Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

UKAID NA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAZINDUA PROGRAM YA MAFUNZO KWA WATUMISHI

$
0
0
Wafanyakazi watano wa Wizara ya Fedha na Mipango (Walioketi) waliopatiwa udhamini wa masomo nchini katika vyuo vikuu nchini Uingereza kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili uliotolewa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (UKAID-DFID), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa British Council-Tanzania ambao ndio waratibu wa Program hiyo ya miaka mitano, itakayogharimu Shilingi bilioni 3.6 kwa  lengo la kuongeza ujuzi na umahili wa rasilimali watu katika masuala ya uchumi, mipango, usimamizi wa fedha za Umma na Sheria za kimataifa. Kutoka kushoto Harieth Lubinga, John Kabiti, Susan Mbayuwayu, Peter Kalugwisha na Gloria Mduda.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiongea ofisini kwake na Mkurugenzi Mkazi wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo kutoka Serikali ya Uingereza (UKAID-DFID), Bi. Beth Arthy, kuhusu masuala mbalimbali ukiwemo ufadhili wa miaka mitano wa Taasisi hiyo wa masomo ya juu nchini Uingereza kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), wakielekea katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa ufadhili wa miaka mitano wa masomo ya juu kwa watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango, uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza wenye thamani za shilingi bilioni 3.6.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), Mkuu wa Shirika la Msaada la Uingereza (UKAID) nchini Tanzania Beth Arthy (wa pili kushoto) na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (kushoto) wakielekea katika uzinduzi wa program ya miaka mitano ya mafunzo ya mafunzo ya juu kwa ngazi ya Shahada ya Uzalimili kwenye vyuo vikuu nchini Uingereza kuhusu masuala ya uchumi, mipango, usimamizi wa fedha umma na sheria kwa baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango uliotolewa na Serikali ya Uingereza.
Mkurugenzi Mkazi wa British Council, Bi. Angela Hennelly, akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa mradi wa miaka mitano wa ufadhili wa masomo ya juu katika ngazi ya Shahada ya Uzamili kwa baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango kwenye vyuo vikuu mbalimbali nchini Uingereza kupitia Shirika la Maendeleo la UKAID-DFID utakaogharimu shilingi bilioni 3.6. British Council Tanzania ni waratibu wa mpango huo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) akizungumza katika uzinduzi wa program ya miaka mitano ya mafunzo kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la  UKAID-DFID, uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa program ya ufadhili wa masomo ya Juu katika vyuo vikuu nchini Uingereza kwa wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango katika ngazi ya shahada ya uzamili kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uingereza UKAID-DFID wenye thamani ya shilingi bilioni 3.6, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na viongozi waandamizi wa UKAID-DFID, British Council-Tanzania, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango walionufaika na ufadhili huo (kushoto) wakifurahia baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mpango wa miaka mitano wa ufadhili wa masomo kwa ngazi ya shahada ya uzamili katika vyuo vikuu vya nchini Uingereza katika Nyanja za uchumi, mipango, usimamizi wa fedha za umma na sheria za kimataifa uliotolewa na Serikali ya Uingereza kwa Wizara hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (UKAID-DFID), Bi. Beth Arthy (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa British Council, Bi. Angela Hennelly na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Serikali na Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango waliopata ufadhili wa Mafunzo kutoka UKAID-DFID, muda mfupi baada ya kuzindua rasmi program hiyo, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)​

Alikiba - Seduce Me (Official Music Video)

DIAMOND PLATNUMZ, HARMONIZE, RICH MAVOKO, RAYVANNY - ZILIPENDWA (OFFICIAL VIDEO)

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO AGOSTI 26,2017

MBUNGE RITTA KABATI APOKEA KERO ZA WENYEVITI WA MITAA 192 YA MANISPAA YA IRINGA

$
0
0
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza na wenyeviti wa mitaa yote ya manispaa ya Iringa wakati wa kusikiliza kero zinazowakabili viongozi hao wakati wa utendaji wao huko wenye mitaa yao. 
Hawa ni baadhi ya wenyeviti wa mitaa ya halmashauri ya manispaa ya Iringa waliohudhuria mkutano huo wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta kabati 



Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wenyeviti wa mitaa 192 katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wamelalamikia ufinyu wa posho wanayopata ukilinganisha na kazi wanazozifanya kuwatumikia wananchi kwa kuleta maendeleo.

Wakizungumza wakati wa mkutano mbunge wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wa kutoa kero zao na changamoto zinazowakabiri katika uwajibikaji wa majukumu yao huko mitaani.Wevyeviti hao walisema kuwa wamekuwa wakicheleweshewa posho zao toafauti na viongozi wengine na kuwasababisha kutofanya kazi kwa weledi wao unaotakiwa kwa kufikisha huduma stahiki.

Lakini wenyeviti hao walisema kuwa viongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamekuwa kero kwao kwa kutowasaidia kutatua changamoto na migogoro zilizopo kwenye mitaa hao.

"Huku mitaani watoto wadogo wanabakwa hovyo ukipeleka kesi polisi wanadai ushaidi haujakamilika na watuhumiwa wanakuwa nje kwa dhamana kitu kinachosababisha kudhohofisha utendaji wa kazi zao,mitaani kwenu kunawizi unaendelea lakini bado viongozi wa polisi wamekuwa kero kwa kutotatua kero hizo na swala jingine ni wenyeviti kudharauliwa na watumishi wa manispaa ya Iringa "walisema wenyeviti

Wenyeviti hao waliwataka viongozi wa Manispaa ya Iringa kutoa kwa haraka vibari vya ujenzi maana kumekuwa na ukilitimba mwingi kitu kinachosababisha ujenzi holela wa makazi kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa hivyo viongozi wanapaswa kuwa makini na mikakati madhubuti kwa kuwa wananchi wanataka kujenga nyumba zao.

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa Sweetbert Maro alisema kuwa kweli posho wanazopewa wenyeviti wa mitaa ni ndogo hivyo uongozi wa halmashauri ya manispaa imejipanga kukaa pamoja wenyeviti kujadili jinsi gani ya kuongea posho hizo kulingana na majukumu wanayoyafanya kuiwakilisha serikali.

"Mnafanya kazi kubwa mno lakini mnapewa posho kiduchu hivyo tutakaa na kulijadili hili swala kwa kina kwa kuwa bila wenyeviti wa mitaa halmashauri haiwezi kupata maendeleo na kukuza mji kwa nguvu zote hivyo tunawaomba wenyeviti muendelee kufanya kazi wakati swala la posho linashughulikiwa"alisema Maro

Maro alisema kuwa atamshauri Mkurugenzi kutafuta muda muafaka wa kukaa pamoja wenyeviti wote wa mitaa 192 ya halmashauri ya Manispaa ya Iringa ili kuzijua changamoto na jinsi gani ya kuzitatua maana leo hii mkutano huu ulikuwa wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati.

Aidha Maro aliwataka wenyeviti wa mitaa kuwabana maafisa watendaji wa mitaa maana uongozi wa halmashauri umekuwa ukitoa posho kwa wakati kulingana na agizo la serikali na kufuata sheria ya ugawaji wa posho kwa walinzi wa amani kwenye mitaa yako.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa kuna kero nyingine atazipeleka bungeni ili kuweza kupatiwa ufumbuzi zaidi na kuzitafutia njia za kuzitatua maana kwa ngazi ya Manispaa wameshindwa kuzitatua.

Kabati aliwaahidi wenyeviti wote wenye kero za ngazi ya manispaa atahakikisha zinatatuliwa kwa wakati lakini amewahakikishia kuwa ataitembelea mitaa yenye kero ambazo zipo kwenye uwezo wake atazitatulia huko huko kwenye mitaa.Wenyeviti hao walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa kuwakutanisha na viongozi wa halmashauri na kusikiliza kero zao kwa pamoja na kuzitafutia ufumbuzi ambao utaongeza tija ya kuleta maendeleo kwenye mitaa hao.

MBUNGE MUSSA NA MKEWE WASHIRIKI ZOEZI LA MSARAGAMBO WA MTARO KATA YA MAWENI JIJINI TANGA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akichukua sururu kwa ajiliu ya kushiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe hadi mtaani hapo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe
 Mke wa Mbunge wa Jimbo la Tanga nae akishiriki zoezi la Uchimbaji wa mtaro huo
 Mke wa Mbunge wa Jimbo la Tanga nae akishiriki zoezi la Uchimbaji wa mtaro huo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na wananchi wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea na kushiriki nao uchimbaji wa mtaro wa kupitishia maji
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (kushoto), akipokea kikombe (tuzo), kutoka kwa Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam Agosti 25, 2017.

 Wahandisi wanawake wa TANESCO walikabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais, baada ya kuibuka wa kwanza kwenye kongamano na maonesho linalowakutanisha wahandisi wanawake kutoka sekta mbalimbali hapa nchini lijulikanalo kama "Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition-TW=AWECE". Wahandisi hao walionesha umahiri mkubwa jinsi wanavyoweza kutumia teknolojia ya kisasa katika usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre) inayotumika kuboresha huduma.



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (pichani), amewataka Wahandisi Wanawake wa Shirika hilo, kutembelea mashuleni ili kuwahamasisha (Motivate), wanafunzi wa kike ili wapende kujisomea masomo ya sayansi na Hisabati na hatimaye baadaye waje kushika nafasi kama walizo nazo wao.

Dkt. Mwinuka ameyasema hayo makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, wakati akiwapongeza Wahandisi wanawake wa Shirika hilo, baada ya kupewa tuzo na Makamu nwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuibuka wakwanza kwenye Kongamano la Wahandisi wanawake Tanzania “Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition, (TAWECE), ambalo huenda sambamba na maonesho ya shughuli za kihandisi lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

“Niwapongeze sana kwa kuibuka washindi wa kwanza kwenye maonesho hayo, lakini niwaase, mpatapo nafasi mtembelee mashuleni ili muwahamasishe wanafunzi wasichana kupenda kusoma masomo ya sayansi na hisabati, na kwa kupitia kwenu, wanaweza kujitokeza wasichana wengi kupenda masomo hayo na hivyo baadaye kufanya kazi za kihandisi kama nyinyi.” Alisema Dkt. Mwinuka.

Dkt. Mwinuka alisema, tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Shirika kwani inajenga picha (image) nzuri mbele ya jamii kuonyesha juhudi zetu za kuwahudumia wateja wetu. Alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye hafla hiyo fupi, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, alisema Wahandisi wanawake kutoka TANESCO, walionyesha umahiri wao katika kuelezea teknolojia ya usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre), inayotumia kuboresha huduma wanazozitoa katika jamii.

“Lakini pia si hivyo tu, tulionyesha uboreshaji wa huduma tunazozitoa kwa wateja kwa kutumia teknolojia ya kisasa kupitia mfumo wa fiber ambao upitishaji taarifa mbalimbali kama vile mawasiliano na picha na hii inawezesha mfumo kuliona tatizo la mteja mara tu linapotokea na kuwezesha TANESCO kuchukua hatua haraka bila mteja kupata usumbufu.” Alisema Mhandisi Lutenganya.

Katika Kongamano hilo la mwaka huu lililofanyika Julai 28, (2017), kulikuwa na makundi matatu ya washiriki, ambayo ni shule za Sekondari, taasisi za elimu ya juu na mashirika ya umma ambapo waandaaji waliangalia uandaaji, uelewa wa washiriki pamoja na teknolojia ilivyotumika.

TANESCO ina wahandisi wanawake 55, na kuifanya taasisi ya kwanza nchini kuwa na idadi kubwa na wahandisi wanawake.

Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, alisema ni wajibu wa wanawake kujiamini katika utekelezaji wa majukumu yao na kuachana na dhana ya woga.

“Fanyeni kazi kwa bidii na maarifa, na niwaambie, utendaji kazi wako ndio utamvutia MD afikie uamuzi wa kukupandisha cheo na sio jambo linguine lolote lile, mimi nitastaafu hivi karibuni, ninawaeleza haya kwavile ninajua umuhimu wa kujituma katika kazi na kujiamini.” Alisema Mhandisi Ngahyoma.Alionyesha kufurahishwa kwake, na angependa idadi ya wanawake viongozi katika Shirika hilo inaongezeka na kufikia sio asilimia 50 tu bali asilimia 75.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akiwa na Dkt. Mwinuka wakati akionyesha tuzo hiyo. 
Dkt. Mwinuka, akiwapongeza baadhi ya wahandisi hao.
Dkt. Mwinuka akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake. 
Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, akizungumza.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Picha ya pamoja.

DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (kushoto), akipokea kikombe (tuzo), kutoka kwa Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam Agosti 25, 2017.

 Wahandisi wanawake wa TANESCO walikabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais, baada ya kuibuka wa kwanza kwenye kongamano na maonesho linalowakutanisha wahandisi wanawake kutoka sekta mbalimbali hapa nchini lijulikanalo kama "Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition-TW=AWECE". Wahandisi hao walionesha umahiri mkubwa jinsi wanavyoweza kutumia teknolojia ya kisasa katika usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre) inayotumika kuboresha huduma.



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (pichani), amewataka Wahandisi Wanawake wa Shirika hilo, kutembelea mashuleni ili kuwahamasisha (Motivate), wanafunzi wa kike ili wapende kujisomea masomo ya sayansi na Hisabati na hatimaye baadaye waje kushika nafasi kama walizo nazo wao.

Dkt. Mwinuka ameyasema hayo makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, wakati akiwapongeza Wahandisi wanawake wa Shirika hilo, baada ya kupewa tuzo na Makamu nwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuibuka wakwanza kwenye Kongamano la Wahandisi wanawake Tanzania “Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition, (TAWECE), ambalo huenda sambamba na maonesho ya shughuli za kihandisi lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

“Niwapongeze sana kwa kuibuka washindi wa kwanza kwenye maonesho hayo, lakini niwaase, mpatapo nafasi mtembelee mashuleni ili muwahamasishe wanafunzi wasichana kupenda kusoma masomo ya sayansi na hisabati, na kwa kupitia kwenu, wanaweza kujitokeza wasichana wengi kupenda masomo hayo na hivyo baadaye kufanya kazi za kihandisi kama nyinyi.” Alisema Dkt. Mwinuka.

Dkt. Mwinuka alisema, tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Shirika kwani inajenga picha (image) nzuri mbele ya jamii kuonyesha juhudi zetu za kuwahudumia wateja wetu. Alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye hafla hiyo fupi, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, alisema Wahandisi wanawake kutoka TANESCO, walionyesha umahiri wao katika kuelezea teknolojia ya usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre), inayotumia kuboresha huduma wanazozitoa katika jamii.

“Lakini pia si hivyo tu, tulionyesha uboreshaji wa huduma tunazozitoa kwa wateja kwa kutumia teknolojia ya kisasa kupitia mfumo wa fiber ambao upitishaji taarifa mbalimbali kama vile mawasiliano na picha na hii inawezesha mfumo kuliona tatizo la mteja mara tu linapotokea na kuwezesha TANESCO kuchukua hatua haraka bila mteja kupata usumbufu.” Alisema Mhandisi Lutenganya.

Katika Kongamano hilo la mwaka huu lililofanyika Julai 28, (2017), kulikuwa na makundi matatu ya washiriki, ambayo ni shule za Sekondari, taasisi za elimu ya juu na mashirika ya umma ambapo waandaaji waliangalia uandaaji, uelewa wa washiriki pamoja na teknolojia ilivyotumika.

TANESCO ina wahandisi wanawake 55, na kuifanya taasisi ya kwanza nchini kuwa na idadi kubwa na wahandisi wanawake.

Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, alisema ni wajibu wa wanawake kujiamini katika utekelezaji wa majukumu yao na kuachana na dhana ya woga.

“Fanyeni kazi kwa bidii na maarifa, na niwaambie, utendaji kazi wako ndio utamvutia MD afikie uamuzi wa kukupandisha cheo na sio jambo linguine lolote lile, mimi nitastaafu hivi karibuni, ninawaeleza haya kwavile ninajua umuhimu wa kujituma katika kazi na kujiamini.” Alisema Mhandisi Ngahyoma.Alionyesha kufurahishwa kwake, na angependa idadi ya wanawake viongozi katika Shirika hilo inaongezeka na kufikia sio asilimia 50 tu bali asilimia 75.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akiwa na Dkt. Mwinuka wakati akionyesha tuzo hiyo. 
Dkt. Mwinuka, akiwapongeza baadhi ya wahandisi hao.
Dkt. Mwinuka akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake. 
Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, akizungumza.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Picha ya pamoja.

STAND UNITED 'CHAMA LA WANA' YAPATA UDHAMINI WA MILIONI 100 KUTOKA KAMPUNI YA BIKO

$
0
0

Wakati pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2017-2018 likitarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Agosti 27, mwaka huu kwa timu zote 16 kuingia viwanjani,Kampuni ya Michezo ya Bahati Nasibu Mtandaoni – BIKO imeidhamini Klabu ya Stand United ‘Chama la Wana’ shilingi milioni 100 kuanzia mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Ijumaa,Agosti 25,2017mjini Shinyanga, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele (CCM) alisema BIKO wameamua kuidhamini timu hiyo baada ya kuridhishwa na mwenendo wa timu hiyo. 

“Baada ya Stand United kupoteza mwelekeo na wadhamini wake Kampuni ya Acacia kujiondoa katika udhamini,hivi sasa nimeamua kuwa msimamizi mkuu wa timu hii,nimetafuta udhamini mwingine,nimeiomba kampuni ya Kitanzania ya BIKO,imekubali kuwa wadhamini wakuu na imetupatia shilingi milioni 100 kwa mwaka huu”,alieleza Masele. 

Mbunge huyo alisema ameamua kuwa msimamizi mkuu wa timu hiyo ili kuhakikisha kuwa timu hiyo inafanya vyema katika michezo mbalimbali. 

“Najua mnaelewa uhusika wangu katika Stand United,mnafahamu jitihada nilizofanya kuhakikisha timu hii inafanya vizuri,ili timu hii iwe ya kimataifa na timu hii baada ya kupata matatizo yaliyotokea,ilikuwa kama timu yatima,haina ulezi,haina msaada,na mimi kama mbunge nilikuwa nimekasirika na nikasema Maeja na wenzake wasinisumbue katika mambo ya mpira”,alisema. 

“Nilitafuta ufadhili wa shilingi bilioni 2.4 kutoka Acacia,lakini tuliuchezea,na baada ya kujiridhisha na uongozi mpya ulioingia ukiongozwa na Dk. Maeja nimetafuta wadhamini wengine ambao ni kampuni ya BIKO ili kuisadia timu yetu,naomba fedha hizi zitumike vizuri”,alisema Masele. Masele alitumia fursa hiyo kuwatahadharisha viongozi wa timu kuhusu matumizi mabaya na ubadhirifu wa fedha zilizotolewa na wadhamini hao na kuwa hawatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

“BIKO itapenda kuona fedha hizi zinatumikaje na kuanzia sasa mtu yeyote atakayejihusisha na ubadhirifu tutamfikisha katika vyombo vya sheria kwa sababu wanaumiza hisia za watu wengi”,aliongeza Masele. 

“Nataka niwahikikishie kuwa timu hii haitashuka daraja kinatochotakiwa ni kutoa msaada kwa timu hii ikiwemo kuishangilia,jambo jingine naomba mjitahidi kubana matumizi katika masuala mbalimbali ikiwemo pale mnaposafiri punguzeni idadi ya watu wa kusafiri lakini pia lipeni mishahara ambayo haiumizi sana”,aliongeza.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United,Dkt. Ellyson Maeja alisema Klabu hiyo ya Stand United imejipanga vizuri kuhakikisha kuwa inafanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2017-2018. "Hivi sasa timu imetulia kiuongozi tatizo ni bajeti,mpira ni pesa,bila pesa hakuna timu,lakini pia hatuna usafiri wala hosteli kwa ajili ya wachezaji,tunaomba wadau waendelee kujitokeza kuisaidia timu hii,tumesajili wachezaji wapya 19,jumla sasa wapo 30,tunaye kocha mzuri,walimu wazuri,malengo yetu ni kushika nafasi ya kwanza hadi ya tatu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 2017-2018",alisema Dkt.Maeja.  Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza katika mkutano wa hadhara leo Mjini Shinyanga ambapo alisema kampuni ya BIKO imedhamini timu ya Stand United kwa kuipatia shilingi milioni 100.  Wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.  Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United,Dkt. Ellyson Maeja akielezea jinsi timu hiyo ilivyojipanga kufanya vizuri katika michezo mbalimbali huku akiomba wadau kuendelea kujitokeza kuisadia timu hiyo.




Dkt.Maeja akizungumzia masuala mbalimbali kuhusu Stand United.




Wananchi wakiwa katika mkutano huo.  Mheshimiwa Stephen Masele akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Dk. Maeja.







Diwani wa kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga,Hassan Mwendapolea akizungumza katika mkutano huo.







Wananchi wakiwa katika mkutano huo. Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Makamu wa Rais ahudhuria Kilele cha Miaka 50 ya NBC

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Bodi na Menejimenti ya NBC na Mabenki mengine kuwa kuanzia sasa Taasisi zote za fedha ziweke kipaumbele cha kwanza katika kuwezesha kuendeleza viwanda nchini hasa viwanda vidogo vidogo na vya kati vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu na madini ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini.Pia viwanda ambavyo vinatumia teknolojia ya kati na nguvu kazi zaidi ( labour intensive technology).
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akihutubua kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya NBC.

Mhe. Samia alisema mabenki mengi yameendelea kutoza riba ubwa hivyo kupelekea wananchi wa kipato cha chini hivyo aliwataka Wataalamu wa NBC na Sekta za Fedha kwa ujumla kutafuta suluhisho la riba zisizo rafiki kwa walio wengi ili amana pamoja na mikopo iweze kuongezeka.

Makamu wa Rais aliziagiza Bodi na Menejimeni ya NBC na Mabenki yote nchini kuzingatia Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha, alisema " Serikali ya Tanzania haitomuonea mtu haya na itachukua hatua kali dhidi ya benki au Taasisi yeyote itakayobainika kukiuka matakwa ya sheria hiyo."

Mwisho Makamu wa Rais aliipongeza benki ya NBC kwa kuweza kutoa gawio la Shilingi Bikioni 1.2 mwaka huu 2017 kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake.

KINANA AMWANDALIA BALOZI WA CHINA HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI KUMUAGA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkabidhi zawadi maalum Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing, wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam,jana Agosti 25, 2017. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, Naibu Spika Tulia Akson, Mabalozi kadhaa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Mawaziri Kadhaa, Makatibu wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Makatibu wa Jumuia za Chama. Picha zote na Bashir Nkoromo.
 Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana baada ya kupokea zawadi maluum, ambayo Kinana alimzawadia wakati wa chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza kabla ya kumkabidhi zawadi maalum Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing (kulia), wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, jana Agosti 25, 2017.
 Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing (kulia) akiifungua zawadi hiyo. 
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa hafla hiyo.
  Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing (kulia) akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing wakiinua glasi za vinwaji kabla ya kuzigonganisha kutakiana heri, wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam,jana Agosti 25, 2017. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge Tulia Akson. Picha zote na Bashir Nkoromo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akigonganisha glasi za viwanywaji na Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing kumtakia heri, wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, jana  Agosti 25, 2017. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge Tulia Akson. Picha zote na Bashir Nkoromo.
  Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing akigonganisha glasi za vinywaji na Spika wa Bunge Tulia Akson kutakiana her,  wakati wa hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kumuaga Balozi huyo, Upanga jijini Dar es Salaam, jana Agosti 25, 2017. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu wa Bunge
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akigonganisha glasi za kinywaji na Waziri Jenista Mhagama wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Balozi Lu na wapili kulia ni Naibu Spika Tulia Akson.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akigonganisha Glasi na Balozi wa Zambia hapa nchini Judith Kangoma-Kapijimpanga wakati wa hafla hiyo.
Katibu wa Jumuia ya wanawake Tanzania Amina Makilagi, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Idara ya Uchumi na Fedha Dk. Frank Hawassi na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka hamdu Shaka wakiwa na glasi za vinywaji vyao wakati wa hafla hiyo. KWA PICHA NYINGI ZA HAFLA HIYO/BOFYA HAPA

IGP SIRRO AFANYA ZIARA MKOANI MANYARA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (aliyesimama), akizungumza jambo mbele ya baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Manyara, wakati alipowasili katika mkoa huo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kujua changamoto wanazo kutana nazo wakati wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kulia), akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa Manyara, Joel Bendera (Kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Babati, Raymond Mushi, wakati alipowasili katika mkoa huo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima ya kijeshi wakati alipowasili mkoani Manyara, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto), akiwa ameongozana na kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, ACP Francis Jacob, wakati alipowasili mkoani Manyara, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.

BRIGEDIA JENERALI MBUNGU AWATAKA ASKARI WA SUMA JKT GUARD KUWA MABALOZI WAZURI WA MAPAMBANO YA RUSHWA MAKAZINI

$
0
0

 Askari wa ulinzi binafsi wa Suma Jkt Guard wakila kiapo cha uaminifu mbele ya  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu akizungumza na askari wa ulinzi binafsi wa kampuni ya Suma JKT wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya sita kwa askari wapya wa kampuni hiyo iliyopo chini ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT). na kuwaasa kuwa mabalozi wazuri katika mapambano ya rushwa katika kazi yao na hasa katika ofisi watakazopangiw akufanya kazi
 Mkurugenzi wa kampuni ya Ulinzi ya Suma Jkt Guard Limited, Meja Alfred Mwaijande akizungumza kabla ya kukamribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga mafunzo ya askari wa kundila sita wa Suma jkt
 Kaimu Mkuu wa chuo cha Uongozi JKT Kimbiji .Meja Josephat Songita akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya askari wa Suma Jkt Guard kundi la Sita
 Mkuu wa kitengo cha Operesheni na Mafunzo wa Suma Jkt Guard ,Luteni Albert Masawe akizunguma namna mafunzo hayo yalivyoendeshwa kwa mgeni rasmi
 Askari wa Jeshi la Kujenga taifa akipiga ngoma wakati akiongoza gwaride la askari wa Suma Jkt Guard
 Askari wa kundi la sita wanaomaliza  mafunzo ya ulinzi binafsi kundi lasita la Suma Jkt Guard wakipita kwa mwendo w aukakamavu
 Askari wa ulinzi binafsi wa Suma Jkt Guard wakionyesha umahiri wao wa kuchez amchezo wa Karate mbele ya mgeni rasmi  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu
 wakionyesha umahiri wao wa kuchez amchezo wa Karate mbele ya mgeni rasmi  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu
    Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu  akiwasili katika uwanja wa kufunga kozi
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu akiwa katika picha ya pamoja na askari wa ulinzi binafsi wanaomaliza mafunzo yao

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZZINDUA JUKWAA LA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI NA MFUMO MPYA WA HUDUMA ZA KIBENKI WA CRDB LEO JIJINI DAR

$
0
0
  Mgeni rasmi  Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan ( wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali na Viongozi waandamizi wa benki ya CRDB ,mara baada ya kuzindua  Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lililokwenda sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount,uliofanyika katika viwanja vya Posta-Kijitonyama mapema leo jijini Dar. 
  Mgeni rasmi  Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan ( wa pili kulia) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali na Viongozi waandamizi wa benki ya CRDB ,akizindua mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount,uliofanyika katika viwanja vya Posta-Kijitonyama mapema leo jijini Dar.  
  Mgeni rasmi  Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan  akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya kuzindua  Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lililokwenda sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount,uliofanyika katika viwanja vya Posta-Kijitonyama mapema leo jijini Dar. 
  Mgeni rasmi  Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount,uliofanyika katika viwanja vya Posta-Kijitonyama mapema leo jijini Dar. 
 Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB,Dkt Charles kimei akizungumza na kumshukuru Mgeni rasmi ,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,viongozi mbalimbali wa serikali na wageni waalikwa kwa ujumla,katika suala zima la kufanikisha uzinduzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi uliokwendaa sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount,katika viwanja vya Posta-Kijitonyama jijini Dar.
 Mgeni rasmi  Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan akisalimia na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB,Dkt Charles kimei alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Posta-Kijitonyama mapema leo kwenye hafla fupi ya kuzindua  jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi inayokwenda sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount. 
  Mgeni rasmi  Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan akisalimia na Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Posta-Kijitonyama mapema leo kwenye hafla fupi ya kuzindua  jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi inayokwenda sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount.
 Mgeni rasmi  Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan akisalimia na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Crdb, Ally Laay  alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Posta-Kijitonyama mapema leo kuzindua  jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi,Hafla hiyo inaenda sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount.
  Baadhi ya akina mama wakiserebuka kwa pamoja kwenye hafla fupi ya  uzinduzi wa jukwaa la kuwawezesha Wanawake kiuchumi, linalozinduliwa na Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan,katika viwanja vya Posta-Kijitonyama mapema leo jijin dar,Hafla hiyo inakwenda sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount
 Mgeni rasmi  Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan akipitia hotuba yake kabla ya kuisoma mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika katika viwanja vya Posta-Kijitonyama mapema leo kushuhudia hafla fupi ya uzinduzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi inayokwendaa sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount.Pichani kulia ni  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Waziri Jenista Mhagama na kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa jukwaa la Wanawake mkoa wa Dar,Mh Sophia Mjema pamoja na Naibu Spika wa Bunge Mhe.Dkt Tulia Ackson
 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Waziri Jenista Mhagama akimueleza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB,Dkt Charles kimei kabla ya uzinduzi wa  wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi inayokwendaa sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount,katika viwanja vya Posta-Kijitonyama jijini Dar
Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi wa  Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi inayokwenda sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount,katika viwanja vya Posta-Kijitonyama jijini Dar.
 Baadhi ya akina mama wakiserebuka kwenye hafla fupi ya  uzinduzi wa jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi iliokwenda sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount, linalozinduliwa na Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan,katika viwanja vya Posta-Kijitonyama jijin dar.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMAPILI LEO AGOSTI 27,2017


TUNAISHUKURU SERIKALI YA CUBA KWA KUTAMBUA MASHUJAA WA AFRIKA-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. kushoto , akiwa na mwenyeji wake kulia ambaye ni Mkurugenzi wa Maswala ya Africa Nnchini Cuba .Balozi Jose Prieta Cintado .August 25/2017 wakiangalia Sanamu ya aliyekuwa Raisi wa Msumbiji Hayati Samora Masheli ambayo ipo katika Makumbusho ya Mashujaa wa Africa yaliopo Havana Cuba Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu .
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .kulia pamoja na Mama Mary Majaliwa ,kushoto pamoja na mwenyeji wao katikati ambaye ni Mkurugenzi wa Maswala ya Africa Nnchini Cuba .Balozi Jose Prieta Cintado .wakiweka Shada la Maua August 25/2017 katika Makumbusho ya Mashujaa wa Africa yaliyopo Havana Cuba .Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

……………………………………………………………………

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameishukuru Serikali ya Cuba kwa kutambua na kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na mashujaa wa ukombozi wa Bara la Afrika, akiwemo Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kuwajengea mnara wa kumbukumbu.

Mnara huo umejengwa katika Manispaa ya Playa jijini Havana kwenye eneo maalumu la makumbusho ya mashujaa hao walioshiriki katika ukombozi wa Afrika, ambapo zimewekwa sanamu zao pamoja na maelezo mafupi ya historia zao na nchi wanazotoka.

Waziri Mkuu alifanya ziara katika eneo hilo jana (Ijumaa, Agosti 25, 2017) na kuweka shada la maua katika mnara huo uliozungukwa na sanamu za mashajuaa wa Bara la Afrika na kuoneshwa sehemu itakayowekwa sanamu ya Mwl. Nyerere.

Akiwa katika eneo hilo, Waziri Mkuu aliishukuru Serikali ya Cuba kwa kujenga makumbusho ya mashujaa hao na kwamba Serikali ya Tanzania itashirikiana na Cuba kuhakikisha kuwa sanamu ya Mwl. Nyerere inawekwa katika sehemu iliyotengwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Instuto Cubano De Amistad Con El Pueblo (Taasisi ya Ushirikiano wa Cuba na Nchi Marafiki), Bw. Jose’ Prieto Cintado alisema mnara huo umejengwa kwa lengo la kutambua thamani na umuhimu wa viongozi hao.

Mkurugenzi huyo alisema Serikali ya Cuba inathamini mchango mkubwa uliotolewa na mashujaa hao katika vita ya ukombozi wa Bara la Afrika, ambapo iliamua kujenga mnara wa kumbukumbu katika nchi yao.

Alisema wananchi wa Cuba pamoja na watu kutoka mataifa mbalimbali ndani na nje ya Bara la Afrika wanakwenda katika eneo hilo la makumbusho na kujifunza historia za viongozi hao. Pia eneo hilo linatumiwa na watafiti wa masuala ya kihistoria.

Mashujaa ambao tayari sanamu zao zimekwishawekwa kwenye eneo la kuzunguka mnara huo ni pamoja na Jomo Kenyatta (Rais wa kwanza wa Kenya), Modibo Keita (Rais wa Mali), Amilcar Cabral (Rais wa kwanza wa Guinea Bissau).

Wengine ni Dkt. Kwame Nkrumah (Rais wa kwanza Ghana), Oliver Thambo (Kiongozi Mwandamizi wa Chama cha Ukombozi cha ANC cha Afrika Kusini), Eduardo Chivambo Mondlane (Kiongozi wa ukombozi nchini Msumbuji).

Wengine ni Samora Moises Machel (Rais wa kwanza wa Msumbuji), Sekou Toure (Rais wa kwanza wa Senegal), Seretse Khama (Rais wa kwanza wa Botswana), Alhaji Aboubakar Tafawa Balewa na Obafemi Jeremiah Awolowo (Mawaziri Wakuu wa zamani wa Nigeria) na Chifu Jeremia Azikiwe (Rais wa zamani wa Nigeria) .

BODI YA CHAKULA DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR YAHARIBU BIDHAA MBOVU NA ZILIZOPITWA NA MUDA WAKE

$
0
0
Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar wakishusha bidhaa zilizoharika katika Dampo la Kibele tayari kwa kuangamizwa.
Moja ya gari lililobeba mchele ulioharibika likishushwa na Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar katika Dampo la Kibele Mkoa Kusini Unguja.
Gari la kijiko kutoka Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano likiangamiza mchele tani 27.5 ulioharibika katika Dampo la Kibele Mkoa Kusini Ungua.
Picha na Makame Mshenga.



Na Ramadhani Ali – Maelezo 

Wafanyabiashara wa Zanzibar wanaoagiza bidhaa kutoka nje wametakiwa kuwa waadilifu na kuwahurumia wananchi wenzao wakati wanaponunua bidhaa kwa kuangali ubora na kuacha tabia ya kuchukua bidhaa dhaifu zenye bei ndogo kwa lengo la kutafuta faida kubwa.

Mkuu wa Kitengo cha ufuatiliaji madhara ya chakula kutoka Bodi ya Madawa na Vipondozi Zanzibar Bibi Aisha Suleiman alitoa ushauri huo wakati bodi hiyo ilipofanya zoezi la kuangamiza tani 27.5 za mchele ulioharibika na chakula mchanganyiko kilo 400 kilichomaliza muda ikiwemo tende na juice katika Dampo la Kibele Mkoa Kusini Unguj.

Bi. Amina ambae alikuwa msimamizi mkuu katika zoezi hilo alisema mchele ulioharibika uliingizwa nchini na Kampuni ya Zenj General Machandise na uliingia maji wakati wa kusafirishwa na chakula kilichomaliza muda wa matumizi kiligundulika katika maduka mbali mbali ya Zanzibar baada ya kufanyika ukaguzi katika maduka hayo.

Alisema kwa mujibu wa sheria bidhaa zinapoharibika wakati wa kusafirishwa na ikagundulika wakati wa ukaguzi bandarini kabla ya kuingia sokoni mmiliki wa bidhaa hiyo huwa hanakosa na hulazimika kutoa gharama za kuangamiza bidhaa hiyo yeye mwenyewe.

Alisema Kampuni ya Zenj General Machandise ilikubali kutoa gharama ya kuangamiza mchele huo na kazi hiyo imefanyika chini ya usimamizi wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi.

Alikumbusha kwamba wananchi wanapotumia chakula kibovu kilichopitwa na wakati wanapata madhara makubwa ikiwemo maradhi hatari ya kensa ambayo matibabu yake yanagharama kubwa na yanapoteza maisha ya wananchi wengi.

Ameongeza kuwa athari ya kutumia chakula kibovu inaweza kuonekana katika kipindi kifupi tu baada ya kula lakini athari nyengine inaweza kuchukua miaka mingi kugundulika.

Hata hivyo amewashauri wananchi kwa upande wao kuwa waangalifu wakati wa kununua bidhaa za chakula na kuhakikisha kuwa bidhaa wanazochukua zinakuwa salama kwa matumizi ya binadamu.

PROFFESA MSAMBICHAKA ASISITIZA NIDHAMU KWA WANAFUNZI NA WALIMU ILI KUINUA ELIMU WAKATI AKIZINDUA KAMPENI YA 3D

$
0
0
WALIMU, Wanafunzi na Wafanyakazi katika shule mbalimbali wametakiwa kuzingatia nidhamu shuleni ili kuweza kuchochea maendeleo ya ufaulu kwenye shule zao.Wito ulitolewa jana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist iliyopo Boko Basihaya jijini Dar es Salaam, Aspiter Kibona wakati wa mahafali ya 10 ya kidato cha nne ya shule hiyo yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya '3D' yenye maana ya !Nidhamu, Nidhamu, Nidhamu!.

Kibona alisema wameamua kuzindua kampeni hiyo ikiwa ni kauli mbio yao kwa wanafunzi wa shule hiyo pamoja na walimu na wafanyakazi wengine kuzingatia nidhamu muda wote ambayo itaendelea kuchochea maendeleo ya ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
"Nidhamu si kwa wanafunzi pekee bali inatakiwa kuanzia hata kwangu mimi mkuu wa shule pamoja na walimu na wafanyakazi wengine katika shule yetu hii, hivyo tumezindua kampeni hii ikiwa ni kauli mbio yetu ya kuendelea kuhamasisha nidhamu katika shule yetu kwa nia kuendelea kuchochea maendeleo ya wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao darasani, " alisema Kibona.
Alisema nidhamu inapoanzia kwa viongozi wa juu, walimu na wafanyakazi wengine inasaidia nidhamu hiyo hiyo kuingia hadi kwa wanafunzi ambayo inawachochea kufanya vizuri katika masomo yao darasani.

Naye Mkurugenzi wa shule hiyo, Jalia Mayanja aliwataka wahimu 53 wa kidato cha nne kuzingatia nidhamu mahali popote watakapokuwa mara baada ya kutoka shuleni hapo kwa faida yao ya huko waendako.

Mayanja alisema nidhamu ndiyo siri ya mafanikio ya shule hiyo katika ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.Alisema ni vema wahitimu hao wa kidato cha nne wakaendeleza nidhamu waliyokuwa wakiionyesha shuleni hapo huko wanapokwenda ili iweze kuwasaidia katika maisha yao ya baadae.Aliongeza kwa kuwataka wazazi wanaopeleka watoto wao katika shule hiyo kukaa kwa amani kutokana na kwamba wapo katika mikono salama.

SIMBACHAWENE AAGIZA BARABARA YA LUMUMA-MBUGA MPWAPWA ITENGENEZWE KWA KIWANGO KINACHOTAKIWA.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George B. Simbachawene (Mb) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Geophrey Mwamkinga na Wataalam wengine juu ya marekebisho ya barabara ya Lumuma hadi Mbuga yenye urefu wa kilomita 21 ambapo alimtaka kuchukua hatua kwa mkandarasi kampuni ya M/S Besta Holding Co Ltd ya Jijini Dar es Salaam kufanya marekebisho ya upanuzi wa barabara, kumwaga kifusi kisicho tereza, kujenga kingo imara za barabara na marekebisho maalum sehemu korofi kabla ya msimu wa mvua.

………………………………………………………………………..

Na Fred Kibano, Mpwapwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George B. Simbachawene (Mb) amemwagiza Msimamizi wa Wakala wa barabara za Vijijini (TARURA) Mhandisi Geophrey Mwamkinga kuhakikisha barabara ya Lumuma hadi Mbuga wilayani Mpwapwa inatengenezwa kwa kiwango kinachotakiwa na kwa thamani halisi ya fedha za Serikali.

Mheshimiwa Simbachawene ameyasema hayo akiwa katika ziara ya kutembelea Mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya vijiji kujionea maendeleo ya vijiji katika sekta za Afya, Elimu, Maji, Ardhi na eneo la Utawala bora ngazi ya vijiji.

Amesema Mkandarasi anayejenga barabara hiyo kampuni ya M/S Besta Holding Co Ltd ya Jijini Dar es Salaam bado haijafanya kazi nzuri ijapokuwa ujenzi wake umefikia asilimia 70 kwani wembamba wa barabara hiyo ambao hauruhusu magari kupishana, kuwa na mitaro midogo ya kutupa maji, uvunjaji wa miamba kwa mita chache pembeni mwa barabara hiyo ya milima ya Kizi haujafanyika ipasavyo, ikiwa ni pamoja na mitaro ya kinga mita kwa pembeni na kujaza kifusi ambacho hakitelezi.

“Kwa hiyo, barabara lazima itanuliwe, mlima huu hapa hakati, huyu jamaa (Mkandarasi), anagusagusa tu lakini hakati, Yule mwenzake wa kule Wotta (kata nyingine wilayani Mpwapwa) anakata, tena ni jiwe tu kutoka chini, yeye huyu ni udongo anafanya hivi, lakini hakati (mlima kwa upande wa pembeni), hivi vifereji ni utapeli mtupu, hivi vifereji wakati wa mvua vitaondoka vyote kwa sababu hujaandaa vizuri njia yenyewe, ukijenga mfereji unacheza (ni kama utani)”

Barabara ya kata za Lumuma na Mbuga yenye urefu wa kilomita 21 inahusisha matengenenezo makubwa, ni barabara ya siku nyingi ambayo haikuwahi kuwa chini ya Halmashauri ambapo ni wananchi pekee na Wamisionari wa Kanisa katoliki ndio walioianzisha na kuikarabati kuweza kupita kwa shughuli zao.

Mradi huo mkubwa wa ukarabati wa barabara ulianza mapema mwezi Februari, 2017 na kutarajiwa kwisha katikati ya mwezi Agosti, 2017 na jumla ya gharama zitakazotumika ni shilingi 641,912,684 na mpaka sasa amekwishalipwa asilimia 33 ya fedha zote.

Kwa mujibu wa Bw. Mwamkinga mpaka sasa mkandarasi huyo amekwishalipwa kiasi cha shilingi 209,175,882 na bado shilingi 432,736,802. Pia mkandarasi ameongezewa muda wa siku 60 kutokana na changamoto za kijiografia zinazosababisha vifaa kutofika kwa wakati na kufanya ufuatiliaji kwa kuweka vikao kazi kwa kila wiki kuona maendeleo na ubora wa kazi na kutoruhusu ucheleweshaji mwingine wa kazi kabla ya msimu ujao wa mvua.

Mheshimiwa Simbachawene anafanya ziara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hasa maeneo ya vijijini ili kujionea hali halisi ya utendaji, migogoro ya ardhi, utunzaji wa mazingira, huduma kwa wananchi na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo ambapo mwishoni mwa wiki ametembelea kata za Mbuga, Kibakwe na Ipera zenye vijiji kadhaa wilayani Mpwapwa kama sehemu ya kazi zake za kujionea maendeleo ya wananchi na kero zao.

TAARIFA KWA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA: WALE WOTE WENYE MATATIZO YA ARDHI MKUU WA MKOA ATAFANYA MKUTANO NANYI AGOSTI 29, 2107 KATIKA UKUMBI WA OFISI YA JIJI ARUSHA

Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images