Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

KATIBU MKUU KITILA AZINDUA JUKWAA LA WADAU WA MAJI ARUSHA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara  ya Maji na Umwagiliaji , Profesa Kitila Mkumbo,Akizindua Jukwaa la wadau kuhusu usimamizi na utunzani wa maji katika Bonde la Pangani jijini Arusha juzi(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)

Mwenyekiti wa Jukwaa Jukwaa la wadau kuhusu usimamizi na utunzani wa maji katika Bonde la Pangani Mhandisi Mbogo Futakamba, alisema pamoja na vyanzo vingi vya maji vilivyopo nchini, lakini kuna changamoto katika matumizi kwa maendeleo ya kiuchumi.


Mhandisi wa Maji Mkoa wa Arusha, Joseph Makaidi, alisema, baadhi ya maeneo hali ya upatikanaji wa maji ni nzuri ikilinganishwa na maeneo mengine.

 Afisa Maji kutoka Bonde la Pangani, Mtoi Kanyawanah,akizungumza na vyombo vya habari 
Baadhi ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja


Na Pamela Mollel,Arusha

WIZARA ya Maji na Umwagiliaji, imeweka mkazo katika utunzaji wa maeneo ya vyanzo vya maji huku ikitaka wadau wa maji kushirikishwa kikamilifu katika mipango ya uanzishwaji wa viwanda.
 
Aidha imetaka sekta binafsi kushirikishwa katika usimamizi wa raslimali maji kwa kutoa elimu kwa wananchi kutovamia vyanzo vya maji huku ikiwataka waliovamia watoke.
 
Akizindua Jukwaa la wadau kuhusu usimamizi na utunzani wa maji katika Bonde la Pangani jijini hapa jana, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Kitila Mkumbo, alisema, maji ni injini ya uchumi.
 
 “Maji yanachangia ukuaji wa kila sekta, bila maji kwa mfano, hakuna viwanda, kilimo, ufugaji wala huduma zingine za kijamii.“Maji ni injini ya uchumi, lakini kwa bahati mbaya maji yamepungua wakati matumizi yake yakiongezeka kila siku,” alisema.Akizungumzia hali ya maji nchini, alisema ina sura mbili, moja ni nchi yenye vyanzo vingi vya maji, wakati sura ya pili ni nchi inayokabiliwa na uhaba wa maji.
 
“Upungufu huu unatufanya kuona ulazima wa kutunza vyanzo vya maji vilivyopo kwa kushirikisha wadau na kutoa elimu kwa wananchi ili wasiendelee kuvamia maeneo ya vyanzo vya maji,” alisema na kuongeza, “waliovamia vyanzo hiyo watoke.”
 
 Alisema kutokana na ongezeko la changamoto kuhusu usimamizi wa raslimali maji, anaamini sekta binafsi ambayo inategemea na kunufaika na matumizi ya maji ina jukumu kubwa la kufanya katika kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Mhandisi Mbogo Futakamba, alisema pamoja na vyanzo vingi vya maji vilivyopo nchini, lakini kuna changamoto katika matumizi kwa maendeleo ya kiuchumi.
 
Alisema kwa mfano, katika suala la uanzishaji wa miradi na viwanda ni lazima kupanga kwa pamoja wakianzia na suala la maji.
“Tukianza na maji tutapata viwanda, mifugo, kilimo na huduma za kijamii,” alisema.
 
Akizungumzia hali ya maji mkoani Arusha, Mhandisi wa Maji Mkoa, Joseph Makaidi, alisema, baadhi ya maeneo hali ya upatikanaji wa maji ni nzuri ikilinganishwa na maeneo mengine.Alisema maeneo ya vijijini yanapata maji safi kwa asilimia 60.25 ingawa hayajatibiwa wakati maeneo ya mijini yanapata kwa asilimia 40.
 
Hata hivyo, alisema kuna tatizo la upatikanaji wa maji safi na kwa baadhi ya maeneo hususan, Arumeru kutokana na wingi wa madini ya 
 fluoride katika maji.Afisa Maji kutoka Bonde la Pangani, Mtoi Kanyawanah, alisema, inategemea na mvua inavyonyesha kwa mwaka.
 
Alisema kama kuna mvua nzuri kwa mwaka upatikanaji wa maji katika Bwawa la Nyumba ya Mungu na Hale na maeneo mengine unakuwa mzuri.
Kwa ujumla, “hali ya maji siyo nzuri wala siyo mbaya, na hii inategemeana na unyeshaji wa mvua.”
 
Pamoja na wadau wengine, uzinduzi wa jukwaa hilo ulishirikisha wawakilishi kutoka taasisi za International Water Stewardship Programme (IWaSP), Ukaid na GIZ.
MWISHO


SERIKALI KUCHUKUA RANCHI ZISIZOENDELEZWA.

$
0
0


 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akilakiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga (DAS) Joseph Sura wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani humo
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga Rashid Gembe 
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akisalimiana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Mkinga (OCD) kushoto ni Katibu Tawala wa Mkinga,Joseph Sura
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili wilayani Mkinga
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega kulia akimsikiliza kwa umakini Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga (DAS) Joseph Sura kushoto wakati akisoma taarifa ya wilaya hiyo
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo kabla ya kuanza ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali wilayani humo

 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akiagana na na Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga (DAS) Joseph Sura kulia mara baada ya kusaini kitabu cha wageni na kupata taarifa ya wilaya hiyo
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akilakiwa na Diwani wa Kata ya Mwakijembe.
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega katikati akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga Rashid Gembe kulia ni Diwani wa Kata ya Mwakijembe
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega katikati akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga,Rashid Gembe
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akizungumza na Jamii wa Wafugaji wa Kimasai na wakulima katika Kijiji cha Perani ambapo aliwataka kuishi kwa amani kwa kufuata taratibu ili kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji 

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega amesema serikali itazirejesha ranchi zote zilizobinafsishwa na kushindwa kuziendeleza.
Amesema ranchi hizo zitagawiwa kwa wafugaji ili kufunguza tatizo la malisho nchini jambo.

Kauli ya Naibu Waziri huyo aliitoa wilayani hapa wakati wa ziara yake ya siku moja ambapo alisema kwamba lengo la kuchukua ranchi hizo ni kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji ambao kwa mara kadhaa wamekuwa wakigombania maeneo ya ardhi kwa ajili ya malisho na kilimo.

Alisema kwamba serikali imeamua kuchukua uamuzi huo ili kuepusha wafugaji waishio mipakani wasipeleke mifugo yao katika nchi jirani ambako kuna malisho.Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

AZANIA BANK YASAIDIA KATIKA ZOEZI LA UTOAJI WA ELIMU NA UCHUNGUZI WA SARATANI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA KCMC,MKOANI KILIMANJARO.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Giliard Masenga (Mwenye miwani) akiwaongoza Maafisa wa Benki ya Azania waliofika katika Hosptali hiyo kwa ajili ya kukabidhi msaada katika Juma la utoaji elimu ya Saratani.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe akikabidhi msaada wa vinywaji baridi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Giliard Masenga kwa ajili ya wiki ya utoaji elimu ya Elimu juu ya ugonjwa wa Saratani pamoja na uchunguzi.wengine kulia ni ,Mkuu wa Kitengo cha Saratani katika Hospitali hiyo,Dkt Furaha Silventi na Afisa Mipango-KCMC,Kiula Kiula na kushoto ni Maafisa waandamizi Benki ya Azania kanda ya Kaskazin, Ali Duru na Caroline Mugendi . 
Sehemu ya Msaada wa vinywaji baridi uliotolewa na Benki ya Azania .
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Dkt ,Giliard Masenga akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Kitengo cha Saratani- KCMC Dkt Furaha Silventi.
Maofisa Waandamizi wa Benki ya Azania kanda ya Kaskazini na Viongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC wakiwa katika picha ya pamoja bara baada ya kukabidhiwa msaada wa vinywaji baridi.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Giliard Masenga akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo.
Mkuu wa Kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Furaha Silventi akizungumza jambo na Meneja wa Benki ya Azania tawi la Moshi.Hajira Mmambe.
Baadhi ya washiriki wa Semina inayoendelea katika ukumbi mdogo wa kitengo cha Saratani inayohusu utoaji wa elimu juu ya Saratani .
Meneja wa Azania Bank ,tawi la Moshi ,Hajira Mmambe akizungungumza na washiriki wa Semina hiyo mara baada ya kuhitimisha zoezi la kutoa msaada.
Maafisa waandamizi wa Benki ya Azania kanda ya Kaskazini wakitembelea maeneo mbalimbali ya kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Na Dixo Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

NAIBU WAZIRI ATIMUA WANANCHI WALIOVAMIA HIFADHI YA KATAVI, AAGIZA WATUMISHI WALIOPIMA VIWANJA NDANI YA ENEO LA HIFADHI WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA

$
0
0

Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (kushoto) akipokea taarifa ya Serikali ya Mkoa wa Katavi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo Mej. Jen. Mst. Rafael Muhuga baada ya kusomwa mbele yake jana alipotembelea mkoa huo kwa ajili ya kutatua migogoro ya hifadhi na wananchi.

NA HAMZA TEMBA -WMU-KATAVI
..............................................................
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga, amewataka  wananchi wa Kitongoji cha Situbwike ambao wamevamia Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kuanzisha shughuli za kibinadamu kinyume cha sheria waondoke kwa hiari ndani ya wiki mbili zijazo kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Naibu Waziri Hasunga amesema hayo jana katika Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi baada ya kutembelea kitongoji hicho chenye kaya zaidi ya 82 ndani ya hifadhi hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutatua migogoro kwenye maeneo ya hifadhi nchini.

"Naagiza, mamlaka husika muhakikishe wananchi hawa wanahama ndani ya wiki mbili zijazo, lazima sheria ziheshimiwe, ifikapo tarehe 10 Novemba, hatutaki tukute mtu hapa, atakayekaidi kitakachompata asitulaumu" aliagiza Naibu Waziri Hasunga.

Kwa upande wa wananchi wa kitongoji hicho ambao wamevamia hifadhi hiyo na kuanzisha shughuli za kilimo, makazi na ufugaji walikiri kuwa wapo ndani ya hifadhi na kwamba walipewa eneo hilo bila ya wao kujua na uongozi wa kijiji cha Stalike ambao kwa sasa haupo madarakani.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga alisema Serikali ya Wilaya hiyo ilitoa notisi ya siku 30 kwa wananchi hao waondoke jambo ambalo halijatekelezwa huku taarifa zikieleza kuwa baadhi yao wamekaidi kuondoka kwa madai kuwa mpaka waone polisi ndio watakusanya virago vyao.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Hasunga ameuagiza uongozi wa TANAPA kuendelea na zoezi la uwekaji wa vigingi vya mpaka katika eneo hilo la hifadhi lenye mgogoro ikiwa ni pamoja na kupima umbali wa mita 500 kutoka kwenye mpaka huo na kuweka mabango yanayoonyesha kuwa eneo hilo haliruhusiwi kwa shughuli za kibinadamu kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Mwailwa Pangani kuwatafuta maafisa ardhi waliohusika kuwapimia wananchi wa kitongoji cha Mgolokani eneo la makazi ndani ya hifadhi ya msitu wa Msanginya kinyume cha sheria.

"Nakuagiza Mkurugenzi wa halmashauri, wale wote waliopima eneo hili ndani ya hifadhi hii watafutwe wahojiwe, labda walikuwa na sababu, wakikutwa na makosa wachukuliwe hatua stahiki za kisheria, hawa wanapaswa kuwajibika" alisema Naibu Waziri Hasunga.

Aidha, alimuagiza mkurugenzi huyo kutafuta maeneo kwa ajili ya kuwagawia wananchi waliondolewa katika hifadhi hiyo ya msitu pamoja na wale walioondolewa hifadhi ya taifa ya Katavi waweze kuanzisha makazi mapya, kilimo na ufugaji.

Mwisho alitoa wito kwa watumishi wa Serikali, taasisi na mamlaka zote za Serikali kufanya kazi kwa ushirikiano kuepuka migogoro isiyo ya lazima inayosababishwa na mkanganyiko wa maamuzji baina ya viongozi wa Serikali.
Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mej. Jen. Mst. Rafael Muhuga (kulia) alipotembelea mkoa huo jana kwa ajili ya kutatua migogoro ya hifadhi.
Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga akizungumza katika kikao na Mkuu wa Mkoa wa Katavi alipotembelea mkoa huo jana kwa ajili ya kutatua migogoro ya hifadhi.
Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mej. Jen. Mst. Rafael Muhuga, Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Katavi na viongozi wa watumishi wa TANAPA,TFS na TAWA. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (kushoto) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mej. Jen. Mst. Rafael Muhuga (kulia) baada ya mazungumzo mafupi ofisini kwake alipotembelea mkoa huo jana kwa ajili ya kutatua migogoro ya hifadhi.
Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (kulia) akikagua eneo lililovamiwa na wananchi wa Kitongoji cha Situbwike na kuanzisha makazi na shughuli za kilimo na ufugaji ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi,  aliagiza wananchi hao kuondoka kwa hiari ndani ya siku 14 kabla ya kuondolewa kwa nguvu alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Katavi. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Stalike, Adam Chala.
Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (wa nne kushoto) akikagua moja ya kigingi cha mpaka kilichovunjwa na wananchi wa Kitongoji cha Situbwike ambao wamevamia Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kuanzisha makazi na shughuli za kilimo na ufugaji, aliagiza wananchi hao kuondoka kwa hiari ndani ya siku 14 kabla ya kuondolewa kwa nguvu alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Katavi. Kulia na Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Martin Loibooki.
Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Situbwike ambao wamevamia hifadhi ya Taifa ya Katavi na kuanzisha makazi na shughuli za kilimo na ufugaji kinyume cha sheria wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (hayupo pichani) wakati akiwapa maelekezo ya kuondoka hifadhini hapo kwa hiari ndani siku 14 zijazo kabla ya kuondolewa kwa nguvu alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Katavi.

Baadhi ya nyumba za makazi zilizojengwa ndani ya hifadhi ya Taifa ya Katavi kinyume cha sheria. Akiwa Mkoani Katavi jana, Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga ameagiza wananchi waliovamia hifadhi hiyo wahamishe makazi yao kwa hiari ndani ya wiki mbili zijazo kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

PPF YAWAPIGA MSASA WADAU WAKE MKOANI TANGA

$
0
0

 Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki Joseph Fungo akizu ngumza na wadau  wa Mfuko wa PPF Mkoa wa Tanga kwenye ukumbi wa Chuo cha Veta Jijini Tanga.

 Mmoja kati ya wadau walioshiriki kwenye semina akiuliza swali
  Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki Joseph Fungo akizu ngumza na wadau  wa Mfuko wa PPF Mkoa wa Tanga kwenye ukumbi wa Chuo cha Veta Jijini Tanga.
 Afisa Mwendeshaji wa wa Mfuko wa PPF Mkoa wa Tanga,Ally Amanzi akisisitiza jambo kwenye semina hiyo
 Mmoja wa washirki katika semina hiyo akiuliza swali kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko huo
 Mmoja wa washirki katika semina hiyo akiuliza swali kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko huo
 Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki Joseph Fungo akizu ngumza na wadau  wa Mfuko wa PPF Mkoa wa Tanga kwenye ukumbi wa Chuo cha Veta Jijini Tanga.
 Sehemu ya washiriki katika semina hiyo wakifuatilia
 Mmoja wa washirki katika semina hiyo akiuliza swali kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko huo
Afisa Mwendeshaji wa Mfuko wa PPF Mkoa wa Morogoro,Edward Kyungu
 Afisa Mwendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga,Jabiri Bundile
 Afisa Mwendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga,Jabiri Bundile kulia akiwa na baadhi ya maafisa wa mfuko huo .Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

DKT MWANJELWA ATUA ARUSHA KUFUNGUA MKUTANO WA TFA KESHO

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro mara baada ya kuwasilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mwingine ni Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza kwa makini maelezo ya hali ya Upatikanaji wa Chakula kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro mara baada ya kuwasilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akijadili jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro wakati akiondoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mwingine ni Katibu Tawala Msaidizi Huduma za Rasilimali watu (Utawala) wa Mkoa wa Arusha.

Na Mathias Canal, Arusha

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) leo Octoba 27, 2017 aewasili Mkoani Arusha Kwa Ziara ya kikazi ambapo kesho Octoba 28, 2017 atafungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA).

Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha utahudhuriwa na viongozi mbalimbali huku ukitaraji kuhudhuriwa na Wanachama wa Tanganyika Farmers’ Association (TFA).

Pamoja na mambo mengine mkutano huo utabainisha vyema kazi na Huduma zinazotolewa na TFA ambazo ni kuuza Zana bora za kilimo, Pembejeo za kilimo kama Mbolea, Mbegu bora, Viuwatilifu mbalimbali pamoja na kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa Wakulima, kama juhudi ya kumpunguzia mkulima karaha ya upataji wa huduma hizo,

TFA ni mojawapo ya Taasisi kongwe na muhimu kwenye maendeleo ya Sekta ya Kilimo nchini Tanzania na imekuwa ikihudumia Sekta hiyo kwa miaka zaidi ya 80 sasa, tangu ilipoanzishwa mnamo mwaka 1935.

Aidha, Kampuni ya TFA imekuwa ikifanya kazi na Serikali kwa njia ya kutoa huduma kubwa kwa Wakulima wote nchini pale ambapo TFA ina matawi ambayo husambaza na kuwafikishia Wakulima, pembejeo za kilimo zenye ubora wa hali ya juu, kwa wakati na kwa bei nafuu.

Kamati ya Bunge yatua Rock City Mall, kuna jambo imelibaini

$
0
0
Kamati ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa leo imefanya ziara katika jengo la kitega uchumi la Rock City Mall ili kujionea utekelezaji wa mradi huo mkubwa Kanda ya Ziwa.

Na Binagi Media Group
Halmashauri za Jiji la Mwanza pamoja na Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, zimeendelea na mazungumzo ya namna ya kugawana mrahada wa mradi wa kitega uchumi cha Rock City Mall, baada ya ujenzi wa mradi huo kukamilika.


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga ameyasema hayo leo mbele ya kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na serikali za mitaa iliyofanya ziara ya kutembelea mradi huo pamoja na miradi ya barabaraba Jijini Mwanza.


Awali kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Jasson Rweikiza ilipongeza ujenzi wa mradi huo, ingawa imesikitishwa ujenzi huo kutowekewa jiwe la msingi wala jengo kuzinduliwa baada ya kukamilika huku wajumbe wengine wakihoji namna mgawanyo wa mrahaba baina ya wabia wa mradi huo ulivyo.


Itakumbukwa kwamba ujenzi wa mradi huo ulianza mwezi Agosti mwaka 2012 baina ya wabia wawili ambao ni mfuko wa pensheni wa LAPF uliyochangia bilioni 74.4 na halmashauri ya Jiji la Mwanza iliyotoa ardhi yenye thamani ya shilingi bilioni 6.16 kabla ya mwaka 2013 Jiji hilo kugawanywa na kuzaliwa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ulipo mradi huo na hivyo kufanya hadi mradi kukamilika mwezi disemba 2015 wabia kuwa watatu.


Aidha gharama za mradi huo hadi kukamilika kwake ilipaswa kuwa shilingi bilioni 74.4 lakini kutokana na ongezeko la gharama mbalimbali za ujenzi, ujenzi huo uligharibu shilingi bilioni 80.56 huku makubaliano ya mrahaba wa LAPF kuchukua asilimia 60 ya mapato ukiongezeka hadi asilimia 90.


Hatua hiyo ilipelekea mrahaba wa mapato wa asilimia 40 zilizokuwa zikigawanywa kwa halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela kushuka hadi asilimia 10 hatua ambayo inazirejesha halmashauri hizo kwenye mazungumzo ya namna ya kugawana mrahama huo kwani awali kila halmashauri ilikuwa ikichukua asilimia 20.


Annette Shaoo ambaye ni Meneja wa kampuni ya Mwanza City Commercial Complex Company Limited (MCCCCL) inayosimamia mradi huo, amesema mwezi septemba mwaka huu makusanyo ya kodi yalifikia bilioni 2.9 kwa mwaka na kwamba matarajio ni kufikia bilioni 4.2 kwa mwaka jengo likijaa wapangaji, ingawa kuna changamoto kwa baadhi ya wapangaji kushindwa kulipa kodi ya pango na hatua zimekuwa zikichukuliwa dhidi yao.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa LAPF, Mwanasheria wa mfuo huo Fidelis Mutakyamilwa amesema mapendekezo yaliyotolewa na kamati hiyo ikiwemo kuboresha uendeshaji wa mradi huo yatafanyiwa kazi ili kuvutia zaidi wawekezaji.


Katika kutamatisha ziara hiyo, pia kamati imekagua ujenzi wa barabara ya Tilapia yenye urefu wa mita 600, Uzinza Rufiji mita 167, Isamilo mita 800 ambapo barabara zote zimejengwa kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa daraja la Msuka Kilimahewa.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza (kushoto) akizungumza wakati kamati yake ilipotembelea mradi wa Rock City Mall. Kulia ni mwanasheria wa mfuko wa pensheni wa LAPF, Adelis Mutakyamilwa
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza (kulia) pamoja na Katibu wa kamati hiyo Chacha Nyakega (kushoto)
Mwanasheria wa mfuko wa pensheni wa LAPF, Adelis Mutakyamilwa akifuatilia mjadala wa kamati hiyo
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mwanne Mchemba akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mjumbe wa kamati hiyo, Venance Mwamoto akizungumza baada ya kutembelea mradi wa Rock City Mall
Mjumbe wa kamati hiyo, Zacharia Issaay akizungumza baada ya kutembelea mradi wa Rock City Mall
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga akizungumza kwenye majadiliano hayo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga (kushoto), Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza (katikati) pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ziara hiyo

KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA ARDHI APOKELEWA KWA SHANGWE

$
0
0
1
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika (Kushoto) akipokelewa na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Ardhi mara baada ya kuapishwa na kuwasili katika ofisi zilizopo kanda ya Dar es salaam.2
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika (Kulia) akipokelewa na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Ardhi mara baada ya kuapishwa na kuwasili katika ofisi zilizopo kanda ya Dar es salaam.
3
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimpokea kwa shangwe Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara ya Ardhi zilizopo kanda ya Dar es salaam.
4
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika (Kulia) akiwa na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Moses M. Kusiluka wakati akiongea jinsi alivyojipanga kufanya kazi na watumishi wa Wizara ya Ardhi mara baada ya kuapishwa na kuwasili katika ofisi zilizopo kanda ya Dar es salaam.5
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika wakati akiongea nao baada ya kuapishwa na kuwasili katika ofisi za Wizara ya Ardhi zilizopo kanda ya Dar es salaam.

TANGAZO LA MAJINA KATIKA UHAKIKI WA MAJINA YA VIWANJA MANISPAA YA KIGAMBONI

RISE CHARITY YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUJIFUNZIA MOROGORO

$
0
0
Shirika lisilo la kiserikali la Rise charity limezindua kampeni iitwayo Mtoto kwanza Elimu ni Msingi Ambapo kampeni hiyo yenye dhumuni la kusaidia watoto wa shule za msingi kwa kuwachangia vifaa mbalimbali vitakavyo wawezesha katika Masomo . 
Kampeni hiyo imezinduliwa kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Morogoro wilaya ya kilosa kijiji cha Ngoisani ndani ya shule ya Mabwegere ikiwa ni kampeni inayotarajiwa kuzunguka katika mikoa mbalimbali Tanzania. 
Aidha wakati wa uzinduzi huo ulioambatana na kutoa msaada wa vifaa vya kujifunzia Katibu wa kampeni hiyo Atley Timothy Kayuni amewaasa watoto kwa kusema.
"Msaada huu umetolewa na watanzania na wapenda maendeleo hivyo muutumie vizuri na kwamanufaa ya upataji elimu bora ambayo itawasaidia mbeleni katika maisha hivyo mkazane ili kutimiza ndoto zenu" amesema Kayuni.
Naye Mmoja wa walimu katika shule hiyo Mwl. Mbapila amelishukuru shirika hilo kwa kuwakumbuka na kwenda kuwaona na kusema ni watu wachache sana wenyemoyo wa kujitolea hivyo wasichoke kutoa kwani shule ni nyingi na nyingi zinahari mbaya hususani vijijini.
 Katibu wa kampeni ya "mtoto kwanza elimu ni msingi" Atley T Kayuni akitoa somo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mabwegere iliyopo Kilosa Mkoani Morogoro kabla yakutoa msaada kwa wanafunzi hao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Rise Media, Innocent Horomo akitoa msaada wa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi, ikiwa ni kampeni inayoendeshwa na Rise Charity iliyofanyika katika shule ya shule ya Mabwegere wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
 Afisa habari wa Rise Media ambae pia ni mwakilishi wa Rise Charity akiteta jambo na wanafunzi wa shule ya msingi mabwegere wakati wa zoezi la uzinduzi wa kampeni ya Mtoto kwanza elimu ni msingi
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mabwegele wakiwa darasani wakati wa zoezi la kampeni ya Mtoto kwanza elimu ni msingi.
 Mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mabwegere akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Rise Charity kwa kuwakumbuka na kuwapa msaada
Wanafunzi wakifurahia msaada waliopewa kwa kunyosha juu vifaa vya kujifunzia 

DKT MWANJELWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TFA JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Mgeni Rasmi- Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha. Picha zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akishiriki sala ya kumuombea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Wanachama wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA) wakifatilia Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha, leo Octoba 28, 2017.
  Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro akitoa salamu za Mkoa muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb)kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Mkazi wa Moshi Mkoani Kilimanjaro ambaye ni Mwanachama wa TFA Shekh Ally Mwamba akiongoza wanachama wa TFA kumuombea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Katibu wa Kampuni ya TFA na Ofisi ya kisheria Bi Pendo Jacob mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA), Mwingine ni Bi Cathy Elizabeth S. Long'lway. leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza maelezo kuhusu Kazi za TFA banda la TFA mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA), Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TFA Ndg Peter Ezrah Sirikikwa, na kushoto kwake ni Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro. leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Mwanachama wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA) Bi Mwanahamisi Salim Bakari akitoa shukrani zake kwa Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha, leo Octoba 28, 2017.

Picha ya pamoja Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb), Mwenyekiti wa TFA Ndg Peter Ezrah Sirikikwa, Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro na viongozi wengine wa TFA mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha, leo Octoba 28, 2017. 
Na Mathias Canal, Arusha

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) leo Octoba 28, 2017 amekipongeza Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA) kwa kuendelea kufungua matawi mengi nchini ya kuuza pembejeo bora za kilimo.

Mhe Mwanjelwa ametoa pongezi hizo wakati akihutubia kwenye Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Tanganyika Farmers’ association (TFA) uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha.

Alisema kuwa hiyo ni ishara njema ya kuunga mkono Ilani ya Chama cha Mapinduzi na juhudi za Serikali katika kuendeleza Sekta za kiuchumi ambazo ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Alisema kuwa Kwa wajibu huo, Wizara ya kilimo imeona juhudi kubwa na za makusudi za  Kampuni ya TFA jinsi ilivyojipanga katika kuwahudumia Wananchi na Wakulima nchini.

Kupitia Mkutano huo Aliwaomba Wananchi wote kuendelea kuiunga mkono Kampuni ya TFA ili waweze kupata maendeleo ya haraka kwa kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo ili kuondokana na kilimo cha mazoea na kuingia katika kilimo cha kisasa.

Mheshimiwa Dkt Mwanjelwa alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imetoa msukumo mkubwa katika  kuendeleza Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na hasa kwa kuzingatia kuwa nchi imeaanza safari ya kuelekea kwenye uchumi wa Viwanda ambao unazitegemea Sekta hizo kama chanzo cha malighafi kwa ajili ya kuziongeza thamani bidhaa lakini pia kuzisindika kwa ajili ya biashara katika soko la ndani na nje.

Alitoa Rai kwa Wananchi wote na Wanachama wa TFA kutumia vizuri mtandao wa Mawakala wa TFA, kwani inalenga kumuondolea Mkulima matatizo ya upatikanaji na matumizi ya pembejeo hafifu za kilimo.

Alisema hiyo ndiyo ishara ya kuifanya TFA iweze kuendelea kutoa huduma zake kwa kipindi chote cha zaidi ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.

“Nichukue fursa hii nafasi hii kuwakumbusha wanachama wa TFA na Wananchi kwa ujumla kuwa, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amedhamiria kuendeleza Viwanda vilivyopo hapa nchini, na kuanziasha vipya, nanyi kama Wabia, Wadau wa Wakulima katika kuchangia maendeleo ya viwanda hivyo, natoa rai kwenu kuendelea kukithamini kilimo kwa kuongeza tija na uzalishaji, ili viwanda vilivyopo na vitakavyoanzishwa viweze kupata malighafi na rasilimali zakutosha na hatimaye tufikie kwenye uchumi wa kati” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa

Mhe Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa alisema kuwa Wizara ya Kilimo imeamua kuweka utaratibu wa kununua mbolea hapa nchini kupitia Mfumo wa Ununuaji wa Pamoja ya “Bulk Procurement System - BPS” na wakati huohuo kuanzisha Mfumo wa Kuuza Mbolea kwa bei Elekezi, ambapo kwa sehemu kubwa ya nchi mbolea imeshuka kwa zaidi ya asilimia 30.

Mfumo huo unalenga kupunguza kero ya upatikanaji na ulanguzi katika bei za mbolea. Kupitia mfumo huo, Serikali inaamini matumizi ya mbolea hapa nchini yataongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka iliyopita, na kuwa na ongezeko kubwa la uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Huduma zinazotolewa na TFA ni kuuza Zana bora za kilimo, Pembejeo za kilimo kama Mbolea, Mbegu bora, Viuwatilifu mbalimbali pamoja na kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa Wakulima, kama juhudi ya kumpunguzia mkulima, mmekuwa mkiagiza baadhi ya pembejeo toka nje ya nchi kwa kuzingatia sheria na taratibu zote.  Nawapongeza kwa jinsi mlivyojipanga vema katika kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi wa hali ya juu ili kuleta mabadiliko makubwa katika Sekta ya Kilimo.

Katika Mkutano huo hoja mbalimbali zimeibuka kutoka kwa wanachama ikiwemo Ongezeko la gharama za mahindi katika Mkoa wa Njombe hoja ambayo Mhe Naibu Waziri ameahidi kuzuru Mkoani Mbeya kufatilia jambo hilo.

Aidha, Baadhi ya wanachama wamempongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kufuta

Jumla ya tozo 80 ambapo kati ya tozo 139 zimefutwa na tozo nne (4) zimepunguzwa viwango. Tozo, kodi na ada zinajumuisha  kufutwa kwa tozo kumi (10) na mbili (2) kupunguza viwango kwenye zao la tumbaku.  Kwenye zao la kahawa zimefutwa tozo 17 na moja (1) kupunguzwa kiwango; sukari zimefutwa 16; pamba tozo zilizofutwa ni mbili (2); kwenye korosho tozo mbili zimefutwa na chai imefutwa tozo moja (1).

Katika kuongeza upatikanaji wa pembejeo tozo tatu (3) zimefutwa na moja (1) imepunguzwa kiwango kwenye mbolea na  tozo saba (7) zilizokuwa kwenye mbegu nazo zimefutwa. Katika Ushirika jumla ya tozo 20 zimefutwa katika ngazi mbalimbali.



MWISHO.

NAIBU WAZIRI AWESO AWATAKA WAKAZI WA PANGANI KUWA NA MSHIKAMANO ILI KUPATA MAENDELEO.

$
0
0

 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Pangani kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika uwanja wa sokoni ambapo alisisitiza umoja na mshikamano kwa wananchi ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo 
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani akizungumza katika mkutano huo
 Mkuu wa wilaya ya Pangani.Zainabu Issa akizungumza katika mkutano huo ambapo alimuomba Naibu Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo kuiwekea msukumo barabara ya Tanga-Pangani ili kufungua fursa za kiuchumi kwa wilaya hiyo
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya PanganiSeif Saidi akizungumza katika mkutano huo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani,Sabas Chamnbasi akizungumza katika mkutano huo
 Diwani wa Kata ya Pangani Magharibi (CCM) John Semkande akizungumza katika mkutano huo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akilakiwa na wananchi wa Jimbo la Pangani wakati alipokwenda kuhutubia wananchi wa wilaya ya Panganikwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika uwanja wa sokoni ambapo alisisitiza umoja na mshikamano kwa wananchi ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akilakiwa na wananchi wa Jimbo la Pangani wakati alipokwenda kuhutubia wananchi wa wilaya ya Panganikwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika uwanja wa sokoni ambapo alisisitiza umoja na mshikamano kwa wananchi ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akiingia eneo la mkutano kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Pangani
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akiwapungia mkono wananchi wa Jimbo hilo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akisalimiana na viongozi mbalimbali waliohudhuria mkutano huo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso katikati akifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Issa kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani.

 Kikundi cha Burudani kikitoa burudani kwenye mkutano huo wa hadhara.
 Mganga Mkuu wa wilaya ya Pangani,Dkt Juma Mfanga akifuatilia mkutano huo
 Sehemu ya umati wa wananchi wa Mji wa Pangani wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso(Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

IGP Sirro atembelea Kibiti na Ikwiriri mkoani pwani kukagua na kuongea na wananchi wa huko

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akimsalimiana na viongozi waandamizi na maofisa wa Jeshi hilo alipowasili Ikwiriri Mkoani Pwani kwa lengo la kuzungumza na wazee na wananchi wa Wilaya zote  mbili  za Ikwiriri na Kibiti. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiteta jambo na Mkuu wa operesheni maalum za Jeshi hilo, DCP Liberatus Sabas alipowasili Ikwiriri mkoani Pwani kwa lengo la kuzungumza na wazee na wananchi wa Wilayay zote  mbili  za Ikwiriri na Kibiti. Kulia ni Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, DCI Robert Boaz. 
Baadhi ya milipuko 16, Visu 96 na mbolea ya chumvi inayotumika katika kuchanganyia milipuko ikiwa imekamatwa Mkoa wa Mtwara kufuatia operesheni zinazoendelea za jeshi la Polisi. Picha na Jeshi la Polisi

Kampuni ya Ujenzi ya CRJE yajitosa udhamini Rock City Marathon

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ujenzi ya CRJE (East Africa Ltd), Bw Xie Zhixiang (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni 10 kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (kulia) ikiwa ni udhamini wa mbio hizo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja na Mahusiano na Utawala wa kampuni ya CRJE Bw Henry Kasapira (wa pili kushoto) na Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Steven Otieno

ZIKIWA zimebaki siku chache tu kufanyika kwa mbio za Rock City Marathon, kampuni ya Ujenzi ya CRJE leo imekabidhi hundi yenye thamani Tsh milioni 10 kwa waandaaji wa mbio hizo ikiwa ni udhamini wa kampuni hiyo.

Mbio zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Akikabidhi hundi hiyo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi, Ofisa Mahusiano na Utawala wa kampuni ya CRJE Bw Henry Kasapira alisema udhamini huo unalenga kuunga mkono juhudi za serikali kuhamasisha michezo na utalii wa ndani hapa nchini.

“Michezo huleta uimara wa afya na uimara wa afya ndio nguzo muhimu katika sekta ya ujenzi na ndio maana pamoja na kuinua utalii tunaunga mkono pia mpango huu unaolenga kuhamasisha uimara wa afya za wananchi.’’ Alisema.

Aliahidi kuwa kampuni yake itaendelea kushirikiana na waandaaji wa mbio hizo katika kuboresha zaidi mbio hizo kwa miaka ijayo huku akitoa wito kwa vijana wengi zaidi kutoka mikoa mbalimbali kujiandaa kwa ajili ya mbio hizo.

Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo, Ngowi alisema ushiriki wa kampuni hiyo ya kimataifa katika kufanisha Rock City Marathon utaongeza viwango vya ubora wa mbio hizo sambamba na kuwavutia zaidi washiri wa kamataifa ambao wamekuwa wakiiamini kampuni kutokana na utendaji wake wenye ufanisi.

Naye, Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Steven Otieno amesema maandalizi ya mbio hizo tayari yamekamilika huku ushiriki wa viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza na wakuu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kwenye mbio hizo ukiwa ni miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyotarajiwa kupamba mbio hizo.

“Tunatarajia kwamba viongozi hawa wa kiserikali pamoja na wadhamini wetu wengine wakiwemo PUMA, Tiper, NSSF, RedBull, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), New Mwanza Hotel, EF Out door, CF Hospital, KK Security, na kampuni ya uchapishaji ya SDS watashiriki kikamilifu katika mbio za KM 5 sambamba na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino,’’ alitaja.

Alisema kamati ya maandalizi ya mbio hizo imejiandaa vilivyo na maandalizi yote yamekamilika, ikiwemo kupokea wakimbiaji kutoka nje ya nchi na washiriki wengine.

“Tunatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 4000 wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa, wakimbiaji kutoka mashirika mbalimbali, walemavu wa ngozi yaani Albino pamoja na wanafunzi.’’ Alitaja.

Akizungumzia usajili wa mbio hizo Bw. Otieno alisema kwa wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa jirani wanaweza kujisajili kwa kuchukua fomu katika Ofisi za michezo wilaya zote za mkoa wa Mwanza, Ofisi za riadha mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga.

Sehemu nyingine ni pamoja na Uwanja wa Nyamagana, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza, Kituo cha michezo Malya, Shule ya Kimataifa ya Isamilo, New Mwanza Hotel na Ofisi za EF Out door zilizopo jingo la Rock City Mall.

“Kwa upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki pia zinapatikana jengo la SHAMO Tower, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam’’ alitaja. Zaidi kuhusu usajili wa mbio hizo zinazoandaliwa kwa kushirikiana na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA), Bidan alisema unaweza kufanyika kupitia tovuti ya kampuni hiyo ambayo ni www.capitalplus.co.tz

CCM YAZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA UDIWANI KIJICHI LEO, KUSILAWE ASEMA CCM ITASHINDA UDIWANI KATA ZOTE TATU DAR.

$
0
0
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akimnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, leo. Akizungumza amesema CCM itashinda Udiwani kata zote tatu ambako uchaguzi unarudiwa mkoani Dar es Salaam. Kata zingine ni Saranga na Mbweni.
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akiwasili kwenye Uwanja wa mkutano kuzindua kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Kijichi, leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Almishi Hazal
 Wananchi na wana CCM wakishangilia wakati Kusilawe na viongozi wenzake wakiingia Uwanjani
 Vijana wa hamasa wakichangamsha mkutano huo
 Madansa wakicheza muziki kuchangamsha mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za CCM za Udiwani kata ya Kijichi.
 Mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Kijichi Eliasa Mtalawanje akisalimia baada ya kutambulishwa kutambulishwa kwenye mkutano huo
 Mtalawanje akitroti baada ya kutambulishwa na Mwenyekiti wa Wazee wa CCM Temeke
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Wilaya ya Temeke Mohammed Mbonde, akizungumza baada ya kukaribishwa jukwaani kusalimia.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Temeke Mohammed Mbonde, akipongezwa na Mgombea Udiwani kata ya Kijichi Eliasa Mtalawanje baada ya kutoka jukwaani kusalimia.
 Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo akisalimia wananchi kwenye mkutano huo, na kuzungumza kuhusu umuhimu wa wananchi kumchagua mgombea wa CCM Udiwani kata ya Kijichi.
 Mbunge wa Mbagala Issa Mangungu, akisalimia wananchi kwenye mkutano huo, na kuzungumza kuhusu umuhimu wa wananchi kumchagua mgombea wa CCM Udiwani kata ya Kijichi.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Almishi Hazal akisalimia wananchi na kumkaribisha Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, kuhutubia mkutano huo na kumtambulisha mgombea wa CCM wa Udiwani Kata ya Kijichi
 Vijana wa hamasa na wananchi wakiwa wametulia kumsikiliza 
 Baadhi ya wananchi kwenye mkutano huo
 Viongozi wa Barza la wazee Temeke wakiwa kwenye mkutano huo
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe akihutubia mkutano huo
 Kusilawe akisisitiza jambo
 Vijana wa CCM wakimshangilia Kusilawe
 Msimamizi wa uchaguzi wa CCM makao makuu Mzee Kazidi (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke Almishi Hazal. katikati ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam
 Mzee Kazidi akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Kuslawe.
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akimnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, leo  
 Kisha akamkabidhi mgombea huyo ilani ya CCM
 Kusilawe akimkabidhi ilani mgombea huyo
 Mgombea akionyesha ilani baada ya kukabidhiwa
 Mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, akizungumza na kuomba kura baada ya kunadiwa na Kusilawe, leo
 Eliasa Mtalawanje akifafanua jambo kwa makini
 Wananchi wakimshangilia mgombea huyo
 Mgombea huyo akiendelea kuomba kura kwa wananchi 
Mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, akiondoka uwanjani mwishoni mwa mkutano. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Tigo yachangia katika ukuaji wa teknolojia na huduma za kifedha kwa njia ya mtandao nchini

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Simon Karikari (Kulia) akichangia mada wakati wa mkutano wa kutangaza matokeo yamakampuni 100 yanayoibukia katika uwekezaji nchini, ambapo zawadi kwa washindi zilitolewa mwishoni wa wiki hii  jijini Dar es Salaam, kushoto ni mkurugenzi wa 361 Degrees Mustafa Hassanali.
washiriki wa  mkutano wa kutangaza matokeo yamakampuni 100 yanayoibukia katika uwekezaji nchini wakifurahia jambo , ambapo zawadi kwa washindi zilitolewa mwishoni wa wiki hii  jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Simon Karikari (Kulia) akichangia mada wakati wa mkutano wa kutangaza matokeo yamakampuni 100 yanayoibukia katika uwekezaji nchini, ambapo zawadi kwa washindi zilitolewa mwishoni wa wiki hii  jijini Dar es Salaam, kushoto ni mkurugenzi wa 361 Degrees Mustafa Hassanali.


Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Simon Karikari akifurahi jambo na mmoja wa washiriki wa mkutano wa kutangaza matokeo yamakampuni 100 yanayoibukia katika uwekezaji nchini, ambapo zawadi kwa washindi zilitolewa mwishoni wa wiki hii  jijini Dar es Salaam.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA ATEMBELEA MAPOROMOKO YA MTO KALAMBO AMBAYO NI YA PILI KWA UREFU BARANI AFRIKA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni ya Greens Construction Limited, Hamimu Bakari wakati akishuka kwenye ngazi maalum zinazojengwa na mkandarasi huyo kwa ajili ya kuwawezesha watalii kushuka hadi kwenye kina cha Maporomoko ya Mto Kalambo wakati wa ziara yake mkoani Rukwa. Maporomoko hayo ambayo ni ya pili kwa kina kirefu barani Afrika baada ya TUGELA yaliyopo Afrika ya Kusini yana kina cha mita 235 na upana kati ya mita 3.6 hadi 18. 

Na Hamza Temba - WMU
...............................................................
SERIKALI imesema imedhamiria kufungua utalii wa Kanda ya Kusini ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini na hatimaye kuongeza idadi ya watalii na kipato kwa Serikali na jamii kwa ujumla.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga katika kijiji cha Kapozwa Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa kina kirefu barani Afrika baada ya Maporomoko ya Tugela yaiyopo nchini Afrika ya Kusini.


Alisema kwa sasa vivutio vingi vinavyotumika kwa utalii nchini ni vile vya ukanda wa Kaskazini hususan vya wanyamapori ambavyo vimeanza kuelemewa kutokana na watalii wengi kutembelea ukanda huo zaidi kuliko Kanda ya Kusini ambayo pia ina vivutio mbalimbali vya asili.


Alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo benki ya Dunia kupitia mradi wa REGROW imepanga kuboresha miundombinu ya vivutio vya utalii vya Kanda ya Kusini na kuvitangaza ili kuimarisha sekta hiyo muhimu ambayo inachangia asilimia 25 ya mapato yote ya kigeni na asilimia 17.5 ya pato la taifa.


Katika ziara yake hiyo Mkoani Rukwa, alitembelea eneo la Hifadhi ya Msitu ya Mto Kalambo na kukagua ujenzi unaoendelea wa ngazi maalum zitakazowawezesha watalii kushuka hadi kwenye kina cha Maporomoko ya Mto Kalambo ambacho ni mita 235 na upana kati ya mita 3.6 hadi 18. 


Alisema Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania inajenga ngazi hizo ili kuongeza thamani ya maporomoko hayo huku akiagiza Wakala hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine kuongeza juhudi za uwekezaji ili kuimarisha utalii wa kivutio hicho na kupanua kanda yote ya kusini.


"Tumekusudia kupanua wigo wa vivutio vyetu vya utalii kwa kufungua Kanda hii ya Kusini ambayo ina vivutio vingi ambavyo havijachangia ipasavyo kwenye uchumi wetu, maporomoko haya ni moja ya kivutio adimu katika ukanda huu. 


"Ni wakati muafaka sasa tushirikiane kuhamasisha wawekezaji kujenga mahoteli ya kisasa katika eneo hili, tuone uwezekano wa kuanzisha utalii wa 'cable cars' kuwezesha watalii kuona maporomoko kiurahisi, tujenge maeneo ya kupumzikia ili kuweka mazingira rafiki ya kupata watalii wengi na mapato yaongezeke" alisema Hasunga.


Aidha, alitoa wito kwa wananchi wa kijiji cha Kapozwa ambao wanaishi jirani na hifadhi hiyo kushirikiana na Serikali katika uhifadhi wa uoto wa asili wa hifadhi hiyo pamoja na kudumisha tamaduni zao kwa kusajili vikundi vya ngoma na kutunga nyimbo za kabila lao kwa ajili ya kutumbuiza watalii watakaofika kuona maporomoko hayo na hivyo kujitengenezea kipato kupitia utalii wa Kiutamaduni.


Pamoja na Maporomoko hayo kivutio vingine kinachopatikana ukanda wa kusini ni Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini baada ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti, hifadhi hii inasifika kwa kuwa na tembo wengi kuliko hifadhi nyingine nchini.


Hifadhi ya Taifa ya Kitulo ni kivutio kingine katika ukanda huu ambacho sifa yake kubwa ni uwepo wa aina nyingi za maua ndwele ya asili ambayo hayapatikani kwingineko duniani, sifa hiyo imesababisha wenyeji kuita hifadhi hiyo 'Bustani ya Mungu'. Wataalamu wa uhifadhi wanasema endapo maua yaliyopo Kitulo yangekuwa ni wanyamapori basi hifadhi hiyo ingeizidi wanyama waliopo Serengeti.


Vivutio vingine ni pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Katavi ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nchini, Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa, Mikumi, Mahale, Gombe, Pori la Akiba la Selous, Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Mlima Rugwe na Kimondo cha Mbozi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akiteta jambo na Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Frank Schalwe wakati akishuka kwenye ngazi maalum zinazojengwa kwa ajili ya kuwawezesha watalii kushuka hadi kwenye kina cha Maporomoko ya Mto Kalambo wakati wa ziara yake mkoani Rukwa. Maporomoko hayo ambayo ni ya pili kwa kina kirefu barani Afrika baada ya TUGELA yaliyopo Afrika ya Kusini yana kina cha mita 235 na upana kati ya mita 3.6 hadi 18. 
Meneja wa TFS Wilaya ya Kalambo, Joseph Chezue (kushoto) akimuonyesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) ngazi maalum zinazojengwa kwa ajili ya kuwawezesha watalii kushuka hadi kwenye kina cha Maporomoko ya Mto Kalambo wakati wa ziara yake mkoani Rukwa. Maporomoko hayo ambayo ni ya pili kwa kina kirefu barani Afrika baada ya TUGELA yaliyopo Afrika ya Kusini yana kina cha mita 235 na upana kati ya mita 3.6 hadi 18.
 Muonekano wa ngazi hizo kuelekea kwenye Maporomoko ya Mto Kalambo.
Muonekano wa ngazi hizo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kukagua ujenzi wa ngazi maalum zinazojengwa kwa ajili ya kuwawezesha watalii kushuka hadi kwenye kina cha Maporomoko ya Mto Kalambo wakati wa ziara yake mkoani Rukwa. Maporomoko hayo ambayo ni ya pili kwa kina kirefu barani Afrika baada ya TUGELA yaliyopo Afrika ya Kusini yana kina cha mita 235 na upana kati ya mita 3.6 hadi 18. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Julieth Binyura. 
Baadhi ya washiriki wa ziara hiyo wakishuka kwenye ngazi ambazo ujenzi wake bado unaendelea. Ujenzi huo ukikamilika ngazi hizo zitakuwa na urefu wa mita 227.
Ngazi hizo zimejengwa kwenye ukingo wa korongo la Mto Kalambo.
Sehemu ya juu ya Maporomoko ya Mto Kalambo.
 Muonekano wa mto Kalambo ambao unaotengeneza Maporomoko ya Mto Kalambo (Kalambo Falls)
Taswira ya maporomoko ya mto Kalambo kutokea angani (Picha hii ni kwa hisani ya Mtandao)

KANDA YA ZIWA WAENDELEA KUJISHINDIA ZAWADI ZA 'MCHONGO CHINI YA KIZIBO' YA COCA-COLA

$
0
0
Washindi wa Mchongo chini ya kizibo ya Coca-Cola ya Mchongo chini ya kizibo wakifurahi na zawadi zao, wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika jijini Mwanza.
Washindi wa Mchongo chini ya kizibo ya Coca-Cola ya Mchongo chini ya kizibo wakifurahi na zawadi zao, wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika jijini Mwanza.
Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Cocacola mkoani Mwanza Samwel Makenge,(kushoto) akimkabidhi pikipiki Marysiana Kijita, baada ya kushinda promosheni ya ‘ Mchongo chini ya kizibo’ wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika jijini Mwanza. 

Wakazi wa kanda ya ziwa na mikoa jirani mambo yanazidi kuwanyokea kutokana na kuendelea kujishindia zawadi za pikipiki,Televisheni bapa za kisasa ,fedha taslimu na zawadi nyinginezo kupitia promosheni ya Coca-Cola inayoendelea ijulikanayo kama ‘Mchongo chini ya kizibo’ Wiki iliyopita washindi wa pikipiki 6 walikabidhiwa zawadi zao sambamba na washindi 2 wa televisheni wakiwemo wengine wengi waliojishindia fedha taslimu na t-shirt kutoka kampuni ya Coca-Cola. 

Waliokabidhiwa pikipiki ni Derick Magnus (Nyakato), Ismail Hamis (Magu), Joseph Mafuru (Mahina Mwanza) Pendo (Bariadi Mkoani Simiyu), Daniel Keheta (Mkolani),na Marysiana Kijita (Hungumalwa).Waliokabidhiwa televisheni ni Rhoda Joel, Marco Kitula. Wakiongea kwa furaha baada ya kukabidhiwa zawadi zao washindi hao waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye lengo la kuinua maisha ya wateja wake “Nimefurahi kujishindia pikipiki kutoka Coca-Cola nitaitumia katika shughuli za biashara ili kuongeza kipato cha familia yangu”.

Alisema Marysiana Kijita,kwa furaha. Derick Magnus alisema kuwa amefurahi kujishindia zawadi ya pikipiki kupitia promosheni ya ‘Mchongo Chini ya Kizibo’na kudai kuwa itamrahisishia usafiri wake binafsi na familia yake “Chombo hiki kitarahisisha usafari katika shughuli zangu za ujasiriamali sambamba na usafiri kwa familia yangu”.Alisema. 

Mmoja wa washindi wa televisheni,Marco Kitula ,alisema kuwa zawadi aliyojishindia imekuja kwa wakati mwafaka ambapo ataweza kuona matukio mengi na michezo mbalimbali kupitia televisheni yake ya kisasa aliyojishindia “Napenda sana kuangalia matukio kupitia luninga na michezo mbalimbali nitaburudika vizuri na familia na marafiki”.

Alisema kwa furaha. Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza mwishoni mwa wiki ,Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Japhet Kisusi,amesema kuwa promosheni hii ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuboresha maisha ya wateja wanaotumia bidhaa za kampuni inaendelea vizuri na washindi wanaendelea kukabidhiwa zawadi zao. 

Aliwataka wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa kuendelea kuchangamkia promosheni kupitia kunywa soda za kampuni ya Coca-Cola na kuongeza kuwa zawadi bado ziko nyingi.”Mchongo Chini ya Kizibo inawezesha kujishindia zawadi nono za fedha taslimu,bodaboda,televisheni aina ya SONY LED,kofia na soda za bure. 

Alisisitiza kuwa ili mteja kujishindia zawadi anatakiwa kubandua kiambatanisho laini kilichopo chini ya kizibo cha soda. Kwa upande wa fedha taslimu kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 “Kwa upande wa zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni kukusanya vizibo vitatu vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda – kuonyesha upande wa Nyuma, Katikati na Mbele na zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia, T-shirt na soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini ya kizibo kama zilivyo zawadi kubwa’’.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMATATU LEO OKTOBA 30,2017

RAIS DKT MAGUFULI AELEKLEA MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI JIJINI MWANZA - RC MONGELLA

$
0
0
  Rais wa Jamhiuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli akisindikizwa ma Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na kamanda wa Jeshi la Polisi  Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa  na maafisa wengine  wakati akiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es  salaam leo Oktoba 30, 2017 kuelekea Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na IKULU
   Rais wa Jamhiuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli akiagana na maafisa
    Rais wa Jamhiuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli akiagana na maafisa
    Rais wa Jamhiuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli akiagana na maafisa
    Rais wa Jamhiuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli akiagana na maafisa
    Rais wa Jamhiuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli akiagana na maafisa
  Rais wa Jamhiuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli akiagwa  na Kamanda wa Jeshi la Polisi  Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa  na maafisa wengine  wakati akiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es  salaam leo Oktoba 30, 2017 kuelekea Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na IKULU
  Rais wa Jamhiuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli akisindikizwa ma Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda  wakati akiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es  salaam leo Oktoba 30, 2017 kuelekea Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na IKULU
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images