Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

Malima atembelea Kiwanja cha ndege cha Musoma

$
0
0
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma, Bi. Betha Bankwa akitoa maelezo mbalimbali kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Kigoma Malima (wa pili kulia) jana Ijumaa alipofanya ziara kwenye kiwanja hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Kigoma Malima (aliyenyoosha mkono), akielekeza jambo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma, Bi. Betha Bankwa jana  alipotembelea kiwanjani hapo

WAJASIRIAMALI WAASWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA MTANDAONI KUKUZA BIASHARA ZAO

$
0
0
 Wajasiriamali wa nchi za Afrika ya Mashariki wametakiwa kuitumia ipasavyo fursa ya kuenea na kukua kwa matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ili kuendana na kasi ya mapinduzi ya biashara duniani kote.
Hayo yalisemwa kwenye semina kuhusu “Biashara za Mtandaoni” ikiwa na lengo la ‘kuongeza ufikiaji wa soko na kukuza mbinu za kibiashara kupitia mtandaoni,’ katika mkutano wa pili wa Maonyesho ya Afrika ya Mashariki ya Biashara na Ujasiriamali mwaka 2017 (EABECE) uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 14 mpaka Novemba 16.

Akizungumza kama mmojawapo wa jopo la wazungumzaji wakati wa semina hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Jumia Tanzania, kampuni ambayo inajihusisha na biashara ya manunuzi na uuzaji wa bidhaa mtandaoni, Bw. Albany James amesema kuwa changamoto kubwa wanayopambana nayo kwa sasa ni kuhakikisha kwamba inawashawishi wafanyabiashara wote kuhamia kwenye mfumo wa mtandaoni ili kuwafikia wateja wengi zaidi.
“Kikubwa tunachokifanya ni kuwakutanisha wauzaji wa bidhaa mbalimbali na wateja mtandaoni. Kupitia uwekezaji mkubwa wa teknolojia tulioufanya, tumedhamiria kuwapatia wauzaji na wanunuaji urahisi mkubwa sawasawa na kama wanavyokwenda madukani,” alisema na kuhitimisha Bw. James, “Tunafahamu kwamba kwenye biashara ili kufikia soko kwa urahisi ni lazima uwajue wateja wako na namna ya kuwafikia ambapo mara nyingi ni kwa njia ya matangazo. Lakini sio wafanyabiashara wote wanaweza kulimudu ukizingatia wengi ndio wanaanza na hawana mitaji au faida kubwa ya kuwekeza kwenye matangazo. Hivyo basi, Jumia tunachokifanya ni kuwapatia fursa ya kujitangaza kwa njia ya mtandao bila ya gharama yoyote kwani ndipo kwenye idadi kubwa ya watu kwa hivi sasa.”  
Naye kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Umma na Masoko wa Jumia Travel Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey, kampuni dada ya Jumia Tanzania ambayo yenyewe inajihusisha na utoaji wa huduma za hoteli mtandaoni nchini na barani Afrika kwa ujumla, ameongezea kuwa fursa iliyopo kwa wafanyabiashara kuhamia mtandaoni ni kubwa na haina gharama kama wengi wanavyofikiri.
“Wafanyabishara wengi bado ni waoga wa kutumia teknolojia kwenye kukuza na kurahisisha biashara zao. Ripoti zinaonyesha kwamba Tanzania ni mojawapo ya nchi 20 zenye uchumi unaokua kwa kasi duniani ambao kwa kiasi kikubwa unachangiwa na sekta za utalii, ujenzi, fedha na biashara ukiacha na nyinginezo. Lakini kikubwa zaidi ni ukuaji wa TEHAMA ambapo takwimu zinaonyesha 40% ya watanzania wamefikiwa na mtandao wa intaneti ambapo wameongezeka na kufikia milioni 19.86 mwaka 2016 kutoka milioni 17.26 mwaka 2015. Takwimu hiyo pia imechochea kuongezeka kwa watumiaji wa simu za mkononi na kufikia milioni 40.17 mwaka 2016,” alisema Bw, Geofrey.
“Hilo ni sawa na ongezeko la 0.9% kwa mwaka na ukuaji wa ueneaji kwa 83% kwenye nchi yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 50. Hii ni dhahiri kwamba kuna mustakabali mkubwa kwa ukuaji wa biashara za mtandaoni kwenye sekta mbalimbali. Kwa sasa mawasiliano ya simu ni mojawapo ya sekta zinazokua kwa kasi nchini Tanzania na inatoa mchango mkubwa katika kuwaunganisha watanzania kwenye mfumo wa kifedha. Kwa kuongezea, idadi ya watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya simu nayo imeongozeka na kufikia milioni 18.08 mwaka 2016 kutoka milioni 17.63 mwaka 2015. Hizi zote ni ishara kwamba watanzania wapo tayari kwa biashara za mtandaoni kitaalamu na kisaikolojia,” alihitimisha Meneja huyo wa Uhusiano wa Umma na Masoko wa Jumia Travel Tanzania.
Akitoa maoni yake wakati wa semina hiyo mmoja wa washiriki, Bi. Isabella Mwampamba ambaye mbali na kuwa ni mjasiriamali lakini pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Upendo Friends iliyopo jijini Arusha, amesema kuwa wanawake wengi ni waoga wa kutumia teknolojia za mtandaoni zilizopo sasa kitu ambacho kinawaacha nyuma na kuwanyima fursa nyingi.

“Mimi kama mmojapo wa wanawake wajasiriamali nchini Tanzania ningependa kusema kuwa wengi miongoni mwetu ni waoga wa kutumia teknolojia za kisasa. Kwa mfano, wengi tunaogopa hata kutumia simu za kisasa ambazo ni rafiki na mifumo ya mtandaoni! Lakini kwa upande mwingine sio makosa yetu kwani tunakosa mafunzo ya kitaalamu ya namna ya kuzitumia,” alisema Bi. Mwampamba na kuhitimisha, “Hivyo basi ningependa kutoa wito kwa wanawake na wajasiriamali wenzangu kwamba tuanze kuzitumia teknolojia hizi zilizopo sasa kwani zitatufungua zaidi na kuongeza tija kwenye biashara zetu. Lakini pia natoa wito kwa makampuni ambayo yanajihusisha na sekta hii kuwakusanya na kutoa mafunzo ya mara kwa mara juu ya namna biashara za mtandaoni zinazofanya kazi.”
Mkutano wa Maonyesho ya Afrika ya Mashariki ya Biashara na Ujasiriamali mwaka 2017 (EABECE) unalenga kutoa fursa kwa kuzikutanisha sekta za biashara na wenzao kwenye biashara pamoja na serikali na sekta za biashara. Ni jukwaa linalowakutanisha kwa pamoja wafadhili wa kifenda na wavumbuzi kwa lengo la kuimarisha ujasiriamali katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambapo mwaka jana ulifanyika Oktoba 10 mpaka 13 jijini Nairobi, Kenya.   

MAJALIWA:MWENENDO WA UKUAJI UCHUMI WA TAIFA UNARIDHISHA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mwenendo wa ukuaji wa uchumi wa Taifa unaridhisha, ambapo katika robo ya kwanza ya mwaka 2017 ulikua kwa asilimia 5.7.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Novemba 17, 2017) wakati akisoma hotuba ya kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Bunge, mjini Dodoma.

“Mwenendo wa uchumi wetu ni wa kuridhisha, mfano, ukuaji wa uchumi katika robo ya kwanza ya mwaka 2017 ulikua kwa asilimia 5.7, robo ya pili ilikuwa asilimia 7.8 na nusu ya kwanza ya mwaka huu ilikuwa ni asilimia 6.8.”

Amesema hali hiyo inafuatia kuongezeka kwa makusanyo ya kodi na usimamizi thabiti wa matumizi ya Serikali, ambapo nakisi ya bajeti ya Serikali imeshuka na kufikia asilimia 1.9 kwa mwaka 2016/2017

Pia amesema akiba ya fedha za kigeni inatosheleza kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi kwa zaidi ya kipindi cha miezi mitano, ikiwa ni zaidi ya lengo la miezi minne.

Akizungumzia kuhusu kasi ya upandaji bei, Waziri Mkuu amesema takwimu zinaonyesha kwamba katika nusu ya mwaka 2017, mfumuko wa bei uliendelea kubaki katika kiwango cha tarakimu moja. 

“Takwimu zinaonyesha kwamba mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Oktoba 2017 ulikuwa ni asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilima 5.3 mwezi Septemba, 2017.”

Amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kumechangiwa na kupungua kwa bei wa bidhaa za vyakula, ambavyo vimepungua kutoka wastani wa asilimia 9.3 mwezi Septemba, 2017 hadi asilimia 8.8 mwezi Oktoba, 2017.


Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii ianzishe Mamlaka ya Fukwe za Bahari na Maziwa ili kutangaza na kuendeleza fukwe ambazo hazina shughuli.

Amesema fukwe za bahari ni eneo mojawapo ambalo likiendelezwa vizuri, linaweza kuwa kichocheo kikubwa cha kukuza uchumi, hivyo ni lazima zipewe kipaumbele.

Pia ametoa wito kwa wizara hiyo iongeze kasi ya kuleta mabadiliko katika sekta nzima ya maliasili ili iweze kuchangia zaidi kwenye uchumi. 

Ametolea mfano Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambayo imefanikiwa kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni 60.1 mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi bilioni 102 mwaka 2016/2017.

Waziri Mkuu amesema ongezeko hilo la mapato limekuja baada ya Serikali kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa kutumia njia ya kielektroniki.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, NOVEMBA 17, 2017.

KAMPUNI YA BLUE COAST INVESTMENT YACHANGIA MADAWATI 200

$
0
0
Madawati mia mbili ambayo yametolewa na kampuni ya Blue coast Investment iliyopo Mkoani Geita kwa lengo la kusaidia mahitaji ya elimu.
Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimshukuru mkurugenzi wa kampuni
ya Blue coast Investment ,Bw Athanas Inyasi ambaye yupo katika kwa kujitolea yeye na kampuni yake kutoa madawati kwenye halmashauri ya mji na wa kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola. 
mkurugenzi wa kampuni ya Blue coast Investment ,Bw Athanas Inyasi akimkabidhi mkuu wa Wilaya madawati mia mbili ambayo ameyatoa. 
Mkuu wa Wilaya ya Geita.,Mwl Herman Kapufi akipokea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita,wakati wa zoezi la kukabidhiwa madawati mia mbili.(PICHA NA JOEL MADUKA) 

HATI ZA KUMILIKI ARDHI KUTOLEWA NDANI YA SIKU 30 TANGU KUPOKELEWA KWA MAOMBI

$
0
0
Na. Frank Mvungi - MAELEZO, Dodoma

Serikali imeanza kutoa Hati za kumiliki ardhi ndani ya Kipindi cha Siku 30 tangu kupokelewa kwa maombi tofauti na awali ambapo mchakato wa kupata hati hizo ulichukua zaidi ya siku 90 ikiwa ni matokeo ya mikakati madhubuti iliyowekwa ili kuondoa changamoto zinazoikabili sekta ya ardhi hapa nchini.

Akizungumza katika kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kuratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO), Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa kila kipande cha Ardhi kinapimwa na kumilikishwa.

“Tumejipanga vizuri na sasa taarifa zote za Ardhi zitakuwa katika mfumo wa kielektroniki utakaounganisha taarifa za nchi nzima hivyo tutaweza kudhibiti vitendo vyote vilivyokuwa vikifanyika awali kinyume na utaratibu na kuchochea kuongezeka kwa migogoro ya Ardhi hapa nchini,” alisisitiza Lukuvi

Ameendelea kwa kusema, hatua zinazochukuliwa na Serikali ni pamoja na kutenga muda wa kuwasikiliza wananchi na kuzipatia ufumbuzi chanagamoto zinazowakabili ikiwemo kudhulumiwa viwanja ambapo Serikali imekuwa ikirudisha umiliki kwa wananchi husika pale inapojiridhisha kuwa ndiye mmiliki halali wa eneo husika.

Aliongeza kuwa, mapato ya Serikali yemeongezeka kutoka milioni 46 hadi Bilioni 100 kwa mwaka ikiwa ni kodi ya Ardhi. Aidha, kuongezeka kwa mapato hayo kumetokana na usimamizi madhubuti wa Serikali katika sekta ya ardhi hapa nchini ili kuwapa wananchi wote fursa yakutumia ardhi na kujiletea maendeleo.

Vile vile amesema, hatua nyingine zinazochukuliwa na Serikali ni pamoja na kuanzisha ofisi za Kanda zitakazokuwa zikitekeleza majukumu yanayotekelezwa na wizara ikiwemo kutoa hati ili kusogeza huduma kwa wananchi hasa wanyonge waliopo Vijjini ambao mara nyingi hushindwa kusafiri hadi makao makuu ya Wizara kufuata huduma hizo.

Pia Lukuvi alibainisha kuwa Serikali imenunua vifaa vya upimaji ardhi vitakavyotumika katika Ofisi za Kanda ili kuwawezesha watumishi wake kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hali itakayosaidia sekta hiyo kutoa mchango mkubwa katika kujenga uchumi.

“Hati za Kimila elfu 46,000 zimeshatolewa kwa wananchi ili kuwawezesha kuwa na milki salama ambazo zitachochea maendeleo katika maeneo yao kwani zinaongeza thamani ya ardhi ya eneo husika, vile vile maeneo ya makazi zaidi ya 200,000 yametambuliwa na kurasimishwa,” alisisitiza Lukuvi

Aidha Mhe. Lukuvi amewaasa wamiliki wa mashamba makubwa kuyaendeleza vinginevyo Serikali itayatwaa na kuyamilikisha kwa wananchi ili wayatumie kwa shughuli za uzalishaji ambapo kwa sasa mashamba makubwa zaidi ya 150 yamefutiwa umiliki na kurudishwa kwa wananchi.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ni moja ya Sekta muhimu katika kujenga uchumi wa Viwanda na imekuwa ikichukua hatua mahususi katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya Ardhi. Hatua hizo zinajumuisha ujenzi wa Kanzi Data ya taarifa za ardhi kwa nchi nzima na pia kuunganisha mifumo yake na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kuimarisha mchango wa sekta hiyo katika kujenga uchumi wa viwanda.






WAJASIRIAMALI WAASWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA MTANDAONI KUKUZA BIASHARA ZAO

$
0
0
WAJASIRIAMALI wa nchi za Afrika ya Mashariki wametakiwa kuitumia ipasavyo fursa ya kuenea na kukua kwa matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ili kuendana na kasi ya mapinduzi ya biashara duniani kote.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungan wa Tanzania, Samia Hassan Suluhuakizungumza na baadhi ya wajasiliamali wa Afrika mashariki.


Hayo yalisemwa kwenye semina kuhusu “Biashara za Mtandaoni” ikiwa na lengo la ‘kuongeza ufikiaji wa soko na kukuza mbinu za kibiashara kupitia mtandaoni,’ katika mkutano wa pili wa Maonyesho ya Afrika ya Mashariki ya Biashara na Ujasiriamali mwaka 2017 (EABECE) uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 14 mpaka Novemba 16.

Akizungumza kama mmojawapo wa jopo la wazungumzaji wakati wa semina hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Jumia Tanzania, kampuni ambayo inajihusisha na biashara ya manunuzi na uuzaji wa bidhaa mtandaoni, Bw. Albany James amesema kuwa changamoto kubwa wanayopambana nayo kwa sasa ni kuhakikisha kwamba inawashawishi wafanyabiashara wote kuhamia kwenye mfumo wa mtandaoni ili kuwafikia wateja wengi zaidi.
Baadhi y washiriki wa semina kuhusu “Biashara za Mtandaoni” ikiwa na lengo la ‘kuongeza ufikiaji wa soko na kukuza mbinu za kibiashara kupitia mtandaoni.

“Kikubwa tunachokifanya ni kuwakutanisha wauzaji wa bidhaa mbalimbali na wateja mtandaoni. Kupitia uwekezaji mkubwa wa teknolojia tulioufanya, tumedhamiria kuwapatia wauzaji na wanunuaji urahisi mkubwa sawasawa na kama wanavyokwenda madukani,” alisema na kuhitimisha Bw. James, “Tunafahamu kwamba kwenye biashara ili kufikia soko kwa urahisi ni lazima uwajue wateja wako na namna ya kuwafikia ambapo mara nyingi ni kwa njia ya matangazo. Lakini sio wafanyabiashara wote wanaweza kulimudu ukizingatia wengi ndio wanaanza na hawana mitaji au faida kubwa ya kuwekeza kwenye matangazo. Hivyo basi, Jumia tunachokifanya ni kuwapatia fursa ya kujitangaza kwa njia ya mtandao bila ya gharama yoyote kwani ndipo kwenye idadi kubwa ya watu kwa hivi sasa.”  
 Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wa wajasiliamali wa nchi za AfrikaMashariki ambao ulikuwa unahusu wajasiriamali hao kutumia Tehama katika ufanyaji wao wa kazi.

Naye kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Umma na Masoko wa Jumia Travel Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey, kampuni dada ya Jumia Tanzania ambayo yenyewe inajihusisha na utoaji wa huduma za hoteli mtandaoni nchini na barani Afrika kwa ujumla, ameongezea kuwa fursa iliyopo kwa wafanyabiashara kuhamia mtandaoni ni kubwa na haina gharama kama wengi wanavyofikiri.
Katikati ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungan wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu akiwa katika mkutan uliowakutanisha wajasiliamali wa Afrika Mashariki. Kulia ni Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

“Wafanyabishara wengi bado ni waoga wa kutumia teknolojia kwenye kukuza na kurahisisha biashara zao. Ripoti zinaonyesha kwamba Tanzania ni mojawapo ya nchi 20 zenye uchumi unaokua kwa kasi duniani ambao kwa kiasi kikubwa unachangiwa na sekta za utalii, ujenzi, fedha na biashara ukiacha na nyinginezo. Lakini kikubwa zaidi ni ukuaji wa TEHAMA ambapo takwimu zinaonyesha 40% ya watanzania wamefikiwa na mtandao wa intaneti ambapo wameongezeka na kufikia milioni 19.86 mwaka 2016 kutoka milioni 17.26 mwaka 2015. Takwimu hiyo pia imechochea kuongezeka kwa watumiaji wa simu za mkononi na kufikia milioni 40.17 mwaka 2016,” alisema Bw, Geofrey.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungan wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu  akizungumza katika semina ya wajasiriamali.
 
“Hilo ni sawa na ongezeko la 0.9% kwa mwaka na ukuaji wa ueneaji kwa 83% kwenye nchi yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 50. Hii ni dhahiri kwamba kuna mustakabali mkubwa kwa ukuaji wa biashara za mtandaoni kwenye sekta mbalimbali. Kwa sasa mawasiliano ya simu ni mojawapo ya sekta zinazokua kwa kasi nchini Tanzania na inatoa mchango mkubwa katika kuwaunganisha watanzania kwenye mfumo wa kifedha. Kwa kuongezea, idadi ya watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya simu nayo imeongozeka na kufikia milioni 18.08 mwaka 2016 kutoka milioni 17.63 mwaka 2015. Hizi zote ni ishara kwamba watanzania wapo tayari kwa biashara za mtandaoni kitaalamu na kisaikolojia,” alihitimisha Meneja huyo wa Uhusiano wa Umma na Masoko wa Jumia Travel Tanzania.
Akitoa maoni yake wakati wa semina hiyo mmoja wa washiriki, Bi. Isabella Mwampamba ambaye mbali na kuwa ni mjasiriamali lakini pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Upendo Friends iliyopo jijini Arusha, amesema kuwa wanawake wengi ni waoga wa kutumia teknolojia za mtandaoni zilizopo sasa kitu ambacho kinawaacha nyuma na kuwanyima fursa nyingi.

“Mimi kama mmojapo wa wanawake wajasiriamali nchini Tanzania ningependa kusema kuwa wengi miongoni mwetu ni waoga wa kutumia teknolojia za kisasa. Kwa mfano, wengi tunaogopa hata kutumia simu za kisasa ambazo ni rafiki na mifumo ya mtandaoni! Lakini kwa upande mwingine sio makosa yetu kwani tunakosa mafunzo ya kitaalamu ya namna ya kuzitumia,” alisema Bi. Mwampamba na kuhitimisha, “Hivyo basi ningependa kutoa wito kwa wanawake na wajasiriamali wenzangu kwamba tuanze kuzitumia teknolojia hizi zilizopo sasa kwani zitatufungua zaidi na kuongeza tija kwenye biashara zetu. Lakini pia natoa wito kwa makampuni ambayo yanajihusisha na sekta hii kuwakusanya na kutoa mafunzo ya mara kwa mara juu ya namna biashara za mtandaoni zinazofanya kazi.”
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia  Suluhu akiwa katika Picha ya pamoja.
 
Mkutano wa Maonyesho ya Afrika ya Mashariki ya Biashara na Ujasiriamali mwaka 2017 (EABECE) unalenga kutoa fursa kwa kuzikutanisha sekta za biashara na wenzao kwenye biashara pamoja na serikali na sekta za biashara. Ni jukwaa linalowakutanisha kwa pamoja wafadhili wa kifenda na wavumbuzi kwa lengo la kuimarisha ujasiriamali katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambapo mwaka jana ulifanyika Oktoba 10 mpaka 13 jijini Nairobi, Kenya.  

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WATOTO NJITI DUNIANI.

$
0
0
 Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mh,Maudline Cyrus Castico akibeba Watoto Njiti katika Maadhimisho ya mtoto  Njiti Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
  Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee , Vijana ,Wanawake na Watoto Maudline Castico akizinduwa Kitabu cha huduma muhimu kwa Watoto Wachanga wakati wa Maadhimisho ya watoto Njiti yaliyofanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni (kushoto) Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman na wapili (kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdalla.

Na Kijakazi Abdalla - Maelezo Zanzibar.  17/11/2017.
WAZIRI wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mh. Maudline Cyrus Castico amesema kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa kabla ya kufika wakati (watoto njiti) Zanzibar imeongezeka kutoka 206  mwaka 2016 hadi kufikia 335 kwa mwaka 2017.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto njiti Duniani huko ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni, Waziri Castico alisema kuwa idadi hiyo ni ya kutisha hivyo jamii inapaswa kufanya juhudi kupunguza tatizo hilo .

Alisema ongezeko hilo la watoto njiti limekuwa likisababisha vifo vingi vya watoto wachanga hasa ndani ya siku saba za awali baada ya kuzaliwa.

Aliipongeza Wizara ya Afya kwa  kuchukuwa juhudi kubwa za kuboresha huduma za afya kwa mama na watoto ambapo hivi sasa huduma hizo  zinapatikana kila pahala mijini na vijijini.

Alizitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na kuongeza wataalamu na vifaa muhimu za kuhudumia mama wajawazito  na wakati wa kujifunguwa pamoja na kusisitiza umuhimu wa kunyonyesha ziwa la mama pekee kwa muda wa miezi sita.

Hata hivyo alisema kuwa katika kuhakikisha huduma hizo zinaboreshwa kwa watoto njiti, Wizara imefanikiwa kutoa mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi wanaoshughulikia watoto hao na kwa wazazi.

Alisema jumla ya wafanyakazi 300 wamepatiwa huduma za watoto njiti Unguja na Pemba ili kuhakikisha watoto hao wanakuwa katika mazingira ya afya bora.

Mapema Naibu Waziri wa Afya Harusi Said  Suleiman amesema kuwa sababu kubwa zinazopelekea kuzaliwa  watoto njiti ni pamoja na  msongo wa mawazo wakati wa ujauzito, kujifungua katika umri mdogo chini ya miaka 20 na umri mkubwa zaidi ya miaka 40.

Aliwataka kinababa kuongeza mapenzi  kwa wake zao wakati wa ujauzito na kuacha kuwatelekeza ili kumpa nafasi kujifungua akiwa salama na mtoto mwenye afya nzuri.

“Kuna baadhi ya kinababa wanapogundua  wake zao  wanaujauzito  huona ndio fursa ya kutafuta mke mwengine na kumuongezea mke mkubwa matatizo zaidi,’’ alisema Naibu Waziri wa Afya.

Alisema kizazi cha mtoto njiti ni kizazi hai ambacho kinazaliwa kabla ya kutimia umri wa kuzaliwa hivyo ni muhimu kwa wazazi wote wawili kushirikiana katika malezi kuhakikisha kinakuwa vizuri.

Nao wazazi wenye watoto  Njiti wamewashukuru wafanyakazi wa Wizara ya Afya kwa huduma wanazozipata wakati wanapofika vituoni jambo ambalo linawapa faraja ya kuendelea kuwalea watoto wao katika misingi mizuri. 

Hata hivyo wamesema wapo baadhi ya watu wanaona kuzaa mtoto akiwana hali kama hiyo  ni mitihani jambo ambalo  linawatia huzuni  sana  hivyo  wameitaka  jamii kuondokana na dhana hiyo.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO   ZANZIBAR

CLOUDS TV yapewa tuzo ya Kituo Bora cha Televisheni 2017

$
0
0
Umoja wa Mataifa kupitia Umoja wa Vijana (YUNA) umetoa tuzo kwa Taasisi na watu binafsi wenye mchango mkubwa katika maisha ya watu barani Afrika.Kupitia tuzo hizo zinazotambulika kama PAHA, kituo cha Televisheni cha Clouds kimetambuliwa kama kituo bora cha Runinga kwa mwaka 2017.
Hiyo ni kutokana na kurusha maudhui yanayomulika maisha ya watu na kutoa tumaini kwao kupitia vipindi na kampeni mbalimbali kama vile...
(#IshiNaMimi #Kipepeo #MalkiaWaNguvu #RudishaTabasamuMiaMoyo na nyinginezo).

Baada ya kupokea tuzo hiyo ya heshima Kampuni ya Clouds Media Group imeishukuru YUNA pamoja na umoja na umoja wa mataifa kutokana na Utambuzi huo.

Sambamba na hilo Clouds Tv imewashukuru Watanzania Kwa kuendelea Kuwaamini na Kuwachagua." Tunaahidi kuendelea kuwatumikia kwa moyo na nguvu zaidi kwani tulishakula kiapo cha kuwa Taasisi ya watu" sehemu ya taarifa hiyo ilieleza.
(#RedioYaWatu #ThePeoplesStation).
#TunakufunguliaDuniaKuwaUnachotaka


SERIKALI YA BURUNDI YANUIA KUWAREJESHA WANANCHI WAKE WALIOKIMBILIA TANZANIA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi wa Tanzania, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika mkutano na wakimbizi wa Burundi wanaoishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Marco Gaguti, akizungumza katika mkutano na wakimbizi wa Burundi wanaoishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.
Mkimbizi wa Burundi anayeishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma Paul Ndalaizye., akitoa maoni kwa niaba ya wakimbizi wanaoishi katika kambi hiyo wakati wa Mkutano uliohutubiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye (hawapo pichani), lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo nchini Burundi, Pascal Barandagiye (kulia), wakipiga ngoma baada ya kuwasili katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, iliyoko Wilayani Kasulu,mkoani Kigoma.
Wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) katika mkutano na wakimbizi hao, Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.


Serikali ya Jamhuri ya Burundi imesema ipo tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kuhakikisha zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi waliopo nchini Tanzania wanarejea nchini Burundi kwa haraka ili wakaijenge nchi yao. Haya yamezungumza na Waziri wa mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo kutoka Jamhuri ya Burundi Mhe. Pascal Barandagiye, alipozuru katika kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtendeli kutoa ujumbe wa kuwaasa kurejea wakimbizi nchini kwao Burundi.

Tangu zoezi la urejeaji wa wakimbizi lilipoanza mwezi septemba 2017 kwa awamu ya kwanza jumla ya wakimbizi 8347 wameshasaidiwa kurejea nchini kwao Burundi sawa na asilimia 100.3 ya lengo ya urejeshwaji kwa awamu ya kwanza. Aidha, mwanzoni mwa mwezi Novemba wakimbizi wapatao 33,948 walijiandikisha kurejea nchini kwao Burundi lakini kutokana na kasi ndogo na taratibu ndefu zinazofanywa na Shirika la kuhudumia wakimbizi Duniani UNHCR wakimbizi waliojiandikisha wameanza kusitisha nia yao ya kurejea kwani hawaoni jitihada zinazofanywa kuwarudisha, ambapo jumla ya wakimbizi 735 kati ya 33948 wamesitisha nia yao ya kureja kwa hiari.

Hali hii inatajwa na viongozi wa Burundi kuwa inachelewesha zoezi kwani wakimbizi wanaorejeshwa kwa mujibu wa mpango wa urejeaji ni ndogo. Mhe. Pascal Barandagiye amesema serikali ya yake ipo tayari kutoa magari kwaajili ya kuwasafirishwa wakimbizi kurudi nchi mwao, pamoja na kuwapa huduma muhimu za kibinadamu.

“zoezi la urejeshaji wa Wakimbizi kwa hiari linaenda polepole mno tofauti na matarajio, shirika la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR linaenda kwa kasi ndogo tofauti na ilivyotarajiwa, hivyo kutokana na zoezi hilonkuenda taratibu Serikali ya Burundi ipo tayari kutoa magari, fedha na huduma nyingine za kibinadamu ili kusaidia kuweza kuharakisha zoezi la kurejesha wakimbizi waliojiandikisha kurejea kwa hiari nchini Burundi” alisisitiza Barandagiye.

Akiongea katika nyakati tofauti tofuti katika kambi za nyarugusu, nduta na mtendeli, amewahakikishia wananchi wa kuwa Amani nchini mwao ipo ya kutosha hakuna vurugu na serikali ya Burundi inawahitaji ili warejee kuenga taifa lao hakuna haja ya kuendelea kubaki makambini.

Wakimbizi wakiongea kwa nyakati tofauti wamemhakikishia kuwa bado wanapenda nchi yao Burundi, na wanatamani kurejea Burundi, lakini changamoto inayowakabili hadi kukata tamaa ya kurudi ni taratibu ndefu zinazowachelewesha kurejeshwa mara tu baada ya kujiandikisha, akiongea kwa niaba ya Wakimbizi walioko kambi ya Nduta Bw. Suleima Hamisi (65) ambaye amekuwa Mkimbizi mara Sita kwa nyakati tofauti tangu mwaka 1972 alisema “ Sisi tulishajiandikisha Zaidi ya miezi mine sasa ili tuweze kurejeshwa cha kushangaza hadi sasa badotupo makambi” ameiomba serikali ya Burundi na Tanzania na Shirika la kuhudumia wakimbizi wakae na kuzungumza kwa pamoja juu ya mustakabali wa kuwarejesha haraka wenye nia ya kurudi Burundi.

Akitoa taarifa kwa Waziri wa mambo ya ndani na mafunzo ya uzalendo wa Burundi na Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Jamuhuri ya Muungani wa Tanzania, Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu ikiyopo Wilayani Kasulu alisema kumekuwa na mwitikio Mkubwa wa wakimbizi wanao jiandikisha kurejea kwa hiari nchini Burundi lakini changamoto imekuwa taratibu ndefu zinazochelewesha kurejea kwao zinawafanya baadhi yao kuahirisha kurejea kutokana na kusubiri kwa muda murefu.

Serikali ya Burundi pia imedai Shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia UNHCR linatakiwa kubadilisha utaratibu wa kuwapatia au kuwagawia vyakula na pesa wakimbizi wanapokuwa wanarejea wameomba zoezi hilo lifanyike wakati tayari wakimbizi wakishapatiwa nyumba na maeneo yao ya makazi kuepusha kukaa kwa muda mrefu kwenye vituo vya kuwapokelea.

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema serikali ya Tanzania itahakikisha wakimbizi waliopo nchi wanahifadhiwa kwa mujibu wa makubaliano ya taratibu za kimataifa na wale wanaopenda kurejea kwa hiari itashirikiana na UNHCR, nchi ya Burundi ili kufanikisha zoezi hilo. 

Hatua ya kuwarejesha wakimbizi katika nchi yao ya asili ni moja kati ya suluhisho la kudumu la ukimbizi kwa mujibu wa sharia ya kimataifa ya wakimbizi ya mwaka 1951 na Sheria ya Wakimbizi ya Tanzania yam waka 1998 kifungu Na. 3 Zoezi la kurejea kwa wakimbizi nchini mwao waliopo Tanzania lilianza kuratibiwa mara tu baada ya tamko la viongozi rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunzinza walipo kutana Mwezi Julai 20, 2017 na kutamka kuwa wakimbizi waliopo Katika Makambi nchi Tanzania warejee nchini kwao kwani Burundi kuna amani ya kutosha.

Hadi sasa idadi ya wakimbizi walioko katika Mkoa wa Kigoma ni 210,005 na waomba hifadhi 26,410, kati ya hao 95,243 wapo kambi ya Nduta, 48147 kambi ya Mtendeli na 66615 Nyarugusu, aidha waombahifadhi wote wapo katika kambi ya nduta.

RPC SIMON HAULE AFUNGA MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI MKOA WA SHINYANGA MWAKA 2017

$
0
0
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amefunga wiki ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga yaliyoanza siku ya Jumatatu Novemba 13,2017 katika viwanja vya jeshi la Zimamoto mjini
Shinyanga.

Akizungumza leo Jumamosi Novemba 18,2017 wakati wa kufunga maadhimisho hayo, yenye kauli mbiu "Zuia ajali,Tii sheria,Okoa 
Maisha",Kamanda Haule aliwataka watumiaji wa barabara kuzingatia alama na michoro ya barabarani na watembea kwa miguu kuhakikisha wanapokuwa barabarani wanavuka katika maeneo yanayostahili ili kupunguza ajali zisizo za lazima.

Katika hatua nyingine aliwataka wananchi kulinda miundombinu ya barabara kwa kushirikiana na serikali na kuhakikisha wanawakata baadhi ya watu wasio waaminifu wanaoiba miundombinu ya barabara.

“Naomba tushirikiane kuwafichua na kuwakamata watu wanaoiba miundombinu ya barabara,na tukiwakamata tuwafikishe katika vyombo vya sheria”,aliongeza Haule.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwakumbusha akina mama kukaa mkao wa kiume wanapopanda pikipiki ama baiskeli badala ya kukaa upande upande ili kupunguza ajali za barabarani.

Naye Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga,Anthony Masanzu alisema katika wiki hiyo ya nenda kwa usalama,wamefanikiwa kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha bodaboda 184.

Alisema mbali na kutoa elimu kwa waendesha bodaboda na wananchi waliotembelea mabanda ya usalama barabarani pia walitembelea shule mbalimbali mjini Shinyanga ambazo zipo karibu na barabara.

“Tumetumia wiki hii kutoa elimu ya usalama barabarani kwa makundi mbalimbali ya watumiaji wa barabara ili kuhakikisha kuwa tunazuia ajali na kuokoa maisha yao”,aliongeza Masanzu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akizungumza wakati wa kufunga wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga mwaka 2017-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akisisitiza watumiaji wa barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga,Anthony Masanzu akizungumza wakati wa kufunga wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Shinyanga,Wilson Majiji akizungumza wakati wa kufunga wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga
Kwaya ya AICT Kambarage ikitoa burudani ya wimbo unaohusu masuala ya usalama barabarani
Wanafunzi wa shule ya msingi Town wakiimba wimbo  unaohusu  usalama barabaraniBurudani ya ngoma ya kucheza na nyoka ikiendelea
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akitoa vyeti kwa mmoja wa waendesha bodaboda (kati ya 184) waliopata mafunzo/elimu ya usalama barabarani wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga mwaka 2017.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.

WAZIRI MKUU AONGOZA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA KATIBU MKUU WA CWT

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Katibu Mkuu. Wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu, Alhaji Yahya Msulwa .leo Novemba,18. 2017. Nyumbani kwa marehemu Toangoma jijini Dar es salaam.Aliye simama kwa kwa Waziri Mkuu ni Mke wake Mama Mary Majaliwa.
 Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Katibu Mkuu. Wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu, Alhaji Yahya Msulwa .aliye simama kushoto kwake ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa  pamoja na Mke wake  leo Novemba,18. 2017. Nyumbani kwa marehemu Toangoma Jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa Pole, Bi. Sharifa Msulwa. kufuatia kifo cha Mume wake aliye kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu Alhaji Yahya Msulwa  ,Waziri Mkuu alifika nyumbani kwa Marehmu Toangoma  jijini Dar es salam leo November 18, 2017. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wanafamilia, Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika kuomboleza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CWT, Bw. Yahya Msulwa nyumbani kwa marehemu, Tuangoma Jijini Dar es Salaam. 

Bw. Msulwa  amefariki dunia juzi (Alhamisi, Novemba 16, 2017) katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Katika maombolezo hayo Waziri Mkuu ameambatana na Mkewe Mama Mary Majaliwa.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali kwa sababu marehemu alishirikiana nayo vizuri akiwa kiongozi wa walimu ambao ni zaidi ya asilimia 65 ya watumishi wa umma.

Waziri Mkuu amesema kuwa marehemu alikuwa mchapakazi na mwenye ushirikiano mzuri na wenzake, ambapo Novemba 12, 2017 alipokea barua kutoka CWT iliyosainiwa na marehemu akimualika kushiriki kwenye shughuli za chama.

“Wote tumeguswa na msiba huu, marehemu alikuwa mtumishi wa muda mrefu wa Chama cha Walimu Tanzania tangu mwaka 1996 na alikuwa rafiki na ndugu wa kila mmoja. Alikuwa na tabia njema, hivyo tunatakiwa kuyaenzi mambo mema aliyotuachia”
Waziri Mkuu ameongeza kuwa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema. Nawaomba wanafamilia, mke wa marehemu na watoto kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.”

Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam

BODI YA CHAKUA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR YAANGAMIZA TANI 11.6 YA MAZIWA NA BIDHAA MCHANGANYIKO ZILIZOHARIBIKA

$
0
0
 Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakishusha maziwa tani 11.6 na bidhaa mchanganyiko zilizo haribika kwa ajili ya kuangamizwa katika dampo la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
Gari la Kijiko likiangamizwa maziwa yaliyoharibika pamoja na bidhaa mchanganyiko katika dampo la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkuu wa Idara ya Udhibiti na Usalama wa chakula Dkt. Khamis Ali Omar (wambele) akisimamia ungamizwaji wa bidha zilizoharibika katika dampo la Kibele.
Meneja wa Kampuni ya Farid Supply iliyoingiza maziwa hayo Mansour Said akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sababu ya sehemu ya maziwa hayo kuharibika.Picha na Makame Mshenga.


Na Ramadhani Ali – Maelezo

Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa nchini kutoka nje wameshauriwa kutoogopa gharama wakati wa kusafirisha bidhaa zao na wahakikishe wanatumia njia bora za usafirisha ili mizigo yao ifike ikiwa salama.

Mkuu wa Idara ya Udhibiti na usalama wa chakula wa Bodi ya Chakula na Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Khamis Ali Omar ametoa ushauri huo wakati wa kuangamiza tani 11.6 za maziwa katika dampo la Kibele yaliyoingizwa nchini baadhi yakiwa yameharibika kutokana na usafirishaji mbaya.

Alieleza kuwa sehemu ya maboksi ya maziwa yalipasuka na kuharibu mengine na baada ya kuyafanyia uchunguzi walijiridhisha kuwa yalikuwa hayafai kwa matumizi ya binaadamu.Alisema waliishauri Kampuni iliyoiingiza maziwa hayo Farid Supply kuyarejesha yanakotoka ama kuyaangamiza baada ya kuona yako katika hali hatarishi ya afya za wananchi na walikubali yaangamizwe ili kupunguza gharama ya kuyarejesha.

Dkt. Khamis aliwataka wafanyabiashara kuelewa kuwa kunatafauti kubwa ya kusafirisha vyakula vya maji maji na bidhaa nyengine za kawaidi na vyakula vya maji maji vinahitaji tahadhari kubwa zaidi wakati wa kusafirishwa.Alisema lilijitokeza katika kusafirisha maziwa hayo ni kukosekana umakini na kusababisha kontena lililobeba maziwa kuserereka wakati wa safari na baadhi ya maboksi yalianguka na kuapasuka nadani ya kontena hilo.

Meneja wa Kampuni ya Farid Supply Mansour Said ambae alishiriki katika zoezi hilo Kibele, alikubali kuwa kulitokea tatizo katika kontena hilo na baadhi ya maboksi ya maziwa yalipasuka lakini sehemu kubwa ya maziwa hayo yalikuwa hayajaharibika na yalikuwa yanafaa kutumika.

Alisema maziwa hayo yaliyokuwa na thamani ya zaidi ya sh. 52 milioni huenda yalianza kuharibika baada ya kuzuiliwa kwa kwa kipindi cha miezi nane katika bandari ya Zanzibar .

TANESCO yafanya Zoezi la Kusafisha na Kuunga Bomba la Gesi-KINYEREZI 1

$
0
0

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawataarifu Wateja wake kuwa leo Jumamosi Novemba 18 na kesho Jumapili Novemba 19, 2017 kuna usafishaji na kuunga bomba kubwa la Gesi katika Mitambo ya Kinyerezi I, sambamba na zoezi hilo pia yanafanyika maandalizi ya kukiunganisha Kituo cha Kinyerezi II, kuanzia Saa:02.00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni, kama tulivyowatangazia.
 
 Kutokana na kazi hiyo kutakuwa na upungufu wa umeme katika Gridi ya Taifa, hivyo baadhi ya Wateja waliounganishwa katika Gridi ya Taifa wa maeneo mbalimbali Nchini watakosa huduma ya umeme. Zoezi hilo linaendelea kwa ufanisi mkubwa na uharaka ili kurejesha huduma ya umeme kwa wakati.
 
 TAHADHARI Kutokana na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo ya Kinyerezi, kutokuwasha moto, kutokufanya shughuli za uchomeleaji vyuma pamoja na shughuli nyingine yoyote yenye viashiria vya moto, ili kujikinga na madhara yanayoweza kutokea iwapo shughuli tajwa zinafanyika maeneo yaliyo karibu na Mitambo. Shirika limesha fanya taratibu zote za ki usalama katika eneo la Mitambo.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO NOVEMBA 18,2017

SHIRIKA LA POSTA LAFADHILI SHINDANO LA 'NATIONAL SPELLING BEE' TANZANIA

$
0
0
SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Coconut Foundtion lenye Makao yake Makuu Kijitonyama Manispaa ya Kinondoni jijini Dar-es-Salaam, leo hii limewatangaza washindi kumi baada ya kumalizika kwa shindano la kutaja herufi sahihi ya sentensi za kiingereza, lililoanza Novemba 11.

Wahusika wa shindano hilo, walikuwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari (English Medium School). Shindano hilo lilikuwa na lengo la kuwajengea uwezo na kujiamini katika matumizi ya lugha ya Kiingereza.

Washindi hao wanatarajia kwenda kwenye mashindano hayo nchini Uganda mnamo mwezi Desemba mwaka huu, ambako mashindano hayo yatazijumuisha nchi za Afrika Mashariki.

Shirika la Posta Tanzania lilikuwa miongoni mwa wafadhili wa shindano hilo.
Afisa Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Maria Sanga (katikati), akiwa na baadhi ya washiriki wa shindano la Spelling Bee pamoja na mwalimu wao baada ya kutembelea meza ya Shirika la Posta Tanzani na kupewa zawadi mbalimbali ikiwepo kofia. 
Washiriki wa shindano la Spelling Bee wakiwa ndani ya ukumbi wakisbiri muda wa kuanza shindano hilo jana katika ukumbi wa jumba la Makumbusho ya Taifa jijini Dar-es-Salaam. 
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Phillip Kowero, akifunga rasmi shindano la Spelling Bee lililomalizika Novemba 18 katika ukumbi wa jumba la Makumbusho ya Taifa, ambapo Shirika la Posta Tanzania wakiwa ni moja kati wadhamini wa shindano hilo. 
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Philip Kowero akimkabidhi cheti Mwalimu wa kutoka Shule ya Feza baada ya shule yao, kufanya vizuri katika shindano hilo. 
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Philip Kowero akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi baada ya shule yake, kuwa moja ya shule zilizoshiriki na kufanya vizuri katika shindano hilo.  
Washindi wakiwa wamekaa na zawadi zao walizotunukiwa. 
Baadhi ya washindi wa shindano la Nationa Spelling Bee wakiwa katika picha ya pamoja wa katikati ni mshindi kutoka Shule ya Feza, Bw. Adnan Abdallah. Kulia kwake ni Prokrith Ghandi kutoka Shule ya Aga Khan na kushoto ni Bi. Jackline, jijini Dar-es-Salaam. 
Walimu kutoka Shule mbalimbali na wazazi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi wa shindano la National Spelling Bee, lililofanyika katika ukumbi wa jumba la Makumbusho jijini Dar-es-Salaam. 
Washindi wa shindano la National Spelling Bee wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya kumalizika kwa shindano hilo.

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO MHANDISI NDITIYE ATEMBELEA SHIRIKA LA POSTA AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia), akisalimiana na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwangombe, wakati alipofanya ziara kwenye shirika hilo, na kuongea na wafanyakazi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo na Mjumbe wa bodi ya shirika hilo, Bi. Khadija Shaaban.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia), akisalimiana na Mjumbe wa bodi ya shirika hilo, Bi. Khadija Shaaban. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia), akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia), akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo mara baada ya kusalimiana naye katika ziara yake kwenye shirika hilo, jijini leo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia), akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo (kushoto), mara baada ya kutembelea Ofisi ya Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwangombe (katikati), katika ziara hiyo, jijini leo. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia), akimsikiliza Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwangombe, wakati akimpatia maelezo kuhusu shirika hilo, katika ziara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.  
Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwangombe (mbele), akimkaguza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, mabasi mapya ya usafirishaji abiria na vifurushi. 
Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwangombe (kushoto), akimweleza jambo Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, wakati akimkaguza mabasi mapya ya usafirishaji abiria na vifurushi.   
Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwangombe (kushoto), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), kuhusu vifurushi vinavyotumwa na kupokelewa kutoka nje ya nchi. 
Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwangombe (kushoto), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), kuhusu ukaguzi wa vifurushi vinavyotumwa na kupokelewa kutoka nje ya nchi, alipofika kitengo cha Mamlaka ya Mapato (Forodha) Posta Kuu jijini Dar es Salaam.  
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), akipatiwa maelezo na mmoja wa wakaguzi wa vifurushi vinavyotumwa nje ya nchi, alipofika kitengo cha kuhudumia vifurushi, Posta Kuu jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (mbele), akipatiwa maelezo na mmoja wa wahudumu wa Kitengo cha Jamii Centre, Veronica Nyindi, alipotembelea Posta Kuu jijini Dar es Salaam katika ziara hiyo leo.
Mmoja wa wateja wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Louis Shika, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma za shirika, alipokutwa na waandishi katika ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye.  
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akielezwa jambo na Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Margreth Mlyomi alipotembelea Posta Kuu jijini Dar es Salaam.  
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akipatiwa maelezo na mmoja wa wafanyakazi wa Posta Kuu, Kitengo cha EMS, Sanjile Mbano (kulia), alipofika kwenye kitengo hicho, katika ziara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), akipatiwa maelezo na Meneja wa Idara ya EMS, John Tinga. 
Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akizungumza na waandishi wa habari katika ziara hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwangombe, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akizungumza na wafanyakazi wa Posta Makao Makuu na wa Mkoa wa Dar es Salaam alipokutana nao katika ziara hiyo. 
Mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Makao Makuu, David Hango, akimuuliza swali Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye katika mkutano huo. 
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TEWUTA-TPC), Makao Makuu, Ahmed Kaumu, akimuuliza swali Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye katika mkutano huo.  
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akijibu maswali yaliyoulizwa na wafanyakazi wa Shirika la Posta Makao Makuu na wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano huo.
Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwangombe, akizungumza wakati akimshukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye baada ya kuzungumza na wafanyakazi hayo. 
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TEWUTA-TPC), Makao Makuu, Ahmed Kaumu, akimshukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye katika mkutano huo. 
Mjumbe wa bodi ya Shirika la Posta, Bi. Khadija Shaaban, akimweleza jambo Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, wakati akiagana naye katika ziara hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo. 

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMPA MRAJISI SIKU 7 ZA KWANINI MAGUNIA KUTOFIKA KWA WAKATI

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kushiriki mnada wa tano wa Korosho, Jana Novemba 17, 2017. Picha na Mathias Canal



Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa akimuonyesha Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa jinsi magunia yalivyopangwa kwa ustadi ktika gala la kuhifadhia Korosho la Mtanda mara baada ya  Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kushiriki mnada wa tano wa Korosho, Jana Novemba 17, 2017.


Badhi ya wakulima wa zao la korosho wa Chama cha Ushirika cha Masasi-Mtwara Cooperative Union Ltd (MAMCU) wakifatilia mnada wa tano wa korosho katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara. Jana Novemba 17, 2017.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa wakiwasili Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara kwa ajili ya kujionea Mnada wa Korosho unavyoendeshwa, Jana Novemba 17, 2017.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Wa Tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wazee maarufu wa kijiji cha Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa (Wa Kwanza Kushoto), na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini Mhe Hawa Ghasia (Wa Kwanza Kulia).

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa wakati wa Mnada wa tano wa Korosho, Jana Novemba 17, 2017.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini Mhe Hawa Ghasia wakati wa ukaguzi wa ghala la Buko Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara  wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Humo, Jana Novemba 17, 2017

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza ushauri sambamba na pongezi kwa kushiriki Mnada wa tano wa Korosho Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara  wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Humo, Jana Novemba 17, 2017



Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa wakikagua magunia ambayo tayari yamewasili katika Ofisi ya Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama Kikuu cha ushirika mara baada ya kumalizika kwa mnada wa tano wa Korosho Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.


Na Mathias Canal, Mtwara

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa leo Novemba 18, 2017 amemuagiza Mrajisi wa vyama vya ushirika kukamilisha haraka kazi ya uchunguzi kwenye Bodi za vyama vya ushirika vya Mkoa wa Mtwara ili kubaini sababu zilizopelekea kuuzwa kwa magunia kiholela.

Alisema kuwa kumalizika kwa uchunguzi huo kutarahisisha kuchukuliwa haraka hatua kali za kisheri kwa wale wote watakaobainika kukiuka sheria No 17 ya vyama vya ushirika.

Naibu waziri alitoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kugundua kuwa kuna viashiria vya ukiukwaji wa taratibu katika upatikanaji wa magunia ya kuhifadhia korosho wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani humo.

Sambamba na hilo Naibu waziri Mhe Mwanjelwa wakati wote wa mkutano huo ameshuhudia malalamiko kutoka kwa wakulima wa zao la korosho wa Chama cha Ushirika cha Masasi-Mtwara Cooperative Union Ltd (MAMCU) kuhusu ucheleweshwaji wa upatikanaji wa maguni kutoka kwa mzabui, Mapungufu ya kilo kati ya PDA na WHRs ghala kuu, ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa malipo ya wakulima kwa njia ya benki kutoka kwa wanunuzi.

Katika ziara yake hiyo kilio cha wananchi wengi na wakulima walisiitiza zaidi kuhusu kukosekana kwa magunia hayo huku wakieleza kuwa wakati mwingine kuchelea kufika ama kutowafikia kabisa jambo ambalo linachangia kupunguza thamani ya zao la korosho.

“Nataka Mrajisi ufanye na ukamilishe kazi yako ya uchunguzi na baada ya kuipata taarifa hiyo hatua stahiki zitachukuliwa kwa wale wote watakaogundulika kukiuka sheria ya nchi” Amekaririwa Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa

Mbali na agizo hilo Naibu Waziri pamoja na wabunge wa Mkoa wa Mtwara walipata nafasi ya kujionea mnada wa tano wa ununuzi wa korosho unavyoendelea.

Hata hivyo Mnada wa tano ulishuhudiwa Kilogramu 7,524,104 za korosho zikiuzwa kwa thamani ya zaidi ya Bilioni 30.

Wakati huo huo Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa amesema Wizara itayafanyia kazi haraka mapendekezo ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa kufanya uchunguzi kuhusu mwenendo mzima wa magunia pamoja na upatikanaji wake.



Hafla fupi ya kumaliza kambi ya siku nne ya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab iliyofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0
Mufti Sheikh Abubakari Zubeir bin Ally akimkabidhi tuzo ya shukrani Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati wa hafla fupi ya kumaliza kambi ya siku nne ya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab iliyofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saudi Arabia. Kushoto ni Balozi wa Saudi Arabia Nchini Mhe. Mohamed bin Mansour Al Malik.
Balozi wa Saudi Arabia Nchini Mhe. Mohamed bin Mansour Al Malik akimkabidhi tuzo ya shukrani Mufti Sheikh Abubakari Zubeir bin Ally katika hafla fupi ya kumaliza kambi ya siku nne ya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab iliyofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saudi Arabia. Jumla ya wagonjwa 33 walifanyiwa upasuaji katika kambi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akiishukuru Serikali ya Saudi Arabia kupitia Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchi hiyo kwa kutuma wataalamu wake hapa nchini kutoa huduma ya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Jumla ya wagonjwa 33 walifanyiwa upasuaji katika kambi hiyo.
Madaktari bigwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saud Arabia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kufanya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa wagonjwa 33.

SIKU YA TAKWIMU AFRIKA KUADHIMISHWA KESHO

$
0
0

Na: Veronica Kazimoto,
Dar es Salaam,

Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatafanyika kesho tarehe 20 Novemba, 2017 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya alisema maadhimisho hayo yanayoratibiwa na ofisi hiyo kwa niaba ya Serikali, yana lengo la kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa Tasnia ya Takwimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii Barani Afrika. 

Ruyobya alisema kuwa kaulimbiu ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka huu ni “Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora" 

"Kaulimbiu hii inalenga kuweka mkazo katika matumizi ya Takwimu za Uchumi kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wote nchini na Afrika kwa ujumla", amebainisha Ruyobya.

Ruyobya alifafanua kuwa matumizi sahihi ya Takwimu za Uchumi yanaiwezesha Serikali kutunga sera na kutathmini programu mbalimbali kama vile Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP-II), Agenda ya Dunia ya Mwaka 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Agenda ya Afrika ya Mwaka 2063. 

"Progaramu zote hizi, zina lengo la kuboresha maisha ya wananchi kwa kuhakikisha kuwa, kuna upatikanaji wa Huduma za afya, Elimu, Miundombinu ya umeme na barabara, Mawasiliano, Utunzaji wa mazingira pamoja na Utawala bora", amesema Ruyobya.

Jumla ya washiriki 200 kutoka katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wadau wa Maendeleo, Vyuo vya Elimu ya Juu, Wanafunzi wa Shule za Sekondari pamoja na Wadau mbalimbali wa takwimu nchini wanatarajiwa kuhudhuria kwenye maadhimisho hayo. 

Siku ya Takwimu Afrika huadhimishwa kila mwaka tarehe 18 Novemba ambapo kwa mwaka huu, Tanzania itaadhimisha siku hiyo kesho tarehe 20 Novemba, 2017.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) hivi karibuni kuhusu maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika kesho tarehe 20 Novemba, 2017 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mwakyembe aipongeza TAMWA kwa kuwa na wanachama wanaokidhi vigezo vya Sheria ya Habari.

$
0
0

 PIX 2
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) Bibi Alack Mayombo akieleza mafanikio ya chama chao ikiwa ni pamoja na kupambana na ukatili wa kijinsia  jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya chama hicho.
PIX 3
Mkurugenzi  wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) Bibi Edda Sanga akieleza majukumu ya chama chao jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya chama hicho.
PIX 4
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe  akikata utepe kuashiria  uzinduzi wa kitabu cha mafanikio tangu kuanzishwa kwa   Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya kutimiza  miaka  30 ya chama hicho.
PIX 5
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe  akibonyeza kitufe  kuashiria  uzinduzi wa  luninga ya mtandaoni ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya kutimiza miaka 30 ya chama hicho. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas.
PIX 6
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akimkabidhi Tuzo ya Heshima Bibi Fatma Alloo kwa mchango wake katika  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya kutimiza  miaka 30 ya chama hicho.
PIX 7
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya wanachama wa  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jana Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya kutimiza  miaka 30 ya chama hicho. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas.
…………………………………………………………………………………..
Na. Shamimu Nyaki –WHUSM.
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa pongezi kwa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kwa kuwa na wanachama ambao wanakidhi vigezo vilivyopo katika Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 ambapo moja ya vigezo hivyo ni kuwa na Wanataaluma ya Habari wenye elimu ya kuanzia Stashahada.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo Jana Jijini Dar es Salaam katika sherehe za maadhimisho ya miaka 30 ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) ambapo amewataka wanachama hao kuendelea na juhudi zao za kukemea ukatili wa kijinsia, ndoa za utotoni, na mauaji ya vikongwe yaliyotoa sifa kubwa kwa  chama hicho.
“Nimefurahi sana kusikia kuwa wanachama wa chama hiki wanaanzia ngazi ya Stashahada kama ambavyo Sheria yetu ya Habari inavyosema kuwa ni lazima kwa mwanataaluma ya Habari kuwa na kiwango cha Elimu kinachoanzia hapo,lakini pia Serikali inatambua sana mchango wenu wa kuilemisha jamii masuala mbalimbali ikiwemo ukatili wa kijinsia endeleeni kufanya hivyo ili jamii yetu iwe jamii bora”.Alisema Mhe. Mwakyembe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Bibi Alack Mayombo ameishukuru Serikali kwa mchango mkubwa inaotoa kwa Chama hicho pindi inapohitaji msaada na kuahidi kushirikiana na Serikali katika kuelimisha jamii hasa masuala ya Ukatili wa Kijinsia.
“Tunashukuru sana Serikali kwa jinsi inavyotuunga mkono katika juhudi zetu za kutatua changamoto zinazoikumba jamii yetu hasa mauaji ya Vikongwe,watu wenye ulemavu wa ngozi,ndoa za utotoni  pamoja na ukatili wa kijinsia mara zote tulizotoa taarifa kwa Serikali imekuwa ikichukua hatua zinazostahili”. Aliongeza Bibi  Alack.
Naye Mkurugenzi wa Chama hicho Bi Edda Sanga ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka 30 tangu kilipoundwa chama hicho kimefanikiwa kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo kiwango cha Ukeketaji, Mimba za utotoni, madawa ya kulevya na athari zake katika jamii na kutoa taarifa ambayo imesaidia kupunguza matatizo hayo.
Chama hicho kilianzishwa tarehe 17 Novemba 1987 na wanahabari wanawake lengo ikiwa ni kupinga ukatili wa aina yoyote katika jamii na tayari kimeefanikiwa kwa kiasi kikubwa,Aidha chama hicho kimezindua luninga ya Mtandaoni itakayotoa taarifa mbalimbali za Ukatili wa kijinsia pamoja na mambo mengine ya kijamii.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images