Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 140 | 141 | (Page 142) | 143 | 144 | .... | 1898 | newer

  0 0  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe wa Taasisi na Ulinzi wa Ikolojia kutoka nchini China, wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Agosti 17, 2013 kwa ajili ya kumkabidhi Tuzo ya Utunzaji wa Mazingira.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe wa Taasisi na Ulinzi wa Ikolojia kutoka nchini China
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Tuzo ya Utunzaji wa Mazingira na Kiongozi wa Ujumbe huo, Dkt. Jiang Ningjun, wakati Ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Agosti 17, 2013 kwa ajili ya kumkabidhi Tuzo hiyo. Kulia ni Xiaoyi Jin. Picha na OMR.

  0 0


  0 0

  Mkuu mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu,Mh Issa Machibya akizungumza machache wakati wa ufunguzi wa Semina ya Fursa kwa vijana zinazopatikana ndani ya mkoa wa Kigoma na kwingineko,mapema leo asubuhi.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group ambao ndio waratibu wa tamasha kubwa la burudani hapa nchini la Fiesta 2013,imehudhuriwa na vijana mbalimbali kutoka kila pembe ya mkoa huo wakiwemo na wasanii mbalimbali maarufu kutoka jijini Dar,ambao wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo jioni ya leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.Aidha katika Semina hiyo ya Fursa,baadhi ya vijana wengi walionekana kuvutiwa kwa kiasi kikubwa kwa yaliyokuwa yakizungumziwa,ikiwemo suala la ujasiliamali.
   Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akimkaribisha mgeni rasmi wa semina hiyo,Mh Issa Machibya mapema leo asubuhi,kwenye ukumbi wa Kibo Peak,uliopo Kigoma mjini,kulia kwake ni msanii mahiri wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto ambae pia likuwa ni mmoja wa watoa mada kuhusiana na suala zima la Fursa.Semina hiyo imewashirikisha wadau mbalimbali,wakiwemo NSSF,Wasanii wa Bongofleva,wakazi  wajasiliamali mbalimbali ndani ya mji wa Kigoma.
   Pichani juu ni baadhi ya Wasanii wa Bongofleva na wadau wengine wakiwemo wakazi wa Kigoma wakisiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo kuhusiana na fursa mbalimbali. 
   Sehemu ya Meza kuu ikishangilia jambo,kutoka kushoto ni Kaimu Meneja wa NSSF mkoani Kigoma,Bwa.Said Abdallah,Mkuu wa Wilaya ya Uvinza ambae alikaimu pia nafasi ya Mkuu wa wilaya ya Kigoma mjini,Mh.Khadija Nyembo,Mkuu wa Mkoa,Mh.Issa Machibya,Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji kutoka  Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,Msanii Mrisho Mpoto (haonekani) pamoja na msanii wa muziki wa kizazi kipya,ajulikanae kwa jina la kisanii AY.
   Baadhi ya Wasanii wa bongofleva ambao wanatarajiwa kutumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,wakitambulishwa kwa wakazi wa Kigoma,wakati wa kuanza kwa semina ya Fursa iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Kibo Peak mjini humo.
   Mkali wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya wakazi mbalimbali wa mji wa kigoma,alipokuwa akiielezea mada mojawapo iliyohusiana na fursa mbalimbali zilizomo ndani ya mji huo na wakazi wake.
  Baadhi akina mama walioshiriki semina hiyo wakijadiliana jambo huku wakinukuu baadhi vipengele vilivyowagusa kwa namna moja ama nyingine.


  Baadhi ya Wasanii wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo,kushoto ni Mwana FA,Sheta,Joe Makini.
    Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza mbele ya umati wa vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye semina ya Fursa,mapema leo asubuhi.Mutahaba aliwafungua vijana wa mji huo kwa kuzichambua mada mbalimbali zilizohusu Fursa ndani ya mkoa wao,ikiwemo nini maana ya fursa,kishindo cha fursa pamoja na mada nyingine iliyohusu Fursa katika kuongeza thamani.
   Baadhi ya vijana mbalimbali kutoka ndani ya mkoa wa Kigoma wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi kwenye ukumbi wa Kibo Peak.
   Kaimu Meneja wa NSSF mkoani Kigoma,Bwa.Said Abdallah akifafanua Fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya shirika la NSSF,zikiwemo za kujiunga na shirika hilo kurahisisha upatikanaji wa mikopo,matibabu na mambo mengine mbalimbali,aidha Bwa,Said amewataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha na shirika la NSSF ambako wanaweza kunufaika na huduma mbalimbali na zenye uhakika.
   Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya na mfanyabiashara,Ambwene Yesaya a.k.a AY akitoa ushuhuda wake na mifano mbalimbali  katika Semina ya Fursa,kuhusiana na fursa alizozipata na kuzifanyia kazi,na kumpelekea mafanikio aliyonayo mpaka sasa,AY amewataka vijana kutokuwa na moyo wa kukata tamaa haraka katika mambo yao wayafanyayo na pia kujali suala la muda katika mambo yao wayanayojishughulisha nayo. 
  Mratibu Mkuu wa Semina ya Fursa,ambaye pia ni Mtangazaji wa Clouds FM,Gerald Hando akitoa utaratibu wa ushiriki kwa wadau mbalimbali waliojitokeza kwa wingi mapema leo asubuhi kwenye ukumbi wa Kibo Peak.Semina hiyo ilioonesha mafanikio makubwa kwa wakazi wa Kigoma,iliwakutanisha Wadau mbalimbali wakiwemo NSSF;Lake Oil,Wasanii wa Bongofleva na wengine wengi . Picha zote na Michuzjr-Kigoma.

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na baadhi ya wakuu wa nchi za SADC muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano wa 33 SADC uliofanyikaKatika ukumbi wa Bingu International Conference centre,mjini Lilongwe Malawi leo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Naibu Waziri Mkuu wa Namibia Marko Hausiku,Makamu wa Rais wa Zambia Dr.Guy Scott,Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma, Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC),Rais Dkt.Jakaya Kikwete,Mwenyeji Rais Dkt.Joyce Banda wa Malawi, Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji,Katibu Mtendaji wa SADC anayemaliza muda wake Dkt.Tomaz Salomao, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, na Rais Ian Khama wa Botswana. Chini Rais Kikwete akiongea na mwenyeji wa mkutano huo Rais Dkt. Joyce Banda wa Malawi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu


  0 0


  0 0


    Msanii mwenye kipaji cha Hali ya juu nchini na Mwenye umri mdogo Elizabeth Michael "LULU"anatarajia kuzindua filamu yake ya Kwanza tokea alipotoka Gerezani, Filamu hii iitwayo FOOLISH AGE ikiwa imetengezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited itazinduliwa Mnamo tarehe 30 August 2013 Katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam. 

  Filamu hiyo inayoelezea Maisha ya LULU ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu kutokana na Kutengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited Katika Uzinduzi huo wa Filamu hiyo ya Lulu Wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi Band anatarajiwa kushusha bonge moja la burudani ya kufa mtu. 

  Kupitia mtandao wa kijamii wa Lulu aliyejaaliwa kuwa na kipaji cha kuigiza na mwenye mvuto mbele ya runinga aliandika "Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu....!!!ninafuraha ya kuwafahamisha kuwa TAREHE 30/8/2013 ndio siku nitakayozindua movie yangu mpya iitwayo FOOLISH AGE....Hatimaye narudi kazini!!!!

  Uzinduzi utafanyika katika ukumbi wa MLIMANI CITY....kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa muziki....na pia LADY JAY DEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo pia!!!nahitaji support ya mashabiki wote wa LULU na mashabiki wa BONGO MOVIE.....♥♥♥♥!!!#PROINPROMOTERS"
  Baada ya uzinduzi wa Filamu hii nakala zitaendelea kuuzwa katika maduka yote ya Filamu nchini na Filamu hii imetengenezwa na itakuwa inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited.

  Usikose uzinduzi Huu utakaofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City tarehe 30 August 2013

  0 0

   Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia kwenye jukwaa la tamasha la Serengeti Fiesta 2013,usiku huu kwenu uwanja wa Lake Tanganyika.
   Sehemu ya umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu wakiburudika na Wasanii wa Serengeti Fiesta 2013
   Burudani ya kutosha kabisa
   Hapatoshi ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu.
   Mwanamuziki mahiri wa muziki wa Dansi,Christian Bella akikamua jukwaani usiku huu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,mkaoni Kigoma ambapo watu wamefurika ile mbaya.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cassim Mganga akiimba jukwaani mbele ya maelfu ya wakazi wa Kigoma ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.
   Sehemu ya umati wa watu waliofurika ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu
   Msaniii anekuja kwa kasi kwenye miondoko ya Hip Hop,Stamina akikamua jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Kigoma waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta
   Ni Shangwe tu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma usiku huu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea
   Yaani hapatoshi kabisa,wakazi wa Kigoma wamecharuka na burudani murua kabisa ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rachael kutoka THT,akionesha umahiri wake wa kutumbuiza jukwaani usiku kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
  Washabiki wa tamasha la Fiesta wakifuatilia kwa makini yanayojiri usiku huu ndani y uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
  Wadau nao wamejitokeza kwa wingi
  Peter Msechu na densa wake wakikamua vilivyo usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
  Pichani ni msanii wa bongofleva akulikanae kwa jina la Shilole na madansa wake wakiwachengua vilivyo wakazi wa Kigoma,waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.

  0 0

  *Ni Baada ya moto kuungunza mitambo  ·      
  *Mtandao ulizimwa kwa saa 16 nchi nzima
  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza, akizungumza na waandishi wa habari, (hawapo pichani) kuhusiana na kurejeshwa kwa huduma za mtandao wa Vodacom baada ya kukosekana kwa saa 16 kufuatia moto kuzuka katika kitovu cha kuendeshea mitambo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifanyika katika hoteli ya Serena. Pamoja nae ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa.
  Dar es Salaam, Agosti 18, 2013: Baada ya kukosekana kwa huduma za mtandao wa Vodacom kwa takribani masaa 16, huduma hizo zimerejeshwa katika hali yake ya kawaida asubuhi  ya Jumamosi ya Agosti 17.
  Akizungumzia tatizo lililosababisha kukosekana kwa huduma za mawasiliano kwa watumiaji wa mtandao huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema chanzo cha kukatika kwa mawasiliano nchi nzima siku ya Ijumaa ni moto uliotokea katika mtambo mkuu wa kuendeshea mtandao (Main Switch) uliyoko Dar es Salaam.

   “Kufuatia hatua hiyo, hatukuwa tena na uwezo wa kutoa huduma kwa watu wote kuanzia siku ya Ijumaa jioni hadi Jumamosi asubuhi, hali hii iliathiri wateja wetu wote kwa ujumla kwani walishindwa kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki ambao wote ni wateja wetu, alisema Meza.

   Aidha, Meza aliomba radhi kwa jamii ya Watanzania na wateja wa Mtandao wa Vodacom kwa kukosa mawasiliano katika kipindi hicho, na kusema kuwa wateja wote wa mtandao wa Vodacom watarudishiwa gharama zote kwa huduma yoyote walionunua na kuhitaji kuitumia wakati ambapo mtandao  haukuwa unapatikana.“Fidia hizi kwa wateja wetu wote zitatolewa siku ya Jumatatu ya Agosti 19, 2013 alisema Meza.

   “Tunaishi katika dunia ambayo mawasiliano ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku hivyo tunaelewa kuwa tatizo hili limekuwa kikwazo kikubwa kwa wateja wetu, Na tunawashukuru kwa kuwa waelewa na wavumilivu katika kipindi chote ambacho tumekuwa tukikabiliana na tatizo hili, alisema Meza.

  Meza alihitimisha kwa kuhakakikishia Watanzania na wateja wa Vodacom kwa ujumla kuwa Vodacom imedhamiria kuendelea kutoa huduma zenye viwango vya hali ya juu nchini.

   “Ninapenda kuwashukuru wafanyakazi wetu wote na washirika wetu ambao kwa pamoja wamefanya kazi bila kuchoka katika kuhakikisha huduma zote zinarejea hadi katika hali ya kawaida hadi kufikia Jumamosi asubuhi, Jitihada zao na kazi kubwa waliyoifanya imewezesha huduma zote kurejea katika hali ya kawaida, alihitimisha Meza.

  0 0

  IMG_2543
  Helikopta maalum iliyowabeba viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh. Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika walipowasili eneo la Mnada Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kufanya mkutano wa hadhara wilayani humo mwishoni mwa Juma. 
  IMG_2579
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh. Freeman Mbowe akihutubia wakazi wa wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza mwishoni mwa juma kwenye mkutano wa hadhara. IMG_2610
  Mwananchi wa Geita ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akitoa maoni yake ya Rasimu ya Katiba Mpya mbele umati wa wafuasi wa Chadema na wakazi wa wilaya hiyo ambapo wengi wao wametaka Ushuru wa Masoko ufutwe pamoja na baadhi ya kinamama kulalamikia shida ya Maji kwenye Wilaya hiyo na Mh.Mbowe aliwaasa kutumia Mabaraza ya CHADEMA kuwasilisha maoni yao wakati wa mkutano wa hadhara.
  IMG_2604
  Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika akiteta jambo na mmoja wa viongozi wa Chadema wilayani Sengerema Hemedi Sabula wakati wa mkutano huo wa hadhara. (Picha na Zainul Mzige wa Dewji Blog).

  Na Mwandishi wetu, Sengerema
  Mwenyekiti wa Chama cha Domekrasia na maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kujadili Rasimu ya Katiba mpya ili ipatikane Katiba itakayokidhi haja ya Watanzania.

  Amesema hayo alipokuwa akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Sengerema mkoani waMwanza alipokuwa kwenye ziara ya kichama kuhamasisha wanachama wa chama hicho kuunga mkono kuwepo na Serikali tatu ndani ya Jumuiya ya Muungano wa Tanzania.

  Amesema kuwepo Serikali tatu siyo mzigo kama kama inavyodaiwa na wengine na kuongeza "tunataka kuwepo serikali ya Tanganyika na Zanzibari na ile ya muungano ili kuleta usawa ndani ya Muungano huo".

  Pia amesema kuwa Lugha ya Kiingereza ipatiwe kipaumbele kufundishwa kuanzia daraja la awali hadi Chuo Kikuu ili kuwajengea Watanzania kufahamu lugha hiyo vyema na kupata ajira kwa urahisi.

  0 0

  Wanamuziki wa Diamond Musica wakiwajibika jukwaani.
    Wanamuziki wa Five Star wakiwajibika stejini.
    Didi Namba wa Diamond Musica akiimba.
    Wanenguaji wa Diamond wakionyesha umahiri wao wa kunengua.
    Ally J wa Five Star akifanya mambo stejini.
    Baadhi ya mashabiki wakiserebuka.
    Mashabiki wakilishana keki kwa upendo.
    Husna Semhando akionyesha umahiri wake wa kunengua.
  BENDI ya Diamond Musica na Five Star Modern Taarab usiku wa kuamkia leo ziliwapagawisha vilivyo mashabiki waliohudhuria katika onyesho la pamoja lililofanyika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live, uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE ISSA MNALLY NA RICHARD BUKOS / GPL).

  0 0


  0 0

  Tatizo la ulanguzi wa mihadarati na madawa ya kulevya limeonekana kuongezeka ncjhini Tanzania na kwenye kipindi cha Live Talk cha  VOA  wamezungumzia tatizo hilo na kufanya mahojiano na waziri Mwakyembe ambaye pia alikanusha taarifa za vyombo vya habari kuwa atatoa orodha ya vigogo wanohusika na biashara hiyo nchini Tanzania.
  Walioshiriki ni mkuu wa kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya nchini Tanzania Godfrey Nzowa , mbunge wa Chadema (viti maalum) mjini magharibi Mariam Msabaha na Meneja wa Trent Recovery nyumba ya kusaidia watu wanaotumia madawa Zanzibar na mtumiaji wa zamani. Abdu Rahman Abdallah. Kusikiliza mahojiano mjadala huo bofya hapa.
  Kusikiliza mahojiano mjadala huo bofya hapa.
  http://www.voaswahili.com/content/article/1731337.html

  0 0

  Major  Highlights
  1.) Kutokana na kutokuwepo na taarifa sahihi kuhusu deni la Taifa kuna umuhimu wa kukutanisha wadau wakuu wanaohusika hususani BOT, HAZINA, Kamati za Bunge na CAG ili kuweza kujua kwa usahihi zaidi ukubwa wa deni hilo.  Vile vile imeamuliwa kuwa Serikali ishauriwe kuunda chombo huru kitakachosimamia deni la taifa.
  2.) Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma haiweki uwazi wa kutangaza umiliki wa mali za viongozi.  Hii inapelekea viongozi kutoweka wazi mali wanazomiliki na ni rahisi mtu kuzushiwa umiliki usio wa ukweli.  Ni vyema Sekretarieti wakafanya utafiti wa umiliki wa mali kwa viongozi wa Umma na kuweka taarifa hizo katika tovuti ya Sekretariati ili kuwawezesha wananchi kuweza kuona mali zinazomilikiwa na viongozi wao; na pale ambapo kiongozi hatakuwa ametoa taarifa ya umiliki huo basi taarifa hiyo itolewe kwa Tume.
  3.) Kwa kuwa leseni za udereva za sasa zinaweza kuweka kumbukumbu za makosa ya usalama barabarani, basi TRA ikishirikiana na  Wizara ya Mambo ya Ndani zihakikishe ya kuwa Askari wa Usalama Barabarani wanatumia utaratibu huu wa kisasa wa kutoa  “notification” na kutoa risiti za malipo za elektroniki.
  4.) Maduhuli ya Serikali sasa yakusanywe kwa kutumia risiti za elektroniki.  Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma yaanze kutumia risiti za eletroniki mara moja ili kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali yanayotokea hivi sasa katika kutumia risiti zinazoandikwa kwa mkono. Pia ofisi za serikali zifanye manunuzi yake kwa wafanyabiashara wanaotumia mashine za kielektroniki.
  5.) “The Proceeds of Crime Act, 1991” ifanyiwe marekebisho na kuweka kifungu kinachomwezesha AG/DPP kuwa na mamlaka ya kuomba mahakama kufungua kesi ya madai (Civil Forfeiture) kwa watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

  0 0

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikane kwa jina la Baba Levo akifunga tamasha la serengeti Fiesta 2013,kwenye uwanja wa Lake Tanganyika usiku wa kumakia leo mkoani Kigoma,na kukusanyika maelfu ya watua.
   Wakazi wa mkoa wa Kigoma jana walijiwekea historia ya pekee kwa kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,lililofanyika jana kwenye uwanja wa Lake Tanganyika,hii ikiwa ni mara ya kwanza tamasha hilo kufanyika mkoani humo,ambao wakazi wake wengi wanaishi kwa kutegemea kilimo.Pichani ni Msanii wa Bongofleva TID a.k.a Mnyama Unyamani akiwatumbuiza wakazi wa Kigoma mapema jana usiku.
   Wakali wengine mahili wa muziki wa Hip hop Bongo,Mwana FA pamoja na AY wakiwarusha vilivyo maelfu ya watazamaji waliojitokeza usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.
   Pichani kulia ni mmoja wa Madj wakali ndani ya Clouds FM,Dj Zero akikamua ngoma mbalimbali kwa ajili ya kuwaburudisha wakazi wa Kigoma,shoto kwake ni Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha XXL,B Dozen akifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri jukwaani-
   Sehemu ya umati mkubwa wa watu waliojotokeza kwenye tamasha la Fiesta 2013.
   Msanii Ommy Dimpo a.k.a Tupogo akiimba wimbo wake mpya wa Tupogo aliomshirikisha mwanamuziiki nguli kutoka nchini Nigeria,J-Martins mbele ya umati mkubwa wa watu (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 2013.
   Wasanii mahiri kutoka kundi la Wanaume Family,Chege na Themba wakilishambulia jukwaa la Fiseta kwa pamoja.
   Sehemu ya umati wa watu.
   Msanii mmojawapo kutoka kundi la Manzese Crew,ajulikanae kwa jina la Madee akiimba wimbo wake wa Nani kaiba pombe yake,huku sehemu ya umati ikishangilia kwa shangwe.
   Sehemu ya umati wa watu ukifuatilia yaliyokuwa yakijiri usiku wa kumakia leo kwenye tamasha la Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,mkoani Kigoma.


  0 0

  DSC_0037
  Meza kuu ya Majaji walioshiriki katika Usaili ya kutafuta Models watakaoshiriki kwenye Ally Rehmtullah 2014 Collection Fashion show kutoka kushoto ni Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja, Ally Hassan, Mrembo na mwigizaji maarufu nchini Wema Sepetu, Mwandaaji wa Onyesho hilo ambaye pia ni Mbunifu wa Mavazi nchini Ally Rehmtullah, Mwanamitindo Jamillah Nyangasa, Sarah Raqey.
  Mbunifu wa mitindo maarufu hapa nchini Ally Rehmtullah amefanya maandalizi ya awali ya fashion show yake itayofanyika Agosti 30,  mwaka huu katika Hoteli ya Serena ambapo zaidi ya wanamitindo 30 wasichana na wavulana watashiriki katika maonyesho hayo kabambe.
  Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi kwenye mahojiano maalum Rehmtullah amesema kwenye onyesho la mwaka huu wasichana watashiriki 20 na wavulana 10 ambao watavaa mavazi mbalimbali yaliotengezwa na kubuniwa na Rehmtullah mwenyewe kwa kuzingatia mila na desturi za Kiafrika.
  Katika mchujo huo majaji watano watashiriki kuchagua warembo wenye mvuto, kujiamini na wenye kuwa na muonekano mzuri kwenye jukwaa ili kuwavutia wageni waalikwa ambao watakuwa ni wabunge, mawaziri na viongozi mbalimbali.
  Rehmtullah alilisitiza mwaka huu kwamba onyesho la mitindo ya mavazi yatafana baada ya kudhamini wa makampuni kadhaa makubwa hapa nchini.
  DSC_0050 
  Pichani juu na chini ni Models wa kike wakipita mbele ya majaji wakati wa Audition ya kutafuta washiriki watakaonyesha mavazi kwenye Onyesho la Mavazi la Ally Rehmtullah 2014 Collection.
  DSC_0049
  DSC_0053
  DSC_0082
  Pichani juu na chini ni Models wa kiume wakipita mbele ya majaji kwa ajili ya kuchaguliwa kushiriki kwenye Ally Rehmtullah 2014 Collection Fashion Show.
  DSC_0080
  DSC_0069
  DSC_0071

  0 0

  Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal akimpongeza Katibu Mtendaji wa SADC Dkt.Stergomena Tax kwa kuchaguliwa kushika wadhifa huo wakati wa mkutano mkuu wa 33 wa viongozi wa nchi za SADC uliofanyika jijini Lilongwe Malawi mwishoni mwa wiki.Wapili kushoto ni Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadik aliyefika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kumlaki Rais na Ujumbe wake. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu. Kwa mapicha zaidi ya mkutano huo BOFYA HAPA

  0 0

  IMG_2735
  Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph Al-Amin asikiliza maoni wakati akiendesha mjadala wa namna ya ku-brand mradi wa Demokrasi na Amani (DEP) kuelekea uchaguzi 2015 kwa Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii 25 nchini zilizohudhuria siku ya kufunga warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na shirika la UNESCO na kufadhiliwa na UNDP.
  IMG_2789
  Meneja wa mradi wa Amani na Demokrasi (DEP ) kutoka UNESCO Courtney Ivins akizungumza na Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii kupata tathmini ya warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa Juma wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
  IMG_2743
  Washiriki wakijadiliana katika makundi mambo mbalimbali ya kuboresha kwenye redio jamii zao katika utekelezaji wa mradi wa DEP kuelekea uchaguzi 2015 wakati wa kuhitimisha warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa Juma.
  IMG_2741
  IMG_2739
  Mkufunzi na Mshauri wa redio za jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo kwa Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph Al-Amin wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja wa redio za jamii katika kuziandaa kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
  IMG_2763
  Msafiri Andrew kutoka Mpanda FM akiwasilisha maoni ya kikundi chake nini kifanyike katika utekelezaji wa mradi wa Demokrasia na Amani kwa redio za jamii kuelekea uchaguzi 2015.
  IMG_2718
  Meneja wa Triple A FM Borry Mbaraka akichangia maoni wakati wa kufunga warsha ya wiki moja kwa Wakurugenzi na Mameneja wa Redio za jamii nchini iliyomalizika mwishoni mwa wiki wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
  IMG_2798
  Meneja Mawasiliano wa Pangani FM Abdullah Mfuruki akichukua matukio mbalimbali ya kumbukumbu wakati wa kuhitimisha warsha warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO na kufadhiliwa na UNDP iliyowakutanisha Mameneja na Wakurugenzi wa radio za jamii 25 nchini kwa ajili ya kuwaandaa kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
  IMG_2714
  Sehemu ya washiriki ambao ni Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha hiyo ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa Juma kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre wilayani Sengerema mkoani Mwanza iliyoandaliwa na shirika la UNESCO na kufadhiliwa na UNDP.
  IMG_2813
  Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre SengeremaFM mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye akitamka kufunga rasmi warsha ya wiki moja kwa redio za jamii katika kutekeleza mradi wa Demokrasia na Amani kuelekea uchaguzi 2015.
  IMG_2823
  Mshauri wa Redio za Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu akigana na Meneja wa Mradi wa DEP kutoka UNESCO Courtney Ivins mara baada ya kuhitimisha warsha ya wiki moja iliyokuwa ikifanyika kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza mwishoni Juma.
  IMG_2825
  Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii nchini kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji mara baada ya kumalizika kwa warsha ya wiki moja kwa ajili ya kuwaanda redio za jamii kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasi kuelekea uchaguzi 2015 iliyoandaliwa na shirika la UNESCO na kufadhiliwa na UNDP.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi akikagua gwaride la Kikundi cha Kukabiliana na Uhalifu kwa Haraka (Rapid Response Team) kilichohitimu mafunzo yao katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mwishoni mwa wiki.
  Wahitimu wa RRT wakiapa Kiapo cha Utii mbele ya Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi.
  Wahifadhi wakifuatilia kwa makini zoezi la uhitimishwaji wa mafunzo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha Dk. Christopher Timbuka, John Shemnkunde, Mtango Mtahiko na Godwell Meing’ataki.
  Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA Martin Loibooki akisoma maelezo kuhusu mafunzo hayo kwa mgeni rasmi.
  Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi akiongea na wahitimu.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


older | 1 | .... | 140 | 141 | (Page 142) | 143 | 144 | .... | 1898 | newer