Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

MKOKO AINA YA SUBARU FORESTA X20 INAUZWA..!

$
0
0
MAZUNGUMZO YAPO /  NEGOTIABLE AVAILABE  ONLY FOR SERIOUS BUYER full duty paid, full A/C ,EXELLENT SOUND SYSTEM
PRICE : TSH 9,700,000/=
FOR MORE INFORMATION CALL 0652-430196 , simathew42@gmail.com , 
SKYPE : simathew1
location : MWENGE {SURVEY} DAR ES SALAAM

BONDIA IDDY MNYEKE AMTWANGA MWALIMU ALONI KWA POINTI

$
0
0

Lucas Mkenya akivalishwa mkana baada ya kumdunda mwenzi.

Mabondia Mwalimu Alon kushoto na Iddy Mnyeke wakioneshana uwezo wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao wa kirafiki uliofanyika manzese mwishoni mwa wiki iliyopita .

Bondia Iddy Mnyeke kushoto akimshambulia Mwalimu Alon wakati wa mpambano wao uliofanyika Manzese Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita MNyeke alishinda kwa pointi
Bondia Lucas Mkenya kushoto akipambana na Adamu Yahaya wakati wa mpambanbo wao wa upingwa wa Taifa uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita 
Bondia Sadick Momba kushoto akipambana na Amos Mwamakula wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa taifa momba alishinda K,O raundi ya kumi .
Bondia Sadick Momba kulia akipambana na Amos Mwamakula wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa taifa momba alishinda K,O raundi ya kumi Picha na  BLOG YA SUPER D

MSHINDI WA NYUMBA YA AIRTEL YATOSHA AKABIDHIWA HATI NA UFUNGUO WA NYUMBA YAKE.

$
0
0

 Mmbando  akitoa ufafanuzi juu ya mshindi  huyo alivyopatikana kabla ya  kumkabidhi hati yake  ya nyumba  leo
 Ofisa mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando  akionyesha  hati ya  nyumba 
 Mshindi  wa  nyumba ya  Airtel yatosha  akisoma hati ya nyumba  yake aliyoshinda  baada ya  kukabidhiwa  leo

 Mshindi  wa  nyumba ya Airtel Yatosha  akionyesha  hati yake ya  nyumba aliyokabidhiwa  leo,huku akiwa na  wafanyakazi  wenzake  waliofika  kushuhudia 
Ofisa mahusiano wa Airtel Bw  Jackson Mmbando akimkabidhi mke  wa mshindi  wa  nyumba ya Airtel yatosha Bw  Sylivanus Juma Wanga Bi Veronica Wanga huku kushoto mume wake ambae ni mshindi akishuhudia mshindi  huyo ni mhasibu  wa taasisi isiyo ya kiserikali ya TARWOC inayojihusisha na mapambano dhidi ya ukatili  wa kijinsia mkoa wa Iringa ,wengine pichani ni wafanyakazi  wenzake waliofika kushuhudia  hafla  hiyo  iliyofanyika Hotel ya M.R mjini Iringa.

Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba Lakutana

$
0
0
Baadhi ya wawezeshaji wakijadiliana jambo katika Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba. Baadhi ya washiriki wa Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba Mmoja wa washiriki wa warsha katika Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba akijadili jambo. Warsha ya wajumbw wa Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba ikiendelea

BARAZA la Mtandao wa Wanawake limekutana lililoshirikisha wajumbe kutoka mikoa mbalimbali limekutana kwa siku mbili kujadili masuala ikiwemo namna ya ushiriki wa wanawake katika mabaraza yanayojadili rasimu ya Katiba Mpya. Kwa mujibu wa vyanzo wa habari hizi washiriki hao walikutana kwa siku mbili, yaani Agosti 16 na 17 mwaka huu Makao Makuu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam. 

 Miongoni mwa mada zilizowasilishwa na kujadiliwa na wajumbe wa warsha hiyo ni pamoja na Mchakato wa Katiba Mpya na Ushiriki wa Wanawake katika Hatua mbalimbali, ikiwemo uchambuzi wa rasimu ya Katiba Mpya iliyowasilishwa na Diana Kidala wa Jukwaa la Katiba na mada ya Umuhimu wa Kuwepo kwa Sauti za Wanawake katika Katiba Mpya iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya. 

 Mada zingine zilizowasilishwa na kujadiliwa na wajumbe hao ni pamoja na Uwasilishaji wa Masuala Muhimu ya Kijinsia yaliyojitokeza katika rasimu ya Katiba Mpya ya Mkurugenzi Mtendaji wa WFT, Mary Rusimbi na ile ya Masuala Muhimu ya Wanawake ya Kuiimarishwa na Kuingizwa katika Katiba Mpya iliyowasilishwa na Vicky Lihiru kutoka ULINGO. 

 Pamoja na mambo mengine pia wajumbe hao walijenga mikakati ya pamoja kuendeleza ushiriki wa mtandao katika hatua zinazofuata kwenye mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya yenye mrengo wa usawa wa jinsia nchini. Baraza hilo la wajumbe lilifungwa na Bi. Betty Minde kutoka KWIECO. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

Wanawake wapokea Mikopo ya MWEI - Tegeta

$
0
0
 Bi. Prisca George (kulia) mkazi kutoka Tegeta, Dar es Salaam, anahesabu kitita cha mpoko alichopokea kupitia mradi wa MWEI unaoendeshwa na kampuni ya Vodacom Tanzania. Bi. Prisca ni mmoja wa wanawake wajasiliamali 150 waliopokea mikopo isiyo na riba ya jumla ya millioni kumi kupitia mradi wa MWEI eneo ya Tegeta ili kuendesha biashara zao. Kulia ni Bi. Grace Lyon, Meneja wa Mradi wa MWEI na katikati ni Bi. Zawadi Bakari, wakala wa M-Pesa. 
 Bi Zaituni Abdalla (kushoto) mkazi kutoka Tegeta, Dar es Salaam, anahesabu kitita cha mpoko alichopokea kupitia mradi wa MWEI unaoendeshwa na kampuni ya Vodacom Tanzania. Bi. Zaituni ni mmoja wa wanawake wajasiliamali 150 waliopokea mikopo isiyo na riba ya jumla ya millioni kumi kupitia mradi wa MWEI eneo ya Tegeta ili kuendesha biashara zao. Anayeshuhudia ni Bi Rukia Mtingwa, Meneja Mawasiliano Vodacom Tanzania.

Bw. Martin Kiswaga (kulia) ofisa kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania, akielezea kikundi cha wanawake wajasiliamali kutoka Tegeta, Dar es Salaam, jinsi chaja ya ReadySet inavyofanya kazi. Chaja hio ilizinduliwa na kampuni ya Vodacom na inatumia nishati ya jua kuchaji simu kumi wakati mmoja. Wanawake hao pia walipata mikopo isiyo na riba kupitia mradi wa MWEI ya ujumla ya million kumi.   

Glamour as Exim Bank marks 16th Anniversary

$
0
0
                       The Exim Bank Tanzania Chief Executive Officer Dinesh Arora (left) briefs the bank’s staff and customers on the bank’s 16 years of operations during an event to celebrate the bank’s 16thAnniversary held in Dar es Salaam at the weekend. 
                       The Exim Bank Tanzania Chief Executive Officer Dinesh Arora (left) briefs the bank’s staff and customers on the bank’s 16 years of operations during an event to celebrate the bank’s 16thAnniversary held in Dar es Salaam at the weekend. 
                       
The Exim Bank Tanzania Chief Executive Officer Dinesh Arora (left) briefs the bank’s staff and customers on the bank’s 16 years of operations during an event to celebrate the bank’s 16thAnniversary held in Dar es Salaam at the weekend. 
                       The Exim Bank Tanzania Chief Executive Officer Dinesh Arora (left) briefs the bank’s staff and customers on the bank’s 16 years of operations during an event to celebrate the bank’s 16thAnniversary held in Dar es Salaam at the weekend. 
 The Exim Bank Tanzania Customer Service Manager Frank Matoro (second right) and other bank staff listen to a speech by the bank’s CEO during the event
 A cross section of Exim Bank Tanzania staff light up candles in commemoration of the bank’s 16th Anniversary
 A cross section of Exim Bank Tanzania staff poses for a photo during the event. 
 Exim bank staff pose for photo during the event.
AN Exim BANJK Staff (centre) shows the bank’s customers how the Queue Management System introduced by the bank works.

mkutano wa baraza la katiba wafunguliwa leo jijini dar.

$
0
0
 katibu mkuu ofisi ya makamu wa rais, bw Sazi salula akizungumza katika mkutano wa baraza la katiba la ofisi ya makamu wa rais jijini dar leo..
 Waziri wa nchi ofisi Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan akifungua mkutano wa baraza la lakatiba la ofisi ya makamu wa rais jijini dar es Salaam leo.
katikati katibu mkuu ofisi ya makamu wa Rais bw. Sazi Salula, naibu katibu Mkuuu Bw. Ngosi mwihava kulia na kushoto Mkurugenzi wa Idara ya Muungano ofisi ya makamu wa Rais bw. Baraka Baraka katika mkutano wa baraza la katiba la ofisi hiyo jijini dar es salaam leo. (Picha na Evelyn Mkokoi wa ofisi ya makau wa Rais).
Watumishi wa ofisi ya makamu wa rais na baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC wakimsikiliza waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano, hayupo pichani alipofungua mkutano wa baraza la katiba la ofisi ya makamu wa rais jijini dar leo.
=========  ======  ======

Baraza la katiba Ofisi ya Makamu wa Rais


Evelyn Mkokoi na Lilian Kisasa


Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais - Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa, ameiomba serikali na baraza la katiba kujadili suala la haki za wanawake katika kupatiwa nafasi za juu za uongozi  Serikalini.  Waziri Huvisa ameeleza hay oleo katika mkutano wa baraza la katiba la Ofisi ya makamu wa rais jijini Dar es salaam.


Waziri Huvisa  amesema kuwa, masuala ya jenda ni muhimu kujadiliwa katika nafasi za uongozi serikalini , hasa katika ngazi za juu za uongozi , hivyo amependekeza kuwa katita rasimu ya katikba, wanawake wapate moja ya tatu ya uongozi wa juu katika Serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.


Awali akifungua mkutano huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais -Muungano  Mh. Samia Suluhu Hassan, amewaomba wajumbe wa baraza la katiba la Ofisi ya Makamu wa Rais, wawe Makini , wastahimilivu na wenye hekima na busara katika kuboresha Rasimu hiyo ya Katiba mpya na hatimaye kupata katiba nzuri  kwa watanzania wote . Mh. Suluhu aliyaeleza  wajumbe  wa baraza hilo kuwa majadiliano hayo ya Rasimu ya Katiba Mpya yasiwe ya Kubomoa bali yawe ya kujenga na kuimarisha jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri  Suluhu, amefafanua kuwa mchakato huu wa kutoa maoni ya Rasimu ya Katiba mpya ulianza kwa kutungwa sheria ya mabadiliko ya katiba yaliyopitishwa na Bunge la jamuhuri la muungano wa Tanzania mwezi November 2011 na kufanyiwa marekebisho mwezi februari 2012 ambapo, sheria hiyo imeainisha hatua  zitazofuatwa  katika upatikanaji wa Katiba ambapo alifafanua kwamba hatua ya kwanza ni kukusanya maoni ya wananchi , hatua ya pili ni kuitisha mabaraza ya katiba , hatua ya tatu ni kuitishwa kwa bunge maalum la katiba , na hatua ya nne ni kura ya maoni ikifuatiwa na kupatikana kwa katiba mpya.


Mheshimiwa Suluhu aliongeza kwa kusema kuwa kuwa tume hiyo ya katiba, imepewa miezi kumi na nane(18) tangu mwezi  mei  2012 kukamilisha kazi yake, hivyo kwa umuhimu huu wa katiba kwa taifa la Tanzania Ofisi ya Makamu ya Rais imeunda baraza la katiba ambalo kwa mujibu wa muongozo wa katiba linatakiwa kujadili na kutoa maoni kwa kuhusisha malengo na majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais amabayo ni Muungano na uhifadhi wa Mazingira , hivyo amewahimiza wajumbe kutoa maoni kwani hawatabanwa na kifungu wala ibara yoyote.


Kwa upande mwingine mheshiwa Suluhu ameipongeza Tume ya mabadiliko ya katiba kwa kazi nzito iliyofanywa ikiwa ni pamoja na kuandika Rasimu ya katiba ambayo wengi wameweza kuisoma na kuielewa.



RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWAKILISHI MAALUM WA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA KATIKA DARFUR LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa  Umoja wa Maitafa katika Darfur Bw. Mohamed Ibn Chambers aliyekutana na kufanya mazungumoz naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa  Umoja wa Maitafa katika Darfur Bw. Mohamed Ibn Chambers aliyekutana na kufanya mazungumoz naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikiza Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa  Umoja wa Maitafa katika Darfur Bw. Mohamed Ibn Chambers aliyekutana na kufanya mazungumoz naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013.PICHA NA IKULU

FORTUNATA MASHINJI AHEHEREKEA SIKU YA KUZALIWA NA WAFANYAKAZI WENZAKE.

$
0
0
 Keki ya Fortunata ambayo ilikuwa maalumu kwenye siku yake ya kuzaliwa ambayo alikula pamoja na wafanyakazi wenzake wa LAPF ,Dodoma.
 Fortunata akimlisha keki rafiki yake Scola
 Wakati wa kugonga glasi kama ishara ya kumpongeza Fortunata kwa kuongeza umri zaidi katika sherehe ndogo iliyofanyika kwennye Pub maarufu ya Ngonyani , Dodoma.
Fortunata akimimina champaigne kwa wafanyakazi wenzake wa LAPF waliojumuika nae siku ya kuzaliwa kwake iliyofanyika hivi karibuni,Dodoma.

The Model Auditions for Ally Rehmtullah's show.

$
0
0
The Model Auditions for Ally Rehmtullah's show was one of the great events this weekend. Hundreds of aspiring models showed up for the auditions in front of six judges (Sarah Raqey, Myler, Missie Popular, Daxx, Wema Sepetu and Alfred Minja). The event was managed by Martin Kadinda.


 And for the men...it wasn't so bad..
 Daxx gave a free session of tips for a successful model,for the men.
 I like Ally's plans for this event...we have this amazing madam who will provide models with shoes!!
 All in all...the judges had a tough time to come up with only 24 female models and 12 male models...that few in a crowd of hundreds! But we managed

 Tanzanian model,Myler...shared her tips with the female models and we selected the list
 And the judges were happy with the choices...hello Alfie :))

 Some moments were just too intriguing to pass...we leaned forward to see it all...hahahahaha

 At the end of the auditions, the day was saved...Judges went through some interviews and posed for pics

 The ever amazing Wema Sepetu was the Kardashian of the moment...I have never seen such a crowd-puller situation before! This girl is huuuuge in the industry..so much love!

Thanks to you all who showed up for the auditions. Congrats to those who got the part...and in case you didn't get it this time,work on all the advice given to you...you never know.

Kudos to you Ally..best of luck on the show

xoxo



 Catherine is the face of Fashion Avenue,the 2014 collection that is due to be launched by Ally Rehmtullah. She has proved to be one upcoming designer too...her outfit is self designed :))
 This is Sarah Raqey, one of the judges who was more like a matron to the models,providing the necessary advice.
 And here are some of the captured moments of the auditions....
 New faces...it was quite refreshing to see how much of the new faces were there in that crowd
 After a long run of auditions in threes, some of the models were selected for round two

 It wasn't an easy task...
 We saw all kinds...trust me..all kinds!


 We were able to see both full figured and the international standard figured models,for the girls' part


 And i was glad to see that most of the models adhered to the outfits requirements

Msama Promotions kumwaga madawati Kinondoni

$
0
0
KAMPUNI ya Msama Promotions imejipanga kutoa madawati kwa shule mbalimbali za msingi zilizoko Wilayani  Kinondoni  Jijini Dar es Salaam kabla ya mwaka 2014. 

Akizungumza  mwishoni mwa wiki , Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Alex Msama alisema ugawaji wa madawati hayo utakwenda sambamba na ugawaji wa sare na vifaa mbalimbali vya shule. Msama  alisema hivi sasa ameunda  kamati maalumu ya kutembelea shule ambazo zina  upungufu wa madawati na vifaa vingine. Msama Promotions ni kampuni ambayo imesaidia jamii kwa muda mrefu, ambapo sasa imeamua kujikita katika suala la elimu.

Alisema mpaka sasa wameshatengeneza madawati yapatayo 50,000 na kwamba dhamira ya kampuni hiyo ni kuinua kiwango cha elimu katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo kwa kuanzia wanaanzia katika wilaya ya Kinondoni.

 “Kampuni ya Msama promotions imedhamiria kuwasaidia waanafunzi wa shule za msingi  wasome kwenye mazingira mazuri ambayo yatafanikisha maendeleo yao na  nchi kwa ujumla” alisema Msama.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha mipango ya kusaidia elimu, hivi sasa kampuni hiyo iko kwenye mchakato wa kupata hati kwa ajili ya ujenzi wa  kituo cha kimataifa cha kulelea watoto yatima na wasiojiweza.  Kituo hicho kinatarajiwa kujengwa    katika eneo walilopewa na Rais Jakaya Kikwete lililopo Pugu, jijini   Dar es Salaam.

Mkazi wa Kigoma ashinda gari la kwanza la tamasha la fiesta

$
0
0
Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya push Push Media Mobile Rugambo Rodney akimkabidhi namba ya gari/funguo mshindi wa kwanza wa gari aina ya Vitz iliyoendeshwa na kampuni hiyo kwa mashabikwa fiesta wa Kigoma. Rugambo alisema kuwa baada ya kugawa zawadi hiyo Kigoma, sasa wanaelekeza nguvu zao zote Tabora ambapo watatoa fedha taslim na pikipiki. Ili kushinda unatakiwa kutuma neno fiesta kwenda namba 15678.

MKAZI wa Kigoma, Abdallah Aly Ngagari (51) ameshinda gari aina ya Vitz iliyoendeshwa na kampuni ya Push Mobile Media ya kunogesha tamasha la Fiesta.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Kigoma, Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa tayari Ngagari amekabiziwa gari yake katika hafla fupi iliyofanyika huko huku Kigoma.

Rugambo alisema kuwa baada ya kukamilisha bahati nasibu hiyo, kwa sasa nguvu zao wanazielekeza mkoani Tabora katika tamasha la Fiesta ambalo litafanyika Ijumaa.

Alisema kuwa watatoa pikipiki kwa wapenzi wa muziki wa Tabora ambapo ili kushinda, mashabiki wanatakiwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 ili kushinda pikipiki au fedha taslim shs 100,000.

“Tumepania kutoa zawadi katika mikoa yote ambayo Fiesta itafanyika, tumetenga zaidi ya sh milioni 80 ili kufanikisha zoezi hili ambapo magari aina ya vitz yapo nane kwa ajili ya kuwapa mashabiki, tunawaomba mashabiki kushiriki kwa nguvu zote,” alisema Rugambo.

Alisema kuwa wamejipanga kufanya zoezi hilo na lengo kubwa ni kuwazawadia mashabiki wao ambao na kufaidika na tamasha hilo. Kwa mujibu wa Rugambo, zawadi zote zipo katika mikoa ambayo fiesta imefanyika na ndiyo maana wameweza kutoa zawadi mkoani Kigoma mara baada ya kuchezesha droo.

RAIS KIKWETE AMFARIJI MZEE PHILIP MANGULA KWA KUFIWA NA BINTI YAKE NEMELA

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula kwa kufiwa na binti yake, Nemela Mangula, aliyefariki mwishoni mwa juma kwa ajali ya gari. Hapa ni nyumbani kwa Mzee Mangula Oysterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Profesa Mark Mwandosya alipoenda kumfariji  Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula kwa kufiwa na binti yake, Nemela Mangula, aliyefariki mwishoni mwa juma kwa ajali ya gari. Hapa ni nyumbani kwa Mzee Mangula Oyterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi kitabu cha maombolezo alipoenda kumfariji  Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula kwa kufiwa na binti yake, Nemela Mangula, aliyefariki mwishoni mwa juma kwa ajali ya gari. Hapa ni nyumbani kwa Mzee Mangula Oyterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 20
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pole Mama Mangula alipoenda kuifariji familia ya Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula  kwa kufiwa na binti yake, Nemela Mangula, aliyefariki mwishoni mwa juma kwa ajali ya gari. Kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Anne Makinda. Hapa ni nyumbani kwa Mzee Mangula Oyterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 20.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

ProSeven ft Mike Tee_Proverb (Official Video)

$
0
0
ARTIST ; Geofrey Mwakatundu AKA ProSeven
SONG ; Proverb
AUDIO PRODUCER ; Mike Tee
VIDEO ;  ShowBiz Defined Media
                Visualized By Mike Tee

shekhe Ponda afikishwa mahakamani mjni morogoro kwa helikopta na kurejeshwa jijiini dar

$
0
0

 Akiwasili viwanja vya Gymkana ambavyo vipo jirani kabisa na mahakama hiyo

          Baadhi ya wananchi waliofurika kwenye mahakma hiyo
 Polisi wakikagua helkopta hiyo baada ya Ponda kushuka
 Helkopta hiyo ikiruka kumrejesha Ponda gerezani jijini Dar es salaam.

  NA DUSTAN SHEKIDELE,MOROGORO-

Katibu  wa taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania Shekhe Ponda Issa Ponda mkazi wa Dar es salaam leo asubuhi  amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Morogoro kwa usafiri wa helkopta ya jeshi la polisi kujibu shitaka linalomkabili.

 Ponda alifikishwa mahakamni hapo chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi wakiwa na mbwa  baada ya kuwasili kwa herikopta hiyo iliyotua majira ya saa tatu subuhi katika uwanja wa Gofu mjini Morogoro ikitokea jijini Dar es salaam.
Wakili wa Serikali,Bernard Kongola alikisoma  mashitaka matatu  dhidi ya Shekhe  Ponda  mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro Richard Kabate alisema, mnamo Agosti 10 mwaka huu katika eneo la Kiwanja cha Ndege  manispaa ya Morogoro Ponda  aliuambia umati wa watu uliokusanyika kwenye mkutano wa hadhaza “ndugu waislamu msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bwakwata ambao ni vibaraka wa CCM na serikali na kama  watajitokeza kwenu watu hao na watajitambulisha kwamba wao ni kamati za ulinzi  na usalama za misikiti,fungeni milango na madirisha ya msikiti yenu na muwapige sana”

Kongola aliimbia mahakama hiyo kuwa kauli hiyo  iliumiza imani za watu wengine na kwamba hatua hiyo ni kinyume cha agizo la mahakama  ya hakimu mkazi Kisutu  Dar-es-salaam iliyotolewa na hakimu V. Nongwa   mei 9 mwaka huu ambayo ilimtaka Ponda ndani ya kipindi hicho cha mwaka mmoja kutohubiri mambo ya uchochezi ambayo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 124 cha mwaka 2002, shitaka ambalo alikana.

KWA PICHA NA HABARI ZADI BOFYA SHEKIDELE.BLOGSPOT.COM

MABOMU YARINDIMA MAANDAMANO YA CHADEMA JIJINI MWANZA LEO.

$
0
0















CHADEMA YATIKISA, NI MABOMU YA MACHOZI KILA MAHALI, OFISI, MADUKA  YAFUNGWA.

MAANDAMANO ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) yamegeuka shubiri kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada ya kuibuka mapambano makali baina ya waandamanaji hao na jeshi la polisi mkoani Mwanza na kusababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.

Maandamano hayo ya amani ambayo yalianzia katika eneo la Buzuruga nje kidogo ya jiji la Mwanza yalikuw ayakiongozwa na wabunge Highness Kiwia wa Ilemela  pamoja na Ezekiel Wenje kuelekea katika viwanja vya Furahisha yalilenga kumshinikiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo kutoa barua zinazodaiwa kuandikwa na ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi kuwarejesha madiwani watatu waliotimuliwa katika Manispaa ya Ilemela kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.


Polisi wenye silaha pamoja na askari kanzu walianza kutanda katika eneo hilo la Furahisha wakiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza RCO Konyo ambaye alikuwa akitumia gari lenye namba za usajili DK 068EXV aina ya Toyota Land Cruiser


Maandamano hayo ambayo awali yalionekana kana kwamba yangelimalizika salama yaliwasili katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 5.38 huku yakiongozwa na gari la polisi lenye namba za usajili za nchi ya Uganda  779 UAG likiwa nimesheheni polisi wenye silaha nzito ikiwa ni pamoja na mabomu ya machozi na bunduki pamoja na askari kadhaa ambao walikuwa katikati ya maandamano hayo.


Baada ya maandamano hayo kuwasili katika viwanja vya Furahisha kwa amani,waandamani hao ambao walikuwa na mabango mbalimbali yaliyosomeka kuwa ‘Matata hatutaki uendelee kuwa Meya wa Ilemela rudia kazi yako ya awali, na jingine Jaji Sumari tumechoka kuahirisha mara kw amara kesi dhidi ya Matata na jingine  lililosomeka kuwa RD Ndikilo tunahitaji barua za kurejeshwa kwa madiwani wetu.


Hata hivyo tofauti na ilivyokuwa imetangazwa kuwa maandamano hayo ya amani yangelipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo,hakukuwa na kiongozi yoyote wa Serikali ambaye alikuwepo uwanjani hapo kupokea maandamano hayo.


Kufuatia kutoonekana kwa kiongozi yoyote wa Serikali,viongozi wa chadema pamoja na wabunge wao walikutana kwa faragha kwa dakika kadhaa kwa ajili ya kujua hatima ya maandamano hayo ambapo Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje alipanda jukwaani saa 6.45 na kuwaeleza maelfu ya waandamanaji kuwa wameamua kumtuma Mbunge wa Ilemela Highnes Kiwia kwenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuchukua majibu kwa ajili ya kuwaletea wananchi walioandamana juu ya hatima ya madiwani hao.

HABARI KWA HISANI YA GSENGO.BLOGSPOT.COM

BALOZI SEIF ALI IDDI AZINDUA MAABARA YA MAFUNZO YA TEHAMA, CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA KITUO CHA URATIBU CHA ZANZIBAR.

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais Balozi Sefu Ali Iddi, akikata utepe kuashiria uzinduzi  rasmin wa maabara ya mafunzo ya TEHAMA Chuo Kikuu Huria Tawi la Zanzibar, huko Beit rasi nje kidogo ya Mji wa Zanziabr.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Prof. Tolly Mbwette akimpa maelezo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Sefu Ali Iddi, kuhusu shughuli za mafunzo wanayoendeshwa chuoni hapo.
  Baadhi ya wanafunzi wanaosoma chuo Kikuu Huria Kituo cha Zanzibar wakiwa kwenye chumba cha Komputa .
 Mkurugenzi wa Kituo cha Uratibu cha Zanzibar cha Chuo kikuu huria cha Tanzania Yusuph Mussa  akitoa maelezo mafupi ya Kituo hicho, , huko Beit rasi nje kidogo ya Mji wa Zanziabr.
 Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wananchi baada ya uzinduzi wa maabara ya mafunzo ya TEHAMA kwenye kituo cha Uratibu cha Zanzibar huko Beit el ras nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Wahaziri na Wakurugenzi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmin mara baada ya uzinduzi wa maabara ya mafunzo ya TEHAMA Chuo Kikuu Huria Tawi la Zanzibar, huko Beit rasi nje kidogo ya Mji wa Zanziabr.

(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo-Zanzibar).


=========  =======  ========
Na Khadija Khamis na Miza Othman –Melezo  Zanzibar .


Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali IDDI amewata wananchi kutumia fursa iliyotolea na Chuo Kikuu Huria Tanzania kujiendeleza zaidi kwa mafunzo yanayotolewa na Chuo hicho  kwani kutawajengea uwezo wa kupata taaluma, maarifa, utambuzi pamoja na kuchanganuwa masuala mbali mbali yatakayosaidia  katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo

Ameyaeleza hayo alipokuwa akizinduwa Maabara ya  Mafunzo ya TEHAMA katika Chuo Kikuu  Huria cha Tanzania Kituo cha Uratibu cha Zanzibar kilichopo Beit el ras.

Balozi Seif amewataka wananchi kutumia fursa ya kujifunza masomo ya TEHAMA kutokana umuhimu wake hasa wakati huu wa  mabadiliko  makubwa  ya Sayanasi na Teknolojia duniani.

Amesema Serikali hivi sasa inaendelea na ujenzi wa mkongo wa Taifa ambao lengo lake  ni kuunganisha Wilaya zote  Zanzibar  na pia kuunganishwa na mtandao wa kimataifa ambao huunganisha nchi zote ulimwenguni.

“Bila shaka wengi wetu tumeshasikia kuhusu Mkongo wa Taifa wa mawasiliano kwa kutumia kompyuta ambayo ujenzi wake unaendelea nchini kote”, alisema Balozi Seif Ali Idd.

Ameongeza kuwa  zoezi hilo litakapo kamilika thamani na manufaa ya Mkongo wa Taifa  yataonekana endapo wananchi watakuwa na ujuzi wa kutumia TEHEMA.

Balozi Seif  aliupongeza uongozi wa Chuo Kikuu huria cha Tanzania kwa kasi kubwa ya maendeleo inayopiga katika kusambaza elimu kwa watanzania.

“Elimu ndio silaha kubwa katika masisha  hivyo juhudi hizi ni za kulindwa, kupongezwa na kujengewa mazingira mazuri ya kuboreshwa kila inapohitajika badala ya kuzibeza kwa sababu wanaofaidika ni Wazanzibari,”alisisitiza balozi Seif Ali Iddi.
  
Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Profesa Tollys. A. Mbwette amesema ni vyema wafanyakazi kutumia fursa ya huduma za Chuo hicho kwa kujiendeleza ili waweze kunufaika na mafunzo yanayotolewa  ambayo yatawasaidia katika kurahisisha utekelezaji wa kazi pamoja na kuongeza ufanisi.

Amesema lengo la kuanzisha kwa mafunzo ya  TEHAMA  hapa Zanzibar ni kuwasaidia wananchi kwenda sambamba na ukuaji wa  matumizi ya Sayansi na Teknolojia.

“Mafunzo haya ya matumizi ya TEHAMA yatakayotolewa na Kituo cha Uratibu cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yamelenga katika kuwahamasisha watu mbali mbali waliopo Zanzibar ili kupata maendeleo ya haraka katika matumizi ya Teknolojia,” alisema Makamu Mkuu wa Chuo.

Chuo cha Kikuu Huria cha Tanzania kimeanzishwa mnamo mwaka 1993 hadi oktoba 2012 jumla ya wahitimu 14,288 ambao kati yao 6075 wamehitimu vyeti na stashahada , 6655 Shahada ya kwanza 1558 walihitimu masomo ya Uzamili, Uzamivu na Shahada za udaktari za heshima.

      IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

NBC yazindua Huduma ya Mawasiliano ya papo kwa papo ya wateja (Hotline Service).

$
0
0
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Maharage Chande akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya mawasiliano ya papo kwa papo (Hotline Service) kati ya mteja wa benki hiyo na maofisa wa benki nhuduma itakayopatikana ndani ya matawi ya NBC. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Maharage Chande (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha benki hiyo, Jane Dogani (kushoto), wakifurahia wakati mmoja wa wateja wao, Amin Juma (katikati) akijibiwa swali alilouliza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
Meneja Mahusiano wa NBC Tanzania, Eddie Mhina akiongoza shughuli za uzinduzi wa huduma ya Hotline Service ya Benki ya NBC katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam. Huduma hiyo pia kwa sasa inaweza kupatikana katikan matawi mengine.

TAHADHARI KWA WANAWAKE! OGOPA MAPENZI YA KICHAWI.

$
0
0
Habari  za  jioni  Ndugu   Ahmed  Michuzi, ninaitwa   Mama  Jeska,Nimekuwa  muhanga  wa  uchawi  wa  mapenzi, yaani  nilienda  kwa  mganga  kutafuta  dawa  ya  mapenzi  ili  nimtulize  mwanaume  wangu, kinyume  chake  dawa  imekuwa  na  nguvu  sana  kiasi  yule  mwanaume  amekuwa  kama  zezeta. Ninaandika  waraka  huu   ili  kutoa  onyo  kwa  wanawake  wenzangu  ambao  wanaendekeza  mapenzi   ya  kichawi. Nitashukuru  sana  endapo  utauchapisha  waraka  wwangu  kwenye  blogu  yako, na  ikiwezekana  uusambaze  kwenye  blogu zingine  pia, ili wanawake  wenzangu  wajifunze .


TAHADHARI  KWA  WANAWAKE! OGOPA  MAPENZI  YA  KICHAWI:

Naitwa  Mama  Jessica, ni mwanamke mwenye  umri  wa  miaka  35, mkaazi  wa  Tabata, Dar  Es salaam.. Baada  ya  kuumizwa  sana    na  wanaume katika  mapenzi, niliamua  kutafuta  mganga wa  kienyeji, shoga  yangu  alinipeleka  kwa Mganga mmoja  anayeitwa  MUNGU  WAKABILI, ambaye  ni  Mtaalamu  aliyebobea   sana katika  masuala  ya  ULIMWENGU  USIO ONEKANA. Wakati naenda  kumuona  huyu  mganga, tayari  nilikuwa nimeanza  uhusiano  na  mwanaume mmoja lakini  na  yeye  akawa   haeleweki  heleweki. 

MUNGU  WAKABILI, alinipa  dawa   ya  mapenzi   ambayo  imenifanya  nijutie   kuitumia , kwani  baada  ya  kumfanyia  dawa  mwanaume  huyo, AMENIPENDA   KUPITA  KIASI! YANI AMEKUWA  KAMA   ZEZETA  KABISA! Alikuwa  na  mke  wa  ndoa na  watoto  watatu, ila amewatelekeza  wote   na  kuja  kuishi  na  mimi. Nyumba  aliyo jenga  na  mke  wake  ameiuza  na  kuninunulia  mimi  nyumba  nyingine   ili  tuishi  pamoja, kama  hiyo  haitoshi  alikuwa  na  magari  mawili  moja  amempa  mdogo  wangu  wa  kiume, jingine  ameliuza  na kunifungulia  duka  la  nguo  Kinondoni.

  Ni mambo mengi  sana, yote  siwezi  kuelezea, ila kibaya  zaidi  ni kwamba, sasa  ameshindwa  kuendelea  na  biashara  zake,anataka  kuwa  na  mimi  wakati  wote  kwa  sababu  amekuwa  na  wivu  sana, anahisi akiniacha  hata  kwa  dakika  mbili tu nitaibiwa  na  mwanaume mwingine. Kibaya  kuliko  vyote  sasa  ndugu  wa  mume, mke  wake  na  ndugu  wa  mke wake, wameanza  kunitishia  maisha  yangu .

 Nilijaribu  kwenda  kumuomba  huyu MUNGU  WA  KABILI  anipe  dawa  ya  kumrudisha  huyu mwanaume  katika  hali  yake  ya  kawaida  lakini  amegoma  kufanya  hivyo, anasema yeye   hawezi  kuharibu dawa  aliyo kwisha  itengeneza tayari  na  kwamba  alinionya  mapema.. Hapa  nipo njia  panda  na  sijui  hatma  ya jambo  hili, natamani  nikimbie  mji  lakini  nashindwa.  Nimeamua  kuandika  waraka huu  ili  kwanza, kuwaonya  wanawake  wenzangu  waachane  na   MAPENZI  YA  KICHAWI  ili  yasije  kuwakuta  kama  yaliyo nikuta  mimi, kwani naona  wanawake  wengi sana, wa  Dar  Es salaam, wanamkibilia  mtu  huyu  kwa  ajili  ya  kupata  dawa  za  mapenzi..

 Nakuonya  usifanye  hivyo mwanamke  mwenzangu, kwani  mtu  huyu  licha  ya  kuwa  na  umri  mdogo  tu tena  wa  miaka  chini  ya  thelathini, lakini  dawa  zake  ni  za  hatari  sana  na  zina  nguvu  za  ajabu  sana! Usijaribu  kabisa  mwanamke  mwenzangu,  utaumbuka,kwani kila  mtu  atajua  umetumia  uchawi!   Lakini, pili, ninawaomba  wanawake  wenzangu  mnisaidie   kumshawishi     MUNGU  WA KABILI  ili  amrejeshe  huyu  mwanaume  katika  hali  yake  ya  kawaida.. 

Naweka  namba  za  simu  za  MUNGU  WA  KABILI  hapa  na  ninaomba sana,  umalizapo  kusoma  waraka  huu, umpigie  simu  au kumtumia  meseji  huyu  Dokta. MUNGU  WA  KABILI   kupitia  simu  yake ambayo  ni       0753106197, mwambie,  Mama  Jesca  anapata shida sana,  na  sasa  ameanza  kusambaza  vipeperushi  mtaani akielezea  jinsi  ulivyo mfanyia  kitu kibaya.  Naamini  hili  linaweza  kumshawishi  na  hatimaye  kumrudisha  kaka  wa  watu  kwenye  hali yake  ya  kawaida.

Namba  za  MUNGU  WA  KABILI  ni  0753106197..UBARIKIWE SANA!

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUADHIMISHA SIKU YA MABUNGE DUNIANI KUHUSU SUALA LA MAKAZI, JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. Kulia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Prof. Anna Tibaijuka. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Ukumbi wa Bunge la Afrika Mashariki, baada ya kufungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, lililofunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha
 
 Baadhi ya wabunge na wageni waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano hilo leo, jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Tree Ltd ya Arusha, Magdalena Ayo, kuhusu utengenezaji wa Majiko Bomba, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, lililofunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. 
Picha  ya pamoja
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images