Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1366 | 1367 | (Page 1368) | 1369 | 1370 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi Leseni ya Usajili wa machapisho mwakilishi wa Jarida la PLUS 255 MAGAZINE Bw. Francis Maduhu mara baada ya kukamilisha taratibu za usajili leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi la utoaji wa Leseni kwa machapisho linafuatia utekelezaji wa kifungu namba 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Usajili Bw. Patrick Kipangula.
   Mwakilishi wa Jarida la PLUS 255 MAGAZINE Bw. Francis Maduhu akionyesha Leseni ya machapisho aliyokabidhiwa kwa ajili ya Jarida lake leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi la utoaji wa Leseni za machapisho linafuatia utekelezaji wa kifungu namba 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimpongeza mwakilishi wa Jarida la PLUS 255 MAGAZINE Bw. Francis Maduhu baada ya kumkabidhi Leseni ya Usajili wa machapisho kufuatia kukamilisha taratibu za usajili leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi la utoaji wa Leseni za machapisho linafuatia utekelezaji wa kifungu namba 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Usajili Bw. Patrick Kipangula.

  Picha na: Idara ya Habari - MAELEZO

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba akielezea alivyoshambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na mguuni wakati akiingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
  ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) wakioneshwa na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Brigedia baadhi ya risasi zilizotolewa kwenye mwili wa Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba baada ya kushambuliwa wakati akiingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe, Brigedia Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba na wauguzi wakiomba dua wakiongozwa na Mama Margareth Vicent Mritaba hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa Meja Jenerali Mritaba akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mtoto Nathan Martin wakati akitoka kumjulia hali Meja jenerali Mstaafu Vicent Mritaba aliyelazwa Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwalimu Aloys Konolipa wa Shule ya Msingi Kidugalo wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani alipopita kuwapa pole wagonjwa wengine baada ya kumjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba aliyelazwa Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni wakati akiingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni. Picha na IKULU.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Septemba, 2017 ametembelea hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Jijini Dar es Salaam na kumjulia hali Meja Jen. Mstaafu Vincent Mritaba aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.Meja Jen. Mstaafu Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana tarehe 11 Septemba, 2017 majira ya mchana na kisha kukimbizwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo kwa matibabu.

  Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa Meja Jen. Mstaafu Vincent Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi alizopigwa mkononi, kiunoni na tumboni.Meja Jen. Mstaafu Mritaba amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumjulia hali na kumuombea dua ili apone haraka.

  Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jen. Venance Mabeyo pia ametembelea wodi ya majeruhi na kuwajulia hali wagonjwa wanaotibiwa katika wodi hiyo na baadaye akawasalimu wananchi waliofika hospitali hapo kwa ajili ya kupata matibabu.

  Mhe. Dkt. Magufuli amewapongeza Madaktari wa hospitali ya Jeshi Lugalo kwa huduma za matibabu wanazotoa kwa askari na wananchi wengine na amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.

  0 0

  Na David John Mwanza

  KIJANA Ruyendela Barugali mkazi wa Nyamagana mkoani Mwanza anamuomba rais Dkt. John Magufuli kumsaidia kwani anaishi katika mazingira magumu na amepotezana na mama yake mzazi tangu akiwa mdogo.

  Pia baba yake mzazi alishafariki miaka mingi hivyo anamkumbuka rais Magufuli kwani kuna wakati aliwahi kuzamia na Treni hadi Dar es Salaam ambapo aliwahi kupewa sh 20000 katika eneo la Magomeni wilaya ya kinondoni wakati huo akiwa waziri wa Ujenzi.

  Ruyendera Ameyasema haya leo jijini Mwanza katika eneo la Makoroboi ambapo maisha yake yote yanapatikana hapo ambapo anamiaka kumi analala nje huku akisema hapendezwi na hali hiyo .Amesema kuwa kimsingj hapendi maisha anayoishi na anatamani kuona rais wake John Magufuli anamsoma ili aweze kumsaidia huku akidai kutokana na ngumu aliyonayo anatamani kusoma lakini hayupo mtu wa kumshika mkono.

  "Simjuwi mama yangu niliwahi tu kuwaambiwa kwamba mama yangu anaitwa Zawadi na nasikia anaishi Nyarugusu.na baba yangu mkubwa anaitwa Kanyikalila Mtalemwa anaishi Mganza wilayani chato. "amesema Ruyendela .Pia anasema baba yake alishafariki siku nyingi tangu yeye akiwa mdogo na kudai bahati mbaya aliyonayo hana ndugu wa jamaa hali inayomfanya kuonekana kama mtoto wa mtaani.

  Anasema msaada pekee anaouna ni rais Dtk John Magufuli kwani anasema kwakuwa alishawahi Kumsaidia na akamtaka arudi chato mkoani Geita na akafanya hivyo lakini bahati mbaya mazingira aliyokutana nayo kwa baba yake mkubwa Mzee Kanyikali yalikuwa sio rafiki.

  Pia ameomba viongozi na wadau wengine kujitokeza kumsaidia kwani hata maeneo anayolala anasumbuliwa na polisi kila wakati hali ambayo inamhuzunisha nakusababisha amkumbuke mama yake.

  Kushoto ni Naibu katibu mkuu wa taasisi ya kutetea Haki Za Binadamu Tanzania (TAHURA) akifanya Mahojiano na kijana Ruyendela Barugali.( Kulia),Kijana ambaye anahitaji msaada wa rais Dkt.John Magufuli picha David John.

  0 0

  Na Mwandishi wetu, Tabora.

  MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameteua Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Queen Mlozi kuongoza Kamati aliyoichagua kwa ajili ya kufuatilia viwanda mbalimbali ili kuangalia hali halisi na kama vimeshindwa kufanyakazi viweze kupewa Wawekezaji wengine. Mwanri aliteua Kamati hiyo jana mjini Tabora wakati wa Mkutano na wadau mbalimbali na Mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi cha Tabora.

  Wengine waliochaguliwa ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philipo Ntiba, Afisa Biashara Mkoa Lucas Kusare ambaye ni Katibu wa Kamati, Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Richard Lugomela na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini, Tiganya Vincent.

  Alisema kuwa Kamati hiyo itaanza na Kiwanda cha Nyuzi Tabora ambapo itaangalia mpango kazi wake , itakagua mashine zote kama zinafanyakazi na uwezo wa kifedha wa mwekezaji huyo kama anao mtaji wa kutosha wa kuendesha kiwanda.Mambo mengine yatakayofuatiliwa na Kamati hiyo ni pamoja na kuangalia matatizo ambayo Mwekezaji huyo aliyaeleza kuwa ukosefu wa soko la nyuzi zake kutokana na viwanda ambavyo ndio vilikuwa vikinunua kwake kuanza kuagiza toka nje bidhaa hizo.

  Mkuu huyo Mkoa aliongeza kuwa mambo mengine ambayo Kamati itayafanya ni kuangalia fursa za masoko ya bidhaa za Kiwanda hicho kama vile Bohari Kuu za Dawa (MSD), Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU) na wafanyabiashara wengine wanaweza kununua bidhaa zake.Alisema kuwa Kamati hiyo itatakiwa kila baada ya siku tatu impelekee taarifa ya maendeleo ya kazi yao.

  Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ametoa mwezi mmoja kwa Mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora kuhakikisha mashine zake zinafanyakazi.Alisema kuwa baada ya kipindi kuisha atakwenda kukagua na akikuta hakuna kitu atalazimika kumuomba Waziri wa Viwanda aje kuchukua hatua ikiwemo kumpa mwekezaji mwingine.

  Mkuu huyo Mkoa alisema kuwa hata kama mali ghafi kwa sasa hivi hakuna anataka ni kujiridhisha kuwa mashine zote ni zima wakati akiwa anasubiri msimu wa pamba ujao ili apate mali ghafi.Mkuu wa Mkoa wa Tabora yuko katika zoezi la kuhakiki viwanda vyote ili kujiridhisha kama vinafanyakazi na vile ambavyo wamiliki wake wameshindwa waweze kuvirudisha Serikalini
   Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akitoa ufafanuzi jambo kwa mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora alipotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kujionea hali halisi ya uzalishaji wa nyuzi. Kulia ni Mkurugenzi wa Kiwanda Mtendaji wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora Urveshi Rajani.
   Kaimu Meneja wa Manunuzi kutoka Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU) Bernard Makhanda (kushoto) akitoa utaratibu wa kufuatwa na Mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora ili aweze kupata fursa ya kuwauzia nyuzi kwa ajili ya wakulima wa tumbaku. Kulia ni Meneja wa Kanda wa Bodi ya Pamba Jones Bwahama.
   Mkurugenzi wa Kiwanda Mtendaji wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora,  Urveshi Rajani akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri mitambo ya kutengeneza nyuzi alipotembelea kiwanda hicho kujionea hali ya uzalishaji.
  Mitambo ya Kiwanda cha Nyuzi Tabora ambayo hivi sasa haifanyi kazi licha ya kuwa mizima.

  0 0

  Katika kuboresha huduma za kibenki nchini Maendeleo Bank lao imetoa zawadi kwa washinidi wake wanne wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya ‘Maendeleo pamoja na wewe’ iliyochezeshwa tarehe 31/8/2017 Jijini Dar es salaamHafla ya kuwapatia washindi hao zawadi ilifanyika leo katika ukumbbi wa ‘Mviringo hall’ uliopo makao makuu ya Benki hiyo ‘Luther House’ posta Jijini hapa ambapo washindi hao wanne walijishindia zawadi tofauti tofauti ikiwemo Ada za shule, tani za Saluji,Mabati pamoja na kiwanja, 
  Akizungumza katika hafla hiyo fupi mkuu wa kitengo cha biashara Maendeleo Bank Peter Tarimo amesema katika kuhakikisha Maendeleo Bank inakuwa karibu na wateja wao imeamua kuwahamasisha hasa wazazi kufungua Account za Benki kwa ajili ya watoto wao ili kuweza kuwajengea utamaduni wa kuhifadhi fedha
  “Mtakumbuka kuwa kampeni hii ilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi wa nane na wateja wengi walishiriki, Droo ilichezeshwa chini ya usimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha (Gaming Board) na kuwapata washindi hawa wanne ambao leo tunakwenda kuwakabidhi zawadi zao” 
  Aidha tarimo aliongeza kuwa Droo ya pili ya bahati na sibu hiyo inatarajiwa kuchezeshwa mwezi wa Novemba mwaka huu na ya tatu itakuwa mwezi Disemba ili kupisha zoezi la uuzaji wa Hisa litakaloanza tarehe 18/9/2017 na kutarajiwa kumalizika mwezi October 
  Droo ya pili ya mwezi Novemba itajumuisha wateja wapya waliofungua Account katika Benki hiyo kuanzia kumalizika kwa Droo hii ya kwanza kwa kuhakikisha kuwa katika Account zao kuna kiasi cha Shilingi Elfu Hamsini na kuendelea.Washindi walioshinda katika Droo hiyo ni Noela George Njavike alieshinda Ada ya shule yenye thamani ya shilingi laki nne, mshindi wa Pili ni Simon Anaufoo Urasa aliejishindia mabati, watatu ni Walter Moses Mchome alieshinda Tani za Seruji na Mshindi wa Nne ni Sarah Fadhili Izumbe aliejishindia zawadi ya kiwanja 
  Maendeleo Bank Plc inatoa huduma za Benki zenye Gharama nafuu na rafiki kwa wajasiliamali, wafanyabiashara , watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa wateja wapya kwenda kufungua Akaunti Mpya

  0 0

  Kocha wa makipa wa timu ya Azam Fc, Idd Abubakar (pili kulia) akiwa pamoja makipa wanaounda kikosi cha timu hiyo.


  KOCHA wa makipa wa timu ya Azam Fc, Idd Abubakar, amekiri upinzani mkali kwa makipa wake kikosini kwani wana jumla ya makipa wanne kikosini, Mghana Razak Abalora, Mwadini Ally, Benedict Haule na Metacha Mnata aliyepandishwa, wote wakiwa wanaunda kikosi cha timu kubwa kwenye eneo hilo.

  Kwa sasa tokea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ianze Agosti 26 mwaka huu, Abalora ameonekana kuwa chaguo la kwanza, akiwa mpaka sasa hajaruhusu wavu wake kuguswa kwenye mechi zote mbili za mwanzo, Azam FC ikiifunga Ndanda bao 1-0 kabla ya juzi kutoka suluhu na Simba.

  Abubakar alisema kuwa upinzani huo ulidhihirika wakati wakiwa kwenye kipindi cha maandalizi ya msimu mpya nchini Uganda, ambapo kila kipa aliyepewa nafasi aliweza kukaa imara langoni.

  “Upinzani upo mkubwa sana na isitoshe vilevile baada ya kuziangalia mechi za pre season tulizocheza kila mmoja anataka nafasi, hawa makipa wote wanne wanahitaji kucheza na viwango vya vyote mazoezini na mechi wanazopewa kila mmoja mechi yake ameitendea haki.

  “Tulianza mechi ya kwanza na Mwadini (Ally) amecheza vizuri tu tumekuja tumecheza na Razak (Abalora) mechi mbili amecheza vizuri kwa hiyo kiwastani kiujumla kabisa upinzani upo mkubwa sana kwamba hakuna golikipa ambaye amebweteka kwamba hapa amefika katika hii nafasi,” alisema.

  Alisema mpaka sasa ndani ya kikosi hicho hakuna kipa ambaye ndiye kila kitu kutokana na ushindani wanaouonyesha na namna kila mmoja alivyopewa nafasi wakati wa maandalizi ya msimu.

  “Nadhani hata kwenye hii ligi hali itakuwa hivyo hivyo kwa kuwa kila mmoja yupo kwenye kiwango kizuri kabisa,” alisema.

  Kocha huyo wa muda mrefu aliyedumu na Azam FC akiwa kama mchezaji aliyeipandisha timu hiyo hadi kuwa kocha wa eneo hilo, aidha amesema kuwa amepata makipa wachanga wanne ambao anawapika kwa ajili ya manufaa ya baadaye ya timu hiyo huku akikiri kuwa wanavimo vizuri.

  “Ukizungumzia kuwaandaa makipa wa chini ambao ni junior (wadogo) yaani tukizungumzia waliochini ya umri wa miaka 20, nina magolikipa wanne kutoka chini hawa magolikipa wanne vilevile wanaushindani kila mmoja amekuja kwa staili yake.

  “Unajua unapomchukua golikipa hasa hawa wa chini ya umri wa miaka 20, wengi wao wanakuwa hawajafundishwa hawajapa mafundisho kabisa yale ya ugolikipa lakini wanakuwa na fikra, sasa ile fikra unaichukua kwa kila mmoja kwa hiyo hivi sasa kila mmoja anauzuri wake,” alisema.

  Alisema makipa hao wamewatoa kwenye programu zao mbalimbali za kusaka vipaji, akiwataja ambao ni Razak, Eliya, Mohamed na Abdulkarim.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  MSANII wa muziki wa kizazi kipya Shaban Mpute 'Ne-Mo' amesema amedhamiria kurudi katika familia ya muziki kivingine, huku akitarajia kuachia wimbo wake mpya unaitwa 'Kipotabo'Septemba 19 mwaka huu ambayo imetengenezwa katika studio za Combination Sound chini ya mtayarishaji Man Water na video kutengenezwa na Kwetu Studio.

  Akizungumzia ujio wake  mpya Ne-Mo chini ya lebo ya 'Digital City Drimz' alisema kuwa amedhamiria kuirejesha RnB ya Bongo katika viwango na pia kuipeleka nje ya mipaka ya Tanzania, kwa sababu anahifahamu vizuri na  kwa sasa kuna wasanii kama Diamond Platnumz, Ali Kiba, Vanessa Mdee, Navy Kenzo na wengineo wameubeba muziki wa Bongofleva na kusaidia kuupenyeza kimataifa, naye ana matumaini makubwa ya kufika walipo wasanii hao.

  Ne-mo ujio wake utakuwa wa aina yake na Watanzania hawatajutia kumsubiri Ne-Mo arudi kwa muda wote huo, kwamba ukimya wake umetokana na masomo ambapo aliamua kutulia amalizie masomi kisha aendelee na Harakati za Muziki na  alikuwa masomoni akiwa amesomea  masuala ya  'Mass Communication' na anaeleza kuwa sasa ametulia na amepata 'Mameneja ' ambao wanamsimamia na kumrejesha kwa kishindo katika muziki.

  "Nimejipanga vuzri pamoja na mameneja wangu narudi kimuziki kikweli kweli, naomba mashabiki wa muziki Tanzania wanipokeekwa mara nyinyingine, nilitoka kidogo kwenda masomini lakini sasa nimerudi rasmi katika muziki"alisema Ne-mo.

  Alisema kwa upande wa mtindo wa Rap na Hip Hop mwanzoni mwa miaka ya 2000 Profesa Jay alichangia kuuweka muziki wa Hip Hop mtaani na kukubalika na kila kundi la jamii., miaka michache iliyopita waliibukakina Child Benz na Nako 2 Nako ambao walisaidia kujenga misingi ya kuufanya muziki wa Hip Hop kukubalika kibiashara.

  Alisema sasa hivi wasanii kama Weusi, Darasa, Billnas, Young Dee na kadhalika ambao wanauwekea vionjo muziki wa Rap kufanya kupenya zaidi na hata uanze kuimbwa na hata akina dada ambao zamani ilikuwa ni nandra kuwa na mapenzi na muziki wa Rap.

  Meneja wa mwanamuziki huyo Habibu Anga 'Guru Picasso' alisema kuwa siku ya Jumatatu wataachia rasmi wimbo wa Kipotabo wa msanii huyo na amekuja kuitikisa zaidi Tanzania na Afrika Mashariki kama ilivyotokea  mwaka 2013 alipoachia wimbo uliokwenda kwa jina la "Number One" ambao alimshirikisha mkali mwenzake 'Ommy Dimpoz' wimbo ambao ulikuwa mkubwa na kugeuka kama 'wimbo wa Taifa' kama wasemavyo mtaani.

  Baada ya mafanikio makubwa ya wimbo huu wa 'Number One' Ne-Mo hakuwahi kutoa kazi yake nyingine yoyote ile, zaidi ya nyimbo za kushikishwa ambazo ni 'Mrs Superstar' ya Young Killer, 'Tulikuwepo' ya Niki Mbishi, 'Sijutii' ya Msamiati na nyinginezo nyingi.


  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua  Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano 2017/18 - 2021/22 kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango ambapo pia ilishuhudiwa na Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Zubeir Ali Maulid, Naibu Waziri Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo, Naibu Waziri Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji na Wadau wa Maendeleo kwenye Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati uzinduzi wa Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano 2017/18 - 2021/22 katika Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. 
  Sehemu ya Waliohudhuria wakipiga makofi mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano 2017/18 - 2021/22 katika Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango wakati akiwasili kwenye uzinduzi wa Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano 2017/18 - 2021/22 katika Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa mwaka 2017.

  Akiwasilisha Bungeni Muswada huo leo Mjini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa lengo la marekebisho yaliyopendekezwa ni kuboresha utekelezaji wa Sheria hizo kwa kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kutumia sheria hizo na kuongeza masharti mengine ili kuleta uwiano kati ya Sheria zilizorekebishwa na sheria zilizopo.

  "Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa mwaka 2017 unapendekeza kufanya marekebisho katika sheria 11 na kufuta sheria moja" amefafanua Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

  Aidha, Masaju amesema kuwa masuala muhimu yaliyozingatiwa katika Muswada huo ni pamoja na kubadilisha vifungu vya Sheria kwa kufuta baadhi ya vifungu vya sheria hizo na kuviandika upya, kufuta baadhi ya maneno kwenye vifungu vya sheria, kuzingatia maneno mapya, kuongeza vifungu vipya na kufuta sheria moja.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mohamed Mchengerwa amesema kuwa Kamati inashauri Serikali kuhakikisha Kamati maalumu ya kumshauri Waziri kuhusu misamaha ya kodi iundwe na wataalamu waliobobea kutoka katika fani na maeneo tofauti tofauti ili kujenga uwezo wa kamati hiyo katika kumshauri Waziri husika kuhusu misamaha hiyo ya kodi.

  Nae Ally Saleh Ally kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Wizara ya Katiba na Sheria amesema kuwa kambi hiyo inashauri kuwa haitoshi kuifuta RUBADA pekee bali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu malalamiko ya wananchi wanaoituhumu kupora ardhi na hatua stahiki kwa wote waliohusika zichukuliwe.

  0 0


  Afisa Mtendaji wa Zuku Fiber, Mhandisi Thomos Hintze akizungumza na waandishi katika uzinduzi wa Internet Fiber iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Meneja wa Zuku Fiber Thomas Wenanga  pamoja na Mkuu wa kitengo cha Fiber, Michael Debaly
  Meneja Uendashaji wa Zuku Fiber, Mcharo Mlaki akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya Internet iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Zuku Fiber, Mhandisi Thomos Hintze akiwa na watendaji wa kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.


  Kampuni ya Zuku imezindua huduma ya Internet yenye uwezo mkubwa wa kuweza kufanya kazi kwa vitu vitatu kwa wakati mmoja.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mtendaji wa Zuku Fiber, Thomos Hintze amesema kuwa Zuku Fiber inawezo mkubwa kuliko mitandao mengine iliyopo nchini.

  Amesema kuwa wamejipanga kutokana na kampuni hiyo kuwa na miundombinu inayojitosheleza ambapo mtu akilipia anapata huduma muda huo huo

  Hata hivyo amesema kifurushi cha Zuku fiber triple Play 100 mbps kimeundwa ili kukidhi mahitaji ya mtandaoni kama video fupi, sinema , michezo ya kuigiza na video za mawasiliano.

  Hintz amesema kuwa gharama za mtandao huo ni sh .79,000 ambapo Mteja anapoanza  kutumia uwezo wake ni uleule mpaka mwisho.

  Amesema kampuni hiyo imekwenda mbali baadhi ya nchi za Afrika ambazo ni Zambia, Malawi, Uganda pamoja na Kenya

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

  Serikali imedhamiria kununua mashine tatu za vipimo vya vinasaba (DNA) ili zitumike katika maabara za Kanda na hivyo kusogeza huduma karibu na wananchi.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala wakati akijibu swali la Mbunge wa Chumbuni Mhe. Ussy Pondeza kuhusu ucheleweshwaji wa matokeo ya uchunguzi wa sampuli ikiwemo sampuli za makosa ya jinai.

  Dkt Kigwangala amesema kuwa Serikali ina mkakati wa kuongeza mashine hizo ili kuwezesha uchunguzi kufanyika kwa wakati kwa vielelezo vya makosa ya jinai ikiwa ni pamoja na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.

  " Sampuli za uhalali wa watoto kwa wazazi zinafanyika kwa wepesi zaidi kuliko sampuli za makosa ya jinai kwani sampuli hizo zinachukuliwa moja kwa moja toka kwa wahusika hivyo kurahisisha uchunguzi wake endapo wahusika wa uchukuaji watachukua kwa umahiri na uhifadhi utafanyika kwa namna stahili" amefafanua Dkt. Kigwangala.

  Aidha, Dkt. Kigwangala amesema kuwa sampuli za uchunguzi wa makosa ya jinai zinachukuliwa toka maeneo ya matukio hivyo uchunguzi wake unaweza kuchukua muda zaidi kutegemeana na aina ya sampuli na eneo zilipotoka.

  Vilevile Dkt. kigwangala aliongeza kuwa Serikali inampango wa kuanzisha kituo cha kupima vinasaba (DNA) Mkoani Mbeya kwa lengo la kupunguza ucheleweshaji wa matokeo ya uchunguzi.

  Mbali na hayo akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Vijijini Mhe. Hawa Ghasia kuhusu Serikali kuagiza tohara kuwa lazima kwa wanaume nchini, Dkt. kigwangala amesema kuwa si rahisi kwa Serikali kuagiza tohara  kuwa lazima japo kuwa inafaida kiafya kwa wananchi.

  " Tohara inasaidia kupunguza maambukizi ya Saratani ya shingo ya Uzazi kwa wanawake pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi" ameongeza Dkt. kigwangala.

  Aidha, amesema kuwa elimu kuhusu tohara imefikishwa kwa wananchi kwa kiasi kikubwa ambapo Serikali kwa kushirikiana na wadau katika Mikoa ya kipaumbele  imekuwa ikitoa elimu kabla na baada ya huduma ya tohara katika vituo vya kutolea huduma za afya.

  0 0

  Aahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini

   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi ambaye ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao.

  Amekutana na Bw. Pardesi leo (Jumanne, Septemba 12, 2017)  kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam na amesema kwamba tayari Serikali imeanza kuwahamasiha wakulima kuongeza uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.

  Waziri Mkuu amempongeza Bw. Pardesi kwa kuiunga mkono Serikali katika mpango wake wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda. Kampuni ya Namera Group of Industries inamiliki kiwanda cha nguo cha NIDA na cha Namera vya jijini Dar es Salaam.Kampuni inatarajia kufungua kiwanda kingine cha nguo wilayani Kahama.

  Pia Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha zao la pamba linapewa kipaumbe alikutana na wakuu wa mikoa yote inayolima pamba Ijumaa, Septemba 8, 2017 na aliwaagiza wasimamie zao hilo kwa karibu ili kuinua uzalishaji wake na kuwaongezea kipato wananchi hususan wakulima wa zao la pamba.

  Amesema Serikali imeamua kufufua mazao makuu matano ya biashara ambayo ni pamba, chai, kahawa, korosho na tumbaku ili kuwawezesha wakulima kupata tija na kuondokana na umasikini wa kipato, hivyo kukuza uchumi wa Taifa.

  Waziri Mkuu amesema Serikali imeamua kusimamia kilimo cha pamba kuanzia maandalizi ya shamba, kupanda, matumizi ya pembejeo na dawa, kuvuna na kutafuta masoko, hivyo ahadi yao ya kununua pamba yote ni faraja kwa wakulima.

  “Nimefurahishwa na uamuzi wenu wa kutaka kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao kwani kwetu sisi ni faraja kwa sababu wakulima walipunguza uzalishaji baada ya kukosa soko la uhakika.”

  Kwa upande wake Bw. Pardesi amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba kampuni yao inauwezo wa kununua pamba yote inayozalishwa nchini na kuichakata katika viwanda vyao na kutengeneza nguo zitakazouzwa nchini kwa bei nafuu.

  Amesema kwa sasa wameajiri mafundi katika viwanda vyao ambao watakuwa wa nashona nguo na kuziuza nchini kwa gharama nafuu ili kuwawezesha wananchi wa hali ya chini kumudu kununua na kuondokana matumizi ya nguo za mitumba.

  “Mheshimiwa Waziri Mkuu sisi Namera tuko tayari kununua pamba yote inayozalishwa nchini kwani viwanda vyetu vinafanya kazi ya kuchambua pamba, kutengeneza nyuzi na majora kisha tunashona nguo na kuziuza. Hapa Kazi Tu maana bila ya kufanya kazi huwezi kuheshimika.”

  Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema kitendo cha kununua pamba inayolimwa nchini na kuchakata katika viwanda vyao kwa lengo la kutengeneza nguo za aina mbalimbali wataiwezesha Serikali kuokoa fedha nyingi za kigeni zilizokuwa zinatumika kuagiza nguo nje ya nchi.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  JUMANNE, SEPTEMBA 12, 2017.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao. Waziri Mkuu amekutana naye leo Septemba 12/ 2017 Ofisini kwake Dar es Salaam
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi   ambaye ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao.(L) Ni Meneja wa Namera Bwana Muhammad Waseem. Waziri Mkuu amekutana nao leo Septemba 12/ 2017 Ofisini kwake Dar es salaam. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ngugai  akisisitiza jambo wakati wa Kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
   aziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akilieleza Bunge leo mjini Dodoma kuhusu mkakati wa Serikali kukamilisha ujenzi wa nyumba elfu kumi za makazi kwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  (JWTZ )  ambapo kati ya hizo zaidi ya elfu sita zimeshakamilika.
   Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid (wakwanza  kulia)  akifuatilia kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma wakati wa ziara yake .
   Mbunge wa Mtwara Vijijini Mhe . Hawa Ghasia akichangia hoja Bungeni leo mjini Dodoma kuhusu maboresho katika sekta ya Afya hasa suala la tohara kwa wanaume ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupunguza  maambukizi ya virusi vya ukimwi.
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akisisitiza jambo mara baada ya kuwasilisha muswaada wa sheria ya marekebisho ya Sheria mbalimbali  namba 3 wa mwaka 2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia  Katiba na Sheria Mhe.  Mohamed Mchengerwa (Mb) akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo kuhusu  muswaada wa sheria ya marekebisho ya Sheria mbalimbali  namba 3 wa mwaka 2017 leo Bungeni mjini Dodoma
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, Kazi,  Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi.
  ( Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma )


  0 0

   Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dkt Ghirmay Andemichael akitoa maelezo ya Shirika hilo kwenye warsha ya siku tatu ya kuimarisha kanuni za kupambana na matumizi ya tumbaku inayofanyika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
   Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib akifungua warsha ya kuimarisha kanuni za mapambano ya matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
   Dkt. William Maina kutoka WHOAFRO akitoa maelezo ya Azimio la WHO na sheria za kimataifa dhidi ya mapambano ya matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku katika warsha ya kuimarisha kanuni za mapambano hayo katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi.
   Baadhi ya washiriki wa warsha ya kumiarisha mikakati ya kanuni za kupiga vita matumizi ya tumbaku inayofanyika Hoteli ya GoldenTulip Malindi Mjini Zanzibar.
  Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa warsha ya kuimarisha mikakati ya kupiga vita matumizi ya tumbaku inayofanyika Hoteli ya Goden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.

  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, akijiandikisha katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la UTT AMIS katika Mkutano wa Wahandisi uliofanyika Septemba 7-8 mjini Dodoma. Kulia ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa UTT-AMIS, Martha Mashiku. 
  Ofisa wa UTT AMIS, Waziri Ramadhani, akitoa elimu kwa watu waliofika katika banda la UTT AMIS huku mwananchi mwingine aliyekaa akifungua akaunti wakati wa mkutano wa Wahandisi mjini Dodoma.
  Mkurugenzi wa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS, Daud Mmbaga akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, alipotembelea banda hilo wakati wa Mkutano wa Wahandisi uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.

  0 0


  Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW

  Sera ya Maendeleo ya Jamii pamoja na mambo mengine, inaelekeza jamii kushiriki kazi za kujiletea maaendeleo yao wenyewe maana jamii ndiyo kitovu cha maendeleo.

  Kwa kutambua hilo, Mkurugenzi wa Maendelo ya Jamii Bw. Patrich Golwike ametembelea katika Kijiji cha Mondo, Kata ya Mondo, kilichopo katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kuhamsha ari ya wananchi kushiriki katika ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya cha kijiji chao.Bw. Golwike alibainisha kuwa maendeleo ya mtu ni mtu mwenyewe na hakuna mtu kutoka nje ya eneo fulani ataleta maendeleo katika eneo husika.

  “Sisi hatukuja hapa kijijini Mondo kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya Mondo, bali tumekuja kuhamsha ari ya wananchi wa kijiji hiki kuwa tayari kushiriki kazi za maendeleo yao kwa kutumia rasilimali zilizopo” alisema Bw. Golwike.

  Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Mondo Bi. Aziza Omary alibainisha kuwa mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mondo uliibuliwa kwenye kikao cha Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mondo, ndipo iliporidhiwa kujenga kituo hicho ili kupunguza tatizo la vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua, na pia kuondokana na kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya za rufaa zikiwemo za wazazi na wagonjwa wengine.

  Awali wananchi walishiriki kubaini changamoto, kupanga, kutekeleza na kusimamia mradi wa ujenzi kuhakikisha kuwa wananchi wanajitolea kuchangia nguvu kazi zao katika zoezi la ujenzi. 

  Kazi nyingine zinazofanywa na wananchi ni kukusanya vifaa vya ujenzi kama vile mawe, kokoto, mchanga, mafundi, na utoaji uchangiaji wa rasilimali fedha.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mondo Bw. Philipo Suleiman ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuchagua kutembelea kijiji cha Monde mio ngoni mwa vijiji takribani 900 vilivyopo katika mkoa wa Mwanza.

  Jengo la Kituo cha Afya cha Kata ya Mondo linakadiriwa kukamilika mwaka 2018 na litagharimu takribani shilingi 150,460,540/- fedha ambayo itatoka kwa wahisani na wananchi wenyewe.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akishiriki ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya katika Kijiji cha Mondo, kilichopo kata ya Mondo, Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza, mapema.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Atupele Mwambene akisalimiana na akinamana wa Kijiji cha Mondo, Kata ya Mondo Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza wakati alipofika kijijini hapo kuhamsha ari ya wananchi kushiriki kazi za maendeleo yao kwa kutumia rasilimali zilizopo katika mazingira yao.
  Mratibu wa Masuala ya Maendeleo ya Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi Mwajina Lipinga(kulia) aliyeshika chepeo) akishirikiana na wananchi kujenga jengo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mondo Wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza kutatua kero ya ukosefu wa huduma za afya katika kata ya Mondo kwa kutumia nguvu za wananchi wenyewe. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Atupele Mwambene(kushoto walioshika chepeo) akichanganya saruji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mondo, Kata ya Mondo kilichoko Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza katika kuhamsha ari ya kushiriki kazi za maendeleo kwa kutumia rasilimali zilizopo katika mazingira husika.
  Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi, Misungwi Mhandisi Harold J. Mtyana akishiriki kujenga jengo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mondo, kata ya Mondo, wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akikabidhi mifuko 50 ya simenti kwa niaba ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mondo Bw. Marthias Lumwagila kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa Kituo hicho cha Afya. 
  Sehemu ya jengo la kituo cha Afya cha Mondo, Kata ya Mondo,Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kama linavyoonekana na wananchi wakiendelea na kazi ya ujenzi. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akiwa katika ziara ya kuzitembelea shule za msingi za kata ya Bomalang'ombe na kujionea jinsi gani shule hizo zinavyoongozwa na kuzitambua changamoto zinazowakabili walimu,wanafunzi,wanachi na viongozi wanaozizunguka shule hizo lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi wa wilaya ya kilolo.
  Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Bomalang'ombe.


  Na Fredy Mgunda,Iringa

  Wanachi wa kijiji cha mwatasi wamekuwa kikwazo cha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya shule ya msingi kutokana na wazazi kutowatimizia mahitaji muhimu watoto wao pindi waendepo shule.

  Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika shule hiyo mwalimu mkuu wa shule ya msingi mwatasi Seth Mfikwa alisema kuwa wazazi wengi wa kijiji hicho wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.

  “Hapa kijijini wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema Mfikwa

  Mfikwa alimuomba mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi wa kijiji cha Mwatasi ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kijiji hicho.

  “Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hii sio mzuri kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu lakini tunaendelea kuwaelimisha kidogo kidogo hivyo kwa kuwa mkuu leo umefika kwenye shule yetu tunaomba msaada wako wa kutoa elimu kwa wazazi ili kukuza elimu kwa wanafunzi wa kijiji hiki” alisema Mfikwa.

  Aidha Mfikwa alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini bado tatizo kubwa hivyo jitihada zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa kuwa bila hivyo watoto wa kijiji hichi wataendelea kuwa wafanyakazi za ndani tu.

  Anderson Mdeke ni diwani wa kata ya Bomalang’ombe alikiri kuwa wazazi wa kijiji cha mwatasi hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.

  “Kweli kabisa wazazi wa kijiji cha mwatasi wamekuwa wakiwaambia watoto wasifanye mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa wakifaulu watakuwa na gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda kuwafanya kazi za ndani na dio furaha kwa wazazi wa kijiji cha Mwatasi” alisema Mdeke

  Mdeke alisema kuwa uongozi wa kata ya bomalang’ombe utaendelea kutoa elimu kwa wazazi hao ili kurudisha morali ya kuendelea kuwapa mahitaji muhimu yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la kuboresha maisha ya watoto hao.

  “Zana potofu zimekuwa kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya wananchi wa kijiji cha Mwatasi hivyo tukiondoa zana hiyo elimu itakuwa kwa wanafunzi wa kijiji hichi” alisema Mdeke

  Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah aliahidi kulifanyia kazi tatizo hilo kwa kuzungumza na wazazi ili kuwaelimisha juu ya umuhimu wa elimu kwa wananchi wa kijiji hiki cha Mwatasi.

  “Tangu nianza ziara katika wilaya ya kilolo leo ndio nimekutana nah ii changamoto ya wazazi kuwarudisha nyuma kielimu hivyo nitatenga muda muafaka wa kuja kuongea na wazazi wa kijiji cha Mwatasi kwanza swala hili limenishtua sana kwakweli lazima nilitafutee ufumbuzi haraka sana”alisema Abdallah

  Aidha mkuu wa wilaya hiyo Asia alisema anatakiwa kujifunza tabia za wananchi wa kijiji cha Mwatasi kwanini wanafanya hivyo kwa kuwa changamoto hiyo ni kubwa na inatakiwa kutatuliwa mapema.

  “Unajua lazima nijue chanzo cha kuwakatisha tamaa watoto wao wasiendelee na masomo ni nini hivyo nikijua tatizo ni nini naweza kutatua tatizo hilo kwa urahisi kabisa maana elimu ni kitu mhimu sana kwa maendeleo ya watoto yao” alisema Abdallah 

  Abdallah alisema licha ya changamoto hiyo ya wazazi hata walimu wa shule wanamatatizo kwani haiwezekani kuwa na walimu wengi hivi lakini ufaulu bado upo chini lazima kukaa chini na hawa walimu kujua tatizo ni nini.

  0 0

  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetoa ripoti ya tafiti ya asali zilizokusanywa zenye chembechembe za nikotini kuwa zimefanyiwa majaribio na  zimedhihirisha kuwa chembechembe  hizo ni chache sana na hazina uwezo wa  kudhuru mwili wa binadamu.

  Akizungumza na Vyombo vya habari, Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Glory Mziray amesema  TFS wamekuwa wakukisanya sampuli kila baada ya miaka miwili  kutoka kwa wafugaji nyuki na kuzipeleka kwenye  Maabara za kimataifa na mara zote  zimekutwa zikiwa na ubora wa hali ya juu unaokidhi masoko yote ya kitaifa na kimataifa.

  Amezitaja tafiti  mbili zilizofanyika mwaka 2016 kuwa  lengo lake lilikuwa ni kuainisha madhara ya  ufugaji nyuki kwenye maeneo yanayolima Tumbaku na ameyataja maeneo yaliyofanyiwa utafiti huo kuwa  ni mkoa wa Tabora na Kigoma

  Mziray  amesema tafiti hizo zimebainisha kuwa kiwango cha nikotini kinachopatikana  kwenye asali iliyochavushwa katika mikoa inayolima Tumbaku ni sawa na nikotini iliyopatikana kwenye asali  ilivyochavushwa na mimea mingine kama vile  nyanya na miombo hivyo kiwango hicho cha nikotini hakina madhara kwa binadamu.

  Amesema  watumiaji wa asali wamekuwa wakihukumu uwepo wa nikotini   kwenye asali kwa kuangalia rangi ya asali sambamba na uchungu wa asali lakini asali za Tanzania zinatengenezwa kwa mchanganyiko wa maua ya mimea mbalimbali  jambo ambalo linathibitishwa si nikotini peke yake ndiyo inasababisha uchungu bali mimea mingine kama vile muarobaini. 

  Mziray amewataka watumiaji wa asali kuendelea kuitumia kwa vile  asali ni chakula cha kiasili kinachotengenezwa kutokana na mchanganyiko wa mimea mbalimbali.Ameongeza kuwa, asali ni mchanganyiko uliotokana na maji, Sukari (fruktosi, glukosi, sakrosi) madini pamoja na vitamin.
  Baadhi ya Sampuli ya asali inayopatikana katika maeneo mbalimbali za nchi. Asali hutumika kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali kwa binadamu.

  0 0

   Kikundi cha burudani ya Uchekeshaji kutoka nchini Kenya maarufu kama Short Stature Society of Kenya kikitoa igizo lake la kuchekesha mbele ya washiriki mbalimbali wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) toka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki 12 Septemba, 2017 Mjini Kampala, Uganda.
  Kikundi cha Sanaa cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Tanzania (TaSUBA) kikionyesha igizo lake mbele ya washiriki mbalimbali toka nchi wanachama wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) ambapo igizo hilo likimaanisha namna gani nchi hizo zinavyopaswa kuonyesha ushirikiano wa karibu katika masuala mbalimbali kwa manufaa ya nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki 12 Septemba, 2017 Mjini Kampala, Uganda.
  (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM, KAMPALA-UGANDA)


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Wamiliki wa mitandao ya kijamii wameaswa kuchuja habari zao ambazo wamekuwa wakizipata na kuzisambaza kwa jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa Redio ama televisheni za Mitandaoni.

  Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui , Valerie Msoka wakati alipokutana wamiliki wa mitandao ya Kijamii pamoja na waandishi wa habari, Valerie amesema kuwa upashanaji wa habari lazima kuangalia na usalama wa nchi pamoja kuacha uchochezi ambao unachonganisha na jamii au mamlaka.

  Amesema kuwa takribani miaka mitano kulikuwa hakuna fursa za kupata matangazo ya televisheni kupitia mitandao ya kijamii, lakini sasa imeenea kwa watanzania wengi na inaendelea kuongezeka kadri ya teknolojia inavyokuwa, hivyo kunahitajika kuwepo umuhimu wa kusimamia huduma ya mitandao hiyo ili iweze kuleta tija kwenye taifa na si vinginevyo.

  Valerie amesema kuwa TCRA kupitia kamati ya maudhui inatambua na kuthamini kuwepo kwa fursa ya upashanaji wa habari na serikali iliamua kuruhusu huduma hiyo wakati miongozo na taratibu stahiki zikiendelea kutayarishwa.
   
  Amesema vyombo vya habari katika mitandao ya kijamii vya Radio, Televisheni na bado teknolojia inaendelea kukua na haviwezi kuzuia kutokana na mfumo wa upashanaji wa habari. Mwenyekiti huyo anasema habari zingine hazina tija kwa jamii na zingine zinaleta uchochezi ndani ya jamii na wakati mwingine kuingilia faragha za watu ambazo ambazo hazitakiwa kufikia jamii kama sehemu ya habari.

  Amesema wadau wa mitandao ya kijami na watumiaji wa mitandao hiyo wanahakikisha wanahabarisha kwa kuzingatia habari zizojenga umoja wa kitaifa, mshikamano na ushirikiano baina ya watanzania bila kujenga hofu , kuchochea chuki na uhasama baina ya watanzania. Aidha amesema habari za matusi katika mitandao ya kijamii hayavumiliki ,kwani zinakiuka misingi ya uandishi na uhuru na wajibu wake.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa TCRA, Valerie Msoka akizungumza na wadau wa mitandao ya kijamii juu uchujaji wa habari ambazo zinatakiwa  kuwafikia jamii na zinazolenga uimarishaji wa usalama wa nchi na mshikamano watanzania, leo jijini Dar es Salaam.Picha na Michuzi Jr-Michuzi Media Group.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa TCRA, Valerie Msoka (katikati) akipitia taarifa wakati wa mkutano wa wadau wa mitandao ya kijamii ambao wanasambaza taarifa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maudhui, Abdul Ngalawa na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka.
  Kaimu Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka akizungumza katika mkutano wa wadau wa mitandao ya kijamii ambao wasambazaji wa taarifa kwa jamii leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya waandishi wa habari na wamiliki wa mitandao ya Kijamii wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.


  Mmoja wa wamiliki wa Mitandoa ya Kijamii, kutoka Jamii Media Maxence Mello akichangia jambo katika suala zima la uchujaji wa Habari katika mitandano ya Kijamii, katika mkutano uliowahusu Wamiliki wa radio, Televisheni za mtandaoni na mitandano mingine ya kijamii uliondaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),mapema leo jijini Dar
  Mmoja wa wamiliki wa Mitandao ya Kijamii,kutoka Mtembezi Media,Antonio Nugaz akichangia jambo katika suala zima la uchujaji wa Habari katika mitandano ya Kijamii,ndani ya mkutano uliowahusu Wamiliki wa radio,Televisheni za mtandaoni na mitandano mingine ya kijamii uliondaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),mapema leo jijini  Dar

older | 1 | .... | 1366 | 1367 | (Page 1368) | 1369 | 1370 | .... | 1898 | newer