Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

IGP SIRRO AKAGUA MAABARA YA KISAYANSI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kulia), akimsikiliza kamishna wa Polisi wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi (CP) Alice Mapunda, alipokagua Kamisheni hiyo kwa lengo la kuona namna wanavyofanyakazi pamoja na changamoto wanazokutananazo wakati wanapotekeleza majukumu yao.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kulia), akiangalia moja kati ya sampuli zinazofanyiwa Uchunguzi wa Kisayansi katika Maabara ya Polisi Makao Makuu, alipofanya ukaguzi kwenye kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi kwa lengo la kuona namna wanavyofanyakazi pamoja na changamoto wanazokutananazo wakati wanapotekeleza majukumu yao.

Picha na Jeshi la Polisi.

WAZIRI KALEMAN ATAKA MADENI YA BILI ZA UMEME KULIPWA KWA WAKATI TANESCO

$
0
0
WAZIRI wa Nishati,Dkt Medard Kalemani akizungumza na uongozi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco na wadau wa mbalimbali wa umeme ili kuweza kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa uhakika ikiwemo kuwahudumia wateja kwa wakati na kuwepo kwa uhakika wa vifaa vyenye ubora ili kuwezesha 
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza katika kikao hicho 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo akiongea katika kikao hicho kushoto ni WAZIRI wa Nishati,Dkt Medard Kalemani 
Wajumbe na wadau mbalimbali wa nishati wakifuatilia kikao hicho leo
Baadhi ya wajumbe wa uongozi wa shirika kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Uzalishaji Umeme Mhandisi Abdallah Ikwasa na kushoto ni Meneja wa Mwandamizi wa Tehama Dudu
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Tanesco nchini Dkt Tito Mwinuka kushoto na Mkurugenzi wa REA Mhandisi Gisima Nyamuhanga wakifuatilia kikao hicho
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) wakimsikiliza kwa umakini Waziri Nishati,Dkt Medard Kalemani katika kikao hicho
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kaleman akiambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Subira Mgalu wamefanya kikao na uongozi wa shirika la Umeme nchini (Tanesco) na wadau mbalimbali wa umeme ili kuweza kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha nishati ya umeme wa uhakika unapatikana.


Aliyasema hayo leo katika kikao cha pamoja baina yake na uongozi wa shirika hilo wakiwemo wadau ambapo alisema watahakikisha wanawahudumia wateja kwa wakati ikiwemo uhakika wa vifaa vyenye bora ili kuwawezesha wananchi kupatiwa umeme kwa haraka zaidi .

Licha ya hivyo lakini pia Waziri huyo alitilia mkazo suala la madeni yote ya bili za umeme kulipwa kwa wakati kwenye shirika hilo ili kuweza kuwezesha ufanisi mkubwa katika utendaji wa kazi .

Akizungumza na wazabuni mbalimbali wa miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo,nyaya na mita,Waziri Kaleman alisema kuanzia sasa vifaa vya umeme vitanunuliwa ndani ya nchi kwani kufanya hivyo itapunguza gharama kubwa na kasi ya kuwahudumia wateja."Kwani kufanya hivyo vifaa hivyo vitakuwa karibu kupatikana ndani ya nchi na kutaongeza mapato ndani ya nchi na uzalendo "Alisema.

Hata hivyo alilipongeza shirika la Umeme nchini Tanesco kwa kufanya kazi kwa bidii na kutoa taarifa kwa wateja juu ya huduma mbalimbali ikiwemo kuwataka kuwajibika kwa kufanya kazi kwa waledi mkubwa

Aidha alisema kuwa mkakati wa shirika hilo ni kuhakikisha mpaka ifikapo 2020 madeni yote shirika hilo wanayoyadaiwa kwa wateja mbalimbali nchini yatakuwa yamekwisha kulipwa.

Sambamba na hayo alikema vitendo vya wizi wa umeme na kuwataka wenye tabia za namna hiyo kuacha mara moja na ambao watabainika watachukua hatua. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

DC SHINYANGA AKABIDHI SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi sare za shule kwa wanafunzi 121 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kizumbi na Kitangili katika manispaa ya Shinyanga.


Zoezi la kukabidhi sare hizo za shule limefanyika leo Alhamis Oktoba 12,2017 katika shule ya msingi Kitangiri.Msaada huo wa sare za shule unatokana na kampeni iliyoanzishwa na mkuu huyo wa wilaya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika wilaya ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi sare hizo,Matiro alisema pamoja na serikali kuwa na sera ya elimu bure lakini wamebaini kuwa kuna watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu hivyo wanahitaji msaada kutoka wadau mbalimbali.

“Tulifanya zoezi la kugawa sare kwa wanafunzi wengine hivi karibuni,na leo ofisi yangu kwa kushirikiana na wadau wengine likiwemo shirika la wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO) nimekuja kukabidhi sare za shule kwa wanafunzi 121 wa kata ya Kitangili na Kizumbi”,alieleza Matiro.Matiro aliwataka wazazi kutimiza wajibu wao wa kulea watoto badala ya kuwatekeleza kwa bibi na babu zao na wao kukimbilia mjini huku watoto wakiteseka na kuishi katika maisha magumu.

Kwa upande wake Mratibu wa miradi kutoka shirika linalohusika na wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO),Venny Raymond alisema walifanya utafiti na kubaini kuwa kuna wanafunzi/watoto wengi katika kata ya Kitangili na Kizumbi wanaishi katika mazingira magumu hivyo kushirikiana na wadau wengine kutafuta sare za shule kwa ajili ya wanafunzi hao.

“Tumebaini kuwa watoto wengi hawaishi na wazazi wao,wengine ni yatima,lakini pia wapo ambao wazazi wao hawana uwezo kiuchumi hali inayosababisha watoto kushindwa hata kuhudhuria masomo yao,wakitumika kama chanzo cha mapato katika familia zao”,alisema Raymond.

Naye Afisa Elimu kata ya Kitangili Mahmood Ibrahim mbali na kushukuru kwa msaada huo wa sare za shule zikiwemo kaptura,sketi na mashati na kueleza kuwa kutokana na ugumu wa maisha wapo watoto wanashindwa kupata chakula na wengine kukosa mavazi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza kabla ya kuanza kugawa sare za shule kwa wanafunzi 121 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kizumbi na Kitangili leo katika shule ya msingi Kitangili mjini Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akiwataka akina mama kuunda vikundi vya ujasiriamali ili waweze kujiinua kiuchumi
Mratibu wa miradi kutoka shirika linalohusika na wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO),Venny Raymond akielezea namna walivyowapata watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kitangili na Kizumbi
Afisa Elimu kata ya Kitangili Mahmood Ibrahim akizungumza wakati wa zoezi la kugawa sare hizo za shule
Diwani wa viti Maalum kata ya Kitangili Mariam Nyangaka (CCM) akimshukuru mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kushirikiana na wadau kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wazazi,walezi na wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kabla ya kugawa sare za shule kwa wanafunzi hao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akimvalisha shati mmoja wa wanafunzi hao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akishikana mkono na mwanafunzi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akivalisha sare ya shule mwanafunzi
Mwanafunzi akiwa ameshikilia sketi baada ya kuvalishwa shati na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akitafakari jambo wakati wa kugawa sare za shule
Zoezi la kugawa sare za shule likiendelea.Wa kwanza kushoto ni Afisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Miradi kutoka shirika linalohusika na wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO).
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kizumbi Marcelina Bwathondi akijiandaa kumpa sare ya shule mmoja wa wanafunzi hao
Wazazi na walezi wa wanafunzi wakishuhudia zoezi la ugawaji sare za shule kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu.


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

DC SHINYANGA AKABIDHI SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi sare za shule kwa wanafunzi 121 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kizumbi na Kitangili katika manispaa ya Shinyanga.


Zoezi la kukabidhi sare hizo za shule limefanyika leo Alhamis Oktoba 12,2017 katika shule ya msingi Kitangiri.Msaada huo wa sare za shule unatokana na kampeni iliyoanzishwa na mkuu huyo wa wilaya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika wilaya ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi sare hizo,Matiro alisema pamoja na serikali kuwa na sera ya elimu bure lakini wamebaini kuwa kuna watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu hivyo wanahitaji msaada kutoka wadau mbalimbali.

“Tulifanya zoezi la kugawa sare kwa wanafunzi wengine hivi karibuni,na leo ofisi yangu kwa kushirikiana na wadau wengine likiwemo shirika la wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO) nimekuja kukabidhi sare za shule kwa wanafunzi 121 wa kata ya Kitangili na Kizumbi”,alieleza Matiro.Matiro aliwataka wazazi kutimiza wajibu wao wa kulea watoto badala ya kuwatekeleza kwa bibi na babu zao na wao kukimbilia mjini huku watoto wakiteseka na kuishi katika maisha magumu.

Kwa upande wake Mratibu wa miradi kutoka shirika linalohusika na wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO),Venny Raymond alisema walifanya utafiti na kubaini kuwa kuna wanafunzi/watoto wengi katika kata ya Kitangili na Kizumbi wanaishi katika mazingira magumu hivyo kushirikiana na wadau wengine kutafuta sare za shule kwa ajili ya wanafunzi hao.

“Tumebaini kuwa watoto wengi hawaishi na wazazi wao,wengine ni yatima,lakini pia wapo ambao wazazi wao hawana uwezo kiuchumi hali inayosababisha watoto kushindwa hata kuhudhuria masomo yao,wakitumika kama chanzo cha mapato katika familia zao”,alisema Raymond.

Naye Afisa Elimu kata ya Kitangili Mahmood Ibrahim mbali na kushukuru kwa msaada huo wa sare za shule zikiwemo kaptura,sketi na mashati na kueleza kuwa kutokana na ugumu wa maisha wapo watoto wanashindwa kupata chakula na wengine kukosa mavazi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza kabla ya kuanza kugawa sare za shule kwa wanafunzi 121 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kizumbi na Kitangili leo katika shule ya msingi Kitangili mjini Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akiwataka akina mama kuunda vikundi vya ujasiriamali ili waweze kujiinua kiuchumi
Mratibu wa miradi kutoka shirika linalohusika na wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO),Venny Raymond akielezea namna walivyowapata watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kitangili na Kizumbi
Afisa Elimu kata ya Kitangili Mahmood Ibrahim akizungumza wakati wa zoezi la kugawa sare hizo za shule
Diwani wa viti Maalum kata ya Kitangili Mariam Nyangaka (CCM) akimshukuru mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kushirikiana na wadau kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wazazi,walezi na wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kabla ya kugawa sare za shule kwa wanafunzi hao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akimvalisha shati mmoja wa wanafunzi hao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akishikana mkono na mwanafunzi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akivalisha sare ya shule mwanafunzi
Mwanafunzi akiwa ameshikilia sketi baada ya kuvalishwa shati na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akitafakari jambo wakati wa kugawa sare za shule
Zoezi la kugawa sare za shule likiendelea.Wa kwanza kushoto ni Afisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Miradi kutoka shirika linalohusika na wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO).
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kizumbi Marcelina Bwathondi akijiandaa kumpa sare ya shule mmoja wa wanafunzi hao
Wazazi na walezi wa wanafunzi wakishuhudia zoezi la ugawaji sare za shule kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu.


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

WAANDISHI WA HABARI ZA VIJIJINI WATUNUKIWA VYETI VYA KUHITIMU MAFUNZO NA UTPC

$
0
0


Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Vijijini kutoka vilabu mbalimbali vya waandishi wa habari hapa Nchini,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari hapa Nchini(UTPC),chini ya ufadhili wa SIDA yaliyofanyika leo Mkoani Morogoro.(Habari Picha na Pamela Mollel).
Mwenyekiti wa Morogoro Press Club Nikson Mkilanya ambae alikuwa mgeni rasmi katika kufunga mafunzo hayo,akisisitiza washiriki wa mafunzo hayo kutumia vyema fursa hiyo waliyoipata katika kuibua changamoto mbalimbali za vijijini.
Mkufunzi wa Mafunzo ya uwandishi wa habari za vijijini Joe Nakajumo akizungumza na baadhi ya wanahabari walioshiri mafunzo hayo leo Mjini Morogoro.
Mshiriki wa mafunzo Edith Karlo kutoka Kigoma PressClub kikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nekson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo oleo.
Mshiriki wa mafunzo Adam Juma kutoka Mtwara Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Pamela Mollel kutoka Arusha Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Agustino Kihombo kutoka Iringa Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Raya Kipingu kutoka Tanga Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Khadija Yussuph kutoka Pemba Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Queen Isack kutoka Kilimanjaro Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Eliza Faustine kutoka Mwanza Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Sunday Bavuga kutoka Njombe Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Ally Hamisi kutoka Zanzibar Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Anita Balingilaki kutoka Simiyu Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Amon Mtega kutoka Ruvuma Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Halima Katala kutoka Morogoro Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Norrah Damian kutoka Dar es saalam Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Alphonce Kabilondo kutoka Geita Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Laudence Semkondya kutoka Mbeya Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Happy Mtweve kutoka Dodoma Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Shija Ferisha kutoka Shinyanga Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

HER INITIATIVE YAPIMA AFYA WATOTO WA KIKE KAWE SEKONDARI KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Her Initiative,Lydia Charles akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kawe wakati  wa mahadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani kwa kutoa elimu ya afya ya Uzazi na kuwapima afya wanafunzi wa kike wa shule hiyo .
 Mmoja watangazaji wa kipindi cha Mitindo cha Clouds Televisheni akiwa na mmoja wanafunzi wa shule ya Sekondari kawe wakati alipokuwa akitoa somo la afya ya uzazi kwa wanafunzi hao  kupitia programu ya Her Initiative.
 Mtangazaji wa kipindi cha Clouds E, Saida Khalifani(Shadey) akizungumza na wanfunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Kawe juu ya hatua muhimu za kupitia kufikia ndoto zao wakati wa tasisi ya Her Initiative ilipokwenda shuleni hapo katika mahadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani
 Madaktari wakiendelea na zoezi la upimaji afya kwa wanafunzi na wadau waliofika katika kuadhimisha siku ya mtoto wa kike katika shule ya Sekondari ya Kawe.
 Wadau wakiwa katika picha ya pozi na wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari ya Kawe katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Kike Duniani.
 Dk. Irene Shirima akimpima mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kawe wakati wa kuahadhimisha siku ya Mtoto wa kike Duniani
 Mtangazaji wa kipindi cha Clouds E, Saida Khalifani(Shadey) akipima afya na  wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kawe wakati wa kuahadhimisha siku ya Mtoto wa kike Duniani
 Dk. Irene Shirima akimpima mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kawe wakati wa kuahadhimisha siku ya Mtoto wa kike Duniani

NBC yazindua Mwezi wa Huduma kwa Wateja kwa kuboresha huduma za bidhaa zao kukidhi mahitaji ya wateja.

$
0
0
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana. Mkurugenzi huyo alisema katika maadhimisho hayo NBC imezidi kuboresha ubora wa huduma na bidhaa mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya wateja wao wa kada zote. Kulia ni Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi wakikata utepe ili kurusha ‘puto’ kuashiria uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha NBC, Ngwitika Mwakahesya akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC jijini Dar es Salaam jana.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia), akizungumza waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo  katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana.

 Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Neema Rose Singo (kushoto), akibadilishana mawazo na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi huku baadhi ya maofisa wengine wa NBC  wakiangalia katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kulia ni , Alina Maria Kimaryo, Jane Mbago, Ngwitika Mwakahesya na Irene Peter.
  Kaimu mKurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Thobald Sabi (kulia) akmsikiliza kwa makini Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa benki hiyo, James Kinyanyi wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakiwa na nyuso za furaha wakati kaimu mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo akizungumza nao.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja jijini Dar es Salaam jana. 
 Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakipozi kwa picha wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.

MRADI WA UMEME MAKAMBAKO-SONGEA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UENDESHAJI SHAMBA LA KAHAWA AVIV MKOANI RUVUMA KWA ASILIMIA 70

$
0
0
Meneja wa Shamba la Kahawa, Aviv, linalomilikiwa na kampuni ya Olam Tanzania Limited lililoko kijiji cha Lipokela, kilomita 45 kutoka Songea mjini Bw.Hamza Kassim, (katikati), akizungumzia mradi wa umeme wa Makambako-Songea ambao utaunganishwa kwenye kiwanda chake, mbele ya wahariri wa vyombo vya habari waliofika kiwandani hapo ili kujionea manufaa yatokanayo na mradi huo katika uwekezaji mkubwa, Oktoba 12, 2017.



UONGZI wa Shamba la Kahawa la Aviv, lililoko kijiji cha Lipokela, kilomita 45 kutoka Songea mjini, umesema Mradi wa umeme wa Makambako-Songea utaleta nafuu kubwa ya kupunguza gharama za kuendesha majenereta ya kufua umeme kwenye shamba hilo kwa asilimia 70, Meneja wa shamba Bw.Hamza Kassim amesema.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea shamba hilo ili kupata maoni ya wamiliki kuhusiana na mradi mkubwa wa umeme wa 220kV, Makambako- Songea Oktoba 12, 2017, Bw. Kassim alisemamahitaji ya umeme kwenye shamba hilo ni Megawati 2.25 hadi 2.5 na zote hizo zinazalishwa na umeme wa kutumia mafuta (Jenereta). 

shamba hilo linalo ilikiwa na kampuni ya Olam Tanzania Limited yenye makao yake makuu nchini Songapo, lina ukubwa wa Hekta 1,012 kati ya hizo, Hekta 1,000,000 zimepandwa mazao.“Mimea ya Kahawa ambayo imefikia hatua ya kupevuka (matured), ni Hekta 800, huku Hekta 200 bado ni Kahawa changa, tunatumia nishati ya umeme kwa shughuli za umwagiliaji na ubanguaji wa Kahawa ambapo kwa siku tunatumia lita 4,000 za dizeli kuendesha jenereta hizo.” Alifafanua Bw. Kassim.

Ujio wa mradi huu ni faraja kubwa kwetu na tunashukuru mradi huu utakapokamilika utatupunguzia gharama za uendeshaji kwa asilimia 70 na hivyo kutupa fursa ya kufanya upanuzi zaidi wa kilimo cha kahawa, Alibainisha Meneja huyo.

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Patrick Lwesya alisema, Shamba la Aviv, ni moja kati ya wateja wake elfu kumi, (10,000), ambao wataunganishiwa umeme, Desemba mwaka huu 2017 baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa usambazaji umeme wa kilovolti 33 pamoja na kuunganisha wateja 22,700, katika mikoa ya Songea na Njombe.

“Shamba hili ndio wateja wetu wakubwa kabisa, na tunamuhakikishia muwekezaji huyu kumpatia umeme zaidi endapo atauhitaji kwani kwa sasa tunazalisha umeme kwa asilimia 99.75, lakini mradi ukikamilika tutazalisha kwa asilimia 100 na umeme utakuwa bora na wa uhakika.” Alisema Mhandisi Lwesya.Alisema, pamoja na mteja huyo wa shamba la Kahawa la Aviv, pia wateja wengine watakaofikishiwa umeme chini ya mradi huo ni pamoja na wale wa Mji wa Songea, vijiji vilivyo katika wilaya za Mbinga, Namtumbo na Halmashauri ya Madaba.

“Nitoe wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza mkoani kwetu kwani tunao umeme wa kutosha kutokana na uzalishaji wake ambapo tunazalisha jumla ya Megawati 6.3 huku mahitaji halisi ya Mkoa ni Megawati 5.3.” Alisema.Hata hivyo kumekuwepo vitendo vya uharibifu wa miundombinu hiyo mipya iliyojengwa chini ya mradi huu vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wanaochoma misitu kwa ajili hya kuandaa mashamba.

Wahariri walishuhudia nguzo mbili moja ikiwa imeungua vibaya huku nyingine ikiwa imeungua kabisa na kubaki nyaya zikining’inia kandokando ya barara ya Songea-Mbinga kwenye kijiji cha Lipokela.

“Vitendo hivi vinasikitisha sana, niwaombe wananchi waache tabia hiyo kwani mradi huu unakwenda kubadilisha maisha yao na kwa kufanya uharibifu huu ni kuhujumu jitihada za Shirika la Umeme TANESCO kwa niaba ya Serikali, kutatua changamoto ya upatikanaji umeme wa uhakika kwa wananchi.” Alisema Meneja wa Mradi wa umeme wa Makambako-Songea Mhandisi Didas Lyamuya.

Maneno ya Meneja huyo yaliungwa mkono na Meneja wa Shamba la Aviv ambalo liko jirani na eneo ambako nguzo hizo zilichomwa moto na kutaka utamaduni wa wananchi wa mkoa wa Ruvuma wa kuchoma moto nyasi na misitu kwa nia ya kutayarisha maeneo ya kilimo waache.

“Nilifurahi ni hivi majuzi tu Mkuu wa Mkoa alizunguzia vitendo hivi na kuwaagiza viongozi wa serikali kwenye kata na vijiji kuwaelimisha wananchi kuhusu madhara ya vitendo hivyo, na kwa uoande etu sisi tumejenga mifumo ya kuzima moto kuzunguka eneo letu la shamba.” Alibainisha.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania, 9TANESCO), Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Patrick Lwesya, (wakwanza kulia), akizungumza kwenye eneo la Shamba la Aviv, kuhusu hatua iliyofikiwa na TANESCO kupeleka umeme wa kutosha kwenye shamba hilo ifikapo Desemba mwaka huu wa 2017. Wengine pichani kutoka kushoto mstari wa mbele, ni pamoja na Meneja Mradi wa umeme Makambako-Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, na Meneja wa Shamba hilo, Bw. Hamza Kassim, (katikati).
Kamimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akiwaonyesha Wahariri kibao cha alama ya hatari, kilichowekwa kwenye moja ya nguzo za umeme zilizoteketea kabisa kwa moto. Nguzo hizo mpya zimesimikwa hivi karibuni ikiwa ni utekelezaji wa ujenzi wa mfumo wa usambazaji umeme wa kilovolti 33 kwenye maeneo ya vijijini chini ya mradi huo wa Makambako-Songea. Uharibifu huo ulifanywa kwenye kijiji cha Lipokela kandokando ya barabara ya Songea-Mbinga, mkoani Ruvuma.
Bi. Leila Muhaji na Bw. Fredrik Lewerstrom kutoka kampuni ya Sweco, wakionyesha kuhuzunika kufuatia uharibifu mkubwa wa kuchoma nguzo ya umeme kijiji cha Lipokela.
Huu ndio uharibifu uliofanywa na wananchi wanaochoma moto nyasi na misitu mkoani Ruvuma na hivyo kuunguza miundombinu ya TANESCO
Wahariri na wahandisi wa TNESCO wakiwepo wakandarasi wa Mradi wa umeme wa Makambako-Songea wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembelea kituo cha sasa cha kufua umeme eneo la Lizaboni mjini Songea Oktoba 12, 2017. 
Wahariri na wahandisi wa TNESCO wakiwemo wakandarasi wa Mradi wa umeme wa Makambako-Songea wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme mjini Songea Oktoba 12, 2017 
Meneja wa Mradi wa umeme wa 220kV, Makambako-Songea Mhandisi Didas Lyamuya, akifafanua baadhi ya mambo kwenye eneo la ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme cha Songea ambacho kiko katika hatua ya ujenzi wa msingi wa kufungia mitambo. Chini ya mradi huo jumla ya vituo vipya viwili vya kupoza umeme vinajengwa huko Madaba na kimoja kinafanyiwa upanuzi huko Makambako
Taswira ya ujenzi wa msingi wa kufungia mitambo kituo kipya cha kupoza umeme cha Songea.

SHAKA AONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIET YA BARAZA KUU UVCCM TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akifafanua jambo wakati akiongoza kikao cha Secretariet ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kwa  maandalizi ya vikao vya kikanuni vya Umoja wa Vijana wa CCM vitakavyofanyika Dodoma
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiongoza kikao cha Secretariet ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kwa  maandalizi ya vikao vya kikanuni vya Umoja wa Vijana wa CCM vitakavyofanyika Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine vitajadili waombaji wa nafasi mbali mbali za uongozi kwa nafasi za Mkoa na Taifa kupitia Umoja wa Vijana wa CCM kabla kuwasilisha katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi kwa uteuzi wa mwisho.(picha na Fahadi Siraji wa UVCCM )

TAASISI YA' ROOM TO READ ' YAMPA TUNZO MAMA SALMA KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI

$
0
0
MKE wa Rais wa awamu ya nne mama Salma Kikwete  jana alikabidhiwa  tuzo ya heshima kutokana na kutambua jitihada zake za kumlinda na kumtetea mtoto wa kike  iliyotolewa na  Taasisi isiyo ya Kiserikali inayifahamika kwa jina la Room to Read.

Mama Kikwete alikabidhiwa tuzo hiyo  Mkurugenzi wa Room To Read  Peter Mwakabwale kwenye hafla iliyofanyika viwanja vya Bwawani Kihaba Maili Moja Mkoani Pwani.

Akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka katika shule mbalimbali za mkoa  wa Pwani mama  Kikwete amezitaka Hamlashari kutenga bajeti ya kujenga mabweni katika shule kwa ajili  ya wanafunzi wakike  sanjari  na kujenga  maabara  na vyumba  vya madarasa  ili kuweza  kuwarahisishia  wanafunzi  hususani wasichana  ili waweze kujifunza  bila  kikwazo chochote na kufaulu vema masomo yao.
Aidha  Mama Salma Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi  katika   maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike  duniani ambayo yameadhimishwa  kimkoa Kibaha Mkoani Pwani.
Mama Salma Kikwete amesema kuwa  Mkoa wa Pwani unashika nafasi ya kumi  kitaifa kwa mimba  huku sababu mojawapo ni  ukosefu wa mabweni ya wasichana hali inayopelekea wasome shule za kutwa na kukutana na vishawishi wawapo njiani kuelekea ama kurudi shule.
Maadhimisho hayo yamefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Room to Read linaloendesha mradi wa Elimu kwa Wasichana  katika mkoa wa Pwani  na  kuzihusisha  Wilaya za Bagamoyo, Chalinze na Kibaha ambapo wamekuwa wakitoa elimu ya stadi za maisha kwa wasichana lakini pia kuwasaidia gharama za mahitaji ya shule pamoja na karo kwa familia zisizo na uwezo wa kifedha 
 Siku ya kumuenzi mtoto wa kike  huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 11 kufuatia  maazimio  ya malengo endelevu  ya Umoja wa mataifa , viongozi  wa nchi mbalimbali  duniani  walikubaliana  na kuyapitisha   huku miongoni mwa malengo  matano   mojawapo  kuhakikisha  tunafikia usawa  wa kijinsia  na uwezeshaji  wa wasichana  na wanawake  wote  duniani ifikapo mwaka 2030.
Wahamasishaji wa Mradi wa Elimu kwa wasichana Room to Read wakionesha kazi wanazozifanya katika maadhimisho ya mtoto wa Kike duniani October 11 mkoani Pwani -kibaha

Upepo umebadilika kesi ya Mwana FA, AY na Tigo

$
0
0


Dar es salaam: Upepo umebadilika katika kesi baina ya Tigo Tanzania na wasanii maarufu wa mziki wa kizazi kipya, Hamisi Mwinyjuma maarufu MwanaFA na Ambwene Yesaya maarufu AY, baada ya Mahakama Wilaya ya Ilala kutupilia mbali pingamizi la awali lililowekwa na wasanii hao.
Mahakama hiyo sasa imekubali kusikiliza maombi ya Kampuni ya Tigo kuhusu kujumuishwa kwa kampuni ya Cellular Tanzania Limited kwenye hukumu kama mmoja wa wadaiwa wa fidia ya Sh 2.1 bilioni. Hapo awali Mahakama ilikuwa imeamuru kampuni ya Tigo kuwalipa wasanii hao kwa madai ya kutumia nyimbo zao zenye hati miliki bila ruksa.
Pia Mahakama imekubali kusikiliza ombi la Tigo la kurekebishwa makosa ya kiuandishi yanayohusu majina ya wahusika katika kesi hiyo, ambapo jina la Hamis Mwinjuma ndilo liloandikwa kwenye hukumu wakati Hamis Mwinyijuma ndilo jina linaloonekana kwenye hati ya madai. Vilevile hukumu inaonesha jina Ambwene Yessayah wakati jina lililopo kwenye hati ya madai ni Ambwene Yesaya.
Vile vile, kampuni ya Cellular Tanzania Limited ambayo Tigo inadai ndio ilioingia nayo mkataba wa kutoa huduma za muziki haikuwa imejumuishwa kwenye hukumu hiyo. Hapo awali, kampuni hiyo ya Ms Cellular Tanzania ilikuwa imeandikia barua Mahakama ikibainisha kuwa ndiyo iliyokuwa imeisambazia kampuni ya Tigo nyimbo hizo. Katika barua yenyewe, Cellular Tanzania ilidai kuwa ilinunua nyimbo hizo za Usije Mjini wa MwanaFA na Dakika moja wa AYkutoka kwa kampuni ya Sony Music Entertainment Africa Limited ambayo walikuwa na mkataba na watayarishaji wa nyimbo hizo.
Wasanii hao kupitia wakili Albert Msando waliweka pingamizi kuhusu maombi ya Tigo, wakiiomba Mahakama iyatupilie mbali. Walidai kifungu cha 96 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai kilichotumika kufungua maombi hakiiwezeshi Mahakama kutekeleza maombi hayo kwa sababu kosa la kutoihusisha kampuni hiyo ya Cellular Tanzania siyo la kiuandishi wa hesabu.
Akitoa uamuzi wa Mahakama, Hakimu Mfawidhi, Ritha Tarimo alisema hoja za wasanii hao hazipaswi kuwasilishwa kama pingamizi, hivyo alipanga kusikiliza maombi hayo Oktoba 18.     
Awali, Tigo ilifungua maombi Mahakama Kuu ikiomba kusimamishwa utekelazaji wa hukumu.  

ETIHAD AIRWAYS TO LAUNCH FLIGHTS TO AZERBAIJAN

$
0
0

Abu Dhabi, UNITED ARAB EMIRATES – Etihad Airways has announced plans to launch scheduled flights between Abu Dhabi, the capital of the United Arab Emirates, and Baku, the capital city of the Republic of Azerbaijan, effective 2 March 2018.

The new route is being introduced to capitalise on the strong and growing demand for flights between the United Arab Emirates and Azerbaijan. The service will be operated three times a week using a 136-seat Airbus A320, configured with 16 seats in Business Class and 120 in Economy.

Azerbaijan introduced a visa waiver programme for UAE nationals in November 2015 and expanded it to other GCC nations in early 2016. This prompted a surge in travel from across the GCC to the emerging tourist destination located at the crossroads of Europe and Asia, which offers visitors access to vast areas of unspoiled nature and centuries-old culture. Baku, which sits on the Caspian Sea, is the country’s primary gateway and commercial centre.

Peter Baumgartner, Etihad Airways Chief Executive Officer, said: “The creation of the first ever air corridor linking the two capital cities demonstrates the importance of strengthening business, tourism and cultural ties between the UAE and Azerbaijan.

“The newest destination on Etihad Airways’ global network also reflects our commitment to linking Abu Dhabi with emerging markets that seek direct flights and onward connections to other parts of the world.

“Based on the growth witnessed in recent months from the UAE and neighbouring Gulf countries to Azerbaijan, we are confident that the new route will boost traffic from the UAE, and in turn we look forward to welcoming Azerbaijanis on our flights to Abu Dhabi and beyond.”

During the first nine months of 2016, foreign tourists visiting Azerbaijan totalled 1.7 million. The number of visitors from the UAE and GCC increased 30 times on the same nine-month period in 2015, fuelled by the easing of visa restrictions.

Earlier this year, the UAE-Azerbaijan Joint Economic Committee said both countries were to focus on nine key areas for bilateral cooperation, including air transport, tourism, communications, environment, water, agriculture, renewable energy, modern technology and industry. Non-oil trade between the two countries reached over US$605 million in 2015, increasing by US$228 million during the first nine months of 2016.

Etihad Airways’ new flights, operating every Wednesday, Friday and Saturday, provide optimum timings for guests departing and arriving in Abu Dhabi and Baku. The schedule also provides convenient connections to and from the airline’s global network.

Flight schedule: Abu Dhabi – Baku, effective 2 March 2018:

Flight No.
Origin
Departs
Destination
Arrives
Frequency
Aircraft
EY297
Abu Dhabi
10:10
Baku
13:15
Wed, Fri, Sat
A320
EY298
Baku
16:30
Abu Dhabi
19:25
Wed, Fri, Sat
A320

Note: All departures and arrivals are listed in local time.

HUONI HAFIFU HUCHANGIA MATOKEO MABAYA KWA WANAFUNZI DARASANI

$
0
0
 Mwalimu wa shule ya Msingi Nguvumali Jijini Tanga akichukua maelezo ya wanafunzi kabla ya kuanza zoezi la upimaji wa huduma ya macho wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo siku hiyo iliendana na sambamba na upimaji macho ulioendeshwa na Duka la Miwani la Noor Optics kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji hilo kwa wanafunzi wa shule za msingi za mabokweni,kwanjeka na nguvumali,
 Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Tanga,Dkt Frida Kassiane akiwapima macho mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Nguvumali Jijini Tanga wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo siku hiyo iliendana na sambamba na upimaji macho ulioendeshwa na Duka la Miwani la Noor Optics kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji hilo kwa wanafunzi wa shule za msingi za mabokweni,kwanjeka na nguvumali,

 Amina Nasoro ambaye Mratibu wa Huduma ya Afya ya Macho katika kampuni ya kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga akichukua maeleza ya wanafunzi kabla ya kuwapima

 Amina Nasoro ambaye Mratibu wa Huduma ya Afya ya Macho katika kampuni ya kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga akichukua maeleza ya wanafunzi kabla ya kuwapima


 Zoezi la Uandikishaji wa majina wanafunzi wa shule ya Msingi Nguvumali kwa ajili ya upimaji wa macho likiendelea
Zoezi la kuwapima wanafunzi likiendelea
SABABU kubwa za wanafunzi wa shule za msingi  kutokufanya vizuri darasani imeelezwa inatokana  na uoni hafifi kwa baadhi yao na sio kwamba hawana akili .

Lakini pia imebainishwa pia kati ya watu 100 kati ya 15 wana kabi liwa na tatizo la macho ambalo limekuwa likiwaathiri kwa asilimia na kushindwa kufikia malengo yao.

Hayo yalibainishwa juzi na Mratibu wa Huduma za Macho Mkoani Tanga Dkt Frida Kassiane wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo yalienda sambamba na upimaji wa macho uliokuwa ukiendeshwa na kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga.

Alisema hatua hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi kuumwa macho huku wakiwa hawajitambui kutokana na kutokuwepo kwa utaratibu za utoaji wa huduma za upimaji machi kwao hususani mashuleni.

“Ukiangalia leo hii baadhi ya wanafunzi utakuwa walikuwa wakifanya vizuri katika mitihani yao lakini ghafla wanaanza kushuka kiwango na hili unaweza kukuta linasababishwea na tatizo la macho kama lilivyogundulika kwa wanafunzi wachache kwenye shule tulizopita “Alisema.

Alisema suala hilo linasababishwa pia na lishe dunia kwa asilimia kubwa ya watoto wengi ikiwemo kukosa kupata vyakula vilivyokuwa na virutubisho vinavyoweza kuongeza nguvu na kinga ya macho.

Alisema zoezi hilo ambalo limeanza siku nne zilizopita limewafikia zaidi ya wanafunzi 1500 katika shule za Msingi,Kwanjeka,Mabokweni na Nguvumali ambapo baadhi yao walibainika kuna matatizo hayo na kusaidia matitabu zaidi na kampuni hiyo.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Noor Optics, Raouf Nasser alisema lengo kubwa ni kutoa huduma hiyo katika shule zote za msingi ili kusaidia kubaini changamoto za macho zinazowakabili na namna ya kupatiwa ufumbuzi.

Alisema alisema kampuni hiyo kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Tanga wameamua kuendesha zoezi hilo kila mwaka ili kuweza kuwasaidia watoto ambao watabainika wanakabiliwa na matatizo hayo ili waweze kufikishwa kwa wataalamu kwa matibabu zaidi.

“Asilimia kubwa ya wazazi hawana uwezo wa kuwapeleka watoto wao katika hospitali kufanyiwa vipimo vya matatizo hayo hivyo sisi tumeamua kwa nia moja kusaidia jamii ikiwa ni kurudisha faida kwao kutokana na huduma tunazotoa “Alisema.

Aidha alisema msingi mzuri wa kuyatunza macho ni lazima kuwepo utaratibu wa kuyafanyia vipimo mara kwa mara hasa wanapokuwa kwenye hatua ya ukuaji kabla ya kufikia umri mkubwa ambapo tatizo hilo linaweza kuwa kubwa zaidi.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

WASHINDI WA SHINDANO LA FIKA NA FINCA WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO LEO

$
0
0
Mtaalamu wa Masoko wa Benki ya FINCA Bw. Noel Mulumba  Akimkabidhi zawadi ya Tiketi ya basi  Bw.Hussein Bashe (katikati) ambaye ni mshindi wa Bahati nasibu inayoendeshwa na Benki hiyo inayoitwa Fika Na FInca anayeshuhudia ni Afisa Usafirishaji wa mabasi ya kampuni ya New Force Masumbuko Masuke mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Finca Jijini Dar es salaam.
Mtaalamu wa Masoko wa Benki ya FINCA Akimkabidhi zawadi ya Tiketi ya basi  Bw.Charles Alfred (katikati) ambaye ni mshindi wa Bahati nasibu inayoendeshwa na Benki hiyo inayoitwa Fika Na FInca anayeshuhudia ni Afisa Usafirishaji wa mabasi ya kampuni ya Ngorika Joyce Assenga     mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Finca Jijini Dar es salaam.

Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance Bw. Nicholous John, akifurahi jambo na  Adam Jumanne wa pili kutoka kulia akipokea zawadi kwa niaba ya Miriam Masanje  ambaye ni mshindi wa Bahati nasibu inayoendeshwa na Benki hiyo inayoitwa Fika Na FInca Mtaalamu wa Masoko wa Benki ya FINCA Bw. Noel Mulumba (katikati) na mwishoni kulia Afisa Usafirishaji wa mabasi ya kampuni ya New Force Masumbuko Masuke mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Finca Jijini Dar es salaam.

Washindi wa Bahati nasibu inayoendeshwa na Benki ya Finca wakiwa katika picha ya pamoja  na viongozi wa benki ya FINCA na maafisa usafirishaji wa Ngolika na New force  mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao mapema leo katika ofisi za makao makuu ya FINCA jijini Dar es salaam.



Washindi wa Bahati nasibu inayoendeshwa na Benki ya Finca wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao mapema leo katika ofisi za makao makuu ya FINCA jijini Dar es salaam.

Wateja wa Tigo Mbeya wapata huduma za bidhaa kwa bei nafuu msimu huu wa Tigo Fiesta

$
0
0
Msimamizi msaidizi wa Duka la Tigo mkoani Mbeya, Elifazi Mtwale akitoa huduma kwa wateja waliofika dukani hapo kupata huduma mbalimbali kwa bei nafuu msimu huu wa Tigo Fiesta leo.
Mtoa huduma wa Duka la Tigo mkoani Mbeya, Janeth  Rwanga akitoa huduma kwa wateja waliofika dukani hapo kupata huduma mbalimbali kwa bei nafuu msimu huu wa Tigo Fiesta leo.

MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA VITUO VYA WATOTO YATIMA NA WAZEE ZANZIBAR LEO

$
0
0
Mama Janeth Magufuli na Mama Mwanamema Shein wakiwa na baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Mazizini Unguja ambako wake hao wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Zanzibar walitembelea ambapo Mama Magufuli alitoa msaada wa vyakula mbali mbali na mafuta ya kupikia na sukari leo Oktoba 13, 2017.
Mama Janeth Magufuli akiwa ameongozana na Mama Mwanamema Shein katika kituo cha yatima cha SOS eneo la Mombasa mjini Unguja ambako wake hao wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Zanzibar walitembelea ambapo Mama Magufuli alitoa msaada wa vyakula mbali mbali na mafuta ya kupikia na sukari leo Oktoba 13, 2017.
Mama Janeth Magufuli akiwa na Mama Mwanamema Shein wakimsalimia Bibi anayelelewa katika kituo cha Wazee eneo la Welezo ambako wake hao wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Zanzibar walitembelea ambapo Mama Magufuli alitoa msaada wa vyakula mbali mbali na mafuta ya kupikia na sukari leo Oktoba 13, 2017.
Mama Janeth Magufuli akiwa ameongozana na Mama Mwanamema Shein wakisalimia baadhi ya wazee wanaolelewa katika kituo cha Welezo Unguja wakati wake hao wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Zanzibar walitembelea ambapo Mama Magufuli alitoa msaada wa vyakula mbali mbali na mafuta ya kupikia na sukari.
Mama Janeth Magufuli akiwa ameongozana na Mama Mwanamema Shein akikabidhio msaada wa vyakula kwa ajili ya wazee wanaolelewa kituo cha Welezo Unguja wakati wake hao wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Zanzibar walitembelea ambapo Mama Magufuli alitoa msaada wa vyakula mbali mbali na mafuta ya kupikia na sukari leo Oktoba 13, 2017.
Mama Janeth Magufuli akiwa ameongozana na Mama Mwanamema Shein wakiwa katika kituo cha kulelea Wazee cha Sebleni Unguja wakati wake hao wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Zanzibar walitembelea ambapo Mama Magufuli alitoa msaada wa vyakula mbali mbali na mafuta ya kupikia na sukari leo Oktoba 13, 2017.
Mama Janeth Magufuli akisalimiana na mwakilishi wa wazee wanaoishi katika kituo cha kulelea Wazee cha Sebleni Unguja wakati alipotembelea ambapo alitoa msaada wa vyakula mbali mbali na mafuta ya kupikia na sukari leo Oktoba 13, 2017. .

Mama Janeth Magufuli akiwa ameongozana na Mama Mwanamema Shein akitoa misaada katika kituo cha yatima cha wazee cha Sebleni Unguja wakati wake hao wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Zanzibar walitembelea ambapo Mama Magufuli alitoa msaada wa vyakula mbali mbali na mafuta ya kupikia na sukari leo Oktoba 13, 2017.
Mama Janeth Magufuli akiaga baada ya kutembelea katika kituo cha kulelea Wazee cha Sebleni Unguja wakati alipotembelea hapo na kutoa msaada wa vyakula mbali mbali na mafuta ya kupikia na sukari leo Oktoba 13, 2017.


PICHA NA IKULU

EXIM BENKI YATUA DODOMA WANANCHI KUNUFAIKA NA HUDUMA.

$
0
0
 Dodoma District Commissioner Christina Mndeme on behalf of the Regional Commissioner Jordan Rugimbana, officially launches Exim Bank Dodoma Branch earlier yesterday during the official ceremony. The branch which is located inside the University of Dar es Salaam Dodoma will serve the captive clients of the University of Dodoma, which consists of over 25,000 students, 2000 employees and over 8 Government Ministries who have moved there. It will also serve the Dodoma City clients, as the branch is only 5 to 7 minutes drive from the city centre. To her right is Mr Fredrick Kanga, head of Human Resources at Exim Bank Tanzania.
 Mr Fredrick Kanga, Head of Human Resources at Exim Bank Tanzania addressing guests, customers and media during the official launch of Exim Bank Dodoma Branch located inside the University of Dodoma, at Chiwaga area yesterday. Others are Mr Stanley Kafu, Head of Marketing at Exim Bank Tanzania (left) and the guest of honour District Commissioner Christina Mndeme.
 Dodoma District Commissioner Christina Mndeme, addressing the guests, customers and media during the official launch of Exim Dodoma Branch located inside the University of Dodoma, at Chiwaga area yesterday. Others are Mr Fredrick Kanga, Head of Human Resources at Exim Bank Tanzania (left) and Mr Stanely Kafu, Head of Marketing at Exim Bank Tanzania (left).
 Exim Bank Dodoma Branch staff interacting with the guest of honour Dodoma District Commissioner, Christina Mndeme during the official launch of the branch located inside the Universty University of Dodoma, at Chiwaga area yesterday.


BENKI ya Exim Tanzania imethibitisha  kujitolea  kuimarisha ushirikishwaji wa wa nanchi kwenye mfumo rasmi wa kifedha nchini kwa kuzindua tawi jipya katika mkoa wa Dodoma,Tanzania. UtanuzihuuutaongezauwepowaBenkiya Exim kuwanajumlayamatawi 33nchinikote.
Akizungumza katika uzinduzi rasmi Fredrick Kanga, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu katika Benki ya Exim Tanzania, alisema, "Utanuzi wa benki ni sehemu ya mkakati wetu wakukuza huduma zetu katika maeneo ambayo yanatuleta karibu na wateja wetu. Tawi litatoa huduma kamili za kibenki kama vile kuhifadhi pesa, huduma za uwekezaji, na suluhisho za malipo ya kampuni."
Tawi la Dodoma, lililopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma, litawahudumia wateja wa Chuo Kikuu hiko, ambacho kina wanafunzi zaidi ya 25,000, wafanyakazi2000 na Wizara za Serikali zaidi ya 8 ambazo zimehamia huko. 
Tawi litawatumikia wateja wa Jiji la Dodoma, kwa kuwa tawili na umbali wadakika 5 hadi 7 kwa mwendo wa gari kutoka katikati ya jiji.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alipongeza Benki ya Exim Tanzania kwa kujitolea kwake "Tunafurahi kuwa na uwepo wa Benki ya Exim katika mji mkuuwa Tanzania, ili kuimarisha ushirikishwaji wa wananchi kwenye mfumo rasmi wa kifedha  unao wawezesha kupata huduma, bidhaa za kifedha,na mitaji kwa jamii na watu binafsi wa Dodoma. "
Benkiya Exim  imeongezeka kwa ujasiri ilikukuza msingi wa mali na kufanikiwa kutanua uwezo  kwa wateja Shughuli za Benki zinapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Iringa, Mbeya na Mtwara ndani ya Tanzania na kampuni tanzu nje ya nchi katika Visiwa vya Anjouan, MohelinaMoroni vya Union of Comoros ,kwenye Jamhuri ya Djibouti na Uganda – uwepo wa benki ya Exim.

WANAFUNZI WAASWA KUNAWA MIKONO WATOKAPO MSALANI.

$
0
0
 Wanafunzi wa shule ya msingi Mkwawa na Mabibo wakiwa katika maadhimisho ya unawaji mikono ambayo hufanyika Oktoba 13 kila mwaka.

SHULE mbili za manispaa ya Kinondoni zaadhimisha siku ya unawaji mikono ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba 13 ikiwa na kaulimbiu ya mikono safi kwa manufaa ya sasa na ya baadae.

 Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta amesema kuwa kila mtoto anatakiwa kunawa mikono kabla na baada ya kula pamoja na watokapo masalani ili kuepukana na maradhi ya kipindupindi na maradhi yaletwayo kwa kula uchafu.

Amesema kuwa siku hii ni muhimu hasa kwa watoto wanaokurupuka kumegeana vyakula au vitafunwa wawapo shuleni bila ya kunawa mikono yao na bila ya kujua ni nini madhara ya kula bila kunawa.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya kunawa mikono iliyofanyika katika shule ya Msingi Mabibo na shule ya Msingi Mkwawa jijini Dar es Salaam leo.
Pia amewaasa wanafunzi wa shule za msingi Kigogo pamoja na Mkwawa kunawa mikono mikono kila wanapotaka kula na baada ya kula pia marabaada ya kutoka maeneo ambayo wanashika uchafu.
 Wanafunzi wa shule ya Msingi Kigogo na shule ya msingi Mkwawa wakiwa katika siku ya kunawa mikono iliyoadhimishwa shuleni hapo kwaajili kuelewa manufaa ya kunawa mikono kabla ya kula, baada baada ya   kula,  na baada ya kutoka msalani kwaajili ya kujikinga na maradhi yanayoletwa na kuto kunawa mikono.
 Wanafunzi wa chuo kikuu cha Muhimbili wanaosoma maswala ya mazingira na afya wakiwasomea watoto jinsi ya kujilinda na maradhi yatokanayo na kuto kunawa mikono.
 Mwanafunz wa chuo Kikuu cha Muhimbili Kerobe  TEHSA akiwafundisha watoto jinsi ya kunawa mikono kwa kutumia kibuyu chirizi ambacho ni rahisi zaidi kuliko kuchota maji kwa kutumia kikombe ambayo ni kwaajili ya kunawa mikono kabla na baada ya kula na wakati watokapo msalani hii ikiwa ni siku ya unawaji Mikono iliyoambatana na kauli mbiu ya Mikono safi kwa manufaa ya sasa na yabaadae.

 Afisa elimu Sayansikimu manispaa ya Kinondoni, Martha Kussaga akizungumza wakati wa kuadhinishi siku ya unawaji mikono iliyofanyika katika shule ya msingi Mkwawa na Kigogo jijini Dar es Salaam leo.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akiwazawadia walimu wakuu wa shule za msingi Mkwawa na Mabibo sabuni kwaajili ya waafunzi kuzitumia kunawa mikono wawapo shuleni kila watokapo chooni hii ni kwaajili ya kuadhimisha siku ya unawaji wa mikono ambayo hufanyika kila Oktoba 13 kila mwaka duniani kote.
Afisa usafi wa Manispaa ya Kinondoni, John Kijumbe akizungumza na wanafunzi pamoja na waalimu katika siku ya maadhimishoya Unawaji Mikono ambayo hufanyika kila Oktba 13 kila mwaka.

HILI HAPA SULUHISHO KWA MADAKTARI WANAO UMIA KAZINI.

$
0
0
Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subby.
Madaktari pamoja na Waganga nchini wametakiwa kutumia weledi wa taaluma yao katika kuhudumia wagonjwa hususani wafanyakazi wanaoumia kazini kwa kuhakikisha wanapata huduma kwa wakati.

Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subby ameyasema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa madaktari na waganga kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi nchini WCF na kufanyika katika ukumbi wa BOT Jijini Mwanza.

Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Madaktari pamoja na Waganga ili kutambua namna bora ya kufanya tathimini kwa mfanyakazi aliyeumia akiwa kazini.

Dkt.Abisalam Omary ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za tiba na tathimini WCF, amesema mfuko huo unawajengea uwezo madaktari hao ili kufanya tathmini sahihi kwa wagonjwa wanaoumia kazini ama wasaidizi wao.
Rehema Kabongo ni Meneja wa Mafao ya Fidia Mfuko wa Fidia Kwa wafanyakazi (WCF) anasema kuwa "Tangu mpango huo ulipoanza mwaka 2015 kila uchwao maajiri wamekuwa wakifumbuka macho na kuona haja ya kujiunga na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kiasi kwamba wengi kwa makundi wameanza kujiunga na mfuko"

"Bado tunapata changamoto katika kutoa elimu kwa sababu mfuko huu bado ni mpya lakini tumejipanga kuhakikisha tunawafikia mmoja mmoja au kwa makundi ili kufikia malengo tuliyojiwekea yenye tija kwa matabibu wetu"
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba WCF, Dr. Abdullssalaam Omary akitoa maelezo kwa ufupi jinsi mfuko huo ulivyonuia kuleta mabadiliko kwa watumishi sekta ya afya.
“Tunataka hawa  madaktari wawe na ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kufanikisha azma yetu, na tumeamua kuwa mafunzo ya aina hii yatakuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kuwapatia muongozo utakaowasaidia kutekeleza majukumu yao ya kufanya tathmini,” alisema.
Mbali na madaktari na watumishi walio katika sekta ya afya wengi wa wafanyakazi waliopatwa na matatizo hayo kazini wanatoka sekta mbali mbali kama migodi, viwanda na usafirishaji. 

Mfuko huo umeingia mkataba na watoa huduma za afya kwenye hospitali na  vituo vya afya  zaidi ya 6,000 nchi nzima ambapo zitahudumia wafanyakazi hao.
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt.Leonard Subi akifunga mafunzo hayo hii leo.
Sehemu ya wadau washiriki wa mafunzo.
Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subby akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya huduma za tiba Dr. Christopher Juma kutoka Hospitali ya Nyamagana baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subby akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya huduma za tiba Dr. Christina Nyandwi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subby akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya huduma za tiba Dr. Frighton Rwechungura kutoka Hospitali ya Nyakahanga baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subby akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya huduma za tiba Dr. Boniphace P. Mayala kutoka Hospitali ya Rulenge baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Hongera mdau wa afya baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Hongera mdau wa afya baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.

Miili ya Askari JWTZ Kurejeshwa Nchini

Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images