Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1394 | 1395 | (Page 1396) | 1397 | 1398 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mhe. Mongella aahidi Zawadi Nono 

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amewataka wavuvi wa kambi ya fuata Nyayo iliyopo Mwalo wa Mihama na wananchi wa Kata ya Kitangili Wilaya ya Ilemela kuhakikisha wanawabaini wale wote wanaotumia Nyavu haramu na kuendesha Uvuvi haramu katika Mwalo huo,ambapo kwa yeyote atakayetoa taarifa za Siri na zilizo sahihi na kupelekea kukamatwa kwa wahalifu hao atapewa zawadi ya Shilingi Laki Moja tasilimu. 

  Mhe. Mongella amesema hayo katika Mkutano wa hadhara alipokuwa akitoa hotuba wakati wa Uzinduzi wa Zana za Uvuvi endelevu na kusisitiza kuwa kila Mwananchi anatakiwa Kumuunga mkono Rais wetu Dkt.John Pombe Magufuli katika kupambana na uvuvi haramu na kuwataka wananchi kuachana na Uvuvi haramu wa kutumia Nyavu zenye matundu madogo,makorokoro,timba na baruti ambapo kila mmoja anatakiwa kutumia zana na nyenzo salama kama vile nyavu zenye matundu ya inchi 6,7,na 8. 

  Hata hivyo Mhe.Mongella amewakabidhi wanakikundi wa Fuata Nyayo jumla ya nyavu mia saba (700 ) na Mitumbwi kuni na nne (14) ambapo kila Mtumbwi una wastani wa nyavu hamsini,zana na Nyenzo jumla zina thamani ya Shilingi Milioni Themanini na nane laki tatu sabini na saba elfu na mia tano tu. (88,377,500) fedha hiyo imetolewa na mfadhili Bwana Vedastus Msizu ambaye ni Mkurugenzi wa Kambi ya Uvuvi ya Fuata nyayo. 

  Aidha,Mhe.Mongella amempongeza Bwana Msizu kwa ufadhili huo na kuiagiza Halmashauri kuhakikisha wanasimamia kikamilifi usajili wa kikundi hicho ili kikundi hicho kiolozeshwe kwenye vikundi vinavyopata mikopo kutoka Halmashauri hiyo. 


  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (mwenye kofia) akisimamia  kurejeshwa kwa maji nyumbani kwa Bi Veronica Mtiro mlemavu wa miguu mkazi wa Nyakato, mara baada ya kumlipia Shilingi Laki moja na elfu arobaini alizokuwa anadaiwa na MWAUWASA baada ya kuugua muda mrefu na kushindwa kulipia deni hilo ambapo amekuwa akiishi kwa kutegemea kuuza maji hayo. 
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akimsikiliza kwa makini mmoja wa wananchi (aliyeweka mkono begani) wa kata ya Kitangili,Wilaya ya Ilemela mara baada ya Mhe Mkuu wa Mkoa kumaliza kuhutubia wananchi wa kata hiyo na kusikiliza kero zao.


  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kushoto), akiwa ameongozana na kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,(ACP) Julius Mjengi (kulia), alipowasili katika mkoa huo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake za kikazi yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia. Picha na Jeshi la Polisi.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili mkoani Iringa, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia. 
   Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa tayari kwa kumpokea Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, ambaye yupo mkoani Iringa, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia.
  Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, wakiwa katika kikao kazi na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wakijadiliana namna ya kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu mkoani humo, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja.


  0 0


   Mwenyekiti wa Kamati ya Radio Uhuru na Mtangazaji wa Kipindi cha Gusa Maisha Yao, Joy Njarabi akizungumza juu ya uendeshaji wa kipindi hicho na kuweza kupata watu ambao wanaguswa moja kwa moja na kutoa msaada ikiwemo kwa kituo cha watoto wenye Kansa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
   Meneja wa Rasilimali Watu wa Radio Uhuru, Paul Mung’ong’o akizungumza baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Watoto wenye Kansa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili vyenye thamani zaidi sh. Milioni Mbili leo ambavyo vimetolewa na watu wanaosikiliza radio hiyo kupitia kipindi cha Kugusa Maisha yao.
   Wafanyakazi wa Radio Huru wakiwa na watoto wa kituo hicho wakati wa kukabidhi msaada wa vitu mblimbali katika kituo hicho kupitia kipindi cha Gusa Maisha Yao.

  Picha mbalimbali za wafanyakazi katika kituo cha watoto wenye Kansa

  0 0


  :Barclays Bank Tanzania Head of Legal and Company Secretary Dotto Kahabi ( left) presents part of a donation of 60 pairs of kids clothes, 48 pairs of kids shoes, 14 pairs of shoes for parents and clothes to the head of Mwanangu Montessori Centre Jannet Manoni donated by the bank’s Legal and Compliance Department staff as part of the Barclays’ ongoing citizenship activities at a function held at the centre’s premises at Vikindu, Coast Region over the weekend.
  Barclays Bank Tanzania Head of Legal and Company Secretarial, Dotto Kahabi (second left), hands over donation of part of 60 pairs of kids clothes, clothes for parents and guardians, 48 pairs of kids shoes and 14 pairs of parents and guardians shoes to Rukia Selemani, parent of a kid cared for at Mwanangu Montesssori centre, donated by BBT Legal and Compliance department as part of the banks ongoing citizenship activities at a function at the centre premises, Vikindu in Coast Region at the weekend.
  Some staff from Barclays Bank Tanzania Legal and Compliance Department talk to one of the kids cared for at Mwanangu Montessori Centre during their recent visit at the centre.
  Mwanangu Montessori Centre president, Walter Miya (right), talks to on-visit Barclays Legal and Compliance Department staff at the centre’s premises at Vikindu, Coast Region recently. The bank’s staff donated 60 pairs of clothes and 48 pairs of shoes for the children, while parents and guardians were given clothes and 14 pairs of shoes.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi (kulia), akimkabidhi kipeperushi cha taasisi hiyo, Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa, wakati uongozi wa shirika hilo, ulipotembelea taasisi hiyo, kuwaona wagonjwa na kutoa msaada wa fedha kwa watoto wawili wagonjwa wa moyo, kusaidia kufanyiwa upasuaji, ikiwa ni katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani leo Oktoba 10, 2017 jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi, akizungumza na baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati wa ziara ya uongozi wa shirika katika taasisi hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Elia Madulesi na katikati ni Hassan Mwang'ombe.  
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa (wa tatu kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi (wa tatu kulia), mfano wa hundi ya sh. milioni 4 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto wawili wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo, wakati uongozi wa TPC, ulipotembelea taasisi hiyo katika kuadhimisha siku ya Posta Duniani, Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Daktari bingwa wa upasuaji moyo watoto, Dkt. Godwin Sharau na wa kwanza ni Meneja Mkuu Usimamizi Biashara wa TPC, Hassan Mwang'ombe.

  Daktari bingwa wa upasuaji moyo watoto wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dkt. Godwin Sharau (wa tano kulia), akiwapatia maelezo baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati uongozi wa shirika ulipotembelea moja ya wodi za wagonjwa wa moyo kwenye taasisi hiyo leo jijini. Wa nne kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Deo Kwiyukwa. 
  Daktari bingwa wa upasuaji moyo watoto wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dkt. Godwin Sharau (wa pili kushoto), akiwapatia maelezo baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati uongozi wa shirika ulipotembelea moja ya wodi za wagonjwa wa moyo kwenye taasisi hiyo leo jijini katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani, Oktoba 10, 2017. Wa nne kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Deo Kwiyukwa.  
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa, akiwa amembeba mtoto Delphina, ambaye ni mmoja wa watoto waliopatiwa msaada wa sh. milioni 2 kila mmoja na TPC kwa ajili ya matibabu ya upasuaji wa moyo, wakati uongozi wa shirika hilo, ulipotembelea kwenye wodi za wagonjwa wa moyo katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili Dar es Salaam leo katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani. 
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa, akifurai na mtoto Zainab Shabani (3), mmoja wa watoto waliopatiwa msaada wa sh. milioni 2 na TPC kwa ajili ya matibabu ya upasuaji wa moyo, wakati uongozi wa shirika hilo, ulipotembelea kwenye wodi za wagonjwa wa moyo katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili Dar es Salaam leo katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani. Kulia ni mama yake, Fatuma Ahmad na kushoto, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Elia Madulesi. 
  Daktari bingwa wa upasuaji moyo watoto wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dkt. Godwin Sharau (kulia), akiwaeleza jambo baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati uongozi wa shirika hilo, ulipotembelea taasisi hiyo, kuwaona wagonjwa na kutoa msaada wa fedha kwa watoto wawili kusaidia kufanyiwa upasuaji ikiwa ni katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani leo Oktoba 10, 2017. Wa nne kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Deo Kwiyukwa.  
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa, akizungumza na  waandishi wa habari, mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, leo jijini Dar es Salaam.
  Daktari bingwa wa upasuaji moyo watoto wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dkt. Godwin Sharau (kulia), akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), ulipomaliza ziara yao kwenye taasisi hiyo, katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani, leo Oktoba 10, 2017. Wa pili kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Deo Kwiyukwa.  
  Uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), ukiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Madaktari bingwa wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, wakati ulipotembelea taasisi hiyo kuwaona wagonjwa na kutoa msaada katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani Dar es Salaam leo. 
  Afisa Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Posta Kuu Dar es Salaam, James Msiani, akiwaeleza jambo wanafunzi wa Shule ya Msingi Olympio, walipotembelea Ofisi za Posta Kuu na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na posta, ikiwa ni katika maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani.
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Olympio, wakiwa na mwalimu wao, wakiwa katika Ofisi ya Posta Kuu kwa ajili kutembelea ofisi hizo, kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na posta, ikiwa ni katika maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani. Wa pili kushoto ni Afisa Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Posta Kuu Dar es Salaam, James Msiani.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi, akizungumza na uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati uongozi wa shirika hilo, ulipotembelea taasisi hiyo, Muhimbili Dar es Salaam, kuwaona wagonjwa na kutoa msaada wa fedha kwa watoto wawili kwa ajili kusaidia kufanyiwa upasuaji, ikiwa ni katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani, leo Oktoba 10, 2017.  Kushoto ni Kaimu Postamasta wa shirika hilo, Deo Kwiyukwa.
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa, akizungumza na  Uongozi pamoja na Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, wakati uongozi wa shirika hilo, ulipotembelea taasisi hiyo, kuwaona wagonjwa na kutoa msaada wa fedha kwa watoto wawili wagonjwa wa moyo, kusaidia kufanyiwa upasuaji, ikiwa ni katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani leo Oktoba 10, 2017 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi.

  0 0

  Nyuku vikiwa vipo tayari kwenye picnic ya familia na nyama choma iliyoandaliwa na Shield Our Watoto siku ya Jumamosi Oktoba 7, 2017 Westerville, Ohio. SOW ni oganaizesheni iliyoanzishwa na Bhoke Kirigiti akishirikiana na mumewe PeterKirigiti inayotetea watoto kutokana na unyanyasaji hasa watoto wa kike inapowapigania hasa unyanyasaji wa kingono chini ya umri mdogo. Oganaizesheni hii hushirikiana na wazazi wa watoto na watu mbalimbali wakiwemo watoa elimu ya unyanyaswaji wa watoto wakishirikiana na mashirika mbalimbali yasiyokua ya Kiserikali. Shield Our Watoto hutoa elimu ya bure kwa wazazi na watoto kuhusiana na unyanyasaji  wa kijinsia wanaofanyiwa watoto wenye umri ndogo ambao kati ya watoto 3 kati ya 10 wamekua wakiathirika kisaikolojia kutokana unyanyasaji huo
  Peter Kirigiti pamoja na mkewe Bhoke Kirigiti wakielezea Shield Our Watoto (SOW) kwa wadu waliohudhuria family picnic na nyama choma siku ya Jumamosi Oktoba 7, 2017 Westerville, Ohio.
  Wadau mbalimbali waliojumuika kwenye nyama choma hiyo wakiwasikiliza PeterKirigiti na mkeweBhoke Kirigiti.
  Clara James mwandishi wa kitabu cha There's Beauty Inside akielezea unyanyasaji wa watoto hasa kwa mtoto wa kike unawezaje kuathiri saikolojia katika maisha yake.
  Rebecca Walters (mwenye miwani) akiwalekeza watoto jinsi ya michezo yao itakavyochezwa.
  Rebecca Walters na Keri Willard (aliyeengemea ukuta) ambao ni wanafunzi wanaosomea MA Counseling Ministries-Pastoral and Professional Counseling katika chuo cha Methodist Theological cha Ohio (MTSO) wakijitolea kucheza na watoto ikiwemo kuwafundisha michezo mbalimbali ya watoto.
  Rebecca Walters na Keri Willard (kushoto) wakiwaonyesha watoto michezo yao.
  Watoto wakikimbia huku wakiwa wamefunga miguu yao kwa pamoja na mkanda.
  Watoto wakifurahia kucheza na mipira aina ya maputo
  Watoto wakicheza kwenye michezo yao.
  Kwa picha zaidi bofya soma zaidi na kuhusu SOW BOFYA HAPA

  0 0

    Mwezeshaji kutoka ‘Shirika la Save the Children’ Bw. John Komba akitoa mada kwa madereva bodaboda wa Wilaya ya Tarime katika Semina shirikishi ya jamii katika kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike itakayofanyika kitaifa Oktoba 11, 2017 Wilayani Tarime Mkoani Mara.
   Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la REPSSI Tanzania Bibi. Edwick Mapalala akizungumza na waendesha bodaboda wa wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara katika Semina ya kuelimisha jinsi ya kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni kuelekea maadhimkisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike itakayofanyika kitaifa Oktoba 11, 2017 Wilayani Tarime Mkoani Mara.
  Baadhi ya waendesha bodaboda kutoka Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolea katika Semina ya kuwaelimisha jinsi ya kuwalinda watoto wa kike na mimba za utotoni kuelekea maadhimkisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike itakayofanyika kitaifa Oktoba 11, 2017 Wilayani Tarime Mkoani Mara.


   Na Mwandishi Wetu- Tarime, Mara
  Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya watoto wa kike hapa nchini wameendesha mafunzo kwa  waendesha bodaboda walioko wilaya ya Tarime mkoani Mara  kuwahamasisha vijana hao  kuunga mkono juhudi za kitaifa za kutokomeza mimba za utotoni kwa wasichana walioko shule ya msingi na sekondari.  

  Akieleza malengo ya mafunzo hayo, Afisa Mkuu wa Maendeleo ya Jamii Bibi Anna Shengweli amebainisha kuwa madreva wa bodaboda ni kundi mahususi katika ulinzi wa watoto wa kike kwani kutokana na shughuli zao wanakutana mara nyingi na watoto wa kike wakiwa katika mazingira hatarishi. 

  “Wakiwa katika kazi zao za kila siku bodaboda na wanapishana na watoto wa kike wakitekeleza majukumu yao mbalimbali ikiwemo kwenda na kurudi kutoka shule, kuteka maji visimani, kuchunga mifugo porini, sokoni, stendi ya basi na kadhalika’’ alisema Bibi Anna.

  Kwa upande wake mwezeshaji kutoka ‘Shirika la Save the Childern’ Bw. John Komba  amesema kuwa ni muhimu kuwajengea uelewa waendesha bodaboda ili wawe tayari kutambua na kutekeleza wajibu wa kuwaelimisha na kuwalinda watoto wa kike waepukane na vitendo vya ngono wawapo nyumbani, shuleni, njiani, sokoni, mitaani, na katika shughuli za kijamii kwa ujumla.  

  “Mafunzo haya yatawasidia waendesha bodaboda kuwa mabalozi wa usalama na ulinzi wa mtoto wa kike ili kupunguza idadi ya wasichana wanaoacha shule kutokana na changamoto ya mimba za utotoni na hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao, pamoja na kuwashirikisha katika mtandao wa usalama wa mtoto katika ngazi ya kata na mitaa. Juhudi hizi zikifanyika zitachangia kupunguza tatizo la mimba za utotoni kutoka asilimia 27 hadi asilimia 8 ifikapo mwaka 2022 alisema Bw. Komba.

  Naye Mkurugenzi Mkazi Shirika la REPPSI Bibi. Edwick Mapalala amefafanua kuwa mafunzo haya yatasaidia kumwezesha mtoto wa kike aweze kuwa na maisha bora yenye usalama maana atahakikishiwa ulinzi na ndugu wa karibu katika familia, watoa huduma wanaomzunguka mtoto, na jamii yote kwa ujumla.
    
  “Mafunzo haya yataimarisha uaminifu wa madreva wa bodaboda kuzingatia umuhimu wa kuzuia na kupunguza matukio ya mimba za utotoni kwa watoto wa kike” alisema Bibi Edwick. 

  Aidha Mwenyekiti wa madreva bodaboda wilayani Tarime Bw. Paschal Joseph, ameishukuru Serikali kwa kuandaa mafunzo hayo pamoja na wadau mbalimbali na ameahidi kuwaheshimu, kuwalinda na kuwapa haki sawa watoto wa kike katika ngazi ya familia na jamii kwa ujumla. 

  Semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa  na mashirika yautetezi haki za watoto nchini wakiwemo UNICEF, Save the Children, Plan International  Tanzania, REPSSI na CDF na jumla ya washiriki 40 wamehudhuria mafunzo hayo kati ya vijana 1600 wanaojihusisha na uendeshaji wa Bodaboda  wilayani Tarime. 

  Mafunzo hayo yamefanyika ikiwa ni moja kati ya shughuli muhimu za maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike 2017 yenye kauli mbiu  inayosema “Tukomeza Mimba za Utotoni Tufikie Uchumi wa Viwanda’.  


  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Katikati) akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ndogo ya TAMISEMI – Dar es salaam baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Joseph Kakunda na kushoto kwake ni Naibu Waziri Mhe. Josephat Kandege
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (aliyesimama katikati) akizungumza na wafanyakazi wa TAMISEMI ofisi ndogo ya dar es salaama mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Katika Picha ya pamoja ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (pili kushoto aliyekaa, Mhe. George Joseph kakunda (kwanza kushoto aliyekaa) Naibu Waziri Mhe. Josephat kandege(Pili Kulia aliyekaa), Naibu katibu Mkuu –Elimu Tixon Nzunda pamoja na watumishi wa TAMISEMI ofisi ndogo ya  Dar es Salaam.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka watendaji wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kubadili utendaji wao wa kazi ili kupata matokeo bora katika kutoa huduma kwa wananchi.

  Akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya TAMISEMI mara baada ya kuapishwa amesema biashara ya kufanya kazi kwa mazoea haina nafasi na maemtaka kila mtumishi kubadilika na kufanya kazi kwa kujituma ili kupata matokea tarajiwa.

  Waziri Jafo amesema “ili tuweze kufikia malengo yetu kwa hataka na ufanisi wa hali ya juu naahidi kutoa  ushirikiano kwa kutosha kwa Manaibu Waziri waliochaguliwa na kuapishwa pamojanami leo hii, viongozi wengine wote wa Wizara, manajiment pamoja na watumishi wote.

  Akizungumza wakati wa kikao hicho Naibu Waziri wa OR- TAMISEMI Mhe. George Joseph kakunda amesema TAMISEMI ni injini ya Nchi na isipofanya vizuri hakuna Wizara nyingine itakayofanya vizuri kwa sababu unapozungumzia tamisemi unagusa wananchi na mengine yote yanayofanyika katika Wizara nyingine ni kwa ajili ya wananchi hawa wa TAMISEMI hivyo ni lazima tuweke mazingira bora na rafiki ili huduma hizo ziwafikie zikiwa na ubora wa hali ya juu.

  “Wizara hii ni muhimu sana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa sababu watekelezaji wa miradi mbalimbali wako katika mamlaka ya serikali za Mitaa hivyo tukifanya kazi kwa bidii na uaminifu hakika mafaniko yatakuja kwa haraka na hilo sisi ndio tunalolihitaji katika Serikali ya awamu ya Tano” alisema Mhe. Kakunda.

  Katika mabadiliko yaliyofanywa juzi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli Wizara ya TAMISEMI itaongozwa na Manaibu Waziri wawili ambao ni Mhe. George Joseph kakunda na Mhe. Josephat Sinkamba Kandege huku Waziri wa Wizaa hii akiwa ni Mhe. Selemani Said Jafo.


  0 0


  Na; Agness Moshi na Pascal Dotto-MAELEZO.

  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imepokea wataalamu 16 kutoka nchini Cuba kama moja ya mikakati yake ya kuboresha utoaji huduma za Afya ikiwemo kutoa huduma za kibingwa hapa nchini.

  Akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk.Mpoki Ulisubisya alisema kuwa Serikali imepokea madaktari bingwa 6, madaktari bingwa wa usingizi 2, madaktari wa wodi za wagonjwa mahututi 2, Daktari bingwa wa  upasuaji wa macho 1, mtaalamu mmoja wa radiolojia pamoja na wauguzi 10 wa vyumba vya wagonjwa mahututi.

  “Wataalam hawa mamekuja wakati muafaka, kwasababu kwa kipindi hiki hospitali ya Muhimbili inafanya maboresho ya utoaji huduma , hivyo nina amini uwepo wao hapa kwa miaka miwili, hautakuwa kwa ajili ya  kuboresha huduma au kusaidia wagonjwa tu , bali ni nafasi nzuri ya  kuwapa ujuzi na mafunzo  wataalamu wetu “,alisema Dk.Ulisubisya.

  Dk. Ulisubisya amesema kuwa uwepo wa wataalamu hao utaongeza nguvu kazi hususani kwenye utoaji huduma kwa wagonjwa mahututi kwani hospitali hiyo imeongeza vitanda vya wagonjwa mahututi kutoka vitanda 21 hadi 88.

  Dk. Ulisubisya ameongeza kuwa wataalamu hao watasaidia kupunguza msongamano kwenye wodi za wagonjwa mahututi pia kupunguza idadi ya wagonjwa kwenda nje kwa ajili ya matibabu kwani huduma za matibabu zitapatikana hapa nchini.

  Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof.Lawrence Museru  amesema kuwa, kutokana na uhaba wa wataalamu kwa kipindi hiki cha maboresho,Hospitali imetafuta wataalamu kutoka Cuba ili kuziba pengo hilo.

  Prof.Museru alisema kuwa kwa kipindi chote cha miaka miwili,wataalamu hao watatoa mafunzo kwa wataalamu wa hapa nchini ambao utawapa ujuzi na kuwasaidia katika maeneo ya utoaji huduma kama vile huduma za upasuaji macho,wagonjwa mahututi ,radiolojia ,na usingizi.

  Aidha,Dkt.Ulisubisya ametoa wito kwa Taasisi nyingine za Afya nchini,kuiga mfumo unaofanywa na hospitali ya taifa Muhimbili ili kusaidia kupunguza utegemezi serikalini katika kuboresha huduma za Afya.
  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeweka mikakati mbalimbali ya kuboresha  utoaji huduma ikiwa ni pamoja na kuongeza wodi za wagonjwa mahututi,Ununuzi wa vifaa tiba,kukarabati na kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka 13 hadi kufikia 20, pamoja na kukabiliana na changamoto ya rasilimali watu kwa kupelekeka wataalamu nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo.
  Katibu mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya(katikati) akieleza jambo wakati wa kuwakaribisha wataalamu 16 kutoka nchni Cuba wakiwemo Madaktari Bingwa 6 pamoja na Wauguzi wa Chumba cha uangalizi maalumu kwa wagonjwa mahutiti mapema leo Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam kushoto ni kiongizi mkuu wa matibabu nchini Tanzania Dkt. Maylen Lopezi na kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Cuba katika hafla ya kuwakaribisha katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefunga mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo” wilaya ya Shinyanga ambapo jumla ya wahitimu 238 wamefuzu mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa miezi minne.

  Sherehe za kufunga mafunzo hayo zimefanyika leo Jumatatu Oktoba 9,2017 katika viwanja vya Sabasaba mjini Shinyanga.Akizungumza katika sherehe hizo,Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutumia vyema mafunzo waliyoyapata huku akiwaasa kufanya shughuli za maendeleo ili kujiinua kiuchumi.

  Matiro aliwataka wahitimu hao kuunda vikundi vya ujasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia. “Mmejifunza mambo mengi,naomba muzingatie mlichojifunza,muwe wazalendo wa nchi yetu,kuweni mstari wa mbele kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa kuwafichua wahalifu na wale wote wanaoleta uvunjifu wa amani katika jamii”,aliongeza Matiro.
  Katika hatua nyingine alizitaka kampuni za ulinzi kutumia walinzi waliopitia mafunzo ya mgambo.

  Naye Mshauri wa Mgambo wa wilaya ya Shinyanga Meja Ford Mwakasege alisema washiriki wa mafunzo hayo mwaka huu wengi wametoka katika makampuni ya ulinzi.“Mafunzo haya yameanza Juni 5,2017 washiriki wakiwa ni 303 lakini leo wamehitimu 238 kati yao wanaume ni 193,wanawake ni 45,na yalikuwa yanaendeshwa na wanajeshi na wanajeshi wa kujitolea,wahitimu pia walishiriki zoezi la upandaji miti lililozinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga hivi karibuni”,alieleza Mwakasege.
  Aidha alisema miongoni mwa changamoto zilizopo ni ukosefu wa sare za jeshi la akiba na utoro kwa washiriki hali inayofanya wengi kutomaliza mafunzo.

  Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo,Chacha Warioba alisema miongoni mwa mambo waliyojifunza kuwa ni pamoja na matumizi ya silaha mbalimbali,kwata,rushwa,usalama wa taifa na zimamoto na uokoaji.

  Hata hivyo alisema changamoto kubwa kwao ni ukosefu wa ajira hivyo aliiomba serikali iwape kipaumbele katika ajira zinazojitokeza.
  Aliitaja changamoto zingine kuwa ni ucheleweshaji wa vyeti vya mafunzo na malipo duni kwenye makampuni wanakoajiriwa hivyo kuiomba serikali kutoa mwongozo wa kima cha chini cha mishahara kwenye makampuni.
  Mwandishi wetu,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri
  Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakiwa wamebeba silaha zao
  Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua gwaride
  Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
  Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
  Meza kuwa wakiwa wamesimama wakati wahitimu wakipita kwa mwendo wa polepole
  Wahitimu wa mafunzo hayo wakipita kwa mwendo wa taratibu/polepole mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
  Wahitimu wa kike wa mafunzo ya jeshi la akiba wakipita mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro
  Wahitimu wakitembea kwa mwendo wa polepole
  Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakipita kwa mwendo wa haraka
  Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakipita kwa mwenda wa haraka mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
  Mkufunzi wa mafunzo ya Jeshi la Akiba na MC wakati wa sherehe hizo,Sajenti Geofrey Kamala akitoa maelekezo
  Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
  Mhitimu Chacha Warioba akisoma risala
  Wahitimu wa mafunzo hayo wakiimba wimbo
  Wahitimu wakiimba shairi
  Wahitimu wakionesha mchezo wa Singe
  Burudani inaendelea
  Wahitimu wakionesha mchezo wa ngumi
  Mkufunzi wa mafunzo ya Jeshi la Akiba na MC wakati wa sherehe hizo,Sajenti Geofrey Kamala akifurahia burudani iliyokuwa inaendelea
  Wadau mbalimbali wakiwa eneo la tukio
  Mshauri wa Mgambo wa wilaya ya Shinyanga Meja Ford Mwakasege akitoa taarifa kuhusu mafunzo ya jeshi la akiba
  Mshauri wa Mgambo wa wilaya ya Shinyanga Meja Ford Mwakasege akizungumza
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo” wilaya ya Shinyanga
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga mafunzo mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo”. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo” 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na wakufunzi wa mafunzo hayo
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti katika shule ya msingi Uhuru iliyopo jirani na uwanja wa Sabasaba palipofanyika sherehe za kufunga mafunzo ya jeshi la akiba.
  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu, Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiwa katika kikao kifupi na baadhi ya Watendaji wa Ofisi yake mara baada ya kuapishwa IKULU jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya Watendaji walioshiriki kikao cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu, Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakipokea maelekezo kuhusu masuala mbalimbali kuhusu utumishi wa umma nchini.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu, Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiongoza kikao chake cha kwanza mara baada ya kuapishwa mapema leo IKULU jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu, Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao na Watendaji wa Ofisi yake  mara baada ya kuapishwa IKULU jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu, Mhe. George H. Mkuchika (Mb) kuongea na baadhi ya Watendaji wa ofisi yake jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Timu ya kata ya Ihembe imeibuka mabingwa wa Bashungwa Karagwe Cup 2017 baada ya kuifunga Nyaishozi mabao 2-1. Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Changarawe huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Mambo ya ndani Mheshimiwa Mwigulu Nchemba uliteka hisia za mamia ya wakazi wa jimbo la Karagwe waliojitokeza kwa wingi.

  Ihembe walikuwa wa kwanza kupata goli dakika 25 kupitia kwa Athumani Chuji aliepiga shuti kali la mpira wa adhabu uliomshinda golikipa wa Nyaishozi na kuingia wavuni. Bao hilo lilionekana kuwachanganya Nyaishozi ambao walionyesha kutoelewana katika eneo la ulinzi na kujikuta wakiruhusu bao la pili katika dakika ya 35 lililofungwa na Mshauri Kato aliewatoka walinzi wa Nyaishozi na kufunga goli la kiustadi. 

   Kipindi cha pili Nyaishozi waliuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 78 lililofungwa na mshambuliaji MC, hata hivyo jitihada za kusawazisha matokeo zilikwamishwa na mlinda mlango wa Ihembe alieokoa michomo mingi.

  Kufuatia ushindi huo Ihembe walijipatia kombe na kiasi cha fedha shilingi milioni moja na nusu huku Nyaishozi wakipata shilingi laki saba na nusu kama kifuta jasho kwa kushika nafasi ya pili. Akizungumza baada ya mchezo huo mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent Bashungwa alisema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila mwaka ili kuibua vipaji vya vijana wa Karagwe waweze kujiajiri kupitia michezo na kuahidi kuboresha mashindano yajayo kwa kusaka wadau wengine watakaohakikisha wilaya ya Karagwe inakuwa na timu bora ya kushiriki ligi kuu.

  Nae kocha bora wa ligi kuu msimu uliopita ambaye pia ni kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime aliyapongeza mashindano hayo na kuahidi mchezo wa kirafiki baina ya Kagera Sugar na kikosi cha wachezaji bora waliochaguliwa toka mashindano hayo.
  Mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent Bashungwa akimpokea mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba
  Mgeni rasmi akiwasili katika uwanja wa changarawe ilipofanyika fainali ya Bashungwa Karagwe Cup
  Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akikagua vikosi vya Ihembe na Nyaishozi
  Mchezaji wa Ihembe akipiga mpira wa kona
  Uwanja wa Changarawe ulihosheheni mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu
  Ihembe wakishangilia baada ya kupata bao la kwanza
  Wadau wakishuhudia mtanange toka jukwaa la “mzunguko”
  Wachezaji wa Ihembe wakiwa wamemzunguka golikipa wao baada ya kupata kash kash
  Mashabiki wa Nyaishozi wakifuatilia kwa makini mchezo wa Bashungwa Karagawe Cup
  Kombe likikabidhiwa kwa mgeni rasmi
  Mbunge wa Karagwe Mh. Innocent Bashungwa akitoa neno la pongezi kwa timu zote shiriki 
  Kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime akimkabidhi kombe nahodha wa Ihembe 
  Ihembe wakifurahia kombe lao la ubingwa wa Bashungwa Karagwe Cup
  Furaha na shangwe baada ya kutangazwa mabingwa

  0 0


  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Kushoto), akisalimiana na Naibu Waziri Eng. Atashasta Nditiye (Kulia), wakati alipomtembelea Waziri Mbarawa ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Dkt Leonard Chamuriho 
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akisalimiana na Naibu Waziri hiyo Mhe. Elias Kwandikwa wakati alipomtembelea Waziri Mbarawa ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. 
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Katikati) akizungumza na Manaibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Atashasta Nditiye (Wa pili kulia) na Mhe. Elias Kwandikwa (Wa tatu kulia), wakati walipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (aliyesimama) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), mara baada ya kuapishwa Jijini Dar es Salaam leo. 
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (aliyesimama) akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), leo Jijini Dar es Salaam kabla ya kikao kazi na Makatibu Wakuu wa wizara na baadhi ya Watendaji waliopo jiji Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akiwakabidhi manaibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Atashasta Nditiye (Kulia) na Mhe. Elias Kwandikwa wakati (Katikati) vitabu vya bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 ya Wizara hiyo kama mwongozo wa utendaji kazi mara baada ya kuapishwa jijini Dar es Salaam leo.

   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (Wa pili kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Joseph Nyamhanga (Kushoto) wakati alipokaribishwa katika ofisi za Wizara leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho na Wa pili kushoto Katibu Mkuu Dkt. Maria Sasabo (Sekta ya Mawasiliano).  Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wote katika sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kufanya kazi kwa uadilifu na ushirikiano katika kuwahudumia Watanzania ili kufikia malengo ya Wizara.

  Prof. Mbarawa ameyasema hayo jana katika mapokezi ya Manaibu Mawaziri wapya wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ofisini Jijini Dar Es Salaam baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Dar es Salaam.

  “Mimi nafurahi sana kufanya kazi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa sababu mimi na wafanyakazi tuko katika timu moja; tunafanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano. Katika kipindi cha miaka miwili tumefanikiwa kufikia malengo mbali mbali ya serikali mfano ujenzi wa reli ya kisasa na barabara “ Mhe. Mbarawa amesema.

   Akiwakaribisha Manaibu Mawaziri hao katika Wizara hiyo Prof. Mbarawa amesema yeye pamoja na wafanyakazi wote wa wizara wamefurahi kupata mawaziri wapya ambao watafanya nao kazi kwa pamoja katika wizara hiyo.
   “Sisi kama viongozi tunapaswa kuwa mfano katika utendaji wetu wa kazi ili kujenga imani na umoja na wafanyakazi wetu. Tunapaswa kufanya kazi kwa uadilifu, ushirikiano na umoja kwani haya ndio masuala ya msingi katika utendaji kazi,” Prof. Mbarawa amesema .

  Waziri amesema Wizara hiyo imefanya kazi nzuri na hili limewezekana kwa sababu sisi kama wizara tumezingatia maadili ya msingi katika utendaji wa kazi zetu, kuna timu nzuri ya watalaam ambao ni wachapa kazi, wana moyo wa kujituma na kazi zote walizozifanya zina matokeo mazuri. 

  Kazi nzuri imefanyika, nawaomba  waheshimiwa manaibu mawaziri tufanye kazi kama timu moja na watalaam wetu ili tuweze kufikia malengo ambayo tumejiwekea katika wizara yetu, amesisitiza Waziri Mbarawa.Kwa upande wake Naibu Waziri anayeshughulikia Eng. Atashasta Nditiye anayeshughulikia Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano amesema kuwa amejipanga kufanya kazi na kulete matokea chanya na kwa maendeleo ya nchi.

  “Nipo tayari kufanya kazi itakayoleta mabadiliko, tutaboresha miundombinu ili kuchochea kasi ya ukuaji wa viwanda na kila nitakachofanya ni utekelezaji wa yale amabayo Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anayatarajia,” amesema mhandisi Nditiye.

  Hii ni mara ya kwanza kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri tangu serikali yake iingie madarakani Novemba 2015.

  0 0

  -Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi akifungua Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini "B" huko Mahonda katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo.
  Baadhi ya Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini "B" wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Dk. Mabodi huko Mahonda.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano huo Balozi Seif Ali Idd akipiga kura katika uchaguzi wa CCM ngazi ya Wilaya ya Kaskazini "B" uliofanyika leo huko Mahonda katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo.

  Na Is-haka Omar, Zanzibar.

  CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar viongozi watakaochaguliwa kupitia Uchaguzi wa ngazi ya Wilaya ya Kaskazini “B” kichama Unguja kuwa mstari wa mbele kukemea vikali tabia ya makundi na safu za uongozi zenye nia ya kuhatarisha uhai wa CCM katika Wilaya hiyo.

  Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Wilaya hiyo wa kuwachagua viongozi wa nafasi mbali za ngazi hiyo huko Mahonda katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja.

  Alisema matarajio ya CCM ni kuona viongozi wanaochaguliwa katika uchaguzi huo wanachukia kwa vitendo uwepo wa baadhi ya makada wanaoendekeza makundi, Safu na rushwa ndani ya chama hicho.

  Dk.Mabodi alieleza kwamba msimamo wa CCM ni kuhakikisha Katiba, kanuni na miongozo inasimamiwa na kufuatwa ipasavyo ili kupata viongozi na makada wenye uwezo wa kuendeleza mafanikio ndani ya chama hicho kwa miaka mitano ijayo.

  Aidha aliwambia viongozi watakaopata nafasi ya kuchaguliwa kupitia uchaguzi huo wahakikishe wanajenga ngome imara ya kisiasa katika wilaya hiyo sambamba na kuwashawishi wapinzani waliomo katika Wilaya hiyo kujiunga na CCM kwani ndio chama pekee kinachojali maslahi ya wananchi wote.

  “Baada ya kukamilika uchaguzi huu wa ndani ya chama chetu tuna jukumu jingine la kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa Dola wa mwaka 2020 pamoja na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kama tulivyoahidi kwa wananchi.”, alisisitiza Dk. Mabodi.

  Aliwasihi makada watakaochaguliwa kuwa viongozi kushirikiana vizuri na makada wenzao ambao hawakupata fursa ya kuchaguliwa kwa lengo la kuendeleza misingi imara ya ukomavu wa kisiasa na Demokrasia iliyotukuka.

  Hata hivyo aliwapongeza wanachama hasa makada waliogombea nafasi mbali mbali kwa kutofanya kampeni za fujo, vurugu na kuchafuana hali aliyosema kuwa inaonyesha ishara njema ya kukamilika kwa uchaguzi huo bila kujitokeza mapungufu.

  Aidha alisema chama hicho baada ya uchaguzi huo kinakusudia kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa ngazi mbali mbali za chama hicho ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

  Naibu Katibu Mkuu huyo Dk. Mabodi aliwataka wanachi hasa wanachama wa chama hicho kupuuza kauli zinazotolewa na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif za kuwa ataapishwa kuwa Rais wa Zanzibar jambo ambalo haliwezi kutokea kwani Rais halali wa Zanzibar ni Dk. Ali Mohamed Shein mpaka mwaka 2020.

  Katika uchaguzi huo nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti wa Wilaya , Katibu wa Siasa na Uenezi, nafasi ya mkutano Mkuu wa Mkoa , nafasi ya Mkutano Mkuu wa taifa pamoja na nafasi ya Halmashauri kuu ya CCM Wilaya.

  0 0

   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Erick Shitindi (katikati) akimkabidhi bendera mmoja wa vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la vijana na wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Bi. Venerose Mtenga.
   Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Bi. Venerose Mtenga toka Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Erick Shitindi juu ya vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la Vijana na Wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi.
    Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Erick Shitindi akizungumza na baadhi ya vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la Vijana na Wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi kabla ya kuwakabidhi bendera mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Erick Shitindi (aliyevaa tai) akiwa katika picha ya pamoja na vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la vijana na wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.

  Na. Eliphace Marwa .

  JUMLA ya Vijana 31 wanatarajia kuiwakilisha Tanzania katika tamasha la dunia la vijana linalotarajia kufanyika Jijini Sochi nchini Urusi  kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 22 Oktoba mwaka huu.

  Akizungumza na ujumbe wa Vijana hao leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhiwa bendera ya Taifa,  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Erick Shitindi alisema tamasha hilo litakuwa na zaidi ya washiriki ishirini elfu kutoka nchi 150 Duniani kote.
   Shitindi aliwapongeza vijana hao kwa fursa ya kuiwakilisha Tanzania katika tamasha hilo na kuwaomba kuitumia vyema fursa hiyo kwa ajili ya kuiwakilisha vema na kutangaza uzuri wa nchi viongozi kwa mataifa mbalimbali.

  “Tamasha hili litatoa fursa kwenu vijana wa Tanzania na mtakapokuwa huko kuzungumzia mambo mazuri ya Tanzania na hasa kutangaza uzuri wa nchi yetu kwa vijana wa mataifa mengine” alisema Shitindi.
  Aidha Shitindi aliwaasa vijana hao kwa kutambua kuwa wanakwenda nchi ya ugenini na hivyo kuwa makini kwa kuwa  watakutana na watu mbalimbali wenye tabia, maadili na itikadi za mlengo tofauti tofauti za kisiasa, kijamii, kiutamaduni na kiuchumi.

  “ Kama mnavyofahamu Tanzania inasifika Duniani kote kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu na ni nchi yenye maadili safi, hivyo tunategemea nanyi mtaenda kuonyesha nidhamu ya hali ya juu huko ugenini” aliongeza Katibu Mkuu Shitindi.

  Shitindi aliwataka vijana hao kueleza uzuri na mandhari ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini ikiwemo Mlima Kilimanjaro, Mbuga za Serengeti na bonde la Ngorongoro ambalo ni moja kati ya maajabu saba ya dunia kuwa vipo na ni mali ya Tanzania na si vinginevyo.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Vijana Bi. Venerose Mtenga kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - ambaye ndiye mkuu wa msafara huo, alimuahidi Shitindi kuwa vijana hao watakuwa mabalozi wazuri kwa Tanzania.
  Lengo la tamasha hilo ni kuwakutanisha vijana kutoka nchi mbalimbali duniani ili kujenga mshikamano, kubadilishana uzoefu kidiplomasia, na uzoefu katika mbinu mbali mbali za maendeleo katika utandawazi”, alisema Venerose Mtenga .

  0 0

  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki, pamoja na Manaibu Waziri wa Wizara hizo wameripoti rasmi katika Ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam.

  Baada ya kuwasili katika Ofisi hizo, Mawaziri hao  walifanya kikao cha pamoja ili kufahamishana masuala mbalimbali. Kikao hicho kiliwahusisha pia  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. James Mdoe na Naibu Katibu Mkuu, Dkt Mhandisi, Juliana Pallangyo.

  Aidha,  Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo walifanya  kikao na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. James Mdoe, Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na Kamishna Msaidizi wa Madini, Latifa Mtoro.

  Viongozi hao wanaosimamia Sekta ya Madini, wanatarajia kufanya kikao na watumishi wa Wizara husika tarehe 10 Oktoba, 2017.Kwa upande wake, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu walikutana na Wafanyakazi wa Wizara husika na kutoa maagizo mbalimbali yatakayoboresha Sekta ya Nishati na hasa upatikanaji wa Umeme wa uhakika, unaotabirika na wa bei nafuu.
   Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kulia), Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki (wa pili kushoto),  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa kwa kushoto) wakiwa katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) wakiwa katika kikao na Watumishi wa Wizara husika katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) na  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) wakiwa katika kikao na Watumishi wa Wizara husika (hawapo pichani )katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki (wa kwanza kulia),  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati), Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. James Mdoe (wa kwanza kushoto) wakiwa katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na Kamishna Msaidizi wa Madini, Latifa Mtoro.

  0 0


  Na Mwandishi Maalumu, Riyadh- Saudi Arabia

  Kundi la madaktari bingwa 18 wa hiyari kutoka nchini Saudi Arabia linatarajiwa kuwasili tarehe 12 Oktoba ambapo wataweka kambi ya tiba (medical camp) kwa muda wa majuma miwili. Madaktari hao wanatarajiwa kufanya matibabu na upasuaji katika hospitali za kisiwa cha Pemba.

  Akizungumza katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Riyadh wakati wa hafla ya kuagana na madaktari hao, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza, alisema kambi tiba hii ni ya pili kufanyika Zanzibar. Mwezi Novemba mwaka 2016 madaktari hao walifika Zanzibar na kuweka kambi ya kwanza katika kisiwa cha Pemba kwa mara ya kwanza kwa mafanikio makubwa.

  Mwaka jana madaktari hao walipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Afya ya Zanzibar na madaktari wenyeji, ndio maana wamependelea kurejea tena mwaka huu.

  Pamoja na kutoa huduma za matibabu, madaktari hao watakwenda na dawa na vifaa tiba vya aina mbalimbali ambavyo Mwisho wa kambi watavitoa kama msaada kwenye hospitali hizo.
  Katika picha ni viongozi wa Madaktari wakiwa na Balozi Hemedi Mgaza na Afisa wa Ubalozi Bw. Ahmada Sufiani walipofika Ubalozi mjini Riyadh kujitambulisha.

  0 0

  Watu 12 wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya daladala waliyokuwa wakisafiria, kutumbukia katika fukwe za Ziwa Victoria katika eneo la Kingo Feri wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.


  Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa tano asubuhi baada ya daladala hiyo yenye nambari za usajili T.229 DDW Toyota Hiace iliyokuwa ikitokea Buhongwa Jijini Mwanza kwenda kivukoni hapo kudaiwa kukatika breki ikiwa kwenye mwendo kasi.

  0 0
older | 1 | .... | 1394 | 1395 | (Page 1396) | 1397 | 1398 | .... | 1897 | newer