Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1389 | 1390 | (Page 1391) | 1392 | 1393 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania

  Saratani ya matiti ni miongoni mwa saratani inayomkumba zaidi mwanamke duniani na ndiyo inayoongoza kwa vifo vinavyotokana na saratani katika nchi zinazoendelea, ambapo watu takribani milioni 1.7 mwaka 2012 waligundulika kuwa na ugonjwa huo (kwa mujibu wa taarifa zilizopo hivi sasa). Viwango vya saratani duniani kwa ujumla vinatarajiwa kuongezeka kutoka milioni 14 mwaka 2012 na kufikia milioni 20 ndani ya miongo miwili ijayo, na kuifanya saratani kuwa ugonjwa unaotakiwa kuchukuliwa tahadhari zaidi.
  Mwezi Oktoba wa kila mwaka dunia huwa imeutenga mahususi katika kukuza uhamasishaji wa kupambana na ugonjwa wa saratani ya matiti duniani. Kampeni hizo huungwa mkono na serikali, taasisi na mashirika mbalimbali duniani kwa kuangazia umuhimu wa kuhamasisha juu ya saratani ya matiti, kutoa elimu na kufanya tafiti. Miongoni mwa shughuli zinazofanywa katika mwezi huu ni pamoja na kukuza hamasa kwa watu wengi kadri iwezekanavyo na kuchangisha fedha kwa ajili ya kufanyia tafiti toauti za ugonjwa huo.

  Miongoni mwa mambo ya msingi unayotakiwa kuyafahamu kuhusu saratani ya matiti ni pamoja na: saratani ya matiti huwakumba zaidi wanawake; dalili zake ni pamoja na uvimbe au kuvimba kwa titi, na mabadiliko ya ngozi au chuchu; sababu zinazoweza kupelekea ni pamoja na kurithi, lakini mitindo ya maisha, kama vile unywaji wa pombe, unaweza kusababisha kutokea zaidi; aina mbalimbali za matibabu zinapatikana, zikiwemo upasuaji, tiba ya mionzi na kimotherapi; uvimbe unaotokea kwenye titi sio saratani, lakini mwanamke yeyote ili kuchukua tahadhari kuhusu uvimbe au mabadiliko yoyote inashauriwa kumuona daktari. 
  Kwa kuwa mwezi huu umelenga kwenye kujenga hamasa juu ya ugonjwa wa saratani ya matiti duniani, Jumia Travelingependa kukufahamisha juu ya sababu hatarishi zifuatazo zinazoweza kupelekea ugonjwa huo. 

  Umri. Hatari ya kuupata ugonjwa huu huongezeka kadri umri nao unavyoongezeka. Katika umri wa miaka 20, uwezekano wa kupata saratani ya matiti ndani ya muongo mmoja ujao huwa ni 0.6%. Lakini katika umri wa miaka 70, takwimu hiyo huongezeka mpaka kufikia 3.84%. Kesi nyingi za ugonjwa wa saratani zimegundulika baada ya umri wa miaka 50.

  Kurithi. Endapo ndugu wa karibu anaugua au aliwahi kuugua, saratani ya matiti, hatari ya kuupata ni kubwa zaidi. Wanawake ambao wanabeba jeni aina ya BRCA1 na BRCA2 wanayo hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti, saratani ya ovari au zote kwa pamoja. Jeni hizi zinaweza kurithiwa. TP53 ni jeni nyingine ambayo inahusishwa zaidi na hatari ya kusababisha saratani ya matiti. 

  Historia ya kuugua saratani ya matiti kipindi cha nyuma. Wanawake waliowahi kuugua saratani ya matiti kipindi cha nyuma wanao uwezekano wa kuugua tena, ukilinganisha na wale ambao hawana historia na ugonjwa huo.
  Historia ya saratani ya matiti katika familia. Hatari kwa mwanamke kupata saratani ya matiti ni kubwa zaidi endapo mama yake, dada au bintiye (ndugu wa karibu zaidi) au ndugu wengi aidha wa upande wa mama au baba walikwishawahi kuugua ugonjwa huo. Kuwa na ndugu wa karibu zaidi wa kiume ambaye aliwahi kuugua saratani ya matiti pia kunaongeza hatari ya kuupata ugonjwa huo kwa mwanamke. 

  Uzito wa mwili uliopitiliza. Wanawake wenye uzito uliopitiliza au utapiamlo hususani baada ya kukoma kwa hedhi wanaweza kuwa na hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti, pengine kwa sababu ya kiwango kikubwa cha estrojeni (homoni inayohusika na ukuaji na uwepo wa tabia za kike mwilini). Utumiaji wa kiwango kikubwa cha sukari pia unaweza kuwa ni sababu.

  Matumizi ya pombe. Matumizi makubwa ya kiwango cha pombe pia huchangia kusababisha ugonjwa huu. Tafiti zimeonyesha kwamba wanawake wanaokunywa zaidi ya mara 3 kwa siku wana hatari ya kupata ugonjwa huo mara 1.5.

  Matibabu kwa njia ya mionzi kipindi cha nyuma. Kuwahi kufanya matibabu ya mionzi kwa saratani isiyo saratani ya matiti kunaongeza hatari ya kupata saratani ya matiti siku za usoni maishani mwako.

  Kutokufanya mazoezi. Wanawake ambao hawafanyi mazoezi ya mara kwa mara pia wanayo hatari ya kupata saratani ya matiti. 
  Majanga yanayoweza kutokea kazini. Tafiti zinashauri kwamba sababu zingine kama vile kuvuta sigara, kufanya kazi mazingira yenye uwepo wa kemikali yanaweza kupelekea saratani, na pia kufanya kazi kwenye zamu za usiku pia kunaweza kupelekea saratani ya matiti. Ingawa baadaye watafiti walikuja kubainisha kwamba kufanya kazi zamu za usiku ni suala ambalo hakuna uwezekano. 

  Kwa kuwa kampeni hii hufanyika duniani kote ikiwemo Tanzania, Jumia Travel inaamini kwamba kuna hospitali zinafanya kampeni za uhamasishaji juu ya saratani ya matiti. Ambapo elimu, vipimo na ushauri hutolewa na wataalamu mbalimbali. Hivyo basi ni fursa kwa kukitumia kipindi hiki ipasavyo ili kuweza kuujua ugonjwa huu na namna ya kukabiliana nao. 

  0 0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Issa Suleim Nassor kuwa balozi wa Tanzania nchini Misri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe. Issa Suleim Nassor kuwa balozi wa Tanzania nchini Misri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Abdulrahman Kaniki Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017 Abdulrhaman Kaniki kuwa balozi wa Tanzania nchini Misri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe. Abdulrahman Kaniki kuwa balozi wa Tanzania nchini Zambia Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli balozi mpya wa Tanzania nchini Misri Mhe. Issa suleiman Nassor na Mhe. Abdulrahman Kaniki balozi mpya wa Tanzania nchini Zambia wakila viapo vya maadili ya viongozi baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017
  Balozi mpya wa Tanzania nchini Misri Mhe. Issa suleiman Nassor akiongea machache baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017
  Blozi mpya wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Abdulrahman Kaniki machache baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza baada ya kumuapisha Mhe. Abdulrahman Kaniki kuwa balozi wa Tanzania nchini Zambia Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza baada ya kumuapisha Mhe. Issa Suleim Nassor kuwa balozi wa Tanzania nchini Misri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa mambo ya Nje Dkt. Suzan Kolimba, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje Dkt. Aziz Ponary Mlima na Viongozi wa vyombo vya ulinzi na Usalama wakiwa katka picha ya pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Abdulrahman Kaniki na balozi mpya wa Tanzania nchini Misri Mhe. Issa suleiman Nassor baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakiwa katka picha ya pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Abdulrahman Kaniki na maofisa waandamizi wa Polisi Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Misri Mhe. Issa suleiman Nassor Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017 

  Picha na IKULU

  0 0

  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na Mjumbe Maalum wa Rais wa Bunge la Nchi za Kiarabu, Dkt. Feda Yehia Ahmed Alhmoud alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini odoma.
  Mjumbe Maalum wa Rais wa Bunge la Nchi za Kiarabu, Dkt. Feda Yehia Ahmed Alhmoud akijadiliana jambo na Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akipokea barua ya ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Bunge lma Nchi za Kiarabu, anayekabibidhi barua hiyo ni Mjumbe Maalum wa Rais huyo, Dkt. Feda Yehia Ahmed Alhmoud wakati alipomtembelea leo Ofisin kwake Mjini Dodoma.
  Mjumbe Maalum wa Rais wa Bunge la Nchi za Kiarabu, Dkt. Feda Yehia Ahmed Alhmoud akipokea zawadi ya kinyago kutoka kwa Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai walipokutana na kufanya mazungumzo leo Ofisini kwake Mjini Dodoma

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mh Juma Homera (Kushoto) akiwa na MWakilishi wa Tatu Mzuka  Bi Kemi Mutahaba, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kiuma Bw. Joseph Mtuma  Wakimpongeza Mshindi wa 9 wa Tatu Mzuka Jackpot Bw Fulko Hyera, kijijini Kiuma, Tunduru
    Mshindi wa 9 wa Tatu mzuka Jackpot Bw Fulko Hyera, Mwalimu wa shule ya sekondari Kiuma,akifurahia alipo kabithiwa cheki  ya Milioni 60 kutoka Tatu Mzuka kijijini kwake Kiuma, Wilaya ya Tunduru.
   Bw. Fulko Hyera  and Mke wake Sigsberta Haule mbele ya duka lao kijijini Kiuma wakisherekea kipato cha Million 60 kutoka Tatu Mzuka.
  Tatu Mzuka walizawadia marafiki wa TATU wa Bw. Fulko Hyera  million 1 moja kutokana na promociona ya Tatu Mzuka ya "Cheza na Washkaji na Shinda na Washkaji".  Robert Mbai na Owne Simwanga


  Mshindi wa droo ya tisa ya Tatu Mzuka amepatikana Jumapili hii ya Oktoba 1, 2017. Mshindi huyu amejinyakulia kitita cha shilingi milioni 60 na ni Bwana Fulko Hyera, mkazi wa kiuma, wilayani Tunduru 

  Ushindi huu wa Bw.Hyera unaonesha namna Tatu Mzuka inavyobadili maisha ya wananchi wa Tanzania sio tu wa mjini bali na vijijini pia. Bw. Hyera ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari ya Kiuma.

  Bw Hyera alisema “Katika muda wangu wote, sikuwaza kuwa na hela hizi. Kama familia zetu nina majukumu mengi yakutimiza na sasa nitakuwa na uwezo wa kusaidia familia. Sasa nimeamua kuanza biashara, niajiri wengine na kuongeza fursa za vijana” 

  Kumkabidhi cheki Bw Hyera, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Juma Homera alimkabidhi cheki mshindi kwenye tulio lilio andaliwa na Tatu Zuka kijijini Kiuma, Tunduru.

  Mheshimiwa Homera alikuwa ana machache ya kusema licha la kumpongeza Bw. Hyera alimuhusia “ Hizi ni hela nyingi sana. Lazima uwe na malengo kamili and pia hii itakupa fursa nyingine ya kusaidia jamii.” Amewapongeza sana Tatu Mzuka kwa kuchangia kubadili maisha ya watu tena ya mwana Tunduru.

  Licha ya ushindi huo, Bw. Hyera alipata pia fursa ya kutaja majina matatu ya rafiki zake ambao pia walijishindia kiasi cha shilingi milioni 1 kwa kila mmoja. Mmoja ya rafiki zake Bi.Marianna Haule ambaye mara nyinji anamuuguza mama yake, ndio alichaguliwa. “Nilimuwaza Marianna ili nijaribu kumpa haueni akiwa anamuuguza mama yake.” Alieleza Bw. Hyera

  Tatu Mzuka hadi leo imetoa zaidi ya Billion 2 kwa washindi na wamepata zaidi ya washindi 900,000.  

  Wiki hii Jumapili kutakuwa na Million 80M.Namna ya kucheza promosheni ya Tatu Mzuka Unatakiwa kwenda kwenye sehemu ya fedha kwenye simu yako na kuchagua Lipana kwa M-Pesa au mitandao mingine. Kisha unaingiza namba zako 3 za bahati katika sehemu inayoonekana. Kisha weka kiwango chako cha fedha kuanzia shilingi 500/- hadi 30,000/-

  Kwa kuanzia kiasi cha shilingi 500,TatuMzuka inatoa fursa ya kushinda hadi shilingi milioni 6 ndani ya saa 24 kwa siku. Chagua namba tatu za bahati kuanzia 0-9 kisha zitume zikiambatana na pesa ya ushiriki kuanzia shilingi 500/. Ukishinda namba zako zote tatu utajinyakulia fedha mara 200 ya ile uliyocheza huku pia kila shilingi 500 unayocheza inakupa nafasi ya kushiriki droo inayochezwa kila wiki ambayo inakupa fursa ya kushinda hadi shilingi milioni 70.

  Ili kupata taarifa zaidi kuhusu washindi wa Tatu Mzuka angalia Televisheni za Clouds na TV1 kila Jumapili kuanzia saa Tatu na Nusu Usiku.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akisisitiza jambo alipokuwa akikagua mfumo wa kielektroniki katika Kituo cha Afya Makole Manispaa ya Dodoma.
  Wagonjwa wakiwa katika dirisha la malipo kwenye kituo cha Afya Makole Manispaa ya Dodoma.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akisalimia wagonjwa alipokuwa akikagua kituo cha Afya Makole Manispaa ya Dodoma.


  ………….

  NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo amefanya ziara leo ya kukagua utekeleza wa maagizo ya serikali aliyoyatoa hivi karibuni katika Kituo cha Afya Makole Manispaa ya Dodoma.

  Pamoja na maagizo mengine, Jafo aliagiza kuhakikisha kituo hicho kinafunga mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji mapato.

  Akiwa katika ziara yake leo, Jafo amepongeza ufungaji wa mfumo huo huku akiwataka kuhakikisha wanaziba mianya ya upotevu wa mapato kwa kuwa hali ya ukusanyaji bado hairidhishi.

  Amesema kwa mujibu wa taarifa aliyoipata kituo hicho kabla ya mfumo kilikuwa kikikusanya Sh.Milioni nne lakini kwasasa kinakusanya hadi Sh.Milioni 9.9 kwa mwezi jambo ambalo linaonesha bado kuna mianya ya upotevu wa mapato.

  “Nawapongeza kwa kutekeleza maagizo ya serikali kwa kufunga huu mfumo lakini sijaridhishwa na ukusanyaji mapato wa kiwango hichi, kuna vituo vinakusanya hadi Sh.Milioni 24 nyie mnakusanya hivi bado haitoshi hakikisheni mnaziba mianya,”amesema Jafo

  Ameongeza “Kuwepo na mfumo ni jambo moja na kuutumia mfumo ni jambo jingine jambo la msingi ni uaminifu kuna watu katika vituo vyetu uaminifu ni mdogo kwenye kukusanya fedha ndio ugomvi huwa unazuka na wakati mwingine watu wanatolewa kwa maslahi yao binafsi,”.

  Amewataka kuhakikisha kunakuwepo na matumizi sahihi ya mfumo huo ili kuongeza mapato.Akizungumzia kuhusu ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya nchini, Jafo amesisitiza Mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha zinasimamia kikamilifu ujenzi huo na ifikapo Desemba 30 mwaka huu uwe umekamilika.

  Amesema hivi karibuni serikali imetoa Sh.Milioni 500 kwa kila kituo kimoja kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo jengo la upasuaji,maabara ya kisasa na wodi ya akina mama na watoto.

  Naibu Waziri huyo amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk.John Magufuli imedhamiria kuboresha huduma za afya na kwamba utoaji wa fedha huo umetokana na hali ya vituo vya afya kuwa si ya kuridhisha.

  Amebainisha Dodoma ni eneo mkakati kutokana na wingi wa watu hivyo ni lazima huduma za afya ziboreshwe ili kuondoa msongamano katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

  Kwa upande wake, Katibu wa Afya wa kituo hicho, Habiba Thabiti amesema kabla ya kufungwa mfumo huo walikuwa wanakusanya Sh.Milioni nne kwa mwezi lakini kwasasa wamefikia Sh.Milioni 9.9.

  Naye, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk.George Matiko amesema kwa siku kituo kinahudumia wagonjwa kati ya 400-800 na akina mama wanaojifungua kwa mwezi ni 400.

  0 0  0 0

  Mmoja wa wafanyakazi katika Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) akitengeneza vigae vya kuezekea nyumba vilivyofanyiwa utafiti Jijini Dar es Salaam tayari kwa matumizi ya ujenzi wa nyumba.
  Ukuta unaofanyiwa utafiti kwa ujenzi wa kutumia tofali mbichi kwa majengo makubwa na nyumba za makazi ulioko katika karakana ya Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) Jijini Dar es Salaam.
  Mhandishi na fundi sanifu wa majengo Bw.Hussein Mataka akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu mashine ya kufyatua tofali iliyoko katika karakana la ofisi hizo Mwenge Jijini Dar es Salaam.
  Mhandisi wa ofisi za Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) Bw. Benedict Chilla akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma zinazotolewa na ofisi hiyo mapema wiki hii Jiji Dar es Salaam.
  Mashine ya kupima ubora na kiwango cha udongo kwa ujenzi wa nyumba ambayo ni moja ya vifaa bora vinavyopatikana Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) kama inavyoonekana kwenye picha.Picha na Paschal Dotto-MAELEZO


  …………


  Na. Paschal Dotto- MAELEZO.

  Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) imewashauri wananchi kufuata maelekezo katika ujenzi wa nyumba za makazi na majengo mbalimbali ili kupata nyumba bora.

  Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mhandisi Benedict Chila alisema kuwa kuna uhitaji mkubwa sana wa utafiti kwa nyumba za makazi kuhusu matumizi bora ya vifaa vya ujenzi kama matofali, kokoto pomoja na mchanga uliobora katika ujenzi.

  “kuna uhitaji mkubwa wa tafiti ambazo zitawawezesha watanzania kupata makazi bora yenye kudumu, kwani katika vifaa na huduma zinazopatikana kwetu zinajikita zaidi katika usanifu majengo pamoja na matumizi ya vifaa, kwa hiyo tafiti hizi ni muhimu kwa wananchi wenye mahitaji ya makazi bora”,.alisema Mhandisi Chila.

  Aidha Mhandisi Chila alisema kuwa katika kutambua uhitaji wa wananchi NHBRA imetoa mlango kwa jamiii kupata huduma bora kwa kufanya tafiti katika sanifu ya majengo na vifaa vya kutumia katika ujenzi ili kupata makazi bora.

  Kwa upande wake fundi sanifu wa Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba bora na vifaa vya ujenzi (NHBRA) Bw. Hussein Mataka alisema kuwa wamejidhatiti katika kutoa huduma bora kwa kufanya utafiti na kutoa bidhaa safi kwa ujenzi wa nyumba za makazi na majengo mengine.

  “Tunahitaji watanzania waje kwa wingi na watambue uwepo wa bidhaa zetu kwani ni bora na zinatoa makazi bora kwa sababu zimefanyiwa tafiti za kutosha na kutengenezwa katika kiwango kizuri zaidi kwa matumizi ya muda mrefu”, .alisema Bw. Mataka

  Akibainisha baadhi ya bidhaa hizo Mataka alisema vifaa vinavyopatikana NHBRA ni matofali ya kufungamana yanayotengenezwa kwa udongo na kiasi kidogo cha saruji, mashine za kutengeneza matofai hayo, vigae vya kuezekea nyumba na mashine ya kutengeneza vigae hivyo.

  Mataka aliongeza kuwa tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanywa na NHBRA zina lengo la kupunguza gharama za ujenzi wa makazi na majengo mengine ya biashara, alieleza baadhi ya tafiti hizo ni utafiti wa kutengeneza frem za milango kwa kutumia zege, utafiti kuhusu matofali yanayofungamana na kuchoma pamoja na vigae vya kuchoma vya kuezekea.

  Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) ulianzishwa mwaka 2001chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa lengo la kutoa huduma na kupunguza gharama kwa vifaa vya ujenzi kwa makazi bora.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza alipokuwa akifungua kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ambayepia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi za Udhibiti Dawa Afrika Mashariki Hiiti Sillo akielezea jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha wataalam toka taasisi hizo leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (katikati) akifuatilia maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Dkt. Hiiti Sillo (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mdhibiti wa Dawa kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wizara ya Afya nchini Rwanda Alex Gisagara na Kamishna wa Huduma za Famasi toka Uganda Seru Morries.
  Afisa Msajili wa Dawa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Dk. Shani Maboko akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.Picha na: Frank Shija – MAELEZO

  0 0

  Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akitoa maelezo wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi cha shilingi laki Tano.
  Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipeana mkono na viongozi wa timu ya Mafinga veterani wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi cha shilingi laki Tano .  Na fredy Mgunda, Mafinga

  Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi amezipiga tafu timu zinazoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Iringa kwa kuzipatia jozi moja moja ya jezi kwa kila timu lakini pia ameichangia timu ya Mufindi United inayoshiriki lingi daraja la kwanza Tanzania bara kiasi cha shilingi laki tano kwa lengo la kuisaidia katika harakati zake za kupanda daraja.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa na pesa hizo Chumi alisema kuwa ameguswa kufanya hivyo kwa kuwa anapenda michezo na anacheza mpira wa miguu kufanya hivyo kutaendelea kuzipa morali timu za jimbo la Mafinga Mji kufanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki.

  "Leo nimekabidhi jezi kwa timu zinazoshiriki daraja la tatu ngazi ya mkoa na timu hizo ni Bajaji Fc,Mabo Fc (Boda Boda) na Kinyanambo United nimefanya hivyo kuzifanya timu hizi kuzihamasisha kufanya vizuri kwenye ligi hiyo" alisema Chumi

  Chumi aliwataka wananchi na wadau wanaoipenda timu ya Mufindi United kuendelea kuisaidia katika haraka za kupanda daraja kwa kuwa kuendesha timu ni gharama kubwa hivyo tuungane kwa pamoja kufanikisha lengo letu ili kupata timu itayokuwa ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.

  “Jamani kushiriki ligi daraja la kwanza ni gharama sana na ligi ya mwaka huu ni ngumu hivyo tunahitaji kuwa na pesa nyingi kufanikisha lengo letu la kuwa na timu ya ligi kuu wenzetu wengine wamejipanga sana na wanapesa hivyo timu yetu ikiwa na njaa itatuwia vigumu kuipandisha” alisema Chumi

  Aidha Chumi hakusita kuwapongeza viongozi wa timu ya Mufindi United pamoja na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William kwa kuendelea kuisadia timu kushiriki lingi hivyo kwa michango na mawazo yao.

  “Mimi nilijua mwaka huu tunashushwa daraja maana hali ilikuwa ngumu wakati wa usajili lakini viongozi hawa walipigana kufa na kupona wakahakikisha timu inasajili na inacheza ligi hiyo” alisema Chumi.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dk. Philip Mpango akizungumza na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa uuzaji hisa za Maendeleo Bank PLC uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  Hisa za Maendeleo Bank zimeendelea kufanya vizuri sokoni tangu kuzinduliwa kwa mauzo ya hisa hizo rasmi Septemba 18, tukio ambalo lilifanywa na Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dk. Philip Mpango.

  Watanzania wengi wameonekana wakiitikia wito wa kuwekeza katika soko la mitaji kwa kufika katika matawi ya Maendeleo Bank ya Luther House, Mwenge na Karikakoo, matawi yote ya CRDB nchini, Uchumi Commercial Bank na Mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) walioidhinishwa kuuza hisa.

  Akizungumzia maendeleo ya ununuzi wa hisa hizi, Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Bw. Ibrahim Mwangalaba alisema “Tumeingia wiki ya tatu sasa katika zoezi letu la uuzaji wa hisa, tumeona watanzania wengi wakijitokeza na kwa kweli sisi kama benki tuna matumaini makubwa ya kufikia lengo ambalo tumekusudia”.Pia tunaendelea kuisaidia Serikali katika kutoa elimu ya uwekezaji katika masoko ya mitaji na faida zake kwa watanzania na nchi kwa ujumla. Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dk. Philip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa uuzaji hisa za Maendeleo Bank PLC. Pamoja nae kutoka kushoto ni Askofu Ambele Mwaipopo, Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Askofu Dk. Alex Malasusa, Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Bw. Ibrahim Mwangalaba na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo Bank Bw. Amulike Ngeliama.

  Mwitikio wa watanzania katika kununua hisa, kujitokeza kuuliza maswali ili kuelewa zaidi juu ya mambo haya ni suala la kujivunia kwetu kwani tunafanya mambo makubwa mawili kwa wakati mmoja, moja ni kuuza hisa lakini la pili ni kusaidia juhudi za Serikali juu ya kutoa elimu ya namna gani watanzania wanaweza kuwekeza katika hisa” aliongeza Mwangalaba.

  Uwekezaji katika hisa ni mfumo wa uwekezaji unaomuwezesha muwekezaji nafasi ya kumiliki kampuni na kupata gawiwo pale kampuni inapopata faida. Pia hisa ni njia ya ukuzaji wa thamani ya fedha yako pale hisa zinapopanda.Pia hisa zinaweza kutumika kama dhamana ya kujichukulia mkopo katika benki.

  Mkurugenzi huyo amewasihi watanzania wengi zaidi kuchangamkia hisa za Maendeleo Bank ili waweze kuwa sehemu ya uchumi wao kwa kumiliki sehemu ya benki hiyo. Hisa za Maendeleo Bank zinaendelea kuuzwa hadi Novemba 3, 2017.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule mbalimbali nchini kusoma kwa bidii na wasikubali kushawishika.

  Pia Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka sheria kali kwa wote watakaobainika kukatisha masomo ya watoto wa kike kwa kuwapa ujauzito au kuwaozesha.Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatano, Oktoba 04, 2017) wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana na WAMA Sharaf.

  Shule ambayo ipo wilayani Lindi inamilikiwa na Taasisi ya WAMA ambapo inasomesha watoto wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira magumu.Waziri Mkuu amewataka wanafunzi hao wa kike kuhakikisha wanatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa bidii na hatimaye watimize malengo yao.

  Amesema ni vema wanafunzi hao wakatumia vizuri fursa hiyo ya elimu wanayoipata shuleni hapo kwa kusoma kwa bidii na wafuate ratiba itakayokuwa inapangwa.“Nawasihi mtumie muda huu kusoma kwa bidii ili muweke msingi imara ya kujenga maisha yenu ya baadae. Msikubali kushawishika na kukatisha masomo yenu.”

  Naye, Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mbunge wa Kuteuliwa alisema shule hiyo inasomesha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kutoka mikoa yote nchini.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  ALHAMISI, OKTOBA 05, 2017.

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimia na wanafunzi Kike wanaosoma WAMA_SHARIF Sekondari .iliyopo Mkoani Lindi .Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kkikwete (MB) Waziri Mkuu ametembelea shule hiyo jana Oktoba 4,2017 alipokuwa katika ziara ya siku moja katika Mkoa wa Lindi jana
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  ahamasisha utunzaji wa mazingira Nchini kwakupanda Mti jana  Oktoba 4/2017 katika Shule ya WAMA_ SHARIF SEKONDARI.iliyopo Mkoani Lindi ,kushoto mwenye fimbo ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Daktari Hamisi Kigwangala na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)  Mama Salma Kikwete (MB) Waziri Mkuu alifanya ziara ya siku moja jana Mkoani Lindi .PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

  0 0

  Kufundisha Kwa Uhuru, Kuwawezesha Walimu Walimu ni msingi mkuu katika ustawi wa muda mrefu wa kila jamii kwa kuwa hujishughulisha kuwapatia watoto, vijana na watu wazima elimu na ujuzi wanaohitaji ili kufikia uwezo wao. 

  Lakini duniani kote, walimu wengi sana hawana uhuru na msaada wanaohitaji kufanya kazi yao iliyo muhimu sana. Ndiyo maana maudhui ya Siku ya Walimu Duniani kwa mwaka huu – ‘'Kufundisha kwa Uhuru, Kuwawezesha Walimu'’ - inathibitisha thamani ya walimu waliowezeshwa na kutambua changamoto ambazo wengi hukabiliana nazo katika maisha yao ya kitaaluma ulimwenguni kote. 

  Kuwa mwalimu aliyewezeshwa ina maana ya kuwa na uwezo wa kupata mafunzo yenye ubora, malipo ya haki, na fursa zisizo na mwisho za kujiendeleza kitaaluma. Pia inamaanisha kuwa na uhuru wa kuunga mkono maendeleo ya mitaala kitaifa – na uhuru wa kitaaluma wa kuchagua njia sahihi na mbinu zinazofaa zaidi kuwezesha utoaji wa elimu yenye ufanisi, jumuishi na ya usawa. Zaidi ya hayo, inamaanisha kuwa na uwezo wa kufundisha kwa usalama wakati wa mabadiliko ya kisiasa, machafuko, na migogoro. 

  Lakini katika nchi nyingi, uhuru wa kitaaluma na uhuru wa mwalimu viko chini ya shinikizo. Kwa mfano, katika ngazi za shule za msingi na za sekondari katika baadhi ya nchi, mipango ya uwajibikaji imeweka shinikizo kubwa kwa shule kutoa matokeo kwa vipimo vilivyowekwa, na kupuuza haja ya kuhakikisha mtaala wa msingi unaofaa mahitaji tofauti tofauti ya wanafunzi. 

  Uhuru wa kitaaluma ni muhimu kwa walimu katika kila ngazi ya elimu, lakini ni muhimu zaidi kwa walimu wa elimu ya juu, ili uwawezeshe kutumi uwezo wao wa kuvumbua, kuchunguza, na kuendeleza utafiti kuhusiana na namnaza kisasa zaidi za kufundisha. Katika ngazi ya elimu ya juu, mara nyingi walimu hupatiwa mikataba ya ajira ya kipindi maalumu. 

  Hii inaweza kusababisha hali ya kutokuwa na uhakika wa ajira kwa walimu, kupungua kwa matarajio ya kukua kitaaluma, mzigo mkubwa wa kazi na malipo duni – yote haya yanaweza kuzuia uhuru wa kitaaluma na kudhoofisha ubora wa elimu ambayo walimu wanaweza kutoa. 

  Katika ngazi zote za elimu, shinikizo la kisiasa na maslahi ya kibiashara yanaweza kuzuia uwezo wa walimu kufundisha kwa uhuru. Waalimu wanaoishi na kufanya kazi katika nchi na jamii zilizoathiriwa na migogoro na machafuko mara nyingi hukabiliwa na changamoto kubwa zaidi, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa kuvumiliana, ubaguzi, na vikwazo vinavyohusiana na utafiti na kufundisha. 

  Mwaka huu unaadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Mapendekezo ya UNESCO ya 1997 kuhusu Hali ya Wakufunzi wa Elimu ya Juu, ambayo inakamilisha Mapendekezo ya UNESCO / ILO ya 1966 kuhusu Hali ya Walimu. Kwa pamoja, vyombo hivi hufanya mfumo mkuu wa rejea juu ya haki na wajibu wa walimu na waelimishaji. Yote yanasisitiza umuhimu wa uhuru wa mwalimu na uhuru wa kitaaluma katika kujenga ulimwengu ambapo elimu na kujifunza ni kwa ajili ya wote. 

  Wakati dunia inapofanya kazi pamoja ili kufikia maono ya Malengo ya Maendeleo Endelevu, tunawaomba washirika wetu katika serikali, sekta ya elimu na sekta binafsi kujitolea kubeba jukumu la kuwaandaa waelimishaji wenye ujuzi ulio bora zaidi, wenye thamani na waliowezeshwa.

   Hii ni njia muhimu katika kuyafikia maono ya Malengo ya Maendeleo Endelevu hasa lengo namba 4 lenye nia ya kuwa na ulimwengu ambapo kila msichana, mvulana, mwanamke na mwanaume wanapata elimu bora na fursa za kujifunza katika maisha yao yote. 

  Hii inamaanisha kuwapatia walimu mazingira mazuri ya kazi na mishahara iliyo bora, ikiwa ni pamoja na walimu wa ngazi ya juu. Inamaanisha kuwapa walimu mafunzo na fursa ya kujiendeleza. Inamaanisha kuongeza idadi ya walimu wenye ubora, hasa katika nchi zenye idadi kubwa ya walimu na waelimishaji wasio na elimu ya kutosha. 

  Inamaanisha ya kuondoa vikwazo visivyo vya lazima katika utafiti na kufundisha na kulinda uhuru wa kitaaluma katika ngazi zote za elimu. Na mwisho, inamaanisha kuinua hadhiya walimu duniani kote kwa namna ambayo inaheshimu na inayoonyesha matokeo waliyonayo walimu katika jamii. 

  Katika Siku hii ya Walimu Duniani, ungana nasi katika kuwawezesha walimu kufundisha kwa uhuru ili kwamba, kila mtoto na kila mtu mzima awe huru kujifunza – kwa manufaa ya dunia iliyo bora zaidi. Imetolewa na Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO; Guy Ryder, Mkurugenzi Mkuu wa ILO; Anthony Lake, UNICEF Executive Director; Achim Steiner, UNDP Administrator; pamoja na Fred van Leeuwen, General Secretary of Education International.

  0 0


  Baadhi ya watumishi na wanawake wajasiriamali wakisikiliza maada.
   Katibu tawala wa Manispaa ya Temeke (DAS), Hashim Komba akizungumza na wanawake wajasiriamali wa wilaya hii katika jukwaa la wanawake jijini Dar es Salaam leo.
  KATIBU Tawala Wilaya ya Temeke Bw:Hashimu Komba aunda jukwaa la wanawake wajasiliamali wa wilaya ya Temeke ambao walijitokeza kwa wingi kutoka kata zote za wilaya hiyo. Akiongea na wanawake hao wajasiliamali leo katika ukumbi wa Iddi Nyundo Manispaa ya Temeke. 


  Kauli mbiu ya kikao hicho ni “Mwanamke tumia fursa kuimalisha uchumi wa viwanda” ambapo Katibu tawala huyo ameungana na juhudi za Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ikiwa ni mwendelezo wa uzinduzi wa jukwaa la wanawake katika kuinua uchumi wa mwanamke ili kuleta Maendeleo ya taifa kiwilaya.

   Kauli mbiu hiyo ilisemwa na Makamu wa Rais katika siku ya uzinduzi wa Jukwaa la uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kimkoa lililofanyika katika viwanja vya Posta,kijtonyama. Ambapo uzinduzi huo ni wa 23,lililoandaliwa na Baraza la uwezeshaji kwa ufadhili wa benki ya CRDB.

  Komba amewamwagia sifa wanawake kwa juhudi zao za kujikwamua kiuchumi katika jamii,aliwapongeza akina mama kwanamna wanavyojituma na kuwa waaminifu na kuwa na uwezo wa kusimamia vipato vyao vidogo wanavyopata kwa kujileta maendeleo makubwa. 

  Ahadi kuwa jukwaa hilo punde litakopo undwa litakuwa na tija kubwa katika kujitangazia biashara na ubunifu wa kazi zao wanazofanya katika ngazi za kimataifa,kitaifa,kimkoa,kiwilaya mpaka kata. Pia watapata fursa mbalimbali za kupiga hatua kama kushiriki maonesho ya kibiashara ya sabasaba na nanenane. 

  Hivyo asisitiza kuchaguliwa kwa viongozi walio na uwezo wakusimamia mawazo,ubunifu na ujuzi wa kazi zao ili kusimamia jukwaa hilo katika kujiletea maendeleo.

  Hata hivyo amewapa moyo kuwa kuelekea katika sera ya uchumi wa viwanda kwa kuanzia waendelea kutumia technolojia hizo hizo ndogondogo wanazotumia nyumbani kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni mfano wa viwanda vidogovidogo,wakati wanajiandaa kupata viwanda vikubwa. Kwakufanya hivyo watakuwa wanajiingizia kipato,pia kuinua uchumi wa viwanda katika nchi yetu.

  Katika kikao hicho katibu Tawala huyo alipongeza Idara  ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii inayoongozwa na John Bwana kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuwatambua wajasiliamali hao ambao wamejitokeza kwa wingi na shauku kubwa kuunda jukwaa hilo.

  Jukwaa hilo linatazamiwa kuzinduliwa hivi karibuni ikiwa lengo kuu ni kumwinua mwanamke kufikia katika uchumi wa kati, ambapo inasemekana mwanamke ni mlezi wa familia na jamii, ukimwezesha mwanamke imeliwezesha taifa.

  0 0  0 0


  Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za juu kusini Jackson Kiswaga (kushoto) Mkuu wa wilaya Wanging'ombe Ally Kasinge Katikati) Mkuu wa shule ya Sekondari Njombe Benard William  wakikata utepe kufungua kufungua  darasa la kusomea wanafunzi kwa njia ya mtandao. Msaada huo umetolewa jana na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo mkoani Njombe.
  Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Ally Kasinge (kulia) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe akipokea kifaa cha kupokelea mawimbi ya intaneti kutoka kwa mkurugenzi wa Tigo kanda ya Nyanda za juu kusini Jackson Kiswaga,   msaada huo umtolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa ajili ya Shule ya sekondari Njombe.
  Mkuu wa Wilaya Wanging'ombe Ally Kassinge (wa pili kushoto) akipata maelekezo ya matumizi ya kompyuta zinazo tumia mtandao wa Intanet toka kwa mkurugenzi wa Tigo kanda ya Nyanda za juu kusini Jackson Kiswaga katika Darasa la wanafunzi wa shule ya sekondari Njombe, Msaada huo umetolewa jana na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo mkoani Njombe.

  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na wananchi wa eneo la Lizaboni wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo na kutii sheria za nchi pamoja na kuwafichua wahalifu waliopo kwenye jamii, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja. 
   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na wananchi wa eneo la Lizaboni wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo na kutii sheria za nchi pamoja na kuwafichua wahalifu waliopo kwenye jamii, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja. 
   Askari wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu na wahalifu katika mkoa wa Ruvuma, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, na kuwataka kufanyakazi kwa kuzingatia sheria na taratibu pamoja na kutimiza wajibu wao wa kutenda haki wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi.

   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro (watatu kulia kwenye meza kuu) na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Binilith Mahenge,  wakiwa kwenye kikao cha pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na Maofisa na askari na kuona changamoto zao ikiwa pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki na kutoa huduma bora kwa wananchi
   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro (watatu kulia kwenye meza kuu) na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Binilith Mahenge,  wakiwa kwenye kikao cha pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na Maofisa na askari na kuona changamoto zao ikiwa pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki na kutoa huduma bora kwa wananchi

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  BENKI ya DCB imesherehea wiki ya huduma kwa wateja kwa kufurahi pamoja na wateja wa benki hiyo huku wakiendelea kuwahamisha kutumia huduma ya DCB Pesa popote nchini.

  Katika maadhimisho ya wiki kwa huduma kwa wateja, Afisa Mikopo wa DCB tawi la Magomeni Miriam Migetto amesema kuwa wanayofuraha ya kujumuika pamoja na wateja wa benki hiyo kusherehekea siku hii muhimu kwao pia na kuwasisitiza kuendelea kutumia huduma za kibenki.

  Miriam amesema kuwa kwa sasa wanaendelea kuboresha huduma za kibenki ikiwemo kutumia huduma ya DCB Pesa na DCB Jirani ikiwa ni katika kurahisisha huduma za kipesa kwa wateja wa DCB.

  Afisa Mikopo wa DCB tawi la Magomeni Miriam Migetto akizungumza na wateja wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ma kuwataka kuendelea kutumia huduma za kibenki kwa njia ya simu pamoja na kuendelea kuchukua mikopo ya riba nafuu.


  Wafanyakazi wa tawi la benki ya DCB Magomeni wakiwa katika picha ya pamoja na wateja wa benki hiyo waliohudhuria kusherehekea maadhimisho ya wiki huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam leo.

  Moja ya wateja wa muda mrefu wa benki hiyo, Mama Fatma  Simba amesema kuwa ameanza kutumia benki hiyo tangu mwaka 2005 na amekuwa akipata huduma za kifedha kwa urahisi zaidi bila usumbufu na hata pia ameweza kupata mkopo wa bei nafuu na riba nafuu.

  "Nimekuwa natumia DCB benki kwa zaidi ya miaka 12 na imeweza kunipatia mahitaji yangu kwa wakati ikiwemo mkopo wa bei nafuu na riba nafuu na hata katika utoaji wa huduma za kibenki kupitia DCB Pesa wameweza kutupunguzia wateja wao kwenda benki mara kwa mara, " amesema mama Fatma.

  DCB benki wamesherehea wiki ya huduma kwa wateja katika matawi tofauti na kufurahi pamoja na wateja wao na kuahidi kuzidi kuboresha na  kuwapatia huduma wanazostahili na wakati sahihi.
  Moja ya wateja wa mda mrefu wa benki ya DCB Mama Fatma Simba akielezea namna benki hiyo ilivyweza kumsaidia katika shughuli zake za ujasiriamali mpaka alipofikia sasa na kuwataka wanawake waache tamaa pindi wanapochukua mikopo na kusifia pia huduma za DCB Pesa katika urahisishaji wa huduma za kipeki kupitia simu ya mkononi.

  Baadhi wa wafanyakazi wa Benki ya DCB Tawi la Mabibo External wakiwa katika picha ya pamoja  katika kuazimisha wiki ya huduma kwa wateja.

  0 0

    Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika hospitali hiyo, Dk. Hedwiga Swai akisisitiza watu kujitokeza kupima afya ili kuthibiti homa ya ini pamoja na magonjwa mengine.
   Baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo wakiwamo madaktari na wauguzi wakifuatilia kongamano hilo.
   Daktari Bingwa wa Magomjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, John Rwegasha wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza katika kongamano jinsi ya kudhibiti na kutibu magonjwa ya mfumo wa chakula na ini.
  Baadhi ya madaktari, wauguzi wa hospitali hiyo na watumishi wengine wakiwa kwenye kongamano hilo leo.
   Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, Priumus Saidia akizungumza kwenye kongamano hilo leo.


  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imetoa ripoti ya robo mwaka tangu ianze kufanya uchunguzi wa Virusi vya Homa ya Ini ( Hepatitis B) na kutoa tiba ya ugonjwa huo kwa kutumia dawa ya Tenofovir .

  Akitoa taathimini hiyo leo jijini Dar es salaam,  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Matumbo John Rwegasha amesema  muamko ni mkubwa  ambapo katika kipindi cha robo mwaka , Hospitali ya Taifa Muhimbili imesajili wagonjwa  950 .

  Akifanunua amesema  hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu idadi  ya wagonjwa itaongezeka na kufika   1800  .Hata hivyo kati ya hao , wagonjwa 540 ndio wamerudi tena Hospitalini kwa ajili ya kuendelea na mchakato wa uchunguzi huku wagonjwa wengine wakishindwa kufika kutokana na sababu za mbalimbali hususani za kiuchumi , nakuongeza kwamba waliopo kwenye tiba ni  wagonjwa 40.

  ‘’Idadi ya wagonjwa imeongezeka mara dufu hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu watafika wagonjwa 1800  lakini pamoja na changamoto hiyo hatuwezi kusimamisha huduma tutaendelea kutoa huduma kwani kwa upande wa dawa tumejidhatiti kwa miaka mitano , wagonjwa  hawa wanatakiwa wafanyiwe uchunguzi  ili aanze kutumia dawa lakini  si wote wanaohitaji dawa’’ amesema DK. Rwegasha.

  Kwa upande wake Dk. Tuzo Lyuu amesema tatizo la ugonjwa huo ni kubwa kwani tafiti ambazo zimefanyika ,  watu wanaoenda kuchangia damu asilimia nane wanatatizo hilo na kusisitiza kuwa tatizo hilo si la Tanzania pekee bali  hata kwa nchi zingine zinazoendelea.Kwa mujibu wa Dk. Lyuu kwa sasa tatizo la Homa ya Ini (Hepatitis B) ni kubwa kuliko Ukimwi .‘’ Hapa MNH watu tunaowaona ni vijana na watu wazima na wanaume ndio wengi ingawa hakuna takwimu halisi’’ amesema Dk. Lyuu.

  Ugonjwa wa Homa ya Ini unasababishwa na Virusi viitwavyo Hepatitis B na maambukizi ya ugonjwa huo yanashabiana na njia ya  maambukizi ya Vrusi vya  Ukimwi kama vile kufanya ngono zisizo salama, kuchangia sindano au vikatio, kupewa damu isiyopimwa , kupitia uzazi wa mama na mtoto hasa wakati wa kujifungua.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  IDARA YA UHAMIAJI   WAGENI WOTE WENYE VIBALI VYA UKAAZI WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA OFISI ZA UHAMIAJI ZILIZOPO KATIKA MAENEO WANAYOISHI NA KUFANYIA KAZI WAKIWA NA VIBALI VYAO.

  Idara ya Uhamiaji inapenda kuwafahamisha Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni, Taasisi mbalimbali na Wageni wote wanaoishi na kufanya kazi nchini kwamba wanatakiwa kuripoti na kuwasilisha taarifa za anuani zao zikiwemo na mabadiliko katika Ofisi za Uhamiaji zilizopo katika maeneo wanayoishi na kufanya kazi katika kipindi cha siku thelathini 30 tangu kutolewa kwa taarifa hii.

  Zoezi hili linafanyika kwa lengo la kuhuisha taarifa na kumbukumbu za Wageni wakaazi ambao baadhi yao wamehama maeneo yao ya awali na kuhamia sehemu nyingine na linafanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 29 (1), (2) na 30 za Kanuni za Uhamiaji za Mwaka 1997 na Marekebisho yake ya Mwaka 2016, chini ya Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 Rejeo la Mwaka 2002.

  Aidha, ieleweke kwamba kutokufanya hivyo ni kosa kisheria chini ya Kanuni ya 29 (3) na 37 ya Kanuni za Uhamiaji za Mwaka 1997 na marekebisho yake ya mwaka 2016 chini ya sheria ya uhamiaji sura 54 rejeo la mwaka 2002.

  Imetolewa na

  SAMWEL RHOBBY MAGWEIGA
  KAMISHNA WA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA MIPAKA,
  MAKAO MAKUU YA UHAMIAJI,
  04 OKTOBA, 2017.

  0 0

  HUDUMA ya upasuaji wa magonjwa ya moyo kwa watoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete imezidi kuimarika tangu ilipoanzishwa rasmi mwaka 2015 hadi sasa.

  Hayo yalielezwa Dar es Salaam jana na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto wa JKCI, Naiz Majani alipozungumza na waandishi wa habari.

  Dk. Naiz alikuwa akizungumza kuhusu upasuaji ulioanza kufanyika hospitalini hapo siku ya jumatatu kwa watoto waliozaliwa na magonjwa mbalimbali ya moyo.

  Alisema JKCI inafanya upasuaji huo ambao unatarajiwa kukamilika kesho (leo) kwa kushirikiana na madaktari bingwa wenzao kutoka Shirika la Kimarekani la Mending Kids International ambapo jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao 19 wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.

  “Huduma za matibabu ya moyo zilianza rasmi kutolewa nchini mnamo mwaka 2008, hadi kufikia 2015 tuliweza kuwafanyia upasuaji watoto 200 pekee utaona hiyo ni ndani ya miaka saba ya kipindi hicho,” alisema.

  Aliongeza “Lakini mwaka 2015 tuliona vema kuanzisha kitengo maalumu cha upasuaji kwa ajili ya watoto, hadi kufikia mwaka huu tumeweza kuwafanyia upasuaji watoto zaidi ya 500 hiyo ni ndani ya kipindi cha miaka miwili pekee.

  “Kwa hiyo tunaona manufaa makubwa ya kuanzishwa kwa kitengo hiki kwani tumeweza kuokoa maisha ya watoto wengi ambao tungewapoteza, kwa mwaka serikali ilikuwa na uwezo wa kupeleka nje ya nchi watoto 40 hadi 80 kupatiwa matibabu haya,” alisema.

  Alisema pamoja na watoto hao, kuna wengine 145 ambao wanasubiri huduma ya upasuaji.

older | 1 | .... | 1389 | 1390 | (Page 1391) | 1392 | 1393 | .... | 1897 | newer