Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1456 | 1457 | (Page 1458) | 1459 | 1460 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mkuu Wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na Vijana wa Jogging mbalimbali za Wilaya ya hiyo zilizofika katika maadhimisho ya Miaka Minne ya Trump Joging ya Vingunguti ambapo aliaahi kuviwezesha vikundi vyote vya Joging kupitai amfuko wa Vijana wa Halmasahuri kupata mikopo ya Asilimia tano kutoka pato la Halmashauri.
   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti Omary Kumbilamoto akizungumza na Vijana wa Joging mbalimbali za Wilaya ya hiyo zilizofika katika maadhimisho ya Miaka Minne ya Trump Joging ya Vingunguti
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akipkea zawadi ya Kondoo kutoka Klabu ya Trump Joging ya Vingunguti
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, akikimbia kwa kupandisha ngazi wakati wa Mazoezi ya pamoja na Vijana wa Joging wa Manispaa ya Ilala waliojumuika na Trump joging kutimiza Miaka minne
   Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa Dansi akitoa shukrani zake zimfikie Rais Magufulikwa kutolewa kwa Nguza Viking na Familia yake katika kifungo kilichokuwa kinawakabili
   Baadhi ya Viongozi wa kisiasa waliofika katika mahadhimisho ya miaka minne ya Klabu ya Trump Joging
   Baadhi ya Wanamichezo walikuwa wanajitolea Damu wakati sherehe hizo zikiendelea jijini Dar es Salaam leo
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwana Viongozi wa Makundi mbalimbali ya Joging
  wanachama wa trump Joging wakiimba kwa shangwe wakati wa mazoezi ya kutimiza Miaka Minne ya Klabu yao

  0 0


  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais Wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM taifa Ndugu Mboni Mhita katika Mkutano Mkuu wa 9 wa Umoja wa Vijana UVCCM unaofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma, wa tatu kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein , Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu Hamidu Shaka.
  2
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais Wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM taifa Ndugu Mboni Mhita katika Mkutano Mkuu wa 9 wa Umoja wa Vijana UVCCM unaofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma, wa tatu kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein
  3
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais Wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM taifa Ndugu Mboni Mhita katika Mkutano Mkuu wa 9 wa Umoja wa Vijana UVCCM unaofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma, wa tatu kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  4
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais Wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 9 wa Umoja wa Vijana UVCCM unaofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma, na kulia Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM.
  05
  Naibu Katibu Mkuu wa UVCM Taifa Ndugu Hamidu Shaka akisoma taarifa ya miaka mitano kwa kwenye mkutano wa 9 wa Umoja wa Vijana UVCCM unaofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
  5
  Baadhi ya Picha zikionyesha wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 9 wa UVCCM unaofanyika kwenye chuo cha Mipango mjini Dodoma.
  78
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
  9
  Mwanamuziki wa bendi ya TOT Khadija Kopa kulia na waimbaji wakundi hilo wakitumbuiza katika mkutano huo.
  10
  12

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ubora wa kiatu cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza Melkior Komba, Katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Viatu hivyo vimetengenezwa na kiwanda cha Jeshi la Magereza Karanga kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro.PICHA NA IKULU

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini Nyaraka zenye majina ya Wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa pamoja na majina mawili(2) ya Familia ya Nguza Viking(Babu Seya), na Johnson Nguza waliopata msahama wa Rais, katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini Nyaraka zenye majina ya Wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa pamoja na majina mawili ya Familia ya Nguza Viking (Babu Seya), na Johnson Nguza waliopata msahama wa Rais, katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akishuhudia.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiyahakiki kwa kuyasoma majina ya Wafungwa 63 waliopata msahama wa Rais kabla ya kutia saini Nyaraka hizo za Msamaha katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kuhakiki nyaraka hizo za Msamaha wa Rais katika Ikulu ya Chamwino mkoni Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa mara baada ya kutia saini majina ya wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa pamoja na majina mawili ya Wafungwa Nguza Viking(Babu Seya), na Johnson Nguza waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akizungumza kuhusu Msamaha wa Rais na namna ulivyopokelewa vizuri ndani nje ya Magereza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumzia msamaha alioutoa jana kwa wafungwa waliokuwa wanatumikia vifungo mbalimbali magerezani. Kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akisikiliza.

  PICHA NA IKULU

  0 0


  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa tuzo ya C40 Bloomberge Philantropies .
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wa kwanza kushoto mstari wa mbele akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine huko Chicago Nchini Marekani wakiwa wameshika tuzo zao.

  Picha ya tuzo ya C40 Bloomberge Philantropies iliyotolewa kwa jiji la Dar es Salaam Chicago Nchini Marekani.

  …………

  JIJI la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji 10 duniani ambayo yamepata tuzo ya C40 Bloomberg Philantropies 2017 kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.

  Katika tuzo hiyo mwaka huu imepokelewa na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Miwta aliyerejea nchini alfajiri ya Desemba 8 mwaka huu.

  Jiji la Dar es Salaam limechangia tuzo hiyo na Jiji la New York nchini Marekani na .

  Mradi wa Mabasi yaendayo haraka unawahudumia abiria 200,000 kila siku kwa kutumia mabasi ya kisasa ambayo yanachangia kupunguza msongamano wa magari barabarani na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na hivyo kuwa siri ya mafanikio ya tuzo jijini hapa.

  Tuzo ya C40 Bloomberg Philanthropies hutolewa kila mwaka katika miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mahususi matano ili kutambua jitihada za majiji wanachama wa Taasisi ya mtandao wa Majiji zaidi ya 90 duniani inayoshughulika na namna bora ya kukabiliana na Athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchi Duniani.

  Imetolewa leo Desemba 10

  Na Christina Mwagala , Afisa Habari Ofisi ya Mstahiki Meya wa jiji.

  0 0

   
   Mhasibu Mkuu wa Serikali, Francis Mwakapalila (kulia), akikabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza wa kipengele cha Wazalishaji katika tuzo za Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ya mwaka 2016 kwa Mdhibiti Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Isaac Lupokela, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaamjuzi. Tanga Cement pia iliibuka na ushindi wa jumla katika tuzo hizo hii ikiwa ni mwaka wa pili mfukulizo kuibuka na ushindi wa jumla.  Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, Pius Maneno. 
   Wahasibu wa Tanga Cement, Edgar Mlenge (kushoto), na Isaac Lupokela wakionesha tuzo ya mshindi wa jumla mara baada ya kampuni yao kutangazwa washindi katikaUwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2016 jijini Dar es Salaam juzi.
   Wahasibu wa Tanga Cement, Edgar Mlenge (kulia), na Isaac Lupokela (katikati), Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa TCPLC, Mtanga Noor (kushoto), wakionesha tuzo ya mshindi wa jumla na mshindi wa kwanza kipengele cha Wazalishaji mara baada ya kampuni yao kujizolea tuzo hizo katikaUwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2016 jijini Dar es Salaam juzi.
  Mdhibiti Fedha wa Tanga Cement, Isaac Lupokela (katikati), akisakata rumba pamoja na baadhi ya waalikwa katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa tuzo za uwasilishaji bora wa mahesabu zilizoandaliwa na NBAA jijini Dar es Salaam juzi.

  0 0

  Dkt. Darius Mkiza akitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika fani ya Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT) na Askofu Flaviani Matindi Kassala wa Jimbo Katoliki la Geita kwa niaba ya Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Tercius Ngalekumtwa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza.
  Dkt. Judith Adongo Aloo akitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika fani ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT)na Askofu Flaviani Matindi Kassala wa Jimbo Katoliki la Geita kwa niaba ya Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Tercius Ngalekumtwa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza.
  Wahitimu wa Shahada ya Uzamivu (PhD) Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT) (mstari wa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo mara baada ya kutunukiwa shahada zao mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza. Wa kwanza kulia ni Dkt. Darius Mkiza, wa pili kulia ni Jacob Roman Lubuva, wa kwanza kushoto ni Neema Bhoke Mwita na Judith Adongo Aloo (wa pili kushoto). (Picha na Martin Nyoni, SAUT, Mwanza)

  Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT) pamoja na Vyuo Vikuu vyake Vishiriki kimetoa jumla ya wahitimu 8,687 kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kwa kutekeleza azma ya Serikali ya kuandaa wataalamu mbalimbali nchini. Uongozi wa Chuo hicho umeishukuru Serikali kwa kuishirikisha sekta binafsi katika kutoa mchango wao katika sekta ya elimu na umeihakikishia Serikali kuwa kanisa Katoliki litaendelea kuwa mdau muhimu kwa taifa katika kutoa huduma za jamii nchini.

  Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwa’ichi wa Jimbo kuu la Mwanza, ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi katika mahali ya 19 ya chuo hicho ambapo wahitimu hao wametunukiwa Astashahada, Stashahada na Shahada ya kwanza, shahada ya uzamili pamoja shahada ya uzamivu. Askofu Ruwa’ichi amewataka wahitimu hao wawe wabunifu hatua itakayowawezesha kujiajiri na kuwaajiri watu wengine kwa kuitambua na kuitumia vema fursa ya uwepo wa tecknolojia pamoja na fursa nyingine zilizopo katika mazingira na jamii wanapoishi wakizingatia maadili ya taaluma zao pamoja na maadili ya jamii ili waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla.

  “Tambueni na onesheni thamani yenu katika jamii kwa elimu mliyoipata hapa SAUT, jamii inatarajia kutumia ujuzi wenu ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi. Kati ya wahitimu hao, chuo kikuu cha SAUT Mwanza na kituo cha Dar es salaam kimetoa jumla ya wahitimu 2147 ambapo asilimia 55 ni wanaume na asilimia 45 ni wanawake kutoka fani mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo. Fani hizo ni Uandishi wa habari, Mahusiano ya Umma, Mahusiano ya Jamii na Masoko, sosholojia, Falsafa ya Elimu, Uhasibu, Utawala wa Afya, Uchumi, Ugavi, Sheria, Isimu ya Lugha Utawala na Biashara.

  Fani nyingine ni, Historia, Utawala wa Elimu na Mipango Usimamaizi wa Maendeleo ya Elimu ya Juu, Uhandisi wa Ujenzi, Sayansi ya Kompyuta, Uhandisi wa umeme, Elimu ya Shule ya Msingi pamoja na Sanaa na Elimu. Miongoni mwa watimu hao wapo wahitimu wane katika ngazi ya shahada ya Uzamivu (PhD) akiwemo Darius D. Mkiza na Jacob Roman Lubuva katika fani ya Mawasiliano ya Umma pamoja na Judith Adongo Aloo na Neema Bhoke Mwita katika fani ya Sheria. Akinukuu maneno ya Rais wa zamani wa Marekani John Kennedy aliyowahi kusema “Usijiulize taifa litakufanyia nini wewe, bali jiulize wewe utalifanyia nini taifa lako”, Askofu Mkuu Ruwa’ichi aliwahimiza wahitimu hao wawe wabunifu ili waweze kuonesha tofauti katika jamii kwa kufanya maamuzi sahihi wakati wa kutekeleza majukumu yao na kuwa mabalozi wazuri wa chuo hicho.

  Zaidi ya hayo, Askofu Mkuu Ruwa’ichi amewataka wahitimu hao kuwa wakweli daima wakati wa kutekeleza majukumu yao huku akiwahimiza waichukie rushwa, wasitoe wala kupokea rushwa bali wafanye kazi kwa juhudi na maarifa wakimtegemea Mungu daima. Aidha, Askofu Mkuu Ruwa’ichi amesisitiza kuwa chuo cha SAUT kimekuwa mdau muhimu kwa Serikali ya Tanzania kwa kutoa mchango uliotukuka kwa taifa kwa kuzingatia Sera ya Elimu ya Mwaka 2014 ambayo ilifanyiwa maboresho ktoka Sera ya Elimu ya mwaka 1995.

  Lengo la sera hiyo ni kuiwezesha nchi kupata watanzania walioelimika ili waweze kuingia katika mazingira ya ushindani ili wanaweze kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa viwanda na wa kati ifikapo mwaka 2025 kulingana na Dira ya Maendeleo ya taifa. Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho Padre Dkt. Thadeus Mukama amesema kuwa SAUT imetoa mchango mkubwa taifa katika fani wanazotoa wakiongozwa na fani kongwe ya uandishi wa habari inayotolewa chuoni hapo tangu kuanzishwa kwake.

  Dkt. amewataja baadhi ya watumishi mbalimbali waliosoma chuoni hapo na kushika nafasi mbalimbali katika taifa na maeneo mbalimbali duniani wakiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas, Emmanuel Buhohela, na Jackson Msangulla ambao wanafanyakazi Ofisi ya Rais katika Kurugenzi ya Mawasiliano.

  Dkt. Mukama aliendelea kuwataja watumishi wengine waliosoma SAUT kuwa ni pamoja na Deodatus Balile mwandishi wa habari wa gazeti la Jamhuri, Hoyece Temu anayefanyakazi katika Ofisi za Umoja wa Mtaifa, Tanzania, Zawadi Machibya na Sami Awami, Ester Namhisa, Liisy Masinga ambao wanafanyakazi ya uandishi wa habari katika Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, Raymondi Nyamwihula anafanyakazi Azam Media, Dotto Bulendu anafanyakazi Radio SAUT, Jonas Songora anayefanyakazi radio Japan pamoja na Maafisa Habari na Mahusiano wengi wanaofanyakazi Serikalini katika Wizara, taasisi, mikoa, majiji na halamashauri na mbalimbali zisizo za kiserikali ndani na nje ya nchi.

  Aidha, katika mwaka huu wa masomo wa w 2017/2017 Dkt.Mukama amesema kuwa chuo hicho kimedahili wanachuo pamoja na matawi yake kimedahili wanachuo wapatao 20600 ambapo lengo la chuo ni kudahili wanachuo wapatao 30,000 ifikapo mwaka 2020. Kwa upande wao wahitimu wa fani ya Mawasiliano ya Umma Dkt. Darius D. Mkiza na Dkt. Jacob Roman Lubuza ambao pia ni wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Tumaini Tawi la Dar es salaam wamesema kuwa watatumia elimu waliyoipaata katika kwa kufundisha vyuo vikuu, kutangaza utalii wa Tanzania, kufanya utafiti, kuandaa mitaala mbalimbali ya elimu na kutoa ushauri wa kitaalam ikiwa ni mchango wao kwa taifa kuelekea kujenga uchumi wa kati.

  0 0

  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akifurahi jambo na Spika wa Bunge la Morocco, Mheshimiwa Habib El Malk (kulia) nyumbani kwake mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akiteta jambo na Spika wa Bunge la Morocco, Mheshimiwa Habib El Malk(kushoto) nyumbani kwake mjini Dodoma ikiwa ni baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru wa Tanzania Bara.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimkaribisha Spika wa Bunge la Morocco, Mheshimiwa Habib El Malk (kushoto) nyumbani kwake mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa mazungumzo yenye lengo ya kudumisha urafiki baina ya nchi mbili.


  0 0

   Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa Umeme kwa njia ya luku na kusema kuwa kwa sasa upo sawa na wanaweza kununua katika mifumo iliyozoeleka.


  Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA)  wa Tanesco, Demetruce Dashina amesema kuwa kulitokea tatizo dogo la mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya Luku kutokana na wataalamu wa shirika hilo walipokuwa wakiamisha mitambo hiyo kutoka ofisi ya Zamani kwenda sehemu nyingine.


  “Jana tulikuwa tunafanya uhamisho wa mfumo wa luku kwende katika ofisi zetu mpya hivyo ikawalazimu wateja wetu kupata usumbufu kidogo, lakini kuanzia saa saba mfumo huo umekaa sawa na wateja wanaweza kununua umeme kama walivyokuwa wanafanya hapo awali bila shida yoyote mara baada ya marekebisho ya kiufundi” amesema Dashina


  Amesema kuwa shirika lilijipanga kuwahudumia wateja wake kama kawaida wakati wa kuhamisha mitambo hiyo lakini Wananchi wengi wakapata taharuki hivyo kufanya mfumo wa ziada kuzidiwa kutokana na watu kununua umeme kuliko Kawaida.


  Kwa upande wake Kaimu Meneja  Uhusiano wa Tanesco Leila Muhaji amewaomba radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na kuwasisitiza kuwa sasa wanaweza kununua katika mifumo iliyozoeleka.


  Muhaji amesema kuwa Tanesco inatambua umuhimu wa umeme hivyo   kuwataka watanzania kuwa na Imani na shirika lao kwani lipo kwa ajili ya kuwahudumia  kama inavyohitajika.

   Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA)  wa Shirika la Umeme nchini Tanesco, Demetruce Dashina Akizungumza na Waandishi mara baada ya kuimarika kwa mfumo wa kununua Umeme kwa njia Luku 
     Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco, Leila Muhaji akifafanua jambo wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari juu ya kuimarika kwa Mfumo wa Ununuzi wa luku mara baada ya kuhamia sehemu nyingine. 
  Waandishi wa habari habari walifika katika mkutano huo wakifatilia kwa Makini.

  0 0


  MBUNGE WA JIMBO LA NKENGE BALOZI DR.DIODORUS KAMALA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KITUO CHA AFYA KABYAILE NA KUBAINI CHANGAMOTO YA HUDUMA WATUMISHI,MIUNDOMBINU NA VITENDEA KAZI 

  0 0

  Wahasibu wa Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50 wakiwa katika picha ya pamoja na Mhasibu Mkuu wa Fungu hilo Bw. Christopher Nkupama (wa pili kushoto) baada ya kupokea Tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 zilizotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam .
  Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wahasibu wa Wizara hiyo fungu 50 baada ya kuwakabidhi tuzo hiyo katika eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, aliyeshika tuzo ni Mhasibu Mkuu wa Fungu hilo Bw. Christopher Nkupama.
  Washindi wa Kwanza wa makundi mbalimbali ya Tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 zinazotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu baada ya kukabidhiwa tuzo hizo eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mmoja wa wahasibu walioambatana na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango-fungu 50, Bw. Christopher Nkupama (hayupo pichani) akisalimiana na meza kuu baada ya kupokea tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 iliyotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji l Dar es Salaam.

  Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila (wa kwanza kulia) akimklabidhi Mhasibu wa Wizara ya Fedha na Mipango-fungu 50 (Vote 50), Bw. Christopher Nkupama (kushoto) tuzo kwa kuwa mshindi wa kwanza wa taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 kwa kundi la Wizara na Idara za Serikali iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju, Nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA. Pius Maneno.
  Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila akieleza kuwa Uhasibu ni taaluma muhimu katika maendeleo ya Viwanda kwa kuwa wawekezaji hutumia taarifa za fedha zinazoandaliwa ili kutoa maamuzi, wakati wa kuhitimisha mkutano wa mwaka wa Wahasibu na kugawa tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa washindi wa mwaka 2016, katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA. Pius Maneno muda mfupi kabla ya kutoa tuzo za taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam

  Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango


  Benny Mwaipaja-WFM, Dar es Salaam

  Wizara ya Fedha na Mipango Fungu Hamsini (Vote 50)linalohusika na masuala ya utawala, limeibuka kinara kwa kupata tuzo ya mshindi wa kwanza katika utoaji wa Taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 katika kundi la Wizara na Idara za Serikali inayoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).

  Tuzo hizo zimetolewa kwa washindi na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa Mkutano wa mwaka wa Wahasibu nchini uliofanyika katika eneo hilo.

  CPA. Mwakapalila alisema kuwa taarifa bora za fedha ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi kwa kuwa walipa kodi, wawekezaji na wadau wengine hutegemea taarifa hizo katika kufanya maamuzi.

  ‘Kama taarifa za fedha hazitatolewa kwa ubora unaotakiwa na kwa wakati mwafaka kunaweza kusababisha athari katika uthabiti wa mifumo ya kifedha nchini’, alieleza CPA. Mwakapalila

  Aidha Mwakapalila amewapongeza wahasibu kwa kuamua kukaa pamoja na kujadili taaluma ya uhasibu katika maendeleo ya viwanda ambayo ni ajenda ya kipaumbele kwa Serikali ya awamu ya tano.

  Amesema suala la Uchumi wa viwanda ni muhimu katika kuongeza kipato na kupata fedha za kigeni kwa njia ya kuuza bidhaa nje na pia kupata mapato ya kodi na yasiyo ya kodi hivyo akatoa rai kwa wananchi kuendelea kujadili masuala ya uchumi wa viwanda na kupata namna sahihi ya kuufikia ili ndoto ya uchumi huo ziweze kuwa za kweli.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA. Pius Maneno amesema kuwa tuzo zinazotolewa na NBAA zinalengo la kuhamasisha uwajibikaji na kuandaa taarifa ya fedha zilizo na viwango vya kimataifa.

  Amesema kuwa washindi wa tuzo hizo wanapatikana kupitia mchakato uliosheheni weledi wa hali ya juu kutoka kwa wabobezi wa taaluma ya uhasibu nchini ambao wanaangalia vigezo kadhaa vikiwemo kuwa na hati safi na kuwasilisha Hesabu kwa wakati na pia kufikisha kiwango cha ubora wa taarifa kuanzia asilimia 75.

  Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50, Bw. Christopher Nkupama, amesema kuwa tuzo hiyo inawapa morali ya kufanyakazi kwa umahili zaidi na kuwapongeza watumishi walioko katika idara yake kwa kufanyakazi kubwa na bila kuchoka kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni na taratibu za uhasibu wanapotekeleza majukumu yao.

  Mshindi wa Jumla katika tuzo hizo kwa taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 ni Twiga Cement Plc na kwa upande wa Wizara na Idara za Serikali ni Wizara ya Fedha na Mipango fungu hamsini (V. 50), tuzo ambayo ilipokelewa na Mhasibu Mkuu wa fungu hilo Bw. Christopher Nkupama, ikifuatiwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji fungu arobaini na nne (V.44) na Ofisi ya Waziri Mkuu fungu ishirini na tano (V. 25)

  Washiriki wa Tuzo hizo ni Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Wakala wa Serikali, Wizara na Idara za Serikali na Sekta Binafsi ambapo kwa mwaka huu waliojitokeza kutoka Mamlaka ya Serikali za Mitaa walikua sita na Wizara na Idara za Serikali walikua sita.

  Jumla ya washidani waliojitokeza ni 56 na waliofanikiwa kuvuka kigezo cha kuwa na zaidi ya asilimia 75 walikua washidi 36 na hao walifanikiwa kushika nafasi ya kwanza hadi ya tatu kulingana na makundi.

  Vilevile Idadi ya Wahasibu ambao wamehudhuria katika Mkutano wa mwaka ambao hufanyika kila mwaka kabla ya kutolewa tuzo hizo imepanda kwa asilimia 60 ambapo mwaka 2016 walihudhuria wajumbe 1700 ilihali mwaka huu 2017 wamehudhuria zaidi ya wajumbe 2700.

  0 0

  SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
  Tunawataarifu Wateja wetu kuwa, hivi sasa mifumo ya LUKU inapatikana katika njia zote za manunuzi.
  Wateja mnaweza kufanya manunuzi kwa kutumia njia zote.
  Asanteni kwa ushirikiano wenu.
  Tovuti: www.tanesco.co.tz
  Mitandao ya Kijamii
  www.facebook/tanescoyetultd

  twitter.com/tanescoyetu
  Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
  TANESCO Makao Makuu
  Desemba 10, 2017

  0 0


   Marehemu Joyce Mmasi enzi za uhai wake.
   Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mwanahabari Joyce wakati ukiwasili viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo kwa ibada ya kuuaga kabla ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.
   Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
   Wanahabari wakiwa kwenye ibada hiyo.
   Wadau mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
   Mchungaji Kulwa wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, akiongoza ibada hiyo.
   Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando akizungumza kwenye ibada hiyo.
   Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo akizungumza. Lyimo na marehemu Mmasi wanatoka kijiji kimoja.
   Familia ya marehemu ikiwa katika ibada hiyo. Kulia ni mtoto wa kwanza wa marehemu, Lawrence Nicky Mayella.
   Mume wa marehemu Joyce Mmasi, Andrew Kamugisha akizungumza kwenye ibada hiyo.

  Rafiki wa marehemu Mashaka Mgeta, akizungumzia maisha ya Joyce na jinsi alivyomfahamu.


   Waandishi wa habari wanawake wanaounda kikundi cha Wawata wakitoa neno katika ibada hiyo.
   Mwanahabari Hellen Mwango akisaidiwa baada ya kupoteza fahamu.
   Mtoto mkubwa wa marehemu,  Lawrence Nicky Mayella, akisoma Historia ya mama yake.
   Mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Thomson, akizungumza katika ibada hiyo.
   Waombolezaji wakiwa katika foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu.
  Foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho.

  Na Dotto Mwaibale

  VILIO Majonzi na simanzi vilitawala   wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa mwanahabari nguri Joyce Mmasi iliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

  Katika ibada hiyo mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wanahabari na wadau wengine walijitokeza katika viwanja hivyo kwa ajili ya kumuaga mpendwa wao Joyce Mmasi ambaye alikuwa akifanyia kazi katika gazeti la Mwananchi.

  Mchungaji Kulwa kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambaye aliongoza ibada hiyo aliwaambia watu waliokuwepo kwenye ibada hiyo kuwa wanapaswa kujitayarisha wakati wote kwani hawajui ni lini wataondoka hapa duniani.

  "Mwenzetu Joyce ametutangulia tulikuwa naye pamoja lakini wewe uliye hai leo hii umejiandaeje katika maisha ya kiroho?" alisema Mchungajia Kulwa.
  Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando alisema kifo cha Mmasi kimemshitua kila mtu na wanahabari wamepata pigo la kumpoteza mwenzao.

  Mhando alihimiza kudumisha upendo kwa watu wote pamoja na wanahabari.

  Katika ibada hiyo makundi mbalimbali yalijitokeza kutoa salamu za rambirambi na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, siasa, serikali na wadau wengine.

  Mwili wa marehemu Joyce umesafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro nyumbani kwao kwa mazishi.

  Marehemu ameacha mume na watoto watatu, Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu.


  0 0

  `Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameziagiza Taasisi zote zenye usimamizi kuhakikisha zinasimamia vyema jukumu lao la kutumia nafasi zao kuongeza juhudi katika kuimarisha misingi ya Utawala Bora, Uwazi, Uadilifu na Uwajibikaji.

  Makamu wa Rais aliyasema hayo leo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa yaliofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma.

  Makamu wa Rais alisema Vita dhidi ya ukiukwaji wa Maadili haiwezi kupiganwa na Serikali peke yake, “Ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa vitendo vya rushwa, ubadhirifu na maovu mengine vinatokomezwa”

  Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kisera na kisheria ambayo itahakikisha vijana wanakuzwa kimaadili kwani hakuna Taifa Duniani linaweza kupata maendeleo bila kuwa na utamaduni unaozingatia maadili alisema Makamu wa Rais.

  Makamu wa Rais alisisitiza kuwa ili kujenga Utawala Bora ni lazima kuweka uwiano wa yanayofanyika na serikali kuu hadi serikali ya mitaa nchi nzima.Serikali ilizindua Rasmi mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu (NACSAP III) Desemba 2016.

  Makamu wa Rais alisema kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya Ofisi za Serikali, Serikali imeamua kufuatilia uhalali wa vyeti vya Watumishi, Idadi halali ya Watumishi wa Umma na ulipaji wa Mishahara Hewa na kusisitiza zoezi ili litakuwa endelevu.

  Mwisho, Makamu wa Rais aliwaeleza wananchi na Watumishi wa Umma kwa ujumla kuwa Maadili ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi yetu. “Ni imani yangu kuwa Wakuu wa Taasisi hizi kuwa mtahakikisha misingi ya haki za binadamu, utawala bora na viwango vya Maadili ya Viongozi wa Umma vinasimamiwa ipasavyo ili kuimarisha nidhamu ya Maafisa na Watumishi wa Umma”.

  Kuimarishwa na kudumishwa kwa nidhamu ya utendaji, huduma zitolewazo Serikalini, Ukusanyaji wa mapato na matumizi bora ya fedha za Serikali kutaleta mafanikio katika kuelekea uchumi wa kati.  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wageni kutoka vyama rafiki toka nchi mbalimbali baada ya kufungua mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifungua rasmi mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wa meza kuu wakimsikiliza mwanachama mpya Ndg. Alfred Msando akisalimia wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
  :Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na aliyekuwa mbunge wa Kinondoni na mwanachama mpya Ndg. Maulidi Mtulia baada ya kusalimia wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo mbele ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi meza kuu wakiimba na kucheza nyimbo za hamasa pamoja na wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi meza kuu wakiimba na kucheza nyimbo za hamasa pamoja na wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017.

  PICHA NA IKULU

  0 0  Nollywood ace actor and movie director, Ramsey Nouah and Tanzanian actress and entrepreneur, Jokate Mwegelo will join Sahara Tanzania Limited to kick start the company’s vision of grooming and empowering future leaders in Tanzania.

  Nouah and Mwegelo will engage young Tanzanians at the Nkrumah Hall, University of Dar Es Salaam on December 14, 2017 on the theme: #MyFutureStartsWithMe. This is coming ahead of the convention of an elaborate empowerment project by Sahara Tanzania in 2018 that will address how youths can harness their potential and prepare for success as entrepreneurs.

  An affiliate of Sahara Group, a leading African energy and infrastructure conglomerate, Sahara Tanzania Limited plans to replicate the Group’s extrapreneurship initiatives in Tanzania to enhance opportunities for socio-economic growth and development. Sahara deploys extrapreneurship platforms to create, preserve and replicate wealth by establishing a network for innovators, entrepreneurs and investors.
  Sahara Group’s Spokesperson, Bethel Obioma, said the project was in line with the Group’s unflinching commitment to promoting the achievement of the Sustainable Development Goals (SDGs) across the globe. “We are so delighted to have Ramsey and Jokate working with us to lay the foundation for the empowerment project which we believe will inspire and transform the lives of youths in Tanzania.”

  Nouah, winner, Best Actor in a Leading Role at the African Movie Academy Award in 2010, said he was excited at the platform Sahara Tanzania was providing for youths to dream and back their aspirations with “the right support and counsel.” He added: “The goal of the project is to produce and empower young extrapreneurs in Tanzania who will transform the world from Africa. The exceptionally gifted youths in the continent need to know that the theme #MyFutureStartsWithMe is not a cliché. It is a clarion call for African youths to take charge of their aspirations.”

  Mwegelo, who was named among Forbes Africa 2017 list of “30 under 30” successful entrepreneurs, is the promoter of ‘Be Kidotified’ a campaign which empowers young girls by building sports facilities in public schools, and promoting education and entrepreneurship. She said the timing of project resonates with Tanzanian youths’ growing awareness of their role in transforming the nation. “Tanzanian youths now have an opportunity to reach for their dreams through the extrapreneurship and empowerment programmes of Sahara Group in Tanzania,” she stated.

  Obioma said the Group also plans to formally launch Sahara Foundation, its corporate responsibility vehicle in Tanzania to ensure it explores all possible avenues and collaborations for “bringing energy to the lives of the good people of Tanzania.”

  In January 2017, Sahara Foundation commissioned its maiden project in Tanzania – the upgrade of the Library at Pugu Secondary School. The intervention which involved renovation of the facilities and donation of textbooks and various aides has transformed the learning experience of over 900 students and 70 teachers at the school. The teachers were also trained on how to maximize the resources in the library for students at various levels.

  Sahara Foundation Manager, Oluseyi Ojurongbe said: "the project represents our commitment to the pursuit of Sustainable Development Goal 4 as well as other SDGs. We are confident that our extrapreneurship model which supports much wider impact through shared resources, expertise and networks will enhance the provision of quality education especially for underserved beneficiaries across Africa.”

  0 0


  0 0

   Mtaalamu wa maji wa Shirika la ICS....linalotekeleza mradi wa kusambaza maji safi na salama kwa kutumia teknolojia ya malipo kabla unaofadhiliwa na HDIF akielezea jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.Kushoto ni kiongozi msaidizi wa HDIF  Be.Joseph Manirakiza
   Matanki ya maji yaliyojengwa na ICS kwa ufadhili wa HDIF katika kijiji cha Maganzo yanayosambazwa katika vibanda vya maji 25 vinavyotumia teknolojia ya walipo kabla.
  Wananchi we Maganzo kata ya Kishapu Shinyanga wakielezea muhimu wa mradi wa kusambaza maji safi na salama kwa kutumia teknolojia ya malipo kabla unaofadhiliwa na HDIF .

  0 0

   Naibu Mkurugenzi Mkuu wa CCTV Li Yi (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa ZMCL Muhammed Seif Khatib wakitiliana sainai makubaliano ya ushirikiano baina ya vituo hivyo viwili vya utangazaji katika sherehe zilizofanyika Ofisi za ZMCL Mombasa Mjini Zanzibar.
  Mkurugenzi Mtendaji wa ZMCL Muhammed Seif Khatib akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar Naibu Mkurugenzi Mkuu wa CCTV mara baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano baina ya Taasisi hizo mbili za utangazaji katika sherehe zilizofanyika Ofisini kwao Mombasa Mjini Zanzibar.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZMCL) Muhammed Seif Khatib (kati kati kushoto) akiongoza mazungumzo ya ushirikiano baina ya Shirika hilo na Channel ya Televisheni ya China {CCTV) yaliyofanyika ukumbi wa Shirika hilo Mombasa ambapo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa CCTV Li Yin (wa pili kulia) aliongoza ujumbe kutoka China.
  Mkurugenzi Mtendaji wa ZMCL Muhammed Seif Khatib akiwatembeza watendaji wa CCTV studio za kutangazia za Redio za shirika hilo kabla ya kutiliiana saini makubaliano ya ushirikiano baina ya Taasisi hzo mbili za utangazaji.Picha na Ramadhani Ali Maelezo Zanzibar

  0 0

   kampuni ya The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka mwishoni mwa wiki imeadhimisha miaka 56 ya Uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kawe Beach,Kinondoni jini Dar Es Salaam.

  Akizungumza wakati wa shughuli hizo za usafi,Mratibu wa mawasiliano kutoka kampuni ya The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka ,Kemi Mutahaba amesema kuwa wameamua kufanya usafi kwa kushirikiana na baadhi ya Wadau kwa kujitolea,lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika suala zima la kuboresha usafi wa mazingira yetu.

  "Tumejitolea kufanya usafi katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kawe Beach,lengo likiwa ni kutunza mazingira na kuweka mazingira yetu safi, lakini pia ikiwa sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika suala zima la kuboresha na kuyaweka mazingira yetu kuwa safi wakati wote",alisema Kemi.

  Kemi alisema yote hiyo ni kuhakikisha wanasimamia mlengo wa kampuni yao,waliounzisha katika suala zima la kusaidia kulinda mazingira,ambapo hivi karibuni walichangia kwa kuikabidhi Serikali kiasi cha fedha milioni 100 ili zitumike  katika kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani kupitia mpango maalum ambao Serikali iliishauandaa.

  Amesema kuwa Kampuni yake itaendelea kuunga mkono Serikali kwa kuhakikisha kuwa wanachangia katika shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo mazingira.
  Baadhi ya Wadau na wafanyakazi kutoka kampuni ya
  The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka wakiadhimisha miaka 56 ya Uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira mwishoni mwa wiki katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kawe Beach,Kinondoni jini Dar Es Salaam.
  Baada ya kumaliza kufanya usafi wakafurahi kwa pamoja
  Shughuli ya usafi ilifanyika kwa umakini kuhakikisha eneo la Fukwe linabaki safi.
  Wadau wa Usafi wakijadiliana jambo

older | 1 | .... | 1456 | 1457 | (Page 1458) | 1459 | 1460 | .... | 1897 | newer