Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1355 | 1356 | (Page 1357) | 1358 | 1359 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva (wanne kushoto) akishukuru kupokea msaada wa Mashuka 900 yenye thamani ya Tshs Milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (watano kushoto)
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva (wapili kushoto) akishukuru kupokea msaada wa Mashuka 900 yenye thamani ya Tshs Milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng Deusdedit Kakoko (watatu kushoto).

  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa mashuka 900 yenye thamani ya Sh. Milioni Kumi kwa Hospitali za Temeke, Mbagala Zakheim na Round zilizopo katika Wilaya ya Temeke.

  Msaada huo umekabidhiwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva ikiwa ni sehemu kutambua na kuthamini dhamira na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli, ya kufikisha huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wote na hasa wa hali ya chini.

  “Menejimenti ya TPA, chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, inaunga mkono kwa dhati kabisa juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuhakikisha jamii inapata huduma muhimu, TPA inayo Sera ya Misaada kwa Jamii ambayo imejikita katika kusaidia jamii kwenye nyanja za Afya, Elimu na Maendeleo ya Kijamii,” amesema Mhandisi Kakoko.

  Mhandisi Kakoko ameongeza kuwa pamoja na kwamba TPA kazi yake kubwa ni kuhudumia shehena mbalimbali zinazopita kwenye bandari zote nchini, lakini pia ina wajibu wa kurudisha kile inachokipata kutokana na huduma zake kwa kuisaidia jamii inayoizunguka na ndio maana imeamua kutoa msaada huo kwa Wilaya hii ya Temeke ilipo Bandari ya Dar es Salaam ambayo kiutendaji ndiyo bandari kubwa kuliko bandari zote hapa nchini.

  Hivi karibuni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alizindua rasmi kuanza kwa kazi ya maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam na mara itakapokamilika mwaka 2022 itaiwezesha bandari hiyo kuhudumia meli zenye uwezo wa kubeba kontena 8,000 kutoka kontena 2,500 za sasa na kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya ushindani na kuliongezea Taifa mapato.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  Prof Kenneth Linyani  Simala wakati  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe alliofuatana nao .
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  Prof Keneth Linyani Simala wakati  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar  jana.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  Prof Keneth Linyani Simala wakati  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar  Jana  29/08/2017. (Picha na Ikulu) 

  0 0


  0 0

  Wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana ya Msalato Manispaa ya Dodoma wamemuahidi Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo kwamba watapambana ili katika matokeo ya kidato cha sita mwakani shule yao iwe miongoni mwa shule kumi bora nchini. 

  Ahadi hiyo ilitolewa na wanafunzi hao katika ziara ya Naibu Waziri Jafo alipotembelea shule hiyo kukagua ujenzi wa miundombinu inayojengwa na serikali ili kuirudisha shule hiyo katika hadhi yake.

  Shule hiyo ni miongoni mwa shule kongwe 88 zilizo katika mpango wa ukarabatiwa na serikali ambapo ndani ya miaka 4 shule hizo zitakuwa ni shule zenye ubora wa hali ya juu kwa kuboreshewa mazingira yake yakiwemo mabweni, madarasa, vyoo, mabwalo, mifumo ya maji na umeme, pamoja na nyumba za walimu. 

  Katika shule hiyo, serikali hadi sasa imeshakamilisha ukarabati wa mabweni nane, mfumo wa umeme na maji.Aidha Serikali imejipanga kuendelea na ukarabati wa madarasa na ujenzi wa madarasa mengine manne mapya, ukarabati wa bwalo la chakula, majengo ya utawala, na nyumba za walimu. 

  Kufuatia uboreshaji huo, Wanafunzi wameishukuru serikali na wamemuahidi Naibu Waziri huyo kwamba watahakikisha wanajitahidi ili mwakani shule yao iwe miongoni mwa shule kumi bora katika matokeo ya kidato cha sita.

  Akizungumza na wanafunzi hao, Naibu Waziri Jafo amewahakikishi watanzania kwamba mpango wa serikali ni kuboresha shule za umma ili ziweze kutoa elimu bora hapa nchini.Mwaka jana, Naibu Waziri Jafo alitembelea shule hiyo na kuwataka wanafunzi wa kidato cha sita kuhakikisha wanafanya vizuri katika mitihani yao ili shule hiyo itoke kutoka shule ya 21 katika matokeo ya kidato cha sita mwaka jana ili waingie 10 bora. Jambo ambalo katika matokeo ya mwaka huu shule hiyo imeshika nafasi ya namba 14 kitaifa.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua maeneo ya vyoo na mifumo ya maji iliyokarabatiwa katika shule ya Sekondari ya wasichana Msalato.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo ya ukarabati wa mabwene kutoka kwa mmoja wa wakandarasi wanaofanya ukarabati huo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa mabweni nane yaliyofanyiwa ukarabati katika shule ya Sekondari ya wasichana.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa shule hiyo pamoja na maafisa wengine wakifanya ukaguzi wa majengo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Msalato Dodoma.
  Miongoni mwa mabweni yaliyokarabatiwa na serikali

  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  Kuna  matatizo  sana   kati  ya  wapangaji  na  wenye  nyumba  kuhusu  notisi  ya  kuondoka  au  kuondolewa.  Wako  wanaosema  notisi  ni  mwezi mmoja,  wako  wanaosema  ni  miezi  mitatu  n.k.  Kama  ni kweli  ama  hapana  tutaona hapa   sheria  inasemaje. 

  Masuala  ya  pango  yanaongozwa  na  sheria  kuu  mbili.  Moja  sheria  ya  ardhi  namba  4  ya  mwaka  1999  na  pili  sheria  ya  mikataba  sura  ya  345.  Kwa  pamoja  sheria  hizi  mbili  husimamia   jambo  hili.

  1.MIKATABA YA  PANGO.                
  Mikataba ya pango  inahusisha  makubaliano  ya  upangaji  kati  ya  mwenye  nyumba  na  mpangaji  au  mpangaji  na  mpangaji  mwingine  wa  pili.  Pango  laweza  kuwa   la  nyumba  ya  kuishi,   kwa  ajili ya  biashara,  nyumba  ya  ibada  au  shughuli  nyinginezo.   Yote  haya  yataingia  katika  maana  ya  pango.

  2.   AINA   ZA  MIKATABA  YA   PANGO.
  Sheria  ya ardhi   vifungu  vya  78  na  79  inatambua   mikataba ya  upangaji  ya  muda  mrefu  na  vipindi  vifupi. Inatambua  pango  la  wiki,  mwezi,  miezi,  mwaka  na  miaka.  Imetoa  uhuru  kwa  wahusika  wenyewe  kuamua  ni  muda  gani  wangependa  kuingia  mkataba. 

  3.   NOTISI  YA  KUONDOKA.
  Katika  vitu  muhimu  sana  katika  suala  la  pango  ni  notisi ya kuondoka   au  kuondolewa  katika  pango.  Jambo  la  kuzingatia awali  kabisa  ni  kuwa   notisi  hii  ni  muhimu  pande  zote  mbili.  Upande  wa  mwenye  nyumba  na  upande  wa  mpangaji.  Kila  mmoja  kwa  nafasi  yake  anawajibika  kutoa  notisi  kwa  mwenzake  panapo  mahitaji  ya  kuondoka  au  kuondolewa.

  Ikumbukwe  notisi  si  kwa  ajili  tu  ya kuondoka  na kuondolewa   bali  pia   hutakiwa  yanapotokea mabadiliko  yoyote  katika  masharti  ya  mkataba. Hii  ina  maana  hata  kuongeza  kodi, kupanga  kukagua  nyumba, kufanya  marekebisho  n.k.  notisi  yafaa  itolewe. 

  KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com


  0 0

  Waziri wa afya ,maendeleo ya jamii,jinsia na watoto HAMISS KIGWANGALA amewataka viongozi wote waliopo kwenye idara hiyo kufanya kazi hasa kwa kuwajali wanawake kutokana na tabu wanazozipata pale wanapofuata mataibabu habari kamili hii hapa video.

  0 0

  Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) akiongea wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi). Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa DTBi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Mhandisi George Mulamula (kushoto) akiongea wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi). Kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando.
  Mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya Msingi ya Kijitonyama Mariam Said akionyesha ujuzi wa kutumia kompyuta huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Mhandisi George Mulamula (kushoto) na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi).
  Mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya Msingi ya Kijitonyama Karim Ramadhan akionyesha ujuzi wa kutumia kompyuta huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Mhandisi George Mulamula (kushoto) na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi).

  Airtel kwa kushirikian na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi)  leo imetangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehema yatakayotolewa katika maabara  iliyopo katika shule ya msingi Kijitonyama na kuwaalika wanafunzi wa shule za msingi, sekondari, wanavyuo na jamii yote kwa ujumla kujiandikisha  katika mafunzo yatakayowapatia ujuzi utakaochochea kuondoa umasikini na kukuza technolojia.

  Maabara  ilianzia kama kituo cha kutoa elimu ya Tehama mwezi Julai 2017 kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi katika masomo ya Tehama yatakayosaidia matumizi ya teknolojia na Tehama katika biashara.  Maabara hii kwa sasa itaanza kufanya kazi kwa kutoa masomo mbalimbali ambayo ni pamoja na  lego Robotics, program za uhuishaji kwa watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D objects”    pamoja na  msingi wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program mbali mbali ,mtandaousalama wa mtandao

  Akitangaza program hizo, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania , Jackson Mmbando alisema “ Tumeanzisha maabara hii ya kompyuta kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi na waalimu wa shule ya msingi  pamoja na vijana  wanaopenda kujikita kwenye masomo ya sayansi na Tehama kupata ujuzi wakiwa katika umri mdogo. Lengo letu ni kuendelea kuiwezesha sekta ya technolojia na Tehama kukua na kuzalisha vijana ambao wataweza kuvumbua na kutengeneza programu zitakazoleta suluhuhisho kwenye mahitaji ya biashara naustawi wa jamii.  Tunaamini maabara hii  ni jukwaa la kukuza vipaji vya vijana na Airtel inajisikia fahari kuwa sehemu ya kuleta mapinduzi na mabadiliko haya katika jamii na nchi kwa ujumla ikiwa ni mwendelezo wa program ya Airtel Fursa inayoendeshwa na Airtel”.

  Mmbando alieleza kuwa maabara hii itatoa mfunzo bure kwa walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kijitonyama ila kwa  kijana yeyote asiyekua mwanafunzi au mwalimu wa shule hii atakayependa kujiandikisha ataruhusiwa kufanya hivyo.
  Fomu za kujiandikisha zitapatikana kwa njia ya mtandao kwa gharama ya shilingi 20,000 kupitia www.teknohama.or.tz na  www.airtelfursa.com  au kwa kutembelea maabara  iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 mchana. Mafunzo yatatolewa  kwa wiki 4 kuanzia tarehe 4 septemba 2017.

  “natoa wito kwa vijana hususani wanafunzi wa shule ya msingi kijitonyama na maeneo ya jirani kutumia fursa hii kujiendeleza zaidi”. Aliongeza Mmbando.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mhandisi George Mulamula alisema “ pamoja na kuwa na wahitimu kutoka katika vyuo mbalimbali  lakini bado Tanzania tuna uhaba wa wataalamu wabunifu wenye ujuzi  wa kutengeneza program u zitakazotatua changamoto za kijamii  za kibiashara na zinazokuza  kipato na kuondoa umasikini”

  “Maabara hii  ina malengo mawili: kuwatayarisha vijana wanaotarajiwa kwenda chuo kikuu kuwa na elimu ya kibiashara ya Tehama zaidi ya kuwa na uelewa wa kompyuta na programu za simu. Lakini pili kuwaunganisha na wadau wa kibiashara ili kuwapa mwelekeo utakaowawezesha kutoa suluhisho la kiteknolojia na Tehama zitakazosaidia nchi kufikia malengo yake ya 2015 ya uchumi wa viwanda pindi watakapohitimu shule.

   DTBi inaishukuru sana Airtel na uongozi wa shule ya Msingi Kijitonyama kwa kuungana nasi na kuwa sehemu ya kuleta mapinduzi haya ya Tehama kwa jamii na katika biashara kwa ujumla” alisema Mulamula
  Aliongeza kwa kusema huu ni mwanzo tu kwani walimu, vijana na jamiii watapata ujuzi na ni  matumaini yetu programu hii pia itafika maeneo mbalimbali nchini.

  DTBi kama msimamizi wa masomo wana timu ya wataalamu ambao wamejitolea kutoa mafunzo kwa vijana na kuleta mabadiliko katika jamii. Tunawakaribisha wale watakaopenda  kushirikiana nasi kujiunga sasa, alimalizia.


  0 0

   NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping (kulia), katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
   NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo (wapili kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping (kulia), katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa KIanali mstaafu Ngemela Lubinga.
   Ujumbe wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM_Bara Rodrick Mpogo na ujumbe wa Naibu Waziri wa mamambo ya Nje wa CPC, wakishangilia baada ya mazungumzo kumalizika. 
   NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping baada ya mazungumzo yao katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).
   Naibu Katibu Mkuu akimsindikiza mgeni wake baada aya mazungumzo hayo
    Naibu Katibu Mkuu akimsindikiza mgeni wake baada aya mazungumzo hayo
    Naibu Katibu Mkuu akimsindikiza mgeni wake baada aya mazungumzo hayo
    Naibu Katibu Mkuu akimsindikiza mgeni wake baada aya mazungumzo hayo
   NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping baada ya mazungumzo yao katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katribu wa NEC Siasa na Uhusian9o wa Kimataifa kanali Mstaafu Ngemela 
   NAIBU Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping baada ya mazungumzo hayo
   UGENI HUU SAFI SANA, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo akimwambia Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole baada ya wageni kluondoka baada ya mazungumzo. PICHA NA BASHIR NKOROMO. PICHA NYINGI ZAIDI ZA TUKIO HILO/ BOFYA HAPA


  0 0


  0 0  0 0

  Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji thamani na Huduma za Kifedha Vijijini(MIVARF), imefanikiwa kupunguza umasikini wa kipato na kuimarisha uhakika wa chakula katika Halmashauri 73 zinazotekeleza program hiyo kwa Tanzania Bara na Visiwani.

  Akiongea wakati wa Mkutano wa wadau wa MIVARF wa siku mbili tarehe 29 hadi 30, Agosti, 2017  mjini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya uratibu wa shughuli za serikali Ofisi ya Wazir Mkuu, Obey Assery alifafanua kuwa lengo la Program hiyo inalenga kuongeza uzalishaji na tija kwa walengwa.

  “Program imelenga kuwajengea uwezo wazalishaji ambao huwa katika vikundi kwa kuvifiki vikundi 2,331 vyenye walengwa 81,677. Kimsingi Programu imelenga kumuwezesha mkulima aweze kufanya  kilimo cha kibiashara” alisema Assery.

  Naye Mratibu wa Program Kitaifa, Walter Swai alibainisha kuwa Program imelenga kuwajengea uwezo walengwa kuyafikia masoko ya uhakika ili waweze kupunguza umasikini wa kipato.

  “Programu imelenga kuboresha 1,000km za  barabara hadi sasa 9991.8km zimeshakamilika sawa na asilimia 92. Lakini pia kwa upande wa miundo mbinu ya masoko tunajenga maghala, hadi sasa kati ya maghala 29 yaliyo kwenye malengo tayari tumekamilisha maghala 24 sawa na asilimia 83 ” alisistiza Swai.

  Swai aliongeza kuwa Program hiyo imepanga kukarabati maghala 6 ambapo tayari yote yamekamilika, pia tumelenga  kujenga masoko 16 ambapo hadi sasa masoko 7 yamekamilika ambayo ni asilimia 44.

  MIVARF;  ni Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini  iliyobuniwa  na serikali ya Tanzania  kwa  kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo yaani (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).
   Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za serkali Obey Assery akisistiza jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa MIVARF Agosti 30, Agosti, 2017  mjini Dodoma.
   Wataalamu kutoka Program ya MIVARF wakifuatilia majadiliano ya wadau wa Program hiyo wakati wa mkutano wa wadau wa MIVARF Agosti 30 Mjini Dodoma.
  Baadhi ya wadau wa MIVARF wakifuatilia mkutano wa wadau wa MIVARF unaofanyika mjini Dodoma Agost, 2017.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda Wamesitisha zoezi la BOMOA BOMOA kwa Nyumba zaidi ya elfu kumi na saba (17, 000) zilizotangazwa KUBOMOLEWA na Baraza la Hifadhi ya Mazingira NEMC.

  Hatua ya kusitisha zoezi hilo, Imekuja kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda kuzungumza na Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuhusiana na Sintofahamu ya bomoa bomoa hiyo ambayo amemueleza Mhe Rais Magufuli kuwa Taarifa za BOMOA BOMOA ya Nyumba elfu kumi na saba iliyotolewa HAIKUFIKA ofisini Kwake, Jambo ambalo ni tofauti na Taratibu za Utendaji kazi wa Serikali.

  Mhe Makonda amesema, hata kama TAMKO hilo limetolewa na watumishi wa Mkoa mfano Wakurugenzi wa Manisapaa au Wakuu wa Wilaya walioko Chini ya Mamlaka ya Mkuu wa Mkoa LAZIMA Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ipate taarifa na iridhie bomoa bomoa hiyo, na pia hata kama Taarifa zimetoka Wizarani inapaswa taratibu za kimaandishi zifuatwe kwa kujulisha Ofisi ya Mkoa.

  "haiwezekani mtu kutoa TAMKO la kuvunja Nyumba elfu kumi na saba bila Mkoa kujua, hilo HALIWEZEKANI" amesema Mhe Makonda.

  Mhe Makonda amefafanua kuwa AMEONGEA na Mhe Rais Magufuli na Kumuuliza kama ana taarifa za zoezi la Ubomoaji wa Nyumba elfu kumi na saba ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda ALIMUELEZA Mhe Rais Magufuli kuwa HANA taarifa hizo za UBOMOAJI, zaidi Ubomoaji wa Nyumba zilizo kwenye Hifadhi ya Barabara ya kuanzia Ubungo kwenda KIMARA na MBEZI Ubomoaji unaofanywa kwa ajili ya upanuzi wa Barabara ya Morogoro, Ubomoaji wa Nyumba zilizo Jirani na Reli hususani ni zile zinazohusiana na Ujenzi wa Reli Mpya na ya Kisasa.

  Kutokana na Sababu hizo, Mhe Makonda amesema Mhe Rais amesikitishwa na TAMKO hilo la kutaka KUBOMOLEWA kwa Nyumba zaidi ya elfu kumi na saba na ametoa pole kwa Wananchi waliokumbwa na TAHARUKI ya TAMKO hilo la Ubomoaji, na kusisitiza kuwa Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli HAKUCHAGULIWA kwa ajili ya KUBOMOA Nyumba za watu na kusisitiza kuwa anataka wananchi WANAOISHI katika maeneo HALALI kuachwa mana AMEPATA taarifa kuwa huenda ZOEZI hilo lingekwenda mbali zaidi mpaka kwa Wananchi WASIOHUSIKA.

  Katika HATUA nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda AMEPIGA MARUFUKU zoezi lolote UBOMOAJI wa Nyumba pasipo Ofisi yake kupewa TAARIFA na kisha KURIDHIA Ubomoaji huo.

  Mwisho, Mhe Paul Makonda AMEWATAKA wananchi na wakazi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam kuzingatia SHERIA na wasivamie maeneo au kuuziwa VIWANJA na Matapeli na pia AMEWATAKA wananchi kuchukua TAHADHARI hususani ni katika maeneo yote HATARISHI ambayo sio SALAMA kwa MAKAZI na kuwataka kila Mwananchi Mwenye Familia KUTAFUTA Salama kwa Maisha yake na ya Familia yake.

  Mhe Makonda Pia ametoa OMBI Maalumu Kwa Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi la KUBORESHA mfumo wa Ardhi katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha mpango wa kuweka MAAFISA ARDHI katika KATA zote za Mkoa wa Dar es Salaam ambao watakuwa na JUKUMU la KUSIMAMIA, KURATIBU masuala yote ya Ardhi ngazi ya KATA hatua ambayo itasaidia kuondoa Migogoro na UTAPELI kwa Wananchi kuuziwa au kununua Ardhi katika maeneo ambayo HAYARUHUSIWI, ambapo amesema amepata wazo hilo kutokana na uzoefu aliopata akiwa Rais wa umoja wa Vyuo vikuu -TAHILISO ambapo alishirikiana na Bodi ya Mikopo kuanzisha mfumo wa kuwa na MAAFISAMikopo katika vyuo hatua iliyosababisha kuondoa kero ya wanafunzi kufuatilia Mikopo katika Ofisi za bodi ya Mikopo hatua ambayo imekuwa mwarobaini wa tatizo la kufuatilia Mikopo kwa wanafunzi, Mhe Makonda amesema atamwandikia OMBI hilo na kulifikisha Rasmi kwa Mhe Lukuvi ili amsaidie kulifikisha kwa Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili utekekezaji.

  Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
  30/08/2017 
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Tuangoma wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam  na kusitisha bomoa bomoa iliyokuwa ikiendelea katika eneo hilo. Pia  amewaomba kujiepusha na kujenga nyumba za kuishi katika maeneo hatarishi.
  Baadhi ya wananchi wa Tuangoma Wilayani Temeke wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo (hayupo pichani),Mhe. Paul Makonda  mara baada ya kutembelea eneo lao na kuzungumza nao.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa amezungukwa na wananchi mbalimbali wa eneo la Tuangoma,akitembelea maeneo ambayo nyumba zake zilikuwa zikitarajiwa kukumbwa na zoezi  la bomoa bomoa.
  Baadhi ya Nyumba ambazo zilitakiwa kubomolewa,ambapo kwa sasa hazitabolewa kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli kusitisha zoezi hilo na kuwataka wahusika wafuate taratibu na sheria za Ardhi .

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  SERIKALI imejipanga katika masuala ya michezo  kutoa nguvu pamoja na kuenzi michezo ya shule za misingi na Sekondari ili kuweza kushiriki mashindano mbalimbali ya Kikanda na Dunia na wachezaji kurudi medali za dhahabu.

   Hayo ameyasema leo Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wakati akipokea bendera ya Taifa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makongo ambao walishiriki mashindao ya Shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Uganda (FEASSSA) hivi karibuni, amesema wanafunzi wameonesha vipaji na kuweza kushika na nafasi ya tatu katika mashindano hayo.

  Amesema kuwa shule zilizoshiriki zimeweza kutangaza Tanzania hivyo katika mashindano yajayo nguvu itaongezeka  kwa sekondari nyingi kushiriki na kasha kuweza kupata wachezaji mbalimbali ikiwemo timu ya taifa pamoja na riadha.

  Dk. Mwakyembe amesema kuwa katika Wizara hiyo atahakikisha wanafnaya vizuri katika michezo kwa kuweza kupata ushindi  ikiwa kwa vilabu vyote vya michezo kujipanga.
  Amesema katika michezo hakuna uchawi kinachohitajika ni juhudi na maarifa kwa wachezaji wanavyoshiriki mashindano yeyote ya ndani na ya nje ya nchi.

  Aidha amesema wanafunzi walioshiriki na kushika nafasi ya tatu waongeze juhudi katika mashindano yajayo waweze kuwa washindi wa kwanza katika mashindano ya (FEASSSA).
  Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akipokea bendera kwa wanafunzi wa sekondari Makongo walioshiriki mashindao ya Shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Uganda (FEASSSA) leo jijini Dar es Salaam.

   Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza baada ya kupokea Bendera kwa wanafunzi wa  Shule ya Makongo walioshiriki mashindao ya Shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Uganda (FEASSSA) leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akimvisha medali mwanafunzi wa Shule ya  Sekondari Makongo, Winfrida Makenji aliyepata medali nne za mshindi wa tatu katika mashindao ya Shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Uganda (FEASSSA) leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Wawakilishi wa Kampuni ya Jamka Enterprise Company wakipokea hundi ya shilingi milioni Tano ambazo wamekopeshwa na  Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) leo mara baada ya kikao cha Wadau wa Maji na Mazingira kufunguliwa jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya kuzungumza masuala ya maji na mazingira.
  WADAU wa maji na Mazingira washauriwa kushirikiana ili kukidhi mahitaji ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam pia washauriwa kutoa namba maalumu ya simu kwaajili ya wananchi waonapo tatizo la maji au maji kutiririka katika maeneo mbalimbali ili kuondoa upotevu wa maji katika mkoa wa Dar es Salaam.

  Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakati akizungumza na wadau wa maji pamoja na wadau wa Mazingira jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Wadau wamaji wanatakiwa kushirikiana na ili kupunguza upotevu wa maji kutokana na ubovu wa miundo mbinu ya maji.

  Kaimu Mkurugenzi Msaidizi,  usambazaji wa maji

  Haruni Josef Kwa upande wake DAWASCO wamewaomba wadau wa maji ili kuendeleza na kukuza maendeleo ya kwaajili ya kujenga mtandao wa maji kwaajili ya kuyasafirisha ili yamfikie kila mwananchi wa jiji la Dar es Salaam.

  Wadau waliokutana leo ni Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), wizara ya Afya, DAWASCO,DAWASA, WATERAID na wadau wa mazingira kwa pamoja wakiwa na kauli mbiu ya maji ni uhai na usafi ni utu. 
   
   Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando akizungumza na wadau maji na usafi wa Mazingira wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakizungumzia masuala hasa ya maji safi na maji taka pamoja na kutatua changamoto za maji katika mkoa wa Dar es Salaam.
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na wadau wa maji safi pamoja na wadau wa maji taka ili kutatua changamoto za maji katika jiji la Dar es Salaam.Pia ameshuhudia kusaini makubaliano kati Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Taasisi ya Borda ya hapa nchini.
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akishuhudia taasisi ya Borda na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya wadau ya maji wa maji safi na wazingira walipokutana leo leo kufanya mazungumzo ya wadau wa maji pamoja na wadau wa mazingira.
   Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando akibadilishana mkataba wa makubaliano kati ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Tasisi ya Borda kwaajili kuendeleza  na kukabiliana changamoto mbalimbali za maji na Mazingira.
  Wawakilishi wa Kimchi  Enterprise Company wakipokea hundi ya shilingi milioni kumi ikiwa wamekopeshwa na Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kikao cha Wadau wa Mazingira kukaa kuangalia changamoto mbalimbali zanazo kabili sekta ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam.
  Wawakilishi wa Enviromenta Management community envelopment wakipokea hundi ya shilingi milioni kumi kwaajili ya kuendeleza sekta ya maji pamoja na maji ambazo wamekopeshwa na  Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) jijini Dar es Salaam leo. kwaajili ya kuendeleza maji na mazingira katika mkoa wa Dar es Salaam.
  Baadhi ya ya wadau wakiwa katika mkutano wa wadau wa maji na mazingira jijini Dar es Salaam  leo.

  0 0


  Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.

  Aidha Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na wahalifu. Jitihada zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha mkoa wetu unakua mahala salama. Hata hivyo kumekuwa na tukio moja la unyang’anyi wa kutumia silaha wilaya ya Chunya kama ifuatavyo :-

  Mnamo tarehe 29.08.2017 majira ya saa 06:00hrs katika kitongoji cha Logia, kijiji na kata ya Upendo, tarafa ya Kiwanja wilaya ya Chunya, mkoa wa Mbeya, dereva HERI ELIA RUBIENO [32], mkazi wa Ilemi – Mbeya akiendesha gari T.767 DDN aina ya Isuzu basi la abiria liitwalo SAFINA mali ya ISAYA SAMWEL MTITU, mkazi wa Njombe ikitokea kijiji cha Mamba kwenda Mbeya mjini njiani ilizuiwa na watu wapatao sita ambao waliweka magogo njiani wakiwa na silaha bunduki moja idhaniwayo kuwa ni shortgun na silaha nyingine za jadi [panga, rungu, na shoka]

  Katika tukio hilo abiria waliporwa simu aina mbalimbali zenye thamani ya Tshs 410,000/= pamoja na pesa taslimu Tshs 2,771,000/=. Aidha wakati wa tukio abiria kadhaa walipata michubuko na mikwaruzo na walipatiwa matibabu katika zahanati ya Makongolosi na kuruhusiwa. Watu hao mara baada ya tukio walifyatua hewani  risasi mbili na kutokomea kusikojulikana kwa kutumia usafiri wa pikipiki.

  Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata majambazi watatu ambao pia walitambuliwa na wahanga pamoja na pikipiki moja MC 388 BFZ aina ya Kinglion. Watuhumiwa hao ni

  i.    JUAKALI MBALAMWEZI [65], mkazi wa Sumbawanga
  ii.    GASPAR MAHINI [22], mkazi wa Sumbawanga
  iii.    PETRO JUMA [21], mkazi wa kijiji cha Mamba [A].

  Ufuatiliaji zaidi kuhusiana na tukio hili bado unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwakamata watuhumiwa wengine pamoja na silaha.

  WITO:
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu  Kamishna wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA  anatoa  wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria, badala yake wahakikishe wanawafikisha katika mamlaka husika watu wanaowakamata kwa tuhuma mbalimbali ili sheria ichukue mkondo wake.

   Aidha Kamanda MPINGA  anatoa rai kwa yeyote mwenye taarifa juu ya  watu wengine waliohusika katika tukio hilo  azitoe katika mamlaka husika ili wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake vinginevyo wajisalimishe mara moja. Pia anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kuwa na tamaa ya kujipatia utajiri wa haraka kwa kutumia njia mkato zisizo halali, badala yake wafanye kazi halalli ili kupata kipato halali.

  Pia  Kamanda MPINGA anawatakia Heri ya sikukuu ya EID EL HAJI wakazi wa Mkoa wa Mbeya washerehekee kwa amani na utulivu na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi. Watumiaji wa vyombo vya moto na watumiaji wengine wa barabara wazingatie  Sheria za usalama barabarani.

  [MOHAMMED R. MPINGA - DCP]
   KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Morogo Dkt Kebwe Stephen akimsikiliza Mwanasayansi Susan Rumisha aliyekuwa akitoa maelezo mbalimbali kuhusu juu ya umuhimu wa utafiti wa vifo vinavyotokea katika Hospitali za Tanzania,
  uliofanyika hivi karibuni uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na mrejesho unaoendelea. Dkt Kebwe aliwatembelea na kuzungumza nao washiriki wa Warsha hiyo iliyofunguliwa jana mkoani Morogo.
   Mwanasayansi Peter Emanuel akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen wakiwemo na washiriki wengine wa Warsha hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogo Dkt Kebwe Stephen (pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mbalimbali wa Warsha hiyo inayoendelea mkoani humo.

  =====   ===== ====== ======

  MUKHTASARI WA TAARIFA YA UTAFITI WA VIFO VINAVYOTOKEA KATIKA HOSPITALI YA TANZANIA

  Utangulizi

  Taarifa za vifo ni moja ya vyanzo muhimu vya takwimu katika kupanga mipango na kuandaa sera ya afya. Kuainisha vyanzo vya vifo katika hospitali zetu ni muhimu ili kufuatilia ongezeko la matukio ya vifo na kuweka vipaumbele katika kuboresha huduma za afya. Hata hivyo, kumekuwa na uhaba mkubwa wa takwimu za vifo vinavyotokea katika hospitali zetu zilizoainishwa kama inavyostahili.

  Utafiti huu ulifanywa kuainisha matokeo ya vifo katika hospitali 39 za Tanzania ili kubaini maradhi yanayoathiri jamii yetu. Utafiti huu pia ulichunguza uwepo, upatikanaji na ubora wa takwimu za vifo hospitalini.

  Mbinu za utafiti: Utafiti huu ulifanyika kati ya Julai na Desemba 2016 na ulihusisha jumla ya hospital 39. Hospitali hizo ni pamoja na hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa, Hospital Maalum na hospitali za Wilaya. Takwimu hizi zilipatikana kutoka kwenye rejesta za hospitali na za Wakala wa Vizazi na Vifo katika ofisi za Mikoa na Wilaya. Taarifa zilizokusanywa zilihusu wasifu wa jinsia ya mgonjwa na chanzo cha kifo.

  Vyanzo vya vifo viliwekwa katika makundi 45 kulingana na utaratibu wa makundi ya magonjwa uliowekwa na Shirika la Afya Duniani.

  Matokeo: Kwa ujumla kulikuwa na ugumu katika upatikanaji wa takwimu. Utunzaji wa takwimu katika hospitali nyingi ulikuwa na mapungufu makubwa, na baadhi ya takwimu hazikupatikana katika baadhi ya hospitali au baadhi ya miaka iliyokusudiwa. Utunzaji wa takwimu ulikuwa mzuri kiasi katika hospitali za kanda kuliko za mikoa na wilaya. Matumizi ya majina ya magonjwa kwa kufuata mwongozo wa kimataifa yalikuwa hafifu.

  Jumla ya vifo 247,976 vilitolewa taarifa katika kipindi cha miaka 10 (2006-2015). Kulikuwa na tofauti kubwa katika idadi ya vifo kati ya jinsia ya kiume na ya kike. Vifo vingi viliathiri zaidi wanaume kuliko wanawake. Vifo vingi vilitokea katika hospitali za Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Mwanza.

  Vifo katika kundi la watoto chini ya miaka 5 vilichangia 20% ya vifo vyote. Vifo vingi viliathiri kundi la watu wenye umri wa miaka 30-45. Kwa wastani, watu wengi hufa wakiwa na umri wa miaka 31 (wanaume miaka 33 na wanawake miaka 29).

  Magonjwa yaliyoongoza kusababisha vifo ni malaria (12.8%), magonjwa ya mfumo wa hewa (10.1%), UKIMWI (8.0%), upungufu wa damu (7.8%) na magonjwa ya moyo na mfumo wa damu (6.3%).

  Vifo kwa baadhi ya magonjwa vilipungua katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Kati ya mwaka 2006 na 2015; vifo kutokana na malaria vilipungua kwa 47%, UKIMWI kwa 28% na Kifua Kikuu kwa 26%. Hata hivyo, kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vilivyosababishwa na magonjwa yanayoathiri kundi la watoto wachanga (chini mwezi mmoja) kwa 128%.

  Hospitali za mkoa wa Dar es Salaam zilikuwa na wagonjwa wengi waliokufa kutokana na malaria, UKIMWI, ajali, maambukizi ya bakteria kwenye damu, upungufu wa damu, saratani na kifua kikuu. Mkoa huu ulifuatiwa kwa karibu na Morogoro ambao ulikuwa na vifo vingi vilivyotokana na malaria na kifua kikuu. Malaria na upungufu wa damu ulichangia vifo vingi kwenye kundi la watoto chini ya miaka mitano. Vifo vingi kutokana na UKIMWI na Kifua Kikuu viliathiri watu wazima. Ajali ziliathiri kundi kubwa la vijana; wakati saratani ziliathiri makundi ya umri wote.

  Uchanganuzi wa maradhi katika makundi ya magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukiza na kundi la ajali na majeraha ulionesha tofati kubwa kati ya mikoa na mikoa. Mikoa ya Pwani, Geita na Katavi iliathirika zaidi na magonjwa ya kuambukiza na utapia mlo. Vifo kutokana na ajali na majeraha viliathiri zaidi mikoa Rukwa, Tabora, Singida na Kigoma. Kundi la magonjwa yasiyoambukiza limeathiri zaidi mikoa ya Ruvuma, Manyara, Dar es Salaam na Mwanza.

  Hitimisho: Utafifi umeianisha changamoto katika ukusanyaji, uchanganuzi na matumizi ya takwimu katika hospitali zetu. Kumekuwa na matumizi hafifu ya majina ya magonjwa kwa kutumia mwongozo wa kimataifa. Vyanzo vikuu vya vifo nchini Tanzania ni malaria, maradhi yanayoathiri mfumo wa kupumua, UKIMWI, upungufu wa damu na magonjwa ya moyo na mfumo wa damu. Kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya watoto wachanga, na ongezeko la vifo kutokana na magonjwa ya mfumo wa kupumua katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

  Mapendekezo: (i) Serikali iandae mwongozo wa ukusanyaji, matumizi, utunzaji na uhifadhi bora wa takwimu za afya; (ii) Kujenga uwezo wa watumishi wa afya katika uchanganuzi ili kuboresha matumizi ya takwimu; (iii) Kuimarisha mfumo wa takwimu wa kielektroniki; (iv) Kuimarisha mafunzo ya madaktari katika utumiaji wa mwongozo wa kimataifa wa kuanisha magonjwa na vyanzo vya vifo.

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kanda ya ziwa, Ally Maswanya akizungumza na wanahabari na wananchi kabla ya kukata utepe wa uzinduzi wa kisima mapema mwishoni wa wiki iliyopita.
  Mbunge wa Rorya- Lameck Airo akipampu maji wakati wa sherehe za uzinduzi wa kisima chenye thamni ya Tsh.18/- milioni kilichodhaminiwa na kampuni ya Tigo.

   

  Mkuu wa wilaya Rorya- Samson Chacha akitwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha  Nyasoro, Penina Bailes
  iMkurugenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kanda ya ziwa,Ally Maswanya,akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Nyasoro kata ya Bukwe halmashauri ya wilaya ya Rorya mkoani Mara,Patero Opiyo mara baada ya uzinduzi wa kisima kilichochibwa kwa udhamini wa Tigo chenye thamani ya Tsh.18/- milioni
  Mbunge wa Rorya- Lameck Airo akizungumza na wanahabari na wananchi kabla ya kukata utepe wa uzinduzi wa kisima  


  Wanachi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kisima jana.


  0 0

  In fulfilment of its Corporate Social Responsibility, the Karimjee Jivanjee Foundation has donated a brand new ambulance to Idodi health centre through the Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development, Hon William Lukuvi worth US$47,519.
  The vehicle is meant to ease the challenges faced by Idodi health centres that hinder them to offer health services to the citizen effectively. 
  Present during the presentation was Karimjee Jivanjee Foundation Chairman, Hatim A. Karimjee and Toyota Tanzania Executive Director, Yusuf A. Karimjee.
  Speaking at the event Karimjee Jivanjee Foundation Chairman, Hatim A. Karimjee said that the Foundation is committed to support communities in Tanzania primarily through education and applauds the efforts of Idodi health centre to support the patients.
  The Hon William Lukuvi thanked the Karimjee Jivanjee Foundation and Toyota Tanzania Ltd for their generosity, said that Toyota is the world’s most successful vehicle manufacturer.
  For seven generation, the Karimjee Jivanjee Group has established a strong record for its philanthropic activities by contributing to the development and growth of Tanzania and East Africa.
  The Karimjee Jivanjee Foundation (KJF) is an amalgamation of various Karimjee Jivanjee charitable institutions since the 1940’s. It was founded as a trust in 2006 and officially registered in 2010.
  Today, KJF’s core charitable and CSR focus centres on Education in Tanzania, most notably by providing annual scholarships to young Tanzanians to study at graduate level.
  Other past projects and partnerships have included: providing scholarships to Doctors to graduate for Masters Degree in Pediatric Oncology at Muhimbili University of Health and Allied Science (MUHAS) through Tumaini la Maisha (NGO), supporting Read International in supplying text books to secondary schools, supporting Rotary International with various projects including the Muhimbili National Hospital (Cancer ward), promoting science and technology in Tanzania through the Young Scientists Tanzania (YST) programme and educational support to TESA, a Tanzanian NGO established by the Canadian alumni of the Karimjee Secondary School in Tanga.
   MINISTER for Lands, Housing and Human Settlements Development, Mr William Lukuvi receives an ignitions keys from Karimjee Rivanjee Foundation Chairman, Mr Hatim Karimjee in Dar es Salaam August 30, 2017 for Idodi Health Centre based in Iringa region. The brand new ambulance worth 106/-m to ease the challenges faced by the centre that hinders them to offer health services to patients effectively. 
  Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development, Mr William Lukuvi tests the brand new ambulance worth 106/-m in Dar es Salaam yesterday, after receiving it from Karimjee Rivanjee Foundation Chairman, Mr Hatim Karimjee (left) for Idodi Health Centre based in Iringa region. The vehicle is meant to ease the challenges faced by the centre that hinders them to offer health services to patients effectively. (Photos by Robert Okanda)

  0 0

  Na Neema Mathias na Paschal Dotto- MAELEZO.
  Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) imeanza rasmi utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari kwa kutoa leseni kwa vyombo vya machapisho yakiwemo Magazeti na Majarida.  

  Akizungumza katika makabidhiano ya leseni hizo Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema  utoaji wa leseni ni utekelezaji wa agizo rasmi lililotolewa Agosti 23, 2017 lililowataka wamiliki wote wa machapisho kujisajili upya na kupewa leseni kwa lengo la kuifanya tasnia ya Habari kuwa taaluma rasmi kama zingine.
  “Leseni hizo zimeanza kutolewa rasmi Agosti 23 na zoezi hilo litaendelea hadi Oktoba 15, 2017 na baada ya hapo wale amabo watachapisha magazeti  na majarida bila kuzingatia Sheria hiyo watakuwa wametenda kosa la jinai”, alisema Dkt. Abasi.
  Katika zoezi hilo Dkt. Abbasi alitoa leseni kwa vyombo vinne ambavyo ni Jarida la Nchi Yetu linalomilikiwa na Idara ya Habari MAELEZO, gazeti la Daily News, Habari Leo pamoja na Spoti Leo ambayo ni magazeti ya Serikali.
  Dkt. Abbasi ametoa wito kwa vyombo vingine vya habari ambavyo bado 
  havijaanza taratibu za upataji wa leseni visisubiri hadi dakika za mwisho za mchakato huo ili kuepuka msongamano na usumbufu usio wa lazima.
  “Nitumie fursa hii kuwaalika ambao hawajapata leseni wafanye haraka, Tanzania Standard Newspaper (TSN) walitimiza masharti ndani ya siku tatu ndio maana leo wamepata leseni hizo, hakuna urasimu wala nia mbaya ya kufungia baadhi ya machapisho kama wengi wanavyodai bali ni katika kutekeleza matakwa ya Sheria”, alisisitiza Dkt. Abbasi.
  Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa TSN Dkt. Jim Yonazi ameviasa Vyombo vingine vya Habari kutekeleza agizo hilo ili kupata uhuru mpana katika uwajibikaji pamoja na kuwa mfano wa kutii Sheria bila shuruti ili taaluma ya habari iendelee kuheshimika kwa jamii.
  “Ukifanya kazi kihalali unakuwa na uhuru wa kufanya kazi vizuri, ubunifu unaongezeka na unafanya biashara bila wasiwasi”, alisisitiza Dkt.Yonazi.
   Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi leseni ya usajili wa Gazeti la Daily News mwakilishi wa gazeti hilo Bi. Pudenciana Temba. Idara ya Habari imetoa imetoa leseni nne kwa ambapo leseni namba moja imetolewa kwa Jarida la Nchi Yetu linalotolewa na Idara hiyo, namba mbili imetolewa kwa HabariLeo, namba tatu Dailynews na nne imetolewa kwa Spotileo.Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Usajili Bw. Patrick Kipangula.
   Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi leseni ya usajili wa Gazeti la HabariLeo mwakilishi wa gazeti hilo mhariri wa gazeti hilo Bw. Amir Mhando leo Jijini Dar es Salaam. Leseni hiyo imetolewa kufuatia kuanza kwa matumizi ya sheria mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.
   Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimpongeza Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayomiliki magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo, Dkt. Jim Yonaz kwa Kampuni yake kuzingatia matakwa ya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016  kwa kujisajili upya na kupatiwa leseni.
  Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wahariri wa magazeti ya HabariLeo, DailyNews, SpotiLeo yanayomilikiwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) pamoja na uongozi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mara baada ya kukabidhiwa Lesini za usajili wa magzeti hayo leo Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Frank Shija - MAELEZO

older | 1 | .... | 1355 | 1356 | (Page 1357) | 1358 | 1359 | .... | 1898 | newer