Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

TMF YAIPATIA REDIO HABARI NJEMA YA MBULU, FEDHA ZA RUZUKU YA SHILINGI MILIONI 112

0
0
Tanzania Media Foundation (TMF) imeipatia ruzuku ya shilingi milioni 112 Radio Habari Njema ya Mbulu Mkoani Manyara, kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi ili waibue kero, changamoto, mafanikio na kuandika kwa wingi habari za wananchi hasa waliopo Vijijini. 

Mkurugenzi wa TMF Ernest Sungura, akizungumza mjini Babati wakati wa zoezi hilo, alisema vyombo vya habari ni mhimili usio rasmi ambao umekuwa ukiibua changamoto mbalimbali za wananchi ikiwemo za maji, elimu, afya na mengineyo ambayo yakipatiwa ufumbuzi jamii inapata furaha. 

Sungura alisema kupitia ruzuku hiyo, hii ni mara ya nne kupatiwa ruzuku na TMF na mara zote wamekuwa wakiomba fedha kwa ajili ya kuandaa vipindi vyenye maslahi ya wananchi. 

Alisema kupitia vipindi vilivyoandaliwa na redio hiyo haki za watoto na wanawake zimepatikana kwa ufadhili wa TMF. 

Alisema kwa kuandika habari za jamii ikiwemo mafanikio, kero, ukosefu wa maji, vyoo, shule na mambo hayo yakapatiwa ufumbuzi wananchi hupata furaha baada ya mafanikio hayo. 

Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga ameipongeza TMF kwa kuiwezesha Redio Habari Njema, ambayo imekuwa inashirikiana na serikali katika kuchochea maendeleo ya jamii kupitia habari wanazozitangaza. 

Mofuga alisema kupitia redio hiyo wamekuwa wanapata taarifa za changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na wao kama serikali wamekuwa wanazifanyia kazi. 

Alisema waandishi wa habari wanapaswa kuiga chombo hicho cha habari kwa kutangaza mambo ya msingi ikiwemo kero za jamii na siyo kuegemea uandishi wa uchochezi usio na tija kwa jamii zaidi ya kuichonganisha na serikali yao. 

Alisema uandishi wa kuangalia maslahi ya Taifa ndiyo wa kupewa kipaumbele kwa kuzingatia weledi na kuweka mzania ikiwemo kuandika taarifa za kumuunga mkono Rais John Magufuli. 

"Tuwe na uzalendo kwa kutambua juhudi za Rais Magufuli kwani amepambana na ufisadi, hivi sasa uadilifu umeongezeka, kero zilishamiri sasa zimepungua na amekuwa mlinzi wa rasilimali za Taifa," alisema Mofuga. 

Mhasibu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbulu, Padri Anthony Lagwen alisema tangu redio hiyo ianzishwe imekuwa nuru ya jamii kwenye eneo lote inaposikika. 

Padri Lagwen alisema kazi za redio hiyo zinalenga mafanikio kwa jamii na tangu wachukue ruzuku kwa mara ya kwanza mwaka 2012 wamepiga hatua kubwa kwa kuhabarisha jamii ipasavyo. 

Alisema kupitia mradi wa kwanza mwaka 2012 wa wanawake tuzungumze, walipata ruzuku ya sh42 milioni kutoka TMF na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia hadi kuheshimika na jamii. 
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Mofuga (kulia) akishuhudia utiwaji sahihi wa kupatiwa shilingi milioni 112 ambazo ni fedha za ruzuku kwa Redio Habari Njema ya Mbulu zilizotolewa na Tanzania Media Foundation (TMF) mjini Babati, (katikati) ni Mkurugenzi wa TMF Ernest Sungura na Mhasibu mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbulu, Padri Anthony Lagwen
 Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF) Ernest Sungura akizungumza mjini Babati wakati wa zoezi la kupatiwa fedha za ruzuku ya shilingi milioni 112 kwa Radio Habari Njema ya Wilayani Mbulu. 
 Mwandishi wa habari mwandamizi wa Mkoa wa Manyara, Joseph Lyimo akizungumza kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa namna ya kuomba fedha za ruzuku Tanzania Media Foundation (TMF) Mjini Babati. 
 Waandishi wa habari wa Mikoa ya Manyara na Arusha, wakiwa kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa namna ya kuomba fedha za ruzuku kupitia Tanzania Media Foundation (TMF) mjini Babati.

KAMISHENI YA KUKABILIANA NA MAAFA ZANZIBAR YAVUTIWA NA URATIBU WA AFYA MOJA TANZANIA BARA

0
0

Na.Mwandishi Maalum
Kamisheni ya Kukabiliana na maafa Zanzibar imevutiwa na shughuli za kuratibu maafa nchini zinazofanywa na serikali ya awam ya Tano kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu,Idara ya Kuratibu maafa ikiwa ni pamoja na kuratibu Afya moja ambapo katika Dhana ya Afya Moja, sekta ya   afya ya binadamu, wanyama (pori na wafugwao) na mazingira, zinakuwa na mawasiliano ya karibu kiutendaji na kupanga  mikakati ya pamoja katika kujiandaa na milipuko ya magonjwa na kukabiliana nayo endapo itatokea.

Akiongea wakati wa  ziara ya Kubadilishana Uzoefu na Idara ya Kuratibu Maafa na Ofisi ya Waziri Mkuu,jijini Dar es salaam leo tarehe 15 Novemba 2017, Mkurugenzi Mtendaji Kamishseni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Shaban Mohamedi amebainisha kuwa kamisheni yake imevutiwa na jinsi idara ya maafa inavyoweza  kuimarisha juhudi na ushirikiano wa sekta mbalimbali katika maandalizi ya kuzuia,kujiandaa na kukabili  magonjwa ambukizi kwa kujumuisha sekta zote muhimu.

“Tutaupitia mpango mkakati wa Afya moja  ili nasisi tuanze juhudi za kuratibu Afya moja  kwani  Kamisheni inajukumu lakukabiliana na Maafa hivyo tutachukua juhudi za kuhakikisha na sisi Zanzibar tunashirikiana na wadau husika ili tuweze kutumia rasilimali ndogotulizonazo kuweza kukabili  magonjwa yatokayo kwa  wanyama kwenda kwa binadamu yanayoiathiri jamii ya Zanzibar” alisisitiza Khatibu

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya , alifafanua kuwa suala la Afya moja linaratibiwa na ofisi yake kupitia Dawati maalum kutokana na kuwa magonjwa ya mlipuko ni masuala mtambuka na yanahitaji rasilimali watu na fedha nyingi hivyo kwa uratibu wa pamoja inasaidia kuhakikisha sekta zote zinashirikiana kukabiliana na athari za magonjwa yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

“Umuhimu huu wa Afya moja unatokana na ukweli kwamba magonjwa na athari nyingine za binadamu kwa kiasi cha asilimia 60 hadi 80 huusisha wanyama. Kwa kufanya hivi ufanisi huongezeka kwani mchanganyiko wa Wataalamu, wakifanya kazi kwa pamoja na ushirikianao mkubwa, huchukua muda mfupi, na  matumizi ya raslimali chache kwa pamoja huleta matokeo mazuri zaidi” Alisema Msuya.

Mwaka 2013, aliyekuwa Makamu wa Rais wa serikali ya awamu ya nne, ya Jamhuriya MuunganowaTanzania, Dk. Ghalib Bilal alizindua mtandao wa afya moja jijini Arusha. Kufuatia uzinduzi huo, mwaka 2015 wadau kutoka sekta mbalimbali walikaa na kutengeneza mpango mkakati wa afya wa miaka mitano (2015 – 2020). Mpango huo umeainisha masuala yahusuyo afya moja, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa utaratibu wa kuratibu shughuli zote za afya moja katika idara ya kuratibu maafa katika ofisi ya waziri mkuu.
 Mratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu , Edgar Senga akiwasilisha mada ya majukumu ya idara hiyo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu na  Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa ya Zanzibar walipofanya ziara ofisini hapo leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Operesheni na Huduma za Binadamu Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa  Zanzibar, Makame Khatib akiwasilisha mada ya majukumu ya Kamisheni hiyo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu na  Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, walipofanya ziara ofisini hapo leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi  Msaidizi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu akifafanua jambo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu na  Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa ya Zanzibar walipofanya ziara ofisini hapo leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam, wengine ni waratibu wa maafa kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.
 Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu,Brigedia Jenerali Mbazi Msuya (Kulia), Mkurugenzi mtendaji  Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa  Zanzibar (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Operesheni na Huduma za Binadamu Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa  Zanzibar, Makame Khatib wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya  Kamisheni hiyo na Idara ya maafa  walipofanya ziara ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam.

HOSPITALI YA MKOA KASKAZINI KIVUNGE YASHEREHEKEA WIKI YA WATOTO NJITI ZANZIBAR

0
0
 Bi Rahma Asheri Mama aliejifungua Watoto Njiti  mapacha Nassir na Yassir akionesha tabasamu katika Sherehe za Wiki ya Watoto njiti Duniani iliofanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Kaskazini Kivunge Zanzibar.
 Muuguzi Mkunga wa Hospitali ya Wagonjwa wa akili Bi Ruzuna Abdulrahim Mohd akitoa elimu kwa Wazazi waliopata watoto njiti katika Sherehe za Wiki ya Watoto njiti Duniani iliofanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Kaskazini Kivunge Zanzibar.
 Madaktari pamoja na wauguzi wakiwa katika Picha ya  pamoja na Wazazi wa Watoto Njiti katika Sherehe za Wiki ya Watoto njiti Duniani  iliofanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Kaskazini Kivunge Zanzibar.
Daktari Bingwa wa Watoto kutoka Shirika la HIPZ(Helth Improvement Project in Zanzibar)Hannah Peters akimfanyia vipimo mtoto njiti kumuangalia uzito wake  katika Sherehe za Wiki ya Watoto  njiti Duniani  iliofanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Kaskazini Kivunge Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZBAR.

NAMTUMBO KUANZISHA TAMASHA LA MUZIKI KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA REDIO YA JAMII NAMTUMBO

0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma katika harakati yake  ya kuhakikisha wanajenga kituo cha Redio ya jamii katika Halmashauri hiyo  imepanga kuanzisha Tamasha la muziki kwa lengo la kupata fedha kujenga kituo cha Redio.

Kamati ya uanzishwaji Redio katika Hamashauri hiyo imependekeza kuundwa kwa kamati ndogo itakayoratibu kuanzishwa kwa Tamasha la muziki kwa lengo la kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha Redio.

Aidha mwenyekiti wa kamati ya uanzishwaji Redio ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Bwana Gwakisa Mwasyeba ambaye ni Afisa mipango wa Halmashauri hiyo alipendekeza majina ya kamati hiyo kuwa ni James komba Afisa utamaduni wa wilaya hiyo , Afisa manunuzi Robert Mahili, Abbas Masawe katibu wa mikutano ya madiwani , na Afisa michezo John Ligoho na kuwataka kuanza mikakati ya kuanzishwa kwa Tamasha hilo la muziki.

Hata hivyo kamati ya uanzishwaji Redio ya Halmashauri hiyo ilipendekeza Hadidu Rejea kwa kamati hiyo ndogo ili zianze kushughulika nazo na kutoa taarifa kamili kwenye kamati kuu ya uanzishaji Redio .

Hadidu rejea ilizotoa kamati ya uanzishaji Redio kwa kamati ndogo ya uanzishwaji tamasha la muziki ni pamoja na kamati hiyo ifuatilie Gharama za kuwaleta wasanii mkoani Ruvuma na aina ya wasanii wanaokubalika kwa sasa katika jamii, wafuatilie pia upatikanaji wa muziki na jukwaa kwa ajili ya wasanii,Muda sahihi wa kufanya tamasha na namna ya kufanya matangazo kwa jamii ili jamii ijitokeze kwa wingi katika tamasha hilo pamoja na kuwasilisha mapendekezo ya uwanja wa kutumia.

Aidha mwenyekiti wa kamati ndogo ya Tamasha aliiambia kamati ya uanzishwaji Redio kuwa kamati yake itafanya ziara mjini songea nakufanya mahojiano na waliobobea na maswala ya matamasha mjini songea pamoja na wadau wengine wa muziki na kutoa taarifa katika kamati ya uanzishaji Redio ya Halmashauri hiyo.

Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo inahitaji kukusanya shilingi milioni 104 ili kukamilisha zoezi zima la uanzishwaji wa kituo cha Redio ikiwa ni gharama za uagizaji wa vifaa , ,utengenezaji wa studio,gharama zinginezo kama utengenezaji wa thamani za ofisi kama meza,kabati na viti vya ofisi ambapo kwa jumla yake inafikia kiasi cha shilingi milioni 104.

Pamoja na mikakati hiyo Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo itawaomba wadau kuweza kushiriki katika tamasha hilo kwa lengo la kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha Redio ambacho kitakuwa ukombozi mkubwa katika Halmashauri hiyo na wilaya kwa ujumla wakati utakapofika.

KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY DAR KUTOA MATIBABU YA BURE KWA WAKAZI WA KEREGE BAGAMOYO

0
0

Dar es Salaam, Novemba 15.2017

Klabu ya Rotary ya Oysterbay Dar es Salaam inatarajia kutoa huduma ya matibabu ya bure kwa wakazi wa Kerege wilayani Bagamoyo mkoani Pwani siku ya jumapili ya tarehe 19.2017.Kambi hiyo ya siku moja itatoa vipimo vya afya, ushauri, matibabu na huduma mbalimbali za meno, macho, malaria, usafi wa mwili, minyoo, masikio, pua na koo (ENT), pamoja na magonjwa ya ngozi na kwa mara ya kwanza itaendesha vipimo vya kansa ya shingo ya uzazi

Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa kambi ya matibabu Bwana Frédéric Morel amesema amefurahishwa na maandalizi ya mwaka huu kulinganisha na miaka iliyopita. “Tumefurahishwa na ushirikiano tunaopata kutoka kwa makampuni na watu binafsi katika kuhakikisha kambi hii inafanyika kwa mara nyingine tena.pili, tunatarajia idadi ya watu kuwa mara mbili kulinganisha na mwaka uliopita”.Alisema, Morel. mbali na kambi ya Kerege, klabu yetu pia mwaka huu imetoa huduma ya matibabu ya bure kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Msasani A. Hivyo tunaomba wakazi wa Kerege na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kupima afya zao.” Frédéric Morel.

Kwa upande wake Rais wa klabu ya Rotary ya Oysterbay Dar es Salaam, Anne Saels, amesema kuwa kuwa kambi hii ni mfano wa huduma Za Rotary kwa jamii. “kutoa huduma za afya kwa watu takribani 2000 hufanywa pindi watu wanaojitolea kukutana pamoja na kushirikiana kufanya kazi ili kubadilisha maisha ya wengine kuwa bora. Mwisho, uhalali wetu kama Rotary hupimwa kwa na huduma tunayotoa na tunajivunia kuwa na uwezo wa kuandaa Matibabu ya Matibabu mwaka baada ya mwaka”.Alisema, Anne Saels.

Mbali na hilo, Mwakilishi kutoka benki ya Diamond Trust, Bwana Sylvester Bahati amesema ushirikiano na klub ya Rotary ya Oyster Bay katika miaka mitano iliyopita umekuwa ni ushrikiano mzuri wenye kubadili maisha ya watu.

“Mpaka sasa zaidi ya watu 1000 wamepatiwa huduma bora za kiafya katika kambi hii na kuhimiza watu kujitolewa kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika jamii zao.Jeshi la wafanyakazi wa matibabu litakalo kusanyika siku ya tarehe 19.11.2017 haliwezi kupatikana popote kama kikundi wakati wowote ule, hii inafanya kambi ya matibabu ya Kerege kuwa ya kipekee na takribani watu 25 kutoka benki ya DTB hujitolea kila mwaka katika kambi.”Alisema ,Bwana Sylvester Bahati.

Kambi hii ya matibabu itafanyika kwa udhamini wa benki ya Diamond Trust, Whitedent, kampuni ya vinywaji ya Peps, Securex , ICAP kutoka chuo cha Colombia, pamoja na madakatri na wanafunzi kutoka Chuo cha kumbukumbu cha Herbert Kairuki, chuo kishirikishi cha afya cha MUHAS, na makundi mbalimbali kutoka asasi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali.

Klabu ya Rotary ya Oysterbay imeanzishwa mwaka 2009 na kwasasa ina wanachama 62. Ni klabu kubwa kati ya klabu 7 za rotary zinazopatikana Dar es Salaam. Klabu ya Rotary imekuwa ikiisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali baadhi yake kati ya hiyo miradi ni pamoja na Kambi ya matibabu kwa shule ya Msasani , Mradi wa vijana Poa kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu, Rotary Dar Marathon, “Rotary Mission Green” mradi wa kupanda miti, na kwasasa Rotary inajiandaa kuja na mkakati mpya utakaofanya kazi ya kuiisaidia jamii moja kwa katika maeneo mbalimbali tofauti na huduma za afya.

TADB YAOMBWA ‘KUSAPOTI’ WADAU WA UFUGAJI WA SAMAKI

0
0
Na mwandishi wetu, Mwanza.

Wadau wa tasnia ya ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba (fish caging) mkoani Mwanza wameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuwasaidia katika kuendeleza tasnia iyo kwa kuwapatia mikopo na mahitaji mengine kwa ajili ya kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa wa samaki mkoani humo.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa  Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju, Bw. Elpidius Mpanju Akizungumza wakati ugeni kutoka TADB ulipotembelea kujionea maendeleo ya tasnia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba mkoani Mwanza.

Bw. Mpanju alisema kuwa ukosefu na ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha za mtaji kwa ajili ya maendeleo ya kilimo hasa katika tasnia hiyo mpya ya ufugaji wa samaki imekuwa inawapa changamoto katika uendelezaji wa tasnia hiyo yenye faida lukuki kwa maendeleo ya kiuchumi nchini.

Bw. . Mpanju aliongeza kuwa ukosefu wa mikopo ya uhakika imekuwa inarudisha nyuma ukuaji wa tasnia hiyo mpya nchini kwa kuwa mahitaji mengi kwa ajili ya kuhudumia ufugaji wa samaki inapatikana nje ya nchi hivyo kuhitaji kiasi kikubwa cha mtaji.
sekta ya mifugo na kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kuendeleza sekta ya mifugo.

“Uduni na ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na kutusahau sisi wakulima na wafugaji, hivyo tunaiomba TADB kutusaidia kutatua changamoto hii,” alisema.

Akijibu changamoto hizo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila alisema kuwa Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Kilimo ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika  kilimo nchini.

Bibi Kurwijila aliongeza kuwa tasnia ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa samaki nchini.

Aliongeza kuwa Benki ya Kilimo imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Samaki na uvuvi nchini ili ziweze kuchangia ukuaji wa uchumi nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha amesema kuwa TADB inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka Miwili (2), Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)).

“Mikopo hii ni ya riba nafuu ambayo inalenga katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (mbele) akiongoza Ujumbe kutoka Benki hiyo walipotembelea Shamba la Ufugaji wa Samaki la Mpanju lililopo Luchelele, mkoani Mwanza.
 Mkurugenzi wa  Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju, Bw. Elpidius Mpanju (kulia) akiuelezea Ugeni kutoka TADB kuhusu tasnia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba.. wanaomsikiliza ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (wapili kulia), Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki hiyo, Bw. Augustino Matutu Chacha (katikati). Wengine pichani ni wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bw. Joseph Mutashubilwa (kushoto) na Bw. Dome Malosha (wapili kushoto).
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (kulia) akihoji masuala mbalimbali kuhusu tasnia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba wakati alipouongoza ugeni kutoka TADB kutembelea Shamba la Ufugaji wa Samaki la Mpanju lililopo Luchelele, mkoani Mwanza. Wanaomsikiliza ni Mmiliki wa kampuni hiyo, Bw. Anuruphus Mpanju (kushoto), Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (wapili kushoto) na Mkurugenzi wa  Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju, Bw. Elpidius Mpanju (kulia).
 Meneja Mradi wa Shamba la Ufugaji wa Samaki la Mpanju, Bw. Artem Ivanieiev (kushoto) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (kulia) kuhusu Shamba la Kutotoleshea vifaranga vya samaki vya Kampuni ya Mpanju.
 Ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakiangalia namna ya vifaranga vya samaki vinavyohudumiwa kwenye Shamba la Ufugaji wa Samaki la Mpanju lililopo Luchelele, mkoani Mwanza.
Sehemu ya vizimba vya kukuzia samaki vinavyomilikiwa na Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju.

Article 0

0
0

RC LUHUMBI ASISITIZA WANANCHI KUTUMIA RASILIMALI WALIZONAZO KUCHOCHEA MAENDELEO

0
0
Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kuchanganya mchanga kwenye shughuli ya ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Kazibizyo wakati wa zoezi la uhamasishaji wananchi kujitolea katika uchangiaji wa maendeleo ya ujenzi wa zahanati,vituo vya afya na shule Wilayani Bukombe. 
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe ambaye yupo (Katikakati)Josephat Maganga akishirikiana na wananchi pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kufanya shughuli ya kuchanganya mchanga. 
Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga msingi wa kujenga zahanati ya kijiji cha Kazibizyo Wilayani Bukombe pamoja na wananchi ambao wamejitokeza kuunga jitihada za serikali za kuleta maendeleo ya huduma za afya maeneo ambayo yanauwitaji . 
Katibu tawala wa wilaya ya Bukombe akishiriki zoezi la ujenzi. 
Wananchi wa kijiji cha Kazibizyo wakishiriki kusomba mawe. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiendelea na harakati za kushiriki ujenzi wa zahanati kijijini hapo. 
Wakina mama wakishiriki zoezi la ujenzi wa zahanati kijiji cha Kazibizyo 
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe,Josephat Maganga akizungumza na wananchi wa kijiji hicho juu ya kujitolea kwenye swala la maendeleo bila ya kutegemea serikali. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kazibizyo baada ya kuzindua kampeni ya ujenzi wa zahanati kijijini hapo.



NA JOEL MADUKA, GEITA

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi amewataka wakazi wa kijiji cha Kazibizyo na Bulama kutumia rasilimali walizonazo ili kuchochea maendeleo ya vijiji vyao.

Mhandisi Luhumbi aliyasema hayo katika uzinduzi wa ujenzi wa zahanati kwenye Kata ya Nga’nzo na Shule kwenye kijiji cha Bulama ili kuwaondolea wananchi tatizo la kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.Alisema matatizo mengi yanasababishwa na baadhi ya viongozi kutowajibika badala yake kuweka mbele maslahi binafsi.

“Shida kubwa wananchi tumefanya makosa mengi mno tumekuwa na viongozi bora viongozi sio viongozi bora viongozi ambao awawezi kuamasisha viongozi ambao kazi yao ni kula michango ya wananchi viongozi ambao fedha zikija wanaangalia kupiga kwanza hela ndio wanaleta yale makombo ambayo yanajenga vitu vibovu vibovu,Sasa viongozi wa namna hiyo hatuwezi kuwavumilia Geita,ni bora wafungashe virago watafute Mikoa mingine,kipindi hiki ni kipindi cha kazi kama unaona kazi ni ngumu achia bodi”Alisisitiza Luhumbi.

Mhandisi Luhumbi alisema wananchi ndio nguzo kubwa ya maendeleo kwenye maeneo yao hivyo lazima wawe na afya bora na elimu ili wafanya kazi za maendeleo.Mmoja wa wananchi Bi Sophia Sangizo alielezea wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya na kusababisha wanawake wengi kujifungulia nyumbani hali ambayo imekuwa ikisababisha matatizo kwao.

Naye ,Mzee Mayoke Ambrose Maziku ambaye ametoa kiwanja kwaajili ya ujenzi wa zahanati kijijini hapo alisema kuwa msukumo mkubwa ambao umepelekea kutoa kiwanja ni kutokana na mwaka 2013 na 2007 alipoteza watoto wake kutokana na kukumbwa na umauti sababu kubwa ikiwa ni kuwa mbali na huduma za afya kwani wamekuwa wakitembea umbali wa kilomita 20 kufuata huduma hiyo.

HATUJAVIFUNGA MDOMO VYAMA VYA SIASA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI

0
0

BENKI YA NMB YAFUNGUA TAWI JIPYA KATIKA MJI WA HEDARU WILAYANI SAME.

0
0
Barabara ya kuelekea tawi jipya la Benkiya NMB katika mji wa Hedaru wilayani Same.
Tawi jipya la Benki ya NMB lililopo katika mji wa Hedaru wilayani Same.
Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Staki akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya NMB katika mji wa Hedaru wilayani Same.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB kanda ya Kaskazini.
Afisa Mkuu wa wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB,Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la NMB -Hedaru.
Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela ,Emanuel Kishosha akifuatilia uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya NMB tawi la Hedaru.
Baadhi ya wateja wa Benki ya NMB waliohudhuria ufunguz rasmi wa tawi la Benki hiyo katika mji wa Hedaru.
Afisa Mkuu wa Wateja wado na wa kati wa Benki ya NMB,Abdulmajid Nsekela akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Same ,Rosemery Staki wakati wa uzinduzi wa tawi hilo.
Afisa Mkuu wa Wateja wado na wa kati wa Benki ya NMB,Abdulmajid Nsekela akimuongoza mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Same ,Rosemery Staki kwenda kuzindua rasmi tawi hilo.
Mkuu wa wilaya ya Same,Roemery Staki akizindua tawi la Benkiya NMB,katika mji wa Hedaru wilayani Same.
Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na wa kati wa Benki ya NMB,Abdulmajid Nsekela na Mkuu wa wilaya ya Same ,Rosemery Staki wakipiga makofi mara baada ya tendo la uzinduzi wa tawi hilo kufanyika.
Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Staki akitia sain kitabu ha wageni mara baada ya kuzindua rasmi tawi la Benki ya NMB,katika mji wa Hedaru.
Mgeni rasmi ,Rosemery Staki akizungumza na mmoja wa wafanyakaz wa benki hiy mara baada ya kuzinduliwa katka mji wa Hedaru.
Meneja wa NMB,Kanda ya Kaskazin Salie Mlay akitoa neno la shukrani mara baada ya kuhitimisha hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la NMBkatika mji wa Hedaru wilayani Same.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

INTERNET GAME CHANGERS, TRUE REVOLUTION IN TANZANIA

0
0
Sometimes it can be painstaking when searching for the right Internet Service Provider (ISP) and your choice can make an enormous difference in your online experience – choose the right one and you are happy and likewise choose the wrong one, and you are left frustrated.

But what tickles your decision making? When I needed an ISP, I asked myself – Is it a good bargain? Are they charging me too much for what I’m getting? Do they provide faster speed? Are they easily available? Will I get online when I need to?

Like handsets, TVs or pair of shoes, you may have a range of ISP choices in your area and trust me I had a whole list of them. Then I realised, ultimately it all dawned back to two crucial things when it comes to internet – accessibility of service and price. I wanted a great bargain but it better work!

A lot of ISPs throw in extras to give you comfort you're getting a great value, free Wi-Fi hotspot access for experience, discounted or lowest packages, good customer care however don’t you agree none of these features matter if you can't use the service when you need to? Like the famous saying, cheap is expensive.

So it’s no wonder I find myself wanting to look at the revolution of internet services in Tanzania. One ISP caught my interest, Smile Communications. It does not represent the country as a whole of course but has been my personal bombshell.

If you recall, the coming of Smile Communications to Tanzania in 2012, for the first time Tanzania got the real taste of internet with no buffering or loading and immediately change came to Tanzania. With its promise for speed, quality and reliability, Smile set the trend of internet experience in a whole new level however their premium internet packages were quickly ridiculed in the market. Shortly after there was this noise about total internet freedom with the ISP’s launch of Unlimited packages with no data caps. You and I know where that went – now everyone can get unlimited bundles – total revolution I say!

Let me ask you something, if you had Tsh 1.4 Million today, imagine the hundreds of things you can use it for – family weekend in Zanzibar, buy one of the latest smartphones, or better yet buy a bodaboda or just crazy and change your wardrobe. But what if I were to ask you instead to recharge your mobile today with the 1.4 million worth of internet bundle, I am crazy right?

This is what it meant getting on SuperFast internet service in Tanzania. But I understand those are now days gone and forgotten. I bumped into an advert just the other day – Bei ya Ndizi – and I was like huh! Is there a new banana price in town? So I did some digging only to discover it’s another one of this ISP surprises. Smile was restructuring its bundle prices with a reduction of up to 80%.This one time bundle worth Tsh 1,400,000 for example is now a mere Tsh 275,000. I got to tell you, it knocked me off my feet. I had to verify it so I checked their website and behold, there it was! I even see you get some as low as Tsh 2,000.

I’m going to start some semi-regular series of “internet game changes”. These articles will largely follow my own buying decisions. The goal here is to dig into the specifics of buying habits of internet services and what drives that decision. Send me your questions and views on what works for you or what you think I should be searching for. I’m not (usually) going to make a specific recommendation however when I see one that speaks to me, well I feel obliged to show you what could be the best.

As an internet user, what’s your take? Talk to me.


RAIS DKT MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA MADARAJA YA JUU YA BARABARA YA TAZARA NA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la juu (Fly Over) eneo la TAZARA jijini Dar es salaam akiwa ameongozana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda mara tu baada ya kuwasili kutokea kijijini kwake Chato mkoani Geita leo Jumatano Novemba 15, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maagizo ya kuvunjwa kwa sehemu ya majengo ya TANESCO (pichani nyuma) na la Wizara ya Maji ili kupisha ujenzi wa miundombinu baada ya kukagua maandalizi  ya ujenzi wa daraja la ghorofa tatu la Ubungo (Ubungo Interchange) jijini Dar es salaam akiwa ameongozana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda mara tu baada ya kuwasili kutokea kijijini kwake Chato mkoani Geita leo Jumatano Novemba 15, 2017.
 Wananchi wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akitoa maagizo baada ya kukagua maandalizi  ya ujenzi wa daraja la ghorofa tatu la Ubungo (Ubungo Interchange) jijini Dar es salaam akiwa ameongozana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda mara tu baada ya kuwasili kutokea kijijini kwake Chato mkoani Geita leo Jumatano Novemba 15, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimsikiliza mwananchi Bi. Nyangoma James akieleza matatizo yake  baada ya kukagua maandalizi  ya ujenzi wa daraja la ghorofa tatu la Ubungo (Ubungo Interchange) jijini Dar es salaam akiwa ameongozana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda mara tu baada ya kuwasili kutokea kijijini kwake Chato mkoani Geita leo Jumatano Novemba 15, 2017
Taswira za maendeleo ya ujenzi wa daraja la juu (Fly Over) eneo la TAZARA jijini Dar es salaam kama lilivyo leo Jumatano Novemba 15, 2017
Picha na IKULU

WAZIRI MKUU AKUTANA AKUANA NA BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI TANZANIA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na Balozi wa China Nchini Tanzani Bibi Wang Ke nakufanya naye mazungumzo ya kikazi ofisini kwake Mjini Dodoma leo  Novemba 15, 2017.
 .Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisikiliza jambo kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani (Mbunge) Mwigulu Nchemba wakati wa  kikao cha Tisa cha Bunge leo Novemba 15, 2017 Mjini Dodoma.
 PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Serikali kuzindua Ripoti ya Utafiti wa Kitaifa wa Matokeo ya UKIMWI 2016/17

0
0
Serikali inatarajia kuzindua Ripoti ya Utafiti wa Kitaifa wa Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016/2017 katika Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Desemba Mosi mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Siku ya Maadhimisho ya UKIMWI Duniani.

"Hii ni ripoti muhimu sana inayotokana na utafiti ambao huwa unafanyika kila baada ya miaka minne, ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003/2004 ni taarifa ambayo husaidia kuonesha hali halisi ya maambukizi ya VVU kwa watu wa marika mbalimbali pamoja na mapendekezo ya kisera namipango ya kudhibiti UKIMWI nchini," amesema Mhe. Mhagama.

Aidha, amesema kuwa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yenye kaulimbiu "Changia mfuko wa maisha, Tanzania bila Ukimwi inawezekana" yatatoa fursa ya kutathimini hali halisi na mwelekeo wa udhibiti UKIMWI Kitaifa na Kimataifa ikiwemo kutafakari changamoto, mafanikio na uimarishaji wa mikakati mbalimbali ya kudhibiti UKIMWI.

" Siku hii pia hutoa nafasi ya kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha yao kutokana na UKIMWI, kuwaenzi wale waliojitokeza na kutoa mchango wao katika kudhibiti UKIMWI, pamoja na kuwajali yatima waliotokana na vifo vinavyohusiana na ugonjwa wa UKIMWI" ameongeza Jenista Mhagama.

Pia amesema kuwa, lengo lingine ni kutafakari na kutekeleza kitaifa na kimataifa kauli mbiu inayotolewa kila mwaka kulingana na vipaumbele vya kidunia, kikanda na kitaifa.

Aidha, Mhe. Mhagama amebainisha baadhi ya matukio makuu yatakayoambata katika maadhimisho hayo ni Kongamano la Kitaifa la kutathimini hali na mwelekeo wa udhibiti UKIMWI nchini litakalofanyika kati ya tarehe 28 hadi 29 Novemba mwaka huu jijini Dar es Salaam ambalo litajadili mawasiliano ya utekelezaji wa afua za ukimwi nchini ili kujua mahali tulipotoka, tulipo na tunakoelekea.

Vilevile amesema kuwa, katika maadhimisho hayo kutakuwa na uzinduzi wa Mkakati/ Mwongozo wa Taifa wa Afua za Matumizi ya kujikinga na VVU ambao utafanyika tarehe 27 mwezi huu.

"Katika Maadhimisho hayo kutakuwepo na maonesho ya shughuli za wadau wa udhibiti UKIMWI nchini yatakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 24 Novemba mwaka huu yakijumiisha huduma mbalimbali na utoaji elimu na burudani kwa wananchi ikiwemo huduma za upimaji wa hiari wa VVU na ushauri nasaha, upimaji wa shingo ya kizazi, sukari, uzito, damu na elimu kupitia vikundi vya sanaa na burudani" amefafanua Mhe. Mhagama.

Mbali na hayo, Jenista Mhagama amesema kuwa, katika maadhimisho hayo Serikali itafaya uhamasishaji wa Mfuko wa Fedha za Kudhibiti Ukimwi nchini kupitia matembezi ya hisani tarehe 25 Novemba na pia chakula cha jioni maalumu kwa kuchangia mfuko huo Desemba Mosi.

Hata hivyo, Waziri Jenista ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo ili kupata huduma mbalimbali zitakazotolewa ikiwemo upimaji wa hiari wa VVU na ushauri nasaha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amewahamasisha wananchi na wadau mbalimbali kuchangia Mfuko wa kudhibiti Ukimwi kwa kushiriki Marathoni, kuchangia kupitia kununua tshirt kwa shilingi 20,000 na pia kuchangia kwa hiari kupitia namba 0684 909090.

SPIKA NDUGAI APOKEA TAARIFA YA MKUTANO WA BUNGE LA AFRIKA ULIOFANYIKA KUANZIA OKTOBA 6 MPAKA 20, 2017 NCHINI AFRIKA YA KUSINI

0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Mjumbe wa Bunge la Afrika anaewakilisha Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Stephen Masele (katikati) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Asha Juma, wa pili kulia ni Mjumbe Mhe. David Silinde na kulia ni Katibu wa Spika, Ndg. Said Yakubu.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Asha Juma (kulia) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Bunge la Tanzania katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania, Mhe. Asha Juma, wa pili kulia ni Mjumbe Mhe. Stephen Masele na kulia ni Mjumbe Mhe. David Silinde.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akipokea taarifa ya Mkutano wa Bunge la Afrika uliofanyika kuanzia tarehe 6 mpaka 20 Oktoba, 2017 nchini Afrika ya kusini, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Asha Juma (wa pili kulia) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. kushoto ni Mjumbe, Mhe. Stephen Masele na kulia ni Mjumbe, Mhe. David Silinde.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

JIUNGE NA ANKO KITIME APP

0
0
KARIBU USHUSHE ANKO KITIME APP KUTOKA GOOGLE PLAYSTORE, ILI UPATE STORI VICHEKESHO NA HABARI MBALIMBALI ZA JAMII KUTOKA KWA ANKO KITIME. 

INGIA KWA KUBOFYA HAPA CHINI

SERIKALI YALIPA FIDIA YA BIMA YA AMANA KWA WATEJA WA BENKI YA FBME SH. MILIONI 728

0
0
SERIKALI imetumia kiasi cha Sh. Mil 728 kuwalipa amana zao wateja zaidi ya 695 wa Benki ya FBME ambayo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeifutia leseni ya kufanya shughuli za kibenki hapa nchini.

Hayo yamesemwa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akijibu maswali ya Mbunge wa Viti Maalum Mhe.  Rukia Kassim Ahmed (CUF), aliyetaka kufahamu, pamoja na mambo mengine, hatma ya wateja wa Benki hiyo baada ya kufutiwa leseni yake ya kujihusisha na masuala ya kibenki Mei 8, 2017.

Mhe. Ahmed alitaka kufahamu msimamo wa Serikali endapo fedha za kuwalipa wateja hao zinazotokana na kuuza mali, makusanyo ya madeni na fedha zilizowekezwa kwenye taasisi nyingine na Benki hiyo hazitatosha.

Aidha, alihoji kuhusu uamuzi wa Bodi ya Akiba ya Amana ambao unaeleza kuwa hata kama mteja aliweka amana yake kwa fedha za kigeni katika benki hiyo, watalipwa kwa fedha za kitanzania kwa kiwango kilichokuwepo wakati Benki hiyo inafilisiwa Mei 8, 2017.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa malipo ya wateja yanalipwa kutokana na sheria ya mabenki na Taasisi za fedha ya mwaka 2006 kifungu cha 39, na kwamba kinachofanyika hivi sasa ni utekelezaji wa sheria hiyo.

 “Serikali haina mpango wa kumuonea mteja yoyote, madeni yatakusanywa  na fedha zitalipwa kwa kila mteja kulingana na amana alizojiwekea, Serikali inalisimamia jambo hilo kwa  umakini wa kiwango cha juu.” alisema Dkt. Kijaji.

Katika swali lake la msingi Mhe. Rukia Kassim Ahmed (CUF), alitaka kujua hatma ya wateja walioweka fedha zao katika Benki ya FBME, baada ya Benki Kuu ya Tanzania kuifutia leseni ya kufanya shughuli zake za kibenki na kuiweka chini ya ufilisi wa Bodi ya Bima ya Amana kuanzia Mei 8, 2017.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa hatua ya kwanza kwa mujibu wa sheria ni malipo ya fidia ya Bima ya Amana ya kiasi kisichozidi Sh. 1,500,000 kutegemea na kiasi cha salio la amana wakati beki inafungwa.

“Fedha za kulipa fidia hiyo zinatoka katika Mfuko wa Bima ya Amana (Deposit Insurance Fund) unaosimamiwa na Bodi ya Bima ya Amana (Deposit Insurance Board (DIB))” alisema Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji aliongeza kuwa wateja waliokuwa na amana zisizozidi kiwango cha juu cha fidia cha Sh. 1,500,000 wakati benki inafungwa watapata fedha zao zote.

“Kiasi kitakachozidi kiwango hicho kitalipwa kutegemea kiasi cha fedha kitakachopatikana kutokana na mauzo ya mali, makusanyo ya madeni na fedha zilizowekezwa katika Taasisi nyingine”.alisema Dkt. Kijaji.

Imetolewa na:                                              




Benny Mwaipaja
Mkuu wa  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

WAANDISHI WA HABARI MKOANI TANGA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HIFADHI YA MAMLAKA YA NGORONGORO

0
0
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mkoani Tanga wakiingia kwenye hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro tayari kuanza ziara ya siku kumi ya mafunzo
 Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakiwa kwenye hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro mkoani Arusha wakati wa ziara ya siku tano kwa ajili ya ziara ya mafunzo kutembelea vivutio vya utalii kulia ni Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la TBC ,Bertha Mwambela ambaye ni mratibu wa ziara hiyo kushoto ni Mbonea Herman wa Kituo cha Star TV kulia ni 
 Mratibu wa ziara ya waandishi wa habari mkoani Tanga waliotembelea hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro,Bertha Mwambele kutoka Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) wakiingia ndani ya mamlaka hiyo kulia ni Sussan Uhinga mwandishi wa gazeti la Mtanzania mkoan Tanga  kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo,Samweli Nsyuka
 Mratibu wa ziara ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga ambaye ni Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la TBC Bertha Mwambele akiwa kwenye picha eneo la Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro mara baada ya kuwasili kwa ajili ya mafunzo ya siku kumi ikiwemo kutembelea hifadhi hiyo.
Waandishi wa habari wakipiga picha kwenye bango la mamlaka hiyo kabla ya kuanza ziara ya siku kumi kutoka kulia ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo,Samweli Nsyuka,Lilian Lucas wa Mwananchi,Nestory Ngwega wa gazeti la Daily News,Bertha Mwambela wa TBC,Alex wa TATV,Pamela Chaula wa Tanga One Blog
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Ngorongoro,Walter Mairo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kabla ya kuanza ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi wakati wa ziara yao ya siku kumi
 Waandishi wa habari wakipata kifungua kinywa kabla ya kuanza ziara ya mafunzo ya siku kumi
 Mwandishi wa Kituo cha Tanga TV cha Jijini Tanga,Abraham Alex akiwa kwenye eneo la mchanga ambalo umekuwa ukihama mara kwa mara
 Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo,Samweli Nsyuka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea eneo la mchanga ambalo limekuwa likihama mara kwa mara
 Waandishi wa habari,Mbaruku Yusuph wa gazeti la Tanzania Daima na Mbonea Hermani wa Star TV wakiangalia eneo la ambalo limegunduliwa fuvu la binadamu wa kwanza wakati wa ziara hiyo
 Jumba la Makumbusho ya Mambo ya Kale ambalo lipo eneo la Mamlaka ya Ngorongoro Mkoani Arusha
Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo,Samweli Nsyuka kulia akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Jumba hilo la Makumbusho .Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MDAHALO WA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE WAFANYIKA CHUO KIKUU CHA MZUMBE

0
0
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika Mdahalo wa Kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliofanyika Novemba 15 2017 chuoni hapo mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurian Ndumbaro akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mdahalo wa Kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliofanyoika katika Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurian Ndumbaro, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mdahalo wa Kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Prof. Ganka Nyamsogoro, akitoa hotuba ya kumshukuru mgeni rasmi.
Sehemu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani).
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Rainfrida Ngatunga (kulia), akifuatilia mada katika mdahalo wa Kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere uliofanyika Novemba 15 chuoni hapo 2017.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakifuatilia mdahalo huo.
Meza Kuu.
Washiriki wa mdahalo huo.
Washiriki.
Jonas Mkuna, akitoa mada.
Prof. Justin Kalisti Urassa, akitoa mada juu ya sera ya viwanda katika Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof. Mathew Luhanga, akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurian Ndumbaro (kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurian Ndumbaro (kulia), akibadilishana mawazo na Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Sylvia Lupembe na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurian Ndumbaro (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakati wa
mdahalo wa Kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurian Ndumbaro (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa mdahalo wa Kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurian Ndumbaro (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watoa mada wa
mdahalo wa Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA ALHAMIS LEO NOVEMBA 16,2017

0
0
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images