Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

BALOZI WA CHINA AAHIDI KUCHIMBA KISIMA DODOMA

$
0
0
Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge ambapo aliahidi kutoa msaada wa kuchimba kisima kimoja cha maji Mkoani Dodoma.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) na Balozi wa China Mheshimiwa Wang Ke (wa pili kulia) mara baada ya kumalizika mazungumzo yao, kushoto ni Katibu Tawala Mkoa Dodoma Ndg. Rehema Madenge na kulia ni Afisa kutoka Ubalozi wa China.

……………..


Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Makao Makuu

Balozi wa China hapa nchini Mhe.Wang Ke ameahidi Serikali yake itatoa msaada wa kugharamia mradi wa uchimbaji kisima kimoja cha maji na miundombinu ya usambazaji wa huduma hiyo kwenye moja ya kijiji cha Mkoa wa Dodoma.

Balozi Wang Ke alimuahidi msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge leo alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo Ofisini kwake Mjini Dodoma, ambapo alimtaka Dkt. Mahenge kutumia timu ya Watalaalamu wa Maji wa Mkoa kufanya usanifu na makadirio ya bajeti ya mradi huo na kuiwasilisha Ofisi za Ubalozi wa China kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi.Aidha, Balozi Wang Ke ameelezea kuwa Uongozi wa Mkoa utaainisha ni kijiji kipi ambacho kitapewa fursa ya kupatiwa mradi huo.

Kwa upande wake, Dk. Mahenge ameishukuru Serikali ya China kupitia kwa Balozi Wang Ke kwa ajili ya mradi huo na amebainisha kuwa mradi huo pia unaweza ukatumika kuwasaidia vijana kwenye kijiji kitachopewa mradi kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji. Dkt. Mahenge amemwelezea Balozi Wang Ke kuwa amefanya ziara kwenye Wilaya za Mkoa wa Dodoma na amejionea namna ambavyo wananchi wanahitaji kubwa la maji na hivyo mradi huo umekuja wakati muafaka kabisa.

Katika mazungumzo ya Viongozi hao, mradi huo utahusisha Utafiti wa uwezekano wa kupata maji chini ya Ardhi, Uchimbaji wa Kisima kirefu, ununuzi wa mashine ya kuvuta na kusukumia maji, ujenzi wa Miundombinu ya kusambazia maji, Tenki la kuhifadhia maji na vituo vya wananchi kuchotea maji.

TUME YAPOKEA TAARIFA YA KUWEPO NAFASI WAZI KATIKA MAJIMBO 2 NA KATA

$
0
0


MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JAJI (R) SEMISTOCLES KAIJAGE AMESEMA WAZIRI WA TAMISEMI AMEITAARIFU TUME KUWEPO NAFASI WAZI KATIKA KATA TANO KATIKA HALMASHAURTI MBALIMBALI NCHINI.
………………
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea taarifa kutoka kwa Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiitaarifu kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini kufuatia Ndugu Lazaro Samwel Nyalandu kuvuliwa Uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Mbunge. 
Aidha, kwa mujibu kifungu cha 113(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume imepokea Hati ya Mahakama Kuu ya Tanzania ikithibitisha uamuzi wa Mahakama hiyo juu ya kutengua matokeo ya Uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo la Longido ambalo Ndugu Onesmo Ole Nangole alikuwa ni Mbunge.
Wakati huo huo Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, ameitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata tano zilizopo katika Halmashauri mbalimbali.
Kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatoa ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi wazi za Majimbo na Kata hizo hapo baadae.
Majimbo na Kata zilizo wazi ni kama ifuatavyo:-
Jedwali Na. 1: Majimbo yaliyowazi
NA.MKOAHALMASHAURIJIMBO
1.SingidaHalmashauri ya Wilaya ya SingidaSingida Kaskazini
2.ArushaHalmashauri ya Wilaya ya LongidoLongido
Jedwali Na. 2: Kata zilizowazi
NA.MKOANA.HALMASHAURINA.KATA
1.Kagera1.Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.1Keza
2.Arusha2Halmashauri ya Jiji la Arusha2Kimandolu
3.Pwani3.

Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.3Kurui
4.Tabora4.Halmashauri ya Wilaya ya Tabora4Bukumbi
5.Tanga5.Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe.5Kwagunda
Jaji (R) Semistocles S. Kaijage
MWENYEKITI
 TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
16 NOVEMBA, 2017

Wananchi Watakiwa Kutumia Mvua Kwa Shughuli za Uzalishaji

$
0
0
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

Serikali imewataka Viongozi na wananchi wote kutumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha nchini kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu leo Mjini Dodoma, wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu tahadhari kwa umma kuhusu mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.

Mhe. Ikupa amesema kuwa, mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania ilitoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Oktoba mpaka Desemba 2017 kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua.

Aidha, ameongeza kuwa kutokana na taarifa hiyo serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ilielekeza Wizara na mamlaka za Serikali za Mitaa kuchukua hatua stahiki kwa kutumia mvua hizo kwa shughuli za uzalishaji mali pamoja na na kuchukua hatua za tahadhari kwa madhara yanayoweza kujitokeza.

“Kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya kijiji na mitaa zinatakiwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa namba 7 ya mwaka 2015 na kanuni za usimamizi wa maafa za mwaka 2017 ya kuchukua hatua za kuzuia, kupunguza madhara na kujiandaa kukabiliana na maafa endapo yatatokea,” amesema Mhe. Ikupa.

Aidha, Mhe. Ikupa amesema kuwa mvua hizo zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini na tayari baadhi ya maeneo yaliyotabiriwa kupata mvua nyingi yameanza kupata madhara mbalimbali yaliyosababishwa na mafuriko vikiwemo vifo, magonjwa ya milipuko, uharibifu wa mazao mashambani, uharibifu wa mazingira, mali na miundombinu.

“Madhara hayo yanaweza kuongezeka endapo hatua stahiki hazitachukuliwa kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu” ametahadharisha Mhe. Ikupa.

Vilevile ameongeza kuwa, Serikali inatoa pole kwa wananchi wote walioathirika na mvua hizo. Aidha, Serikali itaendelea kutoa tahadhari kwa Umma na kuelekeza taasisi na wadau mbalimbali kuchukua hatua stahiki kwa lengo la kupunguza madhara yeyote yanayoweza kujitokeza na kujiandaa kukubaliana na kurudisha hali kuwa bora zaidi ya ile ya awali.

Mbali na hayo, Serikali itaendelea kutoa tahadhari za mara kwa mara kupitia vyombo vya habari kadri ya hali inavyojitokeza, hivyo wananchi mnaombwa kufuatilia kwa makini na kuchukua hatua stahiki.

KAMATI YA BUNGE YA MAADILI YAMHOJI MHE. KUBENEA MJINI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mhe. Almasi Athuman Maige (Mb), akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichokutana kumhoji Mhe. Saed Kubenea (Mb) kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. Mhe. Kubenea alifika mbele ya Kamati hiyo leo ikiwa ni mara ya tatu baada ya kuomba mahojiano yake yaahirishwe mara mbili kutokana na kutokuwa katika hali nzuri kiafya.
Mbunge wa Ubungo, Mhe. Saed Kubenea (Mb) akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. Mhe. Kubenea amefika mbele ya Kamati hiyo leo kwa mara ya tatu baada ya kuomba mahojiano hayo yaahirishwe mara mbili kutokana na kutokuwa katika hali nzuri kiafya.PICHA NA BUNGE

…………..

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemhoji Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa Saed Kubenea kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge.

Akizungumza mara baada ya kumhoji Mbunge huyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Almasi Athuman Maige (Mb) alisema, Mheshimiwa Kubenea amefikishwa mbele ya Kamati hiyo kujibu tuhuma inayomkabili kutokana na kauli aliyotoa kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. 

Mheshimiwa Maige alisema mahojiano hayo yamefanyika leo baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na Mheshimiwa Kubenea kutokua katika hali nzuri kiafya na hivyo kuomba mahojiano yaahirishwe. 

Mheshimiwa Maige aliongeza kuwa baada ya kumsikiliza Mhe. Kubenea itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai kwa hatua zaidi.

“Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa zitabakia kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa Bungeni,” alisema.

KAMATI YA AFCON KUAINISHA MAENEO YATAKAYOFANYIKA MASHINDANO HAYO

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa mkutano wa tisa wa kikao cha nane cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
……………..

Na Lorietha Laurence-WHUSM,Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana
Shonza ameeleza kuwa kazi kubwa ya kamati iliyoteuliwa na Dkt.
Mwakyembe ni kuainisha maeneo yatakayotumika wakati wa mashindano ya AFCON kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 yanayotarajiwa kufanyika
hapa nchini mapema mwaka 2019.

Naibu Waziri huyo, ameyasema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa
akijibu swali la Mbunge wa Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu
aliyetaka kufahamu kama serikali imeteua mji mwingine tofauti na Jiji
la Dar es Salaam kwa ajili ya kuendesha mashindano hayo.

“Moja ya vigezo vya kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 ni kuwa na viwanja vyenye hadhi ya kimataifa
ndio maana haya mashindano yamechaguliwa kufanyika Jijini Dar es
Salaam” amesema Mhe. Shonza.

Aidha Mhe. Shonza amesema,mbali na kuwa na viwanja vyenye kukidhi
viwango vya kimataifa ni lazima mkoa husika uwe na hoteli za kisasa
ambazo zitatosheleza wageni mbalimbali watakaokuja kushuhudia
mashindano hayo kutoka nje na ndani ya nchi.

Tanzania kwa mara ya kwanza inakuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON ya vijana chini ya umri wa miaka 17 jambo ambalo ni fursa kubwa kwa nchi yetu kujitangaza kupitia sekta mbalimbali ikiwemo Maliasili na Utalii na hivyo kuisaidia katika kutangaza na kukuza uchumi wa nchi.

Wakulima 206 Wapata Mafunzo Ya kilimo Cha Chai kutoka NOSC

$
0
0
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Njombe Bwana Lameck Noah(wapili kushoto) akikabidhi cheti bwana Thiemo Msewa(kulia) katika hafla ya kufunga mafunzo kwa wakulima wa chai(farmer field school) mkoani humo yaliyoratibiwa na Kampuni ya kuhudumia wakulima wadogo Njombe(NOSC). Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wakulima katika kilimo cha chai na mazao mengine. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NOSC, Bwana Filbert Kavia. Watatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Ruth Msafiri 
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Njombe Bwana Lameck Noah akizungumza jambo wakati wa hafla hafla ya kufunga mafunzo kwa wakulima wa chai(farmer field school) mkoani humo yaliyoratibiwa na Kampuni ya kuhudumia wakulima wadogo Njombe(NOSC). Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wakulima katika kilimo cha chai na mazao mengine. 
Operation Director wa Wood foundation Tanzania Bwana Mathew Ng’enda(watatu kushoto) akishangilia mara baada ya wakulima kuwasilisha mada mbalimbali juu ya elimu ya kilimo cha chai (farmer field school) waliyoipata kutoka Kampuni ya kuhudumia wakulima wadogo Njombe(NOSC). Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Njombe Bwana Lameck Noah. na watatu kulia ni Mkurugenzi mkuu wa NOSC Bwana Filbert Kavia. 


KUTOKANA na ushirikishwaji wa wakulima wadogo katika zao la chai kupitia Kampuni ya Kuhudumia Wakulima Wadogo Njombe (NOSC), viongozi wa Mkoa wa Njombe wanajivunia mafanikio yaliyopatikana katika kilimo cha chai kilichosaidia kuinua kipato cha wakulima wadogo na kuongeza fedha za kigeni.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Njombe, Bwana Lameck Noah kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Bw. Christopher Ole Sendeka mkoani hapa jana katika mahafali ya mwaka mmoja kuhusiana na mafunzo ya kilimo cha chai kilichohusisha wakulima zaidi ya 206.

“Katika mkoa wetu tulijiwekea utaratibu kuwa kila mkulima alime mazao ya aina mbili ya chakula na biashara, kwa upande wa chai tatizo lilikuwa ni aina ya miche, ilikua inachukua muda mrefu kukua lakini tunaishukuru NOSC imetuletea mice inayokua kwa miezi 12 mkulima anaanza kupata majani mabichi ya chai,” alisema Bw. Noah.

Alibainisha kuwa elimu hiyo ina maana kubwa kwa mkoa wake kwa sababu itawasaidia kulima kisasa na kuwaongezea kipato wananchi wa mkoa huo, lakini pia viwanda vitapata malighafi hiyo muhimu kwa ajili ya soko la ndani na nje.

“Tunafahamu chai inapendwa na mataifa ya magharibi, zao hili lina fedha nyingi za kigeni. Soko la chai lipo na tunawahakikishia wakulima serikali inahangaika kupata mnada wa chai katika ukanda huu badala ya kufanyika Mombasa nchini Kenya.

“Elimu kwa wakulima kupitia huu mfumo ni suala zuri kwa kuwa wakulima watakua na kilimo endelevu waliofundishwa watawafundisha wenzao ili kupata mafuno mazuri na mazao yenye ubora, tunafahamu katika eneo hili kuna kiwanda cha Uniliver kinakaribia kukamilika maana yake watahitaji majani mengi ya chai ili kulisha kiwanda. Wakiendelea kulima zaidi tutawavuta wawekezaji wengi zaidi katika mkoa wetu ili kufikia azama ya serikali ya viwanda,” alisema Bw. Noah.

Mkurugenzi Mtendaji wa NOSC, Bwana Filbert Kavia alisema utaratibu wa kuwafundisha wakulima shambani watajitahidi kuusambaza katika maeneo mengine ya nchi ili wafundishwe wakulima wa mazao mbalimbali kwa lengo la kupunguza tatizo la maofisa ugani.

“Tulianza na vikundi vinane na tutaendelea na vikundi vingine mwakani, huu utaratibu ni mzuri kwa sababu unampa fursa mkulima kujifunza kwa vitendo, kwa kawaida wakulima huelewa zaidi kwa kuona shambani.

“Vilevile nchi yetu ina uhaba wa maofisa ugani, hawa wakulima watawafundisha wakulima wenzao, kama eneo linahitaji maofisa ugani 20 wanaweza kutumika chini ya hapo. Tunaamini kwa sasa tutapata mavuno mengi na yenye ubora kwenye chai baada ya mafunzo haya,” alisema Bw. Kavia.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzie Bw. Thiemo Msemwa alisema: “nashukuru kwa kupewa cheti cha mklulima bora wa chai, nimefurahia mafunzo haya ya kilimo endelevu na kanuni kumi za kilimo endelevu na hata wananvu ninapowaambia waje kwenye shamba la chai wanafurahi kuja shambani kwa sababu kuna mambo mengi ninawafunza.”

Mafunzo hayo yamedhaminiwa na mpango wa Chai Project kwa lengo la kusaidia viwanda vya chai nchini kwa msaada kutoka The Wood Foundation Africa (TWFA), Gatsby Cheritable Foundation (Gatsby) na UKAID ambapo NOSC imedhamiria kulima chai katika eneo lenye ukubwa wa jhekta 3,800 na kufikia wakulima 4,000.

GAVANA WA BENKI KUU ANATARAJIA KUWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA

$
0
0

Mkurugenzi wa Shughuli za Takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw, Irenius Ruyobya akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 20 Novemba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtakwimu Mwandamizi wa ofisi hiyo Bw. Philemon Mwenda.
Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mkurugenzi wa Shughuli za Takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw, Irenius Ruyobya alipokuwa akizungumza kuhusu maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 2o Novemba jijini Dar es Salaam.

Picha na MAELEZO

……………

Na: Veronica Kazimoto,

Dar es Salaam

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika tarehe 20 Novemba, 2017 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya amesema maadhimisho hayo yanayoratibiwa na ofisi hiyo kwa niaba ya Serikali, yana lengo la kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa Tasnia ya Takwimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii Barani Afrika.

Ruyobya amesema kuwa kaulimbiu ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka huu ni “Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora”

“Kaulimbiu hii inalenga kuweka mkazo katika matumizi ya Takwimu za Uchumi kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wote nchini na Afrika kwa ujumla”, amebainisha Ruyobya.

Ruyobya amefafanua kuwa matumizi sahihi ya Takwimu za Uchumi yanaiwezesha Serikali kutunga sera na kutathmini programu mbalimbali kama vile Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP-II), Agenda ya Dunia ya Mwaka 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Agenda ya Afrika ya Mwaka 2063.

“Progaramu zote hizi, zina lengo la kuboresha maisha ya wananchi kwa kuhakikisha kuwa, kuna upatikanaji wa Huduma za afya, Elimu,

Miundombinu ya umeme na barabara, Mawasiliano, Utunzaji wa mazingira pamoja na Utawala bora”, amesema Ruyobya.

Jumla ya washiriki 200 kutoka katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wadau wa Maendeleo, Vyuo vya Elimu ya Juu, Wanafunzi wa Shule za Sekondari pamoja na Wadau mbalimbali wa takwimu nchini wanatarajiwa kuhudhuria kwenye maadhimisho hayo.

Tarehe 18 Novemba ya kila Mwaka, Tanzania huungana na nchi nyingine Barani Afrika kuadhimisha Siku ya Takwimu Afrika, kutokana na siku hii kuwa Jumamosi, maadhimisho haya yatafanyika Jumatatu tarehe 20 Novemba, 2017

WABUNGE VINARA WA JINSIA WAPATIWA SEMINA NA WAWEZESHAJI KUTOKA TGNP MTANDAO

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania( TWPG), Mhe Magreth Sitta (kushoto) akizungumza wakati wa semina kwa vinara wa jinsia katika mpango wa maendeleo kwa mwaka 2018/2019 na Muongozo wa Bajeti kwa Mwaka 2018/2019 ambao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokuwa inahusu mpango kazi wa kurasimisha masuala ya jinsia katika bajeti ya mwaka 2018/2019 ilifanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma, semina iliyokuwa inawezeshwa na wawezeshaji kutoka TGNP Mtandao
Vinara wa jinsia katika mpango wa maendeleo kwa mwaka 2018/2019 na Muongozo wa Bajeti kwa Mwaka 2018/2019 ambao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia semina iliyokuwa inahusu mpango kazi wa kurasimisha masuala ya jinsia katika bajeti ya mwaka 2018/2019 ilifanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma, semina iliyokuwa inawezeshwa na wawezeshaji kutoka TGNP Mtandao
Mwenzeshaji kutoka TGNP Mtandao Ndg. Geofrey Chambua akizungumza na vinara wa jinsia katika mpango wa maendeleo kwa mwaka 2018/2019 na Muongozo wa Bajeti kwa Mwaka 2018/2019 ambao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika semina iliyokuwa inahusu mpango kazi wa kurasimisha masuala ya jinsia katika bajeti ya mwaka 2018/2019 ilifanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.


PICHA NA OFISI YA BUNGE

WAZIRI JAFO:AMEWATAKA WATENDAJI KUTOA USHIRIKIANO ILI KUKAMILISHA MRADI WA UENDELEZAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM (DMDP)

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(aliyesimama) akizungumza na watumishi pamoja na wananchi wa Manispaa ya Temeke(hawapo Pichani) wakati wa ufunzi wa Jengo la Utawala na Maabara iliyojengwa kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam.
Mratibu wa Miradi ya Benki ya Dunia inayosimamiwa na OR-TAMISEMI Erick Rodgers(aliyesimama kushoto) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jengo la Utawala na Maabara lilojengwa na Mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam(kushoto kwake) ni Mratibu wa Mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam katika Manispaa ya Temeke Edward Haule.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(kwanza kulia) akipokea Funguo kama ishara ya kukabidhiwa Jengo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva, Mratibu wa Miradi ya Benki ya Dunia inayotekelezwa na OR-TAMISEMI Erick Rodgers na Mratibu wa Miradi ya Benki ya Dunia toka OR-TAMISEMI.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akikata utepe kama ishara ya kufungua Jengo la Utawala – Manispaa ya Temeke, lililojengwa kupitia mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam(DMDP)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(Kushoto) akionyeshwa Ramani ya Jengo la Utawala –Manispaa ya Temeke alilolifungua mapema leo, na kulikabidhi wa Manispaa ya Temeke; Jengo hilo limejengwa na Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam.
Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Temeke,Wataalam na wananchi wakishuhudia Mhe.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.Selemani Jafo akifungua Jengo la Utawala lililojengwa kwa kupiia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam.
Muonekano wa sehemu ya Jengo la Utawala –Manispaa ya Temeke lililojengwa kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam(DMDP).


…………………..


Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo amewataka watendaji wa Manispaa ya Temeke kutoa ushirikiano ili kuwezesha kukamilika kwa mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) na watendaji watakaoshindwa kutoa ushirikiano huo watashughulikiwa.


Akizungumza leo wakati uzinduzi wa jengo la ofisi na Maabara za mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) lililojengwa katika Manispaa ya Temeke, Jaffo amesema mradi huo utawezesha manispaa ya Temeke kuwa ya sura mpya na kuwa mfano kwa jiji la Dar es Salaam.


Amesema mradi utawezesha kujengwa kwa barabara na mifereji na hivyo kupunguza msongamano wa magari.


Amesema mradi huo ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) utatekelezwa katika jiji zima la Dar es Salaam katika kupanga mji kuwa na makazi bora yenye huduma zinazoendana na makazi hayo.


“Temeke mmekuwa na bahati ya kuwa ya kwanza kutekeleza mradi huu, shirikianeni kuifanya Temeke kuwa ya kisasa kwa kuondoa Temeke iliyokuwepo zamani isiyokuwa na miundombinu rafiki kwa makazi ya wananchi,” amesema.


Mratibu wa mradi huo katika manispaa ya Temeke, Edward Simon amesema Shilingi bilioni 265 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi barabara na mifereji. Amesema jumla ya kilometa 91 za barabara za ndani zitajengwa kwenye manispaa hiyo.


Amesema mradi huo ukikamilika utawezesha barabara kupitika na kupunguza mafuriko kutokana na kutengenezwa mifereji.

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA, BALOZI WA OMAN PAMOJA NA BALOZI WA CHINI NCHINI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa mazungumzo,Ikulu jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke ambaye alimtembelea Makamu wa Rais kwa mazungumzo ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Oman nchini Mhe. Ali A. Al Mahruqi ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe.Wang Ke ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha,Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Mhe.Wang Ke mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA KATIKA NCHI ZA MISRI NA ZAMBIA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa Tanzania nchini Misri, Balozi Meja Jenerali Issa Suleiman Nassoro na Balozi Abdulrahman Kaniki wa Zambia, ambapo amewataka wakaimarishe mahusiano baina ya nchi zote mbili.

Amekutana na Mabalozi hao Balozi leo (Alhamisi, Novemba 16, 2017) katika Ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo Barabara ya Reli na Mahakama mijini Dodoma na kuwasisitiza wakaboreshe shughuli za Kidiplomasia kati ya Tanzania na nchi za Misri na Zambia.

Pia Waziri Mkuu amewataka Mabalozi hao wakahakikishe wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, ukiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, fukwe pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo nchini hususan katika sekta ya viwanda.

Amesema licha ya kutangaza fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii pamoja na kuboresha biashara baina ya Tanzania na nchi za Misri na Zambia pia wakawashawishi wawekezaji waje wawekeze katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya viwanda.

Waziri Mkuu amesema Tanzania ni nchi salama yenye amani na utulivu wa kisiasa, pia Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji jambo ambalo litawawezesha wawekezaji watakaokuja kuwekeza nchini kupata tija.

Pia Waziri Mkuu amewataka Mabalozi hao wahakikishe wanakwenda kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini.Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka Mabalozi hao kwenda kukutana na kufanya mazungumzo na Watanzania waishio kwenye nchi hizo na kuwasisitiza waishi kwa kuzingatia sheria za nchi husika. Pia wawaunganishe pamoja na kuwashauri waje kuwekeza nchini.

Kwa upande wao Mabalozi hao wamesema watahakikisha wanayafanyia kazi maelekezo yote waliyopewa na Waziri Mkuu ikiwa ni pamoja na kwenda kutafuta wawekezaji ili wawe kuwekeza katika sekta ya viwanda na kuboresha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hizo. 


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
S. L. P. 980,
DODOMA.

ALHAMISI, NOVEMBA 16, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi Meja Jenerali Issa Suleiman Nassoro wa Misri  (katikati) na Balozi Abdulrahman Kaniki wa Zambia Ofisini kwake mjini Dodoma Novemba 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi Meja Jenerali Issa Suleiman Nassoro wa Misri  (katikati) na Balozi Abdulrahman Kaniki wa Zambia Ofisini kwake mjini Dodoma Novemba 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michoro ya watoto kutoka Tanzania wazawadiwa Finland.

$
0
0
Michoro mitatu iliyochorwa  na watoto kutoka Tanzania hivi karibuni ilitunukiwa tuzo ya heshima ya vyeti vya stashahada ya maonesho na Taasisi ya Sanaa za watoto na vijana ya Hyvinkää, Finland.

Bryton Manyewa(10), Neev  Mistry (9) wa shule ya Academic International Primary na Mandela Mtaya (5) wa shule ya chekechea ya Upendo Montessori ndiyo waliofanikiwa kupata tuzo hiyo kwa upande wa Tanzania baada ya  kushiriki shindano la michoro liloitwa 'Pamoja' lililotayarishwa na taasisi hiyo ya nchini Finland.

Zaidi ya michoro 6800 toka katika nchi 66 duniani zilishiriki shindano hilo ambapo majaji ambao walikuwa ni wachoraji magwiji a sanaa wa nchi hiyo walichagua michoro 670 kushiriki katika maonesho yaliyoanza Oktoba mwaka huu na yatamalizika 18 Januari 2018 kwenye ukumbi wa Taasisi hiyo inayojihusisha na elimu ya Sanaa kwa watoto na vijana ukuzaji wa muingiliano wa utamaduni wa nchi mbalimbali. 

Maonesho hayo yanaweza pia kutazamwa katika mfumo wa Kidijitali kupitia tovuti ya Taasisi hiyo www.artcentre.fi

Katika miaka ya nyuma, kwa ufadhili wa ubalozi wa Finland nchini, baadhi ya watoto kutoka Tanzania waliweza kuhudhuria mafunzo ya Sanaa yanayotolewa na taasisi hiyo
 

Kwa mara ya kwanza upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) wafanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0

Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saud Arabia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi ya matibabu ya moyo inayoendelea kwenye Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 40 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku tano.


Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge na mwenzake wa Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saud Arabia Ali Al Masoud wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi ya matibabu ya moyo inayoendelea kwenye Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 40 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku tano.

Zoezi la kumfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab likiendelea. Picha na JKCI.

16/11/2017 Jumla ya wagonjwa 20 wamefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa upasuaji wa aina hiyo kufanyika hapa nchini.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo jijini Dar Salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge alisema upasuaji huo unafanyika katika kambi ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na madakatari kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saudi Arabia.

Dkt. Kisenge alisema kuwa kambi hiyo inaenda sambamba na utoaji wa elimu na kubadilishana ujuzi wa kazi kati ya wafanyakazi wa Taasisi hizo mbili ikiwemo aina mpya ya upasuaji wanaoufanya kitu ambacho kinawajengea uwezo zaidi. ”

“Faida ya upasuaji huu ni kumwezesha mgonjwa kutoka chumba cha upasuaji akiwa anatembea na baada ya masaa manne kama hali yake inaendelea vizuri anaweza kuruhusiwa.“Tofauti na upasuaji wa kutumia mshipa wa paja ambao tulikuwa tunaufanya, baada ya upasuaji mgonjwa ni lazima akae Hospitali kwa zaidi ya masaa 24 ili kuangalia maendeleo ya afya yake”, alisema Dkt. Kisenge.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya IIRO Ali Al Masoud alisema kambi hiyo inaendelea vizuri kwani kwa siku wanatibu wagonjwa 10 na baada ya matibabu afya zao zinaimarika tofauti na ilivyokuwa kabla ya matibabu.Dkt. Masoud aliongeza kuwa wamekuja na utaalam mpya wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono ambapo kabla ya hapo matibabu yaliyokuwa yanafanyika ni ya kutumia mshipa wa damu wa kwenye paja.

Alifafanua, “Hivi sasa tunafanya upasuaji wa Moyo wa bila kufungua kifua kitu ambacho wenzetu hawa walikuwa wanakifanya. Sisi tumewaongeza utaalam mpya wa kutumia mshipa ya mkononi badala ya mshipa wa paja.

Naye Bader Alanezi ambaye ni Mtaalamu wa magonjwa ya Moyo na mishipa ya damu kutoka IIRO alimalizia kwa kusema kuwa wamepata muda wa kujifunza vitu vingi na kupata uzoefu mpya wa baadhi ya magonjwa na mambo ya kiteknolojia ambayo katika nchi yao hakuna.

Jumla ya wagonjwa 40 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku tano ambayo imeanza tarehe 14 hadi tarehe 18 mwezi huu.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA IJUMAA LEO NOVEMBA 17,2017

RC GEITA - AUAGIZA UONGOZI WA HALMASHAURI YA MJI GEITA KUPELEKA WAKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI KATA YA MGUSU WILAYANI GEITA

$
0
0
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na wananfunzi wa Shule ya Msingi Shinamwendwa (Halmashauri ya Mji Geita) alipokwenda kushiriki kuchmba msingi wa ujenzi wa nyumba pacha ya Walimu shuleni hapo.
Akina mama wa mtaa wa Machinjioni Kata ya Mgusu Halmashauri ya Mji Geita wakishiriki katika ujenzi wa jengo la utawala kwa kubeba maji kupeleka eneo la mradi.Wananchi wwameamua kujenga Shule ya Sekondari kwa kuwa Kata hiyo haina hata shule moja hivyo watoto wanaofaulu ulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu ya Sekondari katika Kata za jirani.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga msingi wa vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Mgusu baada ya kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati Halmashauri ya Mji Geita.Kata ya Mgusu inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na Shule ya Sekondari. 
Mhandisi Modest Apolinary Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita kitoa ufafanuzi kuhusu ramani ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mgusu kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel kulia ni Herman Kapufi Mkuu wa Wilaya ya Geita. 




Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita Modest Apolinary kupeleka Wakaguzi wa ndani wa Hesabu za Serikali Kata ya Mgusu ili wakakague na kujiridhisha na mapato na matumizi ya fedha mbalimbali katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Mgusu na Mtaa wa Machinjioni Wilayani Geita.

Mheshimiwa Robert amesema hayo wakati wa ziara yake Halmashauri ya Mji Geita yenye lengo la kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati ambapo baada ya uzinduzi kufanyika wananchi wa mtaa wa machinjioni walimueleza kero ya kutopata taarifa ya mapato na matumizi ya michango wanayochangia kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa muda mrefu katika mtaa na kata ya Mgusu.

Akijibu kero hiyo Mkuu wa Mkoa amesema "Kama kuna kiongozi wa mtaa au Kata amekula fedha za wananchi hafai kuwa kiongozi serikali itamchukulia hatua kali za kisheria na atarejesha fedha hizo!, Mkurugenzi leta timu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ili ikague na kujiridhisha kama kuna fedha yoyote iliyochukuliwa pasipo maelezo yanayojitosheleza hatua zichukuliwe haraka kwa wote watakaobainika kuhusika". 

 Mheshimiwa Robert ameongeza kuwa ukaguzi huo ufanyike kuanzia mwaka 2014 hadi 2017 kisha apate taarifa hiyo ofisini. Akiwa katika Halmashauri hiyo Mkuu wa Mkoa amepongeza jitihada zinazofanywa na wananchi za kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo licha ya kuwepo changamoto nyingi katika maeneo yao.

Mkuu wa Mkoa amehitimisha ziara yake ya Mkoa mzima katika Halmashauri ya Mji Geita kwa kutembelea na kushirikiana na wananchi kujenga nyumba pacha ya walimu (Two in one) Shule ya Msingi Shinamwendwa, ujenzi wa kituo cha Zahanati Mtaa wa Nyakato , ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili, ujenzi wa jengo la utawala shule ya Sekondari Mgusu pamoja na kukagua eneo la kujenga Zahanati katika Kata hiyo. 

Katika ziara hiyo ya Mkoa mzima Mheshimiwa Gabriel amefanikiwa kutembelea Wilaya zote tano (5) na Halmashauri sita(6) na kufanikiwa kujenga, kutembelea na kuanzisha jumla ya miradi 19 katika Sekta za Afya, Maji na Ujenzi huku akikusanya zaidi ya mifuko 800 ya Saruji, tofali za Block 500, Mbao 50. Haya yote ni matokeo ya kazi aliyoianza ya kushirikiana na wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo katika kila kijiji ndani ya Mkoa huu lengo kuu likiwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora karibu na maeneo yao pia kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati Mkoa humu.

Wananchi wote katika maeneo aliyopita kufanya kazi wameonyesha kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali na kuamua kuunga mkono juhudi hizi kwa kushiriki katika utekelezaji wa miradi kama vile kusoma maji, kubeba mawe, mchanga, kokoto, kuchimba misingi na vijana kujitolea kujenga miradi hii.

Na: Magesa Jumapili
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
GEITA

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE YA NYABANGE NA KITUO CHA KULELEA WATOTO CHA JIPE MOYO MKOANI MARA

$
0
0
Katibu Msaidizi Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Agnes Mgeyekwa akimkabidhi zawadi ya Sabuni Mkuu wa Makazi ya Wazee wasiojiweza ya Nyabange iliyopo Butiama mkoani Mara Bw. Edward Mbaga wakati Tume ikifanya Utafiti mkoani humo. Kushoto ni Mhadhiri Msaidizi Chuo cha Ustawi wa Jamii Bw. Paulo Mwangosi
Katibu Msaidizi Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Agnes Mgeyekwa akiongea na Wazee katika Makazi ya wazee wasiojiweza ya Nyabange yaliyopo Butiama mkoani Mara wakati wa Tume ilipotembelea makazi hayo ikiwa ni sehemu ya Utafiti wa Mfumo wa Kisheria wa Huduma za Ustawi wa Jamii Tanzania.
Sehemu ya wazee katika Makazi ya Wazee wasiojiweza ya Nyabange yaliyopo Butiama mkoani Mara wakimsikiliza katibu Msaidzi Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Agnes Mgeyekwa. 
Katibu Msaidizi Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Agnes Mgeyekwa akiongea na Wazee wa Makazi ya wazee wasiojiweza ya Nyabange yaliyopo Butiama mkoani Mara wakati wa Tume ilipotembelea makazi hayo ikiwa ni sehemu ya Utafiti wa Mfumo wa Kisheria wa Huduma za Ustawi wa Jamii Tanzania.
Sehemu ya Makazi ya Wazee wasiojiweza ya Nyabange yaliyopo Butiama mkoani Mara.
Katibu Msaidizi Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bi. Agnes Mgeyekwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na uongozi wa kituo cha kulelea watoto cha Jipe Moyo kilichopo Musoma mkoani Mara. Katikati ni mratibu wa kituo hicho sister Annunciata Chacha
Katibu Msaidizi Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Agnes Mgeyekwa akimkabidhi zawadi ya Sabuni na Juisi Mratibu wa Kituo cha Kulelea Watoto cha Jipe Moyo Sister Annunciata Chacha wakati Tume ikifanya Utafiti wa Mfumo wa Kisheria wa Huduma za Ustawi wa Jamii Tanzania.
Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bi Agnes Mgeyekwa (wa tatu kushoto) na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Jipe Moyo kilichopo Musoma mkoani Mara wakati Tume ikiendesha Utafiti wa Mfumo wa Kisheria wa Huduma za Ustawi wa Jamii Tanzania. Kushoto ni Mratibu wa Kituo hicho Sister Annunciata Chacha.
Katibu Msaidizi Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bi Agnes Mgeyekwa akisalimiana na mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Jipe Moyo kilichopo Musoma mkoani Mara wakati Tume ikifanya Utafiti wa Mfumo wa Kisheria wa Huduma za Ustawi wa Jamii.

Huu ndiyo Mrejesho kuhusu Missafricausa 2017.

$
0
0
Hadi wanaingia ukumbini kura zilikuwa:-

D.R.Congo: 8683
Cape Verde: 3248
Tanzania: 2268

Baada ya wawakilishi wa nchi 15 za Africa kushindanishwa haya ndio matokeo :-

Cameroon
Nigeria
Tanzania

Mwakilishi wa Tanzania Lylian Muttakyawa, ametoka na tuzo ya mshindi wa 3 na kubwa zaidi kawa Miss Congeniality.Tunashukuru mno mno, Watanzania kwa support yenu ya kura.
Tafadhali sambaza shukrani hizi.
Mungu awabariki. 




 

WANAODURUFU KAZI ZA SANAA KUFIKISHWA MAHAKAMANI.

$
0
0

 Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart imethibitisha kuwa Watuhumiwa wote waliokwamatwa kushiriki kufanya biashara ya kazi feki za sanaa watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart, Alex Msama amesema kuwa Watuhumiwa hao watapelekwa Mahakamani kutokana na kuwa na kesi ya kujibu.

Ameendelea kusema ni kosa kuuza Kazi za Wasanii hao ambazo hazina Stika ya TRA, kwani zinawakosesha Mapato Wasanii hao na Serikali kwa ujumla.

Amesema wataendelea na zoezi hilo kwa kupita maeneo yote kuhakikisha wanadhibiti uuzwaji wa kazi hizo feki.Kwa jana zoezi letu liliendelea maeneo ya Mbande, Mbagala, Buza Tandika na Chanika", amesema Msama.

Amesisitiza kuwa kazi za nje na ndani lazima ziwe na Stika ya TRA, pia amesema ni marufuku kuweka nyimbo za Wasanii, Kuburn CD na kuweka kwenye Flash.
Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart inashirikiana na Jeshi la Polisi kwa ajili ya usalama, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuendelea na kuikamisha shughuli hiyo,ambayo pia inatarajiwa kufanyika katika mikoa mbalimbali.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart ya jijini Dar es salaam,Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari katika kituo kikuu cha Kanda Maalum Dar es salaam jana kabla ya kuanza kwa zoezi la kukamata wauzaji wa CD Feki katika maeneo mbalimbali ya ikiwemo eneo hatarishi kwa bishara hiyo la Kariakoo .

Baadhi ya Askari na vijana wa Kampuni ya Msama Auction Mart wakipanga mikakati yao kabla ya kuvamia na kuanza kusaka wahalifu hao wa kazi za sanaa.
Baadhi ya watuhumiwa wakipandishwa kwenye gari na vifaa vyao.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart ya jijini Dar es salaam,Alex Msama akikagua baadhi ya CD kwenye moja ya duka.
Baadhi ya wafanyakazi wa Msama Auction Mart wakichukua baadhi ya CD Feki na hazina stika ya TRA,zilizokamatwa katika moja ya duka lililopo Kariakoo.
Mmoja wa watuhumiwa akichukuliwa na na Askari baada ya kugundulika akiuza katika duka lake.
Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart ya jijini Dar es salaam akimhoji mmoja wa watuhumiwa waliokamatwa wakiuza CD Feki,hawana Stika za TRA,sambamba na kutokuwa na leseni ya biashara hiyo.
Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart ya jijini Dar es salaam akikusanya baadhi ya CD zilizokamatwa katika duka hilo.
"Mfano huyu mmiliki wa duka hili, Leseni yake imeisha tangu 2014 mpaka leo na hajui taratibu zozote za kupata leseni mpya wala TIN number,bado anaendelea na biashara yake,kinyume cha sheria",alisema Alex Msama.

JK AWATAKA WASANII WA BONGO MOVIE KUJIONGEZA NA KUACHA KULALAMIKIA SERIKALI

$
0
0
 Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Televisheni  inayoshughulika na masuala ya filamu za Kitanzania kwa Wasanii wa Bongo Movie JTV, ambayo itapatikana kupitia king'amuzi cha Star Times ambapo amewataka wasanii hao kujiongeza ili wafanye kazi kama wasanii kutoka nchi za Magharibi.
 Waziri wa habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dk Harisson Mwakyembe akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya Kikwete katika uzinduzi wa Televisheni ya Jtv  itakayooneshwa kwenye king'amuzi cha Star Times
 Mkurugenzi wa Jtv, Jason Msimbe akizungumza wakati wa hafla ya kumkaribisha  Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye uzinduzi wa televisheni yake
 Baadhi ya Wasanii walioshiriki katika uzinduzi wa Tlevisheni mpya ya Jtv ambayo itakuwa inaonesha filamu za kitanzania kupitia King'amuzi cha Star Times
 Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akiteta jambo naWaziri wa habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dk Harisson Mwakyembe na Mkurugenzi wa JTv Jason Msimbe
  Baadhi ya Wasanii walioshiriki katika uzinduzi wa Tlevisheni mpya ya Jtv ambayo itakuwa inaonesha filamu za kitanzania kupitia King'amuzi cha Star Times
   Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Star Times mara baada ya uzinduzi wa Jtv
 Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na Mkurugenzi wa Star Times juu ya uwezekano wa kampuni hiyo kutoa ufadhili wa mafunzo ya vitendo kwa waandaaji wa filamu nchini  kwenda China
 Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Star Times
Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii wa Bongo Movie walioshiriki uzinduzi wa Televisheni ya Jtv
--

TAASISI YA DORIS MOLLEL YAZINDUA FILAMU YA MTOTO "NJITI" JIJINI DAR

$
0
0
Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa filamu fupi ya "Njiti", Waziri wa Madini, Angella Kairuki (katikati) akiwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (kulia) pamoja na Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel (DMF) na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti", Doris Mollel baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi huo, uliofanyika katika ukumbi wa sinema wa Cinemax, Dar Free Market, jijini Dar es salaam leo. Filamu hiyo ambayo inaelezea maisha ya Mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati "Njiti" imeandaliwa na Taasisi ya Doris Mollel, imelenga kutoa elimu ya uelewa wa namna ya malezi bora kwa mtoto anayezaliwa kabla ya wakati.
Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa filamu fupi ya "Njiti", Waziri wa Madini, Angella Kairuki akitoa hotuba yake, ambapo alitoa pongezi nyingi kwa Taasisi ya Doris Mollel kwa kufanikisha kupatikana kwa elimu ya uelewa wa namna ya malezi bora kwa mtoto anayezaliwa kabla ya wakati kupitia filamu hiyo.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa filamu fupi ya "Njiti", ambayo inaelezea maisha ya Mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati "Njiti" iliyoandaliwa na Taasisi ya Doris Mollel, imelenga kutoa elimu ya uelewa wa namna ya malezi bora kwa mtoto anayezaliwa kabla ya wakati.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel (DMF) na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti", Doris Mollel akizungumza katika hafla hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa sinema wa Cinemax, Dar Free Market, jijini Dar es salaam leo. 
Sehemu ya wageni waliohudhulia hafla hiyo.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images