Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live

USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA MKOA WA GEITA

$
0
0
Wananchi kata ya Bulela Halmashauri ya Mji Geita wakisubiri huduma ya usajili wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Mkoani Geita.
Wananchi kata ya Bulela Halmashauri ya Mji Geita wakisubiri huduma ya usajili wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Mkoani Geita.
Afisa Msajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, akiendelea na zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa kwa Wananchi wa mtaa wa Station kata ya Mtakuja Halmashauri ya Mji Geita.
Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakiendelea na zoezi la uingizaji wa taarifa za wananchi katika zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa linaloendelea katika Halmashauri ya Mji Geita Mkoani Geita.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uratibu Ofisi za wilaya Bi. Rehema Kionaumela akitoa maelekeza kwa Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Mkoani Geita kuhusu taratibu mbalimbali wakati wa maandalizi ya zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji Geita.
 
Wananchi wa mtaa wa Station kata ya Mtakuja Halmashauri ya Mji Geita katika foleni wakisubiri kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa, wakati wa zoezi la usajili linaloendelea mkoani humo.
 
……………..

Wananchi wa Halmashauri ya mji Geita, mkoani Geita wameendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la usajili na utambuzi linaloendeshwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa. Zoezi hili ambalo kwa sasa linaendelea mikoa yote ya Kanda ya Ziwa na Kaskazini limekuwa ni fursa nzuri na muhimu kwa wananchi kusajiliwa na kuwezeshwa kushiriki katika shughuli za maendeleo kutokana na umuhimu wa taarifa zinazokusanywa.

Pindi mfumo huu utakapokamilika wananchi watawezeshwa kupata huduma mbalimbali kwa urahisi pamoja na kusaidia Serikali kuimarisha Ulinzi na Usalama wa nchi kwani Kitambulisho hiki kitakuwa ufunguo kwa mifumo mingine ya Serikali kubadilishana taarifa.

DC Mkuranga kuwa mgeni rasmi kugawa nyumba Jumamosi

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani,Gilberto Sanga amekubali kuwa Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa,Julius Nyerere yatakayofanyika Oktoba 14,2017 katika kijiji cha wasanii Mwanzega wilayani hapa.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib alisema jana kuwa katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya atagawa nyumba 18 zilizojengwa na wanachama wa mtandao kwa njia ya kuchangiana na atakabidhi alama 55 kwa wanachama.

Alisema katika maadhimisho hayo ambayo SHIWATA huadhimisha siku hiyo kila mwaka kwa matukio mbalimbali mwaka jana walikabidhi fedha kwa watu waliopata maafa ya tetemeko la ardhi mkoa wa Kagera.

Taalib alisema SHIWATA ambayo mpaka sasa imekwisha kabidhi nyumba 268 zilizojengwa kwa njia ya kuchangiana pia imekuwa ikiendesha matamasha ya wasanii mbalimbali kuonesha vipaji vyao.

Alisema Julai mwaka huu SHIWATA iliendesha tamasha la wasanii wote na Desemba mwaka huu kutakuwa na mashindano ya soka ambayo yalianza mwaka jana na timu ya maveterani ya Kitunda iliibuka kuwa mabingwa kati ya timu sita zilizoshindana.

Katika hatua nyingine wanachama wa SHIWATA ambao mashamba yao yanachukuliwa na serikali kwa ajili ya kujenga viwanda wameazimia kutafuta mashamba mengine kando kando ya reli ya Kati.

Wasanii wa Tigo Fiesta watembelea Duka la Tigo Iringa

$
0
0
Msanii Madee akisalimiana na  mtoa huduma wa Tigo mara baada ya kuwasili dukani hapo.
                      Wasanii wakisalimiana na watoa huduma wa Tigo Iringa.


Wasanii wakiwa kwenye picha ya pamoja duka la Tigo Iringa


UTPC yawanoa waandishi wa habari Dodoma

$
0
0
 Muwezeshaji wa mafunzo Deodatus Mfugale akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Centurion Nala Hotel Dodoma
Afisa program wa (UTPC) anayefanya kazi kitengo cha Mafunzo ,Utafiti na Machapisho Victor Maleko akizungumza na waandishi katika Mafunzo hayo mkoani Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo hayo

Na.Vero Ignatus,Dodoma

Umoja  wa Vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) inaeendesha mafunzo ya siku (5) ya waandishi  habari za mazingira (27)mkoani Dodoma, kwa waandishi kutoka mikoa yote nchini ikiwa ni awamu wa kwanza

Afisa program wa (UTPC) anayefanya kazi kitengo cha Mafunzo ,Utafiti na Machapisho Victor Maleko amesema kuwa  lengo kubwa la mafunzo hayo ni  kuwapata waandishi waliobobea katika kuandika habari za mazingira katika maeneo yao.

"Unapowapata wabobezi hawa ni rahisi kwa wadau wa habari kutoka mikoani kufanya kazi na waandishi amabao wapo madhubuti kwenye maeneo yao,wapo waandishi wengi makanjanja hawajui wanachokifanya"alisema Victor.

Mafunzo mengine yanayoendeshwa sambamba na haya ni pamoja na  mkoani Pwani yanaendelea mafunzo ya uandishi wa habari za Jinsia ,mkoani Morogoro yanaendelea mafunzo ya uandishi wa habari za Vijijini na mkoani Dodoma mafunzo ya uandishi wa habari za Mazingira

"tunataka tuwapate machampion watakao simamia habari za mazingira peke yayake,Jinsia  pamoja na  waandishi wa habari za vijijini tu"alisema

Amewaasa waandishi wa habari ambao hawajajiunga katika vilabu vya waandishi  habari vilivyopo kila mkoa wajiunge  kwani zinawasaidia kuwakutanisha pamoja watanufaika na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na UTPC ,ambapo amesema  mafunzo kama haya hayawezi kutolewa kwa mwandishi ambaye siyo mwanchama .

Kwa upande wake muwezeshaji wa mafunzo hayo Deodatus Mfugale amesema kuwa lazima mwandishi awe na malengo,waandike habari zinazoleta mabadiliko na zinazogusa hisia za jamii kwa ujumla.''Mwandishi kama unaandika kila kitu muda wako unakaribia kwisha"alisema Mfugale.

Amesema kuwa UTPC itaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa habari chini ufadhili wa Ubalozi wa Sweeden hapa nchini kwa muda wa miaka (5) ambapo huu ni mwaka wa( 2) hadi 2020 wataendelea kubadilisha mafunzo hayo kadri ya  uhitaji wa waandishi .

TAARIFA KWA UMMA

$
0
0


TAARIFA KWA UMMA

Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya umeandaa Misa Maalum ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itakayofanyika tarehe 14 Oktoba, 2017 katika Kanisa la Holy Family Basilica, Nairobi kuanzia saa 4.00 hadi saa 5.00 asubuhi.

Watanzania wote pamoja na ndugu, jamaa na marafiki mnakaribishwa kushiriki katika Misa hii. Kufika kwenu kwa wingi ndio kufanikisha shughuli yetu sote.



TUNATANGULIZA SHUKRANI ZETU ZA  DHATI.



IMETOLEWA NA:

UBALOZI WA TANZANIA

NAIROBI, KENYA

10 OKTOBA, 2017

Zawadi za shs milioni 204 kushindaniwa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya NBC.

$
0
0
 Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbagala,  Sady Mwang’onda (wa pili kulia) na Meneja Bidhaa za Uwekezaji wa benki hiyo, Dorothea Mabonye (wanne kushoto), wakikata utepe kuashirikia uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya malengo ya NBC. Kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu na kufanyika nchini kote itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi wengine 24 watajishindia kila mmoja zawadi ya pesa taslimu shs milioni moja hivyo kufanya jumla ya zawadi zote kufikia thamani ya shs milioni 204. Hafla hiyo ilifanyika katika tawi hiyo, Dar es Salaam leo. Wengine ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo.
 Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbagala,  Sady Mwang’onda (katikati), Meneja wa Bidhaa za Uwekezaji wa benki hiyo, Dorothea Mabonye (kulia kwake), na Mkuu wa  Bidhaa na Wateja Rejareja, Andrew Lyimo (kushoto kwake), pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo wakishangilia mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya malengo ya NBC uliofanyika katika tawi hilo, Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu na kufanyika nchini kote itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi wengine 24 watajishindia kila mmoja zawadi ya pesa taslimu shs milioni moja.
  Mkuu Bidhaa na Wateja Rejareja wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo (katikati), akihojiwa na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya malengo ya NBC uliofanyika katika tawi Mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu na kufanyika nchini kote itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi wengine 24 watajishindia kila mmoja zawadi ya pesa taslimu shs milioni moja.
 Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa tawi la Mbagala, Sady Mwang’onda, Meneja wa Bidhaa za Uwekezaji, Dorothea Mabonye, Mkuu wa Bidhaa na Wateja Rejareja, Andrew Lyimo
Wafanyakazi wa NBC Tawi la Mbagala pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo wakipozi kwa picha mbele ya gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ atakalojishindia mmoja wa washindi sita wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo. Washindi wengine 24 watajindishindia pesa taslimu shs milioni moja kila mmoja.



MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MABALOZI WA UGANDA, CUBA NA IRAN KWA NYAKATI TOFAUTI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Uganda nchini Mhe. Richard T. Kabonero aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha na kufanya mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja Balozi mpya wa Uganda nchini Mhe. Richard T. Kabonero mara baada ya kumaliza mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Cuba nchini Mhe. Lucas Domingo Hernandez . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Iran nchini Mhe. Moussa Farhang aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa mazungumzo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kitabu chenye historia ya miji ya Iran ambacho alikabidhiwa na Balozi wa Iran nchini Mhe. Moussa Farhang aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa mazungumzo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


…………………………………………………………………………

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekutana na Mabalozi kutoka nchi tatu kwa wakati tofauti ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais alianza kwa kukutana na Balozi Mpya wa Uganda hapa nchini Mhe. Richard T. Kabonero ambaye alifika kuonana na Makamu wa Rais kwa mara ya kwanza ambapo alitumia nafasi hiyo kujitambulisha.

Katika mazungumzo na Makamu wa Rais, Balozi Kabonero alizungumzia nia ni ya dhati ya nchi yake katika kudumisha na kuimarisha uhusiano wa kindugu baina ya Tanzania na Uganda hasa ushirikiano wa kijamii, na kiuchumi ambapo tafiti za mafuta zinazoendelea katika ziwa Eyasi, mashirikiano ya sekta ya anga ili kusaidia kukuza utalii, mradi wa ujenzi ya reli ya kati na mradi wa umeme vijijini pamoja na kuanzishwa kwa jukwaa la biashara la sekta binafsi kutoka nchi husika ili kuweza kunufaika na fursa zitakazojitokeza baada ya kukamilika bomba la mafuta .

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewapongeza wananchi wa Uganda kwa kutimiza miaka 55 ya Uhuru.Pia aliipongeza Uganda kwa kutafiti na kugundua mafuta kwa kutumia wataalamu wazawa ambapo alisisitiza ushirikiano wa kitaalamu na wataalamu wa Tanzania.


Makamu wa Rais amemtakia heri na fanaka katika majukumu mapya ya Ubalozi wa Uganda hapa Tanzania na kumhakikishia ushirikiano wa Serikali.Makamu wa Rais alimalizia mazungumzo yake na Balozi huyo wa Uganda hapa nchini kwa kutoa shukrani zake za dhati kwa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kwa ushirikiano wake walioutoa wakati wa ajali mbaya ya gari iliyowakuta Watanzania waliokuwa wanatoka Harusini ambapo watanzania 13 walifariki.

Wakati huohuo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba hapa nchini Mhe. Lucas Hernandez ambaye alisema Cuba imeendelea kuwa rafiki mzuri wa Tanzania na kushukuru sana Tanzania kuisemea Cuba iondolewe vikwazo kwenye mkutano wa 72 wa baraza kuu la usalama la umoja wa Mataifa.

Balozi huyo alisema kuna zaidi ya wataalamu 50 kutoka Cuba wapo nchini katika kusaidia katika Nyanja mbalimbali ikiwemo afya na elimu,Balozi Hernandez alisema wataalam 16 wa masuala ya afya waliwasili jana na kupangiwa kazi katika hospitali ya Muhimbili.

Cuba na Tanzania zimeendelea kuimarisha na kudumisha uhusiano uliohasisiwa na Fidel Castro na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Alisema mwisho wa mwezi huu kutakuwa na maonyesho ya biashara nchini Cuba ambapo Tanzania itawakilishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara na Ujumbe wake.

Kwa upande wake Makamu wa Rais alishukuru Balozi wa Cuba kufika na kumuona na kwamba anatambua uhusiano mzuri uliopo katika nchi hizi mbili ambapo Tanzania imeendelea kufaidika na misaada ya kitaalamu kutoka Cuba haswa katika kutupatia wataalamu wa masuala ya afya, elimu ambapo pia Makamu wa Rais aliitaka Cuba kuja kutangaza vyuo vyao vya elimu ya juu kwani elimu yao haina gharama.

Makamu wa Rais aliishukuru Cuba kwa kuweza kusaidia ujenzi wa Viuatilifu kwa kuzuia malaria nchini.Katika kukuza utalii Makamu wa Rais alisema nchi hizi zinaweza kuimarisha mahusiano ya kitalii kwa kupeana ujuzi mbali mbali ambapo Cuba ni wazuri kwa Utalii wa Ufukweni.

Makamu wa Rais alisema kufunguliwa kwa Ubalozi itakuwa chachu katika kuimarisha na kudumisha uhusiano.Mwisho Makamu wa Rais alimalizia mazungumzo na Balozi wa Cuba kwa kumpongeza Rais wa Cuba Mhe. Raul Castro kwa kusimamia maono na misingi iliyoachwa na Fidel Castro.

Mwisho Makamu wa Rais alikutana na Balozi wa Iran nchini Mhe. Moussa Farhang ambaye alifikisha salaam zake kutoka kwa Makamu wa Rais wa Iran ambaye ameshukuru kwa mahusiano yaliodumu kwa miaka 40 .

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia alisema uhusiano uliopo baina ya nchi mbili hizi umegawanyika sehemu mbili ambapo moja ni uhusiano wa Kiserikali na pili ni husuniano wa kindugu ambapo mpaka leo kuna baadhi ya Vijiji, Makaburi na Misikiti inayoonyesha kuwa wa Persia waliishi Zanzibar.

Uhusiano wa Kiserikali umeendelea kuwa mkubwa katika Nyanja za kilimo na afya pamoja na kuendeleza baadhi ya programu katia vyuo vya ufundi.Makamu wa rais alisema Tanzania inaangalia namna ambavyo itarahisisha kurejesha vikao vya tume ya pamoja ya makubaliano ili kuweza kusukuma mbele maendeleo ya viwanda, Gesi na biashara.

ASKARI WA JWTZ WAUWAWA DRC


WAZIRI KAIRUKI AELEZEA VIPAUMBELE VYAKE

$
0
0
Greyson Mwase na Asteria Muhozya.

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ameeleza vipaumbele  vyake katika Wizara kuwa ni pamoja na  udhibiti wa utoroshaji wa madini nchini, maslahi kwa wafanyakazi huku akiwataka watumishi kufanya kazi kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu.

Kairuki ameyasema hayo mapema leo tarehe 10 Oktoba, 2017 jijini Dar es Salaam  alipozungumza na  watumishi wa Wizara ya Madini pamoja na taasisi zake, waliopo Dar es Salaam na Makao Makuu  ya Wizara Dodoma. Lengo La kikao hicho lilikuwa ni kufahamiana na kupanga mikakati  ya kushirikiana ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa Uchumi wa nchi.

Taasisi zilizoshiriki katika kikao hicho ni pamoja na  Wakala wa Jiolojia  Tanzania (GST), Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO), Chuo cha Madini Dodoma (MRI) pamoja na Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini na Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji (TEITI).

Amesema kuwa Sekta ya Madini  inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuwataka wataalam wa madini kubuni mbinu za ukusanyaji wa maduhuli pamoja na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwenye uchimbaji madini.

Katika hatua nyingine aliwataka wataalam hao kubuni mikakati  ya kuzuia utoroshaji wa madini nchini ili nchi ipate mapato stahiki.Amewataka watumishi kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuwa wabunifu ili  sekta hiyo iwe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Naye Naibu  Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewakumbusha  watumishi kuzingatia Dira na Dhima ya Wizara  ikiwemo kufanya kazi kwa tija ili hatimaye  sekta ya madini iweze kuchangia katika uchumi wa nchi kwa kuwa mchango wa sekta husika bado ni kidogo.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki  (kushoto) akitoa maelekezo kwa watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake (hawapo pichani) Kulia ni Naibu  Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa iliyokuwa  Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (kushoto mbele) pamoja na watendaji wengine wa Wizara wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki. (hayupo pichani).
 Sehemu ya  watendaji wa Wizara ya Madini wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki
 Naibu  Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia)  akifafanua jambo katika kikao hicho. Kushoto ni Waziri wa Madini, Angellah Kairuki.
 Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (kulia mbele) akieleza majukumu ya Wizara ya Madini kwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki na Naibu  Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hawapo pichani) 
 Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Madini, Makao Makuu Dodoma wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (hayupo pichani) kwa njia ya video conference.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo(kulia) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa iliyokuwa  Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (hayupo pichani)

WAFANYAKAZI WA STAMICO WAPATA MAFUNZO YA UKIMWI

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
SERIKALI imedhamiria kupambana na janga la Ukimwi ikiwa ni pamoja na kuandaa muongozo kwa wafanyakazi kupata elimu juu ya ugonjwa huo jinsi ya kujiepusha.

Hayo ameyasema Kaimu Mkurugenzi Masoko na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico),  Aloyce Tesha wakati akifungua semina ya wafanyakazi wa shirika hilo katika kupata elimu ya Ukimwi pamoja na magonjwa sugu yasiyoambukiza , amesema semina hiyo ni muhimu kwa wafanyakazi katika kuweza kujikinga na magojwa ili waweze kutekeleza majukumu yao.

Tesha amesema kuwa wafanyakazi wakipata elimu wanaweza kufundisha familia zao pamoja na jamii zinazowazunguka katika uchukua tahadhari.

Amesema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo wanakwenda sehemu mbalimbali za madini hivyo lazima wawe na elimu ya Ukimwi na magonjwa yasiyoambukiza.
 Kaimu Mkurugenzi na Uwekezaji wa Stamico, Aloyce Tesha akizungumza katika ufunguzi wa semina ya wafanyakazi wa Stamico juu ya Ugonjwa wa Ukimwi na Magonjwa yasiyoambukiza leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mwitikio wa Taasisi za Umma kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk. Hafidh Ameir akizungumza wakati akitoa mada ya Ukimwi katika semina wa wafanyakazi wa Stamico.
Sehemu ya wafanyakazi wakisiliza mada katika semina hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji, Aloyce Tesha akiwa katika picha ya pamoja na wafanyazi wa stamico mara baada ya semina elimu ya ukimwi na Magonjwa yasiyoambukiza.
Sehemu ya kupimia ugonjwa wa kisukari. 

TAARIFA YA MAKUSANYO YA KODI MWEZI JULAI-SEPTEMBA 2017

NAIBU WAZIRI AWESO AKAGUA MIUNDOMBINU YA MAJI UBUNGO

$
0
0
Fundi wa DAWASCO akiendelea na kazi ya kurekebisha bomba lililopasuka eneo la Riverside, Ubungo.2Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na msimamizi wa matengenezo wa DAWASCO Kanda ya Tabata, aliyekuwa akisimamia matengenezo katika eneo la Riverside, Ubungo kwenye moja ya miundombinu ya maji iliyoharibika.
3Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa katika eneo la Kibangu, Ubungo akikagua moja ya maeneo yaliyo na miundombinu mibovu ya maji.
……………………………………………………………
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji leo amefanya ukaguzi wa miundombinu ya maji eneo la Ubungo na kujionea miundombinu hiyo ambayo mingi imepasuka na kuvujisha maji mengi kutokana na uchakavu au kuhujumiwa miundombinu hiyo.
Katika maeneo aliyopita ameweza kuona upotevu mkubwa wa maji unaotokana na mabomba yaliyopasuka kuvuja, na kusababisha maji mengi kupotea baada ya kuwafikia wananchi kwa ajili ya matumizi.
Naibu Waziri Aweso alisema ipo haja ya kuchukua hatua na kuhakikisha miundombinu hiyo inafanyiwa ukarabati, ili kudhibiti tatizo la upotevu wa maji ambalo limekuwa changamoto kubwa jijini Dar es Salaam.
“Nitakaa na taasisi za DAWASA na DAWASCO tuweke mikakati ya kutatua changamoto hii, ili kuhakikisha kiwango cha upotevu wa maji kinapungua, kwa kuwa ni moja sababu ya wananchi kukosa maji ya uhakika, kwa kuwa mengi yanapotea baadala ya kuwafikia walengwa”, alisema Naibu Waziri.

NISHATI YA UMEME NI KIUNGO MUHIMU KUCHOCHEA UWEKEZAJI WA VIWANDA”-DKT MWINUKA

$
0
0
NISHATI ya umeme imeelezwa kuwa ni kiungo muhimu katika kuchochea uwekezaji wa viwanda hapa nchini ambao utasaidia kuinua kwa kasi uchumi ikiwemo maendeleo kwa watanzania.



Hayo yalibainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Dkt Tito Mwinuka hivi karibuni wakati akizungumza katika baraza kuu la 47 la wafanyakazi wa Tanesco mjini hapa ambapo alisema kwa kutambua umuhimu huo wataihakikishia serikali malengo yao ya viwanda yanatimia.

Alisema kutokana na hali hiyo wataendelea kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana katika maeneo mbalimbali hapa nchini bila kuwepo kwa vikwazo vya namna yoyote ile ili azma hiyo iweza kutimia kwa vitendo na hivyo kuchochea kasi ya uchumi.

“Kama mnavyojua serikali ya awamu ya tano imeazimia kukuza uchumi nchi kufikia ule wa kati wa viwanda hivyo kufikia azma hiyo nishati ya umeme ni kiungo muhimu katika kuchochea uwekezaji wa viwanda ambao utasaidia harakati za maendeleo “Alisema

“Hivyo napenda kuihakikishia serikali kwamba tunatambua wajibu tulio nao katika kutimiza malengo hayo kwa kuongeza uwajibikaji na ufanisi kazini ambao ndio utakuwa dira ya kufikia mafanikio “Alisema.

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema tokea kuanzishwa kwa baraza hilo limekuwa ni sehemu muhimu kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali kwa maslahi ya wafanyakazi ambao wamewaamini kuwawakilisha.

“Baraza hili limesaidia shirika kujua changamoto na kero zinazowakabili mahala pa kazi na kwa pamoja ufumbuzi wake na changamoto hizo zimepatiwa ufumbuzi kwa faida ya wafanyakazi na shirika kwa ujumla “Alisema.

Alisema serikali ya awamu ya tano imeazimia kukuza uchumi nchi kufikia ule wa kati wa viwanda hivyo ili kufikia azma hiyo nishati ya umeme nikiungo muhimu katika kuchochea uwekezaji wa viwanda ambao utasaidia harakati za maendeleo.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

UHURU FM LEO TENA WAMWAGA MSAADA KUPITIA KAMPENI YAO YA 'GUSA MAISHA YAO' KUMUENZI BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE

$
0
0

Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Peoples Media inayoendesha Kituo cha Radio cha Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam, Paul Mng'ong'o (wanne kushoto), akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula kwa Mwanzilishi wa Kituo cha kujeresha katika maisha ya kawaida waraibu wa dawa za kulevya cha Pili Misana Foundation, Pili Misana, kilichopo Kigamboni, dar es Salaam, leo, ikiwa ni mwendelezo wa Uhuru FM kutoa misaada kupitia kampeni yao ya 'Gusa Maisha yao' kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere. Wengine katika picha ni baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru FM na Vijana wanaoishi katika kituo hicho.
Aina ya msaada uliotolewa
Dereva akiliungurumisha basi kupitia daraja la Kigamboni kwenda kwenye kituo hicho.
Baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa katika basi kwenda kwenye kituo hicho cha kusaidia waraibu wa dawa za kulevya kurejea katika maisha ya kawaida, baada ya kufika wafanyakazi hao wakaanza kushuka na vitu vya msaada, mmoja baada ya mwingine
Cecy Jeremiah
Binti Abbas Mtemvu
Mwandishi wa Uhuru na Mzalendo, Njumai Ngota
Mhasibu Mkuu wa Uhuru FM Alvera Kabwogi
Mhariri Mkuu wa Uhuru FM Pius Ntiga
Mfanyakazi Uhuru FM Godliver Koplo
Meneja rasilimali watu wa Uhuru FM paul Mg'ong'o
Meneja rasilimali watu wa Uhuru FM paul Mg'ong'o
Meneja Masoko wa Uhuru FM Furaha Luhende
Meneja Masoko wa Uhuru FM Furaha Luhende
Mtangazaji Uhuru FM Zuhura Zidadu
Mtangazaji Uhuru FM Zuhura Zidadu
Mtangazaji Uhuru FM Paul Sigori
Meneja Mawasiliano Uhuru FM Arnold Dominic
Mhariri Mkuu wa Uuhuru FM Pius Ntiga akiingia kwenye kituo hicho
Cecy Jeremiah akitafakari jambo baada ya kufika kwenye kituo hicho Kigamboni
Baadhi wakibadilishana mawazo baada ya kufika kwenye kituo hicho Kigamboni
Baadhi wakibadilishana mawazo baada ya kufika kwenye kituo hicho Kigamboni
Mtangazaji said Ambua akibadilishana mawazo na mwanzilishi wa kituo hicho
Ntiga na wenzake wakifuatilia mambo yalivyokuwa yakienda
Luhende akifuatilia live kutoka Uhuru FM kwa makini kuhusu matangazo kutoka kwenye kituo hicho cha Kigamboni.
Sigori na ambua wakiwa tayari kutangaza live tukio hilo la utoaji msaada
Sigori (kushoto) akitangaza live tukio hilo
Mwanzilishi wa kituo hicho akitoa maelezo
Mmoja wa waraibu wa dawa za kulevya akitoa maelezo
Mmoja wa waraibu wa dawa za kulevya akitoa maelezo
Arnold Dominic wa Uhuru FM akitoa maelezo ya msaada
Ambua akitoa maelezo
Mama kabwogi akitoa maelezo ambapo aliwasihi vijana walioacha matumizi ya dawa za kulevya kuwasaidia wenzao nao kuacha
Mg'ong'o akikabidhi msaada huo kwa mwanzilishi wa kituo hicho cha Kigamboni.
Mg'ong'o akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo
Shughuli ikamalizika kwa watumishi wa Uhuru FM na wenyeji wao kupigwa picha hii ya pamoja. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

BLOGGER AAGANA NA UKAPERA

$
0
0
Blogger wa Jamvi la Habari ambaye pia ni mhadhiri wa chuo kikuu cha SAUT-Songea Willy Migodela. Tarehe 07/10/2017 alifunga harusi na Lightness Ngenzi katika kanisa la KKKT usharika wa Mbarali mkoani Mbeya.
Pichani Bwana Harusi Willy Migodela na Bibi Harusi Lightness Ngenzi
Pichani Bwana Harusi na Bibi Harusi wakiwa na wasimamizi wao Mr & Mrs Pambano Myula
Pichani Bwana na Bibi Harusi wakiwa katika picha ya pamoja na wapambe wao.

Bwana na Bibi Harusi wakiwa katika tabasamu la kufurahia ndoa yao.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 10.10.2017

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO UMATANO OCTOBER 11,2017

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO UMATANO OCTOBER 11,2017

UHURU FM LEO TENA WAMWAGA MSAADA KUPITIA KAMPENI YAO YA 'GUSA MAISHA YAO' KUMUENZI BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE

$
0
0
Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Peoples Media inayoendesha Kituo cha Radio cha Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam, Paul Mng'ong'o (wanne kushoto), akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula kwa Mwanzilishi wa Kituo cha kujeresha katika maisha ya kawaida waraibu wa dawa za kulevya cha Pili Misana Foundation, Pili Misana, kilichopo Kigamboni, dar es Salaam, leo, ikiwa ni mwendelezo wa Uhuru FM kutoa misaada kupitia kampeni yao ya 'Gusa Maisha yao' kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere. Wengine katika picha ni baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru FM na Vijana wanaoishi katika kituo hicho. 
Aina ya msaada uliotolewa 
Dereva akiliungurumisha basi kupitia daraja la Kigamboni kwenda kwenye kituo hicho 
Baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa katika basi kwenda kwenye kituo hicho cha kusaidia waraibu wa dawa za kulevya kurejea katika maisha ya kawaida, baada ya kufika wafanyakazi hao wakaanza kushuka na vitu vya msaada, mmoja baada ya mwingine .
Cecy Jeremiah 
Binti Abbas Mtemvu 
Mwandishi wa Uhuru na Mzalendo, Njumai Ngota 
Mhasibu Mkuu wa Uhuru FM Alvera Kabwogi 
Mhariri Mkuu wa Uhuru FM Pius Ntiga 
Mfanyakazi Uhuru FM Godliver Koplo 
Meneja rasilimali watu wa Uhuru FM paul Mg'ong'o 
Meneja rasilimali watu wa Uhuru FM paul Mg'ong'o 
Meneja Masoko wa Uhuru FM Furaha Luhende 
Meneja Masoko wa Uhuru FM Furaha Luhende 
Mtangazaji Uhuru FM Zuhura Zidadu 
Mtangazaji Uhuru FM Zuhura Zidadu 
Mtangazaji Uhuru FM Paul Sigori 
Meneja Mawasiliano Uhuru FM Arnold Dominic 

Mhariri Mkuu wa Uuhuru FM Pius Ntiga akiingia kwenye kituo hicho 
Cecy Jeremiah akitafakari jambo baada ya kufika kwenye kituo hicho Kigamboni 
Baadhi wakibadilishana mawazo baada ya kufika kwenye kituo hicho Kigamboni .
Baadhi wakibadilishana mawazo baada ya kufika kwenye kituo hicho Kigamboni .
Mtangazaji said Ambua akibadilishana mawazo na mwanzilishi wa kituo hicho .
Ntiga na wenzake wakifuatilia mambo yalivyokuwa yakienda 
Luhende akifuatilia live kutoka Uhuru FM kwa makini kuhusu matangazo kutoka kwenye kituo hicho cha Kigamboni. 
Sigori na ambua wakiwa tayari kutangaza live tukio hilo la utoaji msaada 
Sigori (kushoto) akitangaza live tukio hilo 
Mwanzilishi wa kituo hicho akitoa maelezo 
Mmoja wa waraibu wa dawa za kulevya akitoa maelezo 
Mmoja wa waraibu wa dawa za kulevya akitoa maelezo 
Arnold Dominic wa Uhuru FM akitoa maelezo ya msaada 
Ambua akitoa maelezo 
Mama kabwogi akitoa maelezo ambapo aliwasihi vijana walioacha matumizi ya dawa za kulevya kuwasaidia wenzao nao kuacha 
Mg'ong'o akikabidhi msaada huo kwa mwanzilishi wa kituo hicho cha Kigamboni. 
Mg'ong'o akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo 
Shughuli ikamalizika kwa watumishi wa Uhuru FM na wenyeji wao kupigwa picha hii ya pamoja. (Picha zote na Bashir Nkoromo) 

MAELFU YA WAKAZI WA IRINGA WAJITOKEZA USIKU WA TAMASHA LA TIGO FIESTA WIKIENDI

$
0
0
Wasanii wa kundi la Rostam, Roma na Stamina wakiimba kwenye tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jumatatu lililofanyika uwanja wa Samora mjini Iringa.

Aslay akiimba na mashabiki kwenye tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jumatatu lililofanyika uwanja wa Samora mjini Iringa.
Joh Makini akitumbuiza maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Iringa.
Jux akiburudisha wakazi wa Mkoa wa Iringa .
MauaSama akitumbuiza katika jukwaa la TIgo Fiesta.
Nandy akiimba kwa hisia katika jukwaa la Tigo Fiesta mkoani Iringa mapema jumapili iliyopita.
Ommy Dimpoz akitumbuiza wakazi wa Iringa.



Vanessa Mdee akitoa burudani na madansa wake katika jukwaa la Tigo  Fiesta viwanja vya Samora Mkoani Iringa.

Viewing all 46384 articles
Browse latest View live




Latest Images