Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1373 | 1374 | (Page 1375) | 1376 | 1377 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na. Paschal Dotto- MAELEZO.

  Serikali ya Awamu ya Tano chini ya  uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vitendo vya rushwa katika ofisi za Serikali, taasisi na mashirika ya umma na kuweka usawa katika  upatikanaji wa huduma kwa jamii.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam  na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John  Mbungo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kuhusu rushwa katika taasisi na mashirika ya umma kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Brigedia Jenerali Mbungo alisema kuwa lazima watumishi wajifunze kuwa waadilifu, kwa hiyo kile watakachokipata kutoka katika mkutano huo kikafanye kazi kuleta haki kwa wananchi wakati wa kupata huduma katika ofisi zao ili kuendana na sera ya Awamu ya Tano ya kutokuvumilia vitendo vya rushwa nchini.

  “Tumieni fursa katika kikao hiki ili kuweza kupata elimu itakayosaidia wananchi kuelimika juu ya vitendo vya rushwa na kupata haki zao za msingi wanapopata huduma katika ofisi zenu”,alisema Brigedia Jenerali Mbungo.
  Kikao kazi hiki ni cha kwanza ambacho kinafuatia mkakati wa awamu wa tatu  utakaokuwa wa miaka mitano kuanzia  Julai, 2017 unaolenga kuanzia ngazi za vijiji, wilaya, mkoa, mpaka taifa ili kudhibiti uadilifu, nidhamu na utendaji kazi wenye kuzingatia haki katika ofisi mbalimbali nchini.

  Aidha Brigedia Mbungo alisema kuwa kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali, hali ya rushwa nchini imepungua kwa kiasi kikubwa kwani malalamiko yamepungua katika ofisi, taasisi na mashirika ya umma.

  “Hali ya rushwa sasa hivi imepungua kwa sababu Serikali kwa kutumia juhudi  mbalimbali imedhibiti hali hii, Tanzania ina viwango vya chini sana vya rushwa ikilinganishwa na nchi nyingine za maziwa makuu kwa hiyo naweza kusema kiwango kimepungua sana hususani kwa Jiji la Dar es Salaam ambapo vitendo hivi vilishamiri sana, hivyo katika awamu hii ya tatu ya mkakati huu tunatarajia viwango vitashuka zaidi”, alisisitiza Brigedia Jenerali Mbungo.

  Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi.Theresia Mmbando alisema kuwa katika mkoa wa Dar es Salaam hali ya vitendo vya rushwa imepungua kwa kiasi kikubwa na sasa wananchi wanapata huduma pasipo kuwa na dalili zozote za rushwa.

  “Hali ya rushwa katika mkoa wetu wa Dar es Salaam inapungua siku hadi siku kwa kuwa watu wanaendelea kupata elimu ya haki zao za msingi na kuhudumiwa pasipo kutoa rushwa, wala kuwepo dalili za rushwa”, alisema Bi. Mbando.

  Kwa upande wake Mkuu wa TAKUKURU,  kanda maalum ya Dar es Salaam Bw.Juventus Baitu ameeleza kuwa wamefanikiwa kuweka sawa  mkakati huo kwa kutoa elimu kwa wananchi na kwa sasa kumekuwa na mwamko wa kuripoti matukio ya rushwa katika ofisi yake.

  Aliongeza kusema kuwa katika kitengo cha Dawati la Uchunguzi wamepokea malalamiko yapatayo 665 kwa mkoa wa Dar es Salaam huku kitengo hicho kikifungua majalada ya kesi 40 kwa Mwendesha Mashtaka (DPP) na kusikilizwa kesi 26 ambapo taasisi  hiyo ilifanikiwa kushinda kesi 14 na kuokoa kiasi cha pesa kisichopungua shilingi milioni 791,443,984 katika kesi mbalimbali za rushwa.

  Aidha TAKUKURU kupitia dawati la elimu ya rushwa imeweza kufungua vilabu 94 vipya katika shule mbalimbali mkoani Dar es Salaam, kuendesha semina 91 kwa watumishi wa taasisi na mashirika ya umma pamoja na maonesho 12 yanayohusu vitendo vya rushwa ikiwemo kuwahabarisha wananchi kupitia vipindi vya televisheni 14 kuanzia mwaka 2016 pamoja na kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari kwa kutoa vitini 19 kuhusu mapambano dhidi ya rushwa.

  “Tumeweza kutoa elimu kupitia matamasha mbalimbali zaidi ya 16 katika taasisi na mashirika ya umma ambapo matamasha 7 yalikuwa na lengo la kutoa mazimio kwa taasisi na mashirika ya umma kuhusu kwa vitendo vya rushwa”,alisisitiza Bw.Baitu.Mkakati huo kwa awamu ya tatu ulizinduliwa rasmi, Desemba 10, 2016 wakati wa maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu duniani  na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo utekelezaji wake ulianza tarehe 1, Julai, 2017.
  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu (2017-20120) leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Theresia Mmbando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo.
    Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bibi. Theresia Mmbando akielezea jambo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu (2017-20120) leo jijini Dar es Salaam.
   Mratibu wa Kitengo cha Utawala Bora kutoka Ofisi ya Rais Bi. Christina Maganga akitoa neno la utangulizi kuhusu mkakati wa taifa dhidi ya rushwa awamu ya tatu wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wajumbe wa kamati za kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa mkakati huo leo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudhibiti uadilifu kutoka mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia wakifuatila mada wakati wa kikao kazi cha wajumbe wa kamati hizo kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu (2017-20120) leo jijini Dar es Salaam.
   Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu mkakati wa taifa dhidi ya rushwa toka kwa Mratibu wa Kitengo cha Utawala Bora Ofisi ya Rais, Bi. Christina Maganga (hayupo pichani) wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za kudhibiti uadilifu leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Theresia Mmbando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo.
  Mkuu wa Takukuru Kanda Maalum ya Dar es Salaam Juventus M. Baitu akiwasilisha mada kuhusu hali ya rushwa katika mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu (2017-20120) leo.
  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu (2017-20120) leo jijini Dar es Salaam.
  Picha zote na: Frank Shija- MAELEZO

  0 0

  Na Evelyn Mkokoi – Dar Es Salaam.

  Garage kubwa yenye kutoa huduma kwa magari ya aina mbalimbali iliyopo katika eneo la mtaa wa viwanda mikocheni jijini Dar es Salaam imefungwa kwa kile kinachodaiwa ni kukikuka sheria ya mazingira na kanuni zake kwa kuharibu mazingira kwa kumwaga mafuta machafu,  kutupa vyuma chakavu na kutelekeza  magari  yaliyochoka.

  Hatua Hiyo imechukuliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupitia Afisa Sheria Mkuu wake  Bw. Vincent Haule, ambapo Bwana Haule Alisema kuwa Garage Hiyo ambayo Mmiliki wake hakutambulika Mara moja inatakiwa kusimamisha shughuli zote za uendeshaji katika eneo hilo ndani ya siku saba pamoja na kuondoa magari yote.

  Bw. Haule aliongeza kwa kusema kuwa Mmiliki wa Garage hiyo anatakiwa kufuata taratibu za serikali kwa kupata vibali vyote vya uendeshaji ikiwa ni pamoja na kibali maalum kutoka NEMC.Baada ya kutozwa faini ya shilingi milioni 10 kwa kiwanda cha Bidco kinachotengeneza bidhaa za sabuni na mafuta ya kula na kutakiwa kuilipa faini hiyo ndani ya wiki mbili, Naibu Waziri Ofisi ya Makami wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, alisema viwanda vinavyochukuliwa hatua kwa uchafuzi wa mazingira vinatakiwa  kutii maagizo ya serikali.

   Mpina pia alitoa maelekezo kwa Manisapaa ya Kinondoni ambapo aliitaka ishughulikie mitaro katika maeneo ya mikocheni pembezoni mwa viwanda husika na kuondosha maji katika njia sahihi.Kwa upande wa wenye viwanda, Mpina aliwata kuacha kutiririsha majitaka katika mazingira na kuyatibu na kuyaunga katika mfumo sahihi wa uondoshwaji maji hayo wa DAWASCO ili kunususru uharibifu wa mazingira na afya ya viumbe hai.

  Aidha, Mpina aliwataka wamiliki wa kiwanda cha Bidco kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuziba matundu yanayotoa maji machafu kutoka kiwandani hapo sambamba na kusafisha mitaro yote kiwandani humo. Ziara ya  siku mbili ya Naibu Waziri Mpina  jijini Dar es Salaam ilihusisha Ukaguzi wa Mazingira na Utekelezaji wa Sheria hiyo.
  Naibu Waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina(kushoto) akimsikiliza mtaalam  Bw. Filbert Mdonko, kutoka katika kiwanda cha Intergraded Steel Limited kilichopo katika eneo la viwanda Mikocheni Dar es Salaam namna ambavyo Mtambo wa kusafisha Majitaka unavyofanya kazi.
   Sehemu ya eneo la Garage iliyofungwa kwa uchafuzi wa mazingira katika eneo la viwanda Mikocheni jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano a Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, akiongea na kuonyesha maji machafu na yenye sumu yaliyotuwama na maji hayo yanayotoka viwandani katika eneo la Mikocheni Jijini Dar es Salaam alipoendelea na ziara yake ya ukaguzi wa viwanda na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira leo.  0 0  0 0

  Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) amewataka akina mama kujitahidi kuwekeza katika elimu kwa watoto hususani watoto wa kike na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu bora.
  Mheshimiwa Azza Hilal (pichani) ameyasema hayo leo Jumatano Septemba 20,2017 katika ukumbi wa Mountain View Hotel uliopo katika kata Tinde wilaya ya Shinyanga wakati akifungua Mafunzo ya ujasiriamali,fedha na mikopo kwa akina mama yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB tawi la Shinyanga.Mbali na kuwaasa akina mama kutumia vyema mikopo wanayopata kuitumia kwa malengo waliyokusudia,pia aliwakumbusha kuwekeza kwa watoto wao.
  Alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa inayoongoza nchini kwa kuwa na takwimu kubwa (asilimia 59) ya mimba za utotoni na ndoa za utotoni hivyo jitihada mbalimbali za pamoja zinahitajika ili kuondoa vitendo hivyo ambavyo vinawanyika haki watoto wa kike kuendelea na masomo yao. 
  “Nitumie fursa hii kuwakumbusha kuwa sisi akina mama kuwa tuna wajibu mkubwa kuhakikisha watoto wetu wa kike wanapata elimu iliyo bora,kuhakikisha pia watoto ambao hawakupata fursa ya kufaulu mtihani wa darasa la saba ili kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza tunawatafutia njia mbadala ya kuweza kujikomboa na maisha badala ya kukimbilia kuwaozesha”,alieleza Hilal.
  “Kumekuwa na tabia, mtoto akiingia darasa la saba anaambiwa na wazazi wake kuwa akafanye vibaya kwenye mtihani,naomba tuanze sisi akina mama kukataa,kwanini unakubali mtoto wako aambiwe na baba yake kuwa akafeli mtihani?”,alihoji mbunge huyo.Aidha alisema ili kuondoka kwenye takwimu za kuitwa watu ambao hawajasoma ni vyema akina mama wakawa mstari wa mbele katika kupigania haki za watoto.
  “Wenye kulibeba hili ni akina mama kwa sababu akina baba tunajua wametanguliza pesa mbele,najua hakuna ambacho mwanamke anaweza akaamua kukifanya na kikashindikana,naomba tuanze kuwapatia watoto malezi ya kupenda elimu na kuepuka vishawishi wakiwa wadogo”,alisema Hilal.
  “Niwaombe sana tuwe karibu na watoto wetu wa kike, ili waweze kukushirikisha kwa jambo lolote watakalokutana nalo,usipokuwa karibu na mtoto wako,hata kama atabakwa hawezi kujibu kwako,lakini kama umejenga utamaduni wa kuongea naye kama rafiki yako,kama ndugu yako wa karibu hawezi kusita kukwambia jambo lolote zuri ama baya litakalokuwa limemtokea”,alieleza Mhe. Hilal.
  Mbunge huyo pia alieleza kusikitishwa na vitendo vya baadhi ya wazazi kuficha matukio ya watoto wanapofanyiwa vitendo vya kikatili kwa watoto wa kike.
  “Watoto wengi wa kike wanafanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo kubakwa,kwa taarifa nilizopewa polisi wazazi mnaficha vitendo vya kikatili dhidi ya watoto,kwanini mnaficha vitendo hivi viovu? Mtoto anafanyiwa vitendo vibaya halafu mzazi unaficha?,inakusaidia nini?,ni bora ukakubali fedheha ya siku moja lakini haki ya mtoto wako ikapatikana”,alisema.
  “Inasikitisha sana pale mnapoitwa kutoa ushahidi wa kesi za ukatili dhidi ya watoto halafu mnakataa,kwa kweli hamuwatendei haki watoto wetu,Kama mzazi unatetea uovu wa namna hii wewe ni muuaji kwa sababu wewe mzazi usipotoa ushirikiano hatma ya kesi haitakuwepo matokeo yake mtabaki kulalamika tu kuwa watuhumiwa mnawapeleka polisi lakini mnawaona wapo tu mtaani,sasa mtuhumiwa ataachaje kuwepo wakati hutoi ushirikiano?”,aliongeza Mhe. Hilal.
  Aidha aliwataka wadua wote wa haki za watoto kuendelea kulaani vitendo vya ukatili dhidi ya watoto huku akiwasisitiza wazazi na walezi watoto kutofumbia macho vitendo na kumaliza kesi kienyeji kwani haki za watoto zinapotea.
  Katika hatua nyingine kutokana na maendeleo katika sayansi na teknolojia aliwatahadhalisha wazazi na walezi kuwa makini na matumizi ya mitandao kwani baadhi ya watoto hususani wanaosoma katika shule zenye mabweni ‘Boarding’ wanafanya michezo mibaya kutokana na mambo wanayoyaona mitandaoni.
  Mbunge huyo aliishukuru Benki ya CRDB kkutoa elimu kuhusu masuala ya fedha na mikopo elimu ambayo itawasaidia wananchi kuendesha biashara zao vizuri.
  Hata hivyo Meneja wa Benki ya CRDB alisema benki hiyo itaendelea kufungua matawi katika maeneo mbalimbali ya vijijini na kuwapatia elimu wajasiriamali waliopo kwenye vikundi mbalimbali.
  Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe, akizungumza kabla yakuanza makabidhiano ya zilizo kuwa Nyumba za CDA kutoka Manispaa ya Dodoma iliyopewa hapo awali kwenda kwa Wakala wa majengo Tanzania (TBA).
  Katibu Mkuu Mkuu OR-TAMISEMI,Mhandisi Mussa Iyombe, pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa majengo nchini, Msanifu Majengo Elius Mwakalinga, wakiweka saini makubaliano ya kukabidhiana zilizokuwa nyumba za CDA.

  .Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe, akipokea Nyaraka kutoka kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma kabla yakuzikabidhi kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa majengo Tanzania.

  Katibu Mkuu Mussa Iyombe akifanya makabidhiano rasmi na Mtendaji mkuu wa Wakala wa Majengo nchini. TBA.

  Baadhi ya washuhudiaji wakiwa katika makabidhiano hayo hapa wakishuhudia.


  Na. Angela Msimbira- TAMISEMI.


  Katibu Mkuu Ofisi ya Ras Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe amesema kuwa zaidi ya kaya 438 za watumishi wa umma watakaohamia Dodoma na wenye sifa ya kupatiwa nyumba na Serikali watakuwa na uhakika wa kupata nyumba zilizokuwa zikimilikiwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA)

  Akikabidhi Nyumba zilizokuwa zikimilikiwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu kwa Wakala wa Majengo (TBA) Mhandisi Mussa Iyombe amesema, nyumba hizo zitakuwa maalum kwa watumishi wenye sifa kulingana na miundo ya kitumishi.

  ‘’Nyumba ambazo zinakabidhiwa kwa Wakala wa Majengo ni nyumba za kuishi ambazo awali zilimilikiwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu na kuhamishiwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma” Amesema Mhandisi Iyombe.

  Akitoa Maelezo ya awali Mhandisi Musa Iyombe amesema baada ya kuivunjwa kwa CDA iliagizwa kuwa watumishi wote waliokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kupangiwa kazi kwenye Ofisi za Serikali na kipaombele cha kwanza kilikuwa ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuchagua watumishi wanaomfaa kwa ajili ya kuendeleza kazi zilizokuwa zikifanywa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kazi ambayo kwa sasa imekamilika.

  Mhandisi Iyombe amesema mali zilizokuwa zikimilikiwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu yakiwemo majengo ya kibiashara kama vile maduka na ofisi zimeelekezwa zibaki chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma lakini majengo ya makazi yakabidhiwe kwa Wakala wa Majengo Tanzania(TBA)

  ‘’Hatuna lengo la kuidhoofisha Manispaa ya Dodoma lakini Serikali inaangalia wanafaidika nini na nyumba hizo wakati majengo yote ya serikali yanatakiwa kuwa chini ya Wakala wa Majengo Tanzania na wakati huohuo watumishi wote wa Serikali wanahamia Dodoma na hawana maeneo ya kuishi,nyumba zipo zilizokuwa zinamilikiwa na CDA zinapangishwa kwa wapangaji ambao hawalipi pango za nyumba kwa wakati” Amesema Iyombe

  Akifafanua zaidi Mhandisi Iyombe amesema majengo yaliyopo ni 141 kati ya hayo kuna magorofa 45 hivyo familia ambazo zinaweza kuingia katika majengo hayo ni kaya 438 hivyo matarajio ya Serikali ni kwamba watumishi 438 wenye sifa ya kupatiwa nyumba waliopo Dar-es-salaam watapata makazi hapa Dodoma.

  Amesema kuwa nyumba ambazo zinakabidhiwa kwa Wakala wa Majengo ni nyumba za kuishi ambazo awali zilimilikiwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu na kuhamishiwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na kutokana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli nyumba hizo kwa sasa zitakuwa zikimilikiwa na Wakala wa Majengo (TBA) ili nyumba hizo zitumike kwa watumishi wa Serikali wanaohamia Dodoma.

  Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amesema kuwa wamepokea maelekezo ya Serikali ya kukabidhi nyumba za makazi kwa Wakala wa Majengo Tanzania kwa kuwa Dodoma sasa ni Makao Makuu ya Nchi.

  ‘‘Kumekuwepo na changamoto ya makazi kwa watumishi wanaohamia Dodoma lakini nyumba zinazokabidhiwa zipo katika hali ya matumizi na nyingine zinahitaji ukarabati ambao tunadhani wenzetu wa TBA wataendelea nao.

  Wakati huo Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Majengo Tanzania Msanifu Majengo Elius Mwakalinga amesema kuwa kumekuwepo na tatizo kubwa la upatikanaji wa nyumba kwa watumishi wa umma hivyo nyumba 438 zitasaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa nyumba hasa kwa watumishi wanaohamia Dodoma.

  Amesema kuwa kwa Mkoa wa Dodoma Wakala wa majengo,Tanzania (TBA) ilikuwa na nyumba zaidi ya 400 ambazo zilikuwa kwenye maeneo ya Area D na Kisasa hivyo kwa nyumba hizo sasa watakuwa na jumla ya nyumba zaidi ya 800.


  Amesema pia mbali ya nyumba hizo, ‘’Wakala wa Majengo Tanzania inampango wa kujenga nyumba 100 Mkoani Dodoma kwa mwaka huu na wanategemea ndani ya miaka miwili kukamilisha ujenzi wa nyumba 500 hivyo watajitahidi kuhakikisha nyumba hizo zinakamilika ili kuondoa upungufu wa nyumba kwa watumishi wanaohamia makao makuu ya nchi.

  0 0

  Na Mathias Canal, Kilimanjaro

  Wakulima wa mazao ya jamii ya mikunde hususani maharagwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro wamesifu mbegu bora aina ya Lyamungo 90, Jesca na Uyole Njano zinazotolewa kwa wakulima na Taasisi ya Kimataifa ya utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia Mradi wa N2AFRICA.

  Mradi huo unaotekelezwa kwa wakulima 11 katika vijiji sita vya Wilaya hiyo umekuwa na mafanikio makubwa kwao kutokana na mafunzo waliyopatiwa ya kulima kisasa kwa kutumia mbegu kidogo na mavuno makubwa pamoja na kutumia mbolea. 

  Wakulima hao wanasema awali kabla ya mradi huo walikuwa wanalima kwa kuchanganya zaidi ya mazao ya aina mbili tofauti katika shamba moja, kutotumia mbolea na kulima pasipo kufuata njia za kitaalamu jambo ambalo liliwapelekea kupata mazao kidogo ambayo hayakuwa na ufanisi mkubwa katika kuimarisha uchumi wao.

  Wanasema Kupitia mbinu bora walizojifunza kwa wataalamu kutoka katika Mradi wa N2AFRICA wamebadili mfumo wa maisha kwani kwa sasa wanapata mazao ya kutosha na kuwafanya kuhamia katika kilimo chenya tija kwa ajili ya chakula na biashara.

  Janeth Godwin Shao, Achibold Masimba, Mary Mbuya na Fredy Urio wakazi wa kijiji cha Kiruweni , Elizabeth Paschal,na Ester Mbando wakazi wa kijiji cha Mawanjeni Kata ya Mwika Kusini wanasema kabla ya Mradi wa N2AFRICA walikuwa wanapanda mazao shambani badala ya kupanda mbegu jambo lililofifisha upatikanaji wa mazao mengi.

  Waliomba mradi huo kuongeza zaidi ufanisi baada ya kufanikiwa katika kuwanufaisha wakulima kupitia zao la maharagwe sasa waongeze mafunzo kwa wakulima ili kutoa mbegu za mazao mengine kama vile kunde na choroko.

  Moja ya malengo muhimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, ni kuitoa Tanzania katika kundi la nchi masikini zaidi duniani  na kujenga uwezo zaidi wa kiuchumi kupitia kilimo utakaoifanya iwe miongoni mwa nchi zenye kipato cha kati kimataifa.

  Mtaalamu wa Kilimo katika Kijiji cha Mawanjeni Kata ya Mwika Kusini Elizabeth Josiah alisema kwa sasa Zao la maharagwe linapendwa na wakulima wengi kwa sababu linachukua muda mfupi kukomaa, halina gharama kubwa katika uzalishaji wake na lina bei nzuri sokoni karibu nyakati zote hata wakati wa mavuno (yaani msimu wake). 

  Alisema kuwa Mkulima anaweza kulima maharagwe kwa matumizi ya chakula nyumbani kwake au kwa biashara reja reja au kwa jumla.

  Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Kata ya Mwika Kusini Wilfred Ngile alisema Urahisi wa kulima maharage na faida zake lukuki ni kivutio kwa watu wengi sana kwa sasa huku akisema kuwa lakini bila kufuata muongozo wa kitaalam ni ndoto kwa mkulima kupata mavuno anayotarajia.

  Alisema mafanikio wanayoyapata wakulima sio ya wataalamu bali ni mafanikio yao wenyewe kutokana na kutumia njia bora kutokana na maelekezo wanayoyapata kutoka kwa wataalamu.

  Aidha, aliongeza kuwa mafanikio hayo yanatokana na Mbegu bora zilizofanyiwa tafiti na Taasisi ya Kimataifa ya utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiko (IITA) na kutambulika kisheria ambazo ni pamoja na Uyole Njano, Lyamungu 90, na Jesca.

  Naye Afisa Mazao wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini Bi Joyce Kessy alizitaja changamoto zinazowakabili wakulima kuwa ni pamoja na uzalishaji mdogo kwani wanazalisha chini ya tani moja kwa hekta ambapo unachangiwa na sababu za kurudia mbegu, kutotumia mbegu za viwandani, kupanda bila kuacha nafasi, na kupanda zao moja kwa kuchanganya na mazao mengine.

  Hata hivyo alisema kuwa mara baada ya Mradi wa N2AFRICA kuanzishwa katika Wilaya ya Moshi Vijijini hamasa imekuwa kubwa kwa wananchi kuhitaji mbegu na mbolea kutoka taasisi ya IIAT hivyo ameiomba taasisi hiyo kuongeza utoaji wa mbegu kwa wakulima wote na kutoa mafunzo.

  Alisema kuwa mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha  sekta ya kilimo nchini Tanzania jambo ambalo limerahisisha utendaji wa serikali kupitia Wizara ya Kilimo.

  Alisema kuwa wakulima wanajifunza zaidi kwa vitendo kuliko nadharia hivyo aliiomba Taasisi hiyo ya IITA kupitia Mradi wa N2AFRICA kuvifikia vijiji vyote na kuwanufaisha wananchi kwa mafunzo ya vitendo zaidi.

  Katika awamu ya kwanza ya Mradi huu ilianzishwa mwaka 2009 na kutekelezwa katika nchini DR Congo, Ghana, Kenya, Liberia, Malawi, Nigeria, Rwanda, Sierra Leone na Zimbabwe ambapo  Awamu ya pili ilianza Januari 2014 na kufanyika katika nchi tano za Ethiopia, Ghana, Nigeria, Tanzania, na Uganda.

  Janeth Godwin mkulima wa maharagwe Kijiji cha Kireweni Kata ya Mwika Kusini akielezea jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia mradi wa N2AFRICA
  Wakulima wa zao la maharagwe walipowapokea wataalamu kutoka IITA katika kata ya Mwika Kusini, Wilaya ya Moshi Vijijini
   Achibold Masimba mkulima wa maharagwe Kijiji cha Kireweni Kata ya Mwika Kusini akielezea jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia mradi wa N2AFRICA
   Elizabeth Paschal mkulima wa maharagwe Kijiji cha Kireweni Kata ya Mwika Kusini akielezea jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia mradi wa N2AFRICA
  Mtaalamu wa kilimo kijiji cha Mawanjeni Kata ya Mwika kusini Elizabeth Josiah akielezea jinsi wakulima wanavyonufaika na kilimo cha maharagwe
  Ester Mbando (kulia) Mkulima wa maharagwe Kijiji cha Mawanjeni Kata ya Mwika Kusini akielezea jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia mradi wa N2AFRICA
  Mkulima wa zao la maharagwe Kamili Minja akionyesha jinsi alivyonufaika na kilimo cha maharagwe na hatimaye kununua mbuzi saba wa maziwa.
  Mkulima wa zao la maharagwe Joseph Towo kutoka Kijiji cha Rauya Kata ya Marangu Mashariki akielezea jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia mradi wa N2AFRICA
  Wanufaika wa mradi wa N2AFRICA wakielezea namna walivyonufaika na kilimo cha maharagwe
  Fredy Urio akisimulia changamoto alizokabiliana nazo kabla ya mradi huwa kuwasili kijijini kwao na kuwa na manufaa kwa wakulima
  Afisa kilimo Kata ya Mwika kusini Wilfred Ngileakielezea jinsi wakulima walivyonufaika na Mradi wa N2AFRICA katika kata hiyo
  Mkulima wa zao la maharagwe Kamili Minja akionyesha jinsi alivyonufaika na kilimo cha maharagwe na hatimaye kununua mbuzi saba wa maziwa.
  Mkulima wa zao la maharagwe Kamili Minja akielezea jinsi alivyonufaika na kilimo cha maharagwe na hatimaye kununua mbuzi saba wa maziwa. Wengine ni wataalamu kutoka IITA na Mhariri wa Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Ndg Mathias Canal
  Mkulima wa zao la maharagwe Kamili Minja akionyesha shamba lake jinsi lilivyostawi kutokana na mafunzo ya kilimo bora kwa kutumia mbegu bora za maharagwe

  0 0   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akisaini Mkataba wa Makubaliano kati ya Tanzania na Afrika Kusini wa namna ya kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kwa lengo la kukusanya, kuhifadhi, kuendeleza na kuzitunza urithi huo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo mjini Dodoma jana Tarehe 19 Septemba 2017. Kushoto ni Waziri wa Sanaa na Utamaduni, Afrika Kusini Mhe. Nathi Mthethwa.
  03
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akibadilishana Mkataba wa makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika na  Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika Kusini Mhe. Nathi Mthethwa mara baada ya kusaini mkataba huo mjini Dodoma jana Tarehe 19 Septemba 2017.
  04
  Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na viongozi kutoka Tanzania na Afrika Kusini waliohudhuria hafla ya utiaji saini Mkataba wa Makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika mjini Dodoma jana Tarehe 19 Septemba 2017.
  05
  Waziri wa Sanaa na Utamaduni, Afrika Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akiongea na viongozi kutoka Tanzania na Afrika Kusini waliohudhuria hafla ya utiaji saini Mkataba wa Makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika mjini Dodoma.
  06
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akitambulisha wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria hafla ya utiaji saini Mkataba wa Makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika mjini Dodoma.
  07
  Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimpokea mgeni wake Waziri wa Sanaa na Utamaduni, Afrika Kusini Mhe. Nathi Mthethwaalipowasili Uwanja wa ndege mjini Dodoma jana Tarehe 19 Septemba 2017. Zizra hiyo inalengo la kusaini Mkataba wa Makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara kati ya Afrika Tanzania na Afrika Kusini.
  (Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma)

  0 0


  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo ya shule ya wasichana Dakawa kutoka kwa Makamu Mkuu wa shule hiyo.
  IMG-20170920-WA0091
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua miundombinu ya Shule ya sekondari ya wasichana Dakawa.
  IMG-20170920-WA0092
  Wanafunzi wa shule ya wasichana Dakawa wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipokuwa akizungumza nao.
  IMG-20170920-WA0093
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na baadhi ya walimu wa shule ya sekondari ya wasichana Dakawa wakati akifanya ukaguzi wa majengo ya shule hiyo.
  ………………..
  WANAFUNZI wa kidato cha sita katika sekondari ya wasichana Dakawa iliyopo mkoani Morogoro wamepania kuwashangaza watanzania katika matokeo ya mwaka ujao ya kidato cha sita kwa kuifanya shule hiyo kwa miongoni kwa shule 20 bora kitaifa baada ya matokeo yao.

  Wasichana hao wametoa  kauli hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Saidi Jafo alipofanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo ili kujionea mazingira halisi ya kufundishia na kujifunzia.

  Shule hiyo kwa mwaka huu ilikuwa katika nafasi ya 69 kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita.

  Kutokana na hali hiyo, Naibu Waziri huyo aliamua kufanya ziara hiyo kushtukiza ili aweze kubaini kama kuna changamoto kubwa  zinazo wakabili wanafunzi katika shule hiyo kwa kuwa ni shule ya wasichana pekee.“Nimeona nije kujionea mwenyewe kama mambo mazito yana wakwaza ambayo yanaweza kumkwamisha mtoto wa kike asipate elimu inayo tarajiwa,”amesema Jafo 

  Katika ziara hiyo, Jafo alifanya ukaguzi wa madarasa, mabweni, nyumba za walimu, jiko, vyoo, maktaba, na bwalo la Chakula.Jafo aliwaambia walimu na wanafunzi kwamba serikali ipo katika mpango kabambe wa shule zote kongwe hapa nchini ili ziwe na mazingira mazuri ya utoaji wa elimu bora hapa nchini.

  Aidha Naibu Waziri huyo ameonesha kufurahishwa na suala la utunzaji wa mazingira ya shule ambapo wanafunzi na maeneo yote ya shule ni safi na yanavutia. Naibu Waziri Jafo anaendelea na ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya barabara, afya, Elimu, Maji na kuzungumza na watumishi katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Songwe na Tabora.

  0 0

   Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Charles Paranjo wakifurahi na baadhi ya wawakilishi wa mashirika ya umoja wa Mataifa baada ya kuzindua programu ya pamoja ya Kigoma
   Wawakilishi wa shirika la FAO wakishirikiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma wakikabidhi zana za kilimo wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu kwaajili ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya Kigoma
   Wawakilishi wa shirika la kimataifa la UNESCO wakikabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa utekelezaji wa programu ya pamoja Kigoma. 
  Mgeni rasmi katika uzinduzi wa programu ya pamoja Kigoma Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Charles Paranjo akisoma risala yake kwenye viwanja vya soko la umoja katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilayani Kasulu. 
   Rais wa kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilayani Kasulu Abilola Angelique akiongea neno la shukrani baada ya uzinduzi wa programu ya pamoja ya Kigoma
   Kikundi cha ngoma ya asili kutoka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wakitumbuiza ngoma ya asili ya kabila la warundi wakati wa uzinduzi wa programu ya pamoja ya Kigoma

  Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii,Kigoma

  MASHIRIKA 16 ya umoja wa Mataifa yamezindua programu ya pamoja mkoani Kigoma, ikiwa ni mpango wa pamoja utakaohusisha sekta mbalimbali kwa lengo la kuimarisha maendeleo na usalama kwa watu wa Kigoma.

  Akiongea katika hafla hiyo ya uzinduzi wa programu hiyo iliyofanyika katika viwanja vya soko la pamoja lililopo katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilayani Kasulu ,Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Charles Paranjo alisema kuwa mpango wa programu ya pamoja utatumia njia kamilifu kutatua masuala mbalimbali yanayowakabili wakimbizi,wahamiaji pamoja na jamii za wenyeji wanaoishi Mkoa humo.

  Paranjo alisema kuwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma wamekuwa wakiishi na wakimbizi kwa kipindi cha muda mrefu hivyo kupitia programu hiyo na wao watanufaika.Alisema ingiwa programu hiyo ilianza Julai 1 2017 lakini uzinduzi rasmi umefanyika leo pia mpango huu utadumu kwa muda wa miaka minne.

  Mkuu wa mahusiano kutoka ubalozi wa Norway Trygue Bendiksy alisema kuwa mpango huo una bajeti ya dola za kimarekani milioni 55,ambapo mpaka sasa kiasi cha dola milioni 12 kati ya hizo tayari zimeshapatikana hivyo aliwaomba wadau kuendelea kujitokeza kusaidia ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa katika programu hiyo.

  Alisema mashirika hayo 16 ya umoja wa mataifa katika programu hiyo watashirikiana katika nyana za nishati na mazingira endelevu,uwezeshwaji wa kiuchumi wa vijana na wanawake,vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,elimu inayolenga wasichana wenye umri wa kuvunja ungo,maji safi pamoja na kilimo.

  Mkuu wa kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Abiudi Saidaye alisema hivi sasa kambini hiyo ina jumla wakimbizi na waomba hifadhi 143608 kutoka nchi ya Burundi na Congo.Alisema mpango wa programu wa pamoja ya Kigoma utasaidia kutatua masuala mbalimbali yanayowakabili wakimbizi ikiwa ni sambamba na kuwaendeleza kimaendeleo.

  Rais wa wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu Abilola Angelique kwa niaba ya wakimbizi na waomba hifadhi wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na umoja wa Mataifa kwa kitendo cha kuwapokea na kuwahudimia kwa kipindi chote walichokuwa nchini.


  0 0

  DAR ES SALAAM.
   
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Amina Makillagi, amewataka wagombea na wajumbe wote wa mikutano mikuu ya wilaya kwenye Uchaguzi wa jumuiya hiyo ngazi ya wilaya utakaofanyika leo, tarehe 21/9/2017 kuzingatia maadili ya Chama na UWT.

   "Kubwa ni kutotoa wala kupokea rushwa. UWT imejiandaa vizuri kuhakikisha inafuatilia nyendo zozote ovu zitakazojitokeza katika Uchaguzi.

   Mgombea yeyote atakayetoa rushwa atachukuliwa hatua za kinidhamu kabla na baada ya Uchaguzi kuisha ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nafasi ya uongozi iliyopatikana kwa mazingira tatanishi", amesema Makilagi. 

  Makillagi ambaye amewatakia uchaguzi mwema wanachama wote wa UWT, amesisitiza kuwa rushwa haitavumilika na kwa mjumbe yeyote atakayepokea rushwa na kwamba kanuni zilizopo zitamuwajibisha ipasavyo.


  0 0


  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimpa maelekezo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel (kushoto) ambayo inajenga mradi wa bweni na ukumbi wa mihadhara katika Chuo cha Misitu Olmotonyi alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha. Aliitaka kampuni hiyo iharakishe kumaliza ujenzi wa mradi huo.

  Na Hamza Temba - WMU
  .................................................................
  Chuo cha Misitu Olmotonyi kilichopo mkoani Arusha kimetakiwa kuboresha taaluma na mitaala ya kufundishia iweze kukidhi mahitaji ya jamii ya sasa na ijayo ikiwemo kujibu kero na changamoto zinazoikabili jamii hiyo.  Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipotembelea chuo hicho jana kwa ajili kukagua maendeleo yake na kuzungumza na waalimu pamoja na wafanyakazi ambapo pia alikagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayojengwa chuoni hapo ikiwemo ya bweni na ukumbi wa mihadhara.


  Alisema Tanzania ya leo inahitaji wataalamu watakaojibu kero na kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya uhifadhi nchini ikiwemo ya uharibifu wa misitu kwa njia ya uchomaji wa mkaa, uvunaji haramu wa magogo na vitendo vya uingizaji wa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi nchini. 

  "Ni lazima muwafundishe wanafunzi wenu uaminifu na uzalendo wa kutumia rasilimali za misitu kwa njia endelevu, muwafundishe uhifadhi zaidi na sio uvunaji pamoja kutumia sheria ipasavyo katika kulinda na kusimamia rasilimali hizi huku wakitambua kuwa rasilimali hizo zikitoweka hakuna maisha kutokana na umuhimu wake katika maisha ya binadamu" alisema Prof. Maghembe.

  Pamoja na hayo, alikitaka chuo hicho kujiimarisha zaidi katika mafunzo kwa vitendo kufikia viwango bora vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na kuendeleza waalimu kitaaluma kwa kutumia fursa mbalimbali ikiwemo za mafunzo ya nje ya nchi kwa mfumo wa "Scholarships". 

  Aidha, alikitaka pia chuo hicho kujikita zaidi katika utoaji wa huduma kwa jamii katika sekta ya misitu pamoja na kuanzisha na kuimarisha programu mbalimbali za utafiti ambazo pamoja na faida nyingine pia zitakitangaza chuo hicho ndani na nje ya nchi.

  Katika hatua nyingine, Prof. Maghembe amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel kukamilisha haraka ujenzi unaoendelea wa jengo la bweni na ukumbi wa mihadhara chuoni hapo. Ujenzi huo upo chini ya mradi wa ECOPRC na jengo la bweni litakua na uwezo wa kuchukua wanafunzi 100 na ukumbi wa mihadhara wanafunzi 200. 


  Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Christognus Haule alisema, chuo hicho kinatoa mafunzo ya misitu na hifadhi ya mazingira kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada pamoja na mafunzo ya muda mfupi. Pia kinatoa huduma za ushauri na utafiti wa misitu na hifadhi ya mazingira.

  Akizungumzia udahili wa wanafunzi chuoni hapo alisema umekua ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo katika mwaka wa fedha 2015/2016 idadi hiyo imeongezeka kutoka 499 na kufikia 595 mwaka 2016/2017. Alisema kwa mwaka ujao 2017/2018 wanategemea kupata wanafunzi wengi zaidi kufikia 650.

  Chuo cha Misitu Olmotonyi ni chuo cha Serikali ambacho kilianzishwa mwaka 1937 na kinasimamiwa na Wizara ya Maliasili kwa ajili ya kutoa mafunzo ya misitu na hifadhi ya mazingira. Chuo hicho kwa sasa kina waalimu 21 wa ngazi tofauti.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel ambayo inajenga jengo la bweni na ukumbi wa mihadhara katika Chuo cha Misitu Olmotonyi kuhusu maendeleo ya mradi huo alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha. Aliitaka kampuni hiyo iharakishe kumaliza ujenzi wa mradi huo. 

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Chuo cha Misitu Olmotonyi  Mkoani Arusha jana ambapo alitoa maelekezo mbalimbali na ushauri wa kuboresha chuo hicho. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Christognus Haule. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi Mkoani Arusha alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo jana ambapo alitoa maelekezo na ushauri wa namna ya kuboresha chuo hicho. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na waalimu na wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi mkoani Arusha jana . Kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho, Christognus Haule.

  Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia waliokaa) na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi.

   Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia waliokaa) na baadhi ya waalimu wa Chuo cha Misitu Olmotonyi.
  Ujenzi bweni la wanafunzi chuoni hapo ukiwa unaendelea chini ya mradi wa ECOPRC. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel (kulia) ambayo inajenga jengo la bweni na ukumbi wa mihadhara katika Chuo cha Misitu Olmotonyi kuhusu maendeleo ya mradi huo alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha. Aliitaka kampuni hiyo iharakishe kumaliza ujenzi wa mradi huo.
  Jengo la vukumbi wa mihadhara  (Lecture Theatre) ambalo linaendelea kujengwa chuoni hapo kupitia mradi mradi wa ECOPRC.


  Baadhi ya waalimu na wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi wakisikiliza maelekezo mbalimbali kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (hayupo pichani) alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha. 

  0 0

  "Serikali yasema ipo tayari kugharamia matibabu zaidi ya Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Antiphas Lissu popote Duniani, pindi itakapopata maombi kutoka kwa familia pamoja na taarifa kutoka kwa madaktari kuhusu mahitaji ya matibabu zaidi ya mgonjwa",Waziri Ummy Mwalimu

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akipanda mti na Mwanafunzi wa darasa la tano wa Shule ya Msingi Segera, Jackson Lusajo, wakati alipotembelea shule hiyo kukabidhi Vifaa vya ukarabati wa shule hiyo akiwa katika ziara yake Wilaya ya Rungwe jana Sept 20, 2017. Jumla ya miti 160 ilipandwa katika shule hiyo ikiwa ni sehemu ya kutunza mazingira. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO MEDIA)
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tukuyu, Ezekiel Manyemele, wakifunua kitambaa kuzindua Jengo la Choo cha wanawake katika Hospitali ya Makandana Wilayani Rungwe, jana Sept 20, 2017. Jengo hilo la Choo limegharimu zaidi ya Sh. milioni 50. 
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akipanda mti na Mwanafunzi wa darasa la Sita wa Shule ya Msingi Segera, Tunza Fred, wakati alipotembelea shule hiyo kukabidhi Vifaa vya ukarabati wa shule hiyo akiwa katika ziara yake Wilaya ya Rungwe jana Sept 20, 2017. Jumla ya miti 160 ilipandwa katika shule hiyo ikiwa ni sehemu ya kutunza mazingira.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akiangalia tofali, wakati alipotembelea shule ya Msingi Segera kukabidhi Vifaa vya ukarabati wa shule hiyo akiwa katika ziara yake Wilaya ya Rungwe.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akimkabidhi tofali, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Segera, Fred Mfwea (wa pili kulia) na Diwani wa Kata ya Segera (katikati) wakati alipotembelea shuleni hapo kukabidhi Vifaa vya ukarabati wa shule hiyo akiwa katika ziara yake Wilaya ya Rungwe.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akicheza muziki 'Ndiyo Maana Tenzele' wa asili wa kabila la Wasafa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Unyamwange, Julius Pascal, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya akiangalisha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha afya Kata ya Isongole jana.
   Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Makandana
   Akikagua jengo hilo ndani
   Akizungumza na kina mama wa Rungwe
   Akisalimiana na mwanafunzi Tunza..
   Mwanafunzi akimwagilia mti baada ya kupanda
   Dkt. Tulia akitembelea kukagua madarasa ya shule ya Segera
   Mwalimu mkuu wa shule hiyo akizungumza
   Vijana wa Taasisi ya Tulia Trust
   Walimu na wanachi wa shule hiyi wakisikiliza hotuba ya Dkt. Tulia.
   Dkt. Tulia akizungumza
   Dkt. Tulia akipokea mchango wa pesa Sh. 300,000 kutoka kwa mkurugenzi wa Patrick Mission High School, Ndele Mwaselela, ambaye pia akitoa ahadi ya kuchangia bando 10 za mabati kwa shule hiyo.
   Akitoa zawadi ya hela kwa wanafunzi wa shule hiyo kwa ajili ya sukari
   Dkt. Tulia akikabidhi fedha hizo kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo
  Dkt. Tulia akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa mwalimu wa shule hiyo, Caroline Kilongo. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO MEDIA)

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini zikiwemo wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.

  Amesema Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

  Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumatano, Septemba 20, 2017) alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Chemba na Kondoa waliomsimamisha katika maeneo ya Chemba, Kalema, Bicha na Bereko akiwa njianu kuelekea mkoani Arusha kwa shughuli za kikazi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Chemba mkoani Dodoma wakati alipolazimika kusimama baada ya kuona umati mkubwa wa wananchi hao waliokuwa wakimsubiri alipokuwa akisafiri kwa Barbara kwenda Arusha akitoka Dodoma Septemba 20, 2017.

  Alisema kwa sasa Serikali imeendelea na uchumbaji wa visima virefu, vifupi pamoja na kuweka mtandao wa mabomba ya kusamba maji katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo na ya wilaya hizo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo karibu na makazi yao.

  Pia Waziri Mkuu alisema wananchi wanatakiwa wazingatie sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60 ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.

  Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wawachukulie hatua watu wote watakaokutwa wakiendesha shughuli mbalimbali kama za kilimo, ujenzi wa makazi na uchungaji wa mifugo ndani ya vyanzo vya maji kwa kuwa zinasababisha ukame.

  Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa nishati ya umeme, Waziri Mkuu alisema hakuna kijiji nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa huduma hiyo katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kalema wilayani Chemba wakati alipolazimika kusimama baada ya kuona umati mkubwa wa wananchi hao waliokuwa wakimsubiri alipokuwa akisafiri kwa Barbara kwenda Arusha akitoka Dodoma Septemba 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Ameagiza wakandarasi wamalize maeneo yaliyosalia katika REA awamu ya pili ndipo waendelee na awamu ya tatu. Alisema Serikali imetenga sh. trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo.

  “Rais wetu Dkt. John Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na vya wilaya za Chemba na Kondoa. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”

  Pia Waziri Mkuu alisema  mwananchi hawatowajibika tena katika kulipia nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

  Waziri Mkuu aliongeza kwamba  lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na kwa vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi.

  Awali mbunge wa Chemba, Bw. Juma Nkamia, Mbunge wa Kondoa Mjini Bw. Edwin Sanda na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji ambaye ni Mbunge wa Kondoa Vijijini waliomba Serikali iwasaidie katika kutatua kero ya maji na umeme.

  Walisema katika maeneo mbalimbali ya majimbo yao wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya umeme pamoja na maji safi na salama hivyo kusababisha wananchi kushindwa kushiriki vema kwenye shughuli za kimaendeleo.

  0 0

   Meneja wa kituo cha Nitetee Foundation, Johaness Emmanuel akipokea hundi ya sh. 1,260,000 za malipo ya mchango wa uanachama wa bima ya afya kwa watoto 25 wa kituo hicho kutoka kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana, kulia mwenye kinasa sauti ni Mwenyekiti wa Taasisi ya The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania Sibtain Meghjee ambayo imetoa fedha hizo kwa kituo hicho na Karibu Foundation.Kulia mwenye shati ya draft ni Meneja Matekelezo wa NHIF Mkoa wa Mwanza Calistus Mpangala. Picha ya Baltazar Mashaka.
   Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Mkoa wa Mwanza, Castus Mpangala akitoa ufafanuzi wa huduma zinazotolewa na mfuko huo kwa wananchi waliohudhuria semina ya bima ya afya iliyoandaliwa na Taasisi ya The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania ili kuwahamasisha  kujiunga na mfuko huo kwa ajili ya kupata matibabu kwa gharama nafuu. Semina hiyo ilifanyika jijini Mwanza.
   Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella mwenye kofia akiwa ameshika moja ya mashuka yaliyotolewa msaada na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Mkoa wa Mwanza kwa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe. Wa tatu kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dk.Leonard Subi, Meneja wa mfuko huo mkoani Mwanza Dk. Mohamed Kilolile wanne kulia na  kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Uekerewe Estomiah Chang'a.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella (mwenye kofia) hivi karibuni akinunua samaki aina ya Furu kutoka kwa akinamama wachuuzi wa samaki katika Soko la Kakukulu lililopo wilayani Ukerewe. Mkuu huyo wa Mkoa alikuwa wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali. Picha na Baltazar Mashaka.

  NA BALTAZAR MASHAKA,MWANZA

  TAASISI ya The Desk & Chair Foundation (TD&CF) imekabidhi hundi mbili zenye thamani ya zaidi sh. 2.5 kwa vituo vya Karibu Foundation na Nitetee Foundation ili kuwawezesha  watoto 50 wanaolelewa kwenye vituo hivyo kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF).

  Akizungumza jana baada ya kukabidhi hundi hizo Mwenyekiti wa TD & CF Sibtain Meghjee alisema fedha hizo zitatumika kugharamia matibabu ya watoto hao kwa kipindi cha mwaka mmoja.

  “ Watoto wanaolelewa kwenye vituo vya Nitetee Foundation na Karibu Foundation,  wengi wao wanatoka kwenye familia duni na wanaishi katika mazingira magumu.Tumeona tuwasaidie kwa kuwakinga na magonjwa kwa kuwalipia mchango wa uanachama wa Bima ya Afya wa sh. 54,000 utakaomuwezesha mtoto kutibiwa kwa mwaka mzima ambapo kila kituo kimepewa sh. 1, 260,000 kwa ajili ya watoto 25 ambao wamesajiliwa tayari, ”alisema.

  Meghjee alisema kuwa mbali na vituo hivyo taasisi Bilal Muslim Mission of Tanzania pia itapewa msaada huo wa fedha sh. 1,260,000 kwa watu 50 wasio na uwezo ili wajiuge  na mfuko wa NHIF lakini pia The Deskk & Chair nayo itawafadhili watu 50 kwa kuwalipia gharama matibabu kwenye mfuko huo.

  Hata hivyo, alivishauri vyombo vya habari viteo fursa kwa kutangaza mambo mazuri ya heri kwenye kurasa za mbele za magazeti badala ya kuwalisha sumu wasomaji inayotokana na habari za migororo ambazo huchukua nafasi kubwa kwenye kurasa za mbele za magazeti.

  “ Mkituletea changamoto za wananchi tukazitatua kunairahisishia serikali kuwafikia na itasaidia kuondoa hofu iliyopo baina ya serikali na wananchi dhidi ya Uislamu maana sisi tunaamini uovu hauna nafasi kwa dini yoyote.Niombe magazeti mambo mema na mazuri yatangazwe kwenye kurasa za mbele badala ya mambo mabaya na ya migogoro tu,”alishauri Meghjee.    

  Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo Meneja wa Nitetee Foundation Johaness Emmanuel alisema dhana yao ni kuendelea kuielimisha jamii katika ngazi ya familia ili kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ili kuwe na jamii ya watu salama na Tanzania salama isiyo na vitendo vya ukatili.

  “Ipo dhana kuwa wamiliki wa vituo vya kulea watoto wanajinufaisha kupitia vituo hivyo na vipo kwa maslahi binafsi badala ya watoto.Dhana hiyo ni potofu na ndio maana tunapambana kwa kuelimishaa jamii kupitia vipeperushi, magazeti na vipindi vya televiesheni ili tuwe na jamii ya watu salama bila ukatili,”alisema Emmanuel.

  Kwa upande wake, Asumpta Ngatunga wa Karibu Foundation alieleza kuwa ili kupunguza na kutokomeza ukatili  wana mikakati ya kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwenye jamii ili kuoinga vitendo hivyo.

  Aidha, Meneja Matekelezo wa NHIF Mkoa wa Mwanza Calistus Mpangala asilimia 31 ya Watanzania wamejiunga na mfuko huo ingawa kuna changamoto za baadhi ya watoa huduma kutowahudumia vizuri wanachama wa mfuko huo.

  Alisema NHIF iko mbioni kuajiri wataalamu watakaokuwa wakiratibu huduma zinazotolewa kwenye baadhi ya vituo na hospitali zinazowahudumia wanachama wa mfuko huo na kuhakikisha zinatoa huduma nzuri ili kuondoa malalamiko. 

  Mpangala aliongeza kuwa NHIF imeingia mkataba na watoa huduma mbalimbali ambao malipoya madai yao hulipwa ndani ya siku 60 na hivyo lipo tatizo kwa baadhi yao kuchelewesha madai yao ili yahakikiwe kabla ya malipo kufanyika na hao ndiyo wanaotoa huduma mbaya kwa wanachama wa mfuko.

  0 0

   JESHI la Polisi  Mkoa wa Pwani  wamewakamata watuhumiwa wawili  ambao wameshikwa  wakisafirisha  dawa za kulevya  aina ya Bhangi  magunia nane.
   Watuhumiwa hao walionaswa  na Jeshi la Polisi wamefahamika  kwa  mjina Abraham Michael  mwenye umri wa miaka  31 mkaazi wa Jijini Dar es Salaam na Godfrey  Malakasuka  mwenye umri wa miaka 21 mkaazi wa Kimara  waliokamatwa katika eneo la Ubena Zomozi wakitokea Mkoani Morogoro kuelekea Jijini Dar es Salamaa.
  Akizungumza na  waandishi wa habari  Kamanda wa Mkoa wa Pwani ACP Jonathan Shanna  alisema kuwa watuhumiwa  wamekamatwa na vidhibiti  hivyo wanastahili  kupata adhabu kali pindi watakapofikishwa  mahakamani.

  0 0

   Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Cheil Engineering Bw. Shin Soo akimueleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4. Kushoto ni Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale.
   Mafundi wa Kampuni ya M/S Hanil-Jiangsu J/V wakiendelea na ujenzi wa moja kati ya madaraja makubwa saba yanayojengwa katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4.
   Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) hatua mbalimbali za maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), wakati Waziri huyo alipoikagua, mkoani Arusha.
   Moja kati ya madaraja saba yanayojengwa katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4, jijini Arusha.
   Tingatinga likiendelea na kazi ya ujenzi wa awali ya madaraja katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4, jijini Arusha.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Cheil Engineering Bw. Shin Soo (katikati)alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4 jijini Arusha.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ametoa wito kwa wakazi wa Arusha kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/S Hanil-Jiangsu J/V ili kuweza kukamilisha kwa wakati ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4.

  Akikagua mradi wa ujenzi wa barabara hiyo mkoani humo, Profesa Mbarawa amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutapunguza msongamano wa magari katikati ya jiji hilo na hivyo kuvutia watalii na kukuza uchumi wa mkoa.

  "Kukamilika kwa barabara hii ya Arusha bypass kutapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano kwani magari makubwa ya mizigo yatatumia mchepuo huu na kurahisisha huduma za usafirishaji jijini Arusha", amesema Waziri Mbarawa.Ameongeza kuwa Wizara yake itasimamia kwa ukaribu ujenzi wa barabara hiyo ili ikamilike kwa wakati uliopangwa na viwango vinavyostahili vilivyokubalika.

  Aidha, Prof. Mbarawa ameupongeza Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo kwa usimamizi mzuri wa barabara ya Sakina-Tengeru KM 14.1 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na kusisitiza kuitunza barabara hiyo ili idumu kwa muda uliopangwa.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Barabara wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Eng. Ven Ndyamukama, amesema Wizara kwa kushirikiana na TANROADS itaendelea kuhakikisha barabara na madaraja yote nchini yanajengwa kwa viwango vilivyopo kwenye usanifu wa kina (Detail design), na thamani ya fedha inapatikana.

  Naye, Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuendelea kumsimamia mkandarasi huyo ili akamilishe mradi kwa wakati kama walivyokamilisha ujenzi wa barabara ya Sakina-Tengeru KM 14.1 na kwa ubora unaostahili.

  Mhandisi Kalupale, ameeleza changamoto zinazoikabili barabara hiyo kuwa ni wingi wa  udongo wa tifutifu na  mfinyanzi na hivyo kulazimu Usanifu wa kina wa barabara hiyo kurudiwa upya.

  Ujenzi wa Barabara ya Arusha bypass unatarajiwa kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 67 ikiwa ni ushirikiano wa fedha za Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania na ujenzi wake utahusisha madaraja makubwa 7, maboksi kalvari 55 na madaraja ya bomba 55.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI.

  MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amesitisha mkataba na Kampuni ya Mwamkinga Auction Mart and Brokers iliyokuwa ikifanya kazi ya kudhibiti uegeshaji wa magari katika maeneo yasiyo rasmi kwa Halmashauri ya Temeke na Kigamboni.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mapema leo asubuhi Meya Mwita amesema kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na kampuni hiyo kufanya kazi kwakutozingatia matakwa ya mkataba na hivyo kuanzisha migogoro isiyo ya lazima baina ya halmashauri ya jiji na Wananchi.

  Meya mwita amefafanua kuwa jiji liliingia mkabata na kampuni hiyo Aprili mwaka huu kwa lengo la kufanya kazi hiyo ambapo mkataba huo ulielekeza kufanya kazi kwa weledi mkubwa, kuzingatia sheria, miongozo ,maelekezo, kanuni na taratibu zilizopangiwa bila kusababisha bughudha, uonevu, kero na usumbufu kwa wananchi jambo ambalo halikufanyika.

  “ Hii kampuni imekuwa ikilalamikiwa mno na wananchi, inawasumbua, na sisi kuwapa tenda hii sio kwa ajili ya kuwanyanyasa, kuwasumbua ila ni kufanya kazi kwa weledi”Nakuongeza kuwa” tumefuatilia kwa karibu sana utendaji kazi wao, kutokana na malalamiko ambayo yalikuwa yanatolewa na wananchi, tukajiridhisha, kwa ushahidi uliojitosheleza, hawawezi kunyanyasa watu na mimi kama meya wa jiji hili nikawaachia, hili haliwezekani” amesisitiza Meya Mwita.

  Hata hivyo ameeleza kuwa kampuni hiyo inapaswa kuondoka mara moja kwenye maeneo iliyopangiwa kufanya kazi hiyo na kuhakikisha kwamba katika kuanzia tarehe ambayo mkataba huo umesitishwa iwe imekabidhi mashine zote za kukusanyia mapato kwa halmashauri zikiwa kwenye hali salama.

  Aidha Meya Mwita amesisitiza kuwa hata sita kuzichukulia hatua kampuni nyingine ambazo zimepewa tenda hiyo na kuzionya kuwa iwapo wanatabia hiyo waache mara moja kwani kazi waliyopewa sio ya kusanyanyasa wananchi bali ni kufanya kazi kwa kufuata sheria.

  0 0

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ laanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Meja Jenerali Michael Isamuyo atua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimba na wananchi wa Manyara wafurahi na waahidi ushirikiano.
  Helikopta iliyombeba Meja Jenerali Michael Isamuyo akitua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimba na wananchi wa Manyara wafurahi na waahidi ushirikiano. Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ limenanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

older | 1 | .... | 1373 | 1374 | (Page 1375) | 1376 | 1377 | .... | 1897 | newer