Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1432 | 1433 | (Page 1434) | 1435 | 1436 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Handeni akipiga chapa Ngo'mbe Kama ishara ya uzinduzi wa zoezi hilo
   Baadhi ya wafugaji walioleta mifugo yao kwaajili ya upigaji chapa ya moto
   Mifugo ikiwa imefungiwa tayari kwa zoezi la upigaji chapa.
   Afisa Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Maxmilian Longino akizungumza na Wafugaji.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw William Makufwe akizungumza na wafugaji
   Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizungumza na wafugaji wa Kijiji cha Sua
   Baadhi ya mifugo iliyoletwa kupigwa chapa
   Moja ya chapa Iliyopigwa Ngo'ombe


  0 0

   Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma Bw. Griffin Mwakapeje (aliyesimama) akifafanua jambo katika kikao kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome na wadau wa kimataifa katika masuala ya sheria wakati wakibadilishana mawazo kuhusu sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya ugaidi Tanzania.
   Baadhi ya washiriki wa majadiliano ya sheria mbalimbali nchini kati ya  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome na wadau wa kimataifa katika masuala ya sheria .
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akisisitiza jambo kwa wadau wa kimataifa katika masuala ya sheria walipomtembelea leo (17/11/2017) ofisini kwake mjini Dodoma.

  0 0

  Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ametoa wito huo Novemba 16, 2017 Jijini Dar es Salaam alipokutana na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke na ujumbe alioambatana nao Wizarani hapo kutoka kwenye Ubalozi huo ili kujadiliana masuala mbalimbali ya madini ikiwemo fursa za uwekezaji.

  Waziri Kairuki alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za madini na hivyo zipo fursa lukuki za uwekezaji ambazo zinaweza kutumiwa na kampuni za nchini China kwa manufaa ya pande zote mbili.

  “Rasilimali za madini ni nyingi na hivyo zipo fursa mbalimbali ambazo zinaweza kutumiwa na kampuni za China na wakati huo huo kuchangia katika uchumi na pato la Taifa kwa ujumla,” alisema Waziri Kairuki.

  Waziri Kairuki vile vile alisema yapo maeneo ambayo wawekezaji wanaweza kushirikiana na Serikali ambapo alitaja baadhi yake kuwa ni uchimbaji wa madini kwa kushirikiana na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), tafiti za utambuzi wa maeneo yenye madini kwa kushirikiana na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Chuo cha Madini (MRI).

  Aidha, aliongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha madini yanayochimbwa nchini yanaongezwa thamani kabla hayajasafirishwa ili kukuza uchumi wa Taifa na wakati huo huo, kuongeza mapato ya Serikali na kuzalisha ajira zaidi.

  “Madini yakiongezwa thamani hapa nchini, faida zitakazopatikana ni nyingi na ni kubwa ikiwemo ajira lakini pia mapato nayo yataongezeka kwa kuelewa thamani halisi ya madini husika,” alisema Waziri Kairuki.
  Kwa upande wake Balozi Ke alipongeza juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuwaletea wananchi wake maendeleo endelevu.

  Alisema Serikali ya China itaendeleza ushirikiano wa karibu na wa dhati na Serikali ya Tanzania hususan kwenye Sekta ya Madini ili kuhakikisha sekta hiyo inaleta tija iliyokusudiwa kwa Taifa.

  Alisema kampuni mahiri nyingi kutoka China tayari zimeonyesha nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini na ziko tayari kuja kuwekeza Nchini. 
   Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na ujumbe alioambatana nao (hawapo pichani) walipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akimsikiliza Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam ili kujadili masuala mbalimbali.
   Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke (kulia) akiwa na ujumbe wake kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania walipomtembelea Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (hayupo pichani) ili kujadili masuala mbalimbali ya Sekta ya Madini.
   Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (wa pili kutoka kulia) akijadiliana jambo na ujumbe kutoka Ubalozi wa China nchini ulioongozwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke (katikati).

  0 0

   The Chief of Party of the Sauti Project a Jhpiego’s lead program Dr. Albert Komba elaborating a point to the USAID Mission Director in Tanzanian Andy Karas when he visited projects interventions conducted to reduce HIV/Aids prevalence to the vulnerable groups in Iringa. The program is conducting Behavior Change Communication Sessions, Screening for Gender Based Violence and cancelling on usage of Alcohol and Drugs to the Vulnerable groups including young girls.
   Scholina Charles (22) a young girl from umoja groups in iringa giving her testimony to the USAID Mission Director in Tanzanian Andy Karas and his delegation on the risk she went through before joining the Sauti project to fight HIV/ AIDS. Looking center is the Sauti Project Chief of Party Dr. Albert Komba .
   The USAID Mission Director in Tanzanian Andy Karas,  Deputy Mission Director Helen Pataki (second right), Jhpiego Country Director (right) and Sauti Project Chief of Party Dr. Albert Komba (left) following a Behavior Change Communication Sessions conducted by Zera Mingo (23) to the young adolescences girls as part of HIV/ AIDS intervention to reduce HIV/Aids prevalence to the vulnerable groups in Iringa.
   The USAID Mission Director in Tanzanian Andy Karas and his Deputy Mission Director Helen Pataki looks at the clothes made by Mwanahamisi Mketo (23) during his field visit in Iringa to assess the implementation of USAID funded Project activities. Mwanahamisi Mketo she is a member of Behavior Change Communication group conducted by Jhpiego at kihesa ward in Iringa who are also economically empowered. 

  The United State Agency for International Development (USAID) funded projects in iringa has demostrated how their bringing impacts to the lives of the people in Iringa. This expression was made by USAID funded NGO’s and local CSO’s to the newly USAID Mission Director in Tanzanian Andy Karas who conducted a field visit in Iringa to assess the implementation of USAID funded Project activities.

  Andy who was accompanied by his deputy Mission Director Helen Pataki and other USAID staff expressed his appreciation to the regional administration and local authorities for the support their giving to all implementing partners funded by USAID in the region and thanks them for their work their doing for the people of Iringa.    

  Explaining on how they engage the local authorities and the entire community to fight the spread of the HIV/AIDS in Iringa, the Chief of Party with Sauti Project a Jhpiego’s lead program Dr. Albert Komba said despite the fact that the project works in 14 region countrywide, in Iringa Municipal they targets all Vulnerable groups including young girls by  linking them into services like Behavior Change Communication Sessions, Economic Empowerment groups, Screening for Gender Based Violence and cancelling on usage of Alcohol and Drugs.

  “we are working to ensure we reduce the spread of HIV/AIDS because the groups we are targeting like these adolescence girls and female sex workers are more vulnerable and engaging them in the fight against HIV will lead to an HIV/AIDS free generation in Iringa” said Dr. Komba

  As part of their interventions to reduce HIV/Aids prevalence, the project also has mobilized girls to form WORTH+ groups which is the voluntary money saving groups for income generating activities, and train them on economic empowerment, gender issues and how to protect themselves against high risk behaviors of which most girls from these groups have managed to change their lives by living a decent life.

  Reaching a testimonie delivered by Scholina Charles (22) a young girls from umoja groups on the risk she went through before joining the sauti project, she said the situation was devastating and because of her economic status from her family she got engaged into sex business as part of income generating.

  “The situation was bad, I remember men used to bribe me even for two hundred shilling to have sex with them and I had no option. But now that I have joined this group, I am empowered with self-awareness on the risk of HIV/AIDS, gender violence, and through this group I have also managed to raise money and now I am engaging into agricultural activities and employ men in my maize farm”. Said Scholina.

  Earlier speaking with USAID delegation and other USAID funded implementing partners, the Iringa Regional Administration Secretary Wamoja Ayubu thanks the delegation for the support they are giving to the region level by complimenting government effort in the health sector agriculture sector and other sectors especially by emphasizing the inclusion and empowerment of youth and woman. 

  “The government has policy and laws which advocates for the inclusion of gender especially youth and woman in all activities, I am happy that USAID is also advocating that and we promise to collaborate with all partners to empower them especially locals so that they bring up new ideas for development and at the regional level. In our side we will chip in to address all challenges that might be faced by our implementing partners” she insisted.

  Sauti is implemented by Jhpiego in partnership with Pact, Engenderhealth and NIMR/ Mwanza with support from the American people through USAID under the United States President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) and DREAMS Initiatives.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. George Joseph Kakunda anayeshughulikia Elimu, Maji, Kilimo, Mifugo na Maliasili, amefungua Mkutano wa kwanza wa kazi kwa Kaimu Makatibu Wasaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) katika ukumbi wa chuo cha Mipango mjini Dodoma leo.

  Mkutano huo ni wa kwanza tangu kuanzishwa kwa Tume ya TSC mwaka 2015, ambao hutakiwa kufanyika kila baada ya miaka mitatu kwa malengo mbalimbali likiwemo kupitia kanuni, sheria na taratibu za Tume hiyo.

  Akifungua kikao kazi hicho mjini Dodoma, ameagiza kuwepo kwa ushirikiano baina ya TSC, Idara ya Elimu na Wadhibiti Ubora wa Elimu (Wakaguzi) ngazi ya wilaya bila kuwepo kwa muingiliano wa majukumu ili kuinua kiwango cha elimu nchini badala la kuendelea kubishana na kuingiliana katika majukumu yao.

  “Kuanzia sasa naagiza Maafisa Elimu wa Wilaya wote nchini, Wadhibiti wa Ubora kote nchini na Makatibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu katika Halmashauri zote nchini; kwamba ushirikiano wa kikazi ni jambo la lazima kwenu vinginevyo tutaendelea kudidimiza Ubora wa Elimu nchini”

  Mhe. Kakunda amewaasa Wajumbe wa Mkutano huo kuendeleza mafanikio ambayo Tume mpya ya TSC imeyapata kwa kipindi kifupi cha mwaka mmoja kama kusimamia vema mikataba ya ajira za waalimu wanapoanza kazi, kwani ndio maisha yao.

  “Mnapowasainisha mikataba ya kudumu ya kazi walimu wapya yenye masharti ya pensheni, tambueni kwamba, walimu wanaithamini sana mikataba hiyo kwa sababu licha ya kuhakikishia walimu uhakika wa ajira, mikataba hiyo huwaongoza walimu jinsi wanavyotakiwa kujiheshimu kazini ikiwa ni pamoja na kuainisha baadhi ya maadili yao kazi”

  Aidha, amewataka wajumbe kutumia kanuni ya kuwathibitisha walimu kazini ndani ya mwaka mmoja bila kusubiri malalamiko ya walimu. “walimu wote wanaotimiza masharti yanayoonesha kuwa wameweza kutekeleza majukumu yao kwa ustadi na weledi unaotakiwa, wathibitisheni kazini ndani ya muda usiozidi miezi 12”,

  Katika hatua nyingine, Mhe. Kakunda ameiagiza TSC kuwachukulia hatua wale wote watakaochelewesha kuwathibitisha walimu bila sababu za msingi, “nataka kuona hatua hatua zikichukuliwa dhidi ya wote ambao kwa namna moja au nyingine watachelewesha kuwathibitisha kazini walimu kwa muda mrefu bila sababu za msingi” Pia amewaasa wajumbe kusimamia vema suala la kuwapandisha madaraja walimu kwa mujibu wa kanuni ili kuondoa malalamiko na manung’uniko na kuongeza ufanisi wa kazi.

  Lakini pia, Mhe. Kakunda ameshauri Kitengo cha Sheria katika Tume ya TSC Makao Makuu iwe Kurugenzi ya Sheria (Idara kamili) kutokana na umuhimu wa kazi za Tume kama Mamlaka ya Nidhamu.

  Naye Katibu Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania (TSC), Winfrida Rutaindurwa, amesema Tume hiyo imepata mafanikio makubwa katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa kwake, kwa sheria namba 25 ya mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na kuandaa Mpango Mkakati wa Tume kwa miaka mitano 2017/18 hadi 2021/22, kufunga mtambo wa malipo ya mishahara na upatikanaji wa taarifa muhimu za watumishi kwa wakati.

  Amesema Tume pia imeweza, “kuandaa bajeti ya matumizi ya kawaida na mishahara wa Tume kwa mwaka 2017/2018, kutengeneza barua pepe za Serikali kwa ajili ya Watumishi wa Tume Makao makuu, kutengeneza tovuti ya Tume, kujiunga na Mkongo wa Taifa kutoka TTCL na kuratibu madai ya Watumishi ya likizo, kusafirisha Wastaafu, gharama za matibabu na posho za kujikimuambayo yaliwasilishwa kwa Mwajiri wa zamani ambayo ilikuwa ikiitwa Tume ya Utumishi wa Umma”

  Rutaindurwa amesema pamoja na mafanikio zipo baadhi ya changamoto zinazoikabili Tume ya TSC ambazo ni ufinyu wa bajeti unaopelekea kutofanya uteuzi wa Viongozi wa ngazi ya Wilaya ambao ni Makatibu Wasaidizi, uhaba wa Ofisi za Tume ngazi ya Makao Makuu na Wilaya, upungufu wa vitendea kazi na samani Makao makuu na Wilayani.

  Changamoto nyingine ni upungufu wa watumishi unaozorotesha utendaji wa Tume hiyo, “upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali wilayani na makao makuu. Wanaopaswa kuwepo ni watumishi 775”na waliopo ni 417 na upungufu uliopo ni watumishi 358.

  Aidha, amesema baadhi ya ofisi za TSC  katika mikoa na Halmashauri zisizo na Wakuu wa Wilaya zimeondolewa na kusababisha kupungua kwa ufanisi kwa ofisi za Tume ngazi ya Makao makuu na wilaya 139, ikiwa ni kutokana na ukosefu wa usimamizi wa karibu katika ngazi za mikoa.

  Rutaindurwa amesema TSC inarajia kukamilisha zoezi la uteuzi wa Viongozi wa wilaya kabla ya kuisha kwa mwaka wa fedha 2017/18, kufuatilia mabadiliko ya muundo wa TSC ili kukidhi mahitaji yake, kutafuta uwezeshaji wa kuboresha mawasiliano ya kielektroniki makao makuu na wilayani, na pia kuandaa mazingira ambayo TSC itaongezewa bajeti kwani inahudumia watumishi zaidi ya asilimia 55 wa Serikali. 

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya TSC, Oliva Mhaiki amesema, tangu kuanzishwa kwa TSC mwaka 2015 na kuanza kazi mwaka 2016,  “Tume ilianza kushughulikia mashauri ya kawaida, lakini kutokana na wingi wa mashauri, tuliona tuyarudishe wilayani na kama Tume tumeona tujikite na mashauri ya rufaa”.

  Kikao kazi cha Tume ya Utumishi wa Walimu ni cha siku mbili ambacho ni kikao cha kwanza tangu kuanzishwa kwa TSC mwaka 2015, kabla ya hapo ilikuwa ni Tume ya Utumishi wa Umma ambayo ilivunjwa na kuanzishwa kwa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC).
   Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda anayeshughulikia Elimu, Maji, Kilimo, Mifugo na Maliasili akielekea kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma kwa ajili ya kufungua kikao kazi cha Makaimu Makatibu TSC Wasaidizi mjini Dodoma kushoto kwake ni Katibu Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania (TSC), Winfrida Rutaindurwa na kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya TSC, Oliva Mhaiki.
   Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda anayeshughulikia Elimu, Maji, Kilimo, Mifugo na Maliasili akitoa hotuba wakati wa  kufungua kikao kazi cha Makaimu Makatibu TSC Wasaidizi katika chuo cha Mipango mjini Dodoma, kushoto kwake ni Katibu Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania (TSC), Winfrida Rutaindurwa, Katibu wa Tume ya TSC Dodoma Manispaa na kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya TSC, Oliva Mhaiki. 
  Baadhi ya Washiriki wa kikao kazi cha Makaimu Makatibu TSC Wasaidizi wa Wilaya 139 nchini, wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mhe. Kakunda hayupo pichani katika chuo cha Mipango mjini Dodoma.
  Katika picha ya pamoja waliokaa, katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda anayeshughulikia Elimu, Maji, Kilimo, Mifugo na Maliasili kushoto kwake ni Katibu Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania (TSC), Winfrida Rutaindurwa na kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya TSC, Oliva Mhaiki.

  0 0

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam ametoa msaada wa pampu ya maji na mifuko 10 ya saruji vyenye thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa ajili ya kumaliza tatizo la maji katika kitongoji cha Mwamapalala kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga. 

  Mukadam amekabidhi msaada huo wa pampu ya maji na mifuko ya 10 ya saruji kwa diwani wa kata ya Chibe John Kisandu leo Ijumaa Novemba 17,2017 kwa ajili ya mradi wa maji katika mtaa wa Mwamapalala katika kata hiyo ambayo inakabiliwa na kukosekana kwa huduma ya maji. 

  Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo,Mukadam alisema hivi karibuni alitembelea kata ya Chibe,ndipo diwani wa kata hiyo akaomba msaada wa kutafutiwa pampu ya maji baada ya wananchi kujitolea kuchimba kisima kirefu. 

  “Kutokana na ombi hilo,nimetafuta wafadhili na kupata msaada huu kutoka kwa Farana Hirji aliyenipatia fedha kwa niaba ya Roshan Chatur nikanunua pampu hii na saruji hii itakayotumika kukamilisha ujenzi wa kisima”,alieleza Gulam. 

  “Kupitia msaada huu wananchi wa Chibe watapata huduma ya maji safi na salama kwani mhandisi wa maji wa manispaa amefika katika kisima hicho na kutuhakikishia kuwa maji hayo ni salama kwa matumizi ya binadamu”,alisema Mukadam. 

  Hata hivyo alisema aliwataka wadau kuendelea kushirikiana na serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kama vile maji,afya na elimu. Naye Kaimu katibu mkuu ALAT,Abdallah Ngodu ambaye yupo katika ziara kutembelea halmashauri mbalimbali nchini,alimpongeza Gulam kwa jitihada anazochukua katika kumaliza kero za wananchi. 

  “Lengo la ALAT ni kuhakikisha tunatatua kero za jamii ambazo nyingi zipo katika sekta ya maji,afya na elimu,hivyo kwa kushirikiana na serikali tutaendelea kutatua changamoto hizi”,alisema Ngodu. 

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,Rajabu Masanche alikiri kuwepo kwa changamoto za maji katika manispaa hiyo hivyo kuwaomba wadau kujitokeza kusaidia huku akiwataka wananchi kutunza miundombinu ya maji. 

  Kwa upande wake Diwani wa kata ya Chibe,John Kisandu alimshukuru Mukadam kwa kumpatia msaada huo ambao utakuwa msaada kwa wananchi hao ambao wanakabiliwa na tatizo la maji. 

  “Kata ya Chibe ina wakazi zaidi ya 3,000 na kuna mitaa minne ambayo ni Busambilo,Chibe,Mwalugoye na Mwamapalala,mitaa yote ina shida ya maji,wananchi wa Mwamapalala walijitolea kuchimba kisima nikamuomba mheshimiwa Gulam atupatie msaada wa pampu na leo ametupatia,tunamshukuru sana”,alieleza Kisandu. 
  Zoezi la kushusha pampu ya maji kwenye gari likiendelea wakati Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikabidhi pampu ya maji na mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kisima kirefu cha maji katika kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
  Kaimu Mhandisi wa maji manispaa ya Shinyanga Nkinda Seni (wa nne kushoto) akishusha mabomba ya pampu ya maji.Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam 
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati wa kukabidhi pampu ya maji na mifuko ya saruji kwa diwani wa kata ya Chibe John Kisandu kwa ajili ya ujenzi wa kisima kirefu katika mtaa wa Mwamapalala. Kushoto ni pampu ya maji na mifuko ya saruji. 
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akishikana mkono na diwani wa kata ya Chibe John Kisandu wakati wa akikabidhi pampu ya maji na mifuko ya saruji.Wa kwanza kulia ni Kaimu katibu mkuu ALAT,Abdallah Ngodu na Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,Rajabu Masanche wakishuhudia zoezi la makabidhiano. 
  Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mhandisi wa maji manispaa ya Shinyanga Nkinda Seni na Katibu tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi wakishuhudia tukio la makabidhi 
  Kaimu katibu mkuu ALAT,Abdallah Ngodu akimpongeza Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam (kushoto) kwa kutoa msaada wa pampu ya maji katika kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga. 
  Kaimu katibu mkuu ALAT,Abdallah Ngodu akishikana mkono na diwani wa kata ya Chibe,John Kisandu.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

   Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (aliyesimama) akizungumza wakati walipofanya ziara ya kujionea miradi ya kilimo mkoani Simiyu.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Kilimo, Bibi Rosebud Kurwijila (kulia) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) kuhusu nafasi ya TADB katika kuwasaidia wakulima nchini.
   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Kilimo (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kati ya uongozi wa Mkoa huo, wataalam wa kilimo, mifugo na ushirika na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Kilimo.
   Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bw. Dome Malosha (kulia) akizungumza katika Kikao na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
  Mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Kilimo nchini, Bw. Joseph Mutashubilwa (wapili kulia) akichangia hoja wakati wa walipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka (hayupo pichani).

  Na Mwandishi wetu, Simiyu 
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka  ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuuwezesha mkoa wa Simiyu katika kufanya mapinduzi ya Kilimo kupitia miradi ya kimkakati inayotekelezwa mkoani humo.
  Bw. Mtaka amesema mkoa wa Simiyu umejipanga kutumia fursa za mikopo nafuu inayotolewa na TADB ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha wakulima wanalima kisasa ili kuleta mapinduzi ya kilimo nchini.
  Bw. Mtaka aliongeza kuwa Mkoa wa Simiyu uko tayari kufanya kazi na Benki ya Kilimo kupitia vikundi vya uzalishaji, Halmashauri na Miradi mbalimbali inayotekelezwa mkoani humo, ikiwa ni pamoja na miradi ya mfano ya umwagiliaji ya Mwamanyili Wilayani Busega  ulio katika hatua ya upembuzi yakinifu na Mwasubuya wilayani Bariadi ambao uko katika hatua ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.
  “Tungehitaji kuwa Mkoa ambao kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo tungetengeneza namna ambayo ingewasaidia wakulima na ikasaidia mikoa mingine kuja kuona maendeleo ya kilimo  ambayo ni matokeo ya Serikali kuwekeza katika Benki ya Kilimo” amesema Mtaka.
  "Sisi kama Mkoa tumejipanga, tumetoa Elimu ya utayari na
  namna ya utekelezaji wa shughuli zote kwa wataalam wetu pamoja na wananchi na isitoshe tayari tumeshafanya utafiti na kuandaa mwongozo wa uwekezaji ndani ya mkoa, hivyo tunawakaribisha kuwekeza,” aliongeza.
  Aidha, Bw.Mtaka ameongeza kuwa Mkoa wa Simiyu unatekeleza Sera ya Uchumi wa Viwanda chini ya Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” ambapo hadi sasa kuna kiwanda cha chaki na maziwa na miradi mingine minne ya viwanda iko katika upembuzi yakinifu.
  “Hivyo Benki ya Kilimo inaweza kuwekeza katika miradi hii kwa kuwawezesha wakulima na wafugaji kuzalisha malighafi ya Viwanda hivyo au kuwa mdau katika viwanda hivyo,” aliomba.
  Kwa upande, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila alisema kuwa Benki ya Kilimo imejizatiti katika kuchangia kwa kiasi kikubwa katika  kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo kwa wakulima wa Tanzania ili kusaidia upatikanaji wa fedha na sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.

  Bibi Kurwijila alisema kuwa katika kutekeleza mkakati wa kuwafikia wakulima wengi zaidi nchini TADB imejipanga kutoa huduma kupitia kongani mpya nane (8) ili kuongeza tija kwa wakulima nchini.

  Alizitaja Kongani hizo kuwa ni pamoja na Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Mashariki. Nyingine ni Kanda ya Magharibi, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kusini na Zanzibar.

  “Kongani ni njia ya kimkakati ya kijiografia yenye kujikita katika shughuli za kilimo zinazohusiana, wasambazaji, na taasisi zinazohusishwa katika kujenga usawa wa moja kwa moja miongoni mwa wadau, hivyo ili kukidhi mahitaji ya wakulima nchini, benki ya kilimo itawafikia kupitia njia hii,” alisema.

  Naye Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB Augustino Matutu Chacha  amesema wamefurahishwa na utayari wa Mkoa wa Simiyu juu ya kuwawezesha wakulima na Benki hiyo iko tayari kutoa mikopo pia kwa wakulima wa zao la pamba ambao wanazalisha zaidi ya asilimia 60 ya pamba yote nchini ili izalishwe kwa wingi zaidi na katika ubora wa hali ya juu.
  Bw. Chacha amesema wataalam wa kilimo wa Mkoa wa Simiyu kwa kushirikiana na wataalam wa benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) watakutana ili kuona namna watakavyofanya kazi kwa pamoja ili mikopo itakayotolewa iweze kuwa wa manufaa kwa wakulima na nchi kwa ujumla.
  Aidha amewaeleza Wakurugenzi wa Halmashauri zote kuwa, Halmashauri zinaweza kupatiwa mikopo ili ziweze kuendesha miradi ya kilimo itakayoweza kuwa  vyanzo vipya vya mapato kwa Halmashauri zao.

  0 0

  Mwenyekiti kamati ya Ufundi Bw. Stephen Mapunda kutoka timu ya Majimaji akimkabidhi tuzo maalumu Waziri Makamba kwa kutambua mchango wake katika kukuza timu yao na kuwasaidia kupata ufadhili. Wengine ni Mwenyekiti Bw. Stephen Ngonyani na Shabiki wa timu​ ​hiyo​ ​Bw.​ ​Vian​ ​Nchimbi. 
  Viongozi wa timu ya Majimaji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi tuzo aalumu kwa Waziri Makamba kwa kutambua mchango wake katika kukuza timu yao na kuwasaidia kupata ufadhili. Kushoto ni Mwenyekiti wa Timu hiyo Bw. Stephen Ngonyani, Mwenyekiti Kamati ya Ufundi Bw. Stephen Mapunda na shabiki wa timu hiyo Bw. Vian Nchimbi. 
  Viongozi​ ​wa​ ​Timu​ ​ya​ ​Majimaji​ ​wakiwa​ ​Ofisi​ ​kwa​ ​Waziri​ ​Makamba.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  WAKALA wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) imewataka wanachuo waliopata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo kutilia mkazo suala hilo utovu wa nidhamu unaweza kuwakosesha na kuondolewa kwenye mchakato huo ambapo tayari wanafunzi sita wameondolewa.

  Akizungumza na baadhi ya wanafunzi hao katika mkutano wa majadiliano ya tathmini ya utekelezaji wa mafunzo kwa vitendo kwa wanachuo 100 wa mwaka wa kwanza  kutoka Chuo Kikuu ca Dar es Salaam kwa awamu ya kwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa TaESA Boniface Chandaruba amesema kuwa wanafunzi wanatakiwa kutilia mkazo suala hili kwani wameweza kupata nafasi ya kipekee kwa kuwezeshwa kufanya mafunzo ya vitendo ikiwa bado hawajamaliza chuo.

  Chandaruba amesema kuwa, ILO imeweza kuleta mradi huo kwa lengo la kuwaandaa wanachuo pindi wanapomaliza chuo wanakuwa tayari wameshapata uzoefu pia hata zile taasisi wanazofanyia kazi wanauwezo wa kuwapa ajira.
   Mkurugenzi Mtendaji wa  Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania  (TaESA) Boniface Chandaruba akizungumza na baadhi ya wanachuo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kati ya wanachuo 100 walioteuliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa kushirkiana na Wakala wa Serikali  waliokatika mradi wa awali kwa wanachuo wa mwaka wa kwanza  kupata mafunzo kutoka kwa mashirika na taasisi mbalimbali ikiwa ni katika kipindi cha miaka 3.
  Mradi huu unaodhaminiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) umelenga hasa katika kuwasaidia wanafunzi hususani wana vyuo kupata uzoefu utakaowasaidia baadae katika kupata ajira ikiwemo kufahamu mazingira tofauti ya kazi pale wanapofanyia lwa kipindi cha mafunzo kwa vitendo.

   Kwa upande Mshauri  wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Paulina Mabuga amesema kuwa mradii ni mzuri pia unaweza kuwasaidia wanavyuo kupata uzoefu katika maeneo wanayofanyia kazi na mategemeo yao makuu ni idadi inaongezeka katika awamu ya pili ya wanafunzi watakaochaguliwa kwa ajili ya mafunzo hayo kwa vitendo.

  Moja ya waajiri kutoka Baraza la Sanaa la Taifa ( BASATA) Kitengo cha Fedha na utawala Onesmo Kayanda amewataka wanafunzi wanaopata nafasi kama hiyo kujituma zaidi na kujitolea kwani unapokuwa unafanya vizuri unakuwa unajenga uzoefu mzuri na hata waajiri wanaweza kupendezewa na juhudi zao na hatimaye kukuajiri kabisa.

  Wanafunzi hao wameonekana kupendezwa zaidi na hatua hii ya TaESA na ILO kwa kupewa nafasi hiyo ya kupata mafunzo kwa vitendo na pia chuo chao kikiwa cha kwanza kwenye mradi. 
  Mshauri wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Paulina Mabuga akizungumzia mradi wa utekelezaji wa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi 100 unaoratibiwa na Wakala wa Huduma kwa Ajira Tanzania (TaESA) wakishirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO).Moja ya waajiri kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kitengo cha fedha na utawala Onesmo Kayanda akizungumza namna walivyoweza kushirikiana na wanachuo hao katika mradi huo na kama angepewa nafasi ya kuwaajiri basi angetoa ajira kwa wanachuo watatu ambao wamefanya vizuri sana kwa kipindi cha miaka mitatu.
  Moja ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha Takwimu akizungumzia mardi huo na jinzi gani umeweza kumsaidia kwa kuweza kukutana na watu mbalimbali pia uzoefu alioupata kupitia mafunzo kwa vitendo.

  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha.

  Hifadhi ya Wanyamapori ya Randlen Community Wildlife Management, iliyoko Arusha wilayani Monduli imekabidhiwa gari aina ya Suzuki Jimmy kwa ajili ya kudhibiti vitendo vya ujangili na uharibifu wa mazingira katika hifadhi hiyo ya jamii.

  Akipokea gari hilo kutoka Shirika la Honey Guide, Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddi Hassan alisema,  gari hilo litasaidia juhudi za kupambana na ujangili katika wilayani humo na kukuza utalii endelevu kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

  Akizungumza baada ya kupokea gari hilo, Hassan amesema msaada huo utasaidia kuimarisha shughuli za uhifadhi Wilayani humo, kwa kuwa kuwa hifadhi hiyo ni hifadhi pekee inayofanya vizuri katika wilaya hiyo na kunufaisha vijiji tisa vinavyozunguka hifadhi.

  Alisema,msaada huo wa gari utaongeza nguvu katika mapambano dhidi ya ujangili hasa hasa katika kipindi hiki ambacho wanajipanga katika kuzuia uvunaji holela wa maliasili katika hifadhi hiyo pamoja na kuzuia ujangili

  kwa upande wake, mwenyekiti wa Honey Guide Foundation Olekiri Mbai alisema, wameamua kutoa msaada huo unaogharimu kiasi cha shilingi milioni 25 ili  kusaidia shughuli za uendeshaji wa hifadhi hiyo ya jamii (WMA) katika kuunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha kuwa uhifadhi unafanyika kwa namna ambayo unanufaisha wanajamii wa Monduli.

  “Kumekua na changamoto ya Hifadhi nyingi kutokuwa na Meneja lakini hifadhi ya Randilen ni hifadhi pekee yenye meneja ambaye anasimamia shughuli zote za utawala hivyo msaada huu wa gari utamsaidia kutekeleza majukumu yake ya kila siku” Alisema Olekiri

  Mwenyekiti wa Hifadhi hiyo Daniel Alais ameshukuru shirika la Honey Guide kwa kutoa msaada huo ambao utasaidia kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya ujangili na uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kurahisisha utendaji kazi wa kila siku.


  Mwenyekiti wa HoneyGuide Foundation Olekiri Mbai akikabidhi gari aina ya Suzuki Jimmy kwa Mkuu wa Wilaya wa Monduli Iddi Hassan ikiwa ni msaada wa shirika hilo katika kusaidia hifadhi ya wanyamapori ya Randilen


  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa hafla fupi ya maadhimisho ya siku ya mtoto njiti dunia leo Jijini Dar es Salaam. Maadhimisho ya mwaka huu yameratibiwa na Shirika la Msaada wa Maendeleo la Ujerumani (GIZ) wanaofadhili ,mradi wa kukabiliana vifo vya watoto wenye umri mdogo. Kutoka kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Dkt. Detlef Wachter. Meneja Programu Yakusaidia Afya Tanzania -German, GIZ Dkt. Susanne Grimm na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dk. Wedson Sichalwe.
   Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Dkt. Detlef Wachter akielezea jambo wakati wa hafla fupi ya maadhimisho ya siku ya mtoto njiti dunia leo Jijini Dar es Salaam. Maadhimisho ya mwaka huu yameratibiwa na Shirika la Msaada wa Maendeleo la Ujerumani (GIZ) wanaofadhili ,mradi wa kukabiliana vifo vya watoto wenye umri mdogo. 
    Meneja Programu Yakusaidia Afya Tanzania -German, GIZ Dkt. Susanne Grimm akielezea jambo wakati wa hafla fupi ya maadhimisho ya siku ya mtoto njiti dunia leo Jijini Dar es Salaam. Maadhimisho ya mwaka huu yameratibiwa na Shirika la Msaada wa Maendeleo la Ujerumani (GIZ) wanaofadhili ,mradi wa kukabiliana vifo vya watoto wenye umri mdogo. Kutoka kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Dkt. Detlef Wachter, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dk. Wedson Sichalwe.
   Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt. Wedson Sichalwe akielezea jambo wakati wa hafla fupi ya maadhimisho ya siku ya mtoto njiti dunia leo Jijini Dar es Salaam. Maadhimisho ya mwaka huu yameratibiwa na Shirika la Msaada wa Maendeleo la Ujerumani (GIZ) wanaofadhili, mradi wa kukabiliana vifo vya watoto wenye umri mdogo. Kutoka kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Dkt. Detlef Wachter, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya na Meneja Programu Yakusaidia Afya Tanzania -German, GIZ Dkt. Susanne Grimm.
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akipokea vifaa kwa ajili ya kutolea huduma za matibabu kwa watoto njiti kutoka kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Dkt. Detlef Wachter katika hafla ya maadhimisho ya siku ya mtoto njiti dunia iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Vifaa hivyo vyenye gharama ya Euro 8,538.30 vimetolewa na Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo  Ujerumani(GIZ) kupitia mradi wa kukabiliana vifo vya watoto wenye umri mdogo.
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Dkt. Detlef Wachter wakionyesha vifaa kwa ajili ya kutolea huduma za matibabu kwa watoto njiti katika hafla ya maadhimisho ya siku ya mtoto njiti dunia iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Vifaa hivyo vyenye gharama ya Euro 8,538.30 vimetolewa na Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo Ujerumani(GIZ) kwa ajili ya kusaidi Hospitali za Mikoa ya Mtwara na Lindi iliyo katika mradi wa kukabiliana vifo vya watoto wenye umri mdogo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Dkt. Detlef Wachter wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya mara baada ya kumalizika kwa hafla ya maadhimisho ya siku ya mtoto njiti dunia iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na: Frank Shija -MAELEZO)


  0 0


  Ecobank Tanzania’s Managing Director, Ms. Mwanahiba Mzee (far right) and the bank’s Head of Commercial Banking, Mr. Respige Kimati (left) in a souvenir photo with the Prime Minister, Honorable Majaliwa Kassim Majaliwa when they paid a courtesy call at his office in Dodoma
  Ecobank Tanzania’s Managing Director, Ms. Mwanahiba Mzee (left) and the bank’s Head of Commercial Banking Mr. Respige Kimati (far right) met with the National Assembly Speaker, Honorable Job Ndugai in Dodoma recently during a courtesy visit to his office. 


  0 0

  Msaidizi wa Rais Kanali Msafiri Mkeremy akimkabidhi Imamu wa Msikiti wa Noor kijijini Mkange, Miono, Wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani Sheikh Khamis Nassor wakati alipowasilisha msaada wa zulia la kuswalia msikitini hapo akiwa kaongozana na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Jaffary Haniu (nyuma ya Imamu) leo Novemba 17, 2017.
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

  Waumini wa dini ya Kiislam wa Msikiti wa Noor uliopo katika Kijiji cha Mkange, Miono,  Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani, wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada wa zulia la kuswalia na fedha taslim Shilingi milioni Mbili.
  Zulia pamoja na fedha hizo zimekabidhiwa na Msaidizi wa Rais Kanali Mbaraka Mkeremy kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Imamu wa Msikiti huo Alhaji Sheikh Khamis Nassor wa Msikiti Noor uliopo katika kijiji cha Mkange, Wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani.
  Mara baada ya kukabidhi Zulia na fedha hizo, Kanal Mkeremy kwa niaba ya Rais Magufuli amewataka waumini wa Msikiti huo kutumia msaada huo kwa lengo lililokusudiwa.
  Akiungumza mara baada ya kukabidhiwa Msaada huo, Sheikh Nassor amesema kwa niaba ya waumini wa Msikiti huo wanamshukuru Mhe. Rais kwa kuitikia ombi lao la kupata zulia, na kwamba  kwa kutimiza ahadi yake hiyo Mhe. Rais amedhihirisha kuwa yeye ni mtu wa watu asiyebagua dini wala kabila katika kusaidia jamii ya kitanzania.
  Sheikh Nassor amesema waumini wa msikiti huo wanamuombea na wataendelea  kumuombea Mheshimiwa Rais na kuwataka watanzania wote nchini kuungana nao kumuombea Rais bila kujali itikadi za kisiasa ama imani za kidini kwani anayoyafanya Rais kwa wananchi wa Tanzania ni kwa manufaa ya wananchi wote.

  Jaffar Haniu
  Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Pwani
  17 Novemba 2017.

  0 0


  0 0


  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akimsikiliza mmoja kati ya madaktali wa hospitali ya Jeshi hilo iliyopo barabara ya Kilwa, wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba vilivyotolewa na serikali ya Marekani, vifaa vyenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni mbili, kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaofika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.
  Mkuu wa kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi (SACP) Paul Kasabago (kushoto), akitoa neno la shukurani wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba vilivyotolewa na serikali ya Marekani, kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaofika katika hospitalini ya Jeshi hilo iliyopo barabara ya kilwa kwa ajili ya matibabu.

  Baadhi ya vifaa tiba vilivyotolewa na serikali ya Marekani na kukabidhiwa Jeshi la Polisi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaofika katika hospitalini ya Jeshi hilo iliyopo barabara ya kilwa kwa ajili ya matibabu.

  Picha na Jeshi la Polisi.

  0 0


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa TFC, Bw. Henry Mwantwinza Mwimbe.

  Na Daniel Mbega

  SHIRIKISHO la Vyama  vya Ushirika Tanzania (TFC) limeanza zoezi la kukusanya taarifa na kuhakiki wanachama ili kuimrisha kanzidata yake.

  Akizungumza na MaendeleoVijijini, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa TFC, Bw. Henry Mwantwinza Mwimbe, amesema zoezi hilo litarahisisha utendaji wa shirikisho katika kuwafikia wanachama wake pamoja na kujua changamoto na vipaumbele ili kusukuma mbele maendeleo ya kiuchumi.
  “Tunahitaji tupate idadi halisi ya wanachama wetu kwa sababu tunaamini kwa sasa wameongezeka na hiyo itatusaidia kuweza kuwafikia kwa urahisi tukitambua kila mwanachama anajishughulisha na nini, na nini changamoto zake pamoja na vipaumbele,” alisema Mwimbe.

  Mwimbe amesema kwamba, jukumu la TFC ni kusimamia vyama vya ushirika, lakini katika wakati huu ambao taifa linahitaji kujenga uchumi wake na kuongeza kipato cha kila Mtanzania ili kufikia uchumi wa kati, ni vyema kutambua na kufuatilia kwa karibu shughuli zinazofanywa na wanachama hao.

  Amesema asilimia zaidi ya 80 ya wanachama wao wanajihusisha na shughuli za kilimo ambapo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za ukame, pembejeo pamoja na masoko, hivyo kwa kuimaridha kanzidata yao watakuwa na uwezo wa kutambua fursa na changamoto zilizopo katika maeneo yote.

  “Lazima tuweke kumbukumbu sahihi, kwa sababu hii itasaidia, kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo, kutafuta changamoto za wakulima pamoja na kuwatafutia fursa, hasa za pembejeo na masoko.

  “Kwa kuwa tutakuwa na mawasiliano yote ya wanachama, tunakusudia kuwaunganisha na masoko ya ndani na yale ya nje kupitia simu za mkononi,” amesema Mwimbe.

  Aidha, amesema kwamba, kwa kuimarisha kumbukumbu hizo itawasaidia hata wao TFC kutambua makisio ya uzalishaji wa mazao mbalimbali kwa msimu.

  “Kumbukumbu hizi ni muhimu, tunaweza kuwa tunajua kwamba kwa msimu huu, mathalan tumbaku limelimwa katika eneo lenye ukubwa gani na makisio ya mavuno ni kiasi gani, vivyo hivyo kwa mazao mengine kama kahawa, pamba, mahindi, mbaazi, ufuta, korosho na mengineyo.

  “Kama tukipata taarifa kutoka nje kwamba kuna watu au kampuni inahitaji tani kadhaa za pamba ni rahisi kuwaunganisha wananchama wetu moja kwa moja na kampuni hizo na wakauza kwa uhakika zaidi,” amesema.


  Kuhusu TFC

  TFC ndiye mrithi wa uliokuwa Muungano wa Vyama vya Ushirika Tanzania (CUT) na ilibadilishwa kufuatia sera mpya na kuanzishwa kwa Sheria mpya ya Ushirika ya mwaka 2003 ambayo ilikuwa mbadala wa Sheria ya Ushirika ya mwaka 1991 iliyokuwa inaeleza kwamba vyama vya ushirika vilikuwa kama sehemu ya vikundi vya kisiasa vya chama tawala.

  Kwahiyo, Sheria mpya ya Ushirika ya mwaka 2003 inaelezea tu usimamizi wa vyama vya ushirika na wanachama wanastahili kuwa na sauti na ushiriki wa moja kwa moja.

  TFC ni chombo kinachojitegemea kisichofungamana na upande wowote kikiwa kinamilikiwa na wanachama wenyewe katika mukhtadha wa kufuata sheria na kanuni za kimataifa za ushirika.

   Kwahiyo, TFC ni mwanachama wa Umoja wa Kimataifa wa Ushirika (International Co-operative Alliance - ICA), Shirikisho la Wakulima Afrika Mashariki (East African Farmers Federation - EAFF), Shirikisho la Kimataifa la Wazalishaji Bidhaa za Kilimo (International Federation of Agricultural Producers - IFAP) na Committee of Artisanal and Workers Cooperatives (CICOPA). 

  Kitaifa, TFC ni mwanachama mwanzilishi wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na Baraza la Kilimo Tanzania (Agricultural Council Tanzania - ACT), zamani likijulikana kama Tanzania Chamber of Agriculture and Livestock.

  TFC inashirikiana na wadau kadhaa wa kitaifa na kimataifa kama wizara za Seriali, Shirika la Kazi Duniani (ILO), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Muungano wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO), na kadhalika.


  Wanachama wa TFC

  TFC ilisajiliwa rasmi Desemba 8, 1994 ikiwa na Hati ya Usajili Namba 5503 ambapo wanachama waanzilishi walikuwa 13 tu.


  Pamoja na kwamba hivi sasa wanakusanya na kuhakiki taarifa kwa ajili ya kanzidata, MaendeleoVijijini inafahamu kwamba, hadi kufikia mwaka 2015 TFC ilikuwa na vyama wanachama 3,339 Tanzania Bara vyenye wanachama mmoja mmoja zaidi ya milioni 1.5.


  0 0

  Kiongozi wa msafara wa wawakilishi wa kampuni ya Henan Juren Crane Group kutoka Jimbo la Henan nchini China, Wang Yuheng (wa pili kulia) akisisitiza jambo wakati alipokutana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Bw. Henry Mwatwinza Mwimbe (kulia). Tukio hili lilifanyika jana, Alhamisi, Novemba 16, 2017 jijini Dar es Salaam.

  Na Daniel Mbega

  WANANCHI wa mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga na Simiyu wanaweza kujikwamua kiuchumi kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji ifikapo mwaka 2019 kutokana na kuwepo kwa mpango wa uwekezaji unaolenga kuchimbia visima virefu pamoja na mabwawa katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd), Bw. Henry Mwantwinza Mwimbe, amesema hayo jana baada ya kukutana na wawakilishi wa kampuni ya Henan Juren Group ya China, ambayo imeonyesha nia ya kuwekeza kwa ubia nchini kwa kutengeneza zana mbalimbali za kilimo ikiwa ni pamoja na kuchimba visima katika maeneo yaliyo kame.

  Lengo la uwekezaji huo, kwa mujibu wa Mwimbe, ni kuwakwamua wakulima kiuchumi kwa kuwa na kilimo endelevu cha umwagiliaji badala ya kutegemea mvua, ambazo zimekuwa hazina uhakika kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi yanayotokana na uharibifu wa mazingira.

  “Wanachama wetu karibu asilimia 80 wanajihusisha na kilimo, hivyo tunaona itakuwa ni vyema kama tutabadilisha namna ya uendeshaji wa kilimo hiki ili kilete tija kwao na kwa taifa kwa ujumla.

  “Katika maeneo mengi mvua zinanyesha mara moja kwa mwaka na wakati mwingine siyo za kutosha, matokeo yake wananchi wanashindwa hata kupata mavuno yanayojidhi matumizi ya nyumbani, achilia mbali ziada ya kuuza sokoni, lakini kilimo cha umwagiliaji kina uhakika na kinaweza kuendeshwa wakati wote wa mwaka,” alieleza Mwimbe.

  Alisema kwamba bado wapo katika hatua za awali kuhusu mchakato huo na akafafanua kwamba, mradi huo utawahusisha wanachama wote nchini walio kwenye ushirika ambao watashirikishwa.

  Hata hivyo, alisema mradi mama ni kuunganisha (assembling) zana za kilimo kutoka China kama matrekta na mashine nyingine zinazoendana na kilimo watakazoziuza kwa wakulima wa ndani pamoja na nchi jirani, lakini wanaona kwamba hilo litafanikiwa ikiwa wakulima watajengewa uwezo hasa kwa kuwa na uhakika wa maji ili kuendesha kilimo cha umwagiliaji.

  Mkalimani, Dkt. Chikira Ismail Msangi, akifasili kuhusu azma ya wawekezaji hao katika kuanzisha kampuni ya ubia itakayounganisha zana za kilimo kama matrekta na mitambo ya uchimbaji visima na umwagiliaji hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Bw. Henry Mwimbe. Tukio hili lilifanyika jana, Alhamisi, Novemba 16, 2017 jijini Dar es Salaam.
  “Vijijini watu wana matrekta lakini yanatumika mara moja tu kwa mwaka kwa sababu ya kutegemea mvua, kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji ni wazi kwamba wakulima watahitaji nyenzo zaidi ili kurahisisha kilimo chao, lakini lazima kwanza maji yapatikane.

  “Israel ni nchi ya jangwa, lakini leo ukienda imebadilika kutokana na kuwepo kwa visima vilivyochimbwa pamoja na mabwawa na wanalima mazao mengi yenye ubora na kuyasafirisha duniani kote, sisi Tanzania tunayo ardhi ya kutosha ambayo tunashindwa kuitumia kwa kuwa tu mahali pengi hakuna vyanzo vya uhakika vya maji.

  “Shinyanga, Simiyu, Tabora, Singida, Dodoma na Manyara ni mikoa ambayo ina shida kubwa ya maji japo ina ardhi kubwa, lakini kama watachimbiwa visima wanaweza kufanya kilimo kwa uhakika na kuwavutia hata vijana wanaokimbilia mijini kutafuta ajira,” alisema.

  Mwimbe alisema kwamba, katika maeneo ambayo yana mito na vijito kama ya mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Rukwa, Katavi na mingineyo, wanaweza kuchimbiwa mabwawa makubwa ya kuvuna maji ya mvua ambayo yatatumika kwenye kilimo cha umwagiliaji wakati wa kiangazi.


  Wachina wako tayari

  Hii ni mitambo itakayounganishwa hapa nchini ambayo ni maalum kwa shughuli za ujenzi na uchimbaji wa mabwawa ya maji.
  Bw. Henry Mwimbe (kulia) Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa TFC akionyesha kufurahishwa na picha za mitambo ya uchimbaji mabwawa. Tukio hili lilifanyika jana, Alhamisi, Novemba 16, 2017 jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa TFC, Bw. Henry Mwimbe (kulia), alitazama zana na mitambo mbalimbali ambayo itaunganishwa hapa nchini katika uwekezaji wa pamoja baina ya TFC na kampuni ya Henan Juren Cranes Group kutoka China. Tukio hili lilifanyika jana, Alhamisi, Novemba 16, 2017 jijini Dar es Salaam.
  Uchunguzi wa MaendeleoVijijini unaonyesha kwamba, wawekezaji hao kutoka China wako tayari kwa mradi huo na kwamba wanaweza kukaa chini na TFC kuangalia namna gani utakavyoendeshwa.

  Mmoja wa wawakilishi hao, Wang Yuheng, alisema lengo kubwa ni kuleta teknolojia ya wakulima wa chini ili kuinua kilimo chao kilete tija na ikiwezekana wazalishe bidhaa wanazoweza kuzisafirisha nje ya nchi.

  “Tunataka kuja kuwaletea teknolojia wakulima wa hali ya chini, tunajua zana za kilimo zinaweza kurahisisha kilimo chao, lakini tutazungumza na TFC ili kuona vipaumbele vyao vingine katika kilimo ni nini, mbali ya upatikanaji wa maji,” alisema Wang.

  Wang alisema kwamba, zana zote hizo zitakuja kuunganishwa hapa hapa Tanzania badala ya kuziingiza zikiwa tayari, hali ambayo itasaidia pia taifa kuingiza fedha za kigeni pamoja na kutoa ajira kwa vijana wa Tanzania pamoja na kujifunza ujuzi mbalimbali.

  Maofisa wengine walioongozana na Wang ni Si Yongbin, Si Guanlei na Zhai Qinwu ambao kila mmoja ni mtaalam wa teknolojia mbalimbali.


  Watembelea EPZA

  Wawakilishi hao wa kampuni ya Henan Juren Group, jana walitembelea Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji (EPZA) jijini Dar es Salaam ambapo walionyesha kuridhishwa kwa kiwango kikubwa na maelezo waliyopewa kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo nchini.

  Mkuu wa Mawasiliano ya Umma wa EPZA, Nyanda Shuli, aliwatoa mashaka kwamba hakuna urasimu wowote kwa wawekezaji, wawe wa ndani au wa nje, na kuwahakikishia kwamba mazingira ya uwekezaji nchini Tanzania ni rafiki.

  “Tunayo maeneo mengi ya uwekezaji hapa nchini na kilimo kinapewa kipaumbele kikubwa kwa sababu ndicho kinachozalisha malighafi za viwanda, ardhi inayofaa kwa kilimo imetumika kwa asilimia 35 tu, hivyo bado kama taifa tunahitaji kuwekeza zaidi ili tuzalishe bidhaa za kuuza nje,” alisema Nyanda.

  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa TFC, Henry Mwimbe (wa pili kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya wadau katika makao makuu ya Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji Tanzania (EPZA) jijini Dar es Salaam jana, Alhamisi, Novemba 16, 2017.
  Bw. Nyanda Shuli (wa pili kulia mwenye miwani), Mkuu wa Mawasiliano ya Umma wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji Tanzania (EPZA), akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa TFC, Bw. Henry Mwimbe (wa tatu kushoto) pamoja na ujumbe wa kampuni ya Henan Juren Cranes Group kutoka China walipotembelea makao makuu ya EPZA jana Alhamisi, Novemba 16, 2017.
  Bw. Nyanda Shuli akifafanua jambo katika mkutano huo.

  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika wa TFC, Bw. Henry Mwimbe (kulia) na ujumbe wa wawekezaji kutoka China wakimsikiliza kwa makini Bw. Nyanda Shuli wa EPZA (hayupo pichani).

  Ofisa Mwandamizi wa Promosheni wa EPZA, Bi. Nakadongo Fares (kulia) akisisitiza jambo kwa ujumbe wa wawekezaji kutoka China na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) wakati walipotembelea makao makuu ya EPZA, Ubungo External, jijini Dar es Salaam, jana Alhamisi, Novemba 16, 2017.
  Nyanda aliongeza kwamba, kuna maeneo ya kutosha kwa uwekezaji huko Bagamoyo ambayo yako chini ya EPZA hasa kutokana na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo itakayokuwa mkombozi kwa Watanzania kiuchumi.

  “Pale zitakuja meli kubwa na mizigo, lakini tunataka zikipakua mizigo hiyo ziondoke na mizigo mingine kutoka hapa, kama Watanzania watakuwa wamezalisha bidhaa hata zitokanazo na mazao ya kilimo itakuwa fursa kubwa kupeleka nje,” alisema.

  Kwa upande wake, Ofisa Mkuu wa Promosheni, Bi. Nakadongo Fares, alisema kuna unafuu mkubwa kwa wawekezaji kutoka nje wanaopitia EPZA kuliko kama wakija wenyewe moja kwa moja, kwani mamlaka hiyo inayo maeneo tayari yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa kila aina.

  “Uunganishaji wa matrekta unafanyika hapa pamoja na viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ambayo yanasafirishwa nje kwa ubora wa hali ya juu, tunashauri hata mitambo na zana zenu mje mziunganishie hapa hapa ili kutoa na ujuzi kwa Watanzania,” alisema Bi. Fares.


  Kuhusu Henan Juren Group

  Kampuni ya Henan Juren Crane Group ipo katika Mtaa wa Weizhuang Industrial Park, katika kitongoji cha Changyuan, jijini Xinxiang katika Jimbo la Henan katika Bara China, na inaongozwa na Bw. Jason Zhang.

  Kampuni hiyo, ambayo awali ilijulikana kama Henan Juren Crane Co., Ltd, ilianzishwa mwaka 1987 ikijihusisha zaidi na utengenezaji wa crane, lakini sasa inazo kampuni tanzu kama Henan Juren Crane Services Co., Ltd., Henan Juren Advertisement Co., Ltd. na Hexin Machinery & Electronic Co., Ltd ambayo inajihusisha zaidi na utengenezaji na zana mbalimbali zikiwemo za kilimo na umeme. 

  Kampuni hiyo ina mtaji wa Yuan za Kichina RMB120,000,000 (takriban Dola za Kimarekani 18,108,561.60), na rasilimali zenye thamani ya Yuan 200,000,000 (sawa na Dola 30,180,936.00) ambapo inazo karakana tatu katika wilaya ya kusini, wilaya ya kaskazini na wilaya mpya huku ikimiliki eneo lenye ukubwa wa meta za mraba 460,000 na wafanyakazi zaidi ya 1,200.

  Kwa mujibu wa rekodi za mwaka 2001, uchunguzi unaonyesha kwamba, mapato yalikuwa kati ya Dola 2.5 milioni na Dola 5 milioni.
  Hizi ni crane na madaraja maalum yanayoundwa na kampuni ya Henan Juren Cranes Group inayotaka kuwekeza nchini.
  Makao makuu ya kampuni ya Henan Juren Cranes Group katika Jiji la Xinxiang katika Jimbo la Henan nchini China.


   Imeandaliwa na www.maendeleovijijini.blogspot.com. +255 656 331974.

  0 0


older | 1 | .... | 1432 | 1433 | (Page 1434) | 1435 | 1436 | .... | 1897 | newer