Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

ZAIDI YA SH. BILIONI 70 ZATUMIKA KWA AJILI YA MIUNDOMBINU NA MITAMBO YA TCAA.

0
0

 Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga , Dk. Daniel Kerenge akitoa historia ya chuo hicho katika utaoaji mafunzo mbalimbali ya usafiri wa anga jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kozi mbalimbali kwa wanafunzi wa Wizara ya Ulinzi ya Uganda waliokuja kupata mafunzo katika chuo  cha mafunzo cha usafiri wa anga jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Huduma za Usafiri wa Anga wa TCAA,John Chambo akizungumza juu ya ununuzi wa mitambo mbalimbali ya kisasa watayofunga kwa ajili ya uongozaji ndege , jijini Dar es Salaam.
kulia ni Meneja wa Usafiri wa Anga uwanja wa ndege wa Kimataifa Julius Nyerere wa TCAA, Mwanajumaa Kombo.
Sehemu mitambo ya kupata taarifa za ndege zinazoingia nchini na zile zinazotumia anga ya Tanzania.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga (TCAA) kutumia zaidi ya sh.bilioni 70 kwa ajili ya miundombinu ya mitambo ya  kisasa itakayowezesha utekelazaji wa watumiaji wa usafiri anga kutumia miundombinu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya kutembelea miundombinu mbalimbali katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ndege wa TCAA, John Chombo amesema miundombinu ya mitambo hiyo ni kwa ajili kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na teknolojia iliyopo kwa sasa katika usafri wa wa anga.

Amesema mitambo hiyo ikifungwa kazi itarahisha kwenda kisasa katika usalama wa ndege katika viwanja ndege kwa zile zinazoingia na kutoka katika anga ya nchini.

Chombo amesema miundombinu ya  mitambo mbalimbali  ya kuongozea ndege iliyopo bado inahimiri katika uongozaji wa ndege kinachofanya kununua ni kutokana na teknolojia iliyopo sasa ikiwa ni pamoja na uimarishaji huduma za usafiri wa anga.

Aidha amesema mitambo katika usafiri wa anga ni miaka 10 hivyo kila baada miaka hiyo inahitaji kubadilisha ili kwenda na mazingira yaliyopo pamoja na teknolojia iliyopo sasa inabadilika wakati kwa kuzingatia ni usalama wa ndege zinazoingia na kutoka.

Wakati huo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari amefungua mafunzo kwa wanafunzi 24 wa Wizara ya Ulinzi ya Ulinzi ya Uganda katika kituo cha mafunzo cha usafiri wa anga cha TCAA.
Amesema nchi ya Uganda imekuwa ikileta watu wake katika kupata mafunzo mbalimbali ya usafiri wa anga kituo hicho kwani hivi karibuni walihitimu wanafunzi 17 katika kituo hicho wa mamlaka ya usafiri wa anga wa Uganda.

WATOTO 28 WAFANYIWA UPASUAJI WA MOYO WA KUFUNGUA KIFUA NA BILA KUFUNGUA KIFUA KATIKA KAMBI MAALUM YA UPASUAJI KWA WATOTO INAYOFANYWA NA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA MENDING KIDS LA NCHINI MAREKANI

0
0



Afisa Muuguzi wa chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Veronica Vedastus na Arianna Minghetti wa Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakimnywesha maziwa mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo bila ya kufungua kifua (Catheterization) katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo. Watoto wanaofanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ni wale waliozaliwa na magonjwa ya moyo kuwa na tundu na mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri.
Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kufungua kifua na kuziba tundu la moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo . Jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao 19 upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Shirika la Meding Kids la nchini marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) na kuzibua mishipa ya Moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo . Jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao 19 upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.
Maafisa Uuguzi wa chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwezao wa Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakijadiliana kuhusu maendeleo ya wagonjwa waliolazwa katika chumba hicho baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo. Watoto wanaofanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ni wale waliozaliwa na magonjwa ya moyo kuwa na tundu na mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri.Picha na JKCI

RC SHIGELLA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA KUU LA 47 LA WAFANYAKAZI WA TANESCO NCHINI MJINI TANGA LEO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akifungua Baraza kuu la 47 la Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini Tanzania (Tanesco) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Tanga kulia ni Katibu wa Baraza hilo,Asmaa Myale
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme la Tanzania (Tanesco) Dkt  Tito Mwinuka akitoa hutuba yake wakati wa ufunguzi huo uliofanyika mjini Tanga 
Mwenyekiti wa Tuico Taifa,Paul Sangeze akizungumza wakati wa Baraza hilo kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco,Dkt Tito Mwinukakatika mkutano huo uliofanyika mjini Tanga 
Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale akizungumza katika mkutano huo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)Dkt Tito Mwinuka na Mwenyekiti wa wa Tuico Taifa,Paul Sangeze
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kushoto akipongezwa na Mwenyekiti wa Tuico Taifa,Paul Sangeze mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza kuu la 47 la wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini Tanzania (Tanesco) leo mjini Tanga anayeshughudia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito Mwinuka kushoto ni Katibu wa Baraza kuu la wafanyakazi,Asmaa Myale.
Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martin Shigella .
Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakiufuatilia kwa umakini 
Wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia kwa umakini mkutano huo
Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco Tanzania,Leila Muhaji wa pili kushoto aliyevaa koti jeusi akichukua baada ya dondoo wakati Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella alipofungua Baraza Kuu la 47 la Wafanyakazi wa Tanesco nchini mjini Tanga 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kulia akitoa nje ya ukumbi mara baada ya kufungua baraza hilo kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)Dkt Tito Mwinuka katikati ni Mwenyekiti wa TUICO Taifa Paul Sangeze 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Tanesco kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito Mwinuka kushoto ni Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale mara baada ya kufungua mkutano wa baraza kuu la 47 la wafanyakazi wa Tanesco
Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika hilo mara baada ya kufungua baraza kuu hilo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Dkt Tito Mwinuka kushoto akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza Kuu la 47 la Wafanyakazi wa Tanesco
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tenesco,Dkt Tito Mwinuka akiuzungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa baraza hilo leo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella 
Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale akizungumza na waandishi wa habar,Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

WAZIRI MAKAMBA ATEMBELEA OFISI ZA URATIBU ZA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba hii leo amefanya ziara ya kikazi kutembelea Ofisi za Uratibu wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zilizopo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.

Katika Ziara hiyo Mhe. Makamba amepata fursa ya kuongea na Menejimenti ya Ofisi hiyo na kupata wasaa wa kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kuimarisha ushirikiano zaidi baina yao.

Awali, akimkaribisha Waziri Makamba, Mratibu Mkuu Bw. Issa Mlingoti amemshukuru Waziri Makamba kwa kufika na kuahidi kuimarisha ushirikiano katika nyanja za Elimu, ajira na fursa kwa pande zote za Muungano.

"Sisi tumefarijika sana kwa ujio wako na tunategemea kuwa huu ni mwanzo na mwelekeo mzuri wa kuzidi kuimarisha mashirikiano baina yetu ikiwa sisi ni waratibu wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar" Alisisitiza Bw.Mlingoti

Katika ziara hiyo Waziri Makamba alipata fursa ya kuongea na wafanyakazi, kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuahidi kuzipatia ufumbuzi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa katika kikao wa watumishi wa Ofisi ya Uratibu - Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Waziri Makamba amepata wasaa wa kuzungumza na Menejimenti na watumishi wa Ofisi hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mtaa wa Luthuli.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Uratibu - Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri January Makamba mara baada ya kutembea Ofisi zao zilizopo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.

Wakazi Dar Kunufaika na Huduma ya Dawati la Mhasibu

0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) Dkt. Fred Msemwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma ya Dawati la Mhasibu itakayofanyika tarehe 07 Oktoba 2017 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Dyoya James Dyoya na Afisa Mtendaji Mkuu wa TAA Bw. Patrice Sigungu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) Dyoya James Dyoya (kushoto) akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma ya Dawati la Mhasibu itakayofanyika tarehe 07 Oktoba 2017 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TAA Bw. Patrice Sigungu na Mweneyekiti wa chama hicho Dkt. Fred Msemwa.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina yao na viongozi wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) leo jijini Dar es Salaam.
Picha na: Idara ya Habari – MAELEZO


Na: Frank Shija – MAELEZO

Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) kimeanzisha huduma ya Dawati la Mhasibu itayaofanyika kwa mara ya kwanza tarehe 07 Oktoba 2017 kuanzia saa 3: 00 asubuhi katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaaam.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. Fred Msemwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na huduma hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Msemwa amesema kuwa kupitia Dawati hilo wahasibu, wataalam wa kodi, fedha na biashara watajumuika pamoja na kukutana na wananchi wa kawaida, wafanyabiashara wadogo na wakubwa na kuwapatia huduma bure.

“Kupitia Dawati hili la Mhasibu litatukutanisha na wadau wengine wa masuala ya biashara na ujasiriamali hili kwa pamoja tuweze kutoa huduma za mbalimbali za kijasiriamali zianazohusisha masuala ya mahesabu bila ya malipo” alisema Dkt. Msemwa.

Alizitaja huduma zitakazotolewa kupitia Dawati hilo kuwa ni pamoja na jinsi ya kusimamia biashara endelevu, namna ya kuandika andiko kwa ajili ya kupata mikopo na elimu ya kodi.Huduma zingine ni mikataba ya biashara, usimamizi wa biashara za familia, utunzaji wa kumbukumbu za fedha ambapo huduma zote zitatolewa bila malipo yoyote na hakuna kiingilio.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama hicho Dyoya James ametoa wito kwa wanataaluma za uhasibu na masuala ya kodi kujitokeza kwa wingi ili kuwezesha kufikiwa kwa lengo la utoaji wa huduma kwa wananchi watakaojitokeza.

Pia ametoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kutumia fursa hiyo adhimu kujitokeza kwa wingi katika viwanjwa vya Mnazi Mmoja ili waweze kunufaika na huduma ya Dawati la Mhasibu kwa kukutana na wataalamu mbalimbali watakaowafundisha mambo mbalimbali.

Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) ni chama cha kitaaluma kilichoanzishwa mwaka 1983 kwa ajili ya kuendeleza taaluma ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu Tanzania. Tanzania.

MAVUNDE ATIA FORA MKUTANO MKUU CCM WILAYA

0
0
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza katika mkutano Mkuu wa uchaguzi CCM wilaya ya Dodoma mjini.mavunde (2)
Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi CCM wilaya waliohudhuria
mavunde (3)
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Dodoma mjini aliyemaliza muda wake Paulo Luhamo akifungua mkutano Mkuu wa uchaguzi leo.
mavunde (4)
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Christine Mndeme katika Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa wilaya.
mavunde (5)
Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi CCM wilaya waliohudhuria
mavunde (6)
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akifurahi jambo katika mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa wilaya.
…………
MBUNGE wa Dodoma mjini Anthony Mavunde ameeleza mikakati iliyopo katika kukifanya Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Dodoma kiweze kujitegemea kuwa ni mpango wa ujenzi wa jengo la ghorofa nane ambalo litakuwa jibu katika kuinua uchumi.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa uchaguzi leo uliofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Hall wilayani Dodoma, Mavunde amesema pamoja na mpango huo ni vyema wana CCM wakawa na umoja.
Aidha amewataka kuendeleza mbegu inayoachwa na viongozi wanaomaliza muda wao kwa kufanya kazi kwa umoja,upendo na mshikamano ili hatimaye matunda mazuri ya mbegu iliyopandwa yaweze kuonekana.
“Ndugu zangu tukimaliza uchaguzi mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mwingine na ukitaka kushinda lazima uwe na  mpango wa kisiasa kwak ufanya mikutano ngazi ya kata na katika hili mimi kama mbunge kuanzia mwakani nitagawa vipasa sauti vitatu na spika za kusimama kwa kila kata ili kuwezesha kufanyika mikutano hiyo na baadae nitaangalia suala la usafiri,”amesema Mavunde.
Amewaomba wajumbe wa mkutano huo kuendelea kumshukuru na kumpongeza Rais Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuivunja mamlaka ya ustawishaji makao makuu(CDA) ambayo ilikuwa ni kilio cha wakazi wa Dodoma na kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM aliyemaliza muda wake wilaya ya Dodoma mjini Paulo Luhamo amewataka wajumbe kuzingatia maagizo ya chama kwa kutochagua mtu kwa ajili ya ukabila,dini wala rangi.
 “WanaCCM wenzangu chagueni kiongozi atakayetoka ndani ya CCM na sio nje ya CCM,atakayefanyia kazi maamuzi ya CCM,na mimi pamoja na kwamba nitakuwa nje ya uongozi nitashirikiana na uongozi mpya usiku na mchana,mvua na jua ili kulinda heshima ya Dodoma kuwa makao makuu ya Chama na Serikali,”amesisitiza Luhamo.
Amewataka wana CCM kuachana na utaratibu waliokuwa nao wa kubadilisha mbunge kila baada ya miaka mitano na badala yake wamempa heshima Rais kwa kuendelea kumchagua Mavunde kama mbunge wao,kumlinda na kumuombea.
“Mbunge wetu anafanya kazi kubwa kwa ajili ya CCM,sisi tumekuwa na utaratibu wa kuleta mbunge kila baada ya miaka mitano tuache utaratibu huu,rais ametupa heshima ya kumchagua Mbunge wetu katika baraza la mawaziri heshima ambayo mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1975,hivyo kama rais ametupa heshima hiyo nasi tuilinde,”amesema Luhamo.
Wagombea wanaogombea nafasi ya Mwenyekiti ni pamoja na Adam Msendo, Stephen Mwanga na Robert Mwinje.

Bodi ya Sekretarieti ya Ajira Yatakiwa kuisaidia Serikali Katika Ajenda ya Viwanda

0
0
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimentiya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akihutubia katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Sekritarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma pamoja na Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa ofisi hiyo uliofanyika Maktaba Kuu ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurent Ndumbaro.
Katibu wa sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma Bw. Xavier Daudi akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimentiya utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki jinsi ya ufanyaji kazi wa menejimenti hiyo katika uzinduzi wa Bodi mpya uliofanyika leo katika Maktaba Kuu ya Taifa Jijini Dar es Salaam kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimentiya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki na pili kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurent Ndumbaro
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurent Ndumbaro akitoa salama na kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi Sekritarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma pamoja na Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa ofisi hiyo uliofanyika Maktaba Kuu ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam kutoa kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimentiya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki na pili kushoto ni Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi.
 
Mwenyekti wa Bodi mpya ya Sekritarieti ya Ajira katika utumishi wa umma Bi.Rose Lugembe katika uzinduzi wa tatu wa bodi pamoja na mkataba wa huduma kwa mteja uliofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo Maktaba Kuu ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam kulia ni moja ya wajumbe wa bodi hiyo Bw.Mbaraka Abdul Wakill.Picha na Paschal Dotto-MAELEZO



Na Thobias Robert- MAELEZO

Bodi mpya ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetakiwa kusimamia vyema majukumu yake ya upatikanaji wa rasimali watu wenye weledi, sifa na haiba ambao wataisaidia serikali katika kufikia azma yake ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025.

Agizo hilo limetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Angelah Kairuki alipokuwa akizindua bodi hiyo Jijini Dar es Salaam na kuitaka kuendesha kazi zake kwa uwazi na kwa kuzingatia Sheria kanuni na taratibu.

“Mmeteuliwa katika kipindi cha miaka michache kabla ya Taifa letu kufikia mwaka 2025 ambapo tunalenga kuingia kwenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda hivyo mnalo jukumu kubwa la kulipatia taifa rasilimali watu yenye uwezo wa kutuwezesha kutimiza malengo hayo,” alifafanua Waziri Kairuki. 

Waziri Kairuki alisema kuwa, katika kutekeleza majukumu yake bodi haina budi kutenda haki ili kuepuka malalamiko ya upendeleo wa aina yoyote, kujuana, ukabila, na ukanda ambavyo vimekuwa vikitolewa dhidi ya bodi ya Sekrtarieti ya Ajira,na kuwataka kuandaa mpango mkakati ambao ukitumika kila mwombaji wa ajira ataridhika.

Aidha, Mh.Kairuki alisema kuwa, bodi inapaswa kusimamia Sheria, taratibu na kanuni za ajira zilizowekwa hapa nchini ili kulisaidia taifa kupata nguvu kazi itakayokidhi mahitaji ya waajiri na ambayo italisaidia taifa kupiga hatua za kimaendeleo.

“Ili kutekeleza kwa vitendo falsafa ya HAPA KAZI TU, Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga utamaduni wa watu kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kufanya kazi kwa bidii, weledi, na kuzingatia maadili. Hivyo ni wajibu wa Wajumbe wa Bodi kushiriki kikamilifu katika kufanikisha azma hii kwa kuisaidia serikali kupata watumishi waadilifu,” alisisitiza Waziri Kairuki.

Mh. Kairuki amesema kuwa Sekrtarieti hiyo haina budi kutumia njia za kiteknolojia ili kuwafikia waombaji wengi wa nafasi za kazi waliosambaa kote nchini ili kuwapunguzia gharama za kupeleka maombi yao makao makuu pekee yake, na wakati wa kufanya usaili ambapo waombaji wa mikoani wanalazimika kuja Dar es Salaam, hivyo akashauri usaili uwe unafanyika katika ngazi za mikoa.

Awali akisoma taarifa ya utendaji na utekelezaji wa majukumu wa taasisi hiyo Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi alieleza kuwa, tangu kuanzishwa kwake, taasisi imefanikiwa kujenga mifumo ya mbalimbali ya TEHAMA kwa lengo la kurahisisha uapashanaji wa habari na kuboresha mchakato wa ajira na kurahisisha utendaji kazi.

Aidha Sekretarieti hiyo imefungua tovuti ya ajira (www.ajira.go.tz) , pamoja na kurasa katika mitandaio ya kijamii kama vile facebook, twitter na youtube kwa lengo la kuapanua wigo wa mawasiliano kwa waajiri na waombaji wa ajira hapa nchini.

Alieleza kuwa taasisi hiyo imekuwa na utaratibu wa kuwasiliana na vyuo vya elimu ya juu na vyuo vingine ili kuwa naidadi ya wanafunzi wanaohitimu vyuoni hivyo kurahisisha usaili paindi ajira zinapotangazwa.

“Kukua kwa teknolojia nchini na duniani kumewafanya baadhi ya wadau kuitumia vibaya mitandao hasa ile ya kijamii hadi kufikia hatua ya baadhi ya watu kwa utashi wao usiojali maslahi ya serikali na wananchi na kuamua kuandaa matangazo ya uongo kwa kujifanya Sekretarieti imetangaza ajira kwa kutumia mitandao ya kijamii jambo ambalo ni upotoshaji,” alieleza Bw. Daudi kama changamoto inayoikumba taasisi hiyo.

Kwa uapnde wake Mwenyekiti mteulie wa bodi hiyo Bi. Rose Lugembe alileza kuwa, watafanya kazi kwa umakini, weledi pamoja na kuzingatia maadili ya kazi ili kurahisisha upatikanaji wa rasilimali watu. 

Bodi hii ni yata tu tangu kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira mwaka 2009, sekretarieti hii ilianzishwa kwa lengo la kuendesha mchakato wa ajira katika utumishi wa Umma ili kuziwezesha mamlaka za ajira kupata nafasi ya kutekeleza majukumu yake ya msingi kama yalivyoainishwa katika hati zinazoanzisha taasisi hizo.

DC SHINYANGA AFUNGUA MAFUNZO YA TATHMINI YA UWEZO KANDA YA SHINYANGA

0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefungua mafunzo ya “Tathmini ya Uwezo” kanda ya Shinyanga ikiwa ni jitihada inayofanywa na shirika la Twaweza kwa lengo la kupima uwezo wa watoto juu ya umahiri wao wa kusoma,kuhesabu na kuandika.

Mafunzo hayo yanayofanyika kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga,yameanza leo Alhamis Oktoba 5,2017. 
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo,Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akisema washiriki wa mafunzo hayo ni waratibu wa wilaya na waratibu wa vijiji kutoka wilaya nane za kanda ya Shinyanga inayojumuisha mikoa ya Dodoma,Singida,Simiyu na Shinyanga.

“Mafunzo ya tathmini ya Uwezo yanafanyika nchi nzima na kwa upande wa kanda ya Shinyanga,yanafanyika hapa ambapo tunafundisha mbinu na taratibu za kufanya wakati wa kutekeleza zoezi la Tathmini ya Uwezo kwenye wilaya mbalimbali nchini Tanzania na mwaka huu zoezi litafanyika katika wilaya 56”,alieleza Mgoi.

Alisema washiriki wa mafunzo hayo watafundishwa namna ya kufanya tathmini kuhusu uwezo wa watoto wenye kuanzia miaka 6 hadi 16 katika masomo matatu ya Kiingereza,Kiswahili na Hesabu.
Aliongeza kuwa Twaweza kupitia tathmini ya uwezo imekuwa ikishirikiana na serikali katika kuboresha elimu nchini.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la OPE ambalo ni mdau wa Uwezo,William Shayo alisema lengo la msingi la Uwezo ni matokeo ya kujifunza kwa watoto na swali linaloulizwa kila siku ni “Je watoto wetu wanajifunza”.

“Tunatathmini uwezo ujuzi wa watoto katika kusoma na kuhesabu,lakini pia kusambaza matokeo ya utafiti sehemu kubwa kwa wananchi,wazazi,walimu na serikali hali hii inasababisha wananchi wachukue hatua za kuboresha ngazi za ujifunzaji za watoto kwenye jamii”,aliongeza.

Akifungua mafunzo hayo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema serikali inatambua kazi nzuri zinazofanywa na taasisi katika kuboresha sekta ya elimu na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nao.
Aidha Matiro aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kutoa taarifa kwa serikali kuhusu mambo watakayoyabaini wakati wa tathmini yao ili kuisaidia serikali kuboresha elimu katika maeneo yenye changamoto.

“Mkimaliza kufanya tathmini mtuletee uhalisia,msituonee aibu kutuambia,tunahitaji kujua uhalisia wa mambo kwamba watoto kweli wanaelewa?wanajua kusoma? Hesabu wanazijua?,Mkileta tafiti zenu kwa uhalisia itakuwa rahisi kwa wadau mbalimbali ikiwemo serikali kupata ufumbuzi wa matatizo katika elimu kwa ajili ya kusaidia watoto”,aliongeza Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo amefungua mafunzo ya “Tathmini ya Uwezo” kanda ya Shinyanga katika ukumbi wa Karena Hotel leo Alhamis Oktoba 5,2017-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa siku tatu.
Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akielezea kuhusu Tathmini ya Uwezo
Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akizungumza ukumbini.
Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akisisitiza jambo.
Mkurugenzi wa Shirika la OPE ambalo ni mdau wa Uwezo,William Shayo akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Mkurugenzi wa Shirika la OPE,William Shayo akielezea namna shirika lake linavyoshirikiana na Twaweza kupitia zoezi la Tathmini ya Uwezo katika kuboresha elimu kwa watoto.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Mafunzo yanaendelea
Mafunzo yanaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Anandumi Ndosi akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Mshiriki akinyoosha mkono ili aulize swali.
Washiriki wakifurahia jambo ukumbini.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Anandumi Ndosi akizungumza ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
Picha ya pamoja,washiriki wa mafunzo hayo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.
Picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

MEYA WA JIJI LA DAR ISAYA MWITA AKUTANA NA TAASISI INAYOSHUGHULIKIA MASUALA YA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI DUNIANI

0
0
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kufanya mazungumzo na ugeni kutoka Taasisi inayoshughulikia masuala ya mabadiliko ya Tabia ya Nchini Dunia (C40 CITIES) ofisi kwake Karimjee,wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia kutoka Jijini London Simon Hansen.
 Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia kutoka Jijini London Simon Hansen akizungumza wandishi wa habari leo mara baada ya kufanya mazungumzo na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita aliyesimama katikati, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko. 
 Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya mazungumzo na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaa Isaya Mwita ,kushoto Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia kutoka Jijini London Simon Hansen. 
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati akiwa pamoja na ugeni kutoka Taasisi inayoshughulikia masuala ya mabadiliko ya Tabia ya Nchini Dunia (C40 CITIES) wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia kutoka Jijini London Simon Hansen, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko.Picha zote na Christina Mwagala, Ofisi ya Meya wa jiji.

UHURU FM WAANZA LEO KUMBUKIZI YA BABA WA TAIFA KWA KUSAIDIA YATIMA KATIKA KAMPENI YAO YA 'GUSA MAISHA YAKE'

0
0
 Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali, akikabidhi msada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula kwa Msimamizi Mkuu wa Kituo cha kulelea Watoto yatima na wasio chini ya malezi ya wazazi wao cha CHAKUWAMA, Hassani Hamis, Wafanyakazi wa Uhuru FM walipofika kituoni hapo, Sinza Jijini Dar es Salaam, leo, kutoa msaada katika kampeni ya "Gusa maisha yake" iliyoanzishwa na kituo hicho cha radio ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere. kulia ni Mtangazaji wa Uhuru FM Aggrey Manzi na wanne kulia ni Meja Rasilimali Watu na Utumishi wa Uhuru FM Paul Mng'ong'o. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

SAFARI KUTOKA OFISI ZA UHURU FM MTAA WA KARIAKOO NA UKAMI KWENDA SINZA ILIPOANZA
 Wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa tayari kupanda basi kwa ajili ya safari ya kwenda kwenye Kituo cha kulelea Watoto yatima na wasio chini ya malezi ya wazazi wao cha CHAKUWAMA, Sinza Jijini Dar es Salaam, kutoa msaada katika kampeni ya "Gusa maisha yake" iliyoanzishwa na kituo hicho cha radio ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa
 Wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa tayari kupanda basi kwa ajili ya safari ya kwenda kwenye Kituo cha kulelea Watoto yatima na wasio chini ya malezi ya wazazi wao cha CHAKUWAMA, Sinza Jijini Dar es Salaam, kutoa msaada katika kampeni ya "Gusa maisha yake" iliyoanzishwa na kituo hicho cha radio ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa
 Mpihapicha wa Uhuru FM Online TV akiwajibika wakati wa safari hiyo kwenda Sinza
 Dereva akiwa tayari kwa safari
 Wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa katika basi kwenda Sinza baadhi yao wakitaniana kidogo
 Wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa katika basi kwa mapozi mbalimbali kwa ajili ya safari ya kwenda kwenye Kituo cha kulelea Watoto yatima na wasio chini ya malezi ya wazazi wao cha CHAKUWAMA, Sinza Jijini Dar es Salaam, kutoa msaada katika kampeni ya "Gusa maisha yake" iliyoanzishwa na kituo hicho cha radio ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa
 "NDIYO TUMEANZA SAFARI" Murugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali (kulia) akiwasiliana, wakati yeye na wafanyakazi wenzake wa Uhuru FM wakiwa katika basi kwa ajili ya safari ya kwenda kwenye Kituo cha kulelea Watoto yatima na wasio chini ya malezi ya wazazi wao cha CHAKUWAMA, Sinza Jijini Dar es Salaam, kutoa msaada katika kampeni ya "Gusa maisha yake" iliyoanzishwa na kituo hicho cha radio ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa
 Steven Mhina Dungumalo (kushoto) akionekana kuwa mwenye furaha  wakati yeye na wafanyakazi wenzake wa Uhuru FM wakiwa katika basi kwa ajili ya safari ya kwenda kwenye Kituo cha kulelea Watoto yatima na wasio chini ya malezi ya wazazi wao cha CHAKUWAMA, Sinza Jijini Dar es Salaam, kutoa msaada katika kampeni ya "Gusa maisha yake" iliyoanzishwa na kituo hicho cha radio ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa. Pamoja naye ni Furaha Ruhende
 Mhariri wa habari wa Uhuru FM Pius Ntiga (kulia) ambaye alitangulia kuwasili kwenye kituo hicho cha kulele watoto yatima na wasiokuwa chini ya malezi ya wazazi wao, akiwa tayari kupokea wafanyakazi wenzake mda mfupi kabla hawajawasili. Kituo hicho cha kulelea watoto kipo mtaa wa Ngamia, Sinza
 Timu ya wafanyakazi wa Uhuru FM wakionekana baadhi yao kutafakari jinsi watakavyofanikisha utoaji msaafa kwa watoto wa kituo hicho cha kulelea watoto, Sinza
 DJ Machachari wa Uhuru FM Dast Edie akitia pozi baada ya kushuka kwenye basi
 Mtangazaji wa Uhuru FM Sigori akishuka na furushi la zawadi
 Angel Akilimali na mwenzake baada ya kushuka kwenye gari
 Kituo cha CHAKUWAMA
 Wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa na wadau wengine nje ya kituo hicho wakisubiri kukaribishwa
 Mwandishi wa Channel Ten akisalimiana na Mwandishi wa Uhuru FM Joyce Njarabi baada ya kukutana kwenye eneo la tukio. kulia ni mwandishi wa Uhuru Publications Ltd, Njumai Ngota na kushoto ni Steven Mhina wa Uhuru FM
 Mwandishi wa Channel Ten Said Makala akinong'onezwa jambo na Sheila Simba wa Uhuru FM wakati wa shughuli hiyo. Kushoto ni Steven Mhina wa Uhuru FM
 Vitu mbalimbali vikiwemo vyakula vikiwa vimeandaliwa kwa ajili ya msaada huo
 Watangazaji wa Uhuru FM Steven Mhina na Sheila Simba wakiwa tayari kutangaza Mbashara tukio hilo la  utoaji msaada
 Msimamizi Mkuu wa Kituo cha kulelea Watoto yatima na wasio chini ya malezi ya wazazi wao cha CHAKUWAMA, Hassani Hamis (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhiwa msaana huo
 Mwenyekiti wa maandalizi ya utoaji msaada huo Joyce Njarabi wa Uhuru FM akizungumza kabla ya makabidhiaano ya msaada huo
 Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo
 Mmoja wa watangazaji wa Uhuru FM akiwa amembeba mtoto wa kituo hicho cha kulelea watoto
 Baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa na watoto wa kituo hicho cha kulelea watoto
 Furaha Ruhende wa Uhuru FM akiburudika muziki na watoto wa kituo hicho
 Mmoja wa watoto wa kituo hicho akisinzia kwa raha zake wakati amebebwa na mfanyakazi wa Uhuru FM
 Baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa na watoto wa kituo hicho cha kulelea watoto
 Baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa na watoto wa kituo hicho cha kulelea watoto
 Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akiwa na mtoto wa kituo hicho 
 Cesy Jeremiah wa Uhuru FM akipiga stori na mtoto wa kituo hicho
 Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akimfurahia mtoto wa kituo hicho
 Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akimfurahia mtoto wa kituo hicho
 Fuaraha ya kusaidia watoto yatima 
 Baadhi ya wafaanyakazi wa Uhuru FM wakijipa picha ili kubaki na kumbukumbu ya kutembelea kituo hicho cha kuelea watoto
 Mmoja wa waliolelewa na kituo hicho tangu wakiwa watoto wadogo, Najma Ajuja (15) akizungumza wakati wa kituo kukanidhiwa msaada huo 
 Furaha Ruhende wa Uhuru FM akiwa amempa simu yake kuifurahia mtoto wa kituo hicho
 Pius Ntiga na Wenzake wakipata picha kwenye kituo hicho
 Uongozi wa Uhuru FM ukiwa tayari kukabidhi msada huo
 Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akikabidhi msada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula kwa Msimamizi Mkuu wa Kituo cha kulelea Watoto yatima na wasio chini ya malezi ya wazazi wao cha CHAKUWAMA, Hassani Hamis, Wafanyakazi wa Uhuru FM walipofika kituoni hapo, Sinza Jijini Dar es Salaam, leo, kutoa msaada katika kampeni ya "Gusa maisha yake" iliyoanzishwa na kituo hicho cha radio ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere. kulia ni Mtangazaji wa Uhuru FM Aggrey Manzi. 
 uongozi wa Uhuru FM ukikabidhi Watoto wa kituo hicho baadhi ya vitu vya msaada
 Watoto wa kituo hicho wakienda kuhifadhi baadhi ya vitu ambavyo Uhuru Fm ilikabidhi
 Wafanyakazi wa Uhuru FM wakipeleka eneo la kuhifadhi baada ya makabidhiano ya msaada huo

 Mtoto wa kituo hicho akiufurahia msaada wa Uhuru FM
 Mtoto wa Kituo hicho akifurahia msaada uliotolewa na Uhuru FM
 Watoto wakishiriki kubeba zawadi
 Meneja rasiliamali watu na Utumishi wa Uhuru FM Paul Mng'ng'o akizungumza na Watangazaji wa Uhuru FM Sheila Simba na Steven Mhina baada ya Uhuru Fm kukabidhi msaada huo 

Serikali yadhamiria kufanikisha utafutaji na upatikanaji wa mafuta katika bonde la Eyasi Wembere na ziwa Tanganyika

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kufanikisha utafutaji na upatikanaji wa mafuta yaliyopo katika bonde la Eyasi Wembere na ziwa Tanganyika hapa nchini ili Tanzania ianze kunufaika na rasilimali hiyo.

Mhe. Rais Magufuli amesema hayo leo muda mfupi baada kupokea taarifa ya maendeleo ya utafiti wa mafuta katika maeneo ya bonde la ufa ya Eyasi Wembere na ziwa Tanganyika, iliyowasilishwa na timu ya wataalamu wa Tanzania na Uganda.

Timu hiyo imeelezea uwepo wa viashiria vya uhakika vya kijiolojia vinavyothibitisha kuwepo kwa mafuta katika maeneo ya Senkenke, Mwanzugi na Kining’inila katika bonde la Manonga, Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani na Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Richard Kabonero, timu ya wataalamu hao imesema miamba, uoto na uwepo wa bonde Eyasi Wembere katika mfumo mmoja wa bonde la Afrika Mashariki unaofanana na maeneo mengine yaliyothibitika kuwa na mafuta ni kiashiria muhimu cha kuwepo mafuta.

Kufuatia taarifa hiyo Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo tayari kutekeleza shughuli zote zitakazowezesha kupatikana kwa mafuta katika bonde la Eyasi Wembere na ziwa Tanganyika na amewaagiza wataalamu wa Tanzania kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wataalamu wa Uganda ambao wana uzoefu wa kupata mafuta katika ziwa Albert nchini humo.

Mhe. Rais Magufuli amewashukuru wataalamu wa Uganda wanaoshirikiana na wataalamu wa Tanzania katika kazi hii na amemuomba Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini wa Uganda Bw. Robert Kasande kumfikishia shukrani zake kwa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa ushirikiano anautoa kwa Tanzania katika kufanikisha upatikanaji wa mafuta ya nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Naibu Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani katika kikao na ujumbe wa wataalamu wa Sekta ya Nishati toka nchini Uganda na Tanzania waliompatia taarifa ya maendeleo ya utafiti wa mafuta katika bonde la bonde la ufa ya Eyasi Wembere la Ziwa Tanganyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017. Picha na IKULU

USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA SONGWE

0
0
Afisa Usajili Wilaya ya Mbozi Ndugu Eckson Mwakyembe akiwa na Mtendaji wa Kijiji cha Mlowo Bi. Judith Mtega wakikamilisha fomu za maombi ya Usajili za wananchi wa vijiji vya Shuleni, Mtakuja, Mlowo na Kiwandani kata ya Mlowo wakati zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa likiendelea wilayani humo.
Meneja Mifumo ya Komputa wa ndugu Francis Saliboko akifanyia matengenezo ya kiufundi moja ya kifaa kinachotumika wakati wa usajili katika zoezi linaloendelea Kata ya Mlowo – Mbozi mkoani Songwe. 
Maafisa Usajili wa NIDA wakifanya kazi ya kupiga picha na kuchukua alama za kibaiolojia katika zoezi linaloendelea kata ya Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe. 
Afisa Usajili Bi. Coletha Peter na Bi. Magreth Moshi wakisaidia taratibu za kuchambua na kuhakiki fomu za maombi ya Vitambulisho za wananchi wa kata ya Mlowo kwa ajili ya hatua ya mwisho ya kupiga picha, kuchuliwa alama za vidole na saini ya kielektroniki.
Mwananchi wa kata ya Mlowo akichukuliwa alama za vidole, picha na kuweka saini ya kielektroniki wakati wa Usajili Vitambulisho vya Taifa. kushoto ni Afisa Usajili Ndugu Baraka Haonga.

Zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu limeendelea leo mkoani Songwe, ambapo zaidi ya Kata 5 tayari zimekamilisha Usajili huo uliolenga kukusanya taarifa sahihi za watu wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wakiwemo wageni wanaoishi kihalali mkoani humo.

Wakazi wa Songwe na Mbozi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kusajiliwa ili kunufaika na manufaa mapana ya Kitambulisho hicho na pia kuiwezesha Serikali kutoa huduma bora zaidi.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA IJUMAA LEO OCTOBER 6,2017

0
0





MBUNGE WA MAFINGA MJINI AMEKABIDHI JUMLA YA MIFUKO YA SARUJI 130

0
0
Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya kuchochea maendeleo na kama unavyo muona akiwa anashusha safuji hiyo kutoka kwenye gari
Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mifuko ya saruji akiteta jambo na wananchi waliofika katika eneo hilo alipokuwa akikabidhi saruji hizo.



Na Fredy Mgunda,Iringa

Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mifuko ya saruji 130 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ya Maarifa,kinyanmbo na zahanati ya Rungemba kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, alisema kuwa niliomba kuwa mbunge kwa lengo la kuwatumikia wananchi hivyo najitahidi huku na kuel kuhakikisha natimiza azma yangu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini.

“Nimetoa mifuko 130 ya saruji kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi wa madarasa katika shule mpya ya Maarifa na zahati ya Rungemba hii ni mwamzo tu nitaendelea kutoa saruji nyingine ili kulifanya jimbo la Mafinga Mjini kupata maendeleo kwa kasi” alisema Chumi

Chumi alisema kuwa halmashauri ya Mji wa Mafinga imeshaanda mpango kabambe ambao utakuwa msaada mkubwa kuchochoe maendeleo kwa kasi huku mji ukiwa umeshapangiliwa jinsi gani ya kuitumia vizuri ardhi ya halmashauri hii.

“Ukiangalia miji mingi inakuwa bila kuwa na mpango kabambe kitu kinachokuja kusababisha migogoro ya kugombea ardhi hivyo mpango huu utakuwa namanufaa makubwa kwa jimbo hili la Mafinga Mjini” alisema Chumi.Aidha Chumi alisema kuwa shule zilipata saruji hiyo ni shule mpya ya Maarifa nimekabidhiwa mifuko 50 ya saruji sawa na nyingine ya Kinyanambo lakini pia nimetoa mifuko ya saruji 30 kwa zahanati ya Rungemba lengo ni kuchochoe kuleta maendeleo kwa wananchi.

Chumi amewapongeza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kata za ametoa ahadi ya kuendelea kushirikiana kwa kuchangia ujenzi wa shule zote za jimbo la mafinga mjini.Naye mwenyekiti kata ya Changalawe Emmanuel Kuzugali ameelezea jinsi wananchi walivyochangia kuwezesha ujenzi wa shule ya msingi utakaoanzishwa katika kata hiyo.

Kwa upande wake diwani viti maalumu kata ya changalawe Monica Luvanda ameelezea mchakato ulivyokuwa hadi kupelekea kushirikiana na wananchi kuanzisha ujenzi wa shule ili kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa kata hiyo.

AZANIA BANK ,TAWI LA MOSHI WAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KULA KEKI NA WATEJA WAO

0
0
Wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi wakikata keki kwa pamoja kwa ajili ya kushiriki na Wateja wao ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja inayoendelea.
Wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi wakiwa katika muonekano tofauti ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.
Mfanyakazi wa Azania Bank ,tawi la Moshi ,Aida Mbilinyi akimuelekeza jambo mteja wa Benki hiyo Ibrahim Shoo alipofika katika tawi hilo kwa ajili ya kupata huduma.
Mfanyakazi wa Azania Bank,tawi la Moshi,Asifiwe Musa akiwa ni mwenye tabasamu wakati akitoa huduma kwa mmoja wa wateja wa Benki hiyo waliofika kupata huduma.
Mfanyakazi wa Azania Bank,tawi la Moshi,Diana Ngaiza akimhudumia mmoja wa wateja wa Benki hiyo waliofika kwa ajili ya kupatiwa Huduma za kibenki.
Baadhi ya Wateja wakipata Huduma katika madirisha ya Huduma ndani ya Benki hiyo.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi ,Bi Hajira Mmambe akiwalisha keki baadhi ya Wateja waliofika kupata huduma katika Benki hiyo.
Wafanyaazi wa Azania Bank tawi la Moshi wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jingo la Benki hiyo
Ofisi za Benki ya Azania ,tawi la Moshi .
Keki Maalumu iliyoandaliwa na Azania Bank tawi la Moshi kwa ajili ya Wateja wa Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

WIZRA YA FEDHA NA MIPANGO YAANZISHA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA UTOAJI HATI ZA MALIPO YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO 



TAARIFA KWA UMMA.

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango inaendelea na juhudi za kusimamia, kudhibiti na kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali za kifedha ikiwemo mishahara ya watumishi na wastaafu wa Umma. Aidha, Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Mashirika ya Bima, Mabenki, Taasisi za Fedha, Saccos na wadau wengine wameendelea kufanikisha utoaji huduma mbalimbali kwa watumishi na wastaafu wa Umma kwa kutumia taarifa za mishahara zikiwa kwenye nakala ngumu. 

Hata hivyo, bado kuna changamoto mbalimbali katika upatikanaji wa taarifa hizo ikiwemo kuongezeka kwa gharama za uchapishaji na usambazaji wa nakala ngumu nchi nzima, usumbufu na gharama kubwa kwa watumishi na wastaafu kuzitafuta taarifa hizo Hazina na wakati mwingine kughushiwa. 

Kutokana na changamoto hizo, Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa hati za malipo ya mishahara ya watumishi wa Umma unaojulikana kama “Government Salary Slip Self Service”. Mfumo huu unatumia taarifa sahihi zilizopo kwenye mfumo shirikishi wa taarifa za Kiutumishi na Mishahara (Human Capital Management Information System) wa Serikali ujulikanao kama “Lawson”. Utaratibu wa kujisajili na kutumia huduma hii kwa watumishi wa Umma unatolewa na waajiri wao.

Walengwa na watumiaji wa mfumo huu ni watumishi wa Umma, Wastaafu, Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Mashirika ya Bima, Taasisi za Fedha (Mabenki, Saccos) na wadau wengine wanaotoa huduma  kwa Watumishi wa Umma na wastaafu kwa kutumia hati za malipo ya mishahara (Salary Slip) ikiwa kwenye nakala ngumu.

Wizara inapenda kuzitangazia Taasisi kuwa, huduma hiyo kwa sasa inapatikana kwa njia ya kielektroniki kwa kutumia internet kwa masharti ya kusajiliwa kwanza ili ziweze kuondokana na matumizi ya nakala hizo ngumu kwa kutumia namba maalum ya mshahara wa mtumishi kwa mwezi husika (salary slip token) inayotolewa na mwajiri wake.

Sifa za kusajiliwa kwa taasisi ni kutuma maombi yanayoambatana na namba za makato (Deduction Codes) za taasisi husika pamoja na orodha ya watumiaji wa mfumo wakiwa na taarifa zifuatazo; Namba ya mtumishi (Employee ID), Majina yake matatu, namba ya simu, anuani pepe, namba ya utambulisho iliyoko kwenye kitambulisho chake cha Taifa au namba iliyoko kwenye kitambulisho cha Mpiga Kura au namba ya hati ya kusafiria.

Taasisi zinazotaka kujiunga na mfumo huu ziwasilishe Maombi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Barabara ya Jakaya Kikwete,Jengo la ‘Treasury Square’S.L.P 2802 DODOMA.
Taarifa hii inapatikana pia katika Tovuti ya Wizara (www.mof.go.tz)

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Fedha na Mipango.

UZINDUZI WA KIELETRONIKI WA UKUZAJI AMANI KUZINDULIWA JIJINI DAR

0
0
 Mwenyekiti wa Bodi katika mikutano Mikuu toka Shirika la Alpha and Omega Reconciliation and Peace Building (AREPEB) Yohana Mcharo (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa mfumo wa Kieletroniki wa ukuzaji amani, Haki za Binadamu na misingi ya utawala bora, katikati ni Mwenyeki wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo Bi. Imelda Mushi na kulia ni Katibu Mkuu wa shirika hilo Julius Muganga.
Mwenyeki wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika la Alpha and Omega Reconciliation and Peace Building (AREPEB) Bi. Imelda Mushi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa mfumo wa Kieletroniki wa ukuzaji amani, Haki za Binadamu na misingi ya utawala bora, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi katika mikutano Mikuu toka Shirika hilo Yohana Mcharo na kulia ni Katibu Mkuu wa shirika hilo Julius Muganga.Picha na Eliphace Marwa - Maelezo

MWENYEKITI WA CHADEMA MTAA WA KIHESA KILOLO B AMPIGIA MAGOTI MBUNGE RITTA KABATI

0
0
 Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo akiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakati wa kuzitambua changamoto zinazoikabili shule ya msingi Igeleke iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
 Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo akiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakiwa katika picha nawanafunzi wa darasa la saba
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua madarasa ambayo miundombinu yake imeharibika.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo amempigia magoti mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati kuwasaidia kukarabati shule ya msingi Igeleke kwa kuwa miundo mbinu yake imeharibika na sio rafiki kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.

Akizungumza na blog bwana Madembo alisema shule hiyo inamiundombinu mibovu hivyo ni hatarishi kwa wanafunzi wa shule hii kwanza toka mwaka 1978 hadi leo shule hiyo haijawahi kufanyiwa ukarabati wa kueleweka hivyo inahitajika kukarabatiwa haraka iwezekanavyo.

“Mwandishi ukiangalia majengo ya shule hii unaona jinsi gani yalivyoaribika na ipo katika halmashauri ya manispaa ya Iringa lakini viongozi wengi hawaingalii kwa jicho la tatu kitu kinachotupa shida sisi viongozi wa eneo hili” alisema Madembo

Madembo alisema kuwa shule nyingi zilizojengwa miaka ya 1978 na kuendelea zinamiundombinu ilichoka hivyo serikali na viongozi wa kisiasa kuanza kuzitafutia mikakati ya kuzikarabati ili kuboresha taaluma kwa watoto wetu kuendana na karne ya sasa.

“Hebu angalia hapo juu hili paa muda wowote kuanzia sasa hili paa la darasa linaweza kuleta maafa kwa wanafunzi lakini viongozi wetu hawaliangalii hili swala ndio maana nimemuaomba huyu mbunge Ritta Kabati kusaidia kuarabati” alisema Madembo

Aidha Madembo alisema kuwa haangalii itikadika ya vyama bali anatafuta viongozi waliotayari kule maendeleo kwa kuwa hiyo ndio tija ya kuwa kiongozi kuwatumika wananchi waliotuchagua wakati tukiomba kura za kuwa viongozi.

“Leo hii mimi ni mwenyekiti wa CHADEMA lakini nipo na mbunge wa CCM aliyekubali kuja kusaidia kuleta maendeleo katika shule yetu yaIgeleke hivyo nipende kuweka wazi kuwa mimi kwenye maendeleo siangalii chama gani kinaleta maendeleo” alisema Madembo

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa anafanyakazi na wenyeviti wote wa manispaa ya Iringa kwa lengo la kuijenga manispaa na kuinua uchumi wa wananchi wa mkoa wa Iringa.

“Nimekuwa navikao vya mara kwa mara kwa wenyeviti wa mitaa ya hapa manispaa hivyo wenyeviti wa CHADEMA wamekuwa wa kwanza kuniita kila wakati kusaidia kuleta maendeleo katika maeneo husika ndio maana leo unaniona nipo na mwenyekiti wa CHADEMA kutafuta njia mbadala ya kutatua changamoto za hii shule ya Igeleke” alisema Kabati

Kabati aliwataka viongozi mbalimbali kutafuta njia mbadala ya kuwaletea maendeleo wananchi nsio kuangalia vyama vinafanya nini.

“Mimi ni kada wa chama cha mapinduzi lakini nimekuwa nikifanya kazi vizuri na viongozi mbalimbali wa kiasa kwa lengo la kuleta maendeleo tu ndio sababu inayosababishwa wapinzani kuniona mimi bora wakati wa kufanya shughuri za kuleta maendeleo” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa ataendelea kufanya ziara kwenye shule zote zenye matatizo ili kuzisaidia kuyatatua matatizo hayo na leo amefanya ziara katika shule ya msingi Igeleke kwa kuziona changamoto zinazoikabili shule hiyo ili kuzitafutia ufumbuzi.

Naye mkuu wa shule ya msingi Igeleke Robert Mulilo na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Wakati Maliva walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa jitihada zake za kuendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.

WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU.

0
0
Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

WALENGWA wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) wametakiwa kuanzisha vikundi vya ufugaji kuku ili waweze kuunganisha nguvu zao kwa ajili ya kutafuta dawa za chanjo zitakazowasaidia kukabiliana na ugonjwa wa mdodo na kideri(Newcastle diasese) ambao umekuwa ukiwasababishia hasara.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Richius Bilakwata kwenye mikutano na walengwa wa vijiji vya Itebulanda na Nsenda wilayani Urambo.

Alisema kuwa ili waweze kuepuka kupata hasara kutokana na kuku zao kushambuliwa na ugonjwa huo ni vema wakawa wananunua chanjo na kuwachanja.“Moja ya chanjo inaweza kuchanja kuku wengi kwa pamoja ni vema mkajiunga pamoja ili muweze kuchangia katika ununuzi wa dawa hiyo kwa urahisi” alisema Bilakwata.

Aliwashauri walengwa kuwa wakati mpango huu wa kunusuru kaya ukielekea mwishoni ni vema wakajitihidi kutumia kipato kidogo wanachokipata kuwekeza katika miradi midogo kama vile ufugaji wa bata, kuku, mbuzi na mifugo mingine.

Bilakwata alisema kuwa miradi hiyo itawasaidia wakati mpango huo utakapokuwa umekoma.Nao walengwa wengi walisema kuwa wamekata tama kuendelea na ufugaji wa kuku kwa sababu ya kushambuliwa na magonjwa kama vile mdodo na kideri.

Hivi sasa kuku moja katika maeneo ya Urambo mjini anauzwa kwa wastani wa shilingi elfu 8 hadi elfu 12.

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU MFANYABIASHARA MANJI JIJINI DAR LEO.

0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji jijini Dar es Salaam leo mara baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake yaliyokuwa yakimkabili ya matumizi ya dawa za kukevya.

 Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa hukumu na kujulikana kuwa upande wa mashtaka hawakuweza kuthibitisha kama kweli alikuwa anatumia dawa za kulevya.
 Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akipanda gari akipanda gari mara baada ya kusomewa hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabiri ya kutumia dawa za kulevya ikiwa upande wa mastaka walishindwa kuthibitisha shtaka hilo.
 Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akielekea kwenye gari kwaajili ya kuondoka huku akiwa hana kosa mara baada ya kusomewa hukumu  na kuonekana kuwa hakuwa akitumia dawa za kulevya.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru mfanyabiashara, Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya dawa za kulevya iliyokuwa inamkabili.Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi yake.
Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,akisubiri kusomewa shtaka lake.
Wakili wa Manji akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Mahakama ya hakimu Mkazi kisutu mara baada yakuonekana hana kosa la matumizi ya dawa za kulevya.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images