Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1427 | 1428 | (Page 1429) | 1430 | 1431 | .... | 1897 | newer

  0 0

  NA ESTOM SANGA- DODOMA

  Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa George Huruma Mkuchika amesema serikali itaendelea kuunga mkono mchango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika kutatua kero zinazowakabili wananchi katika kupambana na umasikini ili vita hiyo iwe endelevu .

  Mheshimiwa Mkuchika amesema jambo muhimu kwa TASAF ni kuhakikisha kuwa walengwa wote wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wanafikiwa na kunufaika na huduma za mfuko huo huku akisisitiza juu ya umuhimu wa kuzingatia maadili mema katika utendaji kazi wa wadau wote wanaohusika na utekelezaji wa Mpango huo .

  Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF zilizowasilishwa kwake na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga mjini Dodoma, Waziri Mkuchika ameuagiza uongozi wa TASAF kuhakikisha kuwa unawatumia kikamilifu Maafisa maendeleo ya Jamii walioko katika maeneo mbalimbali nchini kuhamasisha shughuli za maendeleo na kupambana na umasikini.

  “tunao maafisa maaendeleo ya Jamii nchini kote,lakini nina wasiwasi na namna wanavyotumiwa katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi,naagiza TASAF mtumie vizuri hazina hiyo ya wataalamu katika utendaji kazi wenu” ameagiza Waziri Mkuchika.

  Aidha Waziri huyo ameitaka menejimenti ya TASAF kuhakikisha kuwa inaandaa mipango thabiti katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kipindi kirefu huku akisisitiza kuwa walengwa wa Mpango huo wanapaswa kuwekewa mazingira yatakayowawezesha kujitegemea hata baada ya kuondolewa kwenye shughuli za Mpango.

  Akitoa taarifa ya utekelezaji,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema mfuko huo umeendelea kuwajengea msingi wa kujitegemea walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini nchini kote,kazi ambayo amesema imefanyika kwa mafanikio makubwa.

  Walengwa wengi hivi sasa wameweza kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi kwenye maeneo yao huku akitaja mafanikio makubwa katika utekelezaji wa masharti ya elimu na afya kwa walengwa jambo ambalo amesema linaendelea kusaidia juhudi za serikali za kupambana na adua ujinga na maradhi.

  “Kumekuwa na mwitikio mkubwa katika kuwapeleka watoto kutoka kaya masikini kupata elimu na huduma za afya, kwani hayo ni miongoni mwa masharti ya Mpango, na hyo kwetu ni mafanikio makubwa” amesisitiza Bwana Mwamanga.

  Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema mfuko huo kwa sasa unakabiliwa na changamoto ya kufikia takribani asilimia 30 ya vijiji ambavyo havikufikiwa katika awamu inayokaribia kukamilika, hivyo jitihada zaidi zinafanywa ili kupata fedha za kukamilisha vijiji hivyo katika awamu itakayofuata.
   Mheshimiwa Mckuchika akitazama nakala za vipeperushi,taarifa na majarida yenye taarifa za utekelezaji wa shughuli za TASAF,Ofisi kwake mjini Dodoma. 
   Waziri Mkuchika (aliyevaa suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF na Utumishi wa Umma ,baada ya kupata taarifa za utekelezaji wa shughuli za TASAF ofisini kwake mjini Dodoma, aliyevaa Kaunda suti ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga.
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Mhe. George Mkuchika (aliyevaa tai nyeusi) akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislau Mwamanga,ofisi kwa Waziri mjini Dodoma.

  0 0


  0 0


  0 0


  The VIT University of Vellore, India and the State University of Zanzibar (SUZA) have taken a major step in furthering their ties through the collective signing of two addenda to the Agreements of Cooperation on the Bachelor Programme in Multimedia and Animation and Bachelor Programme in Computer Science.  This event was held at Tunguu Campus on Monday 13th November, 2017.
  Dr. Govindasamy Viswanathan, the Founder and Chancellor of VIT University who signed the Agreements on behalf of his university has expressed his institution’s readiness and determination in maintaining concrete relations with SUZA. 

   Prof. Rai and Dr. Viswanathan sign addenda to the Agreements of Cooperation being witnessed by other officials and students.
   Dr. Viswanathan who was accompanied by Dr. C. Vijaykumar, the VIT University Director of International Relations said that the cooperation between the two institutions will benefit students, lecturers and officials of both universities.
   “India and Africa have so much in common and Zanzibar being part of this continent is one of the representatives, so let’s work together, as there are so many things we can benefit from each other if we collaborate,” Dr. Viswanathan insisted.
  In his remarks, Prof. Rai emphasised the need for the ties; he said that it is essential for SUZA to highlight its challenges so as to be able to tackle them through collaborative efforts and viable educational programmes. “We have recently merged with other higher learning institutions of Zanzibar, the issue to proud of, so we need to use this partnership in building our capacity so as to improve the quality of education,” he added.

  Prof. Rai explained that SUZA in the near future anticipates to introduce the School of Computing, Communications and Media hence to make this possible it expects support from VIT University to make this possible. “SUZA is already very strong in natural sciences and now we look for introducing innovation and entrepreneurship thus we can also extend our partnership in that area,” he informed.
  During his visit, Dr. Viswanathan also held a Public lecture speaking on 'Higher Education as tool for development of Africa".
  The State University of Zanzibar and VIT University on 4th July, 2013 signed a Memorandum of Understanding (MoU) aimed at establishing partnership on exchange of students, exchange of faculty, i.e. planning and handling of academic programmes and courses, organization of seminars, workshops and conferences including the exchange of mutual experiences in teaching, research and industrial practice. The MoU also sake to cooperate in exchange of research where joint programmes in research and development including exchange of publications and reports will be introduced.

  Other area focused by the MoU is exploration of possibilities of joint twinning programmes in interdisciplinary areas of specialization of high relevance to both institutions. In addition to this the MoU intended to create Centres of Excellence in specialized fields of mutual interest in Science, Engineering, Technology, Management and Humanities.

  The incident of signing these two addenda is an implementation part of the partnership.

  Before leaving Zanzibar on 15th November, 2017 the delegation from VIT University is expected to meet with Dr. Ali Mohamed Shein, the President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council also the Chancellor of the State University of Zanzibar.
  VIT University, also known as Vellore Institute of Technology (VIT), formerly known as Vellore Engineering College, is a private university in Tamil Nadu, India. Founded in 1984, as Vellore Engineering College, by Dr. G. Viswanathan, a former parliamentarian and minister in the Tamil Nadu Government. 

  0 0

  The VIT University of Vellore, India and the State University of Zanzibar (SUZA) have taken a major step in furthering their ties through the collective signing of two addenda to the Agreements of Cooperation on the Bachelor Programme in Multimedia and Animation and Bachelor Programme in Computer Science.  This event was held at Tunguu Campus on Monday 13th November, 2017.
  Dr. Govindasamy Viswanathan, the Founder and Chancellor of VIT University who signed the Agreements on behalf of his university has expressed his institution’s readiness and determination in maintaining concrete relations with SUZA. 
   Prof. Rai and Dr. Viswanathan sign addenda to the Agreements of Cooperation being witnessed by other officials and students.
   Dr. Viswanathan who was accompanied by Dr. C. Vijaykumar, the VIT University Director of International Relations said that the cooperation between the two institutions will benefit students, lecturers and officials of both universities.

   “India and Africa have so much in common and Zanzibar being part of this continent is one of the representatives, so let’s work together, as there are so many things we can benefit from each other if we collaborate,” Dr. Viswanathan insisted.
  In his remarks, Prof. Rai emphasised the need for the ties; he said that it is essential for SUZA to highlight its challenges so as to be able to tackle them through collaborative efforts and viable educational programmes. “We have recently merged with other higher learning institutions of Zanzibar, the issue to proud of, so we need to use this partnership in building our capacity so as to improve the quality of education,” he added.

  Prof. Rai explained that SUZA in the near future anticipates to introduce the School of Computing, Communications and Media hence to make this possible it expects support from VIT University to make this possible. “SUZA is already very strong in natural sciences and now we look for introducing innovation and entrepreneurship thus we can also extend our partnership in that area,” he informed.

  During his visit, Dr. Viswanathan also held a Public lecture speaking on 'Higher Education as tool for development of Africa".

  The State University of Zanzibar and VIT University on 4th July, 2013 signed a Memorandum of Understanding (MoU) aimed at establishing partnership on exchange of students, exchange of faculty, i.e. planning and handling of academic programmes and courses, organization of seminars, workshops and conferences including the exchange of mutual experiences in teaching, research and industrial practice. The MoU also sake to cooperate in exchange of research where joint programmes in research and development including exchange of publications and reports will be introduced.

  Other area focused by the MoU is exploration of possibilities of joint twinning programmes in interdisciplinary areas of specialization of high relevance to both institutions. In addition to this the MoU intended to create Centres of Excellence in specialized fields of mutual interest in Science, Engineering, Technology, Management and Humanities.

  The incident of signing these two addenda is an implementation part of the partnership.

  Before leaving Zanzibar on 15th November, 2017 the delegation from VIT University is expected to meet with Dr. Ali Mohamed Shein, the President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council also the Chancellor of the State University of Zanzibar.

  VIT University, also known as Vellore Institute of Technology (VIT), formerly known as Vellore Engineering College, is a private university in Tamil Nadu, India. Founded in 1984, as Vellore Engineering College, by Dr. G. Viswanathan, a former parliamentarian and minister in the Tamil Nadu Government.

  0 0

   Katibu Msaidizi Tume ya Kurekebisha Sheria Agnes Mgeyekwa akiongea na Wazee pamoja na wafanyakazi wa makazi ya wazee wasiojiweza ya Kolandoto yaliyopo katika manispaa ya Shinyanga wakati Tume ilipotembelea makazi hayo ikiwa ni sehemu ya Utafiti wa Mfumo wa Kisheria wa Huduma za Ustawi wa Jamii Tanzania.
   Sehemu ya wazee wa Makazi ya Wazee wasiojiweza ya Kolandoto yaliopo katika Manispaa ya Shinyanga wakimsikiliza katibu Msaidzi Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Agnes Mgeyekwa.
   Mkuu wa Makazi ya Wazee wasiojiweza ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga Bi. Sophia Kang’ombe akisisitiza jambo wakati Tume ya Kurekebisha Sheria ilipotembelea makazi hayo wakati wa utafiti wa Mfumo wa Kisheria wa Huduma za Ustawi wa Jamii nchini.
   Mhadhiri Msaidizi kutoka chuo cha Ustawi wa Jamii Bw. Paul Mwangosi akizungumza wakati Tume ya Kurekebisha Sheria ilipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza  ya Kolandoto.
   Katibu Msaidizi  Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Agnes Mgeyekwa akimuelezea Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Bw. Alfred Shayo  lengo la Tume kufanya utafiti kuhusu Mfumo wa Kisheria wa Huduma za Ustawi wa Jamii Tanzania.
   Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Bw. Alfred Shayo akizungumza na ujumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria ulipomtembelea ofisini kwake.
   Katibu Msaidizi Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Agnes Mgeyekwa akimkabidhi  Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Bw. Alfred Shayo  baadhi ya Ripoti zilizofanyiwa kazi na Tume
   Mmoja wa Wazee katika Makazi ya Wazee wasiojiweza ya kolandoto  katika Manispaa ya Shinyanga Bw. Zengo Masemba akizungumza wakati ujumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria ulipotembelea Makazi ya Wazee hao mkoani Shinyanga.  
   Mmoja wa wazee katika makazi ya Kolandoto Zengo Masemba akifurahia kwa kucheza na ujumbe wa Tume  na maofisa wengine wakati ujumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria ulipotembelea makazi yao wakati wa kufanya utafiti kuhusu Mfumo wa Kisheria wa Huduma za Ustawi wa Jamii Tanzania katika mkoa wa Shinyanga
   Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bi Agnes Mgeyekwa  na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja  na wazee pamoja na wafanyakzi wa makazi ya wazee wasiojiweza ya Kolandoto yaliyopo katika manispaa ya Shinyanga mkoa wa Shinyanga
   Mkurugenzi wa  kituo cha kulelea watoto yatima cha ‘Shinyanga Society for Orphans’ bi. Ayam Ally Said akizungumza na ujumbe wa Tume ya kurekebisha Sheria uliokwenda kutembelea kituo hicho wakati wa kufanya utafiti kuhusu mfumo wa kisheria wa Huduma za Ustawi wa Jamii Tanzania.
   Katibu Msaidizi Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bi. Agnes Mgeyekwa akiwa na Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto yatima cha ‘Shinyanga Society for Orphans’ kilichopo mkoani Shinyanga
   Katibu Msaidizi Tume ya Kurekebisha Sheria bi. Agnes Mgeyekwa akiangalia  baadhi ya magodoro yaliyotolewa msaada kwa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha ‘Shinyanga Society for Orphans’  wakati Tume ikifanya Utafiti kuhusu Sheria ya Huduma za Ustawi wa Jamii katika mkoa wa Shinyanga, anayemuonesha ni Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Ayam Ally Said
  Eneo la makazi ya Wazee wasiojiweza ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga mkoa wa Shinyanga

  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa amewasili katika Viwanja vya Kili Golf Jumapili Mkoani Arusha  kwa ajili ya kufunga mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf Kulia ni Katibu Wake Bw. Andrew Magombana na kushoto ni Bw. Chris Martin Makamu wa Rais wa Umoja wa Golf Tanzania(Tanzania Golf Union).
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kili Golf Bw. Bastiaan Bruins (Kushoto) baada ya kuwasili katika viwanja hivyo kwa  ajili ya kufunga mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf katikati ni  Makamu wa Rais wa Umoja wa Golf Tanzania(Tanzania Golf Union) Bw. Chris Martin.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ( wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na waandaji wa mashindano ya Wazi ya Kili Golf Mkoani Arusha.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe  akitoa risala kwa washiriki wa mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf katika halfa ya kufunga mashindano hayo jana Mkoani Arusha.
   Mshiriki kutoka Kenya Bw. Edwin Mudanyi  akijiandaa kupiga mpira wakati wa fainali wa mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf jana Mkoani Arusha ambapo  jumla ya washiriki 250 kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Zambia, Afrika ya Kusini na Tanzania walishiriki.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe  akimpa mkono wa hongera mmoja wa washindi wa kwanza Bw. Victor Joseph kutoka Tanzania baada ya kumalizika kwa mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf jana Mkoani Arusha.(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM).

  Na Lorietha Laurence- WHUSM, Arusha.

  Serikali imeahidi kushirikiana kwa ukaribu na wadau wa mchezo wa Golf nchini katika kuhakikisha mchezo huo unafundishwa kuanzia ngazi ya chini ili kuandaa wachezaji bora wa kimataifa wataoiwakilisha nchi katika mashindano hayo duniani.

   Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akifunga mashindano ya Kili Golf Mkoani Arusha ambapo ameeleza kuwa mchezo huo ni wa muhimu  ukazingatiwa katika kukuza sekta ya michezo.

  “Mchezo huu wa Golf ni mzuri sana kwa kuwa unakusanya watu wa tamaduni mbalimbali na kuwaleta pamoja nami naahidi kuwa Wizara yangu itahakikisha inashirikiana kwa karibu na wadau wa Golf nchini ili kuukuza zaidi” amesema Mhe. Dkt. Mwakyembe.

  Mhe. Dkt. Mwakyembe ameongoza kwa kuwataka washiriki wa mchezo huo kuwa mabalozi wazuri katika kuutangaza mchezo huo ndani na nje ya nchi na kuhamasisha vijana wengine kuwa na moyo wa kujifunza.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kili Golf Arusha Bw.Bastiaan Bruins amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuhakikisha mchezo huo unafahamika kwa watu wengi na kuondoa dhana iliyojengeka kuwa ni mchezo wa kitajiri.

  “Mashindano haya ni kuwapa hamasa watanzania kuupenda,kujifunza na kuelewa mchezo huu wa Golf ambao ni mchezo rahisi sana na unachangamasha akili huku ukiwaleta watu kutoka sehemu mbalimbali kuwa kitu kimoja” amesema Bw.Bruins. Kwa upande wa washiriki wa mashindano hayo hususani kutoka nje ya Tanzania wamewashukuru waandaaji na watanzania kwa ukarimu, upendo,ushirikiano  na umoja waliouonyesha huku wakiahidi kushiriki tena mashindano mwakani.

  Mashindano ya Wazi ya Kili Golf Tanzania yalifunguliwa rasmi Novemba 10 mwaka huu yakiwa na jumla ya washiriki 250 kutoka nchi za Malawi,Zambia, Afrika ya Kusini, Uganda , Kenya na wenyeji wao Tanzania huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na washindi wawili baada ya kutoka sare katika mchezo wa mwisho ambao ni Bw. Edwin Mudanyi kutoka Kenya na Bw. Victor Joseph kutoka Tanzania.

  0 0

  Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria na kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika  kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo kwa wakulima wa kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla ili kusaidia upatikanaji wa fedha na sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.

  Dhamira hiyo imewekwa wazi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila wakati akitembelea miradi mbalimbali ya kilimo mkoani Mwanza hivi karibuni.

  Bibi Kurwijila alisema kuwa katika kutekeleza mkakati wa kuwafikia wakulima wengi zaidi nchini Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imejipanga kutoa huduma kupitia kongane mpya nane (8) ili kuongeza tija kwa wakulima nchini.

  “Kongane ni njia ya kimkakati ya kijiografia yenye kujikita katika shughuli za kilimo zinazohusiana, wasambazaji, na taasisi zinazohusishwa katika kujenga usawa wa moja kwa moja miongoni mwa wadau, hivyo ili kukidhi mahitaji ya wakulima nchini, benki ya kilimo itawafikia kupitia njia hii,” alisema.

  Aliongeza kuwa kongane ya Kanda ya Ziwa ambayo inajumuisha mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Geita na Simiyu itatoa fursa ya ushindani kwa njia endelevu ili kuchagiza uhusiano na ushirikiano katika uongezaji wa thamani hasa katika makundi mbalimbali ya minyororo ya thamani, pamoja na taasisi na mamlaka za udhibiti zinazosaidia sekta ya kilimo nchini.

  “Tunaamini kuwa kupitia mifumo thabiti ya kongane kwenye ongezeko la thamani Benki itawajengea uwezo wakulima katika kuboresha ujuzi katika mapatano na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma pia kuwapatia wakulima katika vikundi faida za kiuchumi kwa kuzingatia nguvu ya masoko ya mazao yao,” aliongeza.

  Kwa mujibu wa mpango kazi wa Benki hiyo, dhana ya Kongane imeandaliwa kwa kutokana na mgawanyo wa kiokolojia kwenye kilimo kuzingatia kanda zilibainishwa kwenye Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP II 2016/17-2020/21) ambapo mikoa imegawanywa ili kurahisisha utoaji wa huduma na mapendekezo ya teknolojia kwenye mifumo sawa ya uzalishaji. Kongane hizi zimezingatia utendaji wa kila mnyororo wa thamani ya kilimo na faida za linganifu katika kila mkoa katika uzalishaji.

  Mpango kazi huo unaweka bayana kuwa matumizi ya Kongane yanalenga kuchagiza ufanisi katika kuimarisha minyororo ya thamani hasa wakati hakuna misingi thabiti katika kuendeleza minyororo hiyo ambayo inajumuisha kuanzia uzalishaji, usindikaji, usafiri, usambazaji, kuwezesha mazingira na soko. Hivyo uhitaji wa kuingilia kati juhudi hizi kutoka kwa wadau wengi ambao hawawezi kutatua suala lolote kwa pekee.

  Akizungumzia mgawanyo wa mazao yatakayopata kipaumbele kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki hiyo, Bw. Augustino Matutu Chacha alisema kuwa uteuzi wa minyororo ya thamani ya kipaumbele katika kila eneo umechukulia mchango wa mnyororo wa thamani katika usalama wa chakula, athari chanya kwa wakulima wadogo wadogo, mchango katika mikakati ya maendeleo ya kitaifa (hasa uendelezaji wa viwanda) - mpango wa maendeleo ya miaka mitano, soko la ndani na mauzo ya nje.

  “Kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mazao ya kipaumbele ni Mihogo, Mpunga, Mikunde, Ng’ombe wa Nyama na Maziwa, Pamba, Miwa na Samaki,” alisema.

  Bw. Chacha aliongeza kuwa Benki ya Kilimo inaamini kuwa kupitia Kongane wakulima wa watafikiwa kwa haraka kwa kuzingatia kuwa Tanzania ni nchi kubwa na yenye maeneo tofauti ya kimazingira/kilimo (Makundi) ambayo yana faida linganifu kwa ajili ya kuzalisha mazao maalum au seti ya bidhaa (mazao, mifugo, uvuvi).

  TADB iliyozinduliwa rasmi mnamo tarehe 08 Agosti 2015 imeanzishwa kwa madhumuni makubwa mawili ya kusaidia utoshelezi na usalama wa chakula endelevu nchini Tanzania; na kuchagiza mapinduzi ya kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
   Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Charles Hotar (kulia) akitoa maelezo juu ya uchakataji wa nyama kwenye Kiwanda hicho kwa ugeni kutoka Benki ya Kilimo. Ugeni huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (wapili kulia).
   Ugeni huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (wapili kushoto) wakiangalia namna ng’ombe anavyoandaliwa mara baada ya kuchinjwa.
   Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Charles Hotar (wapili kushoto) akionesha soseji zilizokuwa katika hatua za ufungaji. Wanaomuangalia ni wageni kutoka Benki ya Kilimo.
   Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB wakiangalia bidhaa mbalimbali zinazosindikwa na Kiwanda cha Chobo. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Bw. Joseph Mutashubilwa (wapili kulia) na Bw. Dome Malosha (kulia).
   Mmiliki wa Kiwanda cha Chobo Investment, Bw. John Chobo  (mbele) akiwaonesha mahala maji taka yanapochujwa ili kulinda mazingira ya kiwanda. Wanaongalia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (kulia) na Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki hiyo, Bw. Augustino Matutu Chacha (kushoto). Wapili kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Charles Hotar.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (kulia) akiangalia pembe ya ng’ombe kutoka Kiwanda cha Chobo. Kwa mujibu wa Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Charles Hotar (kushoto) pembe hizo uuzwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

  0 0
  Mkurugenzi Mtendaji wa Vituo vya ITV, Radio One, Capital TV na Radio, Joyce Mhavile akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati akizindua wiki ya miaka 30 ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mstaafu, Fatuma Mwassa, akizungumza na wanahabari katika uzinduzi huo.
  Mkurugenzi wa Tamwa, Eda Sanga, akizungumza katika uzinduzi huo.
  Wadau mbalimbali na wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
  Uzinduzi wa wiki hiyo ukiendelea.
  Taswira ya ukumbi wa mikutano ulipofanyika uzinduzi huo.
  Mkurugenzi wa Tamwa, Eda Sanga, akimvalisha vitenge Mkurugenzi Mtendaji wa Vituo vya ITV, Radio One, Capital TV na Radio, Joyce Mhavile vilivyo na Tamwa kama zawadi kwake. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mstaafu, Fatuma Mwassa
  Mhavile, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo akiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali.
  Ofisa Biashara wa Tamwa, Leonida Kanyuma (kulia), akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Joyce Mhavile kuhusu utendaji wa Tamwa.
  Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (C.R.C), Gladness Munuo akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi Joyce Mhavile wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya taasisi mbalimbali kwenye uzinduzi huo.
  Mtunza kumbukumbu na Taarifa wa TGNP-Mtandao, Speratus Kyaruzi akitoa maelezo mbele ya mgeni rasmi.
  Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shabani Rulimbiye, akimuonesha mgeni rasmi moja ya vipeperushi vya shirika hilo cha kupinga ukatili wa kijinsia.
  Mhavile akizungumza na wajasiriamali wakati alipotembelea mabanda yao.
  Suleiman Msuya

  WANAWAKE nchini wametakiwa kuonesha uwezo katika nafasi wanazozipata na kauchana na dhana ya kupata upendeleo au kubebwa kama inavyotafsiriwa na jamii.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vituo vya ITV, Radio One, Capital TV na Radio, Joyce Mhavile wakati akizindua wiki ya miaka 30 ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) leo asubuhi jijini Dar es Salaam.

  Mhavile alisema wanawake wengi wanaonesha kushindwa kufikia malengo yao katika nafasi mbalimbali ambazo wanapata kuzitumikia kutokana na kuishi na dhana kuwa watapewa upendeleo fulani.

  Alisema tatizo hilo lipo kwa wanawake wa makundi yote wakiwemo waaandishi wa habari wafanyabiashara na makundi mengine ambayo yanabakia kulalamika.

  “Mi nasema hivi ukipata nafasi katika dunia hii itumie kwa kuonesha uwezo wako ili watu watambue kipaji chako na si kutegemea kubebwa au upendeleo fulani kisa wewe mwanamke hiyo si sawa,” alisema.

  Mhavile ambaye alizindua wiki hiyo ikishirikisha maonesha mbalimbali aliwataka wanawake ambao wanashiriki maonesho hayo kutumia vyombo vya habari kujitanga ili bidhaa zao ziweze kufahamika.

  Mkurugenzi huyo alisema iwapo kila mwanamke ataondokana na dhana ya kuwezeshwa ni dhahiri kuwa watafanikiwa kwa haraka hivyo ubunifu kwa kila wanalofanya ni muhimu kwa sasa.Alisema TAMWA inapaswa kupanua wigo zaidi katika shughuli wanazofanya ili kufikia jamii kubwa kwani changamoto zilizopo ni nyingi na zinahitaji utatuzi.

  “Ukipata nafasi katika dunia hii ichukue na uishughulike pia uwe mwepesi kubuni mbinu mbalimbali ili kufikia malengo kwa haraka naamini tutafikia malengo,” alisema.Alisema vyombo vya habari vinapaswa kuwajibika kwa jamii kwa kuandika habari ambazo zinaonesha matokeo chanya kwa kila kinachofanywa na wanawake.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tamwa, Eda Sanga alisema chama chao kinaazimisha miaka 30 kikiwa kimefanikiwa kutoa mafunzokwa zaidi ya waandishi wa habari 2,000 hali ambayo imechochea uandishi wa masuala ya jinsia kupata nafasi katika vyombo vya habari.Alisema mikakati yao ni kuhakikisha wanatumia kioo walichonacho kumulika changamoto za unyanyasaji wa kijinsia katika jamii.

  Sanga alisema pamoja na mafunzo pia wamekuwa wakitoa ufadhili kwa waandhishi wa habari ili kwenda kwenye jamii iliyoathirika na unyanyasaji wa kijamii kuibua changamoto.

  “Miaka 30 hii ni ya mafanikio sana kwetu kwani tumefanikiwa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari 2,000 ambao wamekuwa mabalozi wazuri katika kuibua habari za unyanyasaji wa kijamii na matarajio ni kuendelea kuwajengea uwezo zaidi,” alisema.

  Mkurugenzi huyo alisema unyanyasaji wa kijinsia mfumo rithiwa tangu huko zamani ila wakati muafaka umefika kwa jamii yote kushirikiana ili kufikia katiia mfumo rafiki na shirikishi kwa kila mtu.

  Alisema kwa sasa hakuna haja ya kundi fulani kulaumu kundi lingine ila kinachohitajika ni jamii kujua kuwa uwasa wa kijinsia ni muhimu kwa maendeleo ya nchi na wananchi.

  0 0

  Mratibu wa Taifa wa mradi wa kupambana na usugu wa vimelea katika Shirika la chakula na kilimo duniani (FAO) Dkt. Bachana Rubegwa (aliesimama) akieleza maudhui ya semina hiyo niliyofanyika mapema leo katika ofisi za FAO jijini Dar es Salaam.


  NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

  WATANZANIA wanatakiwa kwenda vituo vya kutolea huduma za afya kupata vipimo kutoka kwa wataalam kabla ya kutumia dawa kwa mazoea ili kuepuka usugu wa vimelea vya wagonjwa kwenye miili yao na kusababisha vifo vya mara kwa mara.

  Hayo yamezungumzwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mradi wa kupambana na usugu wa vimelea kutoka Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) Dkt. Raphael Sallu wakati wa semina na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

  “Tatizo la kutumia vijiuasumu(Antibiotics) bila ya kupata vipimo na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya limekua kubwa ambalo linasababisha madhara ya kiuchumi na uhai kutokana na kuzidiwa na vimelea vya ugonjwa ambavyo vinakua sugu kutokana na matumizi mabaya ya dawa hapa nchini” alisema Dkt. Sallu.

  Aidha, Dkt. Sallu amesema kuwa elimu ya kutumia dawa bila ya kupata ushauri na vipimo kutoka kwa wataalamu wa afya ianze kutolewa kuanzia ngazi za shule ya msingi na ngazi ya jamii kwa ujumla.

  Mbali na hayo Dkt. Sallu amesisitiza kuwa wanahabari wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kuelimisha umma umuhimu wa kutumia dawa kwa kufuata ushauri kutoka kwa wataalam kuhusu ugonjwa unaomsumbua pamoja na matibabu yake.

  Kwa upande wake Mratibu wa Taifa wa Mradi wa kupambana na na usugu wa vimelea kutoka Shirika la Chakula (FAO) nchini Tanzania Dkt. Bachana Rubegwa amesema kuwa katika kupambana na tatizo hili kunapaswa kuwepo na matumizi ya hali ya juu ya chanjo ili kuweza kuepuka utumiaji hovyo wa dawa bila ya vipimo.

  “Katika kupambana na utumiaji wa madawa bila ya utaratibu mzuri ambao hauhusishi vipimo na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ni lazima maabara ya kutambua magonjwa sugu ijengwe nchini kwetu” alisema Dkt. Bachana.

  Hata hivyo Dkt. Bachana amesema kuwa wazilashaji wa chakula na mifugo wanatakiwa kutumia dawa zinazostahili na sio kutumia antibiotics katika mifugo yao pamoja na shughuli zao za kilimo ili kuepusha watanzania walio wengi kutumia vyakula hivyo vyenye usugu wa vimelea vya magonjwa.

  Mbali na hayo Dkt. Bachana ametoa rai kwa watoa huduma za afya nchini kuacha kutoa dawa ambazo ni feki,zilizokwisha muda na kuwashauri wananchi kuepuka matumizi ya dawa yasiyo ya lazima ili kuepuka usugu wa vimelea vya ugonjwa kwenye miili ya watanzania.

  Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) upande wa kupambana na usugu wa vimelea vya magonjwa Dkt. Rose Shija amesema kuwa watanzania wanatakiwa kutumia dawa sahihi na kwa wakati kadri alivyoelekezwa na mtaalam wa afya ili kuepuka matatizo hayo na kujijengea afya bora.

  “Tubadili tabia katika kupunguza maambukizi kupitia chanjo,kuosha mikono kwa maji safi yanayotiririka,kuepuka ngono zembe na utunzaji salama wa chakula na sio kutumia dawa bila ya ushauri kutoka kwa wataalam wa afya ili kuepuka usugu wa vimelea vya magonjwa mwilini” amesema Dkt. Shija.
  Mwakilishi Mkuu wa mradi wa kupambana na usugu wa vimelea (FAO) Dkt. Raphael Sallu akiwasilisha mchango wake wakati wa semina na Waandishi wa habari kuhusu matumizi bora ya Antibiotic, ilofanyika katika ofisi za FAO jijini Dar es salaam.

   Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) upande wa kupambana na usugu wa vimelea vya ugonjwa Bi Rose Shija akiwasilisha mchango mbele ya wadau wa habari, pembeni yake ni Afisa Habari wa Wizara ya Afya Catherine Sungura.
   04.Mmoja ya wadau wa Habari ambae pia ni mmiliki wa Blog ya Full Shangwe akitoa mchango mbele ya wadau wenzie wa habari na wawakilishi wa Mashirika ya kimataifa katika Semina ya kuhamasisha matumizi bora ya antibiotic.

  Washiriki wa semina hiyo wakifatilia mada mbalimbali.Picha na Emmanuela Massaka,Globu ya jamii.  0 0

  Serikali imesema mapato yatokanayo na kodi ya majengo yanayokusanywa na Serikali yameongezeka baada ya jukumu hilo kukabidhiwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ikilinganishwa na ilivyokuwa chini ya Halmashauri.

  Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Bukoba Mhe. Wilfred Lwakatare (CHADEMA), aliyetaka kujua Serikali inazipa Halmashauri ushauri gani wa kitaalam wa hatua za kuchukua ili kuziba pengo la kibajeti.

  Katika swali hilo Mhe. Lwakatare aliuliza kuwa Serikali haioni kuwa uamuzi wa kuipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kukusanya kodi hiyo ya majengo ni kuzidi kuipa mzigo mkubwa ambao hawatauweza.

  Dkt. Kijaji alisema kuwa baada ya makusanyo yatokanayo na kodi za majengo kuanza kukusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA katika Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji 30, yalipanda hadi kufikia Sh. bilioni 34.09 mwaka wa fedha  2016/2017 ikilinganishwa na Sh. bilioni 28.28 zilizokuwa zimekusanywa na Serikali za Mitaa mwaka wa fedha 2015/2016.

  “Makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la asilimia 20.6 ya makusanyo halisi yaliyopatikana kutoka Halmashauri husika kabla ya kodi hiyo kuhamishiwa TRA hali inayodhihirisha kuwa, TRA imefanya kazi nzuri katika kukusanya mapato ikilinganishwa na kiasi kilichokusanywa na Halmashauri hizo 30 katika mwaka wa fedha 2015/16.”. alisema Dkt. Kijaji.

  “Katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18 Julai hadi Septemba, TRA, ilipangiwa kukusanya kodi ya majengo ya kiasi cha Sh. Bil 11.9 na kufanikiwa kukusanya kiasi cha Sh. Bil. 13.2 ikiwa ni ufanisi wa asilimia 111”.  Aliongeza Dkt. Kijaji.

   “Hatua ya Serikali ya kukasimu jukumu la ukusanyaji wa kodi za majengo kwa TRA, haikulenga kuzinyang’anya Halmashauri vyanzo vya mapato bali ni kuimarisha ukusanyaji wake”. alisema Dkt. Kijaji.

  Aliongeza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kunakuwepo ufanisi katika ukusanyaji na matumizi ya kodi zote zinazokusanywa ndani ya Serikali na kwamba Halmashauri zote zinapata mgao wa fedha kwa kuzingatia makisio ya bajeti zao na makusanyo ya mapato yote ya Serikali.

  Aidha, Dkt. Kijaji alisema kuwa Serikali inatambua kuwa kodi ya majengo imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa mapato ya Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji katika kutekeleza mipango na utoaji wa huduma na maendeleo kwa wananchi.

  Katika swali la nyongeza Mhe. Lwakatare alihoji kwa nini Serikali isichukue maoni yake ya baadhi ya majengo makubwa yatozwe kodi na TRA na yale madogo yatozwe kodi na Halmashauri kwa kuwa kumekuwa na changamoto kwa TRA katika ukusanyaji wa kodi hiyo na kuwatumia Maafisa Watendaji wa Kata katika kukusanya kodi hizo ambao wameajiriwa na Halmashauri.

  Akijibu swali la nyongeza Dkt. Kijaji amesema kuwa Serikali na Bunge lilipitisha sheria ya fedha kwamba kodi ya majengo ikusanywe na TRA kwa lengo la kuimarisha ufanisi wake katika ukusanyaji na matumizi.

  “Serikali itaendelea kusimamia sheria hiyo na kuhakikisha lengo la kuchukua kodi hiyo linafanikiwa na wananchi wanapata huduma stahiki”. aliongeza Dkt. Kijaji.


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (kushoto) na Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Farmster ya Israel, Adam Abramson wakitia sahihi mkataba wa makubaliano ambapo Farmster itatoa huduma za upatikanaji wa masoko ya mazao na bidhaa za wakulima wanachama wa Mkikita kwa njia ya mtandao wa simu. Hafla hiyo ilifanyika viwanja vya Camp of Good Hope, Goba  jijini Dar es Salaam.

  Abramson ambaye ni mwasisi wa Farmster aliwaelezea waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo jinsi  jinsi ya kujiunga na mtandao huo kwa kutumia simu za smart na za kawaida yaani 'vitochi' ambapo mkulima huingiza namba ya simu 0623 753016 kwa kutuma neno Jambo.

  Mkulima atapaswa kutaja jina lake, eneo analoishi yaani shamba lilipo, analima zao gani, heka ngapi na anatarajia kuvuna lini na kwa kiasi gani ambapo huunganishwa moja kwa moja kwa mteja atakayejadiliana bei ya kuuzia.

  Wakala Mkuu kati ya Mkulima na Mnunuzi utakuwa ni Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA), kitendo ambacho kitasaidia sana kuuvunja mtandao wa madadali wanaosumbua na kuwaibia wakulima.

  Wakulima waliohudhuria hafla hiyo walionekana kufurahishwa na ujio wa teknolojia hiyo mpya na ya kisasa itakayowarahisishia wakulima kupata masoko mazao yakiwa shambani.IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (kushoto) akibadilishana hati za makubalino baada ya kutiliana sahihi mkataba  na Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Farmster ya Israel, Adam Abramson ambapo Farmster itatoa huduma za upatikanaji wa masoko ya mazao na bidhaa za wakulima wanachama wa Mkikita kwa njia ya mtandao wa simu
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Dk. Kissui S. Kissui (kushoto), akimpongeza Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Farmster ya Israel, Adam Abramson kutiliana sahihi mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa  Mkikita, Adam Ngamange (katikati) ambapo Farmster itatoa huduma za upatikanaji wa masoko ya mazao na bidhaa za wakulima wanachama wa Mkikita kwa njia ya mtandao wa simu. 
   Abramson akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo
   Akionesha namba ya kujiunga na mtandao huo
   Wanachama wa Mkikita wakisikiliza wakati mtalaamu huyo akiwaelezea faida mbalimbali atakazopata mkulima kwa kutumia mtandao huo
   Abramson akionesha eneo alipo mmoja wa wakulima aliyejiunga na mtandao huo
   Mkulima akipata maelezo kutoka kwa Abramson
   Wakulima wakiwa makini kumsikiliza mtalaam huyo
   Dk. Kissui ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita akiwatambulisha wakurugenzi wa bodi ya Mkikita.
   Wakulima wanachama wa Mkikita wakiwa katika hafla hiyo

   Maofisa wa Mkikita wakiwa katika tukio hilo
   Dk Kissui akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo
   Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akielezea jinsi walivyojipanga kumkwamua mkulima wa Tanzania kwa kutumia mbinu ama njia za kisasa kutafuta masoko

   Mapochopocho yakitayarishwa na wafanyakazi wa Spicy Catering kwenye viwanja mwanana vya Camp of Good Hope, Goba, Dar


   Wakulima wakionesha ishara ya kufurahishwa na  Mkikita kujiunga na Farmster
   Meneja Uhusiano wa Mkikita, Neema akijadiliana jambo na mmoja wa wanachama wa Mkikita
   Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya B&B Insurance Brokers Limited, Basil Bintamanyire wakitiliana sahihi kuingia mkataba ambapo kampuni hiyo ya Bima itakuwa washauri wa Mkikita kuhusu masuala yote ya bima katika kilimo na ufugaji

   Baadhi ya wakulima wakiwa katika hafla hiyp

   Msosi


  0 0

  Dares Salaam, Novemba 14, 2017: Sweden imeipatia Tanzania Msaada wa jumla ya Fedha ya Sweden SEK. Bilioni 1.64 ambayo ni sawa na takribani Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu. 

  Makubaliano ya msaada huo yamesainiwa Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting.

  Bw. James alisema kuwa imesainiwa Mikataba mitatu ya msaada huo ambayo ni; mkataba kwa ajili kusaidia Bajeti ya Serikali wa kiasi cha SEK milioni 600 ambazo ni sawa na Sh. bilioni 159.59 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2017/18 hadi 2019/2020, ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 watatoa takribani Sh. bilioni 53.20.

  Alisema fedha hizo zitaelekezwa katika kuboresha uhalisia wa Bajeti ili kuweza kutimiza majukumu ya kisera, kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ya kikodi na yasiyo ya kodi na pia kusaidia Serikali kutoa huduma nzuri kwa wananchi kupitia taratibu za manunuzi. 

  Mkataba mwingine ni kwa ajili ya kusaidia Mpango wa Elimu kwa Matokeo (EPforR) wa kiasi cha Fedha ya Sweden SEK milioni 885 ambayo ni sawa na Sh. bilioni 235.40 kuanzia mwaka 2017/18 hadi 2020/2021.

  “Lengo la msaada huu ni kusaidia Mpango wa Elimu kwa Matokeo ambapo tunapimwa namna ambavyo tumeweza kutimiza wajibu wetu tuliojiwekea katika bajeti. Baada ya ya Serikali kutimiza wajibu wake wa kupeleka fedha katika Sekta ya Elimu kwa wakati, wameamua kutupatia fedha hizo ambazo Serikali tunazipangia kazi kulingana na vipaumbele”, alieleza Bw. James.

  Alieleza kuwa Mpango wa Elimu kwa Matokeo ulianza mwaka 2015/ 2016 na katika kipindi hicho yamepatikana maendeleo makubwa katika ujenzi wa miundombinu ya madarasa, vyoo, mabweni. Utekelezaji wake umefanywa katika shule 361 kwenye Halmashauri 129 nchini.

  “Katika Mpango huo Vyuo 17 vya Walimu vimekarabatiwa ikiwa ni pamoja na kununua Kompyuta 260, Magodoro 6,730 na viti 1,976. Mpango huu unafanikiwa kutokana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuweka mkazo katika Sekta ya Elimu hivyo kupeleka fedha kwa wakati jambo linalosababisha washirika wa maendeleo wazidi kutuamini” alifafanua Bw. James.

  Mkataba wa tatu ni Marekebisho ya Mkataba wa Mpango wa Kusoma, Kuhesabu na Kuandika ambao una kiasi cha Dola za Marekani 94.8 zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Global Partnership for Education (GEP) na kukabidhiwa kwa nchi ya Sweden ili iweze kuusimamia.

  Akifafanua kuhusu Mkataba huo Bw. Doto James alisema kuwa Serikali ili saini Mkataba huo na Sweden Mei, 2015 na muda wa utoaji wa fedha hizo ulikwisha Agosti, 2016 na kubakia kiasi cha Dola milioni 18.3 ambazo zitapatikana baada ya kusainiwa kwa mkataba huo.

  Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo katika Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting amesema kuwa nchi yake imedhamiria kuhakikisha inajenga uwezo na ujuzi kwa watanzania kuanzia elimu ya Awali kwa kuwa nchi yake inathamini sana elimu.

  Bw. Kallsting alisema kuwa Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Sweden na inatekeleza kwa ufanisi miradi mbalimbali hivyo nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali ya Maendeleo ili kufanikisha mipango yake.

  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James ameishukuru Sweden kwa niaba ya Serikali kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika kutekeleza bajeti yake.


  Imetolewa na;
  Benny Mwaipaja
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Fedha na Mipango.
   Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (wa pili kushoto) wakisaini Makubaliano ya Msaada wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia)na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (kushoto) wakisaini Makubaliano ya Msaada wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (kushoto) wakiwa wameinua juu Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na  kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Maafisa waandamizi kutoka Ubalozi wa Sweden Nchini Tanzania wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Amina Khamis Shaaban (Kushoto), Kamishna Msaidizi wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bi. Mamelta Mutagwaba na wengine wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na  kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msaada wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kutoka Sweden kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, ambapo amesema msaada huo unatoa fursa kwa Serikali kupeleka fedha zilizotakiwa kutekeleza majukumu hayo maeneo mengine ya Maendeleo ya Wananchi, hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (kushoto) wakibadilishana Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.


  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (wapili kulia) pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Ubalozi wa Sweden wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya kusainiwa Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango

  0 0

  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne – Marie Kaarstad (katikati) pamoja na Msaidizi wake katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne – Marie Kaarstad (kulia) alipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Technologies Tanzania, Ndg. Gao Mengdong (katikati) na Msaidizi wa Mkurugenzi, Ndg. Kyle Ma (kulia) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Technologies Tanzania, Ndg. Gao Mengdong pale alipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja  na ugeni kutoka ubalozi wa Norway ulioongozwa na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne – Marie Kaarstad (wa pili kulia) walipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0


   Meneja Mwandamizi  wa Shirika la umeme nchini, TANESCO, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (wapili kushoto), na wafanyakazi wenzake, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, akikabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 10, kwa Mkurugenzi Myendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Profesa Muhammed Janabi, (mwenye miwani), katika hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 14, 2017. Msaada huo w afedha utawezesha matibabu ya moyo kwa watoto watano waliolazwa kwenye taasisi hiyo.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limetoa msada wa Shilingi milioni 10 kusaidia matibabu ya watoto wanaougua maradhi ya moyo kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam leo Novemba 14, 2017.
  Akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya alisema, baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Taasisi hiyo inahitaji msaada ili iweze kuwafanyia upasuaji watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kugharamia matibabu hayo, uongozi wa TANESCO ulisikia maombi hayo.
  Kwa kawaida upasuaji kwa motto hugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 2.
  “Tumekuwa na uhusiano mzuri na Taasisi yako, kwa hivyo japo hatuna uwezo mkubwa lakini Mkurugenzi Mtendaji aliona ni vema tutoe msaada wa kuwezesha upasuaji wa watoto watano, na leo tutakabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10.” Alisema Mhandisi Mgaya katika hafla ya kukabidhi hundi hiuyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa JKCI, Muhimbili jijini Dar es Salaam.
  Aidha Mhandisi Mgaya alisema mbali na msada huo wa fedha, TANESCO pia imeondoa tatizo la upatikanaji wa umeme wa kutosha kwenye taasisi nhuyo kwa kuwawekea huduma maalum ili kuhakikisha umeme unapatikana bila ya shida yoyote.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakayab Kikwete, Profesa Mohammed Janabi, alisema ili kuenzi msada huo wa TANESCO, mmoja wa watoto watakaofaidika na msada huo atapewa jina la TANESCO.
  “Tutawaalika katika hatua ya mwamzo kabla ya upasuaji ili muone hali halisi ya mgonjwa na baada ya upasuaji na tutamuita TANESCO motto huyo.” Alisema Profesa Janabi wakati akitoa shukrani zake.
  Naye Daktari bingwa wa moyo kwa watoto, Dkt. Naiz Majani alisema kwa mwaka Taasisi hupokea wagojwa wanaohitaji upasuaji kiasi cha 200,000, kwa hivyo msada huo na minbgine kutoka kwa wasamaria husaidia pakubwa katika kuokoa maisha ya watoto wa Kitanzania.
  “Tunawashukuru sana kwa msada wenu na tunaomba muendelee kusaidia jamii katika kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapatriwa matibabu ya moyo hata kama uwezo wao ni mdogo.” Alisema Dkt. Majani.
  Katika hatua nyingine wafanyakazi wa TANESCO wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto waliolazwa kwenye taasisi hiyo wanaosubiri kufanyiowa upasuaji.


   Mhandisi Mgaya na Profesa Janabi, wakimsikilzia Mwenyekiti wa TUICO, Tanesco, Bw.Hassan J.M Athumani, wakati akitoa shukrani.
   Profesa Janabi (kulia), akimkabidhi jarida la taasisi hiyo, Mhandisi Mgaya
   Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (kulia), akisalimiana na Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto, Dkt. Naiz Majani.
   Bi. Muhaji akikabidhi msada wa maji, na mahitaji mengine, kwa muuguzi wa zamu wa wodi ya watoto wanaougua maradhi ya moyo, Bi.Joyce Mtanga
   Mwenyekiti wa TUICO Tanesco, Bw. Hassan J.M Athjumani, (kulia), akikabidhi maji kwa mzazi wa mtoto aliyelazwa JKCI akisubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo.


  Mtoto MrishoHaidari(Miezi 7), ambaye anasumbuliwa na maradhi ya moyo akiwa wodini akisubiri kufanhyiwa upasuaji.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)​

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na Balozi mpya wa China nchini Tanzania Balozi Wang Ke alipomtembelea katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.Viongozi hao walizungumza masuala mbalimbali ya Ushirikiano na Uwekezaji.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akimsikiliza Balozi mpya wa China nchini Wang Ke alipomtembelea katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akifurahia jambo na Balozi mpya wa China nchini Tanzania Balozi Wang Ke alipomtembelea katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na Balozi mpya wa China nchini Tanzania Balozi Wang Ke na Ujumbe wake leo katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akimkaribisha Balozi mpya wa China nchini Ofisi kwake Bungeni leo Mjini Dodoma.Picha na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.

  0 0

  The Minister of Trade, Industry and Marketing of the Revolutionary Government of Zanzibar, Hon.Amb. Amina Salum Ali with the Managing Director and CEO of Bank Of Africa Tanzania Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah. The visit was a courtesy with intentions of supporting various Government initiatives in Zanzibar.


  0 0


  Na Hamza Temba – WMU

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali kupitia Wizara yake inakusudia kuandaa mkakati maalum wa kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini China ili kuongeza idadi ya watalii na mapato ya Serikali.

  Dk. Kigwangalla amesema hayo jana ofisini kwake mjini Dodoma akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke ambaye alimtembelea kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya Uhifadhi na Utalii.

  “Moja ya mkakati wangu kama Waziri mpya wa Wizara hii kukuza utalii ni kuweka mkakati wa kuleta watalii wengi kutoka China, China ni Taifa Kubwa lenye watu wengi, tunalenga zaidi kuwafikia watu wanaoishi maisha ya kati ambao ndio wanaopenda kutumia fedha zao kufurahia maisha” alisema Dk. Kigwangalla.

  Katika mazungumzo hayo alimuomba Balozi huyo kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa njia ya ushauri wa kitaalamu au wa kifedha kwa ajili ya kuandaa mkakati mahususi wa kulifikia soko la utalii la China kwa kuainisha vivutio na aina ya huduma ikiwemo hoteli ambazo zitakuwa kivutio kwa watalii kutoka China kuweza kutembelea Tanzania.

  Miongoni mwa mikakati waliojadiliana ni uwezekano wa kutumia fursa ya uwepo wa wawakilishi wa Televisheni ya CCTV ya China nchini Tanzania ambao wanaweza kutumika kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini ikiwemo kuambatana na Waziri Kigwangalla kwenye ziara zake za kikazi kwenye maeneo ya vivutio na baadaye kuvitangaza nchini China na Duniani kote.

  Walijadili pia uwezekano wa kuanzisha safari za moja kwa moja za ndege baina ya nchi hizo mbili kwa lengo la kurahisisha Safari za Utalii pamoja na kuanzisha mtandao wa pamoja wa watoa huduma za utalii wa mataifa hayo mawili.Aidha, Dk. Kigwangalla alimuomba balozi huyo kuleta wawekezaji katika sekta ya Hoteli za kitalii na kuahidi kuwapa maeneo ya kujenga hoteli hizo ili kukuza huduma na soko la utalii nchini kwa kurahisisha upatikanaji wa watalii wa China kutembelea Tanzania.

  Kwa upande wake Balozi Wang Ke alimueleza Waziri Kigwangalla kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali ambapo mwezi Februari mwakani (2018) itaandaa Maonyesho ya Kimataifa ya Kuuza Nje na Kuingiza Bidhaa na Huduma (International Export and Import Fair) ambapo watu mashuhuri kutoka China watashiriki akiwemo mcheza Filamu mashuhuri kwenye filamu ya kichina kwa Lugha ya Kiswahili maarufu kama Maododo.

  Alisema kupitia Maonyesho hayo Tanzania itaweza kujenga mtandao wa utalii na China kwa kunadi vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini kwa watu maarufu watakaoshiriki maonyesho hayo wakiwemo wafanyabiashara na watoa huduma za utalii na ukarimu.
   
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke ofisini kwake mjini Dodoma jana Novemba, 14 ambapo walijadili mikakati ya kuongeza idadi watalii na wawekezaji katika sekta hiyo kutoka nchini China.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala (kushoto) akimkabidhi mteja wa bima ya Kampuni ya UAP Ndugu Godi Sanga kama fidia kutokana kukumbwa na janga la moto la kuungua kwa Soko la Sido Agosti 15 ,2017
  Mteja wa Kampuni ya UAP akikabidhiwa mfano wa hundi ya malipo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala ,ambapo kampuni hiyo ya bima imekamirisha kulipa fidia hizo kwa wateja wake ambapo zaidi ya shilingi milioni 250 zimelipwa huku kiwango cha chini kulipwa katika fidia hiyo ni shilingi milioni Saba huku mteja wa juu kulipwa ni shilingi milioni 180.
  Mkurugenzi Mtendaji wa UAP Mick Itunga akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi wateja wa kampuni ya bima ya UAP jana Nov 14 katika viwanja vya soko la Sido jijini mbeya ambapo amesema kuwa UAP ni kampuni kongwe katika sekta ya Bima duniani kwa miaka zaidi ya 170 ambapo amesema kampuni hiyo ndiyo yenye mtaji mkubwa wa Bima Tanzania ikiwa na zaidi ya shilingi Bilioni 20. Aidha Mkurugenzi huyo pia ametumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara wa mbeya kuendelea kuiamini UAP kama bima bora nchini nakwamba itakuwa mstari wa mbele mara wanapokutwa na majanga ya moto kama yaliyotokea katika soko hilo la Sido jijini Mbeya.
  Mfanyabiashara wa Soko la Sido jijini Mbeya Ndugu Godi Sanga ambaye ni mteja wa Bima ya Kampuni ya UAP akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya malipo kutoka kwa kampuni hiyo ya Bima ambapo ametumia fursa hiyo kuishukuru kampuni hiyo kwa kumlipa fidia yake sanjali na kuwataka wafanyabiashara wenzake kuhakkisha wanajinunga na makampuni ya bima ili kujiwekea usalama wa biasahra zao.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika Picha ya pamoja na wadau wa bima.

older | 1 | .... | 1427 | 1428 | (Page 1429) | 1430 | 1431 | .... | 1897 | newer