Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1396 | 1397 | (Page 1398) | 1399 | 1400 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Muwasilishaji wa mada katika kongamano lililowajumuisha Wasichana wanaosoma kidato cha tano na sita katika shule mbalimbali mkoani Kilimanjaro,Nyamagesa Laban akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika Chuo cha Wanyamapori Mweka. 
  Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kwa karibu ujumbe uliokuwa ukitolewa na Nyamagesa ambaye pia ni mwandishi wa vitabu.
  Baadhi ya wananfunzi walioshiriki kongamano hilo wakiuliza maswali kwa Nyamagesa mara baada ya kumaliza kutoa ujumbe kwa wanafunzi hao.
  Muwasilishaji wa mada katika kongamano la Wasichana wa Shule za Sekondari mkoni Kilimanjaro,Stumai Simba akizungumza katika kongamano hilo.
  Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia Mada zilizokuwa zikitolewa.
  Baadhi ya Wanafunzi wakimuuiza maswali Muwasilishaji wa mada katika ongamano hilo.

   Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
  WASICHANA walioko shuleni  wametakiwa kuacha kuchagua kazi za kufanya pindi wamalizapo masomo na badala yake wafanye maandalizi ya kujiajili kwa kufanya shughuli za ujasiliamali wakati wakiendelea na harakati za kutafuta kazi.
  Mbali na hayo wasichana pia wametakiwa kujenga tabia ya kujiamini na kuacha tabia ya kuwa tegemezi ili kuondokana na mfumo uliopo katika jamii kwa sasa ya kuwa mtoto wa kike ni wa kuwezeshwa na kuhurumiwa.
  Hayo yameelezwa na wawezeshaiji wakati wa kongamano lililofanyika katika Chuo cha Wanyapori (Mweka) na kuandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Africaid kupitia mradi wake wa KISA na kukutanisha zaidi ya wanafunzi 1400 kutoka shule 11 za mkoa wa Kilimanjaro .
  Stumai Simba ni miongoni mwa wasichana walioamua kujiajiri na baadae wanatumika katika kutoa hamasa kwa wasichana hasa wanaojiandaa kuhitimu masomo yao ya ngazi ya sekondari kushiriki kuondoa mfumo dume katika jamii amewataka wasichana kutokata tamaa.
  Msimamizi wa Mradi wa KISA mkoa wa Kilimanjaro ,Devota Mlay amesema lengo la kuwakutanisha wanafunzi wa kike wanaosoma kidato cha tano na sita ni kuwaandaa kwenda kutoa elimu kwa mtoto wa kike katika jamii pindi wamalizapo masomo .

  Kwa upande wa wanafunzi walioshiriki kongamano hilo wameeleza mambo wanayojifunza kupitia makongamano huku wakifurahishwa na namna ambavyo wawasilishaji wa mada walivyofanikiwa bila ya kungojea kupata ajira serikalini.
  Kongamano hilo ambalo limejumisha shule za 11 kutoka wilaya za Mwanga,Rombo,Same,Siha ,Hai  na Moshi mjini linatarajia pia kufanyika katika mkoa wa Arusha na kuhusisha wanafunzi wa kidadto cha tatno na sita katika shule za mkoa wa Arusha.
  Mwisho.

  0 0

   Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akizungumza katika semina ya mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa mtaa, kata na wenyeviti wa mtaa  lengo ni kuwajengea uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali, leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya watendaji wa mtaa, kata na wenyeviti wa mtaa wakimsikiliza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amefungua semina ya mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa mtaa, kata na wenyeviti wa mtaa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali katika maeneo yao kabla hayajafika ngazi za juu.

  Akizungumza mara baada kuzindua mafunzo hayo mstahiki meya Benjamin Sitta amesema kuwa kuna kero nyingi sana katika manispaa ya Kinondoni hivyo kupitia semina hiyo watakumbushwa wajibu wao katika kuwahudumia wananchi na hatimae kero hizi zitaishia ngazi ya chini kwani zipo ndani ya uwezo wao.

  "Tumeshuhudia viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya, mkuu wa mkoa na Rais John Pombe Magufuli wakisimamishwa na wananchi na wakiambiwa kero ambazo zipo chini ya uwezo wa viongozi wa kata jambo ambalo si sahihi" Alisem Meya Sitta.

  Katika hatua nyingine Mstahiki Meya Sitta ameahidi kutowafumbia macho watendaji wazembe kwani wanarudisha nyuma kasi ya maendeleo inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli.

  "Tutawachukulia hatua kali watendaji wazembe ikiwemo kuwasimamisha tumeisha anza na mmoja na wengine watafuata kwani manispaa imelipa fidia ya zaidi ya bilioni 10 kutokana na watendaji wasio tambua majukumu yao, ila wale wenye kufanya vyema tutawapongeza kwa kutambua mchango wao" Alisema Meya Sitta.

  Kwa upande wake Marry Asei Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema mafunzo hayo ni matunda ya ziara ya Dar Mpya chini ya Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Seneta James Inhofe pamoja na Maseneta wa Baraza la Marekani  walipotembelea na kufanya mazungumzo  Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji Charles Mwijage, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamiss Kigwangala, Naibu Waziri wa Mambo ya nje Suzane Kolimba pamoja  Maseneta wa Baraza la Marekani wakiongozwa na Seneta James Inhofe mara baada ya kufanya mazungumzo  Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama kitabu cha Seneta James Inhofe kilichoonyesha picha za maeneo mbalimbali ya Tanzania alipotembelea mwaka mmoja na nusu uliopita, tukio hilo limefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Seneta James Inhofe pamoja na Maseneta wa Baraza la Marekani walipotembelea na kufanya mazungumzo na mhe, Rais Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta  jambo na kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na kiongozi waJumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.

  Picha na Ikulu

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Fabian Daqqaro amewataka wananchi wa wilaya ya Arusha Mjini Kuchangamkia zoezi la Uandikishwaji Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambalo linaendelea katika kata tatu za Wilaya hiyo.
   Akizungumza katika kipindi cha Goodmorning Tanzania kinachorushwa na kituo cha Matangazo cha Redio cha Redio 5 Arusha Daqqaro, amesema kuwa zoezi hili lina manufaa makubwa kwa wananchi na watanzania kwa ujumla lakini pia vitambulisho hivyo vitawawezesha watanzania kutambulika kila mahala, pamoja na raia wa kigeni kufanya shughuli zao bila usumbufu ikiwa ni pamoja serikali kuwa na taarifa sahihi za wananchi.
   Aidha amesema kuwa wananchi wasisubiri mpaka zoezi hilo kufikia tamati ndio kujitokeza Kwa wingi  kwa kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha msongamano na usumbufu mkubwa kwa wananchi.
  “Naomba niwafahamishe na kutoa rai kwa wananchi wangu wajitokeze kwa wingi katika zoezi hili na wasisibirie siku kubaki chache ndio wajitokeze kwa kuwa kunapelekea usumbufu mkubwa sana hivyo,zoezi hili pia litakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi”alisema fabian

   Pia ametaka kila mwananchi kushiriki zoezi hilo na kutolihusisha na masuala ya kisiasa kutokana na umuhimu wake,kwa kuwa lengo ni kutambua na kusajili na kutoa vitambulisho vya taifa.
  Afisa kutoka mamlaka hiyo wilaya ya Arusha Mjini  Juliette Raymond  Amesema lengo la zoezi hilo ni kuwezesha serikali kutambua wananchi wake wapo wapi na wanafanya nini ilimradi  anaishi ndani ya mipaka ya Tanzania ,hivyo zoezi hilo ni  lazima kwa kila mtu kwa Mujibu wa sheria.
  Kwa wilaya ya Arusha Mjini zoezi hilo linaendelea katika kata ya Sombetini,Sekei na Themi ambapo zoezi hilo linafnyika katika Halmashauri ya Jiji la Arusha katika kata ya Sekei,Themi katika viwanja vya nane nane na Sombetini Ofisi za Mtendaji kata eneo la Mbauda Sokoni.

  0 0


   Mkurugenzi wa taasisi ya Binti Foundation Johari Sadiq akizungumza mapema leo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),Katika hafla fupi ya utoaji wa msaada wa vifaa vya shule mbalimbali katika shule ya msingi ya Hananasisifu,jijini Dar,ikiwa ni sehemu yao ya kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike,ambapo Kitaifa inaadhimishwa mkoani Mara,Pichani kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Hananasifu  Idda Uisso.
   Mkurugenzi wa taasisi ya Binti Foundation Johari Sadiq akimkabidhi Mwalimu Mkuu Idda Uisso baadhi ya vifaa vya shule ikiwemo Madaftari,Sale za Shule,Kalamu na vinginevyo kwa ajili ya wanafunzi ambao wanaishi katika mazingira magumu na hawajiwezi.Binti Foundation imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike,ambapo Kitaifa inaadhimishwa mkoani Mara.
   Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Hananasisifu Idda Uisso akitoa neno la shukurani kwa taasisi ya Binti Foundation kwa msaada wao walioutoa kwa shule hiyo,Mwalimu Idda ameziomba taasisi nyingine zenye uwezo kujitokeza kuwasadia watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi wasiojiweza.
  Mkurugenzi wa taasisi ya Binti Foundation Johari Sadiq na baadhi ya wadau wa taasisi hiyo wakishiriki kwa pamoja kugawa vifaa vya shule kwa wanafunzi mbalimbali ambao wanaishi katika mazingira magumu na hawana uwezo.

  0 0


  l-r: Programme Manager, Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship Programme, Mrs Onajite Emerhor-Ogwu; Chief Operating Officer, The Tony Elumelu Foundation(TEF), Mrs Owen Omogiafo; Chief Executive Officer, TEF, Mrs Parminder Vir; Company Secretary, TEF, Mr. Obong Idiong; at the Press Conference announcing the forthcoming 3rd Annual TEF Entrepreneurship Forum, the largest gathering of African Entrepreneurs, to be hosted by the Foundation on 13 & 14 October in Lagos
  3rd Annual TEF Entrepreneurship Forum: l-r: Chief Operating Officer, The Tony Elumelu Foundation(TEF), Mrs Owen Omogiafo; Chief Executive Officer, TEF, Mrs Parminder Vir; and Company Secretary, TEF, Mr. Obong Idiong, at the Press Conference announcing the forthcoming 3rd Annual TEF Entrepreneurship Forum, the largest gathering of African Entrepreneurs, to be hosted by the Foundation on 13 & 14 October in Lagos
  3rd Annual TEF Entrepreneurship Forum: l-r: Chief Operating Officer, The Tony Elumelu Foundation(TEF), Mrs Owen Omogiafo; Chief Executive Officer, TEF, Ms Parminder Vir; and Company Secretary, TEF, Mr. Obong Idiong, at the Press Conference announcing the forthcoming 3rd Annual TEF Entrepreneurship Forum, the largest gathering of African Entrepreneurs, to be hosted by the Foundation on 13 & 14 October in Lagos
  3rd Annual TEF Entrepreneurship Forum 4: l-r: Chief Operating Officer, The Tony Elumelu Foundation(TEF), Mrs Owen Omogiafo; Chief Executive Officer, TEF, Mrs Parminder Vir; Company Secretary, TEF, Mr. Obong Idiong; and Programme Manager, Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship Programme, Onajite Emerhor-Ogwu, at the Press Conference announcing the forthcoming 3rd Annual TEF Entrepreneurship Forum, the largest gathering of African Entrepreneurs, to be hosted by the Foundation on 13 & 14 October in Lagos
  3rd Annual TEF Entrepreneurship Forum: l-r: Chief Operating Officer, The Tony Elumelu Foundation(TEF), Mrs Owen Omogiafo; Chief Executive Officer, TEF, Mrs Parminder Vir; Company Secretary, TEF, Mr. Obong Idiong; Programme Manager, Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship Programme, Onajite Emerhor-Ogwu , at the Press Conference announcing the forthcoming 3rd Annual TEF Entrepreneurship Forum, the largest gathering of African Entrepreneurs, to be hosted by the Foundation on 13 & 14 october in Lagos


  • 3RD ANNUAL TEF ENTERPRENEURSHIP FORUM TO HOLD OCTOBER 13-14 IN LAGOS

  • 1,300 AFRICAN ENTREPRENEURS, BUSINESS LEADERS, POLICYMAKERS FROM 54 COUNTRIES TO ATTEND

  Lagos, Nigeria, 4 October 2017 – The Tony Elumelu Foundation (TEF), Africa’s largest philanthropy focused on supporting entrepreneurship, today announced that the 3rd annual TEF Entrepreneurship Forum – the most inclusive gathering of African SMEs – will take place on October 13-14 in Lagos.

  This is the first year the invitation-only Forum is open to non-TEF entrepreneurs and will allow SMEs from across Africa to attend and form networks, share knowledge, connect with investors, link with corporate supply chains and influence policy makers and business leaders in attendance.

  “Since launching the TEF Entrepreneurship Programme – and committing $100 million to empowering 10,000 African entrepreneurs in a decade – we have unleashed our continent’s most potent development force – its entrepreneurs,” said TEF Founder Tony O. Elumelu, CON. “In just 3 years, our 3,000 entrepreneurs have created tens of thousands of jobs and generated considerable wealth. On October 13 and 14, we invite the global entrepreneurship community to Lagos toward the realization of a New Africa, a thriving, self-reliant continent capable of replicating the results we have seen in our ground-breaking programme.”

  The two-day event features plenary panels, masterclasses, and sector specific networking opportunities as well as policy-led talks focused on improving the enabling environment for African businesses.

  TEF Chief Executive Officer Parminder Vir OBE said: “This is the first year we have opened the Forum up to include not just the 1,000 Tony Elumelu Entrepreneurs from the 2017 cycle of our Programme, but the full pan-African entrepreneurship ecosystem. In doing so, we are allowing disparate SME communities to come together and expand the possibilities for intra-African partnerships. I urge policymakers and investors to join us at the Forum as we empower the next generation of African business titans.”

  Speakers at the event include: Wale Ayeni, International Finance Corporation; Stephen Tio Kauma, Afrexim Bank; Andre Hue, African Development Bank; Stephen M. Haykin, USAID Nigeria; Heikke Reugger, European Investment Bank; Abdoulaye Mar Dieye, United Nations Development Programme.

  The Foundation’s long-term investment in empowering African entrepreneurs is emblematic of Tony Elumelu’s philosophy of Africapitalism, which positions Africa’s private sector, and most importantly its entrepreneurs, as the catalysts for the social and economic development of the continent.

  Forum Documentary: https://www.tonyelumelufoundation.org/tef-forum2017


  @tonyelumelufdn

  0 0


  Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano kizungumza wakati akiwasilisha mada kwenye Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es SalaamNa Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

  WATANZANIA wametakiwa kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli katika adhma yake ya kufanya nchi hii kuwa na uchumi wa viwanda kwa kuendelea kusimamia mawazo wa aliyekuwa Rais wa kwanza nchini Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, William Tata Ole Nasha alipokuwa akifungua kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius .K. Nyerere lilifanyika katika ukumbi wa Utamaduni wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  “Baba wa taifa Julius Kambarage Nyerere anakumbukwa kwa mtazamo wake wa kuanzisha ,kuendeleza na kudumisha viwanda vya ndani ya nchi kukidhi mahitaji ya wananchi pasipo kutegemea Zaidi uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi .uthubutu wa kuanzisha Viwanda vya nguo kama vile Kiwanda cha Urafiki ,Mwatex , Mbeyatex na Mutex ni hatua inayokisi mtazamo wake juu ya Viwanda.” Amesema Ole Nasha.

  Amesema hivyo kwa namna ya pekee nimpongeze Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, anavyosimamia utekelezaji wa mpango huu kwanza kwa kurejesha maadili kwa viongozi na kusimamia matumizi ya rasilimali bora za nchi.

  Kwa upande wake mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ,Prof. Shadrack Mwakalila amesema Baba wa Taifa alisema Julai 29 mwaka 1961 wakati wa ufunguzi wa chuo hicho kuwa alisema kuwa wale wote watakaopata nafasi ya kusoma na kufuzu kivukoni watafanana ma hamira katika mkate. Haiwezekani kutenga hamira katika mkate bali tunajua hamira ipo kwa kutazama jinsi ilivyomua mkate.
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi , William Ole Nasha akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
  Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof Mark Mwandosya akizungumza wakati wa Kongamano la la mahadhimsho ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika katika chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Kongamano la Mahadhimisho ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mama Anna Makinda akizungumza wakati akifungua mdahaloi huo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni , Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa kutoa neno la ukaribisho wa wajumbe waliofika katika kongamano la Maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni.
  Kaimu Balozi wa Jamhuri ya watu wa China nchini akikabidhi zawadi ya Vitabu zinavyomzungumzia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere katika kongamano la Maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni.
  Sehemu ya Wajumbe walio hudhulia Kongamano la kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
  Mkurugenzi wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere , Joseph Butiku akizungumza wakati akiwasilisha mada kwenye Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe walioshiriki kwenye Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndungulile kwenye Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
  Wajumbe walioshiriki kwenye Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe walioshiriki kwenye Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

  0 0   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta  jambo na kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na kiongozi waJumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pome Magufuli na viongozi wengine wa serikali katika picha ya pamoja na kiongozi waJumuiya ya Ismailia duniani H.H. Prince Karim al-Hussayni Aga Khan na ujumbe wake alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 11, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia duniani H.H. Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 11, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia duniani H.H. Prince Karim al-Hussayni Aga Khan wakiongea na wanahabari (hawapo pichani) mgeni huyo alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 11, 2017.


  PICHA NA IKULU


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) alipokuwa akiangalia Friji la mbao na Vifaa mbali mbali mbali vilivyotengenezwa na Jeshi la JKU wakati alipotembelea katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (wa pili kulia) Waziri wa kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe.Hamada Rashid Mohamed.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiangalia Meza za Skuli (Madeski) na Makabati yaliyotenmgenezwa na JKU wakati alipotembelea maonesho mbali mbali katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (kushoto) Waziri wa Nchio Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kher.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiangalia Mashine ya kuchambulia Mahindi ya Taasisi ya Kilimo ya EGYPT ZANZIBAR JOINT FARM wakati alipotembelea maonesho mbali mbali katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko  Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (kushoto) Meneja wa mradi Dr.Reda Abdalla Abdelaziz.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa mradi Dr.Reda Abdalla Abdelaziz,(wa pili kulia) katika Taasisi ya Kilimo ya EGYPT ZANZIBAR JOINT FARM wakati alipotembelea maonesho mbali mbali katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (kushoto).
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiangalia Asali wakati alipotembelea banda la JKU katika maonesho mbali mbali katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (kushoto) .
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Nahodha Khamis Mnungwi (kulia) kuhusu masuala ya Uvuvi mara alipokuwa akiangalia Samaki wakati alipotembelea banda la JKU katika maonesho mbali mbali katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (katikati) Waziri wa kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe.Hamada Rashid Mohamed
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Hoska Gonza Mbilinyi Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Kusimamia Umuhimu wa Bahari Kuu wakati alipotembelea banda la Taasisi hiyo katika maonesho mbali mbali katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (kushoto) Waziri wa kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe.Hamada Rashid Mohamed,

  Picha na Ikulu.

  0 0

  Mwenyekiti wa Umoja wa Vicoba Tanzania (Viguta) Taifa, Dk. Dauda Salmin (kulia) akishikana mikono na Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere mara baada ya kusaini mkataba wa ushirikiano ya kufanyakazi pamoja ambapo UZALENDO KWANZA NA VIGUTA watakuwa bega kwa bega kutoa elimu ya ujasiliamali Tanzania nzima katika hafla iliyofanyika jana Kijiji Cha Kwala - Chalinze. Mwenyekiti wa Umoja wa Vicoba Tanzania (Viguta) Taifa, Dk. Dauda Salmin (kulia) wakisainisha mkataba wa ushirikiano na Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere ili kuendelea kutoa elimu ya ujasiliamali Tanzania nzima katika hafla iliyofanyika jana Kijiji Cha Kwala - Chalinze.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Vicoba Tanzania (Viguta) Taifa, Dk. Dauda Salmin (kulia) akipongezana na Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere mara baada ya kumaliza kusaini makubaliano.
  Salamu za pongezi zikiendelea kutolewa mara baada ya kumaliza zoezi la kusaini mkataba. Mbunge wa viti maalum wa Pwani, Hawa Mchafu Chakoma (CCM) ambaye alikuwa mgeni rasmi akitoa neno kwa wasanii na wananchi walihudhuria hafla hiyo. Mwenyekiti wa Umoja wa Vicoba Tanzania (Viguta) Taifa, Dk. Dauda Salmin akiwatambulisha wanachama
  Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere akitoa neno la shukrani mara baada ya kusaini mkataba wa ushirikino wa kufanya kazi pamoja. Pia aliwashukuru kwa kuweza kuwapatia viwanja kwa ajili ya kujenga nyumba zao za kuishi. Hafla hiyo ilifanyika jana Kijiji Cha Kwala - Chalinze.
  Mbunge wa viti maalum wa Pwani, Hawa Mchafu Chakoma (CCM)
  Wananchama wa Viguta na Uzalendo Kwanza wafuatilia halfa hiyi.
  Wanachama wa Uzalendo Kwanza na Viguta wakielekea eneo la viwanja walivyopewa.
  Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere akikabidhiwa nyumba na Mbunge wa viti maalum wa Pwani, Hawa Mchafu Chakoma (CCM) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa ya ushirikiano na Viguta.
  Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza akionyesha mkataba wa nyumba aliyopewa na Viguta.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Vicoba Tanzania (Viguta) Taifa, Dk. Dauda Salmin akikabidhiwa nyumba na Mbunge wa viti maalum wa Pwani, Hawa Mchafu Chakoma (CCM) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa ya ushirikiano na Viguta.
  Moja ya nyumba aliyopewa mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere na Viguta.
  Burudani ikitolewa.

  0 0
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaban akiongoza Maandamano wakati wa mahafali ya 8 ya  bodi ya Watalaamu wa Ununuzi na Ugazi (PSPTB), Yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaban akizungumza wakati wakati wa mahafali ya 8 ya  Bodi ya Watalaamu wa Ununuzi na Ugazi (PSPTB), Yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi katika Sherehe ya Mahafali ya nane ya bodi  yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
   Wahitimu wa Shahada ya Ununuzi na Ugavi  wakiwa katika Maandamano  wa Mahafali ya nane ya bodi ya watalaamu wa ununuzi na Ugavi

   Makamu Mkuu wa Chuo cha Ushirika  Moshi(MOCU), Neema Kumburu  akipokea cheti cha chuo hicho kuongoza katika utoaji wa masomo hayo mwaka wa pili Mfululizo
   Hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi akitoa nasaha kabla ya kumkaribisha mgeni Ramsi katika Mahafali ya 8 ya chuo hicho
   Wahitimu wa Shahada ya Utaalamu wa Ununuzi na  Ugavi (PSPTB) wakisoma Kiapo Mbele ya Mgeni Rasmiwakati wa mahafali ya 8 ya  bodi ya Watalaamu wa Ununuzi na Ugazi (PSPTB), Yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
   Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi,Ahmed Kilima akitoa hotuba ya Shukrani wakati wa kufunga  mahafali ya 8 ya  bodi ya Watalaamu wa Ununuzi na Ugazi (PSPTB), Yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
   Wahitimu wa Shahada ya Utaalamu wa Ununuzi na  Ugavi (PSPTB),  katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 8 ya bodi

  Wafanyakazi wa bodi ya Ununuzi na ugavi wakiwa katika picha ya pamoja na  mgeni rasmi na meza kuu wakati wa kuhitimisha Mahafali ya 8 ya bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi

  Brass Bendi kutoka Jeshi la Magereza nchini wakitoa Burudani wakati wa Mahafali ya Nane ya Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akiwa na Naibu Mawaziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kakunda (kulia) pamoja na Naibu Waziri Mhe. George Joseph Kakunda mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za OR TAMISEMI mjini Dodoma na kufanya kikao na Watumishi.2Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Joseph kakunda (kushoto) akisaini kitabu mara baada ya kufika Ofisini ‘OfisiyaRais –TAMISEMI’mjini Dodoma
  3Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Josephat Sinkamba Kandege akisaini kitabu mara baada ya kufika Ofisini, ‘Ofisi ya Rais –TAMISEMI, mjini Dodoma.4Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma (hawapopichani) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara hiyo, kulia ni Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kandege pamoja na Naibu Waziri Mhe. George Joseph Kakunda
  5Watumishi wa OR-TAMISEMI wakifuatilia kikao na Waziri pamoja na Naibu Mawaziri (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za TAMISEMI –mjini Dodoma.
  6Katika picha ya pamoja ni viongozi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI (katikati) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Selemani Jafo kushoto akifuatiwa na Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kandege (Afya,Miundombinu,ViwandanaUwekezaji, naSerikalizaMitaa),KatibuMkuu OR-TAMISEMIMhandisiMusa Iyombe, Naibu Katibu Mkuu (Afya) Zainab Chaula na kulia n iNaibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda (Elimu, Maji, Kilimo, MifugonaMaliasili), NaibuKatibuMkuu –ElimuTixonNzunda(Elimu) pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi ya Walimu Tanzania (TSC) Winfrida G.Rutaindurwa.


  NTEGHENJWA HOSSEAH – TAMISEMI, DODOMA

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Said Jaffo amesema hatahamisha Mkuu wa Idara wala Kitengo katika Wizara hii lakini atamtengeneza awe kama anavyotaka ili aweze kuendana na kasi ya utendakaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

  Waziri Jaffo ameyasema hayo wakati wa kikao chake na Watumishi wa Ofisi ya Rais -TAMISEMI mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara hii ambapo aliambatana na Manaibu Waziri wa OR-TAMISEMI .

  Waziri Jaffo alisema kuwa “Siwezi kuhamisha matatizo kutoka eneo kwenda lingine cha msingi ni kuhakikisha tunamtengeneza hapa hapa awe kama tunavyotaka kulingana na mahitaji yetu na aweze kuendana na kasi ya Serikali hii sasa hivi kasi yetu sio ya kutembea bali ni kukimbia na lazima wote twenda pamoja”.

  Aliongeza kuwa nahitaji “Consistency of information” kutoka kwa watalaam wanaofahamu vizuri maeneo yao ya kazi sio kila siku unahamisha unaanza na mtu mpya naye anakuwa hana taarifa za kutosha kuhusu kazi za awali hivyo inachukua muda kuanza kwenda sawa kwangu mimi nasema ntamnyoosha yeyote ambaye haendani na viwango vyangu akiwa hapa hapa na si kwingineko”.

  Aidha Waziri Jaffo aliwata Watumishi wote kuacha kufanya kazi kwa ulegevu na kuwa makini wakati wote wa kazi kwani ndio inayopeleka kupata ujira wako, kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kutoa huduma bora kwa wananchi, kutokujali muda hivyo kutumia muda mrefu kukamilisha jukumu ulilopewa ama kutorudisha mrejesho wa kazi na kutojali utu wa watu wengine.

  “Nataka nione kila mtumishi yuko “busy for something” ili tuweze kuwasaidia Wananchi wetu, na katika hili tutapimana mmoja mmoja katika eneo lake amefanya nini kwa siku, wiki, mwezi mpaka mwaka na yeye mwenyewe atusaidie kujitathmini kuona kama ana umuhimu wowote katika eneo lak ama Lah”

  Wizara hii ni Injini ya mabadiliko katika Nchi yetu hivyo sisi lazima tuwe Wizara bora inayofanya kazi zitakazoleta chachu ya Maendeleo kwa mwanancHi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla, hivyo nitasughulika na watumishi wote mpaka nione mnaendenda kadiri ya kasi ninayoitaka ili mabadiliko chanya yaweze kutokea alisema waziri Jafo.

  “Sitaki kuona mtu anashinda Ofisini Wizara hii ni watekelezaji wa Sera mbalimbali na Sera hizo zinatekelezwa kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa nataka niwaone mkienda kufuatilia utekelezaji na kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa viwango na wananchi wanapata stahiki yao ya huduma bora toka kwenye mamlaka za serikali za mitaa zilizoko kwenye maeneo hayo na sio kushinda Ofisini” Aliongeza Mhe. Jafo.

  Akizungumza wakati wa kikao hicho Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda amesema ninachohitaji toka kwa watumishi wa OR-TAMISEMI tufanye kazi na tuipende Kazi na kwa pamoja tuweze kuisimamia bajeti ya Serikali ambapo Wizara hii tunapata asilimia 20.7 ya bajeti nzima ya Taifa letu ni lazima tuitendee haki kwa sababu Fedha zinakuja kwetu ni nyingi hii inaonyesha umuhimu wa Wizara hii kwa maendeleo ya taifa.

  Amesisitiza mambo matatu anayoyahitaji toka kwa watumishi kuwa ni “clarity” kuwa na uwezo mkubwa wa kuelewa Majukumu, Sera, Sheria, Program, Miongozo na kanuni mbalimbali sambamba na mazingira wezeshi yatakayomuweza mtumishi kufanya kazi ambayo haya yatatengenezwa na mwajiri pamoja kuwa uwezo wa kufanya kazi ulizopangiwa bila kusimamiwa “competency”.

  Naye naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Joseph Sinkamba kandege ninachohitaji zaidi toka kwenu ni ushirikiano kwa sababu hata kama mtu anaweza kiasi gani lazima anahitaji msaada wa mwingine ili aweze kukamilisha kazi yake vizuri hakuna nayeweza peke yake hizi kazi tunategemeana na zaidi ya hapo nahitaji watu wakweli na waaminifu ili tuweze kufikia malengo ya pamoja.

  Kikao hiki na watumishi wa TAMISEMI ni cha pili tangu kuapishwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo pamoja na Manaibu Waziri wake Mhe. Mhe. Joseph Sinkamba kandege pamoja na Mhe. George Joseph Kakunda.


  TAMISEMI YA WANANCHI

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Wasambazaji wa Matangazo kwenye Vyombo vya Habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Daniel Shonza.
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) na Wasambazaji wa Matangazo kwenye Vyombo vya Habari leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo wakati wa kikao baina yake na Wasambazaji wa Matangazo kwenye Vyombo vya Habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Daniel Shonza na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus.
  Mmoja wa wawakilishi wa Kampuni za Usambazaji wa Matangazo kwenye Vyombo vya Habari kutoka Kampuni ya OMD Tanzania Bw. Enos Otieno akichangia hoja wakti wa kikao baina yao na Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe leo jijini Dar es Salaam.


  Picha na: Frank Shija – MAELEZO

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Paul Sherlock, Ikulu jijini Dar Es Salaam.
  Balozi alizungumzia masuala mbalimbali yakiwemo kuwawezesha wanawake katika nafasi za kisiasa, Masuala ya Mimba za utotoni  na namna ya kukabiliana na vifo wakati wa kujifungua.
  Kwa upande wake Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliiomba nchi ya Ireland kuendelea kusaidia Tanzania katika kutoa elimu ya uzazi ili kupunguza Vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifungua.
  Wakati huo huo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amkutana na kuzungumza na Balozi wa Morocco nchini Mhe. Abdelilah Benryane mwenye makazi yake mjini Nairobi,Kenya.
  Katika mazungumzo yao, Balozi wa Morocco alimpatia taarifa ya utekelezaji wa yote yaliokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco na kumueleza Makamu kwamba utekelezaji wa mambo hayo umefikia hatua nzuri.
  Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais alimpongeza Balozi kwa kusimamia utekelezaji huo ndani ya muda mfupi.
  Makamu wa Rais alimueleza Balozi huyo wa Morocco kuwa uhusiano uliopo kati ya nchi mbili hizi ni wa kudumu na utasaidia katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo katika nchi hizi.
  Mwisho Kabisa Makamu wa Rais alikutana na kuzungumza na Balozi wa Sausi Arabia Mhe. Mohammed Almalik .
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia Mhe.Mohammed Almalik(kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar Es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Saudi Arabia Mhe.Mohammed Almalik mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar Es Salaam. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Paul Sherlock alimtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Morocco Mhe. Abdelilah Benryane (kushoto), Ikulu jijini Dar es salaam. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Morocco Mhe. Abdelilah Benryane (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam.
  11:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa kutoka kwa Balozi wa Morocco Mhe. Abdelilah Benryane (kushoto), Ikulu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya makamu wa Rais)

  0 0

   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua kampeni ya kitaifa ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” "Najitambua Elimu ndio Mpango mzima". 
   Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akibonyeza kitufe kuzindua ujumbe wa radio wa kampeni ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima” 
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto, wadau na madereva bodaboda wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara muda mfupi baada ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika kitaifa wilayani Tarime mkoani Mara. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

   Waziri wa Afya, Maendeleo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy  Mwalimu akizungumza na wananchi wa Tarime mkoani Mara na kutoa miezi sita kwa wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kuanzisha madawati ya ulinzi na usalama kwa mtoto kike katika Shule zao.
   Mkuu Wa mkoa wa Mara Mhe. Charles Mlingwa  akihamasisha wananchi wa mkoa wa Mara kuzingatia na kulinda haki za Mtoto katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike iliyofikia kilele chake 11/10/2017.


  Na Mwandishi Wetu Tarime- Mara.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametoa miezi sita kwa Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kuanzisha Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto kwa ajili ya kusikilizamatatizo ya wanafunzi hasa wanafunzi wa kike.

  Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa KikeKitaifa iliyofanyika katika wilaya ya Tarime mkoani Maraamewasisitiza wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kuzingatia uwepo wa dawati la ulinzi na usalama wa mtoto  kike katika shule zao ili kuwa salama na kuwa na mahali pa keleza matatizo yao.

  Mhe. Ummy ameongeza kuwa suala la kumlinda mtoto wa kike ni jukumu la kila moja katika jamii na kuwapongeza wadau wa maendeleo ya watoto kwa jitihada zao na kushirikiana na Serikali kutoa elimu kwa wanajamii kuhusu madhara ya mimba za utotoni, ukeketaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

  “ Niwatake wakuuwashule za msingi na Sekondari kuanzisha madawati kwa ajili ya ulinzi na usalama wa  watoto wa kike kwa ajili ya kusikiliza shida za wanafunzi wa kike na kuwasaidia kutatua shida zao katika ngazi ya shule”.
  Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la kutokomeza ukeketaji Tarime Stela Mgaya amesema kuwa wamefanikisha kuwaondoa mangariba 63 kutokakatika kazi ya ungariba na kuwatafutia kazi zingine za kujipatia kipato.

  Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Watoto Duniani UNICEF Bi. Maniza Zaman amewasihi viongozi wa dini na wale wa Kimila ambao  wana ushawishi mkubwa kuziongoza jamii zetu kuwaangalia na kuwasaidia watoto wa Kike.

  Mwakilishi Shirika la Plan Tanzania Bi. Martha Lazaro ameishukuru Serikali na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiao katika kutekeleza mipango mbalimbali ya mtoto hasa wa kike na vihatarishi vinavyopelekea kuharibu maisha yao.

  Katika Maadhimisho ya mwaka huu Serikali imezindua Kampeni ya Kitaifa ya utokomezaMimba za Utotoni yenye kauli mbiu isemayo:“ Tutokomeze Mimba za Utotoni; Tufikie Uchumi wa Viwanda". Maadhimidho hayo, Waziri Ummy ameteua wimbo wa Shule ya Sekondari ya Welwel na Karatu zote za wilayani Karatu, Arusha kuwa wimbo mahususiutakaotumika kuhamasisha na kuelimisha jamii kutokomeza mimba za utotini.

  0 0

  RC SHIGELLA AFUNGUA KIKAO CHA RCC LEO MKOANI TANGA
  MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akifungua kikao cha kamati ya ushauri cha Mkoa huo (RCC) kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi akizungumza katika kikao hicho leo
   Katibu Tawala Msaidizi Upande wa Miundombinu mkoa wa Tanga,Monica Kinala akifafanua jambo kwenye kikao hicho wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
   Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akielezea mikakati ya Bandari hiyo kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Tanga (RCC)
   Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga akizungumza katika kikao hicho kuelezea mipango yao
   MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Steven Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Gabriel Robert
  Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga (RPC) Benedict Wakulyamba akitoa taarifa ya Jeshi la Polisi katika kikao hicho
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akifafanua jambo kwenye kikao hicho kushoto  ni Katibu Tawala wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kulia Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akisisitiza jambo kwenye kikao hicho

   Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akichangia kwenye kikao hicho
  Mbunge wa Jimbo la Lushoto,Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akiuliza swali kwenye kikao hicho
   Katibu Tawala Msaidizi Upande wa Miundombinu mkoa wa Tanga,Monica Kinala katikati na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga(RMO) Dkt Asha Mahita wakifuatili kikao hicho
   Mbunge  wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda, Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu
   Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini (CCM) Omari Kigoda akifuatilia kwa umakini kikao hicho
   Mbunge wa Jimbo la Tanga,Alhaji Mussa Mbaruku akifuatilia kwa umakini kikao hicho
  Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akiteta jambo na PRO wa Bandari hiyo,Moni Jarufu kulia wakati wa kikao cha kamati ya Ushauri wa Mkoa wa Tanga (RCC)
   Meneja wa Shirika la Taifa la  Nyumba (NHC) Mkoani Tanga,Mussa Kamendu na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa wakifuatilia kwa umakini kikao hicho
   Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga,Mhashamu Anthony Banzi akiwa kwenye kikao hicho
  Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Januari Lugangika kushoto akifuatilia kwa umakini hoja mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Mkoa wa Shinyanga leo umeungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 11 mwezi Oktoba.  Maadhimisho ya  siku ya kimataifa ya mtoto wa kike katika mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.

  Sherehe za maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike yamehudhuriwa na watoto kutoka maeneo na shule mbalimbali mkoani Shinyanga,viongozi wa serikali na vyama vya siasa,wananchi na mashirika na taasisi zisizokuwa za kiserikali likiwemo shirika la kimataifa la Save the Children.

  Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike mwaka huu yamebebwa  na kauli mbiu ya “Tokomeza Mimba za utotoni,Tufikie uchumi wa viwanda”.
  Akitoa hotuba kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza kwa mimba za utotoni nchini hivyo jitihada mbalimbali zinahitajika kuhakikisha mimba za utotoni zinatokomezwa mkoani humo.

  “Ili tufikie uchumi wa viwanda tunahitaji kutokomeza mimba za utotoni ambazo zinachangiwa pia na ndoa za utotoni,ni wajibu wetu serikali,wazazi na wadau wote yakiwemo mashirika na taasisi zinazohusika na masuala ya haki za watoto kuweka nguvu pamoja ili kukomesha vitendo hivi”,alieleza Matiro.

  Aidha aliwanyoshea vidole baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakishirikiana na wanaume wanaowapa mimba watoto kwa kumaliza kesi kimya kimya huku wengine wakidiriki kuozesha watoto.
  Matiro alitumia fursa hiyo kuliagiza jeshi la jadi sungusungu kuwashughulikia watu wanaowapa mimba watoto huku akitaka elimu zaidi kuendelea kutolewa katika jamii kuhusu haki za watoto.

  Matiro pia aliwasisitiza wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao kike na kuwaeleza madhara ya kujiingiza katika mambo ya mapenzi wangali wadogo badala ya kuwaonea aibu huku akiwataka watoto kutokubali kudanganywa na waume ili kuepuka mimba za utotoni.

  Naye Meneja wa Shirika la Kimataifa la Save the Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima alisema vitendo vya mimba na ndoa za utotoni litapungua endapo kesi zinazohusu masuala ya watoto zitachukua muda mfupi kumalizika.

  “Bado tuna tatizo la mifumo ya utoaji haki,matukio ya ukiukaji wa haki za watoto yanapotokea,mara nyingi vyombo vya dola ikiwemo polisi wamekuwa wakitumia muda mrefu kufanya uchunguzi,hali hii inatoa mwanya kwa wahalifu kuwapa hongo wazazi watoto kisha kumaliza kesi kienyeji na haki ya mtoto kupotea”,alieleza Malima.

  Hata hivyo Malima alishauri kuanzishwa mfumo maalumu kutoa elimu kwa jamii kuhusu haki za watoto utakaosimamiwa na serikali kwa kuyahusisha mashirika na taasisi zinazohusika na masuala ya watoto ili jamii iweze kuondokana na mila potofu zinazogandamiza haki za watoto.

  Kwa upande wake,Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Azza Hilal aliwataka akina mama kuwa mstari katika kuhakikisha watoto wanaenda shule na kukataa watoto wao kuozeshwa kwa tamaa ya mali huku akiwasisitiza watoto kusoma kwa bidii na kutokubali kurubuniwa kuacha masomo ama kuambiwa wafanye vibaya katika mitihani yao ili wakifeli waolewe.

  Akisoma risala kwa niaba ya watoto wa kike mkoa wa Shinyanga,Rosemary Richard kutoka shule ya msingi Iselamagazi alisema miongoni mwa changamoto zinazowakabili watoto ni jamii kuwa na uelewa mdogo kuhusu haki za watoto.

  Alizitaja changamoto zingine kuwa ni mila potofu,watoto kutoshirikishwa katika maamuzi na kutoa mawazo katika familia,kubakwa,kupewa mimbana kukatishwa masomo ili wawe chanzo cha mapato wanapoolewa.

  Aliiomba serikali na wadau kutoa elimu kuhusu haki na sera za mtoto huku akiitaka serikali kuwachukulia hatua kali watu wanaowafanyia ukatili watoto lakini pia akaomba katika kila shule kutenga vyumba maalum kwa ajili ya watoto wa kike kujisitiri wanapokuwa katika hedhi. 
  Mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya  siku ya kimataifa ya mtoto wa kike,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,akitoa hotuba katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini leo Oktoba 11,2017.Picha zote Kadama Malunde- Malunde1 blog
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kukataa kurubuniwa ili kuepuka mimba za utotoni.
  Watoto wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro huku wakisoma vipeperushi vinavyohusu masuala ya watoto.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa.
  Mgeni rasmi Josephine Matiro (katikati ya watoto) akicheza muziki na wanafunzi,aliyevaa nguo nyekundu ni Afisa Utamaduni wa wilaya ya Shinyanga,Janeth Elias,aliyekuwa MC katika maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike.
  Meneja wa Shirika la Kimataifa la Save the Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akizungumza katika maadhimisho ya  siku ya kimataifa ya mtoto wa kike kwa mkoa wa Shinyanga ambapo alisema mapambano dhidi ya mimba na ndoa za utotoni yanahitaji ushirikiano baina ya serikali,wazazi na mashirika na taasisi zinazohusika na masuala ya watoto.
  Wanafunzi wakifurahia jambo wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike kimataifa.
  Meneja wa Shirika la Kimataifa la Save the Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima aliwataka wananchi kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati ikiwemo ya Chagulaga ambayo wanaume hutumia fursa kuchagua mchumba na kusababisha watoto wa kike waolewa bila ridhaa yao.
  Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO,Shangwe Kimath akitoa neno wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa Oktoba 11,2017.
  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Ngassa Mboje akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa Oktoba 11,2017.
  Wanafunzi wa shule ya sekondari Iselamagazi wakiimba na kucheza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa Oktoba 11,2017.
  Mtoto akiwa ameshikilia bango lililobeba ujumbe.
  Awali Watoto wakiandamana na mabango wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike.
  Watoto wakiwa wameshikilia bango.
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Azza Hilal (CCM) akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike ambapo aliwasihi wazazi na walezi kupeleka watoto shule kwa ndiyo urithi pekee unaofaa kwa watoto na kuwataka waache kuozesha watoto kwani wanawanyima haki zao.
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Azza Hilal aliwaomba wazazi kuwa karibu na watoto wao ili waweze kuwaeleza matatizo wanayokutana nayo
  Wadau wakiwa eneo la tukio.
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Azza Hilal akicheza na watoto.
  Wananchi wa Iselamagazi wakiwa katika maadhimisho hayo.
  Wanafunzi wakicheza muziki.
  Wadau kutoka taasisi na mashirika mbalimbali yanayohusika na masuala ya watoto wakiwa eneo la tukio.
  Watoto wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa maadhimisho hayo.
  Burudani ya Ngoma ya Mabulo ya Jeshi kutoka kundi linaloongozwa na Msanii wa Nyimbo za asili Wanzigiza ikiendelea.
  Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia akielezea kuhusu hali ya mimba za utotoni mkoani Shinyanga,ambapo alisema mkoa wa Shinyanga unashika nafasi ya tano kwa mimba za utotoni kwa asilimia 34 ambapo mkoa wa kwanza ni Katavi (45% ,Dodoma (43%),Tabora (39%) na Mara (37%).
  Wanafunzi wakiimba kwaya
  Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa yakiendelea.
  Watoto wa kiume wakiimba wimbo kuwaasa watoto wa kike kuepuka vishawishi ili watimize ndoto zao.
  Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.
  Mtoto Rosemary Richard akisoma risala mbele ya mgeni rasmi.
  Watoto wakiwa wameshikilia katarasi zenye maandishi yanayoonesha matukio,matendo,mila potofu zinazomkandamiza mtoto wa kike kabla ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kuzichoma kama ishara ya kupinga vitendo hivyo.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia wakichoma moto katarasi zenye maandishi yanayoonesha matukio,matendo,mila potofu zinazomkandamiza mtoto wa kike.
  Karatasi hizo zikiwaka moto.
  Wadau wakiwa katika eneo la tukio.
  Watoto wakicheza mchezo wa igizo kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.
  Meza kuu wakifuatilia kwa umakini igizo la watoto kuhusu mimba na ndoa za utotoni.
  Wimbo kutoka kwa wananchi wa Iselamagazi ikiendelea.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya Msingi Iselamagazi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akipanda mti.
  Picha ya pamoja ,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro na wadau baada ya kupanda mti.
  Walimu wa shule ya msingi Iselamagazi wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya mti uliopandwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.
  Wanafunzi wa shule ya msingi Iselamagazi wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka Shirika la Save the Children
  Wanafunzi wakifurahia.
  Picha ya kumbukumbu.

  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  Wateja na wadau wa benki ya TPB Mkoa wa Mbeya wakikata keki katika sherehe za kilele cha wiki ya huduma kwa mteja iiliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi kuu za TPB Mwanjelwa .
  Meneja wa Benki ya TPB Mkoa wa Mbeya Ndugu Humphrey Julius (kulia ) akilishwa keki na mteja wa TPB  katika kilele cha wiki ya huduma kwa mteja iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi kuu za benki hiyo Mwanjelwa jijini Mbeya
  Wafanyakazi wa benki ya TPB Mkoa wa Mbeya katika nyuso za furaha siku ya sherehe za wiki ya huduma kwa mteja ambayo imefanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za TPB Mwanjelwa jijini Mbeya na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali. .
  Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya TPB Mkoa wa Mbeya katika Picha ya pamoja katika sherehe za wiki ya huduma kwa mteja iliyofanyika katika Ofisi Kuu za TPB Mwanjelwa jijini Mbeya na kuhudhuriwa na wadau mabalimbali wa benki hiyo.

  Baadhi ya wateja na wadau mbalimbali waliohudhuria kilele cha wiki ya huduma kwa mteja benki ya TPB Mkoa wa Mbeya katika Ofisi za kuu Tpb Mwanjelwa.


  0 0

  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi amesema uzoefu wa Sweden wa miaka mingi katika kuendesha serikali za Mitaa unaweza kuisaidia Zanzibar katika kipindi hiki cha ugatuzi.

  Balozi Seif amesema hayo afisini kwake vuga wakati alipokuwa akizungumza na ujumbe wa watu wanane kutoka sweeden ukiongozwa na Spika wa Manispaliti ya Sundsvall Bibi. Arianne Sundman ambaye yupo nchini kwa ziara ya wiki moja. 

  Amesema Zanzibar hivi sasa inapitia katika kipindi cha mageuzi ya serikali za mitaa unaojulikana kwa jina la ugatuzi ili kuyafanikisha mageuzi hayo ni vyema kujifunza kutoka nchi mbali mbali zenye uzoefu. 

  Balozi Seif amefurahishwa na uhusiano uliopo kati ya Wadi ya Makunduchi na Manispaliti ya Sundsvall na kutaka uhusiano huo uimarishwe zaidi. Naye Spika wa manispaliti ya Sundsvall Bibi. Arianne Sundman amesema Manispaliti yake iko tayari kubadilishana uzoefu na Zanzibar katika sekta mbali mbali ikiwemo elimu. 

  Akielezea uhusiano uliopo kati ya Manispaliti yake na Wadi ya Makunduchi, Bi Arianne amesema ameridhishwa na uhusiano huo ambao unaimarika siku hadi siku. Wakati huohuo spika wa baraza la wawakilishi mh zubeir ali maulid amesema ujio wa wa ujumbe huo ni hatua muhimu ya kuimarisha uhusiano katika masuala muhimu ya maendeleo. 

  Akielezea shughuli zinazo fanywa ba baraza la wawakilishi mh zubeir amesema ni pamoja na kutunga shera, kupitisha bajeti, masuali na majibu pamoja na kupitisha mipango ya maendeleo. Nae spika wa manispaa ya sundsval ametoa shukrani kwa mapokezi mazuri waliyoyapata na kuahidi kuimarisha uhusiano kwa wawakilishi katika kubadilishana mawazo katika utekelezaji wa kazi zao za kila siku. 

  Mapema ujumbe huo ulipata nafasi ya kusikiza kipindi cha masulaa na majibu katika kiao cha baraza la wawakilishi kichoendelea na kutembelea sehemu mbali mbali za baraza ikiwepo chumba acha hansard. 
   Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na ujumbe wa Manispaliti ya Sundsvall Sweden
   Balozi Seif akitoa Zawadi ya kasha kwa Bibi Arianne Sundman, Spika wa Manispaliti ya Sundsvall, Sweden
  picha ya pamoja na ujumbe wa Sundsvall ukiongozwa na Spika.

  0 0

  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MADABA.

  WANANCHI wa Halmashauri ya mji wa Madaba, mkoani Ruvuma, wameipongeza serikali kwa kuwafikishia umeme kwenye eneo lao ambapo wamesema utabadilisha maisha yao.

  Pongezi hizo zimetolewa Oktoba 11, 2017, kufuatia kukamilika kwa kazi ya kujenga njia ya kusafirisha umeme kwenye eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka mtandao wa nyaya (wiring), kwenye eneo hilo na kwenye nyumba za  wananchi kazi iliyokwenda sambamba na ufungaji wa  transofoma pozo.

  Kwa sasa Serikali kupitia Shirika lake la Umeme, TANESCO inatekeleza mradi mkubwa wa umeme wa Makambako-Songea ambao unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa  msongo wa kilovolti 220Kv Transmision Lines na usambazaji umeme vijijini (Rural electrification), katika vijiji vya mkoa wa Njombe na Ruvuma ikiwa ni pamoja na kujenga vituo viwili vipya vya kupoza umeme, huko Madaba na Songea na upanuzi wa kituo kingine mjini Makambako.

  “Nimefurahi sana eneo letu kupata umeme, kwa muda mrefu sana tumekuwa tukitegemea umeme wa solar, sasa nina matumaini makubwa nimeona kazi zinavyoendelea hapa za kuweka nguzo za umeme, kutandaza nyaya majumbani na kuweka transofa, na tumeambiwa tukae mkao wa kula kwani umeem utawaka muda wowote kuanzia hivi sasa.” Anasema  Rehema Maluwa, (pichani juu).

  Bi Maluwa, amesema, yeye ni mjasiriamali kwa hivyo ujio wa umeme utamuwezesha walau kutengeneza askrimu, na hivyo anatatarajia kujiongezea kipato kwa njia hiyo.Mwananchi mwingine Bw. Eliudi Msigwa, yeye anategeema umeme huo sio tu utawaharakishia maendeleo, pia utainua hadhi ya mji wao ambao kwa muda mrefu umekuwa hauna umeme.

  Akizungumzia hatua iliyofikia hadi sasa katika kuhakikisha umeme unawaka kwenye Halmashauri hiyo, Meneja wa Mradi wa umeme wa Makambako-Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, amesema, kilichobaki kwa sasa ni kuunganisha umeme majumbani.

  Mwananchi mwingine Bi.Theresia Justin yeye amefurahishwa na taarifa za ujio wa umeme kwenye Hamlamshauri yao kwani tangu wapate uhuru hawajawahi kuwa na umeme, zaidi ya watu wenye uwezo kutumia majenereta na wengine umeme wa Solar.

  “Niwahakikishie wananchi mwishoni mwa Novemba au mwanzoni mwa Desemba mwaka huu wa 2017, umeme utawaka kwenye Halmashauri ya Mji wa Madaba na wananchi watasherehekea Krismas wakiwa na umeme, alisema.

  Kwa upande mwingine, kazi ya kujenga minara ya njia ya kusafirisha umeme, inaendelea kwa kasi ambapo hadi hivi sasa jumla ya minara, (nguzo kubwa) 266 imejengwa kati ya nguzo 710 ambazo zinatarajiwa kujengwa chini ya mradi huo.

  Kwa upande wake Meneja wa TANESCO mkoani Ruvuma, Mhandisi Patrick Lwesya, amewataka wawekezaji kujenga viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kwani upatikanaji wa umeme kwenye mkoa wake utakuwa wa uhakika na wa kutosha kutokana na utekeelzaji wa mradi huu unavyokwenda kwa kasi. 

  "Mradi huu ifikapo Septemba mwakani kwa asilimia 100 utakuwa umekamilika kwa hivyo wananchi wa Halmashauri ya Madaba, Songea, Mbinga na Namtumbo watakuwa na huduma ya umeme wa uhakika na wa kutosha na hivyo niwaombe tu kujiandaa kwa kuanzisha miradi midogo na mikubwa ya viwanda ili kuongeza pato lao na la taifa kwa ujumla." Alsiema Mhandisi Lwesya.
   Wahandisi wa Shirika la umeem nchini TANESCO na mkandarasi kutoka kampuni ya m/s Isolux, wakijadiliana jambo pembezoni mwa moja ya transofa mpya zilizofungwa kwenye mji wa Madaba Oktoba 11, 2017.
   Meneja wa TANESCO mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Patrick Lwesya, akizungumza na wahariri kwenye eneo la ujenzi wa kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme wa kilovolti 220kV/33kV, eneo la Madaba.
   Nyumba zikiwa na madishi ya tv kwenye Halmashauri ya mji wa Madaba mkoani Ruvuma ambazo bila shaka kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutokana na matumizi ya jenereta kupata umeme lakini ujio wa umeme wa TANESCO utapunguza gharama za uendeshaji.
   Maendeleo ya ujenzi wa msingi wa kufungia mashine kituo cha Madaba, ukiendelea Oktoba 11, 2017.
    Maendeleo ya ujenzi wa msingi wa kufungia mashine kituo cha Madaba, ukiendelea Oktoba 11, 2017.
   Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.
    Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.

    Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.
   Mhandisi kutoka kampuni ya Kalpataru, (kulia), akifafanua jambo kwa wahariri kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha nyaya za umeme wa 220kV eneo la Iboya.
   Wajariri wakiwa kazini eneo la ujenzi wa kituo kipya cha Madaba.
   Mhandisi kutoka kampuni ya Kalpataru, (kulia), akiwatembeza wahariri kwenye eneo la ujenzi wa minara huko Iboya.
   Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi, Leila Muhaji, (kulia), na baadhi ya wahariri wakitembelea eneo la ujenzi wa minara huko Iboya.
   Meneja Mradi wa Makambako-Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, akifafanua jambo kwa waharri kwenye eneo al ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Madaba mkoani Ruvuma Oktoba 11, 2017.
   Mradi wa Makambako-Songea, umehamasisha ujenzi wa viwanda na ujenzi wa kiwanda cha kuchakata chai kinachomilikiwa na kampuni ya Uniliver huko Njombe.
   Tayari eneo la ujenzi wa kiwanda hicho limefikishiwa umeme na TANESCO kama ambavyo transfoma pozo mpya iliyofungwa na Shirika hilo inavyoonekana jirani na eneo la ujenzi.
   Meneja Mradi wa Makambako-Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, akifafanua jambo kwa waharri kwenye eneo al ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Madaba mkoani Ruvuma Oktoba 11, 2017.

older | 1 | .... | 1396 | 1397 | (Page 1398) | 1399 | 1400 | .... | 1897 | newer