Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA

$
0
0
Benny Mwaipaja

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amezindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, utakaogharimu shilingi bilioni 10 zilizotolewa na Benki ya Dunia.

Lengo la utafiti huo utakaofanywa na Ofisi Kuu ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni kupata takwimu zinazohusu shughuli za kijamii na kiuchumi, mapato na matumizi, hali ya makazi na umiliki wa rasilimali katika ngazi ya kaya.

Dkt. Mpango alisema kuwa Utafiti huo utaiwezesha Serikali kupima kiwango cha hali ya umaskini wa kipato, chakula na pengo baina ya matajiri  na maskini kuanzia kipindi cha mwaka 2013 hadi sasa.

“Takwimu zilizopo hivi sasa zinaonesha kwamba kiwango cha umasikini wa kipato ulipungua kutoka asilimia 34 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 28.2 mwaka 2012” Alisema Dkt. Mpango.

Alisema pamoja na takwimu hizo, bado kiwango cha umasikini ni kikubwa na kwamba Serikali kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali inahakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma za msingi za kijamii kwa kadri uchumi unavyokua hivyo kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la umasikini.

“Nimefurahi kuelezwa kuwa utafiti huu utakusanya takwimu katika kaya binafsi 10,460 kwa Tanzania Bara kuanzia Novemba 2017 hadi Novemba 2018 na kwamba kupitia zoezi hili, Serikali ya Awamu ya Tano imetoa ajira kwa vijana wapata 620 katika maeneo ya vijijini na mijini” alieleza Dkt. Mpango.

Aliwaasa wadadisi hao kufanyakazi zao kwa umakini na weredi mkubwa ili takwimu zitakazopatikana ziwe sahihi na kuonya kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaojaribu kuvuruga zoezi hili.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa alieleza kuwa ukusanyaji wa Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi utafanyika katika maeneo 754 yaliyochaguliwa kitaalamu kwa kutumia takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012.

“Utafiti huu utakuwa wa saba tangu Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961, ambapo tafuti nyngine zilifanyika 1969, 1991/92, 2001, 20117 na mwaka 2011/12” aliongeza Dkt. Chuwa.

Alisema kuwa utafiti huo mpya utafanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ijulikanayo kama Survey Solution (CAPI) na kwamba matokeo ya awali ya utafiti huo yanatarajiwa kutolewa ndani ya miezi sita ijayo ili nchi iweze kufahamu kiwango cha umasikini uliopo katika jamii hivi sasa baada ya kufanyika kwa utafiti kama huo miaka mitano iliyopita.

“Utafiti wa mwisho uliofanyika mwaka 2011/2012 uliotumia karatasi uligharimu shilingi bilioni 20 lakini kwa kutumia teknolojia mpya, utafiti huu utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 10 pekee” alisisitiza Dkt. Chuwa.

Dkt. Chuwa alisema kuwa anaamini matokeo ya utafiti huo yatakuwa chachu ya kupata takwimu za msingi kwa ajili ya kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa program mbalimbali za kitaifa na kimataifa zenye kulenga kupunguza kiwango cha umasikini nchini.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu ya TEHAMA Bw. Baltazar Kibola alisema kuwa watatoa ushirikiano wakutosha kwa wadadisi hao katika ngazi zote kuanzia Mikoa, Wilaya, Halmashauri, Kata, Vijiji na Vitongoji ikiwemo kufanyia marekebisho vitendeakazi vya kukusanyia takwimu hizo vikipata hitililafu ili azma ya Serikali ya kupata takwimu sahihi itimie kama ilivyopangwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu  (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo kuhusu namna utafiti  wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi utakavyotekelezwa wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi na uzinduzi wa wa zoezi la ukusanyaji takwimu za utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi, Mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akimkaribisha  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kufunga mafunzo ya Wadadisi, na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, Mjini Dodoma.

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, mjini Dodoma, utakaohusisha kaya binafsi 10,460.

 Meza Kuu (Walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na Wasimamizi wa zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, mjini Dodoma. Utafiti huo utahusisha kaya binafsi 10,460.

 Wadadisi wa Takwimu za Utafiti  wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/2018, wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanywa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), Mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu  (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo kuhusu namna utafiti  wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara utakao gharimu shilingi bilioni 10, wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi na uzinduzi wa wa zoezi la ukusanyaji takwimu za utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi, Mjini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, mjini Dodoma, utakaohusisha kaya binafsi 10,460. 
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, anayeshughulikia TEHAMA Bw.  Baltazar Kibola, akieleza mikakati ya Ofisi yake katika kusaidia kufanikisha zoezi la ukusanyaji wa takwimu za utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, uzinduzi huo umefanyika mjini Dodoma. 
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

RC MAKONDA KUWAKARIBISHA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA KIZALENDO.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA ameandaa tamasha la kuwakaribisha Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza kwa Vyuo Vikuu vya Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo, kuwaepusha kuingia kwenye makundi hatarishi. 

Tamasha hilo linalotaraji kufanyika eneo la Maegesho Mliman City litatawaliwa pia na Burudani kutoka kwa Wasanii Mbalimbali ambapo vyombo vya Habari vya TBC, CHANNEL TEN NA E FM wamejitolea kulibeba tukio hilo la kipekee. RC MAKONDA amesema hayo wakati wa Mkutano na hafla ya kupata Chai na Maraisi wa Vyuo Vikuu vya Mkoa wa Dar es salaam pamoja na Viongozi wa Asasi za Kiraia. 

Katika Mkutano huo Vyuo vikuu vimeunga Mkono kampeni ya ujenzi wa Ofisi za Walimu kwa kuchangia Mifuko 25 ya Saruji na kuahidi kuendelea kuunga mkono kampeni hiyo. Aidha RC MAKONDA ametoa nafasi kwa Vyuo vikuu kumuweka kikaangoni kwa kufanya mdahalo wa kubadilishana mawazo na kuelezana changamoto.

RC MAKONDA pia amesema anao mpango wa kuandaa Shindano la Uongozi Wanafunzi wa Vyuo vikuu kwa lengo la kuwajengea Wanafunzi uwezo wa uongozi bora na namna ya kupatia majibu changamoto ambapo Mshindi atapata ofa ya kusoma Bure Chuo cha Diplomasia. 

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam LAZARO MAMBOSASA amewaomba Wanafunzi wa vyuo vikuu kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi pale wanapobaini uwepo wa Wahalifu.

Kampeni ya Uzalendo na Utaifa kuzinduliwa Disemba nane Mjini Dodoma

$
0
0
Na Shamimu Nyaki –WHUSM.

Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo imeandaa Kampeni ya “Uzalendo na Utaifa” inayotarajiwa kuzinduliwa Disemba nane mwaka huu Mjini Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli lengo ikiwa ni kurejesha hali ya Uzalendo na Utaifa katika kutatua changamoto zilizojitokeza na zitakazojitokeza katika Taifa letu.

Akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Serikali jana Jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Kampeni hiyo inadhamiria kuwakumbusha watanzania Utamaduni wetu na Uzalendo uliokuepo miongoni mwa Watanzania ambao ulileta heshima kubwa ndani na nje ya nchi.

“Kampeni hii ina lengo la kurudisha Uzalendo tuliokuwa nao Watanzania katika kuheshimu mali za Umma, kuogopa rushwa,ubaguzi wa kidini,kikabila,kiitikadi na kikanda ambavyo vilianza kupotea,lakini Serikali ya awamu ya Tano imeanza kurudisha hivyo sisi kama watanzania tunapaswa kuunga mkono jitihada hizi”Alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa Kampeni hiyo inatarajiwa kuleta matokeo chanya ikiwemo kurejesha na kuimarisha moyo wa Uzalendo na Utaifa kwa Watanzania hususan vijana na watoto umuhimu wa kuipenda na kuithamini nchi yao pamoja na kuimarisha umoja upendo na mshikamano wa kitaifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi za Serikali kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geofrey Mwambe amesema Taasisi za Serikali zinaunga mkono Kampeni hiyo kwani itasaidia watanzania wengi kuelewa historia na Utamaduni ya nchi yao na kuitilia maanani popote watakapokuwa.

Kampeni hiyo yenye kauli mbiu “Nchi Yangu Kwanza” itakuwa ni endelevu na inatarajiwa kufanyika kila mwezi Oktoba kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza jana Jijini Dar es Salaam na Wakuu wa Taasisi za Serikali kuhusu Kampeni ya Uzalendo na Utaifa inayotarajiwa kuzindiliwa mwezi ujao Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi za Serikali Bw. Geofrey Mwambe kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) (aliyesimama )akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Wakuu hao kuhusu Kampeni ya Uzalendo na Utaifa inayotarajiwa kuzindiliwa mwezi ujao Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akiwaonyesha Wakuu wa Taasisi za Serikali Jarida la Nchi Yetu linaloelezea mafanikio ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya Tano lililondaliwa na Idara yake kwa kushirikiana na Taasisi hizo jana Jijini Dar es Salaam.

WATUMISHI WA AFYA BADO WANAHITAJIKA NCHINI.

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa kwanza kulia akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wataalam wa chuo cha Afya na Tiba KAM kuhusu vifaa vinavyotumika maabara kwenye moja ya maabara ya chuo cha Afya na tiba cha KAM wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifanya majaribio ya kuchunguza wadudu kwa kutumia hadumini iliyopo kwenye moja ya maabara ya chuo cha Afya na tiba cha KAM wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM hawapo pichani wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba wa Chuo cha Afya na Tiba KAM dkt. Aloyce Musika akiongea na wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM whawapo pichani wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi Wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akigawa vyeti kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afya na Tiba KAM waliofanya vizuri kwenye masomo ya fani mbalimbali ya afya wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akigawa vyeti kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afya na Tiba KAM waliofanya vizuri kwenye masomo ya fani mbalimbali ya afya wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akipokea na zawadio kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba wa Chuo cha Afya na Tiba KAM dkt. Aloyce Musika kulia wakati wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM wakimsikiliza wakati wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.Picha Na Ally Daud- Wizara ya Afya (WAMJW)


WATUMISHI wa kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania ili kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha Afya na tiba cha KAM yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

“Tuna malengo ya kuwa na watumishi wa kada mbalimbali za sekta ya afya wapatao laki 1.849 na kati ya hao tumefanikiwa kuajiri watumishi 89842 na bado tunahitaji watumishi 95800 ili kuweza kuwa na rasilimali watu” alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa wanakishukuru chuo hiko kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa rasilimali watu katika sekta ya afya kwani wametoa wataalamu wa afya wapatao 1600 mpaka hivi sasa.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Serikali kupitia Wizara ya afya imetoa shilingi milioni 700 kwa vituo vya afya ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini.

“Tumetoa milioni 700 kwa kwa vituo vya afya vipatavyo 100 hapa nchini ikiwa milioni 400 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya upasuaji na vyumba vya kujifungulia na milioni 300 ni kwa ajli ya kununua vifaa tiba” alisema dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba dkt. Aloyce Musika amesema kuwa wahitimu wanatakiwa kujiendeleza na elimu ili kuongeza kiwango cha elimu na kuwa wabobezi katika kutoa huduma za afya zilizo bora na kwa uhakika nchini.

“Wahitimu waliotunukiwa vyeti leo hii wasiwaze kuajiriwa tu bali wafikirie kuwa msaada wa kutoa huduma za afya katika jamii huku wakifikiria kuongeza ujuzi zaidi katika taasisi mbalimbali hapa nchini ili watoe huduma za afya kwa uhakika” alisema Dkt. Musika

Mbali na hayo msoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Saleh Said ambaye ni Muhitimu wa fani ya Udaktari ngazi stashahada amesema kuwa anaiomba Serikali kuangalia kwa ukaribu na kuweka utaratibu pindi wanafunzi wanapomaliza mafunzo yao kwenye masula ya afya waweze kupata ajira kwa haraka.

Naibu Waziri wa afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya Chuo Cha Afya na Tiba KAM kwa kuwatunukia wahitimu 600 Shahada na stashahada ya fani mbalimbali katika kada mbalimbali za sekta ya afya.

Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete Aongoza Mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu Dar es Salaam

$
0
0

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Shahada ya Uzamivu katika Uchumi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandara.
Wahitimu wa Shahada ya Sayansi ya Uzamili Katika masuala ya Jiolojia wakifurahia mara baada ya kutunukiwa rasmi shahada hiiyo katika Mahafali ya 47 ya chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia alikuwa amidi wa shughuli za sherehe za chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimkabidhi mrithi wake Profesa Boniventure Rutinwa zana ya kutumikikia nafasi hiyo wakati wa mahafali ya 47 ya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara akitoa neno la shukrani mara baada ya zoezi la kuwatunuku degree zao wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo jijini Dar es Salaam.
: Baadhi ya wahitimu wakiwa katika nyuso za furaha kufuatia kuhitimu masomo yao kama walivyokutwa na mpiga picha wetu katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba mara baada walipokutana katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Jijini Dar es Salaam. Mwigulu Nchemba nimiongoni mwa wahitimu waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Uchumi katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo Mlimani City.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba na Mkurugenzi Mkuu wa Mamala ya Usimaizi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isack. (Picha na MAELEZO).

KAIMU MKURUGENZI MKUU NIDA AWASILI MARA TAYARI KWA UZINDUZI WA ZOEZI LA USAJILI AKIWA AMEAMBATANA NA KAMISHNA GENERALI WA IDARA YA UHAMIAJI NCHINI

$
0
0
Kamishna Generali wa Idara ya Uhamiaji nchini Dkt. Anna Peter Makakala, akizungumza jambo wakati alipowasili ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Annarose Nyamubi (Aliyeketi Katikati).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NIDA) Ndg. Andrew W. Massawe akiweka saini kitabu cha wageni alipotembelea Kambi ya JKT Butiama kukagua mafunzo kwa vijana watakaoshiriki kuendesha zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu akipokea maelezo ya namna mafunzo yanavyotolewa kwa vijana wa JKT. Katikati ni Afisa wa Nida mtaalamu wa mifumo ya komputa Bw Godfrey Surera ambaye amekuwa akiendesha mafunzo hayo.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida akisisitiza jambo mbele ya vijana wa JKT (Hawapo pichani) wakati alipotembelea kambi ya Butiama kukagua mafunzo ya namna ya kutumia mashine yanayoteolewa kwa vijana wa JKT. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Mhe. Annarose Nyamubi 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, viongozi wa Kambi ya JKT Butiama na vijana ambao watashiriki kuendesha zoezi la Usajili kwa wananchi wa Wilaya hiyo linalotarajiwa kuanza Jumatano 22/11/2017


Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NIDA), Ndg Andrew W. Massawe amewasili rasmi mkoani Mara akiwa ameambatana na Kamishna Generali wa Idara ya Uhamiaji nchini Dkt. Anna Peter Makakala tayari kwa uzinduzi rasmi wa kuanza kwa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Mkoa huo utakaofanywa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi Hamad Masauni.


Mara baada ya kuwasili viongozi hao walipokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Malima ambaye aliwatambulisha kwa wananchi wa Bunda kabla ya kukutana na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Annarose Nyamubi ambaye pamoja na kuwapa ripoti ya maandalizi ya Usajili kwenye Wiilaya yake, walipata fursa kutembelea Kambi ya JKT Butiama kukagua mafunzo kwa vijana ambao wataendesha zoezi hilo ndani ya siku 60.


Akizungumza na vijana katika Kambi hiyo, ndg. Masssawe amewataka kuwa wazalendo na makini katika zoezi wanalokwenda kulisimamia kwa kuhakikisha wanalifanya kwa uangalifu na nidhamu ya hali ya juu kwa faida ya Taifa lao.


“ tunafarijika sana tunapoona zoezi hili likiendeshwa na vijana wa JKT kwani mara zote wamekuwa wakijitoa kufanya kazi nzuri yenye uzalendo wa kweli kwa Taifa lao; ndiyo maana nawapongeza kwa dhati uongozi wa Mkoa na Wilaya kwa kuamua kusimamia zoezi hili na kuweka malengo ya utekelezaji, na sisi tunaahidi kwenu hatutawaangusha” alisisitiza.


Uzinduzi wa zoezi la Usajili kwa mkoa wa Mara utafanyika Jumapili 19/11/2017 na unategemewa kuhudhuriwa na viongozi wote wa Mkoa wakiwemo wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Madiwani, watendaji na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji, watumishi wa umma, Viongozi wa Dini na Wananchi.

MELI YA CHINA YATUA JIJINI DAR KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU KUANZIA JUMATATU HADI IJUMAA

MAHAFALI YA UALIMU NA KIDATO CHA NNE YA AL-HARAMAIN YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mhitimu Nahya Nassor, akikabidhiwa cheti chake na mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha nne, Asma Maharagande.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha nne, Ruzna Ali Iddi.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha nne, Ismail Mngoya.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha nne, Amina Mwinyimkuu
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha nne, Abubakar Ali.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha nne, Ikram Alley.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha nne, Waziri Pambo.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha nne, Yakub Sheikh.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu Diploma ya Ualimu Shule za Msingi,Mayasa Mussa.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu Diploma ya Ualimu Shule za Msingi,Siza Mohamed.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu Diploma ya Ualimu Shule za MsingiDogo Salum.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu Diploma ya Ualimu Shule za MsingiKhairat Bakar.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu Diploma ya Ualimu Shule za MsingiFirdaus Abubakar.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu Diploma ya Ualimu Shule za MsingiBwashehe Yussuf.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu Diploma ya Ualimu Shule za MsingiAdolf Baltazar.
Mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akimkabidhi cheti cha kuhitimu Diploma ya Ualimu Shule za MsingiJoseph Mwebeya.
Wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, wakiwa katika gwaride la kuingia kwenye viwanja vya mahafai yao ya 29 ya shule hiyo, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wahitimu wanawake wa Ualimu, Diploma Shule za Msingi, wakiwa katika gwaride, wakielekea kwenye viwanja vya mahafali.
Kikundi cha Kaswida cha Sekondari ya Al Haramain kikitumbuiza wakati wakiongoza gwaride la wahitimu wa kidato cha nne, wahatimu wa Ualimu Ngazi ya 6 na Ualimu Elimu ya Awali, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Wahitimu wa Ualimu, Elimu ya Awali, wakiwa katika mahafali yao hayo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto), akiongozwa na Mkuu wa Sekondari ya Al Haramain, Mwalimu Nuh Jabir (kulia), kuelekea katika viwanja vya mahafali.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Nuh Jabiri (kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Al Haramain, Suleiman Urassa (kulia), wakiuongoza msafara wa mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim (hayupo pichani) kuelekea kwenye viwanja vya mahafali hayo.
Mwanafunzi wa kidato cha sita wa shule hiyo, Omar Maazi akisoma Qur'an, wakati wa mahafali hayo.
Mwanafunzi wa kidato cha nne, Salum Ruta, akitoa tafsiri ya aya za Qur'an iliyosomwa.
Wahitimu wa kidato cha nne, Nahya Salum (kushoto) na Halima Nassor, wakighani utenzi katika mahafali hayo.
Wahitimu wa kidato cha nne wakiwa katika mahafali yao hayo.
Mhitimu wa kidato cha nne, Yassin Omar (kushoto), akisoma risala ya wahitimu. Kulia anayemsaidia ni mhitimu mwenzake, Ismail Omar.
Mhitimu wa Ualimu Ngazi ya 6, Maulid Hamad (kushoto), akighani utenzi wakati wa mahafali yao hayo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwalimu Nuh Jabir, akizungumza wakati akitoa taarifa ya shule hiyo kwa mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum (wa pili kulia) katika mahafali hayo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwalimu Nuh Jabir (kushoto), akimweleza jambo mgeni rasmi katika mahafali hayo, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum.
Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Al Haramain, Mwalimu Suleiman Urassa, akitoa taarifa ya chuo hicho, kwa mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum (wa pili kushoto), katika mahafali hayo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, akitoa nasaha zake.
Mwanachuo wa Ualimu, Zainab Khamis, akighani utenzi wa kuwaaga wahitimu wa ualimu katika mahafali hayo.
Mwalimu wa Taaluma Sekondari, Rashid Kassim akitaja majina ya wahitimu kwa ajili ya kukabidhiwa vyeti vyao na mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum (katikati) katika mahafali hayo.


RC MAKONDA AANDIKA HISTORIA, MELI KUBWA YENYE HOSPITAL NDANI YAWASILI NA MADAKTARI BINGWA KUTOKA CHINA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA akikagua gwaride ndani ya Meli hiyo mara baada ya kuwasili Bandari ya Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA akionyeshwa moja ya Helikopta zilizomo katika Meli hiyo mara baada ya kuwasili Bandari ya Dar es salaam.

………………………………………………………………………………

Meli kubwa ya Jeshi la Jamuhuri ya China yenye Hospital ndani imewasili Leo ikiwa na Madaktari Bingwa 381,Vifaa na Madawa ya kutosha kwaajili ya kuanza kwa zoezi la Upimaji na Matibabu Bure kwa wakazi wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA ametembelea Meli hiyo na kujionea namna imesheheni Vifaa tiba vya Kisasa ambapo ndani yake vipo vyumba 8 vya Upasuaji, Vyumba vya ICU, Wodi za Wagonjwa, Vyumba vya Madaktari, Mitambo ya kisasa, Mahabara na Sehemu ya Wagonjwa kupumzika.

Meli hiyo ya kipekee ina Helicopter kwaajili ya wagonjwa ambapo kwa Ulimwenguni Meli za Aina hiyo zipo Mbili pekee ambapo moja ni hii iliyokuja Tanzania na nyingine ipo Nchini Marekani.

RC MAKONDA amesema Meli hiyo ina mfumo maalumu wa Mawasiliano Kati ya Meli na Taifa la China pale inapotokea Ugonjwa umeshindikana.Tayari Jopo la wataalamu 30 wameenda Hospital za Amana, Temeke, Mwananyamala na Ocean Road kwaajili ya kukarabati na kufunga vifaa vipya kwa vile vitakavyobainika vilivyoharibika au Kufa.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Hakuna mwananchi anaepoteza maisha kwa kigezo cha kukosa huduma.Amewasihi Wananchi wenye magonjwa yaliyoshindikana kwa muda mrefu kuchangamkia Fursa hii ya matibabu Bure chini ya Madaktari Bingwa kutoka China.

Kwa upande wake kiongozi Mkuu wa Meli hiyo Kamanda GUAN BAILIN amesema wamekuja na vifaa vya kutosha na madaktari waliobobea hivyo wananchi Wajitokeze kwa wingi.

Asasi za kiraia zaiomba Serikali kuboresha Sheria ya Usalama Barabarabi ya 1973

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Felician Mkude. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Felician Mkude Mwenyekiti wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA), John Seka akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani.Kushoto ni Isabela Nchimbi kutoka TAWLA na Bi. Edda Sanga wa TAMWA (kulia). Mwakilishi wa TAWLA, Bi. Isabela Nchimbi akizungumza katika mkutano huo. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA), John Seka. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Felician Mkude (kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani. Kushoto ni Bi. Edda Sanga wa TAMWA (kulia). Kushoto ni Mratibu wa Global Road Safety Partnership Tanzania, Bi. Tusa Bernard akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA), John Seka.

MTANDAO wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani umeiomba Serikali kuifanyia maboresho sheria ya Usalama barabarabi ya mwaka 1973 ili iweze kukabiliana ipasavyo na suala la ajali za barabarani pamoja na athari zinazotokana na ajali hizo. 

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga alipokuwa akisoma tamko la pamoja la asasi hizo katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani. 

“Pamoja na mambo mengine, katika kuadhimisha siku hii tunaisihi serikali na watunga sheria kuifanyia maboresho sheria ya Usalama barabarabi ya mwaka 1973 ili iweze kukabiliana ipasavyo na suala la ajali za barabarani pamoja na athari zinazotokana na ajali hizo,” alisema Bi. Sanga. 

 Alisema miongoni mwa maeneo wanaoshauri marekebisho/maboresho ni pamoja na matumizi ya mikanda, ambapo Sheria ya sasa ya Usalama barabarani inasema ni kosa kisheria kwa dereva na abiria anayekaa kiti cha mbele kutokufunga mkanda wakati wa safari lakini sheria haisemi chochote kwa abiria wanaokaa viti vya nyuma. Alisema licha ya Kanuni za SUMATRA zinamtaka abiria yeyote kufunga mkanda ila kwa vile sheria mama (Road Traffic Act of 1973) ipo kimya katika eneo hilo utekelezaji wa kanuni hii unakuwa mgumu. 

Alisema eneo linguine ni pamoja na matumizi sahihi ya kofia ngumu, kwani Sheria ya sasa ya usalama barabarani inatambua kosa kwa mwendesha pikipiki kutokuvaa kofia ngumu lakini sheria hiyo haisemi chochote kwa abiria anayepanda katika chombo hicho wala kutaja aina na ubora wa kofia inayofaa.

 “Kwa matumizi ya vilevi na uendeshaji vyombo vya usafiri: Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa itakuwa kosa kwa mtu yoyote kuendesha chombo cha moto akiwa na kiwango cha kilevi katika damu yake kinachozidi asilimia 0.08% katika mfumo wa mwili. Kiwango hiki ni kikubwa sana kikilinganishwa na tafiti zilizofanywa na Shirika la afya duniani na kupendekeza kiwango asilimia 0.05% kwa dereva aliyebobea na asilimia 0.02% kwa dereva mchanga. 

Hivyo basi ni rai yetu kuwa sheria ifanyiwe marekebisho ili iendane na kiwango cha sasa cha kimataifa kilichofanyiwa utafiti,” alisisitiza Bi. Sanga. Aidha aliongeza kuwa adhabu zinazotolewa kwa sasa hazikidhi wala kuleta hofu kwa maderava wasiotaka kutii sheria na kanuni hivyo kuendelea kufifisha juhudi za kudhibiti tatizo la ajali za barabarani. “Mwendokasi umeendelea kuwa sababu kubwa ya ajali zinazogharimu uhai wa watu wengi. Sheria yetu inayo mapungufu kadhaa pamoja na juhudi nyingi za Jeshi la Polisi na wadau wengine kutaka kudhibiti jambo hili lemeendelea kuwa tatizo. 

Mfano Sheria ya usalama barabarani ya 1973 Kifungu cha 51(8) inatambua maeneo machache katika kuzuia mwendokasi, ni muhimu Sheria sasa itamke maeneo yote na si yale ya mjini tu au makazi, itamke wazi kuhusu maeneo ya shule, nyumba za ibada, maeneo ya michezo na mbuga za wanyama,” aliongeza Bi. Sanga katika taarifa hiyo. Pamoja na mambo mengine, alisema sheria ya sasa ipo kimya juu ya suala la vizuizi vya watoto katika vyombo vya moto hasa kwa magari binafsi na tumeendelea kushuhudia madhara makubwa katika ajali zilizohusisha watoto vikiwemo vifo.

 Hata hivyo mtandao huo umewasihi wananchi kuwa na taadhari pindi watumiapo vyombo vya moto bila kujali mapungufu yaliyopo kwenye sheria za usalama barabarani ili kupunguza matukio ya ajali. Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) usalama barabarani Mary Kessy, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari, alibainisha takwimu zinaonyesha takribani watu milioni 1.25 duniani hufariki kila mwaka; huku nchini Tanzania asilimia 76 ya ajali za barabarani husababishwa na uzembe wa madereva, asilimia 8 ubovu wa barabara na ubovu wa vyombo vya moto kuchangia ajali hizo kwa asilimia 16. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Ifikapo 2020: 

Kupunguza vifo na ajali za barabarani kwa asilimia 50%”. Mtandao wa Wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya Sheria za Sera zihusuyo usalama barabarani Tanzania unaundwa na asasi zifuatazo;- TAWLA, TAMWA, WLAC, TCRF, TLS, TMF, RSA, AMEND TANZANIA, SHIVYAWATA, TABOA pamoja na SAFE SPEED FOUNDATION.   Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (CRC) kilichoko ndani ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Gladness Munuo (kulia) akitoa maelezo kabla ya kuanza kwa mkutano huo. Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) usalama barabarani Mary Kessy (kulia) akizungumza katika mkutano huo. Wanahabari na wageni mbalimbali wakiwa katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani, ulioandaliwa na wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani. 
 Wanahabari na wageni mbalimbali wakiwa katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani, ulioandaliwa na wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani.[/caption] Imeandaliwa;www.thehabari.com

Wadau watakiwa kujitokeza kufadhili Tamasha la Watoto Chrismass

$
0
0
Mratibu wa Tamasha la watoto 'Baby Boxing Day 2017', 
na Mkurugenzi wa Linda Media Solution 
(LIMSO), Bi. Khadija Linda Kalili.
WAANDAAJI wa Tamasha la watoto litakalofahamika kwa jina la 'Baby Boxing Day 2017' wamewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini katika tamasha hilo ili kuweza kufanikisha hiyo ambayo imepangwa kufanyika Desemba mwaka huu (2017) Kibaha Mkoani Pwani.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari jana Mkurugenzi wa Linda Media Solution (LIMSO) ambaye pia ndiyo Mratibu tamasha hilo, Bi. Khadija Linda Kalili amesema kuwa siku hiyo itakuwa ni mahususi kwa ajili ya watoto kuanzia umri wa mwaka mwaka mmoja hadi umri wa miaka 17. "Tunategemea kuwa na watoto wenye umri kunzia siku moja hadi miaka 17 ambao sharti kubwa la kuwepo katika eneo husika lazima kila mtoto aambatane na mzazi, mlezi au mwangalizi wake pia kutakuwa na ulinzi wa kutosha katika kamati ya maandalizi kwa watakaofika siku hiyo.

Aidha Kalili amesema kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na michezo mbalimbali ambayo watoto watafurahia kwa kuzingatia umri wao ikiwemo. "Kwa mara ya kwanza Kibaha pamoja na viunga vyake nawaahidi kuandika historia mpya kutokana na kuwakumbuka watoto kwa aina katika siku hiyo, kwani hapo awali jamii imekuwa ikiwasahau watoto na kushindwa kuwakutanisha hasa katika kipindi hiki cha likizo.

"Tukumbuke watoto nao wanayo haki ya kukutana na kubadilishana mawazo kwani nao wanahitaji kukumbukwa katika masuala ya michezo na burudani hivyo kwa kulizingatia hilo tunatoa rai kwa wadhamini kujitokeza kufanikisha hili. LIMSO inawaahidi haitawaangusha," alisisitiza Bi. Linda Kalili.

Alisema ili kuleta upekee na mvuto wa siku ya tamasha wageni maalum waalikwa watakuwa ni watoto kutoka kwenye kituo kimoja wapo cha kulelea watoto yatima ambao watajumuika na wenzao siku hiyo.

MASAUNI AZINDUA ZOEZI LA USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA MARA

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wakati wa hafla iliyofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo, mkoani Mara.Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima.Kupitia zoezi hilo wananchi wa mkoa huo na wilaya zake watapata fursa ya kupata vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Masawe (katikati), wakishuhudia uchukuliwaji wa alama za vidole za mmoja wa wananchi waliofika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo, mkoani Mara kuandikishwa kwa ajili ya kupata kitambulisho cha utaifa. Kupitia zoezi hilo wananchi wa mkoa huo na wilaya zake watapata fursa ya kupata vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiingiza taarifa za muombaji wa kitambulisho cha Taifa, baada ya kuzindua zoezi la usajili wa vitambulisho hivyo leo Mkoani Mara.Kupitia zoezi hilo wananchi wa mkoa huo na wilaya zake watapata fursa ya kupata vitambulisho vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiakisi fomu ya taarifa za muombaji wa kitambulisho cha Taifa, baada ya kuzindua zoezi la usajili wa vitambulisho hivyo leo Mkoani Mara.Kupitia zoezi hilo wananchi wa mkoa huo na wilaya zake watapata fursa ya kupata vitambulisho vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Masawe (kulia),wakiteta jambo baada ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), kuzindua zoezi la usajili wa vitambulisho vya Taifa lililofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo,mkoani Mara.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakiwa tayari kuhudumia wananchi waliofika katika zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa baada ya kuzinduliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo,mkoani Mara. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMATATU LEO NOVEMBA 20,2017

MAKONDA ATOA MILIONI 10 KWA KAMPUNI YA MSAMA AUCTION MART KUSAIDIA KUTOKOMEZA UHARAMIA WA KAZI SANAA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa Shilingi Milioni 10 za Kitanzania kwa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart inayosimamia zoezi la kutokomeza kazi feki za sanaa nchini.

Kiasi hicho cha Pesa kimetolewa katika Kampuni hiyo ya Msama ili kuendesha vizuri mapambano dhidi ya wanaodurufu kazi hizo sehemu zote za jiji la Dar.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart, Alex Msama amesema kuwa Kampuni hiyo inamshukuru Mkuu huyo wa Mkoa kwa kufanya jambo kubwa na la mfano ambalo hakulitegemea.

"Sikutegemea kuona kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anawapenda Wasanii, baada ya kuniita na kuniambia kuwa kazi ninayoifanya ya kupigania haki za Wasanii ni nzuri", amesema Msama."Ameniita amenimbia kazi inaenda vizuri, kwani amejaribu kupita maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar wala haoni Kompyuta, CD Feki na ameona kila CD anayoishika ina Stika ya TRA", ameongeza Msama

Aidha, Msama ameendelea kusisitiza kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanafanya biashara yakuuza Kazi Feki za Sanaa waache kwa kutafuta kazi zakufanya.Pia amewaasa Wananchi kununua Filamu zenye Stika ya TRA inayong'aa vizuri, kwani watapofanya hivyo Wasanii hao watanufaika na kazi zao pamoja na kulipa Kodi kwa manufaa ya Taifa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart, Bw. Alex Msama akizungumza na Wanahabari mapema jana jijini Dar,akieleza taarifa ya Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam,Mh Paul Makonda kuongeza nguvu katika suala zima la kupambana na uharamia wa kazi sanaa hapa nchini,ambapo Mh Makonda amechangia milioni 10 kwa kampuni ya Msama Auction Mart ambayo inasimamia shughuli hizo za kupambana na Maharamia hao.

VIRTUAL ADVOCATE - A SOLUTION SET TO REVOLUTIONIZE OFFICE PRODUCTIVITY

$
0
0
Virtual Advocate Chief Executive Officer, Nzaro Kachenje (centre), addresses participants during the official launch of Virtual Advocate online document solutions application in Dar es Salaam yesterday. With him are, Virtual account manager, Asha Bura (right) and application’s administrator, Francis Lusinde. Application is said to cut down document processing time and operational costs by over 90 percent. 


‘Virtual Advocate’ is a revolutionary document solution platform that allows users to transform their frequently used documents and forms into intelligent templates, enabling super-fast production of tailor-made documents, increasing efficiency and productivity.

Departments such as legal, credit, human resources, sales and the like, whether in bank, real estate, insurance companies or education providers, can leverage from the myriad of benefits of the new platform.

By streamlining the documentation process, Virtual Advocate guarantees improved productivity by cutting down document processing time and operational costs by over 90 percent. The system reduces the need for multiple editing and dependency on lawyers and thus reduces costs and time spent.

Speaking to journalists, the CEO of Virtual Advocate, Mr Nzaro Kachenje, said that they found the existing traditional processes of drafting, monitoring and managing documents to be unnecessarily time consuming, costly, stressful and prone to errors. To counter this, they endeavored and succeeded to integrate modern technologies into the day-to-day documentation process to produce a robust, one stop center for most documentation needs, which they branded ‘Virtual Advocate’.

Pointing out a few key features of the system, Mr Kachenje said that the system has a dynamic dashboard, enabling quick real-time view of all activities in the system; a bulk document generation feature for the generation of similar documents to multiple addressees at once; a simplified user management module to control accesses of different users; a customer management module where all customer records are stored and easily accessible; and also security alerts to ensure no duplication of information in the system, which is best suited for Banks, as it would prompt the user if the Customer and/or the property pledged as security already exists in the system.

Virtual Advocate also offers complimentary support services such as round-the-clock customer service, training and consultancy to its clients.

Speaking on the novelty of the system, Mr Kachenje said that the system is first of its kind in East and Central Africa; and noted that they intend to export their revolutionary system to international markets, as their research has revealed a need for the product in all neighboring countries. He expressed jubilation to have pioneered such a technology that would put Tanzania in the limelight of innovation.





MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa kaongozana na Katibu Mkuu wake Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM  jijini 
Dar es salaam  leo Jumatatu Novemba 20, 2017
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa kaongozana na Katibu Mkuu wa chama hicho  Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM  jijini Dar es salaam  leo Jumatatu Novemba 20, 2017
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka sawa makabrasha kabla ya kuanza kwa  kikao cha Kamati Kuu ya CCM  jijini Dar es salaam  leo Jumatatu Novemba 20, 2017
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka sawa makabrasha kabla ya kuanza kwa  kikao cha Kamati Kuu ya CCM  jijini Dar es salaam  leo Jumatatu Novemba 20, 2017
  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  Ndugu Abdulrahman Kinana akithibitisha kutimia kwa akidi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam kinachoongozwa na Mwenyekiti wa
chama hicho Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu Novemba 20, 2017.



CHAMA CHA MBIO ZA MAGARI TANZANIA (AAT) CHAWAKUMBUKA WAATHIRIKA WA AJALI NA KUJADILIANA NA WADAU NAMNA YA KUZIPUNGUZA

$
0
0
Mgeni Rasmi Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Afande Deus Sokoni akifungua mjadala katika Siku ya Kukumbuka waathirika wa Ajali Duniani (The World Day Of Remembrance For Road Traffic Victims 19 November 2017) iliyoandaliwa na kufanyika kwenye ofisi za Chama Cha Mbio za Magari Tanzania AAT Upanga jijini Dar es salaam ikishirikisha wadau kutoka taasisi mbalimbali nchini Tanzania.

Wadau mbalimbali wamekutana na kujadiliana namna ya kupunguza ajali hasa katika kuzipitia sheria za usalama barabarani na kuzifanyia marekebisho pamoja na kuwakumbusha watumiaji wa Barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani, Taasisi zilizoshiriki katika mjadala huo ni WHO, KIkosi Cha Usalama Barabarani, SUMATRA, Chama Cha Mbizo za Magari Tanzania AAT, Chama cha Kutetea Abiria Tanzania CHAKUA, TIRA na wawakilishi Idara ya Habari Maelezo.
2
Mratibu wa Semina hiyo Bw. Alferio Nchimbi akizungumza katika semina hiyo na kukaribisha wadau mbalimbai ili kuchangia michango yao katika mada mbalimbali zilizowasilishwa.
3
Mgeni Rasmi Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Afande Deus Sokoni akisisitiza jambo wakati akijibu maswali katika semina hiyo kulia ni Mratibu wa Semina hiyo Bw. Alferio Nchimbi.
4
Bw. Monday Likwepa Katibu Mkuu wa Chama cha Kutetea Abiria akichangia mada katika semina hiyo.
5
Bi Mary Kessi Mratibu Programu ya Usalama Barabarani WHO akitoa mada katika semina hiyo iliyofanyika kwenye ofisi za Chama cha Mbio za Magari Tanzania (AAT) Upanga jijini Dar es salaam.
6
Afisa Leseni Mwandamizi kutoka SUMATRA Bw. Gabriel Anthony akitoa mada katika semina hiyo.
7
Daktari Bingwa wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura na Ajali Muhimbili Dk Juma Mfinanga akitoa ufafanuzi kwa upande wa hospitali ya Muhimbili wakati wa semina hiyo.
8
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semiha hiyo
910

MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO CHA MANJANO BEAUTY ACADEMY YAFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0
 
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema Akizungumza Machache wakati wa Mahafali  ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy .Ambapo amewataka Wanawake Kuchangamkia Fursa ya Urembo kwa kuwa ukuaji wake kwa sasa ni kubwa na inakabiliwa na Upungufu wa Wataalamu hivyo akiwashauri wanawake wengi Kujiunga na Kuiga Mambo Mazuri Yanayofanywa na Chuo cha Manjano Beauty Academy.Akieleza zaidi Alisema Sekta ya Urembo ina Fursa kubwa kwa Ajira kwa sasa,Katika Mahafali hayo  Wahitimu 120 Wametunukiwa vyeti katika  katika nyanja ya urembo.
Mwanzilishi wa Chuo cha  Manjano Beauty Academy Mama Shekha Nasser Akitoa Hotuba yake wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam.Mama Shekha Nasser Amewashukuru wazazi na walezi kwa kuwapeleka Watoto wao kwenye chuo hicho kwa LengoKupata Ujuzi wa Maswala ya Urembo,Aidha Ametaja Changamoto kubwa Alizokabiliana nazo wakati anaanzishi Chuo hicho Ikiwemo ukosefu wa Wataalamu wazawa wa Maswala ya Urembo.
 Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema Akiwa na Wageni Waalikwa wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy 
 Baadhi ya  Wahitimu waliotunukiwa kwenye Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam

 Mshauri wa Maswala ya Kisaikolojia Anti Sadaka Akitoa Neno la Shukrani kwenye Mahafali hayo
 Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema  Akitoa Cheti kwa Mmoja wa Wahitimu Kwenye  Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy..
 Mgeni Rasmi,Uongozi wa Chuo cha Manjano Bauty Academy ,Wageni waalikwa na Wahitimu Wakiwa katika Picha ya Pamoja 

Chuo cha Manjano Beauty Academy  kimetunuku Astashahada (Certificates) na Stashahada (Diploma) kwa wahitimu 120 wa kwanza wa chuo hicho katika nyanja ya urembo na utengenezaji wa nywele.Urembo na mitindo ni moja kati ya sekta zinazoajiri mamilioni ya wanawake kwa sasa, lakini bado sekta hiyo imeendelea kuwa isiyo rasmi.
Wanawake wengi wanaofanya kazi kwenye saluni hawana utaalamu, lakini ndiyo wanaofuatwa na wanaume na wanawake kwa ajili ya kutengenezwa mionekano inayovutia, wanaishi kwa kufanya kazi kubahatisha.


Akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya  Manjano Beauty Academy iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwanzilishi wa Manjano Beauty Academy, Shekha Nasser alisema kuwa maono hayo ndiyo yaliyosababisha yeye kuanzisha Manjano Beauty Academy.Manjano Beauty Academy ni shule kwa ajili ya afya na urembo ambayo ina lengo la kuwawezesha wasichana wa Kitanzania.
“Tunashauri, tunatoa mafunzo na kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya soko kwa kuwapatia ujuzi unaohitajika. Serikali haiwezi kuwaajiri wahitimu wote, hata sekta binafsi haiwezi kwa hivi sasa, kwa hiyo mafunzo haya yanawasaidia wasichana wadogo kuweza kujitengenezea soko kwenye sekta ya urembo,” alisema Shekha.Kwa mujibu wa Shekha, wasichana hao wamekuwa wakipewa mafunzo na wakufunzi bora wanaopatikana katika sekta ya urembo  ambayo yatawatasaidia wao kutimiza malengo yao binafsi pamoja na malengo ya kitaasisi.
 “Naamini kuwa wahitimu hawa watabadilisha sekta ya urembo hapa nchini, kama Korea na Filipino wanavyotambulika ulimwenguni kwa kuwa na bidhaa bora za ngozi na wataalam wa matibabu wenye weledi, huko mbeleni Tanzania itajulikana ni nchi inayotoa bidhaa bora za urembo kwa ngozi za Kiafrika, kuanzia bidhaa za urembo wa uso zinazozalishwa kutokana na Mwani wa baharini toka Zanzibar mpaka bidhaa za poda ambazo zina virutubisho vya Manjano ya asili na vyakutosha,” alisema Shekha ambaye pia ni mwanzilishi wa Shear Illusions.
Mwaka 2015, kupitia bidhaa za LuvTouch Manjano, Shekha alizindua kampeni inayoitwa Manjano Dream Makers iliyokuwa na lengo la kuwawezesha wasichana wenye mafunzo ya kijasiriamali kujikwamua kiuchumi ili kutimiza ndoto zao.
“Katika miaka miwili tangu kuanzishwa kwa taasisi ya Manjano, mtandao wa wanawake wa Manjano Dream-Makers umeweza kuenea katika majiji na miji Saba nchini na kuwasaidia kutengeneza ajira na kutengeneza kipato kwa kuuza bidhaa zao kupitia mfumo wa nyumba kwa nyumba kwa wanawake wasio na ajira,” alisema Shekha. 

Aliongeza kuwa, “Leo tunajivunia kuwa na wasichana 360 katika mtandao wa ‘Manjano Dream-Makers’ wenye matumaini ya kuboresha maisha yao na familia zao kwa kuuza bidhaa za LuvTouch Manjano.

Balozi wa Tanzania nchini Shelisheli awasilisha Hati za Utambulisho

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Shelisheli mwenye makazi yake nchini Kenya, Mhe. Dkt. Pindi Chana akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Mhe. Danny Faure. Makabidhiano hayo yalifanyika tarehe 14 Novemba 2017, katika Ikulu ya nchi hiyo. 
Mhe. Balozi Chana akizungumza na Mhe. Rais Faure ambapo Serikali ya Jamhuri ya Shelisheli imemuhakikishia kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake. 
Mhe. Balozi Chana akiwasili katika Ikulu ya Jamhuri ya Shelisheli.

Mkurugenzi Mkazi wa USAID bwana Andy Karas atembelea walengwa wa TASAF mkoani Iringa.

$
0
0
Na Estom Sanga – Iringa

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekani –USAID-bwana Andy Karas amepongeza jitihada za serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika kuwafikia wananchi wanaokabiliwa na umasikini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ambao umeanza kuonyesha mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali nchini, jambo linalovutia wadau wa maendeleo kuendelea kusaidia jitihada hizo.

Bwana Karas ameyasema hayo alipokutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli katika halmashauri ya Wilaya ya Iringa ,mkoani Iringa ambako licha ya kuelezwa namna TASAF inavyoendelea kutekeleza Mpango huo, lakini pia alishuhudia namna walengwa wa mpango huo walivyoboresha maisha yao kwa kutumia fedha za ruzuku za mfuko huo.

Amesema hamasa inayoonyeshwa na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kujiletea maendeleo kwa kuanzisha miradi midogo midogo kwa kutumia fedha zinazotolewa na Serikali kupitia TASAF, imelivutia Shirika hilo na kuahidi kuwa litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuboresha utaratibu wa kuwainua wananchi kiuchumi .

Bwana Karas amesema utaratibu wa kuwafikia na kuwasaidia moja kwa moja wananchi wanaoishi katika mazingira magumu ya kiuchumi umekuwa ukitumika katika nchi nyingi duniani na umeonyesha mafanikio makubwa kwa kusisimua shughuli za kiuchumi na kijamii kwa kaya masikini .

Aidha Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID amevutiwa na masharti ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kupitia TASAF hususani katika nyanja za elimu, afya, lishe na uwekezaji kwenye shughuli za kiuchumi kwa walengwa wa Mpango huo kuwa umeamusha ari ya kutokomeza umasikini miongoni mwao.

Akiwa katika kijiji hicho cha Igingilanyi kata ya Nduli bwana Karas alitembelea baadhi ya kaya za Walengwa wa TASAF na kujionea namna walivyonufaika na ruzuku ya Mpango huo kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya ufugaji wa kuku na nguruwe na kutumia sehemu ya mapato yao kuboresha makazi kwa kujenga nyumba za matofali na kuezeka kwa mabati.

“ni jambo jema sana mnalolifanya kwa kuwekeza katika elimu ya watoto wenu na kuboresha makazi yenu kwa kutumia ruzuku mnayoipata” alisisitiza bwana Karas.

Bwana Karas pia alionyesha kuvutiwa na utaratibu wa kuanzisha vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana unaofanywa na Walengwa wa Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini ambao alisema ukiimarishwa utatoa fursa kubwa zaidi kwa wananchi hao kukuza shughuli zao za kiuchumi kwa kukopeshana kwa riba ndogo ikilinganisha na ile inayotozwa na taasisi za kibenki.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Miradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF,Bwana Amadeus Kamagenge alimweleza Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID kuwa licha ya Serikali kupitia Mfuko huo kuendelea kutoa ruzuku kwa Kaya Masikini sana katika mikoa yote nchni ,hivi sasa umeanza kujikita zaidi katika kuhamasisha walengwa kuanzisha vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana kwa kuwatumia wataalamu walioko kwenye maeneo yao wakiwemo Maafisa wa Maendeleo ya Jamii, kilimo, Mifugo na biashara ili waweze kuboresha shughuli za kiuchumi kwa walengwa.

“Mkakati huo umeanza kuonyesha mafanikio kwa kuwaongezea walengwa kwa Mpango huo kipato na kuwapa uwezo wa kubuni na kusimamia kwa ufanisi miradi yao midogo midogo wanayoianzisha.

Hata hivyo bwana Kamagenge amesema mafanikio yaliyoanza kupatikana kwa kaya za walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini yameibua kilio kutoka kwa kaya nyingine ambazo hazikuingizwa kuingizwa kwenye Mpango huo kutaka nazo pia zijumuishwe kwenye utaratibu huo. Hadi sasa TASAF inatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika vijiji 9,835 ambayo ni sawa na asilimia 70 ya vijiji na shehia zote Tanzania bara na Zanzibar.


Mkurugenzi M kazi wa Shirika la Misaada la Marekani –USAID-bwana Andy Karas (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa walenwa wa TASAF katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli wilaya ya Iringa baada ya kutembelea nyumba aliyoijenga mlengwa huyo (nyuma yao ) baada ya kupata ruzuku kutoka TASAF.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani USAID bwana Andy Karas akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF katika kijiji cha Igingilanyi wilaya ya Iringa Vijijini ambako akutana na walengwa wa Mpango huo kuona namna wanavyonufaika na Mpango huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID bwana Andy Karas akisoma taarifa kwenye mkutano wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli wilaya ya Iringa Vijijini ambako alitembelea kuona namna walengwa wa Mpango huo wanavyonufaika na ruzuku inayotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.
Baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi wilaya ya Iringa Vijijini wakiwaburudisha wageni kutoka Shirika la Misaada la Marekani –USAID waliotembelea kijiji hicho kuona shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF .
Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani Bwana Andy Karas akisalimiana na mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli wilaya ya Iringa Vijijini wakati alipotembelea kijiji hicho.Katikati yao ni Mkurugenzi wa miradi wa TASAF bwana Amadeus Kamagenge.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images