Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1459 | 1460 | (Page 1461) | 1462 | 1463 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mafundi wa Kampuni ya Yapi Merkezi wakiendelea na kazi ya kujaza zege kwenye moja ya kalvati linalojengwa kwenye Reli ya Kisasa (Standard Gauge), katika eneo la Kisarawe Mkoani Pwani.
  Muonekano wa moja ya kalvati linalojengwa kwenye Reli ya Kisasa (Standard Gauge), katika eneo la Kisarawe Mkoani Pwani. Mradi huo unajengwa kwa awamu mbili ambapo sehemu ya kwanza inajengwa kutoka Dar es Salaaam mpaka Morogoro ambapo sehemu ya pili itajengwa kutokea Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma.
   
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali ya Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (kushoto), kuhusu kusimamia kwa karibu mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge), wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo katika kijiji cha Soga Mkoani Pwani na Ngerengere mkoani Morogoro.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali ya Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (kulia), alipomweleza hatua za ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge), wakati Waziri huyo alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Mkoani Pwani.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akichanganya zege katika moja ya Makalvati yanayojengwa katika mradi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge), katika eneo la Kisarawe alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Mkoani Pwani.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), akibonyeza kitufe cha kuruhusu zege kwenda kwenye kalvati linalojengwa kwenye Reli ya Kisasa (Standard Gauge), wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Mkoani Pwani.
   
  Tingatinga likiendelea na kazi ya kuchenjua tabaka la chini la Reli ya Kisasa (Standard Gauge), katika eneo la Soga, Mkoani Pwani.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa wito kwa mkandarasi Yapi Merkezi na Motaengil Africa wanaojenga reli ya kisasa (Standard Gauge Railway), kufanya kazi kwa uadilifu, kulingana na vipimo vilivyo kwenye mkataba ili kuwezesha mradi huo kukamilika kwa wakati.

  Aidha, ameitaka Kampuni Hodhi ya Rasilimali za reli (RAHCO), kuhakikisha kuwa inafuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo kwani wananchi wamekuwa wakisubiri kukamilika kwake na kuanza kupata huduma za usafiri wa treni zitakazorahisisha shughuli zao za kibiashara na kijamii.

  Akizungumza leo mara baada ya kukagua mradi huo katika kijiji cha Soga mkoani Pwani, Waziri Mbarawa amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya wakandarasi hao na kuagiza kuongeza spidi zaidi ili ifikapo mwaka 2020 mradi huo uwe umekamilika.“Kasi mnayoenda nayo sio mbaya, ila naomba RAHCO mhakikishe mnasimamia kwa karibu kuhakikisha spidi inaongezwa ili kazi ikamilishwe haraka na kwa viwango”, amesema Profesa Mbarawa.

  Akiwa katika kijiji hicho, Waziri Mbarawa amemwagiza Kaimu Mtendaji Mkuu wa RAHCO, Masanja Kadogosa, kukutana na uongozi wa kampuni hizo kujadili na kuangalia fursa za upatikanaji wa ajira kwa watanzania hususan wakazi wa eneo inapopita reli hiyo.

  Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa RAHCO, Masanja Kadogosa, amesema mpaka sasa mradi huo upo ndani ya muda na kumhakikishia Waziri Mbarawa kuwa mradi utakamilka kwa wakati kwani kazi inayofanyika sasa ni kuweka zege kwa ajili ya ujenzi wa boksi kalvati ambapo kazi hiyo inaendelea vizuri.

  Ameongeza kuwa katika kipindi hiki mradi ulisuasua kutokana na changamoto za mvua za vuli, hivyo amefafanua kuwa wana mpango wa kuongeza kambi nyengine nane upande wa Soga na nane upande wa Ngerengere ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.

  Mradi wa SGR unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa reli kutoka Dar es salaam – Morogoro na ya pili itahusisha sehemu ya Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma pamoja na njia za kupishana ambapo kwa pamoja itakuwa na urefu wa kilometa 722 na itajengwa kwa gharama ya shilingi Trilioni 7.1.

  0 0

   MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kampuni ya ulinzi ya Suma JKT kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 832 Kj cha Ruvu Mlandizi - Kibaha.
   Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Suma JKT, Meja Alfred Mwaijande  akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kampuni ya ulinzi ya Suma Jkt kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 832 Kj cha Ruvu Mlandizi - Kibaha.
  Wahitimu wa mafunzo ya kampuni ya ulinzi ya Suma JKT wakiwa kwenye kufunga mafunzo ya kampuno ya ulinzi ya Suma JKT kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 832 Kj cha Ruvu Mlandizi - Kibaha.(picha na Mwamvua Mwinyi)

  0 0

  Na Afisa Habari Mufindi

  Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William amesema, endapo Ofisi za Umma hazitodhibiti ipasavyo mifumo na urasimu uliowekwa kwenye Ofisi za Serikali, masuala hayo yanaweza kuwa kichocheo kikubwa cha kuendelea kukua kwa tatizo la rushwa katika ofisi hizo.

  Mkuu huyo wa Wilaya ametoa kauli hiyo wakati akifunga maadhimisho ya siku ya Maadili na haki za Binadamu, iliyoadhimishwa kiwilaya katika chuo cha maendeleo ya jamii Rungemba kilichopo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi.

  Mh. Jamhuri amesema, urasimu uliyowekwa kwa nia njema ya kuthibiti utendaji kazi ukitumiwa vibaya, unaweza kuwa chanzo cha rushwa, hivyo akatoa rai kwa taasisi zote za umma kuhakikisha zinazingatia suala la kuwa na mkataba wa huduma kwa wateja na kusisitiza kuwa, hiyo ni moja kati ya njia kuu za kuondoa suala la rushwa katika Ofisi za umma.

  Awali Mkuu wa taasisi ya kuzui na kupambana na rushwa Wilayani Mufindi bw. Orest Mushi, ametanabaisha kuwa tafiti za hivi karibuni zinazoonesha kupungua kwa rushwa nchini, zinatokana na utashi wa kisiasa uliopo, chini ya Rais John Pombe Magufuli, huku akibainisha malengo ya maadhimisho hayo, kuwa ni pamoja na kuiwezesha Serikali kufuatilia na kufahamu hali ya rushwa nchini, kubainisha madhara ya rushwa na kutambua umuhimu wa kuendelea kupambana nayo, kutambua changamoto za mapambano dhidi ya rushwa, kuweka mikakati ya kupambana na rushwa, sanajari na kuisaidia nchi kutathimini ushiriki wake dhidi ya mapamabano ya rushwa kimataifa.

  Mwaka 2005 serikali iliamua kwamba maadhimisho haya yawe yanafanyika disemba 10 ambapo, nchi yetu huungana na mataifa mengine duniani kuiadhimisha kama siku ya maadili na haki za binadamu. Kaulimbiu ya mwaka huu ni wajibika piga vita rushwa, zingatia maadili na haki za binadamu, kuelekea uchumi wa kati.
  Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, akiwahutubia wanafunzi wa chuo cha Rungemba pomoja na wananchi wakati maadhimisho ya siku ya Maadili na haki za Binadamu, iliyoadhimishwa kiwilaya katika chuo cha maendeleo ya jamii Rungemba kilichopo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi.
  Sehemu ya Wanachuo wa Chuo cha Rungemba pamoja na Wananchi wakisikiliza hotuba ya mgeni wa heshima wakati wa kufungwa kwa maadhimisho ya siku ya Maadili na haki za Binadamu, iliyoadhimishwa kiwilaya katika chuo cha maendeleo ya jamii Rungemba kilichopo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi.
  Mkuu Takukuru Wilaya ya Mufindi Bw. Orest Mushi, akiwasilisha mada wakati wa maadhimisho ya siku ya Maadili na haki za Binadamu, iliyoadhimishwa kiwilaya katika chuo cha maendeleo ya jamii Rungemba kilichopo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi.

  0 0


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Nzega,Dkt Hamisi Kigwangalla,ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii mapema leo mara baada ya kuwasili kwa ziara fupi ndani ya jimbo la Nzega.kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi pamoja na Katibu wa CCM Wilaya Ndugu Shaibu Ngatiche.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Mbunge wa jimbo la Nzega,Dkt Kigwangalla,mapema leo walipokuwa wakishuhudia ngoma ya asili iliyokuwa ikitumbuiza nje ya Ofisi kuu ya chama  ya wilaya ya Nzega mara baada ya kuwasili kwa ziara fupi kufuatia mwaliko wa Mbunge wa jimbo hilo Dk Hamisi Kigwangalla.kushoto kwake ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi akimkaribisha  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ndani ya Ofisi kuu ya chama  ya wilaya ya Nzega na kuitambulisha kamati kuu ya siasa ya Wilaya mapema leo kabla ya kwenda kwenye mkutano wa ndani wa jimbo hilo.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mbele ya Kamati kuu ya Siasa Wilaya ya Nzega,mkoani Tabora mapema leo,mara baada ya kupokea taarifa fupi za chama ndani ya Ofisi kuu ya chama  ya wilaya hiyo 
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda na viongozi wengine wa chama wakielekea kuweka jiwa la msingi la ujenzi wa Ukumbi utakaotumika kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kijamii,liliojengwa kando kando ya Ofisi kuu ya chama  ya wilaya
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uwekaji rasmi wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ukumbi mkubwa na wa kisasa utakaotumika kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kijamii,uliojengwa kando kando ya Ofisi kuu ya chama  ya wilaya hiyo,kulia kwake ni  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla (aliyevaa mawani katikati).
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla  wakipiga makofi mara baada ya kuwekwa jiwe la msingi la ujenzi wa ukumbi . 
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mbunge wa Jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda pamoja na  Katibu wa CCM Wilaya Ndugu Shaibu Ngatiche wakikagua ujenzi wa ukumbi huo . PICHA NA MICHUZI JR -NZEGA
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mapema leo mbele ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Nzega mkoani Tabora.Ndugu Kinana amefanya ziara wilayani humo mapema leo kwa Mwaliko wa Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla,aidha katika ziara hiyo Ndugu kinana amewapongeza viongozi mbalimbali waliochaguliwa katika ngazi ya chama ya wilaya na pia kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa ukumbi mkubwa wa kisasa ambao utatumika kwa matumizi mbalimbali.PICHA NA MICHUZI JR -NZEGA
   Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM na Wananchi wakishangilia jambo walipokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mapema leo  wilayani Nzega mkoani Tabora.Ndugu Kinana amewasili Wilayani humo kwa ziara fupi ya Mwaliko wa Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla,aidha katika ziara hiyo Ndugu kinana amewapongeza viongozi mbalimbali waliochaguliwa katika ngazi ya chama ya wilaya na pia kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa ukumbi mkubwa wa kisasa ambao utatumika kwa matumizi mbalimbali.PICHA NA MICHUZI JR -NZEGA
  Ndugu Kinana akiagana na baadhi ya Wananchama wa CCM waliofika kumpokea katika Makao Makuu ya Ofisi ya Wilaya hiyo mapema leo mchana.Ndugu Kinana anatarajiwa kuzungumza na wananchi wa jimbo la Nzega katika mkutano wa ndani wa jimbo hilo jioni ya leo.

  0 0

   Meneja Uhusiano wa kampuni ya Aggrey&Clifford, Martha Majura (kulia) akimkabidhi mkurugenzi wa kituo cha Sadeline Health Care Trust, Sara Kitanda (kushoto) mfano wa hundi ili kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Wanaoshuhudia kutoka wa pili kushoto ni wakurugenzi watendaji wa Aggrey & Clifford, Luke Smit, Tel Akuku na Ryan Goslin.
   Wafanyakazi wa Aggrey&Clifford wakigawa zawadi na kufurahi na watoto hao.
   Baadhi ya watoto wakiwa na furaha baada ya kupatiwa zawadi na kuonyeshwa faraja na upendo.
  Wafanyakazi wa Aggrey&Clifford katika picha ya pamoja na watoto hao wanaolelewa katika kituo cha Sadeline.

  Kampuni ya Aggrey&Clifford imetoa msaada wa fedha kusaidia kununua mahitaji kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Sadeline Health Care Trust kilichopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Mbali na msaada wa fedha, imetoa vifaa vya shule na vyakula ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi ambapo pia wafanyakazi wa kampuni walijitolea muda wao kucheza na kufurahi pamoja na watoto hao kwa ajili ya kuwapatia faraja.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Reaching Out Destinies Foundation(RDF) Bi. Jane David akifungua rasmi  kwa maombi sherehe za kuwashukuru wadau wao kwa kuwa nao kwa muda wa mwaka mzima, na baadae kutoa shukurani zake za dhati kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote cha mwaka mzima.
  Mkurugenzi wa Programu na Fedha wa RDF Bi. Queen Mrema akielezea historia ya asasi hiyo,kuwa walianza wakiwa wa 3 lakini kwa sasa wapo zaidi ya 1300,na kwa mwaka huu walifanikiwa kukusanya zaidi ya Tsh milioni 1o ambazo zimeweza kuwasaidia watu wenye makundi maalum wakiwemo yatima na wajane.
   Mkurugenzi wa Miradi ya nje na Mahusiano kutoka (RDF) Bi. Jackline Nicetas akielezea namna asasi yao inavyofanya kazi pia kuwafikia watu mbalimbali wenye uhitaji hasa wale waliopo majumbani, ambapo waliweza kuwaona wajane 3 mkoani Dar es salaam na Mjane mmoja mkoani Pwani, pia wameweza endesha semina,kuwa na camp na mentor ship forum
   Bi Josephine Mbago akitoa shukurani zake za dhati kwa RDF kwa kwenda mpaka mkoani Pwani kumuona Mama yeke ambaye sasa ni Marehemu na kuwasaidia kwa kile walichokuwa nacho, na kusema kuwa alijifunza kuwa 'hautakiwi kuwa na elimu wala pesa ndio uweze kumasidia mtu bali talanta uliyokuwa nayo ndio itakuwa msaada mkubwa kwa wengine', mwisho aliwaombea kwa Mungu awazidishie zaidi pale palipo pungua.
   Mwanadada Pili Amani ambaye pia ni Mwimbaji akitoa ushuhuda wake namna RDF ilivyo msaidia ambapo alisema kuwa unapompa mtu pesa bila kumpa moyo haimsaidii, aliwashukuru sana kwa mambo waliyo mtendea na kuwaombea waendelee kuwa na moyo huo. Alimalizia kwa kusema kuwa kumpenda mtu ambaye haujawahi kuonana nae ni jambo la muhimu na Mungu anakubariki.
   Mwanachama wa RDF Bi. Frida Bariki akishukuru kwa yeye kukutanishwa na RDF ambapo alisema kwake ulikuwa ni ushuhuda mkubwa ambapo amejifunza upendo,moyo mkunjufu na kujitoa pia aliwaombea Mungu awape moyo wa unyenyekevu na awape uwezo wa kutenda mambo makubwa zaidi
   Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwanagati Ambrose Wankamba akitoa pongezi na shukurani kwa asasi ya RDF kwa kuwatembelea ambapo waliweza kuwabadilisha katika mambo mengi sana na kuwaomba wapate kuwatembelea tena pindi watakapo pata nafasi.
   Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mwanagati Bi. Lightness Mamkue akitoa shukurani zake za dhati kwa niaba ya shule yake kwa RDF ambapo wamewafanyia mambo makubwa ambayo kwa moyo wa binadamu hawawezi kuyaona lakini rohoni, ambapo pamoja na wao kuanza kuwalea wanafunzi kiroho zaidi.
   Afisa Elimu Kata ya Mzinga , katika Manispaa ya Ilala Bi. Yusta Grant alisisitiza kuwa pamoja na kuwasaidia watu kifedha au kwa vitu mbalimbali pia ni muhimu kuongea nao na kuwapa moyo kama RDF wafanyavyo.
   Afisa Mtendaji wa Kata ya Mzinga, Manispaa ya Ilala Bw. Geral Salota akitoa salam zake za Shukurani kwa RDF na kuahidi kuendelea kuwaombea kwa kazi kubwa wanayoifanya.
   Bi. Saum Rashid kutoka Ulingo/Jumuia ya Wanawake , akitoa shukurani zake za dhati kwa RDF kwa kuendelea kufanya vizuri katika kazi zao za kuwasaidia wale wenye mahitaji na kuwasihi waendelee hivyo hivyo.
   Mkurugenzi Mtendaji (RDF) Bi. Jane David (kushoto) na
  Mkurugenzi wa Programu na Fedha wa RDF Bi. Queen Mrema (kulia) pamoja na wageni wengine (hawapo pichani) wakimuombea muongozaji wa kipindi cha Jukwaa la mazungumzo kinachoitwa 'Destinies Series' Bi.
  Jackline Nicetas (wa kati kati) kabla ya kipindi hakijaanza.
   Mgeni Rasmi katika sherehe za kutimiza mwaka mmoja wa RDF na ufunguzi wa Jukwaa la mazunguzo la 'Destinies Series' Mchungaji Salome akizungumza mambo mbalimbali ambapo baadhi ya mambo aliyoongelea ni pamoja na kushindwa kujiandaa ama kusimamia vipaumbele vyako sahihi vinaweza kuathiri hatma ya maisha yako.
   'Talk Show' ikiendelea
   Mwongozaji wa kipindi hicho Bi. Jackline Nicetas akiendelea kuchokoza mambo mbalimbali
   Maombi mbalimbali yakiendelea
   Wageni wakiwa wanasikiliza mambo mbalimbali yaliyokuwa yanaendelea wakati wa kutimiza mwaka mmoja wa RDF
   Picha ya pamoja
  Picha zote na Fredy Njeje


  0 0

  Na: Beatrice Lyimo,MAELEZO-DODOMA

  Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameihimiza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuharakisha uandaaji wa Sera ya Riba ambayo zitaifanya taasisi za kifedha kuwa na riba zinazowiana na nafuu.

  Rais Magufuli ameyasema hayo leo Mjini Dodoma wakati wa akizundua tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo jengo la LAPF Makole ambalo ni tawi kubwa kwa mkoa wa Dodoma.

  “Serikali imechukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto za mabenki kutolipwa na wakopaji kwa kuanzisha mfumo wa kuhifadhi taarifa za mkopaji ambazo zitawezesha benki zote kuwatambua wakopaji na kuweza kuchukua tahadhari stahiki, pia itaendelea kutoa vitambulishio vya Taifa ambavyo kwa sasa vina taarifa zote muhimu za mwananchi,” amefafanua Rais Magufuli.

  Aidha, Rais Magufuli ametoa wito kwa BOT kudhibiti matumizi ya dola na fedha nyingine za kigeni hapa nchini kutokana na kuharibu uchumi wa nchi. Dkt. Magufuli ametolea mfano wa fedha zilizoshikiliwa Airport ya Dar es Salaam ambazo ni zaidi ya Dola Bilioni Moja zikiwa hazijulikani zilipokuwa zikipelekwa.

  Vile vile ameiagiza BOT kufungia mabenki na makampuni ya simu ambayo hayatajiunga na kituo cha kuhifadhia taarifa ambacho kina mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali kuhakikisha yamejiunga kufikia mwisho wa mwaka vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

  Rais Magufuli ametoa wito kwa mabenki yote nchini kupeleka huduma za kibenki hadi vijijini kupitia njia mbalimbali kama vile mabenki yanayotembea, mitandao ya simu pamoja na kutumia mawakala ili kuongeza ukwasi kwa mabenki hayo.

  Mbali na hayo Dkt. Magufuli ameitaka Benki ya CRDB kuandaa utaratibu wa kujenga Makao Makuu ya Benki hiyo mjini Dodoma kwani Dodoma ndio Makao Makuu ya nchi na tayari Serikali imeshaanza kuhamia.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amewakaribisha wawekezaji mbalimbali kuwekeza katika Mkoa wa Dodoma na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hao.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei ameipongeza Serikali kwa uamuzi wa ukusanyaji wa kodi kwa kutumia mifumo ya kielektroniki.

  Pia Dkt. Kimei amemkabidhi Rais Magufuli Hundi ya Shilingi Milioni 100 kwa ajili ya ufadhili wa miradi mbalimbali ya kijamii ambapo Rais Magufuli ameikabidhi hundi hiyo kwa uongozi wa Mkoa na kuagiza uongozi huo kujenga Wodi ya wagonjwa katika Hospital ya Mkoa wa Dodoma.

  Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Ali Laay amesema kuwa CRDB imefanikiwa kulipa gawio la shilingi Bilioni 19.5 ambalo lilielekezwa katika uboreshaji wa sekta ya afya nchini.

  0 0  Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla leo amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi na Watendaji wa kata 19 ndani ya jimbo hilo,makabidhiano hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Check Pointi mara baada ya mkutano Mkuu wa jimbo kufanyika.Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana (Wa tatu kushoto) na kulia ni Katibu wa CCM wilaya Nzega Ndugu Janath Kayanda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nzega,Mh.Godfrey Ngapula . Picha na Michuzi Jr-Nzega.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpongeza mmoja wa Watendaji Kata kwa kukabidhiwa Piki Piki na Mbunge wao wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla,jioni ya leo katika ukumbi wa Checki Point,mjini humo mkoani Tabora.
  Katibu Mkuu wa cha cha Mapinduzi (CCM ) Ndugu Abdulrahaman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa jimbo la Nzega vijijini mapema jioni ya leo katika ukumbi wa mikutano wa Check Point,wilayani humo mkoani Tabora.Ndugu kinana amewapongeza Wana CCM wa jimbo la Nzega kwa kushinda uchaguzi wa marudio wa madiwani,viongozi mbalimbali walioshinda nafasi mbalimbali za uongozi kwa ngazi ya Wilaya na kuwataka kuwa wamoja sambamaba na kushirikana katika kuhakikisha wanawaletea maendeleo wananchi na sii kulumbana tena.
  Picha na Michuzi Jr-Nzega.
  Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla akizungumza mbele ya Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo hilo waliojitokeza kwa wingi,katika Mkutano wao Mkuu wa jimbo ambao mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana .Dkt Kigwangalla amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi na Watendaji wa kata 19 ndani ya jimbo hilo. Mkuu wa Wilaya ya Nzega,Mh.Godfrey Ngapula kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Tabora,akitoa salamu mbele ya Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo la Nzega Vijijini kabla ya Mkutano Mkuu wa jimbo hilo kuanza.
  Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo la Nzega Vijijini wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwasalimia kabla ya kuanza rasmi mkutano mkuu wa jimbo hilo,ambapo Mbunge wa jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi wa Kata na Watendaji ili kuwasaidia kupambana na chanagamoto za usafri wakati wakiendelea kusikiliza na kutatua matatizo ya Wananchi wa jimbo hilo.
  Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo la Nzega Vijijini wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia mapema leo katika ukumbi wa Checki Point,mjini humo wakati wa mkutano mkuu wa jimbo hilo,ambapo Mbunge wa jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi wa Kata na Watendaji ili kuwasaidia kupambana na chanagamoto za usafri wakati wakiendelea kusikiliza na kutatua matatizo ya Wananchi wa jimbo hilo.

  0 0

  Mgeni rasmi  Katibu Tawala Wilaya  ya Urambo  Bw.Paschal  Byemelwa  akikata  utepe  ikiwa  ni  Uzinduzi wa Duka la Kisasa la Kampuni ya Simu za kiganjani ya Tigo wilayani Urambo katika kutekeleza adhma ya kusogeza karibu huduma za mawasiliano kwa wananchi wilayani humo,Kutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Urambo Bi.Margareth Nakainga,wapili kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Bw.Gwamaka Mwakilembe,na wa kwanza kushoto ni Meneja wa Tigo mkoa wa Tabora  Bw.Bright Kisanga.

  Duka la kisasa la Huduma kwa Wateja wa Tigo Wilayani Urambo

  Mgeni Rasmi  Paschal  Byemelwa,kulia ni Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Urambo Bi.Margareth Nakainga,wapili kutoka  kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Bw.Gwamaka Mwakilembe,na wa kwanza kushoto ni Meneja wa Tigo mkoa wa Tabora  Bw.Bright Kisanga wakipiga makofi kushangilia tukio la kutaka utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Duka hilo la Kisasa wilayani Urambo.

  Picha ya pamoja baada ya Uzinduzi wa Duka hilo
  Mmoja kati ya maafisa wa Tigo  Bi.Tunu Kazinja  akitoa maelezo kwa huduma ambazo wanazitoa mara baada ya uzinduzi wa Duka hilo la Kisasa wilayani Urambo.

  Mgeni Rasmi  Katibu Tawala wilaya ya Urambo Paschal Byemelwa pamoja na wageni wengine waalikwa katika hafla fupi ya uzinduzi wa Duka hilo la kisasa,walipata fursa ya kuangalia bidhaa mbalimbali za Tigo ambazo zilikuwa zikioneshwa nje ya Duka hilo la Kisasa.
  Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Urambo wakipata maelezo ya huduma zinazotolewa na Kampuni ya Tigo katika moja ya Banda la maonesho wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi wa duka la Kisasa wilayani Urambo.

  Katibu Tawala wilaya ya Urambo Bw.Paschal Byemelwa akihutubia wakati wa Uzinduzi wa duka la Tigo  wilayani Urambo ambapo ameishukuru kampuni ya Tigo kwa kufungua Duka hilo la Kisasa ambalo amesema litasaidia kuwapunguzia adha kubwa wananchi wa Urambo ambao walikuwa wanalazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma. 
  Baadhi ya wananchi wa Urambo wakimsikiliza katibu tawala wilaya ya Urambo Bw.Paschal Byemelwa wakati akiwahutubia katika hafla fupi ya uzinduzi wa duka hilo la kisasa.
  Meneja wa kanda ya ziwa wa Tigo Bw.Gwamaka Mwakilembe akizungumza na wananchi wa Urambo wakati wa uzinduzi wa Duka la kisasa wilayani humo ambapo alieleza kuwa kampuni ya Tigo  ambayo inaongoza kwa mageuzi ya kidigital nchini imeamua kuzindua duka hilo ikiwa ni muendelezo wa juhudi zake kuboresha huduma kwa wateja wake.


  Urambo, 12 Desemba, 2017- Katika mwendelezo wa harakati za kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanapata huduma bora kwa urahisi, kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tigo Tanzania leo imezindua duka kubwa la kisasa wilayani Urambo katika Mkoa wa Tabora.


  Duka hilo jipya linapatikana katika mtaa wa Nsanjo, mkabala na depot ya Pepsi katika mji wa Urambo, lina uwezo wa kuwahudumia wateja zaidi ya 580,000 wa Tigo wanaopatikana wilayani hapo na viunga vyake.


  Akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua duka hilo jipya la Tigo, Meneja wa Eneo la Ziwa wa Tigo, Gwamaka Mwakilembe alisema kuwa ufunguzi wa duka hilo jipya unaendana na mpango wa upanuzi na ukuaji wa kampuni hiyo ya simu unaolenga kuongeza idadi ya vituo vya huduma kwa wateja huku ikihakikisha kuwa bidhaa na huduma zote zinapatikana kwa urahisi na wateja wake nchi nzima.


  ‘Tigo imejizatiti kufanya uwekezaji utakaohakikisha wateja wetu wanapata huduma kwa viwango vya kimataifa ili waweze kupata suluhisho muafaka kwa mahitaji yao. Ufunguzi wa duka hili la kisasa mjini Urambo kunafanya idadi ya maduka yetu ya Tigo kufikia 15 katika Ukanda huu wa Ziwa, huku jumla ya maduka yetu yote ya Tigo nchini ikifikia 75,’ alisema.


  ‘Uzinduzi huu unaendana na sifa kuu ya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa zaidi wateja wake na kuwapa bidhaa na huduma bora, za kibunifu, zinazoendana na mahitaji yao. Tunaendelea kuwekeza katika upanuzi na uboreshaji wa mtandao wetu wa simu, ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa sehemu ya mabadiliko na faida za ulimwengu wa kidigitali unaoongozwa na Tigo,’ Mwakilembe alifafanua.

  Kwa upande wao, wakaazi wa Urambo wameelezea kufurahishwa kwao na ujio wa duka hilo jipya la Tigo kwani litawapunguzia adha ya kusafiri kwa mwendo mrefu kupata ufumbuzi wa matatizo yao ya simu pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za simu katika wilaya hiyo.  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisaidiwa na viongozi wengine kufunua kitambaa kuashiria kufunguliwa kwa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisaidiwa na viongozi wengine kukata utepe kuashiria kufunguliwa kwa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyuma la Taifa (NHC) Mama Blandina Nyoni, Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu wakikagua moja ya nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na NHC eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017
  Muonekano wa baadhi za nyumba nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na NHC na kufunguliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa dini na wananchi wakati wa sherehe za ufunguzi wa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza mshereheshaji Ephraim Kibonde wakati wa ufunguzi wa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa NHC wakati wa sherehe za ufunguzi wa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongozana na Spika Job Ndugai, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi,Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu wakati wa sherehe ya ufunguzi wa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017. PICHA NA IKULU

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akifungua rasmi Tawi la Benki ya CRDB lililopo katika jengo la LAPF mjini wa Dodoma leo. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu mstaafu Mzee John Samwel Malecela (kulia kwa Rais), Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (kushoto kwa Rais), Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei pamoja na viongozi wengine wa kitaifa na wa mkoa wa Dodoma.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua rasmi Tawi la Benki ya CRDB lililopo katikati ya mjini wa Dodoma. Wengine katika picha ni Mke wake Mama Janeth Magufuli watatu kutoka (kushoto), Waziri Mkuu mstaafu Mzee John Samwel Malecela wanne kutoka kushoto pamoja na viongozi wengine wa kitaifa na wa mkoa wa Dodoma.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilanga, katika kambi ya wavuvi Mererani, Wilayani Sumbawanga (hawapo kwenye picha) mara baada ya kufanya ziara katika kambi hiyo ili kujionea mazingira ya kambbi hiyo na hali ya kipindupindu.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilanga, katika kambi ya wavuvi Mererani, Wilayani Sumbawanga , mara baada ya kufanya ziara katika kambi hiyo ili kujionea mazingira ya kambbi hiyo na hali ya kipindupindu.

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesimamisha shughuli za uvuvi katika ziwa Rukwa hadi hapo wataalamu wa afya watakapojiridhisha kuwa hakuna ugonjwa wa kipindupindu katika kambi za uvuvi zinazozunguka ziwa hilo na Mkoa kwa jumla.

  Amesema kuwa athari inayopatikana katika kambi hizo za uvuvi zitawaathiri wala samaki unaotokana na uvuvi wa ziwa hilowaliopo na kuongeza kuwa wale wote wanaovua samaki waliopiga kambi katikakati ya ziwa waache kuvua mara moja na wasiruhusiwe kuingia katika ili kuweza kuudhibiti ugonjwa huo.

  “Kuanzia leo tunapiga marufuku shughuli zote za uvuvi, mpaka tutakapojiridhisha kwamba tuna mazingira safi na salama, na kwamba maisha yetu hayapo hatarini tena na hao mnaosema wanakuja hawatapata maeneo ya kuuzia samaki wao tena watatafuta pa kwenda na tutaweka kambi ya kudhibiti wagonjwa wanaotoka huko wataishia hapa hawatakwenda popote,” Alisisitiza.

  Ameyasema hayo alipofanya ziara katika kambi ya mererani iliyopo katika kijiji cha Ilanga, Kata ya Muze Wilaya ya Sumbawanga katika bonde la Ziwa Rukwa ambapo mpaka anafiak hapo palikuwa na wagonjwa 9 wa kipindupindu.

  Awali akitoa taarifa ya ugonjwa huo Afisa afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Plasidus Malapwa ameeleza kuwa ugonjwa huo ulibainika tarehe 23/11/2017 kutokana na mgonjwa aliyetoka kambi ya Lichili, Kijiji cha Lichili, Wilaya ya Momba, Mkoani Songwe na kufia katika kambi ya kamchanga, Kata ya Muze, wilayani Sumbawanga na wagonjwa kuanza kuongezeka hali iliyosababisha kuanzisha kambi nne kuzunguka ziwa Rukwa.

  “hali ya Wagonjwa toka tarehe 1/12/2017 hadi hivi sasa katika kambi nne ni kama ifuatavyo; Muze wagonjwa 4 wameongezeka leo wawili wapo 6 hakuna kifo, Kipa wagonjwa 8, vifo 2, kamchanga wagonjwa 26, vifo 3, matete wagonjwa 6, hakuna kifo hivyo jumla ya wagonjwa wote tangua kuanza kwa mwezi wa 12 ni waginjwa 46 na vifo 5,” Aliorodhesha.

  Nae Mganga mfawidhi wa Zahanati ya Muze aliongeza kuwa, kuna hatua mbalimbali zilizochukuliwa ili kudhibiti ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kufungia migahawa michafu 8 hadi watakapotekeleza maelekezo ya wataalamu wa afya, pombe mapipa 4 na debe 3 ilimwagwa na wanywaji pombe 14 walilipishwa faini ya shilingi 20,000/= kila mmoja.

  Tangu ugonjwa huo uanze tarehe 20/11/2017 hadi 13/12/2017 kuna wameripotiwa wagonjwa 52 na vifo 6.

  0 0

  Na Robert Hokororo, Kishapu DC

  Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imeendelea kutekeleza miradi yake ya maendeleo katika sekta ya elimu ya msingi kutokana na fedha zilizotolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

  Itakumbukwa hivi karibuni ilitoa fedha kwa Halmashauri hiyo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ambapo pamoja na nguvu za wananchi imepiga hatua katika utekelezaji.

  Baada ya kupokea kiasi cha sh. milioni 25 ujenzi wa nyumba ya walimu wawili pamoja na matundu 18 ya vyoo katika shule ya msingi Idisanhambo ulianza mara moja na tayari umefikia hatua ya umaliziaji.Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga wakati akielezea miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Alisema pamoja na kupokea fedha kutoka TEA, katika mwaka wa fedha 2017/2018, Halmashauri ya Kishapu imetenga jumla ya sh. milioni 90 kupitia mapato yake ya ndani kujenga nyumba sita za walimu.Magoiga alibainisha kuwa Halmashauri hiyo pia iliweza kupokea Ruzuku ya Maendeleo (LGDG) sh. milioni 88 zitakazotumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 11 za walimu.

  Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Halmashauri imetenga jumla ya sh. milioni 48 kupitia mapato yake ya ndani kujenga matundu 24 ya vyoo kwa shule zake za msingi.Pia, Ruzuku ya Maendeleo (LGDG) sh. milioni 75 zitakazotumika katika ujenzi wa matundu 50 ya vyoo pia katika shule za msingi wilayani humo.

  Fedha hizo kwa ujumla zinatarajiwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili katika sekta ya elimu ya msingi hususan upungufu wa nyumba za walimu na matundu ya vyoo.Aidha, pamoja na Halmashauri ikishirikiana na wadau kutekeleza miradi mbalimbali bado inaendelea kuhamasisha jamii kuchangia shughuli za maendeleo.

  Pia kutokana na uelewa mdogo wa baadhi ya wazazi kuhusu masuala ya elimu, imeendelea kuelimisha jamii kuhusiana na suala hilo ili iendelee kupiga hatua wilayani humo.
  Viongozi kutoka Idara ya Elimu ya Msingi wakiangalia maendeleo ya mradi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Idisanhambo ambao umefikia katika hatua za umaliziaji.
  Afisa Elimu Ufundi katika Halmashauri ya Kishapu, Moshi Balele (kushoto) akitoa maelezo kwa viongozi wengine katika idara hiyo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa choo katika shule ya msingi Idisanhambo.
  Mojawapo ya vyoo katika shule hiyo ya msingi kikiwa katika hatua ya umaliziaji kabla ya kukabidhiwa na kuanza kutumika rasmi na wanafunzi.
  Viongozi kutoka Idara ya Elimu ya Msingi wakiendelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa nyumba ya walimu shule ya msingi Idisanhambo.
  Mafundi wakiendelea kuwajibika na ujenzi wa mojawapo ya vyoo vya wanafunzi katika shule hiyo ambavyo viko katika hatua za mwisho.
  Choo cha shule hiyo ya msingi kikiwa katika hatua za umaliziaji wake kabla ya kukabidhiwa na kuanza kutumika.
   

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (kulia), alipokagua miundombinu ya Reli ya Kaskazini ambayo inakarabatiwa na Shirika hilo kutoka Tanga hadi Arusha, katika Kata ya Mombo, wilayani Korogwe, mkoani Tanga.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa wananchi wa Kata ya Mombo, wilayani Korogwe, mkoani Tanga mara baada ya kukagua ukarabati na ufufuaji wa miundombinu ya Reli ya Kaskazini ambayo inatoka Tanga-Korogwe-Arusha.
  Sehemu ya wananchi wa Kata ya Mombo, wilayani Korogwe, mkoani Tanga wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), alipoongea nao baada ya kukagua ukarabati na ufufuaji wa miundombinu ya Reli ya Kaskazini inayotoka Tanga-Korogwe-Arusha.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa, akizungumza na wananchi wa Kata ya Mombo, wilayani Korogwe, mkoani Tanga mara baada ya ukaguzi wa ukarabati wa njia ya reli ya Tanga-Korogwe-Arusha ambapo sehemu ya Tanga-Mombo KM 83 ukarabati wake umekamilika.
  Muonekano wa Reli ya Kaskazini kutoka Tanga hadi Mombo ambayo inakarabatiwa na Kampuni Hodhi ya Rasimali za Reli (RAHCO). Jumla ya KM 438 za reli ya kutokea Tanga kupitia Korogwe hadi Arusha zinatarajiwa kukarabatiwa na kukamilika mwezi Aprili mwakani.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), leo katika Stesheni ya Mombo, mkoani Tanga, baada ya kukagua ukarabati na ufufuaji wa miundombinu ya Reli ya Kaskazini ambayo inatoka Tanga-Korogwe hadi Arusha.


  Serikali imesema imeanza kufufua reli ya Kaskazini ya kutoka Tanga hadi Arusha ambayo ilikufa miaka 14 iliyopita ili kuwezesha wafanyabiashara na wananchi kusafirisha mizigo yao kwa kutumia reli hiyo badala ya barabara hali itakayopelekea kupunguza uharibifu wa miundombinu ya barabara nchini.

  Amesema hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wakati alipokagua ukarabati wa reli hiyo kuanzia eneo la Korogwe hadi Mombo ambalo limekamilika kwa KM 83 na kuwahikikishia watanzania kuwa uendelezaji wa reli hiyo hadi Arusha itakamilika mapema mwezi Aprili mwakani na hivyo kuruhusu huduma za usafirishaji ziendelee hasa za mazao na bidhaa.

  “Niwahakikishie wananchi kuwa hii kazi tuliyoianza haiwezi kusimama kwani Serikali imejipanga na itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri za usafirishaji”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Waziri Prof. Mbarawa, amemtaka Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za reli (RAHCO), Masanja Kadogosa, kuongeza ajira kwa vijana wa maeneo hayo na kuwataka kuwa na uzalendo katika ukarabati wa reli hiyo ili kurahisisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

  Aidha Prof. Mbarawa amezungumzia umuhimu wa kuongeza vichwa vya treni kwa Shirika hilo ambapo Serikali imeamua kununua vichwa 11 vya treni vilivyotelekezwa eneo la Bandari ya Dar es Salaam kwa kiasi cha shilingi dola milion 2.4 kutoka dola milion 3.2.

  “Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa kila fedha inayopatikana itasimamiwa na kuwekeza katika miundombinu ya nchi na zaidi tumeokoa dola laki nane sawa na bilioni 1.7 kwa kila kichwa”, amesisitiza Waziri Mbarawa.

  Kuhusu suala la bomoabomoa katika maeneo ya hifadhi ya reli Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa ataendelea kusimamia Sheria kama inavyosema.

  Prof. Mbarawa ameutaka uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), kutafuta mizigo katika viwanda vyote nchini ili kuongeza huduma za usafirishaji wa mizigo kwani ukarabati wa njia hizi za reli unahitaji fedha nyingi, hivyo upatikanaji wa mizigo hiyo utasaidia kuzalisha faida ambayo itapelekea kuongeza mapato ya Shirika hilo.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Bw. Masanja Kadogosa, amesema kuwa ukarabati wa reli hii utakuwa na mchango mkubwa kiuchumi na kijamii kwani utasaidia kwa wananchi na wafanyabiashara kusafirisha mizigo yao kwa njia rahisi.

  Ukarabati wa reli hiyo yenye urefu wa kilometa 438 ni mkakati wa Serikali katika kufufua huduma za usafiri wa treni hapa nchini na kufungua fursa za kiuchumi na kibiashara kwa wananchi.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

   
   Kampuni ya kutengeneza filamu ya Bongohoodz siku ya Jumamosi ya Desemba 16, 2017 inatarajia kuzindua filamu ya TATU CHAFU, uzinduzi ambao utafanyika kwenye ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Jijini Dar es Salaam.Filamu hiyo inayozungumzia uhuni na vita baina ya magenge sugu manne ya wapiga dili wa mjini. 

  Baadhi ya wasanii ambao wameshiriki kwenye filamu ya TATU CHAFU ni Meya Shabani (Komani), Faraji Mhando (Uswege), James James (Bono), Salum Khalid (Shomari), Hussein Msangi (Mbita), Noriega Francis (Rochi), Laban Mbibo (Frank), Paul Katambo (Machete) na wengine wengi.Uzinduzi wa filamu hiyo unatarajiwa saa 4:00 asubuhi mpaka 5:00 usiku, ambapo pamoja na uzinduzi wa filamu pia wasanii mbalimbali wakiwepo Mapacha, Wakazi na Dabo wanatarajiwa kutoa burudani kwa watu watakaohudhuria uzinduzi huo.

  0 0

  Kama ambavyo mjadala unavyoendelea miongoni mwa wataalamu, wafanyabiashara, wataalamu wa masoko, vyombo vya habari na umma kwa ujumla kuhusu uhalali wa biashara ya mauzo ya moja kwa moja au mtindo wa masoko ya moja kwa moja kama biashara halali, yenye maadili. QNET TANZANIA, kampuni ya masoko ya moja kwa moja ambayo hivi karibuni imefungua wakala wake jijini Dar es salaam, wamejitumbukiza katika mada wakiweka wazi hoja kuhusu mtindo huu wa biashara na kuondoa wasiwasi wowote uliopo kwamba biashara ya mauzo ya moja kwa moja haizingatii taratibu za kibiashara za kimataifa. Katika mahojiano maalumu na vyombo vya habari, Mwakilishi wa QNET Tanzania hapa nchini, BENJAMIN MARIKI anajibu baadhi ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu mtindo wa biashara za mauzo ya moja kwa moja.

  Nukuu kwa Ufupi:
  Swali: Biashara ya moja kwa moja ni nini/ mtindo wa biashara ya masoko -mtandao ni nini?
  Jibu: Biashara ya mauzo ya moja kwa moja inahusu mauzo ya bidhaa au huduma kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine mbali na maeneo ya maduka ya reja reja yalipo. Mfumo huu wa biashara ya mauzo ina zaidi ya umri wa miaka 100 ulimwenguni na mwanzoni kabisa ilianzaia katoka nchi ya Marekani. Leo, ni sekta ya biashara yenye thamani ya dola za kimarekani  bilioni 180 ulimwenguni kote ikiwa inajumuisha takribani watu milioni 180.
  Jinsi gani watu wanaojihusisha na masoko ya mtandao wanavyojipatia kipato? 

  Watu wanaojihusisha na biashara za moja kwa moja au biashara za masoko-mtandao wanajipatia gawio kutokana na mauzo ya bidhaa au huduma ambayo hukokotolewa kwa mtindo wa fidia kutoka katika kampuni ambayo wanaiwakilisha. Mtindo wa biasbara ya moja kwa moja unatoa fursa kwa mtu binafsi kujipatia kipato kupitia kujiajiri mwenyewe na kufanya kazi kwa bidii. Masoko ya mtandao ni moja kati ya mifumo maarufu ya mauzo ya moja kwa moja.

  Kuna tofauti gani kati ya Biashara ya Masoko-mtandao na ‘Mpango wa Upatu’ (Pyramid Scheme)?

  Biashara ya Masoko-Mtandao sio mpango wa kujitajirisha haraka. Inaweza kuwa ni yenye faida kubwa, lakini pia ni biashara ngumu. Tangu mwanzoni, biashara halali itakuambia kwamba matokeo yatakuja pale tu utakapoweka juhudi na muda. Kampuni yoyote ambayo inakuahidi kuwa utapata utajiri kwa urahisi lazima itazamwe kwa tahadhari. Kwa mafano, QNET jna maelezo ya tahadhari kizuizi kuhusu kipato katika mtandao wake na nyaraka zake za masoko.

  Kampuni za masoko ya mtandao yanatoa bidhaa zenye ubora au huduma tofauti na mpango wa upatu ambao huwa hauna bidhaa halali au huduma. Makampuni bora ya biashara za masoko ya mtandao hutumia kiasi kikubwa cha fedha kufanya utafiti na kutengeneza bidhaa bora ambazo zinatumiwa na watu wakati upatu hauna utaratibu huo.
  QNET, Kwa mfano, inatoa zaidi ya bidhaa 300 tofauti katika makundi 9 ya bidhaa tofauti tofauti.
  Zaidi ya hapo, biashara ya masoko ya mtandao huwa yana ukomo katika mpango wa ukomo wao ambayo huwa inadhibiti idadi ya watu ambao wanaweza kujipatia gawio kupitia mauzo. Hii inakusudia kusawazisha uwiano miongoni mwa washiriki. Katika mfumo wa ‘piramidi’ watu walioko mstari wa juu au wale ambao ‘wako juu’ hupata fedha nyingi wakati wale walioko mstari wa chini au wale ‘walioko chini’ mara nyingi huwa wanaachwa nyuma kutokana na kujiunga kwa kuchelewa.
  Katika kampuni ya QNET, kila mtu anaweza kufanikiwa bila kujali alianza lini na mafanikio ya mwakilishi wa kujitegemea (IR) ambaye anasambaza bidhaa hutegemea na mafanikio ya watu walioko katika timu yake.
  Kwa kuongezea, Makampuni halali ya biashara za masoko ya mtandao huwa ya na mfumo imara wa mafunzo ambao huwa unaweka msisitizo katika mafunzo kwa wauzaji katika mtandao wao. Makampuni ambayo yanajali wasambazaji wao kwa dhati na wanataka wafanikiwe ndio ambao wanatoa zana za kibiashara na mafunzo kuwasaidia kukuza biashara zao. Makampuni kama vile QNET yana wakufunzi wenye sifa wenye utaalamu na uzoefu kwaajili ya kuwasaidia wanachama wao waweze kuelewa vyema biashara na bidhaa na kufanya kazi kama washauri na wahamasishaji kwaajili ya kukuza biashara.
  Kwa kumalizia, makampuni ya biashara ya masoko ya mtandao yana sera na taratibu nzuri pamoja na kanuni za maadili. Kampuni yoyote halali ya biashara ya mtandao huwa ina lengo la kufikia ukuaji endelevu kwa kudumisha utamadunj wa mauzo yenye maadili. QNET inaweka msisistizo mkubwa sana katika kanuni za maadili ya utendaji kwa wawakilishi wake na kuwapatia miongozo ya kina kuhusu ufanyaji wa biashara ya masoko ya mtandao kitaalamu  pamoja na sera na taratjbu zake.
  Masoko ya mtandao yanajivunia kukuza na kuendeleza wajasiriamali; jinsi gani inawawezesha wajasiriamali wa ndani katika kuendeleza biashara zao?
  QNET Inatoa msisitizo mkubwa sana katika mafunzo na elimu kwa wawakilishi binafsi (IRs). Hatuweki mkazo katika kuendeleza uwezo wao wa kitaalamu tu bali pia tunatilia mkazo katika ukuaji binafsi na maendeleo. Tunaamini kwamba mafanikio ya kifedha peke yake hayatoshelezi. Tunanaamini kwamba tunahitaji kuwaendeleza watu kuwa wanadamu bora ili waweze kutumia mafanikio yao kuchangia maendeleo ya jamii zao.
  QNET inashirikiana na makampuni bora ya mafunzo na biashara za masoko ya mtandao ambayo yamefanikiwa katika kutoa mafunzo kwa wakufunzi ambayo wanahamasisha wakufunzi kutoa elimu hii kwa watu wengine zaidi katika timu zao kwa lugha zao wenyewe. Wakati mafunzo ya biashara unazingatia mpango wa ulipaji wa fidia, kutokana na uuzaji wa bidhaa na cha muhimu zaidi, umuhimu wa maadili na ufanyaji wa mauzo kwa kitaalamu, ni programu ya mafunzo ambayo sio ya kibiashara ambayo ndio maarufu zaidi na yenye athari zaidi.

  Mada zinazofundishwa katika mafunzo ya maendeleo binafsi yanajumuisha kupokea mabadiliko, kukabikiana na changamoto na kukataliwa, kujenga na kuendeleza mahusiano, mawasiliano yenye tija na pia muonekano binafsi.

  Programu za mafunzo zinatofautiana kutoka katika kundi dogo la washiriki 20-30 mpaka washiriki 1000 kwa mafunzo ya kanda. Mafunzo ya ulimwengu huenda kwa maelfu ya washiriki na hufanyika kwa siku kadhaa.

  Mifano michache ya programu za mafunzo na uzoefu ambayo IR anaweza kunufaika nazo ni:

  Mfululizo wa semina za kutengeneza mtandao (NSS) – NSS inatoa mafunzo ya kujenga mtandao na kuhamasisha ambayo husaidia kuboresha mikakati na mbinu na kusaidia katika maendeleo binafsi na ya kitaalamu ya IR. Tukio hili huwa linaandaliwa mahsusi kwaajili ya kutatua mahitaji maahususi ya mtandao katika nchi au jiji fulani.

  Semina ya Mambo ya Biashara ya Mtandao (NBS) Haya ni mafunzo ambayo huhudhuriwa na washiriki wachache kuliko NSS lakini huwa yana moduli zile zile, mwelekeo na malengo yale yale.  

  Mafunzo ya Bidhaa – Huwa ni programu ya mafunzo ya kina ambayo hufundisha IR kuhusu mambo yote ya msingi kuhusu bidhaa zinazouzwa chini ya bango la QNET. Mafunzo yanaweza kufanyika katika makundi madogo madogo au kama mafunzo ya siku nzima ikihudhuriwa na watu wengi.

  Mafunzo katika Mtandao – QNET hendesha mfululizo wa mafunzo katika mtandao (online) ambayo IRs anaweza kuhudhuria wakiwa nyumbani kwao kwa kuingia kupitia katika computer zao. Kuna kuwa na vipindi vya mazungumzo kuhusiana na mada mahususi  kama vile bidhaa mpya inayozinduliwa, sera na taratibu na mpango wa kufidiwa hufanyika katika lugha mbali mbali na viongozi wa mafunzo wa QNET.

  Kongamano – QNET huandaa kongamano la mwakala kimataifa kila mwaka huko Asia na Mashariki ya Kati kwa kipindi cha siku tano. Katika kongamano hilo takribani IR 8,000-10,000kutoka katoka zaidi ya nchi 40 hukutana pamoja kusikiliza  na kujifunza kutoka kwa wataalamu wa mafunzo na IR wengine waliofanikiwa kutoka duniani kote. Katika kongamano hili QNET pia huwa inaandaa maonyesho ya bidhaa ambayo huwaruhusu IR kushika na kufurahia bidhaa zetu, kuuliza maswali wataalamu na kuangalia mifano. Kongamano huwa pia linafanyika katika kiwango kidogo kulenga kanda fulani mahususi katika kipindi chote cha mwaka.

  Zaidi ya Tanzania, ni wapi ambako QNET ina ofisi zake ndani ya Afrika?

  Tumetengeneza msingi mzuri wa kibiashara katika nchi za Ivory Coast, Burkina Faso, Cameroon, Mali, Guinea and Senegali.
  Ni aina gani ya bidhaa na huduma ambazo mnazo wakati wote?
  Kupitia usimamizi imara wa ubora na kufanya kazi na watafiti wa kiwango cha juu, wanasayansi na wazalishaji katika kila idara, QNET inatoa aina mbalimbali za bidhaa za mitindo ya kimaisha na afya ambazo zimethibitisha ufanisi wake kwa watu duniani kote. Kutoka katika huduma binafsi, lishe, vipodozi, bidhaa za utunzaji wa nyumba na mwili, nguvu za maji, mpaka katika mapambo ya vito na saa za mkononi, na vifurushi vya sikukuu.

  Ni kiasi gani cha mtaji ambacho mjasiriamali anayeanza anahitaji kuwa nacho kuweza kuanzisha biashara hii?
  Mjasiriamali anahitaji Dola 30 (TZS 66,000) kujiandikisha kwaajili ya kuanza biashara hii.

  Biashara za masoko yamtandao kwa ujumla inachukuliwa vibaya na baadhi ya watu katika jamii, lini kwa mtazamo wa QNET, biashara hii inaweza kuanza kuchukuliwa kwa mwonekano mzuri (chanya)?
  Kwa utandawazi na kuondolewa kwa vizuizi vya biashara, ni suala la muda tu kabla ya sekta hii kuanza kupewa mtazamo mzuri zaidi.


  0 0

   Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida akizungumza na waandishi kuhusu mfuko huo kupata tuzo ya uandaaji bora wa hesabu katika sekta ya hifadhi ya Jamii na Bima ya Afya kwa mwaka 2015/2016 ambapo Mfuko huo umeshika nafasi ya kwanza,  Tuzo hiyo imetolewa na  Bodi ya Taifa ya Uhasibu (NBAA) hivi karibuni.Kulia ni Meneja Masoko na Uhusiano wa LAPF Bw. James  Mlowe.
   Meneja Masoko na Uhusiano wa LAPF Bw. James Mlowe akieleza mikakati  iliyouwezesha mfuko huo kupata tuzo hiyo ikiwemo uwajibikaji na utawala bora katika kusimamia rasilimali fedha katika mfuko huo. Kushoto ni   Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. John Kida.
   Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF  Bw. John Kida  (Katikati) akionesha kwa waandishi wa habari  ( hawapo pichani)  tuzo ya uandaaji bora wa hesabu katika sekta ya hifadhi ya Jamii na Bima ya Afya kwa mwaka 2015/2016 ambapo Mfuko huo umeshika nafasi ya kwanza, Tuzo hiyo imetolewa na  Bodi ya Taifa ya Uhasibu (NBAA) hivi karibuni.
   Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa  LAPF  Bw. James  Mlowe akifurahia tuzo ya uandaaji bora wa hesabu katika sekta ya hifadhi ya Jamii na Bima ya Afya kwa mwaka 2015/2016 ambapo Mfuko huo umeshika nafasi ya kwanza,  Tuzo hiyo inatolewa na  Bodi ya Taifa ya Uhasibu (NBAA) hivi karibuni.
  Meneja Matekelezo wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF  Bw. Victor Kikoti (Wakwanza) akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu mafao yanayotolewa na mfuko huo na faida wanazopata wananchi kutokana na mafao hayo .(Picha zote na LAPF).  Mfuko wa Pensheni wa LAPF umepata tuzo ya uandaaji bora wa hesabu katika sekta ya Hifadhi ya Jamii na Bima kwa mwaka 2015/16 inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu (NBAA).

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Mjini Dodoma kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bw. Eliud Sanga, Mkurugenzi wa fedha wa Mfuko huo Bw. John Kida amesema kuwa mfuko huo umepata tuzo hiyo kwa miaka saba mfululizo ikiwa ni ishara ya utendaji mzuri na wenye kuchochea ukuaji wa Mfuko na maendeleo ya Taifa kwa ujumla kutokana na uwekezaji unaofanywa katika sekta mbalimbali.

  “Kwa mwaka 2015/2016 mapato yanayotokana na uwekezaji katika vitega uchumi yalifikia shilingi bilioni 96.03 ikilinganishwa na shilingi bilioni 72.72 kwa mwaka 2014/2015 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 32.” Alisisitiza Kida

  Akifafanua Kida amesema kuwa mafanikio ya mfuko huo yanatokana na kuongezeka kwa wanachama ambao hadi Septemba 2017 walikuwa wamefikia 180,401.

  Aliongeza kuwa Mfuko huo katika kipindi cha mwaka 2015/2016 umelipa mafao kwa wanachama 8,011 ambapo jumla ya shilingi bilioni 107.24 zililipwa kama mafao kwa wanachama.

  Akieleza mafanikio mengine Kida amesema kuwa michango ya wanachama imeongezeka ambapo kwa mwaka 2015/2016 imefikia shilingi bilioni 279.68 ikilinganishwa na shilingi bilioni 210.07 sawa na ongezeko la asilimia 33 hali iliyosababishwa na kuoongezeka kwa wanachama kutoka 150,835 hadi kufikia wanachama 166,260 mwezi June 2016.
  Kwa upande wake Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko huo Bw. James Mlowe amesema mafanikio ya mfuko huo yanatokana na utendaji makini unaozingatia utawala Bora katika kusimamia rasilimali za Mfuko huo ikiwemo fedha. Mfuko wa Pensheni wa LAPF umewekeza katika vitega uchumi mbalimbali ambapo hadi kufikia June 2016 ulikuwa umewekeza jumla ya shilingi trilioni 1.09, wakati kwa kipindi cha mwezi June 2015 mfuko huo uliwekeza bilioni 884.26 katika vitega uchumi mbalimbali kama dhamana za Serikali, Amana za mabenki, majengo, hisa za makampuni na uwekezaji katika Kampuni tanzu.

  0 0

  Barclays Bank Tanzania Limited invests in Education 24 University students from the University of Dar es Salaam receive full scholarships to study.

  Speaking during the announcement, which took place at the Barclays Head office, Barclays Managing Director, Abdi Mohamed said “As a business, we focus much of our efforts on education and skills. As an employer, we are well aware that Tanzania needs a thriving private sector that is investing in productive capacity. youth unemployment is a significant national challenge, we aim to play a role in providing young people with the tools and readiness needed to find meaningful employment and business opportunities. The availability of skills in any country is critical to drive economic growth and development”.

  Barclays Bank Tanzania’s shared growth strategy is committed to enhance socio-economic growth in Africa. As a continent we can only be successful if we connect positively and create value with the society in which we operate. Shared growth means having a positive impact on society while delivering shareholder value.

  He continued, “Our #BaloziMwanafunzi programme is one example aimed at upskilling young people education and skills. This scholarship programme is in partnership with the University of Dar es Salaam – Tanzania’s oldest and largest university. This year alone, 24 undergraduate students have been offered full scholarships,This initiative will help us build a real connection with the students, customers and clients, and other important stakeholders. It is our belief that the programme will have positive implications for our own talent pipeline”

  Abdi concluded, “As a leading bank in Tanzania, and as part of a leading financial services group in Africa, we will continue to use our substantial resources and expertise to develop solutions to the various challenges facing Tanzania, as well as build partnerships to create a more prosperous Tanzania for the next generation”. 
  Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (sixth from right, seated), posing for a souvenir picture together with 24 students awarded the Barclays full sponsorships at University of Dar es Salaam (UDSM), Barclays and UDSM officials during a media conference in Dar es Salaam yesterday. Fifth from right is UDSM Deputy Vichancellor, Academic, Prof. Bonaventure Rutinwa.
   

older | 1 | .... | 1459 | 1460 | (Page 1461) | 1462 | 1463 | .... | 1897 | newer