vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) ili aweze kufungua mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi kwaniaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, uliofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)


  Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania BOT kuzifutia leseni benki zote za biashara pamoja na benki za wananchi zitakazoshindwa kukidhi vigezo vya kuendesha shughuli za kibenki nchini.

  Ametoa agizo hilo mjini Dodoma katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, wakati akifungua Mkutano Maalum wa Wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania (COBAT).

  “kwa taarifa niliyonayo hadi sasa baadhi ya benki hazijatimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji wa kutosha, hali ambayo haiwezi kuachwa iendelea hata kidogo, kwani haiimarishi sekta ya fedha na haiwasaidii wananchi kuendelea kiuchumi” alisema Waziri Kassim Majaliwa katika hotuba hiyo.Alisema Benki Kuu ilitoa muda hadi mwishoni mwa Desemba 2017, benki za wananchi ziweze kuongeza mtaji na kwamba muda huo hautaongezwa na wala Serikali haitatoa mtaji kwa benki hizo.

  “Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania haitasita kuifungia benki yoyote na kufuta leseni yake ya biashara pindi itakapobaini inavunja sheria, ikiwa ni pamoja na kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi ambao unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na amana za wateja kama tulivyofanya kwa Mbinga Community Bank PLC kuanzia tarehe 12/5/2017” alisema Dkt. Mpango kwa niaba ya Waziri Mkuu.

  Maagizo hayo yamekuja siku moja baada ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kuiagiza Wizara ya Fedha na Mipango wakati akifungua tawi kuu la Benki ya CRDB mjini Dodoma, kuhakikisha kuwa Benki Kuu ya Tanzania-BOT, inazifuta benki zote zinazoshindwa kujiendesha kibiashara hata kama zinamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100.

  Alisema Serikali inafanya jitihada mbalimbali ili kuhakikisha benki za wananchi zinaimarika zikiwemo kuruhusiwa kuanzisha mifumo ya ushirikiano katika Nyanja ya Mfumo wa Mawasiliano na Habari (ICT), Idara za Ukaguzi wa Ndani (Internal Audit Services), kupunguza wingi wa idara na kuwa na idara tatu (3) tu muhimu, kuruhusiwa kuungana (Federation), ambazo zitapunguza gharama za uendeshaji wa benki za wananchi na kuleta ufanisi katika kutoa huduma.

  “Napenda kusisitiza kuwa sekta ya benki ni muhimu sana kwa uhai na ukuaji wa uchumi kama ilivyo damu kwa mwili wa binadamu na kutokana na umuhimu wake huo, sekta hii ni kati ya sekta chache zinazosimamiwa kwa karibu sana ili kulinda amana za wateja pamoja na kuhakikisha uhimilivu wa mfumo mzima wa sekta ya fedha na mwenendo wa uchumi wa Taifa” aliongeza Dkt. Mpango

  Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania (COBAT) Bw. Rukwaro Senkoro, alisema hadi kufikia Juni, 2017, Benki za Wananchi nchini zilikuwa na wateja zaidi ya milioni 1.4, wateja wa vikundi zaidi ya 10,000, Matawi 12, Vituo 59, na wanahisa 66,492.

  “Benki hizo zina amana zenye thamani ya shs bilioni 74.2, zimetoa mikopo ya sh. bilioni 56.8, na jumla ya mali zenye thamani ya shs. bilioni 92.3” Alisema Bw. Senkoro.Hata hivyo, kutokana na Utafiti wa Matumizi ya Huduma za Kifedha uliofanyika mwaka 2017 umebaini kuwa asilimia 28 ya wananchi bado hawapati huduma za kifedha hapa nchini hususan vijijini na kutaja changamoto ya ukosefu wa mitaji ya benki hizo kukwaza sekta hiyo. 

  Dhana kuu ya mkutano huo wa COBAT uliowashirikisha wadau mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ni “Mitaji na Mpango wa Kuziunganisha Benki za Wananchi Tanzania”, ambayo ni dhana mpya.

  0 0

  Kisima Cha Maji Kilichochimbwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR)katika Kijiji cha Kasanda ambacho kitawanufaisha Wananchi wa Maeneo hayo na Wakimbizi waishio katika Kambi ya Mtendeli Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.
  Moja wapo ya bomba la maji yaliyosambazwa ndani ya Kambi ya Wakimbizi Mtendeli kutoka katika mojawapo ya Visima Vilivyochimbwa katika Vijiji Jirani na eneo la Kambi.
  Wahandisi wa Maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) na Shirika la TCRS wakikagua chumba chenye mashine ya kuchuja na kusafisha maji yanayotoka katika kisima kilichochimbwa kwa ajili ya matumizi ya Wakimbizi waishio katika Kambi ya Mtendeli Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma.

  Mhandisi wa Maji kutoka shirika la TCRS Linalofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),Emmanuel Busanga akitoa maelezo juu ya mahitaji ya maji katika kambi ya Mtendeli iliyopo Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma
  Muhandisi wa Maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),Mukiza Florinus akitoa maelezo kwa Mwandishi wa habari wa Gazeti la The Guardian ,Getrude Mbago ambaye ni sehemu ya ujumbe wa waandishi watano waliotembelea kambi za wakimbizi

  0 0

   Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega, akizindua  zoezi la upigaji chapa mifugo  katika kijiji cha Kelema wilaya ya Nchemba mkoani Dodoma.
   Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega, zoezi la upigaji chapa  mifugo katika kijiji cha Mungoroma wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.

   Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mungoroma wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.
   Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega akimsikiliza Kaimu Meneja wa poli la akiba Swagaswaga Deogratius Swai kuhusu mifungo iliyokamatwa katika poli hilo kuanzia Julai mwaka hadi Desemba mwaka huu.. PICHA NA HALIMA KAMBI
  Muonekano wa mifungo hiyo iliyo kamatwa katika poli la akiba la Swagaswaga

  0 0

   Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile aliyevaa shati la drafti la mikono mirefu akikagua baadhi ya majengo ya kituo cha afya cha Nduruma  ambayo yapo kwenye ujenzi wakati wa ziara yake Jijini Arusha leo.
   Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa kwanza kulia akiangalia kwa makini dawa zilizopo kwenye hifadhi ya dawa ya kituo cha afya cha Nduruma wakati alipotembelea kituo hiko kwenye ziara yake jijini Arusha.
   Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati akiangia mojawapo ya  nyenzo za kuhifadhia dawa za maji (syrup) katika kiwanda cha kuzalisha dawa nchini TPI  wakati alipotembelea kiwanda hiko kwenye ziara yake jijini Arusha, kushoto ni Naibu Mkurugenzi  Mtendaji wa TPI Bi. Zarina Madaba.
  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  wa pili kulia akipata maelekezo namna kiwanda cha TPI kinavyofanya kazi ya kuzalisha dawa muhimu nchini kutoka kwa Naibu Mkurugenzi  Mtendaji wa TPI Bi. Zarina Madaba.

older | 1 | .... | 1460 | 1461 | (Page 1462) | 1463 | 1464 | .... | 1897 | newer