Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

Twanga Pepeta kumtambulisha Ige Moyaba, Miss Ilala leo

0
0

Bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta' leo itawatambulisha wanamuziki wake wapya akiwemo muimbaji wao wa zamani Ige Moyaba na warembo watakaoshiriki Miss Ilala 2013.

Utambulisho huo ambao  ni sehemu ya shamrashamra za sikukuu ya Idd el Fitri utafanyika leo katika ukumbi  wa Mango Garden, Kinondoni.

Mratibu wa onyesho hilo, Joseph Kapinga alisema maandalizi yote ya onyesho hilo yamekamilika. “Ige Moyaba aliyekuwa Ufaransa amewasili nchini tangu juzi usiku na alishajiunga na wanamuziki wenzake,” Kapinga alisema.

Kapinga alisema warembo watakaoshiriki shindano la kumtafuta Miss Ilala pia watatambulishwa kwenye onyesho hilo linaloandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, Freddito Entertainment, Saluti5 na Twitter Pub.

Pia bendi hiyo itaambulisha wanenguaji wake wapya wa kike kwenye onyesho hilo maalum ya kusherekea Idd Pili.  "Tumeamua kuleta wanenguaji wapya kabisa, wenye damu changa ili kuleta mapinduzi kwenye muziki wa dansi. Madansa wetu ni mabinti warembo, pia tuna  wanenguaji watanashati,” alisema Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka  na kuongeza kuwa;

"Tumebadilisha na kuongeza safu mpya ya unenguaji ili kwenda na wakati pamoja na soko la muziki linavyotaka." Kwa upande wa Ige Moyaba aliyetamba kwenye albamu ya ‘Mtu Pesa’ ya mwaka wa 2004, Asha alisema ameandaa vitu vipya kuwapa mashabiki wa bendi hiyo inayotamba kwa staili ya Kisigino.

“Kwa kweli hi siyo onyesho la kukosa kwani itakuwa ni zawadi yetu ya Idd kwa mashabiki wetu,” mkurugenzi huyo alisema.  Mwezi uliyopita Twanga Pepeta walizindua albamu yao ya 10 iitwayo “Nyumbani ni Nyumbani”, ambapo nyimbo zake zitapigwa katika onyesho hilo la leo.

Nyimbo nyingine zitakazopigwa katika onyesho hilo ni zila za albamu za nyuma kama 'Jirani', 'Fainali Uzeeni', 'Chuki Binafsi', 'Ukubwa Jiwe', 'Mtu Pesa', 'Safari', 'Password', 'Mtaa wa Kwanza', 'Mwana Dar es Salaam' na 'Dunia Daraja'.

Balozi wa Vijana Raymond Maro katika mahojiano VOA.

0
0
??????????????????????????????? 
Raymond Maro akiwa katika picha ya furaha pamoja Laurine Ogoma Prisca na mtangazaji Roger Rajar baada ya mahojiano na idhaa ya Kifaransa ya VOA.
??????????????????????????????? 
Mtangazaji maarufu wa VOA Straight Talk Africa Shaka Ssali akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Vijana katika Jumuiya ya Afrika mashariki kwa upande wa Tanzania ndugu Raymond Maro pamoja na mtangazaji mwenza Mariama Diallo na Martin Buhendwa kiongozi wa kundi la Friends of Congo kwa upande wa Vijana ndani ya studio za VOA siku ya Kipindi cha Straight Talk Africa kilichojadili nafasi ya vijana katika jamii na siasa.

Best moment at VOA 101 
Raymond Maro akishiriki kipindi cha televisheni cha VOA - French akiwa na Laurene Saucer na mtangazaji wa kipindi Roger Rajah Muntu ndani ya jumba la VOA

BENDI YA MSONDO NGOMA ILIVYO PAGAWISHI WAPENZI WAKE SIKUKUU YA IDDI

0
0


Waimbaji wa bendi ya msondo ngoma wakitoa burudani wakati wa onesho lao la Iddi lililofanyika katika ukumbi wa DDC Kariakoo Dar es salaam kushoto ni Eddo Sanga na Hasani Moshi. 
Waimbaji wa bendi ya msondo ngoma wakitoa burudani wakati wa onesho lao la Iddi lililofanyika katika ukumbi wa DDC Kariakoo Dar es salaam kushoto ni Eddo Sanga na Hasani Moshi Picha na www.burudan.blogspot.com
Wapuliza hara wa bendi ya msondo ngoma wakitoa burudani wakati wa sikukuu ya idi kushoto ni Hamisi Mnyupe na Romani Mng'ande.
Saddy Ally akiwajibika wakati wa Onesho Ilo

BONDIA FRANCIS MIYEYUSHO AMKALISHA MZAMBIA KWA K,O RAUNDI YA 8.

0
0

MIYEYUSHO AKISHANGILIA USHINDI.
Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kulia  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane .
Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kushoto  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane.
Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kulia  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane.
BONDI KASIM RAJAB  AKIPAMBANA NA kEVIN fABIAN WAKATI WA MPAMBANO WAKE ULIOFANYIKA SIKU YA SIKUKUU YA iDDI KATIKA UKUMBI WA dAR lIVE dAR ES SALAAM fABIAN ALISHINDA KWA pOINT
Bondia Godfrey Pancho kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Hamisi Mohamedi wakati wa mpambano wao uliofanyika sikukuu ya Iddi mosi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara
Bondia Godfrey Pancho kulia akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Hamisi Mohamedi wakati wa mpambano wao uliofanyika sikukuu ya Iddi mosi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara
Bondia Chipaki Chipindi akiwa na mashabiki wake baada ya kumkarisha raundi ya kwanza bondia Ramadhani Kido


Bondia Fidelis Lupupa wa Zambia akiwa chini amekaa akijifikilia kuwa aendelee au asienderee baada ya kupigwa na bondia Mtanzania Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,o ya raundi ya nane Picha na SUPER D
Bondia Fidelis Lupupa wa Zambia akiwa chini amekaa akijifikilia kuwa aendelee au asienderee baada ya kupigwa na bondia Mtanzania Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,o ya raundi ya nane Picha na SUPER D
Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kushoto  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane picha na SUPER D


MIYEYUSHO AKIWA KATIKA POZI

Mtambo dawa za kulevya waingizwa nchini

0
0
Dar es Salaam. Wakati matukio ya baadhi ya vigogo na wasanii maarufu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulenya hayajapoa, imebainika kuwa mtambo maalumu wa kuchanganya na kuziongezea thamani dawa hizo upo hapa nchini.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa mtambo huo ambao awali ulikuwa unapatikana Mombasa, Kenya, pekee, unatumika kuchanganya dawa za kulevya na kemikali nyingine ambapo nusu kilo ya heroine huongezwa hadi kufikia kilo mbili. Uchunguzi unaonyesha kuwa kuwa mtambo huo ulioingizwa mwaka huu na kigogo mmoja wa dawa hizo, upo katika nyumba moja iliyopo eneo la Mbezi Beach.
Mmoja wa watumiaji wa dawa hizo ambaye hakutaka kutajwa gazetini kwa kuhofia usalama wake, alisema mtambo huo umerahisisha upatikanaji wa heroine nchini maarufu ‘white sugar’ kama inavyojulikana mitaani.
“Zamani ‘white sugar’ ikitoka shamba (nchi inakotengenezwa yaani Pakistan na nchi nyingine) ilikuwa inapelekwa Mombasa, Kenya, ambako kuna mtambo wa kuchanganya na dawa nyingine ili iongezeke wingi wake, lakini kazi hiyo inafanyika hapa hapa nchini kwa sasa,” alisema.
Alipoulizwa kuhusu uwepo wa mtambo huo hapa nchini, Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alisema kuwa kuna taarifa alizonazo ambazo bado anazifanyia kazi.
“Hata kama nikiwa nazo nazifanyia kazi, za kwangu mimi nazifanyia kazi na hata za kwako nazifanyia kazi,” alisema Nzowa.
Hata hivyo, Nzowa akizungumza katika kipindi cha Malumbano ya Hoja kilichorushwa na Televisheni ya ITV juzi, alisema kuwa katika siku za hivi karibuni wafanyabiashara wa heroine wamekuwa wakiingiza nchini malighafi za dawa hizo, tofauti na awali ambapo walikuwa wakiingiza dawa hizo zikiwa tayari kwa matumizi.
Akitoa mfano alisema kuna raia wa kigeni alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, akiwa na malighafi hizo zilizokuwa zikifanana na sukari na kwamba Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Mkemia Mkuu wa Serikali, ndiyo waliobaini kuwa haikuwa sukari kama ilivyodhaniwa.
Alisema kutokana na uhaba wa dawa hizo bei ya kete imepanda ambapo hivi sasa hakuna kete ya gramu 0.11 inayouzwa chini ya Sh 3,000.
Hii ni mara ya pili kubainika kuwepo kwa mtambo wa kutengenezea dawa za kulevya nchini. Miaka ya hivi karibuni jeshi la polisi lilikamata mtambo wa kutengenezea dawa za kulevya katika nyumba moja iliyopo eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa mbali ya kuwepo mtambo huo kuna nyumba tano katika eneo la Tandika jijini Dar es Salaam karibu na soko, ambazo zinatumika kuuza dawa za kulevya huku baadhi ya polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, wakiwalinda wauzaji wake kwa kuwapa taarifa ya mipango inayopangwa na jeshi la kuwatia mbaroni.

dhehebu la Ahmadiya muslim jamat lasherehekea sikukuu ya Eidd na wagonjwa mkoani iringa.

0
0
 Waislamu wa dhehebu la Ahmadiya muslim jamat  jana wamesherekea  sikukuu ya iddy  elfitri na wagonjwa wa hopsitali ya rufaa mkoani iringa kwa kuwapatia vyakula na kuwapa pole wagonjwa wote  waliokuwa wamelazwa katika wodi mbalimbali.

 Akizungumzi hatua hiyo mwenyketi wa vijana wa dhehebu hilo azizi  ally mwalongo alisema hiyo ni moja ya mafundisho ya mtume ya kuwapenda agonjwa, ndugu na jamii kwa ujumla.

Alisema  hatua hiyo ni kuwapa matumaini wagonjwa ambao wamelazwa hospitalini kwani uwepo wao  katika hali hiyo si kwa matakwa yao.


Aidha baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo  wameshukuru kusherekea sikukuu ya iddi na dhehebu hilo na kuongeza kuwa jamii inatakiwa kuwajali wagonjwa kwa kuwathamini kwani  kufarijiwa kwao ndio moja ya matumaini yao.

Rais Kikwete akutana na Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan Mhe. Toshimistu Motegi leo Ikulu, Dar es salaam

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na  Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Mheshimiwa Toshimistu Motegi alipokutana na kufanya mazungumzo naye  Ikulu, Dar Es Salaam, leo Agosti 10, 2013.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Mheshimiwa Toshimistu Motegi (wa tatu kushoto, mbele)  na ujumbe wake pamoja na Waziri wa Uchukuzi  Dkt.  Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia),  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Dr Mary Nagu (wa pili kulia), Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda (wa pili kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe Salome  Sijaona  (wa kwanza kushoto) alipokutana na kufanya mazungumzo naye  Ikulu, Dar Es Salaam, leo Agosti 10, 2013. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na  Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Mheshimiwa Toshimistu Motegi alipokutana na kufanya mazungumzo naye  Ikulu, Dar Es Salaam, leo Agosti 10, 2013.PICHA NA IKULU

Odama Band ikitoa burudani ya awali kabla ya Chamelleone kupanda jukwaani usiku huu escape one

0
0

Dr Josee Chameleon alivyokamua ndani ya Escape one usiku wa kuamkia leo jijini Dar.

0
0

DADA DINACARES YALA CHAKULA CHA MCHANA NA WATOTO YATIMA AZULA BEACH KAWE JIONI YA LEO.

0
0
  Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares (pichani Mbele),akiwa sambamba na baadhi ya Wadau waliojitokeza kuifanikisha hafla hiyo ya chakula cha mchana na watoto Yatima kutoka vituo vitatu,kushoto ni  Dada  Janet Sosthenes  Mwenda wa Ongea na Janet na wadau wengineo.
Mmoja wa Watoto akichorwa. 
 Mtangazaji wa Clouds FM,Dada Regina Mwalekwa na  Dada Janet Sosthenes  Mwenda wa Ongea na Janet wakiwa na baadhi ya watoto waliojumuika kwa chakula cha pamoja,kwenye hafla iliyohusu vituo vitatu vya watoto Yatima iliyofanyika kwenye fukwe ya Azula beach Kawe jioni ya leo.
 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kushoto ni Snura na kulia ni Shilole wakiwa na rafiki yao pichani kati wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja  na watoto.
Dada Janet Sosthenes  Mwenda wa Ongea na Janet akicheza mpira na watoto 
 Watoto wakipakuliwa chakula safi kabisa.
 Baadhi ya Wadau mbalimbali wakiwemo wasanii,wakiwasaidia watoto kuwaandalia chakula.
 Watoto waishio katika vituo vya kulelea watoto yatima na wengineo wakicheza michezo yo kwa pamoja.
 Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares akiongea na Watoto kutoka vituo Yatima,kabla ya kukata keki na kuwalisha.
Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares akimlisha keki mmoja wa watoto waishio katika mazingira Magumu kutoka kituo cha Watoto yatima cha Vetenari Temeke 
Baadhi ya watoto kutoka vituo vya watoto Yatima,kituo cha Sifa Bunju,Zaidia Sinza pamoja na Vetenari Temeke,wamekutana leo mchana kwenye Fukwe ya Azura Beach Kawe kwa ajili ya kupata chakula cha pamoja na watoto wengine,huku michezo mbalimbali kama vile face painting,jumping castle,kuogelea,kuvuta kamba,mpira wa miguu,kucheza mziki n.k.Michezo hiyo iliyoandaliwa na Kids Event na mingineyo ilitawala na kuwaburudisha sana watoto.
Aidha mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares,amesema kuwa mkusanyiko huo unafanyika kufuatia zoezi zima la kukamilisha ule mpango ulioanza wa kuchangia vituo vya watoto yatima.

Pamoja na hafla hiyo pia Keki iliyoandaliwa na flying chefs  ilikatwa huku wasanii mbalimbali wakishiriki kwa pamoja,akiwemo Shilole,Snura,Quenn Darlin,Mwasiti na wengineo.Janet Sosthenes  Mwenda wa Ongea na Janet na Wasanii wengine walijitolea kuwahudumia na kuwaangalia watoto.
Dina Marios anawashukuru watu wote walioshiriki kuchangia vituo hivyo.Wadau wa blog yake www.dinamarios.blogspot.com wasikilizaji wa leo tena ya clouds fm na wote walioguswa. Mpango huo utaendelea siku nyingine tena maana ni endelevu

AJALI MBAYA YA BASI LA MERIDIANI

0
0
Likiwa limetoka rombo kwenda Dar. Limeanguka hapa karibu na mbwewe Bagamoyo. Siti zote ziko nje. Watu wamekufa. Basi limekatika siti zipo njee. Dereva bado hajatolewa.Habari picha na Mdau.

Rais Kikwete amtembelea mzee wa kijijini msoga mzee Khalfan Tengeneza Mchaga

0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mzee Khalfan Tengeneza Mchaga, mmoja wa wazee katika kijiji cha Msoga,kata ya Chalinze ,wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani  leo wakati Rais alipomtembelea kumjulia hali.Rais Kikwete alikuwa katika mapumziko ya mwisho wa wiki kijijini Msoga. Picha na Freddy Maro.

dc makete ataka elimu ya vvu iende pamoja na ujasiriamali

0
0
 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mradi huo ngazi ya wilaya akisikiliza maelezo ya mradi huo kutoka SUMASESU
 Mkurugenzi wa shirika la SUMASESU Egnatio Mtawa akitoa maelezo kwa washiriki kuhusu utambulisho wa mradi uitwao "Vijana wa makete na mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi" katika ukumbi wa HIMA Makete wakati wa utambulisho wa mradi huo ngazi ya wilaya Augusti 09, 2013. Shirika la SUMASESU ndilo litakalotekeleza mradi huo kwa ushirikiano na UNICEF
Na Edwin Moshi, Makete
 Washiriki wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mkurugenzi wa SUMASESU (hayupo pichani)
 Mratibu wa ukimwi halmashauri ya wilaya ya Makete CHAC Ester Lamosai(kushoto) akiwa na Anifa Mwakitalima kutoka SUMASESU
Mtaribu wa ukimwi sekta ya afya (DAC) Dk Shadrack Sanga akichangia hoja kwenye kikao hicho
 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mradi huo ngazi ya wilaya katika ukumbi wa HIMA Makete
Makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Makete Jison Mbalizi akiahirisha kikao hicho
=======

Wadau wa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi kwa vijana wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kutoa elimu hiyo sanjari na elimu ya ujasiriamali kwa pamoja kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza ongezeko la maambukizi ya ugonjwa huo kwa kasi zaidi

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro wakati akifungua mradi wa vijana wa Makete na mapambano dhidi ya UKIMWI uliozinduliwa Ijumaa Agosti 9, 2013 ngazi ya wilaya, mradi ambao utatekelezwa na shirika la sumasesu kwa ufadhili wa UNICEF

Matiro amesema vijana wengi wamekuwa wakipatiwa elimu hiyo ya namna ya kujilinda na maambukizi mapya ya vvu na baada ya hapo wanakosa kazi ya kufanya hivyo kuwa rahisi kwao kujiingiza kwenye vitendo vitakavyowasababishia kupata vvu

"Kijana anapewa elimu sawa lakini hana cha kufanya mwishowe akija mtu wa kuwarubuni hasa kifedha wanaingia kilaini kwa kuwa hana shughuli yeyote inayomuingizia kipato, mwishowe anaweza kupata vvu"alisema Matiro

Amewataka vijana kujiunga na vikundi mbalimbali ili waweze kupatiwa mikopo nafuu kwa ajili ya shughuli hasa kilimo kwa kuwa wakishajiunda na kutoa taarifa yeye kwa kushirikiana na halmashauri watawasaidia kupata mkopo ambapo wakati huo huo wakiwa na shughuli ya kufanya halafu wakapata elimu ya kujikinga na vvu itakuwa bora na yenye manufaa kwao

Wadau walioshiriki katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa HIMA Makete akiwemo mratibu wa ukimwi sekta ya afya (DAC) Dk Shadrack Sanga amelitaka shirika hilo wakati wa kutekeleza mradi huo watoe elimu ya tohara kwa vijana wa kiume ambapo akiwataarifu wao kama idara ya afya wako tayari kuungana nao jambo lililoungwa mkono na kaimu mganga mkuu Boniphace Sanga ambaye alikuwepo kwenye kikao hicho

Kwa upande wao shirika la SUMASESU kupitia kwa mkurugenzi Egnatio Mtawa alipongeza kwa ushirikiano uliooneshwa na wadau wote huku akimuahidi mkuu wa wilaya kuwa wataingiza mada ya ujasiriamali wakati wakitoa elimu ya ukimwi kwa vijana ili iwasaidie huku akiahidi kushirikiana na kila wahusika ili mradi huo ufanikiwe

Mradi huo utakaotekelezwa hadi Julai 2015, utahusisha kata za Ipelele, Iniho, Iwawa, Isapulano na Kitulo

SHEIKH PONDA ISSA PONDA AMELAZWA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI KUTIBIWA JERAHA ALILOPATA JANA MOROGORO

0
0
 KATIBU WA JUMUIYA ZA KIISLAMU TANZANIA  SHEKHE ISSA PONDA NI KWELI HAPO JANA ALIPIGWA RISASI NA KWASASA YUPO HOSPITALI YA  RUFAA YA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI NA SI KWELI KAMA YUPO CHINI YA ULINZI WA POLISI KAMA  SMS MBALIMBALI KUPITIA SIMU ZA VIGANJANI ZINAVYOSAMBAZWA.PIA JUMUIYA NA TAASISI YA KIISLAMU TANZANIA LEO BAADA YA SWALA YA ALASIRI KATIKA MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI ILITARAJIWA KUTOA  TAMKO KUHUSIANA NA TUKIO HILO.

 KATIBU WA JUMUIYA ZA KIISLAMU TANZANIA  SHEKHE ISSA PONDA
 KATIBU WA JUMUIYA ZA KIISLAMU TANZANIA  SHEKHE ISSA PONDA AKIUGUZWA MUHIMBILI
SEHEMU ALIYOJERUHIWA KATIBU WA JUMUIYA ZA KIISLAMU TANZANIA  SHEKHE ISSA PONDA

DAR LIVE YACHENGUA NA EXTRA BONGO, TOT IDD PILI

0
0
Aziza Kimsi wa TOT Taarab akiimba.
Wanamuziki wa TOT wakiimba.
Kiongozi wa Extra Bongo, Ally Choki, akiimba wimbo wa Mtenda Akitendewa.
Wanamuziki wa Extra Bongo wakiwa kazini.
Ally Choki na mnenguaji wake wakionyesha ‘machejo’.
Wanenguaji wa Extra Bongo wakijinafasi.
Naibu Mkurugenzi wa TOT, Gasper Tumaini akionyesha 'matindo' ukumbini.
MASHABIKI wa muziki jana walipata burudani ya kukata na shoka katika sikukuu ya Idd Pili kwenye Ukumbi wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam ambapo walichenguliwa vilivyo na bendi za Extra Bongo na TOT. (NA ISSA MNALLY / GPL)

SHINING THE SPOTLIGHT ON FASHION DESIGNER LINDA BEZUIDENHOUT

0
0
Shining the Spotlight on Linda Bezuidenhout Linda Bezuidenhout (LB) is a fashion designer who is based in Atlanta, USA. Linda has been involved in fashion industry for over 20 years, in Africa, Europe and the USA. The LB line is influenced by a wide range of world fashion, cultures and trends.

Linda comes from a Dutch-Tanzanian background and has been influenced with fashion since the age of 8 when she used to insist on designing her own holiday & special occasion clothes and have local tailors sew the dresses. As a teenager she lived in several different countries in Europe which developed her fashion vision and exposure.

 In her 20′s she moved back to Africa (Tanzania) and continued contributing to the fashion scene there as a top beautician with involvement in various beauty pageants in conjunction with some of the top African female singers such as M'bilia Bel & Vivic Motuwa. In her late 20′s she moved to USA and got involved in the men's world of fashion as well and owned several menswear stores in different malls in the US.

For more video and exclusive interviews go on www.swahilitv.blogspot.com

mwanamuziki dkt jose Chameleone,alivyowakuna wakazi wa jiji la dar mwishoni mwa wiki.

0
0


 
Pichani juu ni sehemu ya mamia ya mashabiki na wapenzi wa muziki wakifurahia nyimbo wakati wa tamasha la Valuvalu lililofanyika kwenye ufukwe wa Escape Complex jijini Dar es Salaam, Jumamosi. Tamasha hilo liliandaliwa na kampuni ya Prime Time Promotions na kudhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania. Msanii kutoka Uganda, Joseph Mayanja, maarufu kama Jose Chameleone, ndiye aliyekuwa msanii rasmi wakati wa tamasha hilo.
Msanii kutoka Uganda, Joseph Mayanja, maarufu kama Jose Chameleone, akiwapagawisha amlefu ya mashambiki waliohudhuria tamasha la Valuvalu katika ukumbi wa Escape Complex jijini Dar es Salaam, Jumamosi. Tamasha hilo liliandaliwa na kampuni ya Prime Time Promotions na kudhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Msanii kutoka Uganda, Joseph Mayanja, maarufu kama Jose Chameleone, akiwa na baadhi ya mashambiki kwenye jukwaa ambao walihudhuria tamasha la Valuvalu katika ukumbi wa Escape Complex jijini Dar es Salaam, Jumamosi. Tamasha hilo liliandaliwa na kampuni ya Prime Time Promotions na kudhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Maelfu ya mashabiki was muziki wakifurahia nyimbo wakati wa tamasha la Valuvalu lililofanyika kwenye ukumbi wa Escape Complex jijini Dar es Salaam, Jumamosi. Tamasha hilo liliandaliwa na kampuni ya Prime Time Promotions na kudhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania. Msanii kutoka Uganda, Joseph Mayanja, maarufu kama Jose Chameleone, ndiye aliyekuwa msanii rasmi wakati wa tamasha hilo.

Exim Bank secures $15 million loan from PROPARCO to support SMEs

0
0
Exim Bank Board Chairman Yogesh Manek
========   ========  ==========
Exim Bank secures $15 million loan from PROPARCO to support SMEs

EXIM Bank Tanzania has secured a USD 15 million (about TSH 24.7 billion) loan from PROPARCO, a French international development finance institution.

The financing will be used for onward lending to support Exim Bank’s growing Small and Medium Enterprise (SME) customers and primarily those requiring medium to long-term credit facilities. The mission of PROPARCO is to boost private investment in developing countries with the aim of supporting growth and sustainable development.

The loan to Exim Bank has been extended at very competitive terms and is the fourth time PROPARCO has supported the Exim Bank Group. Exim Tanzania earlier received two successive loans from PROPARCO. Exim Bank Comoros, a subsidiary, was approved Euro 4 million from PROPARCO for SME lending across the chain of islands.

According to a press statement issued by the Chairman of the Board of Exim Bank, Mr Yogesh Manek at the weekend, the loan will go a long way to help to find solutions for the long term credit needs of the bank’s business customers.

“We are quite pleased with the continued confidence reposed by PROPARCO in the Bank. Our customers will surely welcome longer term credit at competitive rate,” Mr Manek said. Mr Manek further stated that his bank is committed to financing the requirements of small, medium and large enterprises to help accelerating economic development in the country.

“Our long-term relationship with PROPARCO and other key Development Finance Institution (FDIs) is built upon the bank’s posting sustained quantifiable achievements.

Since the commencement of Exim Bank in 1997, the bank has shown consistent growth in terms of deposits, assets and geographical reach.” He added. The PROPARCO’s East Africa Regional Representative, Aïnaché Guédi; re-affirmed his organisation’s commitment to help building sustainable local financing capacity across Africa.

“We are very proud to support a strong and dynamic player such as Exim Bank. This new operation is the continuation of a long term partnership between Exim Bank and PROPARCO. It is the sign of our commitment to support its long-term strategy, notably in favour of SMEs which are vital to economic growth and development in Sub-Saharan Africa” he said.

In a similar development, Exim Bank in December 2011 secured a USD 10 (about 16bn/-) loan from FMO, a Dutch Development Finance Institution, that also contributed to the revitalization of the fiscal environment in the country's banking sector.

With its latest results, Exim Bank has consolidated its balance sheet thus enabling the bank to cross the much anticipated trillion milestone with assets of TSH 1.02 trillion at June 2013.


Tamasha la Afrika lafana Marekani

0
0
IMG_3439
Tanzania iliwakilishwa vyema kwenye tamasha hilo la kila mwaka liitwalo FestAfrica lililofanyika mwishoni mwa juma huko Silver Spring Md na kuhudhuriwa   na mamia ya wakazi.
IMG_3269
Fashion ya mavazi ya Afrika. IMG_3282IMG_3300IMG_3326IMG_3285IMG_3337
Kwa picha zaidi ungana na Sundayshomari.com

Push Mobile kumwaga vitz 4, pikipiki 12 Serengeti Fiesta 2013.

0
0
Meneja Mauzo na Masoko wa Push Mobile, Rugambo Rodney akimkabidhi funguo mbili Diana Elis Mkoba baada ya kushinda shindano la Tamasha la Serengeti Fiesta 2012. Diana alikabidhiwa magari mawili aina ya Vitz yenye thamani ya shs milioni 18.Katikati ni Baba mdogo wa mshindi, Gratian Mkoba ambaye ni Rais wa chama cha Walimu Tanzania (CWT). Mwaka huu, Kampuni hiyo itatoa magari manne, pikipiki 12 na fedha taslim shs 100,000 ikiwa juma ya zawadi zote ni sh million 80. 
===========   ==========
Push Mobile kumwaga vitz 4, pikipiki 12 Fiesta
KAMPUNI ya Push Mobile Media Limited itatoa zawadi za magari aina ya Vitz manne (4) na pikipiki 12 kwa mashabiki mbali mbali watakaoshinda bahati nasibu maalum ya tamasha la Serengeti Fiesta linalotarajiwa kuzinduliwa Jumamosi mjini Kigoma.
Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa zawadi mbali ya magari na pikipiki, pia watatoa zawadi za fedha taslim (sh 100,000) kwa mashabiki hao ambao ili kushinda wanatakiwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 ili kuweza kushinda gari, pikipiki au fedha taslim na unaweza kushinda tiketi ya VIP kwa kutuma jina la msanii kwa mfano Diamond na kuacha nafasi na baadaye kuwema maoni yako kwenda namba hiyo hiyo.
Rodney alisema kuwa mbali ya kushinda tiketi, mshiriki atalipiwa tiketi ya ndege kuja Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki katika tamasha la fiesta la mwisho. Alisema kuwa wameamua kuweza zawadi hizo nono ili kunogesha zaidi tamasha hilo ambalo kwa kuwanufaisha mashabiki  wa muziki hapa nchini.
Aliongeza kuwa wamejipanga ili kuwashirikisha wananchi wote katika tamasha hilo kwani watatoa pia watazindua huduma mpya ijulikanayo kwa jina la Simu TV ambapo itamwezesha mashabiki kuona video mbali mbali za muziki na matukio mengine, kupata nyimbo mbali mbali, kupata taarifa mbali mbali ikiwa pamoja na za michezo kwa kupitia simu ya mkononi.
kuhusiana na zawadi za fedha, Rodney alisema kuwa zawadi hiyo itakuwa inatolewa kila siku kwa mashabiki watakaoshinda bahati nasibu hiyo. Alifafanua kuwa jumla ya sh milioni 80 zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili litakalodumu kwa kipindi cha miezi mitatu.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images