Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Zahanati ya Vingunguti yafuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na serikali

$
0
0
Naibu Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Ilala ambaye pia Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto ameeleza sababu zilizopelekea Zahanati ya Vingunguti kufuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na serikali kupitia wakaguzi wake (TRN) na imekuwa miongoni mwa Zahanati tano zilizofuzu.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Zahanati Ibrahim Aeshi Nduze, Naibu Meya Kumbilamoto ameeleza kuwa hali ya mara ya kwanza katika zahanati hiyo haikuwa shwari lakini kwa jitihada zake na kushirikiana na Halmashauri na Serikali alifanikiwa kufanya mambo mbalimbali katika maboresho ya zahanati hiyo na hatimae imefanikiwa kupewa hadhi ya nyota nne.

Akiyataja mambo waliyoyafanya katika Zahanati hiyo ni pamoja na Ununuzi wa Gari ya Wagonjwa (Ambulance), Mashine ya Kufulia,Jenereta, Choo kwa kinamama wanaojifungua, utanuzi wa maabara, ufungaji wa feni nne, mashne tatu za kupmia uzito kwa watoto,kipimo cha presha na kiti cha kubebea wagonjwa.

Zahanati nyingine zilizoweza kupandishwa hadhi Halmashauri ya Ilala ni pamoja na Zahanati ya Tabata, Mhongo la Ndege, Kinyerezi na Kadlugambwa.

Taarifa kutoka Kamati ya Zahanati imeeleza kuwa mwanzo zahanati yetu ilikua na nyota mbili ambapo hizo zahanati nyingine zilikua na nyota tatu hivyo vingunguti imepanda nyota mbili. Kamati hiyo imewashukuru wananchi kwa mawazo, maoni, na changamoto walizozitoa ambazo zimezifanyiwa kazi na ku pelekea zahanati hiyo kupata nyota mbili za ziada, kamati memshukuru pia Diwani Omary Said Kumbilamoto kwa kuwaongoza, kuwashauri, na kutoa mchango wa hali na mali ii kufikia malengo.

WAZIRI TZEBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA (FAO) JOSÉ GRAZIANO DA SILVA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, leo Jumanne Septemba 5, 2017 amefanya mazungumzo na waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kikazi nchini Tanzania. 

Katika ziara hiyo Bw. Graziano da Silva atafanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Serikali, wadau na anatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein sambamba na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed.

Ziara hii ya Mkurugenzi Mkuu inajili wakati FAO ikiadhimisha miaka 40 toka kuanza shughuli zake hapa Tanzania Hafla ambayo itahudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan. 

Katika mazungumzo na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mkurugenzi Mkuu wa FAO anabadilishana mawazo na Serikali ya Muungano wa Tanzania kwenye masuala makuu yanayohusiana na uhakika wa chakula na maendeleo ya kilimo, ikijumuisha juhudi za FAO kitaifa na kikanda.

Pia yamejadiliwa mambo mengine yanayohusiana na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na FAO, pia masuala ya umuhimu kati ya pande hizo mbili.
Mbali ya Maafisa wa Serikali, Mkurugenzi Mkuu atakutana na wadau wengine wa FAO hapa nchini wakiwa ni pamoja na asasi za kiraia, taasisi za elimu, na taasisi za utafiti. 

Baadae Mkurugenzi Mkuu ataenda Zanzibar ambapo, miongoni mwa mambo mengine, anategemewa kuweka jiwe la msingi katika jengo la Mradi wa Kuzalisha vifaranga vya samaki unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Korea kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa KOICA. 

Pia Bw. Graziano da Silva atapata fursa ya kutembelea mradi wa kilimo cha mwani na pia kuona maonesho ya bidhaa mbali mbali zilizotengenezwa na wanawake wanaojihusisha na kilimo cha mwani. 

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt Charles Tzeba alisema kuwa ujio wa Bw. Graziano da Silva nchini unaakisi ushirikiano bora uliopo kati ya Tanzania na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO) ambapo hivi karibuni ILO walisaidia katika kuandaa mpango wa kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi kwa kutoa fedha ya kutengeneza programu ya kutoa maarifa kwa wananchi ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika kilimo.

Dkt Tzeba alisema kuwa tayari jarida limeshatengenezwa la namna ambavyo wananchi hususani wakulima katika kilimo chao wataweza kukabiliana na hali ya ukame au mafuriko kutokana na mvua zilizozidi kiwango.

Sambamba na hayo Mhe Tzeba alisema pia FAO wametoa simu 50 na Kompyuta 15 kwa wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya wataalamu wake kuwa na urahisi wa kukusanya taarifa na kuzifikisha kwa jamii.

Tanzania ilijiunga na FAO mwaka 1962, na mwaka 1977  FAO ilifungua ofisi zake hapa Tanzania. Katika miaka 40 ya uwepo wake, FAO imeisadia Serikali ya Tanzania katika kupanga na kutekeleza sera, mikakati na mipango ya kilimo hapa nchini. 

Kazi ya FAO imejikita katika kuboresha usalama wa chakula na lishe pamoja na maisha ya wakulima wadogo na hivyo kuwa chachu ya kukua kwa uchumi kupitia sekta ya kilimo. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva (Kulia), akimpongeza Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya kuelezea taarifa mbalimbali zihusuzo wizara hiyo. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, kuzungumzia ujio wake nchini na ushirikiano baina ya FAO na serikali ya Tanzania. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, akizungumzia na wataalamu mbalimbali katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi juu ya ujio wake nchini na ushirikiano baina ya FAO na serikali ya Tanzania. Kulia kwake ni Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba. leo Jumanne Septemba 5, 2017.

Wataalamu mbalimbali katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva (Kushoto) akiteta jambo na mwenyeji wake Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya kutembelea ofisini kwake. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akipokea simu 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silvakwa ajili ya wataalamu wa kilimo kuzitumia kukusanya taarifa mbalimbali na kuziwasilisha kwa jamii. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akionyesha moja ya siku kati ya 15 alizokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva kwa ajili ya wataalamu wa kilimo kuzitumia kukusanya taarifa mbalimbali na kuziwasilisha kwa jamii. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva akiteta jambo na Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya kupokea zawadi. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva akipokea zawadi ya vinyago kutoka kwa Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya mazungumzo ya kikazi kumalizika. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva akiwaaga watendaji wa wizra ya kilimo Mifugo na Uvuvi mara baada ya kumalizika kwa mkutano akiwa na mwenyeji wake Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Picha ya pamoja kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva (Aliyeketi kwenye kiti kulia), Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba, Katibu Mkuu wizara ya kilimo Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Dkt Maria mashingo na wataalamu wengine kutoka FAO na Wizara ya kilimo.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPT 6,2017

Msama atangaza kiama kwa maharamia wa kazi za wasanii

$
0
0


KAMPUNI ya Udalali ya Msama, imetangaza msako wa wezi wa kazi za sanaa kwa ujumla wake ambao wamekuwa kikwazo cha wahusika kutofaidi matunda ya ubunifu, jasho na kazi zao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama alisema kazi hiyo ngumu na muhimu kwa maslahi ya wasanii na Serikali, inaa siku yoyote kuanzia sasa.Msama alisema kutokana na wizi huo kuwanyonya wasanii pamoja na kuikosesha Serikali pato lake halali kupitia kodi, kampuni yake imepewa jukumu hilo kwa msaada wa Jeshi la Polisi.

“Naishukuru Serikali kwa kusikia kilio cha wasanii mbalimbali kuanzia wale wa muziki wa injili, Dansi, Bongo Fleva na hata  wengineo, wamekuwa wakilia kazi zao kutajirisha wajanja,” alisema Msama.Msama alisema kibaya zaidi ni kwamba, wizi huo wa kazi za sanaa  sio tu umekuwa ukiwanyonya wasanii, pia ni kuinyima Serikali mapato halali kwa ajili ya kuzitumia kwa maendeleo ya nchi.

Alisema kazi hiyo itakayofanywa na kampuni yake kwa ushirikiano wa karibu zaidi na Jeshi la Polisi, utagusa mikoa yote ya Bara kwa kukamata wote wenye kuuza kazi zisizotambulika kisheria.“Hii ni pamoja na kazi zote zisizo na stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hivyo wenye kuuza CD, DVD feki pamoja na kunyonya kazi za wasanii katika flash, wote hawatabaki salama,” anasema.

Alisema ni heri wenye kujihusisha na kazi hiyo haramu, wakatafute kazi nyingine halali kwani tayari wanayo majina, hivyo wanajua waanzie wapi siku na saa ya kuanza kutoka mkoa mmoja hadi mwingine.“Tunatangaza kuwa, tunaingia kazini kusaka wote wenye kujipatia vipato kutokana na ubunifu na jasho la wengine, huku wahusika wakibaki masikini. Msako huu hautaacha mtu,” alionya Msama.

Mbali ya ukurugenzi mkuu katika kampuni hiyo ya Udalali, Msama pia ndiye mdau aliyechangia kukua kwa muziki wa injili kupitia uratibu wa matukio ya Tamasha la Pasaka, Krismas ama uzinduzi wa kazi mpya.Alisema katika hatua ya awali, msako huo utakaokuwa chini ya Polisi wapatao 100 katika maeneo mbalimbali ya nchi, utaanzia jijini Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma.
2
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msamaakizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake leo,jijini Dar.

CHAVITA KUENDESHA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA ZA MIKOA MITATU.

$
0
0
Mwenyekiti  wa Chama cha Viziwi Tanzania (Chavita) Nidrosy Mlawa akizungumza na waandishi habari juu ya changmoto ya viziwi katika upatikanaji wa taarifa pamoja na mawasiliano katika jamii kwa kusaiadiwa na Mkalimani Octavian Simba hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam. katika kufanya utendaji  katika maeneo wa ser

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
CHAMA Cha Viziwi Tanzania (Chavita) kimesema kuwa viziwi wanakabiliwa na changamoto kwenye shughuli za maendeleo ya jamii katika nyanja za siasa na kiuchumi kutokana na ulemavu huo kwa kuwa kikwanzo katika mawasiliano na upatikanaji wa habari katika jamii hiyo .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho, Nidrosy Mlawa amesema kutokana na changamoto zinazowakabili watu wasiosikia wanatarajia kuendesha mradi katika mikoa mitatu  katika kutoa mafunzo kwa watendaji wa serikali za mitaa juu kutambua haki za watu wasiosikia.

Mradi huo utaendeshwa kwa kipindi cha miezi sita katika Mikoa ya  Morogoro, Mwanza pamoja na Arusha ambapo watakutana na watendaji wa serikali za mitaa katika mikoa hiyo na kupata taarifa mbalimbali zinahusiana viziwi juu ya changamoto ya mawasiliano  pamoja na utumiaji wa lugha za alama katika shule ambazo zina watoto viziwi.

Mlawa amesema mradi huo utagharimu sh. Milioni 80 ambazo wamepata ufadhili  na The  Foundation For Civil Society  katika kugusa changamoto za viziwi ikiwemo kwa watendaji wa serikali za mitaa kutambua na kufanya ufatiliaji wa matumizi ya mafungu ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya watu wenye Ulemavu katika Halmashauri zao.

Aidha amesema kuwa Chavita kikipata ushirikiano katika mradi huo kwa watendaji katika mikoa hiyo ili kufanya Jamii ya Tanzania kuwa jamii juu jumuishi.

Amesema kuwa sekta ya elimu haina walimu hawajui lugha ya alama na kusababisha wanafunzi viziwi kutopata elimu bora kama sera ya elimu ya 2004 inavyoanisha.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MAKAO MAKUU YA KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwaonyesha wajumbe walioshiriki Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki mpango mkakati wa miaka mitano wa Kamisheni hiyo (kulia) Mtendaji Mkuu wa Kamisheni Prof. Kenneth Simala na (kushoto) Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi.

Maryam Kidiko na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar.
KUANDALIWA kwa kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ni miongoni mwa juhudi za kuendeleza lugha ya Kiswahili katika ukanda huo na Duniani kwa jumla.
 Hayo ameyasema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki huko katika ukumbi wa  Hoteli ya Golden Tulip iliopo Malindi Mjini Zanzibar.
 Alisema kongamano hilo lililowashirikisha wataalamu wa lugha ya Kiswahili wa nchi wananchama wa Afrika Mashariki  lina umuhimu mkubwa katika historia ya maendeleo ya Kiswahili duniani pamoja na kupanga mikutano na kubadilishana utalaamu .
  Hivyo Alieleza kuwa ni muhimu kwa kamisheni kusimamia kwa makini hadhi ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano ikitambuwa kwamba ukanda wa Afrika Mashariki ni sehemu ya Dunia yenye lugha tofauti.
 Samia alisema uratibu na uendelezaji wa Maendeleo na matumizi ya Kiswahili utaimarisha mchakato na utengamano wa Jumuiya kwa maendeleo endelevu. “Utengamano wa Jumuiya sio tukio bali ni mchakato ambao unapaswa kuendeshwa na watu wenye kuelewa vizuri matumizi endelevu ya Kiswahili “Alisema Makamo wa Rais.
 Hata hivyo alielezea kuwa mafanikio kamili yanategemea mkabala wa mawasiliano na ushiriki wa raia wote katika maendeleo endelevu ya Jumuiya . Alisema Kiswahili ni kiungo muhimu kati ya wana Afrika Mashariki katika kujenga utambuzi na kubaini changamoto pamoja na fursa zinazofungamana na maendeleo.
 Alitaka kongamano hilo kuonyesha namna ambavyo Kiswahili kinaweza kufanikisha utangamano na malengo  ya kuimarisha maendeleo ya nchi wanachama Afrika Mashariki.  Waziri Samia alionyesha kkufurahishwa kwake na nchi wanachama kutenga bajeti kila mwaka kwa lengo la kuimarisha na kuendeleza shughuli za Kamisheni hiyo.
Nae Waziri wa Habari  Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe alisema baadhi ya Nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ambazo zilikuwa nyuma katika kutumia lugha ya Kiswahili wamepiga hatua na kimeweza kusaidia katika kuharakisha maendeleo yao.
  Aliitaka Kamisheni hiyo  kushirikiana na Wadau mbali mbali ili iweze kuleta maendeleo kupitia  lugha ya Kiswahili.
 Kwa upande wa Waziri wa Habari Utalii , Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma alisema Serilkali ya Zanzibar  inathamini kuwepo Makao Makuu ya Kamisheni  Zanzibar na ameahidi itaendelea kuunga mkono  kutokana na umuhimu wa lugha hiyo.
 Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Profesa Kenneth Simala alisema Kamisheni itafanya juhudi ya kuziunganisha nchi wanachama na asasi za kiraia  kukikuza Kiswahili.
 Sambamba na hayo alisema Zanzibar imeweza kutowa mchango mkubwa katika Nchi za Afrika Mashariki  kupitia lugha ya Kiswahili katika kukuza lugha hiyo.
 Kauli mbiu ya Kongamano hilo la siku mbili ni ‘KULETA MABADILIKO KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUPITIA KISWAHILI.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA FAO, AAGANA NA BALOZI WA CHINA AONANA NA MZEE BUTIKU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw. José Graziano da Silva  alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitambulishwa kwa  Mwakilishi Mkazi wa FAO  nchini Bw.  Fred Kafeero    na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw. alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Meshack Malo Ofisa aliyeongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw. José Graziano da Silva alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea kitabu na kadi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw.  Bw. José Graziano da Silva alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Butiku aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Butiku aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Butiku aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu Youqing alipofika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya kinyago  Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu Youqing    alipofika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu Youqing    alipofika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017

Matawi saba ya NMB yazinduwa kwa mpigo katika mikoa sita.

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Songwe na Mkuu wa Wilaya ya Songwe - Samwel Jeremiah akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Mkwajuni wilayani Songwe, wengine katika picha (kutoka kushoto) Meneja wa NMB kanda ya Nyanda za Juu - Badru Iddy, Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa ndani wa NMB - Augustino Mbogella, Mbunge wa Jimbo la Songwe - Philipo Mulugo, Katibu Tawala wa wilaya ya Songwe - Johari Samizi na Meneja wa Benki NMB Tawi la Mkwajuni - Michael Mzinga. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.
 
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya – Amos Makalla (katikakati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa tawi jipya la NMB Uyole lililopo Jijini Mbeya. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya – Amos Makalla akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la NMB Uyole uliofanyika jijini Mbeya. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.
 Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani – Augustino Mbogella akizungumza na wateja wa NMB waliokusanyika kushuhudia uzinduzi wa tawi la NMB Mkwajuni wilayani Songwe katika mkoa wa Songwe. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.
BENKI ya NMB Imefungua matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita ikiwa ni juhudi za kujiimarisha zaidi na kuwa karibu na Wateja wake wa kanda ya nyanda za juu.

Matawi hayo yamefunguliwa katika mikoa ya Njombe, Mbeya,Songwe, Rukwa na Katavi. Matawi ambayo yamefunguliwa na yanatoa huduma kwa jamii ni pamoja na NMB  Kasumulu, NMB Uyole, NMB Mkwajuni, NMB Wanging’ombe, NMB Laela na NMB Kalambo lililopo Mlele.

Idadi hii ya matawi mapya inafanya jumla ya matawi ya NMB 31 katika kanda ya Nyanda za Juu huku yakifikia matawi ya NMB 207 nchi nzima.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Tawi la NMB Uyole lililopo mkoani Mbeya, Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu - Badru Iddy amesema kuwa lengo la Benki hiyo ni kusogeza huduma zaidi kwa wananchi ili kuwa karibu na wateja wake.

“Kuzinduliwa  kwa tawi hili la NMB Uyole mahali hapa kunafuatia mahitaji ya muda mrefu ya wateja wetu wa Uyole kupata tawi la NMB lenye nafasi ya kutosha .Aidha  eneo hili ni karibu zaidi na wafanyabiashara wengi ambao ni wateja wetu wakubwa na wananchi kwa ujumla. Tawi hili  kama yalivyo matawi yetu mengine nchini linatoa huduma zote za kibenki zitolewazo na benki yetu," alisema Badru.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la Uyole, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya - Amos Makalla alisema kuwa Wananchi wanapaswa kufungua akaunti katika Benki hiyo na kuitumia kwa kuwa serikali ina hisa ya asilimia 32 katika Benki hiyo.

“Hapa tuelewane, Serikali na Benki ya NMB ni sawa na mapacha kwa kuwa kila mahala ambapo serikali imepeleka huduma zake za kijamii Benki hiyo hufuatia kwa kuweka huduma za kifedha ili kuwahudumia wananchi wa eneo husika,” alisema Mheshiwa Makalla.

Huko Mkoani Songwe Mkuu wa Wilaya ya Songwe  - Samwel Jeremiah ambaye alimwakilisha mkuu wa Mkoa huo  - Chiku Galawa kwenye uzinduzi wa tawi la NMB Mkwajuni, aliwataka wananchi kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha na hivyo kutumia fursa zinazotokana na benki ya NMB kukuza uchumi wao na mwisho kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa ujumla. Alisema desturi ya kuhifadhi fedha  Benki kunajenga nidhamu ya matumizi ya fedha kuepuka madhara ambayo yanaweza kutokea.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa Benki ya NMB Tawi la Mkwajuni, Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani – Augustino Mbogella alisema kuwa mkakati wa kibiashara wa NMB ni kuhakikisha watanzania wengi zaidi wanapata huduma za kifedha na ndio maana kila wilaya benki hiyo inafungua matawi ili kusogeza zaidi huduma kwa wanannchi.

Alisema kuwa NMB ni benki ya wananchi na wanatakiwa kuitumia kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla kwa kupata huduma zote za kibenki ikiwemo mikopo ya kibiashara katika ngazi mbalimbali.

“Benki ya NMB imeendelea kuwa benki yenye mtandao mpana wa matawi na ATM kuliko benki nyingine yoyote hapa nchini kwa kuwa na matawi zaidi ya 200 huku ikiwa na mashine za kutolea fedha (ATM machines) zaidi ya 700 nchi nzima na Wateja zaidi ya Milioni 2 na laki 5.

Mbogella aliongeza pia kuwa “Benki yetu pia inatoa huduma zote zinazotakiwa kutolewa na benki yeyote ya biashara nchini, tuna akaunti mbali mbali za akiba, huduma za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya mahitaji yote kwenye soko, huduma za fedha za kigeni, kukusanya mapato na kulipa kwa niaba ya serikali na taasisi mbalimbali”.

JKCI YATADHARISHA WATUMIAJI WA SIGARA

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari(hawapo pichani) alipokuwa akizungumzia uhusiano wa matumizi ya tumbaku na magonjwa ya moyo jana Jijini Dar es Salaam.Picha na: Frank Shija -MAELEZO

Na Agness Moshi – MAELEZO.

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imetoa taadhari kwa watumiaji wa sigara kujiepusha na matumizi ya sigara kwasababu wapo kwenye hatari ya kuugua magonjwa ya Moyo yanayo sababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu.

Akiongea na Waandishi wa Habari kwenye mahojiano maalum Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi amesema ni vyema wananchi kujiepusha na utumiaji wa sigara kwa sababu moshi unapoingia kwenye moyo huaribu na kuziba mishipa inayopitisha damu kwenye Moyo na hivyo kuusababisha kushindwa kufanya kufanya kazi yake vizuri.

“Moyo umezungukwa na mishipa ya damu ambayo inauwezesha kufanya kazi endapo mishipa hii itaharibiwa na moshi wa sigara,damu inayozalishwa kutoka kwenye moyo itakua chache na hivyo kusababisha mtumiaji kupata matatizo ya moyo kama vile mshituko wa moyo, kushindwa kupumua vizuri kutokana na kubanwa kwa mishipa ya damu”,alisema Prof.Janabi

Prof.Janabi amesema kuwa, kwa kawaida Moyo wa binadamu kila unapopiga unatakiwa uzalishe milita 70 ambapo kwa mapigo 70 ni sawa na mililita 4900 ambazo ni sawa na lita 5 kwenye mwili wa binadamu ikitokea mishipa ya damu imezibwa damu itazalishwa kwa uchache hivyo kusababisha mtu kuvimba miguu, kushindwa kupanda ngazi au sehemu za miinuko na kupata maumivu makali kama amechomwa na kisu.

Prof.Janabi ameongeza kuwa kuziba kwa mishipa ya kupitisha damu kwenye moyo hakuuathiri Moyo tu bali mwili mzima ikiwa ni pamoja na ubongo, hivyo inapotokea mishipa hiyo imezibwa kunahaja ya kutafuta njia ya kusaidia damu ipite vizuri kwenye moyo kwa kupandikiza mishipa mingine ambayo itatolewa kwenye sehemu nyingine za mwili kama kwenye miguu na mikono au kwa kumuwekea mgonjwa chuma ambacho kitasaidia damu kupita vizuri.

Prof.Janabi alisema kuwa, gharama zinazotumika kwa ajili ya kusaidia mishipa iliyoharibiwa ni kubwa ukilinganisha na faida mtumiaji wa sigara anayoipta kutokana na utumiaji wa sigara kwa sababu vifaa vyenyewe viavyotumika ni ghali, gharama za uchunguzi na matibabu, pia muda wa kumuokoa ni muhimu kuzingatiwa endapo mgonjwa ameathirika sana.

“Kama mishipa ya damu imebana kwa asilimia 90 au 100 Mgonjwa anatakiwa afike Hospitalini ndani ya lisaa limoja na nusu endapo atachelewa hakuna kitakachoweza kufanyika zaidi ya Kifo unaweza ukawa na uwezo lakini muda hautakuruhusu”,alisisitiza Prof.Janabi.

Aidha, Prof.Janabi amesema kuwa ,tatizo la uvutaji wa sigara nchini si kubwa sana ukilinganisha na Nchi za magharibi japo linakua kwa kiasi kwenye miji mikubwa ambapo watu watumiaji na watu wanaokaa karibu na mtumiaji kwa muda mrefu wanaathiriwa na Moshi unaotokana na sigara ambapo athari zake huonekana kwa nyakati tofauti.

“Wagonjwa wengi tunapokea hapa wanakua na sababu nyingine kama uzito mkubwa,Kisukari na presha na kwa uchache tunapokea wagonjwa wanaumwa kwa sababu ya matumizi ya sigara kwa wingi ,unakuta wanatumia pakiti moja hadi tatu kwa siku pia mara nyingi tunapowafanyia uchunguzi wa awali wagonjwa ni ni lazima tuwaulize kama wanatumia sigara kwa sababu sigara ni moja ya kisabishi cha ugonjwa wa Moyo”, alisema Prof.Janabi.

Hata hivyo, Prof.janabi ametoa wito kwa Wananchi kuhakiksha wanapima Afya zao mara kwa mara ili waweze kugundua matatizo mapema kabla hayajaleta na madhara makubwa kwenye mwili pia amewataka watumiaji wa sigara kujiepusha na matumizi ya sigara kwani madhara yake ni makubwa.

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI SITA YENYE THAMANI YA SH. 1.2 BILIONI WILAYANI MONDULI

$
0
0
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,Amour Hamad Amour amezindua miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya Sh.1.2 Bilioni.

Miradi hiyo ni wa maji katika Kijiji cha Meserani Juu ambao usanifu wake ulianza mwaka 2013 na umekamilika kwa gharama ya Sh 513 milioni wakati serikali imechangia Sh 444.5 milioni ,halmashauri ya Monduli imechangia Sh 66.6 milioni na wananchi Sh 2.2 milioni.

Pia kiongozi huyo amezindua mradi wa barabara yenye urefu wa kilometa 11kutoka Monduli hadi Kijiji cha Lendikinya uliofadhiliwa na Mfuko wa Barabara(Road Fund) kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kwa jumla ya Sh 272.6 milioni.Imeelezwa kukamilika kwa wa mradi huo kutarahisisha usafiri na kutachochea shughuli za wananchi kujiletea maendeleo na kusadifu azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati wa Tanzania ya viwanda.

Pia kiongozi huyo amefungua nyumba ya wafanyakazi wa afya katika Kijiji cha Mswakini Juu iliyojengwa kwa ushirikiano wa nguvu za wananchi na halmashauri ya wilaya ya Monduli kwa gharama ya sh 53 milioni.

Miradi mingine iliyozinduliwa ni kiwanda kidogo cha kuchakata chakula cha mifugo katika Kijiji cha Mungure na uzinduzi wa mradi wa MMES II (SEDP II)katika shule ya Sekondari Oltinga kwa gharama ya Sh 225 milioni
Imeandaliwa na mtandao wa www.rweyemamuinfo.blogspot.com
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa,Salome Mwakitalima akivalishwa Skafu na mmoja wa watoto wa chipukizi wakati wakiingia wilaya ya Monduli kutoka wilaya ya Arusha. 
Mkuu wa wilaya ya Monduli,Idd Kimanta(kulia)akimpokea mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa. 
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru,Amour Hamad Amour akitoa ujumbe wa Mwenge baada ya kufungua nyumba ya watumishi wa Afya katika Kijiji cha Mswakini Juu wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha kwa gharama ya Sh 53 milioni. 
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru,Amour Hamad Amour akimkabidhi mmoja wa wananchi Chandarua kwaajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa Malaria wakati kufungua nyumba ya watumishi wa Afya katika Kijiji cha Mswakini Juu wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha iliyojengwa kwa gharama ya Sh 53 milioni,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Monduli,Idd Kimanta. 
Wananchi wa kijiji cha Mswakini Juu wakishangilia ujumbe wa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 

MKUU WA WILAYA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA AFUNGA MACHINJIO YA PANGANI KIBAHA KWA MUDA USIOJULIKANA

$
0
0

MKUU wa Wilaya  ya Kibaha  Mkoani Pwani  Bi Assumpter Mshama  ametoa amri ya kufungia  machinjio mapya yaliyopo  Mtaa wa Mtakuja Pangani  Kibaha  Mkoani Pwani kwa muda usiofahamika  kutokana na kukithiri kwa uchafu  unaotishia  afya za walaji  wa eneo  la Kibaha na Vitongoji vyake

Bi Assumpter ametoa amri hiyo muda mfupi uliopita baada ya kufanya ziara ya kushtukiza machinjioni hapo.

Aidha  Bwana Afya Ramadhan Mohammed  ambaye husimamia  shughuli za machinjio hayo amekiri  kuwa  machinjio hayo yanakabiliwa na changamoto nyingi  ikiwa hi pamoja na ukosefu wa maji na umeme.

WAZIRI MKUU APOKEA RIPOTI ZA UCHUNGUZI WA BIASHARA YA ALMASI NA TANZANITE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Spika wa  Bunge, Job Ndugai Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.  Katikati ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza baada ya  kupokea Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Spika wa Buge, Job Ndugai baada ya kukabidhiwa na Spika Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuichunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017. 
Spika wa Buge Job Ndugai akizungumza baada ya kupokea Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati Maalum iliyoundwa na Spika wa Bunge Job Ndugai kuchunguza Biashara ya Tanzaniate wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza  baada ya kukabidhiwa na Spika wa Bunge Job Nduga  Taarifa hiyo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017. 
Baadhi ya Wabunge walioshiriki katika hafla ya kupokea Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuichunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati  Maalum iliyoundwa na Spika ya  Kuchunguza Biashara ya Tanzanite baada ya Spika kupokea Tarifa hiyo na kumkabidhi Waziri Mkuu kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Aliyekaa kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na aliyeka kulia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Job Ndugai. 
Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati  Malum iliyoundwa na Spika   Kuchunguza biashara ya  Almasi baada ya Spika kupokea Taarifa hiyo na kumkabidhi Waziri Mkuu kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septembea 6, 2017. Aliyekaa kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na aliyeka kulia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Job Ndugai. 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea ripoti mbili za kamati ya Maalumu ya Bunge ya kuchunguza biashara ya madini ya almasi na tanzanite na kuahidi kuiwasilisha kwa Rais Dkt. John Magufuli kesho asubuhi.

Pia amesema Serikali haina mchezo katika usimamizi wa rasilimali za Taifa, hivyo amewataka viongozi  na watendaji wote waliokabidhiwa dhamana ya kusimamia sekta ya madini hakikisha wanatimiza vyema wajibu wao.

Waziri Mkuu amepokea ripoti hizo leo (Jumatano, Septemba 6, 2017) kutoka kwa Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai ambaye alikabidhiwa ripoti hizo  na Wenyeviti wa kamati Bw. Mussa Zungu (Almasi) na Bw. Dotto Biteko (Tanzanite).

“Kesho saa 4.30 asubuhi nitaziwasilisha ripoti hizi kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli. Hakuna ucheleweshaji katika jambo hili na Mheshimiwa Spika (Job Ndugai) kesho twende tukakabidhi wote.”

Waziri Mkuu amesema kamati hizo zimefanya kazi nzuri na kwamba Serikali inaimani  na ripoti hizo na ushauri uliotolewa utawezesha Taifa kunufaika na rasilimali zake, hivyo mapendekezo na hoja zote zilizoibuliwa zitafanyiwa kazi katika kipindi kifupi.

Amesema taarifa hiyo zimewasilishwa katika kipindi muafaka na zimeonyesha  dhamira ya dhati ya Bunge, kuunga  mkono juhudi za Rais Dkt. Magufuli  na Serikali yote kwa ujumla katika kulinda rasilimali za Taifa.

“Watanzania ni mashahidi kwamba Mwenyezi Mungu ameijalia Tanzania utajiri wa rasilimali za kila aina.  Tunayo ardhi yenye rutuba, madini ya aina mbalimbali na mengine hayapatikani katika nchi nyingine isipokuwa Tanzania tu kama vile Tanzanite.”

Amesema ni  lazima rasilimali hizo zisimamiwe na kutunzwa vizuri ili ziwezeshe kuboresha hali na maisha ya Watanzania wote na kila mwananchi ana jukumu la kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuleta mageuzi katika Sekta ya madini nchini.

Waziri Mkuu amesema suala la kusimamia rasirimali za nchi ni la Watanzania wote kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 27 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo aliinukuu Ibara hiyo kama ifuatavyo:

“27 (1) kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na Wananchi na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.

“(2) Watu wote watatakiwa na Sheria kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya nchi na pamoja vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu na kuendesha uchumi wa Taifa na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.”

Kamati hizo zilipewa jukumu la kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na Almasi Nchini, ambazo zimeishauri Serikali kuhusiana na mfumo bora wa uendeshaji na udhibiti wa biashara ya Tanzanite na Almasi  nchini.

RAIS DKT MAGUFULI KUPOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA MADINI YA TANZANITE NA ALMASI IKULU JIJINI DAR

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KISWAHILI NA MIRADI YA KUIMARISHA ELIMU MKOA WA KUSINI

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa ofisi ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki mjini Zanzibar
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida wakipeana ishara ya kushukuru mara baada ya Balozi wa Japan kukabidhi miradi miwili mikubwa,mmoja ukiwa ni ujenzi wa uzio wa shule ya Msingi ya Muyuni na wa pili ni mradi wa uboreshaji wa mazingira ya elimu katika wilaya ya ya kusini uliojumuisha ujenzi wa shule ya awali katika kijiji cha Kajengwa na Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida wakikata utepe kama ishara ya kufungua Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuelezea Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida namna Pomboo wanavyovutia utalii katika mkoa wa kusini wakati akimkabidhi zawadi ya sanamu ya Pomboo mara baada ya ufunguzi wa Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

unnamed
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki lililobeba mada isemayo Kuleta Mabadiliko katika jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutumia Kiswahili lilianza leo mjini Unguja, Zanzibar.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoa wa Kusini Unguja kutunza miradi na kuitumia kwa manufaa ya wote.

Makamu wa Rais aliyasema hayo leo wakati wa Ufunguzi wa Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi ambao umefadhiliwa na Ubalozi wa Japan.

Mhe. Samia aliwashukuru Ubalozi wa Japan kwa kufadhili ujenzi wa Uboreshaji wa Mazingira ya Elimu katika Wilaya ya Kusini ambao umegharimu dola za kimarekani laki moja na elfu kumi na mbili na mia nane na arobaini na tano (112,845) ambazo ni sawa na takribani ya shilingi milioni mia mbili arobaini na saba (247) .Awali Ubalozi wa Japan ulitoa dola za Kimarekani elfu ishirini na nane mia nane na sitini (28,860) takribani shilingi milioni sitini na moja za kitanzania kujenga uzio wa shule ya Msingi Muyuni .

Makamu wa Rais alimshukuru sana Balozi wa Japan kwa ufadhili huo ambao umeendelea kuimarisha urafiki na mahusiano kati ya nchi mbili hizi, aliwataka wananchi wa Wilaya ya Kusini kutilia mkazo masuala ya elimu na kutunza miradi yote ili inufaishe na vizazi vijavyo.

Makamu wa Rais pia aliwapongeza viongozi wa halmashauri ya wilaya ya kusini kwa kusimamia vizuri fedha za ufadhili na kufanikisha kukamika kwa ujenzi wa miradi kama ilivyopangwa na kukamilika mapema zaidi .

Kwa Upande wake Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida alisema amefurahishwa na Ushirikiano alioupata kutoka kwa Makamu wa Rais na wakazi wa Wilaya ya Kusini Unguja na kuahidi kwamba Japan itaendelea kusaidia maendeleo ya Tanzania ambapo alisema ufunguzi wa miradi ya leo ni hatua nyingine kubwa ya kuimarisha ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi mbili hizi, Japan na Tanzania.

Wakati huo huoMakamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua Mpango Mkakati wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki 2017-2022 wakati wa Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ambapo aliwataka Viongozi wan chi za jumuiya hiyo kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi ya lugha ya Kiswahili kwani lugha hii inatuunganisha watu wa Afrika Mashariki, pamoja na kuzindua rasmi pia Makamu wa Rais alifungua Ofisi ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki mjini Unguja, Zanzibar.

RC MTAKA APEWA TUZO NA ASASI YA WAZALENDO NA MAENDELEO TANZANIA(AWAMATA)

$
0
0

Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka, tuzo ya cheti kwa niaba ya Mwenyekiti wa UWAMATA Taifa, ambayo imetolewa kwa Mkuu huyu wa mkoa kama alama ya kutambua kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akionesha tuzo ya cheti aliyokabidhiwa na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Kutoka kulia Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka, Katibu wa AMAWATA mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Millensasha Mneo na Afisa Uhusiano wa AWAMATA, Ndg Shushu Joel wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi tuzo ya cheti iliyotolewa kwa Mhe.Mtaka kama alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa AWAMATA na wadau wengine wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kukabidhiwa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa waSimiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akipongezwa na Katibu wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Millensasha Mneo mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya cheti na Asasi hiyo ngazi ya Taifa kama alama ya kutambua mchango na kazi  za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa waSimiyu, Mhe.Anthony Mtaka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Vijana, Zena Mchujuko(kushoto) naAfisa Habari(kulia) wote watumishi katika Ofisi yake mara baada kukabidhiwa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(hayupo pichani) kabla ya kumkabidhi tuzo ya cheti iliyotolewa na Asasi hiyo Ngazi ya Taifa, kama alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo
Katibu wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Millensasha Mneo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(hayupo pichani) kabla ya kumkabidhi tuzo ya cheti iliyotolewa na Asasi hiyo Ngazi ya Taifa, kama alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.



Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amepewa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) ikiwa ni alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.

Akikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa AWAMATA Taifa, Mwenyekiti wa AWAMATA Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo amesema Asasi hiyo imehamasika kutoa tuzo ya cheti kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa sababu ni mzalendo na amekuwa akifikiri juu ya maendeleo ya wananchi na namna mbalimbali za kuzalisha ajira kwa vijana.

Amesema Mhe.Mtaka ni moja ya viongozi wabunifu sana na kama kiongozi kijana amekuwa na maono makubwa yenye manufaa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Taifa kwa ujumla, ambapo amehamasisha uanzishwaji wa viwanda katika Mkoa kupitia Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” na Kilimo cha Umwagiliaji wilayani Busega.

“Mhe.Mtaka tumeanza kumfuatilia toka akiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Wilaya ya Hai mpaka na baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, tumekaa kama asasi tukashawishika kumpa tuzo hii, kwa sababu amekuwa anafanya kazi ya kizalendo na maendeleo hasa anapoumiza kichwa kwa ajili ya kutengeneza ajira; tena kila wilaya kwenye mkoa wake ina kitu cha kufanya” alisema Golyo.

Akipokea tuzo hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameishukuru Asasi ya AWAMATA kwa kutambua mchango wa viongozi wa Mkoa wa Simiyu na akabainisha kuwa imeipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Viongozi wa Mkoa huo pamoja na wadau wote wanaounga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo ya Mkoa na wananchi kwa ujumla.

Mtaka amesema viongozi wa mkoa huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wataendelea kujenga nuru ya matumaini kwa vijana ambao matarajio yao makubwa ni kuona kuwa wanapata kitu cha kufanya ili waweze kuendesha maisha yao.

Ameongeza kuwa miradi mingi inayoendelea ya Kiwanda cha Chaki, kiwanda cha kusindika maziwa na mingine inayofanywa katika ngazi ya viwanda vidogo vidogo ilianzishwa kwa sababu, mkoa unataka kujenga utamaduni kwa wananchi hususani vijana kujua kwamba wanaweza kuthubutu kwa kuanzia ngazi ya chini.

“ Pale Mkula Busega tulianza na vijana waliokuwa wanatengeneza viatu pair mbili tumewapa mtaji wa milioni 12 wameongeza uzalishaji na tumeomba Baraza la uwezeshaji wananchi Kiuchumi watawapa fedha ili wanunue mashine kubwa, pia tunajipanga kwa kilimo cha umwagiliaji; tunataka kuwa Mkoa ambao wananchi wake wana kitu cha kufanya na wanakiona kwenye vitendo badala ya kukiona kwenye hotuba nzuri.”

Katika hatua nyingine Mtaka amewaambia viongozi wa AWAMATA kuwa, pamoja na kutoa tuzo kwa viogozi kama walivyofanya kwake wanapaswa pia kuwakosoa viongozi hususani vijana bila kuwaonea (kuwakosoa katika haki) pale wanapoona hawafanyi vizuri, hii itawasaidia kuthibitisha dhamira ya Mhe.Rais ya kuwateua, maana ya kupewa uongozi katika kipindi hiki na kubeba dhamana kwa vizazi vijavyo.

Wakati huo huo ametoa wito kwa Viongozi wenzake vijana kutimiza wajibu wao, kuepuka maneno yanayowasahaulisha walikotoka wanapozungumzia maisha ya vijana wenzao na kukubali kukosolewa, ili wajengwe kuwa viongozi wazuri wa leo na vizazi vijavyo; kwa kuwa matarajio ya Rais katika kuwateua ni kuwa na kizazi endelevu kwenye uongozi wa nchi.

Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) ni asasi ya Kiraia inayojishughulisha na uelimishaji wa uzalendo kwa Watanzania na kufundisha mbinu za kujitegemea ili kuondokana na umaskini pia inatoa tuzo kwa watu wanaofanya vizuri masuala mbalimbali ya kizalendo na kuwasaidia wananchi kutoka katika umaskini.

ASILIMIA 82 YA WASICHANA HAWANA TAARIFA SAHIHI KUHUSU HEDHI

$
0
0
Afisa Sera kutoka TAWASANET,Darius Mhawi katika warsha ya Afya na Maji wakati wa Tamasha la Jinsia mwaka 2017 linalofanyika jijini Dar es salaam

*****
Imeelezwa kuwa asilimia 82 ya wasichana nchini Tanzania hawana taarifa sahihi kuhusiana na mabadiliko ya miili yao na namna sahihi ya kukabiliana na changamoto kipindi cha hedhi hali inayosababisha baadhi yao kushindwa kuhudhuria masomo yao shuleni.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Septemba 6,2017 na Afisa Sera kutoka Taasisi ya Tanzania Water and Sanitation Network (TAWASANET),Darius Mhawi katika warsha ya Afya na Maji wakati wa Tamasha la Jinsia mwaka 2017 linalofanyika kwenye Viwanja vya TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam.
Mhawi alisema wasichana wengi hawana elimu kuhusu mabadiliko ya miili yao hali inayosababisha washindwe kuwa katika mazingira safi na salama wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.

Alisema kwa Mujibu wa utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mwaka 2014/2015 takwimu zinaonesha kuwa msichana mmoja kati ya 10 hushindwa kuhudhuria shule kwa wastani wa siku nne kila baada ya wiki nne hali inayosababisha kukosa masomo shuleni.

“Hedhi huathiri Wasichana wanapokuwa shuleni kwa kuwafanya kuwa na hofu ama aibu ya kuchafuka,wengine hupata maumivu ya tumbo na kichwa na baadhi kuwa na hisia za kunyanyaswa na wenzao hasa wavulana”,alieleza Mhawi.

Mhawi alisema ili kuondoa changamoto za hedhi katika ngazi ya shule ni wakati mzuri sasa elimu ya hedhi iingizwe katika mtaala wa elimu,jamii kuvunja ukimya na kutoona aibu kuzungumzia masuala ya hedhi kwa rika zote katika jamii.

“Inatakiwa pia kuwepo na upatikanaji wa vifaa salama kwa ajili ya udhibiti wa hedhi na kwa gharama nafuu,kuwepo kwa vyoo bora katika mazingira ya shuleni na utoaji wa huduma ya maji safi na sabuni”,aliongeza Mhawi.
Nao washiriki wa warsha hiyo waliziomba halmashauri za wilaya kutenga bajeti maalum kwa ajili ya kushughulikia changamoto za hedhi kwa wasichana shuleni.

Kwa upande wake Rehema Zobonko kutoka halmashauri ya Kisarawe mkoa wa Pwani alizishauri halmashauri za wilaya nchini kuwa na bajeti zinazozingatia masuala ya kijinsia na kutoa taulo laini bure kwa wasichana na kutenga vyumba maalum kwa ajili ya watoto wa kike kujihifadhi wanapokuwa katika hedhi.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog – Dar es salaam

Afisa Sera kutoka TAWASANET,Darius Mhawi akizungumza katika warsha ya Afya na Maji wakati wa Tamasha la Jinsia mwaka 2017 linalofanyika jijini Dar es salaam.

Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada ukumbini.

Diwani wa kata ya Songwa halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga Mohammed Ngolomole akichangia hoja katika warsha ya maji na afya

Washiriki wakiwa ukumbini.

Afisa Sera kutoka TAWASANET,Darius Mhawi akisisitiza jambo wakati wa warsha hiyo.

Washiriki wa warsha hiyo wakiwa katika kazi ya kikundi.

Washiriki wa warsha hiyo wakijadiliana.

Rehema Zobonko kutoka halmashauri ya Kisarawe mkoa wa Pwani akiwasilisha kazi ya kundi lake.Picha na Kadama Malunde – Malunde1 blog

MIAKA 40 ya FAO NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Bw. Jose Graziano da Silva akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana tarehe 5 Septemba 2017 wakati wa sherehe za miaka 40 ya FAO hapa nchini kwenye hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.




 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Bw. Jose Graziano da Silva akihutubia wakati wa sherehe za miaka 40 ya Shirika hilo hapa nchini ambayo ilifanyika kwenye hotel ya Serena jijini Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana tarehe 5 Septemba 2017.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Bw. Jose Graziano da Silva akihutubia wakati wa sherehe za miaka 40 ya Shirika hilo hapa nchini ambayo ilifanyika kwenye hotel ya Serena jijini Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana tarehe 5 Septemba 2017.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa shrerehe za miaka 40 ya FAO hapa nchini Tanzania ambapo sherehe hiyo ilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Bw. Jose Graziano da Silva pamoja na Mawaziri wa Kilimo kutoka Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na Mabalozi kutoka nchi mbali mbali na viongozi wengine.

SPIKA NDUGAI APOKEA TAARIFA ZA KAMATI MAALUM ZA KUCHUNGUZA BIASHARA YA TANZANITE NA ALMASI LEO MJINI DODOMA

$
0
0

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimkabidhi Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Taarifa za Kamati Maalum ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi katika tukio lililofanyika leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.





Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akikabidhiwa Taarifa ya Kamati Maalum ya Kuchunguza Biashara ya Almasi na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mussa Azzan Zungu (kulia) katika tukio lililofanyika leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Kulia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe



Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akikabidhiwa Taarifa ya Kamati Maalum ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dotto Biteko (kulia) katika tukio lililofanyika leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma. kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Kulia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuchunguza Almasi, Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza wakati wa uwasilishaji wa Taarifa za Kamati Maalum ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi katika tukio lililofanyika leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuchunguza Tanzanite, Mhe. Dotto Biteko akizungumza wakati wa uwasilishaji wa Taarifa za Kamati Maalum ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi katika tukio lililofanyika leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.

Kiongozi wa Upinzani Bunge, Mhe. Freeman Mbowe akizungumza wakati wa uwasilishaji wa Taarifa za Kamati Maalum ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi katika tukio lililofanyika leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza wakati wa uwasilishaji wa Taarifa za Kamati Maalum ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi katika tukio lililofanyika leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza wakati wa uwasilishaji wa Taarifa za Kamati Maalum ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi katika tukio lililofanyika leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia waliokaa), Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (wa pili kushoto waliokaa), Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto waliokaa) na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe (kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati Maalum ya Kuchunguza Biashara ya Almasi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mussa Azzan Zungu katika tukio lililofanyika leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia waliokaa), Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (wa pili kushoto waliokaa), Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto waliokaa) na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe (kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati Maalum ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dotto Biteko katika tukio lililofanyika leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia waliokaa),Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (wa pili kushoto waliokaa), Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto waliokaa) na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe (kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupokea Taarifa ya Kamati Maalum ya Kuchunguza Biashara ya Almasi na Tanzanite katika tukio lililofanyika leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.


PICHA NA OFISI YA BUNGE

TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM

$
0
0


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limekabidhi majengo mawili ya nyumba za walimu, shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Bwawa la kufua umeme wa maji Mtera, (Mtera Hydro Power Plant), lililoko katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa.
Nyumba hizo zilizogharimu shilingi milioni 35, moja ikiwa mpya na nyingine imekarabatiwa, zimekabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa Septemba 6, 2017 na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja, Bi. Joyce Ngahyoma, ambaye alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Dkt. Tito Mwinuka.
Akizungumza kabla ya kukabidhi nyumba hizo, Bi. Joyce Ngahyoma alisema, wakazi wa kata ya Mtera ni wadau na washirika wakubwa wa TANESCO katika kulinda miundombinu ya umeme ya kituo cha kufua umeme cha Mtera ambayo ina gharama kubwa kwa hivyo walipowasilisha maombi ya kujengewa nyumba ya mwalimu Mkuu, TANESCO ilikubali ombo hilo bila kusita.
Alisema, uongozi wa TANESCO baada ya kupokea maombi hayo ulifanya tathmini na kutoa kiasi cha fedha shilingi Milioni 35 ambazo zilitumika kujenga nyumba jipya na kukarabati nyumba nyingine.
Nyumba mpya iliyojengwa na TANESCO kwa ajili ya makazi ya Mwalimu Mkuu, ina vyumba vinne, choo, bafu na jiko, alisema.
“Napenda nichukue fursa hii kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia na niwaahidi tu kwamba Shirika litaendelea kushirikiana na serikali na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha sekta ya elimu, afya na huduma nyingine zinaimarika kwa kutoa michango ya hali na mali.” Alisema Bi. Ngahyoma.
Alisema, sambamba na msada huo, TANESCO imekuwa ikisaidia jamii ya wana Mtera, katika kuwapatia huduma ya afya kwenye zahanati ya wafanyakazi, huduma ya elimu ya awali(chekechea), kwenye shule ya chekechea iliyojengwa kuhudumia watotot wa wafanyakazi, na pia usafiri, ambapo mabasi yanayochukua wafanyakazi kwenda na kutoka kazini, huwasaidia pia wananchi.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia ufuaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa, alisema, Kituo cha kufua umeme wa maji Mtera, kilijengwa kuanzia mwaka 1984 na kukamilika mwaka 1988 na kuwa na uwezo wa kufua umeme Megawati 80 na tangu kipindi hicho hadi hivi sasa, TANESCO imekuwa ikishirikiana na wananchi katika kulinda miundombinu ya kituo hicho.
Mnamo mwaka 2005 na 2006, Shirika lilichangia kiasi cha shilingi milioni 34 kujenga madarasa mawili mapya na ujenzi wa ofisi ya walimu, alisema Mhandisi Ikwasa.
Akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kupokea majengo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. Jabir Shekimweri, amewataka wananchi wa Kata ya Mtera,  kuendelea kushirikiana na TANESCO, katika kulinda miundombinu ya Shirika hilo kwenye bwawa la kufua umeme wa maji la Mtera, (Mtera Hydro Power Plant).
“Ndugu zangu msada huu umekuja kutokana na faida inayopatikana kutokana na miundombinu hiyo, kwa hivyo niwaombe muendelee kushirikiana na TANESCO na viongozi wa serikali ya kijiji katika kuhakikisha usalama wa miundombinu hiyo unaendelea kuwepo kwani wafanyakazi wa TANESCO pekee hawawezi kulinda miungdominu hiyo peke yao kwa sababu eneo ni pana sana.” Alifafanua.
Mhe. Shekimweri alisema, msada wa majengo hayo, utasaidia kutatua changamoto ya nyumba kwa walimu ambao kutokana na uhaba mkubwa wa nyumba walimu wanaishi maeneo ya mbali na shule na hivyo inapelekea utendaji kazi wao kuwa wa chini.
“Nimeambiwa kuwa ufaulu kwenye shule hii ni mzuri na walimu wakiishi maeneo ya karibu na shule, basi ufaulu huo bila shaka utaongezeka sana.” Alisema.
Lakini pia niwaombe wananchi, umeme unaopatikana hapa unategemea sana uwepo wa maji, kwa hivyo nitoe rai, ni lazima tutumie maji haya kwa busara kubwa naelewa zipo shughuli za uvuvi lakini uvuvi mwingine ni ule haramu wa uharibifu, niwajulishe tu hivi karibuni tutakaa kikao ili kuweka matumizi bora ya maji haya ili kuzuia athari zinazoweza kupelekea uharibifu wa vyanzo vya maji yanayoletwa kwenye bwawa hili, alisisitiza.

Mkuu huyo wa wilaya aliishukuru TANESCO kwa kuisaidia serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwenye eneo hilo na .
“ Nimeambiwa kuwa sio tu mmesaidia ujenzi wa nyumba moja mpya na kukarabati nyingine lakini pia mmekuwa mkisaidia wananchi katika kuwapatia huduma za afya kwenye zahanati ya wafanyakazi, hali kadhalika mmekuwa mkiwasaidia wananchi katika usafiri ambapo wamekuwa wakitumia usafiri wa wafanyakazi wenu, hili ni jambo jema katika kujenga mahusiano mema baina yenu na wananchi.” Aliongeza Bw. Shekimweri.


Mkuuwa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mhe.Jabir Shekimweri, (kushoto), akifungua pazia ikiwa ni ishara ya kuzindua nyumba mpya ya Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Kituo cha Kufua Umeme wa maji, Mtera, katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa, Septemba 6, 2017. Nyumba hiyo na nyingine iliyokarabatiwa zimejengwa kwa msada wa TANESCO kwa thamani ya shilingi milioni 35. Wengine pichani, ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja mama Joyce Ngahyoma,(wakwanza kulia), aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, , (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia Ufuaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa. (kushoto), na Mkuu wa shule hiyo, Bw. Simon Dissa.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limekabidhi majengo mawili ya nyumba za walimu, shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Bwawa la kufua umeme wa maji Mtera, (Mtera Hydro Power Plant), lililoko katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa.
Nyumba hizo zilizogharimu shilingi milioni 35, moja ikiwa mpya na nyingine imekarabatiwa, zimekabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa Septemba 6, 2017 na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja, Bi. Joyce Ngahyoma, ambaye alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Dkt. Tito Mwinuka.
Akizungumza kabla ya kukabidhi nyumba hizo, Bi. Joyce Ngahyoma alisema, wakazi wa kata ya Mtera ni wadau na washirika wakubwa wa TANESCO katika kulinda miundombinu ya umeme ya kituo cha kufua umeme cha Mtera ambayo ina gharama kubwa kwa hivyo walipowasilisha maombi ya kujengewa nyumba ya mwalimu Mkuu, TANESCO ilikubali ombo hilo bila kusita.
Alisema, uongozi wa TANESCO baada ya kupokea maombi hayo ulifanya tathmini na kutoa kiasi cha fedha shilingi Milioni 35 ambazo zilitumika kujenga nyumba jipya na kukarabati nyumba nyingine.
Nyumba mpya iliyojengwa na TANESCO kwa ajili ya makazi ya Mwalimu Mkuu, ina vyumba vinne, choo, bafu na jiko, alisema.
“Napenda nichukue fursa hii kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia na niwaahidi tu kwamba Shirika litaendelea kushirikiana na serikali na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha sekta ya elimu, afya na huduma nyingine zinaimarika kwa kutoa michango ya hali na mali.” Alisema Bi. Ngahyoma.
Alisema, sambamba na msada huo, TANESCO imekuwa ikisaidia jamii ya wana Mtera, katika kuwapatia huduma ya afya kwenye zahanati ya wafanyakazi, huduma ya elimu ya awali(chekechea), kwenye shule ya chekechea iliyojengwa kuhudumia watotot wa wafanyakazi, na pia usafiri, ambapo mabasi yanayochukua wafanyakazi kwenda na kutoka kazini, huwasaidia pia wananchi.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia ufuaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa, alisema, Kituo cha kufua umeme wa maji Mtera, kilijengwa kuanzia mwaka 1984 na kukamilika mwaka 1988 na kuwa na uwezo wa kufua umeme Megawati 80 na tangu kipindi hicho hadi hivi sasa, TANESCO imekuwa ikishirikiana na wananchi katika kulinda miundombinu ya kituo hicho.
Mnamo mwaka 2005 na 2006, Shirika lilichangia kiasi cha shilingi milioni 34 kujenga madarasa mawili mapya na ujenzi wa ofisi ya walimu, alisema Mhandisi Ikwasa.
Akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kupokea majengo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. Jabir Shekimweri, amewataka wananchi wa Kata ya Mtera,  kuendelea kushirikiana na TANESCO, katika kulinda miundombinu ya Shirika hilo kwenye bwawa la kufua umeme wa maji la Mtera, (Mtera Hydro Power Plant).
“Ndugu zangu msada huu umekuja kutokana na faida inayopatikana kutokana na miundombinu hiyo, kwa hivyo niwaombe muendelee kushirikiana na TANESCO na viongozi wa serikali ya kijiji katika kuhakikisha usalama wa miundombinu hiyo unaendelea kuwepo kwani wafanyakazi wa TANESCO pekee hawawezi kulinda miungdominu hiyo peke yao kwa sababu eneo ni pana sana.” Alifafanua.
Mhe. Shekimweri alisema, msada wa majengo hayo, utasaidia kutatua changamoto ya nyumba kwa walimu ambao kutokana na uhaba mkubwa wa nyumba walimu wanaishi maeneo ya mbali na shule na hivyo inapelekea utendaji kazi wao kuwa wa chini.
“Nimeambiwa kuwa ufaulu kwenye shule hii ni mzuri na walimu wakiishi maeneo ya karibu na shule, basi ufaulu huo bila shaka utaongezeka sana.” Alisema.
Lakini pia niwaombe wananchi, umeme unaopatikana hapa unategemea sana uwepo wa maji, kwa hivyo nitoe rai, ni lazima tutumie maji haya kwa busara kubwa naelewa zipo shughuli za uvuvi lakini uvuvi mwingine ni ule haramu wa uharibifu, niwajulishe tu hivi karibuni tutakaa kikao ili kuweka matumizi bora ya maji haya ili kuzuia athari zinazoweza kupelekea uharibifu wa vyanzo vya maji yanayoletwa kwenye bwawa hili, alisisitiza.
Mkuu huyo wa wilaya aliishukuru TANESCO kwa kuisaidia serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwenye eneo hilo na .
“ Nimeambiwa kuwa sio tu mmesaidia ujenzi wa nyumba moja mpya na kukarabati nyingine lakini pia mmekuwa mkisaidia wananchi katika kuwapatia huduma za afya kwenye zahanati ya wafanyakazi, hali kadhalika mmekuwa mkiwasaidia wananchi katika usafiri ambapo wamekuwa wakitumia usafiri wa wafanyakazi wenu, hili ni jambo jema katika kujenga mahusiano mema baina yenu na wananchi.” Aliongeza Bw. Shekimweri.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja, Mama Joyce Ngahyoma,(aliyesimama), akitoa hotuba kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.
 Mama Joyce Ngahyoma
 Mkuuwa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mhe.Jabir Shekimweri, (aliyesimama), akitoa hotuba yake kwenye hafla hiyo.
 Nyumba mpya ya Mawlimu Mkuu shule ya sekondari Mtera DAM, iliyojengwa na TANESCO na nyingine iliyokarabatiwa kwa thamani ya shilingi milioni 35.
 Mkuu wa Wilaya Mhe. Shekimweri, (kulia), na Mama Joyce Ngahyoma, wakiwa mbele ya nyumba hiyo baada ya kuizindua na kuikabidhi kwa Mkuu wa shule.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumzia utaratibu wa kukabidhi nyumba hizo.
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo wakiwa na furaha.
 Mkuu wa shule ya sekondari Mtera DAM, Bw. Simon Dissa, akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo aliishukuru TANESCO kwa kupunguza uhaba wa nyumba za walimu na sasa bado wanahitaji nyumba 15.
  Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo wakiwa na furaha.
 Wananchi wakifurahia hotuba
 Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANESCO wakiongozwa na Mama Joyce Ngahyoma.
Meneja wa Kituo cha Kufua Umeme wa Maji Mtera, Mhandisi John Skauki, akielezea ushirikiano baina ya TANESCO na wana jamii ya Mtera ambao alisema ni mzuri.
Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO
Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO walio katika Kituo cha Kufua umeme wa maji Mtera, wakifuatilia hafla hiyo

MAGAZETI YA ALHAMIS LEO SEPT 7, 2017

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images