Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSIANA NA SIKUKUU YA EID-EL-FITR.

$
0
0
Jeshi la Polisi Nchini linatoa shukrani kwa wananchi wote wakiwemo waandishi wa habari, viongozi wa dini, wanasiasa, makampuni binafsi ya ulinzi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa njia mbalimbali katika kuhakikisha kwamba nchi yetu ya Tanzania inakuwa salama na raia wote wanaishi kwa amani na utulivu bila hofu ya uhalifu na wahalifu. 

Katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki na za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo wanamoishi na sehemu mbalimbali zikiwemo maeneo ya biashara. 

Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe. Uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu. Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha kwamba, wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu, pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.  
Aidha, wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara, wanatakiwa kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini.

Katika kuhakikisha usalama kwenye kumbi za starehe, wamiliki wa kumbi hizo wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi. Vilevile, wazazi wawe makini na watoto wao na hasa disko toto, ili kuepuka ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao.

Wananchi wanatakiwa kuwa makini hususani watokapo kwenye makazi yao, wasiache nyumba wazi ama bila mtu na pale inapobidi watoe taarifa kwa majirani zao. Wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu wasikae kimya bali watoe taarifa haraka kwenye vituo vya Polisi vilivyo karibu nao ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.
  
Vilevile, Jeshi la Polisi linawatahadhalisha wananchi kuwa makini na matapeli yanayotumia majina ya viongozi, watu maarufu na wafanyabiashara wakubwa ili kujipatia pesa na vitu mbalimbali. Matapeli hao wamekuwa wakitumia ujumbe mfupi wa simu za mkononi kupata taarifa za mtu binafsi hatimae mtu huyo kuibiwa. 
 
Ndugu wanahabari,

Kufuatia agizo la Mhe. Rais la kuwataka watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha silaha hizo, pamoja na watu wote wanaoingia ama kuishi na kufanya shughuli hapa nchini bila kufuata utaratibu (wahamiaji haramu) kutakiwa kuondoka au kuharalisha ukaazi wao, Jeshi la Polisi linawataka watu hao kuendelea kutekeleza agizo hilo la Serikali kabla ya Operesheni kabambe kuanza itakayoendeshwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo Vingine vya Ulinzi na Usalama.

Aidha, baadhi ya watu hao tayari wamekwishasalimisha silaha wanazozimiliki kinyume cha sheria na pia baadhi ya wahamiaji haramu wameanza kuondoka hususani katika mikoa ya Kagera na Kigoma. Hiyo ni hatua nzuri, tunawataka wale wote ambao bado hawajatekeleza agizo hilo, waendelee kufanya hivyo haraka kabla ya muda wa msamaha kumalizika. 
Mwisho, napenda kuwahakikishia wananchi kwamba, Jeshi la Polisi linatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria za nchi na hivyo halitawajibika kumwonea huruma ama upendeleo mtu yeyote atakayeenda kinyume na sheria. 

NAWATAKIENI WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA
EID –EL-FITR 
Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polis

MGODI UNAOTEMBEA: Tanzania haina sababu ya kuivamia Rwanda

$
0
0
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

NITAMSHANGAA Mtanzania yoyote anayeweza kufurahia nchi za Tanzania na Rwanda kuendelea kurushiana maneno makali kuonyesha uhusiano mbaya ulioanza kwa siku za hivi karibuni.

Tangu Mwezi Mei mwaka huu wa 2013, baadhi ya matamko mabaya yamekuwa yakitolewa na viongozi wa Rwanda. Wanasema mengi kuonyesha chuki zao kwa Watanzania na rais wao kwa ujumla. Kwa kuangalia sakata lote linaloshika kasi, ila si sababu ya Tanzania kujibu mashambulizi dhidi ya Taifa hilo linaloongozwa na Paul Kagame, maana ni kuzidi kukuza uhasama huo.

Ni wazi kuwa nchi ya Rwanda inayotajwa kufadhili machafuko nchini Kongo, hasa kwa kikundi cha M23 inaleta chokochoko kwa Tanzania, pale Rais Kikwete, alipowataka wakae na waasi kujadili tatizo. Hali hii inashangaza mno. Kauli ya furaha inapobadilishwa na kuwa chuki na uhasama, tena bila sababu za msingi. Labda kuna sababu nyingine, ila si haya yaliyozungumzwa na Kikwete.

Wakati naangalia kwa kina mtifuano huo, kwa upande wangu nitakuwa wa mwisho kufurahia au kuombea mabaya kwa mataifa haya mawili, yani Tanzania na Rwanda. Tanzania ili iweze kukua kiuchumi, inahitaji ushirikiano kutoka kwa majirani zake. Nchi hizi zinategemeana. Rwanda wanaihitaji Tanzania na Watanzania wanahitaji uwapo wa ndugu zao.

Sipendi kuona uhusiano mbaya kwa nchi za Tanzania na Rwanda unakua, nikiamini ni hatua isiyokuwa na faida zaidi ya hasara kwa mataifa haya mawili yanayopigania kujitawala wenyewe. Katika hotuba yake aliyoitoa mwishoni mwa mwezi uliopita, Rais Kikwete alielezea mambo mengi dhidi ya Rwanda, akisititiza kuwa alinukuliwa vibaya na ushauri wake kupindishwa. Rais Kikwete aliwatangazia umma kuwa hakuna sababu ya kugombana na Rwanda, japo alikiri kutukanwa na majirani zetu hao.

Haya ni matatizo makubwa kwa viongozi wa Afrika. Kagame, akiwa kama rais wa Rwanda, ni vyema akazingatia nidhamu katika utawala wake. Kagame anapaswa kujua faida ya amani inavyoweza kuwafanya wananchi wake waishi vizuri. Wananchi wa Rwanda wasingependa kuona wapo viongozi wanaotamani kulifanya Taifa hilo liingie kwenye hatari.

Kadhia waliyoipata mwaka 1994 inatosha. Roho za Rwanda ziliangamia bila sababu. Kama hivyo ndivyo, nani anaweza kusimama hadharani akachochea vita, huku akijua kuwa hana faida navyo? Nani anayeweza kuelezea faida ya vita, hasa kwa Tanzania na Rwanda, ambazo zenyewe zinahitaji kuishi kwa kutegemea wahisani, Mataifa makubwa? Huu si wakati wa kujenga uhasama. Huu ni wakati wa viongozi wa nchi za Afrika kukaa pamoja na kusema kwa kauli moja namna ya kuyasaidia mataifa yao.

Mrwanda apinge kwa nguvu zote kama kuna chokochoko zinazofanywa, zinazotakiwa kufanywa na viongozi wao leo au kesho. Mtanzania, Mkenya, Mburundi, Mkongo na wengine wote wapinge kama kuna anayetaka kumsumbua mwenzake kwa namna moja ama nyingine.  Inawezekana wakati mwingine kunatokea migongano ya kimaslahi, ila hakuna ugomvi usiokuwa na njia ya kusuluhishwa. Mazungumzo mara kadhaa huleta tija na kudumisha jamii bora.

Hakuna nchi iliyoendelea kwa kupenda vita, hasa hizi zinazoishi kwa misaada kutoka nchi za watu. Ukiacha roho za watu zinavyoangamia katika machafuko, pia nchi zinatumia gharama kubwa kujilinda au kujibu mashambulizi au kununua silaha kwa fedha za kujenga shule, vituo vya afya na huduma nyingine muhimu kwa wananchi wao.

Rais Kikwete ameyaona haya. Na kutokana na ustahimilivu wake, akabaini kuwa hakuna sababu ya maana ya kulumbana na Rwanda, sababu ikiwa kuwashauri kumaliza tofauti zao na waasi. Kauli hii haikuungwa mkono na Kagame. Maneno ya kejeli yakaanza kushika kasi, sambamba na vijana wao, ikiwa ni njia ya kufikisha matusi kwa Watanzania kwa njia mbalimbali, ikiwamo mitandao ya kijamii.

Ukiingia katika mitandao mbalimbali na kufuatilia uhasama huu, utagundua kuwa umefikia wakati mbaya mno. Inahitaji moyo mno kujitangaza kuwa wewe ni Mtanzania mbele ya Mrwanda.  Hii si njia nzuri kwa mataifa haya. Nchi ya Tanzania amani ni jambo la lazima kwa wananchi wake. Ingawa ina makabila zaidi ya 120, ila yameishi kwa upendo wa hali ya juu.

Wanapokutana Wazigua na Wasukuma, huwezi ona tofauti yao. Wanaishi kama ndugu. Huwezi kuona malumbano kati ya Wangoni na Wachaga. Haya ni mambo ya kupongezwa na Watanzania wote. Amani hii ni tunu kutoka kwa Mungu. Ingawa hatuna utajiri wa kupindukia, ila maisha yetu yamekuwa na furaha tele, jambo linalotangaza sisi ni nani.

Kwasababu hiyo, yoyote anayeona ana hamu ya kulichanganya Taifa hili, basi aangalie mara mbili. Japo uwezo wa kufanya lolote upo, lakini nini chanzo?  Chanzo kiwe hiki cha viongozi kushauriana? Kwani kuna ulazima kufuata ushauri ambao huutaki? Kwanini sasa ubabaike kwa kushauriwa?

Alipokuwa Tanzania katika ziara yake, Rais wa Marekani, Barrack Hussein Obama, aliulizwa juu ya machafuko yanayoendelea nchini Kongo. Obama alijibu huku akionyesha kuwa rais wa Tanzania, Kikwete, ana uwezo wa kuyafanyia kazi hayo, maana yapo ndani ya uwezo wake.

Kauli hii sio tu imemjenga Kikwete nje ya mipaka yake, pia imeonyesha namna gani Watanzania wanaongozwa na rais mwenye mtazamo wa kina.  Haya yanapotokea, kwa rais asiyejitambua, rais mwenye ubinafsi na ubabe usiokuwa na tija, ana uwezo wa kuchukia kama inavyoonekana sasa.

Anawaza kwanini asiwe yeye? Na inapotokea mmoja wapo, ikiwamo Rwanda inaanzisha chokochoko, kama mmoja wao anakuwa hajitambui, uhasama huo utaongezeka. Ni vyema wananchi wakapinga kwa nguvu zote kama viongozi wao wanataka kuwaingiza kwenye uhasama. Watu zaidi 500,000 waliripotiwa kupoteza maisha katika mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Ni idadi kubwa mno. Sitarajii kuona vifo hivyo vimesahauliwa na wananchi sambamba na viongozi wao. Ndio maana nasema, suala la machafuko si la kuchekea. Linazalisha vizazi tegemezi. Linazalilisha watu kwa kiasi kikubwa mno, hivyo halistahili kuchekewa. Watu wanazikimbia nchi zao bado wanazipenda.

Akina mama wajawazito na watoto ndio wanakuwa wahanga wakubwa katika hilo. Wengine wanapoteza maisha kutokana na njaa, shida ya maji na mengineyo. Wengine wanaingiliwa kimwili bila lidhaa yao. Kama haya yanatokea, nani anaumia? Ni wakati sasa wa viongozi wa Afrika kudumisha umoja na mshikamano.

Hakuna Tanzania, Rwanda, Kongo, Burundi, Kenya, Msumbiji ama Uganda. Hizi nchi zote zinapaswa kuishi kwa upendo na kushirikiana kibiashara. Hatuhitaji uhasama wa aina yoyote kutoka Rwanda, kama njia ya kukuza uchumi wa nchi hizi mbili. Wapo baadhi yao wanaochekea machafuko.

Hawa wameshindwa kung’amua machungu wanayokutana nayo wana jamii wengine kutokana na matokeo hayo. Mwisho kabisa, napongeza kwa nguvu zote kauli ya Rais Kikwete, nikiamini kuwa ni mwenye busara. Pamoja na matusi yote anayotukanwa, akidhalilishwa, ila yeye anaona hakuna sababu ya kujibizana vibaya na majirani zao hao, japo uwezo huo upo.

Rwanda ni Taifa dogo mno. Kinguvu halina ubavu hata robo ya kupambana na ubavu wa Tanzania. Na wenyewe wanajua hilo. Hata hivyo hakuna sababu kubwa juu ya suala hilo. Muhimu ni viongozi wa nchi zote za Afrika kupendana, kuhubiri amani katika vikao vyao, maana ndivyo vinavyoweza kuleta maendeleo kwa nchi zao.

Watanzania tunawapenda na kuwaheshimu majirani zetu, japo sio sababu ya kuonekana si lolote, maana tunajua uwezo tunao, tena mkubwa mno.
+255 712053949

Wakazi waishio maeneo ya pembezoni ya Dar es Salaam waifagilia Mobile Clinic ya Benki ya NBC

$
0
0
Mhudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (mobile clinic) la Benki ya NBC, Wilbard Kiria (kushoto) akimpa mtoto Shackshazi Rahim dawa ya minyoo katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari hilo katika eneo la Kunduchi Beach nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini.
Mtoto mkazi wa Kunduchi, Rukia Ramadhani akipimwa uzito katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (Mobile Clinic) la Benki ya NBC mahali hapo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini. Anayempimawa pili kulia ni muuguzi wa gari hilo, Eliza Shayo.
Mhudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (mobile clinic) la Benki ya NBC, Wilbard Kiria (kushoto) akimpa mtoto Gift Lucas dawa ya minyoo katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari hilo katika eneo la Kunduchi Beach nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini. 

SALAMU ZA EID KUTOKA KWA MDAU MAC

Huge fire forces Nairobi airport shutdown

$
0
0
The fire broke out in the immigration section of the departure lounge, and quickly spread to the arrivals hall
A "massive" fire has broken out at Nairobi's Jomo Kenyatta International airport, forcing one of East Africa's largest transport hubs to shut down, officials say.

"There is a serious fire at JKIA [airport], but we are doing everything possible to avert a crisis," Mutea Iringo, a senior official at Kenya's interior and national coordination ministry, said on Wednesday. "Apart from emergency landings, all flights into and out of JKIA have been cancelled, [the] airport has been shut down," added the official.

The fire at east Africa's busiest airport started at around 5:00am local time (02:00 GMT) in the immigration section of the departure lounge and spread to the international arrivals area, a Kenya Civil Aviation Authority official said on condition of anonymity. Kenya's National Disaster Operation Centre, in an update given at 05:00GMT, said that while the blaze had been brought under control in the international departures areas, fire was still burning at the arrivals terminal.
All roads around the airport had been closed except to emergency traffic, it added. "This is a major crisis," said senior transport ministry official Michael Kamau. There were no initial reports of casualties, but Iringo said the fire was "massive", adding that the arrivals and immigration sections were "totally damaged".

Firefighters were tackling the blaze, while flights were being diverted to other airports, the interior ministry said in a statement. Stranded passengers stood on sidewalks outside the airport with their luggage in hand. Al Jazeera's Catherine Soi, reporting from the site of the fire, said that the government had set up a crisis team and investigators were looking into the cause of the blaze.

Images on Kenyan media showed flames rising high in the sky and billowing clouds of black smoke out of the main arrivals and departures terminal, with dozens of police and fire trucks at the scene. The airport serves as a regional hub for east Africa, with many long-distance international flights landing there to connect to countries across the region.

Wednesday's fire comes less than 48 hours after a fuel jet pump failure caused huge delays at the airport, forcing some flights to be rerouted to the airport in the coastal town of Mombasa, Entebbe International Airport in Uganda and Kigali International Airport in Rwanda.
Source:Al Jazeera and agencies.

Nairobi Airport Fire: Large Blaze Closes Jomo Kenyatta Internation

TANAPA NDANI YA MAONESHO YA NANENANE MKOANI MOROGORO.

$
0
0
MHIFADHI mkuu hifadhi ya Taifa mlima Udzungwa Vitalis Uruka akitoa maelezo kwa watu waliotembelea banda la TANAPA ndani ya viwanja vya mwalimu Julius Nyerere maarufu Nanenane mjini Morogoro.Tanzania inajumla ya Hifadhi 16. 
KAIMU Mhifadhi Mkuu hifadhi ya Taifa Mikumi Dattomax Sellanyika akihojiwa na mwandishi wa habari wa kituo cha radio TIMES FM cha Jijini Dar es Salaaam Adam Hussein, pembeni ni Mhifadhi mkuu hifadhi ya Taifa mlima Udzungwa Vitalis Uruka.Tanzania inajumla ya Hifadhi 16,kwenye maonesho yanayoendelea ya Nane nane mkoani Morogoro.

AIRTEL YATOA CHAKULA CHA FUTARI NA IDDI KWA YATIMA DAR

$
0
0
Afisa mauzo wa Airtel, Bw Salehe Safi akimkabidhi Bibi Saada Omary moja ya zawadi zilizotolewa na kampuni za simu za mkononi ya Airtel kwenye kituo cha watoto yatima kinachofahamika kwa jina la Mwana Orphanage Center kilichopo Vingunguti jijini Dar es salaam. AIRTEL ilitoa sukari, mchele, mafuta, sabuni, maziwa na Unga wa ngano kwaajili ya kumalizia mwezi wa Ramadhani na kusheherekea sikukuu ya IDDI

Rais Kikwete na Mama Salma Wamjulia hali Mh. john Momose Cheyo alielazwa hospitali ya Aga Khan jijini Dar

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali mwenyekiti wa UDP Mh.John Momose Cheyo aliyelazwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.Katikati ya Rais na Mama Salma ni Mjukuu wa Mheshimiwa Cheyo anayejulikana kama Gabriel Cheyo. (Picha Freddy Maro) 

PLOT FOR SALE

$
0
0
Eneo linauzwa lipo jirani na hostel za chuo kikuu cha dar es salaam maarufu kama mabibo hostel.
Upana ni mita 37 na urefu n7 mita31
WASILIANA NASI KWA NAMBA
0718910734

BREAKING NEWZZ!!! MFANYABIASHARA MKUBWA WA MADINI NA MMILIKI WA SG HOTEL JIJINI ARUSHA AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WASIOJULIKANA.

$
0
0

Pichani juu ni Askari wakikagua mwili wa Marehemu Erasto Msuya,mara baada kupigwa rasasi kwa majibizano na wanaodaiwa kuwa ni Majambazi.

==========  =======   ========
Habari zilizotufikia hivi punde Kutoka chumba chetu cha habari,zinaeleza kuwa mmoja wa Wafanyabiashara wakubwa wa Madini jijini Arusha,aliyejulikana kwa jina la Erasto Msuya na pia ni mmiliki wa SG HOTEL mkoani humo,amepigwa risasi zaidi ya sita na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi na kufa papo hapo,habari zinaeleza na kubainisha zaidi kuwa Marehemu alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao hawakujulikana mara moja) ili wakafanye biashara. 

Habari zaidi tuvute subra kidoogo,tutazidi kufahamishana kadiri ya taarifa zitakapokuwa zikiingia.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen.

Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania wafunguka leo jijini dar.

$
0
0
 Msemaji wa Wakala wa Huduma za Ajira Bw. Peter Ugata (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jitihada zinazofanywa na wakala hao katika kuhakikisha wanakabiliana na changamoto za ajira nchini, katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, KUSHOTO ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.

Mratibu wa Huduma za Ajira kutoka Wakala wa Huduma za Ajira Bw.Joseph Haule akijibu swali kutoka kwa waandishi wa habari(hawamo pichani) waliotaka kujua ni mafanikio gani wakala hao wamepata tangu kuzinduliwa rasmi mwaka 2008,katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

                             Picha na Elphace Marwa







1.0         UTANGULIZI

Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania(TaESA) ulianzishwa kwa Sheria Na. 30 ya mwaka 1997 (kamailiyorekebishwa mwaka 2009) na kuzinduliwa rasmi tarehe 16 June, 2008 kufuatia Tamko la Serilkali Na.189 la mwaka 2008. TaESA ilianza rasmi utekelezaji wa shughuli zake tarehe 1 Julai, 2008 ikichukua nafasi ya kilichokuwa Kituo cha Ajira nchini (Labour Exchange Centre).


Madhumuni ya kuanzishwa kwa Wakala huu ni katika juhudi za Serikali kuona kuwa utoaji wa Huduma za Ajira kwa umma unakuwa bora zaidi, wenye tija na wenye kuwafikia wananchi wengi zaidi.


Wakala  hutoa huduma zake kwa umma kupitia ofisi zake za kanda zilizopo katika mikoa ya Dar es Salaam (Kanda ya Mashariki na Pwani), Mwanza (Kanda ya Ziwa), Dodoma(Kanda ya Kati) na Arusha (Kanda ya Kaskazini).


Dhima

Kutoa huduma bora za ajira katika sekta ya utumishi wa umma na binafsi kupitia uunganishwaji watafutakazi, taarifa za soko la ajira kwa kuzingatia viwango vinavyokubalika Afrika na kwingineko”.


Dira

“Kuwa Wakala bora, imara na endelevu katika utoaji huduma za ajira katika sekta ya utumishi wa umma na binafsi”.




2.0              SHUGHULI ZA WAKALA

-          Kuunganisha watafutakazi na waajiri wenye fursa za ajira ndani na nje ya nchi.

-          Kuratibu utoaji mafunzo ya ujuzi wa kazi na ushauri wa ajira.

-          Kuandaa mipango ya utoaji huduma za ajira kwa waajiri, watafutakazi na wadau wengine.

-          Kukusanya, kuchambua na kusambaza taarifa za soko la ajira.

-          Kuainisha na kuzitambua Wakala binafsi zinazotoa huduma za ajira

-          Kuratibu utoaji mafunzo yenye kulenga kuwapatia ujuzi wa kazi wanafunzi wanaosoma katika shule za sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu.



2.1          UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA WAKALA

Katika kuhakikisha kuwa Wakala unatekeleza Sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008; Sheria ya Kukuza Ajira Na. 9 ya mwaka 1999 na katika hatua ya kukidhi matakwa ya Azimio Na. 88 la mwaka 1948 la Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambalo Tanzania imeliridhia, Wakala umeendelea kutekeleza shughuli zake kwa njia zifuatazo:-


2.1.1       Kuwasajili na kuwafanyia usaili wa awali watafutakazi

2.1.2       Kutembelea waajiri ili kubaini fursa za ajira zitakazojazwa na watafutakazi waliosajiliwa na wakala

2.1.3       Kutembelea shule/vyuo ili kuwajengea uwezo wanafunzi ili kubaini hali halisi ya soko la ajira na mahitaji yake.

2.1.4       Kuendesha vipindi vya kuwajengea uwezo watafutakazi ili waweze kumudu ushindani na changamoto za Soko la Ajira.

2.1.5       Kufanya mikutano na wadau ili kupata maoni/mapendekezo yatakayofanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wakala.

2.1.6       Kushiriki katika maonesho ya kitaifa na kimataifa kwa lengo la kujitangaza na kufikisha huduma karibu zaidi na wananchi.

2.1.7       Kujitangaza kupitia vyombo vya habari vikiwemo radio, televisheni na magazeti.

2.1.8       Kwa kutumia Tovuti ya Wakala katika kutoa taarifa na kupata maoni ya wadau  na umma kwa ujumla.

2.1.9       Kwa kutumia ofisi zake za Kanda.




3.0         MAFANIKIO YA WAKALA

Tangu kuanzishwa kwake hadi Juni, 2013 Wakala umefanikiwa    katika maeneo yafuatayo:-


3.1         Kuanzisha  Ofisi za Kanda katika Mikoa ya Dare es Salaam, 

Dodoma, Mwanza na Arusha ili kuzifikisha huduma zake karibu na wananchi.

3.2         Wakala umewahudumia jumla ya wateja 13,188 kati yao

Watafutakazi  12,298, waajiri   830 na wakala binafsi 60

3.3      Wakala umeweza kusajili fursa za kazi 2,851kwa kutembelea   Waajiri 830 katika mikoa ya Shinyanga, Kagera,Mara, Mwanza, Singida, Tabora, Iringa, Morogoro, Lindi,Arusha, Kilimanjaro na  Mtwara

3.4             Wakala umeendesha vipindi kwa watafutakazi 1,426 kwa lengo la kuwajengea

uwezo watafutakazi ili waweze kuhimili ushindani na

changamoto za soko la ajira.

3.5             Watafuta kazi 8,294 wamepewa ushauri juu ya uchaguzi wa

fani, mafunzo ya kazi zinazostahili kulingana na sifa zao ili kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kuajirika.

3.6             Wakala umeainisha Wakala Binafsi 60 zinazotoa huduma za

ajira hapa nchini.

3.7             Kupitia kitengo chake cha kuunganisha watafutakazi na

waajiri nje ya nchi, Wakala umeunganisha watafutakazi 1,959katika nchi za UAE, Oman, India, Denmark na Saudi Arabia

3.8             Wakala uko katika hatua za awali za kuwa na mfumo wa

kiteknolojia utakawezesha  kukusanya na kusambaza taarifa za soko la ajira.

3.9             Wakala umeanzisha tovuti yake www.taesa.go.tzambayo

imetembelewa na wadau 440,230 ambao wametoa maoni na mapendekezo mbalimbali juu ya huduma zitolewazo na TaESA.

3.10        Wakala umeweka utaratibu madhubuti wa kuratibu na

kusimamia uunganishaji wa Watanzania kwenye soko la ajira nje ya nchi ili Watanzania waweze kupata kazi za staha na kuepukana na biashara haramu ya usafirishaji watu “human trafficking”.


4.0         CHANGAMOTO


4.1             Kutokuwa na rasilimali za kutosha kuwezesha kufikia malengo ya  Wakala.

4.2         Kutokuwa na fursa za kazi za kutosha ukilinganisha na idadi

ya wahitimu/watafutakazi waliopo katika soko la ajira.

4.3             Watafuta kazi wengi kuwa na matarajio makubwa kuliko hali halisi ya soko la ajira.

4.4             Baadhi ya waajiri na watafutakazi kutotumia huduma za Wakala






5.0         MIKAKATI WA WAKALA KATIKA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIZO


Pamoja na changamoto zilizopo wakala umepanga kufanya

yafuatayo:-


5.1     Kuendelea kuwaunganisha watafutakazi na waajiri ndani  na      

          nje  ya nchi na kufanya utafiti katika nyanja za upatikanaji

          wa fursa  za ajira.

5.2             Kukusanya, kuchambua na kusambaza Taarifa za Soko la Ajira.

5.3             Kuendeleza rasilimali watu ili kuongeza tija na ufanisi.

5.4             Kuendelea kuainisha Wakala binafsi zinazotoa huduma za ajira nchini.



6.0         HITIMISHO


Lengo la kuandaa taarifa hii ni kuwajulisha Watanzania na umma kwa ujumla kuhusu huduma zitolewazo na Wakala kwa kuainisha sheria iliyoanzisha, shughuli za Wakala, utekelezaji wa shughuli za Wakala, mafanikio, changamoto na mikakati ya kukukabiliana nazo. Aidha, Wakala unachukua fursa hii kutoa shukrani za dhati kwa kutupatia fursa hii ya kuuelezea Wakala kwenu na Watanzania kwa ujumla.

RAIS KIKWETE AKITANA NA WABUNGE WA TANZANIA KATIKA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na baadhi ya wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2013. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki,  Dkt. Abdala Juma Abdulla Saadalla

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2013. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki,  Dkt. Abdala Juma Abdulla Saadalla. Picha na IKULU.

Balozi wa Vijana wa Tanzania (East African Coommunity ) ndani ya Newyork.

$
0
0
???????????????????????????????
Mwakilishi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa kwa vijana Bw. Ahmed Alhendawi alipokutana na Raymond Maro balozi wa Tanzania kwa upande wa vijana kwenye jumuiya ya afrika mashariki. ???????????????????????????????
Raymond Maro akiwa na mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa mataifa Flora Nducha. DSC04584
Raymond Maro ndani ya jiji la Newyork akijionea jiji lisilolala.

MKURUGENZI WA MAELEZO-MWAMBENE NA MKURUGENZI WA UTAMADUNI-MWASOKO WATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA HABARI NANE NANE NZUGUNI DODOMA

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Assah Mwambene (kulia) akizungumza jambo wakati yeye na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya  Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko walipotembelea banda la Magazeti ya Serikali  Tanzania Standard Newspapers (TSN) Wachapishaji wa magazeti ya Daily News, HABARILEO, Sunday News, HABARILEO  Jumapili  na Spotileo, jana Nzuguni Dodoma. Kushoto ni Afisa Masoko na Mauzo wa TSN, Chikira Mgheni na Afisa Masoko, Francis Kihinga.

Viongozi hao kutoka Wizarani walitembelea Taisisi zote zilizo chini Ya Wizara hiyo ikiwa ni Idara ya MAELEZO, TSN, TBC, BASATA, BODI YA FILAMU, TASUBA, IDARA YA MICHEZO NA ILE YA VIJANA.


 Kihinga akizungumza jambo na Wakurugenzi hao.
 Chikira akimkabidhi zawadi Mwasoko.
 Mwambene akipokea zawadi kutoka kwa Chikira wa TSN
 Wakurugenzi hao walifika banda la MAELEZO na kumkuta Lidya Chuzri na kuwapa maelezo ya banda.
 Wakiwa Bodi ya Filamu na Kulia ni Afisa Ukaguzi wa Filamu, Tabu Magembe
 Wananchi wakiwa banda la TASUBA

 Wakurugenzi wakiwa Banda la TASUBA
 Wakiwa Idara ya Michezo
 Wakurugenzi wakiwa Banda la Idara ya Vijana


MKURUGENZI WA MAELEZO-MWAMBENE NA MKURUGENZI WA UTAMADUNI-MWASOKO WATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA HABARI NANE NANE NZUGUNI DODOMA

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Assah Mwambene (kulia) akizungumza jambo wakati yeye na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya  Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko walipotembelea banda la Magazeti ya Serikali  Tanzania Standard Newspapers (TSN) Wachapishaji wa magazeti ya Daily News, HABARILEO, Sunday News, HABARILEO  Jumapili  na Spotileo, jana Nzuguni Dodoma. Kushoto ni Afisa Masoko na Mauzo wa TSN, Chikira Mgheni na Afisa Masoko, Francis Kihinga.

Viongozi hao kutoka Wizarani walitembelea Taisisi zote zilizo chini Ya Wizara hiyo ikiwa ni Idara ya MAELEZO, TSN, TBC, BASATA, BODI YA FILAMU, TASUBA, IDARA YA MICHEZO NA ILE YA VIJANA.


 Kihinga akizungumza jambo na Wakurugenzi hao.
 Chikira akimkabidhi zawadi Mwasoko.
 Mwambene akipokea zawadi kutoka kwa Chikira wa TSN
 Wakurugenzi hao walifika banda la MAELEZO na kumkuta Lidya Chuzri na kuwapa maelezo ya banda.
 Wakiwa Bodi ya Filamu na Kulia ni Afisa Ukaguzi wa Filamu, Tabu Magembe
 Wananchi wakiwa banda la TASUBA

 Wakurugenzi wakiwa Banda la TASUBA
 Wakiwa Idara ya Michezo
 Wakurugenzi wakiwa Banda la Idara ya Vijana

KONYAGI WAIOMBA SERIKALI KUONDOA KODI KATIKA ZAO LA ZABIBU.

$
0
0
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distileries Limited (TDL), David Mgwassa, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kuhusu kuiomba serikali kuondoa kodi inayotoza kiwanda hicho kutokana na ununuzi wa zao la zabibu kwa kuwa bado hakijajiimarisha kiuzalishaji. Kushoto ni Mwakilishi wa waandishi wa habari wa kiwanda hicho, Spear Patrick.
                                                              
========  =======   ==========
UONGOZI wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distileries Limited (TDL), umeiomba serikali kuondoa kodi inayotoza kiwanda hicho kutokana na ununuzi wa zao la zabibu kwa kuwa bado hakijajiimarisha kiuzarishaji.

Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam ambapo alielezea wasiwasi wa zao kuja kudorora iwapo kodi hiyo itaendelea kutozwa.

Alisema kutokana na uendeshaji wa kampuni kwa miaka sita tangu ifufue mashamba ya zabibu miaka saba iliyopita kwa kuagiza mbegu kutoka Afrika Kusini ni kipindi kifupi kuanza kukatwa kodi.

"Kipindi cha miaka sita kuanza kukatwa kodi ni mapema mno kwani bado hatujasimama sawasawa tunaomba serikali kuangalia kwa makini jambo hilo ili kunusuru kilimo cha zao hilo na kuwakomboa wakulima" alisema Mgwassa.

Alisema TDL kwa mwaka huu imenunua lita milioni 1.720 za zabibu na kuwa lita milioni 1.1 ni kwa ajili ya kinywaji cha Valuer na 0.7 zilienda kwenye bidhaa nyingine.

Mgwassa alisema kwa mwaka jana kampuni hiyo imetumia sh.bilioni 1.8 kwa ajili ya kununua zao hilo ambapo mwaka huu watatumia bilioni 2.3 na kuwa hali ya kilimo cha  zao hilo ni nzuri pamoja na soko lake tofauti ni inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Aliongeza kuwa iwapo serikali itaendelea kotoza kodi hiyo upo uwezekano wa vinywaji vinavyozarishwa na kiwanda hicho bei yake kuwa juu kutokana na bei ya soko kulingana na ile ya vinywaji kutoka nje ya nchi.

MATOKEO YA UCHAGUZI MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO

$
0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akizungumza na madiwani wa CCM wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wiki iliyopita.

WAPINZANI WACHEZEA KICHAPO KIBONDO

Katika hali inayothibitisha ule usemi wa mwanamuziki Chamilion wa Uganda kuwa "fitina yako bahati yangu" wapinzani wamechezea kichapo cha mwaka kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kibondo baada ya CCM kushinda kwenye nafasi zote za kuongoza Halmashauri hiyo, ushindi uliowaacha midomi wazi wapinzani waliokuwa wakisubiri kufaidi kwenye ugomvi wa madiwani wa CCM wilayani hapo.


Diwani wa CCM Ndugu  Emily Msanya kuibuka Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya kupata kura 14 kati ya 17 zilizopigwa na Makamu Mwenyekiti ni Apronary Mazinda ambaye pia alishinda kwa kura 14 kati ya 17.



Kuchaguliwa kwa madiwani hao na ushindi huo wa CCM kwenye ngome ya upinzani ambapo Mbunge wa jimbo hilo ni Ndg. Mkosamali wa NCCR-Mageuzi ni uthibitisho dhahiri kuwa CCM ina mkakati mkubwa wa kuzidhibiti ngome zote za upinzani nchini kuelekea uchaguzi wa 2014 na 2015.


Kabla ya uchaguzi huo palikuwa na mgogoro mkubwa kati ya madiwani wa CCM, mgogoro ambao ulitatuliwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye kufuatia ziara yake ya kimyakimya ya siku moja wilayani Kibondo ambapo alikutana na madiwani hao wa CCM kwa zaidi ya masaa manne.


Matokeo haya ni kinyume kabisa na kile kilichoandikwa na Gazeti la Tanzania Daima la Agosti 7,2013 kuwa ' WIKI NGUMU KWA CCM" wakieleza kuwa CCM wangepoteza uchaguzi huu. Fitina hiyo ya TanzaniaDaima imegeuka kuwa bahati kwa CCM maana imetembeza kichapo cha haja kwenye uchaguzi huo.



Nape akiongea juu ya ushindi huo akinukuliwa na redio moja ya Mjini Mwanza alisema "ushindi huo ni mawingu mvua zenyewe zinakuja. Unajua hawa jamaa wanawekeza kwenye migogoro ndani ya CCM ili ikitokea hatukuelewana mahali basi wanazamia, hapa nimewazidi akili" alikaririwa Nape.

DK MAHANGA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM WAKAGUA UJENZI WA MIUNDOMBINU SEGEREA

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Segerea, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akiwaonesha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala (Jimbo la Segerea), kituo kipya cha Polisi cha Tabata, Dar es Salaam, walipokuwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu jimboni humo.
 Dk. Makongoro Mahanga na Diwani wa Kata ya Tabata, Mtumwa Mohamed pamoja na wajumbe wakikagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne akatika Shule ya Msingi Tabata
 Dk. Mahanga akitoa maagizo kwa watendaji wa Kata ya Kimanga, kuhakikisha wanabomoa haraka msingi wa bendera ya CHADEMA, uliojengwa kwenye eneo la Stendi ya Dcaladala ya Kimanga inayotarajiwa kufanyiwa matengenezo wiki hii.
 Dk. Mahanga akizungumza wakati wa kukagua ujenzi wa daraja la maji ya chumvi.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Ilala, wakikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kinyerezi- Segerea.
 Mhandisi wa Manispaa ya Ilala, Muhinda Kassim akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa miradi
 Mkazi wa Kinyerezi akitoa ushauri kwa wahandisi wa Tanroads Dcar es Salaam kuhakikisha wanatunza vizuri barabara ikiwemo kuwela alama.
 Mmoja wa wahandisi wa Tanroads akielezea kuhusu maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kinyerezi-Segerea
 Wajumbe wakiwa site ya daraja hilo
 Dk. Mahanga akizungumza na wahandisi wa Tanroad Mkoa wa Dar es Salaam
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala, wakikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tabata-Liwiti.
 Mhandisi Mwandamizi wa Tanroads DSM, Eliakim Tenga akielezea kuhusu maendeleo ya ya ujenzi wa barabara ya Tabata-Liwiti.
Msafara wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala, ukiwa kwenye magari ukikagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Liwiti-Baracuda.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

Shusho, Kilahiro kuhudumu Washington DC wikiendi hii

$
0
0
Watumishi wa Mungu Christina Shusho na Upendo Kilahiro, mwishoni mwa wiki hii watahudumu katika jiji la Washington DC na Vitongoji vyake (DMV).
Shusho na Kilahiro ambao ni miongoni mwa waimbaji mahiri wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, wameshawasili Washington DC tayari kwa huduma hiyo ambayo ni sehemu siku tatu za Maadhimisho ya miaka mitano ya kanisa la The Way Of The Cross Gospel Ministries. Maadhimisho haya yataanza siku ya Ijumaa na kumalizika Jumapili
Maadhimisho haya yatafanyika

The Way of the Cross Gospel Ministries
(at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa watumishi hawa kuhudumu pamoja kanisani hapo katika kipindi cha miaka miwili, ambapo mwaka 2011waliungana na Upendo Nkone kuhudumu katika Mkutano mkubwa wa Injili ulilofanyika kanisani hapo.
Watazame na kuwasikiliza wanavyoelezea siku hizo
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images