Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1362 | 1363 | (Page 1364) | 1365 | 1366 | .... | 1897 | newer

  0 0

  KAMPUNI inayojishughulisha na huduma za hoteli na tiketi za ndege kwa njia ya mtandao barani Afrika, Jumia Travel imemtangaza Bw. Joe Falter (pichani) kuwa Ofisa Mtendaji 

  Mkuu mpya akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Paul Midy ambaye amechaguliwa kushika wadhifa mkubwa zaidi kwenye makampuni ya Jumia. Bw. Falter ambaye pia ni mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni dada ya Jumia Food, amechukua majukumu hayo ikiwa ni jitihada za kuimarisha zaidi shughuli za uendeshaji wa kampuni hiyo.

  “Nimefurahia sana kujiunga na timu mpya ya Jumia Travel ambayo imejizatiti kwenye kuleta mabadiliko ya namna watu wanavyosafiri ndani na nje ya bara la Afrika. Ikiwa na idadi ya orodha kubwa ya hoteli na kuongoza kiubunifu, bila ya shaka Jumia Travel ni kinara katika masuala ya usafiri, utalii na ukarimu, nimejawa na shauku kubwa ya kuhakikisha tunasonga mbele zaidi,” alisema Joe.

  Kabla ya hapo, Joe alikuwa ni mshauri wa masuala ya usimamizi katika taasisi ya McKinsey ya jijini London nchini Uingereza, akiwa na rekodi nzuri ya kuyanyanyua makampuni ya Ulaya na Afrika, hivyo amekuja na ujuzi wa kipekee wa mikakati ya kiusimamizi ambayo itasaidia katika kukuza fursa za biashara zinazochipukia.

  Akizungumzia juu ya kuteuliwa kama bosi mpya wa Jumia Travel, Joe anahakikisha kwamba, “Jumia Travel imekua kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka miwili iliyopita na lengo kubwa ni kuendeleza jitihada hizi za ukuaji wa haraka huku tukiimarisha huduma zetu kwa wateja na hoteli tunazofanya nazo kazi. Washirika wetu wa hoteli ambao ni zaidi ya 30,000 Afrika na mamia ya maelefu ya wateja watajionea maboresho mapya kwenye njia za mtandao na za kawaida.”

  “Nina ujasiri kwamba Joe ni chaguo sahihi la kiongozi ambaye ataipelekea Jumia Travel kuwa chaguo pekee kama wakala wa usafiri Afrika na nje ya mipaka,” alisema mwanzilishi mwenza wa Jumia, Sacha Poignonnec.

  Ikiwa imeanzishwa mwaka 2013, Jumia Travel imejitengenezea rekodi nzuri katika masuala ya huduma za kimtandao na ubunifu wa kiteknolojia, na kuwa kinara katika makampuni ya uwakala wa usafiri barani Afrika. Inatoa huduma za hoteli na tiketi za ndege kwa njia ya mtandao pamoja na kuandaa vifurushi vya aina mbalimbali kwa ajili ya wateja wake, watu binafsi na kwa ajili ya makampuni.

  Kuhusu Jumia Travel

  Jumia Travel (www.travel.jumia.com) ni kampuni nambari moja barani Afrika katika utoaji wa huduma za usafiri mtandaoni, inarahisisha huduma za usafiri kwa kumpatia uzoefu mtumiaji kwa kulinganisha bei na huduma zinazopatikana kwa njia ya haraka na salama zaidi.

  Ikiwa ina hoteli zaidi ya 30,000 Afrika (na zaidi ya hoteli 300,000 duniani) na makampuni ya ndege zaidi ya mia moja kama washirika wake, Jumia Travel inalenga kutoa uhuru wa kusafiri kupitia kupunguza gharama za kusafiri, kutoa orodha kubwa ya hoteli na kuwezesha huduma bora na zenye viwango vya juu kwenye kila nchi husika ili kuwa mojawapo ya sehemu ambayo mteja atakidhi haja zake zote za kiusafiri barani.

  Jumia Travel inafanya shughuli zake katika nchi zaidi ya 40 za Afrika, ikiwa na ofisi kwenye nchi 10 miongoni mwake, na wataalamu wa masuala ya kusafiri zaidi ya 400 ambao wapo tayari kuwahudumia wateja wakati wowote. Ofisi zetu kuu zinapatikana Lagos (Nigeria), Accra (Ghana), Dakar (Sénégal), Abidjan (Ivory Coast), Algiers (Algeria), Douala (Cameroon), Kampala (Uganda), Dar Es Salaam (Tanzania), Nairobi (Kenya) na Addis Ababa (Ethiopia). Kabla ya mwezi Juni 2016, Jumia Travel ilikuwa ikijulikana kama Jovago.

  Ilianzishwa 2013 na Jumia huku ikiendeshwa kwa ushirikiano wa MTN, Rocket Internet, Millicom, Orange, Axas na washirika wengine.


  0 0

  Mkuu wa Wilaya Kibaha, Assumpter Mshama akizungumza katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS). Mkuu wa Wilaya Kibaha Assumpter Mshama alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo.
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Maggid Mwanga akizungumza jambo katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS). 
  Mkurugenzi wa THPS Dk. Mbatia akimkabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo na kumwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Everist Ndikilo
  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akimkabidhi zawadi Dk. Beatrice (RMO PWANI) iliyotolewa na wafanyakazi wa THPC kutokana na mchango wake katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS). 
  Mgeni rasmi wa hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akimkabidhi zawadi pamoja na cheti Batuli Mituro ya Muuguzi bora kutoka kituo cha Ikwiriri HC katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS). 
  Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akipatiwa maelezo juu ya upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi kwa kina kutoka kwa mtaalamu wa THPS.
  Mgeni rasmi Assumpter Mshama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa wilaya wenzake wa mkoa wa Pwani pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa THPS
  Baadhi ya wakuu wa wilaya wa Mkoa wa Pwani akibadilishana mawazo mara baada ya kumalizika kwa kutano huo


  Wakurugenzi wameagizwa kuhakikisha wanafuatilia watumishi wa afya waliojiriwa kwa ufadhili wa mfuko wa dharura wa rais wa marekani ( PEPFAR) kupitia THPS katika vituo mbalimbali mkoani Pwani wanalipwa mishahara yao kwa wakati.

  Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alipokuwa mgeni rasmi akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo, katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS).

  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alilipongeza shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS) katika juhudi wanazofanya katika sekta ya afya hususani mapambano dhidi ya ukimwi mkoani humo na kuwataka watumishi wa afya kuhakikisha wana wanatoa huduma ya vvu kila mahali katika vituo vya kutolea huduma za afya , mawodini, kliniki maalumu, kwenye mikusanyiko ya watu, na maeneo mengine maalumu ili malengo ya serikali ya 90 ya tatu yatimie ifikapo mwaka 2020 .

  Mshama alisema serikali iliridhia maazimio ya shirika la umoja wa mataifa ya kupambana na ukimwi ya tisini ya tatu ambapo alifafanua azimio hilo ni ifikapo 2020 asilimia 90 ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi wawe wanatambua hali zao za maambukizi, asilimia 90 ya hao wawe wanatumia dawa na asilimia 90 ya walioko kwenye dawa wafubaze virusi kwa kiwango kinachotakiwa cha kopi 1000 za virusi kwa milimita moja ya damu.

  Mapema akiongea katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa THPS Dk. Redempta Mbatia alisema shirika limekuwa likitoa huduma mbalimbali hususani katika sekta ya afya katika mapambano dhidi ya vvu katika mradi wake kwa kipindi cha miaka mitano Mkoani Pwani ikiwa ni pamoja nakuboresha miundo mbinu ya vituo vya afya, kununua vifaa tiba, kutoa mafunzo elekezi kwa watumishi pia kuhakikisha kila kituo kina dawa za kutosha.

  “Tunatoza ruzuku kwa mkoa wa Pwani zaidi ya shilingi million 700 kwa mwaka, fedha hizi zinatakiwa zihudumie wananchi , zifanye mambo mbalimbali ikiwemo kulipa mishahara baadhi ya watumishi wa afya walioajiriwa kwa ufadhili wa PEPFA kupitia shirika letu, lakini pia tunatoa kiasi cha shilingi 10,000 kwa kila mtumishi atakayemgundua mteja wa VVU na kuhakikisha anamshika mkono kwa mkono na kumwandikisha kwenye huduma na tiba”, alisema Dk. Mbatia

  Shirika laTHPS linapata ufadhili wake kutoka mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na ukimwi (PEPFAR) na hapa nchini shirika hilo limekuwa likiendesha miradi ya kutoa huduma za VVU katika mkoa wa Pwani, Mbeya, Kigoma na Zanzibar.

  0 0


  Na  Bashir  Yakub.

  1.UKOROFI  WA  WASIMAMIZI  WA  MIRATHI.

  Baadhi  ya wasimamizi  wa  mirathi  ni  wakorofi.  Baada   ya  kuteuliwa  kwa  jukumu  hilo   hawapendi  kugawa  mali  ili  kila  mtu  achukue  chake. Inapaswa  kufahamika  kuwa  mali  si  za  msimamizi  wa  mirathi .  Mali  ni  za  warithi  halali  isipokuwa  msimamizi  ni  kiongozi  tu.  Kwa  maana  hii  anawajibika  kusikiliza  warithi  wanasema  nini  ili  mradi  kile  wanachosema  kisipingane na  sheria.

  Wakati  mwingine  warithi  wanataka  wagawiwe  mali  zao   ili  kila  mtu  endelee  na  maisha  yake lakini  msimamizi  hataki  tena  bila  sababu  za  msingi. Hili  linakuwa  si  sawa  isipokuwa  kama  kuna sababu  za  msingi  za kufanya  hivyo.

  Sababu zaweza kuwa labda   anayetaka kugawiwa mali  ni  mtoto  mdogo asiyeweza  kumiliki  mali kwa wakati  huo, ni  mtu  asiye na  akili  timamu kwa  muda  huo,  kuna  shauri  mahakamani kuhusu  hiyo  mirathi  linaendelea, mali hazijakusanywa  zote, kuna  ugomvi  kwa  warithi  kuhusu  mali  ambao  utaathiri  mgao  nk.                      

  2. WAJIBU  MKUU  WA  MSIMAMIZI   WA  MIRATHI.      
                                   
  Kifungu  cha 108(1)  cha  Sheria  ya  Usimamizi  na  Uendeshaji  wa  Mirathi,  Sura  ya  352  kinaeleza  wajibu  wa  jumla  wa msimamia  mirathi. Kifungu  kinasema  kuwa  kazi  kubwa  ya  msimamizi  wa  mirathi  ni  kukusanya, mali  na  madeni  ya marehemu,kutunza  mali  hizo, kusimamia  gharama  za  mazishi  na  msiba, na  kugawa  mali kwa  wanaostahili. Na  kazi  hii yote  ifanyike  kwa  uadilifu  mkubwa.

  Kwahiyo  kumbe  moja  ya  kazi  ya lazima  na ya  kisheria  ya  msimamizi wa  mirathi  ni  kugawa mali  kwa  warithi.  Huu  ni  wajibu  ambao  msimamizi  anawajibika  kuutekeleza. Na  atagawa  kwa  mujibu  wa  wosia  au sheria  husika kama  hakuna  wosia. Hagawi  anavyotaka  yeye. Nani  apate  nini  halipo  katika  hiari  yake.
                  
     KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com


  0 0


  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini – Thobias Andengenye anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna wa Operesheni Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CF (OPS) Rogatius Peter Kipali, kilichotokea mapema leo Semptemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Mombasa, Ukonga jijini Dar es Salaam.

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anatoa pole kwa Maafisa, Askari na Watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.

  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na familia ya Marehemu linaendelea kuratibu shughuli za msiba huo na taarifa za Mazishi zitatolewa baadaye baada ya taratibu zote kukamilika.

  Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi

  Amina.
  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.


  0 0


  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inalaani vikali mauaji ya watoto wawili ambao walitekwa na kukutwa wameuawa katika mkoa wa Arusha.
   
  Wizara imepokea taarifa ya vifo hivyo kwa simanzi kubwa na inalaani vikali mauaji hayo ambayo yamekatisha uhai wa watoto hao katika umri huo mdogo. Mauaji na utekaji waliofanyiwa watoto hawa ni ukiukwaji mkubwa wa Haki za Mtoto ikiwemo haki ya Kuishi ambayo ndiyo haki kuu kati ya haki zote. 

  Wizara inawaasa wazazi, walezi na jamii kuimarisha mifumo ya ulinzi wa watoto katika ngazi ya mitaa, vijiji  na jamii ili kuwa na mifumo madhubuti katika kudhibiti ukatili unaofanywa dhidi ya watoto na kusababisha majonzi makubwa kwa wazazi, familia na jamii kwa ujumla.

  Jamii inakumbushwa kuwa tatizo la utekaji wa watoto linahitaji juhudi za pamoja katika kupambana nalo ili kuzifanya jamii zetu kuwa mahala salama kwa watoto wetu kuishi. Wizara itaendelea kuimarisha Kamati za ulinzi na usalama wa Mtoto katika ngazi za kata, vijiji na mitaa ili kuboresha huduma za ulinzi wa watoto wetu. 

  Aidha, Wizara inalipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zilizofanyika za kutaka kuwaokoa watoto hao  wakiwa hai, ingawa juhudi hizo hazikufanikiwa.  

  Wizara inaomba wazazi, walezi, familia, walimu na marafiki kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
  07/09/2017.


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa Uwekezaji katika Kiwanda cha Machinjio ya kisasa na Usindikaji wa Nyama cha Nguru 'Nguru Hill Ranch Ltd' kilichopo Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Zubair Corporation ya Oman, C.S.Badrinath na katikati ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Clliford Tandari.
   Baadhi ya wadau walioshiriki katika hafla hiyo.
   Wadau wakifuatilia hafla hiyo.

  Wadau.


  Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Zubair Corporation ya Oman, C.S.Badrinath, akitoa hotuba yake katika hafla hiyo.
   Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Regina Chonjo, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kutiliana saini wa makubaliano ya Uwekezaji katika Machinjio ya Kisasa ya Nguru mkoani Morogoro.
   Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiwa katika hafla hiyo.
   Sehemu ya wadau waliohudhuria hafla hiyo.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Clliford Tandari, akitoa hotuba yake kabla ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga, kusaini makubaliano ya uwekezaji katika machinjio ya kisasa ya Nguru Wilayani Mvomero.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga (wa pili kushoto), akisaini mkataba wa makubaliano ya uwekezaji katika Kiwanda cha Machinjio ya kisasa na Usindikaji Nyama cha Nguru Wilayani Mvomero.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga (wa pili kushoto), akibadilishana hati na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zubair Corporation ya Oman, C.S. Badrinath, baada ya kusaini makubaliano ya uwekezaji katika machinjio ya kisasa ya Nguru.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Clliford Tandari (katikati), akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni wa LAPF, Eliud Sanga, baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya uwekezaji katika Kiwanda Machinjio ya kisasa na Usindikaji Nyama.

  Eneo litakalotumika kupitishia ng'ombe wakati wakienda katika machinjio hayo.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Clliford Tandari (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji katika machinjio ya Nguru.
  Picha ya pamoja.
  Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama.
  Eneo la machinjio ya kisasa ya Nguru.
  Eneo la Ranch ya Nguru.
  Maeneo ya machinjio ya Nguru.

  NA MWANDISHI WETU, Mvomero-Morogoro

  MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanya uwekezaji wa Dola za kimarekani  Milioni 3.90 katika kiwanda cha machinjio  na usindikaji nyama cha Nguru ‘Nguru Hills Ranch Limited’ kilichoko nje kidogo ya Morogoro Wilaya ya Mvomero.

  Akizunguza katika  uwekaji wa saini kwenye mkataba wa uwekezaji, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga, alisema uwekaji wa saini umefikiwa baada ya tathini ya kina iliyofanywa na mfuko huo.Alisema mfuko umejiridhisha  kuhusu usalama wa rasilimali za wanachama kwenye uwekezaji huo.

  “Tunatambua kuwa Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji katika viwanda lakini LAPF imeona fursa hii ni moja wapo ambayo inakidhi vigezo vyote vya ajenda ya uwekezaji”alisema Sanga.

  Alisema LAPF imewekeza kwenye kiwanda hicho kwa ubia na kampuni ya ‘Eclipse Investments LLC’ inayotokana na kampuni tanzu ya Zubair Corporation ya Oman na kampuni ya ‘Busara Investments LLP’ na kufanya wabia kuwa watatu.

  “Kiwango cha uwekezaji kilichofanywa na LAPF ni USD 3.9 Milion ambayo ni sawa na asilimia 39 ya hisa za kampuni,ambapo Eclipse Investments LLC inaa hisa asilimia 46 na Busara Investments LLP ina hisa asilimia 15”alisema Sanga.

  Alisema kiwanda hicho kina ukubwa wa ekari 6,000 ambapo ekari 1,200 zimejengwa miundombinu ya malisho ya mifugo kwa kipindi kisichopungua siku 90 kwaajili ya kuwanenepesha na kuwapa ubora kabla ya kuchinjwa.

  Sanga alisema kiwanda hicho kitakuwa na uwezo kuchinja na kuchakata ng’ombe 300 na mbuzi 2,000 kwa siku na kusafirishwa mara moja.

  “Nyama itakayozalishwa kwa kiwango kikubwa itasafirishwa nje kwenye nchi za mashariki ya kati na mashariki ya mbali ambako soko ni kubwa na Oman”alisema Sanga.

  Alisema kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja 500 na nyingine zisizo za moja kwa moja na kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya viwanda vingine.

  0 0

  NEC -  Dar es salaam.

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemteua Ndugu Rehema Juma Migilla kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) ,kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Hindu Hamisi Mwenda aliyefariki  dunia Septemba 1, 2017.


  Akizungumzia uteuzi huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amesema kuwa Tume imemteua Ndugu Rehema Juma Migilla mara baada ya kupokea taarifa ya kuwepo kwa nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kutoka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  Amesema kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 Mhe. Spika aliitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu kuwepo kwa nafasi wazi ya mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi CUF baada ya aliyeteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Malum kupitia chama cha CUF Ndugu Hindu Hamis Mwenda kufariki dunia.


  Katika hatua nyingine Mkurugenzi  huyo amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 86 A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa imewateua Madiwani Wanawake wa Viti Maalum watatu (3) kujaza nafasi wazi za madiwani katika Halmashauri tatu za Tanzania Bara.


  Madiwani walioteuliwa ni Ndugu Jane I. Chungwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Rosana S. Mwinyi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Ndugu Pili M.Mfaume kupitia Chama Cha Wananchi CUF kutoka Halmashauri ya Temeke.


  Amesema uteuzi huo umefanyika baada ya Tume kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 aliitarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu uwepo wa nafasi wazi za madiwani.


  0 0


   

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Madini ya Tanzanite kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati Maalumu ya Bunge ya Kuchunguza Madini ya Almasi kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipitia Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Madini ya Almasi na Tanzanite mara baada ya kukabidhiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi Taarifa hiyo kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Wajumbe wa kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiendelea na majadiliano na timu kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation leo Septemba 7, 2017 kuhusu madai ya Tanzania juu ya upotevu wa fedha nyingi katika biashara ya madini ya dhahabu inayofanywa na kampuni hiyo hapa nchini. Majadiliano hayo yanafanyika jijini Dar es salaam

  0 0

  Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mtambile Mhe. Masoud Abdallah Salim (CUF), aliyetaka kujua mpango wa Serikali katika kuboresha mafao ya uzeeni ili kuondoa malalamiko ya hali ngumu ya maisha wanayoishi Wastaafu.

  Mhe. Salim alisema kuwa kumekuwepo malalamiko mengi kutoka kwa Wastaafu ambao wakati wa utumishi wao walilitumikia Taifa kwa uwaminifu na uadilifu mkubwa, kuhusu kuishi maisha magumu yanayotokana na kucheleweshewa mafao yao ya uzeeni yasiyolingana na kupanda kwa gharama za maisha.

  Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa, Serikali kwa sasa imejielekeza zaidi katika kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, nishati ya umeme, maji, huduma za afya, elimu na kiuchumi hususan katika ukusanyaji mapato kwa lengo la kuboresha maisha ya Wastaafu na Wananchi kwa ujumla.

  “Tuendelee kuiunga mkono Serikali yetu katika juhudi zake za kujenga uchumi imara, uchumi wa viwanda ambao ndio msingi mkuu wa kuimarisha mapato ya Serikali”. Alisema Dkt. Kijaji.

  Alisema kuwa maboresho ya viwango vya pensheni kwa Wastaafu yasiyoendana na maboresho ya miundombinu ya kiuchumi na huduma za kijamii hayawezi kuondoa malalamiko ya Wastaafu hivyo Serikali imelenga zaidi kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii ili kupunguza malalamiko hayo.

  Dkt. Kijaji alifafanua kuwa nyongeza ya pensheni kwa Wastaafu, mishahara na maslahi mazuri kwa Watumishi wa Umma itaongezeka kama mikakati na azma ya Serikali ya kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi itafanikishwa.

  Aidha Dkt. Kijaji aliongeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kuboresha viwango vya pensheni ili kukidhi mahitaji muhimu ya Wastaafu, kwa kutambua hilo Mwezi Julai 2015, Serikali iliboresha kiwango cha pensheni kutoka Sh. 50,114 hadi Sh. 100,125 kwa mwezi.

  Imetolewa na:

  Benny Mwaipaja
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Fedha na Mipango
  Serikali imeahidi kuendelea kuboresha mifumo ya kukusanya mapato pamoja na kuboresha miundombinu ya kiuchumi na kijamii ili kuleta unafuu wa maisha ya Wastaafu na Wananchi kwa ujumla.

  0 0


  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini– Thobias Andengenye anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna wa Operesheni Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CF (OPS) Rogatius Peter Kipali, kilichotokea mapema leo Semptemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Mombasa, Ukonga jijini Dar es Salaam.

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anatoa pole kwa Maafisa, Askari na Watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.

  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na familia ya Marehemu linaendelea kuratibu shughuli za msiba huo na taarifa za Mazishi zitatolewa baadaye baada ya taratibu zote kukamilika.

  Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amina.


  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

  0 0
 • 09/07/17--08:42: MATUKIO BUNGENI LEO
 • Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Muungano na Mazingira) Mhe.January Makamba akizungumza  jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde katika kikao cha tatu cha Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo  Mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe.Dk.Suzan Kolimba  akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba  na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline  Mabula katika kikao cha tatu cha Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo  Mjini Dodoma.
  Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Halima Bulembo akiuliza swali katika kikao cha tatu cha Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo  Mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  akimskiliza Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba katika kikao cha tatu cha Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo  Mjini Dodoma.
  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Makame Mbarawa akizungumza jambo na Mbunge wa Chalinze Mhe.Ridhiwani Kikwete katika kikao cha tatu cha Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo  Mjini Dodoma.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tatu cha Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo  Mjini Dodoma.
  Picha na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.  0 0  0 0

  Mhandisi wa Maji toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Gratius Haule akisisitiza jambo kwa wakazi wa Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti (hawapo pichani) wakati wa sherehe za kukabidhi vyoo kwa baadhi ya wakazi hao ambavyo vimejengwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti wakimsikiliza Mhandisi wa Maji toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Gratius Haule wakati wa sherehe za kukabidhi vyoo kwa baadhi ya wakazi hao ambavyo vimejengwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi Bridge for Change Bw. Ocheck Msuva akifafanua jambo kwa wakazi wa Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti (hawapo pichani) wakati wa sherehe za kukabidhi vyoo kwa baadhi ya wakazi hao ambavyo vimejengwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa wakazi wa Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti Mzee Mbesela akiwashauri wakazi wa mtaa huo waliobahatika kujengewa vyoo na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI) kuvitunza vyoo hivyo ili viweze kuwasaidia kwa muda mrefu.
  Mwenyekiti wa Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti Bw. Rahim Gassi akitoa salamu za shukrani kwa viongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) na Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI) kwa kufanikisha mradi wa ujenzi wa vyoo katika mtaa wake.


  Mhandisi wa Maji toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Gratius Haule (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa vyoo katika Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti, vyoo hivyo vimejengwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI).
  Moja ya choo cha kisasa kilichojengwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI) kwa wakazi wa Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti.Picha na Eliphace Marwa -Maelezo

  0 0

  Mstahiki Meya wa jiji la Xn’an Nchini China Zhu Huan akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kufaya mazungumzo na mwenyeji wake Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya mbalimbali.
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari leo ,mara baada ya kufanya mazungumzo na Meya wa jiji la Xin’an Zhu Huan alipomtembelea ofisini kwake leo. wa kwanza kulia ni Meya wa jiji la Xin’an,
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akisalimiana na Meya wa jiji la Xin’an Zhu Huan alipomtembelea ofisini kwale leo na kufanya nae mazungumzo.
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mwenye suti nyeusi akiwa na Meya wa jiji la Xin’an Zhu Huan akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya mazungumzo leo alipomtembelea mfisini kwake.


  …………………….


  NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

  MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amekutana na kufanya mazungunzo na Meya wa Jiji la Xin’an Nchni China Zhu Huan ofisini kwake Karimjeee.

  Katika mazungumzo hayo , Meya Mwita na mgeni wake wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kukuza na kutangaza utalii wa ndani na nje ya Dar es Salaam.

  Aidha Meya Mwita amesema jiji la Dar es Salaam lina kila aina ya vivutio vya utalii wa ndani na nje ambavyo vinaweza kuwavutia wageni mbalimbali kutoka nje ya Nchi kufika jijini hapa na kutalii badala ya kwenda Zanzibar , Kilimanjaro na maeneo mengine.

  Ameongeza kuwa anaamini kuwa mazungumzo hayo na mgeni wake yataleta tija na kwamba jiji la Dar es Salaam litapata watalii kutoka sehemu mbalimbali na hivyo kuliwezesha jiji kupata mapato makubwa kupitia vivutio vilivyopo.

  “ Tunania ya kulitagaza jiji letu kwenye sekta ya utalii, kutokana na rasilimali za vivutio vilivyopo, ukienda kwenye maeneo mengi ndani ya jiji letu utaona kuwa tunavyo vivutio vyakutosha kabisa ambavyo vikitangazwa kila mmoja atapenda kutalii katika jiji hili” amesema Meya Mwita.

  “ Yapo maeneo mengi ambayo watanzania hawayajui, lakini kupitia mpango huu ambao nimekuja nao hivi sasa ninaimani kwamba watu ambao walikuwa wanafika kwenye jiji letu na kupanda ndege kwenda Zanziba ama Arusha na maeneo mengine, sasa watafanya utalii hapa kwetu” amesisitiza.

  Meya Mwita ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa , hivi karibuni jiji la Dar es Salaam linaratajia kupokea magari ya utalii ambayo yamenunuliwa kupitia fedha za jiji, ambapo baada ya kufika yatazinduliwa na hivyo kuanza kutangaza utalii wa ndani.

  Kwaupande wake Meya wa jiji la Xin’an Zhu Huan amempongeza Meya Mwit kutokana na uendeshaji wake wa jiji, ambapo amesema jiji la Dar es Salaam limepata Meya bora ambaye anaamini kwamba ataleta mabadiliko makubwa ndani jiji hili.

  Mbali na pongezi hizo, pia ameahidi kushirikiana nae katika sekta mbalimbali ikiwemo kutangaza utalii wa jijini hapa ili uweze kutambulika katika maeneo mengine Nchini China.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kuzindua Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia kwake) wakishangilia baada ya Waziri Mkuu Kuzindua Mpango Mkakati Jumuishi wa kitaifa wa Lishe kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Selemani Jaffo na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde.
  Baadhi ya Washiriki wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua Mpango huo kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya kuzindua Mpango huo kwenye ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango(kushoto kwake) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia kwake) wakionyesha vitabu vya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katia Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe uliofanywa na Waziri Mkuu, kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 11 ili kukabiliana na utapiamlo na amemtaka kila mdau wa lishe aonyeshe bayana mchango wake katika kukabiliana na utapiamlo nchini.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Septemba 6, 2017) wakati akifungua mkutano wa nne wa mwaka wa wadau wa lishe wa kutathmini afua za lishe nchini kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. Pia alizindua Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe wa mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 (Joint Multisectoral Nutrition Review).

  “Viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali wabaini kiwango cha utapiamlo katika maeneo yao, waonyeshe mbinu za kukabiliana na hali hiyo, wafanye tathmini ya ufanisi na watoe taarifa za ufanisi,” amesema.

  Amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote, wahakikishe shilingi 1,000 ambazo Halmashauri zilielekezwa kutenga kwenye bajeti kutoka kwenye vyanzo vyao vya mapato kwa ajili ya kuboresha lishe kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano, zinatolewa na kutumika kama ilivyopangwa.

  “Tulikubaliana kila Halmashauri lazima ikusanye makusanyo ya ndani kwa asilimia zaidi ya 80. Nilisema kiwango cha chini kisipungue asilimia 80. Na kupitia makusanyo hayo, ndipo tunapata fedha za kutenga kwa masula kama haya,” alisisitiza.

  “Napenda kusisitiza kwamba ni lazima tufanye tathmini ya wapi tumefikia na wapi tumekwama katika kupambana na tatizo la utapiamlo hapa nchini,” alisema.

  Pia amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya wahakikishe wanaisimamia mikoa na halmashauri zao kutekeleza afua zilizoainishwa katika Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe kwa kuzijumuisha katika mipango yao na kuzitengea fedha kwenye bajeti zao za kila mwaka. 

  Wakati huohuo, Waziri Mkuu alisema amefurahishwa sana na kaulimbiu ya mkutano huo isemayo “Lishe Bora: Msingi wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania” ambayo kimsingi inaendana na dhamira yetu ya kujenga uchumi wa viwanda kama kichocheo cha mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu.

  Pia alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wadau wawekeze kwenye viwanda vya usindikaji wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi ili kuongeza wingi wa vitamini na madini katika vyakula na hatimaye kuboresha lishe na afya ya jamii. “Napenda kusisitiza kuwa Serikali imeandaa mazingira mazuri ya uwekezaji hivyo tutumie fursa hii kikamilifu,” aliongeza.

  Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Ummy Mwalimu alisema kuna baadhi ya Halmashauri na mikoa hazijaunda Kamati za Afua za Lishe.

  “Ninaomba Halmashauri na mikoa ikamilishe kuunda kamati za mikoa na pia watendaji wahakikishe fedha zimetengwa na zinatolewa. Lakini cha msingi ni kwamba fedha hizi zitumike kwa matibabu ya utapiamlo na masuala ya lishe na si vinginevyo,” alisisitiza.


  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  L. P. 980, 
  40480 DODOMA, 
  ALHAMISI, SEPTEMBA 7, 2017.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi tuzo ya kutambua mchango wake katika kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na China Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu Youqing alipotembelea ofisi kwake leo Jijini Dar es Salaam.


  Na: Bushiri Matenda- MAELEZO

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga ameagana na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing.


  Katika hafla fupi iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dkt. Mahiga alimshukuru Balozi Dkt. Lu kwa kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali ya nchi yake na Tanzania kwa muda wote alipokuwa nchini akitekeleza majukumu yake.


  Dkt. Mahiga alimueleza Balozi huyo kuwa Tanzania na China ni ndugu kwani tangu Tanzania ilipopata Uhuru imekuwa ikishirikiana na nchi hiyo yenye maendeleo makubwa kiuchumi.


  “Kwa muda mrefu wizara zetu zimekuwa zikifanya kazi kwa karibu sana ambapo sasa tumekuwa washirika wa karibu. Wewe Balozi umekuwa kielelezo tosha cha kutekeleza tafsiri ya sera nzuri ya nchi yako kwa mataifa mengine ikiwamo Tanzania” alisema Dtk. Mahiga.


  Aidha, Dkt. Mahiga alisifu utendaji wa balozi huyo kuwa wa ni wa kipekee kwani amekuwa mnyenyekevu, msikivu na anafanya kazi zake kwa utaratibu na uhakika.


  Alimshukuru balozi huyo kwa jitihada zake za kuhakikisha watushishi wa wizara kuendelea kupata mafunzo nchini China na kuomba kuendelea kushirikiana katika masuala ya tafiti mbali mbali baina chuo cha Diplomasia nchini na vyuo vyao vya Diplomasia vya China.


  Waziri Mahiga alitumia fursa hiyo kumshukuru Balozi Lu kwa jitihada zake za kuhakikisha maombi mbali mbali ambayo Serikali imekuwa ikiomba Serikali ya China katika sekta mbalimbali na kutolea mfano ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) ambapo ulikamilika kwa wakati.

  Aidha, aliishukuru serikali ya China kwa kukubali kujenga jengo la ofisi za wizara yake huko Dodoma ombi ambalo waziri Mahiga alilotoa kwa waziri wa China alipotembelea nchini hivi karibuni.

  Kwa upande wake Balozi Dkt. Lu ameishukuru wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki chini ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli kwa ushirikiano wanaoendelea kutoa kwa Ubalozi na serikali ya China

  “Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni familia yangu, kwa muda wote nimekuwa mwenye furaha na ari kufanya kazi na nyinyi kwa maslahi ya nchi zetu hivyo nawashukuru sana kwa ushirikiano wenu”Dkt Lu alisema.

  Alimueleza Dkt. Mahiga kuwa anajisikia furaha kuona Sera ya Serikali ya kuliletea taifa maendeleo na wananchi wake kwa ujumla inatekelezwa kwa vitendo hivhyo kuongeza kasi ya maendeleo hadi Tanzania sasa inaweza kuuza bidhaa zake nchi za nje.

  “Narudi nyumbani China lakini naahidi nitakuwa balozi wenu huko nyumbani, Ubalozi wa China hapa nchini utaendelea kushirikiana na wizara na Serikali kwa kila hali” alisisitiza Dkt. Lu

  Balozi Lu pia ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa mchango wake katika ukombozi wa nchi za Afrika ikiwemo Afrika ya Kusini na jitihada za wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili watanzania wanaoishi nchi za nje.

  Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Bw. Rogers William Sian’nga amemshukuru Balozi Lu kwa ushirikiano wake na Mamlaka hiyo ambapo Ubalozi wa China umetoa vifaa mbalimbali wenye lengo la kuongeza ufanisi na kutoa fursa za watumishi kwenda China kupata mafunzo ili yaweze kuwasaidi katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini.

  “Serikali ya China naifananisha na mshumaa kwani inamulika Tanzania katika mapambano dhidi ya madawa haramu ya kulevya, Mamlaka imepata kibali kwenda China kutembelea magereza yote ili tuweze kuwahoji wafungwa wote kwa lengo la kubaini wafanyabiasha wakubwa wanaofanya biashara hii haramu” alisema Bw. Sian’ga.

  Katika hafla hiyo Waziri Mahiga alimkabidhi Balozi Lu zawadi kinyago cha Ujamaa kinachoashiria udugu na mshikamano wa Watanzania na picha yenye mchoro wa Tembo na Mlima Kilimanjaro wenye ishara ya kutambua mchango wa Balozi huyo katika mapambano dhidi ya ujangiri na wizi wa Maliasili nchini.

  Katika hatua nyingine Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers William Siang’a kwa niaba ya Mamlaka yake alimkabidhi Balozi Lu zawadi ya ngozi ya pundamilia kwa kutambua mchango wake wa kupambana na madawa ya kulevya nchini ambapo serikali ya China ipo mstari wa mbele katika mapambano hayo.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa katika moja ya shule za msingi wilayani kilolo akiwa amefika kaunagalia hali ya mitihani inaendeshwani na usalama wake upoje 
   Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akizungumza na wanafuzi waliohitimu elimu ya shule ya msingi katika shule ya msingi Boma la ng'ombe wilaya kilolo mkoani Iringa 

  Na fredy Mgunda,Iringa.

  Wananchi wa wilaya ya kilolo mkoani iringa watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamemalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza uchumi wa taifa.

  Akizungumza wakati wa kuangalia amani ya wanafunzi wa darasa la saba waliokuwa wanafanya mitihani ya kuhitimu elimu ya shule ya msingi mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alisema sasa imefika mwisho wa wilaya hiyo kuwa soko la wafanyakazi wa ndani.

  “Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka iringa kilolo sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawakamata na kuwafungulia kesi serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Abdallah.Abdallah aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuwapeleka shule watoto waliofaulu kinyume cha hapo wazazi watachukulia hatua kali.

  “Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubari hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Abdallah

  Aidha Abdallah aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo.“Acheni kuwavulia chupi wanaume mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu kama mimi ambavyo leo hiii nimekuwa kiongozi wenu kwa kwasababu nilikataa kuvua chupi nikiwa na umri kama wenu ndio maana leo hii nipo hapa”alisema Abdallah

  Aidha Abdallah aliwapongeza walimu wa shule za msingi za wilaya ya kilolo kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri wilaya ya kilolo kupitia elimu.“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu wa wilaya hii kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika wilaya yangu ya kilolo na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Abdallah

  Kwa upande wake diwani wa kata ya boma la ng’ombe Anderson Mdeke alikiri kuwepo kwa tatizo la mimba shuleni limekuwa sugu hivyo wameanza kuridhibiti na limepungua kwa kiasi kikubwa.“Kwa kweli tatizo la mimba kwenye shule za kata yangu ya lipo na tumeanza kutafutia ufumbuzi ili kulikosesa kabisa ili watoto wetu wasome bila kuwa na buguza” alisema Mdeke

  Naye mwalimu wa shule ya msingi Mwanzala Grace Magawa alikiri kuwepo kuwepo kwa mimba za utotoni katika  baadhi ya shule za msingi za wilaya ya kilolo kutokana mazingira yanayowakabili baadhi ya wanafunzi ndio husababisha mimba za utoto.“Mwanafunzi akirudi nyumbani anawakuta wazazi wake washakunywa pombe na hawana habari ya kuulizia maendeleo ya mtoto wake hivyo mtoto anaamua kufanya anachotaka kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha kutoka kwa wazazi wake au walezi wake” alisema Magawa

  0 0

  SPIKA Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda, amewataka watanzania kutumia Mfuko wa Taifa wa Bima hiyo ili kupata unafuu wa matibabu pindi wanapougua.

  Wito huo alitoa jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti huyo wakati alipozindua kitengo cha kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo katika Hospitali ya Kairuki.Alisema, kutokana na gharama ya matibabu kupanda kila siku,kadi za  bima ya afya zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupata unafuu wa matibabu kipindi mgonjwa anapokuwa hana fedha.

  Makinda, alisema bima hiyo inatoa fursa kwa wanachama kupata huduma za matibabu katika hospitali wanazoona zinatoa huduma nzuri na kumjali mgonjwa.

  “Vituo vyenye huduma ya NHIF vinapaswa kutibia wagonjwa kwa kuwajali , kuwapenda pamoja na kuwa wakarimu kwa wagonjwa kwani huduma hii inasaidia sana watu hasa wale wanaougua magonjwa yenye kulipia  gharama kubwa,”alisema Makinda.

   Aidha alisema ni watu wachache ambao wanauwezo wa kujitibu bila bima ya afya lakini watu wengi wanategemea huduma hiyo kulingana na gharama kubwa za matibabu katika baadhi ya magonjwa.

  Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki Dk. Asser Mchomvu, alisema nchini Tanzania watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa  na magonjwa yanayosababishwa na matatizo ya figo.

  “Kwa hivi sasa ugonjwa huo umeonekana kuathiri  kati ya asilimia 7 hadi 13 ya watanzania, wengi wao wakiwa wagonjwa wa  kisukari (Diabetes Mellitus)na shinikizo la damu(Acute Kidney  injury) ,”alisema.

  Alisema kwa muda mrefu hospitali yao  imekuwa ikipokea wagonjwa wenye matatizo ya figo na kulazimika kuwapa rufaa kwenda nje ya hospitali hivyo kupitia kitengo hicho kitaweza kutibu wagonjwa 40 kwa siku.

  Alisema kuwa kutakuwa na mashine  10 zenye uwezo wa kuwahudumia wagonjwa na hadi kufikia sasa wamepata kibali cha wizara husika ambapo miongoni mwa mashine hizo ipo ya  kuchuja damu itakayosaidia kuzuia uharibifu wa figo wa kudumu na wa muda hivyo kuokoa gharama.

  Dk. Mchomvu, alisema hospitali hiyo inatarajia  kuongeza idadi ya mashine ili kuweza kuwahudumia wagonjwa wengi  pamoja na kutoa huduma ya kupandikiza figo na kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda (kushoto), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha Kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijjini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki, Kokushubila Kairuki.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda (kushoto), akipata maelezo alipotembelea kitengo cha kuchuja damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo.
   Dk. Muga akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda.
  Dk. Muga akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda. 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Muuguzi wa Kitengo cha Kuchuja Damu, Eva Beatus.
   Jengo la Kitengo hicho.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda, akitoa hotuba yake.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHJF), Anne Makinda (katikati), akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki Hospitali, Kokushubila Kairuki (kushoto), wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Kairuki Hospitali. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Kairuki Hospitali Dk. Asser Mchomvu, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Kairuki Hospitali.
  Baadhi ya madaktari waliohudhuria hafla hiyo wakisikiliza hotuba za viongozi.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki Hospitali, Kokushubila Kairuki akitoa hotuba yake.

older | 1 | .... | 1362 | 1363 | (Page 1364) | 1365 | 1366 | .... | 1897 | newer