Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 137 | 138 | (Page 139) | 140 | 141 | .... | 1897 | newer

  0 0

  .  Aashika nafasi ya juu Afrika na Kimataifa kwa kipato

  NYOTA ya mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata amezidi kung’ara baada ya kuingia katika orodha ya wanamitindo saba bora kwa upande kipato. Kwa mujibu wa gazeti la biashara la kimataifa la Forbes kwa bara la Afrika (Forbes Africa) lililotolewa hivi karibuni, Flaviana ni mrembo pekee aliyeingia katika orodha hiyo kwa wanamitindo wa Afrika Mashariki na kuzidi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.

  Katika orodha hiyo, mwanamitindo Maria Borges wa Angola ndiyo aliibuka namba moja na  wengine sita pamoja na Flaviana wakibaki kutoa ushindani mkubwa kwa mlimbwende huyo wa Angola. Mbali ya Flaviana, wanamitindo wengine ambao wapo katika orodha hiyo ni Candice Swaenpoel, Katryn Kruger wote wakitokea Afrika Kusini, Ajak Deng, Grace Bol ( Sudan) na Liya Kebede wa Ethiopia,.

  Flaviana Matata aliibuka katika jukwaa la kimataifa kama Miss Universe Tanzania mwaka 2007 na aliweka historia kwa kuingia 10 bora na baada ya kumaliza muda wake aliendelea na fani ya  uanamitindo Afrika kusini na baadaye alipata nafasi ya kufanya kazi Marekani na Ulaya katika makampuni makubwa ya uanamitindo ya Next Models International na sasa yuko Wilhelmina Models.  Akizungumza kutoka New York, Flaviana ameeleza kufurahia mafanikio haya hata hivyo ameongeza “Mpango wangu ni kuzidi kumweka Mungu mbele na kuhakikisha kuwa najitahidi kadri ya uwezo wangu na kuiletea sifa familia yangu na nchi yangu”.


  0 0


  IN A LOVING MEMORY OF OMARY SAIDI ULEMBO
  05-05-1966 – 12-08-2010

  Ni miaka 3 sasa tangu ututoke ghafla, wakati ulipotuaga kuwa unaenda Nairobi Kenya kwa shughuli za kikazi ukiwa mzima wa afya lakini ukarejea ukiwa marehemu.

  Unakumbukwa zaidi na mpenzi mke wako Sheilla, watoto wako Harith na Shamim, mama yako Bi. Husna, mama zako wadogo na wakubwa,  dada zako, kaka zako, wadogo zako, ndugu jamaa na marafiki wote.

  Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho yako mahali pema peponi, 

  AMEEN.
   
   HIDAN .O. RICCO..

  0 0

  The Weruweru Girls met this Sunday at Cine Club,Mikocheni..being part of the meetings for the Golden Jubilee Celebrations scheduled for September 21st.
   The different committees and members of the Weruweru Family from the era of Asumpta to present (1963-2012) were all invited for the meeting

   Besides discussing the preparations for the celebrations, the Weruweru girls also had fun talking about their various memories of the Weruweru Days. Do you remember scrabbing the covered-ways? Do you remember burning VIGODORO? hahahah what memories!

   The Golden Jubilee meetings and preparations gave me a chance to meet and know many of Weruweru Alumni that I never knew went to the same school as me! Did you know Dr Asha Rose Migiro went to Weruweru Secondary? What about Ambassador Mwanaidi Maajar? Dr Mary Nagu? Dr. Hellen Kijo Bisimba? Dr. Mary Nagu?....Missie Popular?hahahahha
   Yes...we do run things in all spheres of lives! Now,I know there are so many others out there...Lawyers,Entrepreneurs, Farmers, Teachers, Artists, Engineers, Architects etc...Please register yourself on our DATABASE http://www.weruweru.mediart.co.tz and let's re-connect!
   The Next meeting is on 25,August,2013 at the same place,Cine Club.
  Looking foward to seeing many more of my classmates...the Rafikiel, Beatrice Dengenesa, Rachael George, Catherine Matasha, ...RED SKIRTS at its best! What about the Green skirts? The Blue Skirts?All of you...Let's show up at 25,August at Cine Club and remember the good old days :))

  0 0

  YULE muongozaji na mwigizaji Jimmy Mponda 'Jimmy Master' aliyetikisa  na mfululizo wa filamu za misuko iliyotoka sehemu ya kwanza hadi ya tatu na baadaye kujiongezea jina lingine akiitwa J Plus.
  Jimmy Master

  Kwa sasa nyota huyo amefunguka  kuwa yukombioni kutoa muvi ya mwisho inayoitwa Doble J Final  huku ujio huo ukiwa ni wa mwisho kutoka baada ya kutangulia  na Doble J sehemu ya kwanza na yapili zilizotoka mwaka jana.

  "Mwaka jana nilifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa filamu hususani  wanaopagawa na filamu za mapigano na kujawa mambo ya  kipelelezi,"alisema J Plus.

  Alisema Doble J Final pia ni ujio wake wa filamu nyingine ya mapigano na  kuna heka heka za kipelelezi ndani. J Plus aliyezoeleka sasa katika kuonesha ubabe wa kufa mtu , kwa sasa ujio wake huo unao tazamiwa kuingia sokoni mapema tu , mwezi ujao . Pia Jimmy Master amemshirikisha mbabe mwingine katika filamu za mapigano Ibrahim Mbwana  'Bad Boy' na pia wamo nyota wengine katika dulu la filamu kama Charles Magari , Hashim Kambi na Veronica Viankero.

  0 0

   Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Serengeti Breweries wakionesha muonekano mpya wa chupa ya Kibo Gold.
   Meneja Miradi endelevu na uwajibikaji lampuni  ya bia ya Serengeti  Nandi Mwiyombela (Katikati), Meneja wa mauzo wa kanda ya kaskazini Patrick Kisaka (kushoto) na Attu Mynah (kulia) kutoka idara ya mipango  wakionyesha mbele ya wasambazaji wa bia na waandishi wa habari aina mpya ya chupa yenye shingo ndefu ambayo bia ya Kibo Gold itapatikana kuanzia sasa, hafla hiyo ilifanyika katika kiwanda cha Serengeti Breweries kilichopo mjini Moshi.
   Meneja wa miradi endelevu na uwajibikaji Bi Nandi Mwiyombella akizungumza jambo mbele ya Wanahabari na wageni waalikwa kwenye hafla ya muonekano mpya wa bia ya Kibo Gold
  Meneja wa kiwanda cha bia cha Serengeti cha njinpi Moshi Bw. Coleman Hanna (katikati) akibadilishana mawazo na meneja mauzo wa kanda ya kaskazini Bw. Patrick Kisaka (kulia) wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa bia ya Kibo Gold uliofanyika kiwandani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita. 
  Msambazaji wa kwanza kabisa wa bia za Serengeti mkoa wa Kilimanjaro Mama Kisela, akipokea bia ya Kibo Gold yenye muonekano mpya na ladha ileile  kutoka kwa Attu Mynah wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa wa bia hiyo katika hafla fupi iliyofanyika katika kiwanda hicho wmwishoni mwa wiki.

  =========  ======   =====

  KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAFANYA UZINDUZI WA MUONEKANO MPYA WA BIA YA KIBO.

  *Sasa  Kibo yang’ara katika chupa ya kisasa kabisa*


   Kampuni ya bia ya Serengeti leo imezindua  muonekano mpya wa bia inayosherehekewa sana mkoani hapa, Kibo Gold.   Uzinduzi huu uliofanyika katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichopo Moshi, ulifikia kileleni kwa shughuli murua iliyoandaliwa na kampuni hii na kushuhudiwa na waandishi wa habari pamoja na wadau mbali mbali.    Bia hii ya Kibo sasa ina muonekano mpya wa chupa inayoashiria ubora wa kilichopo ndani.  Bia ni yenye ubora uleule wenye kiwango cha hali ya juu ila kwa chupa ya rangi ile ile iliyongarishwa na  shingo ndefu. 


  Akiongea kwenye hafla hii Meneja wa miradi endelevu na uwajibikaji Bi Nandi Mwiyombella alisema bia hii ya Kibo Gold imekuwa ikitambulika kwa ubora na ladha nzuri kwa wateja.   “Kwa muonekano huu mpya wa chupa ya kisasa, tunaamini wateja wengi watavutiwa na kuipenda zaidi kwani ni muonekano unaokwenda na wakati.   Ubora wa bia hii, unakuwa dhahiri kweli kabisa ukizingatia kwamba inatengenezwa kwa maji yatiririkayo kutoka katika kilele cha juu kabisa cha mlima Kilimanjaro ambapo pia bia inazoa jina lake hili la ‘KIBO’, aliongeza Bi Nandi.


  Kampuni ya bia Serengeti chini ya kampuni mama ya Diageo, inazingatia kanuni  na sheria zilizowekwa na kampuni hii kwenye ubora katika uzalishaji wa  bidhaa zote.  Muonekano wa bidhaa ni ule unaondena na soko za kimataifa na wa kuvutia.  Kampuni ya bia ya Serengeti  inatumia malighafi za kitanzania ili kuleta ubora halisi na vile vile kukuza uchumi wa Tanzania katika sekta ya kilimo. 

  Kwa Mhariri:  Bia ya Kibo Gold ilirudishwa sokoni hapa Tanzania mwaka jana, 2012, mwezi wa sita baada ya kuwa haipo kwenye soko kadri ya miaka kumi.   Ni mojawapo ya bia zinazoongoza nyanda za kaskazini sasa hivi.  Bia hii inazalishwa katika kiwanda cha bia cha Serengeti cha Moshi na inasambazwa mkoani hapo na mikoa jirani, Arusha, Tanga, Manyara na Tanga kwa wingi.


  Tafadhali kunywa kistaarabu.  Haiuzwi kwa walio chini ya miaka 18.  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA MALIASILI NA UTALI

    
  TAARIFA KWA UMMA

  WIZARA YA MALIASILI NA UTALII IMEKANUSHA UVUMI KUWA WATEULE WA WAZIRI WAMESAINI POSHO MBILI.


  Wizara ya Maliasili na Utalii  inakanusha uvumi ulioandikwa na kuchapishwa na gazeti la Raia Mwema mnamo tarehe 07/08/2013 ukurasa wa kwanza lililobeba kichwa cha habari UFISADI kama wabunge, wateule wa waziri wasaini posho mara mbili  ikiwa na ufafanuzi kuwa yumo Ofisa Takukuru,walipwa na taaasisi wanayoichunguza. Taarifa hii ilikuwa na muendelezo zaidi ukurasa wa tatu wa gazeti hilo.


  Wizara inasisitiza kuwa uvumi huo siyo kweli kutokana na sababu zifuatazo:

  ·        Wajumbe wa kamati husika (iliyoundwa kuchunguza tuhuma kuhusu matumizi mabaya ya fedha unaowahusisha watendaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro) (NCAA) HAWAKULIPWA POSHO MARA MBILI.


  ·        Malipo waliyolipwa wajumbe wa kamati husika yalilipwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro  (NCAA) kama ilivyo kwenye Hadidu za Rejea za kazi husika na hawakulipwa malipo yoyote na wizara ya maliasili na utalii.


  ·        Viwango vya posho vilivyotumika ni kwa mujibu wa Waraka wa Serikali namba 2 wa Mwaka 2010, Ref.Na C/AC/.17/45/01/125


  ·        Malipo yaliyofanywa kwa wajumbe wa kamati husika yalikuwa na kibali halali cha Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Khamis Suedi Kagasheki


  ·        Kamati husika ilifanya kazi vizuri na kukabidhi ripoti ya awali iliyomridhisha Waziri Kagasheki aliyewaagiza kuifanya kazi tajwa hapo juu. Ripoti hiyo ya awali na hii ya mwisho ZITAWEKWA HADHARANI ili Umma uelewe hali halisi ya Mamlaka ya Ngorongoro na siyo upotoshaji wa Raia Mwema.


  ·        Kamati iliyoundwa na Waziri Kagasheki ilikuwa na kazi tofauti na ile kamati ya awali iliyowahi kuongozwa na Jaji Robert Mihayo aliyeteuliwa na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige mwaka 2011. Raia Mwema ingejiridhisha kwa kutazama hadudi za rejea za Kamati hizo mbili. Si jambo jema Raia Mwema kuupotosha Umma.


  Wizara ya Maliasili na Utalii imesikitishwa na kitendo cha gazeti la Raia Mwema, gazeti ambalo limejijengea sifa na kuaminiwa na jamii kwa  kutoa taarifa  za uhakika zinazofuata maadili ya utoaji taarifa kwa vyombo vya habari, kuchapisha habari zinazochafua jina la Wizara, Wabunge na Serikali kiujumla  bila kujihakikishia ukweli wa taarifa hizo kutoka wizara husika.


  Kwa taarifa hii, Wizara inalitaka Gazeti la Raia Mwema kufuta uvumi waliochapisha kwenye gazeti lao kama ilivyotajwa hapo juu na pia kuiomba radhi Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuchapisha habari ambazo si sahihi na pia kuchafua jina la Wizara.


  IMETOLEWA NA  KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

  WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

  12/08/2013
  0 0

    Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Balozi wa Caanada hapa nchini, Alexandre Leveque, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 12, 2013. Balozi huyo alipomtembelea na kuwa na mazungumzo naye. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimwelewesha jambo Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre  Leveque, alipomkaribisha Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 12, 2013.  Balozi huyo alipomtembelea na kuwa na mazungumzo naye. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa  Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza Balozi wa Caanada hapa nchini, Alexandre Leveque, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 12, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
    Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsindikizaa Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque,  baada ya mazungumzo  yao, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti  12, 2013.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque, baada ya mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti  12, 2013. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi Mteule wa Uholanzi hapa nchini Mhe Jaap Frederiks Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 12, 2013. 
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Balozi Mteule wa Uholanzi hapa  nchini Mhe Jaap Frederiks baada ya kupokea hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 12, 2013.


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe kwa Balozi Mteule wa Uholanzi hapa nchini Mhe Jaap Frederiks Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 12, 2013.PICHA NA IKULU.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mkurugenzi wa Taasisi ya Chama Cha Democrat cha Marekani, inayojishughulisha na programu mbalimbali za mamboresho ya kisiasa (NDI), Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dk. Keith Jennings, mgeni huyo alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, na kuwa na mazungumzo, leo Agosti 12, 2013. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose Migiro
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi ya Chama Cha Democrat cha Marekani, inayojishughulisha na programu mbalimbali za mamboresho ya kisiasa (NDI), Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dk. Keith Jennings, mgeni huyo alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Agosti 12, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose Migiro. 
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Chama Cha Democrat cha Marekani, inayojishughulisha na programu mbalimbali za mamboresho ya kisiasa (NDI), Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dk. Keith Jennings (watatu kushoto), baada ya mazungumzo na  mgeni huyo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Agosti 12, 2013. (Wapili Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose Migiro.Wengine ni ujumbe aliofuatana nao Mkurugenzi huyo. Ofisa Mkuu wa Programu wa NDI Kusini na Mashariki mwa Afrika, Martha Haile (kushoto) na kulia ni Ofisa wa Programu wa NDI, Tanzania, Mahija Dodd na Dk. Bernadeta Killian kutoka Idara ya Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Tanzania Teddy Mapunda akiwagawia soda wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakati wa sherehe za sikuku ya Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo jana. Wafanyakazi wa kampuni hiyo walisherehekea sikuu hiyo na wanafunzi hao ili kuonyesha upendo.
  Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Daud Nasibu akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama inayomilikiwa na taasisi hiyo wakati wa sherehe za Eid Mubarak ziliyofanyika shuleni hapo jana.
  Wafanyakazi wa Kampuni ya Montage ya jijini Dar es Salaam wakiwahudumia chakula cha mchana wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani. Wafanyakazi wa kampuni hiyo waliamua kusherehekea sikukuu ya Eid Mubarak na wanafunzi hao jana ili kuonyesha upendo.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakila chakula cha mchana kilichoandaliwa na kampuni ya Montage Tanzania wakati wa sherehe za Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo jana.
  Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakicheza mziki aina ya Kwaito jana wakati wa sherehe za Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo. Picha na Anna Nkinda - Maelezo

  0 0

   Mratibu wa Mpango kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MURABITA)  Bibi Seraphia Mgembe akieleza kwa waandishi wa habari juu ya mipango mkakati mbalimbali inayotekelezwa na ofisi hiyo inayolenga kumuinua mwananchi kutoka katika umaskini,katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es salaam kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi Kawawa.

  Mkurugenzi wa Urasimishaji kutoka mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania(MURABITA) Stephen Rusibamayila KUSHOTO akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya mipango mkakati mbalimbali inayotekelezwa na ofisi hiyo inayolenga kumuinua mwananchi kutoka katika umaskini,katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.


  0 0

  Mkurugenzi wa Stopper Entertainment,  Mukhsin Mambo,(katikati) akifafanua  jambo  kuhusiana na Mashindano ya Shule za Sekondari(Interschools Debate Compatitions) katika Semina iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa  JB. Bellemonte Hoteli, iliyopo jijini Mwanza. kulia Meneja Mipango, Aisha Eddy na Mratibu wa Mashindano Baraka Samson. (Picha kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania)
  =======   ========   =========
  Mashindano ya Mijadala kwa shule za sekondari mkoani Mwanza (Interschools Debate Compatition), yanatarajiwa kuanza septemba 02 mwaka huu.

  Akizungumza katika semina elekezi, iliyowakutanisha baadhi ya walimu wa mijadala kutoka katika  shule mbalimbali za sekondari mkoani Mwanza, mkurugenzi wa Stoppers Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo, Bwana Mukhsin Mambo, amesema jumla ya shule 32 kutoka mkoani Mwanza, zitashiriki katika shindano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika mkoani humo na Tanzania kwa ujumla.

  Mambo, amesema shindano hilo pia litaonyeshwa kwenye moja ya runinga hapa nchini kuwapa fursa watazamaji kushuhudia vipaji vya wanafunzi katika kujieleza mbele ya jamii.

  Amesema nia na madhumuni ya shjindano hilo, mbali na kuondoka na kitita cha zawadi kwa washindi lakini pia ni njia mojawapo ya kuinua kiwango cha elimu hapa nchini kwa wanafunzi kupata nafasi ya kujieleza mbele za watu, kufanya utafiti kutokana na mada itakayowekwa mezani, kuweka mahusiano mema dhidi ya wanafunzi na kujenga kizazi kipya katika nyanja ya elimu kupitia mfumo wa mijadala.

  Miongoni mwa shule zitakazoshiriki shindano hilo ni pamojana Nsumba sekondari, Nganza Sekondari, Butimba sekondari, St. Joseph Girls Sekondari, Buswelu Sekondari, New Hellen Sekondari, Hill crest Sekondari, Bismark Sekondari.

  0 0

   Wafanyakazi  wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 kushoto ni Semio Sonyo ,Sarah Keiya meneja masoko,katikati ni David Rwenyagira na Deo Gee wakifurahia  kikombe cha ushindi ambapo jana waliibuka washindi wa kwanza kwenye maonyesho ya 20 ya Nane nane kwa kanda ya kaskazini,yaliyofanyika katika viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha.
  Meneja masoko wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio5 Sarah Keiya pamoja na Dadiv Rwenyagira wakiwa wameshikilia kikombe mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza maonyesho ya 20,ya nane nane kwa kanda ya kaskazini yaliyofanyika katika viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha.

  0 0

   Warembo wanaotarajia kushiriki Redd's Miss Ilala, wakiwa wamepozi wakati wa mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini.
   Warembo wanaotarajia kushiriki Redd's Miss Ilala, wakiwa wamepozi wakati wa mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini
   Warembo wakiwa katika moja ya miondoko wakati wamazoezi
   Mwalimu wa warembo hao, AKHSAS PETER akiwapanga vizuri kabla ya kupigwa picha na wandishi wa habari.
   Warembo wakipita Mtaa wa Makunganya katikati ya Jiji la Dar es Salaam, wakitokea mazoezini katika Mgahawa wa Billicanas.
   Mwandishi Mwandamizi wa Habari za Michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula (kulia), akitoa maelezo kuhusu kazi za kila siku za waandishi wa habari kwa warembo wa wanaotarajia kushiriki mashindano ya Redd,s Miss Ilala walipotembelea chumba cha habari cha Jambo Leo
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL), Juma Pinto (aliyekaa kulia), akizungumza na warembo hao waliomtembelea ofisini kwake, Dar es Salaam. Aliyekaa katikati ni Mratibu wa mashindano hayo, Juma Mabakila. JCPL ni wachapishaji wa magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti, Dar Metro na jarida la Jambo Brand Tanzania.

  0 0


  NA James Festo, Makete

  Mkuu wa wilaya ya makete bi. Josephine matilo amewataka viongozi wa dhehebu la kanisa la kiinjili la kilutheli KKKT Dayosisi ya kusini kati kumaliza tofauti zilizopo baina yao na viongozi wa huduma ya maisha mapya ndani ya kristo NLC wilayani hapa.

  Ameyasema hayo akiwa mgeni rasmi wakati wa kufungua mkutano wakuelekea kilele  maadhimisho ya miaka hamsini ya huduma hiyo ya maisha mapya ndani ya kristo ambao utadumu kwa siku saba ambao unafanyika  katika viwanja vya mabehewani kijiji cha iwawa  na kuwataka kudumisha amani na mshikamano ili kuweza kuyafikia malengo yao.

  'viongozi tunakaa tunarumbana tunawapotosha wananchi tukae meza moja ili kuweza kumaliza tofauti zetu na si kuendelea kila watu kivyao hapo mnawaumiza  wananchi sote mungu wetu ni mmoja malumbano  yanatoka wapi?' aliuliza bi matilo.

  Aidha mgeni rasmi huyo bi matilo ameeleza kuitambua huduma hiyo na kuwashauri viongozi na kuwataka kueneza dini jinsi katiba yao inavyosema  bila ya kuvunja katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania

  sisi kama serikali tunatambua huduma yenu na tunataka injili ifike kila mahala  kwa jinsi mlivyoyaainisha malengo yenu ya kuweza kuimarisha amani na utulivu kwa wananchi na hatutakaa kimya kama kuna kanisa linapotosha wananchi  alisema bi matilo.

  kwa Upande wake katibu mkuu taifa  wa huduma hiyo bw. Daimon Mwandambo wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi alisema kwa huduma hiyo imesambazwa katika mikoa 18 ya tanzania bara na kuufanannisha utofauti huo na uliowahi kujitokeza jijini dar es salaam na ule wa mkoani iringa ambao ulidumu kwa miaka saba.  

  Mkutano huo utakaodumu kwa siku saba ambapo kilele cha maadhimisho hayo yatakuwa septemba 13 na mkutano mkuu kitaifa utafanyika mkoani morogoro pia katika ufunguzi huo  ulilhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa huduma hiyo  wakiwemo uongozi wa mkoa serikali akiwemo mwenyekiti wa halmashauri bw daniel Okoka na mwakilishi wa mkurugenzi bw. jakob mena, viongozi siasa nawageni wengine waalikwa.  

  0 0

  Hii ndiyo hati ya Ushindi tuliyopewa na TASO
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawilo aliye simama Mbele akipokea Maelezo ya Kina juu ya Mbeya yetu Blog inavyofanya kazi na mitandao mbalimbali ya Kijamii kutoka kwa Mtaalam wa Mambo ya Mitandao ya Digitali kutoka Tone Multimedia Group Fredy Anthony, alipo tembelea katika Banda la Mbeya Yetu Blog.
   Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Dr. Christine Ishengoma aliyevaa kofia akipokea Ufafanuzi wa Jambo Kuhusu Blog ya Mbeya yetu kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa Mtandao wa Mbeya yetu Ambaye Pia ni mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Tone Multimedia Ndugu Joseph Mwaisango wa Pili kutoka Kushoto
  Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma akitaka kupata ufafanuzi wa jinsi gani Mbeya yetu Blog tunavyopata habari na kuziweka kwa Muda kama alivyo kuta tukio lake likiwa Live mara alipotembelea Banda la Mbeya yetu na kujionea mwenyewe.
  Kutoka Kushoto ni Venance Matinya na David Nyembe wote kikosi kazi cha Mbeya yetu Blog, wakiwa wanapita Mbele kuonesha Bango la Mbeya yetu kwa Mgeni Rasmi wakati wa sherehe za Kilele cha siku  ya Wakulima Nane nane Mbeya.
   Msimamizi Mkuu wa Mtandao wa Mbeya yetu Ambaye Pia ni mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Tone Multimedia  Ndugu Joseph Mwaisango akipokea Hati ya Ushindi kutoka kwa Mgeni Rasmi aliyevaa Skafu Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Capt (RTD) Aseri Msangi 
  Baadhi ya kikosi kazi cha Mbeya Yetu Blog, Kutoka kushoto ni Venance Matinya, Joseph Mwaisango, Ezekiel Kamanga na Fredy Anthony

   ********************
  Chama Cha Wakulima Tanzania (TASO) kanda ya Nyanda za juu Kusini, kimeutunuku cheti mtandao wa kijamii wa www.mbeyayetu.blogspot.com ambao upo chini ya Tone Multimedia Company Limited kutokana na kuibuka mshindi wa kwanza wa kurusha matangazo kwa njia ya Kidigitali katika maonesho ya Wakulima nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakagale Uyole Jijini Mbeya.
  Tuzo hiyo imekuja kutokana na kikosi cha Mtandao huu kuweka kambi katika maonesho hayo na kufanya shughuli za kurusha matangazo moja kwa moja kutoka uwanjani hapo na kuwapagawisha wakulima ambao walipata fursa ya kutembelea banda letu na kujionea habari zilizotokea muda huo huo na kuonekjana hewani.
  Mbali na wakulima na watu mbali mbali waliokuwepo uwanjani hapo pia viongozi wa Taso na wakuu wa Mikoa pia walipata fursa ya kutembelea banda la Mtandao huu katika ziara zao za kukagua mabanda na hivyo kutoa sifa kwa wamiliki wa Mtandao huu namna habari zilivyokuwa zikienda kwa wakati.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawilo ndiye aliyekuwa wa Kwanza kufanya ziara hiyo na kukuta habari zake tokea akipokelea mlangoni hadi kufikia mabanda habari zilikuwa hewani, mwingine alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma ambaye pia alionekana kuufagilia mtandao huu kwa namna walivyoweza kutangaza Nanenane  iliyofanyika kikanda na kuonekana kama ni Kitaifa.
  Aidha kufuatia mchango huo wa Taso na wakulima kwa ujumla Uongozi wa Tone Multimedia Group Kupitia  Mbeya Yetu Blog unatoa shukrani kwa wote waliuofanikisha shughuli za Nanenane hadi zinafikia kilele Agosti 8,  na kupelekea kupata cheti cha ushindi.
  Tunapenda kuwashukuru TASO kwa namna ya pekee, SBC (T) Ltdkupitia kinywaji chao cha Pepsi, Shirika la Bima ya Afya (NHIF) kwa kutupatia gazebo lililotusitili tukiwa kazini na wengine wengi ambao hatutaweza kuwataja majina lakini tunaahidi kuendelea kushirikiana kwa pamoja.

  Pia tunapenda kuwashukuru Bloggers wote na waandishi wa habari kwa ujumla hatutaweza kutaja kila chombo lakini tumekuwa pamoja mpaka kufanikisha yote haya.

  Mwisho kabisa Tunapenda kukushukuru wewe Mdau wetu Mkubwa wa Mbeya yetu Blog kwa kuonesha Moyo na Kutembelea kila wakati mtandao huu, Tunasema asanteni sana, Bila nyie sisi hatuwezi fanya kazi.
  KWA PAMOJA TUUPENDE MKOA WETU WA MBEYA, KUPITIA MTANDAO WA MBEYA YETU BLOG.

  0 0


  Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' katikati akiwamulizia mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto na Simba Watunduru baada ya kusaini mkata wa kupambana August 30 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam.   
  Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' akimkabizi mkataba wa makubaliano bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kutia saini jana katika ofisi za TPBO LTD Dar es salaam.
  Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' akimkabizi mkataba wa makubaliano bondia Simba Watunduru baada ya kutia saini jana katika ofisi za TPBO LTD Dar es salaam.
  Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' kushoto akimwangalia bondia Simba Watunduru anavyo usoma mkataba wake kabla ya kutia saini Dar es salaam jana.
  Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' kushoto akimwangalia bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akitia saini mkataba wake Dar es salaam janaPicha na BLOG YA SUPER D.
  Mabondia Simba Watunduru kushoto na Ibrahimu Class 'himu Class' King Class Mawe' wakiangaliana kwa usongo wakati wa kutambilisha mpambano wao wa masumbwi utakaofanyika August 30 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam Picha na BLOG YA SUPER D
  Mabondia Simba Watunduru kushoto na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakitunisha misuli wakati wa kupiga picha kwa ajili ya kutangaza mpambano wao Picha na BLOG YA SUPER D
  Mabondia Simba Watunduru kushoto na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakitunishiana misuli wakati wa kutangaza mpambano wao Picha na BLOG YA SUPER D
  KING CLASS MAWE
  Simba Watunduru
  Ibrahimu Class 'King Class Mawe'
  Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' katikati akiwamulizia mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto na Simba Watunduru baada ya kusaini mkata wa kupambana August 30 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam Picha na BLOG YA SUPER D 
   Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' katikati akiwamulizia mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto na Simba Watunduru baada ya kusaini mkata wa kupambana August 30 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam Picha na BLOG YA SUPER D
  Na Mwandishi Wetu 
   MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Simba Watunduru wamekiuka miko ya mchezo wa masumbwi baada ya kuchapana makonde kavu kavu mbele ya Rais wa TPBO Yassini Abdallah 'Ostadhi' wakati wa utiaji saini mkataba  wa makubaliano wa kupambana mchezo wa kirafiki August 30 katika ukumbi wa Diamondi Jubilee

  Akizungumzia tukio hilo rais huyo alisema sijawai kuona vitu kama hivi vya ajabu mana vijana wamekamiana mpaka kufikia atua ya kuchapana kavu kavu mbele yangu ata hivyo mzozo uwo umekubaliana kumalizika siku ya mpambano wao  ambapo atajulikana nani mbabe zidi ya mwenzake

  Nae bondia Ibrahimu Class aliyeanzisha mzozo uho ameaidi kumaliza mapema mpinzani wake ambapo anatarajia kumchakaza raundi za awali na bondia Simba ame aidi kumchapa class kwa K,O

  wakati wowote ule unajua huyo ni kijana mdogo sana mmemuaisha kwangu sasa siku hiyo mimi nita mpiga K,O mbaya sana najua kuwa  kwa Tanzania hii mimi ndie naongoza kuwapiga wapinzani wangu kwa K,O pindi nikutanapo uringoni


  Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zitakazokuwa zikisabazwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'


  DVD hizo mpya ni kati ya  

  mike tyson vs evander holyfield na felix trinidad vs roy jones jr

  Felix 'Tito' Trinidad vs Pernell Whitaker


  ambapo dvd hizo zilizo rekodiwa kwa ubora wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mchezo wa masumbwi nchini na kuelekeza mbinu na sheria za mchezo huo kwa mashabiki,mabondia na wanaoitaji kuwa marefarii wa pembeni kujifunza 


  0 0

  Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Bw, jackson Mmbando (Kulia) akiwa na mshindi wa zawadi ya shilingi milioni moja kwa wiki hii Bw, Rakesh Mawji huku akitoa pesa zake mara baada ya kutumiwa kupitia huduma ya Airtel Money. Hafla ya makabidhiano na mshindi huyo ilifanyika katika ofisi za Airtel jiji ni Dar es salaam leo.
  Meneja wa Duka la Airtel Makao makuu Bi, Happy John (kulia) akiwa na mshindi wa zawadi ya shilingi milioni moja kwa wiki hii Bw, Rakesh Mawji akihesabu pesa zake mara baada ya kuzitoa kupitia huduma ya Airtel Money. Hafla ya makabidhiano na mshindi huyo ilifanyika katika ofisi za Airtel jiji ni Dar es salaam leo.
  Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Bw, jackson Mmbando (kushoto) akiwa na mshindi wa zawadi ya shilingi milioni moja kwa wiki hii Bw, Steven Maguru huku akihesabu pesa zake mara baada ya kuzitoa kupitia huduma ya Airtel Money. Hafla ya makabidhiano na mshindi huyo ilifanyika katika ofisi za Airtel jiji ni Dar es salaam leo.
  Kulia ni Meneja uhusiano wa Airtel Bw jackson Mmbando akimpongeza mume wa mshindi wa wiki hii Bw, Hassan Abdalah mara baada ya mke wake (kati) Bi Mwajuma kukabidhiwa zawadi yake shilingi milioni moja na kuitoa kupitia huduma ya Airtel Money Hafla ya makabidhiano na mshindi huyo ilifanyika katika ofisi za Airtel jijini Dar es salaam leo.
  Kati ni Mwalim steven Maguru akionyesha pesa yake kwa furaha kiasi cha shilingi laki moja aliyotoa kupitia Airtel money mara baaada ya kushinda milioni moja na kupokea yote kupitia Airtel Money. Kulia ni mshindi mwingine wa wiki hii Bw, Rakesh Mawji na kushoto ni meneja Uhusiano wa Airtel bw, jackson Mmbando mara baada ya kukutana na washindi hao makao makuu ya Airtel jijini dar es salaam leo

  0 0


   kamanda mkuu wa FFU ,Ras Makunja akiwa na Tuzo ya kimataifa ya best Africa band.

  Balozi wa DRC Excellence Madame Clémentine Shakembo Kamanga,akiipongeza Ngoma Africa,mabalozi wengine wa nchi za kiafrika,ujerumani wakishuhudia.
  Mabalozi wa nchi za Togo,Senegal na Kongo DRC wakiwa jukwaani kuipongeza Ngoma Africa band mwenye kipaza sauti Kamanda Ras Makunja.

  FFU wa Ngoma Africa band wamechukua tena International Diaspora Award 2013,Bendi bora ya kiafrika ulaya.

  Mabalozi wa kiafrika nchini Ujerumani waipongeza FFU !
  Maelfu ya washabiki wadatishwa akili na Ngoma Africa Band,
  Mzimu wa Dansi "Ngoma Africa Band umetimiza miaka 20 na bado unatisha !
  Si nyingine bali Ngoma Africa band aka FFU ilifanikiwa kuutetea ubingwa wake wa bendi bora na kujichukulia Tuzo ya kimataifa ya IDA kule mjini Tubingen,Ujerumani katika maonyesho ya kimataifa ya International African Festival Tubingen 2013.

  Bendi hiyo maarufu kwa kuwatia kiwewe washabiki na mdunduko wake imevunja rekodi kwa kuwa na washabiki wa kimataifa kila pembe.
  Katika maonyesho ya International African festival 2013,yaliyofanyika mjini Tubingen,ujerumani Ngoma Africa band imekubalika sio na washabiki tu bali pia mabalozi kutoka nchi mbali mbali za kiafrika nchini Ujerumani ! bendi Tusikose kuwasikiliza ffu at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

  0 0

  IMG_2158

  Makao Makuu ya kituo cha habari na mawasiliano cha Redio ya jamii Sengerema Fm mkoani Mwanza kunakofanyika warsha ya wiki moja kwa redio za jamii nchini kwa ajili ya kuziandaa kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
  IMG_1954
  Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Radio Sengerema mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye akiwakaribisha na kuwatambulisha wawezeshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa Wakurugenzi na Mameneja wa redio za jamii nchini wanaohudhuria warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO kupitia mradi wa DEP kwa ajili ya kuwaanda kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia kwa jamii kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
  IMG_1906
  Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin akizungumza na mameneja , wakurgenzi wa redio za jamii Tanzania nchini katika warsha ya wiki moja juu ya matayarisho ya mradi wa kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia kwa jamii kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
  IMG_1964
  Mshauri wa Redio Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo kwa washiriki wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani Sengerema mkoani Mwanza. Wa pili kushoto ni Meneja wa Mradi wa DEP kutoka UNESCO Courtney Ivins, Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambaye pia ni Mtafiti kutoka ECOM Research Dr. Ambrose Kessy.
  IMG_1943
  Meneja wa Redio Sibuka Fm Maswa Bi. Bhoke Okachu akiwasilisha maoni wakati wa kujadili mradi wa DEP kwenye warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
  IMG_1909
  Picha juu na chini ni Sehemu ya washiriki ambao ni Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaohudhuria warsha hiyo.
  IMG_1971
  IMG_1917
  Meneja wa Kyela Fm Lucas Kulwa akichangia maoni yake wakati wa warsha hiyo.

  Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni(UNESCO) limesema kwamba linakusudia kuvijengea uwezo vyombo vya habari vya jamii ili kuviwezesha vyombo hivyo kuandaa vipindi vya elimu kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia (DEP) kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.

  Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin amesema UNESCO, UNDP, UN WOMEN, wamekusudia kufanya hivyo kwa dhamira ya kuvitayarisha vyombo hivyo mapema baada yakuona changamoto nyingi zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka 2010, ambapo elimu ya kutosha haikuwafikia wananchi waliowengi.

  Yusuph ameyasema hayo katika kituo cha habari na mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza, wakati akiwasilisha mada ya amani na demokrasia kwa mameneja , wakurgenzi wa redio za jamii Tanzania, wasimamizi wa redio za halmashauri na mazingira Tanzania bara katika warsha ya wiki moja juu ya matayarisho ya redio hizo katika uchaguzi ujao.

  Uhamasishaji wa elimu ya wapiga kura, usawa wa kijinsia katika kuhamasisha kinamama kushiriki katika uchaguzi kwenye kujiandikisha, kupiga kura nakujitokeza kugombania nafasi mbalimbali za uongozi na kutoyafikia makundi maalum ipasavyo licha ya mafanikio makubwa yaliyofikiwa ukilinganisha na muda mchache wa elimu uliotumioka kabla ya uchaguzi ni mambo muhimu yaliyohamasisha elimu hio kutolewa mapema Yusuph alisema.

  Amebainisha kuwa katika kuhakikisha ufanisi mkubwa unafikiwa katika uchaguzi ujao, wameongeza redio shiriki kutoka 12 hadi 25, huku manufaa zaidi yakielekea visiwani ambapo redio ya jamii Tumbatu na redio jamii kusini Pemba, zitaanzishwa na redio Uvinza mkoani Kigoma ambazo kwa pamoja zitapewa mafunzo yakutosha ikiwa ni pamoja na viongozi wa bodi, watu mashuhuri, viongozi wa halmashauri na viongozi wa dini.

  Al Amin amesema kutokana na uzoefu, chaguzi zilizopita katika nchi jirani na matokeo yake, uchaguzi ujao huenda kukawa na changamoto nyingi, hivyo ni vyema kuhamasisha majadiliano ya amani yatiliwe mkazo na kuboresha mawasiliano na taasisi husika ambapo watendaji 250 wa habari watapewa mafunzo na watanzania milioni nane watafikiwa kupata taarifa kupitia redio za jamii.

  Amesisitiza kuwa kazi ya kuhubiri amani na demokrasia inahitaji kuvumiliana kutokana na changamoto zilizopo na kuwa vyombo vya habari, ni vyema kujua miiko na usawa katika utendaji hasa katika kuandika na kutangaza taarifa zinazohusu uchaguzi, huku akivilaumu vyombo vya habari kwa kuhubiri uajibikaji kwa wengine, bali wao wamekuwa na mapungufu mengi na hawanabudi kufanya marekebisho mapema.

  Amesema vyombo vya habari vya jamii, huu ni wakati muafaka wa kufanya mabadiliko katika watendaji wake kutokana na idadi ndogo ya watangazaji na waandishi na maripota wanawake kupungua siku hadi siku, kuboresha vipindi na kufahamu kuwa utamaduni wa watanzania ni amani na vyema kudumisha utamaduni huo kuanzia vyombo vya habari vya jamii.

older | 1 | .... | 137 | 138 | (Page 139) | 140 | 141 | .... | 1897 | newer