Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1407 | 1408 | (Page 1409) | 1410 | 1411 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.

  Na Mathias Canal, Singida

  Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Kazizi Ndg Kurwa Maduka amevuliwa uongozini na Wananchi Wakati wa Mkutano wa hadhara kutokana na tuhuma za kuruhusu na kuingiza wavamizi katika hifadhi ya msitu zinazomkabili huku wananchi hao wakipendekeza Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Ndg Mussa Mkumbo kuendelea Kuhudumu katika nafasi hiyo.

  Mkutano huo uliofanyika katika eneo la Ofisi ya Kijiji Cha Mtavira na kuhudhuriwa na wananchi 353 kutoka Kijiji Cha Makilawa, Mtavira na Mteva Kata ya Makilawa umepelekea pia Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mtavira Ndg Jilala Lutelemula kujiuzulu kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili ikiwemo tuhuma za kuchukua Rushwa ili kuwaacha wafugaji waendelee kuishi na kuharibu msitu.
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.

  Mara Baada ya Mwenyekiti huyo kujiuzulu katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Aliagiza kuitishwa Mkutano wa wananchi haraka iwezekanavyo ili kuchagua Mwenyekiti mpya ambapo pia ameagiza Mwenyekiti huyo kutiwa nguvuni ili kulisaidia Jeshi la polisi kubaini wahujumu wa msitu huo.

  Mhe Mtaturu pia aliliamuru Jeshi la polisi kumtafuta popote alipo aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Kazizi Ndg Kurwa Maduka kutokana na tuhuma zinazomkabili ikiwemo kuzuia wananchi kuhama katika msitu huo Jambo ambalo Ni kosa kisheria.

  Usiku wa kuamkia Octoba 17, 2017 Mhe Mtaturu aliongoza Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Ikungi kuwasaka na kuwakamata wavamizi wa msitu wa Minyughe wanaoendesha shughuli za kibinadamu ikiwemo Makazi, kilimo na Ufugaji kinyume na Tangazo la serikali (GN) ya kuanzisha hifadhi ya msitu wa Minyughe ya Mwaka 2007.
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mtavira, Makilawa na Mteva wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.

  Katika Oparesheni hiyo Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na mambo mengine pia iliyobaini ukiukwaji wa taratibu unaofanywa na baadhi ya viongozi wa Vijiji na Vitongoji ikiwemo kuwauzia mavamizi maeneo kwa kutoa Rushwa ya fedha au Mifugo.

  Mhe Mtaturu ameiagiza Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Kuwahoji wote wanaotuhumiwa katika sakata la kuruhusu wavamizi wa hifadhi ya msitu.

  Alisema kuwa Ni aibu kubwa kwa viongozi kujihusisha na tuhuma mbalimbali zinazoichafua serikali, Kuvunja heshima na Uaminifu wa wananchi kwa serikali yao.

  "Dhambi ya viongozi kuwaacha kwa makusudi wananchi waharibu misitu itaendelea kuwatafuna viongozi hao kwani wamewasababishia wananchi kuingia hasara ya kuchomewa nyumba zao ambazo walidhani Ni makazi ya kudumu, Ni dhahiri kuwa hatuwezi kuvumilia Nchi ikawa inaongozwa ovyo ovyo ilihali Kuna sheria, taratibu na kanuni" Alikaririwa Mhe Mtaturu

  Mhe Mtaturu pia alisema kuwa ili kunusuru misitu kuharibiwa na wavamizi itaundwa Bodi ya Misitu ambayo itashirikisha Wajumbe kutoka kila Kijiji katika Vijiji 24 vlivyopo katika Kata 8 zilizopitiwa na msitu huo wa hifadhi.

  Pia aliwataka viongozi wa Vijiji, Kata na Kamati zote za misitu kushirikiana kwa karibu na serikali ili kutunza misiti kwani ndio Msingi wa uimarishaji wa Mazingira na uoto wa asili.

  Mhe Mtaturu alisema kuwa dhamira ya kuhifadhi misitu Ni kutunza Mazingira na uoto wa asili hivyo wananchi kufanya shughuli za kibinadamu Ni kinyume na sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2002.

  Sambamba na hayo pia Mhe Mtaturu aliwasihi wananchi kuanza kuandaa mashamba kwani msimu wa Kilimo umekaribia huku akiwasisitiza kuendelea kumuunga Mkono Rais wa Awamu ya Tano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi kubwa ya kusimamia Rasilimali za Nchi anayoifanya.

  Mhe Mtaturu alichangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya ukarabati wa jengo litakalotumika kwa ajili ya kituo cha polisi cha muda huku Akielekeza wananchi, serikali ya kijiji na Kata kusaidia ukarabati wa kituo hicho sambamba na ujenzi wa kituo kipya cha Polisi cha Kata ya Makilawa.

  Hifadhi ya msitu wa Minyughe ilianzishwa kwa Tangazo la serikali (GN) Mwaka 2007 ina jumla ya hekta 264,600 ina manufaa makubwa katika utunzaji wa mazingira na uoto wa asili kwa urahisi wa upatikanaji wa mvua na urahisi katika uimarishaji wa sekta ya kilimo sambamba na ushoroba (Njia ya Tembo).

  Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mtavira aliyejiuzuru Ndg Jilala Lutelemula akizungumza mbele ya wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara kabla ya kujiuzuru.
  Mkazi wa Kijiji cha Mtavira Wilayani Ikungi Ndg Nchambi Kadawi akieleza changamoto inayowakabili wakati wa mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu. 
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mtavira, Makilawa na Mteva wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mtavira, Makilawa na Mteva wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.

  0 0

  Majaji wakijadiliana jambo.

  Top 6 walioingia kwenye mchujo

  Mshindi wa Tigo Fiesta SupaNyota 2017 mkoani Rukwa , Ze Battle 16 akifanya yake kwenye steji.

  Meneja Biashara na Masoko Tigo nyanda za juu kusini, Oliver Baltazar  akishuhudia mshindi wa Tigo fiesta supanyota mkoani Rukwa, Ze Battle 16 akipongezwa na mshindi wa pili, Ambrose mara baada ya kumtangaza mshindi. Kushoto ni Meneja Mauzo Tigo mkoa Rukwa Francis Ndad
  Majaji wa Tigo Fiesta Supa Nyota wakiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi aliyepatikana mkoani Rukwa, Ze Battle 16.

  0 0

  Baadhi ya Wanafunzi wa Taasisi ya Mwanamke kwenye Usukani ambao wamefanya ziara katika Hospitali ya Muhimbili Moi kwa ajili ya kutoa damu na misaada mbalimbali.IMG_6547
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake Usukani Bw.Martin Gabone akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Ziara yao ya kuwatembelea wagonjwa pamoja na kutoa  misaada mbalimbali katika kitengo cha Moi-Muhimbili jijini Dar es salaam
  IMG_6544
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake Usukani Bw.Martin Gabone wa kwanza kushoto akiwa na wanafunzi wake ambao wanasomea mambo ya udereva walipofanya Ziara yao ya kuwatembelea wagonjwa pamoja na kutoa  misaada mbalimbali katika kitengo cha Moi-Muhimbili 
  IMG_6554
  Mwanafunzi kutoka Taasisi ya Mwanamke Usukani,Mary Kihanga akiongea na waandishi wa habari ( hawapo pichani) akielezea namna walivyoweza kujitolea kwa ajili ya kusaidia wagonjwa mbalimbali katika hospitali ya Muhimbili.
  IMG_6563
  Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Moi, Patrick Jonh akiishukuru Taasisi ya Mwanamke Usukani kwa kuweza kutoa misaada mbalimbali katika kitengo hicho .
  IMG_6568
  Wakitoa misaada katika vitanda vya wagonjwa ambao wamelazwa Muhimbili.
  IMG_6571
  Mwakilishi wa Polisi WP Saburi Chutto wa kwanza kushoto wakimsikiliza mgonjwa aliyelazwa katika hospitali ya Muhimbili
  IMG_6573
  Wanafunzi toka Taasisi ya Mwanamke Usukaniwakisubiri kutoa damu kwa ajili ya wagojnwa mbalimbali katika Kitengo cha Moi
  ………………….
  Taasisi ya tiba na mifupa Muhimbili MOI imewashukuru taasisi ya Wanawake Usukani  kwa kwenda kutoa misaada mbalimbali katika kitengo hicho ambacho ni muhimu kwa jamii .

  Afisa uhusiano wa taasisi hiyo Patrick Jonh amesema hayo leo jijini Dar es salaam alipotembelewa na taasisi hiyo  kwenda kuchangia damu kwa wagonjwa wanaohitaji damu, kwani katika kitengo hichi kina uhitaji mkubwa wa damu ili waweze kusaidia wagonjwa.

  Kupitia mkurugenzi wa kampuni ya Wanawake Usukani Martin Gabone ambae anendesha mradi wa kuwajengea wanawake uwezo amesema kuwa wamenda kutoa misaada hiyo kwani kupita taasisi hiyo wanawake wanafursa ya kujifunza udereva hivyo ni chachu hata wao pindi watakapopata ajali waweze kusaidiwa kama leo walivyofanya wao pia iwe kioo kwa watu wengine waweze kwenda kuchangia damu na kutoa misaada.

  Aidha aliongeza kuwa jamii inabidi iondokane na dhana ya kwamba wanawake hawawezi kuamua jambo, kwani sasa kuna fursa nyingi ambazo wan awake wanaweza kujikomboa kiuchumi na hata kijamii.

  0 0


  Mwenyekit wa  Umoja wa wanawake Tanzania ( UWT ) mkoa wa Dar es salaam Mama Janeth Masaburi aliye nyoosha mkono juu  akiimba wimbo na wanawake wa umoja huo  katika maandalizi ya kutoa tamko la umoja huo  mkutano ulio fanyika ilala Jijini Dar es salaam ( na John Luhende wa  Mwambawa habari)


   Wanacha wa UWT mkoa wa Dar nes salaam wakicheza wimbo wa CCM mbelekwa mbele katika kumpongeza mwenyekiti wa chamama Cha  Mapinduzi CCM, Dr John Pombe Magufuli ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzaia .


  Wanawake wa umoja wa wanawake  Tanzania (UWT)  mkoa wa Dar es salaam, wakisikiliza tamko la umoja wao likisomwa na Mwenye kiti wao Mama Janeth Masaburi.( na John Luhende wa  Mwambawa habari)

  Na John Luhende . 
  Umoja wa wanawake wa Tanzania UWT  Mkoa wa Dar es salaam , umempongeza Rais wa jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kufikia makubaliano ya na kampuni ya ya uchimbaji madini ya Dhahabu ya balick  Gold mine na kumtaka kuendelea  na hatua hiyo kwa ulinzi wa lasilimali za taifa  kwaajili ya vizazi vijavyo.

  Akisoma tamko hilo  mwenyekiti wa UWT  Mkoa wa Dar es salaam ,Janeth Masaburi, amesema ,hatua hiyo ni ushindi dhidi ya wapinga Maendeleo,na kusema kuwa kutokana na hatu anazo zichukua  mhe. Rais Magufuli nidhahiri kuwa kunabaadhi miongoni mwa watanzania watabeza hatua hizo lakini nivema wakapuuziwa na kuwakitu kimoja ili tuweze kushinda vita hivi vya kiiuchumi.

  Aidha amesema makubaliano hayo yaliyofikiwa yanatija na faida kwa Taifa na watanzania kwa kutoa ajira na mazingira bora ya kazi tofauti na hapo awali ambapofaida ya madini hayo ilikuwa inaishi kwa makampuni ya wageni.
  Pamoja na hayo Mama Masaburi amesema ,  umoja huo huo umemwomba kushugulikia pia na madini aina ya Urenium na joto ardhi ili nayo yaweze kunufaisha Taifa.  0 0
  Mtaalam wa Tehama wa Nordic Foundation Tanzania Dickson Leonard (katikati) akibadilishana mawazo na Mkaguzi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha, Emmanuel Ndaki (kushoto) na Mkurugenzi mwendeshaji wa Kampuni ya Bima ya Zurich Group/ Jubilee wakati wa zoezi la kuendesha kampeni ya Afyabando ya tatu kuwapata washindi 10 watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya kwa ajili ya matibabu pamoja na familia. Mchezo huo umechezeshwa jijini Dar es Salaam Oktoba 22. 2017. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)
  Mtaalam wa Tehama wa Nordic Foundation Tanzania  Dickson Leonard (kulia) akiwasiliana na mmoja wa washindi wa kampeni ya Afyabando ambapo washindi 10 watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya kwa ajili ya matibabu pamoja na familia. Mchezo huo umechezeshwa jijini Dar es Salaam Oktoba 22. 2017.  Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha, Emmanuel Ndaki.
  Mtaalam wa Tehama wa Nordic Foundation Tanzania  Dickson Leonard (kulia) akiwasiliana na mmoja wa washindi wa kampeni ya Afyabando ambapo washindi 10 watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya kwa ajili ya matibabu pamoja na familia. Mchezo huo umechezeshwa jijini Dar es Salaam Oktoba 22. 2017.  Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha, Emmanuel Ndaki.

  Mtaalam wa Tehama wa Nordic Foundation Tanzania  Dickson Leonard (kulia) akibonyeza kitufe kuwapata washindi wa kampeni ya Afyabando ambapo washindi 10 watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya kwa ajili ya matibabu pamoja na familia.  Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha, Emmanuel Ndaki.
  Mkurugenzi mwendeshaji wa Kampuni ya Bima ya Zurich Group/ Jubilee akiongea wakati wa zoezi la kuendesha kampeni ya Afyabando ya tatu ambapo washindi 10 wamepatikana na watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya kwa ajili ya matibabu pamoja na familia.

  0 0


   Afisa Metekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Arusha,Miraji Kisile akiwahamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma zinazotolewa ikiwemo za matibabu
    Afisa Metekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Arusha,Miraji Kisile akiwahamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma zinazotolewa ikiwemo za matibabu
   ELIMU ikiendelea kwenye moja ya masoko Jijini Arusha kuhusu umuhimu wa wajasiriamali kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo za matibabu
  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Arusha (NHIF) umeanza kutoa elimu ya bima ya afya mtaa kwa mtaa kwa wakazi wa mkoa huo ili waweze kujiunga nao ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo za matibabu.
   
  Hayo yalibainishwa na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Arusha ,Miraji Kisile  ambapo alisema lengo ni kuhamasisha wazazi na walezi kuwaandikisha watoto wao na mpango wa toto afya kadi kwa chini ya miaka 18.

  Alisema mfuko huo umeamua kushiriki katika zoezi hilo kikamilifu kwa kupita katika masoko na magulio ambayo asilimia kubwa ya wananchi wamekuwa wakipatikana huko.

  Aidha alisema sambamba na hilo lakini pia uongozi wa mfuko huo wamedhamiria kuwahamasisha wajasiriamali mbalimbali kujiunga na mfuko huo kupitia mpango wa kikoa ili kulinda mitaji yao kwa kuwa na uhakika wa huduma za afya na matibabu kupitia NHIF kwa gharama nafuu.

  “Zoezi hilo limeanza Octoba 18 mwaka huu na litafanyika kikamilifu kwa muda wa miezi miwili lengo ni kuwafikia wakazi wengi wa mkoa wa Arusha na viunga vyake “Alisema.

  Alisema kwa sasa mfuko huo unatoa kipaumbele kusajili watoto kupitia mpango wa Toto Afya Kadi kwa gharama za kitanzania 50400 kwa mwaka  ambapo ataweza kuhudumiwa kwa vituo 7000 vilivyosajiliwa na bima ya afya vikiwemo hospitali zote za serikali,Hospitali zinazomilikiwa na Madhehebu ya dini,Hospitali za watu binafsi, maduka ya dawa pamoja na vituo maalumu vya uchunguzi.

  Zoezi hilo limefanyika na kutarajiwa kuendelea kufanyika kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo soko la Tengeru,Soko la Ngaramtoni,Soko Kuu,Soko la Kilombero,Soko la Mbauda,Soko la Namanga, Mnadani Monduli,Loliondo,Digodigo Ngorongoro na Waso Ngorongoro.
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Mhe Jordan Rugimbana Mkuu wa mkoa wa Dodoma akikabidhiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka Taarifa ya  Tamko la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kulinda Rasilimali Za Nchi lilifanyia mkoani Dodoma
  Kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka ( MNEC ) akitoa Tamko la Vijana wazalendo la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kulinda Rasilimali Za Nchi(picha na Fahadi Siraji wa UVCCM )
  Mhe Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana ajira na Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akizungumza na Vijana wazalendo  katika Hafla fupi ya Kukabidhi tamko  la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kulinda Rasilimali Za Nchi Mjini dodoma.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Lugimbana akizungumza na Vijana wazalendo mara baada ya  kupokea taarifa ya Tamko la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kulinda Rasilimali Za Nchi.
  baadhi ya mabango yakiwa na ujumbe mbalimbali za kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kulinda Rasilimali Za Nchi. ( Picha na Fahadi Siraji wa UVCCM )
  Vijana wakiwa katika burudani.(picha na Fahadi Siraji wa UVCCM )
  Vijana wakiwa katika burudani.(picha na Fahadi Siraji wa UVCCM )


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mtavira, Makilawa na Mteva wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
  Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mtavira aliyejiuzuru Ndg Jilala Lutelemula akizungumza mbele ya wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara kabla ya kujiuzuru.
  Mkazi wa Kijiji cha Mtavira Wilayani Ikungi Ndg Nchambi Kadawi akieleza changamoto inayowakabili wakati wa mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mtavira, Makilawa na Mteva wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
   Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mtavira, Makilawa na Mteva wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.

  Na Mathias Canal, Singida

  Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Kazizi Ndg Kurwa Maduka amevuliwa uongozini na Wananchi Wakati wa Mkutano wa hadhara kutokana na tuhuma za kuruhusu na kuingiza wavamizi katika hifadhi ya msitu zinazomkabili huku wananchi hao wakipendekeza Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Ndg Mussa Mkumbo kuendelea Kuhudumu katika nafasi hiyo.

  Mkutano huo uliofanyika katika eneo la Ofisi ya Kijiji Cha Mtavira na kuhudhuriwa na wananchi 353 kutoka Kijiji Cha Makilawa, Mtavira na Mteva Kata ya Makilawa umepelekea pia Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mtavira Ndg Jilala Lutelemula kujiuzulu kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili ikiwemo tuhuma za kuchukua Rushwa ili kuwaacha wafugaji waendelee kuishi na kuharibu msitu.

  Mara Baada ya Mwenyekiti huyo kujiuzulu katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Aliagiza kuitishwa Mkutano wa wananchi haraka iwezekanavyo ili kuchagua Mwenyekiti mpya ambapo pia ameagiza Mwenyekiti huyo kutiwa nguvuni ili kulisaidia Jeshi la polisi kubaini wahujumu wa msitu huo.

  Mhe Mtaturu pia aliliamuru Jeshi la polisi kumtafuta popote alipo aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Kazizi Ndg Kurwa Maduka kutokana na tuhuma zinazomkabili ikiwemo kuzuia wananchi kuhama katika msitu huo Jambo ambalo Ni kosa kisheria.

  Usiku wa kuamkia Octoba 17, 2017 Mhe Mtaturu aliongoza Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Ikungi kuwasaka na kuwakamata wavamizi wa msitu wa Minyughe wanaoendesha shughuli za kibinadamu ikiwemo Makazi, kilimo na Ufugaji kinyume na Tangazo la serikali (GN) ya kuanzisha hifadhi ya msitu wa Minyughe ya Mwaka 2007.

  Katika Oparesheni hiyo Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na mambo mengine pia iliyobaini ukiukwaji wa taratibu unaofanywa na baadhi ya viongozi wa Vijiji na Vitongoji ikiwemo kuwauzia mavamizi maeneo kwa kutoa Rushwa ya fedha au Mifugo.

  Mhe Mtaturu ameiagiza Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Kuwahoji wote wanaotuhumiwa katika sakata la kuruhusu wavamizi wa hifadhi ya msitu.

  Alisema kuwa Ni aibu kubwa kwa viongozi kujihusisha na tuhuma mbalimbali zinazoichafua serikali, Kuvunja heshima na Uaminifu wa wananchi kwa serikali yao.

  "Dhambi ya viongozi kuwaacha kwa makusudi wananchi waharibu misitu itaendelea kuwatafuna viongozi hao kwani wamewasababishia wananchi kuingia hasara ya kuchomewa nyumba zao ambazo walidhani Ni makazi ya kudumu, Ni dhahiri kuwa hatuwezi kuvumilia Nchi ikawa inaongozwa ovyo ovyo ilihali Kuna sheria, taratibu na kanuni" Alikaririwa Mhe Mtaturu

  Mhe Mtaturu pia alisema kuwa ili kunusuru misitu kuharibiwa na wavamizi  itaundwa Bodi ya Misitu ambayo itashirikisha Wajumbe kutoka kila Kijiji katika Vijiji 24 vlivyopo katika Kata 8 zilizopitiwa na msitu huo wa hifadhi.

  Pia aliwataka viongozi wa Vijiji, Kata na Kamati zote za misitu kushirikiana kwa karibu na serikali ili kutunza misiti kwani ndio Msingi wa uimarishaji wa Mazingira na uoto wa asili.

  Mhe Mtaturu alisema kuwa dhamira ya kuhifadhi misitu Ni kutunza Mazingira na uoto wa asili hivyo wananchi kufanya shughuli za kibinadamu Ni kinyume na sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2002.

  Sambamba na hayo pia Mhe Mtaturu aliwasihi wananchi kuanza kuandaa mashamba kwani msimu wa Kilimo umekaribia huku akiwasisitiza kuendelea kumuunga Mkono Rais wa Awamu ya Tano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi kubwa ya kusimamia Rasilimali za Nchi anayoifanya.

  Mhe Mtaturu alichangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya ukarabati wa jengo litakalotumika kwa ajili ya kituo cha polisi cha muda huku Akielekeza wananchi, serikali ya kijiji na Kata kusaidia ukarabati wa kituo hicho sambamba na ujenzi wa kituo kipya cha Polisi cha Kata ya Makilawa.

  Hifadhi ya msitu wa Minyughe ilianzishwa kwa Tangazo la serikali (GN) Mwaka 2007 ina jumla ya hekta 264,600 ina manufaa makubwa katika utunzaji wa mazingira na uoto wa asili kwa urahisi wa upatikanaji wa mvua na urahisi katika uimarishaji wa sekta ya kilimo sambamba na ushoroba (Njia ya Tembo).

  MWISHO.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi cheti cha kuhitimu Kidato cha Nne mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jitegemee ya Jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 33 ya Shule ya hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Brigedia Jenerali Mstaafu Lawrence Magere. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo Luten Kanali Robert Kessy.JT5b
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi cheti na zawadi ya kuwa mwanafunzi bora katika somo la Historia  Kidato cha Nne mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jitegemee alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 33 ya Shule ya hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Brigedia Jenerali Mstaafu Lawrence Magere.JT6
  Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Jitegemee ya Jijini Dar es Salaam wakiwa katika Mahafali ya 33 ya Kidato cha Nne ya shule hiyo leo.JT7
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akikabidhiwa risala ya wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Jitegemee ya inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati wa Mahafali ya 33 ya Shule hiyo leo Jijini Dar es Salaaam.
  JT8
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akionyesha zawadi ya picha yake aliyopewa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya Jijini Dar es Salaam inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 33 ya Shule hiyo leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya Jijini Dar es Salaam inayomilikiwa ma Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Mstaafu Lawrence Magere.
  JT9
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali (kulia) Dkt. Hassan Abbasi akiongozana na  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya Jijini Dar es Salaam inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luten Kanali Robert Kessy wakati akiondoka shuleni hapo alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 33 ya Kidato cha Nne ya Shule hiyo leo.
  JT0a
  Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 33 ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
  JT0aa
  JT0b
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya Jijini Dar es Salaam inayomilikiwa ma Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Mstaafu Lawrence Magere akizungumza wakati wa mahafali ya 33 ya shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam
  JT0c
  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya Jijini Dar es Salaam inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luten Kanali Robert Kessy akizungumza wakati wa mahafali ya 33 ya shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Brigedia Jenerali Mstaafu Lawrence Magere.
  JT1
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya Jijini Dar es Salaam inayomilikiwa ma Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Mstaafu Lawrence Magere alipowasili kwa ajili ya kuongoza mahafali ya 33 ya shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katika ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya Jijini Dar es Salaam inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luten Kanali Robert Kessy.
  JT2
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya Jijini Dar es Salaam inayomilikiwa ma Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipowasili kwa ajili ya kuongoza Mahafali ya 33 ya Shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
  JT3
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akivalishwa Skafu na mmoja wa Skauti wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya Jijini Dar es Salaam inayomilikiwa ma Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipowasili katika shule hiyo kwa ajili ya kuongoza Mahafali ya 33 ya Shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
  JT4
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiangalia vitabu alipotembelea Maktaba ya  Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya Jijini Dar es Salaam inayomilikiwa ma Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati wa Mahafali ya 33 ya Shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

  Picha na: Frank Shija – MAELEZO

  0 0


  Aslay akiwa jukwaani akiburudisha wakazi wa Sumbawanga kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga usiku wa kuamkia jumapili

  Mashabiki wakiimba pamoja na Aslay.

  Msanii Barnaba akiwa jukwaani kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja
  wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga usiku wa kuamkia jumapili.
  Benpol akitumbuiza wakazi wa Sumbawanga jukwaani kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga usiku wa kuamkia jumapili

  asanii Chege na Aslay wakiwa jukwaani wakiimba pamoja kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga usiku wa kuamkia jumapili
  Mimi Mars naye aliburudisha maelfu ya wakazi wa Sumbawanga usiku wa kuamkia jumapili katika tamasha la Tigo Fiesta.
  Wasanii Roma Mkatoliki na Stamina (ROSTAM) wakiwa jukwaani wakiimba pamoja kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga usiku wa kuamkia jumapili

  0 0

  Meneja Mkazi wa Statoil, Øystein Michelsen, akizungumzia umuhimu wa ujenzi wa Mtambo wa Kusindika Gesi ya Kimiminika (LNG) wakati wa warsha ya siku moja ya waanahabari (hawapo pichani) iliyofanyika kwenye makao makuu ya kampuni hiyo, Masakini jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya washiriki wa warsha ya uelewa wa sekta ya mafuta na gesi iliyoandaliwa na kampuni ya Statoil Tanzania katika ofisi zake zilizoko Masaki jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa taasisi ya Environmental Media Agenda – EMA, Secelela Balisidya (kushoto), akibadilishana mawazo na mwandishi mwandamizi, Nelson Goima, kabla ya kuanza kwa warsha ya uelewa wa sekta ya mafuta na gesi iliyoandaliwa na Statoil na kuratibiwa na taasisi yake na kufadhiliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori Duniani (WWF).

  Na Daniel Mbega

  KAMPUNI ya utafiti na uchimbaji wa gesi ya Statoil ya Norway imesema serikali inapaswa kuona kipaumbele cha kufikia makubaliano ya kujengwa kwa mtambo wa kusindika gesi ya kimiminika (Liquified Natural Gas – LNG) kwa faida ya usafirishaji wa gesi hiyo kwenye soko la kimataifa pamoja na matumizi ya ndani.

  Akizungumza mwishoni mwa wiki katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na kampuni yake, Meneja Mkazi wa Statoil, Øystein Michelsen, alisema mtambo wa LNG ndio utakaosaidia kuchakata na kusindika gesi hiyo ili kurahisisha kuisafirisha nje.

  “Huwezi kusafirisha gesi katika hali yake ya kawaida, ni lazima kuisindika kwa kuibadili kuwa katika hali ya kimiminika, hivyo mtambo wa LNG una umuhimu mkubwa kwa biashara ya gesi kwa kusafirisha kwenye soko la kimataifa pamoja na matumizi ya ndani,” alisema Michelsen.

  Statoil na mshirika wake ExxonMobil wamefanya ugunduzi mkubwa wa gesi asilia katika visima vya Zafarani, Lavani, Tangawizi, Piri, Giligilani na Mronge katika Kitalu namba 2, chenye eneo la takriban kilometa za mraba 5,500, ambalo lipo umbali wa zaidi ya kilometa 100 kutoka ufukweni katika kina cha maji kati ya meta 1,500 hadi 3,000. 

  MaendeleoVijijini inafahamu kwamba, Statoil na ExxonMobil vilevile wanafanya kazi kukuza maeneo mengine tarajiwa katika kitalu hicho na wamekamilisha upatikanaji wa taarifa za kitaalam katika maeneo hayo, ambapo kwa mujibu wa Michelsen, wanatarajia kuchimba kisima kingine kuanzia Januari 2018. 

  Katika warsha hiyo iliyofanyika kwenye makao makuu ya kampuni hiyo, Masakini jijini Dar es Salaam na kuratibuwa na taasisi ya Environmental Media Agenda (EMA) na kudhaminiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori (WWF), ilielezwa kwamba, umuhimu wa kujenga mtambo huo utasaidia kuongeza mapato ya taifa, kutengeneza fursa nyingi za ajira kwa wazawa na kukuza uchumi.

  “Tunaangalia namna ya kuzungumza na serikali kuona watachukua hatua gani na lini kuruhusu ujenzi wa mtambo wa LNG, serikali haijaamua kwa kuwa inaonekana kama iko bado iko kwenye maandalizi ya kanuni na taratibu hasa baada ya kupitishwa kwa sheria mpya za gesi na mafuta, hata hivyo inapaswa kuangalia vipaumbele ili kufanikisha mradi huu,” aliongeza Michelsen.

  Mapema mwaka huu wa 2017, serikali ilisema kwamba mtambo huo wa LNG utajengwa mara baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria.

  MaendeleoVijijini inafahamu kwamba, katika ujenzi wa mtambo wa LNG, gharama zote zitalipwa na wawekezaji wakati serikali jukumu lake ni kutoa ardhi mahali mtambo huo utakapojengwa.

  Kampuni ya Statoil na mshirika wake ExxonMobil ya Marekani ambazo zinamiliki Kitalu namba 2 kwa asilimia 65 na 35 mtawalia ambazo zimegundua kiasi cha futi za ujazo trilioni 22 kwenye eneo hilo, ziliingia ushirika na kampuni za BG (Shell), Ophir na Pavillion zinazomiliki vitalu namba 1 na namba 4 ili kujenga mtambo huo.

  Shughuli hiyo ya pamoja itakuwa ya kwanza nchini ambako hadi sasa akiba ya gesi yenye futi za ujazo zaidi ya trilioni 57 imegundulika nchini kote. 

  Hata hivyo, ratiba ya utekelezaji wa mradi huo bado haijawekwa wazi ingawa tayari eneo maalum la ujenzi wa mtambo huo limekwishapatikana mkoani Lindi na taarifa zinasema tathmini inatakiwa kufanyika ili kuwalipa fidia wananchi pamoja na kuwatafutia eneo jingine.

  Statoil na BG walipendekeza mtambo wa gesi ya kimiminika ujengwe eneo la Likong’o-Mchinga kusini mwa mji wa Lindi. 

  Tayari serikali imetenga eneo lenye ukubwa wa hekta za mraba 2,071.705 (ekari 5,119) katika Kijiji cha Likong'o kusini mwa mji wa Lindi katika mwambao wa bahari ya Hindi, takriban kilometa 460, kwa barabara, kusini mwa Dar es Salaam. Huo ni umbali wa kilometa 103 kaskazini-masharibi mwa mji wa Mtwara, ambao uko jirani.
  Kwa mujibu wa mkataba, MaendeleoVijijiniinafahamu kwamba, pamoja na kuisafirisha katika soko la kimataifa, lakini asilimia 10 ya gesi itakayopatikana itasambazwa kwa matumizi ya ndani ya nchi, na serikali inaweza kuuza ziada kwa nchi jirani zenye uhitaji.

  Mkuu wa kitengo cha uwezeshaji cha Statoil, Profesa Richard Rwechungura, aliwaeleza waandishi wa habari kwamba, gesi iliyowekwa katika hali ya kimiminika (LNG), ni safi, isiyo na rangi, yenye kimiminika kisicho na sumu, inayotengenezwa kwa kuipoza gesi ya asili kufikia kipima joto cha Sentigredi -163°, ambapo inakuwa kimiminika na husindikwa hadi mara 615 ya gesi iliyo katika muundo wa hewa. 

  “Mchakato huu hufanywa ili kurahisisha usafirishaji wa gesi asilia uwe na ufanisi zaidi kwa kutumia maroli au meli,” alisema.
  Zaidi ya hayo, gesi ya kimiminika hailipuki katika mazingira yasiyodhibitiwa, kwa hiyo, katika hali isiyotegemewa ya kumwagika kwa gesi ya kimiminika, gesi hiyo inakuwa na uwezekano mdogo wa kutoa mlipuko.


  Faida nyingine za gesi ya kimiminika inajumuisha ukweli kwamba mchakato wa kuifanya kimiminika unapunguza oksijeni, carbon dioxide, salfa na maji kutoka kwenye gesi hiyo, inayofanya gesi hiyo kuwa karibu na metheni asilia. Gesi hiyo ikifikishwa mwisho wa safari yake, huifadhiwa katika hali yake ya kimiminika hadi inapotiwa joto tena kurudi katika hali yake ya gesi ya asilia.


  0 0

  Naibu waziri wa TAMISEMI MH.Joseph Kakunda ameipongeza kampuni ya AVIV limeted iliyopo mkoani ruvuma inayojishughulisha na kilimo cha kahawa,waziri Kakunda amesema hayo wakati ziara yake katika mkoa huu kwa siku habari ikamili hii hapa video yake.

  0 0

  NA HAMZA TEMBA - WMU - DODOMA
  ...................................................................................
  Katika kile alichoeleza kuwa ni kuimarisha sekta ya maliasili na utalii iweze kutoa mchango unaostahili kwa jamii na taifa kwa ujumla, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amesitisha utaratibu wa kuhuisha upya vibali vyote vya makampuni ya uwindaji wa kitalii ambavyo vilitolewa mwaka huu mwezi Januari ili kupisha utaratibu mpya wa utoaji wa vibali hivyo kwa njia ya mnada.

  Dk. Kigwangalla ametangaza uamuzi huo jana mjini Dodoma katika mkutano alioutisha wa wadau wa sekta ya maliasili na utalii ambao ulilenga kukusanya maoni, kero na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo muhimu nchini kwa ajili ya kuzitafutia utatuzi wa haraka.


  “Kwa mamlaka niliyopewa na sheria ya wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009, nimeamua bila kushawishiwa na mtu yeyote yule wala kushauriwa na mtu yeyote yule zaidi ya kusikiliza tu ushauri wa kitaalamu na ushuari wa ndugu yangu Mhe.  Naibu Waziri, lakini  sasa hivi ninavyotamka haya sijamshirikisha mtu yeyote yule, nimeamua kwa mamlaka yangu, nasitisha vibali vyote  vya uwindaji wa makampuni ambavyo vilitolewa mwaka huu mwezi Januari kwa maana ya ‘kurenew’ (kuhuisha).


  “Nasitisha ili kupisha mchakato wa kutengeneza taratibu mpya za kuendesha ugawaji wa vitalu kwa njia ya mnada, tunataka twende kwenye ‘auction’ (mnada) ya vitalu, na auction (mnada) iwe ya wazi, iwe na faida kubwa  zaidi, na natoa siku sitini utaratibu huo uwe umekamilika ili tuweze kuendesha ‘auction’ (mnada) kabla ya muda wa kuanza kwa awamu ya miaka mitano ambayo ni january 2018 mpaka 2022.


  “Kwahiyo ndani ya siku sitini, wataalam mkae mniletee utaratibu wa namna bora zaidi ya uwazi inayotoa haki ya kugawa vitalu lakini pia yenye faida kubwa zaidi kama tunavyoelekezwa na mpango wa taifa wa miaka mitano kwamba ni lazima vitalu vyote vifanyiwe ‘auction’ (mnada)”. alisema Dk. Kigwangalla.


  Alisema utaratibu huo hautahusisha vitalu vilivyopo kwenye maeneo yenye migogoro ya ardhi kwa sasa mpaka pale migogoro hiyo itakapomalizika.


  “Ni mwiko kugawa vitalu kwenye maeneo yenye mgogoro, kuna maeneo kama vitalu vilivyopo Loliondo, kuna mgogoro, ni mwiko kugawa vitalu, kuna maeneo kama Lake Natron kuna mgogoro, mwiko kugawa vitalu, mpaka tutatue migogoro kwanza, Kama kuna mtu alipewa kibali huko nyuma ajue hicho kibali cha renewal  kimekufa leo na mimi ndio nimekiua” alisema Dk. Kigwangalla.


  Kuhusu uwindaji wa Wenyeji kwenye maeneo ya wazi uliosimamishwa kwa muda wa miaka miwili sasa, Dk. Kigwangalla alitoa muda wa siku sitini kwa watendaji wa wizara yake kukamilisha masharti mapya ya uendeshaji wa biashara hiyo na kuyawasilisha kwake aweze kuyasaini ili kufungulia biashara hiyo.


  “Natoa siku sitini, wataalam wetu mnaohusika na utoaji wa vibali vya uwindaji wa wenyeji mkamilishe masharti mapya mniletee nisaini tutoe vibali, hatuwezi kuzuia wenyeji wanufaike na rasilimali ambazo ziko huko vijijini alafu tukaruhusu makampuni ya watu kutoka nje kuja kuwinda wakaondoka na nyama, ni lazima tutoe haki kwa wazawa kama wapo wanaovunja masharti sisi tudhibiti na tusimamie sheria” alisema Dk. Kigwangalla.


  Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mej. Jen. Gaudence Milanzi kuwasiliana na Msajili wa Hazina kwa ajili ya kuanza mchakato wa kuzirudisha serikalini hoteli za kitalii kumi zilizobinafsishwa miaka 1990 kufuatia kushindwa kutimiza masharti ya mkataba wa uendeshaji.


  “Niagize Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii uwasiliane na mamlaka ambayo ina dhamana ya kushikilia mali zilizokuwa za Serikali ambazo ziliuzwa kwa maana ya msajili wa hazina, umueleze nimetoa agizo kwamba hizi hoteli zote ambazo zimekiuka masharti na hivyo kuathiri utendaji wa sekta ya utalii nchini na hivyo kuathiri uchumi mpana wa taifa letu, zichukuliwe na zirudi kuwa mali ya serikali ili serikali ipate fursa ya kuzitangaza upya na kutafuta waendeshaji wapya watakaoweza kuendesha hoteli hizi  kwa tija na ufanisi kwa maana ya kukuza sekta ya utalii ambayo inachangia asilimia 17 ya pato la taifa.


  “Nimetoa agizo hoteli hizi 10 ambazo zimeshindwa kukidhi masharti ya mikataba ya mauziano, mchakato wa kuzirudisha Serikalini uanze mara moja na ukamilike ndani ya siku sitini.


  Alisema kumekuwepo na changamoto kubwa ya uhaba wa vyumba katika sekta ya utalii hali iliyosababishwa na ubinafsishaji wa hoteli 17 za Serikali uliofanywa miaka 1990 kwa nia njema ya kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa hoteli hizo kupitia sekta binafsi lengo ambalo halikufikiwa kwa baadhi ya hoteli hizo.


  “Baada ya kufanya uchunguzi katika hoteli zote 17 tulizouza ni saba tu zinafanya vizuri, hoteli zinazofanya vizuri na zimekidhi masharti yote ambayo yalikuwepo kwenye ile mikataba ni Kilimanjaro Hotel, Kunduchi Beach Hotel, Mt. Meru Hotel, New Africa Hotel, New Safari Hotel, Mafia Highland Hotel na Hotel 77.


  “Hoteli 10 zimeshindwa kukidhi masharti ya mikataba ya mauziano na mwaka ulioisha Serikali ilifanya uchunguzi kwenye hoteli nyingine nne kati ya hizo 10 ambazo ni Robo Wildlife Lodge, Seronera Wildlife Lodge, Ngorongoro Wildlife Lodge na Lake Manyara Hotel, na zote zilionesha zipo chini ya kiwango na hazikidhi mahitaji.


  “Kwa kuwa watu hawa wamekiuka masharti ya ubinafsishaji kama walivyopewa wakati wananunua hizo hoteli ni wakati muafaka sasa kwa Serikali kuvunja hii mikataba kuzichukua hizi hoteli na kuzibinafsisha kwa watu wengine watakaoweza kuziendesha kwa faida lakini pia kuziendesha kwa tija zaidi” alisema Dk. Kigwangalla.


  Awali akijibu baadhi ya hoja za wadau wa mkutano huo kuhusu wizara yake kuwa na vishawishi vingi vya rushwa na fitna ambazo husababisha viongozi wengi kutodumu kwenye nafasi zao, Dk. Kigwangalla alisema kamwe hatoruhusu hali hiyo ijitokeze kwa kuwa hata aliyemteua anamjua vizuri kuwa ni muarobaini wa changamoto hizo.


  “Mimi nipo hapa kwenye hiki kiti, na nitakuwepo kama sababu ni hiyo ya maslahi, Mimi sihongeki, sinunuliki, na sishawishiki, najua hata aliyeniweka hapa ananijua vizuri, kwahiyo alivyoniweka hapa alishajua hii ni dawa, muarobaini.


  “Watu wote humu ndani tuna njaa, lakini njaa yangu nabaki nayo mwenyewe, bora nife kwa heshima zangu kuliko kuaibika na kudharaulika kwa kuchukua rushwa ama kwa kutokutenda haki ama kwa kumuonea mtu.


  “Hilo nina uhakika nalo, kwa maana ya rushwa, maslahi ya kibiashara hapana, hutonikuta mimi huko, na kama kuna mdau mmoja anadhani kuna siku anafkiria anaweza kuja kuongea na mimi kwa maslahi binafsi akaweka mbele mazingira ya rushwa, sana sana ataona nimemuaga na kikao chetu kimeishia hapo, kwahiyo ukija kwangu njoo na ishu ambayo ipo straight maslahi ya umma yapo ndani yake utaraibu wa kisheria upo”. Alisema Dk. Kigwangalla.


  Miongoni mwa maagizo mengine aliyoyatoa kwenye kikao hicho kwa watendaji wa wizara yake ni kuandaa taratibu za kuanzishwa kwa mwezi maalumu wa kuadhimisha utamaduni wa Mtanzania (Tanzania Heritage Month), Makumbusho ya Marais wa Tanzania (Presidential Museum) na Utalii wa Mabasi kwa Miji ya Dar es Salaam na Arusha (Dar Bus Tour/ Arusha Bus Tour) ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa watalii katika miji hiyo.


  Katika mkutano huo wadau wa maliasii na utalii walipata fursa ya kutoa maoni, mapendekezo ushauri na kero mbalimbali wanazokumbana nazo katika sekta hiyo ambazo ziliahidiwa kufanyiwa kazi kwa haraka na Waziri Kigwangalla.  Miongoni mwa ushauri na mapendekezo waliyotoa ni pamoja na kuanzishwa kwa mamlaka moja inayosimamia rasilimali za misitu nchini na kufunguliwa kwa biashara ya kusafirisha viumbe hai nje ya nchi.


  Mkutano huo wa siku moja ulihudhuriwa na viongozi wakuu wa Wizara ya Maliasili ambao ni Naibu Waziri, Mhe. Japhet Hasunga, Katibu Mkuu, Mej. Jen. Gaudence Milanzi, Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki, Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo.  Wengine ni wadau zaidi ya 200 kutoka sekta mbalimbali ya maliasili na utalii ambao ni wawakilishi kutoka vikundi, taasisi, vyama na vyombo mbalimbali vinavyoshughulika na utoaji wa huduma katika sekta ya utalii, wanyamapori, misitu na nyuki pamoja na waandishi wa habari. 

  Waziri wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa sekta ya maliasili na utalii kutoka nchi nzima katika mkutano aliotisha mjini Dodoma jana kwa ajili ya kupokea maoni, kero na ushauri mbalimbali wa kuboresha sekta hiyo. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga na kushoto kwake ni Katibu wa Wizara hiyo, Mej. Jen. Gaudence Milanzi. 
   Waziri wa wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa sekta ya maliasili na utalii kutoka nchi nzima katika mkutano aliotisha mjini Dodoma jana kwa ajili ya kupokea maoni, kero na ushauri mbalimbali wa kuboresha sekta hiyo. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga. 
   Mkutano ukiwa unaendelea.
   Mkuu wa Wilaya Chemba, Simon Odunga ambaye kabla ya kupewa nafasi hiyo na Mhe. Rais alikuwa mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii akichangia katika mkutano huo.
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili, Dkt. Aloyce Nzuki akchangia hoja katika mkutano huo.
   Baadhi ya wadau wa sekta ya maliasili na utalii ambao walioshiriki kwenye mkutano huo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexandre Songorwa akijibu baadhi ya hoja zilizoibuka katika mkutano huo.
   Mdau wa maliasili na utalii kutoka Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Asser Mwambene akichangia hoja katika mkutano huo.
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo akijibu baadhi ya hoja zinazohusu taasisi yake kwenye mkutano huo.
   Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akijibu baadhi ya hoja kuhusu Idara yake katika mkutano huo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA, Dkt. Alan Kijazi akijibu baadhi ya hoja za shirika lake katika mkutano huo.
   Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dkt. Fredy Manongi akijibu baadhi ya hoja kuhusu mamlaka hiyo katika mkutano huo.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori, Dkr. James Wakibara akijibu baadhi ya hoja kuhusu mamlaka hiyo katika mkutano huo.
   Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Mlozi akichangia baadhi ya hoja kuhusu chuo hicho katika mkutano huo.

  0 0

  Na Binagi Media Group.
  Ni katika Mahafali ya 11 ya darasa la saba shule ya msingi Eden iliyopo Nyakato Jijini Mwanza, mamia ya wahudhuriaji yanashuhudia wahitimu wakiuchambua ubongo wa mwanadamu kwa kiwango cha hali ya juu.

  Mahafali yalifanyika ijumaa Septemba Mosi,2017 shuleni hivyo tazama video hii kisha kama una mwanao wasiliana na uongozi wa shule za Eden (Awali, Msingi na Sekondari) kwa nambari 0765 80 63 51 au 0768 93 54 76 ili mwanao akasome katika shule hizo ambapo matokeo ya darasa la saba mwaka huu wanafunzi wote 74 wamefaulu.
  Bonyeza BMG Habari, Pamoja Daima picha za mahafali

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo ya uharibifu wa tuta la mto mkondoa mjini Kilosa kutoka kwa Meja. Yenu Mgugule, kulia kwa Waziri ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brg. jen. Mbazi Msuya.
  Muonekano wa tuta la mto mkondoa mjini Kilosa ambalo limeanza kupasuka kutokana na shughuli za kibinadamu zinazofanywa kando ya mto huo na baadhi ya wananchi wa mji huo. Tuta hilo lenye urefu wa km 4.36 na kimo cha wastani wa mita 5 lilijengwa na serikali baada ya tuta la awali kuharibika kutokana na mafuriko yaliyotokea mwaka 2010.
  Sehemu ya tuta la mto mkondoa mjini Kilosa ambayo nyasi zinazozunguka tuta hilo kuzuia maji wakati wa mafuriko zimechomwa moto na baadhi ya wananchi wa mjini humo. Nyasi hizo zilipandwa na Jeshi la Wananchi Tanzania waliokuwa na jukumu la urejeshaji wa tuta hilo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea na wananchi wa mjini Kilosa (hawapo pichani), ambapo alielekeza Halmashauri hiyo kuw na mpango mkakati wa kulilinda tuta hilo pamoja na kuwaonya wananchi kufanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa tuta hilo.
  Baadhi ya Wananchi wa mjini Kilosa wakinyoosha mikono kuashiria kuunga mkono magizo juu ya kulilinda tuta la mto mkondoa kwa kutofanya shughuli za kibinadamu zilizokuwa zinaendelea pembenzoni mwa mto na tuta. Maagizo hayo yalitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).


  Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  0 0

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha zoezi la ukamataji wa wezi wa kazi za sanaa kwa kurudufu bila kibali na kuwauzia watu kwenye simu zao za mkononi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya haki miliki na haki shiriki.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama  akiwa amebeba vifaa  vilivyokamatwa ambavyo vinatumika kurudufu kazi za wasanii

   Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama  akionyesha watu wanaotakiwa kukamatwa ambao wamekutwa wanafanya kazi ya kurudufu kazi za wasanii
   Askari wa jeshi la Polisi wakiwa wamemkamata mmoja wa wezi wa kazi za wasanii wanaorudufu kwa kutumia kompyuta eneo la Kariakoo
   Askari wa jeshi la Polisi wakiwa wamemkamata mmoja wa wezi wa kazi za wasanii wanaorudufu kwa kutumia kompyuta eneo la Kariakoo
   Askari wa jeshi la Polisi wakiwa wamemkamata mmoja wa wezi wa kazi za wasanii wanaorudufu kwa kutumia kompyuta eneo la Kariakoo ambapo Msama SAuction Mart inafanya zoezi la kuwakamata watu wanaorudufu kazi za Wasanii kwa kutumia Kompyuta.
   Vijana wa kazi kutoka Msama Auction Mart wakipakia vyombo vinavyo tumika kurudufu kazi za wasanii kinyume cha Sheria.

  0 0

  Mamlaka ya mapato nchini (TRA) iliendesha na kudhamini shindano la shule za sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani jijini humo. Mashindano hayo yaliyoshirikisha shule mbalimbali za Dar es salaam na Pwani lilipambwa na maigizo ya maswala ya kodi ambapo mgeni Rasmi alikuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere.

  Shule ya Sekodari Misitu iliyotia fora katika ufunguzi wa mashindano hayo ulimvutia mgeni rasmi na kudhamiria kushiriki mashindano hayo mwanzo hadi mwisho ambapo alipata fursa ya kujionea na kufurahia vipaji vya wanafunzi waliondaliwa vyema kuwa mabalozi wa maswala ya kodi katika nyanja mbalimbali kwa sasa na siku zijazo.

  Baada ya kufungua mashindano hayo yaliyonogeshwa na wanafunzi wenye vipaji mbalimbali vya kuwasilisha mada hatimaye shule ya sekondari Tumbi iliibuka kidedea na kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo Kombe, Luninga ya Kisasa, Saa ya Ukutani pamoja na cheti. Shule ya Sekondari Minaki ilichukuwa nafasi ya pili ikijinyakulia pia Kikombe, Komputa, Printa, Saa ya ukutani na cheti huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Shule ya Sekondari Maarifa ambayo kadhalika ilipata Kikombe, Komputa, Saa ya Ukutani pamoja na cheti.

  Hadija Jumanne Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Misitu aliibuka Muwasilishaji mada bora na kujinyakulia Komputa mpakato, Saa ya Ukutani, Kikombe cha chai chenye chapa ya TRA. Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere baada ya kukunwa na uzuri wa mashindano hayo aliahidi kuyaboresha zaidi mwakani ili kuwapa motisha zaidi wanafunzi na walimu wao kujiandaa vyema na kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kodi ambayo ndio mhimili muhimu wa kuboresha huduma za jamii na kuleta maendeleo kwa nchi.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akiwasili ukumbi wa Chuo cha Kodi (ITA) kuhudhuria mashindano ya Kodi kwa Shule za Sekondari za Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani yaliyoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka (kulia) ni Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akimkabidhi Hadija Jumanne Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Misitu baada ya kuibuka mwanafuzi bora katika uwasilishaji wa mada ihusuyo kodi ya ongezeko la thamani (VAT), wakati wa shindano la maswali ya Kodi lililoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho. Pamoja naye (kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna wa idara ya walipakodi wakubwa, Yeremiah Mbaghi na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)


  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akimkabidhi Mwalimu shule ya Sekodanri Jangwani zawadi ya kikombe baada wakati wa shindano la maswali ya Kodi lililoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho. Pamoja naye (kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna wa idara ya walipakodi wakubwa, Yeremiah Mbaghi, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo (wa tatu kulia) na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee wakiwa wamembeba mwalimu wao Boniface Mulambo baada yakukadidhiwa zawadi ya Kikombe na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere kwa kuwaandaa vyema wanafunzi wake walioshiriki mashindano hayo.

  0 0

  Sehemu ye Ukuta Mkubwa ndani ya Mji wa Beijing nchini China (The Great Wall),kama uonekanavyo pichani mapema leo mchana,ambapo Maelfu ya watu wakiwemo Wenyeji na wageni hufurika kutembelea ukuta huo wenye historia kubwa nchini humo.Kuusoma zaidi BOFYA HAPA,Ukuta huo umekuwa kivutio kikubwa kwa wenyeji na wageni mbalimbali ambao wamekuwa wakifurika kila kukicha na kujionea historia kubwa ya ukuta huo nchini China,inaelezwa kuwa ukuta huo ni mojawapo ya chanzo kikubwa cha mapato katika nchi hiyo hasa kwa upande wa sekta ya Utalii.

  Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies wapita maelezo mafupi kutoka kwa wenyeji wao kabla ya kupanda Ukuta wa The Great Wall mapema leo mchana,ikiwa ni sehemu ya kujifunza,kuona na kutazama fursa mbalimbali za Kiutalii mjini humo na namna wenyeji wa mji wa Beijing wanavyofanya shughuli zao kiutalii.
  Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies na baadhi ya wenyeji wakielekea kwenye geti kuu la kuingilia Ukuta huo wa The Great wall,mapema leo mchana.
  Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies wakiwa na Mwenyeji wao,wa tatu kulia wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya The Great Wall,mjini Beijing nchini China.Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies Mohamed Said Kiluwa (mwenye njano),akipata maelezo mafupi kutoka kwa mmoja wa wadau wake aliombatana nao Risasi Mwaulanga,huku baaadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani wakisikiliza kwa makini,kulia ni Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha,Mansoury Kisebebo pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani (pichani kati)Zuberi Mhinana na nyuma yake ni Katibu Tawala Msaidizi – Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala pamoja 
  Sehemu ye Ukuta Mkubwa ndani ya Mji wa Beijing nchini China (The Great Wall),kama uonekanavyo pichani mapema leo mchana,huku ukiwa mesheheni Maelfu ya watu wakiwemo Wenyeji na wageni (watalii) wakipanda ukuta huo ikiwa kama sehemu ya utalii na kujua historia ya ukuta huo uliopo nje kidogo ya mji wa Beijing nchini China.
  The Great Wall ndani ya mji wa Beijing kama uonekanavyo mapema leo.

  Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies wakiwa katika  picha ya pamoja mapema leo mara baada ya kupanda Ukuta wa kihistoria ndani ya mji wa Beijing,nchini China
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies Mohamed Said Kiluwa akiwa na Wenyeji wake,ambao kwa pamoja wanatarajia kuandaa kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda kwa kuwaalika viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Pwani (ambao tayari wamekwishawasili mjini humu),wafanyabiashara wakubwa ambao ni wamiliki wa viwanda na makampuni mbalimbali,litakalofanyika jijini Beijing,nchini China Oktoba 25,2017 ,litakalojumuisha wafanyashabiashara, wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.

  0 0

  Mgeni rasmi ambaye ni afisa elimu manispaa ya Iringa MWL .Tupe Kayinga akizungumza na walimu wanawake waliojitokeza kuelekea mkutano mkuu wa chama cha walimu manispaa ya Iringa.
  katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale akizungumza na walimu wanawake waliojitokeza kuelekea mkutano mkuu wa chama cha walimu manispaa ya Iringa.
   Baadhi ya walimu wanawake waliohudhuria mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.


  Na Fredy Mgunda,Iringa.

  Walimu wanawake manispaa ya Iringa walalamikia kutokuwepo kwa uwiano wa viongozi wanawake na wanaume katika sekta nyeti kama vile wakuu wa shule,maafisa elimu kata na wilaya wakati walimu wa wanawake ndio wengi hivyo inafifisha ndoto za kuwa viongozi kwa kuwa wanauwezo wa kuongoza na kusimamia mambo mengi yakaenda kama yalivyopangwa.


  Hayo yamesemwa na walimu wanawake katika mkutano mkuu wa chama cha walimu wanawake kilichokuwa kinaongozwa na katibu wa wilaya mwl. Fortunata Njalale katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.


  Akisoma risala iliyoandaliwa na kamati ya kitengo cha walimu wanawake MWL. Evon Mhewa alisema kuwa walimu wanawake wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi katika kukamilisha majukumu yao.


  “Mwalimu wa kike anacheleweshewa kulipwa madeni mbalimbali anayokuwa anaidai serikali maana bila kulipwa madeni yetu walimu hawawezi kufundisha kwa moyo kwa kuwa maisha yanakuwa magumu na kuwapelekea kubuni njia mbadala za kujiingizia kipato” alisema Mhewa


  Mhewa alizitaja changamoto nyingine ni kutopata nyongeza ya mishahara ya kila mwaka na kusimama kwa mwaka wa pili sasa,walimu kutopandishwa madaraja na wengine kupandishwa na kupokwa mshahara pamoja na walimu wanawake kutokuwa na uwiano wa vyote katika sekta nyeti.


  “Sisi walimu wa kike kwa sasa tumesoma sana na tunaweza kuwa viongozi sehemu yoyote kwa kuwa tayari tumethibisha hilo kwa wanawake waliopewa kazi hiyo kwani wameifanya ipavyo na kuleta matokeo chanya kwa serikali hivyo tunaomba walimu wanawake tupewa nafasi katika ngazi ambazo tunastahili” alisema Mhewa.


  Akijibu risala hiyo mgeni rasmi ambaye ni afisa elimu manispaa ya Iringa MWL .Tupe Kayinga alisema kuwa ni kweli walimu wanamadi mengi serikalini lakini akasema kuwa hiyo yote imetokana na swala la uhakiki wa watumishi hivyo mchakato wa uhakiki ukimalizika kila kitu kitakuwa sawa ninauhakika na hilo.


  “Unajua serikali imechelewesha maswala mbalimbali ambayo ni kero kwa walimu kutokana na uhakiki hivyo nawaomba walimu wawe na uvumilivu kwa kuwa kila kitu kitakuja kutengemaa kama ilivyokuwa hapo awali” alisema Kayinga


  Kayinga aliwataka walimu wanawake kuendelea kusoma ili kuwa na elimu ndio itakayowapa nafasi mbalimbali ambazo zinashikiriwa na walimu wanaume hivyo bila kuwa na elimu walimu wanawake wataendelea kuongozwa na walimu wanaume kila sekta.


  “Najua kuwa walimu wanawake wanakipawa cha kuwa viongozi lakini mitaala mingi inataka walimu kuwa na elimu ili kupata kuongoza sekta mbalimbali sasa inatubidi walimu kujiendeleza kimasomo ili kukidhivigezo ambavyo mara nyingi imekuwa ni elimu ya walimu anayepaswa kupewa kitendo husika” alisema Kayinga


  Aidha Kainga aliwataka walimu wanawake kugombea nafasi mbalimbali zinazojitokeza ili kupata nafasi za kuongoza na sio kila wakati kuwaacha walimu wanaume wakigombea pekee yao.


  “Tumieni fursa za kugombea nafasi zinazojitokeza msiogope wanawake mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kuogmbea kwa kuwa katika kada ya ualimu walimu wanawake tupo wengi hivyo kuanzia saizi walimu wanawake amkeni mjitume kuhakikisha mnagombea” alisema Kayinga


  Naye katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alisema kuwa mkutano huo ni wa kikatiba kwa mjibu wa katiba ya chama cha walimu taifa hivyo katiba imewaagiza kukaa na viongozi wa walimu wanawake kuzijadili changamoto za wanawake ili kuzipeleka katika mkutano mkuu wa wilaya.


  “Leo tupo walimu wanawake pekee yetu ili kubaini changamoto zetu na kuzipeleka kwenye mkutano mkuu na kuweza kuzitetea kwa pamoja ili kuboresha maslai ya walimu wanawake ambao wamekuwa wanakumbana na changamoto nyingi sana wawapo kazini” alisema  Njalale


  Njalale alisema kuwa walimu wanawake wamekuwa na mwamko wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuwa wanauwezo wa kuwa viongozi na kuongoza kwa kupata matokeo chanya.


  “Tunakitengo cha walimu wanawake taifa kimetusaidia sana walimu wanawake kupata ujalisi na kuacha uoga kugombea nafasi mbalimbali hivyo kwa sasa walimu wakiume wajipange sana maana walimu wanawake tumedhamilia kugombea nafasi yeyeto itakayojitokeza katika chama chetu cha walimu” alisema Njalale  Njalale aliwapongeza walimu wanawake wanaothubutu kugombea nafasi mbalimbali kwa kuwa wamekuwa wakishinda na wanafanya kazi ipasavyo na kusema kuwa walimu wanawake wanaweza bila kuwezeshwa.


  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu  (wa tatu kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi  rasmi wa mashamba darasa ya kilimo bora cha mihogo na migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa (tissue culture), kwa ufadhili  wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB) katika vijiji vya  Bunazi na Kashaba wilayani Missenyi mkoani humo leo. Shamba hilo litasimamiwa na Kikundi cha Ushirika cha Batekaka. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Luteni Kanali, Denis Mwila, Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Belington Kyokwete, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Missenyi, Projestus Tegamaisho.

   Miche ya migomba ikiwa tayari kupandwa.
   Ofisa Ugani wa Kata ya Kasambya, Hakika Ibrahim, akizungumza kataika uzinduzi huo.
   Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein, akizungumza katika uzinduzi huo.
   Mtafiti kutoka OFAB, Dk. Beatrice  Lyimo akizungumza katika uzinduzi huo.
   Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku akielezea mbegu hiyo mpya ya migomba. 

    Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu (wa tatu kulia),  Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein na Mkuu wa  Mkuu wa Wilaya hiyo, Luteni Kanali, Denis Mwila (kulia), pamoja na Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushirika cha Batekaka, Belington Kyokwete, wakiwa wameshika mmoja wa mche wa mgomba katika uzinduzi huo. 

   Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu , akipanda mche wa mgomba kwenye shamba darasa katika Kijiji cha Bunazi.
   Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein, akipanda mgomba kwenye shamba darasa hilo.     Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu , akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kashaba kabla ya kuzindua shamba darasa la zao la mhogo.
   Usikivu katika uzinduzi huo. Kutoka kulia ni Mtafiti kutoka OFAB, Dk. Beatrice  Lyimo, Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Adam Swai na Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein, akipanda mgomba kwenye shamba darasa hilo.
   Wananchi wa Kijiji cha Kashaba wakiwa kwenye uzinduzi huo.
   Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu , akimpongeza kijana, Shafii Idrisa wa Kijiji cha Kashaba ambaye ameamua kujishughulisha na kilimo kijijini hapo badala ya kukimbilia mjini na kuendesha bodaboda kama walivyofanya wenzake.


   Mtafiti wa mazao ya jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku, Jasmeck Kilangi, akimueleza Mkuu wa Mkoa namna ya upandaji wa zao la mihogo.
    Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu, akipanda mbegu ya mhogo katika shamba darasa katika Kijiji cha Kashaba.
  Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Missenyi, Projestus Tegamaisho, akitoa shukurani baada ya uzinduzi huo.


  Na Dotto Mwaibale, Missenyi Kagera

  WAKULIMA  wilayani Missenyi Mkoani Kagera wametakiwa kuyatumia matunda ya tafiti za kisayansi yanayoletwa na wataalamu kuboresha kilimo chao na kuongeza tija kwenye mazao mbalimbali ili kuweza kuchangia  malengo ya nchi kufikia uchumi wa kati.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu,  Salumu Mustafa Kijuu wakati akizungumza na wanakikundi cha Batekaka kwenye Kijiji cha Bunazi na kikundi cha Obumo wa Kijiji cha  Kashaba  kwenye uzinduzi wa zoezi la utoaji wa Mbegu bora za zao la migomba  iliyozalishwa kwa njia ya chupa na Mihogo yenye ukinzani na magonjwa ya batobato na michirizi ya kahawia zoezi lililofadhiliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo Tanzania (OFAB).

  Alisema Kilimo pekee ndicho kinachoweza kuwakwamua wananchi kutokana na wimbi la umasikini lakini akasisitiza kuwa kilimo hicho lazima kizingatie mbinu zote za kilimo bora ambacho kitamuwezesha mkulima kulima eneo dogo na kupata mavuno makubwa na kuchana na kile cha zamani na mazoea cha kulima bila kutumia mbinu za kisayansi.

  “Tafiti nyingi zinafanyika hapa nchini lakini zinaishia kwenye makabati na haziwafikii wakulima ambao ndio walengwa wa tafiti hizo lakini nawashukuru COSTECH kwa kushirikiana na watafiti wetu kwa kutuletea mbegu hizi bora mlizozitafiti na kujihakikishia kuwa zinauwezo wa kutatua changamoto za wakulima wetu na kuongeza tija”Alisema Mkuu huyo wa mkoa wa Kagera.

  Mkuu huyo wa mkoa wa Kagera ameshukuru COSTECH kwa kuamua kusaidia kuwafikishia wakulima mbegu bora za MIhogo na Migomba na kuanzisha mashamba darasa kwenye wilaya zote za mkoa huo ambayo yatawezesha wakulima wengi zaidi kujifunza kwa vitendo na hatimae kuweza kuinga mbinu hizo za kisasa zilizotafitiwa na kwenda kuzitumia kwenye mashamba yao baada ya kuona matunda yatokanayo na mshamba hayo.

  Meja Jenerali Mstaafu Kijuu pia alibainisha kuwa hivi sasa mkoa umejipanga kuhakikisha kila wilaya inakuwa na kiwanda kimoja kikubwa cha kuchakata zao moja na kila wilaya kuwa na zao moja la biashara hali ambayo itasaidia katika kuwahakikishia masoko ya uhakika wa mazao ya wakulima na hivyo kuongeza ari ya uzalishaji kwenye maeneo mengi.

  Aliwataka maofisa ugani kuwasaidia wakulima katika kutumia mbinu bora za kilimo ili kuweza kuzalisha kwa tija na kuwataka kila mmoja kuwa na shamba lake ambalo wakulima wataweza kuona na kujifunza kwao badala ya kuwa wazungumzaji tuu bila wao kuonyesha mfano.

  Awali akizungumza malengo ya mpango huo wa ugawaji mbegu na malengo yake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa COSTECH, Shabani Hussein alisema kuwa mpango huo ni moja ya utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo kwa mujibu wa sheria ya uanzishwaji wake ya kuhakikisha matokeo mazuri ya sayansi na teknolojia yanawanufaisha walengwa kwenye maeneo mbalimbali nchini.

  Alisema kuwa ili kuweza kufikia adhima ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa Tanzania ya viwanda ni lazima suala la kilimo lipewe msisitizo wa kutosha ili kuweza kuzalisha malighafi za kutosha kulisha vwanda vitakavyojengwa  lakini bila kilimo mpango huo unaweza kukwama.

  Alisema pamoja na COSTECH kuwa mshauri mkuu wa serikali katika masuala yote yanayohusu sayansi,teknolojia na uvumbuzi lakini pia wanashirikiana na watafiti na vituo vya utafiti katika kusaidia kufikisha matunda hayo ya tafiti kwa wakulima ili kusaidia kuongeza tija na kuwakwamua wakulima katika wimbi la umasikini.

  ‘’Naamini mbegu hizi tulizozileta leo na mashamba darasa haya yatakuwa chachu kwa wakulima wengine kuona na kujifunza mbinu bora za kilimo kwenye maeneo yao na baadae mbinu hizo kusambaa kwa wakulima wengine kwenye maeneo ya jirani" alisistiza Hussein

  Mwakilishi huyo wa Mkurugenzi mkuu wa COSTECH alisema mbegu hizo bora za Migomba safi isiyo na magonjwa pamoja na mbegu bora ya mihogo aina ya Kiroba yenye ukinzani na magonjwa ya batobato kali na michirizi ya kahawia itagaiwa kwenye vikundi kwenye wilaya zote za mkoa huo wa Kagera na kupewa mbinu bora za kilimo kutoka kwa wataalamu.

  Mkuu wa WIlaya ya Missenyi, Luteni Kanali Denis Mwila amewapongeza COSTECH na OFAB kwa kutimiza ahadi yao ya kuwaletea wakulima mbegu hizo na kuwaahidi kuwa watasimamia mashamba darasa hayo vizuri hadi kuvuna ili wakulima waweze kuona umuhimu wa sayansi na mbinu bora za kilimo kwenye uzalishaji.

  “ Tumepata bahati kubwa sana wana Missenyi uzinduzi huu kimkoa kufanyika kwenye wilaya yetu maana zipo wilaya nyingi lakini bahati imetuangukia sisi hivyo tuyatunze mashamba na mbegu hizi na tusiwaangushe COSTECH waliotuletea mbegu hizi bora” alisema Mwila.

  Pia ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kutoa ruzuku za pembejeo mara mbili kwa mwaka kwenye mkoa wa Kagera kutokana na kuwa na misimu miwili ya kilimo badala ya kuwapatia pembejeo msimu mmoja pekee sawa na mikoa mingine yenye msimu mmoja.

  Ameahidi kushirikiana na COSTECH na wataalamu katika kila aina ya teknolojia na mbinu bora inayowafaa wakulima wa wilaya yake ili kuwawezesha kuzalisha chakula kingi na mazao ya biashara ambayo wananchi watauza na kujipatia kipato.

  Kwa upande wao wakulima kwenye vikundi hivyo wameahidi kuyatunza na kuyalinda mashamba hayo na mbegu hizo ili kuzizalisha kwa wingi na kuweza kuwasambazia wakulima wengine kwenye maeneo yao ili kujihakikishia usalama wa chakula kwa kulima zao bora la muhogo na kulima migombo bora iliyozalishwa kwa njia ya chupa baada a migomba yao kushambuliwa sana na ugonjwa hatari wa mnyauko.


  Pia wakapaza sauti zao kwa serikali kuhakikisha wanawapelekea mbegu bora za mahindi na mazao mengine kwa wakati kupitia mpango wa serikali wa kutoa ruzuku ya pembejeo maana kilimo mbili za mbegu bora ya mahindi wananunua kwa wastani wa shilingi 15  bei ambayo ni kubwa kwa wakulima wengi.


older | 1 | .... | 1407 | 1408 | (Page 1409) | 1410 | 1411 | .... | 1898 | newer