Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

HUDUMA YA USAFIRI WA APP YA TAXIFY YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Taxify Kanda ya Afrika Mashariki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa App hiyo leo jijini Dar es salaam. Taxify ni App inayotoa huduma ya Usafiri ambayo inakuwa kwa kasi barani Ulaya na Afrika. App hiyo mpya imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo TZS; Sh 600, TZS 300 kwa kila kilometa moja. TZS 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000. Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka.
 Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Taxify Afrika Mashariki (kulia) na Remmy Eseka, Meneja Uendeshaji wa Taxify Tanzania wakibonyeza vitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma ya Taxify leo jijini Dar es salaam. App hiyo mpya imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo TZS; Sh 600, TZS 300 kwa kila kilometa moja. TZS 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000.
 Nyota wa filamu za bongo, Wema Sepetu (katikati) akijumuika pamoja na Meneja Masoko wa Taxify Afrika Mashariki, Lorreen Ajiambo (kulia) na Meneja Uendeshaji wa Taxify nchini Tanzania, Remmy Eseka kuzindua App mpya ya Taxify inayotoa huduma ya usafiri leo jijini Dar es salaam. App hiyo mpya imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo TZS; Sh 600, TZS 300 kwa kila kilometa moja. TZS 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000.
(Kutokea kushoto) Maafisa wa Taxify, Shivachi Muleji Meneja Maendeleo wa Taxify Kanda ya Afrika Mashariki, Remmy Eseka Meneja Uendeshaji wa Taxify nchini Tanzania na Meneja Masoko wa Taxify Afrika Mashariki, Lorreen Ajiambo kwa pamoja wakimuonyesha Nyota wa filamu za kibongo Wema Sepetu jinsi App hiyo inavyofanya kazi katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. App hiyo mpya imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma yao kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi. Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo TZS; Sh 600, TZS 300 kwa kila kilometa moja. TZS 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 3000.

MAKAMU WA RAIS MH.SAMIA SULUHU ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI KATIKA KILELE CHA SIKU YA MAADILI DESEMBA 10

0
0

 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,George Mkuchika akizungumza na waandishi wa habari juu ya Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasimi katika kilele cha siku ya maadili na haki za binadamu Desemba 10 mwaka huu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere mkoani Dodoma.kulia ni Kamishna wa Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold R.Nsekela. Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,George Mkuchika Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,George Mkuchika akitembelea mabanda mbalimbli katika viwanja vya Mwalimu Nyerere mkoani Dodoma.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Dodoma.

WAGONJWA 80 WENYE MATATIZO YA MOYO KUFANYIWA UPASUAJI WA KUFUNGUA NA BILA KUFUNGUA KIFUA KATIKA KAMBI YA MATIBABU YA MOYO INAYOTARAJIA KUANZA TAREHE 10/12/2017

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza ( wa pili kushoto) pamoja na Madaktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa JKCI na Taasisi ya Little Hearts ya nchini Saudi Arabia. Mhe. Balozi Mgaza alitembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi ya upasuaji wa Moyo kwa watoto na watu wazima inayotarajia kuanza siku ya jumapili tarehe 10/12/2017.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani na Ali Al-Akhfash wa Taasisi ya Little Hearts ya nchini Saudi Arabia mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea JKCI kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi ya upasuaji wa Moyo kwa watoto na watu wazima inayotarajia kuanza siku ya jumapili tarehe 10/12/2017. Jumla ya wagonjwa 80 wanatarajia kufanyiwa upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua katika kambi hiyo.

Picha na JKCI

……………

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Little Hearts ambao wanafadhiliwa na Taasisi ya Al- Murtada ya nchini Saudi Arabia wanatarajia kufanya matibabu ya moyo kwa wagonjwa 80 katika kambi maalum inayotarajia kuanza tarehe 10 – 14/12/2017.

Matibabu yatakayofanyika katika kambi hiyo ni ya upasuaji wa kufungua kifua na upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa watoto na watu wazima.

Leo tarehe 08/12/2017 madaktari bingwa wa Moyo wameanza kufanya uchunguzi kwa wagonjwa wote watakaofanyiwa upasuaji. Katika kambi hii ya siku tano tumepanga kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 30 na upasuaji wa bila kufungua kifua kwa wagonjwa 50. Upasuaji wa kufungua kifua utafanyika zaidi kwa watoto na watu wazima watafanyiwa zaidi upasuaji wa bila kufungua kifua.

Kwa nama ya kipekee tunaishukuru sana Serikali kupitia Balozi wetu wa nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza kwa kutoa kibali cha kuingia nchini (Visa) bila malipo kwa wataalamu wetu hawa ambao wamekuja nchini kutoa matibabu ya moyo bure kwa wagonjwa wetu.

Kama mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama hivyo basi tunaendelea kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya ambao utawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi watakapougua na kuhitaji kupata matibabu.


Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
08/12/2017

MAKAMU WA RAIS AFANYA UZINDUZI WA KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Uzalendo na Utaifa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha muonekano wa kitabu cha Uzalendo na Utaifa mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya Uzalendo na Utaifa uliofanyika jana usiku kwenye ukumbi wa mikutano Chimwaga mkoani Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Uzalendo na Utaifa uliofanyika jana usiku kwenye ukumbi wa mikutano Chimwaga mkoani Dodoma (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Uzalendo na Utaifa kwenye ukumbi wa mikutano Chimwaga, mkoani Dodoma.
 Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Kampeni ya Uzalendo na Utaifa Kwanza katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

SALAMU ZA MIAKA 56 YA UHURU KUTOKA PSPF

0
0

TANESCO yakabidhiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Kwa Mwaka 2016/2017

0
0

Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limekabidhiwa tuzo ya Utunzaji bora wa Mahesabu na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA), baada ya kufanya Vizuri kwenye kada hiyo katika Mwaka wa fedha 2016/2017.

Akipokea tuzo hiyo Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa TANESCO, Bi RENATA NDEGE ameishukuru Bodi ya Wahasibu na wakaguzi (NBAA), kwa kutambua Utendaji Kazi wa Shirika hilo la Ugavi wa umeme hapa Nchini.
" Napenda kuishukuru Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi kwa kuonesha imani katika Utendaji kazi wetu hususani kwenye Kada hii ya Masuala ya Utunzaji wa fedha, Sisi kama Idara tunaahidi Kuimarisha Utendaji Kazi wa TANESCO kwa Kushirikiana na NBAA" alisema Bi RENATA.

Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Fedha katika Shirika la Umeme (TANESCO), wakionekana kufurahia tuzo waliyokabidhiwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu, wameuambia Mtandao wa www.habari360.co.tz kwamba Wataendelea Kuchapa kazi Kwa weledi ili Kulisaidia Shirika Kutimiza Majukumu yake kwa Umma wa Watanzania.
Tuzo hiyo iliyokabidhiwa kwa Idara ya Fedha ya Shirika la Umeme (TANESCO), imeakisi Ubora wa Shirika hilo la Umma katika Utunzaji wa Mahesabu ya Fedha.
 
Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Bi RENATA NDEGE akizungumza na Waandishi wa habari (Hawapo pichani), mara baada ya Kupokea tuzo ya utunzaji Bora wa Mahesabu kutoka Bodi ya wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) katika mwaka wa fedha 2016/2017, Sherehe hizo Zimefanyika Jijini Dar es Saalam.
 
Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Bi RENATA NDEGE, akionesha tuzo ya utunzaji Bora wa Mahesabu aliyokabidhiwa na Bodi ya wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) kwa niaba ya Shirika la umeme, Baada kufanya vizuri kwenye kada ya utunzaji Mahesabu ya fedha kwa Mwaka 2016/2017.
Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Bi RENATA NDEGE, akiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya watumishi katika Idara ya Uhasibu Mara baada ya Kukabidhiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu katika Mwaka wa fedha 2016/2017.
Watumishi katika Idara ya Uhasibu Kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), wakifurahia tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu BAada ya Kukabidhiwa na Bodi ya Wahasibu na wakaguzi wa Mahesabu (NBAA), Sherehe hizo zimefanyika Jijini Dar es Salaam.

“HITILAFU YA UMEME YAUNGUZA BAADHI YA VIFAA OFISI YA ELIMU SEKONDARI JIJI LA TANGA”

0
0
Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoa
wa Tanga,Inspekta Kumenya Bakari akizungmza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji wakitoa
vitu nje kwenye ofisi ya Elimu Sekondari ya Jiji hilo baada ya kuungua kutokana na hitilafu ya umeme .

HITILAFU ya Umeme iliyotokana na mgandamo wa hewa imesababisha ofisi ya Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Tanga kuungua moto ikiwemo baadhi ya vitu vilivyo kuwemo ndani kabla kuzimwa ili usiweze kusambaa kwenye maeneo mengine ndani ya Halmashauri ambao ungeweza
kuleta athari kubwa.

Jitihada za kuufanya moto huo usiweze kusambaa kwenye maeneo mengineulifanywa na watumishi wa halmashauri hiyo  ambao walitumia vifaa vya kuzimia moto huo baada ya kupatiwa elimu ya kupambana na majanga ya
moto.

Akizungumza jana,Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Tanga,Inspekta Kumenya Bakari alithibitisha kuungua kwa ofisi hiyo ambapo alisema tukio hilo lilitokea  Desemba  8 asubuhi  saa tano asubuhi baada ya kupata taarifa kutoka kwa kijana wa boda boda na ndipo walipoamua
kutoka na magari yao.

Alisema pamoja na kupewa taariufa hizo wakiwa wanajiandaa kufika eneo la tukio wakasikia alamu iliyopo ofisini iliwaonyesha kuna moto unawaka eneo la ofisi ya halmashauri na ndipo vijana wakatoka kwa haraka sana pamoja na askari waende kuona na kuchukua hatua ya kuuzima.

Aidha alisema ushupavu wa watumishi hao kuwahi na kuuzima moto huo kwa kuanzia na uzimaji wa swichi kubwa ya umeme inatokana na elimu ambayo walikwisha kuwapatia namna ya kukabiliana na majanga ya namna hiyo pindi yanapotokea kwenye maeneo yao na hivyo kuweza kuuzima mapema.

Naye kwa upande wake,Msaidizi wa Afisa Habari wa Kikosi hicho mkoani Tanga,Sajenti Mussa Msengi alisema baadhi ya vitu ambavyo vimeungua niSimu moja,pazia, Fax  Mashine,Printer,Meza ,Rimu na Nyaraka mbalimbali
zilizokuwemo ndani ya ofisi hiyo.

Akizungumzia tukio hilo, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Alhaj
Mustapha Selebosi alisema baada ya kutokea tukio hilo watakachokifanya hivi sasa ni kurekebisha kutokana na kuwepo kwa vitu vingi ambavyo vimejaa hivyo kunaweza kupelekea matukio ya namna hiyo.

Alisema iwapo wasingekuwa na mitambo yao ya kuzimia moto inaweza kupelekea hasara kubwa kwa kuungua jengo lote.

“Kwanza nishukuru kuwepo kwa mitambo yetu wenyewe ya kuzimia moto hasa yanapojitokeza majanga ya moto ni moja kati ya vitu muhimu vilivyosaidia kukabiliana na janga hili “Alisema.

MBUNGE WA TANGA ASHIRIKI KUUZIMA MOTO.

Awali akizungumza na gazeti hili,Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) AlhajiMussa Mbaruku  alikuwa ni miongoni mwa  watu walioshiriki kwenye zoezi la kuuzima moto huo ili usiweze kuleta madhara katika maeneo megine.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo,Mbunge Mussa alisema ipo haja halmashauri kuongezwe vifaa vya kuzimia moto lakini pia kuwepo na alama ambazo zitakuwa zikitoa ishara wakati yanapojitokeza mambo ya namna hiyo.

"Kwa kweli hali ilikuwa mbaya sana wakati wa tukio hili linatokea kwa sababu na mimi nilikuwepo na nimeshuhudia lakini niseme upo umuhimu mkubwa kuwepo kwa vifaa vya kutosha vya kuzimia moto katika maeneo mbalimbali ya majengo ya serikali kuweza kunusuru na hasara zinazoweza kutokea kama ilivyokuwa leo(jana) tulivyoweza kupambana na moto na
kuuzima "Alisema.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAWAPATIA MAFUNZO YA HUDUMA YA KWANZA MADEREVA WA GARI ZA KUCHUKULIA WAGONJWA (AMBULACE)

0
0
Mkuu wa Usafiri Wizara ya Afya Zanzibar Ali Nassor Juma akitoa maelezo ya mafunzo ya huduma ya kwanza waliyopewa madereva wa magari ya Ambulance yaliyosimamiwa na Chama cha Msalaba Mwekundu (Red Crooss) katika sherehe za kuyafunga mafunzo hayo yaliyochukua wiki moja yaliyofanyika Karakana kuu ya Wizara ya Afya Mombasa, Mjini Zanzibar
Madereva wa gari za Ambualce wakitoa huduma ya kwanza wa majeruhi alievunjika mguu katika sherehe za kukabidhiwa vyeti baada ya kumaliza mafunzo yao yaliyofanyika Karakana kuu ya Wizara ya Afya, Mombasa Mjini Zanzibar.(anaetoa maelekezo) ni Afisa mafunzo kutoka Red Cross Ali Haji Khamis
Madereva waliopatiwa mafunzo wakionyesha njia bora za kumbeba mgonjwa kwa kutumia kiti cha kawaida katika sherehe za kumaliza mafunzo yao na hatimae kukabidhiwa vyeti



Madereva walioshiriki mafunzo ya huduma ya kwanza wakimsikiliza mgeni rasmi Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa Wizara ya Afya Ramadhani Khamis Juma (hayupo pichani)


Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa Wizara ya Afya Ramadhani Khamis Juma akimkabidhi cheti cha kumaliza mafunzo ya huduma ya kwanza dereva Salum Abdall Salum katika sherehe zilizofanyika Mombasa Mjini Zanzibar
Picha na Makame Mshenga.
…………..


Na Ramadhani Ali – Maelezo

Wizara ya Afya Zanzibar imeanza utaratibu wa kuwapatia mafunzo ya huduma ya kwanza madereva wake 43 wa magari ya kuchukulia wagonjwa (Ambulance) yenye lengo la kuwawezesha kusaidia matibabu ya awali kabla ya mgonjwa kumfikisha kwa daktari.

Akizungumza katika sherehe za kuwapa vyeti madereva 12 wa awamu ya kwanza waliomaliza mafunzo yao yaliyofanyika Karakana kuu ya Wizara ya Afya iliyopo Mombasa, chini ya usimamizi wa Red Cross, Mkuu wa Usafiri wa Wizara hiyo Nd. Ali Nassor alisema awamu ya pili ya madereva 11 wa Unguja wataanza mafunzo wiki ijayo na madereva 20 wa Pemba wataanza kupatiwa mafunzo ya huduma ya kwanza tarehe 18 hadi 29 mwezi huu.

Ali Nassor alisema mafunzo hayo yanayosimamiwa na Chama cha Msalaba Mwekundu (Red Cross) yameanza kuonyesha mafanikio makubwa na ameishauri Wizara ya Afya kuyafanya kuwa endelevu.

Aliitaka Wizara kutenga fungu maalumu katika bajeti yake ya kila mwaka kwa ajili ya mafunzo ya madereva na wafanyakazi wa kanda nyengine ambazo hazipewi nafasi kubwa katika suala la mafunzo.

Alisema utaratibu huo utasaidia kuongeza ushirikishwaji wa moja kwa moja wa huduma za afya kwa wafanyakazi wengine wa Wizara hiyo na wananchi wengine katika hatua za awali na hivyo kupunguza ulemavu ambao sio wa lazima kutokea.

Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi katika Wizara ya Afya Ramadhani Khamis Juma ambae alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo alisema suala la mafunzo kwa wafanyakazi wa kada mbali mbali ni muhimu na Wizara itaendelea kutilia mkazo.

Aliwashauri madereva waliopatiwa mafunzo hayo kuyatumia kikamilifu na kuwataka kuwa na tahadhari wanapokuwa wanasafirisha wagonjwa ili isitokee gari lenye mgonjwa linapata ajali.

Mkurugenzi Ali Nassor aliwakumbusha madereva wa Ambulance kuyatumia magari hayo kwa kazi iliyokusudiwa ya kuchukulia wagonjwa na kuwa na kitabu cha safari (Log book) ili kuwa na kumbukumbu sahihi za safari walizokwenda, muda waliotumia na mafuta yaliyotumika.

Madereva hao walionyesha mbinu mbali mbali walizofundishwa za kuwasaidia wagonjwa na majeruhi wakati wa kuwasafirisha kuwapelekea Hospitali na vituo vya afya.

DKT NCHIMBI ASHAURI WAHADZABE WAPEWE AJIRA ZA MUDA KUPITIA TASAF

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na Wahadzabe waliokuwa wakijiandaa kupokea fedha kutoka Mpango wa Tasaf katika kijiji cha Munguli Wilayani Mkalama, Dkt Nchimbi amewatahadharisha kutofanya matumizi mabaya ya fedha hizo.
Walengwa wa Tasaf wa kijiji cha Singa Wilayani Mkalama wakimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (hayupo pichani) alipowatembelea kushuhudia ujenzi wa bwawa walilolijenga katika mpango wa ajira za muda za Tasaf.
Bwawa lililopo katika kijiji cha Singa Wilayani Mkalama lililojengwa na walengwa 246 wa Tasaf katika mpango wa ajira za muda, bwawa hilo linaujazo wa mita 5777.6 ambalo litasaidia upatikanaji wa maji na uanzishwaji wa kilimo cha umwagiliaji, Dkt Nchimbi ameagiza halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kuweka miundombinu ya kunyweshea maji mifugo kutoka katika bwawa hilo.

…………..

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ameshauri Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) uanzishe kazi za ajira za muda, kwa walengwa wa Mpango huo kutoka jamii ya Wahadzabe waliopo Wilayani Mkalama ili uwasaidie kuinua uchumi wao.

Dkt Nchimbi ametoa ushauri huo mara baada ya kutembela kijiji cha Singa Wilayani Mkalama na kuona bwawa litakalotumika kuhifandhi maji ya mvua kwa ajili ya shughuli mbalimbali lililojengwa na walengwa wa Tasaf Kijijini hapo kisha kutembelea kijiji cha Munguli Kata ya Mwangeza Wilayani humo aliposhuhudia malipo ya walengwa wa kihadzabe wa Mpango wa Tasaf.

Ameeleza kuwa jamii ya wahadzabe hawana mradi unaohusisha kazi za ajira za muda ambazo zimekuwa zikisaidia katika kuongeza kipato, kuwafundisha thamani ya kazi pamoja na kutekeleza miradi ambayo imekuwa ikisaidia jamii nzima kama vile mabwawa na barabara.

“Nashauri TASAF kabla ya msimu huu wa mvua kuisha muwaletee na hawa wahadzabe mradi wa ajira za muda kama ambavyo walengwa wa vijiji vingine wamekuwa wakifanya kazi hizo na zimekuwa zikichangia maendeleo kwa vijiji vyao”, ameeleza na kuongeza kuwa,

“Miradi ya ajira za muda zitawafundisha Wahadzabe kujituma kufanya kazi ambazo zinachangia maendeleo ya jamii huku kazi hizi zikiwa kama darasa la wao kujifunza kwa vitendo kuwa kama anaweza kwa mfano kushiriki kujenga bwawa basi anaweza kufanya jambo kubwa katika familia au maisha yake”, amesisitiza Dkt Nchimbi.

Aidha ametoa tahadhari kwa walengwa hao wa kihadzabe kuwa wasitumie pesa wanayopewa kwa kunywa pombe badala yake pesa hiyo itumike sawasawa na maelekezo ya mpango huo na hatua zichukuliwe kwa wale watakaokaidi.

Kwa upande wake Afisa Ufuatiliaji Kutoka Tasaf Makao Makuu Anna Njau ambaye aliambatana na Mkuu wa Mkoa Dkt Nchimbi katika ziara yake ameeleza kuwa ushauri huo ni mzuri na una lengo la kuwasaidia wananchi kama ambavyo Tasaf imekuwa na lengo la kuinua jamii hasa kaya masikini hivyo wazo hilo ataliwasilisha makao makuu kwa ajili ya utekelezaji.

Baadhi ya wahadzabe waliofika kupokea fedha za Mpango wa Tasaf wameeleza kuwa fedha hizo zimewasaidia kuwainua kiuchumi kwa kuhakikisha wana chakula cha kutosha, watoto wameenda shule, watoto wadogo wamepelekwa kliniki huku wakijiendeleza zaidi kiuchumi kwa ufugaji mdogo wa kuku na mbuzi pamoja na kuboresha makazi yao.

Jamii ya Wahadzabe waliopo Kijiji cha Munguli na hasa kitongoji cha Kipamba Wilayani Mkalama wamekuwa wakiishi kwa kutegemea uwindaji wa wanyama pori, kula asali, ubuyu, matunda na mizizi mbalimbali ambapo juhudi za Serikali kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (Tasaf) umesaidia jamii hiyo kuanza kupeleka watoto shule, kuanzisha shughuli za uzalishaji mali kama vile kilimo na ufugaji.

MIAKA 56 YA UHURU:RAIS MAGUFULI AELEZA MAFANIKIO YA SERIKALI.

0
0

MAADHIMISHO YA MIAKA 56 YA UHURU YALETA NEEMA KWA FAMILIA YA BABU SEYA, NI BAADA YA RAIS MAGUFULI KUTOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiingia kwa gari maalum akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambako ndiyo makao makuu ya Nchi. 

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ,Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa dini pamoja na wananchi wa viunga vya mji wa Dodoma, Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia amemsamehe Nguza Viking "Babu Seya" na Mwanaye Johnson Nguza "Papii Kocha" waliokuwa wamefungwa Kifungo cha Maisha Gerezani.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA)
24
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride huku akiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
567
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea jukwaa kuu mara baada ya kukagua gwaride huku akiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mh.Jenista Mhagama Waziri Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu baada ya kukagua gwaride katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
9
Picha mbalimbali zikionyesha Vikosi vya Ulinzi vikitoa heshima kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Uinzi wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
3
1011121314
Kikosi cha Makomandoo wa Jeshi la Ulinzi JWTZ kikipita kwa Gwaride la heshima mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
1516
Baadhi ya wananchi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho hayo wakiwa jukwaa kuu.
18
Makomandoo wakionyesha onyesho lao la kuokoa kiongozi aliyetekwa kwa kushuka na Helkopta ya kijeshi.
20
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

DOKTA MPANGO AWASHAURI WAKANDARASI KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI KATIKA SEKTA YA UJENZI

0
0
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amekagua ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu-NBS mjini Dodoma na kutoa wito kwa wakandarasi wanaojenga miundombinu mbalimbali yakiwemo majengo kutumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini ili kuongeza mapato ya Serikali na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Amesema hayo baada ya kushuhudia mkandarasi anayejenga jengo hilo Hainan International Ltd ya China, akitumia vifaa mbalimbali vya ujenzi vinavyopatikana hapa nchini zikiwemo mbao na vifaa vya umeme, hatua ambayo amesema inachangia kuwaongezea kipato wananchi.

Akizungumzia ujenzi huo, Dkt. Mpango amesema jengo hilo litatumika ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa kwakuwa litatumika kuchakata takwimu mbalimbali zitakazotumika katika kutunga sera na mipango mbalimbali ya kuendeleza nchi.

“Huwezi kupanga mipango yoyote bila kuwa na takwimu nzuri na bora, hapa ndipo vile “vichwa” vyetu vya takwimu nchini vitachakata takwimu hizo ndipo zitumike katika kutunga sera bora kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu” Alisistiza Dkt. Mpango
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), akitoa maelekezo wakati alipokagua ujenzi wa Jengo la ghorofa 5 la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, kulia kwake ni  Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa na kushoto kwake ni Mhandisi Mshauri Bw. Abdulkarim Msuya.
 Mhandisi Mshauri na Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, Mhandisi Abdulkarim Msuya (kulia) akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipotembelea ili kukagua ujenzi wa Jengo hilo ambalo litagharimu shilingi bilioni 11.6.
 Mhandisi Mshauri na Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, Mhandisi Abdulkarim Msuya akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipotembelea ili kukagua ujenzi wa Jengo hilo ambalo litagharimu shilingi bilioni 11.6.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa, (wa tano kulia) mjini Dodoma.

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA MIAKA 56 YA UHURU MJINI DODOMA LEO

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi wakati akiwasili kuongoza  sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli na Mama Mwanamema Shein kwenye sherehe hizo
 Marais Wastaafu Mhe Benjamin Mkapa na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakiteta jambo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017.
 Viongozi mbalimbali katika Jukwaa kuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017. Picha na Ikulu

-RAIS MAGUFULI AWASAMEHE WAFUNGWA 8157

0
0

Rais Magufuli Asamehe Wafungwa 8157

0
0
Na Lilian Lundo na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesamehe jumla ya wafungwa 8,157 katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri, Mjini Dodoma.

Msamaha huo umehusisha wafungwa 1828 ambao watatolewa kaunzia leo na wengine 6329 wamepunguziwa muda wa vifungo vyao, aidha kati ya wafungwa watakaoachiwa huru wafungwa 61 ni wafungwa ambao walihukumiwa kunyongwa.

“Kuna wafungwa ambao wamehukumiwa kunyongwa wana umri wa miaka 85 na wapo waliokaa gerezani zaidi miaka ya miaka 45, ambao wametubu na kukiri makosa na wapo ambao hawakuwauwa maalbino wala hawakuwa majambazi,” amesema Dkt. Magufuli.

Dkt. Magufuli ametoa mfano wa mfungwa anayejulikana kama Mganga Matonya mwenye umri wa miaka 85 yupo kwenye orodha ya wafungwa watakaoachiwa huru leo ambapo amekaa gerezani kwa miaka 37 na mahabusu miaka saba (7) kabla hajahukumiwa.

Katika hatua hiyo, Rais Dkt. Magufuli amewaachia huru Nguza Viking na Johson Nguza (Papii Kocha) waliohukumiwa kifungo cha maisha.

Aidha Mhe. Rais amesema kuwa msamaha huo alioutoa leo umetokana na mamlaka aliyonayo kutoka kwenye Ibara ya 45 (a) (b) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayomruhusu Mhe. Rais kutoa msamaha, kumuachia huru, kubadilisha adhabu au kufuta adhabu kwa mtu yoyote aliyehukumiwa kwa kosa lolote.

Wakati huo huo, Rais Magufuli ametoa wito kwa watanzania wote kuenzi na kudumisha tunu na amani zilizoachwa na waasisi wa Taifa.

Aidha, Rais Magufuli ameeleza kuwa tangu nchi ipate uhuru kumekuwa na maendeleo katika nyanza mbalimbali ikiwemo barabara, madaraja, vituo vya afya, shule za msingi na shule za sekondari.

“Wakati nchi inapata uhuru kulikuwa na jumla ya kilometa 32,600 za barabara ambapo kilometa 1360 zilikuwa katika kiwango cha lami, lakini mpaka sasa nchi inapotimiza miaka 56 ya uhuru kuna jumla ya kilometa 122,500 za barabara ambapo kati ya hizo kilometa 12,679.55 zipo katika kiwango cha lami, kilometa 2,480 zinaendelea kujengwa katika kiwango cha lami na kilometa 7087 zipo kwenye hatua mbalimbali za maandalizi za kujengwa katika kiwango cha lami” anasema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa, Mfalme wa Morroco amemtuma Spika wa nchi hiyo kuja kuangalia eneo litakalojengwa uwanja mkubwa wa Kimataifa Mkoa wa Dodoma ambapo unatarajiwa kuwekwa jiwe la msingi mwezi Machi au Aprili mwaka 2018.

Mbali na hayo Sherehe hizo zilipambwa na gwaride kutoka Majeshi ya Tanzania, onesho la kikundi cha Komando, onesho la gwaride la Uzalendo la wanafunzi, vikundi mbalimbali vya kwaya, ngoma za alisi na Tanzania Allstars.

RC MAKONDA ATOA RUNINGA 69 KWA MAGEREZA NA HOSPITAL ZA DAR, AJUMUIKA NA WAFUNGWA KWENYE CHAKULA CHA PAMOJA

0
0

Mkoa wa Dar es Salaam umeadhimisha Siku ya Uhuru kwa Kuwatembelea Wafungwa na Maabusu kisha kupata Chakula cha Pamoja na kutoa huduma ya Masaada wa Kisheria na Ushauri na Saha kwa Wafungwa na Mahabusu.

Katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA ametoa Msaada wa Runinga za Kisasa 69  (Flat Screen) Touch zenye ukubwa wa Inch 40 kwa Magereza na Hospital zote za Dar es Salaam kuwezesha Wafungwa na Wagonjwa kupata haki ya kikatiba ya kupata Habari.

Hii ni Historia kwa Dar es salaam kuwa Mkoa wa kipekee wenye Runinga Magerezani zinazowawezesha Wafungwa na Mahabusu kupata Habari na Hotuba za Rais ili kuwapunguzia Msongo wa Mawazo ili wasiwe na Mawazo ya kujiua ambapo zitagawanywa kwenye Magereza ya Segerea, Keko na Ukonga. 

RC MAKONDA aliongozana na Viongozi wa Dini waliowafariji Wafungwa na Kuwafanyia Sala na Dua huku Watu wa Ustawi wa Jamii wakitoa Msaada wa Ushau na Saha kwa Wafungwa.

MAKONDA ambae amepokelewa kwa Furaha kubwa na Wafungwa wa Gereza hilo amewasihi *kutokata Tamaa kwakuwa bado wanayo nafasi ya kutimiza ndoto zao baada ya kumaliza kifungo ambapo amewahimiza kuwa Mabalozi Wazuri kwa Jamii.

Ili kupunguza msongamano wa Mahabusu Gerezani RC MAKONDA amesaidia zaidi ya Mahabusu na Wafungwa 200 wa Gereza la Segerea kupata  Msaada wa Sheria ambao walikuwa hawana uwezo kifedha.

Aidha MAKONDA ametoa Magodoro 100, Vifaa vya Usafi na Sabuni za Kuoga na Kufua kwa Wafungwa na Mahabusu.

Baadhi ya Maabusu na Wafungwa wamemshukuru RC MAKONDA kwa kuwa kiongozi wa Kwanza na wa pekee aliewatembelea na kupata chakula cha pamoja, kuwapatia Runinga, kusikiliza changamoto zao na kuwapatia Wanasheria na watu wa Ustawi wa Jamii kitendo kilichowafariji.

Aidha Wameshukuru pia kitendo cha RC MAKONDA kusikiliza Changamoto zao na kuzipatia majibu ambapo wamemuahidi kuwa wamebadilika na watakuwa mabalozi wazuri kuhimiza jamii kuzingatia Sheria.






Kauli mbiu ya “Nchi Yangu Kwanza” Imebeba Dhana Kubwa Kwa Taifa Letu-Mhe. Samia Suluhu Hassan

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Uzalendo na Utaifa uliofanyika jana usiku kwenye ukumbi wa mikutano Chimwaga mkoani Dodoma
Na Lorietha Laurence – WHUSM, Dodoma.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Kauli mbiu ya _”Nchi yangu Kwanza”_ya  kampeni ya Uzalendo na Utaifa imebeba dhana kubwa kwa taifa letu.
Mhe. Samia ameyasema hayo leo Mkoani Dodoma alipokuwa akizindua kampeni ya Uzalendo na Utaifa iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo yenye lengo la kukumbusha na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuwa wazalendo.
“Kampeni hii ni muhimu sana katika kuwakumbusha watanzania maana ya uzalendo na umuhimu wa kuudumisha kwa maslahi ya nchi yetu na kizazi kijacho” alisema Mhe. Samia.
Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ni kielelezo tosha cha uzalendo kwa namna anavyoyapigania maslahi ya nchi kwa kupiga vita rushwa na matumizi mabaya ya rasilimali ya nchi.
Vilevile Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.  Mwakyembe kuunda kamati ndogo za kitaifa zitazozunguka nchi nzima kuhamasisha uzalendo.
Naye Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein ametoa maana ya uzalendo kuwa ni kitendo au hulka ya binadamu kuwa mstari wa mbele kuitetea nchi yake ili kuleta maendeleo.
“Lazima tujitathimini kama kweli tuna uzalendo ndani yetu,  je tupo tayari kusimama na kutetea maslahi ya nchi yetu ” alisema Dkt. Shein.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Mwakyembe aliwashukuru viongozi wa Serikali kwa kuitikia wito na kuunga mkono kampeni hiyo muhimu kwa maslahi ya nchi.
Pia, Dkt. mwakyembe aliahidi kushirikiana na Wizara ya Habari, Utalii Utamaduni   na Michezo ya Zanzibar kuhakikisha kampeni  hiyo inafanyika kwa  kuwawenzi waasisi na wazalendo wa taifa la Tanzania ambao ni Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Shekhe. Abeid Amani Karume.
Mbali na hayo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge ameishukuru Serikali ya Awamu ya tano kuona umuhimu wa kufanyia matukio makubwa ya kiserikali katika Mkoa wa Dodoma na kueleza  kuwa kitendo hicho ni uzalendo wa hali ya juu.

MAKAMU WA RAIS AFUNGA MKUTANO MKUU WA TISA WA UWT

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akihutubia wakati wa kufunga mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania Ndugu Gaudensia Kabaka baada ya kutangazwa mshindi katika mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma ambapo aliwasihi uchaguzi umeisha waimarishe Jumuiya hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akimpongeza Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania Ndugu Gaudensia Kabaka katika mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma ambapo aliwasihi uchaguzi umeisha waimarishe Jumuiya hiyo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akiwapungia mkono wajumbe wakati wa kufunga mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akiwahutubia wajumbe wakati wa kufunga mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania Ndugu Gaudensia Kabaka akihutuba baada ya kuchaguliwa katika mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea waliogombea nafasi ya Uenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania katika mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma ambapo aliwasihi uchaguzi umeisha waimarishe Jumuiya hiyo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
…………………………………………………………………………..


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi waliochaguliwa kuongoza kwa kuzingatia Katiba, Kanuni za UWT, CCM na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Jakaya Kikwete.

Makamu wa Rais aliwasihi viongozi hao kuvunja makundi ya kampeni nwaliyokuwa nayo na kujenga Umoja na Mshikamano ndani ya Jumuiya na Chama.

Makamu wa Rais alisisitiza kufanya kazi kwa umoja, mshikamano na kwa uzalendo “Kushinda kuwa Kiongozi haina maana unajua yote, tuwe tayari kukosoana lakini tusisingiziane”

Makamu wa Rais aliwakumbusha Viongozi hao kuhakikisha Jumuiya inashiriki kikamilifu katika kuandaa mazingira mazuri ya ushindi wa CCM katika chaguzi za Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020.

Makamu wa Rais alisema Viongozi waliochaguliwa wanajukumu kubwa la kujenga Jumuiya imara kwa kuitoa hapo ilipo na kuipeleka mbele ikiwa na kuongeza wanachama wapya kutoka katika makundi mbali mbali.

Mkutano Mkuu wa Tisa wa UWT ulifunguliwa jana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kufungwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo ulifanyika uchaguzi na Mhe. Gaudensia Kabaka alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Wanawake Tanzania na Bi. Thuwayba Kisasi alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMAPILI LEO DECEMBER 10,2017

0
0

SERIKALI KUFANYA MAPITIO YA MIRADI YA MAJI KUANZIA MWAKA

0
0
Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe. Joseph G.Kakunda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Arusha, wilaya ya Longido, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Haki kazi Catalyst wa mjini Arusha
Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe. Joseph G.Kakunda akitoa maelekezo kwa watendaji wa maji katika mradi wa maji wilayani Longido
Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe. Joseph G.Kakunda akikagua mradi wa maji wilayani Longido
Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe. Joseph G.Kakunda akipanda kwenye tanki la maji linalojengwa katika mradi wa maji wilayani Longido
Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe. Joseph G.Kakunda akipiga picha na akina mama na watoto wakati waziara yake ya kukagua mradi wa maji wilayani Longido.


Serikali imewaagiza Wahandisi wa maji kuhakikisha wanasimamia miradi ya sekta ya maji nchini inayozingatia thamani ya shilingi na yenye kuleta tija kwa Watanzania.

Akiongea katika ziara yake mkoani Arusha katika wilaya ya Longido Mhe. Joseph George Kakunda, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, amesema kumekuwepo na ufujaji wa fedha za katika Miradi ya maji nchini na mara nyingi imekuwa sio endelevu na yenye kuleta hasara kubwa kwa Taifa.

“Wahandisi hakikisheni mnasimamia utekelezaji wa miradi ya maji kwa thamani ya shilingi, wale wote wanaojenga miradi hiyo muwasimamie vizuri, fedha tunazozikopa hakikisheni mnazitumia vizuri, acheni kupokea rushwa, nataka kuona Wahandisi wanajenga mradi kwa maslai ya watu wa Longido ili kuondoa kero za maji, zingatieni taratibu, kanuni na sheria ili tupate tunachostahili” 

Mhe. Kakunda amewataka Watendaji na Wahandisi kufanya mapitio ya miradi ya maji nchini ili kuona miradi iliyotekelezwa kwa halali na pia ili iliyotekelezwa kwa wizi ionekane. “haiwezekani tangu tuanzishe Programu ya Maji Vijijini tumekwisha tumia zaidi ya shilingi trilioni 1.6lakini bado kila sehemu kuna shida ya majikwa nini kila mradi una maisha yake kama miaka 10, 15, 20, 25 hili haliwezekani, hatuwezi kwenda namna hiyo, mimi nitapendekekeza tufanya mapitio ya miradi yote ya maji iliyojengwa hasa kuanzia mwaka 2008. Kwanini watu wa kawaida wanajenga mradi mkubwa kutoka kwenye chanzo hadi hapa”

Akiwa kijijini Elondeka, Mhe. Kakunda amepongeza hatua zilizofikiwa za Mradi wa maji unaotekelezwa na Mradi wa Tabia nchi (DCFP)ambao umegharimu kidogo cha fedha shilingi milioni 36 na kushauri wananchi kuulinda siku zote. Pia alikagua mradi wa maji unaotekelezwa na Halmashauri ya wilaya Longido ambao bado haujakamilika.

Akisoma taarifa ya mradi mbelel ya Mheshimiwa Naibu Waziri Kakunda, Mtesigwa Missana ambaye ni Afisa Tarafa Longido amesema kuongezeka kwa kutotabilika kwa tabia ya hali ya hewa yanazidisha changamoto kama vile kubadilisha mtindo wa maisha ya wananchi.

Aidha, Mhe. Kakunda amewaasa wananchi kuulinda mradi wao waliouchagua wenyewe, “toeni ushirikiano kwa mradi huu kwa sababu mmeuchagua wenyewe, lindeni sana mradi huu ili uweze kuhudumia ninyi wenyewe na mifugo, mradi huu una faida kwenu ninyi, mifugo na wanyama wa porini”

Wananchi walibuni Mradi wa tanki la maji lenye ujazo wa mita 50,000 unaotekelezwa na Mkandarasi J.J.Gwakisa ambao upo katika hatua za mwishoni. Mradi wa huo wa maji unaopata maji toka katika bomba lililotoka kwenye chanzo naotarajiwa kuhudumia watu 4,814 kwa mujibu wa takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Njungolo amesema wilaya ya Longido inakabiliwa na changamoto ya kuwa na watumishi wengi wanaokaimu na kufanya maamuzi yao kuwa sio ya kuridhisha na pia sekta ya afya imekumbwa na uhaba mkubwa wa watumishi na kuathiri kabisa utolewaji wa huduma ya afya wilayani humo kwani zaidi ya asilimia 15 ya watumishi wa sekta hiyo waliondolewa katika zoezi la vyeti bandia.

Mheshimiwa Kakunda anaendelea na ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kujionea hali ya utendaji na kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo shule, miradi ya maendeleo na miradi ya tabianchi Mkoani Arusha.
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images