Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1408 | 1409 | (Page 1410) | 1411 | 1412 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtunuku Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi cheti cha pongezi na shukrani  katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtunuku Profesa Nehemiah Eliakim Osoro  cheti cha pongezi na shukrani katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtunuku  Mwenyekiti wa Kamati ya Kwanza ya Makinikia Profesa Abdulkarim Mruma     cheti cha pongezi na shukrani  katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtunuku Mama Fatuma Ndugai ambaye ni Mke wa Spika Mhe. Job Ndugai cheti cha pongezi na shukrani katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Katibu wa Bunge Mhe. Stephen Kagaigai baada ya kumtunuku Spika Job Ndugai (kupitia kwa mkewe Mama Fatuma Ndugai) cheti cha pongezi na shukrani  katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtunuku  Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi  cheti cha pongezi na shukrani  katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtunuku Profesa Frolens Luoga cheti cha pongezi na shukrani katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia baada ya kutunuku vyeti vya pongezi na shukrani kwa wajumbe wa Kamati Maalumu za Uchunguzi na Majadiliano kuhusu Rasilimali za madini nchini  katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu baada kutunuku vyeti vya pongezi na shukrani kwa wajumbe wa Kamati Maalumu za Uchunguzi na Majadiliano kuhusu Rasilimali za madini nchini  katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017.
   Mhe Mussa Azzan Zungu, Mwenyekiti wa kamati Maalumu ya Bunge ya kuchunguza  mfumo bora wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa biashara ya Madini ya Almasi   wajumbe wa Kamati Maalumu za Uchunguzi na Majadiliano kuhusu Rasilimali za madini nchini  katika hafla kutunuku vyeti vya pongezi na shukrani kwa wajumbe wa Kamati Maalumu za Uchunguzi na Majadiliano kuhusu Rasilimali za madini nchini  iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017.
   Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry  Ally akiongea katika hafla kutunuku vyeti vya pongezi na shukrani kwa wajumbe wa Kamati Maalumu za Uchunguzi na Majadiliano kuhusu Rasilimali za madini nchini  iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017.
   Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongea katika hafla kutunuku vyeti vya pongezi na shukrani kwa wajumbe wa Kamati Maalumu za Uchunguzi na Majadiliano kuhusu Rasilimali za madini nchini  iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Mwenyekiti wa UDP Mhe John Cheyo katika hafla kutunuku vyeti vya pongezi na shukrani kwa wajumbe wa Kamati Maalumu za Uchunguzi na Majadiliano kuhusu Rasilimali za madini nchini  iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiongea katika hafla kutunuku vyeti vya pongezi na shukrani kwa wajumbe wa Kamati Maalumu za Uchunguzi na Majadiliano kuhusu Rasilimali za madini nchini  iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimkaribisha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi na wageni wengine kupata chakula cha mchana baada ya hafla kutunuku vyeti vya pongezi na shukrani kwa wajumbe wa Kamati Maalumu za Uchunguzi na Majadiliano kuhusu Rasilimali za madini nchini  iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017.
   Gavana wa Benki Kuu mteule Profesa Frolens Luoga
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Serikali imewahakikishia wakazi wa halmashauri ya mji wa nanyamba mkoani Mtwara kuanza kupata huduma ya upasuaji miezi mitatu ijayo kufuatia kuanza ujenzi wa kituo cha afya katika halmashauri hiyo Wakazi wa halmashauri hiyo kwasasa wanalazimika kusafiri kwenda halmashauri ya jirani ya tandahimba au Mtwara jambo ambalo wamekuwa wakilalamikia kwamba linaongeza gharama za matibabu.

  0 0


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo kwa baadhi ya viongozi wa Chama cha Mashua Tanzania (TSAA) wakati alipokutana na viongozi hao kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.
  Mwanyekiti wa Chama cha Mashua Tanzania (TSAA) Bw. Philemon Nasari (kushoto) akimueleza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.

  Mwanyekiti wa Chama cha Mashua Tanzania (TSAA) Bw. Philemon Nasari (kulia) akimkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe DVD yenye matukio mbalimbali ya chama hicho wakati alipokutana na viongozi hao kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (mwwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Mashua Tanzania (TSAA) na maafisa wa Idara ya Michezo wakati alipokutana na viongozi hao kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.

  Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya  katika  kikao cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,(kushoto) Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,DSC_2328
  Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali katika   Wizara ya Afya   wakiwa katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),
  DSC_2331
  Baadhi ya Maafisa  wa Idara mbali mbali katika ya Wizara ya Afya wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akifungua  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,
  DSC_2341
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,
  DSC_2434
  Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dk.Jamala Adam Taib (wa pili kulia) alipokuwa akisisitiza jambo wakati wa kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),
  Picha na Ikulu.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka  kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa unaofanyika  katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma.
   Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI Mhe.Tixon Nzunda  akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka  kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa unaofanyika  katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma. 
   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongela wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa na Taasisi ya Uongozi Institute wanaoendesha  warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka  kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inayofanyika katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma.
   Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI Dk Zainabu  Chaula(kushoto mwenye miwani) pamoja na washiriki wengine wa warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka  kwa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(hayupo pichani) leo mkoani Dodoma.  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki (tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo uliomtembelea ofisini kwake mapema leo .Picha na Ahmad Michuzi-China.
  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies  ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Mohamed Kiluwa (pichani kulia) pamoja na viongozi Waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani wakiongozwa na Katibu Tawala mkoa wa Pwani Zuberi Samataba, mapema leo kwenye Ofisi za Ubalozi huo,Ujumbe huo umewasili mjini Beijing,nchini China kushiriki Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda linalotarajiwa kufanyika mjini humo kesho Oktoba 25,2017 .

  Kongamano hilo kubwa lenye uhamasishaji mkubwa wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,limeandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies na litawashirikisha wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao zaidi ya 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.

  Balozi Kairuki amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies  Mohamed Kiluwa kwa kuonesha juhudi kubwa za kuwahamasisha na kutafuta washirika mbalimbali katika suala zima la uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania.

  Balozi Kairuki amesema kuwa,Kampuni ya Kiluwa kwa kufanya hivyo  wanaibeba dhana ya Tanzania ya Viwanda kwa utekelezaji kwa vitendo,na pia kuunga mkono dhamira ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Viwanda,na kuongeza kuwa yuko tayari kutoa kutoa ushirikiano wa kutoka katika suala zima la kuwahamasisha wawekezaji kutoka nchini China na kwenda kuwekeza nchini tanzania katika suala zima la Viwanda.
  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies, Mohamed Said Kiluwa (pichani kulia) pamoja na Muwakilishi wa baadhi ya viongozi waandamizi wa mkoa wa Pwani,Katibu Tawala mkoa wa Pwani Zuberi Samataba waliofika mjini Beijing,nchini China kushiriki Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda linalotarajiwa kufanyika mjini humo kesho Oktoba 25,2017, Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,litajumuisha wafanyashabiashara, wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao zaidi ya 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.
  Katibu Tawala mkoa wa Pwani Zuberi Samataba akifafanua jambo mbele ya Balozi wa Tanzania nchini China,Mh. Mbelwa Kairuki mapema leo walipokwenda kumtembelea Ofisini kwake,pamoja na kupanga maandalizi ya Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda linalotarajia kufanyika mjini Beijing hapo kesho Oktoba 25,2017. Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies na kuwaalika viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Pwani,wafanyabiashara wakubwa ambao ni wamiliki wa viwanda na makampuni mbalimbali.

  Mkurugezi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Naima Kiluwa akiandika kilichokuwa kikijiri kwenye mazungumzo hayo mafupi na Balozi Mh.Mbelwa Kairuki mara baada ya kuukaribisha ujumbe huo Ubalozini kwake na kuzungumza mambo mbalimbali yaliyohusu masuala ya uwekezaji kwa Tanzania,na baadae kupata chakula cha pamoja.
  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki akimkabidhi zawadi mmoja wa watakaoshiriki Kongamano la Viwanda linalotarajia kufanyika kesho mjini Beijing,likatalojumuisha Wamiliki wa Viwanda,Wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali wapatao zaidi ya 200,anaeshuhudia kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Samataba
  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa 
  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki akimkabidhi zawadi Mkurugezi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Naima Kiluwa 
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa akiwatambulisha baadhi ya washirika wake mbele ya Balozi Kairuki (hayupo pichani),mapema leo mjini Beijing nchini China,wakiwa tayari kwa maandalizi ya Kongamano la Uwekezaji wa Viwanda linalotarajia kufanyika hapo kesho Octoba 25,2017 mjini humo.
  Rais wa wanafunzi wasomao nchini China,Hussein Mtoro akiukaribisha Ujumbe kutoka Serikali ya Mkoa wa Pwani ikiongozwa na Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Samataba pamoja na uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies ukiongozwa na Mohamed Said Kiluwa (njano),walipofika Ofisini kwa Balozi wa Tanzania nchini China,Mh Mbelwa Kairuki,mapema leo mchana .Picha na Ahmad Michuzi-China.

  0 0

   Wafanyakazi wa Benki ya NBC Tawi la Samora wakipozi kwa picha ya pamoja wakiwa katika umbo la moyo ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na ukarimu kwa wateja wao kipindi hii benki yao ikiendelea kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja.
   Mteja wa Benki ya NBC, Neema Xibona (kulia) akionyesha furaha mbele ya wafanyakazi wa benki hiyo Tawi la Samora,  Dar es salaam ambapo sasa NBC inaendelea kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Wafanyakazi hao wanatumia muda wao kuwa karibu na wateja kusikiliza maoni yao kuhusu huduma na changamoto wazipatazo na kuzitafutia ufumbuzi.
   Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbagala, Sady Mwang’onda (kulia), akizungumza na mmoja wa wateja, Elias Kaaya alipofika katika tawi lake kupata huduma.
   Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Kichwele, Frank Mwanga (kushoto), akisalimiana na mmoja wa wateja waliofika katika tawi hilo jijini Dar es Salaam kupata huduma ambapo pia alipata nafasi ya kutoa maoni yake kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo.

   Wafanyakazi wa Benki ya NBC Tawi la Chang’ombe wakirusha maputo pamoja na wateja wao kusherehekea mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo. 
  Meneja wa NBC Tawi la Samora, Faustina Maeda, akimkaribisha Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi (kulia) alipotembelea katika tawi hilo kuangalia ubora wa huduma zinazotolewa kwa wateja na pia alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wateja. 

  0 0

   Askofu Mkuu wa  Jimbo Kuu  Katoliki  la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akiaga  mwili wa Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa mara baada ya Misa iliyofanyika katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam.
    Askofu Mkuu wa  Jimbo Kuu  Katoliki Tabora, Paul Ruzoka akiaga  mwili wa Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa mara baada ya Misa iliyofanyika katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.
    Katibu wa Rais, Ngusa Samike akiaga mwili wa Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa mara baada ya Misa iliyofanyika katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Mapadri nao wakipita mbele kuaga mwili wa Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa mara baada ya Misa katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.
   Jeneza lenye mwili wa marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa likiwa limebebwa na Mapadri wakielekea ndani ya Kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.
   Viongozi mbalimbali, Mapadri, Maaskofu pamoja na waamini wa Kanisa Katoliki wakiwa katika misa ya kumuombea Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Askofu Mkuu wa jimbo Kuu la Dodoma Beatus Kinyaiya akizungumza kabla ya kuaga mwili wa marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa katika kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.
   Askofu Mkuu wa  Jimbo Kuu  Katoliki  Tabora Paul Ruzoka akizungumza katika Misa ya kumuombea Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa katika kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.
   Waumini wa kanisa Katoliki wakiwa katika Ibada ya kumuombea Marehemu katika Kanisa hilo jijini dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Baraza la Maaskofu Tanzania Benard James akizungumza mara baada ya Misa hiyo. Picha na Mpiga Picha wetu.

  0 0

  Frank Shija -MAELEZO
  Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ametoa wito kwa Kampuni na Taasisi mbalimbali nchini kujitokeza kusaidia tasnia ya sanaa ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.
  Wito huo ameutoa leo jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya utiaji saini makubailiano ya mradi wa utambuzi wa sanaa za ufundi na uchoraji (TACIP),mkataba uliosainiwa baina ya Kampuni ya Data Vision International na Shirikisho la sanaa za ufundi na uchoraji (Tafca).
  Naibu Waziri Shonza amesema kuwa mradi huo wa TACIP utasaidia kuwaletea maendeleo wasanii husika kwa kuwa watakuwa wanatambulika kisheria hivyo itakuwa rahisi kwao kupata fursa mbalimbali ndani na nje ya nchi.
  “Mradi huu utawezesha upatikanaji wa masoko ya uhakika ya kazi za sanaa kwani utawaleta wasanii wote pamoja, ambapo wataweza kujadiliana na kutatuaa kero zao kwa pamoja” alisema Mhe. Shonza.
  Aidha Mhe. Shonza alitumia fursa hiyo kuwaponge wabia wote wa mradi huo kwa ubunifu mkubwa waliouonyesha nakuwataka wasanii wa fani zingine waige mfano huo.
  Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi na Uchoraji Tanzania (Tafca) Adrian Nyangamale amesema kuwa mradi huu wa utambuzi wa sanaa za ufundi na uchiraji umekuja wakati muafaka jambo litakalosaidia kulete maendeleo katika tasnia hiyo.
  Amesema kuwa lengo kubwa la kubuni mradi huo ni kuhakikisha kuna kuwa na kanzi data ya wasanii wote wa sanaa za ufundi na uchoraji nchini ili waweze kutambuliwa na mamlaka husika.
  Naye Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Data Vision International William Kihula amesema kuwa kutokana na ukweli kuwa Kampuni yao inajihusisha na masula la ya ukusanyaji wa takwimu,utoaji wa vitambulisho wameona watoe mchango wao kwa tasnii ya sanaa kama jitihada zao za kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano iliyoahidi kupitia Ilani ya uchaguzi kuinua wasainii.
  Aliongeza kuwa Data Vision watahakikisha mradi huu wa Jitambue,Tambulika, Inalipa unafanikiwa kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau ambao ni wasanii wa sanaa za ufundi na uchoraji.
  Data Vision ni Kampuni inayijishugulisha na masuala ya ICT, UTAFITI, Vitanmmbulisho ambapo limekuwa likifanya kazi kwa karibu zaidi na Serikali kwa takribani miaka 20 sasa limeamua kugeukia sekta zisizo rasmi ili kuweza kutoa mchango wake.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza (aliyesimama katikati) akishuhudia Utiaji Saini wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Shirikisho la Sanaa za Ufundi (TAFCA) na Kampuni ya Data Vision International 24 Oktoba, 2017 Jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiongea na wadau wa Sanaa na Ufundi wakati wa Hafla ya Utiaji Saini wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Shirikisho la Sanaa za Ufundi (TAFCA) na Kampuni ya Data Vision International 24 Oktoba, 2017 Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sanaa za ufundi pamoja watendaji wa Kampuni ya Data Vision International mara baada ya kukamilisha Hafla ya Utiaji Saini wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Shirikisho la Sanaa za Ufundi (TAFCA) na Kampuni ya Data Vision International 24 Oktoba, 2017 Jijini Dar es Salaam. 
  PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride maalum katika sherehe ya Siku ya Umoja wa Mataifa ambapo Umoja huo umetimiza miaka 72 tangu kuanzishwa kwake na sherehe hizo zilifanyika kwenye viwanja vya Karimjee kwenye sherehe za kutimiza miaka 72 ya Umoja wa Mataifa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye sherehe ya siku ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Ndugu Alvaro Rodriguez mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Karimjee kwenye sherehe za kutimiza miaka 72 ya Umoja wa Mataifa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Dunia wa Wanawake kuhusu masuala ya Benki uliofanyika kwenye hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker (kulia) mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Dunia wa Wanawake kuhusu masuala ya Benki uliofanyika kwenye hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. 

  0 0


  Mwenyekiti mweza wa mkutano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akielezea kuhusu umuhimu wa majadiliano katika kutatua changamoto za kibiashara nchini, mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Godfrey Simbeye akifafanua jambo kwa wafanyabiashara waliohudhuria katika Mkutano kati yao na Serikali uliolenga kujadili mafanikio na changamoto za pande hizo mbili, uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza na wafanyabiashara Jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa kupeleka taarifa za changamoto zao Serikalini ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia) akifuatilia majadiliano kati ya Sekta Binafsi na ya Umma yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam lengo likiwa kutatua changamoto mbalimbali.

  Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde (Mb) wakibadilishana mawazo wakati wa Mkutano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi.

  Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Bw. Salum Shamte akishukuru juhudi za Serikali katika kuzileta pamoja Sekta binafsi na ya umma, wakati wa Mkutano kati ya Sekta hizo mbili Jijini Dar es Salaam.

  Baadi ya Wafanyabiashara Jijini Dar es Salaam wakifuatilia Mkutano kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliolenga kutatua changamoto za Sekta hizo ili kuharakisha ukuaji wa uchumi.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa pili kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Sera kutoka Wizara hiyo Bw. Shogholo Msangi na wafanyabiashara wakifuatilia maelezo kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) kuhusu umuhimu wa majadiliano katika kujenga uchumi wenye tija kwa Sekta Binafsi na ya Umma.

  Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb) akizungumza kuhusu namna Serikali ilivyojipanga katika kutatua tatizo la Nishati ya umeme ili kuweza kuchochea uchumi wa Viwanda wakati wa Mkutano kati ya Sekta Binafsi na Umma uliofanyika Jijini Dar es Salaam.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango
  …………….
  Sekta Binafsi imetakiwa kuwasiliana moja kwa moja na Serikali ili kutatua changamoto zinazoikabili badala ya kupitia wadau wa nje kwanza, kwa kuwa mlango wa Serikali uko wazi kwa ajili ya majadiliano na kutatua matatizo ya Sekta hiyo.
  Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) katika Mkutano na Sekta Binafsi nchini (TPSF), Jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mpango amesema kuwa ni vema Sekta Binafsi ikashirikiana na Sekta ya Umma kwa kuwa zote zinategemeana na hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa na Sekta Binafsi ambayo ni imara.
  “Sekta Binafsi na Sekta ya Umma hazina budi kufanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu, tena kwa kuaminiana kwa faida ya Sekta zote mbili na kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla” aliongeza Dkt. Mpango.
  Amesema kuwa, lengo la pande zote mbili ni kuharakisha utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuongeza fursa za ajira, kipato cha mwananchi na kuondokana na umasikini uliokithiri kwa kujenga Tanzania inayoongozwa na uchumi wa Viwanda.
  Dkt. Mpango alifafanua kuwa Serikali imeendelea kuyafanyia kazi mapendekezo mengi yaliyotolewa na Sekta Binafsi ikiwemo katika kuboresha mazingira ya biashara nchini ikiwemo kuondoa baadhi ya kodi zilizokuwa kero kwa wafanyabiashara.
  Baadhi ya hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Serikali kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kumpa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Fedha mamlaka ya kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani bila kuhusisha utaratibu wa kulipa kwanza Kodi ya Ongezeko la Thamani na baadaye kuomba kurejeshewa (Refund) kwenye miradi inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo (Grants) au mikopo yenye masharti nafuu (Concessional Loans) ambayo mikataba husika ina masharti ya kutoa msamaha wa kodi hiyo.
  “Hatua hii itawezesha wakandarasi wanaotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini kutopata tena usumbufu katika kutekeleza miradi hiyo na miradi kutekelezwa kwa muda uliopangwa” alisema Dkt. Mpango
  Ili kuvutia uwekezaji katika sekta za viwanda, kilimo cha mazao na mifugo nchini, Serikali imesamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa za mtaji (capital goods) za viwanda vya mafuta ya kula, nguo, ngozi, madawa ya binadamu na mifugo ili kupunguza gharama za ununuzi/uagizaji wa mashine na mitambo watakayonunua wawekezaji kwa ajili ya kusindika na kutengeneza bidhaa mbalimbali.
  “Serikali sasa inatoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kiwango cha asilimia sifuri katika huduma zinazotolewa kwenye usafirishaji wa bidhaa/mizigo nje ya nchi (ancillary transport services), hatua itayopunguza gharama za usafirishaji katika bandari zetu na kuifanya Tanzania kuwa njia bora zaidi ya kupitisha bidhaa zinazotoka nje ya nchi kwenda nchi nyingine hususan zisizo na bandari.
  Kwa upande wa hali ya Uchumi, Waziri Mpango amesema kuwa robo ya kwanza ya mwaka 2017, uchumi ulikua kwa asilimia 5.7, robo ya pili ulikua kwa asilimia 7.8, hivyo kufanya nusu ya kwanza uchumi kukua kwa asilimia 6.8.
  Baadhi ya shughuli za kiuchumi zilizokuwa kwa kasi ni usafirishaji na uhifadhi wa mizigo ambao umekua kwa asilimia 19.8, uchimbaji madini na mawe asilimia 18.0, uzalishaji viwandani asilimia 9.3 na ujenzi asilimia 8.8.
  Dkt. Mpango alisema Sekta ya Benki kwa ujumla imeendelea kuwa imara ikiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha juu ya viwango vinavyokubalika kisheria. Kwa kipindi cha mwaka  2009 hadi 2017 huduma jumuishi za fedha zimeongezeka kutoka  asilimia 15.8 hadi asilimia 65.3. Upatikanaji wa huduma za kifedha umeongezeka kutoka asilimia 29 kwa mwaka 2009 hadi asilimia 86 kwa mwaka 2017.
  Aidha kwa upande wa mikopo kwa Sekta Binafsi ilipungua kutokana na Benki kuchukua tahadhari kutokana na kuongezeka kwa mikopo chechefu (Non-performing loans) ambapo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilichukua hatua kwa kupunguza kiwango cha amana ambacho benki za biashara zinatakiwa kuhifadhi Benki Kuu kama dhamana kutoka asilimia 10 hadi asilimia 8 na riba za mikopo ya benki hizo kushuka kutoka asilimia 16 hadi 12.
  Naye mwenyekiti mwenza wa Mkutano huo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (Mb) amesema kuwa njia bora ya kutatua matatizo ya Sekta Binafsi ni kuendelea kufanyika kwa majadiliano yenye tija.
  Mmoja wa wajumbe wa Mkutano huo wa wafanyabiashara ambaye ni wakili wa kujitegemea Bi. Eve Hawa Sinare amesema kuwa ni vema kuangalia mfumo mzuri wa kuweka riba unaofanywa na Benki za biashara ili kuwa na uwiano mzuri.
  Vilevile Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Bw. Salum Shamte ameishukuru Serikali kwa kuonesha nia ya dhati ya kushirikiana na Sekta hiyo kwa lengo la kufanikisha ukuaji wa uchiumi wa Viwanda.
  Waziri mpango amewahakikishia wafanyabiashara kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha kuna majadiliano ya mara kwa mara na wadau hao ili kutatua changamoto zao na pia ameahidi kuandaa Mkutano mwingine ambao utajikita katika masuala ya kodi kabla ya Sekta Binafsi kuwasilisha mapendekezo ya kodi.
  Mkutano huo wa Sekta Binafsi na Umma ni wa pili kufanyika, kwa mara ya kwanza Mkutano kama huo ulifanyika tarehe 11 Aprili, 2017 mjini Dodoma ambapo  ulisaidia kutatua changamoto nyingi ikiwemo kusaidia kuongezeka kwa ufanisi katika huduma za bandari nchini.
  Imetolewa na: Benny Mwaipaja

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Kazi, Ajira,Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati) akifurahia kitendo cha Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uuzaji Mafuta ya Puma, Philippe Corsaletti (kushoto) akibadilishana hati za mkataba  wa hiari uboreshaji hali bora za Wafanyakazi wa kampuni hiyo na Mkuu wa  Kitengo cha Biashara cha TUICO, Jonathan Peres wakati wa hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Puma, Dar es Salaam leo.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati) akishuhudia  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uuzaji Mafuta ya Puma Energy, Philippe Corsaletti (kushoto) na Mkuu wa  Kitengo cha Biashara cha TUICO, Jonathan Peres wakitiliana saini mkataba  wa hiari uboreshaji hali bora za Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Puma, Dar es Salaam leo.
   Baadhi ya Wafanyakazi na wanahabari wakishuhudia tukio hilo

   Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Kampuni ya Puma, Raymond Tungaraza akitoa shukrani kwa Uongozi wa Puma kwa kukubali mabrosho hayo kwa wafanyakazi ambao hivi sasa kima cha chini kitaanzia sh. mil. 1, Puma italipia ada za watoto wa wafanyakazi sh. 900 Shule ya msingi,  Mil. 1.2 Sekondari na Mil. 1.5 sekondari pia inawalipia wafanyakazi Bima ya Maisha.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati) akizungumza jambo na   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uuzaji Mafuta ya Puma, Philippe Corsaletti.

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama akihutubia wakati wa hafla hiyo, ambapo aliagiza waajiri wote kuiga mfano wa Puma kwa kuingia mikataba ya hiari na wafanyakazi.

   Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Aggrey Mlimuka akizungumza wakati wa hafla hiyo
  Meneja Rasilimali Watu wa Puma, Loveness Hoyange akielezea kwa ufupi kuhusu makubaliano ya mkataba huo


  Mwandishi Wetu
  KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania, imetiliana sahihi mkataba wa hiari kati yake na Chama cha wafanyakazi Tanzania (Tuico) huku Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu), Jenista Mhagama akipongeza hatua hiyo na kuzitaka kampuni zingine kuiga mfano huo.

  Akasisitiza kuwa Kampuni ya Puma kutokana hatua hiyo na historia yao kati ya uongozi na wafanyakazi, ameridhika na namna ambavyo wanashirikiana katika masuala ya kulinda maslahi kazini.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam jana Makao Makuu ya Puma Energy Tanzania, Waziri Mhagama alisema kampuni hiyo ameiondoa kwenye orodha ya kampuni zenye migogoro kati ya menejimenti na wafanyakazi.

  “Puma mnastahili pongezi kwa hatua hii ambayo mmeifanya, kwetu Serikali tumefarijika sana na tunaunga mkono juhudi hizi.Pia nasi ni sehemu ya kampuni hii kutokana na umiliki wa hisia wa asilimia 50 kwa 50, hivyo kila mnachokianya na kuleta mafanikio nasi serikali ni sehemu ya ufanikishaji huo.

  “Tunaamini kwa maboresho ambayo mmeyafanya kwenye kuangalia maslahi ya wafanyakazi wenu ni jambo muhimu na jema kwa nchi yetu.Tunaamini wakanyakazi wakiwa salama kazini na kupata stahiki zao inaleta tija na ufanisi na matokeo uchumi wa nchi kukua,”alisema Waziri Mhagama.

  Aliisifu pia hatua ya kwamba kampuni hiyo imefikia makubaliano kati yake na wafanyakazi kuwa kuanzia mwakani  kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wake kitakuwa Sh. milioni moja huku pia ikilipa ada za shule  ya msingi, sekondari na Chuo Kikuu kwa wale ambao watakuwa  wakisomesha watoto zao katika shule hizo.

  Alisema kwa niaba ya Serikali anakumbusha waajiri wote nchini kutafuta suluhu ya migogoro kwani anaamini kila kampuni, taasisi au shirika kuna vyama vya wafanyakazi na wanaoshindwa kufanya hivyo wanakiuka sheria za kazi.

  Awali Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti alisema wamefikia hatua hiyo muhimu katika uendeshaji wa shughuli zake hapa Tanzania kwa kufanya mapitio na kusaini mkataba wa hiari kati yake na chama cha wafanyakazi ambacho kiliwakilisha wafanyakazi.

  “Mkataba huu wa leo unachukua nafasi ya ule uliokuwepo. Na ambao umebaki katika kutekelezwa kwa viwango vyote hadi sasa. 

  “Jambo la muhimu sana la kufahamu ni kwamba kwa nyakati zote za makubaliano, mazungumzo yamekua yakifanyika katika hali ya utulivu, kuaminiana na katika mazingira rafiki,”alisema.  

  Alifafanua makubaliano ya mwaka huu yametiwa sahihi na kushuhudiwa na Waziri Mhagama ambapo Puma Tanzania ilianza uwepo wake hapa Tanzania mwaka 2011 baada ya kuchukua hisa zilizokua zikimilikiwa na kampuni ya BP.
  Alisema kwa sasa kampuni inamilikiwa kwa pamoja kati ya Puma Group kwa asilimia 50 na Serikali ya Tanzania asilimia 50.


  “Wafanyakazi wetu ndio moyo wa biashara yetu na ningependa kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa utendaji wao wa pekee na kujitoa pasipo kuchoka katika kuifanya Puma Energy kuwa kampuni ya kiwango cha kimataifa” alisema Corsaletti.

  Alisema kampuni ya Puma inajivunia mahusiano maalumu na kuaminiana ambako kumejengeka kati ya wafanyakazi pamoja na chama ambako kumewezesha maboresho katika maeneo mbalimbali.

  Alitaja baadhi ya maeneo hayo ni kuboresha mahusiano na wafanyakazi kupitia uwazi na kujifunga kwa kusaini mkataba wa hiari (CBA) ambapo tumeboresha baadhi ya mahitaji ya kisheria  ya sheria za kazi pamoja na kanuni zake.

  Pia Puma Tanzania imekua moja ya kampuni zinazotimiza sheria pamoja na kanuni mahali pote tunapofanya kazi na mfano mwaka huu Puma imepewa tuzo kutoka PPF kwa kuwa mshindi wa pili katika kulipia wafanyakazi wake michango yao ya akiba.

  Aliongeza Kuhakikisha wafanyakazi wake wanatenda kazi katika kiwango cha juu cha ubora katika masuala ya Afya usalama na mazingira na kutimiza viwango vya kimataifa vya usalama. 

  “Kwa sasa Puma Tanzania ni kampuni pekee katika kampuni za mafuta ambayo imetimiza vigezo na kupewa cheti cha ubora wa bidhaa cha kimataifa (ISO 9001-2008) na cheti cha ubora wa mazingira cha kimataifa (ISO 14001-2004),”alisema.
  Pia imejizatiti katika kuwaendeleza wafanyakazi wake kupitia mfumo wa mafunzo na uendelezaji kazini ambapo kampuni hutumia takribani Sh. milioni 200 kwa mwaka katika mafunzo na uendelezaji.

  Eneo jingine Puma Tanzania pia imejizatiti katika kujenga uwezo na kutengeneza fursa kwa vijana kupitia mpango wake wa uendelezaji wa wahitimu wa vyuo vikuu ambapo kila mwaka tunaajiri hadi vijana watano na kuwabakisha wale wanaoonesha bidii katika utendaji.

  “Mkataba wa hiari wa mwaka 2017 umeboresha mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuongeza ada za shule kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi kuanzia shule za Msingi hadi Chuo Kikuu ambapo wafanyakazi wenye watoto wanapewa kiasi cha Sh 900,000 kwa shule za Msingi, Sh milioni 1.2 wa shule za sekondari,

  “Na Sh. milioni 1.5 kwa vyuo vikuu. Malipo haya hulipwa moja kwa moja katika akaunti ya mfanyakazi kila mwezi Desemba ili kusaidia katika malipo ya ada za shule,”alisema.

  Corsaletti alisema kuwa wameboresha Bima ya maisha pamoja na malipo yanayofanywa na mfuko wa serikali wa kulipa fidia kwa wafanyakazi na  utaratibu wa kampuni wa kutoa matibabu bure kwa wafanyakazi na familia zao, kila mfanyakazi anakatiwa bima ya  maisha kila mwaka ili kuisaidia familia endapo kutatokea kifo cha mfanyakazi akiwa kazini ambapo ni sawa na mshahara wa miaka mitatu.

  “Kuongeza alawansi zaidi kwa wafanyakazi wanaofanya kazi nje ya muda kama vile malipo ya kuitwa kazini baada ya saa za kazi, malipo ya usiku n.k.

  “Mwaka 2016, Puma Tanzania ilishinda tuzo kutoka katika umoja wa waajiri Tanzania (ATE) kama mwajiri bora katika kundi la mahusiano na wafanyakazi. Hii ni mfano mmoja tu kuonyesha namna ambavyo tumejizatiti katika kuimarisha mahusiano na wafanyakazi wetu.

  “Tutaendelea kushirikiana bega kwa bega pamoja na wizara yako, chama cha waajiri, chama cha wafanyakazi, pamoja na wafanyakazi wetu katika kuhakikisha kwamba tunatengeneza mazingira tulivu ya kazi kwa watu wetu,”alisema  Corsaletti.

  0 0

   Warembo wa shindano la kumsaka Miss Vyuo Vikuu 2017, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mazoezi yao ya pamoja katika Ukumbi wa Maisha kujiandaa na shindano lao linalotarajia kufanyika Ijumaa ya wiki hii kwenye Uwambi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO BLOG)
   Warembo wa shindano la kumsaka Miss Vyuo Vikuu 2017, wakiwa katika mazoezi ya Shoo yao ya pamoja katika Ukumbi wa Maisha kujiandaa na shindano lao linalotarajia kufanyika Ijumaa ya wiki hii kwenye Uwambi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es Salaam. Picha na Mafoto Blog
   Warembo wakisikiliza maelekezo ya shoo kutoka kwa mwalimu wao
   Mkuu wa Itifaki na Nidhamu wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye, akizungumza na warembo wa shindano la Miss Vyuo Vikuu 2017, wakati alipowatembelea kwenye Kambi yao ya mazoezi ya kujindaa na shindano hilo linalofanyika Ijumaa wiki hii kwenye Ukumbi wa King Solomon Namanga.
   Warembo wa shindano la kumsaka Miss Vyuo Vikuu 2017, wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja katika Ukumbi wa Maisha kujiandaa na shindano lao linalotarajia kufanyika Ijumaa ya wiki hii kwenye Uwambi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es Salaam. 
  Warembo wa shindano la kumsaka Miss Vyuo Vikuu 2017, wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja katika Ukumbi wa Maisha kujiandaa na shindano lao linalotarajia kufanyika Ijumaa ya wiki hii kwenye Uwambi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO BLOG)

  0 0

  Askofu wa jimbo la mbinga ASKOFU JOHN NDIMBO leo ameongoza mapokezi ya kuupokea mwili wa hayati askofu CASTOR MSEMWA aliyefarika dunia tarehe 19.10.2017 saa saba mchana ana amzishi yake yatafanika hapo kesho katika jimbo la MASASI TUNDURU mkaoni RUVUMA ,Akofu CASTOR MSEMWA ALIZALIWA TAREHE 13.02.1955 katika kijiji cha KITULIRA WIALAYANI NJOMBE .

  0 0


  0 0

  Baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo maarufu wamachinga na waendesha pikipiki maarufu kama waendesha bodaboda waliokusanyika katika viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.
  Msanii Sholo Mwamba akitoa burudani kwa wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo maarufu wamachinga na waendesha pikipiki waliokusanyika katika viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.
  Mwakilishi wa wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo maarufu wamachinga Bw.Namoto Yusuf Namoto akisoma risala ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.
  Mwakilishi wa waendesha pikipiki Wilaya ya Ilala Bw. Athanas Kitime akitoa salamu za waendesha bodaboda kwa Mgeni Rasmi, Waziri wa Madini Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo maarufu wamachinga na waendesha pikipiki wakimpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.
  Mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo maarufu wamachinga Bw. Steven Lusinde (kulia) na Mwakilishi wa waendesha pikipiki maarufu kama waendesha bodaboda Bw. Athanas Kitime wakimkabidhi risala Mgeni Rasmi, Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo na waendesha pikipiki wakimpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.

  Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azan akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo na waendesha pikipiki waliokusanyika katika viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo na waendesha pikipiki waliokusanyika katika viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.
  Mgeni Rasmi, Waziri wa Madini Angellah Kairuki akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo maarufu wamachinga na waendesha pikipiki waliokusanyika katika viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.

  Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akijitambulisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitazama vitabu alivyokabidhiwa na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akiwa amesimama wakati wa nyimbo za Mataifa ya China na Tanzania zikipigwa katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Uholanzi hapa nchini Jeroen Verheul Ikulu jijini Dar es Salaam.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Uholanzi hapa nchini Jeroen Verheul mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Oman hapa nchini Ali Al Mahruqi Ikulu jijini Dar es Salaam
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Oman hapa nchini Ali Al Mahruqi Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Oman hapa nchini Ali Al Mahruqi Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Oman hapa nchini Ali Al Mahruqi akiwa amesimama wakati wa nyimbo za mataifa mawili ya Oman na Tanzania zikipigwa mara tu baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

  PICHA NA IKULU.
   

  0 0


  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akiwaeleza jambo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka katika eneo la kuchukua mizigo baada ya kuwasili.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (aliyenyoosha mkono), akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa nne kulia) wakiwa kwenye eneo la abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi.
  Bw. Kaanankira Mbise, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhamiaji Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akieleza namna abiria anavyopata huduma ya viza mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), huku Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) akisikiliza kwa makini.

  …………………

  TBIII kutumia e-visa

  Na Mwandishi Wetu

  JENGO la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) linalotarajiwa kukamilika Desemba 2018, litafungwa mfumo wa huduma ya viza kwa njia ya mtandao (e-visa), ambao utarahisha na kuharakisha upatikanaji wake.

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhamiaji cha JNIA, Bw. Kaanankira Mbise amemwambia jana Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye alipotembelea eneo la uombeaji viza kwa abiria wa kimataifa wanaowasili, kuwa wanatarajia kutumia huduma hiyo ambayo ni rahisi na haraka.

  “Tayari mkakati umeanza wa kuanzisha huduma hii ya e-visa hivyo tukifanikiwa utafungwa katika jengo hili jipya, ambapo itasaidia kwa abiria kuipata huduma hiyo kwa haraka kwani itatumia mtandao,” amesema Bw. Mbise.

  Hata hivyo, Bw. Mbise amesema kwa sasa wameboresha huduma hiyo kwa wasafiri wanaowasili katika jengo la pili la abiria (JNIA-TBII) , ambapo tayari wamepatiwa mashine nne za kisasa zinazosaidia kupunguza msongamano wa abiria wenye kuhitaji huduma hiyo, hususan kipindi cha mchana chenye ujio wa ndege nyingi za nje ya nchi.

  “Hizi mashine zimeharakisha upatikanaji wa huduma kwani tumeweza kuhudumia abiria wengi kwa wakati mmoja, na msongamano umepungua kiasi tofauti na awali mashine zilikuwa chache.” amesema Mbise.

  Naye Mhe. Mhandisi Nditiye amesema baada ya ziara yake amegundua mashine za viza ni za muda mrefu na zinahudumia abiria mmoja kwa mrefu, na tayari ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuwasilisha kwa maandishi mapendekezo yao ya namna ya kuharakisha huduma hiyo, ili serikali iyafanyie kazi kwa kusaidia kuondoa kero hiyo.

  “Nimegundua kuna baadhi ya mashine za viza zimeongezwa lakini pia zilizopo zimechoka kwani ni za muda mrefu na zinahudumia abiria mmoja kwa muda mrefu na hii inaharibu sifa ya kiwanja chetu kwa wageni wanaokuja hapa nchini,” amesema Mhandisi Nditiye.

  Hata hivyo, amesema wanampango wa kuongeza madirisha ya benki yanayolipia viza hizo ili kuharakisha huduma hiyo, ambapo sasa ni machache kulinganisha na idadi kubwa ya abiria wanaowasili kwa ndege kubwa. Ndege hizo ni Emirates, Etihad, Oman Air, Qatar, South Africa Air na Ethiopia, ambazo zimekuwa zikipishana kwa muda mfupi.

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa TAA, Richard Mayongela amesema tayari wanampango wa kuongeza upana wa eneo hilo la wasafiri wanaowasili wa kimataifa, ambapo sasa kumekuwa na msongamano kutokana na ufinyu wake.

  “Hili jengo linazaidi ya miaka 30 na ukiangalia abiria waliokuwa wamekadiriwa wakati ule lilikuwa likikidhi mahitaji, lakini sasa abiria wameongezeka na eneo limekuwa dogo, hivyo tayari tumeanza kwa kuondoa baadhi ya ofisi ili kuongeza upana wake, ninaimani litapunguza msongamano uliopo sasa,” amesema Bw. Mayongela.

  Lakini pia Bw. Mayongela amesema sasa wapo katika mazungumzo na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), ili kuangalia namna bora ya kuzipangia muda ndege zinazopishana muda mdogo kwa wakati wa mchana ili ziachiane muda mrefu, ambapo kutasaidia kupunguza msongamano

  Awali eneo hilo linakumbwa na changamoto kubwa ya msongamano wa abiria wanaohitaji huduma ya viza baada ya uchache mashine zinazosimamiwa na Idara ya Uhamiaji zilizokuwepo na kufanya abiria wanaohitaji huduma hiyo kutumia muda mrefu kuipata.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,wa pili kushoto ,katibu tawala wilaya ya Kibaha Sozi Ngate wa kwanza kulia ,pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Leonard Mloe wa pili kutoka kulia ,wakiwa wameshika tuzo ya kuwa wa kwanza katika ufungaji wa mahesabu ya serikali kati ya halmashauri zote nchini mwaka 2014/2015  iliyopatiwa halmashauri hiyoIMG_20171024_121805
  Mkuu wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akipatiwa maelezo na kuonyeshwa ramani ya ujenzi wa kituo cha mabasi cha kisasa kinachojengwa eneo la CBD mjini Kibaha itakavyokuwa na uwezo wa kuhudumia mabasi 60 kwa wakati mmoja ,na kugharimu bil.3.4 wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kutembelea baadhi ya miradi iliyopo katika halmashauri ya Mji wa Kibaha.
  Picha na Mwamvua Mwinyi
  ……………
  Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
  HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha,mkoani Pwani,imewachukulia hatua ya kinidhamu kwa kuwafukuza kazi watumishi 28 kwa makosa ya utoro kazini,kughushi vyeti na upotevu wa mali za halmashauri.
  Aidha halmashauri hiyo ,inakabiliwa na upungufu wa watumishi 164,ambapo uhaba mkubwa upo katika idara ya utawala ,maji na afya.
  Licha ya upungufu huo,halmashauri hiyo imekua ya kwanza katika ufungaji wa mahesabu ya serikali kwa mwaka 2014-2015 kati ya halmashauri 186 nchini.
  Hayo aliyasema katibu tawala wa wilaya ya Kibaha,Sozi Ngate kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo,wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya halmashauri hiyo katika ziara ya siku moja ya mkuu wa mkoa wa Pwani,:’Alipotembelea baadhi ya miradi ikiwemo kituo cha mabasi cha kisasa kitakachogharimu bilioni 3.4 na ujenzi wa jengo la halmashauri hiyo.
  Sozi alisema ,kati ya watumishi waliofukuzwa kazi ni pamoja na walimu 20,watendaji watatu,tabibu wawili,katibu muhtasi ,afisa ardhi na daktari mmoja.
  Hata hivyo alieleza,ili kukabiliana na upungufu wa watumishi halmashauri inategemea kuajiri watumishi 73 ambao mishahara yao imetengwa na ofisi ya rais –utumishi na wizara ya fedha na mipango kwa mwaka 2017/2018.
  Akielezea zoezi la uhakiki wa vyeti vya elimu,,Sozi alieleza ulifanyika kwa watumishi wote 1,529 ambapo watumishi 73 wameondolewa kwa kukutwa na vyeti feki.
  “Kwa upande wa uhakiki wa watumishi hewa ulianzia machi 2016 hadi april,jumla ya watumishi 20 waligundulika ni watumishi hewa na jumla ya fedha mil 19.161.557 ziliokolewa”alifafanua Sozi.
  KATIKA HATUA NYINGINE,akizungumzia kuhusu ukusanyaji wa mapato ya halmashauri hiyo ,alisema wanaendelea kusimamia ukusanyaji huo .
  Sozi alisema mwaka 2016-2017 halmashauri ilikadiria kukusanya zaidi ya sh.bil.3.954.4 katika vyanzo vya ndani na makusanyo halisi hadi kufikia juni 30 mwaka huu ilifanikiwa kukusanya sh.bil.3.671.950.5 sawa na asilimia 93.
  Mwaka 2017-2018 halmashauri ya mji huo imekisia kukusanya sh.bil.3.705.549 ambapo mapato halisi hadi septemba 30 ,2017 imekusanya sh.bil.1.431.090.552 sawa na asilimia 38.6 ya makisio.
  “Tusipojisifu wenyewe hakuna wa kutusifia,tujipongeze halmashauri yetu imekuwa ya kwanza katika ufungaji wa mahesabu ya serikali kwa mwaka 2014-2015 kati ya halmashauri zote nchini ,
  VIWANDA….Halmashauri ya mji Kibaha inaendelea kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji ambapo katika robo ya kwanza ya 2017/2018 imeweza kutumia mil.100 kufungua barabara eneo la viwanda Zegereni na inaendelea kupokea maombi ya wawekezaji.
  Sozi alielezea,mji huo una jumla ya viwanda 119 vinavyofanya kazi kati ya hivyo vikubwa ni vitano,vya kati 16 na vidogo 98 huku viwanda vinne vinaendelea kujengwa .HATA HIVYO ,kuhusu soko jipya la Mnarani (Loliondo)alisema zimeshawekwa taa na wameshatenga eneo la kujengwa kituo cha polisi .
  MKUU WA MKOA WA PWANI,mhandisi Evarist Ndikilo ,aliipongeza halmashauri hiyo kwa jitihada mbalimbali wanazozifanya kimaendeleo.Alisema anaendelea kufuatilia maombi ya halmashauri hiyo ya mji kuwa manispaa ambayo yalishayapelekwa TAMISEMI .
  Mhandisi Ndikilo alisema ,mji huo unakua siku hadi siku,huduma za kijamii zinaongezeka,idadi ya watu imeongezeka hivyo vigezo vya mji kuwa manispaa vimeshafikiwa.“Mkoa wa Pwani unaongoza katika kukuza uchumi wa viwanda ,nawaombeni tuongeze jitihada kuboresha miundombinu ya maji,barabara na umeme kuvutia wawekezaji zaidi ya sasa”alifafanua mhandisi Ndikilo.
  Mhandisi Ndikilo,aliitaka halmashauri hiyo kuweka ulinzi kwenye soko la Mnarani ili kulinda mali zao sokoni hapo.Alisema kuna kila sababu ya kuweka mikakati ya muda mrefu na mfupi ikiwemo kufanya doria za mara kwa mara usiku kwa ajili ya ulinzi, kuwasaidia watu na mali zao.
  Katika ziara yake mhandisi Ndikilo,alitembelea ujenzi wa jengo la ofisi za halmashauri hiyo na kituo cha mabus kipya kinachojengwa eneo la CBD kitakachogharimu bilioni 3.4 hadi kukamilika.
  NAE meneja wa kampuni ya Group Six International Ltd ,inayojenga kituo cha hicho ambayo ilijenga stendi ya kisasa ya Msamvu mkoani Morogoro,mhandisi Chen Xlong ,alisema ujenzi umefikia asilimia 45.
  Alisema licha ya kuwa nyuma kidogo ya wakati katika kukamilisha ujenzi huo lakini wanatarajia kukamilisha ujenzi huo desemba mwaka huu.
  Stendi hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia mabasi 60 kwa wakati mmoja na inajengwa kwa ufadhili wa bank ya dunia kupitia fedha za ruzuku kwenye mradi wa uendelezaji wa miji (ULGSP) unaoendeshwa kwenye miji 18 hapa nchini ikiwemo Mji wa Kibaha.

older | 1 | .... | 1408 | 1409 | (Page 1410) | 1411 | 1412 | .... | 1898 | newer