Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1397 | 1398 | (Page 1399) | 1400 | 1401 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Jonas Kamaleki-MAELEZO

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Meneja wa Kampuni ya Accaso International Limited, William Kafipa katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.

  Kafipa amesema mkaa wa mawe wa kupikia unatumika kwa kiasi kidogo na unawaka kwa muda wa saa nne mfululizo hivyo kuwezesha mtumiaji kupika vitu vingi kwa mkaa kidogo ukilinganisha na mkaa unaotokana na miti.

  “Mkaa huu ni bora sana na watu wengi wakiutumia wataachana na kukata miti ovyo hivyo kutunza mazingira na kuepusha nchi kuwa jangwa,”alisema Kafipa.

  Aliongeza kuwa badala ya kutumia gunia moja la mkaa wa kuni ambalo gharama yake ni kati ya shilingi 60,000/= na 85,000/=, unaweza kutumia boksi mbili hadi tatu za mkaa wa mawe kwa matumizi sawa na gunia hilo ambayo jumla yake ni shilingi 36,000/=. Kwa kufanya hivyo mtumiaji ataokoa fedha yake na pia atatunza mazingira kwani hatalazimika kukata miti ili kupata mkaa.

  Kwa upande wake, Afisa Masoko na Mauzo wa Accaso, Monica Cornelius amesema mkaa wa mawe utampunguzia mwanamke adha ya kutembea mwendo mrefu kutafuta kuni endapo atatumia mkaa huo ambao bei yake ni nafuu hata kwa mtu wa kipato cha chini.

  “Mkaa huu hautoi moshi jambo ambalo ni zuri kwa mazingira na kwa kwa afya ya mtumiaji, hii itaepusha pia mauaji ya vikongwe ambao walikuwa na macho mekundu kutokana na kupikia samadi au kuni mbichi,” alisema Monica.Monica ameongeza kuwa akina mama na watu wengine waipokee teknolojia hii mpya ya mkaa wa mawe wa kupikia ili iweze kubadilisha maisha yao.

  Naye Afisa masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Abdullatif Ramadhani amesema mkaa huo wa mawe umeboreshwa na unafaa kwa matumizi ya nyumbani kwa kupikia hata kwenye taasisi kubwa kama shule, vyuo na magereza kwani upo kwa viwango tofauti.

  “Kwa sasa soko letu lipo Dar es Salaam ambapo tumeanzia lakini tunalenga na mikoa ya jirani kama vile Pwani, Morogoro, Tanga na mikoa mingine hadi kuifikia mikoa yote ya Tanzania,”alisema Ramadhani.

  Akizungumzia changamoto kampuni yake inazokumbana nazo, Ramadhani amasema ni watu kutobadilika na kupokea teknolojia mpya. Ameongeza kuwa baadhi wana dhana potofu kuwa mkaa wa mawe unaweza kutoboa sufuria zao, jambo ambalo si kweli kwani mkaa huo umetafitiwa kwa kina, na joto lake ni la wastani ambalo haliwezi kuharibu sufuria au chombo chochote cha kupikia.

  Mkaa huu unaotokana na vumbi la makaa ya mawe unaweza kutumika kwenye majiko ya kawaida ya mkaa na unawaka kwa muda mrefu, pia ni rafiki wa mazingira na hauna madhara kwa binadamu. 

  Hivyo watanzania wengi wautumie ili kuepuka ukataji miti kwa wingi unaoharibu mazingira. Mazingira yakiharibika, ukame unatokea na kusababisha upungufu au ukosefu wa chakula.

  0 0

   Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi  wa baraza hilo  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Mkutano wa kuzindua baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ukiendelea.
  Picha na JKCI
   Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Ulemavu Andrew Mwalwisi wakati wa uzinduzi  wa baraza hilo  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu   Andrew Mwalwisi akizindua baraza la Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya JKCI Prof. William Mahalu na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
   Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu   Andrew Mwalwisi akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa baraza la Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Restituta Rugaganya mara baada ya kuzindua baraza hilo leo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
   Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu   Andrew Mwalwisi akimpongeza  Katibu wa baraza la Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Samweli Rweyemamu mara baada ya kumkabidhi vitendea kazi wakati wa uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   
   Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu   Andrew Mwalwisi akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa baraza la Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rajabu Matiku  mara baada ya kuzindua baraza hilo leo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la Taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa baraza uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu mwenyekiti wa TUGHE Rajabu Hamisi.
   Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Ulemavu Andrew Mwalwisi wakati wa uzinduzi  wa baraza hilo  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Ulemavu Andrew Mwalwisi wakati wa uzinduzi  wa baraza hilo  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.


  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega akizungumza na watendaji  wa Halmashauri pamoja na kamati ya ulinzi na usalama kuhusu kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji ili kupunguza migorogoro ya wakulima na wafugaji mkoani Pwani.
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, filiberto Sanga akizungumza katika mkutano huo amewataka wananchi kutouza ardhi hovyo ili kupunguza migogoro ya ardhi pamoja na kuwa na maeneo ya kilimo. 
  Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akizungumza na viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi alipokutana nao na kufanya mazungumzo kuhusu usawa na wajibu wa kila mtu ili kufikia malengo ya taifa kiujumla mkoani Pwani.
  Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama hicho leo mkoani Pwani.(Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).
   
  Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi, Mh. Abdalah Hamisi Ulega ameitaka Halmashauri ya wilaya Mkuranga kushirikiana na wananchi kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji ili kupunguza migorogoro ya wakulima na wafugaji.

  Akizungumza na watendaji wa Halmashauri pamoja na kamati ya ulinzi na usalama katika ziara yake ya wilayani Mkuranga mkoani Pwani alisema tatizo la wakulima na wafugaji ni changamoto kubwa kwahiyo ni muhimu kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji ili wasizagae hovyo.

  Ametaka maafisa mifugo wasikae maofisini bali waende kutoa huduma vijijini na kuwasiliza wananchi kero zao.Ulega amesema vikundi vya wafugaji wakina mama na vijana vipewe kipaumbele, vitambuliwe na kudhaminiwa kwenye utoaji mikopo kwa ajili ya kuinua kipato na kuongeza pato la taifa na la mtu mmoja mmoja

  "Tunahitajika tutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji, na hii ni changamoto tunayotakiwa kuifanyia kazi hatupaswi kuwaacha wafugaji wakihamahama" amesema Ulega. 

  Aidha alisema kuwa Halmashauri inatakiwa kufanya utafiti na kupima ardhi ambayo watawatengenezea miundombinu bora kwa ajili ya wafugaji. Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mkuranga, Filiberto Sanga alisema kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ardhi, wananchi wanauza ardhi kiholela kiasi kwamba wanakosa maeneo ya kilimo hivyo amewataka wananchi kutouza ardhi hovyo. 

  Sanga alisema kuwa agizo la naibu waziri wamelipokea japokuwa wanauhaba wa ardhi lakini wameanisha baadhi ya maeneo yaliyopo tarafa ya Mkamba ambayo watayafanyia utafiti kwa ajili ya wafugaji.
   

  0 0

  Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika moja ya shule ya msingi akiwa katika ziara ya kutambua changamoto na kuzifanyia kazi ili ziwe na ubora kama shule za watu binafsi na kuongeza ufaulo kwa wanafunzi wanasoma katika shule hizo.
  Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa darasani na wanafunzi wa shule ya msingi Kibwabwa iliyopo kata ya Kitwiru manispaa ya Iringa
  Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa wakati wa ziara ya kuzitambua changamoto za shule za msingi.
   
   
  Na Fredy Mgunda,Iringa.

  Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amefanya ziara kwenye baadhi ya shule za msingi za manispaa ya Iringa kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo na kuanza kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuboresha mazingira ya wanafunzi kusomea.

  Akizungumza mara baada ya kumaliza zira hiyo ya wiki moja Kabati alisema kuwa amefanya ziara katika shule ya msingi Kihesa,Igereke,Mtwira na shule ya Kibwabwa na kubaini changamoto nyingi ambazo anaanza kuzitafutia ufumbuzi hivi karibuni.

  “Nimejionea mwenyewe changamoto zilizopo na naona kama changamoto kwa asilimia kubwa zinafanana hivyo ni kazi yangu kuanza kutafuta njia ya kuanza kuzitatua changamoto hizo”alisema Kabati

  Kabati alisema kuwa atakikisha anazikarabati shule hizo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kama nilivyofanya hapo awali katika shule za msingi za Azimio na Kigonzile ambazo kwa sasa zinaubora kama shule za watu binafsi.“Kwa kweli wadau wamekuwa wakinisaidia kufanikisha swala la kukarabati shule za msingi zilizopo hapa manispaa ya Iringa ili kuhakikisha mazingira ya shule zote yanakuwa bora kama shule za watu binafsi” alisema kabati

  Aidha Kabati aliwataka viongozi wa serikali na viongozi wa kisiasa kuzitembelea shule hizo mara kwa mara ili kutatua matatizo haya mapema kwa sababu shule nyingi ni kongwe ndio maana miundombinu imeharibika kwa kiasi kikubwa.

  “Viongozi wengi tunashinda sana maofisini kuliko kwenda kuyatembelea maeneo yenye changamoto kama hizi za shule za msingi za manispaa ya Iringa kwasababu ukitembelea maeneo yenye changamoto mara kwa mara inakuwa kazi rahisi kuzitafutia ufumbuzi mapema” alisema Kabati

  Kabati alisema kuwa shule nyingi za msingi manispaa ya Iringa zilijengwa miaka 1980 ndio maana saizi miundombinu imeharibika kutokana na kutokarabatiwa mara kwa mara na kusababisha kuendelea kuharibika kwa kuwa hakuna mikakati ya makusudi ya kukarabati shule hizo.

  Kabati aliwaomba wananchi na wadau wa maendeleo kutoa ushirikiano wa kutosha ilikufanikisha azma ya kuzikarabati shule hizo na kuacha kuangalia Itikadi ya vyama vya siasa kwa kuwa maendeleo hayana siasa.Naye mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Kibwabwa Isumael Mlenga alimpongeza mbunge huyo kwa kazi anayoifanya ya kusaidia kukarabati shule za msingi za manispaa ya Iringa ni jukumu kubwa analolifanya kwa wanairinga.

  “Ni wabunge wachache wenye moyo kama wa Ritta Kabati hivyo tunapaswa kuendelea kumuunga mkono kwenye kazi anazozifanya kwa maendeleo ya watoto wetu wanaosoma katika shule hizo zinazokarabatiwa na mbunge huyo” alisema Mlenga

  Karumerita Mbuta,Zubeiry Mlowela na Romana Lutenga ni wajumbe wa kamati ya shule ya Kibwabwa walimpongeza mbunge huyo kwa ziara zake anazozifanya kuzitambua Changamoto zilizopo mashuleni hasa kwenye shule za msingi hivyo tunaomba ziara zako ziwe na matunda kwa kuboresha miundombinu ya shule ulizotembelea.

  Kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi Igeleke Robert Mulilo na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Wakati Maliva walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa jitihada zake za kuendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.
   

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameahidi kuhakikisha kwamba suala la uharamia wa kazi za filamu za Watanzania nchini unakomeshwa mara moja kwa kuwasaka wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya Sheria.

  Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Wamiliki wa Majumba ya Kuonyeshea Sinema ambapo moja ya changamoto kubwa aliyotajiwa na wamiliki hao ni suala la uharamia wa kazi za sanaa jambo ambalo linawakwamisha wamiliki hao kutokana na ukweli kwamba baadhi ya watu wasio waaminifu wamekuwa wakivujisha filamu mpya kwa kuziuza kiholela mitaani na wengine wakihuisha filamu hizo katika mitandao ya kijamii jambo linalosabibisha hasara kubwa kwa wasanii na wamiliki wa majumba ya sinema.

  Mhe. Mwakyembe amesikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu hao wanaojihusisha na uharamia wa kazi za filamu za Watanzania huku akiapa kuwashughulikia popote walipo watu hao ili kuhakikisha kuwa Wasanii wananufaika na kazi zao na pia Wamiliki wa Majengo ya Sinema wananufaika pia kwa kuonyesha kazi za wasanii hao kwa utaratibu ambao hautomuumiza msanii mwenye kazi yake.

  “Najua baadhi ya Wamiliki wa Majumba ya Sinema mnapata hasara, na hata baadhi ya Wasanii pia, suala hili linanikera sana na kamwe haikubaliki hata kidogo, tutahakikisha kwamba watu wa namna hii wanatoweka katika tasnia yetu, tutawasaka popote walipo na kuwapeleka kwenye vyombo vya Sheria kwani Serikali hii sio ye mchezo na watu wa namna hii”, alisema Dkt. Mwakyembe.

  Ameongeza kuwa, yeye kama Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo atahakikisha kwamba hamasa ya kutosha inatolewa kwa Watanzania ili wawe na utamaduni wa kuangalia sinema zinazotengenezwa nchini katika Majumba ya Sinema yaliyopo nchini.

  Aidha, Dkt. Mwakyembe amewapongeza Wasanii nchini kwa kutoa kazi nyingi huku akiwataka kuhakikisha kwamba ubora unazingatiwa na maadili yanazingatiwa kwa ajili ya jamii na pia amewashauri Wamiliki wa Majumba hayo kutenga siku maalum ambayo itakuwa ikitumika kuonyesha Sinema za Kiswahili zenye maadili na kuzitaka sinema hizo kupewa muda wa kutangazwa katika vyombo vya habari nchini ili wananchi wengi wapate kuzijua na kuweza kutembelea majumba hayo kwa ajili ya kuzitazama.

  “Mi nadhani na sisi Tanzania tukianzisha utamaduni wa kwamba siku Fulani ni siku ya kuonyesha Sinema za Kiswahili tu, hii itaweka historia nchini lakini iwe picha nzuri tu na tuzitangaze filamu hizo na sisi kama Wizara tuna haja ya kuongea na baadhi ya vituo vya televisheni, magazeti pamoja na redio kuzitangaza filamu hizo kwani hii itasaidia kuinua soko la filamu nchini. Bodi ya Filamu Tanzania hakikisheni kwamba pindi itakapoamuliwa kuwa siku fulani ni siku ya kuonyesha filamu za Kiswahili basi muone haja ya kuzipunguzia tozo baadhi ya filamu hizo zitakazokuwa zikionyeshwa lakini tu mpaka hapo itakapoamuriwa”, alisema Dkt. Mwakyembe.

  Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza amewapongeza Wasanii wa Tanzania kwa kujitoa kwao katika kuonyesha vipaji vyao katika kuhakikisha kwamba vipaji hivyo vinaitangaza Tanzania Kimataifa.

  “Nafurahi kuona kuwa Filamu za Watanzania zinafanya vizuri na Tanzania tuna Waigizaji wanaofanya vizuri kwahiyo naamini kwamba mkiitumia vizuri hiyo fursa ya uigizaji mtakuwa mnaitendea haki nchini yetu na kuinua vipaji vyenu lakini pia mtakuwa mmeitangaza Tanzania Kimataifa”, alisema Mhe. Shonza.

  Mhe. Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na Naibu wake Mhe. Juliana Shonza kwa pamoja wamekuwa wakikutana na wadau mbalimbali wa kisekta ikiwa ni sehemu ya utaratibu waliojiwekea lengo likiwa kutambua changamoto zao na namna ya kuzitatua kwa manufaa ya Taifa.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza (katikati) wakiwa katika moja ya Jumba la Kuonyeshea Sinema lililopo Jijini Dar es Salaam wakati walipokutana na Wamiliki wa majengo hayo na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na uonyeshaji wake 11 Oktoba, 2017. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa wa Wizara hiyo, Bibi Leah Kihimbi.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza (katikati) wakiwa katika moja ya Jumba la Kuonyeshea Sinema lililopo Jijini Dar es Salaam wakati walipokutana na Wamiliki wa majengo hayo na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na uonyeshaji wake 11 Oktoba, 2017. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa wa Wizara hiyo, Bibi Leah Kihimbi.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza (kushoto) wakiangalia moja ya kifaa kikubwa kitumikacho kuonyeshea sinema maarufu kama Projekta wakati walipokutana na Wamiliki wa Majumba hayo na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na uonyeshaji wake 11 Oktoba, 2017.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza (kushoto) wakiangalia moja ya kifaa kikubwa kitumikacho kuonyeshea sinema maarufu kama Projekta wakati walipokutana na Wamiliki wa Majumba hayo na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na uonyeshaji wake 11 Oktoba, 2017.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza (katikati) wakiwa wameongozana na baadhi ya Wamiliki wa Majumba ya Kuonyeshea Sinema wakati walipokutana na Wamiliki wa majengo hayo na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na uonyeshaji wake 11 Oktoba, 2017.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

   

  0 0

  Jonas Kamaleki- MAELEZO

  Serikali yawataka watanzania kurejesha nchi katika misingi iliyoachwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kuwa na viongozi waadilifu,wazalendo na wenye uchungu na nchi yao.

  Wito huo umetolewan jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. William Ole Nasha wakati akifungua Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 18 ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


  Ole Nasha amesema kuwa kumekuwa na ombwe kubwa la kuporomoka kwa maadili, kushamiri kwa rushwa, ufisadi, kukosekana kwa uzalendo na uwajibikaji, kuwepo kwa wafanyakazi hewa na biashara ya madawa ya kulevya.

  Ameongeza kuwa wengi waliokuwa wakiharibu nchi hii ni watanzania wenyewe kwa ajili ya tamaa na ubinafsi wao. Nimefarijika sana kusikia kuwa Chuo kimeanza kurejesha hadhi yake iliyokuwepo hapo awali kilipoasisiwa kwa kuanzisha program maalum ya Uongozi, Maadili na Utawala Bora,”alisema Ole Nasha.

  Akizungumzia Mada Kuu ya Kongamano ambayo ni Mtazamo wa Mwalimu Nyerere katika Uchumi wa Viwanda na Maendeleo ya Jamii, Naibu Waziri amesema kuwa ni ukweli usiopingika katika uchumi wa maendeleo ya viwanda, Uzalendo, Utaifa, Uadilifu na Uongozi Bora vinapaswa kuzingatiwa. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema kuwa viwanda si maendeleo bali ni matokeo ya maendeleo.

  Amesema nchi inawezakuwa na viwanda lakini vinamilikiwa na wageni huku watanzania wakiwa manamba na vibarua. Hivyo amewataka wananchi wenyewe wajitahidi kuanzisha viwanda ambavyo vitatoa ajira kwa vijana wa kitanzania. Butiku amesema kusema nchi imeendelea wakati bado kuna rushwa na kutokuwajibika huko sio kuendelea bado inahitaji kuendelea.

  Akimzungumzia Mwalimu alisema kuwa Nyerere alisema huwezi kujenga viwanda bila kujali misingi. Misingi hiyo Butiku ameitaja kuwa ni kuhtambua kuwa Tanzania ni nchi ya watanzania, usawa wa binadamu msingi ambao Mwalimu alikuwa muumini. Jambo ambalo limejitokeza kwa wingi katika Kongamano hilo ni msisitizo ulikuwa juu uzalendo, utaifa,uadilifu na uwajibikaji.

  Kongamano hilo lilihudhuriwa na wanataaluma, wananchi wa kawaida, wanafunzi, wanavyuo na viongozi wastaafu akiwemo Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda, Ibrahim Kaduma, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Mark Mwandosa na Viongozi wa Vyama vya Siasa akiwemo Prof. Ibrahim Lipumba na John Shibuda.

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi zao ili kuleta mabadiliko makubwa kwa wakulima.

  Akiongea katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea (TFRA) jana na kuwahusisha Watumishi wote wa Taasisi hiyo, Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi hao kuwa na malengo na mpango kazi ambao kila mtu atautekeleza  na atapimwa kutokana na mpango kazi huo.

   Hata hivyo Dkt. Mwanjelwa amewapongeza  kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao kwa sasa, hususan katika zoezi la uagizaji wa mbolea kwa mfumo wa pamoja (Bulk Procurement System) ambao umechangia kwa kiasi kikubwa mbolea hiyo kumfikia mkulima kwa bei nafuu.Pamoja na pongezi hizo Naibu Waziri, Dkt. Mwanjelwa ameitaka  TFRA  kuongeza bidii katika utendaji wao wa kazi na kuhakikisha kuwa wanaondoa kero zinazowakabili Wakulima.

  Aidha ameitaka Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea kuhakikisha kuwa mambo matatu muhimu yanazingatiwa ambayo ni upatikanaji wa mbolea (Availability) ufikishaji wa mbolea karibu zaidi kwa Wakulima (Accessibility) na kwa bei ambayo wakulima wanaweza kumudu kuinunua (Affordability) .“Mhakikishe mbolea inakuwepo nchini kote na wakulima wanapohitaji inapatikana na iwe kwa gharama ambayo Mkulima anaweza akanunua. “Amekaririwa, Naibu Waziri.

  Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa mamlaka hiyo bwana Lazaro Kitandu amemshukuru Naibu waziri kwa kuwatembelea na kuwatia moyo katika utendaji kazi wao na kumhakikishia kwamba TFRA imejipanga vizuri kupambana na changamoto za baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu hasa katika kuzingatia bei elekezi ya mbolea.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza viongozi pamoja na wafanyakazi katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea (TFRA)
   Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akipata maelezo kuhusu sampuli ya mbolea aina ya DAP kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mbolea (TFRA) Bwana Lazaro Kitandu  alipotembelea ofisi hiyo.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Puma Energy Bw Phillipe Corsaletti (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni 25 kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (wa tatu kushoto) ikiwa ni udhamini wa mbio hizo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja na Meneja Masoko wa Kampuni ya Puma Energy Bw Machumani Shebe (wa tatu kulia) na Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Bidan Lugoe (kulia) 
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Puma Energy Bw Machumani Shebe (kushoto) akizungumza kwenye warsha hiyo. 
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (katikati) akizungumza kwenye warsha hiyo. Pamoja na mambo mengine Ngowi alisema uwepo wa kampuni ya Puma katika kufanisha Rock City Marathon utaongeza hadhi na ubora wa mbio hizo ili ziende sambamba na ubora wa huduma na bidhaa zinazoandaliwa na kampuni hiyo.
  Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Bidan Lugoe akizungumza kuhusiana na maandalizi ya mbio hizo ambazo pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, Sh mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu.
   
  KAMPUNI ya mafuta ya Puma Energy leo imekabidhi hundi yenye thamani Tsh milioni 25 kwa waandaaji wa mbio za Rock City Marathon ikiwa ni mwendelezo wa kampuni hiyo kudhamini mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  Akikabidhi hundi hiyo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi, Meneja Mkuu wa  kampuni ya Puma Energy Bw Phillipe Corsaletti alisema udhamini huo unalenga kuunga mkono juhudi za serikali kuhamasisha michezo na utalii wa ndani hapa nchini.

  “Michezo huleta uimara wa afya na uimara huo ndio umetufikisha Puma Energy hapa tulipo kimafanikio. Ni wazi ushiriki wa Puma kwenye mbio hizi utawajaza nishati ya nguvu na ubora washiriki wote’’ alisema.

  Aliahidi kuwa kampuni yake itaendelea kushirikiana na waandaaji wa mbio hizo katika kuboresha zaidi mbio hizo kwa miaka ijayo huku akitoa wito kwa  vijana wengi zaidi kutoka mikoa mbalimbali kujiandaa kwa ajili ya mbio hizo.

  Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo, Ngowi alisema uwepo wa kampuni hiyo katika kufanisha Rock City Marathon utaongeza hadhi na ubora wa mbio hizo ili ziende sambamba na ubora wa huduma na bidhaa zinazoandaliwa na kampuni hiyo.

  Naye, Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Bidan Lugoe  alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, Sh mil 2/-  kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu.

  Kwa upande wa mbio za  Kilomita 21, Bidan alisema pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh.  Mil 2/- kila mmoja, sh. Mil 1/-  kwa washindi wa pili na sh. Laki 5/- kwa washindi wa tatu.

  “Zaidi tunatarajia kwamba viongozi wa kiserikali pamoja na wadhamini wetu wakiwemo PUMA, Tiper, Precision Air, RedBull,  Bodi ya Utalii Tanzania(TTB), New Mwanza Hotel, EF Out door, CF Hospital, KK Security, Jambo Food, SDS,  watashiriki kikamilifu katika mbio za KM 5 sambamba na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino,’’ alitaja.

  Akizungumzia usajili wa mbio hizo Bw. Bidan alisema kwa wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa jirani wanaweza kujisajili kwa kuchukua fomu katika Ofisi za michezo wilaya zote za mkoa wa Mwanza, Ofisi za riadha mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga.

  Sehemu nyingine ni pamoja na  Uwanja wa Nyamagana,  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino  Mwanza, Kituo cha michezo  Malya, Shule ya Kimataifa ya Isamilo, New Mwanza  Hotel na Ofisi za EF Out door zilizopo jingo la Rock City Mall.

  “Kwa upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki pia zinapatikana katika ofisi za Kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya sita jengo la SHAMO Tower, Mbezi Beach , jijini Dar es, Salaam na EFM Jogging Club iliyopo Coco Beach  Dar es Salaam” alitaja.

  Zaidi kuhusu usajili wa mbio hizo zinazoandaliwa kwa kushirikiana na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA), Bidan alisema unaweza kufanyika kupitia tovuti ya kampuni hiyo ambayo ni www.capitalplus.co.tz

  Alitoa wito kwa washiriki zaidi kujisajili ili kuthibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo ambazo mbali na kuibua vipaji vya mchezo wa riadha hapa nchini pia zinalenga kutangaza utalii katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ya Ziwa.
   
   

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameitahadharisha Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini kutorudia makosa yaliyokuwa yanafanywa na Halmashauri kabla ya wakala huo kuanzishwa.

  Amesema kuwa matumizi mabaya ya fedha za barabara pamoja na barabara hizo kujengwa chini ya viwango na kuisababishia serikali hasara ya kufanya matengenezo ya mara kwa mara ni miongoni mwa changamoto ambazo serikali imeamua kuzitafutia ufumbuzi kwa kuanzisha Wakala huo.

  “Ukiitwa Injinia na kazi yako iendane na cheo chako, sio unafanya kazi mpaka hata sisi ambao hatuna ujuzi huo tukiona tunasema hii ipo chini ya kiwango, na hapo mwanzo serikali ilikuwa inaelekeza pesa nyingi sana kwenye barabara lakini kiuhalisia barabara hazipo na muda mwingine mvua zinataka kuanza ndio utaona mkandarasi anaingia barabarani kwenda kutengeneza barabara,” Mh. Zelote alifafanua.

  Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha kwanza cha bodi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

  Amesisitiza kuwa kwa kuimarisha sekta ya barabara vijijini ndio miongoni mwa hatua za kuuendea uchumi wa Viwanda ambao ndio kipaumbele cha serikali ya wamu ya tano inayoongozwa na Mh. Dk. John Pombe Magufuli.

  Hivyo ametoa wito kwa wakala huo kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa uadilifu na kuhakikisha mabadiliko yanaonekana na kuwaasa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na hatimae kurudisha nyuma azma ya serikali ya awamu ya tano. 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto) wakati akifungua kikao cha bodi ya barabara, (katikati) Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule pamoja na Katibu tawala wa Mkoa wa Rukwa Bernard Makali.

  0 0


  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Wadau wa Usalama Barabarani, kinachojadili mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara, Joyce Momburi na Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Japhet Lusingu.Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Wadau wa Usalama Barabarani, kinachojadili mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara, Joyce Momburi na Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Japhet Lusingu.Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam

  Mdau wa Usalama Barabarani, Henry Bantu, akitoa Historia ya Baraza la Usalama Barabarani wakati Kikao cha Wadau wa Usalama Barabarani, kinachojadili mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani.Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.

  Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Deus Sokoni, akisoma vifungu vya Sheria ya Usalama Barabarani mbele ya wadau mbalimbali wa Usalama Barabarani (hawapo pichani), wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Wadau wa Usalama Barabarani, kinachojadili mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani.

  Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Joyce Momburi na kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Theopista Mallya.Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

  0 0

   Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika ofisi za wilaya za chama hicho zilizopo sabasaba manispaa ya Iringa.


  Na Fredy Mgunda,Iringa.

  Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir amewataka wapinzani kujipanga vilivyo kwa kuwa amechaguliwa kwa lengo la kuhakikisha vijana wengi na wananchi wa manispaa wanakuwa na imani na kukirudisha chama hicho madarakani katika chaguzi zote zitakazo jitokeza hapo baadae.

  Akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Bashir alisema kuwa atahakikisha anakieneza chama vilivyo ili kuongeza wanachama wanaokipenda chama hicho.


  “Mimi mwenezi hivi nilivyo nitakieneza chama kwa nguvu zote kwasababu tunavijana na viongozi wa kuleta mabadiliko ndani ya chama hata mkisema ninyoe nywele nitanyoa(hata wakisema tumooge mafwiri tumoga eeela) kwa lengo la kuhakikisha tujakijenga chama kuwa chama cha wananchi” alisema Bashir


  Bashir aliwataka wanachama kushikana kuahakikisha wanakuwa wamoja ili kuongeza wanacha wengine na kuendelea kuimalisha jumuhiya zote za chama hicho za  manispaa ya Iringa.


  “Bila kuwa na umoja hatuwezi kwenda mbali wala kufikia malengo ambayo tumejiwekea hivyo mmenichagua kuwa mwenezi hivyo nitaifanya kazi yangu kwa moyo wangu wote” alisema Bashir


  Aidha Bashir aliwashukuru wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwa na imani naye na kuhakikisha amekuwa mwenezi hivyo ametoa pongezi kwa wale waote waliomchagua kwa kura nyingi.


  “Mmenifanya niwe na furaha sana maana sio kwa wingi wa zile kura mlizonipa  na kunifanya leo hii nasimama kama mwenezi kwa ajili ya kura zenu sasa subirini kazi yangu ya kukieneza chama na naomba tusahau yote yaliyopita na kuhakikisha tunaijenga CCM mpya hapa manispaa ya Iringa” alisema Bashir


  Naye katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Marko Mbago alimpongeza Edwin Bashir kwa ushindi alioupata na kumuomba kukieneza chama kwa nguvu zote hata kwa kuutumia umaarufu wake kuongeza wanachama ambao watakitumikia chama hiki hapa manispaa.


  “Wewe ni maarufu na unapendwa sana hivyo tunatengemea mengi kutoka kwa kutokana na uzoefu wako wa kuishi vizuri na wananchi wa manispaa ya Iringa na kuijenga CCM mpya hapa manispaa” alisema Mbago


  Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya alisema kuwa sasa ni muda mwafaka wa kuongeza wanachama wapya na kuimarisha jumuhiya zote hapa manispaa ili kuhakikisha wapinzani hawapati nafasi ya kushinda tena.


  “Mimi nakufahamu muda mrefu sasa tumia vijana wako wote ambao umewapa mafanikio kwa muda mrefu kukurudisha fadhila na kukuunga mkono katika harakati zako za kisiasa” alisema Rubeya


  Ritta Kabati ni mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) alimpongeza mwenezi Edwin Bashir kwa ushindi alioupata lakini akawataka viongozi wengine kumuunga mkono na kumpa ushirikiano katika haraka zake za kueneza chama.


  “Kufanya kazi pekee yake hawezi kupata matokeo chanya hivyo ni lazima sisi viongozi na wanachama kumpa ushirikiano wakutosha kuhakikisha mikakati yake inaenda vile chama kinataka na kuahikisha anaijenga CCM mpya hapa manispaa ya Iringa” alisema Kabati


  0 0

  Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.
  UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50) umeileza mahakama kuwa, sehemu kubwa ya upelelezi umekamilika bado maeneo machache.

  Wakili wa Serikali, Wankyo Simon alimeeleza hayo leo mbele ya Hakimu Hakimu Mwandamizi, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kesi hiyo ilipofika kwa ajili ya kutajwa.

  Wakili Wankyo amedai wanakamilisha upelelezi katika sehemu ndogo iliyobakia na  wamewaelekeza polisi kufanya hill na kwamba tarehe ijayo wataieleza mahakama hatua ya upelelezi ilipofikia

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 26, itakapokuja kwa ajili ya kutajwa

  Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa  kusababisha hasara ya dola za Kimarekani 1,118,291.43 sawa na Sh 2,486,397,982.54.

  Kalugendo ambaye ni Mkazi wa Kinyerezi na Rweyemamu Mkazi wa Mwananyamala wote ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na  Madini.

  Wanadaiwa kati ya Agosti 25 na ,31, mwaka huu, katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, washtakiwa kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini walioajiliwa na Wizara ya Nishati na Madini walisababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha.
  Watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50) wakitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kusomewa Mashataka yanayowakabiri  jijini Dar es Salaam leo.
   Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 26, itakapokuja kwa ajili ya kutajwa
  Washtakiwa wa kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini  na mthamini wa madini ya almasi, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50)  wakiingia katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu kwaajili ya kusomewa mashtaka yanayo wakabali jijini Dar es Salaam leo.
   Na upande wa mashtaka umeileza mahakama kuwa, sehemu kubwa ya upelelezi umekamilika bado maeneo machache.

  0 0

   Mkurugenzi wa Shule Direct Faraja Nyarandu akizungumza na washiriki wa mkutano maalum  wa siku ya Mtoto wa Kike Duniani ulioandaliwa na Tasisi ya HDIF kwa wanufaika wake wanaopigania maendeleo ya mtoto wa kike nchini,uliofanyika jana jijini Dar.
   Mkurugenzi wa Shule Direct Faraja Nyarandu akizungumza na washiriki wa mkutano maalum  wa siku ya Mtoto wa Kike Duniani ulioandaliwa na Tasisi ya HDIF kwa wanufaika wake wanaopigania maendeleo ya mtoto wa kike nchini
   Meneja Mipango na Mahusiano kutoka HDIF ,Emma Devies akizungumza na wadau waliofika katika mkutano maalum wa maahdhimsiho ya siku ya mtoto wa kike Duniani,uliofanyika jana jioni jijini dar.
   Wadau walioshiriki katika mkutano huo ulioandaliwa na HDIF  Katika ukumbi wa COSTECH Jijini Dar es Salaam.
   Binti amabye ni mtaalamu wa Panya kutoka Chuo Kikuu cha kilimo cha SUA,Mariam Juma akitoa maelezo jinsi Panya hao wanvyoweza kumgundua mtu mwenye Vimelea vya ugonjw awa Kifua kikuu
   Meneja mrradi wa kupinga ukeketaji afya ya uzazi na Mazingira kutoka Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga kutoka Shirika la Amref Afrika , Dr. Jane Sempeho akiwaonyesha wadau waliofika kutaka kujua juu ya kameoni yake ya Stop Cut
   Wataalamu kutoka HDIF wakifatilia mkutano huo kwa makini.
  wanafunzi wa sekondari walioshiriki katika mkutano huo
  --

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Sweden Nchini, Katarina Rangnitt (kulia) katika kikao chake kilichofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais  jijini Dar es Salaam tarehe 12 Oktoba, 2017. Kikao hicho kilishirikisha pia wataalamu kutoka Idara ya Mazingira. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora.
   Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya kumtembelea hii leo Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mhe. Balozi amezungumzia namna ya kushirikiana katika sekta ya Mazingira.

  Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt na Naibu Balozi wake Bw.  Ulf Kallstig ambae pia ni Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wakiwa Ofisini kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya kufanya mazungumzo hii leo.

  0 0


   Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ukuaji wa Biashara wa Benki ya TPB,  Frank Mushi (Katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya huduma ya Western Union ambayo itawawezesha watumiaji wa huduma hiyo ya kifedha kushinda fedha, simu za kisasa za mkononi na  kompyuta mpakato (laptop). Kushoto ni Kaimu Meneja wa  Huduma za Fedha na Uwakala wa shirika la Posta,  Rehema Mbunda  na kulia ni Kolimba Tawa wa Benki ya TPB ambaye ni Afisa Mkuu wa Uendeshaji
   Wafanyakazi wa TPB Benki na wafanyakazi wengine wa benki hiyo na wadau kutoka Amana Benki, Azania Benki na Shirika la Posta (TPC) wakionyesha baadhi ya zawadi ambazo washindi wa promotion ya Western Union watashinda.
   Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa benki ya TPB, Kolimba Tawa akizungumza katika uzinduzi wa promosheni ya Western Union. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ukuaji wa Biashara wa Benki ya TPB, Frank Mushi (Katikati) na Rehema Mbunda wa Shirika la Posta.
  ‘Warembo’ wa TPB Benki wakiwa katika pozi mara baada ya kufanikisha uzinduzi wa promosheni maalum ya Western Union ambayo itawazawadia washindi zawadi mbalimbali nono.
   
  Benki ya TPB imezindua rasmi promosheni ya huduma ya Western Union ambayo itawawezesha watumiaji wa huduma hiyo ya kifedha kushinda fedha, simu za kisasa za mkononi na kompyuta mpakato (laptop).

  Akizungumza jijini jana, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ukuaji wa Biashara wa Benki ya TPB, Frank Mushi alisema kuwa wameamua kuanzisha shindano hilo kama kuwazawadia wateja wake katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

  Mushi alisema kuwa washindi wanaweza kupata kiasi cha fedha ambacho kitawawezesha kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka, kulipa kodi ya nyumba na ada za watoto wao kwani watumiaji wawili wa Western Union wanaweza kushinda zawadi hadi kufikia sh Milioni 3.

  Alisema kuwa mbali ya benki yao, promosheni hiyo pia itawashirikisha washirika wao kama Shirika la Posta Tanzania (TPC), Benki ya DCB, Benki ya Azania, Benki ya Wakulima ya Kagera, Benki ya Mwanga, Benki ya Amana, Benki ya Uchumi, Benki ya Maendeleo, Benki ya Njombe, Benki ya Mufindi na Benki ya Kilimanjaro.

  ‘’Promosheni tunayozindua leo ni ya miezi mitatu ambayo itaisha mwezi Januari 2018 na inakusudia kuwashukuru na kujiweka karibu zaidi na wateja wetu ambao wanaitumia huduma hii ya Western Union’’, alisema Frank Mushi.

  ‘’Kushiriki kwenye promosheni hii, wateja wanatakiwa kutuma au kupokea pesa kupitia tawi lolote la Benki ya TPB na washiriki wake, pindi unapotuma au kupokea pesa kuna kuponi utapewa na wafanyakazi wa benki kwenye tawi husika, utajaza na itakupeleka kushiriki kwenye droo hiyo. Droo ya kwanza itafanyika katikati ya mwezi Novemba 2017 ambayo itatoa washindi awwili na kila mmoja atapata laptop, na washingi watano ambao kila mmoja atapata simu za kisasa za mkononi,” alisema Mushi.

  Alisema kuwa droo ya pili itafanyika katikati ya mwezi Desemba 2017 na ya mwisho itafanyika Januari 2018. Alifafanua kuwa utoaji wa zawadi za washindi utafanyika kwenye tawi husika ambako mteja ametuma au kupokea pesa na kujaza kuponi ya kushiriki kwenye promosheni.

  Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Huduma za Fedha na Uwakala wa shirika la Posta, Rehema Mbunda alisema anakaribisha wateja wote watembelee ofisi za Shirika la Posta kwa ajili ya kupata huduma za Western Union ambazo zitawapeleka moja kwa moja kwenye shindano la droo ya Western Union.

  0 0


  Mkuu wa masoko na mahusiano wa Benki ya TIB, Theresia Soka akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa benki ya TIB waliofika katika benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. 
  Amewashukuru  wateja wa benki hiyo kufka katika taw la Samora kwaajili ya kusheherekea pamoja wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kuwaomba kutoa maoni yao ili kwenye mapungufu wajirekebisha.
  BENKI ya biashara  inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania Investment Bank (TIB) inaendelea kutoa huduma mbalimbali za kibenki zenye ubunifu wa hali ya juu ili kufikia dira ya kuwa benki  ambayo ni chaguo la wateja.

  Hayo yamesemwa ka Mkurugenzi mtendaji wa benki ya TIB, Frank Nyabundege wakati akizungumza na wateja wa benki ya TIB waliofika katika tawi la Samora jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa benki hiyo inatoa huduma za TIB mobile, Utoaji wa bure wa dhamana za kibenki, sms alert, Premier banking, uboreshaji wa kazi za ATM, kutua huduma masaa 24 ya katika tawi la bandari, huduma za malipo ya kodo kirahisi pamoja na JIPANGE Plan.

  Amesema kuwa "Huu ni mwaka ni waka wetu wa pili tangia kupata kibali cha kutoa huduma za kibenki na kuendelea kujenga uwezo wa kuwapa wateja huduma za kipekee."

  Amesema kuwa hudum nzuri kwa wateja ndio kipaumbele katika maendeleo ya benki hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya TIB, Frank Mwabundege akihudumia wateja ikiwa ni wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba duniani kote.
  Wafanyakazi wa benki ya TIB wakiwahudumia wateja wa waliofika katika benki hiyo jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba duniani kwote.
  Mteja wa benki ya TIB, Irene Kiwia akizungumza na Michuzi TV jijini Dar es Salaam leo wakati alipofika katika benki ya TIB jijini Dar es Salaam wakati wa kuwashukuru wateja wa benki hiyo.
  Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa benki ya TIB wakiwa katika hafla fupi ya kuwashukuru wateja wao katika wiki ya huduma kwa wateja.
  Mteja wa benki ya TIB, Irene Kiwia  pamoja na wateja wengine wakishirikiana kukata keki kwaajili ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba.
  Mkuu wa masoko na mahusiano wa Benki ya TIB, Theresia Soka akikatakata keki kwaajili ya kulishwa wateja wa benki ya TIB jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Frank Nyabundege akimlisha keki Mteja wa benki ya TIB, Irene Kiwia ikiwa ni kuadhmisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila wiki ya kwanza ya Oktoba kila mwaka.
  Kushoto ni Mfanyakazi mstaafu wa benki ya TIB akilishwa keki jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja.
  Baadhi ya wateja wa benki ya TIB wakilishwa keki jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila wiki ya kwanza ya Oktoba kila mwaka.
  Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya TIB, Adolphina William akimpa zawadi mteja  wa benki ya TIB kutoka jijini Mbeya na mmiliki wa Kampuni ya GDM Ltd, Grivas Mwangoka.
  Mkurugenzi wa biashara wa benki ya TIB, Mwallu Mwachang'a akizungumza na wateja pamoja na kuwashukuru kufuka katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika Kila Oktoba kila mwaka duniani kote.
  Meneja wa tawi la benki ya TIB tawi la Samora, Philipo Pilla akiwashukuru wateja wa wa benki ya TIB na waendelee kufurahia huduma za benki ya TIB.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa kwa furaha na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari wa ziara ya siku tatu visiwani humo ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Magharibi Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama janet Magufulki wakisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama janet Magufulki wakisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama janet Magufulki wakisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama janet Magufulki wakisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere. 

  0 0

  Na.Paschal Dotto-MAELEZO

  Mama Maria Nyerere amewaasa vijana kuzingatia utamaduni na michezo ili kuweka sawa akili yao na kuendelea na ujenzi wa taifa kwani michezo hukutanisha watu wengi na kuwawezesha kubadilishana mawazo yenye kujenga katika maisha.

  Akizungumza leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam, Mama Maria Nyerere alisema kuwa michezo ni hatua muhimu ya ukombozi wa fikra kwa vijana kwani wakizingatia michezo wataweza kufanya kazi na kujipatia mahitaji muhumi kama chakula na kuondokana na dhana ya utegemezi.

  “Vijana wamajikita katika mambo maovu, sasa kitakachoweza kusaidia ni michezo kwani inawachangamsha, kuwakutanisha na kuweza kubadilishana mawazo mazuri na kwa sasa wanaendelea vyema na masuala haya ya michezo ambayo yanadumisha pia utamaduni,” alisema Mama Maria

  Aidha, Mjane wa Hayati Baba wa Taifa alisema kuwa kwa sasa vijana wameanza kujirudi katika kudumisha utamaduni kwani walitaka kupotoka na kuacha utamaduni wao, alieleza kuwa watoto wanazaliwa bila ukomavu wa akili katika utamaduni, lakini pia hawapati elimu ya kutosha kutoka kwa wazazi kuhusu utamaduni matokeo yake ni kuishia kuwa na watu wenye tabia za ajabu.

  “Kitakachoweza kuwasaidia vijana wetu ni kuwafundisha utamaduni wetu ili wawe na maadili kwani sasa hivi mtoto anazaliwa hapati elimu ya utamaduni wake, wazazi wametupa utamaduni mbali, ni lazima mtoto atakuwa na tabia za ajabu ajabu,”alisisitiza Mama Maria Nyerere.

  Aliongeza kuwa jukumu la ukombozi wa vijana kutoka katika vitendo vibovu ni la watanzania wote kuweza kuwaelimisha vijana kuhusu michezo ili kuweka akili zao sawa katika kuzalisha na kusaidia kujipatia kipato chao na taifa kwa ujumla.

  Mama Maria Nyerere alisema kuwa kujitegemea kwa vijana hasa katika kufanya kazi kutawawezesha kutimiza ndoto zao na za taifa lenye uchumi wa viwanda kwa ujumla.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO ) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abassi akisikiliza jambo kutoka kwa Mama Maria Nyerere kuelekea kumbukizi ya miaka 18 ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa mahojiano maalum na Mjane huyo nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO ) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abassi akifanya mahojiano na Mama Maria Nyerere kuelekea kumbikizi ya Baba wa Taifa , Mjane huyo aliwasisitiza vijana kuzingatia michezo na utamaduni.Picha na Paschal Dotto- MAELEZO

  0 0

  Madini ya Tanzanite yakipimwa kabla ya kuanza kufanyiwa mnada.
  Vifaa maalum( drum) vilivyohifadhia madini ya Tanzanite.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa , John Nayopa ( aliyesimama)akifatilia zoezi la uthaminishaji, uchambuzi,na ukokotoaji wa mrabaha wa madini yaliyoletwa kwa ajili ya mnada, linalofanywa na watendaji wa Wizara ya Madini.
  Vikosi vya ulinzi na usalama, pamoja na watendaji wa Wizara ya Madini wakihakikisha usalama wa Madini ya Tanzanite yaliyohifadhiwa katika vifaa maalum.
  Usajili wa washiriki wa mnada wa madini ya Tanzanite ukiendelea mkoani Manyara.


  Na Zuena Msuya, Manyara


  Wizara ya Madini kwa mara ya kwanza itafanya mnada wa madini ya Tanzanite kutoka katika Kampuni nne za uchimbaji na biashara ya madini katika eneo la Mirelani wilayani Simanjiro mkoani Manyara,Mnada huo utafayika tarehe 15, Octoba mwaka huu mkoani Manyara.

  Akizungumza mkoani Manyara, Kaimu Kamishna Msaidizi sehemu ya Uchumi na Biashara ya Madini, Godleader Shoo alisema kuwa utaratibu wa kufanya mnada wa Tanzanite ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje nchi na pia kuwasaidia wachimbaji kuuza madini yao kwa bei ya ushindani inayoendana na soko la dunia.

  Shoo alifafanua kuwa mnada huo utashirikisha wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo atakayefanikiwa kununua madini hayo katika mnada huo ni yule tu atakayeshinda bei iliyowekwa kwa ajili ya kununua madini husika.Alitaja kampuni zitakazouza madini katika mnada huo kuwa ni Kampuni ya uchimbaji madini ya TanzaniteOne, Franone, Glitter Germs pamoja na Classic Gems ambazo zitazouza madini ghafi na yale yaliyokatwa.

  Akizungumzia mnada huo, Shoo alisema zoezi hilo linafanyika kwa njia ya uwazi kwa kushirikisha wachimbaji, wanunuzi, Shirika la Madini la Taifa( STAMICO), Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro pamoja na Wizara ya Madini, ili kuhakikisha kuwa wauzaji na wanunuzi wa madini hayo wanapata kile wanachostahili.

  ” Mnada huu utaendeshwa kwa usalama mkubwa kwani Madini ya Tanzanite yana thamani kubwa. Serikali imeimarisha ulinzi wakati wa zoezi hili ili kujihadhari na watu wasio waaminifu,” alisema Shoo.Aidha mnada huo utaiwezesha Serikali kupata mrabaha stahiki na kodi nyingine za serikali kwa uwazi ili kuchangia pato la taifa; vilevile kuimarisha ulinzi na usalama kwa wauzaji , wanunuzi pamoja na mali zao.

  Alisema kuwa minada kama hiyo pia hufanyika kwa nchi za Afrika zenye madini ya Vito kama vile Zambia( emerald), Zimbabwe ( Almasi) pamoja na Afrika kusini ( Almasi).Washindi wa zabuni za ununuzi wa madini ya Tanzanite wanatarajiwa kutangazwa Octoba 15 mwaka huu mkoani Manyara.

older | 1 | .... | 1397 | 1398 | (Page 1399) | 1400 | 1401 | .... | 1898 | newer