Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1378 | 1379 | (Page 1380) | 1381 | 1382 | .... | 1897 | newer

  0 0

   
   Askari wa JWTZ wakibeba Jeneza la mwili wa marehemu Praiveti Mussa Jumanne Muryery tayari kwa safari ya kuelekea Dodoma kwa ajili ya mazishi. Mwili wa Marehemu uliagwa leo katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.


  0 0


  Majaji na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola wakimsikiliza Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi mkutano wa Majaji na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola ambao alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  Picha ya pamoja.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa Majaji na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam. 

  Katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais alipongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Chama cha Majaji na Mahakimu wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola (CMJA). Makamu wa Rais alisema” jitihada zenu katika kuendeleza na kuimarisha viwango na uhuru wa mahakama na vilevile kuendeleza utawala wa sheria vimeendelea kuimarika na kuifanya jumuiya yenu kuwa imara zaidi”. 

  Kwa miaka mingi mmeendelea kuchochea na kuimarisha uhuru wa mahakama huku mkijitahidi kuendeleza utawala wa sheria katika nchi za jumuiya ya madola, alisema Makamu wa Rais.

  Aidha, mkutano huo uliohudhuriwa na Majaji Wakuu wa Mahakama, majaji na mahakimu, Makamu wa Rais aliuasa mhimili wa Mahakama kuunga mkono jitihada za serikali katika mapambano ya kuondoa umaskini na rushwa ili kufikia maendeleo ya kweli. “Naamini kwamba nia ya kujenga mahakama yenye ufanisi, uwajibikaji na jumuishi haitafikiwa kama mahakama ya Tanzania itajitenga na jitihada za serikali za kuondoa umaskini na rushwa”, alisisitiza Makamu wa Rais.

  Pia Makamu wa Rais alisisitiza kuwa rushwa huondoa uhuru wa mahakama na hivyo kupoteza utawala wa sheria. Aliwataka washiriki wa mkutano huo kupambana na rushwa katika mahakama ili kuhakikisha haki na maendeleo vinapatikana. 

  Mwisho Makamu wa Rais aliwahakikishia washiriki wa mkutano huo kwamba serikali ya Tanzania itaendelea kuheshimu na kuimarisha uhuru wa Mahakama kwa kuhakikisha inaendelea kupambana na kuondoa vitendo vya rushwa. 

  Imetolewa na :-

  Ofisi ya Makamu wa Rais


  0 0

  Meneja wa huduma kwa wateja,Celine Njuju akionesha simu na vifaa vilivyopunguzwa bei katika maduka yote ya Airtel nchini, kulia ni Meneja mauzo wa bidhaa za mawasiliano Airtel Bw, Pascal Maziku. Ofa ya simu na vifaa hivyo vya mawasiliano pia inaambatana na ofa ya dakika za muda wa maongezi pamoja, bando la intaneti na SMS bila kikomo kwa miezi sita

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetoa rai kwa wateja kuhakikisha wananunua bidhaa bora zinazopatikana kwenye maduka yake kwani imetoa punguzo kubwa ya bei kwa bidhaa hizo.

  Haya yamesemwa na Meneja wa Huduma kwa wateja Celina Njuju huku akithibitisha kuwa bidhaa hizo zitakuwa zikipatikana kwenye maduka yote ya Airtel na hivyo kuwashauri wateja kuhahakisha kuwa wanatumia nafasi hiyo kujipatia bidhaa bora kwa punguzo la bei.
   ‘Tunataka wateja wafaidi fedha zao, siku zimepita ambapo Watanzania walikuwa wanaenda madukani na kununua bidhaa feki kwani kwa sasa tunazo bidhaa halisi kabisa ambazo zinapatikana kwa bei nafuu, alisema Njuju.
  Kulingana na Njuju, Wingle USB Modem ambayo hapo awali ilikuwa ikipatikana kwa Tshs60,000 kwa sasa itakuwa ikipatikana kwa Tshs45,000 pamoja na kifurushi cha intaneti cha bure cha 5GB. Uzuri wa hii modem ni kwamba unaweza ukatumiwa na watu mpaka kumi kwa wakati mmoja, alisema Njuju huku akiongeza ya kwamba modem hii inafaa sana kwa watu wanaofanya kazi maofisini, wafanya biashara na wanafunzi.

  Kampuni ya Airtel Tanzania pia imetoa punguzo la bei kwa Magnus Bravo Z11 ambapo hapo awali ilikuwa inauzwa Tshs79,000 lakini kwa sasa ni Tshs69,000 ambapo pia itakuwa na kifurushi cha bure cha 12GB, dakika 300 kupiga mitandao yote na sms 300 kwa muda wa miezi sita. Pia kwenye punguzo ni simu ya Huawei Y3C ambapo hapo awali ilikuwa ikipatikana kwa Tshs140,000 na kwa sasa itakuwa inauzwa Tshs100,000 na itakuwa na kifurushi cha 12GB, dakika 300 kupiga mitandao yote na sms 300 kwa muda wa miezi sita.

  Wateja pia watajipatia simu aina ya FERO 280 kwa Tshs30,000 kutoka bei ya awali ya Tshs38,000 ambapo itakuja na 150MB, dakika 150 kupiga Airtel kwenda Airtel na sms 150 kwa muda wa miezi mitatu.
   ‘Natoa wito kwa wateja wa Airtel kujitokeza na kufaidika na punguzo la bei ya bidhaa hizi kwenye maduka yote ya Airtel nchi nzima kwani muda wa punguzo ni mdogo, alisema Njuju.

  0 0


  Na John Stephen, Muhimbili

  Dar es Salaam, Tanzania. Serikali imesema itaendelea kuiwezesha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) katika mikakati yake ya kutoa huduma bora za afya zikiwamo za ubingwa wa hali ya juu pamoja na upasuaji katika maeneo mbalimbali.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katika hospitali hiyo wakati akizindua vyumba viwili vya upasuaji wa watoto wadogo (Pediatrick operating theatres) vyenye thamani ya Dola za Marekani 675,000 sawa na Tsh. 1.5 bilioni pamoja na uzinduzi wa wodi ya watoto yenye vitanda 25.

  Katika uzinduzi huo Waziri Mwalimu ameitaka Muhimbili kutokutoa rufaa kwa mgonjwa yoyote ambaye anaweza kupatiwa mabatibabu katika hospitali hiyo.

  “Narudia tena, hata kama ni mimi au kiongozi yoyote asipewe rufaa kama ugonjwa wake unaweza kutibiwa hapa, mimi naweza kuja hapa nikawashinikiza mnipeleke nje, msikubali, simamieni taaluma yenu. Kama madaktari wamezibitisha mgonjwa anaweza kutibiwa hapa, hakuna haja ya kupelekwa nje,” Mhe. Ummy.

  Vyumba hivyo vya upasuaji vimewekewa vifaa vya upasuaji kwa msaada wa mfuko wa ARCHIE WOOD FOUNDATION ya Scotland. “Napenda kuwashukuru kwa namna ya pekee wahisani wetu Sir.Ian Wood na mtoto wako Garret Wood ambao mlipoletewa wazo la kuisaidia Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia taasisi yenu ya Archie Wood Foundation mlilipokea kwa mikono miwili na kulitekeleza. Nichukue nafasi hii kwa niaba ya Serikali chini ya Uongozi wa wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwashukuru sana kwa msaada huu,” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

  Waziri ameutaka uongozi wa Muhimbili kuweka mpango mzuri wa matengenezo kinga ili kuhakikisha kila kifaa kinatunzwa na kutumika kwa lengo lililokusudiwa.

  Naye Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amefafanua kuwa msaada uliotolewa na mfuko huo kuwa ni taa za kufanyia upasuaji (operating lights), mashine za usingizi (anesthetic machines with monitors), mashine za kuzuia damu isiendelee kupotea wakati wa upasuaji (diathermy machines), mashine ya kutasisha vifaa vya upasuaji na vifaa vyake, vitanda vya kufanyia upasuaji (operating tables) na vifaa mbalimbali vya upasuaji (surgical kits).

  Profesa Museru amesema kuwa leo wamepatiwa vifaa vya kisasa kwa kutumia vyumba hivyo viwili na kwamba upasuaji utakuwa ikifanyika mara 10 kwa wiki badala ya mara tatu kwa wiki kama ilivyokuwa awali.

  “Hii itaondoa kero ya msongamano kwa watoto wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wakati mwingine ilibidi wasubiri kwa muda wa miaka miwili ili kufanyiwa upasuaji,”amesema Profesa Museru.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akizindua vyumba viwili vya upasuaji wa watoto wadogo leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Wood na Archie, Sir. Ian Wood na maofisa wengine wakiwa kwenye uzinduzi huo leo.
    Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiangalia baadhi ya vifaa vilivyotolewa na Mfuko wa Wood na Archie katika vyumba vya upasuaji wa watoto wadogo kwenye hospitali hiyo.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza kabla ya kuzindua vyumba vya upasuaji wa watoto. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dk. Julieth Magandi na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wood na Archie, Ian Wood akiwa kwenye mkutano huo leo.
   Baadhi ya watoto wanaotibiwa katika hospitali hiyo wakiwamo madaktari, wauguzi na baadhi ya watumishi wakimsikiliza Waziri Ummy Mwalimu leo.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akizungumza leo kwenye mkutano huo kabla ya kuzinduliwa kwa vyumba vya upasuaji wa watoto.
    Baadhi ya watumishi wa Muhimbili wakifuatilia mkutano huo leo
   Profesa George Youngson akizungumza kwenye mkutano huo leo kabla ya kukabidhi vyumba vya upasuaji na wodi ya watoto yenye vitanda 25.  Pembeni ni timu ya wataalamu wa Wood na Archie Foundation.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Wood na Archie, Sir. Ian Wood akizungumza katika mkutano huo leo.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha akiwa na mmoja wa watoto ambaye amemweleza Waziri Ummy Mwalimu kwamba ndoto yake ni kuwa daktari. Waziri ameahidi kumsomesha mtoto ili kufikia ndoto yake.

  0 0

  Na Kajunason/MMG-Handeni-Tanga. 

  Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Godwe amekabidhi ardhi yenye ukubwa wa hekari 282 katika kijiji cha Kitumbi kwa wasanii na wadau wengine wanaofanya kampeni ya UZALENDO KWANZA. 

  Akizungumza wakati akikabidhi ardhi hiyo katika kijiji cha Kitumbi, Handeni mkoani Tanga, alisema kuwa hatua hiyo inalenga kukuza kilimo na maendeleo katika kijiji hicho ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Dkt. John Pombe Magufuli kuendeleza nchi ya viwanda na biashara. Wadau wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza wakiwemo wasanii wa filamu, muziki na wachezaji mpira wa zamani wameamua kushiriki katika maendeleo ya taifa kwa kujihusisha na kilimo tofauti na kazi zao za kila siku za sanaa. 

   "Handeni ni sehemu ambayo korosho, alizeti, ndizi vinakuwa sana na niwaambie tu mapema mwakani kiwanda kutengeneza juisi ya nanasi kinafunguliwa Kwa Msisi, tena kitakuwa na uwezo wa kuchukua tani 80,000 za nanasi kwa mwaka na kitakuwa cha pili Afrika kwa kuzalisha juisi ya nanasi, hapo kazi kwenu kuchangamkia fursa," Alisema Mhe. Gondwe. 

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, msanii Steve Nyerere alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Gondwe na vingozi wa kijiji kwa kuwapa eneo la kuwekeza katika sekta ya kilimo. 

   "Sisi tunawashukuru wote kwa moyo mliotuonyesha, hatuna cha kuwalipa bali tutapambana kwa nguvu zetu ili kutimiza malengo ya eneo mlilotupa, Uzalendo Kwanza Oyeeee!," alisema Msanii Steve Nyerere. Nae diwani wa Kata ya Kitumbi, Charles Abeid amewakaribisha wasanii hao kwa mikono miwili na kuwaomba wawasaidie kumalizia ujenzi wa zahanati yao ambao umekuwa ukisua sua kutokana na kukosekana kwa fedha.
  UZALENDO KWANZA wakiongozwa na mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Gondwe wakielekea katika kijiji cha Kitumbi wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga, ambapo walipatiwa Mashamba yenye ukubwa wa hekari 282 za ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa Kilimo. Picha zote na Kajunason/MMG-Handeni.
  Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Godwe akiongea mara baada ya kuwakabidhi ardhi yenye ukubwa wa hekari 282 katika kijiji cha kitumbi kwa wasanii na wadau wengine wanaofanya kampeni ya UZALENDO KWANZA. Tukio hilo lilifanyika kijijini Kitumbi, Muheza - Tanga mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Msanii Steve Nyerere akitoa shukrani zake za pekee kwa mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Gondwe mara baada ya kuwakaribisha wana- UZALENDO KWANZA na kuwapatia hekari 282 za ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo katika kijiji cha Kitumbi wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga.
  Diwani wa Kata ya Kitumbi, Charles Abeid akiwakaribisha wasanii na wadau wengine wanaofanya kampeni ya UZALENDO KWANZA.
  Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Gondwe akiwatambulisha viongozi wa kijiji cha Kitumbi, Handeni -Tanga.
  Eneo ambalo wasanii na wadau wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza wamepewa kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya kilimo.

  0 0

   Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kulia) akimkabidhi funguo ya Pikipiki Kiongozi wa Kundi la Ngoma la Kannengwa Rungwe, Nolbert Mwandinga, baada ya kundi lake kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Ingoma Kituli, wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Katika Tamasha hilo jumla ya washindi 10 wa kwanza kutoka kila kundi walizawadiwa Pikipiki.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akicheza ngoma ya asili ya kundi la  Banyampulo ya kabila la Wanyakyusa, wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Katika Tamasha hilo jumla ya washindi 10 wa kwanza kutoka kila kundi walizawadiwa Pikipiki.
   Wacheza Bao Gabriel Mwasankinga wa timu ya CCM (kushoto) akichuana na Pascal Mbwelembweta wa timu ya Kawechele, kutafuta mshindi wa tatu katika mchezo wa fainali za mchezo huo kuadhimisha Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
   Wacheza Bao Kocha Lufingo wa timu ya Stendi Kuu (kushoto) akichuana na Six Willson wa timu ya Soko Kuu, kutafuta mshindi wa kwanza na wapili katika mchezo wa fainali za mchezo huo kuadhimisha Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.


  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akipokea michango ya hela kutoka kwa wananchi wa Tukuyu kwa ajili ya harambee ya kuichangia timu ya Tukuyu Stars ''Changia Tukuyu Stars irudi Ligi Kuu'' wakati wa  Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Katika Tamasha hilo jumla ya washindi 10 wa kwanza kutoka kila kundi walizawadiwa Pikipiki. Picha na Muhidin Sufiani

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya soka ya Vodacom 2017/18 wenye thamani ya shilingi 325,000,000 uliotolewa na benki ya KCB Tanzania kwa Shirikisho la Soka Tanzania TFF.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Zuhura Muro akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla hiyo.
   Raisi wa Shirikiso la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia akiishukuru benki ya KCB Tanzania kwa udhamini huo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario (aliyekaa Kulia) na Raisi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia (aliyekaa kushoto)wakisaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya soka ya Vodacom 2017/18 wenye thamani ya shilingi 325,000,000 uliotolewa na benki ya KCB Tanzania kwa TFF.Pamoja nao wakishuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Zuhura Muro (aliyesimama kulia), Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura (aliyesimama katikati) na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao (aliyesimama kushoto). 

   Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario (Katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Zuhura Muro (wapili kulia) wakikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 325,000,000 kwa Raisi wa Shirikiso la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia (wapili kushoto), ikiwa ni udhamini kwa ajili ya ligi kuu ya soka ya Vodacom 2017/18. Pamoja nao kwenye picha ni Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura (wakwanza Kulia) na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao (wakwanza kushoto).

    

  Benki ya KCB Tanzania leo imetangaza rasmi udhamini mwenza wa ligi ya soka ya TFF Vodacom 2017/18 wenye thamani ya shilingi za kitanzania 325,000,000. Mkataba wa makubaliano hayo ulisainiwa rasmi leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario na Raisi WA TFF Wallace Karia.

  Hafla hiyo ya makubaliano ilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya KCB Tanzania, Bi, Zuhura Muro, Mwenyekiti wa bodi ya Udhamini TFF, Mhe, Mohammed Abdulaziz, Wakurugenzi wa Bodi ya KCB Tanzania, Wafanyakazi Benki ya KCB Tanzania, wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya soka na waandishi wa habari.

  Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario alisema kuwa udhamini huo upo ndani ya vipaumbele vya benki kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo. “Sekta ya michezo ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na pia ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi nchini, hivyo benki ya KCB imechukua uamuzi huu kujiunga na TFF kukuza mchezo wa mpira wa miguu” alisema Kimario.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania Zuhuru Muro alisema kuwa “Benki ya KCB Tanzania tunajivunia kuwa sehemu ya ligi hii na tunaamini kuwa udhamini wetu utachangia kuleta hamasa kubwa kwa wapenzi wa mpira wa miguu na kukuza vipaji vya vijana.” Alieleza kuwa udhamini huo utakuwa chachu ya maendeleo kwa benki, wateja wake, TFF, wachezaji, mashabiki na wananchi kwa ujumla.

  Rais wa TFF aliishukuru benki ya KCB kwa kuidhamini Ligi kuu Vodacom jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2017/18. Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa Pole, Bi. Maudia Abdaallah ambaye ni Mjane wa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Ruangwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya ya Ruangwa, Marehemu Selemani Bakari wakati alipokwenda kuhani msiba huo, Majohe, Ilala jijini Dar es salam Septemba 25, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  PMO 9669 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji katika msiba wa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Ruangwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ruangwa , Marehemu Selemani Bakari wakati alipokwenda Majohe wilayani Ilala jijini Dar es salaam kuhani msiba huo, Septemba 25, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Jonas Kamaleki- MAELEZO

  The Vice President of the United Republic of Tanzania, H.E. Samia Suluhu Hassan has urged the Judiciary to be independent, accountable and effective in order to come up with a foundation of a democratic system.

  She made this remark while officiating at the opening of the Commonwealth Magistrates and Judges Association Conference held in Dar es Salaam today.

  H.E. Samia said that the expectations of the people to the judiciary may at times be overwhelming given the capability challenges

  “Regardless of these challenges and independent, effective and accountable judiciary needs to be in place to ensure the adherence of the rule of law, equal access to justice, security of livelihoods of all and peoples’ participation in peaceful governance of their countries,” said Samia.

  Vice President said that she was glad that Magistrates and Judges had taken upon themselves the leading role to ensure effective judiciary was in place by including such topics perennial complaints of our people on issues regarding to delays, financial and procedural constraints on access to justice which threaten loss of trust and confidence in Judiciary, in the program.

  She further said the Government of Tanzania has played its safeguarding role by enacting the Judiciary Administration Act, 2011 which established Judiciary Fund, designed to fund the disposal of cases. Despite all those efforts, in developing countries like Tanzania, funding was not always sufficient to cover all requirements of the Judiciary, she added.

  H.E. Samia said that according to Tanzania’s Vision 2025, the country is supposed to graduate from its current position as one of the Least Developed Countries, to a middle income country enjoying a high level of human development. According to the Vice President, that graduation has to be undertaken by all arms including the Judiciary, which is implementing its 2015/2016-2019-20 Strategic plan.

  Meanwhile, The Chief Justice of the United Republic of Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma said that accountability, effectiveness and efficiency of the Judiciary in Tanzania has improved significantly where judicial officers were freed from day to day administrative functions.

  He added that the Judiciary of Tanzania realized its vision of separation of judicial functions from purely administrative function following the enactment of the Judiciary Administrative Act, 2011.

  On court buildings, the Chief Justice said in the Strategic Planning and Citizen-Centric Judiciary Modernisation and Justice Service Delivery Project funded by the World Bank, the Judiciary of Tanzania had adopted MOLADI TECHNOLOGY to fast track construction of court buildings.

  “I confidently proclaim that by 2020 the Judiciary would have constructed 48 Districts courts, 100 Primary courts, 14 Resident Magistrates courts and a Judiciary Head-quarter (Judiciary Square),”said Prof. Ibrahim.

  This is the Second Commonwealth Magistrates and Judges Association Conference to be held in Africa while it is the first one to take place in Tanzania. The 5 days Conference has attracted 13 Chief Justices from Commonwealth countries and dozens of Judges and Magistrates.

  0 0


  Msanii Ommy Dimpoz akipamtia zawadi ya pesa taslimu ya shilingi 50,000/-mwanafunzi bora wa kidato cha sita wa shule ya sekondari Nganza jijini Mwanza, Glory Wilfred wakati wasanii wa Tigo Fiesta walipotembelea shule hiyo juzi kwenye programu ya kuelimisha wanafunzi msimu huu wa Tigo Fiesta ijulikanayo kama ‘Kipepeo’.
  Msanii Alli Kiba akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Nganza iliyopo Mwanza juzi kwenye programu ya kuelimisha wanafunzi msimu huu wa Tigo Fiesta ijulikanayo kama ‘Kipepeo’.
  Wasanii wakiwa wamesimama kusali pamoja na wanafunzi wa shule ya Nganza, maombi yaliyoombwa na mmoja kati ya wanafunzi wa shule hiyo(hayupo pichani).
  Msanii Alli Kiba akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Nganza iliyopo Mwanza juzi kwenye programu ya kuelimisha wanafunzi msimu huu wa Tigo Fiesta ijulikanayo kama ‘Kipepeo’.
  Msanii Ray Vanny akisalimiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Nganza jijini Mwanza mara baada ya kumaliza programu ya Kipepeo.
  Msanii Roma Mkatoliki akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Nganza iliyopo Mwanza juzi kwenye programu ya kuelimisha wanafunzi msimu huu wa Tigo Fiesta ijulikanayo kama ‘Kipepeo’.

  Msanii Saida Karoli akiwapungia mikono kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nganza .
  Msanii Ray Vanny akipiga picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Nganza .

  Sehemu ya wanafunzi wakifuatilia progamu ya Kipepeo.

  Wasanii wakiwa wamesimama kusali pamoja na wanafunzi wa shule ya Nganza, maombi yaliyoombwa na mmoja kati ya wanafunzi wa shule hiyo(hayupo pichani)
  Wasanii wakiondoka mara ya kumaliza programu yao ya kuelimisha wanafunzi jinsi ya kujitambua maishani , wakati wa shule na baada ya shule.

  0 0

  Kama ulipitwa na matukio ya wiki nzima yaliyojili mkoani Ruvuma na nje ya mkoa wa Ruvuma kuanzia Sep 18 hadi Sep 24, 2017 basi usipate tabu tumekusogezea , Matukio ni haya hapa kazi yako ni kubonyeza hii video uweze kuyafahamu na kuyatazama.

  0 0

  Home Gym Mwenge yafikisha miaka 19 kwa kishindo. Weekend iliyopita ilishuhudia Home Gym Mwenge moja ya Gym maarufu ya mazoezi ya viungo jijini Dar es salaam ikitimiza miaka 19 yangu ianzishwe. 
  Sherehe hizo zilifanyika kwenye viwanja vya Shule ya wanasheria jijini na kuhudhuriwa na Mamia ya watu. Akiongea wakati wa sherehe hizo mwanzilishi na mmiliki wa Gym hiyo Andrew Mango alishukuru wanachama wa Gym hiyo na Wadhamini. 
  Pia aliwataka wakazi wa Dar es salaam kupenda kufanya mazoezi ili kujenga afya bora.

  0 0

  NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara ya kukagua miundombinu katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na kuahidi kuwa serikali itafanya ukarabati wa baadhi ya majengo haraka iwezekanavyo.

  Akizungumza mara baada ya kukagua miundombinu ya hospitali leo mjini Dodoma, Jafo amesema hospitali hiyo ndio kimbilio la watu wengi na kwamba baadhi ya majengo yake yanahitaji kufanyiwa maboresho ili yaendane na hadhi ya Makao makuu ya Nchi.

  Amesema majengo hayo yamejengwa tangu enzi za Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ni ya zamani hivyo yanatakiwa kufanyiwa maboresho ili yawe ya kisasa na kwamba serikali inajipanga kufanya maboresho hayo na kwa kuanzia itapeleka Sh.milioni 500 kuanza ukarabati katika jengo la upasuaji.

  Ameeleza jengo la upasuaji ni la muda mrefu na miundombinu yake kwa ndani haiendani na hali ya sasa na kwamba inatakiwa kukarabatiwa ili iwe ya kisasa.“Serikali tutaleta fedha ili tukarabati jengo hili liendane na hali halisi ya mahitaji hasa ikizingatiwa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi hivyo ni kimbilio la watu wengi,”amesema Jafo

  Aidha amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa Dk.Charles Kiologwe na uongozi wa hospitali hiyo kuanza mchakato wa kuwasilisha maombi serikalini kwa ajili ya kuboresha majengo ya hospitali hiyo ambayo asilimia kubwa yalijengwa wakati Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

  Kadhalika, amepongeza ujenzi wa jengo jipya la kisasa la akina mama na watoto na kuagiza ujenzi wake ukamilishwe kabla ya mwisho wa mwezi wa oktoba mwaka huu kwa kuwa serikali imeshapeleka fedha za ukamilishaji.

  Aidha amepongeza ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Bima ya Afya na kwamba linapokea wagonjwa wengi kwa siku kutokana na ubora wa miundombinu yake.Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Caroline Damian amesema jengo hilo limekuwa likitumika kufanya upasuaji kwa wastani wa watu 500 kwa wiki.

  Naye, Mganga Mkuu Dk. Kiologwe amesema miundombinu ya hospitali hiyo ilijengwa mwaka 1929 na kwamba licha ya changamoto ya miundombinu lakini huduma za afya zimekuwa zikitolewa kwa ufanisi.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali wa serikali katika ukaguzi wa jengo la Akinamama na watoto katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua miundombinu ndani ya jengo la upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.Charles Kiologwe akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipokuwa akikagua chumba cha kufulia nguo za Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa wakandarasi wa ujenzi wa jengo la Akinamama na watoto alipofanya ziara ya kukagua miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.

  0 0

  Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, Bw. Hiiti Sillo akitoa maelezo ya utangulizi kwa washiriki.
  Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto , Dkt. Ulisubisya Mpoki akisisitiza jambo katika hotuba yake ya ufunguzi.
  Picha ya pamoja baina ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto , Dkt. Ulisubisya Mpoki (wa tatu kushoto, msitari wa mbele), akiwa na waratibu, na washiriki wa mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Sekeretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wameshiriki katika uratibu wa mafunzo hayo na kutoa misaada ya hali na mali.


  Serikali imesisitiza umuhimu wa mafunzo zaidi kwa wataalamu wa ukaguzi na udhibiti ili kuhakikisha dawa zinazoingizwa na kutengenezwa nchini zina ubora kwa kuzingatia viwango na vigezo vilivyowekwa.

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Ulisubisya Mpoki amesema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazozikabili nchi nyingi barani Afrika katika kuwapatia wananchi wake huduma bora za afya ni ukosefu wa wataalamu wa kutosha wa ukaguzi wa dawa hivyo mafunzo ya wataalamu hao hayana budi kupewa kipaumbele.

  “Tanzania tunaagiza asilimia themanini ya mahitaji yetu ya dawa na kutengeneza kiasi kilichobaki hivyo suala la weledi katika ukaguzi na udhibiti wa dawa ni jambo linalopaswa kupewa umuhimu mkubwa” Dk. Mpoki alisema.

  Katibu Mkuu huyo amesema hayo leo wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku tisa ya ulinganishaji wa viwango vya dawa kwa wakaguzi na wataalamu wa udhibiti wa dawa kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika kituo Mahsusi cha Kanda cha Ukaguzi na Udhibiti wa Dawa kwa Afrika Mashariki kilichopo Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi ya Afya, Muhimbili.

  Kwa hivyo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia kwa makini mafunzo hayo kwa kuwa yatawaongezea uwezo wa kuhakikisha dawa zinazotumiwa wananchi wa nchi zao ni zenye ubora na salama.

  “Tumieni fursa ya mafunzo haya kuhakikisha mnapata ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kufanya maamuzi sahihi katika kuamua ubora wa dawa katika nchi zenu” Dk. Mpoki alisisitiza.

  Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa kituo hicho ni hatua muhimu ya kukabiliana na changamoto hiyo na kueleza utayari na dhamira ya Serikali ya kuendelea kukiunga mkono kituo hicho ili kiweze kutimiza majukumu yake.

  Wakati huo huo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo amesema lengo la kituo hicho ni kufundisha wataalamu wengi zaidi kutosheleza mahitaji ya nchi wanachama ili kuhakikisha kazi ya ukaguzi na udhibiti wa ubora wa dawa unaimarika katika nchi hizo.

  Alifafanua kuwa katika Programu ya Ulinganishi wa Dawa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, TFDA ndio taasisi kiongozi wa kuratibu na kusajili dawa.Aliongeza kuwa uamuzi wa TFDA kupewa dhamana hiyo unatolaka na uwezo wa kitaalamu na miundombinu iliyopo nchini katika kutekeleza jukumu hilo.

  Mkurugenzi Mkuu huyo alibainisha kuwa kituo hicho ambacho kilianzsihwa mwaka 2014 na kuanza shughuli zake mwaka 2015 na kinaendeshwa kwa pamoja kati Jumuiya ya Afrika Mashariki, TFDA na Shule ya Phamasi ya Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akishiriki kazi ya uzalishaji chaki wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea Kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki cha Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akikagua kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki cha Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi wakati wa ziara ya kikazi 
  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimkabidhi boksi tano za chaki Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi mara baada ya kutembelea na kukagua kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki
  cha Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi wakati wa ziara ya kikazi
  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akishiriki kazi ya uzalishaji chaki wakati wa ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi kutembelea Kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji
  chaki cha Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akisalimiana na Meneja wa kiwanda cha Uzalishaji chaki cha Dober Color Ndg Mukhtar Mahamood mara baada ya kuwasili kiwandani hapo
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akikagua mizinga ya nyuki mara baada ya kutembele kiwanda Uzalishaji chaki, Mafuta ya Alizeti na Asali cha Fahari Kilichopo katika eneo la
  Tambukareli Halmashauri ya Mji wa Itigi wakati wa ziara ya kikazi, Kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
  Ukaguzi wa kiwanda cha uzalishaji Chaki
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akikagua eneo la kutunzia Unga wa Gypusm katika kiwanda cha uzalishaji Gypsum cha Sanjaranda, Halmashauri ya Itigi
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akizungumza kwa njia ya simu na mmiliki wa kiwanda cha uzalishaji unga wa Gypsum cha Sanjaranda Bw Rashid Said Rashid akiwa Dar es salaam ambaye alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa mpaka kufikia Januari 2018 uzalishaji wa Gypsum utaanza katika eneo la Sanjaranda, Halmashauri ya Itigi ili kurahisisha huduma hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akiwa kwenye shamba la Mkulima Juma Patrick na kujionea mikorosho inavyoharibika kwa kukosa dawa ambapo alizungumza kwa njia ya simu na muwakilishi wa Bodi ya Korosho akiwa Dar es salaam ambaye alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa dawa za kuua wadudu kwenye Mikorosho zitawasili kati ya Jumanne Septemba 26 na Jumatano 27, 2017
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akionyesha chaki bora zinazozalishwa Wilayani Manyoni Mkoani Singida
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi Mhe Ally Minja mara baada ya kuwasili Kwa ajili ya kutembelea Kiwanda vya usagaji unga wa Gypsum na uzalishaji chaki.
  Miongoni wafanyakazi wa kiwanda cha Uzalishaji chaki cha Dober Color wakiendelea na kazi wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi 

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigallla King (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kizengi (hawapo pichani) kilichopo kata ya Kizengi wilaya ya Uyui mkoani Tabora baada ya kukagua ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini wakati wa ziara ya Kamati hiyo. 
  Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Eng. Peter Ulanga(aliyesimama mbele) akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini kwenye kijiji cha Mayamaya kilichopo Kata ya Zanka wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
  Meneja wa Kampuni ya Simu ya TTCL Mkoa wa Tabora Bwana James Mlaguzi (wa kwanza kulia) akitoa taarifa kwa wajumbe wa Kamati hiyo wakati wa ziara yao ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano viijini kwenye kijiji cha Kizengi kilichopo kata ya Kizengi wilaya ya Uyui mkoani Tabora.
  Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Mussa Ntimizi akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Kizengi kilichopo kata ya Kizengi wilaya ya Uyui mkoani Tabora wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini.

  …………………

  Kamati ya Miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania inaendelea na ziara ya kukagua ujenzi wa minara ya simu, ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini na kwenye maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata na kutumia huduma za mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali nchini. Kamti hiyo imeendelea na ziara yake kwenye mikoa ya Dodoma na Tabora ili kujiridhisha na utendaji kazi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wa kufikisha mawasiliano kwa wananchi.

  Katika ziara hiyo, Mtendaji Mkuu wa UCSAF Eng. Peter Ulanga amesema kuwa Mfuko umetoa ruzuku kwa Kampuni ya simu ya TIGO kujenga mnara ili kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi. Mfuko umetumia zaidi ya dola za marekani elfu arobaini na moja na mia tano (41,500) ambapo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 85 kuipatia kampuni ya TIGO kujenga mnara ambao sasa unahudumia zaidi wa wakazi 4,000 wa kijiji cha Mayamaya na vijiji vingine vya kata ya Zanka wilaya ya Bahi mkoani Dodoma ambapo walikuwa hawana huduma za mawasiliano na sasa wananufaika na uwepo wa huu mnara na wanapata huduma za mawasiliano. Mnara huu ulikamilika mwezi Machi mwaka jana na kuanza kutoa huduma ya mawasiiano kwa wananchi.

  Naye mwakilishi wa kampuni ya simu ya TIGO mkoa wa Dodoma mhandisi Hassan Said Gimbo wa kampuni hiyo amewaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu waliofanya ziara ya kukagua ujenzi wa minara, ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano kuwa kampuni yao imekamilisha ujenzi wa mnara na sasa unatoa mawasiliano kwa wananchi. Pia ameongeza kuwa kampuni ya TIGO inafuatilia mara kwa mara kwenye eneo hilo na kuhakikisha kuwa mawasiliano yanapatikana. “Tunajitahidi kwa kiasi kikubwa kukarabati na kuhakikisha kuwa pale mawasiliano yanapopotea au kuwa hafifu tunafanya haraka kuyarudisha”, amesema mhandisi Gimbo.

  Naye Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu akizungumza kwa niaba ya Kamati hiyo Mhe. Mussa Ntimizi ameipongeza Serikali kwa kutoa ruzuku kwa kampuni za simu za mkononi kupitia UCSAF ili kufikisha huduma za mawasiliano vijijini. Mhe. Ntimizi ameongeza kuwa kwa sisi wawakilishi wa wananchi tunaotoka vijijini tunaelewa mahitaji na kiu ya wananchi ya kupata mawasiliano kwenye makazi yao na umuhimu wa huduma nyingine za mawasiliano. “Ukiangalia eneo kama hili halivutii kibiashara hivyo sio rahisi kwa kampuni za simu kama hii ya TIGO kuja kuweka mnara wa simu hapa” amesema Mhe. Ntimizi.

  Tumepata taarifa kuwa zaidi ya vijiji vitano vyenye wakazi zaidi ya watu 4,000 wanapata mawasiliano kupitia mnara huu wa TIGO. “Kwa wananchi zaidi ya 4,000 kukosa mawasiliano sio kitu kidogo na Mfuko huu unafanya kazi kubwa ya kufikisha mawasiliano vijijini na Serikali inatumia gharama kubwa kujenga minara ya simu za mkononi na kutoa huduma za mawasiliano vijjijini, hivyo wahakikishe kuwa huduma za mawasiliano zinapatikana muda wote”, amesema Mhe. Ntimizi.

  Pia, ametoa rai kwa kampuni za simu nchini kuboresha na kukarabati miundombinu ya mawasiliano na minara yao ili wananchi waendelee kupata mawasiliano muda wote kwa kuwa serikali inatoa fedha nyingi kwa maana ya ruzuku na kuwapatia kampuni za simu ili ziweze kufikisha huduma za mawasiliano kwa wanachi muda wote.

  Amesema kuwa huduma hizi zina gharama kubwa sana na wananchi hawajui gharama kubwa ambayo Serikali imeingia kutengeneza mnara huu ambazo ni kodi zao na hawaoni thamani ya Serikali kuwaletea huduma hii. Wananchi muendelee kulinda miundombinu ya mawasiliano na kusiwepo na wizi wa mafuta ya dizeli, mitambo na vitu vingine kwa kuwa Serikali inatumia gharama kubwa kufikisha huduma za mawasiliano vijijini ambapo ujenzi wa mnara mmoja unagharimu zaidi ya shilingi milioni 200, hivyo kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake ili kulinda miundombinu hii ya mawasiliano.

  Tunaipongeza Serikali kwa kujenga mnara kwenye kijiji chetu kwa kuwa tunapata mawasiliano na pale yanapokuwa hayapatikani yanakatika wataalamu wa kampuni ya TIGO wanafika na kurekebisha hali hii, “hakuna mawasiliano ya kampuni nyingine yoyote zaidi ya hii ya TIGO kwenye eneo hili”, amesema mkazi wa kijiji cha Mayamaya, Bwana Emmanuel Konyanza kilichopo kata ya Zanka wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.

  Katika ziara hiyo ya Kamati kwenye kijiji cha Kizengi kata ya Kizengi iliyopo wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Meneja wa TTCL mkoa wa Tabora Bwana James Mlaguzi ameihaidi Kamati hiyo kuwa wataongeza upana wa masafa ya TTCL ili yaweze kufika kwenye vijiji vya mbali zaidi kwenye kata ya Kizengi ndani ya kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa. Naye Diwani wa Kata hiyo Bwana Magindika Lugaira Masaga akizungumza kwa niaba ya wananchi mbele ya wajumbe wa Kamati hiyo amesema kuwa hapo mwanzo wananchi walikuwa na shida kubwa ya mawasiliano. 

  Bwana Masaga anawashukuru wajumbe wa Kamati hiyo kufanya ziara na wanategemea kuwa huduma za mawasiliano zitaongezeka na kuwa bora zaidi kwa kuwa mawasiliano ya minara ya kampuni nyingine sio mazuri sana bali wanategemea mnara wa Halotel pekee ambao una masafa marefu na kufikia wananchi walio wengi zaidi. hivyo mnara wa TTCL ukikamilika utasaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi wa kata hii yenye vijiji saba na wakazi 23,534.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0  0 0


  Na Mwashumgi Tahir     Maelezo Zanzibar 
  SERIKALI ya  Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya Zanzibar imewahakikishia wananchi kuwa Bohari kuu ya Dawa inadawa za kutosha za kuhudumia wagonjwa wanaofika kupata matibabu katika Mahospitali na vituo vya Afya.
  Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman wakati alipofanya ziara katika Bohari kuu ya Dawa na kuangalia namna ya upatikanaj i wa dawa.
  Amesema uwepo wa Dawa katika Bohari kuu ya dawa nikuonesha kuwa Serikali   ina imani na wananchi wake kwa kuongeza Bajeti ya ununuzi wa dawa kwa asilimia mia moja ambapo upungufu upo kidogo kwenye dawa za wagonjwa wa akili ambap o Wizara iko mbioni kutatua tatizo hilo.
  ”‘Wananchi msininuwe dawa katika mahospitali na vituo vya Afya zipo za kutosha  kwani Serikali imefanya jitihada kubwa ya kueneza dawa na kuzisambaza mahosptalini    mote na vituo vya afya ambapo kama kutakuwa na upungufu wa  dawa  Wizara tutatoa taarifa maalum kwa wananchi wake”. Naibu Waziri huyo Alisisitiza.
  Amewataka wafanyakazi wa Mahospitalini na Vituo vya Afya kuagiza dawa kwa wakati kwani kufanya hivyo kutasaidia kuondosha urasimu kwa wagonjwa ambao wanaokwenda kupata huduma ya matibabu na kuwambiwa dawa hakuna ambapo kuna dawa za kutosha katika Bohari ya dawa.
  Kwa upande wa Mkurugenzi Bohari kuu ya Dawa Zahran  Ali  Hamad amesema kwa mujibu wa mahitaji ya dawa muhimu zinazotumika katika visiwa vya Unguja na Pemba dawa zipo za kutosha kwa kuwahudumia wananchi.
  Amezitaja dawa hizo ni pamoja na za akinamama wanofika kujifungua,dawa za mpango wa uzazi, dawa ya kisukari na pressure na maradhi mengine na kuwasisitiza wahudumu wa afya kuagiza dawa  kwa wakati.
  Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa Zahran Ali Hamad alipotembea kuona dawa katika bohari hiyo, iliyopo Maruhubi Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii

  CHUO Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili kupitia Shule ya Famasi kwa kushirikiana kwa Kituo cha cha Mafunzo ya Kutathimini Dawa cha Afrika Mashariki wameendesha mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Sekeretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wameshiriki katika uratibu wa mafunzo hayo na kutoa misaada ya hali na mal.i

  Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto , Dk. Ulisubisya Mpoki amesema mfumo kutathimini dawa za Afrika Mashariki ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wa ukanda huo wanapata dawa bora, salama na zenye ufanisi mkubwa.

  Dk. Mpoki amesema mafunzo hayo ya nadharia na vitendo kwa wataalam wa dawa wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki yanalenga kuhakikisha kuwa dawa zote zilizokidhi vigezo zinasajiliwa kwa mfumo wa ulinganifu unaotumika baada wataalam hao kujiridhisha kisayansi.

  Nae Mkuruenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bw. Hiiti Sillo amesema kuwa kumekuwa na ushirikiano wa karibu na wananchi katika utoaji wa taarifa pale wanapoona kuna dawa zenye mashaka ziko mtaani, hivyo kusaidia katika dhima ya kulinda afya ya jamii.

  Amesema kuwa kuanzishwa kituo cha kutathimini Dawa cha Afrika Mashariki kitakuwa ni msaada mkubwa katika kuhakikisha kuwa kila dawa zilizo katika nchi za Afrika Mashariki ni zilizosajiliwa na usajili kwa matumizi ya wananchi wote wa ukanda husika.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo  ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na usalama wa  dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki yalifanyika leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA , Hiiti Sillo , Kulia ni Mkurugenzi wa Shahada za awali  wa MUHAS, Profesa Mainen Moshi.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafunzo  ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na usalama wa  dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam
   Mratibu wa Mafunzo  wa MUHAS –TFDA , Profesa Eliangiriya  Kaale akitoa neno la shukrani baada ufunguzi wa mafunzo  ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na usalama wa  dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akiwa katika pamoja na Maprofesa wa Chuo cha Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi pamoja na Watalaam leo jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1378 | 1379 | (Page 1380) | 1381 | 1382 | .... | 1897 | newer