Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1403 | 1404 | (Page 1405) | 1406 | 1407 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Meneja Masoko na Mahusiano wa Shirikala la Ndege la Precision Air Bw Hillary Mremi (wa pilikushoto) akikabidhi mfano wa tiketi ya ndege kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za Rock City Marathon, Bw Zenno Ngowi ( wa pili kulia) ikiwa ni ishara ya udhamini wenye thamani ya Sh 20 milioni kwa ajili ya mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mratibu wa mbio hizo kutoka Kampuni ya Capital Plus, Bw Bidan Lugoe (wa tatu kushoto) pamoja na maofisa wa makampuni hayo mawili.
  Meneja Masoko na Mahusiano wa Shirikala la Ndege la Precision Air Bw Hillary Mremi akizungumza wakati wa makababidhiano hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi pamoja na Mratibu wa mbio hizo kutoka Kampuni ya Capital Plus, Bw Bidan Lugoe
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi (katikati) akizungumzia udhamini huo. Kwa mujibu wa Ngowi udhamini huo unamaanisha kwamba uhusiano wa Precision Air na wateja wake hautaishia ndani ya ndege bali utaendelea zaidi hadi kwenye mitaa, fukwe, viwanja vya michezo na sehemu zote za utalii katika jiji la Mwanza na Kanda ya Ziwa yote.
  Mratibu wa mbio hizo kutoka Kampuni ya Capital Plus, Bw Bidan Lugoe (katikati) akizungumzia udhamini huo. Kwa mujibu Lugoe maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba wamejipanga kupokea washiriki zaidi ya 4,000 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo viongozi na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.
   
   
  SHIRIKA la ndege la Precision Air leo limetangaza udhamini wake wenye thamani ya Sh 20 milioni kwa ajili ya mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 jijini Mwanza.

  Kwa udhamini huo, shirika hilo sasa linatambulika rasmi kama shirika maalumu la usafiri wa mbio hizo miongoni mwa wadhamini wengine zikiwemo kampuni za PUMA, Tiper, RedBull, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), New Mwanza Hotel, EF Out door, CF Hospital, KK Security, na kampuni ya uchapishaji ya SDS.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo ,Meneja Masoko na Mahusiano wa Precision Air Bw Hillary Mremi alisema udhamini huo kwa kiasi kikubwa umechagizwa na malengo ya mbio hizo yaliyojikita katika kutangaza utalii wa ndani kupitia mchezo wa riadha.

  “Lakini pia kibiashara tunaona kwamba mara nyingi watu wanaopenda kushiriki riadha wamekuwa na ‘hobby’ pia kusafiri sehemu tofauti tofauti ndani na nje ya nchi hivyo ushiriki wetu kwenye mbio hizi utazidi kutukutanisha na kundi hili muhimu,’’ alibainisha.

  Zaidi alionyesha imani kuwa mbio hizo zitakazofanyika jijini Mwanza zitakata kiu ya washiriki wake wakiwemo abiria wa shirika hilo kwa kuwa tofauti na mchezo huo, jiji hilo lina vivutio vingi vya kitalii ikiwemo fukwe za Ziwa Victoria, Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane na makumbusho ya kabila la wasukuma (Bujora)

  Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi alisema kwao ni heshima kubwa kushirikiana na shirika hilo lenye heshima kubwa kwenye usafiri wa anga hapa nchini.

  “Tunaamini kwamba ushirikiano huu na shirika hili linalotambulika kimataifa kwa ubora wa huduma zake za usafiri wa anga utaziweka na mbio hizi pia katika ngazi ya kimataifa.’’ alisema.

  Aliongeza kuwa udhamini huo unamaanisha kwamba uhusiano wa shirika hilo na wateja wake hautaishia ndani ya ndege bali utaendelea zaidi hadi kwenye mitaa, fukwe, viwanja vya michezo na sehemu zote za utalii katika jiji la Mwanza na Kanda ya Ziwa yote.

  Kwa upande wake Mratibu wa mbio hizo kutoka Kampuni ya Capital Plus, Bw Bidan Lugoe alisema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba wamejipanga kupokea washiriki zaidi ya 4,000 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo viongozi na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.

  “Kiukweli muitikio ni mkubwa sana kutoka ndani na nje ya nchi! Tofauti na washiriki wa kawaida kuna idadi kubwa ya viongozi wa serikali na kisiasa ambao tayari wamethibitisha ushiriki wao,’’ alisema Lugoe.

  Aliwataja baadhi ya waliothibitisha ushiriki wao kuwa ni pamoja na baadhi ya wakuu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Makamanda wa Jeshi la Polisi pamoja na wale wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

  Akizungumzia usajili wa mbio hizo Bw. Bidan alisema kwa wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa jirani wanaweza kujisajili kwa kuchukua fomu katika Ofisi za michezo wilaya zote za mkoa wa Mwanza, Ofisi za riadha mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga.

  Sehemu nyingine ni pamoja na Uwanja wa Nyamagana, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza, Kituo cha michezo Malya, Shule ya Kimataifa ya Isamilo, New Mwanza Hotel na Ofisi za EF Out door zilizopo jingo la Rock City Mall.“Kwa upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki pia zinapatikana jengo la SHAMO Tower, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam’’ alitaja.

  Zaidi kuhusu usajili wa mbio hizo zinazoandaliwa kwa kushirikiana na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA), Bidan alisema unaweza kufanyika kupitia tovuti ya kampuni hiyo ambayo ni www.capitalplus.co.tz


  0 0

  Ndugu zangu Wanahabari,

  Assalaamu Alaykum (Amani ya Mwenye ezi Mungu iwe kwenu)

  Napenda kuufahamisha umma wa kiislamu kuwa kufuatia kuanza mradi wa ujenzi wa msikiti wa Mohammed VI unaojengwa katika eneo la Bakwata makao Makuu Kinondoni Road.

  Hivyo basi napenda kuchukua nafasi hii kuufahamisha umma kuwa ili kupisha mradi huo Bakwata Makao Makuu imehamisha ofisi zake na kuzipeleka katika mtaa wa Togo jengo linalotambulika kama TIGER TOWER na shughuli zote zinaendelea kama kawaida.

  Mwisho kabisa tunaomba radhi kwa usmbufu wowote uliojitokeza katika kipindi hiki cha ujenzi.

  Wabillahi TTaufiiq

  USTAADH TABU KAWAMBWA

  MKURUGENZI HABARI NA MAHUSIANO.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  wakishuhudia wakati Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kulia)  akitia saini Makubaliano ya ujenzi wa Msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25,2016. PICHA NA MAKTABA

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Balozi wa Uganda katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Richard Mabonero  leo  alipofika Ikulu Mjini Unguja.
   Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na mgeni wake Balozi wa Uganda katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Richard Mabonero, alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
   Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na mgeni wake Balozi wa Uganda katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Richard Mabonero, alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
  Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  akifuatana  na mgeni wake  Balozi wa Uganda katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Richard Mabonero, alipofika Ikulu Mjini Unguja leo baada ya mazungumzo yao. (Picha na Ikulu).

  0 0

  Kamati ya kuchunguza migogoro ya ardhi iliyoundwa na ofisi ya katibu tawala mkoa wa Ruvuma imekabidhi ripoti hiyo kupitia Mwenyekiti wa kamati, ambaye pia ni katibu tawala wilaya ya songea,PENDO NDUMBARO amekabizi taarifa hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma dkt bilinith mahenge,baada ya kufanya kazi kwa miezi mitatu,

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni
  Naibu Mkurugenzi wa Halotel , Trieu Than Binh.
    Naibu Mkurugenzi wa Halotel , Trieu Than Binh akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala.
   Mkuu wa kitengo cha Mawsiliano kampuni ya simu za mkononi ya Halotel, Mhina Semwenda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.Kusoto ni Naibu Mkurugenzi wa Halotel , Trieu Than Binh.
   KAMPUNI ya Simu ya Mkononi ya Halotel imesema kuwa serikali imeweka mazingira bora kwa wawekezaji kupitia vyombo vyake ambavyo vimefanya Halotel kupata mafanikio katika kutoa huduma ya mawasiliano.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Mkurugenzi wa Halotel , Trieu Than Binh amesema Halotel imetimiza miaka miwili tangu ilivyoanzishwa mwaka jana Oktoba 15.
  Amesema kuwa katika mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka miwili ni kuwa na wateja zaidi ya milioni 3.5  wanaotumia mtandao  huo katika mawasilino.

  Than Binh, amesema kuwa katika miaka miwili ya utoaji huduma, wamefanya mapinduzi na mabadiliko makubwa katika sekta hiyo katika nyanja za Mawasiliano ikiwemo kuboresha miundombinu ya Mawasiliano, Mabadiliko katika Elimu, huduma za kifedha pamoja na kupunguza gharama za mawasiliano.

  “Tangu tumeanza kutoa huduma kwa mwaka wa pili sasa idadi ya wateja imeendelea kuongezeka kwa kasi. Hii inatokana na huduma ambazo tumekuwa tukizibuni kwa pamoja na kuwekeza zaidi katika kutoa huduma bora na kuboresha miundombinu ya mawasiliano hasa katika maeneo ya vijijini.” Amesema

  “Kwanza tunafurahishwa na Serikali kutokana na mazingira bora ya uwekezaji ambayo imeweka hadi sasa,  na pia mazingira mazuri ya ukusanyaji wa kodi kwa uwazi zaidi suala ambalo hata kwetu limeondoa usumbufu kwa kiasi kikubwa, kuzinduliwa kwa kituo cha ukusanyaji kodi kwa njia ya kielectroniki ilikuwa faraja kubwa kwetu na ndio maana tulikuwa miongoni mwa kampuni za kwanza za simu kujiunga na mfumo huo.”

  Binh, amesema kuwa wamefurahi pia kuwa kampuni inayoongoza kwa kutoa ajira kwa Maelfu ya Watanzania ikiwa ni ajira za moja kwa moja zaidi ya elfu moja na mia mbili 1200, na ajira zisizo za moja kwa moija zaidi ya Elfu Ishirini 20000 na kusema kuwa kutokana na uwekezaji ambao kampuni hiyo imeendelea kufanya wanaamini wataendelea kuongeza idadi ya ajira nchini.

  Aidha Binh, aliongeza kuwa wanaamini bado wana nafasi kubwa zaidi ya kufanya uwekezaji na kubadili kabisa mfumo wa Mawasiliano nchini kwa kuanzisha njia mpya za mawasiliano kwa kutumia vifaa vya kisasa zaidi na kuwa kampuni itakayo ongoza katika utoaji wa huduma za Mawasiliano kupitia Tehama na Teknolojia ya Mawasiliano.

  Amesema wanaelekea kuanzisha mtandao wa 4G LTE kwa wateja wetu wote wa Halotel, hatuta bagua maeneo tutafanya uwekezaji huu katika maeneo yote nchi nzima ili wateja wetu waweze kufurahia huduma bora za mawasiliano na kwa bei rahisi,” alisema na kuongeza, “Pia tunaangazia sekta ya elimu ambayo hadi sasa kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar Es Salaam, tumeweza kuanzisha mfumo wa kujisomea kwa shule za sekondari nchini kwa masomo ya Sayansi Mfumo ambao utapatikana bure kwa shule zote zinazotumia Mtandao wa Intaneti wa Halotel, Tumeanza na masomo ya sayansi na kadri muda unavyokwenda tutaangalia namna ya kuingiza masomo mengine, baada ya kukamilisha kutia saini Mkataba wa Maelewano kati yetu na Wizara ya Utawala bora TAMISEMI.

  0 0  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Khadija Nyembo akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella.
  Rai hiyo imetolewa jana na wataalam wa uwekezaji katika masoko ya dhamana na mitaji walipokuwa wakizungumza na wafanyabiashara, wadau wa sekta binafsi na sekta ya umma Jijini Mwanza kwenye mjadala ulioandaliwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) kwa ushirikiano na Best Dialogue (Mpango wa Uboreshaji Mazingira ya Biashara nchini).

  Mjadala huo ulilenga kuangalia fursa na changamoto za biashara zinazoikumba sekta binafsi na namna ya kuzitatua na kuwezesha ustawi wa biashara jijini Mwanza ili kuweza kufikia uchumi wa kati na viwanda.Mgeni rasmi katika mjadala huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Khadija Nyembo ambaye alisema kuwa Serikali iko tayari kuboresha mazingira ya kibiashara ili kufikia uchumi wa kati pamoja na Tanzania ya viwanda.
  Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akielezea umuhimu wa kuwekeza kwa njia ya hisa za jana Jijini Mwanza ambapo mafunzo ya mjadala kati ya sekta ya umma na sekta binafsi yalifanyika. 

  Akizungumza katika mjadala huo Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank ,Ibrahim Mwangalaba alitoa rai kwa wadau wa sekta binasfi, sekta ya umma na wakazi wa Mwanza kuwekeza katika ununuaji wa hisa za Maendeleo Bank ambazo zimeanza kuuzwa tangu Septemba 18 hadi Novemba 03 mwaka huu.Mwangalaba amesema hisa za benki hiyo zinauzwa kwa thamani ya shilingi 600 kila moja na kwamba kiwango cha chini ya ununuzi ni hisa 100 zenye thamani ya shilingi 60,000 hivyo wananchi wote wachangamkie fursa hiyo muhimu.
  Wadau wa sekta binafsi na sekta ya umma wakifatilia mkadala wa uboreshaji wa mazingira ya biashara ulioambatana na umuhimu wa kuwekeza kwa njia ya hisa ulioletwa na Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba pamoja na mshauri wa uwekezaji katika masoko ya mitaji Richard Manamba.

  Tunauza hisa sokoni sasa na hisa hizi zinauzwa kwenye matawi yote ya benki ya CRDB ambapo tunaunga mkono juhudi za Rais wetu anayesema uchumi wa Tanzania umilikiwe na watanzania wenyewe na njia mojawapo ya kuwajumuisha watanzania wengi ni uuzaji wa hisa sokoni”. 

  Amesisitiza Mwangalaba na kuongeza kwamba hisa hizo pia zinapatikana ofisi za TCCIA.Naye Mshauri wa Hisa, Richard Manamba amesema ununuzi wa hisa una faida nyingi ikiwemo wanunuzi kupata gawio la faida ambalo benki hulipata na kwamba hisa hizo huongezeka thamani kulingana na nguvu ya soko.Maendeleo Bank yenye mtaji wa shilingi bilioni 10 sokoni inaendelea kuongeza mtaji wake hadi kufikia shilingi bilioni 17 ambapo inatarajiwa kufungua matawi yake katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Khadija Nyembo akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella.
  Rai hiyo imetolewa jana na wataalam wa uwekezaji katika masoko ya dhamana na mitaji walipokuwa wakizungumza na wafanyabiashara, wadau wa sekta binafsi na sekta ya umma Jijini Mwanza kwenye mjadala ulioandaliwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) kwa ushirikiano na Best Dialogue (Mpango wa Uboreshaji Mazingira ya Biashara nchini).

  Mjadala huo ulilenga kuangalia fursa na changamoto za biashara zinazoikumba sekta binafsi na namna ya kuzitatua na kuwezesha ustawi wa biashara jijini Mwanza ili kuweza kufikia uchumi wa kati na viwanda.Mgeni rasmi katika mjadala huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Khadija Nyembo ambaye alisema kuwa Serikali iko tayari kuboresha mazingira ya kibiashara ili kufikia uchumi wa kati pamoja na Tanzania ya viwanda.
  Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akielezea umuhimu wa kuwekeza kwa njia ya hisa za jana Jijini Mwanza ambapo mafunzo ya mjadala kati ya sekta ya umma na sekta binafsi yalifanyika. 

  Akizungumza katika mjadala huo Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank ,Ibrahim Mwangalaba alitoa rai kwa wadau wa sekta binasfi, sekta ya umma na wakazi wa Mwanza kuwekeza katika ununuaji wa hisa za Maendeleo Bank ambazo zimeanza kuuzwa tangu Septemba 18 hadi Novemba 03 mwaka huu.Mwangalaba amesema hisa za benki hiyo zinauzwa kwa thamani ya shilingi 600 kila moja na kwamba kiwango cha chini ya ununuzi ni hisa 100 zenye thamani ya shilingi 60,000 hivyo wananchi wote wachangamkie fursa hiyo muhimu.
  Wadau wa sekta binafsi na sekta ya umma wakifatilia mkadala wa uboreshaji wa mazingira ya biashara ulioambatana na umuhimu wa kuwekeza kwa njia ya hisa ulioletwa na Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba pamoja na mshauri wa uwekezaji katika masoko ya mitaji Richard Manamba.

  Tunauza hisa sokoni sasa na hisa hizi zinauzwa kwenye matawi yote ya benki ya CRDB ambapo tunaunga mkono juhudi za Rais wetu anayesema uchumi wa Tanzania umilikiwe na watanzania wenyewe na njia mojawapo ya kuwajumuisha watanzania wengi ni uuzaji wa hisa sokoni”. 

  Amesisitiza Mwangalaba na kuongeza kwamba hisa hizo pia zinapatikana ofisi za TCCIA.Naye Mshauri wa Hisa, Richard Manamba amesema ununuzi wa hisa una faida nyingi ikiwemo wanunuzi kupata gawio la faida ambalo benki hulipata na kwamba hisa hizo huongezeka thamani kulingana na nguvu ya soko.Maendeleo Bank yenye mtaji wa shilingi bilioni 10 sokoni inaendelea kuongeza mtaji wake hadi kufikia shilingi bilioni 17 ambapo inatarajiwa kufungua matawi yake katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza.

  0 0

    Katibu Mkuu wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi akizungumza wakati wa Kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyi Taifa, kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, 2017. Kulia ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Pereila Silima na katikati ni Mwenyekiti wa muda wa kikao hicho Diana Chilolo. (Picha na Bashir Nkoromo)
   Mwenyekiti wa muda wa kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyo Taifa, Diana Chilolo, akizungumza wakati wa kikao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, 2017.  Kushoto ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Pereila Silima na kulia ni Katibu Mkuu wa 
  UWT Amina Makilagi. 
   Wajumbe wakishangilia wakati wa kikao wa kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya ya wanawake Taizania (UWT) kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, 2017
   Maofisa wa UWT wakiandaa makabrasha kabla ya kuanza kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyi Taifa, kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, 2017.
  Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma akisalimia alipotambulishwa katika kikaocha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya ya wanawake Taizania (UWT) kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

    Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura leo mjini Dodoma.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) baada ya kuwasili ofisini leo mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizra hiyo Mhe. Anastazia Wambura.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi za Wizara leo mjini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara wakati wa kumkaribisha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Nuru Millao.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wa pili kushoto) akiongea na baadhi ya viongozi wa Wizara akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili ofisini mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni aliyekuwa Naibu Waziri wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Nuru Millao (kulia) mara baada ya kuwasili ofisini mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akipokelewa watumishi wa Wizara hiyo mara baada ya kuwasili ofisini mjini Dodoma.(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM,Dodoma)

  Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ameahidi kushirikiana na Watendaji wa Wizara, wadau pamoja na wananchi kwa ujumla kusimamia maadili ya Mtanzania ili kuendelea kuwa na taifa bora.

  Mhe. Shonza ameyasema hayo alipowasili katika ofisi za Wizara leo mjini Dodoma ambapo alipokelewa na Waziri mwenye dhamana Dkt. Harrison Mwakyembe, viongozi wa Wizara pamoja na  watumishi.

  “Wizara hii ni muhimu sana kwa kuwa inajenga taswira ya taifa kupitia sekta zake ambazo ni Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo hivyo ntahakikisha tunashirikiana kwa karibu katika kuwatumikia wananchi “alisema Naibu Waziri Shonza.

  Aliongeza kwa kueleza kuwa atahakikisha suala la maadili bora kwa jamii  linazingatiwa ili kuendelea kujenga taifa imara kwa kuzingatia mavazi yenye heshima na  nyimbo zenye kujenga.

  Aidha, Naibu Waziri Shonza amesema ni wajibu wetu kama watumishi wa umma kuhakikisha tunatekeleza Ilani ya chama tawala ambacho kiliahidi kuwatumikia watanzania ili kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa kwa wakati.

  Naye aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo Anastazia Wambura amempongeza Naibu Waziri Shonza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo na amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumuamini kuwatumikia Watanzania.

  Akizungumzia utendaji kazi, Mhe. Wambura ameufananisha utumishi wa umma na chombo cha usafiri ambapo abiria hushuka kituo mara baada ya kufika na dereva kuendelea na safari.

  “Mhe.Waziri, viongozi wenzangu na ndugu zangu watumishi wa Wizara, mimi nimefika kituoni, Naibu Waziri nakukabidhi kijiti endelea na safari, endelea kuwatumikia Watanzania kama ambavyo ilani ya chama tawala inavyoeleza” alisema Mhe.Wambura

  Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amemuahidi Naibu Waziri Shonza ushirikiano wa hali na mali katika kuwahudumia wananchi kupitia sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

  0 0


  NA K-VIS BLOG, MTWARA

  SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco), limefanikiwa kukarabati mashine namba 6 iliyokuwa imeharibika na kuiwasha kwa ajili ya kutoa huduma ya umeme kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.

  Hatua ya kuwashwa kwa mtambo huo ni juhudi za shirika hilo za kuimarisha hali ya upatikanaji umeme kwa wananchi kusini huku ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani alipotembelea Kituo cha kufua umeme kwa gesi .

  Akizungumza leo mjini hapa, Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Mhandisi Dk. Tito Mwinuka ambaye amepiga kambi mkoani humo pamoja na watalaamu wengine, alisema kuwa mitambo iliyokuwa ikifanya kazi ilikuwa minne lakini baada ya juhudi kubwa za wataalamu wa Tanesco hadi kufikia jana jioni wamefanikiwa kuwasha mashine hizo zenye uwezo wa kuzalisha Megawati 16.

  “Tanesco tumeshagiza vipuri vya aina mbalimbali ili kutengeneza mashine hizi na pia Shirika katika kuhakikisha kazi inakwenda kwa kasi zaidi itaongeza nguvu ya wataalamu kutoka vituo vingine vya TANESCO hapa nchini.“Tunawaomba wateja wetu wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuendelea kuwa wavumilivu wakati uongozi wa Shirika, Kanda na Mkoa ukiendelea na juhudi za kumaliza kabisa upungufu wa umeme katika mikoa hii,” alisema Dk. Mwinuka.

  Alisema kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya umeme kwa mikoa hiyo, alisema Shirika limeshaanza taratibu za kupata Megawati nne za haraka kwa kuagiza mitambo mwili mipya.“Tuna imani kubwa na wafanyakazi wa Kituo cha kufua umeme wa gesi cha Mtwara na wataweza kukarabati mitambo yote pindi vipuri vitakapowasili,” alisema

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo amewashukuru wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kwa uvumilivu waliouonesha katika kipindi cha matengenezo ya mitambo hiyo.

  Mafundi wakiratibu zoezi la ukarabati wa mshine .
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Tito Mwinuka, (wakwanza kushoto), na viongozi wengine wa Shirika hilo, wakifuatilia maendeleo ya ukarabati wa mitambo ya kufua umeme mkoani Mtwara leo Oktoba 17, 2017.
  Mafundi wa TANESCO wakiendelea na ukarabati wa mshine.

  0 0

  Madiwani na Watendaji wa kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga,wameshauriwa kuhakikisha wanasimamia vizuri miradi ya maendeleo hususani inayofadhiliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali iliyopo kwenye maeneo yao ili iweze kujengwa kwa kiwango kinachohitajika.

  Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hamlamashuri ya wilaya ya Handeni William Makufwe kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika Oktoba 16 na kueleza kuwa kuna umuhimu wa viongozi wa Kata kuwa karibu na wafadhili wanaojenga miradi kwenye maeneo yao kwani wao ndio wasimamizi.

  Makufwe alisema ofisi ya Mkurugenzi inakuwa na imani kwamba Madiwani na Watendaji wa Kata ndio wasimamizi wakuu wa miradi iliyopo kwenye kata zao hivyo ikitokea miradi haina kiwango ina maana viongozi ngazi ya Kata hawakutimiza wajibu wao.

  Aliongeza Kuwa ni kweli Serikali inahitaji kufadhiliwa lakini sio kwa kujengewa miradi ambayo ipo chini ya kiwango hali inayopelekea kuharibika Kwa muda mfupi na kutokufikia malengo yaliyokusudiwa.

  " Waheshimiwa mnaopata miradi hii ya ufadhili hakikisheni inaleta tija kwa kusimamia hususani wanaopewa tenda ya kujenga kuepuka madhara yanayoweza kuepukika kwa kuisimamia tu" alisema Makufwe. 

  Kwaupande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni,Ramadhan Diliwa alisema kuwa kuna baadhi ya miradi ni kweli mapungufu yapo na yamesababishwa na kutokuwepo uangalizi wa karibu na kusisitiza Madiwani kusimamia vyema miradi kwa manufaa ya wananchi wao. 

  Alitolea mfano eneo la Kata ya Kabuku mjini kuwa kuna madarasa yaliojengwa na wafadhili miaka iliyopita lakini ipo chini ya kiwango hali iliyopelekea wanafunzi kutolewa ndani ya madarasa hayo na kutafutiwa mengine kutokana na kuwa hatarishi kwao.

  Aidha Sharifa Abebe diwani kata ya Kwamgwe alisema ni kweli awali hali kama hiyo ilikuwa ikitokea ila kwasasa wanasimamia vizuri miradi iliyopo kwenye maeneo yao ambapo kwake ipo miradi inayofadhiliwa na inajegwa katika ubora unaohitajika kutokana na usimamizi uliopo Kwa kushirikiana na watendaji ngazi ya Kata.

  Imetolewa na 

  Kitengo cha Habari
  Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni akizungumza kwenye kikao cha baraza na kutoa ushauri kwa viongozi.
  Diwani Kata ya Kwamgwe Mh Sharifa abebe akizungumza kwenye kikao hicho cha baraza
  Wataalamu wa Halmashauri na Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza
  Mwenyekiti wa Halmashauri MH Ramadhani Diliwa katikati akizungumza na wataalamu na Madiwani, kulia ni kaimu Mkurugenzi kwa Muda Fatuma Kalovya , kushoto ni Makamu mwenyekiti Mh. Abdalla Pendeza.

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na  Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Maafa  Ofisi ya Waziri Mkuu, Jane Alfred, namna mtambo unavyosaidia kupatikana kwa taarifa za dharura kwa ajili ya kufuatilia maafa nchini, leo tarehe 17 Oktoba, 2017, Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na  Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akiangalia mitambo inayotumikakutunza takwimu za taarifa za dharura kwa ajili ya kufuatilia maafa nchini, leo tarehe 17 Oktoba, 2017, Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na  Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mchabuzi wa Mifumo ya Kompyuta  Ofisi ya Waziri Mkuu, Alex Ndimbo, namna taarifa zinavyochakatwa na  kupatikana kwa taarifa za dharura kwa ajili ya kufuatilia maafa nchini, leo tarehe 17 Oktoba, 2017, Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya akieleza umuhimu wa mpango wa uendeshwaji wa kituo Cha Operasheni na Mawasiliano ya Dharura kwa ajili ya kufuatilia maafa nchini kwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na  Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama, leo tarehe 17 Oktoba, 2017, Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Dkt. Agnes Kijazi akimueleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na  Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama,jinsi Mradi wa Uboreshaji wa Mifumo ya Tahadhari za Awali na Mabadiliko ya Tabianchi ulivyoboresha utabiri wa hali ya hewa nchini, alipotembelea mamlaka hiyo, leo tarehe 17 Oktoba, 2017, Dar es Salaam.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na  Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (walio kaa katikati) akiwa na Menejimenti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini mara baada ya kutembelea mamlaka hiyo kwa ajili ya kuona jinsi Mradi wa Uboreshaji wa Mifumo ya Tahadhari za Awali na Mabadiliko ya Tabianchi ulivyoboresha utabiri wa hali ya hewa nchini, , leo tarehe 17 Oktoba, 2017, Dar es Salaam. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina katikati, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Aaron Mbogho, kushoto kwake  katibu tawala wa wilaya ya Mwanga Bw. Yusuph  Kasuka wakiangalia ng'ombe waliotaifishwa  wakati wakinywa maji katika kijiji cha Mgagau wilayani Mwanga.
  Waziri Mpina , Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Maria Mashingo na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Aaron Mbogho wakijadili jambo baada ya kuongea na wanahabari kuhusu amri ya mahakama ya kupiga mnada ngombe walitaifishwa na Serikali.
  Ng’ombe walioamriwa na mahakama kupigwa mnada, mnada utapigwa siku ya ijumaa. 

  NG’OMBE waliotaifishwa na serikali katika wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, wamatarjiwa kupigwa mnada kufuatia uamuzi wa mahakama.
   Hayo yameelezwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, wakati alipokwenda kukagua lindo la ng’ombe hao, jana eneo la Mgagao, wilayani Mwanga, walikohifadhiwa.

  “Kufuatia uamuzi wa mahakama, ng’ombe hawa watauzwa kwa njia ya mnada siku ya Ijumaa, Oktoba 20, mwaka huu, kutokana na hali za ng’ombe hawa kutokuwa nzuri”, alisema.

  Aliongeza, “Tayari mahakama imeridhia ombi la serikali la kutoka kuuzwa kwa ng’mbe hawa na ishamteua dalali wa kufanya mnada huo ambaye ni Marepelanto ya mjini Moshi na kazi hii itafanywa haraka kutokana na ng’ombe wengine kuanza kufa, kama mlivyosikia tayari sita wameshakufa”.

  Aidha alisema serikali itaanza operesheni maalum ya kuwakamata ng’ombe walioingizwa nchini kinyume cha sehria kuanzia Jumatatu ijayo.

  “Baada ya operesheni ya hapa Kilimanjaro, nilitoa siku saba kwa Mikoa mingine kuiondoa mifugo iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria kupitia Mikoa hiyo, muda huo umekwisha, Jumatatu tunaanza ingine itakayochukua siku 15 ili kuhakikisha mifugo hiyo inaondolewa yote”, alisema.

  Akijibu maswali kutoka kwa baadhi ya viongozi wa eneo hilo, Bw. Mpina alisema kuwa iwapo kuna mifugo ya wenyeji ilikamatwa wakati wa operesheni hiyo wapeleke orodha ya wenye ng’ombe hao kwa kupitia ngazi husika ili waweze kurudishiwa.

  “Wenyeji wenye ng’ombe waliokamatwa watumie taratibu kuzifuatilia kwa kuanzia kwa viongozi wa maeneo wanayotoka hadi ngazi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ikidhibitishwa bila mashaka mifugo hiyo ni ya kwao zitatumika taratibu zinazohitajika kisheria kwa kuwa ng’ombe hizi sasa ni mali ya serikali”, alisema.

  Aidha alitoa onyo kwa viongozi hao kuhakikisha wanafanya zoezi hilo kwa weledi na kwamba iwapo watafanya udanganyifu hatua kali za kisheria zitachuliwa dhidi yao bila kujali nyadhifa zao.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo, aliyeiongoza operesheni hiyo, alisema kuwa mwendelezo wa operesheni hiyo umepelekea serikali kukamata ng’ome wengine takribani 2,000.

  “Tunawashukuru Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kutupatia ndege ambayo ilitusaidia sana katika zoezi hili tulilofanya kupitia vyombo vya ardhini na angani”, alisema.

  Alisema kuwa amebaini ya kuwa wizara ya Mifugo na Uvuvi ina changamoto ya uhitaji wa vifaa kama ndege kwani operesheni hiyo imebainisha wazi uhitaji huo.

  Awali akitoa rai yake kwa niaba ya wafugaji wenyeji ambao ng’ombe zao zimekamatwa kufuatia operesheni hiyo, Diwani wa Kata ya Kirya, Bw. Nyange Laizer aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa ng’ombe hizo kurudishiwa wenyewe.

  “Unajua sisi malisho yetu tunafanya hapa hapa na ndiyo maana operesheni hii ikawakumba na watu wetu na hii ni kutokana na ukweli kuwa huwezi kutofautisha ng’ombe za hapa kwetu na zile zinazoingizwa kinyume cha sheria”, alisema.

  Uamuzi huu wa mahakama unakuja baada ya ng’ombe hao kutaifishwa na serikali hivi karibuni baada ya kuingizwa hapa nchini kinyume cha sheria.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitoa hundi ya Mkopo uliotolewa na SIDO kwa mjasiriamali Sarah Isaya kutoka Singida katika hafla fupi ya kukabidhi mikopo kwa wajasiriamali mbalimbali mkoani hapa.
    Mkurugenzi Mtendaji SIDO Taifa Mhandisi Profesa Sylvester Mpanduji akitoa nasaha zake kwenye hafla ya utoaji wa hundi za mikopo kwa wajasiriamali mbalimbali mkoani Singida uliofanyika kwenye viwanja vya SIDO mjini hapa. Wa kwanza kushoto (aliyekaa) ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi.
   Meneja wa SIDO Mkoa wa Singida Shoma Kibende akitoa taarifa ya Viwanda Vidogo vidogo na ujasiriamali Mkoa wa Singida kwenye hafla ya utoaji wa hundi za mikopo kwa wajasiriamali mbalimbali. Wa kwanza kushoto (waliokaa) ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na Mkurugenzi Mtendaji SIDO Taifa Mhandisi Profesa Sylvester Mpanduji.
   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitazama ubora wa mafuta ya alizeti  na kupata maelezo ya mafuta hayo yanayosindikwa katika viwanda vya Mkoa wa Singida kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya kuzalishaji  Mafuta ya alizeti  ya  Sunshiwe Oil Mill, Salum Khalifan.  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amelitaka shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) kuandaa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo mbali mbali mkoani hapa ili wakihitimu waweze kujiajiri

  Dkt. Nchimbi ametoa wito huo wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo ya SIDO kwa wajasiriamali iliyofanyika kwenye viwanja vya SIDO ambapo amesema mafunzo hayo yatawajengea mazingira mazuri wahitimu kujiajiri.

  Amesema Mkoa wa Singida una fursa nyingi za kujiajiri pamoja na kuwa na vijana wengi hasa walipo katika vyuo mbalimbali lakini hawawekezi katika fursa hizo kwa kutokujua au kukosa elimu ya kutosha juu ya ujasiriamali, na hata waliopo vyuoni wakihitimu wanasubiri kuajiriwa badala ya kujiajiri.

  Dkt. Nchimbi amesema ili wananchi wakiwemo vijana waweze kuzitambua fursa hizo, SIDO Mkoa na wadau wengine wanapaswa kuongeza juhudi zaidi katika utoaji mafunzo ya ujasiriamali ambapo amewataka wajielekeze kwenye vyuo mbalimbali.

  “Singida ina kila aina ya fursa ambazo zinaweza kumkomboa mwananchi kiuchumi. Kwa hiyo hakuna sababu vijana au watu wengine kuukimbia mkoa wao na kwenda kutafuta maisha katika mikoa mingine. Ni suala la kujipanga na kupata fursa ya mafunzo kutoka SIDO mkoa”, amefafanua.

  Aidha ameziagiza halmashauri zote na manispaa Mkoani hapa kutangaza fursa, bidhaa, mazao, na huduma zinazopatikana katika maeneo yao ili kuwasaidia wajasiriamali kupata soko la uhakika.

  “ Halmashauri zote tumieni fedha mnazopata kwenye vyanzo vya mapato ya ndani muwasaidie wajasiriamali wenu kutangaza kwenye vyombo vya habari, nina imani na uhakika kuwa mkitangaza bidhaa na mazao yao yatapata soko na nyinyi halmashauri mtapata mapato yenu”, amesema Dk.Nchimbi.

  Awali Mkurugenzi Mtendaji wa SIDO Taifa Mhandisi Profesa Sylvester Mpanduji amesema SIDO imekuwa tegemeo kubwa kwa wajasiriamali hasa katika kutoa mafunzo na kusaidia teknolojia ya kuongeza thamani ya mazao na malighafi.

  “Mikopo ya SIDO imeweza kuwasaidia wajasiriamali kuthubutu na kuanzisha miradi ya usindikaji mara tu baada ya kupata mafunzo. Kundi hili limekuwa na changamoto ya mitaji kwa kuwa halikidhi na halijaweza kuthubutu kuzifikia benki kutokana na woga na gharama za mikopo”, amesema.

  Mhandisi Profesa Mpanduji amesema kwa kipindi cha mwaka 2016/2017 SIDO imeweza kutoa mikopo 4,464 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 7.2. Mikopo hiyo imetengeneza ajira 11,861 kati ya ajira hizo asilimia 51 ni wanawake.

  Kwa upande wake Meneja wa SIDO Mkoa wa Singida Shoma Kibende amesema kwa Mkoa wa Singida wametoa mikopo yenye jumla ya shilingi milioni 724.6 kwa wajasiriamali 693 na vikundi 47. Hali ya urejeshaji wa mikopo hiyo ni asilimia 98.

  Kibende amesema SIDO wameweza kutoa mafunzo ya wajasiriamali mbalimbali 37 kwa wajasiriamali 996 ambao kati yao wanawake walikuwa 536 na wanaume 460.

  Amesema baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni upungufu wa wafanyakazi na ukosefu wa fedha kwa ajili ya kutekeleza mipango waliyojiwekea ikiwemo kuendeleza na kuboresha mtaa wa viwanda.

  Naye Mjasiriamali kutoka Kampuni ya Singida Super Quality Oil and Rice mills Simon Kitundu amezishauri halmashauri na manispaa kutenga maeneo maalum ya kufanyia biashara wajasiriamali waweze kuondokana na adha mbalimbali ikiwemo ya kuuza bidhaa zao kwenye madirisha ya mabasi.

  0 0

  Na Veronica Simba - Dodoma

  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linawajibika ipasavyo kwa wateja wake ili kukuza imani yao kwa shirika hilo.

  Akizungumza na viongozi mbalimbali wa shirika hilo wa Mkoa wa Dodoma, leo Oktoba 17, 2017, Naibu Waziri amebainisha kuwa mojawapo ya njia muhimu ya uwajibikaji kwa jamii ni kupitia utoaji taarifa kwa wateja kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu.

  “Mathalani, kunapokuwa na katizo la umeme, wateja walioko eneo husika wanapaswa kutaarifiwa kabla ya katizo hilo ili wajipange,” alisisitiza.

  Ameeleza njia nyingine ya shirika hilo kuwajibika kwa jamii, kuwa ni kushughulikia matatizo mbalimbali ya wateja wao kwa wakati na kuachana na utaratibu wa kufanya kazi kwa mazoea.

  Kwa upande wake, akiwasilisha taarifa ya kazi ya ofisi yake kwa Naibu Waziri, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu, ametaja baadhi ya mafanikio ambayo Ofisi hiyo imepata kuwa ni pamoja na kukusanya mapato kwa zaidi ya asilimia 100 pamoja na kubadilisha mita ndogo zote, zilizokuwa zikitumika zamani na kufunga LUKU.

  Naibu Waziri Mgalu, ametembelea Ofisi za TANESCO Dodoma kwa lengo la kuzungumza na wafanyakazi na kujitambulisha kwao.
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma (hawapo pichani), alipowatembelea kwa lengo la kujitambulisha kwao na kueleza vipaumbele vyake vya kazi.
  Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu (kushoto), akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi yake kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), wakati Naibu Waziri alipotembelea Ofisi hiyo na kuzungumza na viongozi.
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (aliyesimama) akizungumza na viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, alipotembelea Ofisi hizo leo Oktoba 17, 2017.
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dodoma, alipotembelea Ofisi hizo na kuzungumza na viongozi wake (hawapo pichani). Kushoto ni Meneja wa Shirika hilo Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.
  Baadhi ya viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, wakimpokea Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye nguo nyeusi) alipowasili katika Ofisi hizo kuzungumza na viongozi wake.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina (wa tatu kushoto), wakati alipokagua daraja la Kinambo lililopo katika barabara ya Kasansa-Muze KM 31.90 wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa
  Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina (wa tatu kushoto), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa fulana nyeusi), wakati alipokagua daraja la Kinambo lililopo katika barabara ya Kasansa-Muze KM 31.90 wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
  Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa daraja la Kinambo lililopo katika barabara ya Kasansa-Muze KM 31.90 wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
  Muonekano wa mitambo ya kuchimbia nguzo za Daraja la Mto Momba unaounganisha mikoa ya Rukwa na Songwe.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Groups) Corporation, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mto Momba linalounganisha mikoa ya Rukwa na Songwe
  Mbunge wa Jimbo la Kwela Mhe. Ignas Malocha, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati wa mkutano na wananchi wa Kilymatundu mara baada ya kukagua ujenzi wa Daraja la Mto Momba, wilayani Sumbawanga.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wananchi wa Kilymatundu mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mto Momba, wilayani Sumbawanga.
  Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Kilyamatundu kilichopo wilayani Sumbawanga akimkabidhi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ushahidi wa picha za miti iliyokatwa katika shamba lake kupisha mradi wa ujenzi wa Daraja la Mto Momba, mkoani Rukwa.


  ……………….


  Imeelezwa kuwa kukamilika kwa Daraja la Mto Momba linalounganisha mikoa ya Rukwa na Songwe kutafufua fursa za kiuchumi katika mikoa ya magharibi na kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema hayo leo alipokagua ujenzi wa daraja hilo na kuwahakikishia wananchi wa Wilaya ya Sumbawanga kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha daraja hilo linakamilika mwezi Agosti mwakani.

  “Toeni ushirikiano unaostahili kwa mkandarasi ili Daraja hili la Momba na madaraja madogo saba yanayojengwa katika barabara ya Kasansa-Kilyamatundu yenye urefu wa KM 210.38 yakamilike kwa wakati”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Prof. Mbarawa amesisitiza nia ya Serikali ya kujenga barabara ya Kasansa-Kilyamatundu KM 210.38 na Stalike-Kilyamatundu-Mloo KM 500 kwa kiwango cha lami ili kuongeza kasi ya uzalishaji na usambazaji wa mazao ya kilimo na mifugo katika Bonde la Mto Rukwa kwenda maeneo mingine ya nchi.

  “Wale wote ambao wamewekewa alama za kubomoa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara nawaomba wafanye hivyo mapema ili kuwawezesha wakandarasi kufanya kazi zao kwa uhuru na kuiwezesha TANROADS kufanya usanifu wa kina”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

  Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina, amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa watamsimamia kikamilifu mkandarasi anayejenga Daraja la Momba na madaraja madogo saba katika barabara ya Kasansa-Kilyamatundu KM 210.38 ili kazi ujenzi huo ukamilike kwa wakati.

  Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kwela Mhe. Ignas Malocha, amewataka wananchi watakaopata fursa za ujenzi wa madaraja hayo kuepuka vitendo vya wizi na hujuma kwa wakandarasi.

  Amesema kukamilika kwa Daraja la Momba kuna manufaa mengi kiuchumi, kijamii kwa kuwa daraja hilo litawaunganisha wakazi wa jimbo lake na mkoa wa Songwe na hivyo kuharakisha shughuli za kimaendeleo.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonga kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu kwa Shule za Jiji la Dar es Salaam hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Mpirani Zanzibar. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonga kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu kwa Shule za Jiji la Dar es Salaam hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Mpirani Zanzibar. kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayuob Mohammed Mahmoud na Mkurugenzi Masoko wa PBZ Said Ali Mwinyigogo.  
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonga kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu kwa Shule za Jiji la Dar es Salaam hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Mpirani Zanzibar. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini kwa ajili ya kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu wa Mkoa wa Dar es Salaamkulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paulo Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marine Thomas  
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonda akizungumza na kutowa shukrani kwa Uongozi wa PBZ kwa msaada wao huo kufanikisha ujenzi wa Ofisi za Walimu wea Shule za Dar es Salaam,kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Ameir Hafidhi.

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akisalimiana na badhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera alipowasili katika Ofisi hiyo ili kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera kuhusu masuala ya kiutendaji alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani humo.
  Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani Kagera, Bw. Adam Ntoga, akiwasilisha taarifa ya utendaji ya Mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani Kagera.


  Baadhi ya Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzia kuhusu uadilifu katika kazi na utoaji wa elimu kwa mlipakodi baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara ya kikazi katika Ofisi hiyo.


  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera, alipofanya ziara ya kikazi katika Mkoa huo ambapo amewaasa kuwa waadilifu katika kazi zao.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati -walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kagera na baadhi ya Maafisa Waandamizi katika Mkoa huo.
  Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Kagera Bw. Seif Mkude (kulia) akielezea kuhusu utayari wa wafanyabiashara wa Mkoa huo kulipa kodi wakati wa Mkutano kati ya wafanyabiashara wa Mkoa huo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati).


  Mfanyabiashara wa Mkoa wa Kagera Bw. Taimur Manyilizo, akieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wafanyabiashara Mkoani humo ikiwemo kile alichoeleza uwepo wa taasisi nyingi zinazodai kodi nyingi ikiwemo OSHA, TFDA, Zimamoto ambapo aliiomba Serikali iziangalie na kuzifanyia kazi.


  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akizungumza kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Kagera katika kukuza Uchumi wa nchi baada ya Naibu Waziri huyo kufanyaziara ya kikazi Mkoani humo.


  Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – WFM


  Benny Mwaipaja, KAGERA

  Serikali imelipa madeni ya wazabuni, wakandarasi na malimbikizo ya wafanyakazi yanayofikia kiasi cha shilingi bilioni 190 katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu baada ya kufanya uhakiki wa madeni halali inayodaiwa na wafanyakazi na watoa huduma mbalimbali.

  Hayo yamesemwa Mjini Bukoba mkoani Kagera na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Ashatu Kijaji (Mb), wakati akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa mkoa huo akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).


  Dokta Kijaji alisema kuwa wazabuni wamelipwa kiasi cha shilingi bilioni 67.2, wakandarasi wamelipwa shilingi bililioni 24.2, watoa huduma mbalimbali wamelipwa Shilingi bilioni 38, watumishi wa umma wamelipwa Shilingi bilioni 37, huku wadai wengine wakilipwa shilingi bilioni 24.


  Alisema kuwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017, Serikali imetenga zaidi ya Shilingi trilioni 1 kwa ajili ya kulipa madeni mbalimbali na kwamba itaendelea kulipa madeni yote yaliyohakikiwa.

  Dkt. Kijaji aliiambia Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kagera kwamba Serikali inatambua mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa kutokana na kulipa kodi zinazochangia kuboresha miundombinu na huduma mbalimbali za jamii.

  Alitoa wito kwa wafanyabiashara kutumia mashine za kielektroniki katika biashara zao, kutoa stakabadhi wanapouza bidhaa na huduma huku wananchi wakiaswa kudai stakabadhi wanapofanya manunuzi ya aina yoyote na kuhakikisha kuwa stakabadhi hizo zinaonesha kiasi halisi walicholipia huduma na bidhaa walizonunua.

  Akizungumza kwaniaba ya Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kagera, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Seif Mkude, alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa namna inavyohamasisha na kushikia bango masuala ya kodi kwa manufaa ya Taifa.

  Alisema kuwa wafanyabiashara wameridhika na namna kodi wanazolipa zinavyosimamiwa kikamilifu na kutekeleza miradi dhahiri ya maendeleo na kuahidi kuwa wataendelea kulipa kodi hizo ili kujenga uchumi wa nchi.

  Alitoa wito kwa wafanyabiashara wenzake kuendelea kulipa kodi kwa hiari ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli huku akiishauri Serikali kuondoa kero ndogondogo zilizotolewa na wafanyabiashara wakati wa mkutano huo.

  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kagera, Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro, aliwashauri wafanyabiashara hao kupanua wigo wa biashara zao ili waweze kunufaika na uwepo wa soko huru katika nchi zaidi ya nne zinazopakana na mkoa huo ikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi, DRC Kongo, Kenya na nchi nyingine.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Walemavu Jenista Mhagama akiambatana na Makamishna, Maafisa na Askari kuelekea Ofisi za Kituo cha Zimamoto Mkoa wa Ilala mara baada ya kuwasili Kituoni hapo kwa ajili ya kukagua Mradi wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na Mifumo ya utolewaji wa tahadhari za awali (DARMAERT), mapema leo asubuhi tarehe 17/10/2017.
  Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage akitoa taarifa fupi juu ya utendaji wa Jeshi hilo mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Walemavu Jenista Mhagama kuwasili Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala, kwa ajili ya kukagua Mradi wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na Mifumo ya utolewaji wa tahadhari za awali (DARMAERT), mapema leo asubuhi tarehe 17/10/2017.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akizungumza na Makamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Uongozi wa Darmaert, mara baada ya kuwasili Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala, kwa ajili ya kukagua Mradi wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na Mifumo ya utolewaji wa tahadhari za awali (DARMAERT), mapema leo asubuhi tarehe 17/10/2017.
  Kamishna wa Operesheni wa Jeshi La Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (kulia), akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya (aliyevaa suti), na Mratibu wa Darmaert Dkt. Christopher Mzava (kushoto), mara baada ya kuwasili Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala, kwa ajili ya kukagua Mradi wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na Mifumo ya utolewaji wa tahadhari za awali (DARMAERT), mapema leo asubuhi tarehe 17/10/2017.

older | 1 | .... | 1403 | 1404 | (Page 1405) | 1406 | 1407 | .... | 1897 | newer