Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 138 | 139 | (Page 140) | 141 | 142 | .... | 1898 | newer

  0 0

   
   Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ali Abdalla Ali (mwenye kofia)akipokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim kwa ajili ya timu ya mpira wa miguu na wa pete za Baraza la wawakilishi. Vodacom imezipatia timu hizo jezi, suti za michezo, viatu na mipira vikiwa na thamani ya Sh 4.5Milioni. Wanaoshuhudia ni Meneja wa timu Nassor Salum Aljazera(kushoto) na Meneja wa Vodacom Zanzibar Mohamed Mansour. 
   Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ali Abdalla Ali (mwenye kofia)akipokea mipira ya soka na pete  kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim kwa ajili ya timu za baraza la wawakilishi. Vodacom imezipatia timu hizo jezi, suti za michezo, viatu na mipira vikiwa na thamani ya Sh 4.5Milioni. 
  Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ali Abdalla Ali (mwenye kofia)akipokea mipira ya soka na pete  kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim kwa ajili ya timu za baraza la wawakilishi. Vodacom imezipatia timu hizo jezi, suti za michezo, viatu na mipira vikiwa na thamani ya Sh 4.5Milioni. 
   .Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na Vodacom kwa timu za Baraza la Wawakalishi iliyofanyika ofisi za Baraza hilo Mjini Zanzibar. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheri na Naibu Spika wa Zanzibar Ali Abdalla Ali.   
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheri akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na Vodacom kwa timu za Baraza la Wawakalishi iliyofanyika ofisi za Baraza hilo Mjini Zanzibar. Wengine pichani ni Naibu Spika wa Zanzibar Ali Abdalla Ali(katikati) na  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. 

  0 0

   Mwandishi wetu, Arusha
   TAMASHA la nane la vyombo vya habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa kufanyika Septemba 8 katika viwanja vya General tyre Arusha na kushirikisha waandishi kutoka jijini Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro na mkoa wa Manyara.
  Tamasha hili, ambalo hufanyika kila mwaka, limedhaminiwa na kampuni ya bia nchini(TBL).
  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA) Mussa Juma, alisema  zaidi ya waandishi wa habari na wadau wa habari 500 wanatarajiwa kushiriki katika Tamasha hilo.
  Juma alisema kwa upande wa michezo timu ambazo zitashiriki ni TASWA FC kutoka jijini Dar es Salaam, TASWA Arusha, Radio Sunrise, Radio 5, Radio Triple A, Arusha One Radio na Chuo cha Uandishi wa habari Arusha ambao ndio mabingwa watetezi.
  Alisema pia kutakuwa na timu ambazo zimealikwa ambazo ni timu ya TBL Arusha ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, timu ya Wazee Klabu,Kitambi Noma, Timu ya Pepsi na timu ya NSSF Arusha.
  Juma alisema katika tamasha hilo, ambalo huandaliwa na TASWA na kampuni ya Ms Unique, kutakuwa na michezo ya soka, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, mpira wa mikono na mbio za magunia.
  Alisema Septemba 7 bonanza hilo, litatanguliwa na semina ya siku moja kwa waandishi wa habari mkoa wa Arusha kuhusiana na sheria za michezo, masuala ya afya na jinsi ya kutumia michezo katika kutangaza utalii.

  Hata hivyo, Juma alisema bado wadhamini wanaombwa kujitokeza kudhamini tamasha hilo.

  0 0

   Meneja wa Benki ya KCB tawi la Arusha,Bi.Juvita Lubuva(kulia)akisalimiana na maofisa wa Kituo cha Afya cha Ngarenaro jijini Arusha,alipofika kukabidhi msaada wa  mashine ya Ultrasound yenye thamani ya Tsh Milioni 14 iliyotolewa na benki hiyo  kwa Kituo cha hicho cha Afya.KCB Arusha Bank Manager, Juvita Lubuva (right) greets officers of Ngarenaro health clinic, in Arusha, when she arrived there do donate an Ultrasound machine worth Ths14 million to the clinic.
   Mwakilishi wa Meya wa jiji la Arusha Bw.Michael Kivuyo(kushoto)akipokea msaada wa  mashine ya Ultrasound yenye thamani ya Tsh Milioni 14  kwa niaba ya Kituo cha Afya cha Ngarenaro,kutoka kwa Meneja wa Benki ya KCB tawi la Arusha,Bi.Juvita Lubuva(kulia),Michael Kivuyo, Arusha a representative of Arusha town Mayor (left) receives an Ultrasound machine worth Ths14 million on behalf of Ngarenaro health clinic, from KCB Arusha Bank Manager, Juvita Lubuva (right)
  . Meneja wa Benki ya KCB tawi la Arusha,Bi.Juvita Lubuva(kulia)akimsikiliza jambo Mwakilishi wa Meya wa jiji la Arusha Bw.Michael Kivuyo(kushoto)pindi alipomkabidhi msaada wa  mashine ya Ultrasound yenye thamani ya Tsh Milioni 14 iliyotolewa na benki hiyo  kwa Kituo cha Afya cha Ngarenaro . KCB Arusha Bank Manager, Juvita Lubuva (right) keenly listens to Michael Kivuyo, Arusha a representative of Arusha town Mayor (left) after handing him over an Ultrasound machine worth Ths14 million on behalf of Ngarenaro health clinic.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mlezi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania, (SHIMUTA) Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Nyaraka za Katiba ya Shirikisho hilo, kutoka kwa Mwenyekiti wake, Khamis Mkanachi, wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salam, leo Agosti 13, 2013 kwa ajili ya mazungumzo. Katikati ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais Mohamed Khamis. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mlezi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania, (SHIMUTA) Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Viongozi wa Shirikisho, wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salam, leo Agosti 13, 2013 kwa ajili ya mazungumzo na kumkabidhi Katiba ya Shirikisho hilo.  
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mlezi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania, (SHIMUTA) Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Shirikisho hilo baada ya maongezi yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Picha na OMR

  0 0


  0 0

   Njia panda kuelekea Kalambo Falls. Maporomoko hayo yanayopatikana Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Kalambo ni pili kwa ukubwa barani afrika yakiwa na urefu wa mita 235.  Maporomoko hayo yapo mpakani na nchi jirani ya Zambia. 
   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akitoa baadhi ya maelekezo kwa wataalam hao wa majenzi kutoka MUST na wale wa ardhi kutoka Halamashauri ya Wilaya ya Kalambo juu ya mpango wa majenzi wa eneo hilo la kitalii hivi karibuni. Mpango huo ni pamoja na kujenga geti la kukusanyia ushuru, eneo la mahoteli, na huduma nyingine muhimu.
   Wataalamu wa majenzi kutoka chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Kutoka kushoto Omary Mwenunge na Mark Nassary wakiwa kazini kupata taswiraya maeneo hayo na kuyafanyia kazi ikiwa ni kuweka michoro ya huduma mbalimbali zitakazokuwa zinapatikana katika eneo hilo la kitalii Mkoani Rukwa.
   Wataalam hao wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya hivi karibuni walipotembelea eneo hilo. Nyuma yao ni Maporomoko ya Mto Kalambo yenye urefu wa mita 235.
   Wataalam hao kutoka MUST wakistaajabu maporomoko ya mto Kalambo. 
  Sehemu ya maangukio ya mto kalambo
  Sehemu ya mapitio ya mto kalambo baada ya kupita kwenye maporomoko. 
  Picha ya maporomoko hayo ikionekana kwa urefu yakiwa na mita 235  (kutoka juu hadi chini).(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa "rukwareview.blogspot.com")

  0 0

  Baadhi ya wafanyabiashara vijana wa Kata ya Doma-Mvomero wakijadili rasimu ya katiba mpya pamoja na wawezeshaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) hivi karibuni. Wanakijiji wa Kijiji cha Kambala Kata ya Hembeti wilayani Mvomero wakijadili rasimu ya katiba mpya pamoja na wawezeshaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). Mmoja wa wawezeshaji jamii wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bw. Zakayo akihamasisha wananchi wa Kata ya Doma-wilayani Mvomero kushiriki katika mchakato wa katiba mpya.

  0 0  0 0

  8E9U39338E9U3935

  Kijana Jimmy Changchuu alieachana na matumizi ya dawa za kulevya akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete picha aliyochora yeye na kijana mwenzake wakati vijana hao walimpomtembelea Rais Ikulu jijini Dar es Salaam leo.Vijana hao wanalelewa katika kituo cha Pilli Missanah Foundation kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  20130812_122751_resized
  Picha juu na chini Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akikabidhi rasmi msaada wa taa hizo kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana Dk.Meshack Shimwela kwenye hafla fupi iliyofanyika hospitalini hapo.
  20130812_122844_resized
  20130812_123726_resized
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh.Jerry Silaa akiongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana Dk.Meshack Shimwela (kulia) kuelekea kukagua chumba cha upasuaji katika hopspitali hiyo.

  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh.Jerry Silaa kupitia wadau wake ametoa msaada wa taa hizo zenye thamani ya shilingi Millioni sita laki saba na tisini elfu 6,790,000/= ambapo msaada huu wa taa umefika kwa wakati muafaka utakaowawezesha madaktari kuwahudumia wagonjwa wengi na kupunguza msongamano mkubwa wa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ambao kwa hakika walilazimika kufanya pasuaji muda wa mchana peke yake hali ambayo ilisababisha msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo.

  Kwa upande wa huduma ya upasuaji hospitali ya Amana inahudumia wagonjwa kati ya 20 mpaka 30 kwa siku kwa kutumia theater mbili ambazo ni main theater na maternity theater zenye vyumba vinne vya upasuaji (theater rooms). Kwa muda mrefu Hospitali hiyo ilikuwa inakabiliwa na tatizo la kuharibika kwa taa ya upasuaji (operating lamp) ambayo imepelekea kutumia vyumba vitatu vilivyopo theater kubwa (Main theater).

  0 0

  Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

  NI ajabu kama kuna Mtanzana mwenye mapenzi mema na Taifa lake, bila kuanagalia anatokea Tanzania Bara au Visiwani, kisha akatembea akicheka kwasababu ya matukio yanayoichafua nchi yake.
  Watu hao ni wale wanaopita kona zote wakifanya fujo au hata kumwagia wageni acid tindikali, wakiwamo mabinti wawili wa nchini Uingereza waliojikuta wakikumbwa na balaa hilo mjini Zanzibar.  Kirstie Trup na rafiki yake Katie Gee walikutana na dhahma hiyo, wakiwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yani Zanzibar, ambapo sasa wamerudishwa nyumbani kwao kwa matibabu.
  Baada ya kutokea kwa kadhia hiyo ambapo ni mwendelezo wa matukio yanayoichafua Tanzania nje ya mipaka yake, kila mtu anasema lake, hasa vyombo vya habari vya Kimataifa vinavyoandika habari zinazoonyesha namna gani watalii hao wametiwa vilema vya maisha.  Wapo wanaondika kwa kupoza, akiwamo mhariri wa masuala ya Utalii wa Gazeti la Mirror, nchini Uingereza aliyeandika kwa kupoza kidogo katika tukio hilo ambalo kila Mtanzania anapaswa kulikemea kwa vitendo.
  “Ninaweza kusema kwamba hakuna sababu ya kutokwenda Zanzibar kwa vile ni mahali salama, panafurahisha na kuna fukwe nzuri na mambo ya kihistoria yenye umaarufu mkubwa,” aliandika Nigel Thompson kwenye gazeti hilo. Hizi ni miongoni mwa kauli mbalimbali zilizotolewa na wadau wa amani, utalii duniani, ikiwa ni saa chache baada ya raia wa Uingereza kumwagiwa tindakali, wakiwa mjini Zanzibar, Agosti 8 mwaka huu.
  Kwa tukio kama hilo, hakika Dunia inatupa jicho lake visiwani Zanzibar, huku hisia za kila aina zikishika kasi katika wakati ambao kila Mtanzania anatamani kuona nchi yake inapiga hatua. Japo uchunguzi haujaweza kuthibitisha chanzo cha tukio hilo, zaidi ya wale wanaodhamiwa, akiwamo Sheikh Ponda Issa Ponda, aliyetajwa hadharani katika vyombo vya habari vya Kimataifa kuwa anajua kilichotokea juu ya tukio la kumwagiwa tindikali kwa mabinti wa Uingereza.
  Hilo halijabainika, japo najua kuwa kitendo kama hicho ni kuichafua nchi katika ramani za Kimataifa, ukizingatia kuwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, hakuna anayepaswa kuchekea hilo.
  Endapo nchi itatumbukia katika hatari hiyo ya kumwagia watalii tindikali, sekta ya utalii inaweza kushuka kwa kiasi kikubwa mno, hivyo kuufanya umasikini uote mizizi kwa Watanzania wote. Watalii zaidi ya 17,000 kwa mwaka wanaotembelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watasusa, wakihofia usalama wao ambao kwa siku za hivi karibuni habari mbaya zinaripotiwa kutokea.
  Vyama vyote vya siasa sambamba na wadau wa utalii wanapaswa kuwa makini katika suala hili, ukizingatia kuwa ndio kinachoweza kukuza uchumi wan chi endapo suala la utalii litapiga hatua. Chama Cha Wananchi (CUF), Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama Cha Mapinduzi (CCM) TLP, UDP na vinginevyo vinatakiwa kuizungumza hoja hii bila woga kwa wanachama wao.
  Dk Ali Mohamed Shein kama Rais wa Zanzibar kwa kushirikiana na serikali yake ya Umoja wa Kitaifa (SUK) sambamba na CUF, huku Maalim Seif Sharrif Hamad ambaye ndio Makamu wa Kwanza wa Rais, wanapaswa kuwa wamoja kujadili tukio hili na mengineyo yasiyokuwa na tija kwa Watanzania.
  Hatuhitaji matukio hayo yawe sehemu ya kawaida kwa Tanzania, bila kusahau Zanzibar inayotegemea utalii ili kukuza uchumi wao. Vikundi vya kidini vinavyoibuka vinaishia kuivua nguo Zanzibar inayopendeza na kuvutia watu kuingia humo kujionea mambo ya kale na madhari inayovutia kuitazama kila wakati.
  Uamsho wanaotajwa kila pembe ya nchi yetu nao wanapaswa kufahamu kelele zote zinazotokea sasa, ni kwa sababu ya amani iliyopo na uchumi unaokuzwa na sekta ya utalii. Lazima wajuwe kuwa wakitumia vibaya nafasi zao, kuheshimiwa kwao mbele ya jamii wataiweka Zanzibar katika wakati mgumu mno. Vizazi vijavyo havitaweza kuishi kwa amani na utulivu. Watoto wao watakufa njaa na kushindwa kuongoza, maana sekta ya utalii inayotegemewa itakuwa imeanguka.
  Nani asiyejua kuwa Tanzania imekuwa ikitegema misaada ya wahisani kutoka nchi mbalimbali duniani. Wahisani ambao wanapojaribu kuja, wanahofia usalama wao, hivyo hili haliwezi kuchekewa. Sekta ya utalii ni muhimu na imekuwa ikitegemewa na Mataifa mengi duniani, ili kukuza uchumi wao, ingawa Watanzania wao hawaoni thamani hiyo na kujikuta wakiwakimbiza watalii.
  Kuwamwagia tindikali wageni wetu ni kurahisisha umasikini wetu. Hatuna tunachoweza kuambulia katika suala hilo. Nini faida ya vitendo hivi? Nani amekusudia kuliangamiza Taifa nje ya mipaka yake. Hakuna dini inayoruhusu machafuko au kuwamwagia binadamu wenzao tindikali kwa faida wanayojua wenyewe. Kama hivyo ndivyo, hatuwezi kubaki kimya wakati nchi yetu inaangamia.
  Haya ni mambo yanayotakiwa kupigwa vita na Watanzania wote, ndio maana hata Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi ambaye pia ni kiongozi kutoka CUF, Ismail Jussa, hajabaki nyuma kukemea suala hilo. Lazima serikali ifanye juhudi katika hili ili vikomeshwe. Kuna hatari ya Tanzania kushindwa kupiga hatua, kama watalii wataona nchi hii sio mahali sahihi kwa kuishi wala kutembelea.
  Doria za polisi ndani ya Mji Mkongwe ambao bado unabakia kuwa ndiyo mji mkuu wa Zanzibar na pia kituo kikuu cha harakati zote za kiuchumi ikiwemo biashara na utalii, ziongezwe ili kupambana na watu wenye mtazamo wao usiokuwa wa Kitaifa zaidi.Wananchi nao waingie kwenye imani ya kulitetea Taifa, huku vitendo visivyokuwa na tija kupingwa, ukiwamo utaratibu wa kuwafichua watu wanaofanya uhalifu wa aina hiyo. Ni kweli Zanzibar inavutia. Inapendeza kutembelewa na kila mmoja wetu, lakini kama hakuna amani hizo ni porojo. 

  Hakuna anayeweza kujitoa mhanga katika hilo, ndio maana kuna haja sasa ya kuliwekea mkazo suala la amani, ushirikiano na kuwakemea wanaofanya vitendo vya uhalifu, hasa kuwamwagia tindikali na mengineyo. Zaidi Watanzania wenyewe tutajaribu kuharibu mfumo mzima wa utalii wetu, bila kujua athari zinazoweza kulitia Taifa katika umasikini wa milele. Naungana na Jussa aliposhauri kamera za mitaani za kufuatilia nyenendo za watu (Surveillance Cameras).

  Mpango huu pia utaleta amani na kuondoa hofu watalii wanaoamua kuitembelea Tanzania ili wajionee vivutio vya utalii vilivyozagaa kila pembe ya nchi yetu. Kuiweka Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika hali ya amani na utulivu ni jukumu letu sote, maana jambo hilo litatuweka katika mazingira mazuri kwenye sekta ya utalii duniani.

  Wapo wanaotaka Zanzibar liwe Taifa la Kiislamu. Hao wanafika mbali kwa kuingiza chokochoko za kila aina, ukiwamo mgogoro wa Muungano unaoleta vuta nikuvute kwa Watanzania wote. Kama kuna anayetaka kuleta chokochoko kwasababu za Muungano, basi ni bora akatumia njia nzuri ya maelewano, mazungumzo huku akichambua kwa hoja namna gani nchi ifuate anachotaka.

  Lakini kuonyesha hasira zake kwa kutoa uhai wa mwingine au kumpa kilema cha maisha, ni jambo lisilovumilika hata kidogo. Tuyaseme haya bila woga kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. Tanzania ni nchi yote. Tukiichafua kwa namna yoyote ile, hasara yake ni kubwa mno, hivyo lazima tuwe makini katika suala hili. Huu ndio ukweli wa mambo. Tuujuwe na kuuzingatia pia.

  0 0

  Mkurugkenzi wa Swahili Radio Bwana Dickson Mkama (DMK) akiwa hewani wakati  wa majaribio.
  Mkurugenzi wa Swahili Radio Bwana Alex Kassuwi (King) akiwa hewani akifanya majaribio.

   Wakurugenzi wa Swahili Radio Bwana Alex na DMK wakiendesha kipindi cha majaribio hewani

  SWAHILI RADIO.'
  Ni Radio iliyoanzishwa Jijini Washington DC USA na Kampuni ya "MMK MEDIA GROUP LLC " ambao wanamiliki Swahili Radio On Line,Swahili TV on Line,Swahilitv Blog, Swahili Magazine USA-AFRICA,na The Bridge Show ndani ya DCTV.

  Radio hii pamoja na TV ziko kwenye majaribio kwa sasa na zitaanza kuwa hewani kwa watu wote kusikiliza na kuangalia punde muda wa majaribio utakapo malizika.Watanzania hao watatu wote kwa pamoja wanayofuraha kubwa kwa jinsi ambavyo majaribio ya kazi hizi yanavyoendelea na kwa kingereza wanasema THEY CAN'T WAIT TO BRING TO YOU WHAT YOU HAVE BEEN WAITING FOR.

  "PROGRAMS ZA RADIO KWA KUANZIA"

  *KIPINDI CHA BURUDANI NA MICHEZO DUNIANI*
  *MAPENZI NA MAISHA*
  *MAISHA UGHAIBUNI*
  *HABARI ZA DUNIA*
  *THE WEEKEND SPECIAL*

  KWA HABARI ZAIDI TEMBELEA SWAHILITV.BLOGSPOT.COM

  0 0

   


  0 0

  Waziri wa habari,Vijana,utamaduni na michezo Dr Fenella Mukangara akitangaza majina ya wanakamati aliowateuwa kuratibu mbio za uhuru mwaka huu nchini,Dkt Mukangara amewataja wajumbe hao kuwa ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq  (Mwenyekiti) na  Wajumbe wengine katika kamati hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, Naibu Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda na Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa. Wengine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Intellectuals, Innocent Melleck, Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), Gabriel Nderumaki, George Kavishe kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mhariri Mtendaji wa Uhuru, Jossiah Mfungo na Habib Gunze wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
   Mratibu wa mbio za uhuru nchini Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari juu ya mipango mbalimbali ya mbio za uhuru nchini ,Kulia ni Waziri wa habari,Vijana,utamaduni na michezo Dr Fenella Mukangara ambapo waziri amewateuwa wajumbe kumi watakaoratibu mbio hizo mwaka huu.
  Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali nchini wakiwa katika chumba cha mikutano cha wizara ya habari tayari kumsikiliza Mheshimiwa waziri atangaze kamati hiyo.
  ==========   ========   =========
  Waziri Dr Fenella Mukangara atangaza wajumbe wa Uhuru Marathon

  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mukangara jana alitangaza wajumbe watakaosimamia mbio za Uhuru Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8, mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Dk. Fenella alisema wajumbe wa kamati hiyo itakayokuwa na watu 10 itakuwa na jukumu la kuhakikisha mbio hizo zinafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
  Kamati hiyo inatarajiwa kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq huku ikiwa na wajumbe wengine kutoka katika sekta mbalimbali nchini.

  Wajumbe wengine katika kamati hiyo iliyoundwa na waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, Naibu Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda na Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa.

  Wengine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Intellectuals, Innocent Melleck, Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), Gabriel Nderumaki, George Kavishe kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mhariri Mtendaji wa Uhuru, Jossiah Mfungo na Habib Gunze WA Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

  Waziri Fenella alisema mbio hizo zitakuwa zimegawanyika katika sehemu nne kukiwa na mbio ndefu za kilomita 42, mbio za kati kilomita 21, mbio za kujifurahisha kilomita 5 na mbio fupi ambazo ni maalumu kwa viongozi zikiwa za kilomita 3.

  “Mbio hizi zina lengo kuu la kuimarisha umoja, upendo, mshikamano na amani kwa Taifa letu. Tunategemea Watanzania wengi, ikiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, wanafunzi wa ngazi mbalimbalio na wananchi kwa ujumla wataungana na kushiriki mbio hizi,” alisema.
  Naye Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema wazo kubwa la kuanzisha mbio hizo ilikuwa ni kutaka kuwakumbusha Watanzania kuuenzi umoja, amani, mshikamano ulipo pamoja na uhuru wetu.

  Mratibu huyo alisema, mpaka sasa wanariadha zaidi ya 300 kutoka nje ya Tanzania wameomba kushiriki mbio hizo za aina yake hapa nchini.
  “Sisi kama vijana tukaona kuna haja ya kufanya kitu cha kuwakumbusha Watanzania wenzetu kwani tunatakiwa kudumisha urithi wa amani, mshikamano na uhuru wetu tulioachiwa na mababu zetu,” alisema.

  Melleck alisema mbali na mbio hizo kufanyika siku hiyo, pia kutakuwa na tamasha kubwa la burudani litakalofanyika katika Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaam ikiwa ni mkesha wa kusubiri siku ya Uhuru.

  Mbali na hayo Waziri Fenella naye alizitaka taasisi mbalimbali kuhakikisha wanazidhamini mbio hizo kwani zina manufaa kiubwa kwa taifa.

  0 0
 • 08/14/13--03:08: TAARIFA KWA UMMA.
 • Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera jana tarehe 13/08/2013 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika mjini Bukoba imetangaza uamuzi wake wa kuwafutia dhamana ya CCM hivyo kuwavua Udiwani Madiwani wanane wa Manispaa ya Bukoba waliotokana na CCM.

  Kwa mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya dola hasa Wabunge na Madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Mkoa sio wa mwisho.  Uamuzi huo unapaswa kupata Baraka za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe.


  Hivyo basi, mpaka sasa Madiwani hao wanane waliosimamishwa wanapaswa kuendelea na kazi zao kama kawaida wakisubiri kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti, 2013 mjini Dodomaambacho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera.


  Pamoja na hilo, tumepokea barua za Madiwani hao za kukata rufaa kupinga uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa kwa msingi wa madai ya kukiukwa kwa utaratibu katika kufikia uamuzi huo.


  Tunawasihi wananchi wa Bukoba na Kata husika, wanachama na viongozi wote kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo suala hili linashughulikiwa na vikao vya Kitaifa.


  Imetolewa na:-


   Nape M. Nnauye,
  KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA

  ITIKADI NA UENEZI


  14/08/2013


  0 0

  Creditinfo is proud to present its first official Global Forum, to be hosted in the beautiful city of Prague. 
  The Conference will bring together a number of influential specialists, practitioners and providers within the Credit Industry. It will present an excellent opportunity for these experts to share ideas about the challenges and best practice worldwide. ¨


  Amongst the speakers are representatives from Paypal, Societe Generale Group, International Finance Corporation (IFC), Bank of Georgia as well as Credit Bureaus in 4 continents.


  Creditinfo greatly appreciates the contributions of its speakers who will be delivering informative and comprehensive presentations focussing on the following key areas:


  1.    The major challenges when setting up a Credit Bureau

  2.    Innovative data sources to enhance traditional credit bureau data

  3.    How to overcome concerns with data acquisition

  4.    How to ensure data quality in an imperfect world

  5.    The use of credit reports when making a credit decision

  6.    Development of Data Roadmap with Lenders working together with Credit Bureaus

  7.    In an on-line world how best to use data for identification and fraud prevention

  8.    Implementing credit bureau scorecards

  9.    The usage of Credit Bureau data to better manage your portfolio

  10.  Using blended data and scorecards to make better SMEs decision

  11.  Support strategic direction by Benchmarking your portfolio against the market

  12.  Psychographic profiling, does it have a role in credit granting?


  Reynir Grétarsson, CEO Creditinfo, is a firm believer that “Information is the lifeblood of the modern economy.” He advises that “Creditinfo will always be an innovator taking the initiative in the development of new services and processes in the Credit Bureau industry. We continue to strive to enrich business performances and consumers lives by converting data to intelligent decisions. 

  Through our partnership programmes and Global Forums, we are able to develop & improve on financial infrastructures for the benefit of the overall economy, whilst facilitating access to (affordable) credit, increasing financial inclusion and lowering interest rates.

  Creditinfo’s strategy continues to be direct, fast and flexible thanks to a growing, experienced and professional worldwide team who are continually creating & developing credit risk and information solutions to meet current market demands.

  For more information and registration:  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Adam H. Mayingu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

  Taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam jana, Jumanne, Agosti 13, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi unaanzia Juni 8, mwaka huu, 2013.

  Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mayingu alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wa PSPF.

  Bwana Mayingu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bibi Hawa Mmanga ambaye amestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu.
  Dar es Salaam.

  14 Agosti, 2013

  0 0

   Askari Bandia wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliyekamatwa leo mchana maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya sare zake mara baara ya kukamatwa. Askari huyu feki amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa juu yake.
  Afande huyo akiwa chini ya ulinzi wa Polisi mara baada ya kukamatwa mchana wa leo akila vichwa maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam.Askari huyu feki amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa juu yake.
  Afande huyo akiwa Kituo cha Polisi Stakishari.

  0 0
 • 08/14/13--08:43: JK RECEIVES BARCA JERSEY
 •  The Tanzania Breweries Marketing Director, Kushilla Thomas hands over a jersey signed by all FC Barcelona first team players to President Jakaya Kikwete at the State House in Dar es Salaam today in honour of the historic Castle Lager and FC Barcelona partnership signed last month at Camp Nou in Spain. Looking on is the Sales Manager - Southern Zone, James Bokella (1st on the right) and the TBL Marketing Manager, Natalia Celani (2nd right).  On the left is Kabula Nshimo, the Castle Lager Brand Manager and Aggrey Marealle, the Managing Director for Executive Solutions who are TBL's public relations consultants.  Below is after the President was presented an FC Barcelona jersey with his name imprinted on it during the short ceremony


older | 1 | .... | 138 | 139 | (Page 140) | 141 | 142 | .... | 1898 | newer