Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

JUMIA TRAVEL YAUNGANA NA DUNIA KUADHIMISHA SIKU YA UTALII

$
0
0

Na Jumia Travel Tanzania

Kila ifikapo Septemba 27 ya kila mwaka dunia huadhimisha siku ya utalii duniani. Maadhimisho hayo hufanywa na kila nchi ambapo kunakuwepo na shughuli kadhaa zikiongozwa na malengo na kauli mbiu tofauti zilizoazimiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO).

Mnamo mwaka 2015, Mkutano Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa uliutangaza mwaka 2017 kama Mwaka wa Kimataifa wa Utalii Endelevu kwa Maendeleo. Na hivyo kuifanya kauli mbiu ya mwaka huu kuwa ni ‘Utalii Endelevu kwa Maendeleo.’

Maeneo matano ambayo yanaangaziwa na kufanyiwa kazi mwaka huu ni; Ukuaji wa uchumi endelevu na wa pamoja; Ujumuishwaji wa jamii, ajira na kupunguza umasikini; Ufanisi wa rasilimali, utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa; Amali za kiutamaduni, utofauti na urithi; na Maelewano ya pamoja, amani na usalama.

Katika kuunga mkono maadhimisho haya, Jumia Travel ikiwa ni mdau wa masuala ya utalii Tanzania na Afrika kwa ujumla imekuwa ikifanya jitihada za kukuza ufahamu juu ya maeneo na vivutio mbalimbali vya utalii nchini.

Hivi sasa kuna kampeni inayoendelea kwa jina la ‘Destinations Campaign’ ikiwa inalenga kukuza ufahamu juu ya maeneo tofauti nchini ambayo watanzania hawafahamu kama ni vivutio vya kitalii.

Tanzania imebarikiwa kuwa na maeneo mengi lakini hayapewi kipaumbele wala kutangazwa vilivyo. Na endapo ikiwa yanatangazwa, sio yote yanayopata fursa sawa kama vile Zanzibar, Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo watu wengi nchini na duniani wanayafahamu.

Jumia Travel imeamua kuitumia fursa ya kufanya kazi na maelfu ya hoteli nchini na Afrika kuyaangazia maeneo hayo na sehemu ambazo wageni wanaweza kulala. Kikubwa kinachofanyika ni kuwafahamisha watanzania juu ya shughuli tofauti wanazoweza kuzifanya pindi wakitembelea maeneo hayo. Mbali na hapo wamiliki na mameneja wa hoteli huhojiwa juu ya masuala wanayoona yanaweza kuwavutia wateja kwenye hoteli zao.

Jitihada za kukuza ufahamu na kutangaza maeneo mbalimbali nchini zinafanywa pia na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Bodi ya Utalii imekuja na mkakati na mbinu mpya kwa kuyatenga maeneo ya usimamizi wa wanyama tofauti na ya kawaida yaliyozoeleka na watalii wengi.

Kwa mfano, hivi sasa TTB inafanya jitihada kubwa za kukuza maeneo matano yaliyomo kwenye mpango wa usimamizi huo ambayo ni Burunge ipo Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, Randilen ipo Wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha, Ikona ipo katika Wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara jirani na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Ipole ipo katika Wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora na Mbomipa ambayo ni muunganiko wa vijiji zaidi ya 21 vya tarafa  za Idodi na Pawaga vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Kwa kufanya hivyo inatoa fursa kwa watalii kuwa na machaguo ya sehemu za kutembelea tofauti na yaliyozoeleka. Kwa sababu hata kwenye maeneo haya watalii wanaweza kukidhi haja zao kwa kuwaona wanyama na kufanya shughuli nyinginezo za kitalii.

Kwa mujibu wa ripoti ya utalii ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii Duniani, Mwaka 2016 umethibitisha kuwa ni mwaka mwingine wa mafanikio katika sekta ya utalii kimataifa licha ya changamoto kadhaa. Idadi ya watalii kimataifa imekuwa kwa mwaka wa saba mfululizo na kufikia bilioni 1.2, idadi ya ukuaji ambayo haijawahi kutokea tangu miaka ya ‘60’ (1960). Ukuaji mkubwa zaidi umeonekana kwenye sehemu za Afrika, Asia na Pasifiki.
Tunakukaribisha katika kuungana nasi na kusherehekea Mwaka wa Kimataifa wa Utalii Endelevu kwa Maendeleo 2017.


SERIKALI YAIPONGEZA COSTECH-OFAB KWA KUANDAA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA SAYANSI 2017

$
0
0
Mwandishi wa Habari wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu akipeana mkono na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa kwanza kwenye kuandika na kuelimisha umma kuhusu matumizi ya sayansi, Teknolojia na ubunifu hususani Bioteknolojia katika kuendeleza kilimo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Hassan Mshinda
Washindi wa tuzo hizi wakisubiri kutangazwa.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Jim Yonaz akitoa hutuba katika hafla hiyo.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyindondi akielezea tuzo hizo
Mkurugenzi Mkuu wa COTECH, Dk.Hassan Mshinda akizungumzia tuzo hizo
Waziri Ndalichako akihutubia katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk.Ayoub Rioba akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mshindi wa tuzo hizo kutoka mkoani Kagera, Benson Eustace wa Clouds Media kikabidhiwa cheti chake.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Jim Yonaz akikabidhiwa cheti kutokana na mchango mkubwa wa vyombo hivyo katika kuandika habari za sayansi.
Mwakilishi wa TBC, akikabidhiwa cheti kutokana na mchango wa kuandika habari za sayansi.
Ofisa Mawasiliano wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha SUA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Kujiendeleza (ICE), Bujaga Inzengo Kadago akipokea cheti kutokana na mchango wa vyombo vya habari vya chuo hicho wa kuandika habari hizo.
Mwanahabari wa gazeti la Habari Leo, Lucy Ngowi akikabidhiwa cheti.
Mwanahabari Hellen Kwavava akikabidhiwa cheti.
Mwanahabari wa Gazeti la Nipashe mkoani Kagera, Restuta Damian akipokea cheti.
Mwanahabari wa gazeti la Guardian, Daniel Simbei akipokea cheti.
Mwanahabari Calvin Gwabara kutoka SUA akipokea cheti.
Mwanahabari wa gazeti la Daily News, Fatma Abdul akipokea cheti.
Mwanahabari Elias Msuya wa Gazeti la Mwananchi akikabidhiwa cheti.
Mwanahabari wa RFA kutoka Mwanza, Coleta Makulwa akipokea cheti
Mwanahabari wa gazeti la Habari Leo, Shadrack Sagati akikabidhiwa cheti.
Mwanahabri Dino Mugunde wa Star TV Mwanza akipokea cheti.
Waziri Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na washindi. 
Mshindi wa kwanza wa tuzo hizo, Gerald Kitabu akitoa shukurani zake. 
Mwanahabari Calvin Gwabara kutoka SUA, akipongezwa na dada yake huku akionesha vyeti vyake.



Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka waandishi wa habari nchini kutumia taaluma zao kuelimisha jamii kuhusu habari za sayansi na teknolojia ili kuleta maendeleo nchini.

Akizungumza wakati wa utoaji tuzo za umahiri katika uandishi wa habari za Sayansi zilizoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknlojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknojia (OFAB), Waziri Ndalichako alisema tuzo hizo iwe ni chachu za kuandika habari za sayansi kwa undani ili kuwajengea uelewa wananchi wa.kawaida.

Alisema ufundi wa waandishi katika.kuandika habari za sayansi utasaidia kutangaza ubunifu na kuongeza tija thamani katika teknolojia mbalimbali."Wananchi wanahitaji teknolojia za kisasa katika kurahisisha utendaji kazi hivyo uandishi wenu utasaidia kuinua sekta ya kilimo na mifugo ambayo ndio kundi.muhimu katika jamii hasa katika kuelekea uchumi wa viwanda,"alisema Ndalichako.

Aliwataka Costech na taasisi nyingine kuendelea kushirikiana na wanahabari kuelimisha jamii katika masuala ya sayansi.Ndalichako alipongeza COSTECH na OFAB kwa kuandaa tuzo hizo kwani zitaongeza mori kwa wanahabari wa kuandika habari za sayansi.

Akielezea ushiriki wa.waandishi katika shindano hilo lililoanza Januari hadi Agosti mwaka hii, Mkurugenzi Mkuu wa COTECH, Dk.Hassan Mshinda alisema, shindano hilo hapa nchini sasa ni mara ya tisa kufanyika na kwa upande wa Afrika ni la kumi.

Alisema katika shindano hilo jumla ya makala 200,vipindi vya radio 20 na televisheni 15 vilishindaniwa.Mshindi alisema watalaam waliobobea ambao walifanyakazi ya.kutafuta washindi ambao walipata dola 250, 750, 1,000 na 1,500.Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Jim Yonaz aliwataka waandishi kuwa daraja kati ya wana sayansi na jamii.

Alisema wana sayansi wana lugha ngumu hivyo kupitia waandishi na aina ya uandishi wao wamesaidia jamii kuelewa habari mbalimbali za sayansi."Katika kuchangia uchumi wa viwanda waandishi wanakazi kubwa kuhakikisha wanatoa elimu ya sayansi na kilimo ili kuelimisha jamii,"alisema Yonaz.

Yonaz pia aliiomba Serikali kuhakikisha inawawezesha waandishi kwa kuwajengea uwezo wa ufahamu ili waweze kuelewa zaidi sababu zinazowafanya kuandika habari mbalimbali.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk.Ayoub Rioba alisema, wana sayansi wana jukumu la kuboresha maisha ya jamii kwa kuhakikisha wanatumia zana zilizoboreshwa kiteknolojia.Alisema kwa sababu ya lugha itumikayo na wana sayansi upo umuhimu wa wanahabari kuandika.habari nyingi za sayansi.

Rioba pia aliitaka taasisi ya Costech pamoja na taasisi nyingine kuendelea kufanya kazi za kuelimisha jamii kwa kushirikiana na wana habari ili kujenga jamii yenye uelewa wa masuala ya sayansi.Miongoni mwa waliopata tuzo za umahiri wa habari za Sayansi ni pamoja na mshindi wa jumla Gerald Kitabu (Guardian), Shedrack Sagati(Habari Leo), Elias Msuya (Mwananchi), Calvin Gwabara, Fatma Abdul (Daily News) na Dino Mugunde.

Wengine ni Lucy Ngowi, Hellen Kwavava, Coleta Makulwa, Daniel Simbei, Benson Eustace na Restuta Damian.

MARUFUKU SHULE MKOANI SINGIDA KUNUNUA CHAKI NJE YA MKOA-RC NCHIMBI

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akishiriki zoezi la kutengeneza chaki katika kiwanda cha Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Miraji Jumanne Mtaturu akiwa amebeba ili kuzianika chaki alizotengeneza Mkoa Singida Dkt Rehema Nchimbi katika kiwanda cha Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akikagua kiwanda cha kutengeneza jasi cha Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Dober Color wakifungasha chaki, Meneja wa Kiwanda hicho amesema sehemu ya kufungasha chaki hiyo inafanywa na wanawake kwakuwa wako makini na haraka.
Mkuu wa Mkoa Singida Dkt Rehema Nchimbi akikagua ubora wa chaki inayozalishwa katika kiwanda cha Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, kushoto kwake ni Meneja wa Kiwanda hicho Abdul Razak Mahamoud.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amepiga marufuku Shule zote Mkoani Singida kuagiza chaki nje ya Mkoa kwakuwa kuna viwanda vinavyozalisha chaki bora mkoani hapa.

Dkt Nchimbi ametoa katazo hilo mara baara ya kufanya ziara katika viwanda viwili vinavyozalisha chaki katika halmashauri ya Itigi na kushuhudia chaki yenye ubora ikiwa imezalishwa kwa wingi na ikiwa haijapata soko.

“Hawa wenye viwanda wamejitahidi kuzalisha chaki bora haina vumbi na inauzwa kwa bei sahihi lakini shule zetu badala ya kuja kununua hapa ambapo ni karibu wanaagiza Dar es salaam na mikoa mingine”, amesema na kuongeza kuwa,

“Yani mnasubiri chaki hii hii iende Dar es Salaam halafu mnainunulia kutoka huko, hii haikubaliki, kuanzia leo shule zote zinunue chaki hapa hapa ili tupunguze gharama pamoja na kuinua viwanda vyetu”.Dkt Nchimbi ameongeza kuwa Mikoa ya Jirani itakayonunua chaki katika Viwanda vya Singida, vitasafirishiwa chaki hiyo bure kama motisha kwa kuunga mkono viwanda hivyo.

Amezitaka halmashauri kushirikiana katika kuboresha mazingira ya utendaji wa viwanda hivyo hasa kwa kuangalia namna ya kuboresha barabara zinazoenda katika machimbo ya jasi yanayotumika kutengeneza chaki kwakuwa wenye viwanda wamekuwa wakilalamikia ubovu wa barabara hizo.

Aidha Dkt Nchimbi ametoa wito kwa wenye viwanda wote nchini ambao wanatumia madini ya jasi (gypsum) katika shughuli zao wasihangaike kutafuta madini hayo bali waje singida kuna viwanda vinatengeneza madini hayo kwa ubora mzuri na bei nzuri.

Amesema viwanda vya kutengeneza jasi Singida vimekuwa vikizalisha madini hayo kwa wingi hivyo wenye uhitaji wa madini hayo kutengenezea chaki, gypusum board POP, wanakaribishwa kununua madini hayo mkoani hapa.

Dkt Nchimbi amewapongeza wenye viwanda hivyo kwa kutumia rasilimali kama madini ya jasi iliyopo Singida kwa kuanzisha viwanda mabavyo vinatengeneza ajira na kukuza uchumi kwa kuwa wao wamekuwa walipa kodi wazuri.

Naye Meneja wa kiwanda cha chaki cha Dober Color kilichopo Itigi Abdul Mahamoud amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa hatua yake ya kukataza kuagizwa chaki nje ya Singida kwakuwa kutaongeza soko ambalo litasaidia viwanda hivyo kukua.

“Mkuu wa Mkoa tunashukuru kwa katazo hilo kwakuwa litafanya viwanda vyetu vikue na kuongeza uzalishaji, lakini pia itafanya viwanda hivi viongeze ajira na hata kodi tunayolipa itaongezeka hivyo kukuza uchumi wa Singida”, amesema Mahamoud.

Ameongeza kuwa kwa sasa kiwanda hicho kinazalisha tani hamsini kwa siku lakini kutokana na katazo hilo matarajio ni kuongezeka uzalisha hadi kufikia tani 200 za chaki kwa siku.

PROF. MAGHEMBE AONGOZA MAADHIMISHO YA 87 YA SIKU YA TAIFA LA SAUDI ARABIA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya 87 ya Taifa la Kifalme la Saudi Arabia yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Prof. Maghembe alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kulia ni Balozi wa taifa hilo nchini Tanzania, Balozi Mohammed Bin Mansour Al Malik.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour Al Malik (wa pili kulia) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakijiandaa kukata keki ya maadhimisho hayo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour Al Malik (katikati) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakikata keki ya maadhimisho hayo.
Baadhi ya watoto wa Taifa la Kifalme la Saudi Arabia wakiinua bendera ya nchi hiyo kuashiria maadhimisho ya siku ya 87 ya Taifa hilo yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

Mara Paaap! Tigo Fiesta TAMADUNIKA 2017 ndani ya Tabora

NSSF ARUSHA KUWASHTAKI WAAJIRI 126 KWA KOSA LA KUTOWASILISHA MICHANGO YA WAAJIRIWA INAYOFIKIA SHILINGI BILIONI

$
0
0
NA: ANDREA NGOBOLE, PMT

Jumla ya Kampuni 126 zinazodaiwa kiasi cha shilingi bilioni moja pointi tano zinatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo na shirika la Taifa la hifadhi ya jamii NSSF mkoani Arusha kwa kosa la kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mapema jana meneja kiongozi wa NSSF mkoani Arusha Dr. Frank Maduga amesema kuwa makampuni hayo yamegawanyika kati ya waajiri wakubwa 14 wanaolipia kiasi cha shilingi milioni 50 na kuendelea, wajiri wa kati 69 wanaolipia milioni 5 hadi 49.9 na wale waajiri wadogo 53 wanaolipia kiasi cha shilingi elfu ishirini hadi milioni 4.9 kwa mwezi ambapo jumla ya michango yao inafikia Zaidi ya bilioni moja nukta tano mpaka sasa.

“Waajiri wakubwa wote wamekwisha pelekewa onyo la Mwisho na sasa taratibu za kimahakama zinaendelea hivyo kuanzia jumatatu ya tarehe 2 october 2017 mtawajua ni waajiri gani wameshindwa kutekeleza wajibu wao na kwa kiasi gani wanadaiwa kila mmoja wao” alisema dokta Maduga

Amesema kuwa Mashitaka yatakayokuwa yakiwakabali waajiri hao ni kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati na kwa muda unaozidi miezi sita, kitendo hicho kimekuwa na madhara makubwa kwa wafanyakazi na wategemezi wao kwa kukosa huduma za matibabu , fao la uzazi na pia kuna baadhi ya wanachama taarifa zao za kumbukumbu hazioneshi fedha yoyote katika muda ule ambao michango haijawasilishwa na kusababisha taharuki na msongo wa mawazo kwa wafanyakazi husika.

Mwanachama ana haki ya kulipwa michango yake yote akiacha kazi au kampuni ikifa na kuacha kuendesha biashara hulazimika kulipa fedha zote za michango ya wanachama na wao kama taasisi inayosimamia haki za waajiriwa huhakikisha malipo yote yanalipwa na kutolea mfano kampuni za snowcrest na mukidoma zilizositisha shughuli zake na kutangaza kufilisika walihakikisha kuwa kila mfanyakazi anapata mafao yake bila wasiwasi wowote.

Amesisitiza kuwa mwanachama akishaacha kazi atasubiri kwa kipindi cha miezi sita ndiyo aweze kupewa fao la kustaafu na kipindi hiki huwekwa ili kumpa nafasi mwanachama kuweza kutafuta kazi na ama kuajiriwa na kampuni nyingine na changamoto inayowakabili ni kuwa baadhi ya wanachama hufoji barua za kuacha kazi ili waweze kupewa mafao yao huku bado wanafantya kazi jambo ambalo halikubaliki kwa mwanachama kulipwa fao lake huku anafanya kazi.

Naye Straton Simon Afisa msimamizi wa fao la matibabu NSSF kanda ya kaskazini inayowakilisha mikoa ya ARUSHA,KILIMANJARO, TANGA na MANYARA amesema kuwa fao la matibabu hutolewa bure na mfuko huo kwa kila mwanachama anayekuwa amewekewa michango yake kwa miezi mitatu na kuendelea na fao hili halihusiani na kukatwa akiba yako siku utakayostafu kazi au kampuni yako kusimama kufanya kazi hivyo amewataka wanachama wasiwe waoga kutumia fao hili kwani lina faida kwa mwanachama na wategemezi wake wane ambao ni mke au mume na watoto wane.

Amesema kwa Arusha pekee NSSF ina mkataba wa matibabu kwa wanchama wake na hospitali 34 zinazotibu wanachama wote wa hiari na wale waajiriwa ambao mpaka sasa wanafikia 18,400 na kwa kanda nzima ya kaskazini wanafikia wanachama 34000 wanaopata fao hilo la matibabu na kuwasihi wanachama wengine wote wahakikishe wanajaza fomu na kuchagua moja ya hospital ambayo ungependa kutibiwa kati ya hizo hospitali 34 ili wanufaike na fao hilo muhimu kwa maisha ya mwanachama.
 Meneja kiongozi wa NSSF mkoa wa Arusha katikati Dr. Frank Maduga akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuwapeleka waajiri 126 mahakamani kwa kosa la kutowasilisha michango ya waajiriwa inayofikia kiasi cha shilingi bilioni moja nukta tano kwa kipindi cha miezi sita sasa. 

Muhimbili Yazindua Mwongozo wa Kuwahudumia Watoto Wachanga

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika uzinduzi wa kitabu chenye mwongozo jinsi ya kutoa huduma ya afya kwa watoto wachanga wenye umri sufuri hadi siku 28. Uzinduzi huo umefanyika leo katika hospitali hiyo.
 Madaktari na wauguzi wakiwa kwenye mkutano wa kuzindua kitabu kinachoelezea jinsi ya kuwahudumia watoto wachanga baada ya kuzaliwa.
  Daktari wa watoto wa hospitali hiyo, Dk. Judith Cosmas ambaye ameshiriki kuaanda kitabu hicho akizungumza kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya wataalamu wa afya wakiwa kwenye mkutano huo leo.
 Mkuu wa Idara ya Watoto, Dk. Merry Charles akisisitiza jambo huku akionesha kitabu hicho ambacho kitakuwa kikitumika wakati wa kuwahudumia watoto hao.
 Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Museru (kaunda suti) akiwa kwenye mkutano huo leo.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya MNH na wadau mbalimbali.
 
 
 Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imezindua muongozo utakaosaidia kuwahudumia watoto wachanga ( Neonatal Guideline) wenye umri kuanzia siku 0 hadi siku 28 ili kuhakikisha wanapata huduma inayostahiki.

Muongozo huo umeandaliwa na madaktari wa MNH na kupitiwa na wadau mbalimbali wakiwemo wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) pamoja na Chuo Kikuu cha Kwazulu Natal kilichopo Afrika Kusini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema muongozo huo si tu unamanufaa kwa MNH bali pia una manufaa kwa hospitali zingine kwani utawezesha mtoto kupata tiba inayotakiwa hata sehemu ambazo hakuna watalaam.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Watoto Edna Majaliwa ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Watoto Wachanga wa hospitali hiyo amesema kuwepo kwa muongozo huo kutasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga sanjari na kupunguza rufaa za watoto hao kuletwa Muhimbili .

‘’ Kusudio letu ni kuendelea kupunguza vifo vya watoto wachanga , MNH tumefanikiwa kupunguza vifo hivyo kutoka 26 kwa kila vizazi hai 1,000 na kufikia 18 kwa kila vizazi hai 1,000. Kwa mwaka watoto wanaozaliwa hapa ni takribani 10,000 hivyo naamini muongozo huuu utaleta mabadiliko makubwa‘’ amesema Dk. Majaliwa.

Pia ameelezea vyanzo vinavyosababisha vifo vya watoto wachanga kuwa ni madhara ya kuwa njiti, mtoto ambaye amezaliwa na hakulia pamoja na mtoto mwenye vimelea vya bakteria.

Akiwasilisha mada kuhusu muongozo huo , Daktari wa watoto , Jullieth Cosmas ametaja sababu zinazochangia watoto wachanga kulazwa Hospitalini kuwa ni mtoto kuzaliwa kabla ya wakati(Njiti) mtoto kushindwa kupumua vizuri pindi anapozaliwa , mtoto kupata maambukizi , mtoto kutolia wakapi alipozaliwa na mtoto kuumia wakati akizaliwa.
 

"Mafunzo ya Elimu ya ufundi yana nafasi ya kukuza ajira"- Rutayuga

$
0
0
Mafunzo ya elimu ya ufundi yananafasi kubwa ya kuongeza, kusaidia na kukuza ajira kwa vijana wanaosoma masomo hayo kwenye vyuo vya ufundi kwa kuajiriwa au kujitengenezea ajira wao wenyewe.
 
 Kaimu katibu mtendaji wa baraza la taifa elimu ya ufundi (Nacte), Dkt, Adolph Rutayuga amesema hayo leo jijini dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya mradi wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO.
 
Akizungumza kwa niaba ya Katibu mkuu wizara ya elimu,sayansi na teknolojia, Dkt, Rutayuga amesema nia kubwa ya mradi huo ni kuangalia ufundi unaumuhimu gani kwenye sekta ya uchumi hasa unapozungumzia sekta ya uchumi wa viwanda. Aidha tunaangalia ubora wa mafunzo yanayotolewa kwenye elimu ya ufundi sababu kukiwa na vyuo vingi ambavyo vinaendeshwa katika ubora usiotakiwa, wanafunzi wanaotoka kwenye vyuo hivi hawatakuwa wazuri. 
 
“Tunalenga kujenga mazingira ya kutoa mafunzo bora kwenye elimu ya ufundi, elimu iliyobora kwa kusapoti walimu wanaofundisha,miundombinu ya kujifunza na kufundishia na pia kujaribu kuangalia mahusiano yaliyopo kati ya viwanda na soko la ajira kwa kile kinachotolewa kwenye vyuo vya ufundi.
 
 Ameongeza,kama suala zima la mambo ya mitaala, linaweza kuboreshwa, na ile dhana potufu ya kizamani iliyokuwepo kwamba kwamba Tivet ni kwa wale walioshindwa,inapaswa iondoke, watu wajue kwamba mchango mkubwa kwenye uchumi unafanywa na hawa watu kwenye sekta ya kati “Malengo makubwa ni kujaribu kuinua ubora wa mafunzo yanayotolewa na vyuo vya ufundi, kuinua umuhimu mafunzo ya ufundi na Jinsi inavyoweza kisaidia kwenye maendeleo ya kukuza uchumi,” amesema. 
 
Naye, Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe amesema warsha hiyo itajadili kwa undani vitendo vya ufanisi, utekelezaji na jukumu la uwezo ambao kila wadau watafanya katika mradi uliopendekezwa chini ya maeneo matatu umuhimu, ubora na mtazamo wa elimu na ujuzi wa kiufundi. “Elimu bora kwa Afrika itatekelezwa kuanzia mwaka huu hadi 2021 kwa lengo la kukuza elimu na ujuzi wa kitaaluma na mafunzo ambayo ni muhimu kwa mahitaji ya soko la ajira na mahitaji ya watu binafsi na jamii”amesema Plathe. Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii .Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe akizungumza washiriki wa warsha ya kuzindua Mradi wa mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Rutayuga akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wakati wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Unesco ya kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washririki na Meza kuu wakiwa katika warsha ya uzinduzi wa Mpangowa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya washririki wa Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Lutayuga wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Mtoa maada akizungumza na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)

Prof. Maghembe Kufungua Maonesho ya Utalii Iringa leo

$
0
0
Mhandisi Kerdick Chawe (kushoto) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (mwenye ushungi) kwenye banda la maonesho la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wanaoshiriki kwenye maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Richard Kasesela (kulia) akisalimiana na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa kilichopo Kata ya Nduli, katika banda la maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Bahati Mollel akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Richard Kasesera katika banda lao la maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Katioliki cha Iringa (RUCU), wakipata maelezo mbalimbali ya viwanja vya ndege kutoka kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa kilichopo Kata ya Nduli, Bi. Hana Kibopile katika maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
Meneja wa SUMATRA mkoa wa Iringa, Mhandisi Patel Ngereza(kushoto),akimsikiliza maelezo mbalimbali kutoka kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Iringa kilichopo kata ya Nduli,Bi. Hana Kibopile katika maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwenye Viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
Mhandisi Kedrick Chawe (wa pili kushoto), akimpa maelezo mbalimbali Bw. Nathan Hesketh wa Iringa alipotembelea banda la maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.



WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe leo atafungua rasmi maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim, yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.

Maonesho hayo yenye kaulimbiu ya Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda yanashirika taasisi za serikali, mashirika ya umma na kimataifa zaidi ya 400, ambapo yatamalizika Oktoba 2, 2017, ambapo yanalengo la kuweka uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa utalii na thamani thamani ikiwa ni pamoja na kuutangaza utalii kwa kuihamasisha jamii kutumia fursa za utalii zilizopo katika kuinua uchumi wa wakazi wa Ukanda wa Kusini mwa Tanzania na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa Wizara mbalimbali zipo na taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Idara ya Utalii, Wanyamapori, Mambo ya Kale na Misitu na Nyuki, Chuo cha Taifa cha Utalii, Makumbusho ya Taifa, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mamlaka ya Usimamizi ya Wanyamapori (TAWA) Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF).

Taasisi nyingine ni Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, (TFS) Taasisi ya Utafiti wa Misitu na Wadau wa Wizara ya Maliasili na Utalii.Wadau wa Sekta ya Utalii kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini watashiriki kuonesha bidhaa na huduma zao muhimu na mikoa inayoshiriki ni pamoja na wenyeji Iringa, Mbeya, Ruvuma, Songwe na Njombe.

Fursa zilizopo nyanda za Juu Kusini ni pamoja na Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa, Ismila,Kalenga na Boma la Mkuu wa Wilaya, Hifadhi za Mahale, Katavi, Ruaha, Kitulo na Selous.

RAIS WA BURUNDI PIERRE NKURUNZINZA ATEMBELEA MAONESHO YA KWANZA YA BIASHARA YA TANZANIA MJINI BUNJUMBURA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mheshimiwa Pierre Nkurunziza, leo tarehe 28.9.2017 ametembelea Maonesho ya Kwanza ya Biashara ya Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya Maonesho vya Tempete vilivyopo Mjini Bujumbura.
 
 Maonesho haya yaliandaliwa na TANTRADE kwa ushirikiano na Ubalozi wa Tanzania Burundi pamoja na Mamlaka ya Bandari Tanzania ( TPA ) yamefunguliwa rasmi tarehe 27.9.2017 na Dr Joseph Bitore, Makamu wa Pili wa Rais wa Burundi yanatarajia kumalizika tarehe 1.10.2017. 
 
Baada ya kutembelea Maonesho haya, Mh. Rais Nkurunziza alisifu uhusiano uliopo baina ya Burundi na Tanzania na aliahidi kuunga mkono juhudi zote za kuimarisha uchumi baina ya Nchi hizi mbili. 
 
Picha chini zinamuonesha Rais Nkurunzinza akiongozwa na Mh. Christopher Chiza, Mwenyekiti wa Bodi TanTrade, Balozi Rajabu Gamaha, Balozi wa Tanzania Burundi pamoja na Bw. Edwin Rutageruka, Kaimu Mkurugenzi Mkuu TanTrade ambao wapo Mjini Bujumbula kwa sasa kubudhuria Maonesho haya.

  Rais Nkurunzinza akipata maelezo mafupi kuhusu bidhaa mbalimbali zinazouzwa kwenye maonesho hayo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu TanTrade Bw. Edwin Rutageruka,ambao wapo Mjini Bujumbula kwa sasa kubudhuria Maonesho hayo.
 Rais Nkurunzinza akiongozwa na Mh. Christopher Chiza, Mwenyekiti wa Bodi TanTrade, Balozi Rajabu Gamaha, Balozi wa Tanzania Burundi pamoja na Bw. Edwin Rutageruka, Kaimu Mkurugenzi Mkuu TanTrade ambao wapo Mjini Bujumbula kwa sasa kuhudhuria Maonesho hayo.
 Mheshimiwa Pierre Nkurunziza, Rais wa Jamhuri ya Burundi, leo tarehe 28.9.2017 ametembelea Maonesho ya Kwanza ya Biashara ya Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya Maonesho vya Tempete vilivyopo Mjini Bujumbura.
 
 Rais Nkurunzinza akihojiwa na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani),kwenye maonesho hayo, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi TanTrade, Christopher Chiza pamoja na  Kaimu Mkurugenzi Mkuu TanTrade Bw. Edwin Rutageruka,ambao wapo Mjini Bujumbula kwa sasa kubudhuria Maonesho hayo.

KAMPUNI YA BIMA YA MGen INSURANCE YATOA MSAADA WA MASHINE MBILI ZA KUPIMA KIWANGO CHA HEWA NA MAPIGO YA MOYO KWA WATOTO WACHANGA HOSPITALI YA MAWANANYAMALA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya MGen Insurance Tanzania ya jijini Dar es salaam Bw. Charles Sumbwe akikabidhi msaada wa mashine mbili za Kupima Kiwango cha Hewa na Mapingo ya Moyo kwa Watoto wachanga (Pulse Oxmeter) kwa Daktari Bingwa wa Watoto katika hospitali ya Mwananyamala Dkt. Elnestina Mwipopo leo jijini Dar es salaam, Kampuni hiyo imetoa mashine hizo zenye thamani ya shilingi milioni 2.8 na vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto katika hospitali hiyo jumla ya msada wote ni shilingi milioni 3.8.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya MGen Insurance Tanzania ya jijini Dar es salaam Bw. Charles Sumbwe akikabidhi msaada wa Vifaa mbalimbali vya kuwahudumia watoto kwa Daktari Bingwa wa Watoto katika hospitali ya Mwananyamala Dkt. Elnestina Mwipopo leo jijini Dar es salaam, Kampuni hiyo imetoa mashine hizo zenye thamani ya shilingi milioni 2.8 na vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto katika hospitali hiyo
3 4
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya MGen Insurance Tanzania ya jijini Dar es salaam Bw. Charles Sumbwe na Daktari Bingwa wa Watoto katika hospitali ya Mwananyamala Dkt. Elnestina Mwipopo mara baada ya kukabidhiana msaada wa mashine mbili za Kupima Kiwango cha Hewa na Mapingo ya Moyo kwa Watoto wachanga (Pulse Oxmeter) kwa leo jijini Dar es salaam.
5
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya MGen Insurance Tanzania ya jijini Dar es salaam Bw. Charles Sumbwe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi misaada hiyo.
6
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya MGen Insurance ya jijini Dar es salaam Bw. Charles Sumbwe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi misaada hiyo wa pili kutoka kulia ni Lugano Mkisi Mkuu wa Masoko Kampuni ya Bima ya MGen Insurance Tanzania.
7
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya MGen Insurance ya jijini Dar es salaam wakiwa katika hospitali ya Mwananyamala tayari kwa kukabidhi misaada hiyo.
8
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya MGen Insurance ya jijini Dar es salaam wakibeba miziogo baada ya kuwasili katika hospitali ya Mwananyamala tayari kwa kukabidhi misaada hiyo.
9
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya MGen Insurance ya jijini Dar es salaam wakishusha mizigo kwenye gari mara baada ya kuwasili katika hospitali ya Mwananyamala tayari kwa kukabidhi misaada hiyo.

MISA TANZANIA YAZINDUA RIPOTI YA UTAFITI KUHUSU UWAZI KWENYE TASSISI ZA UMMA

$
0
0
Wadau wa habari nchini wameomba kupata taarifa iwe ni haki ya kila mtu ambayo inapaswa kulindwa kwa nguvu  zote na ni kiashiria kimoja wapo cha serikali yenye uwazi na inayothamini mchango na ushiriki wa wananchi wake katika ujenzi wa taifa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upatikanaji wa habari yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, wamesema kila mtu ana haki ya kupokea na kutoa taarifa ili mradi tu asiende nje ya swala husika.
Wamesema kuwa, lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya haki ya kila mtu na kupata taarifa muhimu kwa Maisha yao ikiwa ndani ya hifadhi ya Serikali na kwingineko, namna viongozi waliyochaguliwa na wanavyotekeleza majukumu yao.
Katika maadhimisho hayo MISA-TAN walikabidhi tuzo kwa taasisi mbali mbali za umma zinazotoa taarifa kwa uwazi na zile zinazobana taarifa. Kwa mwaka 2017, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeibuka mshindi wa kwanza kwa utoaji na upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma na taasisi iliyokuwa mshindi wa mwisho ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) baada ya kubainika kuwa inabana taarifa.  Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Kila Mtanzania Anayo Haki Ya Kupewa Taarifa."

Kaimu Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania. Bi. Lianne Houben akizungumzia jinsi ubalozi unavyofanya kazi na taasisi za habari hapa nchini ili kuweza kufanikisha upatikanaji wa habari kwa wananchi nchini Tanzania.

Mgeni Rasmi Jaji Mstaafu na Mwenyekiti aliyepita wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala,   Amiri Ramadhani Manento, akifungua maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upatikanaji wa taarifa yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Charles Stuart akizungumza akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa zinazoadhmishwa Septemba 28 kauli mbiu ya mwaka huu "Kila Mtanzania anayo haki ya Kupewa Taarifa" 
Makamu Mwenyekiti wa MISA Tanzania, WakiliJames Malenga akizungumzia vigezo vilivyotumika kuchagua taasisi zilizofanyiwa utafiti mwaka huu, Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN) katika katika Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.
 Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Charles Stuart( wa pili kutoka kulia) pamoja na wadau mbalimbali wakiwaonesha waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa Chapisho la Upatikanaji Taarifa kwa taasisi za umma kwa mwaka 2017.
  Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Charles Stuart  akionesha kufuli la Dhahabu lililokwenda kwenye Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) baada ya kubainika kuwa inabana taarifa kwa umma.
Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Charles Stuart akimkabidhi tuzo ya Funguo la dhahabu Afisa Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima Ya Afya (NHIF), Shani Mussa walioibuka washindi wa kwanza upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma.
Baadhi ya wadau mbalimbali wakifuatilia mada kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upatikanaji wa habari

SERIKALI: KASI YA MENDELEO YA TEKINOLOJIA INATULAZIMU KUFANYA MABORESHO YA MARA KWA MARA YA KANUNI ZETU

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta habari ili kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta habari ili kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka TCRA, Fred Ntobi, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Rodney Thadeus akielezea jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya habari ili kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni leo Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Maudhui kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka akiwasilisha mada kuhusu kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya habari ili kujadili kanuni hizo leo Jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Phillip Filikunjombe akiwasilisha mada kuhusu kanuni za maudhui ya utangazaji wa na mitandao wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya utangazaji na mitandao ili kujadili kanuni hizo leo Jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Evodi Kyando akitoa maelezo kuhusu kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya utangazaji na mitandao ili kujadili kanuni hizo leo Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katika) akifuatilia majadiliano ya wawakilishi kutoka vyombo vya habari vya elekroniki na mitandao wakati wa kikao cha kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba.
Mmoja wa washiriki wa kikao cha wadau wa utangazaji na waendeshaji wa mitandao Maria Sarungi Tsese (katikati) akichangia hoja wakati wa kikao cha kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na televisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (waliokaa katika) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Televisheni na Redio mara baada ya kikao cha kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni leo Jijini Dar es Salaam.

Picha na: Frank Shija – MAELEZO

……………….

Na Pascal Dotto, MAELEZO

Serikali imesema kasi kubwa ya maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo imeikumba sekta ya habari inalazimu jamii kufanya maboresho ya mara kwa mara ya Sera na Kanuni ili kuepusha matumizi mabaya ya vyombo vya habari.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa katika kufanya hivyo ni wajibu wa wadau wote kushirikiana kutumia vyema maendeleo hayo ya tekinolojia kwa ajili ya ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa.

Profesa Elisante alisema hayo leo wakati akifungua mkutano wa siku moja wa mashauriano miongoni mwa wadau wa sekta ya habari kuhusu mapendekezo ya Kanuni za maudhui yanayorushwa na vituo vya Utangazaji vya Redio na Televisheni na Kanuni za Maudhui Mtandaoni.

“Ni wajibu wetu kama taifa linalosimamia maadili na ambalo lingependa kudumisha amani na mshikamano, kutunga kanuni ambazo zitahakikisha kuwa kunakuwa na matumizi mazuri, sahihi na salama ya maudhui ya mtandaoni”Profesa Elisante alisisitiza.

Aliwaambia washiriki wa mkutano huo kuwa kuweka kanuni ni suala muhimu na kuwakumbusha matumizi ya mfumo wa habari mtandaoni wakati mwingine umetumika kupotosha jamii, kujenga chuki, kutoa habari za faragha za watu binafsi au habari zilizoleta sintofahamu miongoni mwa jamii.

Aliongeza kuwa kufanyika kwa mkutano huo ni jambo muhimu kwa kuwa washiriki watapata fursa ya kujadili kanuni hizo ambazo baadhi zinadaiwa kuwa zimepitwa na wakati na pia haziendani na utendaji na kazi katika ushindani wa soko.

Katika mkutano huo ambao Profesa Elisante alikuwa mwenyekiti wake alieleza kuwa pamoja na kuwa bado kumekuwepo na mijadala mikali katika nchi nyingi zikiwemo za Magharibi kuhusu uwekaji kanuni lakini ukweli unabaki kuwa nchi hizo zimeweka sheria na kanuni zinazosimamia matumizi ya intaneti.

“Ni kweli kwamba tekinolojia hii ina changamoto katika usimamizi lakini hakuna uhuru usio na mipaka. Kwa hiyo imekuwa ni wajibu wa kila nchi kutafakari mahitaji na umuhimu wa kutoa miongozo itakayosaidia jamii na taifa” Alieleza Profesa Elisante.

Mapema akimkaribisha Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abassi aliwaeleza washiriki kuwa Mkutano huo ni muhimu katika historia ya maendeleo ya tasnia ya habari nchini kuwa umelenga kuweka kanuni bora zitakazoratibu tasnia.

“Tumeitana hapa kushauriana kuhusu kanuni hizi hivyo hakuna haja ya kueneza wasiwasi kuwa katika mitandao ya kijamii kuwa serikali imedhamiria kudhibiti vyombo vya habari” Dk. Abbassi aliwaeleza washiriki.

Wakati huo huo, Serikali imeongeza muda wa siku saba kwa wadau wa sekta ya utangazaji na mitandao kuwasilisha maoni yao kuboresha kanuni zilizopendekezwa. Uamuzi huo umefikiwa mwishoni mwa mkutano wa mashauriano kujadili kanuni hizo ambapo wadau wengi waliomba muda zaidi.

Akifunga mkutano huo Profesa Elisante alisema ni vyema wadau wakaitumia fursa hiyo kuwasilisha maoni yao kwa maandishi ili kuboresha kanuni hizo hatimae taifa kuwa na kanuni bora kwa faida ya jamii yote.

Katika maelezo yake kufunga mkutano huo Profesa Elisante aliwashukuru washiriki kwa kutoa maoni yao na kuahidi kuwa serikali itayafanyia kazi maoni hayo.

Alieleza kuwa ni ukweli kuwa vyombo vya habari vinafanya biashara na pia vina wajibu wa kuelimisha jamii hivyo vitu viwili havina budi kwenda sambasamba bila kuathiri upande mwingine.

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AONGOZA KIKAO CHA MASHAURIANO KUHUSU MAUDHUI NA KANUNI MPYA ZA HUDUMA YA UTANGAZAJI TANZANIA (TV, RADIO, BLOG, ONLINE TV)

$
0
0
 Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii (Bloggers, Online Media) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (Katikati waliokaa), viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kumalizika kwa kikao cha mashauriano na Wadau kuhusu  huduma ya Utangazaji  (Maudhui) na kanuni za maudhui mitandaoni leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam

Kanuni  ziizojadiliwa ni maudhui yanayorushwa na vituo vya uatangazaji  vya Redio na Televisheni n maudhui mitandaoni (Online Content) Jumla ya vyombo vya habari 76 vilishiriki kwenye kikao hicho.

Wadau wamepewa wiki moja kuwasiliasha maoni yao kwenye kamati ya mashauriano ili yajadiliwe na kufanyiwa kazi kwa lengo la kuboresh kanuni/
 Wamiliki wa Wmiliki na wafanyakazi wa Vituo vya Televisheni na Radio wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (Katikati waliokaa), viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kumalizika kwa kikao cha mashauriano na Wadau kuhusu  huduma ya Utangazaji  (Maudhui) na kanuni za maudhui mitandaoni leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza  kuhusu mambo mbalimbali waliyokubaliana katika kikao cha mashauriano na Wadau kuhusu  huduma ya Utangazaji  (Maudhui) na kanuni za maudhui mitandaoni leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam

 Wadaui wa habari wakiwa katika kikao hicho



 Meneja Mipango na Utafiti wa Sahara Media Group,  Nathan Rwehabura akichangia mada wakati wa kikao hicho, ambapo pia alilalamikia ada kubwa inayotozwa kwa mwaka wamiliki wa vituo vya tv ambayo ni dola 25,000 swa na sh/ mil/ 60

 Dina Chaali wa Chanel Ten akitafakari jambo katika kikao hicho
 MMkurugenzi mstaafu wa Utangazaji wa TCRA, Habby Gunze akifafanua jambo katika kiao hicho

 Wakili wa Jamii Forum Benedict akichangia mada wakati wa kikao hicho

  Mkuu wa Vipindi wa EAST aFRICA radio, Nasser Kingu akichangia mada wakati wa kikao




WANAHABARI WATEMBELEA MITAMBO YA UZALISHA MAJI YA DAWASCO YA RUVU CHINI NA JUU

$
0
0
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wamefanya ziara ya siku moja katika Mitambo ya Uzalishaji Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini  iliyopo Mlandizi na Bagamoyo mkoani Pwani ,ziara iliyoandaliwa na Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salamaa (DAWASCO) kwa lengo la kujifunza namna matibabu ya maji yanavyofanyika kuanzia yanapotoka mto Ruvu.
Mbali na kutembelea Mitambo ya uzalishaji maji pia Wanahabari hao wametembelea ofisi za Dawasco mkoa wa Tabata kujionea utendaji kazi kwa watendaji wa Shirika hilo ,kituo cha Tabata. 
Meneja wa Dawasco Tabata, Victoria Masele akiwakaribisha wanahabari ofisi kwake mara baada ya kumtembelea.
Meneja Biashara wa Dawasco Tabata, Jamal Chuma kifafanua jambo kwa wanahabari.
Vifaa vilivyopo katika ofisi za Dawasco Tabata.
Mtambo wa kuzalisha Maji Ruvu Juu.
Maji yakiingia katika mitambo.
Kina cha maji kinavyoonekana.
Meneja 
Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu, Edward Mkilanya akiongea machache na wanahabari.  
Mhandisi wa Mtambo wa Ruvu Chini, Emaculata Msigali akitoa ufafanuzi jinsi unavyofanya kazi.

MBOLEA KUTOKA NJE YA NCHINI IWE CHACHU YA KILIMO CHENYE TIJA

$
0
0
Jovina Bujulu-MAELEZO

Hivi karibuni, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea (TFRA) imeingiza nchini mbolea yenye uzito wa tani 55,000 kwa mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja bila kuwepo malipo ya ziada bandarini. 

Mfumo huo utasaidia kupunguza bei na kuhamasisha matumizi ya mbolea kwa wakulima wengi nchini.

Uingizwaji wa mbolea hiyo ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2017/18, mjini Dodoma.

DKt. Tizeba alisema kuwa kuanzia msimu wa 2017/18  Serikali itaanza kuagiza mbolea kwa mfumo wa pamoja kwa kuanza kuagiza aina mbili za mbolea ambazo ni mbolea ya kupandia (DAP) na ya kukuzia (UREA), kwa kuwa ndizo  zinatumika sana nchini.

Alitaja sababu za kutumia mfumo huo kuwa ni pamoja na kuongeza matumizi ya mbolea nchini kwa kuhakikisha kuwa wadau wote wanapata uhakika wa upatikanaji wa mbolea kwa bei ya ushindani. 

Aidha, mfumo huo unawawezesha wafanyabiashara wadogo wanapata nafasi ya kuagiza mbolea na kuimarisha mtandao wa usambazaji hadi ngazi ya mkulima.

Vilevile utaratibu huo unawawezesha waagizaji kununua mbolea wakati bei ikiwa ndogo na TFRA  kufuatilia bei hiyo ili kuepuka mwanya wa waagizaji kuongeza bei zaidi ya ile iliyonunuliwa kwa bei ndogo.

Kabla ya uamuzi wa Serikali wa kuagiza mbolea kwa kutumia mfumo huu matumizi ya mbolea hayakuwa ya kuridhisha  kutokana na mbolea kuwa na bei kubwa jambo ambalo liliwafanya wakulima, hasa wadogo kushindwa kumudu bei hiyo.

Hivyo baada ya Serikali kupitia tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu waelekezi wa ndani na nje ya nchi kwa kutumia uzoefu wa taasisi nyingine zinazofanya ununuzi wa bidhaa kwa pamoja,ikaamua kutumia njia ambayo inawapa wakulima unafuu wa bei wakati wa kununua mbolea hizo.

Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Lazaro Kitandu amesema kuwa mbolea iliyoletwa nchini imegharimu zaidi ya shilingi bilioni 10, ambapo wafanyabiashara wa Morocco kupitia kampuni ya OCPSA wameingiza tani 23,000 za mbolea ya kupandia (DAP) na kampuni ya Premium Agro Chem ya Tanzania wameingiza tani 32,000 za mbolea ya kukuzia (UREA).

Mamlaka imehakiki vyombo vya kupimia mbolea hiyo ili iwe na viwango vinavyokidhi ikiwa ni pamoja na kusimamia ugawaji bila kuwepo uchakachuaji.

Kitandu amesema kuwa Serikali imepanga kutoa mbolea hiyo kwa bei nafuu ambapo mamlaka itasimamia katika kila ngazi ili kusaidia wakulima kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kudhibiti bei toka kule inapotoka na kuhakikisha inauzwa kulingana na bei ya soko la dunia.

Kuhusu namna mbolea itakavyowafikia wakulima, Kitandu alisema kuwa mbolea hiyo inatarajiwa kusambazwa zaidi kwa kutumia usafiri wa treni ili kupunguza gharama za usafirishaji.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba alisema kuwa bei elekezi ya mbolea itatangazwa kupitia vyombo vya habari na kutoa onyo kwa mawakala kujipangia bei kwa kuuza mbolea nje ya bei elekezi na kwamba ikibainika hatua za kisheria kama vile kunyang’anywa leseni,kufungiwa, faini au hatua zote kwa pamoja zitachukuliwa.

Aidha, alisema kuwa bei hizo zitasimamiwa katika kila ngazi na kuzitaka mamlaka husika kuanzia Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na vijiji kuhakikisha kuwa bei elekezi itakayotolewa na Serikali inafuatwa kwa sababu mamlaka ya mbolea pekee haiwezi kuwa na wasimamizi kila mahali.

“Ununuzi wa mbolea kwa pamoja utasaidia kudhibiti bei, iwapo iwapo kutajitokeza ongezeko lisilokuwa na sababu (soko holela), kwa kuwa bei itatangazwa kwa kuzingatia bei halisi ya mbolea na gharama halisi za usafirishaji ikiwemo kiwango stahiki cha faida kwa mfanyabiashara” alisema Kitandu.

Utaratibu huu utawainua wakulima katika uzalishaji wa mazao kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kununua mbolea kwa bei nafuu  pia wakati huo huo watakuwa na uhakika mbolea hiyo ina viwango vinavyokidhi kwa kuwa inaingizwa nchini na kusambazwa na mamlaka yenye dhamana.

Pamoja na uhakika wa mbolea yenye bei nafuu na yenye viwango stahiki, wakulima wanatarajiwa kupata faida ya kupatiwa mafunzo kuhusu matumizi ya mbolea hizo kutoka kwa wataalamu wa mamlaka ya udhibiti, hivyo kuwa na matumizi sahihi ya mbolea. Ikiwa wakulima watatumia nafasi hii vizuri, sekta ya kilimo nchini inategemewa kuwa na manufaa wakulima na taifa kwa ujumla.

Mfumo huo utawawezesha wafanyabiashara wadogo kukua na kushiriki katika biashara ya mbolea na kuimarisha mtandao wa usambazaji kuanzia ngazi ya wakulima wakubwa hadi kwa mkulima mdogo.

Serikali inatarajia matokeo chanya katika kupunguza bei ya mbolea kwa wakulima itakayosaidia kuongeza matumizi ya mbolea na uzalishaji wenye tija ambao utachochea na kuimarisha uchumi wa viwanda.

JAFO AWATAKA WATENDAJI MANYONI KUSIMAMIA MIRADI IPASAVYO

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu wakikagua chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha Afya Kintinku wilayani Manyoni.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua magodoro katika wodi ya wagonjwa kwenye Kituo cha Afya Kintinku wilayani Manyoni.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua chumba cha dawa katika Kituo cha Afya Kintinku wilayani Manyoni.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua Kituo cha Afya Kintinku wilayani Manyoni.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua Kituo cha Afya Kintinku wilayani Manyoni.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua mradi wa maji Kintinku wilayani Manyoni.



NAIBU waziri wa Nchi ofisi Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amefanya ziara katika kituo cha Afya cha Kitinku kilichopo wilayani Manyoni mkoani Singida na kueleza dhamira ya serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya kwa kuboresha na kujenga miundombinu.

Akizungumza katika ziara hiyo JAFO amesema uboreshaji wa kituo hicho unatarajia kugharimu kiasi cha Sh.Milioni 500 na kwamba tayari serikali imeshaingiza kiasi hicho cha fedha.

Jafo amesema uboreshaji huo utajumuisha ujenzi wa chumba cha upasuaji,chumba cha kuhifadhia maiti,wodi ya kisasa ya akina mama na maabara na kuwataka viongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha hadi desemba 30, mwaka huu ujenzi huo uwe umekamilika.

“Awamu ya kwanza zimeingizwa shilingi milioni 500 kwa ajili ya miundombinu na baada ya ujenzi kukamilika serikali itaweka vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 220,nataka ujenzi huu uende kwa kasi atakayeleta masihara atajuta,”alisema Jafo.

Amewataka watendaji kutimiza wajibu kwa kusimamia malighafi zitumike vizuri na mafundi wajenge majengo kwa ubora na kusisitiza kuwa mafundi wa kujenga majengo hayo watatoka wilayani humo.

Naibu Waziri Jafo amemtaka Mganga Mkuu wa wilaya Dk.Nelson Bukuna kuhakikisha anawajibika ipasavyo kwa kutembelea mara kwa mara kwenye zahanati na vituo vya afya badala ya kusubiri hadi kiongozi afike.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Miraji Mtaturu na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Charles Fussi wameahidi kuhakikisha wanatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na serikali na ujenzi wake utafanyika kwa viwango vinavyotakiwa.

Katika hatua nyingine, Jafo ametembelea mradi wa maji wa Kitinku na kumuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Manyoni Charles Fussi kuhakikisha anasimamia timu yake ili azma ya serikali ya kuhakikisha wanamtua ndoo mama ndoo ya maji kichani inafanikiwa kama Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)inavyosema.Jafo amesisitiza uaminifu na kufanya kazi kwa kasi ili wananchi wapate huduma ya maji wanayotarajia.

“Katika utekelazaji wa miradi hii wakandarasi wengi sio waaminifu,Mkurugenzi hii ni sehemu ya kupima performance yako,usilale hakikisha watu wanapata maji,”amesema Jafo.Kwa upande wake mhandisi wa maji wilaya Gasto Mbondo amesema mradi huo hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi bilioni 9.9 na utahudumia wananchi elfu 45,417 wa vijiji 11.

“Mradi huu unatekelezwa kwa awamu tano,na changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni upungufu wa wataalamu wa maji,ukosefu wa gari la kubebea mizigo ya maji na ukosefu wa fedha za kuendesha ofisi,”amesema Mbondo.Naye kaimu Mkuu wa wilaya hiyo, Miraji Mtaturu amepongeza na kumhakikishia Naibu waziri huyo kuwa atasimamia utekelezaji wa mradi huo na kwamba wilaya yake imeweka utaratibu wa kupokea taarifa kwa kina kuhusu miradi ya maji kila mwezi.

Kwa upande wake, Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Daniel Mtuka ameishukuru serikali kwa jitihada zake za kutatua kero ya maji katika jimbo hilo na kwamba kwa muda mrefu wananchi wake wamekuwa wakikabiliwa na changamoto hiyo.

MARIE STOPES TANZANIA YAZINDUA TENA HOSPITALI ILIYOBORESHWA NA KITUO CHA KUPOKEA SIMU ZA WATEJA MWENGE

$
0
0
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Hebogard Jensen (katikati) akikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali iliyoboreshwa ya Marie Stopes Mwenge leo jijini Dar es salaam. Hospitali hiyo pia imezindua kituo cha kupokea simu na pia kuanzisha huduma ya bure ya siku tatu kwa watakaopenda kupima magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, Ukimwi, ushauri wa masuala ya uzazi wa mpango, Kansa ya mlango wa kizazi huku huduma nyingine za kitabibu zikitolewa kwa gharama.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Hebogård Jensen akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa hospitali iliyoboreshwa ya Marie Stopes Mwenge leo jijini Dar es salaam. Hospitali hiyo pia imezindua kituo cha kupokea simu na kuanzisha huduma ya bure ya siku tatu kwa watakaopenda kupima magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, Ukimwi, ushauri wa masuala ya uzazi wa mpango, Kansa ya mlango wa kizazi huku huduma nyingine za kitabibu zikitolewa kwa gharama. Anayeshuhudia (kulia) ni Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay.
Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali iliyoboreshwa ya Marie Stopes Mwenge leo jijini Dar es salaam. Hospitali hiyo pia imezindua kituo cha kupokea simu na kuanzisha huduma ya bure ya siku tatu kwa watakaopenda kupima magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, Ukimwi, ushauri wa masuala ya uzazi wa mpango, Kansa ya mlango wa kizazi huku huduma nyingine za kitabibu zikitolewa kwa gharama. 
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Hebogard Jensen (katikati) akikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha kupokea simu cha Marie Stopes Mwenge leo jijini Dar es salaam.Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa marie Stopes Tanzania Anil Tambay na Mratibu wa huduma ya Afya ya Mzazi na Mtoto Edith Manase Mboga.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Hebogard Jensen (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa dawa za usingizi na ganzi, David Chiunga wakati wa uzinduzi wa hospitali iliyoboreshwa ya Maries Stopes Mwenge pamoja na kituo cha kupokea simu leo jijini Dar es salaam.
 
Marie Stopes Tanzania (MST) leo imeizindua upya hospitali yake iliyopo Mwenge inayopatikana kwenye kitalu namba 421 na 422 Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Hebogard Jensen ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliipongeza MST kwa kuonyesha juhudi za dhati za kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba wananchi wengi zaidi wanapata huduma za afya zilizo bora na bei nafuu.

“Nchini Tanzania, Marie Stopes inatambulika kwa utoaji wa huduma bora za afya ambazo wananchi wengi wanaweza kuzimudu, lakini kubwa zaidi ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za afya,” alisema Jensen.

Kuzinduliwa upya kwa hospitali hiyo ni matunda ya ushirikiano kati ya MST na DANIDA/ Ubalozi wa Denmark ambapo wameifanya hospitali hiyo kuwa miongoni mwa vituo bora vya afya kwa ajili ya uzazi wa mpango na huduma ya elimu ya afya ya uzazi.

Alisema ushirikiano wa DANIDA na Marie Stopes Tanzania utakuwa endelevu kwa manufaa ya Watanzania wote.“Tutaendelea kuwekeza kwenye jamii ambayo tunafanya kazi ili kusaidia kutekeleza miradi yetu mbalimbali ya afya, elimu na pamoja na vita ya kutokomeza umaskini,” alisema.

Jensen pia alizindua kituo cha mawasiliano cha ‘MST Contact Centre’ ambacho kitakuwa ni kitovu cha huduma ya kupiga simu bure kutoka kwa wateja na umma kiujumla ili kuimarisha mawasiliano na watoa huduma wa MST.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay alisema hospitali hiyo iliyozinduliwa upya itatoa huduma nzuri kwa wateja ikiwa pamoja na mazingira mazuri zaidi kwa wagonjwa.

Aliongeza kuwa huduma mbalimbali zinapatikana na kwenye vituo vya MST ikiwa ni pamoja na huduma ya afya ya uzazi inayotolewa mikoa yote ya Tanzania kupitia njia ya simu ya mkononi.

MST inafanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Tanzania kwa hatua zote ikiwa ni pamoja na kusaidia awamu ya nne ya Mpango Mkakati wa Afya wa HSSP-IV wa mwaka (2015-2020) ikiwa kama mshirika wa sekta binafsi (PPP).

Kwa fedha zinazopatikana kutoka DFID, DANIDA, USAID na wengine wengi, MST imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali na kutekeleza utoaji wa huduma ya uzazi wa mpango wa familia na afya ya uzazi, huduma ya baada ya mimba kuharibika (CPAC) pamoja na unyanyasi wa kijinsia (GBV), vipimo vya HIV, utoaji wa huduma ya uzazi wa mpango pamoja na uchunguzi wa Miradi hii imezingatia kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na uzazi kwa jamii zenye mahitaji nchini Tanzania.

Marie Stopes Tanzania imejikita katika kutoa huduma bora za afya ya uzazi na uzazi wa mpango ambazo zinapatikana karibu mikoa yote nchini Tanzania kupitia huduma zinazohamishika. Aidha, huduma za matibabu za jumla zinatolewa pia katika vituo vya afya vya MST. MST hufanya kazi kwa ukaribu sana na Serikali ya Tanzania katika ngazi zote, kusaidia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya - HSSP-IV (2015 - 2020), kama ushirikiano wa kibinafsi wa umma (PPP). Mnamo mwaka wa 2016, MST iliwapokea wateja milioni 7 na kutoa huduma ya uzazi kwa wateja zaidi ya milioni 2.1.
 

TEMBO ZAIDI YA LAKI MOJA WALIUWAWA KATIKA HIFADHI YA WANYAMA PORI SELOUS MKOANI RUVUMA.

$
0
0
Hayo yamebainishwa katika maadhimisho ya siku ya tembo kitaifa katika mji mdogo wa LUSEWA wilayani NAMTUMBO mkoani ruvuma katika pori la hifadhi ya wanyama pori SELOUS HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

BODI YA WADHAMINI YA TANAPA IKIONGOZWA NA MWENYEKITI WAKE JENERALI (MSTAAFU) WAITARA YATEMBELEA HIFADHI YA KATAVI

$
0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), na wajumbe wa bodi hiyo, wakikaribishwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Katavi, Mhifadhi Izumbe Msindai, walipowasili kwenye hifadhi hiyo leo Septemba 28, 2017.

BODI ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa bodi, Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara, leo Septemba 28, 2017 imetembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa ajili ya kukagua utendaji kazi ambapo ilipata fursa ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi Izumbe Msindai.

Bodi imepongeza utendaji kazi katika Hifadhi ya Katavi hususani suala zima la kupambana na ujangili na juhudi zinazofanywa katika kuongeza idadi ya watalii hifadhini.Aidha, Jenerali Waitara aliutaka uongozi wa hifadhi kuongeza jitihada katika kukabiliana na changamoto za mifugo ambayo ni kubwa kwa Katavi na pia alipongeza uongozi wa mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali mstaafu Raphael Muhuga kwa ushirikiano mkubwa anaotoa kwa hifadhi katika kupambana na mifugo hifadhini.

Mapema kabla, bodi iliweza kutembelea kituo cha mafunzo cha Mlele na kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Kituo Mhifadhi Genes Shayo na kupata nafasi ya kuongea na askari wapya wanaoendelea na mafunzo katika kituo hicho.

Jenerali Waitara aliwataka askari hao kuwa na nidhamu, uwajibikaji, bidii na uzalendo katika mafunzo yao na kuwa ni lazima waonyeshe kuiva ili waweze kupambana vilivyo na changamoto ya ujangili katika Hifadhi za Taifa nchini.
Jenerali Waitara, akionyesha kitu wakati yeye na wajumbe wa bodi walipotembelea enelo wanakohifadhiwa Viboko

Jenerali Waitara akizungumza na askari wanaopatiwa mafunzo kwenye kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi


Baadhi ya wajumbe wa bodi waliofiatana na Jenerali Waitara

Baadhi ya askari wanaopatiwa mafunzo ya ulinzi wa wanayamapori kwenye kituo cha mafunzo cha Mlele wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi za Taifa, (TANAPA), Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (hayupo pichani), alipowatembelea leo Septemba 28, 2017
Baadhi ya askari wanaopatiwa mafunzo ya ulinzi wa wanayamapori kwenye kituo cha mafunzo cha Mlele wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi za Taifa, (TANAPA), Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (hayupo pichani), alipowatembelea leo Septemba 28, 2017
Jenerali Mstaafu George Waitara, (kushoto) akipkewa na viongozi wa Hifadhi ya Taifa Katavi, alipowasili mapema leo.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images