Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 142 | 143 | (Page 144) | 145 | 146 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wengine wakiwa katika msiba wa binti wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Mhe Phillip Mangula nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013. Marehemu Nemela amafariki Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari. mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Njombe kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Agosti 21, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Nemela Phillip Mangula, binti wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Mhe Phillip Mangula nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013. Marehemu Nemela amafariki Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari. mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Njombe kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Agosti 21, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakitoa pole kwa familia ya marehemu baada ya kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Nemela Phillip Mangula, binti wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Mhe Phillip Mangula nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013. Marehemu Nemela amafariki Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari. mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Njombe kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Agosti 21, 2013. PICHA NA IKULU

  0 0

   Balozi wa China nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing (kushoto), akikata utepe kuzindua huduma mpya ya kifedha kwa kutumia fedha ya China (Yuan) ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi

  Mtendaji wa benki hiyo, Mizinga Melu.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam.

   Meneja Mkuu Kitengo cha Uhusiano cha NBC, William Kallaghe (kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa wenzake katika hafla ya uzinduzi wa huduma za kifedha za NBC kwa kutumia fedha ya kichina. Mgeni rasmi

  alikuwa Balozi wa China nchini, Dk. Yu Youqing.
   Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Maharage Chande (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha benki hiyo, Jane Dogani (kushoto), wakifurahia wakati mmoja wa wateja wao, Amin Juma (katikati) akijibiwa swali alilouliza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo. 
    Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Benki ya NBC, Jane Dogani akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Hotline Service inayomwezesha mteja wa NBC kuuliza maswali yake moja kwa moja kwa ofisa wa benki hiyo awapo ndani ya tawi la benki.
   Meneja Mahusiano wa NBC Tanzania, Eddie Mhina akiongoza shughuli za uzinduzi wa huduma ya Hotline Service ya Benki ya NBC katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam. Huduma hiyo pia kwa sasa inaweza kupatikana katikan matawi/

  0 0

  0 0

   Mgeni rasmi  Mama Tunu Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma ya kumsadia mtoto wa kike,  kushoto kwake ni Mkururugenzi Mtendaji wa Tmarc Bibi Diana Kisaka ambao ndio wandaji wa mradi huo,kulia kwa mama Pinda ni Ludovicka Tarimo mshauri wa maswala ya jinsia kutoka USAID anayefuatia ni Mkuu wa vodacom Foundation Bwana Yessaya Mwakifulefule.Sherehe hizo zimefanyika mkoani Mtwara. picha na Chris Mfinanga.
   Meneja wa voda com foundation Bwana Mwakifurefure akiwahutubia wageni walikwa voda com wamehusika katika kuweza mradi huo ambawalichangia kiasi cha shilingi milioni miamoja sitini
  Mama Tunu Pinda naonekana akicheza  ngoma marufu ya kimakonde ambayo ilikuwa ikiburusha wageni katika uzinduzi wa mradi wakumsaidia mtoto wa kike
  ============  =========  ============
  MKE WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda amewataka Watanzania washirikiane na wazazi na walimu kuhakikisha watoto wa kike wanasoma kwa bidii na kutimiza ndoto zao za ukubwani.
   
  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Agosti 20, 2013) wakati akizindua Mradi wa Hakuna Wasichoweza katika Shule ya Msingi Chilongola, iliyoko Manispaa ya Mtwara Mikindani, mkoani Mtwara. Mradi huo unafadhiliwa na Taasisi ya T-MARC inayojihusisha na Masuala ya Afya na Maendeleo, umelenga kuwafikia wasichana 10,513 katika wilaya mbili za mkoa wa Mtwara, yaani Manispaa ya Mtwara Mikindani na Wilaya ya Mtwara Vijijini.
   
  Kabla ya kuzindua mradi huo, Mama Pinda aliwaita wasichana watatu na kupanda nao jukwaani na kuwahoji mmoja baada ya mwingine kwamba wangependa kufanya nini wakiwa wakubwa.
   
  Mwanafunzi wa kwanza, Rahma Jamaldini (14) anayesoma darasa la saba katika shule ya msingi Chikongola alijibu kwamba yeye angependa kuwa rubani na akaambiwa na Mama Pinda ajitahidi katika masomo ya sayansi na hisabati ili asome hadi Chuo Kikuu kuweza kutimiza ndoto yake hiyo.
   
  Wa pili alikuwa ni Eliza Paulo (8) mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Chikongola aliyesema angependa kuwa mama. Aliwavunja mbavu watu waliohudhuria uzinduzi huo alipoulizwa tena ni kitu gani angependa kufanya mbali ya kuwa mama kwa kujibu kwamba angependa kupika. Alipoulizwa mara ya tatu kitu kingine ambacho angependa kufanya, akajibu kuosha vyombo. Mama Pinda allimhimiza asome kwa bidii ili awe mama mzuri.
   
  Wa tatu alikuwa ni Bora Hamisi (8) ambaye pia ni mlemavu wa ngozi. Bora anasoma darasa la pili katika shule ya msingi Msufini mjini Mtwara. Yeye alisema angependa fundi wa kushona nguo. Naye aliambiwa asome kwa bidii hasa somo la stadi za kazi.
   
  Mama Pinda alisema amewaita watoto hao ili wawe mfano wa kudhihirisha ndoto na matamanio ambayo watoto wa kike wanayo na kwamba wasiposaidiwa kwa kuwekewa mazingira mazuri yatakayowafanya wahitimu masomo yao, kamwe hawataweza kutimiza ndoto zao.
   
  “Watawezaje kutimiza ndoto zao kama hawahudhurii masomo kama wanafunzi wengine? Wanapaswa wasome vizuri, waende sekondari na hata vyuo vya elimu ya juu. Tuweke miundombinu itakayowasaidia kuhudhuria masomo bila kukosa,” alisema.
   
  Mapema, Mkurugenzi Mtendaji wa TMARC, Bi. Diana Kisaka alisema mradi huo umelenga kuinua uelewa wa wasichana kuhusu miili yao na mabadiliko yanayotokea katika kipindi cha balehe; kuwapa ufahamu kuhusu makundi mbalimbali miongoni mwa jamii iliyowazunguka na kuwapa upeo wao kuhusu umuhimu wa kuzingatia malengo yao katika maisha.
   
  Naye Mkuu wa Vodacom Foundation, Bw. Yesaya Mwakifulefule alisema Vodacom Foundation imechangia sh. milioni 160 kwenye Mradi wa Hakuna Wasichoweza kwani inatambua umuhimu wa elimu na suala zima la kuendeleza wasichana kielimu.
   
  “Vodacom Foundation inashugulika na masuala ya elimu kwa kuchangia madawati na teknolojia ya habari na mawasiliano katika shule mbalimbali hapa nchini. Hapa Mtwara tumetoa kompyuta 20 kwenye shule ya sekondari ya wasichana ya Mtwara ambazo zimeunganishwa na intaneti ya Vodacom,” alisema.
   
  Naye mwakilishi kutoka Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani (USAID), Bi. Ludovicka Tarimo, alisema taasisi yake imechangia Dola za Marekani 196,650 kwenye  mradi huo ambao wanaamini kupitia utekelezaji wake, utawasaidia mamilioni ya watoto wa kike hapa nchini kupata mafunzo ya kujitambua na hatimaye kufanikiwa kielimu.

  0 0


  0 0  0 0

  Wafanyakazi wa Airtel wanategemea  kuiingiza rasmi promosheni ya Airtel money, Hakatwi mtu hapa kwenye mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kuanzia jumatano wiki hii.
  wafanyakazi wa kampuni ya mitandao ya simu za mkononi Airtel wanafanya hivyo kwa dhumuni la kuelimisha na kuikaribisha rasmi promosheni ya Airtel money, Hakatwi mtu hapa kwa watanzania.
  Airtel imechukua maamuzi hayo katika muendelezo wa kuhakikisha inajenga mahusiano mazuri kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na wateja wake na kuwapatia huduma bora kwa kuwatembelea maeneo walipo.
  Akizungumza juu ya ziara hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema dhumuni la ziara hiyo ni kuhamasisha na kuwaelewesha wateja mbalimbali wa Airtel juu ya huduma mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na kampuni hiyo ya mitandao ya simu za mkononi hususani promosheni mpya ya Airtel money, hakatwi mtu hapa.
  “Tumeamua kuingia mtaani kuwahamasisha wateja wetu juu ya huduma ya Airtel Money Yatosha kwamba inamuwezesha mteja yeyote wa Airtel kutuma na kupokea pesa bure katika Mtandao wowote hapa Tanzania,” alisema Mmbando.
  Kwa mwaka huu ziara hii inakuwa ni ziara ya tatu kufanywa na kampuni hiyo ya simu za mkononi baada ya ziara nyingine mbili zilizofanywa hapo awali mwaka huu kuwa na mafanikio makubwa sana kwa kuweza kupata nafasi ya kuweza kukutana na wateja wao kwa kutoa Elimu  na kuweza kuwasaidia katika  maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

  0 0

   Balozi wa Malaria ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodger Tenga akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa malaria iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya maofisa wa NSSF wakiwa katika uzinduzi huo. 
   Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla hiyo.
   Baadhi ya maofisa wa NSSF wakiwa katika uzinduzi huo.  
   Balozi wa Malaria ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodger Tenga akipeana mkono naMeneja Kiongozi, Uhusiano Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa malaria iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
   Meneja wa Mafao ya Matibabu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ali Mtulia akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa malaria kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) pamoja na NSSF.

  0 0

   Katibu Idara ya Oganaizeshen Asiya Sharifu, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka ili azungumze na waandishi wa habari wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Utawala UVCCM ofisi ya Zanzibar Mbaruk Mrakib, mkutano huo umefanyika Gymkana Mjini Zanzibar.
   Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Gymkana Mjini Zanzibar kuliani kwake ni Mkuu wa Utawala UVCCM afisi ya Zanzibar Mbaruk Mrakib, kushoto Katibu Idara ya Oganaizeshen Asiya Sharifu.
   Mwandishi wa habari Jacoub Joseph wa Hits fm radio akimuliza sualia Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka,huko ofisini kwake Gymkana Mjini Zanzibar.


  Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka akisisitiza kitu alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Gymkana Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar)

  0 0
 • 08/20/13--11:20: WERUWERU GOLDEN JUBILLEE.


 • 0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na Balozi wa Kenye nchini Tanzania, Mutiso Mutinda, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 20, 2013 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mutiso Mutinda, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 20, 2013 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mutiso Mutinda, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 20, 2013 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Kushoto ni Kaimu Balozi wa Kenya, Peter Sang.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mutiso Mutinda, aliyeongozana na ujumbe wake wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 20, 2013 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Kitabu cha Kamusi ya Kiswahili, kutoka kwa balozi wa Kenya nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mutiso Mutinda, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 20, 2013 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Kushoto ni Kaimu Balozi wa Kenya, Peter Sang. Kitabu hicho kimetungwa na Balozi huyo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, aliyemaliza muda wake, Mutiso Mutinda, na ujumbe wake baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Balozi huyo alifika kwa ajili ya kumuaga Makamu baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Picha na OMR
  ============   ========  ==========

  MAKAMU WA RAIS AAGANA NA BALOZI WA KENYA NCHINI TANZANIA
  JUMANNE 20, 2013.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo ameagana rasmi na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mheshimiwa Balozi Mutiso Mutinda. Shughuli hiyo ya kuagana imefanyika ofisini kwa Mheshimiwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Balozi Mutiso amemueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, amefurahi kufikia kikomo cha utumishi wake kama Balozi nchini Tanzania na kwamba siku zote alizokuwa akifanya kazi hapa nchini ziliambatana na furaha kufuatia kuishi katika nchi yenye amani tele na watu wakarimu na wanaoheshimu utu wa watu.

  Balozi Mutiso alisema katika kipindi chake hapa Tanzania uhusiano baina ya Kenya na Tanzania umeimarika zaidi na kwamba pale Kenya ilipohitaji msaada wa aina yoyote Tanzania imekuwa rafiki na jirani mwema. “Nashukuru sana Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa kunipa fursa ya kuja kuagana nawe. Kwa kweli umekuwa kiongozi wa karibu nami na kwamba katika kipindi ambacho nimekuwa Tanzania mengi yamefanyika ambayo yanaashiria kuimarika kwa uhusiano baina ya nchi zetu. Ni wazi kuwa mengi yataendelea kufanyika hata katika kipindi ambachio nitakuwa nje ya hapa,” alisema.

  Balozi Mutiso ambaye pia katika kazi nyingine alizofanya amefanikiwa kuandika Kamusi ya Diplomasia, alimkabidhi Kamusi hiyo ambayo imechapishwa na TUKI na kisha kufafanua kuwa, Kamusi hiyo itakuwa chagizo la kuongeza ari ya uzungumzaji wa lugha ya Kiswahili katika nchi za Afrika Mashariki. Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal mara baada ya kupiokea Kamusi hiyo alimtaja Balozi Mutiso kama Balozi mfano wa kuigwa kutokana na kutumia nafasi yake vema kuimarisha mahusiano baina ya Kenya na Tanzania.

  Mheshimiwa Makamu wa Rais alieleza kuwa, katika kipindi Balozi Mutiso akiwa nchini Kenya imefanikiwa kutanua uwekezaji katika Tanzania na kwamba uhusiano wa kiuchumi baina ya nchi hizi mbili umeimarika zaidi jambo analotarajia kuwa litazidi kuendelea hata wakati ambapo Balozi Mutiso atakuwa katika majukuimu mengine.

  “Nakupongeza kwa kazi nzuri uliyofanya na nakutakia mafanikio zaidi katika majukumu mapya utakayopangiwa,” alisema 
  Mheshimiwa Makamu wa Rais huku akimuahidi Balozi Mutiso kuwa kazi nzuri aliyoifanya atahakikisha kuwa inaendelea hasa 

  katika eneo la utunzaji mazingira.
   Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
  Ikulu, Dar es Salaam

  0 0  "Rain or Shine"

  WE LET THE DOGS OUT
   
  mahali ni ile ilee Kijenge ya Juu mwisho wa Daladala Chaliangu

  "WE BARK  BACK TO THE SUA....BARK! BACK! TO THE SUA"

  Graffiti Toka Wachata Crew Dar es Salaam,
  Njoo Ushuhudie Underground Mc kutoka mitaa yote ya Arusha,
  Undeground Dj'z  ,Cypher....SUA-DUKA kwa ajili ya manunuzi
  ya Cds,Tshirts,badges,bracelet na mating'a kibao.  

  Maraia watapiga MAFREESTYLE hujawai kusikiaga!  

  Unajua Niaje?

  Kama ni FULL ILE LAANA basi tukutane K JUU

  Usilipe Hata kumi BABA LA BABA ibuka na MAMA LA MAMA....

  Mwisho ni saa kumi na bee arifu

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na Bw.Teo Siong Seng Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore ikulu jijini Dar es Salaam leo .
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Bw.Teo Siong Seng Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore(wanne kushoto) na ujumbe wake ikulu jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  BerdinaMajinge,Iringa.


  ZAIDI ya million 200 zimetumika kununua maabara ndogo ya kupima dawa bandia ili kudhibiti uingizaji wa madawa feki nchini.


  Akizungumza Mkurugenzi wa huduma za maabara mamlaka ya chakula na dawa mkoa wa dar e s salaam, Charys Ugulum wakati wa uhamasishaji kutumia maabara kupima ubora wa dawa, alisema kuwa kuwepo kwa dawa bandia nchini ni moja ya sababu zinazochangia ongezeko la vifo.


  Iringa ni kati ya mikoa mitano iliyobahatika kupewa msaada wa maabara ndogo kutoka ujerumani kwa kushirikiana na mamlaka ya chakula TFDA kwa lengo la kupima ubora wa dawa kabla ya kuzitumia.


  Tumamua kuleta maabara hapa mkoani na itakaa hapa katika hospital ya mkoa ili kusaidia zoezi la upimaji wa dawa fki na zisizo na ubora na kuwasaidia wagonjwa waweze kupona haraka na kuondokana na matumizi ya dawa zisizo na ubora ,alisema Charys.


  Kwa upande wake kaimu katibu tawala mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu ambaye alikuwa mgni rasim katika uhamasishaji huo alisma kuwa anashukuru mkoa huu kuwa mmoja kati ya mitano iliyopata msaada wa maabara na anaamini kuwa kutokana na uhamasishaji huu viongozi watumie fursa hii kumaliza tatizo la matumizi ya dawa bandia .


  Tutahakikisha kwa kushirikiana na halmashauri ya mkoa huu ili kupata huduma bora na kutoa taarifa za dawa na sampul zilizopimwa kwa mwzi mzima ili kujua tatizo limepungua kiasi gani.alisema Wamoja  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 amefanya marekebisho katika muundo na majukumu ya baadhi ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Kufuatia marekebisho hayo, baadhi ya shughuli za Wizara zimeunganishwa na kuundiwa Wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika wizara nyengine.
  Hata hivyo marekebisho hayo hayakuongeza idadi ya Wizara na kwa hivyo zinaendelea kubaki wizara 16. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya MzeeMarekebisho ya muundo na shughuli katika baadhi ya Wizara ni kama ifuatavyo.
  BOFYA HAPO CHINI.


  1.      Shughuli za Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ zimeondolewa katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kuundiwa Wizara mpya.
  2.      Shughuli za Utawala Bora zimeondolewa kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kuhamishiwa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
  3.      Shughuli za kazi zimeunganishwa na shughuli za utumishi na kuundiwa Wizara mpya.
  4.      Shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika zimeondolewa kutoka Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika na kuunganishwa na shughuli za ustawi wa jamii, vijana, wanawake na watoto.
  5.      Shughuli za Tume ya Mipango zimeondolewa kutoka Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo na kuhamishiwa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
  6.      Idara ya Uratibu na Shughuli za SMZ, Dar es salaam imeondolewa kutoka Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo na kuhamishiwa Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais.
  Kufuatia marekebisho hayo, zimeundwa Wizara mpya nne ambazo ni  (i) Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ  (ii)  Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma (iii) Wizara ya Fedha na (iv) Wizara ya uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto.
  Kufuatia kuundwa kwa Wizara hizo mpya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya kifungu 44 (1) na kifungu 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Wizara kwa kuwabadilisha Wizara baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kama ifuatavyo.
  1.      Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
  (a)   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Mheshimiwa Dkt. Mwinyihaji Makame.
  (b)   Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Nd. Salum Maulid Salum
  (c)    Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala bora Nd. Said Abdalla Natepe.
  2.        Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ
  (a)   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mheshimiwa Haji Omar Kheir
  (b)   Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Nd. Joseph Abdalla Meza
  (c)    Naibu Katibu  (Tawala za Mikoa) Nd. Mwinyiussi A. Hassan
  (d)   Naibu Katibu Mkuu (Idara maalum za SMZ) CDR Julius Nalimy Maziku

  3    Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma
  (a)   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa umma Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman
  (b)   Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Nd. Fatma Gharib Bilal
  (c)    Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Nd. Yakout Hassan Yakout

  4      Wizara ya Fedha
  (a)   Waziri wa Fedha Mheshimwa  Omar Yussuf  Mzee
  (b)   Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd. Khamis Mussa Omar
  (c)    Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd. Juma Ameir Hafidh.

  5     Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto
  (a)   Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii,  Vijana, Wanawake na Watoto   Mheshimiwa  Zainab Omar Mohamed.
  (b)   Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto  Nd. Asha Ali Abdalla.
  (c)    Naibu Katibu Mkuu (Uwezeshaji na Ushirika) Nd. Ali Khamis Juma
  (d)   Naibu Katibu Mkuu (Ustawi wa Jamii, Vijana,Wanawake na Watoto) Nd. Msham Abdalla Khamis.
   IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR             

  0 0


  Bondia Ramadhani Shauri kushoto akisaini mkataba wa kucheza ubingwa wa UBO utakaofanyika tarehe 27 mwezi wa 10 jijini Dar es salaam na mpinzani wake kushoto Cosmas Cheka wa Morogoro wengini ni Promota Kaike Silaju na Makamu Mwenyekiti wa PST Aga Peter nyuma.
  Bondia Cosmas Cheka wa Morogoro  akisaini mkataba wa kucheza ubingwa wa UBO utakaofanyika tarehe 27 mwezi wa 10 jijini Dar es salaam na mpinzani wake  Ramadhani Shauri kushoto wengini ni Promota Kaike Silaju na Makamu Mwenyekiti wa PST Aga Peter nyuma pamoja na kocha wa Cheka Power Iranda.
  Promota wa Mpambano wa Ubingwa wa UBO Kaike Siraju katikati akiwanyoosha mikono juu mabondia Ramadhani Shauri kushoto na Cosmasi Cheka watakaopigana tarehe 27 jijini Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Bondia Ramadhani Shauri akizungumza na waandishi wa habari kushoto ni kocha wake Christopher Mzazi na Promota Kaike Siraju

  Bondia Ramadhani Shauri akizungumza na waandishi wa habari

  Bondia Cosmas Cheka akiongea na waanishi wa habari

  0 0

  Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO  Bw. Assah Mwambene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa News for Rwanda na  wanyarwanda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana.  “Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,”amesema Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.
  Madai  hayo  yaliandikwa  jana  na  mitandao  ya  Rwanda  wakidai  kuwa  mama  Salma  Kikwete  ni  Mnyarwanda  na  ni  binamu  wa  aliyekuwa  rais  wa  zamani  wa  Rwanda. 

  Wakati huo huo, wadadisi wa mambo wa kimataifa wameonesha kushangazwa na hatua ya makusidi ya Wanyarwanda ya kujaribu kumpakazia Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete, Mmakonde  wa Lindi, kwa kumzushia mambo ya ajabu na kushangaa zaidi kuona mitandao hiyo ya udaku ya Rwanda haijaonesha jinsi Rais Kagame alivyovurumishiwa mawe na Wanyarwanda wenzake alipokuwa Chuo Kikuu ya Oxford nchini Uingereza.


  "Unajua ustaarabu wa Watanzania ni wa hali ya juu ndio maana mitandao yake iliamua kuacha kuripoti habari za kutukanwa na kupigwa mawe Rais Kagame na Wanyarwanda wenzake wanaomchukia (angalia video) alipotembelea Chuo Kikuu cha Oxford hivi karibuni", amesema mdadisi mmoja  wa Uingereza, James Parker wa North London.


  Mdadisi mwingine wa Uingereza, Bw. Mark Sutton, amesema hiyo ni moja ya njia chafu za Wanyarwanda katika kujaribu kulipiza kisasi kwa kutimuliwa maelfu ya ndugu zao waliokuwa wakiishi kinyume cha sheria nchini Tanzania, na sasa wanahaha wapi kwa kuwaweka kwenye ka-nchi hako kadogo ka Afrika Mashariki.

  "Kutimuliwa kwa Wanyarwanda nchini Tanzania kutaleta vituko vingi sana, na hii ya kumsingizia Mama Salma Kikwete kuwa anahusiana nao ni mojawapo - mengi yatakuja na Watanzania wasishangae maana Wanyarwanda wametaharuki na hawajui wafanyeje kwa kupokea zaidi ya wenzao 10,000 waliokuwa wakiishi kinyume cha sheria nchini Tanzania," amesema mdadisi mwingine, Adam Hayes.

  0 0


  *Utajiri, safari zake nje ya nchi vyatiliwa shaka
  *Ahusishwa na mtandao hatari wa Masogange.  KWA mara ya kwanza tangu lilipoibuka sakata la watu maarufu kujihusisha ama na utumiaji au usafirishaji wa dawa za kulevya, jina la mwanamuziki anayeaminika kuwa na ukwasi mkubwa kwa sasa hapa nchini, Nasseeb Abdulmaliki, maarufu zaidi kwa jina la Diamond, limeanza kutajwa kuwa ni miongoni mwa vigogo wa ‘unga.’

  Tayari mjadala mkubwa wa chini chini umeibuka kwa watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wake, na taarifa ambazo zimelifikia MTANZANIA Jumatano kutoka vyanzo mbalimbali zimedai kuwa, mwenendo wa maisha ya Diamond sasa unachunguzwa na baadhi ya maofisa wa vyombo vya dola vya ulinzi na usalama.

  Kutajwa kwa jina la Diamond katika sakata hili, kunatiwa nguvu zaidi na mwenendo binafsi wa maisha wa msanii huyo maarufu wa muziki wa kizazi kipya, unaokwenda sambamba na ukwasi mkubwa alioupata katika kipindi kifupi.


  0 0

  Na Amina Abeid Salum  (ZJMMC).

  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesimamisha ujenzi wa skuli tatu za Sekondari zinazofadhiliwa na Benki ya Dunia kufuatia kampuni  ya Electrics International Company Limited ya Dar es salaam, inayojenga skuli hizo, kwenda kinyume na mkataba waliokubaliana.

  Afisa  majenzi Wizarani hapo Riziki amezitaja skuli hizo kuwa ni Paje Mtule,Tunguu pamoja na Dimani na kueleza kuwa kutokana na kampuni kwenda kinyume na muda waliopewa, Wizara iliamua kuisimamisha kampuni hiyo.

  Ameeleza kuwa Wizara imeipa Kampuni hiyo muda wa kutosha  kukamilisha kujenga majengo hayo lakini   imeshindwa kumaliza kazi hiyo kwa muda waliokubaliana. Amefafanua kuwa  kampuni ilitakiwa kuanza kazi ya ujenzi  mwezi Ogasti 2010 na kukabidhi mwezi  Agosti 2011 lakini walishindwa na  kuomba kuongezewa muda hadi  Novemba 2011  na walishindwa kukamilisha kazi hiyo.   

  “Mkandarasi tulimpa muda wa mwaka mmoja  kukamilisha ujenzi  lakini hakumaliza na akaomba  aongezewe muda  na tulimpa kuanzia  Novemba 2011 mpaka Desemba 2011 lakini  hatukuona jitihada yoyote ya mabadiliko ya ujenzi huo”, alisema Riziki.
  Kuanzia  mwezi Juni 2013 mkandarasi huyo alianza  kukatwa malipo ya fidia kwani ndio muda uliotarajiwa kukabidhi  kazi hiyo.

  Sababu zilizopelekea mkandarasi kushindwa kumalizia kazi hiyo ni uwezo mdogo wa kifedha , uongozi mdogo wa  pamoja na ukosefu wa vifaa na wafanyakazi katika maeneo ya ujenzi. Pamoja na kufikia hatua kubwa ya ujenzi, Mkandarasi huyo  amesababisha kusimama kwa kazi za utiaji wa maji unaotarajiwa kutiwa na Mamlaka ya Maji ZAWA  pamoja na Umeme ambapo Kampuni ya ZECO imeshindwa kutokana na kutokamilika ujenzi wa skuli hizo.

  Wizara inaendelea kuikata fidia kampuni  ya asilimia 0.1 ya gharama kwa siku mpaka wafikie asilimia 10 ambayo ni sawa na siku 100 na Wizara itaendelea kuikata pesa nyengine pindi itakapoleta maombi mengine.

  Sheha wa Shehia ya Dimani Mussa Khamis Mussa amesema yeye hana  taarifa yoyote kuhusiana na kusimamishwa kwa ujenzi huo kwani hakuletewa taarifa yoyote ya kusimamishwa.

  Wizara ya Elimu imeamua kulipeleka suala hilo kwa mwanasheria  mkuu kwa ajili ya kulipeleka katika vyombo vya sheria  na  kampuni kwa upande wake inajiandaa na  imeshataarisha mwanasheria  kusimamia kesi hiyo iwapo itafikishwa mahakamani.                              
                                                 
  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI ZANZIBAR

  0 0

  Chinese UK Base Company, Owin Media Limited have signed Agreement with Tanzania Optima Aviation & Security Co. Ltd to organize first ever Tanzania – Chinese Lantern Festival to be held next year 2014, in Dar es Salaam.

  Ian Yiang Creative Director of Owing Media Limited said, This is Great opportunity for Tanzania and China Government and its people to promote Tanzania and Chinese Culture and strengthen good and long relationship between Chinese people and Tanzania.


  We are very excited to work with our Tanzania partner friends to organize Tanzania – China Lantern Festival for the first time in Africa, especially Tanzania, the country that has great good historical relation with Chinese people and we are expected to invest 2 million US Dollar for installation of equipment’s and event promotion”, he said.


  Managing Director of Optima Aviation Security and Jambo Concepts (T) Ltd publishers of Darleo newspaper, Dar Metro and Jambo brand Tanzania, Mr. Juma Mabakila said, “we are very excited to get this opportunity to work with our partner Owin Media to organize the first ever Tanzania – China Lantern Festival in Africa (Tanzania), the unique festival, which will promote our Tourism, Business and culture Internationally, as well as provide employments for local Tanzanian’s. 


  Owin Media has been organizing the same event in different countries and major cities, such as Canada, USA, Indonesia and this year Chines – London Festival to be held, London - England at Clapham Common.  Juma Mabakila,


  Managing Director – Optima Aviation Security 


older | 1 | .... | 142 | 143 | (Page 144) | 145 | 146 | .... | 1898 | newer