Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

BOT YAKANUSHA TAARIFA KUHUSU KUBADILISHA FEDHA

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kupuuza taarifa zinazozunguka katika mitandao ya kijamii kwamba kutakuwa na ‘mabadilisho ya fedha zote za zamani kuanzia tarehe 04/09/2017 hadi tarehe 01/12/2017’.

Taarifa hizo ni za uongo na hazijatolewa na Benki Kuu ya Tanzania. Wananchi mnaombwa kuendelea na taratibu zenu za kawaida za kufanya miamala yenu mbalimbali kwa kutumia fedha zetu kama kawaida.

Aidha, Benki Kuu ya Tanzania inawaasa watumiaji wa mitandao ya kijamii kutumia vizuri nyenzo hiyo ya kupashana habari na kuacha kuzusha uongo ambao unaleta usumbufu usio wa lazima kwa wananchi.

Imetolewa na:
Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
Barua pepe: info@bot.go.tz

Simu: +255 22 2233167

VIJUSO VYA MAGAZETI YA IJUMAA LEO SEPT 1,2017

CAG ATOA SEMINA KWA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI

$
0
0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad akiwasilisha mada kwa Kamati ya Bunge ya Bajeti katika semina iliyohusu Ripoti za CAG kuhusu kaguzi za taarifa za fedha kwa mwaka ulioshia tarehe 30 Juni, 2016.

MBUNGE COSATO CHUMI AKABIDHI BESENI 100 KWA KINAMAMA WAJAWAZITO NA WALIOJIFUNGUA KATIKA HOSPITAL YA MJI WA MAFINGA

$
0
0
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwapa akina mama waliojifungua mabeseni kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma ya afya kwa kinamama wa jimbo la mufindi na wananchi wote wanotumie hospitali ya mafinga mjini lakini mabeseni hayo yametolewa kwa msaada wa ubalozi wa kuwait hapa nchini Tanzania.
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipeana mkono na mmoja wa kinamama alifanikiwa kupewa msaada wa beseni





Na Fredy Mgunda,Mafinga.


Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mabeseni mia moja kwa akina mama waliopata watoto kwenye wodi ya wazazi ya hospitali ya Mafinga.

Mabeseni hayo yalikabidhiwa kwa kina mama waliojifungua na ambao wanatarajia kujifungua hivi karibuni hospitalini hapo.Msaada huo wenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni nne, umetolewa na Ubalozi wa Kuwait hapa nchini mapema wiki iliyopita.

`ndugu zangu zawadi hii tumepewa na Balozi wa Kuwait hapa Nchini kwa ajili yenu kina mama kama sehemu ya mwanzo wa ushirikiano kati ya Mafinga na Ubalozi wa Kuwait' alisema Chumi.

Akifafanua, alisema kuwa msaada huo ni uthibitisho wa upendo alionao Balozi wa Kuwait hapa nchini kwa watu wa Mafinga.`Mheshimiwa Balozi Jasem Al- Najem hajawai kufika Mafinga lakini kwa upendo mkubwa akasema, naomba hiki kidogo uwafikushie kina mama wa Mafinga' alisema Chumi na kuongeza kuwa ushirikiano kwenye jambo dogo ndio mwanzo wa ushirikiano wa mambo mengine makubwa.

Akishukuru wakati wa kukabidhi msaada huo wa mabeseni, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mhe Charles Makoga alipongeza ushirikiano wa Mbunge na wadau mbali mbali na kuwasihi watendaji kuendelea kufanya kazi kwa kujituma.`sisi halmashauri tuko bega kwa bega na mbunge, na ninyi watumishi kwa pamoja tuendelee kushirikiana na kufanya kazi kwa kujituma' alisisitiza Makoga.

Wakati akikabidhi msaada huo wiki moja iliyopita kwenye ofisi za Ubalozi wa Kuwait Masaki Jijini Dar es Salaam, Balozi Jasem Al-Najem alisema kuwa lengo la Ubalozi ni kugawa jumla ya mabeseni elfu moja kwa ajili ya mama na mtoto.`katika awamu ya kwanza ya kutoa msaada huu wa mabeseni haya ya mama mtoto kits, tumeona tuwakumbuke na kina mama wa Mafinga japo kwa mabeseni mia moja'

Ubalozi wa Kuwait umekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada ya kijamii na kibinadamu ambapo mpaka sasa wameshachimba visima arobaini kwenye shule mbali mbali za Mkoa wa Dar na Pwani.

Aidha Ubalozi umeshatoa msaada wa vifaa vya theatre katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na pia kuendesha zoezi la kuchangia damu miezi sita iliyopita.

Migogoro mingi ya Ardhi ni kutokujituma kwa watu wetu - RC Gambo

$
0
0
"Migogoro mingi ya Ardhi ni kutokujituma kwa watu wetu" RC Gambo
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati anahitimisha mkutano wake na wananchi wa wilaya ya Karatu wenye kero mbalimbali za Ardhi,Nyumba na Makazi.
"Toka nianze mikutano mikutano hii na wakazi wa Jiji la Arusha na leo nipo hapa Karatu migogoro mingi si mikubwa kama inavyoonekana bali inachangiwa na uzembe wa watu wetu katika mabaraza ya Ardhi na mahakama kutokutimiza wajibu wao ipasavyo" alisema Gambo.
Katika mikutano hiyo maalum ambayo mkuu huyo wa mkoa ameshaifanya katika jiji la Arusha na Karatu amekutana na migogoro mingi ambayo kiuhalisia imeshasuluhishwa katika hatua mbalimbali za kimaamuzi lakini wananchi hao hawajapewa mrejesho.

"Tatizo letu sisi watendaji ni kutokuwaandikia watu hawa wa nini tumekifanya katika maamuzi yetu na kutokuweka kumbukumbu sahihi, kama mmeshughulikia tatizo la mtu mpeni mrejesho kwa maandishi na kama ataona hajaridhika mshaurini hatua zaidi za kufuata na jambo hilo liwekwe kwenye kumbukumbu zetu ili akija wakati mwingine tusipate shida kwa kudhani ni jambo jipya" alisisitiza Mhe Gambo.

Vilevile amemuagiza Kamishna wa Ardhi kutuma timu maalum itakayoshughulikia kero hizo ndani ya muda mfupi na kuyafanyia ukaguzi mabaraza yote ya Ardhi wilaya za Arusha mjini na Kararu.

"Kamishna nitakutana mara baada ya ziara ya mwenge kupita mkoani mwetu ulete timu maalum itakayopiga kambi hapa kumaliza kero hizi kwani hapa kuna wengine wala hawana migogoro ya ardhi bali wamevamiwa kwenye maeneo yao watu kama hawa polisi ndio sehemu husika na sio kwenye mabaraza ya ardhi, vilevile ukayafanyie ukaguzi mabaraza ya Ardhi ya Arusha mjini na Karatu kwani nayo sioni kama wanafanya kazi zao sahihi sana" aliagiza mkuu huyo wa mkoa.

Katika mikutano hiyo maalum aliyoianza tarehe 29/08/2017 kwa Jiji la Arusha na tarehe 30/08/2017 kwa wilaya ya Karatu Mkuu huyo wa mkoa ameambatana na wataalam wa Ardhi toka ofisi ya Kamishna wa Ardhi,Msajili wa hati Kanda, wataalam wa Ardhi mkoa wa Arusha, mwanasheria toka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali na wataalam mbalimbali toka halmashauri husika.

Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa kua na migogoro mingi ya Ardhi na ya muda mrefu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo(katikati) akiendesha mkutano wa kuwasikiliza wanachi wa Jiji la Arusha kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fabian Daqqaro na kulia ni Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bwana. Chitukuro .
Baadhi ya wananchi wa Jiji la Arusha wakisubiri kumuona mkuu wa mkoa wa Arusha na kumweleza kero zao
Wananchi wa wilaya ya Karatu wakiwa katika makundi kusubiri kuonana na RC Gambo na kutoa malamimiko yao.

KUZIONA TANZANIA VS BOTSWANA KESHO NI BUKU TANO TU, MSUVA ATUA STARS

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza viingilio vya mchezo kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Botswana utakaofanyika Jumamosi Septemba 2, mwaka huu.

Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) viingilio vitakuwa Sh 10,000 kwa Jukwaa Kuu na Sh 5,000 kwa mzunguko.

Wakati huo huo, Kiungo Taifa Stars, Simon Msuva tayari amejiunga na timu hiyo akitokea Klabu ya Difaa El Jadidah ya Morocco baada ya Shirikisho la Soka Morocco na timu yake kumfanyia mpango wa visa ya muda mrefu iliyomwezesha kusafiri.

Mchezaji ambaye imeshindikana kuja ni Orgenes Mollel wa FC Famalicao ya Ureno. Sababu ni taratibu za ruhusa za kimataifa zinafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria za nchi ya Ureno ambako anacheza soka la kulipwa.

Nyota wengine walikwisha kuripoti ni pamoja na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Elias Maguli (Dhofar FC/Oman), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya) wakati Farid Mussa wa CD Tenerif ya Hispania anatarajiwa kutua leo.

Wengine ambao wako kambini Hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam ni makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).

Pia wamo Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).

Viungo ni Himid Mao – Nahodha Msaidizi (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Shiza Kichuya (Simba SC), wakati Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans), Kelvin Sabato (Azam FC) na Emmanuel Martin (Young Africans).

Katika hatua nyingine, Botswana inatarajiwa kuingia usiku wa saa 3.00 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) na watafikia Hoteli ya Urban Rose iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Botswana inayonolewa na David Bright inakuja na wachezaji 18 wakiwamo makipa Mampule masule, Noah Maposa na Antony Gouws.

Walinzi ni Letsweletse, Mosha Gaolaolwe, Simisane Mathumo, Thabang Mosigi, Lesenya Ramorake, Tapiwa Gadibolae na Bokani Leeton.

Viungo ni Alphonse Modisaotsile, Maano Ditshupo, Katlego Masole, Gift Moyo, Segolame Boy, Lemponye Tshireletso, Thero Setsile, Kabelo Seakanyeng,Jackson, Lemogang maswena.

Washambuliaji ni Tumisang Orebonye, Jarome Ramathakwane, Tebogo Sembowa, Hendric Moyo na Boipelo Oaitse.

KAMISHNA WA MADINI ASHIRIKI ZOEZI LA UHAKIKI WA DHAHABU INAYOSAFIRISHWA NJE

$
0
0

Na Veronica Simba – Geita

Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, ameshuhudia na kushiriki katika zoezi la kuhakiki na kufunga madini ya dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Kamishna Mchwampaka alishiriki zoezi hilo hivi karibuni, akiwa katika ziara ya kazi mkoani Geita kukagua shughuli mbalimbali za sekta ya madini. 

Zoezi la uhakiki na ufungaji wa dhahabu inayosafirishwa, hufanyika katika chumba maalum kijulikanacho kama gold room kilichopo mgodini na hushirikisha maafisa mbalimbali wa Serikali kutoka Jeshi la Polisi, Wizara ya Nishati na Madini na Mamlaka ya Mapato Tanzania pamoja na maafisa wa Mgodi.

Akizungumzia lengo la maafisa wa Serikali kutoka sekta husika kushiriki katika zoezi hilo; Kamishna Mchwampaka alieleza kuwa ni kwa Serikali kujiridhisha na thamani ya dhahabu inayosafirishwa ili kuhakikisha inapata mapato stahiki na kuepusha udanganyifu wowote unaoweza kujitokeza.

“Katika hili, tuko imara na makini. Ni lazima tuhakikishe kuwa Serikali inapata mapato stahiki kulingana na dhahabu inayosafirishwa. Ndiyo maana unaona maafisa wetu kutoka sekta zote muhimu wanashiriki kikamilifu katika zoezi hili.”

Aliwataka watanzania kuondoa hofu na kuiamini Serikali ya Awamu ya Tano inayowaongoza kuwa iko makini na imejipanga kusimamia kikamilifu maslahi ya wananchi.

Kamishna wa Madini yuko katika ziara ya kazi Kanda ya Ziwa kukagua shughuli mbalimbali za sekta husika.


Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mwenye koti), akihakiki uzito wa Mkuo wa Dhahabu, katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kabla ya kufungwa na kusafirishwa nje ya nchi. Wengine pichani ni baadhi ya maafisa wa Serikali na GGM.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mwenye koti-kulia), akishuhudia Mkuo wa Dhahabu wenye uzito wa kilogramu 26, ukiwekwa ndani ya mfuko maalum kabla ya kufungwa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi. Wengine pichani ni baadhi ya maafisa wa Serikali na GGM.
Afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Anuari Fadhili akiweka ‘seal’ maalum ya Serikali kwenye Kasha lenye Mkuo wa Dhahabu baada ya ukaguzi katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi. Wanaoshuhudia ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati) na maafisa wengine wa Serikali na GGM.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati),  akitoa maelekezo kwa maafisa wa Serikali pamoja na wale wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kuhusu zoezi la uhakiki na ufungaji dhahabu inayosafirishwa nje ya nchi.

Kasha lenye Mkuo wa Dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), lililohakikiwa na kufungwa tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. 

Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati) na timu yake, wakiondoka ndani ya eneo la Mtambo/kiwanda cha kuchakata dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), baada ya kushiriki zoezi la uhakiki na ufungaji wa dhahabu inayosafirishwa nje ya nchi. Pamoja nao ni maafisa wa GGM.

Wakili: Sethi kupoteza maisha asipotibiwa haraka

$
0
0
WAKILI wa Utetezi, Joseph Makandege ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha inayomkabili Herbinder Seth kuwa asipotibiwa ipasavyo, puto lililowekwa kwenye tumbo lake linaweza kupasuka na kusababisha kifo.

Makandege alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na kueleza mahakama kuwa mshitakiwa huyo alifanyiwa upasuaji na kuwekwa puto tumboni.

Alidai kuwa  katika mashauri yaliyopita, mahakama ilitoa amri mara mbili, zote zikielekeza mshitakiwa huyo apelekwe Hospitali ya Muhimbili lakini haijatekelezwa.

Aliomba mahakama izingatie ugonjwa wa mshitakiwa na iamuru apelekwe moja kwa moja Muhimbili kwani  ndio hospitali ya juu  ya serikali nchini ambayo inategemea kuwa na wataalamu na vifaa stahiki vya ugonjwa unaomkabili.

"Upande wa jamhuri unatambua haya lakini kwa ridhaa yao wao wamempeleka mshitakiwa Amana hospitali. Swali ambalo mahakama isaidie kujibu pamoja na jamhuri, ni  je, kumpeleka mshitakiwa wa kwanza hospitali ya Amana,  magereza na jamhuri wameshindwa kutii amri ya mahakama?," alihoji Makandege.

“Mahakama haikumungunya maneno katika kutoa amri yake, ambapo ilitamka kwenye amri hiyo kwamba mshitakiwa huyo  apelekwe katika hosipitali ya taifa ya Muhimbili, wao kumpeleka Amana wametekeleza amri gani?” Makandege aliendelea kueleza.

Alidai  amri ya mahakama  haijatekelezwa hivyo upande wa mashitaka umekaidi amri hiyo.

"Mahakama ndio mahala amri zote zitaheshimiwa kwa pande zote mbili kwa kuwa nchi inafuata demokrasia na utawala wa sheria," alidai Makandege.

Makandege alidai kuwa kilichofanyika ni kinyume na amri ya mahakama na kinyume na sheria za magereza kifungu cha 53 (1) ambacho kinatoa fursa kwa mtu yoyote aliyeko gerezani kama anaumwa kufikishwa hospital ili apate matibabu.

Alidai kuwa ni rai yake kuwa mahakama haina uwezo wa kusikiliza shauri husika lakini inamamlaka ya kuhakikisha tararibu za mahakama zinafuatwa na kuhakikisha haki inatendeka.

Wakili wa Serikali, Vitalis Peter  alidai  hakuna amri yoyote ya mahakama ambayo jamhuri haijaitekeleza.

Alidai kuwa ni kweli kifungu cha 53 (1) cha sheria ya magereza kinaipa mamlaka magereza kumpeleka mtuhumiwa hospitali kama anaumwa na kwamba magereza wana wataalamu wao na hospitali yao na ndio wanakaa na mtuhumiwa na wanamuangalia kwa mara ya kwanza, wakishindwa kumtibu ndio wanampa rufaa.

Wakili Peter alidai kuwa mshitakiwa alihudumiwa na wataalamu wa magereza na kumpeleka hospitali ya juu yao  ambayo ni Amana, baada ya Amana alipatiwa matibabu na daktari bingwa kutoka muhimbili Dk Wilson Mgamba ambaye alimuona mtuhumiwa na kujiridhisha na afya yake.

"Wakili awasiliane na mteja wake kwanza kwasababu kashapatiwa matibabu na magereza hawachaguliwi kumpeleka mtu hospitali ambao ndio wanaweza kujua ugonjwa alionao na wapi pa kumpeleka," alidai Vitalis.

Baada ya kuwasilisha hayo, Wakili Makagande alidai kuwa haiwezekani daktari kuchukua vifaa vyote kuvipeleka katika magereza ya Segerea na kwamba mteja wake hajapatiwa matibabu hayo na yuko mahakamani anaweza kuongea mwenyewe.

Wakili Makandege alieleza mahakama kwamba kauli ya wakili wa serikali kudai kwamba Magereza hawapangiwi sehemu ya kumpeleka mtuhumiwa au mfungwa ambaye yupo mikononi mwao kwa matibabu, ni dharau kwa amri na heshima ya mahakama.

Pia aliongeza kuwa taratibu za ndani zilizowekwa na Magereza haiwezi ikawa juu ya amri za mahakama na sheria za nchi. “Uwepo kwa taratibu za magereza haiwezi ikaifanya amri za mahakama kusiginwa. Taratibu za ndani za magereza haiwezi ikawa juu ya amri za mahakama. Kauli hiyo ya wakili msomi mwandamizi wa serikali inaonyesha ni jinsi gani magereza wameidharau mahakama yako tukufu,” aliongeza Makandege.      

Hata hivyo, Hakimu Shaidi alisisitiza mshitakiwa huyo apelekwe katika hospitali ya Muhimbili kama ilivyotoa maagizo awali.

Kwa upande wake, James Rugemarila  aliiomba mahakama, magereza waweze kumruhusu kuonana na mawakili wake kwasababu anambambo mengi ya kuongea nao.

Alidai kuwa anamawakili 10 na kunawakati anahitaji kuongea nao lakini anauwezo wa kuwaona wawili tu hivyo anaomba aweze kupatiwa dakika 30 kuzungumza nao kabla hajarudishwa mahabusu.

Seth  na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kighushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA LAADHIMISHA MIAKA 53 TOKA KUANZISHWA KWAKE

$
0
0

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akizungumzia maadhimisho ya miaka 53 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo la Wananchi katika Makao makuu ya Jeshi hilo Ngome jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha na Jenerali wa kwanza Mzalendo kuliongoza Jeshi hilo Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya wa kwanza kushoto pamoja na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange mara baada ya kuzungumza kuhusu kuhusu miaka 53 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo la Wananchi katika Makao makuu ya Jeshi hilo Ngome jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha na Jenerali wa kwanza Mzalendo kuliongoza Jeshi hilo Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya wanne kutoka kushoto Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wanne kutoka kulia Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Mwakibolwa watatu kutoka kushoto mstari wa mbele pamoja na Wakuu wa Kamandi na machifu wa Makao makuu ya Jeshi hilo.

PICHA NA MPIGA PICHA WETU

MBUNGE MAJI MAREFU AWA GUMZO ASHIRIKI KUFYATUA MATOFALI BAADA YA KUFUNGUA KIWANDA

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akishiriki kufyetua matofali 10000 ambayo baadae yatagawiwa kwa kata 29 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na zahanati ikiwemo nyumba za wafanyakazi wa serikali  baada ya kupata saruji mifuko 200 kutoka kwa Mohamed MO na Hoza Farm naye amempa mifuko mingine 100

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akishiriki kufyetua matofali 10000 ambayo baadae yatagawiwa kwa kata 29 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na zahanati ikiwemo nyumba za wafanyakazi wa serikali

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akiwa kwenye harakati za kufyetua matofali hayo
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akibeba tofali mara baada ya kulifyetua
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akiendelea na kazi
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu mwenye shati za njano akishiriki kufyatua matofali na viongozi wa CCM Korogwe Vijijini
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akiwa amebeba tofali mara baada ya kulifyetuaa(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

DKT SHEIN AONGOZA BARAZA LA EID FUMBA-UNGUJA,MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman alipowasili katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi katika sherehe za Baraza la Eid el Hajj lililofanyika leo.


Wananchi na Viongozi wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi katika sherehe za Baraza la Eid el Hajj lililofanyika leo,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.




Baadhi ya Akinamama waliohudhuria katika sherehe za Baraza la Eid el Hajj lililofanyika leo,katika ukumbi wa mkutano wa Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (kushoto) akiwa na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa katika sherehe za Baraza la Eid el Hajj lililofanyika leo katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Viongozi wengine wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika sherehe za Baraza la Eid EL Hajj lililofanyika katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.


Baadhi ya Wake wa Viongozi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika sherehe za Baraza la Eid EL Hajj lililofanyika katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.




Baadhi ya Akinamama waliohudhuria katika sherehe za Baraza la Eid el Hajj  wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akipokea salamu ya heshma kwa kikosi cha pilisi cha FFU mara alipowasili katika sherehe za Baraza la Eid el Hajj lililofanyika leo katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.]01/09/2017.




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akisalimiana na Wananchi na Viongozi mbali mbali baada ya kutoa hutuba yake katika sherehe za Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akisalimiana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Viongozi mbali mbali baada ya kutoa hutuba yake katika sherehe za Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akipungia mkono Viongozi mbali mbali kama ishara ya kuwaaga baada ya kumalizika kwa sherehe za Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.

JAPAN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA AJILI YA KUFANYA USANIFU WA KINA WA BARABARA YA MWENGE HADI MOROCCO, DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kulia), akifurahia jambo katika Mkutano na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (wa pili kushoto) muda mfupi kabla ya hafla ya kusainiwa kwa mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya Usanifu wa kina wa Barabara ya Morocco hadi Mwenge yenye urefu wa kilometa 4.3, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (katikati), Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (kulia) na Mwakilishi Mkuu Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama (kushoto) wakielekea katika hafla ya kusaini mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 1.4, kwa ajili ya Usanifu wa kina wa Barabara ya Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.


alozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (kulia) akimweleza jambo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) kabla ya kusainiwa kwa mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 1.4 zilizotolewa na Japan kwa ajili ya kufanya Usanifu wa kina wa upanuzi wa Barabara ya Morocco hadi Mwenge ili kupunguza msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam.




Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kulia) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (wa pili kushoto), wakisaini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa barabara ya Morocco hadi Mwenge, yenye urefu wa kilometa 4.3, ambapo Japan imetoa msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa barabara hiyo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida akibadilishana hati za makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa barabara ya Morocco hadi Mwenge, yenye urefu wa kilometa 4.3, ambapo Japan imetoa msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa barabara hiyo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkuu mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama (wa pili kushoto) wakisaini Mkataba wa makubaliano ya msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya Usanifu wa kina wa upanuzi wa Barabara ya Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Mwakilishi Mkuu Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama wakibadilishana hati ya Mkataba wa makubaliano ya msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya Usanifu wa kina wa upanuzi wa Barabara ya Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini humo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Mwakilishi Mkuu mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama wakipeana mkono baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa makubaliano ya msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya Usanifu wa kina wa upanuzi wa Barabara kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kushoto) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (wa tatu kulia) pamoja na maafisa waandamizi kutoka Tanzania na Japan wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla ya kusainiwa kwa Mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya Usanifu wa kina wa upanuzi wa barabara ya Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akibadilishana jambo na Mtendaji Mkuu wa wakala wa Barabara Nchini-Mhandisi Patrick Mfugale, baada ya Tanzania na Japan kutiliana saini makubaliano ya Japan kuipatia Serikali msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa upanuzi wa barabara ya kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.


Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango


………………………….


Dar es Salaam, Septemba 1, 2017: Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), imeipatia Tanzania ruzuku ya Yen milioni 69 sawa na Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa awamu ya pili ya mradi wa upanuzi wa barabara ya New Bagamoyo, kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.

Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Septemba 1, 2017, Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kwa niaba ya Serikali, Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida na Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Satoru Matsuyama.

Tukio hilo limekwenda sambamba na kuingia makubaliano kuhusu muda wa kukamilisha mradi huo pamoja na kupeana taarifa ya namna mradi huo utakavyotekelezwa.

Mradi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.3 utahusisha barabara yenye njia nne pamoja na kuanza kwa awamu ya nne ya barabara itakayotumiwa na mabasi ya mwendo wa haraka (BRT phase IV).

Akizungumza baada ya kutiwa saini wa makubaliano hayo, Dkt. Mpango amesema kuwa barabara hiyo ikikamilika itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya msongamano wa magari kutoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Ameishukuru Japan kwa msaada huo wa awamu ya pili ya ujenzi wa barabara hiyo ambapo katika awamu ya kwanza, Japan ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 99.5. kujenga barabara ya njia nne katika kipande cha kilometa 12.9 kutoka makutano ya barabara ya Tegeta na makutano ya barabara ya Mwenge.

“Si mara ya kwanza kwa Japan kuisaidia Tanzania, wanajenga barabara za juu katika makutano ya Tazara, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Dodoma hadi Babati mkoani Manyara (km 188.15), Tunduru-Mangaka – Mtambaswala (km 202) na barabara ya Iringa hadi Dodoma (259.9)” alisisitiza Dkt. Mpango.

Alisema kuwa upanuzi wa barabara ya Bagamoyo si tu kwamba itapunguza msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam lakini pia utaunganisha Jiji na Bandari ya Bagamoyo ambayo ni muhimu kwa ajili ya usafirishaji wa watu, bidhaa na huduma kutoka Jijini, mikoa ya Pwani na maeneo mengine ya nchi.

Balozi wa Japan, Mhe. Masaharu Yoshida ameeleza kuwa kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa awamu ya pili ya barabara ya Morocco hadi Mwenge kumekuja baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza iliyohusisha ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Tegeta hadi Mwenge ili matokeo ya mradi huo yaweze kuonekana dhahiri.

Ameahidi kuwa baada ya kukamilika kwa usanifu wa kina wa barabara hiyo, Serikali ya Japan kupitia JICA, itasaini mkataba wa kuanza ujenzi huo Mwezi Juni mwakani.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama, amesema Japan imeamua kufadhili mradi huo baada ya utafiti kuonesha kuwa Barabara ya Bagamoyo ndiyo yenye msongamano mkubwa wa magari ambapo inakadiriwa kuwa magari 52,000 yanapita kila siku katika barabara hiyo.

Alielezea matumaini yake kwamba mradi huo utakapo kamilika utasaidi kukuza shughuli za kiuchumi katika Jiji la Dar es Salaam kwa kuwa ndicho kitovu cha biashara kwa maeneo mengine ya ndani ya nchi na kimataifa na kuwaomba wataalamu pamoja na TANROADS kuharakisha usanifu huo wa kina.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini-TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale, amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo hautahusisha ubomoaji wowote wa makazi ya watu wala majengo ya biashara.



Imetolewa na:

Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA MAPANGO YA AMBONI JIJINI TANGA LEO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, kutembelea Mapango ya Amboni Jijini Tanga leo. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Atashasta Ndetiye (wa pili kushoto), Wajumbe wa kamati hiyo, Nape Nnauye (kushoto) na Shaban Shekilindi (kulia). 
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia sehemu ya barabara iliyomeguka ndani ya eneo la Mapango ya Amboni.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakisikiliza maelezo kuhusu mapango hayo kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Jumanne Gekora.
Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Jumanne Gekora (kushoto) akitoa maelezo kwa wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea mapango ya Aboni Jijini Tanga leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akizungumza na wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii muda mfupi kabla ya kuanza ziara ya kuingia ndani ya mapango ya Amboni. Mhandisi Makani alisema mipango ya Serikali ni kutambua vivutio vya aina mbalimbali ikiwemo vya mambo ya kale kama yalivyo mapango ya Amboni kuviboresha na kuvitangza ili vichangie zaidi katika pato ta taifa.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakipata maelezo ya vivutio mbalimbali vilivyopo ndani ya Mapango ya Amboni kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Jumanne Gekora (kushoto).
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiwa ndani ya Mapango ya Amboni. Wajumbe hao waliishauri Serikali kuongeza thamani ya mapango hayo kwa kuboresha miundombinu na vivutio vilivyopo pamoja na kuvitangaza ili yachangie zaidi kwenye mapato ya Serikali.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (wa pili kulia) na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia vivutio mbalimbali vya maumbo asilia ikiwemo ya wanyama na alama za kuabudia vilivyomo ndani ya mapango hayo.
Muoneshaji wa Kujitolea katika Mapango ya Amboni, Othman Mangula (kulia) akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii moja umbo la asili lenye taswira ya Chui ndani ya Mapango ya Amboni ambapo ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii ndani ya mapango hayo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Dkt. Iddi Mfunda (kulia) na Muwakilishi wa Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Canisius Karamaga (wa pili kulia) wakiangalia baadhi ya vivutio katika mapango ya Amboni.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani na baadhi ya wajumbe wa msafara huo wakiwa ndani ya mapango ya Amboni.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani akipenya kwenye njia nyembamba iliyopo ndani ya mapango ya Amboni.
Moja ya umbile la asili lililojitengeneza ndani ya mapango ya Amboni likiwa na taswira ya kwato za ngo'mbe.
Maumbo mbalimbali ya asili yenye taswira ya viumbe ni moja ya kivutio kikubwa ndani ya mapango ya Amboni, Pichani ni umbo la asili lenye taswira ya matiti ambalo lipo ndani ya mapango hayo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) akimsaidia Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bungu Ardhi, Maliasili na Utalii, Neema Mgaya kushuka katika moja ya mteremko uliopo ndani ya mapango hayo.
Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Canisius Karamaga akifurahia jambo ndani maporomoko hayo.
Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mtango Mtahiko ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Alan Kijazi akiwa ndani ya mapango hayo.
Picha na; Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO SEPT 2, 2017

MADIWANI JIJINI TANGA WATAKIWA KUHESHIMU TARATIBU ZA VIKAO

$
0
0
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga (CCM) Alhaji Mustapha Selebosi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nguvumali akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akipitia kabrasha kushoto ni Naibu Meya wa Jiji hilo,Mohamed Haniu ambapo Meya huyo aliwataka madiwani kuheshimu taratibu za vikao. 
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji hilo,Alhaj Mustapha Selebosi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa .
Naibu Meya wa Jiji la Tanga,Mohamed Haniu akizungumza wakati wa kikao hicho kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji hilo(CCM) Alhaj Mustapha Selebosi kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku .
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa kikao hicho. 
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza wakati wa kikao hichi
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku 
Waheshimiwa madiwani kutoka kata mbalimbali wakifuatilia hoja mbalimbali kwenye kikao hicho
Wataalamu kutoka idara mbalimbali katika Halamshauri ya Jiji la Tanga wakifuatilia kwa umakini kikao hicho
Wakuu wa Idara mbalimbali wakifuatilia kwa umakini katika kikao hicho katika ni Mchumi wa Jiji la Tanga,Ramadhani Posi
Waheshimiwaa madiwani wakifuatilia kikao hicho kulia ni diwani wa kata ya Central Khalid Mohamed
Waheshimiwaa madiwani wakifuatilia kikao hicho.
Meneja wa kituo cha TV cha Halmashauri ya Jiji la Tanga (TATV) Mussa Labani akifuatilia mijadala mbalimbali kwenye kikao hicho.
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku katikati akifuatilia taarifa mbalimbali kwenye kikao hicho kulia ni Naibu Meya wa Jiji la Tanga (CUF) Mohamed Haniu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Kassim Mbuguni.
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali wakifuatilia kikao hicho kulia ni Dege Masoli wa Nipashe Tanga,Mbaruku Yusuph wa Tanzania Daima kushoto,Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha 



WANANCHI WAHIMIZWA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizugumza na wananchi wa Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi katika Mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Mchungaji Nicholuos Chimbu mkazi wa Kijiji cha Ngulyati(kulia) wilayani Bariadi akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) alipofanya ziara wilayani humo kwa lengo la kuzikiliza kero za wananchi na kuzitafuatia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga wakiteta jambo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa katika Kata ya Ngulyati aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Minza Maduhu mkazi wa Kijiji cha Ngulyati wilayani Bariadi akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) alipofanya ziara wilayani humo kwa lengo la kuzikiliza kero za wananchi na kuzitafuatia ufumbuzi
Eliasi Hopi mkazi wa Kijiji cha Nyasosi Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi aliwasilisha kero kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) alipofanya ziara wilayani humo kwa lengo la kuzikiliza kero za wananchi na kuzitafuatia ufumbuzi.
Afisa Uhusiano wa TANESCO Mkoa wa Simiyu akitolea ufafanuzi suala la utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini REA Awamu ya III ambalo liliulizwa na wananchi wa Kata ya Ngulyati wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyoifanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kikundi cha Burudani cha Msanii Polepole kutoka Ngulyati kikitoa burudani ka wananchi na viongozi katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) aliyoifanya katika kata ya Ngulyati wilayani Bariadi kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.


Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi Wilayani Bariadi mkoani humo kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF).

Mtaka ametoa wito huo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Amesema azma ya Serikali ni kuwa ifikapo mwaka 2020 Watanzania wote wawe wamejiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) au Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), hivyo akawahamasisha wananchi ambao bado hawajajiunga na CHF kujiunga kwa kuwa gharama yake ni nafuu.

“Watu wa Ngulyati ni wafanyabiashara wazuri, wafanyakazi wazuri, wakulima wazuri ningetamani kuwaona wote hapa mnakuwa na kadi za Mfuko wa Afya ya Jamii ambazo zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000, hii ni sawa na kuku mmoja tu mnapata matibabu watu sita kwa maana ya baba, mama na watoto wa nne” amesema.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha vituo vya kutolea huduma za afya ili wananchi waweze kupata huduma bora, ambapo Serikali kupitia Mradi wa RBF(Result Based Financing/Kulipa kulingana na Matokeo) imetoa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma.

Akitoa ufafanuzi wa fedha hizo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi, Ndg.Abdallah Malela amesema, kupitia mradi wa RBF Halmashauri hiyo imepokea shilingi milioni 260, zilizogawanywa katika vituo vilivyopo 26 vya kutolea huduma za afya ambapo kila kituo kimepokea shilingi Milioni 10 ili kuboresha utoaji wa huduma za Afya.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga kufuatilia na kuhakikisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi anawasilisha kwake taarifa ya fedha za Mradi wa RBF alizopokea na kazi zilizofanyika katika vituo vya kutolea huduma.

“Mhe. DC umesikia hapa hawa watu wamepokea fedha toka mwezi saba mwaka huu na leo ndio wamekaa kikao cha mpango, maana yake ni kwamba mwezi wa nane wananchi hawajapata huduma zilizokusudiwa na Wizara ya Afya, na naamini yanayofanyika kwenye kituo hiki yapo katika vituo vyako vyote, sasa nimuombe Mkurugenzi wa Mji Jumatatu atuletee taarifa ya mpango uliotekelezeka” amesema Mtaka.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuwa atalifuatilia suala hilo pamoja na kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa katika ziara hiyo na ameahidi kuwachukulia hatua watumishi watakaoshindwa kutimiza wajibu wao katika kuwahudumia wananchi.

Kuhusu suala la taratibu za uwekaji wa umeme wa REA awamu ya III kwa wananchi na Taasisi za Umma ambalo liliwasilishwa na wananchi akiwemo Mwl. Daudi Jackson, Mkuu wa Mkoa, Mhe.Anthony Mtaka amesema atakutana na Meneja wa TANESCO Mkoa siku ya Jumatatu Septemba 04, ili wajadili namna na kushughulikia suala hilo.

Katika hatua nyingine Mtaka amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kuhakikisha Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri anafika eneo la ujenzi wa Soko la Ngulyati Jumatatu tarehe 04 Septemba kukutana na viongozi wa Kijiji na Kata, kwa ajili ya kuanza mpango wa ujenzi wa soko hilo ili kutatua kero ya ukosefu wa soko na kuwawezesha wananchi kupata sehemu ya kuuzia bidhaa zao.

Wakati huo huo Mtaka amewataka wananchi kutumia vizuri msimu wa kilimo, kulima mazao yanayostahimili ukame na akawasisitiza kutunza chakula walichokipata katika msimu uliopita kwasababu Serikali haitakuwa na chakula cha msaada.

Z Anto amng'ang'ania Diamond na Alikiba 'wote nawaweza vizuri'

$
0
0
Msanii wa muziki aliyewahi kufanya vizuri na wimbo Malavidavi, Mpenzi Jini na nyingine nyingi, Z Anto, amefunguka kwa kusema kuwa wiki hii ataachia kazi yake mpya huku akidai haamini kama kazi yake hiyo itashindwa kufanya vizuri kwa kuwa Diamond na Alikiba wameachia kazi zao mpya ambazo zinashindanishwa mitandaoni.

Akiongea na waandishi wa habari Jumamosi hii jijini Dar es salaam, Z Anto amedai yeye atapita katikati ya Diamond na Alikiba kwa kuwa muziki wake unapendwa na watu wa rika zote na pia hauna makundi kama ulivyo wa wawili wao.

"Wote nawaweza sana, muziki wangu ni mtamu na hauna makundi kwahiyo kila mtu anaweza kuusikiliza hata hao bila shaka ni mashabiki wa muziki wangu ndio maana nikasema kuogopa kuachia ngoma sasa hivi kwaajili ya Diamond na Alikiba utakuwa ni ujinga," alisema Z Anto.

Aliongeza "Binafsi najiamini sana kwa sababu muziki wangu ni mzuri na tayari kuna platfom ambayo niliiweka toka kipindi cha nyumba sema tu ukimya wangu ndio umewapa nafasi hawa ndugu zangu lakini sioni kama nitatizo kwasababu bado nafasi yangu naiona,"

Muimbaji huyo amesema anajua muziki umebadilika sana ndio maana na yeye amejipanga kuvingine ili kukabiliana na watu ambao wanashindana kwa sasa kwenye muziki.

"Kila mtu anatakua kuwa juu zaidi ya mwenzake na ukimya wangu umewapa nafasi wasanii wengi sana na lengo langu ni kufanya vizuri zaidi ndio maana nikasema sishindani na Diamond wala Alikiba mimi nitapita katikati yao na mashabiki ndio wenye maamuzi ya mwisho katika hili kwahiyo mimi ningesema tusubiri kazi mpya waisapport halafu ndio tuanze kupima," alisema Z Anto.

"Mimi naamini msanii yoyete anaweza kufanya vizuri zaidi ya hata wakongwe kama akijipanga vizuri muziki una sifa hiyo, kwahiyo mimi naweza kusema lolote linaweza kutokea kwenye muziki lisiwe leo au kesho muda ukifika hauwezi kushindana nao, wakati ni ukuta," alifafanua zaidi.

Katika ujio wake muimbaji huyo amesema tayari ameandaa audio na video ambayo itaanza kutoka na kuleta picha mpya katika muziki wake.

"Kazi zipo tayari kwa sababu ni nyingi na naanza na moja moja, siku yoyote kuanzia leo nitaachia kazi moja na baada ya upepo wa hapo nitaendelea kasi hiyo hiyo kadri mambo yanavyokwenda," alisema Z. 
Attachments area

Tiketi za ‘Tigo Fiesta 2017 - Tumekusomaa’ Zaanza Kuuzwa Kupitia TigoPesa.

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko Tigo, William Mpinga, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu namna ya kununua tiketi za Tigo Fiesta 2017 kwa njia ya Tigo Pesa. Kulia ni Mratibu wa Tigo Pesa, Daniel Mmbaga. (Na Mpiga Picha Wetu).

Tiketi za mapema zinapatikana kwa mitandao yote kwa 10% punguzo  la bei


Dar es Salaam,  Jumamosi  2 Septemba, 2017- Tigo inatoa punguzo la asilimia 10% kwa wateja wote watakaonunua tiketi zao za msimu wa Tigo Fiesta 2017 Tumekusomaa kupitia huduma ya Tigo Pesa.

Akizindua mauzo ya tiketi za Tigo Fiesta 2017 kupitia njia ya mtandao jijini Dar es Salaam leo, Mtendaji Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Tigo, William Mpinga aliwashauri wapenzi wa Tigo Fiesta kuchukua fursa hii kupata tiketi zao kwa TZS 9,000/- tu, hii ikiwa ni punguzo la 10% ya bei kupitia TigoPesa, au mtandao wowote wanaotumia kwa sasa. Bei halisi ya tiketi getini itakuwa ni TZS 10,000/-.  

Tigo ndio kampuni ya kwanza kuwezesha wateja kutuma pesa kwa njia ya mtandao kwenda mitandao mingine nchini. Kwa moyo huo huo, Tigo sasa inawapa wateja wa simu wanaotumia mitandao mingine nchini kununua tiketi za Tigo Fiesta 2017 kupitia mitandao yao.

‘Kununua tiketi ni rahisi. Fuata utaratibu wa kawaida wa kutuma pesa na tuma TZS 9,000 kwenda namba ya TigoPesa 0678 888 888. Hapo hapo utapokea ujumbe mfupi wa SMS unaothibitisha manunuzi yako ya tiketi. Hifadhi huo ujumbe mfupi. Baadaye utapokea maelekezo ya jinsi na wapi pa kwenda kuchukua tiketi yako,’ alisema.

‘Tigo inajiandaa kutoa ofa nyingine kibao katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2017 kwa hiyo wateja wetu wa Tigo, watumiaji wa TigoPesa na wapenzi wote wa Tigo Fiesta 2017 wakae tayari kufurahia ofa hizi bomba kadri ya tutakavyokuwa tunazitangaza.,’ Mpinga aliongeza.

Mwaka huu msimu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa utajumuisha mikoa ya Arusha Kahama, Musoma, Mwanza, Tabora na Dodoma. Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa pia itatua katika mikoa ya Iringa, Songea, Njombe, Sumbawanga, Morogoro, Tanga, Moshi na Mtwara, kabla ya kuhitimishwa jijini Dar es Salaam.


RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WASALI KATIKA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO LA MAGOMENI JIJI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amepiga magoti pamoja na  mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakiombewa sala  na Maaskofu wa Kanisa hilo la Waadventista Wasabato, Sala iliyokuwa ikiongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania Marc Walwa Malekana(wa kwanza kushoto)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakikabidhi mifuko 400 ya Saruji itakayotumika katika ujenzi wa Kanisa hilo la Wasabato la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mama Navana Cable aliyeambatana na mtoto  wake Rebecca Cable ambao familia yao imeahidi kumalizia ujenzi wa Kanisa hilo la Waadventista la Wasabato mara baada ya Rais Dkt. Magufuli kuendesha Harambee ya Papo kwa papo Kanisani hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mhariri Mtendaji waMagazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz mara baada ya kuahidi kuchangia katika kanisa hilo.
 Waziri Mstaafu katika awamu iliyopita Steven Wasira naye akichangia katika Harambee hiyo Kanisani hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Ndugu Dkt. Edward Hosea mara baada ya kuchangia katika ujenzi wa kanisa hilo la Wasabato lililopo Magomeni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshika mkono mtoto ambaye alikua anamsalimia wakati akitoka ibadani katika kanisa hilo la Magomeni.
Waumini mbalimbali wa Kanisa hilo wakiwa ibadani kama wanavyoonekana pichani. PICHA NA IKULU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amepiga magoti na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waumini wengine wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ushirika wa Magomeni Mwembechai katika Ibada ya Jumamosi kanisani hapo  jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na   mkewe Mama Janeth Magufuli wakiimba nyimbo katika ibada hiyo ya Jumamosi katika Kanisa la Waadventista Wasabato Ushirika wa Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na   mkewe Mama Janeth Magufuli wakisikiliza neno katika Ibada hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisoma neno pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli kanisani hapo wakati wa Ibada ya jumamosi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista la Wasabato Ushirika wa Magomeni Mwembechai  kabla ya kuendesha Harambee ya Ujenzi wa kanisa hilo ambapo zaidi ya Sh. 25milioni ziliahidiwa kukusanywa.


EFM NJE NDANI , SINGELI MICHANO ZAPAGAWISHA WAKAZI WA TABATA

$
0
0
 Msanii Chipukizi wa Muziki wa Singeli nchini akionyesha umahiri wake wa kuimba katika jukwaa la Singeli michano linaloendeshwa na programu ya Mziki mnene na Nje ndani  ya Efm Radio
 Mashabiki wa Muziki wa Singeli wakiwa wanashangilia ndani ya Uwanja wa Toto Tundu Tabata Jijini Dar es Salaam leo.
 Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Harmorapa akiongoza kundi la Efm Joging Tabata katika mazoezi ya mbio za pole yaliyofanyika asubuhi ya eo jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya Wanachama wa Efm Jogging  wakiwa katika mazoezi ya mbio za pole Tabatajijini Dar es Salaam leo
 Mkurugenzi wa Radio ya Efm na Tv E Sebo akiwania mpira mebele ya beki wa Tabata Veterans katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Tabata Sigara Jijini Dar es Salaam
 Benchi la Ufundi la timu ya Soka ya Efm na Tv E likiongozwa na Sudi Mkumba
 Wacheaji wa Efm wakifanya mazoezi kablaya mchezo huo kuanza mapema leo
Mashabiki wa soka waliofika kutazama mchezo kati ya timu ya Efm na Tabata Veterans
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images