Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 143 | 144 | (Page 145) | 146 | 147 | .... | 1897 | newer

  0 0
 • 08/20/13--22:55: JIUNGE NA FLATBELLY TANZANIA
 •             Neema  Herbalist  & Nutritional  Foods  Clinic  kwa  ushirikiano  mkubwa  na  Taasisi  ya  Flatbelly  Tanzania  wamedhamiria   kuwasaidia  wadada  kwa  wakaka  wanao  taka  kutengeneza  shape  za matumbo  yao   kwa  kuyafanya  kuwa  flat pamoja  na  watu  wote  wenye  nia  ya  kuondoa  vitambi  vyao, kupunguza  unene  na  uzito   kwa  njia  ya  tibalishe  na  mazoezi,  kuhakikisha  wanafikia  malengo  yao. 

  Hili  litafanyika  kupitia  mradi  wa    Flatbelly   Project  unao  ratibiwa  na  Neema  Herbalist  kwa  kushirikiana  na    Flatbelly  Tanzania.
  Programu   hii  inafanyika  kwa  lengo  la  kusogeza  huduma  zetu  kwa  wananchi  walio  wengi    kwa  urahisi  na  ukaribu  zaidi.  Kupitia  program  hii, tutahakikisha  kuwa, kila  memba  anaye  jiunga  na  program  anaya  fikia  malengo  yake   kwa  asilimia  mia  moja. 

   Tutakuwa   tukiweka  picha  za    memba  kabla  na  baada  ya  kujiunga  na  program  ili  kuwaonyesha  watanzania  ni  kwa  namna  gani  tumedhamiria  kuimarisha  afya  za  watanzania  kupitia  program  hii. Gharama  za  kujiunga  na  programu  hii  ni  rahisi  sana  na  mtanzania  wa  rika  lolote  lile  anaweza  kujiunga. 
  Unapo chukua  uamuzi  wa  kuja kujiunga  na  programu  hii, unapaswa  kuwa  na  uhakika   kwamba   utayafikia  malengo  yako  kwa  asilimia  mia  moja.
   Kwa  wewe  unayetaka  kujiunga  na  program  hii, fika  katika  ofisi  zetu  zilizopo  jijini  Dar  Es  salaam, katika  eneo  la  Changanyikeni, karibu  na  Chuo  Cha  Takwimu, au  tuandikie  barua  pepe :neemaherbalist@gmail.com  au   tupigie   0766538384.
  Kauli  mbiu  ya   program  hii  ni 
             “ FLATBELLY  IS  SEXY!
  Kwa  maelezo  zaidi, tembelea 

  0 0

  IMG_3248

  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jinsi waandaaji wa vipindi wanavyoweza kutafuta habari nzuri zenye kuelimisha kwa ajili ya redio za jamii na pia mbinu wanazoweza kutumia ili kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii.

  Akizungumza katika warsha ya siku nne inayoshirikisha waandishi na maripota wa redio za jamii inayofanyika Wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Bi. Ledama ameongeza kuwa upo umuhimu wa kuwajengea uweze watendaji katika redio hizo ikiwemo kuwafundisha namna ya kutumia mtandao wa Intaneti kwa ajili ya kuboresha uandishi na utangazaji , haswa katika maeneo muhimu yanayoigusa jamii ikiwemo Elimu, Afya na Kilimo na pia jinsi redio hizo zinavyoweza kuandaa vipindi vitakavyoigusa jamii moja kwa moja.

  Kwa jumla warsha hiyo ya siku nne kwa waandishi wa habari wa redio za jamii imeangalia kwa mapana mambo muhimu ya kijamii, na kuchambua mambo hayo ni yapi ambapo imegusia masuala ya Afya na Kilimo pamoja na mambo mengine na kuangali fursa zinazopatikana, pia changamoto zinazokabili masuala hayo na kutathmini nini kifanyike ili kuboresha utendaji na utoaji huduma katika sekta hizo.
  IMG_3079
  Mtaalam wa Kilimo kutoka Idara ya Kilimo wilayani Sengerema Bw. Joseph Manota akizungumza katika warsha ya waandishi wa habari wa redio za jamii inayofanyika mkoani Mwanza ambapo fursa zinazopatikana katika sekta ya Kilimo na jinsi ya kuzitumia ili kufanikisha sera ya Serikali ya Kilimo Kwanza na pia amezungumzia changamoto zilizopo katika kutimiza sera hiyo na namna gani maafisa wa Kilimo pamoja na Serikali kwa ujumla wanaweza wakafanya kukabiliana nazo ili kutimiza malengo ya kukuza Kilimo.
  IMG_3223
  Mshauri wa redio za jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
  IMG_3191
  Pichani juu na chini ni waandishi na maripota wa redio za jamii wanaohurudhuria mafunzo hayo yanayofanyika kwenyen kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre Wilayani Sengerema mkoani Mwanza.


  IMG_2996IMG_3295
  Mwezeshaji kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mtaifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akionyesha baadhi ya machapisho ya Umoja wa Mataifa ambayo yatawasaidia katika kuandika habari zao kiufasaha.
  IMG_3043
  Mmoja wa watangazaji wa Redio Kahama FM William Bundala (Kijukuu cha Bibi K) akitoa mrejesho wa mafunzo yaliyopita ambayo yameleta mabadiliko makubwa kwa kituo chao kwa Mshauri wa Redio za Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu
  IMG_3226
  Afisa Elimu, Takwimu na Vifaa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Pius Lwamimi akizungumza na waandishi wa habari na maripota wa redio za jamii nchini ambapo aligusia changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta Elimu wilayani humo na kuwaasa kutumia redio zao katika kutoa taarifa muhimu kwa jamii zitakazopelekea kukua kwa Sekta ya Elimu nchini. Pia amewataka wazazi kuwa mstari wa mbele na kujitokeza kuhudhuria vikao katika shule na kutoa maoni yao kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo mitaala ya elimu na pia kushirikiana na redio za jamii kwa kutoa taarifa muhimu na pia kuwahamasisha watoto wao na jamii nzima kujenga utamaduni wa kusikiliza vipindi vya redio hizo kwa manufaa yao.
  IMG_3205
  Sehemu ya washiriki wanaohudhuria mafunzo hayo.

  0 0

   Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.


  BINADAMU anazidi kuandamwa na mabalaa mengi, yakiwamo mabaduliko ya tabia nchi yanayosababishwa na uchafuzi wa mazingira sehemu mbalimbali duniani.


  Uzalishaji viwandani na ukataji wa miti usiozingatia utamaduni wa kutunza mazingira yanasababisha mkanganyiko mkubwa duniani. Kama hivyo ndivyo, walau sasa kunahitaji maandalizi ya kutosha. Kinyume na hapo, Tanzania kama moja ya nchi zinazoathiriwa na suala hilo, itajiweka katika mazingira magumu.

  Jamii ya Tanzania na Serikali kwa ujumla inahitaji kuliangalia hilo kwa mapana, ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira ili iwe chanzo cha watu kuishi katika Dunia salama. Bila kuzingatia hilo, hata wakulima wetu wa Tanzania hawawezi kuishi maisha bora ukizimngatia kuwa mazao yao mengi yanashindwa kustawi kutokana na ukosefu wa mvua au kunyesha bila mpango.

  Tanzania inaamini kuwa uchimi wake ili ukuwe kunahitajika juhudi za wakulima wetu waliosambaa kwenye mikoa mbalimbali. Je, Watanzania wangapi wanamasika katika kujishughulisha na kilimo? Je, ni vijana wangapi wanajiingiza kwenye sekta hiyo iliyopewa jina la uti wa mgongo?

  Hayo yanasababisha watu wengi kuona hawawezi kuishi bila kufanya kazi za kuajiriwa, ikiwa ni tofauti na uzalishaji mali kwa kupitia sekta ya kilimo yenye changamoto mbalimbali. Wanafanya hivyo bila kujua kuwa sekta ya kilimo ndio inayoweza kutoa nafasi nyingi za ajira, tofauti na fikra za waliokuwa wengi.

  Mbali na kujiongezea kipato kwa kujiingiza kwenye kilimo, pia tunaweza kujiweka kando na baa la njaa kwa kuhakikisha kwamba tunakuwa na akiba ya kutosha, tofauti na sasa kila wakati kusikia habari mbaya zinazohusu njaa kwa vijiji na wilaya mbalimbali za Tanzania. Njaa barani Afrika ni tatizo kubwa. Ndio maana  Nchi nane tajiri duniani, maarufu kama G-8, zimekuwa zikifanya mikutano ya kila wakati kujadili namna ya kupambana na hilo.

  Katika mikutano hiyo, nchi ya Tanzania ni miongoni mwa zile zinazojadiliwa mara kwa mara kwa ajili ya kupewa misaada, ambapo hata hivyo sio jambo geni kutokana na viongozi wake kuona hilo ni jambo la maana kwao. Pamoja na misaada hiyo inayotolewa mara kwa mara kutoka kwenye mashirika ya Kimataifa au serikali, ila ni vipi tunaweza kufanya kazi hiyo kwa unafanisi kwa ajili ya kuboresha maisha yetu?

  Hii ni kwasababu baadhi ya viongozi wengi wa Tanzania ni wasemaji wasiozingatia vitendo katika harakati zao. Tunaishi kwa ahadi. Tutafanya hivi na kufanya lile, ila hakuna kitu. Ndio maana hata kwenye kujikita katika suala la kilimo bado hatuna jipya.


  Mipango yetu mingi inaishia kwenye makaratasi. Kwa miaka 51 ya uhuru, kumekuwa na mipango mingi ingawa yote haina matunda. Hadi leo, bado hatuwezi hata kujiendesha wenyewe.  Serikali pia inashindwa kuwaongoza wakulima kama inavyotakiwa sambamba na kuwapatia pembejeo za kilimo, kuwa karibu nao kila wakati, hasa wakati wa majanga ya wadudu kushambulia mazao yao.

  Suala hili ni kati ya changamoto nyingi zinazoongeza joto la ugumu wa maisha, maana wote wanakosa akiba ya chakula cha kujikimu wao na familia zao sambamba na kuuzwa nje. Mwaka 2008, Serikali na wafanyabishara waliweza kukaa na kuliangalia hilo suala la kilimo. Lakini mpango wa kuendeleza kilimo, naweza kusema kwamba haukufanikiwa kwa vitendo.

  Kitendo cha kukaa pamoja, ni kuonyesha kwamba wanatambua changamoto za kilimo, lakini ajabu ni maoni yao yanavyoishia kwenye karatasi. Hii ni mbaya na ndio sababu ya nchi inakwenda ndivyo sivyo na hakuna mipango ya kuinusuru zaidi ya kusubiria hisani kutoka kwa wengine. Nchi sasa inaendeshwa kwa hisani ya watu fulani. Tumekubali kuwa watu wa misaada kutoka kwa wanaojiweza. Tukiliangalia hili, kila mtu ataelekeza lawama zake kwa serikali, ambayo kwa bahati mbaya ipo chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Hapo tutasema na kujikuta kuamini kumbe tatizo ni serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete. Hawa wameshindwa kabisa kutuletea maisha bora kwa kila Mtanzania. Na wameshindwa walau kuwasimamia na kuwaendeleza wakulima ili kazi zao zikuze uchumi wa Taifa lao. Nao wanufaike ili waone kazi hiyo ni nzuri.


  Wameshindwa hata kusimamia sera ya kilimo kwanza walioasisi kwa mbwembwe nyingi. Pamoja na yote hayo, je Watanzania nao wamekubali kukaa na kusubiria ahadi za serikali? Watu wa aina hiyo wapo wengi katika jamii. Wanalalama sana. Hata hivyo, wale ambao pamoja na kukabiriwa na changamoto za aina hiyo lakini wanajihusisha na kilimo hoja wanayo.

  Ni wakati wa kukaa chini na kuamua sasa tufanye kazi za kweli kwa ajili ya kuinua uchumi wa Taifa letu, ikiwamo changamoto zinazowasumbua wakulima wetu ziweze kufanyiwa kazi.  Kama serikali inashindwa kuwakopesha wakulima walau kiasi kidogo cha pesa, tunawezaje kuwaongezea morali wa kufanya kazi?


  Hii vita ya tatu ya Dunia ambayo ni maji na chakula, hakika kwa sisi Watanzania, upo uwezekano wa kutuangamiza. Maana wenyewe hatuna na mipango wala uelewa wa kujiingiza kwenye kilimo. Katika sekta hiyo kuna matatizo mengi mno.

  Zipo sehemu zilizokumbwa na migogoro mikubwa ya wakulima wakubwa na wadogo. Hilo linapaswa kuangaliwa upya kwa ajili ya kuhakikisha tunainua uchumi wetu. Bila hivyo vita ya umasikini ama maisha bora kwa kila Mtanzania ni ndoto. Hatuwezi kusonga mbele kama hatuna mipango endelevu ya utendaji kazi kwa vitendo na sio porojo na hadithi.

  Tufanye kazi kwa nguvu zote ili tuweze kukwamua uchumi wetu kwa kupitia sera ya kilimo. Kilimo kinachoweza kufanywa na kila mmoja wetu na sio kukaa na kusubiri hisani ya Wamarekani kama tulivyozea. Hapa sina lengo la kulaumu upande wowote, maana mambo hayo licha ya kushamiri sana, ila hayajaweza kutusaidia. Malalamiko ya wapinzani bado sio suluhu la kuwapatia maisha bora kwa Mtanzania kama wote hatuna uthubutu katika utendaji wa kazi.

  Tunahitaji moyo wa uzalendo, ushirikiano kwa ujumla, maana ndio mbeleko ya kutuweka katika nafasi nzuri na kuacha kasumba zisizokuwa na mpango wowote ule. Huo ndio ukweli wa mambo. Kuna mengi yametufanya tushindwe kusonga mbele, ikiwa ni pamoja na kutojua makosa yetu, hasa kuachia sekta muhimu kama kilimo kuendeshwa kienyeji.

  Suala kama hilo tusipokuwa makini nalo basi hakuna tutakachoweza zaidi ya kusubiria hisani ya Wazungu. Na bado tujiandae kusubiria chakula kutoka kwao, wakati Tanzania ina ardhi kubwa yenye rutuba. Hakuna tutakachopata zaidi ya aibu, maana licha ya kuzunguukwa na mapori kila mahali, kama vile Tanga, Rukwa, Morogoro, Mbeya, Iringa na mikoa mingine ila hatuwezi kuitumia ipasavyo.

  Suala la kilimo linahitaji mkazo na watu wote bila kuangalia nafasi zao kwenye jamii ili tija kwao. Kila Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa, lazima ahakikishe kwamba katika eneo lake, wananchi wake wanatembelewa na kusaidiwa katika kazi zao za kilimo.

  Pale wakulima wanapovamiwa na wadudu hatarishi, Serikali iwasaidie kwa kuwanunulia dawa, pembejeo za kilimo na sio kuwaangalia tu, maana huo sio mtindo utakaonusuru sekta ya kilimo. Tukiweza kufanya hivyo, sio tu tutakuwa na akiba ya chakula, bali pia tunaweza kuingiza fedha za kigeni kwa kuuza nje  na kukuza uchumi wa Taifa letu.

  0 0

   Katibu Mtendaji Bodi y Filamun Tanzania, Bi Joyce Fissoo akionyesha bango la filamu mpya ya “TABIA” ambalo alilizindua katika ukumbi wa May Fair Plaza uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

   Baadhi ya Wasanii maarufu wa filamu nchini Tanzania wakisikiliza hotuba fupi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi Joyce Fissoo (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa filamu hiyo katika ukumbi wa May Fair Plaza, Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
   Baadhi ya Wasanii na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa filamu ya “TABIA” wakiwa wameketi wakiangalia filamu hiyo mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania BI. Joyce Fissoo hivi karibuni katika Ukumbi wa May Fair Plaza uliopo eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO. 


  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la michezo (sports bonanza) la uzinduzi wa michezo ya SHIMIWI litakalowashirikisha Watendaji Wakuu wa Serikali na watumishi wa umma litakalofanyika siku ya jumamosi Agosti 24 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Hayo yalisemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Bw. Moshi Makuka akiwa ofisini kwake mapema leo.

  Alisema dhumuni la michezo hiyo ni kujenga na kulinda afya za viongozi na watumishi,kuboresha mahusiano kazini,kujenga mshikamano kwa watumishi,kujenga utaifa na kuondoa tofauti baina ya watumishi. Alifafanua kuwa bonanza hilo litaambatana na matembezi na mazoezi ya viungo.

  “Bonanza litahusisha matembezi (jogging) kutoka Uwanja wa Taifa kupitia Klabu ya Sigara,mataa ya Chang’ombe polisi hadi Uwanja wa taifa pamoja na mazoezi ya viungo yatayoendeshwa na wakufunzi wa michezo” Aidha,amewahimiza watendaji wakuu wa Taasisi za Serikali na watumishi wa umma kuhudhuria tamasha hilo la michezo lililoandaliwa kwa ajili yao.


  Kufanyika kwa tamasha hilo ni utekelezaji wa agizo la Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma Balozi Ombeni Sefue ambapo aliziagiza taasisi zote za serikali nchini kushiriki kwenye michezo ili kuimarisha afya zao.


  0 0

   Na www.sufianimafoto.com
  Mfanyakazi wa Inayojiita kampuni ya kukusanya Ushuru ya MTAA WA OYSTERBAY BEACH PARKING, ambaye hakutaka kutaja jina lake akiandika risiti ya ushuru wa maegesho ili kuweka katika moja ya gari lililokuwa katika ufukwe wa Coco Beach, ili alipwe ushuru wa maegesho hayo kiasi cha Sh. 1000 kila gari. Mfanyakazi huyo alipohojiwa na mtandao huu alisema kuwa anauwezo wa kukusanya hadi magari 20 kwa siku jambo ambalo si la kweli kwani kwa muda mchache tu alishapitia magari zaidi ya hayo.

  Na alipoulizwa zinapopelekwa fedha hizo baada ya kukusanywa alisema ''Mimi sijui zinapopelekwa kwani mimi ni mfanyakazi tu na nikishakusanya nampelekea Bosi ndo anajua zinapokwenda, kwa siku naweza kukusanya ushuru hadi wa magari kama 15 hivi,kwa sababu sipo peke yangu tupo wengi katika eneo hili lote''. alisema mfanyakazi huyo.

  Hata hivyo baadhi ya watu waliokuwapo ufukweni hapo, walisikika wakin'gaka kutoa ushuru huo, huku wakimhoji ''Tutoe ushuru wa Parking kwa lipi, hata usafi tu hamfanyi nyie mnajua kuchukua hela tu, na kwanza mlishazuiliwa kukusanya pesa hizi bado tu mnaendelea na wizi wenu''. alisikika akilalama jamaa mmoja

  Imeelezwa kuwa Kampuni hiyo inayojishughulisha na kukusanya ushuru huo, ilishawahi kuwa na mgogoro kipindi cha nyuma, ambapo wahusika waliwahi kukamatwa na kufikishwa hadi Kituo cha Polisi na kuzuiliwa kufanya kazi hiyo, kutokana na kutokuwa na ruhusa ya kufanya hivyo na kwamba hawatambuliki na Halmashauri wala serikali, lakini wanaendelea kinyemela na kufanya baadhi ya watu wanaowafahamu kuwagomea kutoa ushuru huo wanapofuatwa kulipia parking hiyo.

  Na hata ukiitazama kwa makini Risiti hii haionyeshi Adress kamili ya wahusika, haina mhuri wala namba za simu zaidi ya kuandika jina la Serikali ya Mtaa wa Oysterbay Beach, Sasa kuna kila haja ya kuwahoji Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo ili kujua Mapato na Matumizi ya ukusanyaji wa Ushuru huu, unaokusanywa kuanzia Jumatatu hadi Jumapili bila kupumzika na zinapokwenda Fedha hizo. 
   Hii ndiyo Risiti yenyewe inayotolewa baada ya kutoa Sh. 1000 kwa mkusanyaji, ambaye pia anakuwa ameambatana na vijana wawili waliovalia kiraia Jinzi na Tisheti na makofia ya Sweta, wakimlinda mkusanyaji huyu mdada na kupiga mkwara kwa anayeonekana kukaidi kutoa Buku.
   Mkusanyaji akiandika Risiti hiyo, ambayo hata akiisha ichana haibaki Kopi yake kuonyesha kilichoandikwa, Yaani ni Vishina kwa kwenda mbele.
   Akienda kuweka risiti  katika gari
   Akitimiza wajibu wake kuweka katika gari....
  Huyu ndiye mkusanyaji wa ushuru katika Fukwe hiyo.

  0 0

   Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa na wake zao, Mama Sitti Mwinyi na Mama Anna Mkapa, wakiwasili katika Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Harare, Zimbabwe, walikoalikwa kushiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Zimbambwe, Mhe Robert Mugabe, inayotarajiwa kufanyika kesho.Alhamisi Agosti 21, 2013 PICHA NA IKULU. 
  Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa na wake zao, Mama Sitti Mwinyi na Mama Anna Mkapa, wakiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Harare, Zimbabwe, kushiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Zimbambwe, Mhe Robert Mugabe, inayotarajiwa kufanyika kesho Alhamisi Agosti 21, 2013

  0 0

  Na James Festo,Makete

  Wanachama na viongozi wa chama cha wakulima wa nyanda za juu kusini  RUMBIA, waliopo makete wameshindwa kufika katika mkutano  na rais wa chama hicho uliotarajiwa kufanyika hapo juzi katika  ukumbi wa kata ya Iwawa 
  wilayani makete.

  Akiongea na vyombo vya Habari mara baada ya kushindikana kufanyika kwa mkutano huo  Rais wa chama hicho bw.Tudui Mwang'amba, Alionyesha Kusikitishwa kwa Kutofanyika kwa mkutano huo uliokuwa na lengo la kuchagua  viongozi na kuanza maandalizi ya mkutano mwingine ambao unatarajia kufanyika  mwezi oktoba mwaka huu.

  kwa hatua ambayo tulikuwa tumefikia kwa wilaya ya makete ilikuwa ni nzuri lakini kwa hili ambalo leo limejitokeza kuna haja ya kuanza tene kuwahamasisha   wakulima kama awali inasikitisha sana.alisema rais huyo ,Pia rais Huyo bw mwang'amba Aliyataja Malengo mengine yaliyotarajiwa  kujadiliwa katika mkutano huo Kuwa ni kujadili jinsi gani wataweza kuunda amkos na saccos ili kuweza kuanza kunufaika na mikopo kutoka kwa taasisi  mbalimbali za kilimo  kwa lengo la kuwaendeleza wakulima wa hali ya chini. 

  Aidha rais huyo alikiri kuwa katika eneo la makete watendaji wamekuwa changamoto katika utekelezaji wa majukumu yao tangu makao ya chama hicho wilaya  yalipohamishwa kutoka bulongwa hadi eneo la makete mjini Katika Hatua nyingine Rais Huyo aliongeza kuwa endapo Wangefanikiwa kuunda  saccos yenye nguvu miongoni mwa mafanikio ambayo wangeyapata ni pamoja  na kuanza kujishughulisha na usambazaji wa pembejeo za kilimo ikilinganishwa  na mfumo wa sasa wa usambazaji wa pembejeo hizo.

  Rais Huyo Pia aliwasihi wakulima wilayani hapa kuwa na umoja baina yao na kuwataka kukitumia chama hicho kama daraja  kuelekea mafanikio na kuwafanya kuwa na sauti moja. Akizungumzia tathmini ya mafanikio ya chama  hicho  katika eneo la nyanda za  juu kusini alisema kuwa wamefanikiwa kwa asilimia sabini na tano  na katika  mkutano mkubwa utakaofanyika mkoani mbeya wanatarajia kuwa na mgeni rasmi waziri mkuu wa jamhuli ya muungano wa Tanzania mh Mizinge kayanza 
  peter Pinda. 

  Chama hicho ambacho kirefu cha jina lake ni herufi zinazotoka katika mikoa mama ya nyanda za juu kusini na kimesambaa katika wilaya zote na kimefanikiwa kuanzisha saccos katika baadhi ya maeneo  ingawa baadhi yake  bado hazijasajiliwa kwa mujibu wa rais huyo


  0 0

  Na Hamida Maulid {ZJMMC}

  Wananchi wa Shehia ya Kombeni Wilaya ya  Magharibi  wameilalamikia  Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kutokana na tatizo la maji linaloendelea kuwakabili kwa kipindi cha mwaka   mmoja  sasa  na kusababisha  kuzorotesha harakati zao za kiuchumi.
  Wakizungumza na waaandishi wa habari wananchi wa shehia  hiyo, wamesema upungufu maji katika vijiji  vingi vya shehia hiyo na kuongeza  ugumu   wa maisha  kwa wananchi wengi. 
  Wamesema  maji  yamekuwa yakipatikana   kidogo sana  na baadhi ya vijiji  hayatoki  kabisa  na wamevitaja vijiji hivyo kuwa ni  Kombeni  hospitali, Kombeni  branji  na Komboni michenzani.
  “Maji yanatoka  kiduchu kiduchu sisi hatupati, na  tukipata ni kidogo sana na kwa muda mdogo  na hayana muda maalumu”. alifahamisha mwanakijiji wa Kombeni  branji bi. Afua  Abdalla kwa masikitiko.
  Sheha wa shehiya ya Kombeni  Mussa Khamis Mussa  amesema  tatizo la maji lipo kwa muda mrefu na linawakabili baadhi ya wananchi wake licha ya juhudi aliyofanya ya kuwafuata  maafisa wa ZAWA  ili kutatua ufumbuzi wa tatizo hilo. 
  Sheha Mussa  amesema    amewafuata  wahudumu  wa maji  katika kisima cha Dimani ambacho ndicho wanachotumi na kuelezwa  kwamba  mashine inayo tumika  katika kisima hicho  hivi sasa ni moja  tu    na yapili  imeharibika na  ndio ililiopelekea upungufu wa maji katika shehia hiyo.
   Kutokana na kasoro hizo sheha ameiomba Mamlaka ya Maji  Zanzibar   kuwasaidia  mabomba  mengine ya maji ili kuyafunga katika kisima chengine cha Kombeni  kwa ajili ya kupunguza  tatito hilo la muda mrefu.
   Hata hivyo Afisa uhusiano wa ZAWA  Zahor Suleiman Khatib  amekanusha  kuharibika kwa mashine katika kisima cha Kombeni na wamesema  kisima hicho kina mashinei tatu na zote zinafanya kazi.

  Zahor amewatupia lawama wananchi wanaounga maji   kiholela bila kufuata   taratibu  za Mamlaka na baadhi ya wakulima wanaotumia maji mengi  kumwagilia  mashaba yao  jambo ambalo linapelekea ukosefu wa maji katika baadhi ya vijiji.                    

  0 0

   1
  Hakuficha mapenzi ya kweli aliyonayo kwa mpenzi wake mpya aliekutana nae kwenye jumba la BBA 2013, Mbotswana Oneal… kuna wengine walichukulia kama mzaha pale Feza alipohojiwa na kusema wazi kwamba anampenda kiukweli Oneal na chochote kinaweza kutokea kati yao.Feza Kessy na Mpenzi wake Oneal wakiwa kwenye gari ya wazi huku shangwe kutoka kwa watu mbalimbali waliokwenda kumlaki zikiwa zimetanda eneo la tukio
  Taarifa ikufikie kwamba tayari Feza ameshaondoka Tanzania na kwenda Botswana kwa mpenzi wake ambapo amepata mapokezi makubwa ,kama vile haotoshi baada ya kupata mapokezi makubwa nchini humo pia anatarajiwa kuangushiwa bonge la party i.e chakula cha jioni cha mastaa hao ambao watajumuika na watu wengine pia watakaolipa kiingilio.
   


  0 0


  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamisi Kagasheki amewataka wahariri wa vyombo vya habari nchini kupanga utaratibu wa kukutana na viongozi wa wizara kwa shabaha ya kuuliza ama kupata uhakika wa mambo yaliyojitokeza ndani ya wizara.

  Mhe. Kagasheki aliyasema hayo katika mkutano na wahariri wa Jukwaa la Wahariri uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, kuhusu vipaumbele na mwelekeo wa mpango wa bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2013/2014.

  Mhe. Waziri anabainisha kwamba, kuna mambo mengi yanayoripotiwa kuhusu Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo hayako sawa. Hivyo Wizara imeona kuna haja ya kuweka utaratibu ambao utawalazimu viongozi wakuu kukutana na wahariri mara kwa mara kuwapa nafasi ya kuuliza mambo mbalimbali wanayotaka kuihabarisha jamii.

  “Kuna nchi nyingine kuna uataratibu ambao hauepukiki ,ambapo mawaziri ama viongozi wa juu inabidi wakutane na wahariri pengine mara moja kwa wiki ama kwa mwezi kwa shabaha ya kuuliza na kupata uhakika wa mambo ambayo yametokea kwa wiki ama kwa mwezi huo na kuuhabarisha ulimwengu,

  “Mimi ni utaratibu ambao naupenda kwa maana ya kusema kwamba tunawekana wazi, kwani kuna mambo mengi ambayo yanaripotiwa ambayo hayana uhalisia wa ukweli ndani yake, hii ni Wizara muhimu inayogusa maisha ya kila mtanzania. Hivyo kuna umuhimu wa Jukwaa la Wahariri kuzungumza na kuafikiana juu ya mara ngapi Wizara ikutane na wahariri ili tuweze kuwapa tarifa na kuwapa nafasi ya kuuliza mambo mbalimbali,” Alisema Mhe. Kagasheki.

  Alisema kuwa, Wizara imefikia uamuzi huo si kwa sababu ina mambo ya kuficha ama inahitaji upendeleo maalumu katika uripotiwaji wa habari zake, bali inataka kutumia fursa hiyo kuweza kujua mambo mbalimbali ambayo yapo ili kuweza kuyafanyia kazi.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda aliishukuru Wizara kwa kutoa nafasi hiyo na kuahidi kukaa na kuamua muda wakukutana na Wizara.

  Aidha, Kibanda aliwataka wahariri kuona haja ya kuripoti habari zinazolenga kujenga na si kuibomoa tu Wizara ili kuisaidia Wizara na Watanzania.

  Akichangia hoja hiyo, Katibu wa TEF, Neville Meena, aliipongeza wizara kwa kuona umuhimu wa kupanua wigo wa mawasilinao na wahariri wa habari na kutaka kuangalia uwezekano wa kufanya mikutano ya namna hiyo nje ya jiji la Dar es Salam ili kuweza kutoa nafasi kwa wahariri kushiriki kikamilifu na kufanya kazi kwa pamoja.

  Meena aliongeza kuwa, Wizara ina haja ya kubadiri utaratibu wa kutoa habari kwa kutumi makaratasi na kuona umuhimu wa kutoa taarifa kwa wakati ili wanahabari waweze kutoa taarifa sahihi kwa wananchi.

  Akizungumzia suala la utoaji wa habari Wizarani, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara, Yustina Mallya alisema Wizara imepanua wigo wa utoaji wa habari kwa kuanzisha ukurasa wake facebook na twitter ambao kila mtu anaweza kuuliza chochote na kupata majibu ndani ya wakati.

  Mallya alitoa wito kwa wananchi kutumia ukurasa wa facebook, Ministry of Natural Resources and Tourism – Tanzania na twitter, @Maliasilitz pindi wanapotaka kufahamu juu ya jambo lolote ama kutoa maoni yanayoihusu Wizara ya Maliasili na Utalii.

  0 0

  Kamati ya Hesabu za Serikali imekutana na Wizara ya Ardhi kwa madhumuni ya kupitia Hesabu za Wizara kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 2012. Changamoto za Wizara ni nyingi sana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amehoji mambo mengi sana na mengi ni wizi, upotevu wa mapato ya Serikali na malalamiko ya wananchi kuhusu ardhi.  CAG alitoa hoja za ukaguzi maeneo ya mapato kutokusanywa, kulimbikizwa na hata kukusanywa bila kuyawasilisha Wizarani.
   
  Katika Mwaka wa Fedha 2011/12 Wizara ilipangiwa kukusanya jumla ya Shilingi bilioni tisini na tisa (99 bilioni) lakini ilikusanya shilingi bilioni ishirini tu (20 bilioni) sawa na asilimia 21 ya makadirio.
   
  CAG pia alihoji masuala ya viwanja vilivyopimwa, kugawiwa watu lakini watu hawakupewa hati ambapo zaidi ya viwanja 7, 342 vilikutwa ni viwanja vyenye shaka. Pia viwanja 160 jijini Dar es Salaam vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 555.8 milioni viligundulika ni viwanja ambavyo walijigawiwa maafisa wa Ardhi maana haoakuwa na ushahidi wowote wa mauzo ya viwanja hivyo. Hoja nyingine ni pamoja na ukiukaji wa sheria kwa kujengwa kwenye fukwe nk.
   
  Katika Ripoti ya Hesabu za Serikali Kuu 2011/12 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alipendekeza kuanzishwa kwa haraka mfumo fungamanifu wa Taarifa za Ardhi, kutunza kumbukumbu kielektroniki na kuunganisha kuanzisha utaratibu wa kwamba wakati wa kusajili hati ya ardhi anayesajili kuwa na namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN).
   
  Baada ya mjadala wa kina na kushauriana na wakaguzi na wataalamu Kamati ya Hesabu za Serikali iliona kuwa kuna haja kubwa sana ya kufanya mabadiliko makubwa kwenye mfumo mzima wa kutoa hati za kumiliki Ardhi. Hivyo Uamuzi mkubwa tuliochukua ni kuagiza kuwa hati zote za kumiliki ardhi zitolewe upya, ziwe za dijitali na hati ziendane na namba ya Mlipa kodi (TIN). 
   
  Kamati imeagiza kuwa  Wizara kutoa majibu ya utekelezaji wa agizo hilo ifikapo Mwezi Januari mwaka 2014. Tunaamini kuwa iwapo hati zote za ardhi zitakuwa za dijitali, tutaondoa kabisa tatizo la hati mbili kwenye kiwanja au shamba moja, itakuwa ni rahisi kwa usimamizi wa ardhi na itaondoa mgogoro mingi ya ardhi hapa nchini. Pia tunadhani pia itakuwa rahisi kujua nani anamiliki ardhi kiasi gani, wapi nk. 
   
  Tunaamini kuwa mfumo wa dijitali katika hati za ardhi utaongeza usalama zaidi kwa wamiliki wadogo wa ardhi na kuondokana kabisa au kwa kiasi kikubwa na hati za bandia ambazo zinaumiza zaidi wananchi masikini wanaotapeliwa kila wakati. Ardhi yenye hati za kidijitali na zinazotunzwa kielektroniki zitakuwa na thamani zaidi na zitawezesha mahitaji zaidi ya hati hizo kwa shughuli mbalimbali za wananchi.
   
  Mapato yatokanayo na umiliki yatakusanywa kirahisi sana na kwa kuwa kila hati itakuwa na namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN)  itakuwa ni njia rahisi ya kuzuia ukwepaji kodi ya ardhi.  Kwa kuwa kamati imeagiza kuanza kutumika kwa risiti za elektroniki kwa malipo ya serikali, tutaweza kupandisha mapato ya Serikali na hasa kwenye halmashauri za wilaya na kuepukana na kodi sumbufu kwa wananchi.
   
  Changamoto kubwa ni kama matajiri wenye ardhi kubwa watakubali mageuzi haya kwani hawapendi ijulikane kiwango cha ardhi wanachomiliki na pia itazuia ukwepaji kodi na kupunguza rushwa kwa watendaji wa Wizara ya Ardhi. 
   
  Mfumo huu hata hivyo uwezeshe watu kuweza kutafuta kwenye mtandao hati, iwe rahisi kutafanya utafutaji. Pia mfumo huu unaweza kusaidia sana suala la fidia kwa wananchi wanaohamishwa kupisha uwekezaji mkubwa kama kwenye sekta za madini na gesi asilia. Kwa mfano mwekezaji atapaswa kuhakikisha hati za kijiditali zinapatikana kwa wananchi wanaohamishwa kupisha mradi baada ya maridhiano ya wananchi hao kuhusu kupisha mradi na mahala watakapohamia. Kuna haja pia hata hati za madini (mining rights) na leseni mbalimbali ziwe za dijitali na kuhusishwa na TIN. Huko ndipo tunapaswa kuelekea.
   
  Zitto Kabwe
  MwenyeKiti PAC  
  Agosti 21, 2013 - Dar es Salaam

  0 0


  PIX1
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel aliyesimama akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa semina ya siku mbili kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamin William Mkapa leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bibi Mwinda Kiula Mfugale, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Bibi Mizinga Melu na kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamini William Mkapa Mwl. Gebo Steven Lugano.
  PIX2 Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Bibi Mizinga  na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NBC Bibi Mwinda Kiula Mfugale wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ilyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Profesa Elisante Ole Gabriel hayupo pichani alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamin William Mkapa leo jijini Dar es Salaam.Mafunzo hayao yanalenga kumjengea kijana tabia ya kujiwekea akiba ikiwa ni njia ya kumfanya aweze kujitegemea.
  PIX2AMkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NBC Bibi Mwinda Kiula Mfugale akielezea jambo kwa waandishi wahabari kuhusu mpango wa NBC benki kutoa mafunzo kwa wanafunzijuu ya umuhimu wa kuweka akiba kwa manufaa ya baadaa. NBC inaendesha mafunzo kwa vijana walioko mashuleni nchini kote ambapo mpango huo w2ameupa jina la VIJANA LEO NA KESHO
  PIX3PIX3AMeneja Mkuu wa Masuala ya Jamii kutoka benki ya NBC akitoa mada kuhusu namna ya kuweka akiba kwa manufaa ya baadaye kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa leo jijini jijini Darc es Salaam 
  PIX4Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamin William Mkapa akichangia mada wakati wa mafunzo kuhusu umuhimu wa kuweka akiba benki, mafunzo ambayo wanafunzi hao wanawezeshwa na wafanyakazi wa benki ya NBC.
  PIX5Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel mwenye suti nyeusiakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya umuhimu wa kuweka akiba benki mafunzo ambayo yanaendeshwa na wafanyakazi wa benki ya NBC kote nchini.Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bibi Mwinda Kiula Mfugale, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Bibi Mizinga Melu.Kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamini William Mkapa Mwl. Shanina Athman na Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Gebo Steven Lugano

  0 0

   Mhasibu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Octaty Minja (kushoto), akioneshwa na mkurugenzi wa kampuni ya Agric Evolution inayomiliki shamba la kuzalisha shayiri katika Kijiji cha Sigino, Kata ya Sigino, , wilayani Babati, Manyara, .David Bagereza  (wa pili kushoto), ubora wa shayiri ambayo amekuwa akiilima katika shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 3000.Kulia ni mwandishi wa habari,Eliya Mbonea. Maofisa wa TBL na wageni wengine wakiwemo waandishi wa habari walitembelea hivi karibuni shamba hilo la shayiri inayotumika kutengenezea bia katika viwanda vya TBL nchini.TBL imekuwa ikiwasaidia pembejeo wakulima  zao hilo.
   Mhasibu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Octaty Minja (kushoto),
  akioneshwa na mkurugenzi wa kampuni ya Agric Evolution inayomiliki shamba la kuzalisha shayiri katika Kijiji cha Sigino, Kata ya Sigino, , wilayani Babati, Manyara, .David Bagereza  (wa pili kushoto), ubora wa shayiri ambayo amekuwa akiilima katika shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 3000. Maofisa wa TBL na wageni wengine wakiwemo waandishi wa habari walitembelea hivi karibuni shamba hilo la shayiri inayotumika kutengenezea bia katika viwanda vya TBL nchini.TBL imekuwa ikiwasaidia pembejeo wakulima  zao hilo.

   Machine ya kuvuna shayiri ikimwaga shayiri iliyokwishavunwa hivi karibuni katika shamba lenye ekari 3000 la David Bagereza lililopo katika Kijiji cha Sigino, Kata ya Sigino, , wilayani Babati, Manyara, kabla ya kupakiwa kwenye magunia na kusafirishwa kwenda viwanda vya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)  kutengeneza bia. Kampuni ya TBL imekuwa ikiwasaidia pembejeo  wakulima zao hilo.

  Wafanyakazi wa shamba la kampuni ya Agric Evolution lililoko katika Kata ya Sigino, Kijiji cha Sigino, wilayani Babati, Manyara,wakiweka shayiri iliyokwisha vunwa kwenye magunia tayari kusafirishwa kwenda kiwanda cha biacha TBL jijini Arusha hivi karibuni.

  0 0

  Afisa kitengo cha rasilimali watu Airtel Tanzania bi Josephine Kajembe akiongea na wateja juu ya huduma ya Airtel money yatosha na promosheni ya Airtel money Hakatwi mtu hapa wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea wateja sokoni katika maeneo mbalimbali jijini Dar es saalam.
  Meneja huduma kwa wateja Godfrey kavishe akitoa elimu kwa wateja juu ya huduma ya Airtel money yatosha wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es saalam na kutoa elimu juu ya huduma ya Airtel Money yatosha kwa watanzania.
  Mfanyakazi wa Airtel akimuunganisha moja ya wateja katika maeneo ya msasani katika huduma ya Airtel money wakati Airtel ilipowatembelea wateja wake sokoni kuitambulisha promosheni ya Airtel money yatosha Hakatwi mtu hapa.

  Wananchi katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam leo wamepokea kwa kishindo promosheni ya Airtel money yatosha inayofahamika kwa jina la Hakatwi mtu hapa kwenye mitaa mbalimbali ya jiji hilo

  Promosheni hiyo ilipokelewa kwa kishindo baada ya wafanyakazi wa Airtel kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaa na kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali na kuitambulisha rasmi sokoni promosheni ya Airtel money yatosha hakatwi mtu hapa.

  Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Tandika wilaya ya Temeke walisema kuwa huduma hiyo ya Airtel money Hakatwi mtu hapa imeweza kurahisisha baadhi ya kazi zao na kuwawezesha kuhifadhi kiasi flani cha fedha ambacho awali kilikuwa kinakatwa kutokana na kutuma na kutoa pesa.

  “Katika biashara zangu mimi huwa natuma na kupokea pesa mara nyingi tu, lakini awali nilikuwa nakatwa kiasi flani cha pesa ambacho mtu mwingine anaweza akaona kidogo lakini si kidogo ni kikubwa sana. Naishukuru Airtel kwa huduma hii ya Hakatwi mtu maana inanisaidia kiuchumi pale ninapotuma na kupokea pesa bure,” alisema Said Mrisho mfanyabiashara ndogondogo katika soko la Tandika.

  Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso alisema “ Airtel tunawajali wateja wetu na kwetu mteja ni namba moja na ndio maana kwa mara nyingine tena wafanyakazi wote wa Airtel leo wanaingia sokoni ili kutoa elimu na kuwaelimisha watanzania na wateja wetu juu ya huduma zetu haswahaswa promosheni maalumu ya Hakatwi mtu hapa .

  Tunazo huduma nyingine nyingi ambazo tunazitoa kwa wateja wetu kama vile Data 3.75G, Airtel Yatosha , na Huduma ya Airtel money ambayo sasa tunaendelea kuiboresha zaidi na kuwapa wateja wetu fulsa ya kutuma na kupokea pesa bure bila makato yoyote.

  Lengo letu ni kuhakikisha Airtel inaendelea kutoa huduma zilizo na ubunifu, za kisasa zinazokithi mahitaji ya wateja wake na tunaamini Airtel money hakatwi mtu ni suluhisho sahihi na litaleta unafuu katika huduma za kifedha nchini.

  Akizungumza katika ziara Mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano Bi Beatrice Singano alisema” watu wameonesha muitikio mkubwa sana katika kuipokea huduma yetu ya Airtel money hususani promosheni ya Airtel money Hakatwi mtu na hiyo inaonesha wazi ni jinsi gani Airtel inavyotoa huduma zilizo bora na zinazokubalika kwa wateja wake na jamii nzima kiujumla.

  “Promosheni hii ya Hakatwi mtu hapa inawawezesha mtu kutuma na kupokea pesa bure, yaani bila makato yoyote hivyo nachukua fulsa hii kuwahimiza watanzania kutumia huduma zetu za Airtel money ambazo ni rahisi , salama na zinapatikana nchi nzima.

  Ili kutumia huduma ya Airtel money mteja anatakiwa kupiga *150*60# na kuunganishwa moja kwa moja na menu ya Airtel money kisha kufanya miamala mbalilimbali ikiwemo kutuma pesa, kulipa bill, kuongeza salio kununua LUKU, USA visa na nyingine nyingi. Aliongeza Singano.

  0 0

    Msimamizi wa Masoko na Biashara wa Tigo, Gaudens Mushi  akimtazama mmoja ya washindi wa droo ya tano ya Promotion ya Miliki Biashara yako na Tigo, Furaha Hasani akipunga mkono kwa watu mara baada ya kukabidhiwa Bajaji yake katika eneo la Tandika  Jijini Dar es Salaam.
    Meneja Uzalishaji Tigo, Hussein Seif akikimkabidhi funguo ya Bajaji mmoja ya washindi wa droo ya tano ya Promotion ya Miliki Biashara yako na Tigo,  Michael Mtenzi (Kushoto) mara baada ya kukabidhiwa  Bajaji yake katika eneo la Tandika  Jijini Dar es Salaam.
   Meneja Uzalishaji Tigo, Hussein Seif akimkabidhi funguo ya Bajaji mmoja ya washindi wa droo ya tano ya Promotion ya Miliki Biashara yako na Tigo, Bi Happines Ndeki Mkazi wa Kinondoni (Kushoto) mara baada ya kukabidhiwa Bajaji yake katika eneo la Tandika  Jijini Dar es Salaam.
    Meneja Uzalishaji Tigo, Hussein Seif akimkabidhi funguo ya Bajaji mmoja ya washindi wa droo ya tano ya Promotion ya Miliki Biashara yako na Tigo, Mussa Suleimani (Kushoto) mara baada ya kukabidhiwa  Bajaji yake katika eneo la Tandika  Jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 08/22/13--01:05: TAARIFA YA MSIBA


 • FAMILIA ya Mzee Augustino Mgonja wa Pugu Kajiungeni Dar es Salaam na Familia ya Marehemu Bwana na Bibi Henry Kitosi (Mwakitosi) wa Iringa zinasikitika kutangaza kifo cha Mtoto wao, VICTORIA KITOSI (DOTTO) kilichotokea Alfajiri ya leo Agosti 22, 2013 katika Hopitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam alikolazwa baada ya kuugua ghafla.

  Mipango ya Mazishi inafanyika Pugu Kajiungeni nyumbani kwa Mjomba wake Agustino Mgonja.

  Habari ziwafikie, Mama Mdogo wa Marehemu, Mary Nathan wa Kinyenze Kipera Mkoani Morogoro, Kaka wa Marehemu Bosco Kitosi wa Mwanza, Bibi wa Marehemu,Balozi Christina Shogholo wa Kisiwani Same-Kilimanjaro, Ukoo wote wa Mwakitosi na Shogholo popote pale walipo, Ndugu Jamaa na Marafiki popote pale walipo.

  Marehemu ameacha Mume na watoto wawili, Sanden na Sabri. 

  BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. AMEN.

  0 0


  Swahili TV inakuletea kipindi maalumu sherehe za watanzania waishio DC, Maryland na Virginia walipokutana kwa siku maalum ya familia (Picnic Day) iliyofanyika Wheaton Reginal Park, MD, jumamosi August 17, 2013. Muhimu zaidi waliweza pia kuchangia rasimu ya marekebisho ya katiba mpya ya Tanzania. 

  0 0  Hilikuwa majira ya saa 11.00 alfajiri kwa saa za afrika mashariki,
  Mtangazaji wa Radio VOA-Kiswahili,mpiganaji Sunday Shomari
  alisikika akimuhoji Kiongozi wa Ngoma Africa band a.k.a FFU
  ughaibuni almaarufu "Watoto wa Mbwa" mwanamuziki Ebrahim
  Makunja aka Kamanda Ras Makunja mwenye makao kule
  Ujerumani. 

  Katika mahijiano hayo mpiganaji Sunday Shomari
  alikuwa anataka kujua nini haswa siri ya mafanikio ya Ngoma Africa band, 
  na kwanini ? bendi hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwateka washabiki
  wa kimataifa kwa kutumia muziki wa dansi.

  Kamanda Ras Makunja anakumbana na maswali ya asubuhi ! Asubuhi !
  tena kawekwa mtu kati na Sunday Shomari ! msikilize at

  0 0

  Na Onesmo Ngowi, Rais wa IBF/Africa
   Katikati ya miaka ya 90, nchi ya Tanzania ilipata bahati ya kuwa na bingwa wa ngumi wa dunia ambaye alitambuliwa na Umoja wa Ngumi wa Dunia (WBU). 
  Rashid Matumla aliweza kuonyesha dunia kwamba Tanzania pia inaweza kushindana na kushinda katika medani ya ngumi za kulipwa hivyo aliweza kujizolea sifa kemkem yeye binafsi pamoja na nchi yetu ya Tanzania.  Ilikuwa ni miaka ya msisimko kwenye ngumi za kulipwa na wadau pamoja na mabondia wengi walisisimka na uwezekano wa nchi yetu kuweza kushinda mataji mengi zaidi ya Afrika, Mabara pamoja na dunia. 
  Wakati Rashidi akiwa bingwa wa dunia, mdogo wake Mbwana naye alikuwa bingwa wa mabara alietambuliwa na WBU pia. Hiyo iliongeza chachu na hamasa kwa wadau wa ngumi za kulipwa hivyo nchi ilikuwa kwenye shamrashamra za aina ya pekee. 
  Mkuzaji (Promota) aliyefanya mambo yote hayo si mwingine bali ni Kampuni ya DJB Boxing Promotions iliyokuwa inamilikiwa na kuendeshwa kwa umahiri na ndugu wawili Dionis Malinzi na Jamal Malinzi. Ndugu hawa wazalendo kweli waliweza kuwekeza kiasi kikubwa sana katika kuwaendeleza  kina Matumla pamoja na mabondia wengine wengi hapa Tanzania.  Ni Watanzania wachache alioweza kushiriki au kuwekeza katika michezo kama kina Malinzi na hiyo iliweza kuitangaza nchi yetu kwa kiasi kikubwa. 
  Kina Malinzi hawakuwaandalia tu mapambano kina Matumla bali walienda mbali na kuwapeleka nchini Afrika ya Kusini ili waweze kufanya mazoezi kwenye gyms zilizokwa na vifaa vya kisasa pamoja na wataalamu mahiri waliowafanyia mazoezi na kubadili kabisa uwezo wao wa kupigana kuwa wa hali ya juu kama mabondia wezngie katika nchi zilizoendelea. 
  Tanzania imepita katika kipindi kirefu na kigumu bika kuweza kuwa na msisimko kama ule ambao kina Matumla chini ya kina Malinzi waliuleta nchini. Pamoja na kwamba Magoma Shabani kutoka Tanga alikuja pia kuwa bingwa wa dunia aliyetabuliwa pia na WBU lakini ule msisimko waliouleta kina Matumla na kima Malinzi ulishafifia. 
  Ujio wa bondia Francis Cheka na wengine wa jika lake umeanza tena kufufua matumaini na msisimko wa ngumi za kulipwa hapa Tanzania. Cheka bondia kutokaMorogoro ameweza kuwa kivutio pekee wa ngumi za kulipwa kwa sasa hapa Tanzania na Afrika ya Mashariki kwa ujumla. 
  Francis Cheka ni bondia pekee katika bara la Afrika ambaye ameweza kushinda na kutetea taji la IBF kwa kipindi kirefu. Nikiwa kama Rais wa IBF katika bara la Afrika,Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, ninaona faraja kubwa sana kuwa karibu na bondia Francis Cheka. Kwa kweli umahiri wake sio tu kwenye ulingo bali ni namna Cheka anavyojichanganya na watu wengine katika jamii.
   Francis Cheka anatambuliwa kuwa bondia namba 4 katika viwango vya mabara vya IBF na ni bondia pekee katika bara la Afrika aliye na kiwango cha juu kama hicho katika orodha ya mabondia wa kiafrika katika uzito wake wa Super Middle.
   Tanzania imeona na kushughudia malumbano mengi katika ngumi za kulipwa ambayo yanaletwa na sababu ambazo hazina msingi.  Tumefikia mahali tumalize tifauti zetu na kukaa meza moja ili tuweze kuuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini kwa faida ya taifa letu ili kuwapata kima Matumla na kina Cheka wengi zaidi. Pia ushirikiano wetu utawapa moyo kina Malinzi wengi zaidi kuweza kushirikiana katika kuuendeleza mchezo wa ngumi.
   Nataka itambulike rasmi kuwa bondia ana HAKI ya kuchagua ni taji lipi au chama kipi anataka kupigania. Chaguo lake lisilete mzozo au vivu kati ya wanaosimamia mchezo wa ngumi badala yake ulete ushirikiano utakaoweza kumsaidia bondia mwenyewe ili aweze kushinda na kuitangaza nchi yetu vizuri.
   Ndiyo maana naona faraja sana kwa bondia Francis Cheka kupata nafasi ya kupigana pambano la dunia. Kwangu mimi Francis Cheka ni bingwa wangu wa Afrika (IBF) mpaka atakapopanda ulingoni siku ya tarehe 30 Augusti katika ukumbi ya Diamond Jubilee. Mimi itakuwa mmoja wa maelfu ya Watanzania watakaokwenda katika ukumbi ule kumshangilia Francis Cheka akiipeperusha bendera ya Tanzania.
   Kwa kawaida bingwa wa shirikisho moja akishaamua kuwania mkanda wa shirikisho lingine anapoteza ubingwa wa shirikisho alilokuwa analishikilia. Lakini nimechukua pia jukumu la kuhakikisha kuwa kwa bahati mbaya kama Cheka akishindwa kuupata ubingwa wa dunia hatapoteza ubingwa wake wa IBF Afrika. Pia hatapoteza viwangio vyake alivyonavyo katika IBF. Hii itamsadia kuweza kung’ara zaidi.
   Mimi nadhani imefikia wakati sasa sisi watanzania wenye nia nzuri ya maendeleo kushirikiana na kuhakikisha kuwa nchi hii inapiga hatua kwenye medani ya ngumi.
   Hongera Sana Francis Cheka pamoja na waandaaji wa mpambano huo muruwa.

older | 1 | .... | 143 | 144 | (Page 145) | 146 | 147 | .... | 1897 | newer