Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 139 | 140 | (Page 141) | 142 | 143 | .... | 1897 | newer

  0 0


  0 0

   Afisa Uhusiano toka Mfuko wa Pensheni wa PPF Lulu Mengele (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari  mafanikio ya mfuko na aina za mafao ambazo  mfuko inatoa kwa wanachama wake, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi Kawawa.

   Meneja Uratibu Ofisi za Kanda toka Mfuko wa Pensheni wa PPF Mbarouk Magawa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya namna mwanachama anavyoweza kupata taarifa mbalimbali za michango yake.

  Meneja Uwekezaji toka Mfuko wa Pensheni wa PPF Selestine Some akielezea mafanikio mbalimbali ambayo mfuko umepata tangu kuanzishwa kwake miaka 35 iliyopita .  =======  ==========   ========


  UTANGULIZI

  Mfuko wa Pensheni wa PPF  ni Mfuko mkongwe hapa nchini, ulianzishwa mwaka 1978 kwa Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa PPF Sura na. 372kwa madhumuni ya kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendena na hayo kwa wafanyakazi wote walio katika sekta rasmi na zisizo rasmi.


  majukumu ya mfuko


  PPF ina majukumu yafuatayo:-

  i)     kuandikisha wanachama,

  ii)   kukusanya michango,

  iii)  kuwekeza michango inayokusanywa na

  iv)kulipa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa wanachama wake.


  WIGO WA UANACHAMA

  Mfuko unaandikisha wanachama kutoka katika sekta zote za uchumi mashirika ya umma, makampuni binafsi, waliojiajiri wenyewe na sekta isiyo rasmi


  Mafao ya PPF: Mfuko wa PPF una mafao saba

  baadhi ya mafao ambayo Mfuko unatoa ni

  1. Mafao ya Pensheni ambapo hutolewa pale ambapo mwanachama anapokuwa amechangia kwa kipindi cha miaka 10 au zaidi na amefikia umri kustaafu yaani miaka 55 mpaka 60.Na awe ameondoka kwenye ajira.

  Mpaka sasa PPF ina wastaafu  wapatao 25,896 na tunalipa kila mwezi Billioni 3.7

  Hii ni kwa mafao ya uzeeni tu mnaweza kuona jinsi tunavyosaidia kuondoa umaskini na kukuza uchumi wa nchi.

  1. Mafao ya Ugonjwa

   Hutolewa pale ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa ameondoka kazini kwa sababu za ugonjwa na imedhibitishwa na Daktari kwamba kweli hawezi kufanya kazi tena

  1. Mafao ya Elimu:

  Hutolewa pale ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa amefariki dunia baada ya kuchangia kwa muda wa miaka 3 au zaidi.

  Fao hili hutolewa kwa watoto wa mwanachama wasiozidi 4 kwa kulipia gharama ya elimu ya chekechea mpaka kidato cha nne.

  Kwa kutambua umuhimu wa elimu kuanzia mwakani 2014 Mfuko unaongeza muda wa kuwasomesha watoto mpaka kidato cha sita.

  Tunalipa mmoja kwa mmoja kwenye shule za watoto wanachama

  UWEKEZAJI

  Jukumu linginge kubwa ni kuwekeza; Mfuko wa PPF unawekeza kwa mujibu wa sera ya uwekezaji sambamba na mwongozo wa uwekezaji wa SSRA na BOT.  Baadhi ya sehemu Mfuko unawekeza katika

  ·         Majengo kama vile ofisi mfano PPF Tower,PPF Plaza Mwanza,vile vile wekeza kwenye hoteli,nyumba za kupanga vile vile tume tumeshiriki kwenye ujenzi wa vyuo vikuu kama vile UDOM-kwenye chuo cha Mifumo ya Komputa na chuo kikuu cha sayansi na Teknologia Nelson Mandela kilichopo Mkoani Arusha.

  ·         Tumeshiriki kwenye uwekezaji katika sekta ya Kilimo Kagera Sugar, 21st Century kiwanda cha Nguo Morogoro

  ·         Uwekezaji mwingine ni kwenye Mikopo ya Saccos kwa wanachama wetu ambapo PPF unakopesha wanachama kwenye maeneo ya Kazi ambapo inasaidia kukuza uchumi


  MAFANIKIO YA MFUKO

  • Mfuko umetimiza miaka 35 mwaka huu na ulianza kwa mtaji wa shilingi million 50 mwaka 1992.lakini Mfuko unaendelea vizuri kwa kuwa na uwezo wa kulipa mafao kwa wakati bila kulazimika kuuza vitega uchumi au kukopa mahali popote

  • Kwa upande wa thamani ya Mfuko:

  Mfuko umeendelea kukua mwaka hadi mwaka ambapo kwa sasa thamani ya Mfuko ni shilingi trillion 1.3ukilinganisha na mwaka jana 2012 Desemba ambapo thamani ya Mfuko ilikuwa trillion 1.09

  • IDADI YA WANACHAMA

  Mfuko umeendelea kukua kwa upande wa uanachama ambapo hadi kufikia mwezi Juni 2013, tulikuwa na jumla ya wanachama 224,193 ukilinganisha na wanachama 203,981 kwa mwezi Desemba 2012


  • Matumizi ya mifumo ya habari:

  Mfuko umefanikiwa sana katika nyanja ya teknolojia kwa kuweza kulipa mafao kwa kutumia mtandao, hivyo kulipa kwa wakati.


  Vile vile Mfuko umepunguza matumizi ya karatasi yaani ‘paper work’ kwa kurahisisha malipo kwa wanachama na kwa upande wa watoa huduma tunatumia  mfumo wa ‘E-banking’ yaani pesa zinatumwa moja kwa moja kwenye akaunti ya mhusika.

  Kupitia mifumo ya kisasa ya PPF, mwanachama anaweza kupata taarifa zake za michango, dai au pensheni kwa mstaafu kupitia simu ya kiganjani au tovuti ya Mfuko ambayo ni www.ppftz.org

  Mwanachama anaandika neno michango anaacha nafasi anaweka namba ya   uanachamana kutuma kwenye namba 15553

  Si hivyo tu , bali hata mwajiri anaweza kupata taarifa za michango ya wafanyakazi wake akiwa katika sehemu yake ya kazi bila kwenda katika ofisi za PPF hii inaokoa muda na pia kuongeza uhakika wa uwasilishwaji wa michango ya wanachama.


  Kwa kutambua umuhimu wa matumizi ya mifumo ya habari mwaka huu 2013 katika wiki ya Hifadhi ya Jamii, Mfuko wa Pensheni wa PPF ulitunukiwa hati ya  utambuzi kama Mfuko bora kwenye matumizi ya Mifumo ya habari. Hati hiyo ilitolewa na Mhe. Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,kwa kuwa Mfuko bora katika Nyanja ya mifumo ya habari kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwenye kutoa huduma mbalimbali.

  • Utoaji wa Mikopo ya SACCOS

  PPF ni waanzilishi wa mikopo ya SACCOS tulianza kutoa mikopo ya saccos mwaka 2004.

  Tunatoa mikopo hii kupitia SACCOS za wanachama wetu zilizopo kwenye maeneo yao ya kazi.

  Mpaka sasa tumeshatoa zaidi ya Billioni 56 kwenye SACCOS 46

  • Tuzo katika Utawala bora

  Kwa kutambua uwazi katika uendeshaji wa Mfuko Umoja Mifuko ya hifadhi ya Jamii Duniani (issa) uliweza kutupatia Tuzo katika utawala bora kwa kuendesha shughuli mbali mbali kwa uwazi kama vile mikutano ya wanachama na wadau PPF huu ni mwaka wa 23 tuna desturi ya kukutana na wanachama na wadau wetu.

  • Hati safi kutoka kwa CAG kwa kuwa na mahesabu yaliyo safi

  • Uwekezaji ni mzuri ambapo tumewekeza katika sehemu mbalimbali kama vile hoteli za kitalii mfano East African Hotel Arusha na Gold Crest Mwanza ambapo watalii wengi wanafika hivyo inasaidia kwenye ukuaji wa Uchumi.


  Tumewekeza kwenye ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa ajili ya kuwauzia wanachama wetu.PPF imekuwa Mfuko wa kwanza kwa kuanzisha miradi ya nyumba za bei nafuu.

  Tulijenga nyumba 580 Kiseke Mwanza na tuliziuza kwa bei nafuu ya kati ya  shilingi millioni 16 mpaka million 33. Zoezi hili ni endelevu kwa mikoa mingine

  • Fao la Elimu:

  PPF imekuwa Mfuko wa kwanza kuwa na Fao la elimu kwa watoto wa wanachama wetu.Ambapo lilianza kutolewa mwaka 2003 ambapo tangu tuanze kwasomesha kiasi cha shilingi billion 3.6  LENGO

  Katika Mpango mkakati wa Mfuko kwa kipindi cha miaka 3 (2013-2015) baadhi ya malengo ya Mfuko ni kama ifuatavyo:

  Thamani ya Mfuko ni kukua kutoka trillion 1.09 Desemba 2012 na kufikia trillion 2 ifikapo  Desemba 2015

  • Na Idadi ya wanachama kuongezeka kutoka wanachama 203,981 Desemba 2012 kufikia laki 4 Desemba 2015.

  Lengo kuongeza mara mbili thamani ya Mfuko  Mwisho kabisa ningependa kuwashukuru wanachama na wadau wote wa Mfuko kwa Mchango Mkubwa Mliotupa

  Hivyo tunaomba tuendelee kushirikiana kwa kuendelea kuwa wanachama wa PPF na wale ambao bado hamjajiunga na PPF tunaomba mjiunge ili muweze kuwa na uhakika wa maisha yenu ya sasa na baadaye.

  Asanteni

  Lulu Mengele

  Meneja Uhusiano na Masoko

  Mfuko wa Pensheni wa PPF

  Simu: 0782 249994


  0 0


  0 0

   Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifungua majadiliano. Katikati ni Mwenyekiti wa Majadiliano hayo kutoka Kituo cha Demokrasia na Maendeleo Mhe.Agustine Lyatonga Mrema.

  Mhe. Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto afungua  Majadiliano kuhusu Utafiti wa Vyama vya Siasa na namna vinavyozingatia masuala ya Kisiasa katika Mtizamo wa Kijinsia nchini. Majadiliano hayo yameandaliwa  na Kituo cha Demokrasia na Maendeleo kwa Kushirikiana na Shirika la Kimataifa la IDEA. Aidha Utafiti kama huo umefanyika katika nchi 38 za Barani Afrika kutoka Vyama  mbalimbali 220 vya Siasa.
   Baadhi ya Washiriki wa Majadiliano hayo kutoka katika Vyama mbalimbali vya Kisiasa nchini wakifuatilia Taarifa ya Utafiti
   Mwakilishi wa Shririka la Kimataifa la IDEA Bibi. Rumbidzai Kandawasvika Nhundu akielezea sehemu ya taarifa ya Utafiti huo. Inaefutia ni Mhe.Ummy Mwalimu na Mhe.Agustine Lyatonga Mrema Mwenyekiti wa Majadiliano hayo
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar- es Salaam Dr. Bernadetha Kilian akiwasilisha taarifa ya Utafiti

  0 0


  Juhudi za Dk. Mwakyembe na Dawa za Kulevya, Amnasa Rasta Akisafirisha Madawa Uwanja wa JNIA Dar es Salaam

  JUHUDI za Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe za kupambana na dawa za kulevya nchini Tanzana zimeanza kuzaa matunda baada ya jana akiwa katika ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Julius Nyerere kunaswa kijana akijaribu kupita na dawa za kulevya katika uwanja huo.

  Kwa kile kuoneshwa kukerwa na tabia hizo, Dk. Mwakyembe amempiga picha kijana huyo ambaye ni rasta na pita yake itasambazwa maeneo tofauti, huku kesi yake ikiendelea ya kupatikana na madawa hayo ya kulevya.

  Akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe alimtaja kijana aliyekamatwa jana kuwa ni Leonard Jeremiah Monyo (Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroin akitaka kusafiri nazo kuelekea misokoto ya bangi 34 akiwa ameficha kwenye begi lake.

  Alisema kijana huyo rasta alinaswa na mtambo wa kukagua mzigo baada ya wakaguzi kuushuku mzigo wake hivyo kuamuru ukaguliwe ndipo alipokutwa na madawa hayo haramu akijaribu kusafiri nayo kwa ndege.

  Alisema kijana huyo kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukutwa na dawa hizo haramu. Alisema kwa kile kuoneshwa kukerwa na vitendo hivyo na kuamua kwa dhati kupambana navyo wamempiga picha kijana huyo na picha zake zitasambazwa maeneo mbalimbali ili aonekane na umma kujua watua ambao wamekuwa wakilichafua taifa nje na ndani kutokana na biashara hizo haramu.

  Dk. Mwakyembe amesema atahakikisha anafuatilia kesi ya kijana huyo hadi itakapoishia ili uona hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika na vitendo hivyo kukomeshwa. Alisema maofisa wakaguzi wa mizigo wawili (wote wasichana) ambao walimnasa kijana huyo watazawadiwa na kupandishwa daraja kutokana na kazi nzuri waliyoifanya.

  "Jana tu baada ya ukaguzi wenzetu ambao wanaona kama tunafanya mzaha jana tena wakapitisha mzigo wa madawa ya kulevya kiwanja cha ndege cha Dar es Salaam, kwa sababu vijana wetu sasa wameamka na hawataki mchezo wakamkamata kijana huyo...," alisema.

  "Picha yake itasambazwa kila sehemu...sidhani kama tunahitaji upelelezi kwa sababu tumekukamata na dawa za kulevya. Mimi na viongozi wangu kupitisha dawa za kulevya akikisha kuuhakikisha.

  Alisema kijana huyo alikamatwa majira ya saa mbili na nusu usiku akiwa anasafiri kwenda nchini Italia kwa kutumia ndege ya kampuni ya Swissair. Alisema kwa sasa kila atakayekamatwa na dawa za kulevya picha yake itasambazwa maeneo mbalimbali ya nchi ili watu hao wajulikane.

  Alisema kwa sasa taratibu zinafanywa ili kuhakikisha mizigo ya abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi kuingia Tanzania nao mizigo ikaguliwe ili kuwabaini wanaoingiza bidhaa hiyo haramu ichini pia. Aliongeza zoezi hilo litafanyika katika viwanja vya ndege na bandarini kwa kila mizigo inapowasili.


  Alisema lengo ni kuhakikisha viwanja vya ndege vinakuwa salama na kuacha kutumika vibaya na baadhi ya watu, jambo ambalo limeendelea kulichafua taifa. Alisem kiwanja cha Dar es Salaam ni kizuri na kina vifaa vya usalama vya kutosha ila mapungufu yaliyopo ni kwa baadhi ya wafanyakazi ambao wanatumia vibaya madaraka yao.

  Dk. Mwakyembe ameahidi kuwataja na kuweka picha zao hadharani watu ambao wanajihusisha na madawa hayo ya kulevya. Amesema wanatarajia kutaja majina ya Watanzania ambao hivi karibuni walinaswa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo. Alisema Watanzania wengine wamekamatwa Hong Kong wakihusishwa na dawa hizo na wanafuatilia pia picha na majina yao yatawekwa hadharani muda wowote. 

  0 0

  8E9U4168

  Rais Kikwete akikmkaribisha Ikulu,Rais na Mtendaji Mkuu wa African Gold,Bwana. Greg Hawkins na kufanya nae mazungumzo.
  8E9U4180
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais na mtendaji Mkuu wa African Barrick Gold Bwana Greg Hawkins(wapili kushoto) ikulu jijini Dar es Salaam leo.kushoto ni Afrisa mwandamizi wa African Barrick Gold Bwana Deo Mwanyika(picha na Freddy Maro).

  0 0

  FAMILIA YA BWANA SHANE OMARY BENDERA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA DR STELLA BENDERA KILICHOTOKEA JUMATATU USIKU KATIKA HOSPITALI YA MAMA NGOMA SINZA.
   
  MIPANGO YA MAZISHI INAFANYWA NYUMBANI KWAKE OYSTERBAY.
   
  TUNATEGEMEA KUFANYA IBADA YA MAZISHI KKKT MSASANI  SAA SABA MCHANA NA BAADAYE MAZIKO MAKABURI YA KINONDONI SAA KUMI JIONI SIKU YA IJUMAA TAREHE 16TH AUGUST 2013.
   
  HABARI ZIWAFIKIE NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WA UKOO WA BENDERA NA UKOO WA MWANRI.
   
  BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE.

  0 0

  Huduma ya Maombezi zatimiza miaka 25 Mkoani Rukwa.


  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mheshimiwa Injinia Stella Manyanya, atakuwa mgeni rasmi Jumamosi Agosti 17, 2013 katika Matembezi ya Sala ya kumshukuru MWENYEZI MUNGU kwa Amani tuliyonayo hadi leo katika taifa letu na huduma za Maombezi kutimiza miaka 25 katika mkoa wa Rukwa.


  Matembezi haya yameandaliwa na Kituo cha Huduma za Maombezi (Marian Faith Healing Centre) zinazoongozwa na Mtumishi wa Mungu, Rev. Fr. Felician Nkwera; yataanzia Mazwi saa 12.00 asubuhi, kupitia Katandala, Sokoni, Majengo hadi kituo cha Sala za Maombi kilichopo Hillside Majengo Sumbawanga mjini.


  Haya ni Matembezi ya kumi ya sala katika mfululizo wa matembezi ya sala ambayo Huduma za Maombezi zimekuwa zikifanya jijini Dar es salaam, Mbeya na Sumbawanga tangu kuanzishwa kwake mwaka 1969. Matembezi ya sala ya tisa yalifanyika Disemba 1, 2012 kuanzia TAZARA hadi kwenye kituo cha Huduama za Maombezi cha Riverside kilichoko eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi  katika matembezi hayo alikuwa Mheshimiwa Pereira Silima, Naibu Waziri kwa niaba ya Dkt. Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Mambo ya Ndani. Takriban watu  3000 walishiriki katika matembezi hayo


  Malengo makuu ya matembezi haya ni pamoja na :-:

  1.      Kumshukuru MWENYEZI MUNGU kwa amani ambayo tunayo katika Taifa letu hadi leo.

  2.      Kumuomba MWENYEZI MUNGU azidi kutulindia amani ya ndani ya Taifa letu na katika mipaka na majirani zetu.


  3.      Kumuomba MWENYEZI MUNGU aponye maradhi makubwa yanayolidhoofisha Taifa letu (Rushwa, Ufisadi, Ushirikina na Ukimwi).

  Huduma za Maombezi ni utume maalum wa sala za tiba: Yaani uponyaji wa maradhi na kupunga pepo. Haubagui kwa misingi yoyote ile. Ni zawadi kubwa kutoka kwa MWENYEZI MUNGU kwa watu wa Tanzania na ulimwengu mzima. Huduma za Maombezi zimeenea sehemu mbalimbali Tanzania na nchi nyingine za Africa, pia Ulaya, Amerika na Asia.


  Watanzania wote mnaalikwa kushiriki katika nafasi hii ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupatia Huduma za Maombezi pia kuzidi kuliombea Taifa letu amani ya kudumu.

    
  Sylivester Shayo


  MWENYEKITI, HUDUMA ZA MAOMBEZI


  0 0

   Katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu akitoa maagizo kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika kijiji cha Usililo kata ya Luwumbu wilaya ya Makete
   katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu (kushoto)akimuagiza diwani wa kata ya Bulongwa ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya fedha na mipango wilaya ya halmashauri ya makete kupeleka maagizo ya kutolipwa kwa mkandarasi huyo
   Mwenyekiti wa CCm wilaya ya makete Francis Chaula akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha luwumbu makete
  Moja ya sehemu ya barabara ya Bulongwa - Luwumbu ambayo imewekwa kifusi ambacho si rafiki na mazingira ya kata hiyo

  Na Edwin Moshi, Makete

  Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Makete kimeishukia serikali ya halmashauri ya wilaya hiyo kwa kumtaka mkandarasi anayekarabati maeneo korofi katika barabara ya Bulongwa-Luwumbu kurudia kuweka kifusi imara kwenye barabara hiyo na kutoa udongo waliouweka kwani hauna msaada kwenye barabara hiyo

  Chama hicho kimekwenda mbali zaidi kwa kumtaka diwani wa kata hiyo kukataa kusaini hati ya kuidhinisha mkandarasi huyo alipwe fedha za kazi hiyo mpaka atakaporekebisha barabara hiyo kwa kuweka kifusi imara ambacho kitawaridhisha wananchi na watumiaji wa barabara hiyo

  Kauli hiyo imetolewa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Usililo kata ya Luwumbu wilayani hapa na katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu, ambapo pamoja na mambo mengine wananchi wameoneshwa kukerwa na ukarabati wa barabara hiyo, ambapo kabla ya mkutano huo msafara wa viongozi hao ulishangazwa na uwekaji wa kifusia ambacho si rafiki wa mazingira ya kata hiyo

  Kufuatia sakata hilo, chama hicho kupitia kwa katibu Mtaturu walimuagiza diwani wa kata ya Bulongwa ambaye ni mjumbe wa kamati ya fedha na mipango ya halmashauri ya wilaya ya Makete ambayo inaidhinisha malipo ikiwemo ya wakandarasi, kupeleka taarifa wilayani kuwa mkandarasi huyo asilipwe fedha mpaka arekebishe barabara hiyo kwa kuweka kifusi kinachokubalika

  "wananchi nawahakikishia mkandarasi huyo hatalipwa fedha, maana kifusi alichokiweka mvua ikinyesha tu maeneo yote yatakuwa na utelezi na hayatapitika, na huku kuna mazao na shughuli nyingi sasa hii kero hadi lini, sisi hatutaki matusi baadaye kutoka kwa watu, tunataka kazi hii ifanyike mara moja" alisema Mtaturu

  Akihutubia wananchi mkutanoni hapo mwenyekiti wa CCM wilaya Makete Francis Chaula amewataka wananchi hao kutokubali kurudishwa nyuma kimaendeleo na kuzitumia rasilimali zilizopo katani hapo kwa maendeleo yao wote huku wakiwakemea na kukaa mbali na wale wanaokwamisha maendeleo yao

  Amesema kutokana na kata hiyo kupewa mfereji wa umwagiliaji ambao hivi sasa una mgogoro na mtu aliyejitokeza na kudai eneo lililojengwa mfereji huo ni lake na kupeleka kesi hiyo mahakamani, wapambane hadi dakika ya mwisho kutetea mfereji huo na kwani chama hicho kipo nyuma yao kuhakikisha wanashinda katika kutetea mradi huo wenye manufaa kwa kata hiyo

  Ziara hiyo ya viongozi wa CCM wilaya ya makete wakiongozwa na mwenyekiti Francis Chaula imefanyika katika vijiji vya Uganga, Luwumbu, Unenamwa na Usililo ambavyo vipo katika kata ya Luwumbu kwa lengo la kusikiliza kero na maoni ya wananchi hao

  0 0

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo huku Mama Salma Kikwete akisubiri zamu yake wakati walipokwenda kuomboleza na kufariji wafiwa  kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu Abel Mwaisumo aliyefariki juzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 16, 2013.
   Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo  kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu Abel Mwaisumo aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es salaam  leo Agosti 16, 2013.
   Mama Salma Kikwete akifariji wafiwa wakati yeye na Rais Kikwete walipokwenda kuomboleza na kutoa pole kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu Abel Mwaisumo aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es salaam  leo Agosti 16, 2013.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wengine wakiomboleza na kufariji wafiwa  katika  msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu Abel Mwaisumo aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es salaam  leo Agosti 16, 2013.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu Abel Mwaisumo aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa.

  BOFYA HAPA 
  AU
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

    Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais Joyce Banda wa Malawi muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lilongwe tayari kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC leo
    Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtoto muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lilongwe tayari kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC leo. 
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana nawakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama muda mfupi baada ya kuwasili Lilongwe Malawi kuhudhuria Mkutano wa SADC
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Rais Joyce Banda muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lilongwe tayari kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC leo.
  Picha na Fred Maro

  0 0

   Mtaalamu wa Biashara na Masoko wa Tigo, Gaudence Mushi,  akimkabidhi funguo mmoja ya washindi wa droo ya Nne ya Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo Beatrice Gelvas Mkembo  wakati wa hafla iliyofanyika Manzese  Jijini Dar es Salaam
   Mtaalamu wa Biashara na Masoko wa Tigo, Gaudence Mushi akimkabidhi funguo mmoja ya washindi wa droo ya Nne ya ya Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo, Amiri Hamis Chiumbo  wakati wa hafla iliyofanyika Manzese  Jijini Dar es Salaam.
  Bi Jamila Habib Daudi  mmoja ya washindi wa  Bajaji wa wiki ya Nne ya Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo akijaribu kuendesha  Bajaji yake mara baada ya kukabidhiwa katika Viwanja Manzese Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Meneja Uzalishaji wa Kampuni hiyo, Suleiman Mushagama.


  0 0

  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Uganga wilayani Makete akizungumza na mwandishi wetu kuhusu tatizo la upungufu wa waaalimu shuleni hapo.
  Mwalimu Yuda Kiluswe ambaye anafundisha darasa la awali hadi la pili akiwa darasani akifundisha. 
  =========   =======  =======
  Edwin Moshi wa Globu ya Jamii, Makete.

  Tatizo la upungufu wa waalimu katika shule mbalimbali wilayani Makete mkoani Njombe limezidi kushika kasi baada ya shule ya msingi Uganga kata ya Luwumbu wilayani hapo kuwa na waalimu wanne tu na wote wakiume licha ya shule hiyo kuwa na wanafunzi wa kike na wakiume.

  Tukio hilo la aina yake limedhihirika baada ya mwandishi wa mtandao huu kufunga safari na kwenda shuleni hapo na kuwakuta waalimu hao wakijitahidi kufundisha wanafunzi ambapo jumla ya wanafunzi wote wapo 112.

  Mwandishi wetu ameshuhudia mwalimu Yuda Kiluswe ambaye ni mwalimu wa darasa la awali, la kwanza na la pili, akiwafundisha wanafunzi jambo lililomshangaza mwandishi na kwenda kumhoji kulikoni yeye kama mwalimu mwanaume anawafundisha wanafunzi wa darasa la awali hadi la pili ili hali imezoeleka wanafunzi wa madarasa hayo hufundishwa na waalimu wa kike.

  Mwalimu Kiluswe amesema analazimika kufundisha madarasa hayo kwa kuwa hakuna mwalimu wa kike shuleni hapo hivyo kulazimu waalimu hao wane waliopo shuleni hapo kufanya kazi zote za kufundisha pamoja na misaada yote wanayohitaji wanafunzi wawapo shuleni hapo.

  “Ni kweli imezoeleka wanafunzi hawa wadogo wanafundishwa na waalimu wa kike, lakini kwa kuwa hawapo je tufanye nini, hapa hakuna cha kufanya zaidi ya mimi kuingia darasani na kuwafundisha na wameshazoea na hata mimi pia nimeshazoea” alisema mwalimu Kiluswe.

  Akizungumzia suala hilo mwalimu mkuu wa shule hiyo Eliuda Daniel Msigwa amesema ni kweli kuwa shule hiyo ina waalimu wane wote wa kiume wanaohudumia wanafunzi 112 wanaosoma shuleni hapo.

  Amesema ni kweli wameshatoa taarifa wilayani kuomba kupatiwa mwalimu wa kike hata mmoja lakini bado kilio hicho hakijasikika hivyo kuiomba halmashauri ya makete kuona namna ya kufanya kuwapa waalimu wa kike hata kwa kuhamisha kutoka shule nyingine na kuwapeleka shuleni hapo.

  “Ni kweli tunajua kuwa waalimu hawatoshi lakini mimi ningeshauri, hapa tuna waalimu wanne wakihamisha hata mmoja wa kiume na kumleta mwalimu wa kike badala yake, hii itasaidia wakati tunasubiri serikali kupangia waalimu wengine wapya shuleni hapa” alisema mwalimu mkuu.

  Amesema mbali na kuwepo waalimu wanne bado hawatoshi na kusema wakiongezeka angalaua watatu kutawarahisishia kupungua kwa kazi nyingi kwani wanafanya kazi kupita kiasi kutokana na uchache wao.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (kushoto), akieleza mafanikio ya TDL ikiwa ni pamoja jinsi inavyolipa kodi serikalini ambapo kwa mwezi hulipa sh. bil. 7.  Mgwassa alikuwa akizelezea mafanikio hayo wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari ya kuwajengea uwezo wa kuthamini bidhaa za ndani leo kwenye Hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.Kulia ni mgeni rasmi katika semina hiyo, Mbunge wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Tanzania, Mussa Zungu.
   Mgeni rasmi katika semina hiyo, Mbunge wa Jimbo la Ilala ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu, akitoa pongezi kwa Mkurugenzi wa TDL, David Mgwassa kwa kukipatia mafanikio makubwa kiwanda hicho.
   Mkurugenzi wa Masoko wa TDL, Joseph Chibehe 9kulia) akielezea mbele ya wahariri, historia ya kinywaji cha Konyagi.


   Baadhi ya wahari walioalikwa kwenye semina hiyo, wakisikiliza kwa makini wakati Chibehe aielezea historia ya TDL.
   Seheumu ya wahariri wa vyombo vya habari waliohudhuria semina hiyo
   Baadhi ya wahari walioalikwa kwenye semina hiyo, wakisikiliza kwa makini wakati Chibehe aielezea historia ya TDL.
   Picha juu na chini ni baadhi ya wahariri na wanahabari wakiwa katika semina hiyo iliyoandaliwa na TDL.

   Mgeni rasmi, Mussa Zungu 9katikati waliokaa) akiwa na MD wa TDL , Mgwassa, Mkurugenzi wa Masoko, Chibehe katika picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya habari nchini.
   MD wa TDL, Mgwassa (katikati) akimuaga Mussa Zungu. Kulia ni Chibehe.
  Baadhi ya wahariri walioalikwa kwenye semina hiyo, wakisikiliza kwa makini wakati Chibehe aielezea historia ya TDL. PICHA  ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

  0 0

  Dkt.Haroun Nyagori ambaye ni bingwa wa Magonjwa ya moyo katika Hospital ya Mkoa wa Morogoro,akielezea umuhimu wa mashine ya Cardiac Monitor yenye thamani ya Tsh Milioni 12 mara baada ya kupokea msaada wa mashine hiyo toka kwa Meneja wa benki ya KCB tawi la Morogoro Bi.Hogla Laiser (katikati)
  Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt.Rita Lyamuya(kulia)akipokea msaada wa Mashine ya Cardiac Monitor kutoka kwa Meneja wa Benki ya KCB tawi la Morogoro Bi.Hogla Laiser.
  Swaumu Hassani ambaye ni Mama mzazi wa Mtoto Ibrahim Salum akishuhudia mwanae akipatiwa vipimo kupitia mashine ya Cardiac Monitor na Dkt.Haroun Nyagori ambaye ni bingwa wa Magonjwa ya moyo katika hospital ya Mkoa wa Morogoro,Mashine hiyo yenye thamani ya shilingi Milioni 12 ilitolewa msaada na Benki ya KCB tawi la Morogoro hapo jana,anaeshuhudia kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Dkt.Rita Lyamuya.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro na wafanyakazi wa Benki ya KCB tawi la Morogoro wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano rasmi ya Mashine moja ya Cardiac Monitor iliyotolewa msaada na Benki hiyo hapo jana. 

  0 0

  IMG_2404

  Mshauri wa Redio za Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu akitoa mada kwa wadau wakati wa warsha ya Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii kuhusiana na umuhimu wa kutengeneza vipindi vyenye ubora vitakavyovutia jamii wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema FM mkoani Mwanza ambayo imefadhiliwa na UNDP na kuratibiwa na UNESCO.
  IMG_2285
  Mwezeshaji kutoka Search for Common Grounds Patricia Loreskar akizungumza na Mameneja wa redio za jamii nchini kuhusiana na shirikika lake linavyofanya kazi ya kutoa Elimu kujenga Amani na kutatua migogoro mbalimbali inayojitokeza kwenye jamii yetu na kuwataka redio za jamii zisiwe chanzo cha kuvuruga Amani bali zitoe Elimu ya kudumisha Amani kwa jamii nchini kwenye warsha ya wiki moja inayoendelea kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema FM kwa redio za jamii nchini kwa ajili ya kujiandaa kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
  IMG_2393
  Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph Al-Amin akifafanua jambo wakati wa warsha ya wiki moja ya Majadiliano baina ya Vyombo vya habari vya kijamii (redio) na nafasi yake katika kuhamasisha Demokrasia na Amani kwenye mazingira shirikishi na umuhimu wake katika kuunganisha jamii na kutatua migogoro ikiwa ni moja ya jitihada za kuendeleza Elimu haswa katika kuboresha sera za uhariri wa habari.
  IMG_2306
  Picha juu na chini ni Baadhi ya Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii wakifuatilia mada mbambali zilizokuwa zikitolewa kwenye Warsha ya wiki moja inayoendelea katika kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema FM mkoani Mwanza.


  IMG_2121
  IMG_2331
  Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Grace Mapunda akizungumzia uhusiano wao na redio ya jamii Sengerema FM ambao amesema redio hiyo imekuwa mchango mkubwa sana kwa wananchi wa wilaya hiyo katika kupashana habari.
  IMG_2424
  Meneja wa Redio Jamii ya Orkonerei Fm ya Wilayani Simanjiro Khadija Abdallah akiwasilisha mada kwenye warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.
  IMG_2102
  Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambaye pia ni Mtafiti kutoka ECOM Research Dr. Ambrose Kessy akielezea umuhimu wa kufanya utafiti kwa redio za jamii kwa ajili ya kuboresha usikivu na vipindi vyao kwa jamii.
  IMG_2346
  Meneja wa Kituo cha redio ya Jamii FADECO Adeline Lweramula akichangia maoni yake wakati wa kujadili uboreshaji wa sera za uhariri wa habari. Kulia ni mwezeshaji Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph Al-Amin.
  IMG_2323
  Meneja wa mradi wa DEP kutoka UNESCO Courtney Ivins (kushoto) akibadilishana mawazo na wadau wa Search for Common Grounds wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema FM mkoani Mwanza.

  0 0   Ndugu zangu,
   Umezinduliwa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ( MMMS) kwenye Sekta ya Elimu.  Kwa kimombo unaitwa ‘ Big Results Now’ ( BRN).
  Kwa lugha nyingine ni mpango wa ‘ Mavuno Makubwa Sasa’. Na mkulima anayetarajia mavuno makubwa ya mahindi  ni lazima awe amefanya makubwa matatu; kulima shamba lenyewe, kupanda mbegu bora na kulipalilia vema shamba lake.

  Na jana nilipokuwa nikifuatilia ‘ live’ TBC1 uzinduzi ule wa ‘ Mavuno’ makubwa sasa nilijiuliza; Je, maofisa wale wa elimu wa mikoa wenye kula kiapo hadharani kuhakikisha ‘ mavuno’ makubwa yanapatikana SASA walielewa hasa  changamoto ya jukumu walilotwishwa la kuhakikisha tunapata ‘mavuno’ makubwa sasa.

   Maana, kiapo kile kingeweza pia kuwa ‘ ungamo’ la dhambi tuzitendazo zenye kupelekea kila mwaka tupate ‘ mavuno’ hapa na wakati mwingine kuambulia debe mbili tatu tu kwenye ‘ mavuno’ yetu ya elimu. Niaonavyo, sambamba na mpango huu ulioandaliwa kwa dhamira njema kabisa, bado kunahitajika Mjadala Mkubwa wa Kitaifa kujadili namna ya kuinasua elimu yetu kutoka hapa tulipo.

  Maana, inabaki, kuwa dhumuni kubwa la maisha ya mwanadamu ni kufanya juhudi za kutafuta namna ya kuyaelewa mazingira yake na hivyo kupiga hatua za maendeleo. Na juhudi hizo za mwanadamu  ndicho chenye kujulikana kama ‘ Elimu’. Naam, mwanadamu anapaswa aitafute elimu, hivyo basi, maarifa.

  Na shule  yaweza kutafsiriwa kuwa ni ‘ Maabara’ ambamo hutengenezwa ‘ chanjo’ ya maradhi ya kimaisha kwa mwanadamu. Wale wenye maarifa na busara  za kuandaa ‘ chanjo’ hiyo  ndio wanaoitwa walimu.

  Maana, shule ni mahali pa kujifunzia, ambapo yote yenye kuhusiana na maisha  ya sasa na hata yajayo hufundishwa. Ni mahali ambapo hupatikana tafsiri za vitu na matukio katika jamii. Ni mahali ambapo, mbali ya mambo mengine,  mwanafunzi anapaswa kusaidiwa kuweza kupata maarifa ya kujitambua na kuyatambua mazingira anamoishi.
  Twaweza kabisa kusema, kuwa shule ni mahali pa ‘ ibada’. Na ‘ viongozi watakatifu’ wenye kupaswa kuongoza ‘ ibada’ hizo ni  WALIMU.

  Hivyo, enyi walimu ‘ watakatifu’ , mnapaswa kuianza sasa kazi ya kuitambua nafasi yenu katika jamii. Vile vile, kulitambua jukumu lenu, vinginevyo, Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa yumkini yaweza kuwa sawa na mkulima anayesubiria ‘ mavuno’ makubwa sasa ilihali  shamba alilolima ni dogo. Amepanda mbegu dhaifu  na ameshindwa hata kupalilia shamba lake.

  Ni Neno La Leo.
  Maggid,
  0754 678 252

  0 0

  Bajaji wakiwa kwenye foleni kuwekewa mafuta na mtu ambaye hakutaka kujitambulisha
  ======  =========
  Mwanamme mmoja, ambaye amekuwa akiongozana na maaskari polisi wawili, amekuwa akigawa fedha za bure kwa watu mbalimbali jijini Dar.


  Kijana huyo wa makamo, ambaye kwa wiki hii nzima amekuwa akitajwa kwenye radio mbalimbali, aliwalipia bili wagonjwa wote waliokuwa wamelazwa hospitali ya Mwanyamala na Muhimbili, wodi ya wanawake.


  Alkizungumza na mwandishi wetu,mmoja wagonjwa wa hospitali ya Muhimbili, Subira Juma alisema kijana huyo alikuja hospitali na kuuliza wangapi wanadaiwa halafu akawalipia bili zao na kisha kuondoka zake bila kujitambulisha.


  ‘Kwa kweli hata mimi sifahamu kijana huyu katokea wapi, lakini sijwahi kuona mtu akitoa hela bila kujuana, na kisha kuondoka billa kusema lolote’ alisema Subira.


  Wakati huo huo, wasafiri wa daladala nao, hasa ziendazo Mbagala nao wametajwa kunufaika na mgawo huo, ambapo wamekuwa wakilipiwa nauli mara kadhaa na mtu huyo.  Mbali na kulipia watu usafiri, kijana huyo pia anatajwa kuwanufaisha maderva boda boda na bajaji kwa kuwawekea mafuta kwenye vyombo vyao vya usafiri.


  0 0

  Tume ya Mapendekezo ya  katiba kwa watanzabia wanaoishi Marekani imeundwa ili kukusanyamaoni na mapendekezo kutoka kwa watanzania wore waishio nchini Marekani na Canada.


  0 0

    ANY INFOS FOR NOW CALL 202-830-8904

older | 1 | .... | 139 | 140 | (Page 141) | 142 | 143 | .... | 1897 | newer