Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1409 | 1410 | (Page 1411) | 1412 | 1413 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufungua kambi ya uchunguzi wa macho, kisukari na shinikizo la damu.

  Kambi hiyo ya siku tatu imeandaliwa kwa pamoja kwa kushirikiana na Klabu ya Lions ya Dar es Salaam (Host), kwa kushirikiana na Hospitali ya Regency ya jijini hapa.

  Kambi hiyo itakuwa bure kwa wananchi wote watakaojitokeza kuanzia siku ya Ijumaa katika Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Lions Klabu iliyotolewa na Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency Dk. Rajni Kanabar, ufunguzi rasmi wa kambi hiyo utafanyika siku ya Jumamosi na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

  Kambi hiyo itafanyikia kwenye kiwanda cha KNAUF Gypsum Wilaya ya Mkuranga, Kata ya Vikindu kijiji cha Kisemvule Mkoa wa Pwani kuanzia siku ya Ijumaa wiki hii.

  Alisema kambi hiyo ya bure ya siku tatu itaanza tarehe 27 hadi 29 mwezi huu 
  Dk. Rajni Kanabar, aliwataka wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam na Pwani kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo.

  Alisema Lions Klabu ya Lions imeamua kuandaa kambi hiyo ya bure baada ya kubaini kuwa kuna wananchi wengi wanasumbuliwa na maradhi hayo lakini wanakosa uwezo wa kwenda kupima.

  “Hii ni fursa adimu watu wajitokeze kwa wingi kuja kupima afya zao bure, huduma hiii itatolewa kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia siku ya Ijumaa hadi Jumapili hivyo wananchi wote wachangamkie hii fursa,” alisema.

  Klabu ya Lions ya Dar es Salaam (Host), imekuwa ikiandaa kambi ya uchunguzi mbalimbali kila mwaka ambapo wananchi hupata fursa ya kwenda kupima bure.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza leo na ujumbe kutoka Kampuni ya GeoPoll wakati wa kikao cha kujadili Takwimu za Idadi ya Wasikilizaji wa Redio na Watazamaji wa Televisheni zinazotolewa na kampuni hiyo hapa nchini. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa GeoPoll kutoka Marekani Steve Gutterman.PICHA 2

  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya GeoPoll kutoka Marekani Steve Gutterman akizungumza leo wakati wa kikao cha kujadili Takwimu za Idadi ya Wasikilizaji wa Redio na Watazamaji wa Televisheni zinazotelewa na kampuni hiyo hapa nchini.

  PICHA 3

  Baadhi ya wajumbe kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Kampuni ya GeoPoll wakifuatilia kwa makini kikao cha kujadili Takwimu za Idadi ya Wasikilizaji wa Redio na Watazamaji wa Televisheni zinazotelewa na Kampuni ya GeoPoll hapa nchini.

  PICHA 4

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa GeoPoll kutoka Marekani Steve Gutterman na Mwakilishi kutoka Idara ya Habari -MAELEZO Casmir Ndambalilo baada ya kumaliza kikao cha kujadili Takwimu za Idadi ya Wasikilizaji wa Redio na Watazamaji wa Televisheni zinazotelewa na Kampuni ya GeoPoll hapa nchini.
  PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO

  0 0

   Katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka akiwa kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa akizungumza na baadhi ya walimu walihudhuria mkutano huo. 
  Baadhi ya walimu waliokuwa wanaimba wimbo wa walimu wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.

  Na Fredy Mgunda,iringa. 

  Walimu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa wametakiwa kutumia kondomu ili kujikinga na magonjwa ya zinaa amboya yamekuwa yakipunguza nguvu kazi ya taifa.

  Hayo yamesemwa na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa.


  Chintinka alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la waathirika wa ugonjwa wa ukimwai kutokana na kufanya mapenzi bila kutumia kondomu.


  “Jamani hapa Iringa kuna tatizo kubwa la ugonjwa wa ukimwi hivyo niwaombe walimu wangu tutumie kondomu ili kujiepusha na gonjwa hili vinginevyo vizazi vyetu vyote vitaambukizwa ukimwi” alisema Chintinka


  Chintinka alisema njia ya kuwa salaama kuepukana na gonjwa hili ni kujikinga kwa kutumia kondomu maana hata watoto wetu wameathirika kutokana na wazazi kutokuwa makini na matumizi ya kinga


  “Naombeni tuwakinge hawa watoto wetu ambao wameathirika ili wasiwaambukize watoto wengine maana bila hivyo tutakuwa na kizazi kilichoathirika” alisema Chintinka


  Aidha Chintinka aliwaomba walimu walioathirika kujitokeza ili kupewa lishe ambayo inatolewa na serikali bure hivyo walimu wametakiwa kujitokeza na kuweka wazi kwa mwagili wake ili aweze kupata mgao wa pesa za lishe.


  “Jamani walimu fungu la lishe kwa walimu walioathirikia ni nono kweli naombeni walimu mjitokeze ili mfaidi fungu hili nono maana mimi nafahamu sisi ndio tunaotenga naombeni fikisheni ujumbe huu kwa walimu wengine ambao hawajafika hapa” alisema Chintinka


  Chintinka aliwataka watumishi wanaotoa siri za watumishi walioathirika kuacha tabia hiyo mara moja ili kuwaweka huru waathirika na wengine waweze kujitokeza na wapate lishe iliyotengwa na wilaya.


  Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho manispaa ya Iringa MWL. Zawadi Mgongolwa alikiri kuwepo kwa viongozi wa sekta hiyo ambao wemekuwa wakitoa siri za walimu na watumishi walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.


  Kwa kweli mgeni rasmi umeongea ukweli kero kubwa kwa walimu ni kutolea siri nje kitu kinachowafanya walimu waathirika kujificha na maradhi yao” alisema Mgongolwa


  Naye katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alimpongeza mgeni rasmi kwa ujumbe wake ambao umekuwa faraja kwa walimu na kuwaongezea hali ya kwenda kufanya kazi ya uwalimu kwa kujituma na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wao.
  0 0

  Mhandisi John Gunda wa karakana ya Magari katika Chuo Cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College) akimuelezea mgeni rasmi Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo kupitia “Screen” namna mfumo wa Injini ya gari unavyofanya kazi.
  Naibu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha (Mwenye koti la bluu) Mhandisi Dr. Erick Mgaya akimuelezea Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo namna mashine mbalimbali zinavyofanya kazi katika karakana ya magari iliyopo chuoni hapo.


  Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya udereva katika chuo cha ufundi Arusha, mwenye koti la bluu ni Naibu Mkuu wa Chuo Mhandisi Dr. Erick Mgaya na kushoto kwake ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi Joseph Bukombe.

  Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

  …………………
  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

  Wamiliki wa vyuo vya udereva mkoani Arusha wameombwa kuongeza muda wa mafunzo ya udereva kutoka wiki nne hadi wiki nane ili kuweza kutoa madereva wahitimu wenye viwango vya hali ya juu.

  Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alipokuwa akizindua mafunzo ya udereva yanayoendeshwa na Chuo Cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College) jijini hapa.

  Kamanda Mkumbo alisema endapo vyuo hivyo vitatoa mafunzo hayo kwa muda mrefu bila kuogopa gharama za uendeshaji vitawasaidia wahitimu kupata uzoefu na wakati mwingine kupata fursa za ajira moja kwa moja pindi wamalizapo mafunzo yao.

  Kamanda Mkumbo aliwashauri madereva wasiopitia mafunzo wajiunge na vyuo kwani ajira zao zipo hatarini na kuwaeleza wahitimu wapya milango yao ya ajira kwa sasa imefunguliwa kwa kuwa ujuzi wao na vyeti vyao ni sifa mojawapo.

  Aidha Kamanda Mkumbo ambaye alikuwa ameambatana na Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mrakibu wa Polisi Joseph Bukombe, amewataka wahitimu hao kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zilizo ndani ya uwezo wao.

  “Hayo yatawezekana endapo mtafuata sheria za udereva kama vile kufanya ukaguzi wa chombo cha usafiri kabla ya kuanza safari, kutoendesha gari mkiwa mmechoka au kulewa pombe na kutotumia simu wakati mnaendesha”. Alifafanua Kamanda Mkumbo.

  Mwisho alitoa pongezi kwa Chuo hicho kwa kuanzisha Progamu hiyo ya mafunzo ya udereva kwani anaamini kitakuwa kinatoa madereva wenye uweledi wa hali ya juu kutokana na kuwa na wataalamu waliobobea na hii ni ishara ya kuliunga mkono Jeshi la Polisi katika kupunguza ajali za barabarani kama si kukomesha kabisa.

  Akitoa historia ya chuo hicho Naibu Mkuu wa Chuo hicho cha Ufundi Arusha Mhandisi Dr. Erick Mgaya alisema kwamba awali chuo kilianza udahili mwaka 1978 ambapo kilikuwa kinatoa mafunzo katika progamu tano.

  Na kuongeza kwamba, pamoja na chuo hicho kukua na kutoa elimu kwa kiwango cha Shahada ya kwanza lakini pia walisukumwa kuanzisha progamu ya udereva kwa nia ya kutoa fursa kwa wanafunzi wa chuo hicho hasa wa ufundi wa magari kujifunza udereva na kuwa na leseni.

  Alisema wanafunzi hao lazima wawe wanafanya majaribio ya uendeshaji wa magari hivyo mafunzo hayo pamoja na leseni watakazopata zitawasaidia kuendesha magari yao ndani na hata nje ya chuo bila kuwa na shaka.

  Jumla ya wahitimu 76 baadhi yao wakiwa wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho pamoja na watu wengine wasio wanafunzi kutoka nje ya chuo hicho walioanza mafunzo hayo toka tarehe 15.08.2017 wametunukiwa vyeti baada ya kuhitimu mafunzo hayo ambayo yalikuwa yanasimamiwa na Mhandisi David Mtunguja pamoja na walimu wengine 14.

  0 0  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akizungumza mbele ya Wamiliki wa Viwanda,Wafanyabiashara na makampuni mbalimbali wakati wa kufungua Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda lililofanyika jana Oktoba 25,2017 mjini Beijing,nchini China.Kongamano hilo kubwa lenye uhamasishaji mkubwa wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,liliandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies.Picha Ahmad Michuzi-China.

  Balozi Kairuki ameupongeza uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies kwa kuthubutu na kuonesha juhudi kubwa za kutafuta na kuwahamasisha washirika mbalimbali katika suala zima la uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania.

  Balozi Kairuki amesema kuwa,yeye yuko tayari kushiriki kwa pamoja kusaidia kuendelea kuwahamasisha Wawekezaji wa nchini China,kuja kuwekeza nchini Tanzania,ili kuhakkisha dhana ya Tanzania ya Viwanda inatimia na hatimaye nchi ya Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

  "Kwa kufanya hivyo sote kwa pamoja tutakuwa tunetekeleza kwa vitendo,na pia kuunga mkono dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Viwanda",alisema Balozi Kairuki.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa akizungumza mbele ya Wamiliki wa Viwanda,Wafanyabiashara na makampuni mbalimbali waliojitokeza kushiriki Kongamano la uwekezaji wa Viwanda lililofanyika jana Oktoba 25,2017 mjini Beijing,nchini China.Kongamano hilo kubwa lenye uhamasishaji mkubwa wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,liliandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa akipongezwa mara baada ya kutoa hotuba yake .
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa akiwalekeza jambo baadhi ya Wadau wenye nia ya Uwekezaji nchini Tanzania,mara baada ya Kongamano la uwekezaji wa Viwanda kumalizika.Kongamano hilo lilifanyika Oktoba 25,2017 katika moja ya ukumbi wa hotel ya King Wing,mjini Beijing nchini China,ambapo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini humo,Mh Mbelwa Kairuki.
  Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Samataba akijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yameulizwa na baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo la Uhamasishaji wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya King Wing mjini Beijing nchini China.Mh Semataba ambaye aliongozana na baddhi ya viongozi waandamizi wa Serikali mkoa wa Pwani,aliwahikikishia mazingira mazuri Washiriki hao wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalibali ikiwemo Viwanda,madini na kilimo na kuwa.
  Kongamano la Uhamasishaji uwekezaji wa Viwanda kwa nchini Tanzania likiendelea mjini Beijing,nchini China.
  Sehemu ya meza kuu na baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.
  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi akiwasili ukumbini kufungua kongamano la Uwekezaji wa Viwanda akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa (wa pilia kulia) ambao ndio waandaaji wa kongamano hilo ambalo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo la Uwekezaji wa Viwanda,wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakjiri ukumbini humo,pichani kati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Naima Mohamed Kiluwa ambao ndio wameandaa kongamano hilo.
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo la Uwekezaji wa Viwanda,wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Naima Mohamed Kiluwa akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibaha Vijijini,Bi.Tatu Selemani.
  Picha ya pamoja kutoka meza kuu na baadhi ya Wadau wakuu wa Kongamano hilo la Uwekezaji wa Viwanda.

  0 0

  Fainesy Matiholo akishangilia ushindi wake wa kitita cha Milioni 65 akiwa baba na Mama yake Tabora Mjini.

  Fainesy Matiholo, mkazi wa Tabora Mjini ambaye amekuwa akicheza Tatu Mzuka huku akiwaa kuwa itatokea siku aibuke msndini basi, siku hiyo ikawa ni Jumapili iliyopita ambapo akaibuka kuwa mshindi wa 12 wa droo kubwa ya Tatu Mzuka na kujinyakulia kitita cha shilingi za Kitanzania Milioni 65.

  Bi. Matiholo amekabidhiwa zawadi yake ya ushindi na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mheshimiwa Queen Mlozi ambaye alitoa zawadi hiyo akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Aggrey Mwanri. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Mkoa wa Tabora.

  “Nimekuwa nikicheza Tatu Mzuka kila juma lakini lengo langu kubwa lilikuwa kupata ushindi wa kila saa. Sikutarajia kabisa kuwa nitaibuka mshindi wa droo kubwa ya Tatu Mzuka,” anasema.

  Katika hafla hiyo ya kukabidhi zawadi, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bi. Mlozi alizungumza kuwa; “tumefurahi sana kuona kuwa juma hili mshindi wa Tatu Mzuka katika katika Mkoa wetu. Ushindi huu umetusaidia kuamini kuwa mchezo huu unatoa fursa sawa kwa watu wote. Naamini sasa wananchi wa Tabora watahamasika zaidi kushiriki katika mchezo huu.”

  Katika ushindi huu wa Bi. Matiholo pia rafiki zake watatu ambao hushiriki kucheza Tatu Mzuka nao wamefanikiwa kujishindia kiasi cha Shilingi milioni 1 kila mmoja kupitia kipengele cha Tatu Mzuka “cheza na washkaji na washikaji promosheni.” Walioshinda kipengele hiki ni Jacqueline Samuel, Sande Kabaye na Lilian Tegete.

  “Tatu Mzuka imebadili maisha yangu,” Bi. Matiholo anasema na kuongeza kuwa; “naweza sasa kuanza kupanga namna ya kuishi maisha bora zaidi, nitaweza kumpatia mwanangu elimu bora zaidi na pia kuboresha biashara yangu,“ alieleza.

  Hata wewe unaweza kuwa mshindi ajaye wa Tatu Mzuka na safari hii mshindi anatarajiwa kupata kitita kinachofikia milioni 110. Hadi sasa kumekuwepo na washindi zaidi ya milioni 1.7 waliojishindia zawadi mbalimbali kutoka Tatu Mzuka. Pia kuna zaidi ya shilingi milioni 500 zinazosubiriwa kushindaniwa kadri siku zinavyoenda. Unaweza kuwa mshindi lakini jambno la kufanya ni kushiriki mchezo huu mara nyingi zaidi uwezavyo.
  Fainesy Matiholo mshindi wa 12 wa droo kubwa ya Tatu Mzuka na kujinyakulia kitita cha shilingi za Kitanzania Milioni 65.

  Mheshimiwa Queen Mlozi Mkuu wa Wilaya wa Tabora akitoa zawadi kwa Fainesy Matiholo akimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Aggrey Mwanri.Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Mkoa wa Tabora.

  0 0


  Kaimu mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo    akijitambulisha wakati wa kuzindua mbio za Kili Half Marathon kwa mwaka 2018, mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio za Kili Marathon kwa mwaka 2018, uzinduzi huo umefanyika jana jijini Dar es Salaam ambapo kampuni ya simu za mkononi ya Tigo itadhamini mbio za kilomita 21 kwa jina la Tigo Kili Half Marathon.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mbio za Kili Marathon kwa mwaka 2018, uzinduzi huo umefanyika jana jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni  Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo ambao wamedhamini mbio za kilomita 21 ziitwazo Tigo Kili Half Marathon


  0 0

  The TBL Managing Director who is also AB-inBev’s President of the East African Business Unit,Roberto Jarrin ,at the Second Ministerial Dialogue with the Private Sector whose theme was “ The Sate of Doing Business in Tanzania”. --- We have experienced phenomenal growth from the second quarter of this year and will soon be looking to increase our production capacities, says the TBL Managing Director, Roberto Jarrrin. Jarrin was speaking at the Second Ministerial Dialogue with the Private Sector whose theme was “ The Sate of Doing Business in Tanzania”. The dialogue was hosted by the Minister of Finance and Planning - Honourable Philip Mpango and the Minister for Industry, Trade and Investment - Honourable Charles Mwijage in Dar es Salaam this week. 
  This was a follow up to a similar meeting that was held in Dodoma early this year. The TBL Managing Director who is also AB-inBev’s President of the East African Business Unit, said that existing market conditions – the company had previously been growing at the rate of negative 0.3% - had forced the company to re-think its operating model and realign it to the realities of the market . 
  This had in turn led to TBL growing its business by 20% since June this year. Adding that, “We are optimistic that this growth will continue and are looking to invest in increased production capacity to cater for this because our plants are currently operating at maximum capacity.” On what was driving the growth, Jarrin said it is mainly driven by the affordable brands and packs segment which are primarily sorghum based. 
  “The affordable segment of our market which essentially sources its growth from the informal sector, is price sensitive and for us to invest in a new brewery we would like to work with the Government of Tanzania to create a stable and predictable excise regime. Increased production volumes will in turn translate into increased revenue collection,” he said. Insofar as supporting the government’s industrialisation drive is concerned, the Managing Director had this to say, “ We at TBL Group consider ourselves an agro-processing industry because agricultural produce – barley, sorghum, maize and sugar - are the key ingredients in our products.
   Increased production levels thus require increased purchases of the cereals that we use in our breweries. Our continued growth as a business has a direct impact on many sectors of which agriculture is the main one.” TBL Group has been a consistent top performer since its privatization in 1993. 
  The business has also doubled in size over the past five years due to the on-going investments in our operations. “We plough back between TShs. 90 -150 billion in the upgrading of our breweries and distilleries to world-class standards around the country every year, “ says Jarrin.

  0 0

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi (wa pili kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank (MCB),Ronald Manongi, wakibadilishana hati za makubaliano jijini Dar es Salaam leo ambapo wateja wa benki ya upande mmoja wataweza kupata huduma za kibenki katika matawi ya  benki ya upande mwingine. 
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi ( kushoto waliokaa) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank (MCB),Ronald Manongi, wakisaini hati za makubaliano jijini Dar es Salaam leo ambapo wateja wa benki ya upande mmoja wataweza kupata huduma za kibenki katika matawi ya  benki ya upande mwingine. 
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TPB na Mwalimu Commercial Bank (MCB), ambapo wateja wa benki ya upande mmoja wataweza kupata huduma za kibenki katika matawi ya  benki ya upande mwingine. Kushoto kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Mwalimu,  Ronald Manongi .
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank (MCB),  Ronald Manongi (kulia),  akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya MCB na Benki ya TBP ambapo wateja wa benki ya upande mmoja wataweza kupata huduma za kibenki katika matawi ya  benki ya upande mwingine. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi. 
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi (wa tano kushoto) akishikana mikono na  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank (MCB),Ronald Manongi mara baada ya kumalizika kwa tukio la utiaji saini makubaliano hayo. Pamoja nao ni baadhi ya maofisa wa benki za TPB na MCB.

  0 0
  Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelacius Byakanwa akikata utepe kuzindua rasmi maabara yenye nyenzo za elimu ya kidigitali ya Tigo eSchools kwa shule ya sekondari  wasichana Machame jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo.


  Mkuu wa wilaya ya Hai, Gelacius Byakanwa (aliyekaa kulia)akipata maelezo ya matumizi ya kujisomea vitabu kwa njia ya mtandao kupitia Tigo eSchools toka kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari wasichana Machame, Delynes Laurian mara baada ya kampuni ya Tigo kukabidhi huduma hiyo shuleni hapo jana.

  Mtaalam wa tovuti toka Shule Direct, Emmanuel George akielezea jambo kwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Gelacius Byakanwa wakati wa uzinduzi wa Tigo eSchools shule ya wasichana Machame leo. Wengine nyuma kushoto Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda kaskazini, Henry Kinabo, mwalimu mkuu wa shule ya Machame, Asteria Massawe

  Umati wa wanafunzi wa  shule ya wasichana Machame Machame wakiwa wanashuhudia uzinduzi wa Tigo eSchoolsl mapema jana.


  0 0  0 0
  Fainesy Matiholo mshindi wa 12 wa droo kubwa ya Tatu Mzuka na kujinyakulia kitita cha shilingi za Kitanzania Milioni 65.
  Mheshimiwa Queen Mlozi Mkuu wa Wilaya wa Tabora akitoa zawadi kwa Fainesy Matiholo akimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Aggrey Mwanri.Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Mkoa wa Tabora.

  Fainesy Matiholo akishangilia ushindi wake wa kitita cha Milioni 65 akiwa baba na Mama yake Tabora Mjini.

  ...................

  Fainesy Matiholo, mkazi wa Tabora Mjini ambaye amekuwa akicheza Ttau Mzuka huku akiwaa kuwa itatokea siku aibuke msndini basi, siku hiyo ikawa ni Jumapili iliyopita ambapo akaibuka kuwa mshindi wa 12 wa droo kubwa ya Tatu Mzuka na kujinyakulia kitita cha shilingi za Kitanzania Milioni 65.

  Bi. Matiholo amekabidhiwa zawadi yake ya ushindi na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mheshimiwa Queen Mlozi ambaye alitoa zawadi hiyo akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Aggrey Mwanri. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Mkoa wa Tabora.

  “Nimekuwa nikicheza Tatu Mzuka kila juma lakini lengo langu kubwa lilikuwa kupata ushindi wa kila saa. Sikutarajia kabisa kuwa nitaibuka mshindi wa droo kubwa ya Tatu Mzuka,” anasema.

  Katika hafla hiyo ya kukabidhi zawadi, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bi. Mlozi alizungumza kuwa; “tumefurahi sana kuona kuwa juma hili mshindi wa Tatu Mzuka katika katika Mkoa wetu. Ushindi huu umetusaidia kuamini kuwa mchezo huu unatoa fursa sawa kwa watu wote. Naamini sasa wananchi wa Tabora watahamasika zaidi kushiriki katika mchezo huu.”

  Katika ushindi huu wa Bi. Matiholo pia rafiki zake watatu ambao hushiriki kucheza Tatu Mzuka nao wamefanikiwa kujishindia kiasi cha Shilingi milioni 1 kila mmoja kupitia kipengele cha Tatu Mzuka “cheza na washkaji na washikaji promosheni.” Walioshinda kipengele hiki ni Jacqueline Samuel, Sande Kabaye na Lilian Tegete.

  “Tatu Mzuka imebadili maisha yangu,” Bi. Matiholo anasema na kuongeza kuwa; “naweza sasa kuanza kupanga namna ya kuishi maisha bora zaidi, nitaweza kumpatia mwanangu elimu bora zaidi na pia kuboresha biashara yangu,“ alieleza.

  Hata wewe unaweza kuwa mshindi ajaye wa Tatu Mzuka na safari hii mshindi anatarajiwa kupata kitita kinachofikia milioni 110. Hadi sasa kumekuwepo na washindi zaidi ya milioni 1.7 waliojishindia zawadi mbalimbali kutoka Tatu Mzuka. Pia kuna zaidi ya shilingi milioni 500 zinazosubiriwa kushindaniwa kadri siku zinavyoenda. Unaweza kuwa mshindi lakini jambno la kufanya ni kushiriki mchezo huu mara nyingi zaidi uwezavyo.

  0 0


   Wagombea Udiwani wa CCM katika Uchaguzi wa marudio katika Kata ya Saranga Wilayani Ubungo na Kata ya Kijichi wilayani Temeke leo wamerudisha fomu zao kwa wasimamizi wa uchaguzi katika kata hizo kwa kishondo huku wakisindikizwa na viongozi kadhaa ya wa CCM wakiongozwa ana Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe. Pichani, Mgombea wa CCM katika Kata Saranga, Manispaa ya Ubungo Haroun Mdoe akimkabidhi fomu yake Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo Dandasi Kijo kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Saranga, leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja.
   Waendesha bodaboda wakiwa kwenye msafara kumsindikiza mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi wa marudio Kata ya Saranga, leo
   Mashabiki wa CCM wakiwa kwenye bajaji kwenye msafara kumsindikiza mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi wa marudio Kata ya Saranga, leo
   Masafara wa baadhi ya viongozi wa CCM wakipeleka mgombea wa CCM kurejesha fomu kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Saranga  
   Mwananchi aliyekuwa katika shughuli zake akishangilia msafaya wa mgombea huyo wa CCM wa Udiwani Kata ya Saranga
   Shamrashamra za wana CCM zikihanikiza baada ya msafara wa mgombea wa CCM wa Udiwani Kata ya Saranga kufika kwenye Ofisi za Afisa Mtendaji wa wakata hiyo
   Mgombea Udiwani wa CCM katika uchaguzi wa marudio Kata ya Saranga Haroun Mdoe (mwenye fulana yenye jina kubwa la Samia) akishangiliwa wakati akiwasili kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya saranga kurejesha fomu yake.
   Wanachi na wana CCM wakimsindikiza kuingia kwenye Ofisi mgombea huyo
   Mgombea wa CCM katika Kata Saranga, Manispaa ya Ubungo Haroun Mdoe akikabidhiwa fomu za kiapo na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo Dandasi Kijo, kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Saranga, leo, huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe (kulia) Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja (kushoto) wakishuhudia.
   Msimamizi huyo msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Saranga akitazama kama Mgombea huyo wa CCM anajaza fomu yake kwa usahihi. Kulia ni Kusilawe. 
   Mgombea wa CCM akiijaza fomu yake ya kiapo
   Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akimwelekeza mgombea wa CCM ili asikosee wakati wa kujaza fomu yake ya kiapo 
   Mgombea wa CCM katika Kata Saranga, Manispaa ya Ubungo Haroun Mdoe akimkabidhi fomu yake Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo Dandasi Kijo kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Saranga, leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja.
   Mgombea huyo wa CCM akiwa katika picha ya pamoja na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kata ya Saranga (wapili kushoto) na baadhi ya viongozi wa CCM baada ya kukabidhi fomu yake ya kuomba kuteuliwa kugombea
   Baadaye mgombea huyo akapiga picha ya pamoja na viongozi wa CCM waliosindikiza na baadhi ya wana CCM waliofika kwenye Ofisi ya Ofisa Mtendaji wa Kata ya Saranga kushuhudia akirejesha fomu. 
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam saad Kusilawe akimpongeza Mgombea Udiwani wa CCM katika Uchaguzi wa marudio Kata ya Saranga Haroun Mdoe baada ya urejeshaji fomu kukamilika. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ubungo Lucas Mgonja na kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo Salum Kalli.
   ---------------------
    UREJESHAJI FOMU KATA YA KIJICHI
   Mgombea CCM katika uchaguzi wa marudio Kata ya Kijichi Eliasa Mtarawanje akishangiliwa na wananchi wakati wakiwapungia mkono alipokuwa akienda kurejesha fomu kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Kijichi, Temeke Dar es Salaam, leo.
   Eliasa Mtarawanje akipunga mkono kuonyesha furaha yake ya kwenda kurejesha fomu
   Mwananchi akimshangilia Eliasa Mtarawanje msafara ulipopita eneo la makazi yake.
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe na baadhi ya viongozi wa CCM wakimsubiri kumpokea Mgombea huyo Eliasa Mtarawanje, kwenye ofisi ya Afisa Mtendaji kaya ya Kijichi.
   Eliasa Mtarawanje akisalimia viongozi wa CCM baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Kijichi kurejesha fomu yake.
   Eliasa Mtarawanje aakisimama wakati wa utambulisho
   Katibu wa CCM mkoa wa Sar es Salaam Saad Kusilawe akizungumza kwa niaba ya msafara baada ya kufika katika Ofisi ya Afisa Mtedaji Kata ya Kijichi
   Mgombea wa CCM katika Uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi Eliasa Mtarawanje akikabidhiwa fomu ya kiapo ili kuijaza kabla ya kukabidhi fomu zake.
   Eliasa Mtarawanje akijaza kwa makini fomu yake ya kiapo
   Eliasa Mtarawanje akikabidhi fomu zake kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kata ya Kijichi baada ya kuzijaza
   Akikabidhi rasmi fomu hizo baada ya kuhakikiwa 
   Eliasa Mtarawanje Akisaini kuthibitisha kuwa amerejesha fomu zake
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, saad Kusilawe na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Ndugu Mishi wakimsindikiza kutoka katika Ofisi ya Afisa Mtendaji baada ya kujeresha fomu
  Eliasa Mtarawanje akitoka kwa shangwe na nderemo kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Kijichi baada ya kurejesha fomu zake za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa Udiwani wa kata hiyo kwa tiketi ya CCM. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0


  Watafiti, Dk.Beatrice Lyimo (wa tano kushoto) na Bestina Daniel (wa pili kulia), kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),wakiwakabidhi mbegu bora ya mihogo Wanakikundi cha Chapakazi katika  Kijiji cha Kalebezo wilayani Biharamulo mkoani Kagera jana, kwa ajili ya kuanzisha shamba darasa wakati wa uzinduzi wa shamba hilo wilayani humo. 

   Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala (kulia), akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi wa upandaji wa mbegu ya mhogo kwenye shamba darasa katika Kijiji Kalebezo wilayani humo.
   Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapakazi, Thadeo Kibuka akizungumza katika uzinduzi huo.
   Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel, akizungumza.
   Mtafiti, Dk.Beatrice Lyimo kutoka COSTECH, akizungumzia kuhusu mradi huo wa mbegu bora
   Mtafiti wa mazao jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Josianas Kabura (mwenye mbegu), akitoa mafunzo kwa wakulima jinsi ya kupanda mbegu hiyo ya mhogo aina ya Mkombozi iliyozalishwa kitaalamu. 
  Mtafiti wa mazao jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Josianas Kabura, akielekeza namna ya upandaji wa mbegu ya viazi lishe katika kijijini cha Msenyi
   Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala, akipanda mbegu hiyo katika shamba darasa kijijini Kalebezo.   Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapakazi, Thadeo Kibuka akipanda mbegu ya mhogo.
   Ofisa Ugani, Jonas Kamugisha akipanda mbegu ya mhogo.
   Ofisa Ugani wa Kijiji cha Kalebezo, Juster Nkuna akipanda mbegu ya mhogo.
   Mbegu ya mhogo ikishushwa kutoka kwenye gari tayari kwa uzinduzi wa shamba darasa katika Kijiji cha Kalebezo.
   Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapajembe wa Kijiji cha Msenyi, Josia Kagwingi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la viazi lishe katika kijiji hicho. Kutoka kushoto ni Katibu wa Kikundi hicho, Mariana Mariko na kulia ni mwanakikundi, Zabia Emanuel.


  Mkulima wa Kijiji cha Msenyi, Martin Tibenda akipanda mbegu ya viazi lishe katika uzinduzi wa shamba darasa.

  Na Dotto Mwaibale, Biharamulo Kagera.

  WAKULIMA wilayani Biharamulo mkoani Kagera wameipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kwa kuwapelekea mbegu bora ya migomba,mihogo na viazi lishe ambayo itapandwa katika mashamba darasa na kusambazwa kwa wakulima wengine katika wilaya hiyo.

  Pongezi hizo zimetolewa na Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala wakati wa uzinduzi wa upandaji wa mbegu ya mhogo kwenye shamba darasa katika Kijiji Kalebezo wilayani humo.

  "Kwa niaba ya Ofisa Kilimo wa wilaya napenda kuishukuru COSTECH kwa kutuletea mbegu hizo katika wilaya yetu hasa baada ya kuona changamoto tuliyokuwa tukikabiliana nayo ya magonjwa ya mihogo kama batobato" alisema Ngawagala.

  Ngawagala alisema msaada huo hautapotea bure kwani watahakikisha wanayahudumia vizuri mashamba darasa hayo likiwemo la mihogo lililopo katika Kijiji Kalebezo na lile la viazi lishe lililopo Kijiji cha Msenyi ambayo yamezinduliwa na kuhudhuriwa na wakulima kutoka vikundi vya Chapakazi katika Kijiji cha Kalebezo na Chapajembe cha Kijiji cha Msenyi vyote vya wilaya hiyo.

  Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Chapakazi, Thadeo Kibuka alisema mbegu hiyo waliyoletewa itakuwa mkombozi wao kwani kwa muda mrefu walikuwa na changamoto ya kupata mazao yenye magonjwa kutokana na kukosa mbegu bora na ukame.

  "Tutahakikisha shamba ili tunalo lizindua leo hii kwa msaada wa COSTECH na OFAB linakuwa la mfano wa kuzalisha mbegu bora katika wilaya hii" alisema Kibuka.

  Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Mtafiti Dk. Beatrice Lyimo alisema COSTECH kwa kushirikiana na OFAB wanaendesha mradi huo ili kuhakikisha kuhakikisha matokeo mazuri ya kazi za tafiti yanawafikia wakulima na kupata chakula cha kutosha.


  Alisema COSTECH ndio mshauri mkubwa wa serikali katika masuala ya kilimo cha kitafiti hivyo wanakila sababu ya kuhakikisha tafiti zinazofanyika nchini zikiwafikia walengwa ili waweze kufanya vizuri katika kilimo.


  Dk. Lyimo aliwataka wakulima hao kwa kushirikiana na maofisa ugani kuyatunza mashamba darasa hayo ili kupata mbegu nyingi za mazao hayo na kuzisambaza kwa wakulima wengine.

  Ofisa Kilimo Mkoa wa Kagera, Louis  Baraka alisema mkoa huo umepata bahati kubwa kwa kupelekewa mbegu hizo katika wilaya tano ambapo katika kila wilaya vijiji viwili vilichaguliwa kuanzisha shamba darasa la mbegu ya mhogo na migomba na viazi lishe kutegemea uhitaji wa zao gani katika kijiji husika.

  "Tuna bahati kubwa kuletewa mradi huu katika mkoa wetu hivyo tusiwaangushe hawa wenzetu tuwe wa mfano tuyatunze haya mashamba ili tupate matokeo mazuri" alisema Baraka.

  Mtafiti wa mazao jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Josianas Kabura amewataka wakulima hao kutambua kuwa mbegu hizo za mihogo walizokabidhiwa zinatunzwa vizuri kwani zinauwezo wa kutoa tani 32 za mhogo kwa ekari moja na kwa viazi lishe zinatoa tani 7 hadi 9 kwa ekari tofauti na mbegu za zamani ambazo hazina tija.

  Mashamba darasa ya mbegu bora za Mihogo,Viazi lishe na Migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa yaliyoanzishwa katika mkoa huo yanajumuisha wilaya tano za Mkoa wa Kagera baada ya COSTECH na OFAB kutoa mafunzo kwa wataalamu wa kilimo wa wilaya hizo na  kata zote ikiwa na lengo la kuwasaidia wakulima kuzalisha mazao yao kwa tija na kuachana na kilimo kisicho bora na tija.

  0 0

  Jonas Kamaleki- MAELEZO

  Serikali imewataka wataalam wa mipangomiji kuandaa mwongozo wa upimaji wa mitaa na vijiji maeneo ya vijijini ili kuboresha makazi.

  Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Wiliam Lukuvi wakati akifungua Mkutano wa Nne wa Bodi ya Usajili ya Wataalam wa Mipangomiji (TPRB).

  Waziri Lukuvi amewataka pia wataalam hao watengeneze mwongozo wa kuharakisha urasmishaji wa makazi holela. “Nataka mtengeneze mwongozo wa uendelezaji fukwe na kuangalia namna ya kurekebisha sheria zinazokinzana,” alisema Lukuvi.

  Aidha, Lukuvi amewataka wapangamiji kuandaa mpango mwepesi wa kuondoa urasimu wa utoaji wa vibali vya ujenzi ili kuwaondolea adha wananchi ambao pengine wanakopa ili wajenge na kufanya biashara. Amependekeza vibali vya ujenzi vitolewe ndani ya mwezi mmoja au hata wiki moja itoshe kutoa vibali hivyo ili kuondokana na urasimu katika ujenzi.

  Wale waliojenga kwenye maeneo yaliyopimwa lakini hawana vibali vya ujenzi, Lukuvi amesema wasisumbuliwe kwani watoa vibali ndio waliowachelewesha. Ameongeza kuwa kwa waliojenga kwenye maeneo yasiyopimwa, maeneo yao yarasimishwe.

  Kuhusu ajenzi wa uchumi wa viwanda, Waziri Lukuvi amesema upangaji miji uzingatie kutenga maeneo kwa ajli ya ujenzi wa viwanda katika miji na Halmashauri zote nchini. Lukuvi amesema wapangamiji wazingatie pia miundombinu ya umeme, maji, maeneo ya huduma kama makaburi, maaeneo ya wazi, shule na maeneo ya ibada.

  Waziri amewataka watumishi wa Serikali wa mipangomiji wasiowaadilifu wachukuliwe hatua kali za kisheria na TPRB. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Wataalam wa Mipangomiji, Prof. Wilbroad Komba amesema kuwa Bodi inajitahidi kufanya kazi zake kwa weledi licha ya changamoto ya kuwa na wataalam wachache.

  Tanzania inao wataalam wa mipangomiji 306 waliosajiliwa ambao ni asilimia 25 tu kati ya wale wanaohitajika kwa shughuli za kupanga miji.

  Mkutano huo wa Nne wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji una kaulimbiu isemayo: “Mipangomiji na Uchumi wa Viwanda.”

  0 0

  Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures iliyopo katika eneo la Bugayambele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga leo Alhamis Oktoba 26,2017 wametembelea kituo cha watoto wenye ualbino cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga na kuwapatia zawadi mbalimbali.

  Miongoni mwa zawadi zilizotolewa na wanafunzi hao waliokuwa wameongozana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Paul Kiondo ni pamoja na nguo,viatu,sabuni,mchele,mabegi ya o amesema shule hiyo imekuwa na utaratibu wa kila mwaka kwa wanafunzi wao kutembelea kituo cha Buhangija kwa ajili ya watoto kubadilishana mawazo na kuwapatia zawadi mbalimbali watoto waliopo katika kituo hicho. 
  “Little Treasures imekuwa karibu na kituo hiki,na kila mwaka tumekuwa tukiwaleta wanafunzi wetu hapa kuwasalimia watoto wenzao,lakini pia tumekuwa tukiwahamasisha wanafunzi wetu kuwaomba wazazi wao wawape chochote ili wawapelekee watoto wenzao waliopo katika kituo cha Buhangija”,alieleza Kiondo.
   
  Wanafunzi 81 kuanzia darasa la awali hadi la sita wamefika katika kituo cha Buhangija kuwawakilisha wanafunzi wengine zaidi ya 600 wanaosoma katika shule hiyo.
   
  Shule ya msingi Little Treasures ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri katika mitihani mbalimbali ambapo katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2017 katika kundi la shule zenye watahaniwa pungufu ya 40 imeshika nafasi 1 kati ya 14 katika wilaya ya Shinyanga nafasi ya kimkoa 7 kati ya shule 231 na ya 64 kitaifa kati ya 6839.

  Mlezi wa wanafunzi waliopo katika kituo cha Buhangija Flora Kankutebe akiwakaribisha wanafunzi kutoka shule ya msingi Little Treasures walipotembelea kituo hicho leo Oktoba 26,2017.-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Wanafunzi kutoka shule ya msingi Little Treasures wakijitambulisha kwa kunyoosha mikono 
  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akizungumza wakati wa ziara ya wanafunzi wa shule hiyo walipotembelea kituo cha Buhangija.
   Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiwa na mwalimu wao wakifurahia jambo kwa kupiga makofi katika kituo cha Buhangija
  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
  Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures  wakiwa katika kituo cha Buhangija
  Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiwa katika kituo cha Buhangija
  Kulia ni Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akitambulisha wafanyakazi wa shule ya msingi Little Treasures
  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akiongea na watoto waliopo katika kituo cha Buhangija kabla ya zoezi la ugawaji zawadi
  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akielezea kuhusu zawadi zilizotolewa na wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Little Treasures.Pichani ni zawadi hizo ambazo ni nguo,sabuni,mabegi ya shule,madaftari,kalamu,mchele,sukari
  Wafanyakazi kutoka shule ya Little Treasures wakipanga vizuri zawadi hizo kabla ya zoezi la ugawaji kuanza
  Wanafunzi wa shule ya Little Treasures(kulia),wakijiandaa kugawa zawadi kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
  Wanafunzi wa shule ya Little Treasures wakiwa wamebeba zawadi kabla ya kuanza kukabidhi kwa wanafunzi/watoto wanaolelewa katika katika kituo cha Buhangija
  Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Little Treasures akigawa zawadi ya biskuti kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya msingi Buhangija anayelelewa katika kituo cha Buhangija
  Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Little Treasures akigawa zawadi ya begi la shule
  Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Little Treasures akigawa zawadi ya sabuni
  Zoezi la utoaji zawadi linaendelea
  Zoezi la kugawa zawadi linaendelea
  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo na Msimamizi wa kituo cha Buhangija Seleman Kipanya wakipanda mti wa kumbukumbu katika kituo cha Buhangija
  Mwanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures akimwagia maji mti huo wa kumbukumbu
  Wafanyakazi,Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures na wanafunzi/watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija wakiwa katika picha ya pamoja
  Picha ya kumbukumbu
  Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakijiandaa kupanda kwenye magari ili warudi shule kuendelea na masomo yao
  Moja ya magari ya shule ya msingi Little Treasures ikiondoka katika kituo cha Buhangija.
  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA WOTE WALIOOMBA KUTEULIWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI NGAZI YA MIKOA NA TAIFA

  Kwa Wana Jumuiya wote hususan wale wote walioomba kuteuliwa kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kwenye UVCCM ngazi ya Mikoa na Taifa. Kila mmoja anapaswa kuusoma, kujilinda, kuzingatia, kuufahamu na kuuelewa ujumbe huu muhimu.

  Zipo taarifa za uhakika zenye vielelezo vyenye ushahidi kuwa baadhi ya walioomba nafasi za kuteuliwa kugombea ndani ya UVCCM, wameanza kuitisha vikao vya mizengwe na kufanya kampeni za chini kwa chini kinyume na Kanuni, Taratibu  na mwenendo wetu wa Uchaguzi.

  Ukusanyaji wajumbe kwa maana ya wapiga kura katika eneo ambalo si halali kikanuni na kiutaratibu linatoa tafsiri na kujenga  mazingira ya rushwa pia ukiukaji na uvunjaji wa kanuni  za Uchaguzi za Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi.  

  Ifahamike kuwa uchaguzi huongozwa na Katiba, Kanuni, Taratibu, miongozo na maadili halali hivyo kila mgombea anapaswa kuheshimu taratibu hizo, sambamba na kuheshimu miiko ya uchaguzi. 

  Hadi sasa hakuna mwombaji wa nafasi yoyote aidha wa nafasi ya Mkoa au Taifa aliyeteuliwa jina lake na kuwa mgombea halali. Mamlaka za uteuzi kwa mujibu wa Katiba, Kanuni hazijatangaza majina ya wagombea walioteuliwa kutoka miongoni mwa waomba nafasi waliojaza fomu ndani ya UVCCM.

  Ni kosa na marufuku Kikanuni na Kikatiba kwa muomba nafasi yeyote kuanza kupitapita Wilayani, Mikoani, mitaani, vichochoroni, kuitisha vikao haramu vya kampeni , kujinadi na kujieleza kabla ya ukamilishaji wa mchakato wa uteuzi na majina  kutangazwa.

  Vitendo vyovyote vitakavyofanywa namuombaji wa nafasi aidha kwa kujinadi kwa kuitisha vikao haramu,  kujielezea, kutaja malengo au kuwashawishi wapiga  kura kwa njia ambayo si ya kidemokrasia ni kinyume na taratibu.Ushahidi ukipatikana na  kuthibitika kunaweza kukuondolea sifa ya kuteuliwa katika nafasi uliyoomba.

  Tunaendelea kukumbusha kuwa hatutasita kumchukulia hatua za kimaadili mpambe wa muomba nafasi yoyote atakayebainika anakwenda kinyume na maelekezo haya pamoja na matakwa ya Katiba ya Chama Chama Mapinduzi na Kanuni za UVCCM.

  Hata baada ya vikao vya uteuzi kukamilika mwongozo utatolewa kwa ngazi ya Mkoa hadi Taifa namna ya kufanikisha chaguzi hizo.

  Chama Cha Mapinduzi ni baba na kinara wa demokrasia Tanzania, Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla, chaguzi hizi zinazoendelea ndani ya Chama na Jumuiya zake ni kielelezo tosha cha ukomavu wa demokrasia na kioo kinachoakisi heshima ya Chama na Jumuiya ndani na nje hasa katika kusimamia mambo yake ya msingi ya Kikatiba na Kikanuni.

  Naendelea kuwakumbusha Vijana wote kuendelea kuishi katika maneno ya Usia ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. John Pombe Joseph Magufuli aliyowahi kutuasa wakati chaguzi hizi zikiendelea nanukuu

  Natambua mnaendelea na Uchaguzi ni lazima kuheshimu Katibaya Chama chetu na Kanuni zetu katika mchakato wa kuwapata Viongozi tutakaowapa dhamana. Vijana lazima wachague Viongozi wazuri, wazalendo,waadilifu, wachapa kazi watakaolinda maslahi ya CCM na UVCCM  na simaslahi binafsi kataeni na kupiga vita rushwa kwa nguvu zote na watakaobainika kutoa au kupokea rushwa hatua za haraka zichukuliwe”; Dk. John Pombe Joseph Magufuli.

  Nachukua nafasi hii kwa sauti ya juu kabisa kuwaonya, kuwaasa, kuwakanya na kuwazuia wale wote ambao aidha wanafanya kwa makusudi au kujisahau waelewe kuwa Kanuni ya Uchaguzi iko pale pale na itatenda haki kama msumeno. Vile vile watambue kuwa tunawamulika na kuwafuatilia nyendo zao zote na ikibainika, taarifa zao zitawasilishwa katika vikao kwa hatua zaidi za Kimaadili.

  Ahsanteni 

  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI


  Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
  KAIMU KATIBU MKUU

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa kikao cha kazi na Wakuu wa Idara na Vitengo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa wizara ya Kilimo (Kilimo IV)
  Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao cha kazi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa wizara ya Kilimo (Kilimo IV)
  Kikao kikiendelea
  Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza wakati wa kikao cha kazi kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa (Mb)
   Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) (Kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe wakifatilia kikao cha kazi kilichowakutanisha na Wakuu Idara na Vitengo
  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utafiti Dkt Mansoor Hussein
  Picha ya pamoja Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) (Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe na wakuu wa Idara na Vitengo mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kazi.
  Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Ndg Seushi Mburi akisoma taarifa fupi ya Wizara ya kilimo
  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) akitafakari jambo wakati kikao kikiendelea
  Na Mathias Canal, Dodoma

  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa leo Octoba 26, 2017 amewaagiza watumishi kutofanya kazi kwa mazoea badala yake kuongeza ufanisi katika kazi kwa kuwa wabunifu, na waadilifu.

  Mhe Naibu Waziri ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha kazi alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa wizara hiyo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa wizara ya Kilimo (Kilimo IV), kwa lengo la kufahamiana na kujua majukumu ya kila idara na vitengo.

  Alisema kuwa ili kutimiza adhma ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dokta John Pombe Magufuli katika kuboresha huduma za wananchi ni lazima watumishi kubadili taswira ya kufanya kazi kwa mazoea na kuhamia kwenye kasi ya viwango yakinifu na weledi.

  Mhe Mwanjelwa alisema kuwa Wakuu hao wa Idara na Vitengo wanajukumu kubwa la uwakilishi wa watumishi wenzao 1828 wanaohudumu katika Wizara ya kilimo kote nchini hivyo ili kuwafanya wananchi kubadili mbinu za kilimo kutoka kilimo kwa ajili ya chakula pekee hadi kufikia kilimo kwa ajili ya chakula na biashara ni lazima watumishi wote kuwa wabunifu na kutumia taaluma zao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

  Katika kikao hicho kilichoongozwa na Naibu Waziri Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa Kilihudhuriwa na Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu, Sera na Mipango, Mafunzo, Zana za kilimo, Utafiti na Maendeleo, Usalama wa Chakula, Maendeleo ya mazao na Matumizi bora ya Ardhi.

  Wengine ni Wakuu wa Vitengo; Kitengo cha Fedha na Uhasibu, Kitengo cha Ukaguzi wa ndani, Kitengo cha Habari na Mawasiliano serikalini, Kitengo cha sheria, Kitengo cha Ugunduzi na Ugavi na Kitengo cha TEHAMA.

  “Kubwa na la msingi ambalo ningependa kuwaasa na ninyi kukumbuka kuwa hii ni awamu ya tano  ya kazi na mchakamchaka, hivyo badilisheni Mindset ili tufanye kazi kwa kumsaidia Rais kwa weledi, ubunifu, Maarifa, Juhudi na uzalendo, bado kuna watu wanatembea badala ya kukimbia’’

  “Ni lazima tukimbie lakini uwe mchakamchaka with Quality kwani watu wanaamini katika matokeo chanya, kwahiyo kuanzia sasa ni lazima tukimbizane na kasi ya awamu ya tano kwa kuongeza ufanisi kwenye wizara ya kilimo na business As Usual ni Marufuku” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa

  Mhe Naibu Waziri Dkt Mwanjelwa alisema kuwa wataalamu wanapaswa kutumia utaalamu wao na kuonyesha matokeo chanya kwani kufanya hivyo kutaongeza imani kubwa kwa serikali inayotekeleza ilani ya ushindi ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

  Aliongeza kuwa Kilimo ni uti wa mgongo kwani zaidi ya asilimia 75 ya wananchi ni wakulima ambapo mtaji wake ni nguvu na ardhi hivyo wasiposaidiwa kuboresha kilimo chao na kuongeza uzalishaji ni wazi kuwa Taifa litaendelea kusalia nyuma kimaendeleo.

  0 0

  From far left Smile Tanzania Country Manager Mr Walingo Chiruyi, Smile Group's Executive Director Mr Ahmad Farroukh, Manager of Usage and Retention Mr Eric Mchaki and Smile Tanzania's Chief Commercial Officer Mr Arindam Chakrabarty together cutting the cake to indicate the launching of the best value internet bundles offered by Smile Tanzania.

  Today 27 October 2017, Smile Communications Tanzania (“Smile Tanzania”) brings a new range of data bundles at the lowest data prices with the highest internet data speeds to Tanzanians with ‘Bei ya Ndizi’.

  With Bei ya Ndizi all Tanzanians have access to the lowest data prices with SmileAnytime bundles (daily, weekly and monthly validity), setting a new trend for the best value internet at SuperFast speed over 4G LTE, starting from only Tsh 2,000.

  Smile Chief Commercial Officer, Arindam Chakrabarty says, “It is our endeavour that everyone in Tanzania is able to fully benefit from the internet world and we now bring our customers’ a wider range of data bundles that is more affordable and still offers the fastest internet in Tanzania”.

  He further said that Bei ya Ndizi will see Smile customers being rewarded with BONUS data plus FREE data for Social Media, each time they recharge with SmileAnytime bundles. The FREE data for Social Media gives customers FREE access to Facebook, Instagram, WhatsApp and Twitter.

  Smile, known for championing InternetFreedom in Tanzania, is also introducing new bundles for daily, weekly and monthly use, giving customers more freedom of choice and affordability.

  “Smile’s SuperFast affordable internet service is available in Dar es Salaam, Mwanza, Moshi, Dodoma, Morogoro, Arusha and Mbeya. We’ve reduced our prices that everyone can have the opportunity to experience Smile’s TRUE 4G LTE service and to stay productive and entertained at the fastest data speeds; daily, weekly or monthly.” concluded Mr Chakrabarty.

  Customers in Dar es Salaam, Arusha, Moshi, Mwanza, Dodoma, Mbeya and Morogoro can now experience the fastest, most reliable internet in Tanzania at the best data rates in town and can look forward to further 4G LTE innovations form Smile.


  0 0

   Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Haki Elimu nchini John Kalage akipanda mti katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu jana (Habari Picha Na Pamela Mollel,Arusha)

   Wafanyakazi wa shirika la Haki Elimu nchini wakiongozwa na Mkurugenzi wao John Kalage wa tatu kushoto, wakichimba shimo kwaajili ya kuhifadhi taka ngumu katika shule ya Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii


  Wafanyakazi wa shirika la Haki Elimu nchini wakijiandaa kwenda kupaka rangi madarasa katika shule ya Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii

    Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Haki Elimu nchini John Kalage akipongezwa na Mkuu wa shule hiyo Vitalis Nada mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti katika shule hiyo jana

  Mmoja wa wazazi shuleni hapo akishiriki zoezi la umwagiliaji wa maua katka maadhimisho ya huduma kwa jamii iliyoratibiwa na Shirika na Haki Elimu


  Wafanyakazi wa Haki Elimu wakiwa wananendelea na zoezi la upakaji rangi shule hapo jana

  Aliyeshika ndoo nyekundu ni Abraham Lazaro kutoka  Idara ya Habari na uchechemuzi akiwa na mfanyakazi mwenzake wakiendelea na zoezi la umwagiliaji  katika shule ya sekondari ya mukulati iliyopo Mkoani Arusha katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii
  Mwanafunzi shuleni hapo akiwa amebeba ndoo kwaajili ya kubebea maji kwaajili ya shughuli ya umwagiliaji shuleni hapo jana


  Meneja Idara ya Huduma, fedha na Utawala Daniel Luhamo akichimba shimo la kuhifadhia taka ngumu shuleni hapo


  Mfanyakazi wa Haki Elimu Raphael akiendelee na shughuli ya upakaji rangi


  Rose Mwenda Mmoja wa wafanyakazi wa HakiElimu kutoka Idara ya Ushiriki na Uwajibikaji wa jamii akipaka rangi bati katika shule yaMukulat iliyopo Mkoani Arusha
  Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari  Mukulat Stella Massawe akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa HakiElimu John Kalage, zawadi  iliyotengeneza katika klabu yao ya wanafunzi ya Njoo Tuzungumze

  Mkuu wa Miradi HakiElimu - Boniventura Godfrey akibeba ndoo za kuchotea maji kwaajili ya umwagiliaji


  Baadhi ya wazazi wakisalimia katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na uapandaji wa miti na tunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya mukulati iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu


  Afisa Elimu Taaluma Halmashauri ya Wilaya Arusha Vijijini ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri   akimkabidhi zawadi iliyotolewa na bodi ya shule kwa Mkurugenzi wa Haki Elimu nchini John Kalage kwa kutambua umuhimu wa elimu Nchini

   Picha ya pamoja

  Na Pamela Mollel,Arusha


  Shirika lisilo la kiserikali nchini Haki Elimu limetoa shilingi milioni ishirini ya kuanzishwa kwa ujenzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari mukulat katika kijiji cha lemanyata kata ya lemanyata wilaya ya arusha vijijini ili kuwaondolea adha wanafunzi i wa shule hiyo wanaolazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia muda mwingi  kwakutafuta maji.


  Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na uapandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat Mkurugenzi wa haki elimu nchini john kalaghe amesema shirika la haki elimu limeamua kushirikiana na jamii katika kuondoa changamoto katka sekta ya elimu katika shule hiyo ikiwamo tatitzo la maji pamoja na kuboresha mazingira kwa kupanda miti pamoja na kukarabati majedarasa hayo kwa kupiga rangi.


  Shirika hilo la haki elimu kwa kupitia kwa mkurugenzi huyo wameahidi kutoa ufadhi kwa kuwalipia karo wanafunzi wa shule ya sekondani ya mukulat  watakaofanya vizuri kwa ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani wa kidato cha nne unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine kufanya vizuri katika mitihni hasa kwa mtoto wa kike ambaye anaonekana yuko nyuma kwa mambo ya elimu hasa katika jamii ya kifugaji.


  Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaa ya Arusha vijijini katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii  ,afisa elimu wa wilaya hiyo B akari kimath amelipongeza shirika la haki elimu kwa kuanzisha mradi wa maji katika shule hiyo pamoja na upandaji wa miti na ukarabati wa madarasa na amesema miradi hiyo itapunguza changamoto za elimu zinazozikabili shule za msingi na sekndari wilayani humo na kuliomba shirika hilo kuendela na msaada huo katika shule zilizoko pembezoni mwa wilaya ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora


  Ameiomba jamii kushirikiana na mashirika yasyoyakiserikali kupungumza changamoto  yanaozikabili shule za msingi na sekondari na kuitaka jamii kuhakikisha wanatunza miradi hiyo ili iweze kuwasaidia wanafunzi walikuwa wanapata shida kwa usafuri umbali mrefu kutafuta maji.


  Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha miradi shirika la haki elimu Boniventura Godfrey amesema kwa kutambua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchni tayari wameanzisha mpango maalumu wa kuzisaidia shule za msingi na sekondari 127  katika wilaya ishirini na mbili kwa kuwasaidia miradi ya maji,uwekaji wa umeme wa jua ,ukarabati wa madarsa,na upelekaji wa vifaa vya elimu ili kuwawezesha wanafunzi kuapata elimu katika mzngira bora.  Awali wakizungumzi miradi hiyo wanafunzi wa shule ya sekondari Mukulat  Stella Massawe wamelishukuru shirika la haki elimu kwa uboreshaji wa miundombinu katika shule hiyo kwa kuwa mradi huo wa maji utawapungumzia changamoto iliyokuwa ikiwakabili kwa kusafuri umbali mrefu kwa kutafuta maji pamoj na kutumia muda wa masomo hivyo ,kupungua kwa changamoto hizo kutapunguza suala la utoro kwa wanafunzi. 


older | 1 | .... | 1409 | 1410 | (Page 1411) | 1412 | 1413 | .... | 1896 | newer