Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NI JESHI LA MAENDELEO YA WATU: NAIBU KATIBU MKUU OR TAMISEMI TICKSON NZUNDA.

$
0
0
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 

Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wana jukumu la kuhamasisha wananchi kubadili fikra zao ili wawe na mtazamo chanya unaowapa hamasa ya kushiriki kazi za kujitolea ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na Taifa lao. 

Hayo yamezungumzwa Mjini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu kutoka OR TAMISEMI Bw. Tickson Nzunda wakati wa Mkutano wa Mwaka kwa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii na kuwataka washiriki kufanya kazi zao kwa umahiri, kujenga uelewa kwa viongozi wa Halmashauri, kuchochea mabadiliko sehemu za mitaani na vijijini, kuelimisha jamii kubadili mitazamo na fikra, na hivyo kukuza ari ya wananchi kushiriki maendeleo ili kufikia uchumi wa kati na wa viwanda. 

Pamoja na mambo mengine, Naibu Katibu Mkuu amewataka Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kuratibu shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu ili kuhakikisha kuwa mashirika hayo yanakuwa na mchango unaokusudiwa katika kufanikisha mipango ya Halmashauri, Mikoa na Taifa ili kuboresha ustawi na maendeleo ya watu.

“Tunatarajia kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiseriklali yangehakikisha kuwa yanasaidia kutoa mchango katika kuwekeza kwenye uwekezaji wa vipaumbele vya kitaifa vilivyoainishwa ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya elimu mashuleni ili kuwa na mazingira wezeshi ya kufundishia na kujifunzia, jambo ambalo halifanyiki ipasavyo” alisema Bw. Nzunda.

Naye Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amefafanua kuwa watumishi wa maendeleo ya jamii ndiyo washawishi na waragibishi wakuu katika kuamsha ari ya wananchi kushiriki mipango ya maendeleo kwa ajili ya mabadiliko ya watu wenyewe.

“Tutambue dhamana tuliyonayo lakini pia umahiri wenu utumike kusaidia watu masikini, wananchi wa vijijini na makundi maalumu katika kuwaongoza kupata haki na fursa sawa” alisema Bibi Sihaba. 

Akizungumza katika mkutano huo Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Nyasa Bw. Protas Sule amesema kuwa wataalamu wa maendeleo ya jamii wanajukumu la kuhimiza wananchi, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kusaidiana na Serikali na jamii kutatua matatizo haya bila kusubiri Serikali kutekeleza kila kitu.

“Afisa Maendeleo ya Jamii akifanikiwa kubuni mradi utatoa majawabu ya kero za vikundi vya vijana na wanawake atakuwa amefanya kazi kubwa ya kuaminisha jamii kwa Serikali na kuamsha ari yao kufanya kazi za maendeleo” alisema Bw. Sule

Maafisa Maendeleo ya Jamii wanatakiwa kuonesha utumishi uliotukuka katika kuhamashisha na kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo yao bila kutegemea Serikali kuwafanyia kazi

“TAHLISO YAIOMBA HESLB KUHARAKISHA FEDHA ZA WANAFUNZI VYUONI”-MWENYEKITI WA JUMUIYA

$
0
0
JUMUIYA wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso) wameiangukia bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu (HESLB) kuharakisha fedha za wanafunzi waliofeli baadhi ya masomo kwa kupata alama D waliopo vyuoni(supplementary).

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Stanslaus Kadugalize wakati akizungumza na mtandao huu ambapo alisema idadi ya wanafunzi waliofeli baadhi ya masomo vyuoni ni kubwa na mpaka sasa hawajapata fedha za kujikimu .

Alisema fedha hizo ni kama kauli ya Naibu Waziri wa Elimu alivyosema kuwa ifikapo ijumaa wiki iliyopitia fedha ziwe zimefika vyuoni lakini mpaka sasa fedha hizo hazijafika jambo ambalo linawapa wakati mgumu wanafunzi hao.

Mwenyekiti huyo alivitaka vyuo visiweke sababu zisizo za msingi juu ya kuwapa wanafunzi fedha zao za kujikimu kwa wale ambao tayari fedha zimekwisha fikishwa vyuoni kwa kigezo cha kujisajili.

“Tunatambua umuhimu wa kujisajili ila vyuo vitambue pia kwamba wapo wanafunzi wengi wanategemea fedha hizo hizo za bodi ya mikopo (HESLB) ili kulipia gharama za kujisajili kuweza kukamilisha zoezi la kujisajili hivyo vyuo viache kuweka sababu zinazopelekea usumbufu kwa wanafunzi “Alisema.

Kuhusu zoezi la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza alisema sasa bodi ya hiyo imekwisha kutoa kwa wanafunzi 29,000 kwa wale wote ambao wanasifa na hawajapata katika upangaji wa awali aliwashauri kutumia dirisha la rufani linalofunguliwa Novemba 13 mwaka huu ambapo rufaa hizo itakuwa ni bure.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo hakisita kuzungumzia kuhusu zoezi la udahili ambapo ambapo aliitaka TCU kuingilia kati kwani bado kuna usumbufu mkubwa wa wanafunzi wanaoupata na una hatarisha baadhi yao kukosa nafasi ya kusoma.

Alisema vipo vyuo vimefahili wanafunzi zaidi ya idadi wanayotakiwa mfano chuo cha Mwenge na vyenginevyo jambo la ajabu wanapokwenda kuripoti vyuoni wanaambiwa wamekwisha kamilisha idadi walizopangiwa.

“Sasa tunajiuliza kwanini walikubali idadi kubwa ya wanafunzi
wathibitishe kwenye vyuo vyao? kwanini wasiweke ukomo wa idadi kulingana na wanayotakiwa  lakini pia mpaka sasa wapo wanasumbuliwa vyuoni hawajapokelewa na wametoka makwao “Alisema.

“Mfano yupo mwanafunzi ametoka kwao Arusha amekwenda Mwanza kuripoti chuo kalipa na ada kabisa ya chuo sikitaji  na alithibitisha kusoma hapo ajabu amekwenda kuripoti wana mwambia wameshajaza idadi hivyo subiri maamuzi ya TCU kama wataruhusu kuwapokea “Alisema.

Aliongeza kuwa vyuo visipelekee vurugu zisizo na maana yoyote ile endapo wanafunzi hao watakosa nafasi za masomo kwa mwaka huu kwa uzembe wa vyuo kudahili zaidi ya idadi yao kwa hofu ya kukosa wanafunzi .

“Lakini niwaambie sisi kama Tahliso hatutasita kuvichukulia hatua vyuo hivyo kwa kuwalipa fidia ya usumbufu wanafunzi  ambao wamekumbana naowakati wa kufuatilia michakato hiyo “Alisema.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Article 2

$
0
0
Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT) wametembelea katika hifadhi ya ya Taifa ya Selous ili kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA. Akizungumza mwenyekiti wa umoja huo, Dkt. Liggyla Vumilia alisema kuwa wameamua kuandaa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa wa mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kampeni hiyo imeandaliwa na Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania -CAAT) kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania - (TTB) na TAZARA. PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG - SELOUS-MATAMBWE, MOROGORO.
Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT) wakifurahia ndani ya treni ya TAZARA wakati wakielekea ndani ya hifadhi ya Selous.
 Ilikuwa ni furaha kila kona.
Treni ya TAZARA ikichanja mbuga.
 Mahojiano yakiendelea ndani ya treni.
 Moja ya pango ambao treni inapita.
 Reli ya TAZARA imenyooka.
Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT) wakifurahia ndani ya treni ya TAZARA wakati wakielekea ndani ya hifadhi ya Selous.
 Makaribisho ndani ya hoteli iliyopo nje kidogo ya hifadhi ya Selous eneo la Kisaki.
 Wakipata chakula cha usiku.
 Nami mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Kajuna (kulia) niliweza kuwakilisha vyema na wana-CAAT. Pembeni yangu ni Chris na Yusuph.
 Wazee wa kazi Kaijage (mbele) akiwa na Dr. Heri.
 Wana-CAAT wakipata kifungua kinywa.
 Wana-CAAT wakiwa tayari kuingia mbugani kujionea vivutio mbali mbali. Wana-CAAT wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari ya kuingia mbugani.
 Moja ya wanyama wanapatikana hifadhi ya Selous.
 Eneo la Matambwe gate.
 Furaha baada ya kufika eneo la geti kuu.
 Mhifadhi wa Wanyama Pori wa Selous kanda ya Matambwe, Gregory Kalokole akitoa maelezo machache juu ya hifadhi ya Selous. PORI la akiba la Selous ni moja kati ya hifadhi zenye utajiri wa vivutio adimu vya utalii na ambavyo vinapaswa kutangazwa zaidi kwa ajili ya watalii wa ndani na wa nje. 

Selous ni pori la akiba lenye ukubwa wa kilometa za mraba 54,000 likijumuisha maeneo ya ardhi oevu, misitu ya miombo, tambarare, nyasi za kuvutia, maziwa na mito inayotiririka, vyote vikifanya vivutio vya aina yake mbali na wanyama wa aina mbalimbali. 

Pori hili la akiba la Selous lilianzishwa mwaka 1896 na Wajerumani likiwa ni pori la kwanza kutengwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori katika Bara la Afrika na la pili duniani kwa ukubwa baada ya hifadhi ya pori la Marekani ambalo linaitwa Yellowstone. Poro hili limegawanyika katika kanda 8 kiutawala. 

 Umaarufu wa Selous si katika wanyama pekee ambao ndiyo kivutio kikubwa cha utalii wa uwindaji, utafiti umebaini kuwa katika eneo la Selous kuna utajiri mkubwa wa maliasili ya mimea ambayo ikitambuliwa na kutangazwa inaweza kuwa kivutio adimu na cha kipekee cha kitalii.
 Wakisoma ramani mbali mbali inayoonyesha hifadhi hiyo.
 Moja ya ramani.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia akizungumza machache na Mhifadhi wa Wanyama Pori wa Selous kanda ya Matambwe, Gregory Kalokole.
 Moja ya wanyama wanaopatikana katika hifadhi ya Selous.

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA FINLAND NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Adolf Mkenda akimkaribisha Wizarani Balozi wa Finland nchini, Mhe. Pekka Hukka alipofika kwa ajili ya kujitambulisha kwake kama Katibu Mkuu mpya na kuzungumzia jinsi ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Finland. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 09 Novemba, 2017. 
Prof. Mkenda akimweleza jambo Balozi Hukka wakati wa mazungumzo yao. Pamoja na mambo mengine wlizungumzia kuimarisha ushirikiano katika masuala ya elimu, biashara na uwekezaji ambapo Prof. Mkenda alitumia fursa hiyo kumshukuru Balozi Hukka kwa msaada unaotolewa na Serikali yake kwa Taasisi ya Uongozi. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvatory Mbilinyi kwa pamoja na Bi. Tunsume Mwangolombe wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Balozi Hukka (hawapo pichani) 
Mazungumzo yakiendelea

VIONGOZI WOTE WALIOHUSIKA KUPOKEA MIFUGO PAMOJA NA WAFUGAJI KUTOKA NJE YA NCHI WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA-WAZIRI MPINA

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoama.

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, ameagiza Viongozi wote waliohusika kupokea mifugo Pamoja na wafugaji kutoka Nje ya nchi kuchukuliwa hatua za kisheria baada ya uchunguzi kukamilika ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji watakao gundulika walijihusisha na suala hiloni kinyume na maadili ya utumishi wa uuma.

Hata hivyo waziri huyo aliongoza zoezi la ukamataji wa Ng'ombe zilizo ingizwa nchini kinyume na utaratibu jumla ya Ng'ombe 1580 wanashikiliwa na kuagiza Ng'ombe hizo zitaifishwe na kupigwa mnada baada ya uchunguzi kukamilika na kuhakikisha ifikapo Novemba 10 mwaka huu Mifugo yote iliyoingia kinyume na utaratibu ziwe zimeondolewa kabisa.

Akizungumza juzi mara baada ya ukamataji wa Ng'ombe Wilayani kasulu Mkoani Kigoma, Mpina alisema viongozi walioshiriki kupokea mifugo kutoka Nje ya Nchi viongozi wa aina hiyo washughulikiwe kisheria anaejihusisha na suala la kuingiza mifugo hiyo kama itathibitika hawawezi kuwa na viongozi wanowahifadhi wahalifu wanaoingia Nchini bila kujali masilahi ya nchi na Ng'ombe zimekuwa kero kwa kuharibu Mashamba ya wananchi na Katika maeneo mengi ya hifadhi yameharibiwa sana na Wavamizi hao.

Alisema mpaka sasa mifugo yote iliyokamatwa kwa Nchi nzima ni mifugo 9500 na mifugo hiyo itatakiwa kutaifishwa baada ya Wanasheria na maafisa uhamiaji kuthibitisha kuwa iliingia kinyume cha sheria ilikuifanyia mnada na kukomesha wavamizi wote wanaoingia kinyume na utaratibu na kuharibu misitu na kuwa kichocheo cha migogoro ya wakulima na Wafugaji katika Maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake kaimu Mkuu wa Wilaya ya kasulu ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Buhigwe, kanali Marco Gaguti alisema katika msako walioufanya wilayani humo wamefanikiwa kukamata Ng'ombe 1580 na kwamba mpaka sasa wanaendelea na oparesheni ya kusaka mifugo hiyo ilikuhakikisha ifikapo novemba10 mifugo hiyo iweimekwisha ondoka na kuhakikisha klhakuna mifugo mingine inayoendelea kuingia kinyume na utaratibu.

Aidha Mkuu huyo alisema ,wapo baadhi ya viongozi walioshirikiana na wafugaji kwa kupokea fedha na kuruhusu mifugo hiyo iendelee kuishi Nchini bila utaratibu, uchunguzi unaendelea kuwabaini na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakao bainika na upelelezi unaendelea kufanyika kwa haraka kuhakikisha kuwa wamesafisha maeneo yote ambayo yamevamiwa na Wafugaji kutoka Nje na kuwabaini wale wote walioshirikiana nao.

Hata hivyo aliwaomba Wananchi kuendelea kutoa taarifa endapo kunawafugaji waliingia katika maeneo yao bila utaratibu na kuacha kuwahifadhi ilikuepusha migogoro ya Wafugaji na wakulima kutokana na wafugaji hao kuingilia maeneo ya wakulima.
 WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza jambo na
kaimu Mkuu wa Wilaya ya kasulu ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Buhigwe, kanali Marco Gaguti mara baada ya ukamataji wa Ng'ombe Wilayani kasulu Mkoani Kigoma
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza jambo na
kaimu Mkuu wa Wilaya ya kasulu ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Buhigwe wakitafakari jambo kwa pamoja.

NEWZ ALERT:WAZIRI WA KILIMO DKT TIZEBA AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA BODI YA SUKARI TANZANIA

$
0
0

Na Mathias Canal, Dodoma

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kumsimamisha kazi mara moja Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Henry J. Semwanza kuanzia leo Novemba 9, 2017.

Kwa agizo hilo lililotolewa na Waziri wa Kilimo Dkt Tizeba, Mkurugenzi huyo atatakiwa kurejea kwa mwajiri wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kupangiwa kazi nyingine.

Simwanza anasimamishwa kazi kutokana na mwenendo wake wa utendaji akiwa Msimamizi Mkuu wa Bodi ya Sukari kutoridhisha.Simwanza amehudumu katika nafasi hiyo akiwa Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari tangu mwaka 2011.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Henry J. Semwanza

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI MJINI DODOMA LEO NOVEMBA 9,2017

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akimsikiliza Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mhe.Freeman Mbowe wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu leo Bungeni Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akiteta jambo na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) Mhe.Dk Imaculate Semesi wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Mbunge wa Bukombe(CCM) Mhe.Doto Biteko akiuliza swali wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.William Ole Nasha akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Wanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya sekondari Dodoma wakiwa bungeni kujifunza shughuli mbalimbali za bunge ilo wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza mkutano wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof Joyce Ndalichako akiwasilisha kauli ya Serikali kuhusu udahili na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka 2017/2018 Bungeni mjini Dodoma.

Picha zote na Daudi Manongi.MAELEZO,DODOMA.

DK.SHEIN AKUTANA NA MWAKILISHI MPYA WA UNFPA NCHINI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na mgeni wake Mwakilishi mpya wa Shirika la UNFPA Nchini Tanzania Bibi.Jacqueline Mohan alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao,(kushoto) Bibi.Azzan Amin Nofly Ofisa katika Shirika hilo,[Picha na Ikulu.] 09 /11/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza Mwakilishi mpya wa Shirika la UNFPA Nchini Tanzania Bibi.Jacqueline Mohan alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao (haupo pichani ),[Picha na Ikulu.] 09 /11/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza Mwakilishi mpya wa Shirika la UNFPA Nchini Tanzania Bibi.Jacqueline Mohan alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao (kushoto) wengine (kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi (wa pili kulia) akiwa na Katibu Mkuu pia kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Nd,Salum Maulid Salum,[Picha na Ikulu.] 09 /11/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na mgeni wake Mwakilishi mpya wa Shirika la UNFPA Nchini Tanzania Bibi.Jacqueline Mohan baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 09 /11/2017.

NEC YASAMBAZA VIFAA VYA UCHAGUZI

$
0
0
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa maandalizi ya vifaa kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa madiwani unaofanyika katika kata 43 yamekamilika na awamu ya pili ya vifaa vitaanza kusafirishwa leo Ijumaa kwenda katika kata husika.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Kailima Ramadhani, alisema kwamba vifaa vitakavyosafirishwa kuanzia kesho ni maalumu kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo, makarani waongozaji pamoja na  mfano wa karatasi za kupigia kura.

Alisema awamu ya kwanza ya kusafirisha vifaa ulifanywa na tume wakati wa mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi ambayo yalifanyika mjini Dodoma ambavyo vilitumika wakati wa uteuizi wa wagombea udiwani katika kata zote.

“Napenda kuwahakikishia umma kwamba tume imejipanga vizuri kwa ajili ya uchaguzi huu na maandalizi ya kupeleka vifaa katika husika yako vizuri na awamu ya pili ya upelekaji wa vifaa itapaelekwa kesho (leo),”alisema Ramadhani.

Alisema awamu ya tatu ya usafirishaji wa vifaa itahusisha  vifaa vichache ambavyo ni karatasi za kupigia kura pamoja na fomu za kutangazia washindi ngazi ya kituo na ngazi ya kata.

Naye Mkurugenzi wa Manunuzi, Ugavi na Logistiki wa NEC Eliud Njaila, alisema kwamba NEC imepeleka vifaa vya kutosha katika vituo vyote 893  vilivyoko katika kata 43 na hakutakuwa na upungufu wowote.

Alisema kwamba katika awamu ya pili ya upelekaji wa vifaa, wameweka na mfano wa karatasi za kupigia kura ili wadau ambavyo ni vyama vya siasa vijiridhishe kuhusu karatasi hivyo zitakavyokuwa pamoja na kufanya uhakiki wa majina wa wagombea wao.

“Tunaamini kwamba vyama vya siasa vitahakiki majina ya wagombea wao kwa kila kata ili kama kuna masahihisho wayalete mapema na NEC iweze kufanya masahihisho haraka wakati wa kuchapa karatasi halisi za kupigia kura,” alisema Njaila.

Njaila pia aliwataka wasimamizi wa uchaguzi wa wilaya kuwatumia maafisa boharia katika kupokea na kutunza vifaa hivyo. Alisema wataalamu hao pia ndio watumike pia kusafirisha vifaa hivyo kwa kuwa wao wana ujuzi wa namna ya kutunza na kugawa vifaa.

Aliongeza kuwa iwapo wasimamizi wa uchaguzi watawatumia maafisa ugavi ni wazi kuwa hakutakuwa na malalamiko ya kupungua kwa vifaa katika vituo vya kupigia kura.

 Naye Ofisa Uchaguzi wa NEC Sada Kangeta, alisema kuwa tayari wameshafanya uhakiki wa vifaa vya uchaguzi na wamejiridhisha kuwa vifaa vyote vipo kama inavyopaswa na kwamba hatua itakayofuata ni usafirishaji wa vifaa hivyo katika maeneo husika.

Aidha aliwataka wapiga kura wote wa maeneo husika, wagombea wa vyama vyote vya siasa na wadau wa siasa kutokuwa na hofu juu ya vifaa hivyo kwa madai kuwa hakuna upungufu wowote utakaojitokeza.

KIGAMBONI KINARA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Mikoa na Halmashauri nchini kabla ya kutoa Tuzo kwa Mikoa na Halmashauri zilizofanya vizuri katika kuwawezesha wanawake kiuchumi.
  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akizungumza na Maafisa maendeleo ya Jamii katika siku ya ufungaji wa Mkutano wa 12 wa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii  na kuwasisitiza kuwajibika na kujituma katika kuleta  maendeleo katika maeneo yao.
 Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni Bi. Mwajuma Magwiza akitoa neno la shukurani kwa mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (hayupo pichani) na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa katika Mkutano huo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akimkabidhi tuzo kwa Afisa Maendeleo ya Jamii Kutoka Mkoa wa Dar es Salaam Bi.Esterine Sephania kwa niaba ya Halmashauri ya Kigamboni iliyoibuka kinara wa uwezeshaji wanawake kiuchumi kupitia mchango wa asilimia 5 katika mfuko wa maendeleo ya wanawake. 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) na Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na watoto Bibi. Sihaba Nkinga(wa tano kushoto mstari wa chini) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Mikoa na Halmashauri nchini, mara baada ya kufungwa kwa Mkutano wa 12 wa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii ulioambatana na utoaji Tuzo kwa Mikoa na Halmashauri zilizofanya vizuri katika kuwawezesha wanawake kiuchumi. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
  

Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni imekuwa kinara wa kuwawezesha wanawake kiuchumi katika vikundi vya uzalishaji mali katika halmashauri zao.

Hayo yamebainika katika utoaji wa tuzo kwa Mikoa na Halmashauri zilizofanya vizuri katika kuwawezesha wanawake kiuchumi katika kwa kutenga asilimia tano (5) katika Bajeti ya mapato ya Halmashauri katika  Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kiuchumi fedha inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.

Akitoa tuzo hizo Mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amewapongeza washindi wote waliofanikiwa kutekeleza mpango wa kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwatengea asilimia 5 katika Bajeti ya mapato ya halmashauri.

Ameongeza kuwa njia pekee ya kufikia maendeleo ya uchumi wa viwanda ni kuwawezesha wanawake kiuchumi kwani wengi wao wanashiriki katika shughuli za kijasilia mali ambazo zinawapa uwezo wa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali na uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo. 

Mhe. Jafo amesisitiza Maafisa Maendeleo ya Jamii kujituma katika maeneo yao na kuleta mabadiliko kwa kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za kujiletea maendeleo kufikia uchumi wa viwanda.

Naye Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bibi. Sihaba Nkinga amesema kuwa Serikali imedhamilia kuwawezesha wanawake kiuchumi na wao kama wasimamizi wa Sera watahakikisha wanafuatilia utekelezaji wake katika ngazi za Mikoa na Halmashauri.

“Tumejipanga kuwawezesha wanawake kiuchumi ambao watasaidia kuiwezesha jamii nzima kupitia shughuli zao za maendeleo kuelekea kufikia uchumi wa viwanda” alisema Bibi Sihaba.

Aidha Bibi Sihaba amewataka maafisa maendeleo kutumia weledi katika kusimamia uratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika ngazi ya halmashauri kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu katika kushirikiana kuwezesha wanawake kiuchumi ili kusaidia taifa kufikia azam ya uchumi wa kati na viwanda .  


Kwa upande wake Mwakilishi wa Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Kinondoni Bi. Mwajuma  Mwagiza ameishukuru Serikali kwa kuwezesha wananchi kiuchumi na kuahidi kuendelea kuhamasisha wanawake kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali ili kuwezesha kuleta maendeleo katika maeneo yao kufikia uchumi wa viwanda. 

Tuzo hizi za vinara wa uwezeshaji wa wanawake kiuchumi zimetolewa kwa Mikoa na Halmashauri kumi zikiongozwa na vinara Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni itasaidia kuleta chachu ya mabadiliko katika kuwawezesha wanawake kiuchumi Tanzania.

HATUJASHINDWA KUCHUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesisitiza kwamba vyombo vya dola vya ndani ya nchi havijashindwa kuchunguza matukio ya kihalifu yaliyotokea nchini, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuwa na subira.

Amesema Serikali hairidhishwi na matukio mbalimbali ya kihalifu yaliyofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa, ambayo yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini na baadhi yake yamesababisha vifo na wengine kujeruhiwa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Novemba 9, 2017) wakati akijibu swali la Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.

Bw. Mbowe alitaka apew kauli ya Serikali juu ya hatua zilizochukuliwa kuhusu tukio la kushambuliwa na mbunge wa Singida Mashariki Bw. Tundu Lissu, ambapo alishauri uchunguzi huo ufanywe na vyombo vya kimataifa, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo linashughulikiwa na vyombo vya ndani vya dola.

“Vyombo vya ndani vya dola vina uwezo mkubwa wa kusimamia usalama wa nchi na vinaendelea na uchunguzi wa matukio hayo yaliyofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa letu. Nawaomba wananchi waendelee kuwa na imani na vyombo vyetu vya dola na mara uchunguzi utakapokamilika taarifa itatolewa.”

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi waendelee kushirikiana na Serikali kwa kutoa taarifa mbalimbali juu ya vitendo vya kihalifu vinavyotokea kwenye maeneo yao kwa lengo la kudumisha amani na utulivu nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema ahadi ya Rais Dkt. John Magufuli ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma imeanza kutekelezwa kwa kuwapandisha madaraja watumishi wanaostahili sambamba na kulipa malimbikizo yao mbalimbali.

Waziri Mkuu amesema baada ya kumaliza ulipaji wa malimbikizo ndipo Serikali itaendelea na hatua ya uboreshaji wa mishahara kwa watumishi wote wa umma, hivyo amewaomba waendelee kuwa na subira na imani na Serikali. Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilindi, Bw. Omary Kigua aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itapandisha mishahara ya watumishi wa umma.

Pia Waziri Mkuu amezungumzia changamoto ya masoko kwa mazao ya mbaazi na tumbaku ambayo yanashughulikiwa na Serikali na tayari baadhi ya nchi zimeanza kuonyesha nia ya kununua mazao hayo, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuwa na uvumilivu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu Bibi Munde Tambwe aliyeiomba Serikali kumpatia ufafanuzi juu ya kukosekana kwa soko la tumbaku ambayo imelundikana katika maghala na Bibi Pauline Gekul Mbunge wa Babati aliyelalamikia kukosekana kwa soko la zao la mbaazi.

Akizungumzia kuhusu zao la tumbaku, Waziri Mkuu amesema changamoto hiyo imetokana na wakulima wa zao hilo kuongeza uzalishaji tofauti na makubaliano yaliyofikiwa awali na wanunuzi. “Nawaomba wakulima waendelee kuwa wavumilivu Serikali inafanya mazungumzo na nchi za lran, Korea Kusini, Misri na Indonesia ili waweze kununua tumbaku hiyo na kuwaondolea usumbufu wakulima.”

KATIBU MKUU MPYA OFISI YA WAZIRI MKUU APOKELEWA KWA SHANGWE DODOMA

$
0
0
 Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola wakati wa kumpokea alipowasili katika  ofisi yake  Mjini Dodoma  Novemba 9, 2017.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Ofisi hiyo wakati alipowasili katika ofisi yake mpya Mjini Dodoma Novemba 9, 2017.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Ofisi hiyo wakati alipowasili katika ofisi yake Mjini Dodoma Novemba 9, 2017.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchansi (kushoto) akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola katika ofisi yake mpya mara baada ya kuwasili Mjini Dodoma Novemba 9, 2017.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola akisaini kitabu cha wageni wakati alipowasili katika ofisi yake mpya Novemba 9, 2017 Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola akiteta jambo na Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi mara baada ya kuwasili katika ofisi yake Mjini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchansi akizungumza jambo wakati wa kikao cha Wakuu wa Idara na Vitengo Ofisi hiyo walipokutana kumkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola katika ofisi yake Mjini Dodoma Novemba 9, 2017.
 Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Packshard Mkongwa akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola mara baada ya kumpokea rasmi katika Ofisi hiyo Novemba 9, 2017 Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchansi akiwatambulisha Wasaidizi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola mara baada ya kuwasili katika ofisi yake Mjini Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU - DODOMA)

MAKAMU WA RAIS AFUNGA MAADHIMISHO YA MIAKA KUMI YA MTANDAO WA POLISI WANAWAKE TANZANIA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride maalum la polisi wanawake kwenye kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya umuhimu wa alama za barabarani kutoka kwa Koplo Faustina Nduguru wa Kitengo cha Usalama Barabarani makamo makuu ya polisi Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu kamera kugundua wanaoendesha kwa mwendo mkali kutoka kwa Konstabo Sharifa Ismail wa Kitengo cha Usalama Barabarani makamo makuu ya polisi Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Ali Mussa ambaye alimkaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi  kwenye kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

SERIKALI YAZINDUA NDEGE MAALUMU ITAKAYOFANYA DORIA ENEO LA BAHARI KUU KUDHIBITI UVUVI HARAMU

$
0
0


Serikali imezindua mkakati unaolenga kutokomeza uvuvi haramu kwa kuanzisha operesheni ya kutumia ndege maalumu itakayofanya doria katika eneo la bahari kuu.

Akizungumza wakati wa kuzindua safari ya ndege ya kutoka nchini Mauritius iliyotua hapa nchini, kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kufanya doria ya majini, Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega alisema lengo ni kudhibiti uvuvi haramu katika eneo la bahari kuu.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imejipambanua juu ya ulinzi wa rasilimali za nchi, ikiwamo meli ya uhakika ya majini, licha ya kukumbwa na dhoruba kubwa.

Amesema kutokana na hali hiyo ndiyo maana wameunganisha nguvu kwa pamoja kati yao na Ukanda wa nchi za Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi kudhibiti uvuvi haramu kwa njia zote.

“Tunaruhusu ndege ya doria leo, ili kuongezea nguvu njia za kudhibiti wavuvi haramu, tulianza kwa njia ya bahari na sasa ni kwa njia ya anga.

“Changamoto ya uvuvi haramu ni kubwa, mtu anapiga bomu kwenye matumbawe anafanya uharibifu ambao kuyatengeneza tena yanachukua zaidi ya miaka 100, huku yeye akiharibu kwa dakika tano, ” alisema Ulega.

Ulega alisema uharibifu huo ndiyo unachangia kuwatia umasikini wavuvi wengi kwa sababu siyo rahisi kupata samaki karibuni na kulazimika kwenda mbali ambako siyo rahisi kufika bila kuwa na vyombo maalumu.

Kwa upande wa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hamad Rashid alisema atashauriana na marais wa pande zote mbili kuangalia namna ya kurudisha Shirika la Uvuvi Tanzania (Tafico) na Shirika la Uvuvi Zanzibar (Zafico).

Alisema mashirika hayo yakifanya kazi kwa kushirikiana wananchi watapata fursa ya kufurahia matunda yatokanayo na utajiri uliomo baharini.

“Katika mwendelezo wa kupambana na uvuvi haramu na kulinda bahari ya Hindi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilifanya mazungumzo ya kuingia ubia na Serikali ya China na tayari kuna meli 10 zinafanya doria.

“Serikali pia imeagiza boti 500 watakazopewa wavuvi ili wazitumie kuvua kisasa, pia inasimamia ujenzi wa soko la samaki la kisasa na namna bora ya kuhifadhi samaki awe katika hali yake ile ile hadi anamfikia mlaji, ” alisema Rashid.

Alisema uvuvi haramu siyo tu janga kwa kuondoa rasilimali za bahari, pia ukiachwa uendelee unaweza kuwa chanzo cha biashara nyingine haramu ikiwamo usafirishaji wa watu, biashara ya dawa za kulevya na utakatishaji fedha.

Nae Katibu mkuu Uvuvi Dk Yohana Budeba alisema ndege hiyo itafanya doria ya anga kwa siku nne.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu Hosea Mbilinyi alisema ndege hiyo licha ya kuzunguka angani ikifanya doria, ina uwezo wa kupiga picha na kueleza kinachoendelea.

Alisema doria hiyo ni ya kikanda ambayo inahusisha nchi nane zikiwamo Tanzania Kenya, Msumbiji, Ushelisheli, Reunion, Comoro, Mauritius na Madagascar.

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya operesheni ya kutumia ndege maalumu itakayofanya doria katika eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu, leo jijini Dar es Salaam. Kulia  ni Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akishuka kwenye ndege maalumu itakayofanya doria katika eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu mara baada ya kuikagua ndani.
 Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega pamoja na viongozi mbalimbali wakiangalia ndege maalumu ya doria katika eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu.
 Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed naNaibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed akitoa zawadi kwa marubani wa ndege hiyo. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu yajamii.




USAMBAZAJI WA VIFAA VYA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI WAENDELEA.


JAFO AZINDUA KAMPENI YA MKOA WETU VIWANDA VYETU

$
0
0
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akizindua Mwongozo wa Kampeni ya uanzishwaji wa Viwanda kwa kila Mkoa hapa nchini ili kuendana na dhana ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisistiza ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akisisitiza umuhimu wa Wakuu wa Mikoa Kusimamia Kampeni ya uanzishwaji wa viwanda 100 katika kila Mkoa wakati akizindua kamapeni hiyo leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akieleza umuhimu wa Ujenzi wa Viwanda katika kuzalisha ajira kwa Vijana na kukuza uchumi wa nchi.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akionesha moja ya viatu vinavyozalishwa hapa nchini katika Viwanda vidogo na vya Kati wakati akikagua mabanda ya wajasiriamali wanaozalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo za ngozi mara baada ya kuzindua kampeni yenye kauli Mbiu ya “Mkoa Wetu Viwanda vyetu” ili kuhamasisha ujenzi wa Viwanda katika Mikoa yote nchini.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Mikoa(kushoto), kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya ujenzi wa Viwanda vidogo na vya kati katika kila Mkoa.

( Picha zote na Frank Mvungi – Maelezo, Dodoma)

…………………………………………………………………

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo amezindua kampeni ya “Mkoa wetu, Viwanda vyetu” yenye lengo la kuanzisha viwanda 100 katika kila Mkoa nchini, leo Mjini Dodoma.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Jafo amesema kuwa ni jambo lililowazi kuwa ili nchi iweze kuendelea inahitaji kufanya mapinduzi makubwa katika viwanda.

“Historia ya Viwanda siyo ngeni katika nchi yetu, tangu tupate Uhuru mwaka 1961 Serikali imekuwa ikilenga katika kujenga Uchumi kupitia Viwanda ambapo tokea wakati huo viwanda vingi vidogo vya kati na vikubwa vilianzishwa na kusimamiwa huku sehemu kubwa ya viwanda hivyo vikisimamiwa na Serikali” ameeleza Mhe. Jafo.

Aidha amesema kuwa ili azma hiyo iweze kufikiwa TAMISEMI itashirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika kuweka mazingira wezeshi pamoja na kutoa mwongozo wa namna ya kushirikisha Tasisi za Serikali na Sekta Binafsi na wadau wa maendeleo katika kuanzisha, kuendesha na kusimamia Viwanda ili kuikuza sekta hiyo nchini.

“TAMISEMI kupitia Mikoa na Halmashauri imedhamiria kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Viwanda, hivyo kila Mkoa uanishe Viwanda vya vipaumbele kwa kuzingatia Malighafi muhimu za Viwanda zinazopatikana kwenye maeneo yao pamoja na mahitaji muhimu ya soko” amefafanua Mhe. Jafo.

Hata hivyo, Mhe. Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na Halmashauri kuwatumia ipasavyo Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ugani ili kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa Wizara yake itaendelea kuweka mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na kuanza kujenga majengo maalumu kwa ajili ya uendelezaji viwanda katika Ofisi zote za SIDO Mikoani.

Naye Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Kauli Mbiu ya Mkoa wetu viwanda vyetu itapunguza changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana nchini.

JAMII YATAKIWA KUACHA ITIKADI ZA VYAMA KATIKA KULETA MAENDELEO

$
0
0
NA DENIS MLOWE, IRINGA

MBUNGE Wa viti maalum Mkoa Wa Iringa, Ritta Kabati ametoa wito kwa jamii kuondoka na itikadi za kisiasa pindi linapokuja suala la maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza na wazazi na walezi wa shule ya msingi Igeleke wakati wa ukarabati wa madarasa ya shule hiyo mwishoni mwa wiki ikiwa ni ahadi yake ya kukarabati shule za msingi zenye miundo mbinu mibovu na zamani, Kabati alisema kuwa suala la ujenzi wa madarasa hauna siasa.

Alisema kuwa maamuzi ya kukarabati shule za msingi lengo ni kuyaweka mazingira bora ya kusomea wanafunzi na kuwaepusha na ajali zinazoweza kujitokeza kutokana na uchakavu wa majengo.Kabati alisema kuwa imekuwa kawaida pindi mtu akitaka kufanya maendeleo mambo ya siasa yanaingizwa ila kwa serikali hii ya hapa kazi lazima tufanye kazi za kuleta maendeleo kwa wananchi.

Aliongeza kuwa maamuzi kufanya shughuli za kijamii hasa katika elimu ni kuifanya jamii ya watu wa Iringa kuwa na Elimu iliyo bora na kuweza kuwa na kizazi ambacho kitakuwa cha kimaendeleo kama ilivyo kanda za Kaskazini ambapo elimu ni kipaumbele cha kwanza.

“Mimi sipendi kuona watoto wa Iringa wanakuwa wafanyakazi wa kazi za ndani kwa watu kwenye Pesa au wafanyakazi wengi najiuliza tu kwanini ile Iringa ndio chimbuko la wafanyakazi wa kazi za ndani,nitapambana kuhakikisha Iringa inakuwa na wasomi wengi ili kupunguza utegemezi na kuondoa kasumba ya watu wengi wafanyakazi wa ndani ni kutoka mkoani hapa”alisema

Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo alisema shule hiyo inamiundombinu mibovu hivyo ni hatarishi kwa wanafunzi wa shule.Madembo alisema kuwa haangalii itikadika ya vyama bali anatafuta viongozi walio tayari kuleta maendeleo kwa kuwa hiyo ndio tija ya kuwa kiongozi kuwatumika wananchi waliotuchagua wakati tukiomba kura za kuwa viongozi.

“Leo hii mimi ni mwenyekiti wa CHADEMA lakini nipo na mbunge wa CCM aliyekubali kuja kusaidia kuleta maendeleo katika shule yetu yaIgeleke hivyo nipende kuweka wazi kuwa mimi kwenye maendeleo siangalii chama gani kinaleta maendeleo”
Kabati (mwenye njano) akishirikiana na wananchi kubeba zege kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Igeleke
Kabati (mwenye njano) akishirikiana na wananchi kubeba zege kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Igeleke
 Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akikabidhi saruji kwa uongozi wa shule kabla ya kuanza ukarabati katika shule ya msingi Igeleke.

LUSINDE AUWASHA MOTO KOROGWE MKOANI TANGA WAKATI WA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UDIWANI

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde  akiunguruma katika mkutano wa hadhara wa kumuombe kura mgombea Udiwani Kata ya Majengo wilayani Korogwe Mkoani Tanga Mustapha Shengwatu wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo zilizofanyika kwenye uwanja wa sabasaba wilayani Korogwe ambapo aliwataka wananchi kumchagua mgombea wa CCM kwani ndiye ambaye anaweza kuwapa maendeleo kwa haraka zaidi
 Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde  akiunguruma katika mkutano wa hadhara wa kumuombe kura mgombea Udiwani Kata ya Majengo wilayani Korogwe Mkoani Tanga Mustapha Shengwatu wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa sabasaba wilayani Korogwe ambapo aliwataka wananchi kumchagua mgombea wa CCM
Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde kushoto akimnadi mgombea udiwani Kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mji kupitia Chama cha Mapinduizi (CCM) Mustapha Shengwatu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba sokoni wilayani humo
 Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi akizungumza katika uzinduzi huo wa kampeni kumuombea kura mgombea wa CCM Mustapha Shengwatu kupitia kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mji
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi akizungumza katika uzinduzi huo wa kampeni kumuombea kura mgombea wa CCM Mustapha Shengwatu kupitia kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mji
Mwenyekiti wa CCM Korogwe Vijijini,Nassoro Hemedi Malingumu akizungumza katika mkutano huo wa hadhara
Mwenyekiti wa CCM Korogwe Mjini Emanuel Charles akizungumza katika mkutano huo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni hizo
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi wa Kata ya Majengo kumchagua mgombea wa CCM ili waweze kushirikiana naye kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa kasi zaidi
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi kuhakikisha hawafanyi makosa kwa kumpa kura nyingi za kutosha mgombea udiwani wa CCM kwani dhamira yake ni kuhakikisha anawapatia maendeleo kwa kiwango kikubwa
Katibu wa CCM Korogwe Mjini Ally Issa Ally akizungumza katika mkutano huo wa hadhara
Mgombea Udiwani wa Kata ya Majengo katika Halmashauri ya Korogwe Mji kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mustapha Shengwatu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba sokoni 


 Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi katikati akifuatilia hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda na kushoto ni Mgombea Udiwani wa CCM Mustapha Shengwatu
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi kushoto akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma (CCM) Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji wakati wa uzinduzi huo katikati anayeshughudia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda (Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma (CCM) Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji akisalimiana na makada wa CCM mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sabasaba sokoni  wakati wa uzinduzi huo kampeni za mgombea Udiwani kupitia chama hicho kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi
Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma (CCM) Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji katikati akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Tanga kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi kulia ni Katibu wa CCM Korogwe Mjini,Ally Issa Ally na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu wakiingia uwanja wa Sabasaba sokoni tayari kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni za mgombea udiwani wa CCM Kata ya Majengo.
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu kushoto akifuatilia kwa umakini hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde alimaarufu Kibajaji wakati wa uzinduzi wa kampeni za Udiwani Kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mjini huku akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM
 Sehemu ya umati wa wananchi wakifuatilia kampeni hizo

WATU MILIONI 126 KUAJIRIWA NA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA KUFIKIA 2024

$
0
0
Na Jumia Travel Tanzania

Usafiri wa anga ni miongoni mwa sekta inayochangia ukuaji wa uchumi wa dunia kwa kiasi kikubwa. Ilichangia moja kwa moja kiasi cha dola za Kimarekani trilioni 2.2 ya Pato la Taifa (GDP) la dunia (sawa na 10% ya uchumi wa dunia) mwaka 2015 na kutoa ajira kwa zaidi ya watu milioni 108 duniani kote. Kufikia mwaka 2024, Baraza la Dunia la Utalii na Usafiri linatarajia ajira za moja kwa moja kwenye sekta ya utalii kuwa zaidi ya watu milioni 126 duniani kote.

Ukiachana na mchango wa usafiri wa anga kwenye sekta nyingine pia ina umuhimu mkubwa kwenye utalii. Zaidi ya 54% ya watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani husafiri kwa kutumia usafiri wa anga. Jumia Travel inatambua kwamba utalii ni sekta muhimu kwa nchi nyingi za Afrika, ambapo ni nyanja muhimu katika mikakati ya ukuaji wa uchumi.

Barani Afrika, inakadiriwa kwamba takribani watu milioni 5.8 huajiriwa kwenye maeneo ambayo hupokea wageni wengi kutoka nje ya nchi, hususani wanaoingia kwa kutumia usafiri wa anga, na ilichangia dola za Kimarekani bilioni 46 ya Pato la Taifa katika uchumi wa nchi za Kiafrika kwa mwaka 2014.
Utalii kama sekta nyinginezo za huduma inaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuunga mkono ukuaji wa uchumi endelevu. Ikikuzwa kwenye namna ya uwajibikaji na mikakati mizuri, utalii unaweza kuwa na mchango mkubwa katika kutoa ajira huku ikitunza na kuenzi rasilimali zetu bila ya kuziharibu.

Ingawa, kuna umuhimu mkubwa kwa sekta binafsi na serikali kukaa kwa pamoja na kujadiliana. Lengo ni kuhakikisha mipango ya maendeleo ya sekta hii inafanywa kwa kuzingatia utunzwaji wa mazingira, ustawi wa jamii pamoja na faida za kiuchumi inazoweza kuzileta.

Katika serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania ikiwa chini ya uongozi wa Mh. John Pombe Magufuli tumeshuhudia jitihada kubwa katika ukuzaji wa sekta ya usafiri wa anga. Jitihada hizo ni pamoja na manunuzi ya ndege za abiria, upanuzi wa viwanja vya ndege na maboresho kadhaa kwenye wizara husika kwa ujumla.
Hivi karibuni Rais Magufuli akiwa katika ziara yake ya kikazi Kagera alizindua uwanja wa ndege ambao si tu utaongeza fursa za kiuchumi mkoani humo bali pia utaufungua mkoa huo kiutalii. Majengo ya uwanja huo ni ya tatu kwa uzuri baada ya Dar es Salaam na Kilimanjaro.

Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Rais alisema kuwa mbali na uwanja huo wa ndege kukuza na kurahisisha shughuli za kibiashara mkoani humo kama vile usafirishaji wa samaki, ndizi na mazao mengine ya biashara, lakini pia utapelekea watalii kufika kwa urahisi na kutalii vivutio mbalimbali kama vile kwenda Burigi na kujionea wanyama na vivutio vingine vilivyopo huko.
Ukiachana na uzinduzi wa uwanja huo, pia mkoani Geita liliwekwa jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Profesa Makame Mbarawa.

Mbali na ujenzi wa uwanja huo Waziri huyo alibainisha kuwa serikali ina mpango wa kuhakikisha kwamba kila mkoa unakuwa na uwanja wa ndege utakaokuwa unahudumia wananchi wasiopungua 100.

Aliongezea kuwa mbali na ujenzi huo pia imeboresha na kuimarisha ujenzi katika viwanja vya ndege vya Lindi, Iringa, Moshi, na Simiyu. Lengo ni kuviwezesha kusaidia shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo na inatarajia katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha wa 2017/2018 kutenga fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi kwenye viwanja vya ndege vya Iringa, Musoma na Songea.

Kuna jitihada mbalimbali ambazo serikali inaweza kuzifanya katika kukuza na kuimarisha sekta ya utalii. Mbali na serikali nyingi kutumia gharama kubwa kwenye kuzitangaza nchi zao kama sehemu zinazovutia kutembelea, kuna masuala kadhaa yanaweza kukwamisha zoezi hilo. Kwa mfano, serikali zinaweza kuanza kushughulikia muda wa utolewaji wa viza kwa wageni uwe mfupi zaidi, kutazama tozo mbalimbali zinazotozwa kwa watalii wanaoingia au kutoka, lakini pia kwa kujihusisha na mashirikisho kadhaa ya kimataifa katika sekta hii.
Hivyo basi, Jumia Travel inashauri kwamba serikali iwe inafanya tathmini ya mara kwa mara kwenye miundombinu ya viwanja vyao vya ndege ili kuendana na uhitaji wa soko kwa wakati uliopo. Hii itahakikisha kuwa sekta ya usafiri wa anga itaendelea kuunga mkono maendeleo ya sekta ya utalii na kuleta manufaa makubwa ya kiuchumi.

DC NZEGA ASEMA SAYANSI NA TEKNOLOJIA HAIKWEPEKI KATIKA KILIMO

$
0
0

 Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Shila Wilayani Nzega mkoani Tabora wakiwa wamebeba mbegu ya Viazi lishe wakielekea kwenye shamba darasa wakati wa uzinduzi wa shamba hilo wilayani humo leo. Shule hiyo ni shule pekee wilayani humo kupata bahati ya kuanzisha shamba hilo.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa (kulia), akimkabidhi mbegu ya mihogo Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngapula kwa ajili ya kupandwa katika mashamba darasa katika uzinduzi wa mashamba hayo ya mbegu wilayani humo leo. 
 Wanafunzi wa Shule ya Shila wakiwa shambani wakati wa uzinduzi wa shamaba darasa hilo.
 Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza kabla ya kuanza uzinduzi huo uliofanyika katika Wilaya hiyo Shule ya Msingi, Shila.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akielezea ubora wa mbegu ya mihogo iliyofanyiwa utafiti kabla ya uzinduzi wa shamba darasa katika Shule ya Msingi ya Shila.
 Kaimu Ofisa Ugani wa Halmshauri ya Wilaya ya Nzega, Hassan Mtomekela akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akielekeza jinsi ya kupanda mbegu ya mihogo hiyo kiutaalamu.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akimuonesha mbegu hiyo mkuu wa wilaya hiyo.
 Mkuu wa Wilaya hiyo akizindua shamba darasa hilo kwa kupanda mbegu ya mihogo katika Shule ya Msingi ya Shila.
 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Gunguti Awadh Mzee akipanda mbegu hiyo.
 Dada Mkuu wa Shule ya Shilwa, Maria Kulwa akipanda mbegu hiyo.
 Upandaji ukiendelea katika shamba hilo.
 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Gunguti Awadh Mzee, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu bahati iliyopata shule yake kwa kupatiwa mradi huo wa shamba la mbegu.
 Mkulima wa Kijiji cha Shila, Zainabu Kanijo akizungumza na wanahabari.
 Wanawake wa Kikundi cha Wasafi Camp Imala Makoye kilichopo Kijiji cha Iyombo Kata ya Utwigu wakiwa wamebeba mbegu ya Viazi lishe wakielekea kupanda katika shamba darasa.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza wanakikundi hicho jinsi ya kupanda mbegu hiyo.
 Wanawake wa Kikundi cha Wasafi Camp Imala Makoye kilichopo Kijiji cha Iyombo Kata ya Utwigu wakipanda mbegu hiyokatika shamba lao.
 Wanawake wa Kikundi cha Wasafi Camp Imala Makoye kilichopo Kijiji cha Iyombo Kata ya Utwigu wakiimba nyimbo za kabila la kisukuma kufurahi mbegu hiyo.
Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Upungu Kata ya Puge jinsi ya kupanda mbegu ya mihogo

Na Dotto Mwaibale, Nzega Tabora

MKUU wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Godfrey Ngapula amesema Sayansi na Teknolojia haiwezi kuepukika katika kilimo nchini.

Ngapula ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109, mihogo na Viazi lishe kwa ajili ya kuanzisha mashamba darasa katika vijiji vya Shila, Iyombo, Upungu, Lububu na Kapanga wilayani humo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema ili kufanya kilimo chenye tija sayansi na teknolojia haiwezi kuepukika kutokana na changamoto mbalimbali zilizopo.

Alisema kilimo cha kisayansi kina tija kwani mkulima anaweza kulima eneo dogo na kupata mavuno mengi kuliko kilimo cha mazoea ambacho mkulima hulima shamba kubwa mazo kidogo.

Ngapula aliipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuwapelekea mbegu hizo kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) 

Akizungumzia matumizi ya mbegu zilizozalishwa kwa teknolojia  ya uhandisi jeni (GMO) alisema hayakwepeki kwa kuwa mbegu hizo zinasifa ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukame na wadudu waharibifu wa mazao.

Alisema wilaya hiyo kupelekewa mbegu hizo kwao ni fursa kubwa na kwa kushirikiana na wakulima na maofisa ugani atahakikisha mashamba darasa hayo yanatunzwa vizuri na kuwa ndio chanzo za kutoa mbegu nyingi na kuzisambaza katika maeneo mengine.

Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura aliwaambia wakulima hao kuwa hekta moja ya mihogo iwapo watalipa kwa kufuata ushauri wa wataalamu wataweza kupata tani 25 hadi 32 kwa zao la mihogo na viazi lishe watapata tani 7 hadi 9 kwa hekta moja.

Alisema matokeo hayo watayapata endapo watafuata kanuni bora za kilimo cha mazao hayo kwa kuzingatia nafasi kati ya mche na mche na mstari kwa mstari na matumizi ya mbolea hivyo wataweza kuongeza uzalishaji zaidi tofauti na sasa ambapo kwenye hekta moja ya mihogo wanapata tani nane hadi kumi wakati kwenye viazi lishe wanapata tani moja hadi 3.

Mtafiti huyo alisisitiza kuwa mbegu hiyo ya Mihogo ya Mkombozi imefanyiwa utafiti na kuonekana kustahimili magonjwa hatari ya mihogo ya batobato kali na michirizi ya kahawia ambayo imekuwa ikiwapatia hasara kubwa wakulima wengi na kupoteza hadi asilimia 90 za mazao.

Akizungumzia kuhusu mbegu Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, alisema mbegu hizo ya mihogo aina ya Mkombozi imefanyiwa utafiti na kuonekana ina uwezo mkubwa wa kustahimili magonjwa kama ya batobato kali na michirizi ya kahawia ambayo imekuwa ikiwapatia hasara kubwa wakulima na ya mahindi ikistahimili hali ya ukame na kutoa mazao mengi.

Mutagwa aliwaomba wakulima hao kuyatunza mashamba hayo ambayo yamegharimu fedha nyingi hadi kukamilika kwake hivyo wayaendeleze kwa ajili ya kuja kutoa matunda kwa wakulima wa wilaya hiyo na kupata chakula cha kutosha na ziada kuuza.

Aliongeza kuwa kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala mbalimbali ya sayansi na teknolojia na kuhakikisha matokeo ya tafiti zinazofanyika nchini yanawafikia walengwa ambao ni wakulima.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Shila ambayo ni shule pekee iliyopata baada ya kuwa na shamba darasa la mihogo katika wilaya hiyo,  Gunguti Awadh Mzee alisema shamba hilo litakuwa la mfano na kuwa mradi huo utasaidia kuwapatia wanafunzi wake chakula wakiwa shuleni hapo.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images