Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1457 | 1458 | (Page 1459) | 1460 | 1461 | .... | 1896 | newer

  0 0


  Vijana kutoka Zanzibar na Tanzania Bara wakiwa katika mkutano wa majadiliano ya kuangalia fursa zilizopo nchini ili kuzifanyia kazi kwa ajili ya kulitetea taifa maendeleo. Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki Makao Makuu ya Kampuni ya Trumark jijini Dar es Salaam.
  Majadiliano yakiendelea.
  Msisitizo katika majadiliano hayo.
  Fursa mbalimbali zikiandikwa katika makundi.
  Picha ya pamoja ya vijana hao.


  Na Dotto Mwaibale

  VIJANA wa Zanzibar na Tanzania Bara wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia fursa zilizopo nchini ili kuliletea taifa maendeleo.

  Katika mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki Makao Makuu ya Kampuni ya Trumark vijana hao wapatao 14 kwa niaba ya wenzao walijadiliana mambo mbalimbali na kuangalia fursa za maendeleo zilizopo nchini.

  Kwa ujumla fursa zilizokuwa zimeangaliwa katika maeneo mbalimbali na wazo hilo limekuja baada ya baadhi yao kutembea nchi nzima Tanzania Visiwani na Tanzania Bara na kuziona hivyo wakaona ni vema kuunganisha nguvu ya pamoja kwa kuwashirikisha wenzao na kuona waanzie wapi.

  "Tumetembea nchi nzima na kuona fursa mbalimbali tukaona ni vizuri vijana wa Zanzibar na Tanzania Bara tukutane tujadiliane na tuone ni fursa zipi tuzifanyie kazi kwa manufaa yetu kama vijana na taifa kwa ujumla" alisema mmoja wa vijana hao ambaye hakupenda kuingia kiundani zaidi kwa kuwa mchakato wa jambo hilo ndio kwanza upo jikoni.

  Alisema hivi sasa vijana wasitegemee kuajiriwa badala yake waziangalie fursa zilizopo nchini na hizo ndizo zitakazo waondoa katika mawazo ya kutegemea kuajiriwa.Alisema kuna fursa za kuanzisha viwanda vidogo vidogo, ufugaji, ufundi mbalimbali, kilimo na mambo mengine hivyo ni vema vijana wakaangalia huko zaidi.

  Alisema wamekutana katika mkutano huo kuangalia fursa hizo na wapi pa kuanzia na mchakato huo ukikamilika wataweka mambo hadharani na kukamilisha mambo yote lengo likiwa ni kuwaunganisha vijana wa nchi nzima.

  0 0  Na Hamza Temba, Arusha
  ..............................................................
  Wadau wa Utalii Jijini Arusha wamempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kwa kukubali kuyafanyia kazi mapendekezo yao ya kuwaingiza wajasiriamali wadogo katika utoaji wa huduma za kusafirisha watalii nchini.


  Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo wakati akichangia mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini humo.


  Chambulo alisema kwa muda mrefu sasa kanuni zinazotumika zinamtaka mfanyabiashara ya usafirishaji watalii awe na magari matatu kwa kiwango cha chini ikiwa ni pamoja na kulipia ada ya leseni ya Dola za Kimarekani 2,000 sawa na wafanyabiashara wengine matajiri jambo ambalo limekuwa likiwabagua wafanyabiashara wadogo.


  “Tunakupongeza sana Mhe. Waziri kwa kutupa angalao hilo moja, tuliomba mwenye kagari kamoja nae aruhusiwe na apewe leseni walau ya dola 200 ili afanye biashara kidogo kidogo mwishowe atanunua gari tano na kuendelea, tunataka sisi Watanzania wote tufaidike na rasilimali zetu,” alisema Chambulo.


  Awali akiwasilisha mapendekezo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara ya utalii, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deogratias Mdamu alisema kwa upande wa watanzania ambao ni wajasiriamali wadogo wenye gari moja hadi magari matatu watatakiwa kulipa ada ya leseni ya dola za Kimarekani 200.


  Kwa upande wa wafanyabiashara wenye magari kuanzia manne hadi kumi alisema imependekezwa walipe Dola za Kimarekani 2,000, wenye magari 11 hadi 50 Dola za Kimarekani 3,000, magari 51 hadi 100 Dola za Kimarekani 10,000 na magari 100 na kuendelea Dola za Kimarekani 15,000.


  Kwa upande wa wafanyabiashara ambao sio Watanzania wenye magari 10 hadi 30 imependekezwa walipe Dola za Kimarekani 10,000, magari 31 hadi 100 Dola za Kimarekani 15,000 na magari 101 na kuendelea Dola za Kimarekani 20,000.


  Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la kuwasilishwa kwa mapendekezo hayo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara ya utalii kwa wadau ni kuweka ushirikishwaji na makubaliano ya pamoja ya kutekeleza kanuni hizo.


  Alisema sehemu kubwa ya mapendekezo hayo imezingatia maombi na maoni ya wadau hao ambayo yaliwasilishwa kwake awali. “Kilio chenu nimekisikia mimi mwenye mamlaka ya kufanya mabadiliko, lengo kubwa la mapendekezo haya ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo wenye gari moja waweze kuingia kwenye biashara hii ya utalii pamoja na kuongeza mapato ya Serikali na jamii kwa ujumla,” alisema Dk. Kigwangalla.


  Katika hatua nyingine amewaagiza watalaamu ndani ya Wizara yake kuhakikisha wanakamilisha kanuni hizo mpya ndani ya mwa mwaka huu ili utekelezaji wake uanze mapema mwakani, 2018.


  Akizungumzia wafanyabiashara wanaofanya biashara ya kuwasafirisha watalii nyuma ya pazia bila kulipia leseni, alisema Wizara yake inaandaa mfumo maalumu wa kielektroniki utakaowezesha ukaguzi wa magari kwenye mageti ya kuingilia hifadhini ili kudhibiti vitendo hivyo.  Aidha, ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara hao na kuwataka kufanya biashara hiyo kwa weledi na kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa ikiwemo kulipa ada ya leseni husika kwa mujibu wa sheria. 

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deogratias Mdamu (kushoto).
  Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.

   Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
   Baadhi ya wadau wa Utalii walioshiriki mkutano huo.

  Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo akichangia mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika mkutano huo.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akitambulishwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki (kushoto) kwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Merywn Nunes muda mfupi baada ya kikao na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. 

  0 0

  Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Selemani Jafo amewapongeza viongozi na watendaji wa wilaya na Halmashauri ya wilaya ya Mvomero kwa usimamizi wa Miradi ya maendeleo. 

  Jafo aliyasema hayo alipokuwa ziarani wilayani huko ambapo alifanikiwa kutembelea ujenzi wa hospitali ya wilaya, shule ya kidato cha tano na sita ya kumbukumbu ya Sokoine, mradi wa ujenzi wa barabara ya lami, kituo cha mafunzo ya kilimo na mifugo, pamoja na mradi wa umwagiliaji. 

  Katika ziara hiyo,Jafo ameagiza kuanza kwa utoaji wa huduma ya matibabu kwa wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Mvomero ifikapo keshokutwa Desemba 13,mwaka huu wakati serikali ikitafuta fedha kwaajili ya ujenzi wa jengo la upasuaji, maabara, wodi ya watoto na majengo mengine ambayo yatagharibu zaidi ya sh.milioni 700 ambapo matarajio ni kupata fedha hizo na kukamilisha majengo hayo kabla mwezi Machi 2018. 

  Pia Jafo ameagiza kuongezeka kwa kasi ya kukamilisha madarasa, bwalo la chakula na mabweni katika shule ya sekondari ya Sokoine Memorial kabla mwezi April 2018 ili shule hiyo iweze kupokea wanafunzi wa kidato cha tano hapo mwakani kwani serikali imepeleka fedha zote za ujenzi zaidi ya sh.billioni 1.6.

  Aidha Jafo amewataka viongozi na watendaji kuendelea kushikamana ili kuwaletea wananchi maendeleo.
   .Jengo la utawala na wagonjwa wa nje ya Hospitali ya Mvomero.
  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akikagua shule ya kisasa ya Sokoine Memorial inayojengwa na serikali ya wilaya Mvomero.
  .Jengo la kituo cha Mafunzo ya kilimo na mifugo kinachomaliziwa kujengwa wilayani Mvomero.
  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa miundombinu wilayani Mvomero.
  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi wa mkoa na wilaya ya Mvomero wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakishuhudia tukio la utiaji saini wa mikataba minne ya mradi wa ujenzi wa barabara za Tabora – Koga- Mpanda na Mbinga – Mbaba Bay (kilomita 402) lililofanyika leo jijini Dar es salaam
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini, Mhandisi Patrick Mfugale, akibadilishana nyaraka za mkataba mara baada ya kusaini na Mkandarasi wa Kampuni ya Jiangxi Geo Bw. Chen Xianghua leo jijini Dar es salaam, atakayejenga barabara ya Usesula hadi Komanga km 108.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipokea zawadi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji kama ishara ya shukrani kwa ajili ya ujenzi wa barabara jimboni kwake, mara baada ya kushuhudia tukio la utiaji saini mikataba minne ya mradi wa ujenzi wa barabara za Tabora – Koga- Mpanda na Mbinga – Mbaba Bay (kilomita 402) lililofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, akimkabidhi zawadi Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Bi. MarieHellen Minja, mara baada ya kushuhudia tukio la utiaji saini wa mikataba minne ya mradi wa ujenzi wa barabara za Tabora – Koga- Mpanda na Mbinga – Mbaba Bay zenye jumla ya (kilomita 402), jijini Dar es Salaam.

  ……………….

  Serikali imesaini mikataba minne na kampuni nne za ujenzi wa barabara yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 702 kwa ujenzi wa kilomita 402.

  Tukio hilo la kusaini mikataba hiyo limeshuhudiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Mandeleo ya Afrika (AfDB), MarieHellen Minja, wabunge ambao miradi hiyo ya Barabara itapita majimboni mwao, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na wakandarasi walioshinda zabuni.

  Akizungumzia utiaji saini huo, Waziri Mbarawa amesema fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Tabora (Usesula)- Koga hadi Mpanda yenye urefu wa kilomita 335 na kilomita 67 kutoka Mbinga hadi Mbamba Bay mkoani Ruvuma.

  Waziri Mbarawa amesema ujenzi wa barabara hizo ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na ahadi za Rais John Pombe Magufuli wakati wa kampeni.

  Aidha, Waziri Mbarawa ametumia nafasi hiyo kuwataka wakandarasi walioshinda zabuni kujenga barabara zenye ubora na viwango kwa kuzingatia muda wa ujenzi.

  Profesa Mbarawa ameongeza kuwa nia ya Serikali ni kuona ujenzi wa barabara hiyo unakamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

  “Naomba TANROADS msimamie ujenzi wa barabara yenye ubora kwani wakandarasi wengi ni wajanja na ikitokea mtu ameharibu asipewe nafasi kabisa ya ujenzi wa barabara hapa nchini,” amesema Waziri Mbarawa.

  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale, amesema kuwa wakandarasi waliopewa kazi wametokana na uchambuzi mkubwa uliofanyika kati ya wakandarasi 129 waliojitokeza mwaka 2016 kuomba zabuni za ujenzi wa barabara hizo.

  Mhandisi Mfugale amefafanua kuwa ili kurahisisha ujenzi wa barabara hizo wamegawa kwa wakandarasi wanne ambapo barabara ya Usesula hadi Komanga kilomita 108 itajengwa na Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering Group Corporation Limited ya China kwa gharama ya zaidi ya Sh.Bilioni 158 na itajengwa kwa miezi 36.

  “Komanga hadi Kasinde kilomita 108 itajengwa na Mkandarasi Kampuni ya China Wu Yi Co. Limited kwa zaidi ya sh.billioni 140 na Kasinde hadi Mpanda kilomita 105 Mkandarasi Kampuni ya China Railway Seventh Group Co.Ltd kwa sh. Bilioni 133,” amesema Mhandisi Mfugale.

  Mhandisi Mfugale ameongeza kuwa barabara ya Mbinga hadi Mbamba Bay kilomita 67 inajengwa na Mkandarasi China Henan International Corporation Group Co.Ltd (Chico) kwa sh. Bilioni 129.

  Amesema TANROADS imejipanga kusimamia ujenzi huo kwa kufuata viwango vinavyohitajika vya ujenzi wa barabara nchini.

  Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Bi. Minja amesema ofisi yake itaendelea kutoa mchango kwa serikali katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini pale watakapo hitajika.

  Bi. Minja amesema kuwa matarajio ya AfDB ni kuona Tanzania inapata maendeleo kwa haraka na njia rahisi ni kupitia miundombinu.

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe ambaye barabara ya Tabora hadi Mpanda inapita jimboni kwake ambapo amesema kuwa ujenzi huo utafungua fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

  Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, amesema barabara hiyo itakuwa kiungo muhimu kati ya Tanzania, Msumbiji na Malawi.

  Amesema kuwa Nyasa ina vivutio vingi vya utalii hivyo ujio wa barabara hizo utakuwa njia rahisi ya kuwafikisha watalii eneo hilo.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipata maelekezo juu ya upatikanaji wa dawa kutoka kwa mtoa huduma kushoto katika Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akifurahia jambo na baadhi ya wazee wa kijiji cha Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.PICHA NA WIZARA YA AFYA –KAHAMA.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi kitambulisho cha matibabu bila ya malipo mmoja wa wazee wa kijiji cha Segese Bibi. Shija Petro (60) kulia wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi, Bibi huyo aliwawakilisha wazee 413 waliopata vitambulisho hivyo katika Halmashauri ya Msalala ambapo lengo ni kuwafikia wazee742 kufikia Machi 2018.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimsalimia mgonjwa aliyekuwa anasubiri huduma katika Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akisisitiza jambo kuhusu upatikanaji wa dawa katika Zahanati ya Mhandu wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
  Baadhi ya Wanakijiji wa Kijiji cha Segese wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiangalia friji la kuhifadhia chanjo kwa ajili ya watoto katika Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
   
  ……………
  Na.WAMJW-Msalala

  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto aweka historia kwa kutembelea Zahanati ya Mhandu kata ya Chela Wilayani Msalala ambapo tangu Uhuru wa Tanzania kijiji hicho hakijawahi kutembelewa na Kiongozi wa Kitaifa.

  Waziri Ummy Mwalimu yupo ziara ya kikazi Wilayani Msalala kujionea Utekelezaji wa Mpango wa Malipo kwa Ufanisi(RBF) ambapo ulianza Januari 2016 kwa Mkoa wa Shinyanga

  RBFni Mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi ambapo vituo vinapewa maeneo ya utekelezaji na kupimwa kuona kama wamekidhi na kufikiwa malengo hivyo kituo huhakikiwa na hatimaye kutolewa fedha kulingana na matokeo ya idadi za huduma zilizotolewa na ubora kulingana na miongozo ya utoaji wa huduma za Afya.

  Fedha zinazopatikana zinafanya maboresho ya vituo ikiwemo miundombinu ya kituo,madawa na vifaa tiba

  Waziri Ummy Mwalimu ameipongeza halmashauri ya wilaya hiyo kwa kufanya vizuri katika kutekeleza Mpango huo hata hivyo aliwataka watendaji kufanya uhakiki na kujiridhisha kwamba huduma za Afya zitolewazo zinakidhi viwango kulingana na miongozo ya Afya ndipo malipo yatolewe

  Alisema Mpango huo unahakikisha huduma ya Afya ya msingi zinatolewa bila vikwazo,”nimekuja kufuatilia utekelezaji kwakweli nimefurahi kwani mnatekeleza na mmeboresha huduma zenu”

  Aidha,alisema kabla ya utekelezaji wa Mpango huo kuanza mwaka 2015 hali ya miundombinu ilikua mibovu,hakukuwa na dawa,hivyo kupitia Mpango huo Serikali hupeleka fedha ambazo zinasaidia kuimarisha mifumo ya vituo vya Afya,kuongeza huduma za huduma,kuchochea jamii kutumia vituo vya Afya hususan wanawake wajawazito pamoja na kutoa motisha kwa wahudumu na watumishi wa Afya katika vituo vya kutolea huduma.

  “Mpango huu tunataka wanawake wajawazito waje vituoni ndani ya miezi mitatu ya mwanzo na serikali tunaleta shilingi 8290,na mjamzito akihudhuria kliniki angalau Mara NNE wakati wa ujauzito tunaleta shilingi 6210 kwenye zahanati” alisema Waziri Ummy

  Alitaja kiasi cha shilingi 20,700 serikali inatoa kwa mjamzito akienda kujifungua kwenye Zahanati hivyo alitoa ari kwa wanawake wajawazito wilayani Msalala kuacha kwenda kujifungua kwa wakunga wa jadi kwani Serikali ya awamu ya tano imeboresha huduma za Afya nchini ikiwemo hali ya upatikanaji wa dawa ambapo Msalala kwa mwaka wa fedha 2017/2018 wametengewa shilingi milioni 417 tofauti na ile ya mwaka 2015/2016 ya shilingi milioni 108.

  0 0

  Afisa Masoko wa Nssf Riziki Kibwasali (kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja waliotembelea banda lao wakati wa maonyesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Saba saba jijini Dar es Salaam.
  Afisa Masoko wa Nssf Riziki Kibwasali (kushoto),akiwaonyesha fomu baadhi ya wateja waliotembelea banda lao wakati wa maonyesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Saba saba jijini Dar es Salaam.
  Afisa Masoko wa NSSF, Salama Mbarak (kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja waliotembelea banda lao wakati wa maonyesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Saba saba jijini Dar es Salaam.
  Afisa Masoko na UhusianoNSSF, Aisha Sango (kulia), akizungumza na baadhi ya wateja waliotembelea banda lao wakati wa maonyesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Saba saba jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wateja wakiuliza maswali iliwaweze kupata kadi ya bima ya matibabu  walipotembelea banda la Nssf wakati wa maonyesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Saba saba jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wateja wakijaza fomu kwa ajili ya kupata kadi ya bima ya matibabu walipotembelea banda la Nssf wakati wa maonyesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Saba saba jijini Dar es Salaam.


  0 0


  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu toka kulia leo asubuhi alishiriki mazoezi ya utayari na kuwatia hamasa Askari wa Mkoa wa Tabora, katika ziara yake ya siku moja mkoani humo, hatua hiyo ni kutokana na kuwataka askari wa Jeshi la Polisi kuwa na utayari wakati wote.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akiwa amembeba Joshua mtoto wa muumini wa kanisa la Siroham mkoani Tabora kabla ya uzinduzi wa zahanati ya Polisi iliyojengwa kwa hisani ya kanisa hilo.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu kutoka kushoto akiangalia mmoja wa askari wa Jeshi la Polisi akiwa katika mazoezi ya utayari kupita juu ya kamba mkoani Tabora leo. Picha na Jeshi la Polisi.

  0 0


  0 0

  Mshindi wa Pili katika Mashindano ya Miss Tanzania U.S.A. mwaka 2017, Neema Olory (wa pili toka kushoto) akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Meneja wa Masoko toka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Meena (kushoto) kama ishara ya kuwa balozi wa Utalii nchini Marekani, kulia ni Mwanzilishi wa Kampuni ya Coutious on Tanzania Justa Lujwengana na wa pili kulia ni Afisa Uhusiano Mkuu toka Bodi hiyo Geofrey Tengeneza. Meneja wa Masoko toka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Meena (kushoto) akimkabidhi Mshindi wa Pili katika Mashindano ya Miss Tanzania U.S.A. mwaka 2017, Neema Olory baadhi ya vitabu vinavyoelezea vivutio mbambali vya utalii vilivyopo Tanzania mara baada ya kumkabidhi Bendera ya Taifa kama ishara ya kuwa balozi wa Utalii nchini Marekani Mshindi wa Pili katika Mashindano ya Miss Tanzania U.S.A. mwaka 2017, Neema Olory akionesha baadhi ya vitabu vinavyoelezea vivutio mbambali vya utalii vilivyopo Tanzaniakwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa kama ishara ya kuwa balozi wa Utalii nchini Marekani mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Eliphace Marwa – Maelezo).

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Rais Dkt Ali Mohamed Shein akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw.Kheri James mara baada ya kushinda katika uchaguzi wa jumuiya hiyo uliofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Chuo Cha Mipango mjini Dodoma wa pili kutoka kulia anayeangalia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Bi. Tabia Mwita.
  Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Rais Dkt Ali Mohamed Shein akimpongeza Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Bi. Tabia Mwita baada ya ushindi wake katikati anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Kheri Denis James akiwa amebebwa na baadhi ya Wajumbe mara baada ya kutajwa kuwa ndiye Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo kwa miaka mitano
  Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu na Mkutano mkuu wa UVCCM wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi katika mkutano huo.

  Mara baada ya kutangazwa tu kuwa ndiye Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya umoja wa Vijana (UVCCM),Kher Denis James,kwa furaha kubwa iliyokwenda mpaka kwa Wajumbe wenzake,ilibidi zitumike nguvu za ziada kupunguza vurugu za shangwe zilizotarajiwa kutokea ukumbini hapo,kama uonavyo Mwenyekiti akiwa katika mikono salama ya utuliu akielekezwa kwenda jukwaa kuu.

  Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa tisa wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM),wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo,ambapo Jumuiya hiyo leo imefanya chaguzi zake za viongozi mbalimbali. 
  Makamu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake Mh. Mboni Mhita akimpongeza Makamu Mwenyekiti mpya Bi. Tabia Mwita.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Kassim Majaliwa pichani kushoto akitazama tukio la pongezi kutoka Makamu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake Mh. Mboni Mhita  akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Kheri  James.
  Makamu Mwenyekiti wa CCM na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt Ali Mohamed Shein akuhutubia wakati akifunga mkutano huo leo kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa UVCCM Kheri James, nje ya Ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma Desemba 11, 2017 (katikati) ni Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mh. William Lukuvi ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi huo akitangaza matokeo ya uchaguzi huo katika uchaguzi wa UVCCM uliofanyika kwenye Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
  Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa (Zanzibar),Rais wa Zanzibara Dkt Shein akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakiwasili ukumbini

  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa tisa wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM),wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo,ambapo Jumuiya hiyo leo imefanya chaguzi zake za viongozi mbalimbali.
  Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa tisa wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM),wakishangilia ukumbini mara baada ya kuwapata viongozi wao katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo,ambapo Jumuiya hiyo imefanya chaguzi zake za viongozi mbalimbali.

  MATOKEO UCHAGUZI UVCCM TAIFA 2017

  1. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Tanzania 2017-2022 ni Ndugu Kheri Denice James.

  2. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti... 

  Kura halali 565 
  Thabia Mwita 286 (Mshindi)
  Rashid Mohamed Rashid 282 

  #MatokeoUchaguziUVCCM

  3. Wajumbe wa NEC kutoka Tanzania Bara.. 

  Sophia Kizigo 
  Musa Mwakitinya 
  Keisha 

  #MatokeoUchaguziUVCCM

  4. Wajumbe 2 kwenda Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka Zanzibar.. 

  Abdallaghari Idrisa Juma 
  Maryam Mohamed Khamis 

  #MatokeoUchaguziUVCCM

  5. Wawakilishi kutoka Tanzania Bara kwenda Baraza kuu UVCCM Taifa nafasi 3.. 

  Rose Manumba 
  John Katarahiya 
  Secky Katuga

  #MatokeoUchaguziUVCCM

  6. Wawakilishi kutoka Zanzibar kwenda Baraza kuu UVCCM Taifa 

  Nasra haji 
  Abdallah Rajabu

  #MatokeoUchaguziUVCCM

  7. Mshindi nafasi ya Uwakilishi kutoka Vijana kwenda Jumuiya ya Wazazi ni AMIR MKALIPA
   #MatokeoUchaguziUVCCM

  8. Mshindi nafasi ya Uwakilishi Vijana kwenda UWT ni DOTO NYIRENDA

  0 0

  ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM), Sadifa Juma Khamis amepandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Mkoa wa Dodoma kwa makosa mawili yanayohusu rushwa.

  Sadifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge alifikishwa Mahakamani hapo majira ya 4:55 asubuhi na maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru)akiwa katika gari lenye namba za usajili T994 BEM.

  Akisoma kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Joseph Fovo, Wakili wa serikali kutoka Takukuru Biswaro Biswaro alisema katika kesi hiyo ya jinai namba 232 ya mwaka 2017, mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Desemba 9, mwaka huu akiwa nyumbani kwake maeneo ya Kata ya Mnadani Manispaa ya Dodoma.

  Alisema katika kosa la kwanza Sadifa anadaiwa kuwa akiwa nyumbani kwake alitoa rushwa ya vinywaji kwa wajumbe ili wamchague mgombea wa nafasi ya Makamu mwenyekiti wa UVCCM Rashid Mohamed Rashid.

  Biswaro alisema kosa la pili analokabiliwa nalo Sadifa ni kutoa ahadi ya kuwalipia gharama za usafiri wajumbe hao kutoka Dodoma –Kagera kama zawadi kwao baada ya kumpigia kura mgombea huyo.

  Wakili huyo aliwataja wajumbe hao kuwa ni Kadogo Shabani, Abdallah Hamimu, Octavian Andrea, Didas Zimbihile, Tasinta Nyamwiza, John Lufunga, Mtwawafu Kantangayo, Haleluya Ivody, Deocres Kagunila, Emmanuel Shitobelo, Happiness Rynyogote, Adolf Andrew, Adinani Musheruzi, Editha Domisian na Hashim Abdallah.

  Biswaro alisema mshtakiwa huyo alitenda makosa hayo kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15(1)(b) na (2).

  Hata hivyo alisema upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na upande wa jamhuri unaweka pingamizi la dhamana kwa mshtakiwa.Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Hakimu Fovo alimhoji mshtakiwa huyo ambapo alikana kutenda makosa yote mawili.


  Sababu za kuzuiliwa dhamana 

  Wakili Biswaro alisema sababu za kuzuia dhamana ya mshtakiwa huyo kutokana na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi UVCCM ni wa siku mbili mfululizo 10-11 Desemba 2017 na matokeo bado hayajatangazwa hivyo kuna uwezekano wa kuingilia uchaguzi huo.

  “Naomba Mahakama itambue uchaguzi bado unaendelea na mshitakiwa hadi sasa hajakabidhi uongozi bado ni mwenyekiti,”alisema

  Aidha alisema sababu nyingine ni kuwa mashahidi wengi ni viongozi ambao ni Mwenyekiti na Makatibu na endapo akiachiwa kwa dhamana ana kila aina ya ushawishi anaweza kuvuruga upelelezi.

  Kufuatia maelezo hayo, Wakili wa utetezi Godfrey Wasonga alipinga kuzuiwa kwa dhamana na kudai kuwa ni haki ya mtu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Alibainisha kiapo cha kuzuia dhamana hicho kilichowasilishwa mahakamani ambacho kimetolewa na Emma Kuhanga (Kamanda wa Takukuru Dodoma) hakina mashiko.

  “Uchaguzi wa UVCCM umeshaisha na mshindi tayari ameshapatikana na hakuna uchaguzi mwingine wa kuingilia au kama kuna uchaguzi utafanyika kiapo kingesema,”alisema Wasonga

  Alihoji sababu za kupelekwa kesi ambayo haijakamilika upelelezi na kuzuia dhamana kwa mshtakiwa na kwamba mshtakiwa huyo hataweza kuingilia uchunguzi kwa sababu walizozitoa.“Hawa mashahidi atawezaje kuwashawishi wakati mtu ameshatoka madarakani?mteja wangu ni mbunge ni mtu makini na anaaminiwa asihukumiwe kwa kuwekwa ndani kwasababu zisizo na mashiko,”alisema Wasonga.

  Aliomba Mahakama itupilie mbali pingamizi hilo na mshtakiwa apewe dhamana kwa kuwa hataweza kuingilia uchaguzi na uchaguzi mwingine wa Umoja huo ni hadi mwaka 2022.

  Kutokana na mvutano huo, Hakimu Fovo aliahirisha kesi hiyo hadi desemba 19, mwaka huu na kwamba Mahakama ndipo itatoa maamuzi kuhusu suala hilo na mshtakiwa ataendelea kuwa rumande.

  0 0


  0 0

  Mradi wa majaribio wa miezi 15 wa watoto waliokosa shule, kujifunza wenyewe kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayotumia tableti umezinduliwa mkoani Tanga.
  Mradi huo uliozinduliwa katika kijiji cha Zenith ya Kati, wilayani Muheza ni sehemu ya mradi mkubwa wa miaka mitano wa majaribio duniani chini ya Global Learning Xprize wenye lengo la kutatua matatizo ya kujifunza.
  Mradi huo hapa nchini unaendeshwa kwa pamoja na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na XPrize ambao wametoa tableti husika.
  Aidha kuwezekana kuwapo kwa mradi huo kumetokana pia na makubaliano kati ya serikali ya Tanzania kupitia Wizara yake ya elimu na TAMISEMI na mashirika.
  Katika utoaji elimu huo watoto wanaohusika ni wa miaka kuanzia 9 hadi 11 na watajifunza kwa kutumia program tano zilizowekwa katika tableti zitakazomuwezesha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.
  Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akivishwa skafu na kukaribishwa katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Kushoto ni Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo.
  Mradi huo wa Tanga ambao utagusa watoto 2,400 kutoka katika vijiji 167 vya wilaya za Handeni, Korogwe, Lushoto, Muheza, Mkinga na Pangani unatoa changamoto kwa timu ya wabunifu kuwezesha watoto walio na fursa ndogo ya kuingia katika elimu darasani kujifunza stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa kutumia tableti wakijifunza wenyewe.
  Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo katika kijiji cha Zenith, Muheza Mkoani Tanga, Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi huo Faith Shayo alisema kwamba mradi huo unaendana na majukumu ya Unesco ya kuhamasisha elimu jumuishi katika kuhakikisha kwamba watoto wote wa Tanzania wakiwemo wa jamii za pembezoni zilizo nyonge zinapata fursa.
  Alisema UNESCO inatekeleza majukumu yake kwa kuisaidia serikali ya Tanzania kuwezesha kutoa elimu bora kwa wananchi wake wote na hata wale ambao hawana uwezo wa kupata elimu kutokana na mazingira yao au maeneo yao.
  Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo akivishwa skafu na kukaribishwa katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Kulia ni Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu.
  Alisema Unesco kwa kuangalia mahitaji imekuwa ikisaidia serikali ya Tanzania katika vitu mbalimbali vya kiufundi ili iweze kufanikisha lengo la kuwa na taifa la watu walioelimika hivyo kuwa na nafasi ya kushiriki katika kazi za kujenga uchumi.
  “Mradi huu unawapa watoto ambao hawakuwahi kujiunga na shule ya msingi, fursa nyingine”alisema Faith na kuongeza kwamba juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa utaimarisha viwango vya weledi nchini.
  Faith anasema kwamba kwa sasa japo upo kwenye majaribio utakapofanikiwa utaweza kufanyiwa kazi maeneo mengine ya Tanzania.
  Aidha Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu alisema kwamba watoto hao wataangaliwa kwa namna ambavyo wanaelewa kila wiki, wanapoenda kuchaji tableti zao.
  Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu na Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo wakiwasili katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
  “wakati wa kuchaji pia tunaangalia matumizi ya tableti na ufaulu wa mtoto katika kumaliza porogramu utaonekana na kama ikionekana hasongi mbele itaangaliwa kasoro” alisema Njovu.
  Alisema kuna vijana 10 wanaojua Tehama na wamefundishwa kusaidia wanafunzi hao katika kuhakikisha kwamba tableti hazikwami au kuharibika. Watu hao wanaoishi vijijini hukohuko pamoja na kulipwa mishahara wamepewa pikipiki mpya aina ya Yamaha kwa lengo la kuhakikisha wanafika kila kata yenye wahusika na kuzungumza nao.
  Pamoja na tableti hizo pia kumefungwa sola za kuchajia na seva ya kuangalia mwenendo wa watumiaji wa tableti.
  Kabla ya kuzinduliwa kwa mradi huo watu 282 walifunza namna ya kuhudumia vijana hao ambao wanashiriki katika program.
  Mwenyekiti wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza, mkoani Tanga, Juma Killo akitoa salamu kwa XPrize, UNESCO, WFP na wageni waalikwa katika hafla hiyo. Wa pili kulia ni Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo, Afisa Miradi wa UNESCO, Nadia Marques (wa tatu kushoto), Ofisa Elimu wa wilaya ya Pangani, Mbwana Mohamed (wa tatu kulia), Kaimu Ofisa Elimu Lushoto, Beatus Kipfumo (wa pili kulia) na Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, Xavery Njovu (kulia).
  Katika mafunzo hayo wasimamizi hao ambao wanajulikana kama mama au baba vitongoji walifunza malengo ya mradi na namna ya kuangalia mwenendo wa watoto na mradi wenyewe.
  Mgeni rasmi katika ukabidhiaji wa tableti, Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu aliwataka wazazi kuhakikisha kwamba tableti hizo zinatumiwa na watoto kwa makusudi yaliyopangwa ili kuwa na taifa la watoto wenye weledi mkubwa.
  Alisema tableti hizo maalumu ni msaada mkubwa kwa wananchi na serikali hivyo hawana budi kuzitunza na kuzitumia kwa makusudio husika.
  “teknolojia hii inayowezesha watoto kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu pasipo msaada wa mwalimu ni ubunifu wa kiwango cha juu kabisa” alisema Mayasa na kuongeza kwamba hali hiyo itabadili kabisa fikra za utoaji elimu na kuwakomboa watoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu.
  Mgeni rasmi Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (kushoto) akitoa hotuba wakati wa hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza mkoani Tanga, Juma Killo, Mchumi katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza, Nelson Mwanuna pamoja na Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo.
  Aliwataka wazazi kuunga mkono jitihada za serikali kupitia kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ kwa kusaidia kujenga taifa lenye uelewa mkubwa kupitia chanzo cha sasa cha maarifa pasipo msaada wa mwalimu darasani.
  Alisema msaada huo ni pamoja na kutunza vifaa vyote vya mradi na kutumiwa na wahusika bila kukosa.
  Aidha alishukuru Shirika la UNESCO, XPRIZE na WFP kwa kuonesha njia na kusema kwamba mkoa utafanya kila linalowezekana kuona mradi huo wa majaribio unafanikiwa.
  Katika makadihiano hayo watoto zaidi ya 10 walipewa tableti kwa niaba ya wenzao ambao wanashiriki katika mradi.
  Mmoja wa wazazi wa watoto waliokabidhiwa tableti aliyejitambulisha kwa jina la Musa Ramadhani alisema amefurahishwa sana na mpango huo na kuahidi kuhakikisha kwamba anatunza kifaa hicho ili mtoto wake afaidike nacho.
  Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo akitoa salamu za UNESCO katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
  “Mtoto wangu mimi anaitwa Amir Musa na ana miaka 9; hapa tulipo ni ndani sana kupatiwa kifaa hicho kitatusaidia sisi maskini tuliosahaulika kuwa katika utaratibu tena wa weledi” alisema.
  Aidha alisema kwamba dhamana ya utunzaji inamuangukia yeye kwa kuwa anaamini ni kazi yake kuhakikisha kwamba mtoto wake anapata mafanikio kutokana na mradi huo.
  Naye mama Kitongoji Hilda Hule alisema kwamba ana uhakika kwamba watoto hao watapata maarifa na kujua kusoma kwa kasi zaidi kwa kuwa hatua za mwanzo zilionesha hamu yao ya kutaka kujua.
  Anasema kwa upande wake yeye anawaangalia watu wa kitongoji cha Zeneth na anaamini kwamba kwa mradi huo watoto wengi watafunguka.
  Mmoja wa mateknisheni wa mradi huo ambao watasaidia uwapo wa tableti na program zake Francis Kibaja mwenye makazi yake Korogwe alisema kwamba mfumo huo wa kitabu cha kielektroniki kinamfanya mwanafunzi ajifunze na kujisahihisha na kama watamaliza programu mapema kutokana labda kwa urahisi watawapangia programu ngumu zaidi ili kuwakomaza.
  Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu akitoa salamu za WFP katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
  Aidha alisema kwamba tableti hizo zinagemu kwa ajili ya mtoto akichoka na pia wakati wa mazoezi program itamwambie mtoto kama amekosea au amepatia.
  Programu zilizowekwa kwa sasa katika tableti hizo ambazo hazina uwezo wa simu ni sawa na mtu kuanza darasa la awali na kuingia shule ya msingi.
  Katika mradi huo WFP wamepewa dhamana ya kusimamia uendeshaji wa kitengo cha lojistiki na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama-ICT) cha majaribio katika mazingira halisi.
  Mama Kitongoji wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza, Hilda Hule ambaye anajukumu la kuchaji na kutunza tableti hizo akitoa maelezo ya namna zinavyotumika kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa watoto wa kijiji hicho.
  Aidha jukumu lake ni pamoja na kuingiza programu katika tableti, kuanzia vituo vya kuwekea umeme unaotokana na jua kwenye tableti hizo vijijini, kusimamia matengenezo, marekebisho na kutoa tableti mpya kipindi chote cha majaribio.
  Uzinduzi huo ulipambwa na mambo mbalimbali ukiwemo muziki wa asili ambapo kikundi cha JAHAZI ASILI zilitumbuiza kwa ngoma za asili za wakazi wa Tanga na pia muziki wa singeli.
  Ofisa wa Xprize naye alitumbukia katika burudani za singeli na kuwa burudani kubwa kwa watu ambao walienda naye sambamba na kama yeye alivyokuwa akienda sambamba na wenyeji katika zungusha.
  Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi programu mbalimbali za kujifunzia zinavyofanya kazi kwenye tableti hizo.
  Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akisisitiza umuhimu wa wazazi (hawapo pichani) kushiriki katika utunzaji wa tableti hizo kabla ya kuzigawa rasmi. Kushoto ni Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo.
  Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wa pili kulia) akisalimiana na mtoto Saidi Hausi wa kijiji cha Zeneth wakati wa zoezi la kukabidhi tableti hizo. Kulia ni Mama Kitongoji Hilda Hule mwenye jukumu la kutunza na kuchaji tableti hizo kwa umeme wa sola na Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu na Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo.
  Mama Kitongoji wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza, Hilda Hule (kulia) akikabidhi tableti kwa mtoto Saidi Hausi huku Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wa pili kulia), Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu (kushoto) wakishuhudia tukio hilo wakati wa hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
  Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wa pili kulia) akisalimiana na mtoto Juma Saidi wa kijiji cha Zeneth wakati wa zoezi la kukabidhi tableti hizo. Wanaoshuhudia tukio hilo ni kulia ni Mama Kitongoji Hilda Hule mwenye jukumu la kutunza na kuchaji tableti hizo kwa kutumia umeme wa sola, Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu (wa kwanza kushoto), Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo (wa pili kushoto).
  Tala Loubieh wa WFP akitoa maelekezo ya jinsi ya kutumia programu ya kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu kwa mtoto Gabu Lakiki mara baada ya kukabidhiwa rasmi tableti hizo kwenye hafla hiyo.
  Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller akiwapongeza baadhi ya watoto wa kijiji cha Zenith ya Kati, wilayani Muheza, mkoani Tanga waliokabidhiwa tableti hizo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa WFP wanaotoa msaada wa Tehama kwenye tableti hizo kwa watoto wa kijiji cha Zeneth pamoja wanakijiji wakifurahi jambo katika katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
  Baadhi wazazi/walezi wa watoto wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
  Kikundi cha ngoma cha Jahazi Asilia cha wilayani Muheza wakitoa burudani katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
  Makomandoo wa Skauti wakionyesha umahiri wao wakati wa kusherehesha hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
  Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller akijumuika na watoto wa kijiji cha Zeneth kucheza SINGELI wakati wa hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
  Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller aliponogewa na SINGELI katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
  Mgeni rasmi na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto waliowakilisha wenzao kwenye hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
  Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE ambao ndio wafadhili wakuu, Matt Keller akiwa kwenye picha ya pamoja na Wataalamu wa Tehama walioajiriwa na mradi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tableti na mifumo yote ya kusomea zinafanya kazi inavyopaswa katika mkoa wa Tanga na vitongoji vyake.
  Wafanyakazi wa WFP wakiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu wa Tehama walioajiriwa na mradi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tableti na mifumo yote ya kusomea zinafanya kazi inavyopaswa katika mkoa wa Tanga na vitongoji vyake.

  0 0

  Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akiwa katika kituo cha Afya Ubwari wakati wa ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.

  Waziri Jafo akiwa katika Ukaguzi wa Miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.


  Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI akiwa na baadhi ya viongozi katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.


  Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI akiwa na baadhi ya vijana waoashiriki kuchimba mitaro ya mradi wa Maji Kivindo.

  ………………  Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametoa wiki sita kwa Mkandarasi wa mradi wa maji Kivindo Wilayani Muheza kukamilisha mradi huo na uanze kutoa huduma kwa wananchi.  Waziri Jafo ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake Wilayani Muheza ambapo alikagua miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.  Alisema Mradi huo kwas asa umefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake na Mkandarasi umeahidi hapa mbele ya wananchi kwamba utaukamilisha ndani ya muda niliokupa ambao ni wiki sita kuanzia hivi sasa.

  “Sitegemei kuskia sababu zozote zitakazofanya mradi huu usikamilike ndani ya wiki sita ni mategemeo yangu wananchi wataanza kufaidi matunda ya mradi huu baada ya muda mfupi tu kuanzia sasa, Mkandarasi fanya kazi yako” Alisema Jafo.

  Katika ziara hiyo Waziri Jafo amefanikiwa kutembelea Miradi ya afya na elimu katika kituo cha afya Mkuzi na Ubwari pamoja na kutembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kilulu. 

  Waziri Jafo amewapongeza wadau mbalimbali wanaoshirikiana na Serikali katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika Maeneo ya Umma. Hususan ni Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI) kwa kutoa mifuko 50 ya Saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miundombinu katika kituo cha Afya Ubwari.  Halkadhalika Waziri Jafo ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kufanikisha ajenda ya maendeleo kwa wananchi.  Tamisemi ya Wananchi.

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akipanga tofali kwenye msingi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino)  na wasioona ya Pongwe Jijini Tanga ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo
   Mkurugenzi  Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia akijenga tofati katika vyumba vipya vitatu vya madarasa kwenye shule ya Msingi ya
  ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na wasioona  ya Pongwe Jijini Tanga ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa
   Mkurugenzi  Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia akiweka  tofati katika vyumba vipya vitatu vya madarasa kwenye shule ya Msingi ya
  ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na wasioona ya Pongwe Jijini Tanga ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa

   Mkurugenzi  Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia akiweka sawa tofati katika msingi wa moja ya vyumba vipya vitatu vya madarasa kwenye shule ya Msingi ya  ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na wasioona ya Pongwe Jijini Tanga ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo
   Mkurugenzi  Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia akimuelekeza jambo mmoja wa wakandarasi watakaojenga vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya wanafunzi wenye maahitaji maalumu ikiwemo wasiona na wenye ulemavu wa ngozi (Albino) ya Pongwe Jijini Tanga ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo

   Mkurugenzi  Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia akiweka sawa tofati katika msingi wa moja ya vyumba vipya vitatu vya madarasa kwenye shule ya Msingi ya  ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) ya Pongwe Jijini Tanga ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo
   Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza katika halfa hiyo iliyofanyika leo kwenye shule ya Msingi Pongwe Jijini Tanga
  Mkurugenzi  Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo leo
   Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Pongwe Yahaya Mafita mara baada ya kutoa hotuba fupi katika uzinduzi huo leo  ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kuthamini juhudi za kuinua elimu
   Diwani wa Kata ya Pongwe(CCM),Mbaraka Sadi akizungumza katika uzinduzi huo ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo
  Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga akizungumza katika uzinduzi huo leo kwenye shule ya Msingi Pongwe ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo
   Mkurugenzi  Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kushoto akipongezwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Pongwe Yahaya Mafita mara baada ya kutoa hotuba fupi katika uzinduzi huo leo  ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo
  Mkurugenzi  Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart katikati akifuatilia uzinduzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule hiyo uliofanywa leo na Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kushoto ni Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga

  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  BOHARI ya Dawa (MSD) imeibuka kidedea kwa kuwa mshindi wa pili (2) kwa upande wa Sekta za Umma katika tuzo ya Mwajiri Bora mwaka 2017 zinazoandaliwa na Chama cha Waajiri nchini ( ATE). 

  Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo hizo, Mgeni rasmi Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema uanzishwaji wa vipengele vipya katika tuzo hizo unazipa fursa za kipekee taasisi za serikali kupata nafasi ya kushiriki na kushinda. 

  Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Bi.Victoria Elangwa amesema tuzo hiyo ni matokeo ya maboresho ya kiutendaji kwa MSD ambayo yanafanyika kulingana na Mpango Mkakati wa MSD wa mwaka 2017 -2020.

  Ameongeza kuwa hatua hiyo ya MSD kupata tuzo ya Taasisi ya Umma inayofanya vizuri ni motisha kwa wafanyakazi na MSD kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii zaidi.
  Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Bohari ya Dawa (MSD), Victoria Elangwa (kulia), akipokea tuzo ya mshindi wa pili Sekta za Umma katika Tuzo ya Mwajiri Bora 2017 katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
  Wafanyakazi wa MSD wakiwa kwenye hafla hiyo.
  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama, akimkabidhi cheti cha ushiriki wa tuzo hizo Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Bohari ya Dawa (MSD), Victoria Elangwa. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Anthony Mavunde.
  Wafanyakazi wa MSD wakifurahia ushindi huo wakiwa na tuzo zao.

  0 0

  Chairperson of TADB’s Board of Directors, Madame Rosebud Kurwijila (left) talks with a delegation from Group Credit Agricole of Morocco (GCAM) on the right side when the delegation meets with Bank’s Board of Directors.
  TADB Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (standing) briefs Bank’s Board of Directors on importance of GCAM visit in the country. Looking on is delegation from Group Credit Agricole of Morocco (GCAM) and TADB’s Manager for Credit Appraisal, Mr. Samuel Mshote (left).
  Chairperson of TADB’s Board of Directors, Madame Rosebud Kurwijila (left) emphasizes on the need of the Credit Scoring System in Banks’s operations to delegation from Group Credit Agricole of Morocco (GCAM) (not in picture). According to Madame Kurwijila the System is important in supporting Tanzania’s agricultural development. Right is Bank’s Board Director, Madame Rehema Twalib.
  GCAM delegation together with TADB’s TADB Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (second left) and TADB’s Manager for Credit Appraisal, Mr. Samuel Mshote (left) attentively listen to Chairperson of TADB’s Board of Directors, Madame Rosebud Kurwijila (not in picture)
  Head of delegation from Group Credit Agricole of Morocco, Mr. Jalal Bouchama (right) who is a Director of Engineering and Agro business hints the role of GCAM on agriculture and socio-economic development in Morocco to the TADB’s Board of Directors (not in picture).
  Some members of TADB’s Board of Directors listen to Head of delegation from Group Credit Agricole of Morocco, Mr. Jalal Bouchama (not in picture). From left is Madame Rehema Twalib, Mr. Dome Malosha and Mr. Hassan Mbululo. Others are Mr. Joanes Kerenge and Mr. Joseph Mutashubilwa.


  By Our Reporter,

  A delegation from Group Credit Agricole of Morocco (GCAM) has met the Tanzania Agricultural Development Bank (TADB)’s Board of Directors in order to brief the Board the purpose of their visit.

  Speaking with TADB’s Board of Directors, Mr. Jalal Bouchama who is GCAM’s Director of Engineering and Agro business said that his team is in the country to facilitate to develop a Credit Scoring System that means to be used in scoring small holder’s farmer’s projects in Tanzania.

  “We intend to develop Credit Scoring System that will speed up the process of identifying viable projects through scoring small holder’s farmer’s projects in Tanzania,” he said.

  According to Mr. Bouchama, since its inception in 2004 the Credit Scoring System has assisted Morocco to advance its agriculture and socio-economic development in rural areas by identifying visible agricultural and rural development projects in Morocco.

  On her part, Chairperson of TADB’s Board of Directors, Madame Rosebud Kurwijila said the Bank appreciates GCAM visit in the country hoping once the System will be operationalized will enhance TADB to achieve Government’s intentions in supporting Tanzania’s agricultural development.

  “We do appreciate your visit hoping that we will work together to achieve Bank’s main objectives that are bestowed by our Government in efforts to bring about economic growth and poverty reduction in the country,” she said.

  Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) and Group Credit Agricole of Morocco (GCAM) signed a memorandum of Understanding (MoU) IN October 2016.

  The MoU intends to promote productive investments in the agriculture sector and development of agro-industrial value chains in the respective countries.

  According to the signed MoU, these objectives will be achieved through promotion of financing and support systems, especially for smallholder’s farmers.

  The delegation from GCAM led by Director of Engineering and Agro business, Mr. Jalal Bouchama, other members include Chief of Agroindustry Department, Mrs. Sanae Benmali, Director of Credit Information System, Mr. Abdessamad Danguir and Ms. Sara Nachid, IT Developer.


  0 0


  Na Jumia Travel Tanzania

  Kipindi cha sikukuu na mapumziko ya mwisho wa mwaka huongoza kwa watu kufanya manunuzi ya aina mbalimbali. Ni kipindi ambacho si watu hujikita zaidi kwenye kufurahia likizo zao bali hata kuwa huru kutumia pesa kwa ajili ya chakula, zawadi na huduma kadha wa kadha.
  Kama wewe ni mfanyabiashara iwe ya kubwa au ndogo,  kipindi hiki cha mwaka huambatana na faida lukuki za kujitangaza na kujitafutia masoko zaidi. Yafuatayo ni mambo tisa ambayo Jumia Travel inapendekeza kuwa unaweza kuyatumia kama fursa ili kuwavutia wateja zaidi na kujitangaza katika msimu huu.   

  Punguzo la bei. Kwa kawaida kipindi kama hiki cha msimu wa sikukuu wateja wengi hutegemea punguzo la bei kwenye bidhaa na huduma tofauti. Unaweza kuitumia fursa hii kwa kutoa punguzo la bei pia. Mbali na kutoa punguzo kwenye biashara yako lakini pia unaweza kushirikiana na wafanyabiashara wengine. Kwa mfano, kama unauza nguo unaweza kutoa punguzo la bei ambapo wateja wakifanya manunuzi ya kiwango fulani watajipatia fursa ya kupata chakula kwenye mgahawa fulani.

  Maazimio ya biashara kwa mwaka ujao. Kama ni mfanyabiashara ambaye una dira na malengo ya kuifikisha biashara yako mahali fulani lazima utakuwa na maazimio. Unaweza kukitumia kipindi hiki kwa kuwajulisha wateja wako maboresho unayotarajia kuyafanya mwaka ujao ili kuwavutia zaidi.

  Chakula. Hakuna mtu asiyependa chakula. Zipo njia nyingi za kuwashukuru wateja na wadau mbalimbali waliofanikisha kwa namna moja ama nyingine kufikia hapo ulipo. Unaweza ukaanda chakula cha pamoja na kupata fursa ya kuzungumza na kujadili masuala mbalimbali yanayoweza kusaidia kukua kwa biashara yako.

  Kadi za kushukuru. Nguvu ya kushukuru kwa kutendewa jambo fulani ni kubwa tofauti na unavyofikiri. Kwa kuonyesha kwamba unajali na kutambua mchango wa wateja kwenye biashara yako kunaweza kufungua milango mingi zaidi. Unaweza kuandaa kadi zenye ujumbe mzuri wa shukrani na kuwatumia wateja wako njia ya barua pepe au kuwapatia pale wanapotembelea biashara yako.

  Mauzo kwa wateja maalumu. Kila biashara inakuwa na wateja ambao ni waaminifu kwa namna moja ama nyingine. Kwa kutambua mchango wao unaweza kuandaa mauzo maalumu kwa ajili yao. Unaweza kulifanikisha hili kwa kuandaa kuponi na kuwapatia kisha kuwajulisha kwamba wanaweza kutembelea kwenye biashara yako na kufanya manunuzi ya kiwango ulichowapatia.
  Saidia jamii inayokuzunguka. Miongoni mwa mbinu ya kujenga uhusiano mzuri na jamii inayokuzunguka na ili kukubalika ni pamoja na kutoa msaada kwa masuala mbalimbali. Zipo nyanja mbalimbali unaweza kulifanikisha hili. Fanya utafiti mdogo kujua changamoto zinazoizunguka jamii yako na kisha omba kutoa mchango wako. Inaweza kuwa ni usafi wa mazingira, elimu, watoto yatima nakadhalika.

  Andaa shindano dogo kwa wateja. Kama mfanyabiashara unaweza ukaandaa shindano dogo kwa wateja wanaotembelea dukani kwako na kisha kujishindia zawadi mbalimbali. Unaweza ukaweka tangazo nje ya duka lako ambapo unaweza kuwavutia hata wapita njia.    

  Andaa burudani kidogo. Haijalishi biashara yako ipo kwenye hali gani lakini unaweza ukaanda chochote kuwaburudisha wateja wako. Zipo namna nyingi za burudani kama vile kuandaa michezo kwa ajili ya watoto au hata burudani ya muziki.

  Tumia mitandao ya kijamii kushirikisha matukio yote. Kwa dunia tunayoishi sasa kamwe hauwezi kuidharau nguvu ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Itumie fursa inayoitoa mitandao hii kuwashirikisha wateja wako na jamii kwa ujumla mambo yanayotukia kwenye biashara yako na utaona mabadiliko.
  Zipo njia nyingi ambazo unaweza kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara na sehemu tofauti ili kuongeza thamani ya biashara yako. Jumia Travel inakushauri kujaribu kufanya kitu tofauti katika biashara yako kabla ya mwaka kuisha. Ubunifu ni kitu muhimu ili kukua zaidi lakini pia jifunze kutoka kwa wafanyabiashara wengine wanatumia njia zipi kufanikiwa.

  0 0

  NA. Estom Sanga- Tanga

  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Huruma Mkuchika amewaagiza viongozi wa halmashauri za wilaya nchini kote kusimamia kwa karibu utekelezwaji wa miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

  Akizungumza mwanzoni mwa ziara yake ya kukutana na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- katika jiji la Tanga Waziri Mkuchika amesema ufanisi wa Mpango huo umeanza kuonekana kutokana na idadi kubwa ya Walengwa kuanza kuboresha maisha yao hivyo kinachotakiwa ni kuweko na dhamira thabiti ya wataalamu hususani wa Maendeleo ya Jamii ambao wanaweza kutoa mchango muhimu zaidi kwa Walengwa.

  Mheshimiwa Mkuchuka amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi hususani wanaokabiliwa na umaskini ili waweze kuondokana na kadhia hiyo kupitia mipango mbalimbali ukiwemo Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF.

  Aidha Mhe. Mkuchika ameonya dhidi ya uwezekano wowote wa kuhudumia wananchi wenye uwezo katika Mpango huo na kuagiza Watendaji wa halimashauri za Wilaya kuhakiki mara kwa mara majina ya kaya zilizoko kwenye Mpango ili kujiridhisha na walengwa wa Mpango ambao ni kaya Maskini sana.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuchika ametembelea kaya za baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini katika jiji la Tanga na kujionea namna ruzuku wanaoipata ilivyoanza kuboresha maisha yao kwa kuboresha makazi ,kuanzisha miradi midogo midogo ya biashara, kusomesha watoto na kuimarisha huduma za kliniki kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

  Taarifa ya Mkoa wa Tanga imeonyesha kuwa tangu shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini zianza takribani miaka mitatu iliyopita Kaya zilizokuwa zinaishi katika umaskini mkubwa wa kipato zimeanza kuboresha maisha huku changamoto kubwa iliyobakia ikiwa ni idadi nyingine ya wananchi wanaoishi kwenye Umaskini mkubwa wa kipato kutojumuishwa kwenye mpango kutokana na uhaba wa fedha. 

   Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora,Mhe. George Huruma Mkuchika (aliyevaa Kaunda suti )akiangalia ‘genge’ la bidhaa zinazouzwa na mmoja wa Walengwa wa TASAF katika mmoja wa mtaa wa jiji la Tanga.

   Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika akimpongeza mmoja wa Walengwa wa TASAF jijini Tanga baada ya kukagua nyumba aliyoijengwa kwa kutumia sehemu ya ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini .
   Baadhi ya Viongozi walioambatana na Mhe. Mkuchika (wa nne kulia walioketi) wakisikiliza taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF katika mmoja wa mitaa ya jiji la Tanga. Wa pili kulia waliosimama ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,bwana Ladislaus Mwamanga. 
   Waziri Mkuchika akiwa ameketi nje ya mgahawa wa mmoja wa Walengwa TASAF katika jiji la Tanga ,Mgahawa ambao ameuanzisha mlengwa huyo baada ya kupata ruzuku kutoka Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. 
   Mhe. Mkuchika akiwa ndani ya nyumba ya mmoja wa Walengwa wa TASAF ,katika jiji la Tanga ,nyumba ya mlengwa huyo imeezekwa kwa mabati kwa kutumia sehemu ya ruzuku kutoka Serikalini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika akizungumza na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Tanga na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga kabla ya kuwatembelea walengwa wa TASAF kuona namna wanavyonufaika na huduma za Mfuko huo mkoani humo.

older | 1 | .... | 1457 | 1458 | (Page 1459) | 1460 | 1461 | .... | 1896 | newer