Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, MHANDISI RAMO MAKANI AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUTUNDIKA MIZINGA KITAIFA MKOANI SIMIYU

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu baada ya kuwasili wilayani hapo kwa ajili ya kuongoza maadhimisho ya siku ya utundikaji wa mizinga kitaifa yaliyofanyika jana mkoani humo.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akitundika mzinga wa kisasa wa nyuki katika Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Jumla ya mizinga 50 ilitundikwa wilayani humo. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ni “Ufugaji nyuki kibiashara unachangia katika ukuaji wa viwanda”.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa (kulia) akitundika mzinga wa kisasa wa nyuki katika Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Jumla ya mizinga 50 ilitundikwa wilayani humo. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ni “Ufugaji nyuki kibiashara unachangia katika ukuaji wa viwanda”. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akimuelekeza jambo Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa kuhusu upatikanaji wa vifungashio bora vya mazao ya nyuki (asali na nta) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. 
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Nyuki wa TFS Kanda ya Ziwa, Samuel Magire kuhusu kifaa maalum aina ya Analogy Honey Refractometer kinavyopima ubora wa asali kwa kuangalia wingi wa maji na sukari wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ni “Ufugaji nyuki kibiashara unachangia katika ukuaji wa viwanda”. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akipima ubora wa asali kwa kutumia kifaa maalum aina ya Analogy Honey Refractometer  ambacho huangalia wingi wa maji na sukari wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza na Afisa Nyuki wa TFS Kanda ya Magharibi, Karim Solyambi kuhusu ufugaji wa nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa ambayo huongeza uzalishaji wa asali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. 
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akizungumza na Afisa Nyuki wa TFS Kanda ya Ziwa, Samuel Magire kuhusu ufugaji wa nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa ambayo huongeza uzalishaji wa asali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Benson Kilangi.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akiangalia tuzo na cheti walichopewa kikundi cha Isengwa Lagangabilili kwa kuwa wafugaji bora wa nyuki katika Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Benson Kilangi
 Baadhi ya wananchi walioshiriki Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa maadhimisho hayo kutoka kwa mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (hayuko pichani). Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ni “Ufugaji nyuki kibiashara unachangia katika ukuaji wa viwanda”. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani azingumza katika mkutano wa hadhara kwenye maadhimisho hayo katika kijiji cha Lagangabilili wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili akizungumza katika maadhimisho hayo.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Tele Ndaki akiwasilisha salamu za Mkoa kwenye maadhimisho hayo.
Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama (CCM), Serikali, waandaji pamoja na waratibu wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa yaliyofanyika jana katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.
Mbunge wa Itilima, Njalu Daudi Silanga akisalimia wananchi kwenye mkutano wa hadhara wakati wa maadhimisho hayo.
Burudani ya kucheza na nyoka pia ilikuwepo katika maadhimisho hayo. 
(PICHA NA HAMZA TEMBA - WIZARA YA MALISILI NA UTALII)
HOTUBA YA NAIBU WAZIRI, MHANDISI RAMO MAKANI KATIKA MAADHIMISHO HAYO

HOTUBA YA MKURUGENZI WA IDARA YA MISITU NA NYUKI, DKT. EZEKIEL MWAKALUKWA KATIKA MAADHIMISHO HAYO


JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAFANYA KIKAO NA SHIRIKI LA VIWANGO TANZANIA (TBS) JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Prof. Egird Mubofu (kulia), akizungumza na Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, (kushoto) alipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhali dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, akimkabidhi kipeperushi chenye namba ya dharura 114 ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Prof. Egird Mubofu (kulia), wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhali dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, akielekea katika ukumbi wa Mikutano kwa mazungumzo, akiwa ameambatana na mwenyeji wake ambaye ni Afisa habari wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bi. Neema Mtema (wapili kulia), pamoja na Maafisa wa Jeshi mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Shirika hilo, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhali dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, akimuelezea majukumu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mwenyekiti wa Kikao Kaimu Mkuu wa Kitengo cha uhakiki (HCERT), Eng. Agnes Kiweru ambaye hayupo pichani, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhali dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Viwango wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Bi. Edna Ndumbaro (katikati), akitoa ufafanuzi kwa hatua walizozichukua kuhusiana na vifaa vya Zimamoto, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhali dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha uhakiki (HCERT), Eng. Agnes Kiweru (kulia) mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Bodi ya TPSC Yaagizwa Kusimamia Utoaji wa Elimu Bora

$
0
0
Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Henry Mambo akitoa taarifa ya chuo hicho wakati wa uzinduzi wa bodi ya ushauri ya chuo hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (katikati) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa bodi ya ushauri ya chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro na kushoto ni Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Henry Mambo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (katikati) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa bodi ya ushauri ya chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania pamoja na menejimenti ya chuo hicho wakati wa uzinduzi wa bodi ya chuo hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (kushoto) akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Charles Msonde wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Charles Msonde (kulia) akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania mara baada ya kuizindua mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo


Thobias Robert – Maelezo


Bodi ya ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) imetakiwa kuhakikisha inaimarisha utoaji wa elimu bora na yenye viwango kwa watumishi wa umma ili kuendana na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano inayotaka watumishi wenye weledi na wenye maadili katika sekta za umma na binafsi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki alipokuwa akizindua Bodi ya washauri wa chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.

Waziri Kairuki ameeleza kuwa ni wakati sasa kwa chuo hicho kuwa mfano bora wa kutoa watumishi ambao watarejesha nidhamu, utumishi bora na uadilifu wa hali ya juu katika sekta za umma na binafsi ili kumaliza tatizo la watumishi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo viovu kama rushwa na matumizi mabaya ya ofisi.

“Chuo cha utumishi wa umma hapa nchini kilianzishwa kwa lengo la kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma, hivyo Bodi ya ushauri wa chuo cha utumishi wa umma wa Tanzania inalo jukumu la kuhakikisha kuwa lengo hili linatekelezwa kwa ufanisi mkubwa,” alisema Waziri Kairuki.

Aliongeza kuwa bodi hiyo pia inalo jukumu la kutoa ushauri katika mipango yote ya maendeleo, kushauri na kupitisha mpango kazi na bajeti ya chuo pamoja na kufanya tathimini ya mwaka ya utendaji wa chuo na masuala mengine ya muhimu yanayopaswa kutolewa ushauri.

“Nina matarajio makubwa kwamba, mtatekeleza majukumu hayo na mengine ambayo sikuyataja lakini yameelezwa katika sheria husika ili kuhakikisha kwamba, chuo cha utumishi wa umma kinakidhi matarajio ya serikali pamoja na wadau na kuleta tija na ufanisi katika utumishi wa umma hapa nchini,” alifafanua Waziri Kairuki.

Katika hafla hiyo iliyojumuisha wajumbe waliomaliza muda wao pamoja na wale waloteuliwa Waziri kairuki alisema kuwa, chuo hakina budi kupunguza kozi zisizo na soko kwa ajili ya kutoa elimu kwa ufanisi na tija kwa wanafunzi kama ilivyo kusudi la kuanzishwa kwa chuo hicho ambalo ni kutoa elimu kwa watumishi wa umma.

Aidha Waziri Kairuki amewapa changamoto wajumbe wa bodi hiyo walioteuliwa katika bodi hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia, uendelevu wa chuo (Sustainabilty), kujitangaza kwa chuo ili kuongeza idadi ya wanafunzi, kozi gani zinazoweza kuwavutia wanafunzi, kufanya tathmini ya wanafunzi wanaohitimu chuoni hapo kama wanakidhi vigezo katika ofisi za waajiri wa ofisi za umma na zile za binafsi.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC), Dkt. Henry Mambo alisema kuwa kwa sasa chuo hicho kimefanikiwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi, kutoa machapisho mbalimbali ya ndani na nje, kuanzisha kozi za shahada na kuongeza idadi ya wahitimu.

Dkt. Mambo alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa chuo hicho kimeweza kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi takribani 58221, katika Nyanja za uongozi, menejimenti na utawala bora, chuo kinadahili na kutoa mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi wa umma na watumishi tarajali wapatao 132890 na kati ya hao watumishi wa umma wanatarajia kuwa 29240 ambayo ni sawa na asilimia 22.

Naye Mwenyekiti mteule wa Bodi hiyo Dkt. Charles Msonde alisema kuwa atashirikiana na wajumbe, watendaji na Wizara ya utumshi kuendeleza mafunzo bora kwa watumishi wa umma ili kuendana mabadiliko ya sayansi na teknoljia pamoja na uhitaji wa soko hapa nchini na nje ya nchi.

Bodi hiyo inaundwa na wajumbe sita ambao ni Dkt. Charlse Msonde (Mwenyekiti), na Prof. Bernadetha Killian,Bibi. Anna Maembe, John Ullanga, Solanus Nyimbi, Bi. Roxana Kijazi

Chuo cha utumishi wa Umma kilianzishwa mwaka 2000 kwa lengo la kutoa elimu na mafunzo kwa watumishi wa umma hapa nchini na nje ya nchi,chuo hiki kipo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kina matawi sita katika mikoa ya Mbeya, Dar es Salaam (Magogoni), Mtwara, Singida, Tabora na Tanga

BALOZI WA MOROCCO ATEMBELEA TADB

$
0
0
Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane (kulia) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea Ofisi za Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco (GCAM), Bw. Jamal Eddine el Jamali (katikati).DSC02842
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akizungumza wakati wa kikao cha pamoja cha ushirikiano kati ya TADB na GCAM.
DSC02843
Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane (kulia) akizungumzia mafanikio ya utekelezaji wa makubaliano kati ya Mfalme wa Morocco na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco (GCAM), Bw. Jamal Eddine el Jamali (katikati) na Mkurugenzi wa masuala ya kilimo ya GCAM, Bw. Mustapha Chehhar.
DSC02844
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akimsikiliza kwa makini Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Saleh (kulia) wakati wa kikao cha pamoja kati ya GCAM na TADB.
DSC02845
Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane (kushoto) akiangalia zawadi aliyokabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) mara baada ya kikao cha pamoja kati ya GCAM na TADB.
DSC02846
Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane (wapili kushoto) akionesha picha ya mchoro wa tembo aliyokabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (wapili kulia) mara baada ya kikao cha pamoja kati ya GCAM na TADB. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco (GCAM), Bw. Jamal Eddine el Jamali (kushoto) na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Saleh (kulia).
DSC02847
Picha ya pamoja! Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na mara baada ya kikao cha pamoja kati ya GCAM na TADB.
……………..
Na mwandishi wetu,
Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane ametembelea Ofisi za Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kufuatilia utekelezaji wa  Mkataba wa Ushirikiano uliosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Morocco wakati wa Ziara ya Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI alipotembelea nchini Tanzania mwezi Oktaba mwaka jana.
Mheshimiwa Benryane ambaye alifuatana na uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco (GCAM), ulioko nchini kwa ajili ya kikao cha pamoja cha ushirikiano na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya kilimo inayotekelezwa kati ya Benki hiyo na TADB.
Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kati ya GCAM na TADB, Mheshimiwa Benryane alisema kuwa utekelezaji wa makubaliano kati ya Mfalme wa Morocco na Rais Dkt. John Pombe Magufuli yanaendelea vizuri na kutolea mfano mashirikiano kati ya benki hizo mbili kwa upande wa miradi ya kilimo.
“Ni chini ya mwaka mmoja tangu viongozi wetu wakubaliane utekelezaji wa mikataba 21 katika nyanja mbalimbali zikiwamo za kilimo, gesi, madini na na usafiri wa anga,” amesema.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga aliishukuru GCAM kuichagua TADB kusimamia miradi ya utekelezaji wa makubaliano hayo kwa upande wa kilimo.
Kwa mujibu wa Bw. Assenga, pamoja na kupanga mikakati hiyo, ujumbe huo ulipata fursa ya kukagua miradi kadhaa ya kilimo na ufugaji ambayo Tanzania inaweza kuianzisha kwa mafanikio.
TADB imeanzishwa kwa malengo makuu ya Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania; na Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

KATIBU MKUU MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO BIBI SIHABA NKING AFUNGUA MKUTANO WA MKUU WA MWAKA KWA MAAFISA WA USTAWI WA JAMII NCHINI MJINI DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akisikiliza Maelezo kutoka kwa washiriki tofauti wa Mkutano Mkuu wa Maafisa Ustawi wa Jamii nchini katika moja ya eneo la maonesho ya masuala yahusuyo Ustawi wa Jamii wakati wa Ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi akipokea moja ya kitabu kinachoelezea masuala mbalimbali ya Ustawi wa Jamii kutoka kwa mshiriki wa Mkutano Mkuu wa Maafisa wa Ustawi wa Jamii nchini wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Maafisa wa Ustawi wa Jamii nchini uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa TASWO Dkt. Zena Mabeyo akitoa salamu za wananchama wa TASWO kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(kulia waliokaa) wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Maafisa wa Ustawi Jamii nchini uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Taasisi ya JSI Dkt.Tuli Tuhuma akitoa maelezo kuhusu kazi za Taasisi yake kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(kulia waliokaa) katika kuleta ufanisi wa kazi za Ustawi wa Jamii nchini wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Maafisa Ustawi wa Jamii nchini uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.
Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Abu Mvungi akitoa mada kuhusu umuhimu wa Maafisa Ustawi wa Jamii nchini wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Maafisa hao uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(kushoto) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa TASWO Dkt. Zena Mabeyo(kulia) wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Maafisa Ustawi wa Jamii nchini uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akizungumza na Maafisa Ustawi wa Jamii nchini kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Maafisa hao uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.
Baadhi ya Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Serikalini na Taasisi na Mashirika yasiyo ya kiserikali wakimsikiliza Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(hayupo pichani) wakati akizungumza nao kabla ya kufungua wa Mkutano Mkuu wa Maafisa hao uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(wa pili kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii nchini mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Maafisa  hao uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

NMB MD INEKE BUSSEMAKER SPEAKS DURING THE OFFICIAL LAUNCH OF CUSTOMER CARE WEEK OCT 02 2017

BENKI YA WALIMU, (MCB), YAUNGANA NA WATEJA WAKE KUADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DUNIANI

$
0
0

 Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc, (MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia Ndongole,(kulia), akimpatia zawadi, mmoja wa wateja wa benki hiyo, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Oktoba 4, 2017, kwenye tawi la benki hiyo barabara ya Samora jijini Dar es Salaam.
NA K-VIS BLOG
Wiki ya kwanza ya Mwezi Oktoba kila mwaka, hutumika kama Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani, ambapo taasisi za umma na binafsi, hujumuika pamoja na wateja wao kwa lengo la kuonyesha mahusiano mema katika kutoa huduma na pia kuzunhumzia changamoto za kihuduma kwa mwaka mzima na hatimaye kutafuta njia za kuzitatua changamoto hizo.

 Kwa upane wake, MCB iliwaalika wateja wake, na kujumuika nao kwenye tawi la benki hiyo, barabara ya Samora jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi wa benki hiyo walitumia wasaa huo kuwashukuru, wateja lakini pia kuwahamasisha zaidi kutumia huduma za benki hiyo ambazo ni pamoja na kutoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa serikali, wafanyabiashara, wakulima na wananchi kwa ujumla. Hali kadhalika huduma za ATM ambazo zinapatikana Umoja Switch wenye mtandao mpana nchi nzima.

Maafisa wa benki hiyo pia ili kurahisisha huduma zaidi za kibenki, pia huduma ya kiganjani, sim banking ni miongoni mwa huduma zitolewazo na benki hiyo.Katika hafla hiyo, MCB ilitoa zawadi mbalimbali kwa wateja ili kuonyesha shukrani na kuwaahidi kuendelea kutoa huduma bora zaidi.
 Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc, (MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia Ndongole,(kulia), akimpatia zawadi, mmoja wa wateja wa benki hiyo, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Oktoba 4, 2017, kwenye tawi la benki hiyo barabara ya Samora jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc, (MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia Ndongole,(kulia), akimpatia zawadi, mmoja wa wateja wa benki hiyo, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Oktoba 4, 2017, kwenye tawi la benki hiyo barabara ya Samora jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Huduma kwa Wateja, MCB, Bi.Flora C. Mbogo, akziungumza wakati wa hafla hiyo.
 Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko cha benki hiyo,  Bw. Valence Luteganya, (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Wateja, MCB, Bi.Flora C. Mbogo,na Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc, (MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia Ndongole.
 Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc, (MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia Ndongole, (kushoto), akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko cha benki hiyo,  Bw. Valence Luteganya, wakati akizungumza na wateja wa benki hiyo.
 Viongozi wa MCB, wakiungana na baadhi ya wateja wao kukata keki, ikiwa ni ishara ya kusherehekea pamoja katika kipindi cha wiki ya Huduma kwa Wateka, wkenye tawi la benki hiyo la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam.
 Meneja wa Huduma kwa Wateja, MCB, Bi.Flora C. Mbogo,akikata keki.
  Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc, (MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia Ndongole, akimlisha keki, mmoja wa wateja waliohuduria hafla hiyo.
 Wafanyaakzi wa MCB, wakiwa katika picha ya pamoja.
 Baadhi ya wateja waliohudhuria hafla hiyo kwa kutumia simu zao wakirekodi matukio.
 Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko cha benki hiyo,  Bw. Valence Luteganya,(kushoto), akifurahia pamoja na wafanyakazi wenzake wakati akitambulisha picha ya Mfanyakazi bora wa mwezi wa benki hiyo, Bw. Ombeni S. Kaale.
 Picha ya pamoja ya wafanyakazi na wateja wa MCB.
Baadhi ya wafanyakazi wa MCB.

SBL yatoa bajaji kwa wasambazaji wake bora

$
0
0

Meneja usambazaji wa SBL kanda ya Dar es salaam , Malila Mmasi akikabidhi funguo kwa mwakilishi wa kampuni ya Smart  Builders wakati wa makabidhiano kwa kampuni  nne zinazofanya vizuri katika usambazaji wa bidhaa zinazozalishwa na SBL,bajaj yenye thamani ya shilingi milion 3.9 kila moja kwa ajili ya kurahisisha shughuli zake za usambazaji, kwa ujumla bajaj hizo zina thamani ya sh milioni 15.6. Hafla ya makabidhiano zilifanyika mapema leo katika ofisi za makao makuu SBL Temeke Jijini Dar es salaam.



Meneja usambazaji wa SBL kanda ya Dar es salaam , Malila Mmasi akikabidhi mwakilishi wa kampuni ya Mount Cameroon.

Meneja usambazaji wa SBL kanda ya Dar es salaam , Malila Mmasi akikabidhi mwakilishi wa kampuni ya  kimori investment mara ya kuibuka mshindi wa msambazaji bora katika hafla iliyofanyika mapema leo Jijini Dar es salaam.

Mwakilishi kutoka kampuni ya  kImori investment akiongea kea niaba  ya washindi

Meneja usambazaji wa SBL kanda ya Dar es salaam , Malila Mmasi, akiongea na wanahabari wakati wa hafla ya utoaji zawadi.
Bajaji zilizotolewa kwa washindi wa usambazaji wa Bidhaa za SBL.

Mwakilishi kutoka kampuni ya Smart builders akijaribu kuendesha bajaj aliyokabidhiwa kama zawadi.



Waandishi wa habari wakishuhudia makabidhiano ya zawadi.
Mwakilishi kutoka kampuni ya Kimori Investment akijaribu kuendesha bajaj aliyokabidhiwa kama zawadi mapema leo katika ofisi za makao makuu ya SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam, Oktoba 3, 2017 - Kampuni nne za usambazaji wa vinywaji kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Rukwa na Arusha zimejishindia bajaji moja moja yenye thamini ya shilingi 3.9m/- kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).
Kampuni hizo zimezawadiwa bajaji baada ya kuibuka wasambazaji bora wa bidhaa za SBL katika mikoa yao. Kampuni zilizoibuka washindi ni MM Group, Smart Builders, Kimori Investments NA Mount Cameroon inayofanya kazi katika mikoa ya Mbeya na Rukwa, Arusha na Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa hafala fupi ya kukabidhi zawadi hizo iliyofanyika Meneja usambazaji wa SBL kanda ya Dar es salaam , Malila Mmari amewapongeza washindi kwa kufanya kazi kwa bidii na kuweza kushinda bajaji hizo zenye thamani ya jumla ya shilingi 15.6m/-
Mmasi amesema kampuni hizo nne zimeweza kuibuka washindi katika usambazaji wa pombe kali pamoja na bidhaa nyingine za kampuni hiyo zikiwamo bia.
Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kusambazwa na SBL ni pamoja na bia ya Serengeti, Pilsner, Tusker Lager, Tusker Lite, Pilsner King, Kibo Gold, Guinness stout na Kick. Kampuni hiyo pia inasambaza pombe kali maarufu duniani kama Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum na Baileys Irish Cream.
“Tunawapongeza wasambazaji wetu hawa wanne ambao leo wameibuka washindi. Hii inaonyesha namna ambavyo wanafanya kazi kwa bidii na bajaji hizi zitawawezesha kufanya shughuli zao za usambazaji kwa urahisi zaidi,” alisema
Mmasi aliongeza kuwa zawadi kama hizo hutolewa na SBL kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya kuwapongeza na kuwatia nguvu wasambazaji wake wanaofanya vizuri
Aliwataka wasambazaji ambao hawakuweza kuibuka washindi kuendelea kufanya kazi kwa bidii huku akiwahakikishia kuwa zawadi zipo na kikubwa ni wao kuongeza jitihada

Mmasi aliwataka wasambazaji kufanya kazi kwa kushirikiana na kujituma lakini kwa ushindani ili pia waweze kushinda zawadi kubwa zaidi ambayo ni magari mapya aina ya Canter ambayo hutolewa wasambazaji wanaofanya vizuri kuliko wengine
Wakiongea wakati wa makabidhiano, wasambazaji hao wameshukuru SBL kwa kuwapa tuzo jambo ambalo wamesema litesaidia kukuwa kwa biashara zao huku wakiwataka wenzao ambao hawakufanikiwa kuibuka washindi kuongeza bidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kimori Investments Eden Kimori ambaye aliongea kwa niaba ya washindi wenzake alisema, motisha ya zawadi iliyoanzishwa na SBL imewafanya wasambazaji kufanya kazi kwa bidii zaidi
Alisema bajaji walizopewa zitawasaidia kuweza kufanya kazi ya usambazaji kwa urahisi zaidi na hivyo kuongeza mauzo yao.
Hii ni mara ya tatu kampuni ya SBL inawatunukia zawadi wasambazaji wanaofanya vizuri kwenye usambazaji wa bidhaa zake katika sehemu mbali mbali nchini. Mwezi Mei na Agosti mwaka huu, SBL ilitoa magari aina ya Eicher kwa sambazaji wake wa Katavi na Mwanza.

Benki ya UBA Tanzania wazidi kung'ara wiki ya huduma kwa wateja

$
0
0
 Afisa huduma kwa wateja wa Benki ya UBA Tanzania, Bi Stella Matau akifurahia kumuhudumia mmoja wa wateja wao wakubwa aliyefika katika benki hio huku benki hio ikiendelea kung'ara katika kutoa huduma bora kwa wateja kwa wakati wote
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya UBA Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wateja wao waliofika katika benki hio kwaajili ya kupata huduma za kibenki
Meneja Uendeshaji wa Benki ya UBA Tanzania, Bw Chriss Byaruhanga (wa Kwanza kushoto) akikata keko na baadhi ya wateja wao ikiwa ni ishara ya kuendeleza shamrashamra za wiki ya huduma kwa wateja ambapo wateja hao wameisifu benki hio kwa kutoa huduma bora wakati na sio kwa kipindi cha kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja Uendeshaji wa Benki ya UBA Tanzania, Bw Chriss Byaruhanga akigawa keki kwa baadhi ya wateja na wafanyakazi wa benki hio ikiwa ni ishara ya kuzindua wiki ya huduma kwa wateja.
Mmoja wa wateja wa benki ya UBA Tanzania akipata huduma ya kuweka pesa 
Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya UBA Tanzania, Brendasia Kileo akigawa keko kwa mmoja wa wateja waliokuwa wakipata huduma ndani ya benki mapema leo ikiwa ni muendelezo wa wiki ya Huduma kwa wateja
Wiki ya huduma kwa wateja inaendelea huku benki ya uba tanzania ikiendelea kutoa huduma bora na zenye kutimiza malengo ya wateja wao huku kituo chao cha huduma kwa wateja kikiendelea kushika hatamu kwa wateja wao kwa kuwapa huduma bora masaa 24.

 Uba Bank ambao hivi karibuni walijidhatiti tena kwa kuanzisha kituo cha huduma kwa wateja kwa masaa 24 wamezidi kuwapatia huduma bora wateja wao bila kuangalia kuwa ni wiki ya huduma kwa wateja wao Hutoa huduma bora siku zote.
Uba bank wanafurahi kuwahudumia wateja wao siku zote huku wiki ya huduma kwa wateja ikiendelea kuwa sehemu tu ya kuendeleza kutoa huduma bora kwa wateja.

NEC yatangaza uchaguzi mdogo kata 43

TCAA KUBORESHA MIUNDOMBINU UONGOZAJI NDEGE

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji Ndege Bw. Tuju Sharali akitoa maelezo kwa waandishi wa habari katika chumba maalumu kinachotumika kurusha na kutua ndege mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha juu cha kuongozea ndege wakiwa katika kazi ya mawasiliano kutoka vituo vingine vya kimataifa ili kuwezesha kuruka na kutuo kwa ndege za abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutembelea kituo hicho ili kujionea vifaa hivyo ambavyo vitabadilishwa na kuingia katika mfumo mpya wa uongozaji ndege .
Chumba na vifaa vya kuongozea ndege kuanzia umbali wa futi 24000 kwenda juu kinachotumika katika kuongozea ndege zikiwa juu zaidi, kurusha pamoja na kuziendesha wakati wa kutua katika idara ya uendeshaji na huduma za ndege(TCAA) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),leo jijini Dar es Salaam.
Rada inayotumika kwa sasa katika kuongoza ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kama inavyoonevyoonekana katika picha.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasilisno ya Uendeshaji Ndege wa (TCAA) Bw.Deodore Mushi akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu ufanyaji kazi wa mitambo ya kuongozea ndege katika kituo cha kuongoza ndege cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),leo jijini Dar es Salaam.Picha na: Paschal Dotto – MAELEZO

TANZANIA NA UINGEREZA ZAJADILIANA KUHUSU BIASHARA NA UWEKEZAJI

$
0
0
Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (kushoto) akizungumza kuhusu ushirikiano wa kibiashara na Tanzania alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani), katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (kushoto) akizungumza jambo aliokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa tatu kulia) kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na uwekezaji, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), wakimsikiliza kwa makini Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (hayupo pichani) alipokua akizungumzia mazingira bora ya kibiashara kwa maendeleo ya Taifa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akieleza kuhusu uimara wa Serikali katika kusimamia mazingira bora ya biashara ili kusaidia kuinua Sekta binafsi nchini, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamisha wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi (kulia) akizungumzia masuala ya kodi katika Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu na Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (hayupo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bw. John Rubuga.
moja wa wajumbe walioongozana na Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, (katikati) akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu na Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza Bw. Lord Clive Hollick (kushoto), mkutano huo umefanyika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa tatu kulia), Mwakilishi wa Biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (wa nne kushoto) na Maafisa waandamizi kutoka Uingereza na Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano kuhusu Biashara kati ya nchi hizio mbili Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – WFM)

VIJUSO VYA MAGAZETI YA ALHAMIS LEO OCTOBER 5,2017

BENKI YA AZANIA YAAMUA KWENDA BEGA KWA BEGA KUWATEMBELEA WATEJA WAKE

$
0
0
Na Mwandhishi Wetu
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, Benki ya Azania imeanza kuwatembelea wateja wake katika maeneo yao ya kazi ili kusikiliza kwa ukaribu changamoto wanazokutana nazo zinazohusu  huduma za kibenki, ikiwa ni pamoja na kuwashukuru kwa kuwa wateja wake.

Aidha, katika wiki hii ya huduma kwa wateja, Benki ya Azania imemtambulisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Azania Bank Limited, Ndugu Charles Jackson Itembe, ambaye pia ameongoza msafara wa kutembelea wateja katika maeneo yao ya kazi, ambapo mteja aliyetembelewa leo na Benki hiyo, Ndugu Augustine Nyato amekabidhiwa hati ya kuthaminiwa pamoja na biashara ya mteja huyo kuwa katika biashara watakazozipa kipaumbele.

Akizungumza na mteja huyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe amesema ikiwa Azania Benki inamjali mteja wameamua kuwatembelea wateja wadogo, wa kati na wakubwa ili kuwapa shukrani kwa kuendelea kuwa na wao katika biashara kwa kipindi kirefu na hata kwa kipindi kijacho ili kunafaika na benki hiyo.

Naye Mteja huyo ambaye ni Mkurugenzi wa  Israel Aaron & Company Augustine Nyato ameishukuru benki ya Azania kwa kutambua mchango mkubwa wa wateja wao mpaka wakaamua kumtembelea ili kusikiliza changamoto anazozipata katika benki hiyo pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana vyema katika kutoa huduma iliyobora ili kufikia malengo aliyojiwekea.

Wiki ya huduma kwa wateja imeanza rasmi Jumatatu ya Oktoba 2, 2017 na itamalizika baada ya wiki moja. Ni wakati wa taasisi kuwa karibu zaidi na wateja wake. Ni wakati wa kwenda bega kwa bega katika kuleta maendeleo kwa taifa letu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kushoto) akimkabidhi  hati ya kuthaminiwa mteja wa Benki ya Azania, Bwana Augustine Nyato leo ofisini kwake katika mtaa wa Survey jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Tawi wa Benki ya Azania  Tawi la Masdo, Benson Msuya.
 Mteja wa Banki ya Azania bwana Augustine Nyato( wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kushoto), Meneja wa Tawi wa Benki ya Azania  Tawi la Masdo, Benson Msuya(wa pili kutoa kulia) na Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati (kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kushoto) akimkabidhi  hati ya kuthaminiwa mteja wa Benki ya Azania, Bwana Augustine Nyato leo ofisini kwake katika mtaa wa Survey jijini Dar es Salaam.





WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2017: WATEJA NA WANACHAMA WA PSPF WAPATIWA HUDUMA ZA ZIADA

$
0
0
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

WATEJA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wanaofika kwenye ofisi za makao makuu jengo la Jubilee Tower jijini Dar es Salaam ili kujipatia huduma katika kipindi hiki cha Wiki ya Huduma Kwa Wateja Duniani, wamekuwa wakifaidika na huduma za ziada zinazotolewa na washirika wa Mfuko huo ambao wameweka kambi kwenye eneo hilo.

Washirika wa Mfuko walioweka kambi kwenye ofisi hizo tangu Otoba 2, 2017, ili kuwahudumia wateja ambao ni pamoja na Wastaafu na Wanachama wa PSPF ni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Benki ya CRDB, Benki ya Posta Tanzania, (TPB), Benki ya NMB na Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), Menenja wa Huduma kwa Wateja wa PSFP, Bi. Laila Maghimbi amesema.

“Kama mnavyoona, mwaka huu tumeamua kuongeza huduma za ziada kwa wateja wetu, yaani wastaafu na wanachama wanaofika kupatiwa huduma ofisini kwetu, ambapo Mteja baada ya kuhudumiwa pia anaweza kuonana na washirika wetu, ambapo NHIF wanafanya uchunguzi wa afya bure, mabenki nayo yapo hapa kuwaelimisha kuhusu jinsi wanavyoweza kuweka fedha zao na kupatiwa mikopo nafuu ili kuendesha miradi mbalimbali na hivyo kujiongezea kipato.” Alifafanua Bi. Maghimbi.

Alisema, nia ya Mfuko ni kuhakikisha wanafurahia huduma zitolewazo lakini pia kuonyesha kuwajali wateja wao kwa kuwasogezea karibu huduma muhimu za afya na kibenki.Wateja wamekuwa wakifurika kwenye ofisi hizo tangu Wiki ya Huduma kwa Wateja ianze Oktoba 2, 2017 na miongoni mwa huduma zitolewazo ni pamoja na wastaafu kufuatilia taarifa za michango yao, kuhakikiwa, kulipwa mafao na kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS).

Aidha wanachama wanaofika kwenye ofisi hizo wamekuwa wakipatiwa maelezo ya namna wanavyoweza kupatiwa mikopo ya viwanja na nyumba za makazi ambapo kampuni mshirika ya PSPF, Ardhi Plan Limited kupitia afisa wake, Bi.Anna Lukindo imekuwa ikifanya kazi hiyo.



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa pspf, Bw, Andrew Mkangaa, (wapili kulia), Meneja wa Huduma kwa Wateja, Bi. Laila Maghimbi, (watatu kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward(kulia), wakimsikiliza Daktari kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), kuhusu huduma wazitoazo kwa Wateja na wanachama wa PSPF kwenye ofisi za Mkao makuu ya Mfuko katika kipindi hiki cha Wiki ya Huduma kwa Wateja.


Maafisa wa Benki ya CRDB, Afisa Uendelezaji Biashara, Bw. Peter Christopher, (wapili kulia), na Afisa Mikopo kwa watumishi, Bi.Diana Jekela, (kushoto), wakiwahudumia wateja.

Afisa wa Benki ya NMB GTawi la Sinza jijini Dar es Salaam, Bi. Nadina Mpasha, (kulia0, akimpatia maelezo mteja aliyefika kwenye banda la benki hiyo kwenye ofisi za PSPF.
Dkt. Jason B.B Bagonza, (kushoto), ambaye ni Mchumi Mkuu kutoka Idara ya uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, akihudumiwa na maafisa wa benki ya Posta Tanzania, (TPB), Maafisa Masoko, Bi. Heavenlight A.Uiso na Bw.Nelson Mwakilasa

Maafisa wa Mwalimu Commercial Bank, (MCB), Plc, Mwajuma Gilbert, (kulia) na Michael Kachala, ambao ni maafisa wan huduma kwa wateja, wakitoa huduma.
Faiza Masoli, Afisa kitengo cha simu (Call Centre), cha PSPF, akiwa kazini.
Bi.Valley Malinga, Afisa kitengo cha simu (Call Centre), cha PSPF, akiwa kazini.

Afisa Huduma kwa wateja, PSPF, Bi.Elizabeth Shayo.
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa PSPF, Bi. Costantina Martin, akipitia taarifa za Mteja aliyefika kuhudumiwa
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa PSPF, Bi. Costantina Martin, akizungumza na mteja huku akimuonyesha taarifa yake.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward, akiwaeleza wateja hawa wa Mfuko huo, kuhusu huduma za ziada zinazopatikana kweye eneo hilo.
Afisa wa PSPF(kulia), akimpatia nyaraka Mwanachama huyu aliyefika kuhudumiwa kwenye ofisi hizo.
Anna Lukindo, (kulia), kutoka kampuni ya Ardhi Plan Limited, akimpatia maelezo Mwanachama wa PSPF aliyetaka kujua ni jinsi gani anaweza kupatiwa mkopo wa kiwanja.
Wanachama kushoto, wakihudumiwa na maafisa wa PSPF ambao wako makini katika kuwahudumia wateja wanaofika kwenye ofisi hizo.
Maafisa waandamizi wa PSPF, Bw. Gabriel P.Maro, (kushoto) na Bw. Abdul Njaidi wakifurahia jambo

SBL yakabidhi mradi wa maji wa thamani ya shilingi 80m/- kwa wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza

$
0
0

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. Angelina Mabula (aliyevaa kofia) akikata utepe kuzindua kisima cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh Milioni 80.



Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh,Angelina Mabula,akifungua kitambaa cha jiwe la msingi la kisima cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion.








Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula(aliyevaa kofia) akijaribu kumtiwhsa ndoo mara baada ya kuzindua kisima cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion










Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. Angelina Mabula(wa pili kulia) na Meneja wa Kiwanda cha bia cha Serengeti Mwanza Shekhar Makasare, wakimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela jana,anayeshuhudia pembeni ni Meneja Uwajibikaji kwa jamii wa SBL Hawa Ladha, wakati wa uzinduzi kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh Milion 80 .

















Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula,akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SBL Mwanza mara bada ya uzinduzi wa kisima cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion.

Meneja Uwajibikaji kwa jamii wa SBL Hawa Ladha, akizungumza na waandishi wa habari kijijini Maguha jana, wakati wa uzinduzi wa kisima,nkilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion
Kisima,kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti ambacho kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.
Wananchi wakichota maji mara baada ya uzinduzi.
Wafanyakazi wa SBL Mwanza na wakazi wa Ilemela wakishuhudia hafla ya uzinduzi wa kisima hicho.
Mkazi wa Ilemela akinywa maji kwenye ndoo mara baada ya uzinduzi wa kisima hicho.

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula(aliyevaa kofia) akicheza ngoma ya bugobogobo wakati wa kuzindua kisima cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion
Wananchi wakitoka kuchota maji mara baada ya kuchota maji katika kisima kilichozinduliwa mapema jana
wakazi wa kaguhwa Ilemela wakishangilia jambo wakazi wa Hafla ya uzinduzi wa kisima hicho mapema jana katika Jiji la Mwanza.


Kaguhwa Nyamhogolo Octoba 4, 2017 Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imekabidhi mradi wa maji safi wenye thamani ya shilingi milioni 80 kwa wakazi wa Kaghwa Nyamhogolo Wilayani Ilemela, Mkoani Mwanza.


Msaada huo ni sehemu ya jitihada za SBL kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama kwenye sehemu zenye uhitaji wa huduma hiyo muhimu. Ukiwa na uwezo wa kuhudumia watu 7,560, mradi huo unahusisha kisima, pampu ya maji pamoja na tanki lenye uwezo kuzalisha maji lita 4,000 kwa saa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi, Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL John Wanyancha alisema, mradi huo unaojulikana kama ‘Maji ni Uhai’ ni mmoja kati ya miradi ambayo SBL inaifadhili kwenye mikoa kama Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvunma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwezesha upatikanaji wa maji safi na salama kwa zaidi ya watu milioni moja.

Wanyancha alisema, mradi wa Kaghwa Nyamhogolo hautasaidia tu kuboresha afya za wakazi wa eneo hilo, bali pia utaongeza uzalishaji mali kwa kuwa wasichana na akina mama hawatatembea tena umbali mrefu kutafuta maji na kuongeza kuwa utawapa wasichana muda zaidi wa kuhudhuria shule.

SBL inayo sera inayolenga kuboresha maisha ya jamii zetu na Maji ni Uhai ni moja kati ya vipau mbele ambavyo vimeelezewa kwenye malengo ya kampuni yetu kuboresha maisha ya jamii inayotuzunguka,” alisemaWanyancha

Mkurugenzi huyo alitaja vipaumbele vingine kuwa ni pamoja na Kutoa ujuzi kwa ajili ya Maisha, Utunzaji wa Mazingira na Unywaji wa Kiasi.

Zaidi, Wanyancha alisema SBL inao mpango wa kusaidia wakulima ambao kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita umefanikiwa kuwafikia na kuwasaidia wakulima 100 kwa kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha hivyo kuweza kuboresha maisha yao na ya jamii zao

“Kupitia mpango huu, SBL imeweza kupata malighafi kwa ajili ya uzalishaji wake kutoka tani 0 hadi 10,000 zinazozalishwa na wakulima wa ndani jambo ambalo limesaidia ukuwaji wa kampuni na kuongeza kipato kwa wakulima pia,” alisema.

“Ukiachana na kuchangia uchumi wa nchi kupitia ulipaji kodi, SBL inatoa mchango wake kwa maendeleo ya nchi haswa kwa kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama hapa nchini,” aliongeza


Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni pia na Mbunge wa eneo hilo Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula aliishukuru SBL kwa msaada huo muhimu na uliokuwa unahitajika sana na kuongeza kuwa kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada ya kimaendele inayoigusa jamii

JARIDA LA NCHI YETU LA MWEZI SEPTEMBA

MKOA WA ARUSHA WAJIZATITI KUKAMILISHA ZOEZI LA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro akiwa kwenye kikao na Uongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kujadili kuanza kwa zoezi la Usajili Wilayani humo.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mhe. Viola Lazaro Likindikoki alipokutana na watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kujadili mpango wa Usajili kwenye Halmashauri hiyo.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha ndugu David Mwakiposa akizungumza na Viongozi wa NIDA walipotembelea ofisi yake leo kukamilisha mpango wa Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi na wageni wanaoishi mkoani humo.
Kamishna Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Arusha Bw. Ali Mohamed akisikiliza kwa makini mpango wa utekelezaji zoezi la Usajili wananchi mkoani humo wakati alipokutana na Viongozi NIDA na kukubaliana mpango wa pamoja wa utekelezaji wa zoezi hilo.


Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro ameuhakikishia Uongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) dhamira waliyonayo ya kuhakikisha wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea waishio mkoani humo hususani katika Wilaya ya Arusha wanasajiliwa Vitambulisho vya Taifa kwa wakati uliopangwa.

Kauli hiyo ameitoa leo alipokutana na uongozi wa Mamlaka, kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kuendesha zoezi hilo ambalo litaanza rasmi katika Wilaya hiyo Ijumaa Kata za Sekei, Themi na Sombetini.

Katika awamu hii ya kwanza takribani wananchi 45,000 watasajiliwa. Ametoa wito kwa wadau wote wakiwemo viongozi wa Dini, wanasiasa na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanasaidia kuhamaisha wananchi kushiriki kikamilifu zoezi hili ambalo lina manufaa makubwa katika maendeleo ya Taifa. Aidha; ameonya zoezi hilo kuhusishwa na siasa.

Naye Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mhe. Viola Lazaro Likindikoki ameahidi ofisi yake kwa kuhusisha wadau muhimu kushiriki kikamilifu kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa, na kwamba wakazi wa jiji hilo wanahamasishwa kushiriki.

Viongozi wengine waliopata fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo na uongozi wa NIDA ni Naibu Katibu Tawala wa Mkoa huo na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Arusha Bwana Ali Mohamed. Wilaya zingine za Mkoa wa Arusha tayari zimeanza zoezi la Usajili zikiwemo Monduli, Arumeru na Karatu.

Uongozi wa Mkoa wa Rukwa Waungana Kuwafariji Wafiwa Ajali Iliyoua 15 na Kujeruhi 9

$
0
0
Uongozi wa Mkoa wa Rukwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen umeungana na ndugu wa majeruhi 9 na wafiwa wa vifo vya watu 15 vilivyotokea katika ajali ya lori aina ya fuso eneo la Ntembwa, Wilayani Nkasi.

Katika kuhakikihsa tukio hilo halijirudii Mh. Zelote amepiga marufuku ukiukwaji wa sheria ya kupandisha abiria katika magari ya mizigo na kuonya kuwa yeyote atajayefanya hivyo achukuliwe hatua haraka iwezekanavyo.

“Nimekataza binadamu kugeuzwa kuwa ni mifuko ya misumari, ni bora tubakie na wananchi wetu salama, watu wasipande kwenye malori, nimefikiria ni vyema tutumie zile chai maharage kuliko kupanda kwenye malori,” Alisisitiza.Mh. Zelote alifika katika eneo la tukio mara tu baada ya kupokea habari hiyo ili kuweza kusaidia na kuhakikisha maiti na majeruhi hao wanapatiwa huduma stahiki na kufanikisha zoezi la uokoaji.


Ajali hiyo ilitokea baada ya lori aina ya fuso yenye namba za usajili T 425 BFF kuacha njia na kupinduka ilitokana na mwendo kasi wa dereva uliochangiwa na ugeni wa barabara hiyo.

Lori hiyo mali ya Bakari Ali Kessy iliyokuwa imetokea Kijiji cha Mvimwa kuelekea Kijiji cha Wampembe ilikuwa imepakiwa shehena ya viroba vya mahindi na watu iliacha njia, kupinduka na kusababisha vifo vya watu 15 kati yao wanawake 10 na wanaume 05.

Abate wa Pambu Martin Mkolwe Abasia ya Mvimwa akiongoza ibada fupi ya kuwaombea marehemu wa ajali iliyoua watu 15 na kujeruhi 9 iliyofanyika katika kituo cha afya Mvimwa, Wilayani Nkasi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kaunda Suti ya ugoro) akitoa salamu zake za pole kwa wafiwa, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda na kuliani kwake ni Abate Pambu Mkolwe wa Abasia ya Mvimwa.
 
Lori aina ya Fuso kama lionekanavyo mara baada ya kupata ajali


Waliofariki katika ajali hiyo ni BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2017: PSPF YATEMBELEA WATEJA MAJUMBANI, NIA NI KUWAJULIA HALI NA KUWAHAKIKI

$
0
0


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

Wakati Wiki ya Huduma kwa Wateja ikiendelea kote Duniani, Mfuko wa Pensheni wa PSPF, umeitumia wiki hiyo sio tu kwa kuhudumia wateja ofisini bali pia kutoka nje ya ofisi na kuwatembelea Wanachama na Wastaafu wa Mfuko huo majumbani kwao.

Mmoja wa waiotembelewa ni Mstaafu Bw. Kassim Salehe Mafanya,(63), anayeishi Kipunguni B, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kitendo ambacho kilimfurahisha sana.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu, wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa akifuatana na timu yake, Oktoba 4, 2017 alifika nyumbani kwa Bw. Mafanya, na kufanya mazungumzo naye ikiwa ni pamoja na kumpatia fomu ili aijaze kwa nia ya kumuhakiki kama ambavyo sheria inataka.

Kwa mujibu wa Sheria, Mstaafu anatakia kufika kwenye ofisi za PSPF kuhakikiwa kila mwaka ili kujua uwepo wake, anasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa 

“Kama mnavyofahamu wiki hii ni wiki ya huduma kwa wateja Duniani kote, na sisi PSPF kupitia ofisi zetu nchi nzima tunajitoa na kutembelea wateja wetu ambao ni pamoja na wanachama na wastaafu, na leo tuko hapa eneo la Kipunguni B, tumekuja kumtembelea Bw. Kassim Salehe Mafanya, ambaye ni mstaafu na lengo ni kumjulia hali na kumuhakiki uwepo wake kama ambavyo sheria inataka.” Alisema.

Afisa Uendeshaji wa PSPF ambaye pia alifuatana na Bw. Mkangaa, alimsomea Mstaafu huyo, maelezo yaliyomo kwenye fomu ya uhakiki kabla hajaweka saini kenyefomu hiyo.Aidha kwa upande wake, Mstaafu huyo Bw. Mafanya aliishukuru PSPF kwa kitendo hicho cha kuwatembelea wateja wao yeye akiemo na kwamba ni kitendo kinachofaa kupongezwa.

“Siku ya leo nimefarijika sana, kwanza sikutegemea kama nigepokea ugeni kama huu kutoka PSPF wa kunitembelea mimi Mstaafu hapa nyumbani kwangu,” Alianza kwa kusema Bw. Mafanya wakati akiwakaribishas viongozi hao wa PSPF.“Kitendo cha kuwakumbuka wastaafu kama sisi na kuwatembelea majumbani kwao kimenifurahisha sana na niwapongeze kwa tabia hiyo, Alisema.

Bw. Mafanya alimuhakikishia Kaimu Mkurugenzi Mkuu, kuwa amekuwa akipokea pensheni yake kila mwezi na bila matatizo yoyote na amekuwa akipata ushirikiano mzuri kutoka kwa maafisa wa PSPF kila anapokwenda kufuatilia pensheni yake.

“Nashukuru pensheni yangu inaendelea vizuri, huu ni mwaka wa 14 tangu nistaafu, nachukua vizuri tu pensheni ya kila mwezi na uzuri nikwamba inaboreshwa, na ndio maana mpaka hivi sasa tunaonekana tuna afya nzuri na ninaendelea na shughuli zangu mimi na familia yangu.” Alipongeza.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa, (kushoto), na Mteja wa PSPF, ambaye ni Mstaafu, Bw. Kassim Salehe Mafanya, (63), wakifurahia jambo wakati kiongozi huyo wa alipomtembelea Mstaafu Mafanya nyumbani kwake Kitunda B, nje kidogo ya jiji Oktoba 4, 2017 wakati Dunia ikiadhimisha Wiki ya Huduma Kwa Wateja.
Bw. Mafanya, (kulia), akipokea fomu hiyo 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa, (kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, wakishuhudia Bw. Mafanya akijaza fomu ya uhakiki ya Mstaafu, kutoka PSPF hapo nyumbani kwake. 
Bw. Mkangaa, (Kushoto), akipeana mikono na Bw. Mafanya baada ya kumtembela nyumbani kwake.
Bw. Mkangaa akisalimiana na familia ya Bw. Mafanya
Bw. Mkangaa akiwa amembeba mjukuuu wa Bw. Mafanya.
Bw. Mafanya (kushoto), akifurahia jambo na Afisa Uendeshaji kutoka PSPF, Bw.Ernest Massay
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, na timu yake akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafamilia wa Bw. Mafanya mbele ya nyumba yake.
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images