Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1350 | 1351 | (Page 1352) | 1353 | 1354 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Filbert Rweyemamu,Arusha

  Benki ya Dunia imetoa Sh 200 Milioni ili kuwezesha miradi ya elimu na ujuzi kwa ajili ya kazi zinazoleta uzalishaji wenye tija pamoja na vituo viwili vya umahiri vya kikanda vitakavyofungua ajira kwa vijana mara baada ya kuhitimu elimu. 

  Akizungumza katika uzinduzi wa miradi hiyo,Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa miradi hiyo itasaidia kuongeza watu wenye ujuzi wa kati ambao watafanya kazi katika sekta za kilimo,utalii,ujenzi ,nishati na madini.

  Alisema kuwa miradi iliyofadhiliwa ni pamoja na vituo vinne vya umahiri katika masuala ya utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pia ipo miwili iliyochini ya taasisi ya Chuo Kikuu ya Nelson Mandela pamoja na vituo vingine viwili vilivyopo katika Chuo cha Kilimo cha Sokoine(Sua).

  Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Malawi ,Burundi na Somalia, Bella Birds alisema kuwa uboreshwaji wa rasilimali watu kwa kuongeza ujuzi uliokosekana utasaidia taifa kufikia malengo yake ya kufikia uchumi wa viwanda.

  Bella alisema inakadiriwa kuwa vijana milioni 1 huitimu katika vyuo na kuingia katika soko la ajira kila mwaka hivyo anatarajia kuwa nafasi za ajira kwa vijana hao zitatengenezwa na sekta binafsi iwapo zitashirikiana vyema na serikali .

  Makamu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Karoli Njau alisema kuwa mradi huo utasimamiwa kwa makini ili kuhakikisha kuwa malengo yanafikiwa hususan katika vituo vya umahiri pamoja na mradi wa ujuzi.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye amesema kuwa kulikua na upungufu mkubwa wa watu wenye ujuzi nchini kutokukidhi mahitaji ya soko la ajira hivyo kulazimu waajiri kuajiri watu kutoka nje jambo linalogharimu fedha nyingi hivyo mradi huo utasaidia vijana 30,000 kupata ujuzi utakaokidhi mahitaji ya soko la ajira.
  Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(wa pili kushoto) akiwasili katika taasisi ya Chuo cha Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela(NM-AIST) kuzindua mradi wa Vituo vya umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pamoja na mradi wa kuongeza ujuzi kwa kazi za uzalishaji zinazoleta tija uliofadhiliwa na Benki ya Dunia,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NM-AIST,Profesa David Mwakyusa na Makamu Mkuu wa taasisi hiyo,Profesa Karoli Njau .
  Waziri wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (wa pili kulia) akipata maelekezo juu ya utendaji wa Kituo hicho 
  Waziri wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akizindua mradi wa Vituo vya Umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Malawi ,Burundi na Somalia Bella Bird.

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa sambamba na mkuu wa mkoa wa iringa wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la chanzo cha mradi huu wa maji katika mji mdogo waIlula
   Mkuu wa mkoa wa iringa Amina masenza akifurahia kufika kwenye chanzo cha maji pamoja na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kwa kuwa wanajua hilo ndio litakuwa suluhisho la mda mrefu kwa wakazi wa mji mdogo wa Ilula
  viongozi wa kamati ya siasa ya mkoa wa iringa wakiwa wanaelekea kwenye chanzo cha maji kwa ajili ya kujua jinsi gani kitaweza kutatua kero za wananchi wa mji wa mafinga
   mjumbewa kamati ya siasa ya mkoa wa iringa ndugu mosha akiwa njiani kuelekea kukikagua chanzo hicho cha maji
   katibu msaidizi wa chama cha mapinduzi mkoani iringa akiwa sambasamba na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdalla wakielekea kukagua chanzo kipya cha maji kwa ajili ya wananchi wa mji mdogo wa mafinga


  Na Fredy Mgunda,Iringa

  Halmashauri ya wilaya ya kilolo inatarajia kutatua kero ya maji iliyodumu kwa miaka mingi katika mji mdogo wa Ilula mkoani Iringa kwa kutenga kiasi cha dola za kimarekani 9,548,827 kwa ajili ya kujenga chanzo kipya cha maji yatakayo weza kutatua changamoto hiyo.

  Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekeleza wa ilani ya chama cha mapinduzi  wilayani kilolo mkuu wa mkoa wa iringa ambaye ndio mwenyekiti wa kamati ya siasa ya mkoa bi Amina Masenza alisema kuwa wameamua kutafuta chanzo kipya ili kutatua tatizo la maji katika mji mdogo wa Ilula.

  “Leo nimefika hadi huku kwenye chanzo cha maji ambacho naamini kuwa kitafanikiwa kutatua kero ya muda mrefu kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula hivyo lazima waisimamie ipasavyo ilani ya chama na kuhakikisha kuwa wanatatua  matatizo ya wananchi”alisema Masenza

  Aidha Masenza alisema kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kumuunga mkono rais wa jamhuri ya muuungano wa Tanzania dr John Pombe Maguli kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

  Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alivitaja baadhi ya vyanzo ya maji na uwezo wa uzalishaji ambavyo vinatoa huduma kwa mji mdogo wa Ilula ni Ilomba kutoka kijiji cha Imalutwa na Idemule kutoka kijiji cha Mazombe kwa ujumla vinazalisha wastani wa uzalishaji wa maji wa mita za ujazo 1,142 kwa siku.

  Abdallah alisema kuwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula unamahitaji makubwa ya matumizi ya maji ambapo kwa siku wanahitaji maji ya mita za ujazo 2687 kwa siku hivyo hadi sasa kunaupungufu wa mita za ujazo 1545 kwa siku.

  “Mji huu unakuwa kwa kasi kubwa hivyo matumizi ya maji yamekuwa makubwa mno ndio maana tumeanza  kujenga chanzo kingine ambacho kitakuwa na suluhisho kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula na kutaua kabisa tatizo la maji” alisema Abdallah 

  Abdallah aliwataka wananchi na viongozi wa ngazi zote kuacha tabia ya kuharibu vyazo vya maji na mazingira kwa ujumla hivyo atakaye kamatwa anafanya uhalibifu wowote ule sheria itachukua mkondo wake.

  “Ni malufuku kwa wakulima kulima kwenye vyanzo vya maji,wafugaji kufujia mifugo kwenye vyanzo vya maji pamoja na ukaji wa miti hovyo hapo nitakuwa mkali sana kwa watu ambao watakiuka haya nayoyasema hii leo kwa kuwa kila kitu kipo kisheria “ alisema Abdallah

  Naye meneja wa mamlaka ya maji wa mji mdogo wa Ilula Enock Ngoyinde aliiomba serikali ya na kamati ya siasa ya mkoa wa iringa kusaidia upatikanaji wa pesa kwa wakati za kumaliza mradi huu wa maji ili wananchi waanze kupata huduma bora mapema iwezekanavyo.

  Ngoyinde alisema kuwa mradi huo ukikamilika utakuwa umeongeza eneo la utoaji wa huduma vya maji kutoka wastani wa asilimia 62 hadi asilimia 75 na kuwahudumia wananchi zaidi ya elfu ishirini na tano (25000) ambao watakuwa na mtandao wa bomba za maji.

  0 0

   

  0 0


  Na Mathias Canal, Zanzibar

  Kongamano lilodumu kwa siku mbili kwa kuwakutanisha watanzania waishio Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) limehitimishwa hii leo Agosti 24, 2017 huku likiwa limehudhuriwa na Diaspora 350 na kuchagizwa na wahudhuriaji wengine ambao ni watendaji kutoka taasisi za serikali na wadau katika uwekezaji na uchumi.

  Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) lilifunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan ambapo limefikia ukomo kwa kupatikana majibu ya changamoto mbalimbali ziwahusuzo Diaspora ikiwemo uraia pacha na sera ya utambuzi wao nchini Tanzania.

  Akihutubia mamia ya watanzania walioshiriki katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd alisema kuwa serikali inawatambua Diaspora kama mabalozi muhimu katika kutangaza utalii Duniani kote jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaongeza kipato cha nchi.

  Alisema kuwa serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Diaspora katika kuitangaza nchi ya Tanzania na vivutio vyake hivyo kuwataka kutumia fursa hiyo pia kuwatangaza viongozi wa serikali kwa weledi mpana pasipo kueneza chuki dhidi ya viongozi wao.

  Mhe alozi Seif alisema kuwa kumekuwa na watanzania waishio nje ya nchi wasiokuwa na weledi na nidhamu dhidi ya viongozi wa serikali kwani wamekuwa wakiwasema vibaya kwa kuwatukana na kejeli jambo ambalo linarudisha nyuma heshima yao waliyonayo na kutia doa serikali.

  Alisema kuwa Diaspora wanapaswa kuendelea kushiriki katika makongamano mengine yajayo kwani kufanya hivyoi kunatoa fursa kwao kuishauri serikali na kuona namna bora ya utambuzi wao.

  Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili Diaspora waweze kutumia fursa ya uwekezaji nchini kwa urahisi huku akiwasihi kutumia fursa muhimu za uwekezaji katika Nyanja zote kwani faida itakuwa kwa Diaspora wenyewe, watanzania waishio nchini na Taifa kwa ujumla wake.

  Alisema kuwa ushirikiano huo wa Diaspora kupitia makongamano yote yaliyopita umeimarisha zaidi mahusiano chanya bila kujali dini wala kabila jambo ambalo limeongeza utu, umoja na mshikamano.

  Mhe alozi Seif alisema kuwa Diaspora wanatakiwa kuheshimu sheria, taratibu na taratibu za nchi wanazoishi ili kue delea kuipatia sifa chanya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  “Naomba nikukumbusheni nyote mliohudhuria hapa hii leo kutamnbua kuwa mchumia juani hulia kivulini nanyi kivulini kwenu ni hapa nyumbani hivyo tumie fursa ya uwekezaji vizuri huku mkikumbuka kuwa mkataa kwao ni mtumwa zaidi endelezeni umoja na mshikamano kwani inafahamika kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.” Alisema Balozi Seif Ally Idd

  Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) linaratibiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusudio la kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna ya kutumia fursa za uwekezaji.

  Kongamano kama hilo linaakisi makongamano matatu ya utangulizi yaliyofanyika mwaka 2014 na 2015 Jijini Dar es Salam huku kongamano la mwaka 2016 na mwaka huu 2017 yakifanyika visiwani Zanzibar huku likiwa limebebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao”

  Kongamano la watanzania waishio ughaibuni kwa mwaka 2017 limedhaminiwa na PBZ Bank, ZSSF, Idara ya Uhamiaji, Sea Cliff Hotel, CRDB Bank, Mult Colour, Equity Bank, Zanzibar Cable Television, ZBS, Watumishi Housing Cooparation na Petro.
  Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy akihutubia wakati wa kufungaKongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara. (Picha zote na Mathias Canal)
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe Issa Haji Gavu akitoa salamu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.
  Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia hotuba ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddykatika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.
  Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy (Kushoto) akifatilia burudani mbalimbali wakati wa kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara, Mwingine ni Balozi Anisa Mbega Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.

  Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy akihutubia wakati wa kufungaKongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.

  TAZAMA PICHA ZAIDI  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,kushoto akikabidhi Jarida lakutangaza Utalii wa Tanzania Kwa Kiongozi wa maswala ya Utalii katika Mkoa wa Matanzas .Bwana Luis Marines ,jana August 23/2017 wakati alipokuwa katika Ziara ya kikazi kwenye Mji wa Varadero Mkoa wa Matanzas Nchini Cuba, katikati katika picha ni Mama Mary Majaliwa
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (mwenye miwani)na Mama Mary Majaliwa (kulia) .pamoja na Ujumbe wa Serekali ya Tanzania wakipata maelezo jana August 23/2017kutoka kwa Kiongozi wa Utalii katika Mkoa wa Matanzas ,Bwana Luis Martines. jinsi fukwe za Bahari zinavyo tunzwa nakuwa kivutio kwa Watalii wanao tembelea Mji wa Varadero Mkoa wa Matanzas Nnchini Cuba
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (mwenye shati jeupe) na Mama Mary Majaliwa (kushoto)pamoja na ujumbe wa serekali ya Tanzania jana August23/2017. wakipata maelezo kutoka kwa muongoza wa Talii Bibi Yanseli Marrero kuhusu biashara ya Boti za Utalii kwenye fukwe za Bahari katika Mji wa Varadero Mkoa wa Matanzas Nnchini Cuba

  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Waziri wa michezo nchini Tanzania Mh.Dk Harrison Mwakyembe amewatakia safari njema watoto waliochaguliwa na kampuni ya Tecno mobile kwenda kufanya majaribio ya kucheza mpira wa miguu katika academy ya klabu ya Manchester City nchiniUingereza.
  Malimi Majaliwa wa kwanza kushoto na Daudi DAmasi wakiwa katika picha ya pamoja baada yakupewa Baraka za safari na Mh. Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe)

  Akiongea katika hafla hiyo fupi kutambulisha mbele ya waziri mpango huo, Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Tecno Mobile Bwana, Eric Mkomoya alisema kua kampuni ya Tecno Mobile ndio wadhamini pekee wa safari hiyo kupitia simu yao mpya Tecno Camon Cxto leo maalumu la machester city ambapo watoto hao wawili wataenda kupewa mafunzo yenye kiwango cha kimataifa lakin pia endapo watafanya vizuri wanaweza kuchaguliwa kuendelea kucheza katika klabu hiyo. ,(wadhamini wa kuuwa safari

  (Wazazi na walezi wa vijana wanaokwenda Manchester city wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa kuu kutokea Tecno Mobile.)

  Alisemaa . ”Tumefurahi kukutana na serikali hasa Waziri wa michezo na kuamua kuwapa Baraka zake vijana wetu wanaokwenda huko wataondoka usiku wa tarhe 23 na kurudi tarehe 30 mwezi wa nane”.

  Akikaribishwa na mkurugenzi wa michezo, waziri wa michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema kua serikali ina furaha kuona wadau wanajitokeza kukuza vipaji nchini Tanzania, hasa kwa watoto wanao chipukia.

  Dk Harrison Mwekyembe pia amesema “niwaombewa dau katika sekta ya michezo tushirikiane katika kukuza michezo, na washukuru kampuni ya Tecno Mobile kwa kuonesha juhudi za wazi katika kufanikisha hili, serikali pia inafanya jitihada kwa nafasi kuhakikisha viwango vya soka na michezo kwa ujumla vinakua.”alimaliza.)

  Mzazi wa mtoto mmoja wapo Malimi, Majliwa Mbasa amesema anafuraha kuona kijana wake amepata nafasi hiyo anaamini atafanya vizuri liafungue milango kwa vijana wengine wadogo wa kitanzania walioko nchini waweze kwenda kucheza soka la kulipwa nchini uingereza.

  Watoto wawilli Daudi Damasi pamoja na Malimi Majaliwa wanaocheza nafasi ya kipa na ushambuliaji wamepata nafasi hizo kutokana na ushirikiano wa Tecno Mobile naasasi ya michezo ya Magnet, watoto hao ambao wote wana miaka kumi na mbili wataondoka kuelekea manchster city mnamo tarehe 23 mwezi wa nane na kurudi nchini tarehe 30.

  Msafara huo utaongozwa na wazazi na walezi wa watoto hao akiwemo kocha mwenye utalaamu wa kulea vipaji vya vijana kocha Juma Maswanya. Tecno mobile ndio wadhamini wakuu wa safari hii wanajumuisha vijana kutoka nchi za afrika ambako kampuni hii inapofanyakazi hivyo Nigeria, misri ,Tanzania, Ghana pamojana Kenya.
  Afisa Mahusiano wa Tecno Mobile Eric Mkomoya wa kwanza kushoto, meneja Masoko Franck Luo, wa kwanza kulia)
  aziriwaHabari, Utamaduni, Utalii na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na watoto wawili Daudi Damasi na Malimi Majaliwa wanaokwenda kufanya Majaribio,

  0 0

   
  Katika kile kinachoonekana kutekeleza dhana ya ‘hapa kazi tu’, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akipanda juu ya tanki kuchungulia maji katika vyanzo vya maji kijiji cha Mwankoko Manispaa ya Singida.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akiambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina M Lutambi(katikati) na Mhandisi wa maji SUWASA Robert Sunday (kushoto), wakikangua vyanzo vya maji kijiji cha Mwankoko Mnispaa ya Singida.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo (wa pili kulia) akipewa ufafanuzi wa mashine ya kupampu maji katika chanzo cha maji cha kijiji cha Mwankoko Manispaa ya Singida na Mhandisi wa SUWASA Patrick Nzamba
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na watumishi watumishi wa Mamlaka ya SUWASA, bonde la maji la kati na maabara mjini hapa. Wa kwanza kulia ni Mhandisi SUWASA, Patrick Nzamba.
  Mhaidrolojia bonde la maji la kati Robert Sunday akichangia hoja kwenye mkutano ulioitishwa kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kuzungumza na watumishi wa SUWASA, bonde la maji kati na maabara.

  ……………………………………

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amezihimiza mamlaka za maji na mabonde ya maji kubuni vyanzo vipya vya mapato vitakavyosaidia kujiendesha vyenyewe bila kutegemea serikali kuu.

  Profesa Mkumbo ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa mamlaka ya maji Singida (SUWASA), Bonde la maji kanda ya kati na maabara, mjini hapa mjini .

  Amesema Serikali haina fedha za kukidhi mahitaji yote ya mamlaka za maji na mabonde nchini hivyo ni vema vikaweka mikakati ya kujitengemea kimapato.

  “Duniani kote hata Marekani haitoi fedha kwa taasisi kama hizi zenu. Tumieni kalamu na akili zenu kwa ajili ya kuandika maandiko yatakayowasaidia kupata fedha za kujiendesha bila kutegemea serikali au wafadhili”, amesisitiza.

  Akisisitiza zaidi, kwa kusema umefika wakati sasa mamlaka na mabonde ya maji, zifikirie kuwekeza na kujiwekea mipango thabiti ya kuongeza mapato yao.

  Aidha, Katibu Mkuu huyo amewataka watumishi wa SUWASA, kutoa huduma bora itakayovutia wananchi wengi zaidi kupata huduma ya maji katika mamlaka hiyo.

  “Wateja wa maji ndio wanaowalipa ninyi mishahara na stahiki zingine. SUWASA ikiwa na wateja wachache kwa vyo vyote uendeshaji wake utakuwa mgumu na hivyo hivyo upatikanaji wa mishahara yenu nao utakuwa mgumu”, amesema Profesa Mkumbo.

  Ameongeza kuwa SUWASA na mamlaka nyingine za maji nchini ni lazima ziwe na mkakati wa kupanua wigo wa wateja.

  “Utamaduni wa kutoa huduma bora unamfurahisha mteja na atapenda kuendelea kuwa mteja wa SUWASA wakati wote. Pia itawavutia watu wengi kukimbilia huduma bora zinazotolewa na SUWASA”,alisema.

  Katika hatua nyingine, Profesa Mkumbo ametumia nafasi hiyo kusisitiza utaratibu wa kulipia kwanza (pree paid) maji kabla ya kupata huduma ya maji.

  Amesema utaratibu huo utasaidia kuepukana na wateja wakorofi ambao huzalisha madeni sugu na kusababisha mamlaka kushindwa kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja.

  “Kupitia utaratibu huu mteja husika ni lazima ajue matumizi yake ya maji kwa kipindi cha mwezi. Baada ya hapo analipia kiwango hicho cha maji halafu ndipo apewe maji ya kiwango alicholipia”, amesema katibu mkuu huyo.

  Awali Afisa Maji bonde la kati Benard Chikarabhani amesema wameanza utekelezaji wa ujenzi wa bwawa la Farkwa kwa lengo la kuongeza usambazaji wa maji katika mji wa Dodoma, Bahi, Chamwino na halmashauri ya wilaya Chemba.

  “Bwawa hilo linatarajiwa kuwa na kiasi cha maji cha mita za ujazo 470,000,000 na litachukua eneo la kilometa za mraba 68 pia bwawa litatumika kuboresha kilimo cha umwangiliaji katika mradi wa umwangilaji Bahi”, amesema Chikarabhani.

  Wakati huo huo, Chikarabhani amesema bodi ya maji bonde la kati inatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 2.4 kugharamia ujenzi wa ofisi makao makuu mjini hapa.

  “Fedha hizo zitagharamia pia ukarabati wa ofisi na maabara katika ofisi ndogo ya bodi zilizopo mkoani Shinyanga. Vile vile ujenzi wa ofisi ya jumuiya ya watumijai maji ya Mto wa Mbu”, amesema afisa huyo.

  0 0

  Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
  Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea kuona Ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Maji Lamadi itakayosimamia mradi wa maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali .
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kutembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya wakati alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) (wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Busega mara baada ya kutembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali, (kushoto) Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe.Tano Mwera.
  Msajili Msaidizi wa Baraza la Ardhi Kanda ya Ziwa, Dorothy Moses akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi hao Wilayani Busega(hawapo pichani).


  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), ameziagiza Halmashauri nchini, kuyatambua na kuyatolea taarifa maeneo yanayohodhiwa na watu bila kuendelezwa na yale ambayo hayakupatikana kihalali ili Wizara iweze kuchukua hatua stahiki.

  Naibu Waziri huyo ameyasema hayo alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali, kisha Halmashauri ya Busega Mkoani Simiyu kuanza ujenzi wa mradi wa maji katika eneo hilo utakaonufaisha vijiji vinne vya kata ya Lamadi.

  Mhe.Mabula amesema Halmashauri zinapaswa kutambua maeneo yasiyoendelezwa na yanayomilikiwa kinyume cha sheria na kuwasilisha taarifa katika Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili yaweze kuyarejesha kwa wananchi na kupangiwa matumizi mengine yenye manufaa zaidi kwa jamii.

  “Maeneo yote yaliyohodhiwa ambayo hayajaendelezwa na ambayo pengine hayakupatikana kihalali, ni jukumu la Halmashauri kuyatambua na kuleta taarifa zake Wizarani ili Wizara iweze kuchukua hatua ya kuweza kuyarudisha katika matumizi kwa Umma na yaweze kufaidisha watu wengi zaidi badala ya mtu mmoja” amesema Naibu Waziri Angelina Mabula

  Aidha,Naibu Waziri Mabula amebainisha sababu zilizopelekea Mwekezaji Hermati Pateli kufutiwa hati ya eneo hilo na Serikali kuwa ni udanganyifu wa Uraia pamoja na upatikanaji wa hati ambao haukuzingatia sheria na taratibu za nchi.

  Naibu Waziri huyo amesema eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji huyo isivyo halali ambalo limefutiwa hati miliki limegawanyika katika ploti mbili, ploti Namba 01 na Namba 02 Block C lenye ukubwa wa hekta 7.62 na Block Namba 03 C hekta 5.45.

  Akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Maji wa Lamadi kutoka Kampuni ya EAU Consult, Baraka Felix amesema Tanki la Maji litakalojengwa katika eneo hilo litakuwa na uwezo wa kuzalisha mita za ujazo 3000 kwa siku.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya amesema Mradi wa Maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo hilo utawanufaisha wananchi wa Vijiji Vinne vya Kalago, Lamadi, Lukungu na Mwabayanda.

  Mradi huu wa maji unaojengwa katika eneo hili lililokuwa linamilikiwa isivyo halali na Mwekezaji Pateli, utagharimu kiasi cha Yuro milioni 2.8, na unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei, 2019.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kulia) akiwasilisha mada katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Wajumbe hao walikutana Makao Makuu ya Ofisi za Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujenga mtandao na ushirikiano. Katika mada yake kwa washiriki wa mkutano huo, Bi. Bussemaker alielezea benki ya NMB ilivyo na fursa mbalimbali kwa makundi tofauti na hasa inavyowasaidia wafanyabiashara kupitia bidhaa yake ya Trade Finance. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kushoto) akimkaribisha mmoja wa washiriki katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Sehemu ya washiriki katika mkutano ulioandaliwa na Benki ya NMB na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Wajumbe hao walikutana Makao Makuu ya Ofisi za Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujenga mtandao na ushirikiano. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kulia) akiwasilisha mada katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Wajumbe hao walikutana Makao Makuu ya Ofisi za Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujenga mtandao na ushirikiano. Katika mada yake kwa washiriki wa mkutano huo, Bi. Bussemaker alielezea benki ya NMB ilivyo na fursa mbalimbali kwa makundi tofauti na hasa inavyowasaidia wafanyabiashara kupitia bidhaa yake ya Trade Finance. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kulia) akiwasilisha mada katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Wajumbe hao walikutana Makao Makuu ya Ofisi za Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujenga mtandao na ushirikiano. Katika mada yake kwa washiriki wa mkutano huo, Bi. Bussemaker alielezea benki ya NMB ilivyo na fursa mbalimbali kwa makundi tofauti na hasa inavyowasaidia wafanyabiashara kupitia bidhaa yake ya Trade Finance.

  0 0

    Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimia na baadhi ya vijana aliokutana nao wakati akisubiri kivuko mapema leo asubuhi alipotembelea eneo la Feri, na kuvuka kwa kutumia kivuko cha Mv Kigamboni kwenda Kigamboni.
   Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza mmoja wa walemavu mapema leo asubuhi alipotembelea eneo la Feri, na kuvuka kwa kutumia kivuko cha Mv Kigamboni kwenda Kigamboni.
    Rais Dkt John Pombe Magufuli ( wa pilia kulia akiwa na baadhi ya Wananchi wengine walipokuwa wakisubiri kivuko mapema leo asubuhi alipotembelea eneo la Feri, na kuvuka kwa kutumia kivuko cha Mv Kigamboni kwenda Kigamboni

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo ya ukarabati wa kiwanda cha Sukari cha UGB  kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari nchini Cuba Bwana Francisco Martin, jana August 24/2017 kiwanda hicho kipo katika Mji wa San Nicola's de Bari nchini Cuba
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia shehena ya sukari iliyozalishwa katika kiwanda cha UGB Central Azucarero 30 Noviembre wakati alipotembelea kiwanda hicho jana August 24/2017 kilichopo katika mji wa San Nicola's de Bari nchini Cuba

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Viwanda vya Sukari nchini Cuba, Bw. Francisco Lled, ambaye amekubali kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuongeza uzalishaji wa sukari nchini.

  Shirika la Sukari la nchini Cuba linauwezo wa kuzalisha tani milioni nne za sukati kwa mwaka huku mahitaji ya ndani ni tani 700,000, ambapo kiasi kinachobaki huuzwa nje ya nchi. Kwa sasa shirika hilo linazalisha tani milioni mbili tu katika viwanda vyake 56.

  Waziri Mkuu alikutana na Bw. Lled jana (Alhamisi, Agosti 24, 2017), wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha UGB Central Azucarero 30 de Noviembre katika mji wa San Nicola’s de Bari ambacho ni kati ya viwanda 27 vya shirika hilo linalomilikiwa na Serikali ya Cuba kwa asilimia 100.

  Katika mazungumzo yao Waziri Mkuu alimshawishi Bw. Lled kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha sukari. Alisema kwa sasa Tanzania kuna viwanda vikubwa vitano vya sukari ambavyo uzalishaji wake hautoshelezi mahitaji ya ndani.

  Waziri Mkuu alivitaja viwanda hivyo ambavyo ni Mtibwa na Kilombero (Morogoro), Mahonda (Zanzibar), TPC (Kilimanjaro) na Kagera ambavyo vyote vinazalisha jumla ya tani 320,000 za sukari kwa mwaka huku mahitaji yakiwa ni zaidi ya tani 400,000.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi inatarajia kujenga viwanda vitatu vya kuzalisha sukari, ambavyo vitazalisha sukari itakayotosheleza mahitaji na ndani ya nchi na kiasi kitakachosalia kitauzwa nje.

  Kwa upande wake Bw. Lled alisema sera za Cuba haziruhusu shirika kwenda kuwekeza nje ya nchi na badala yake wanaruhusiwa kuzisaidia nchi zinazohitaji kujenga viwanda hivyo kwa kutoa ushauri na usimamizi wa ujenzi wa miradi hiyo.

  Alisema Shirika lake lipo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika usimamizi na kutoa ushauri wa ujenzi wa miradi ya viwanda vya kuzalisha sukari na kwamba walishatoa huduma kama hiyo katika nchi mbalimbali zikiwemo Brazil na Bolivia.

  Katika hatua nyingine, Bw. Lled alisema mbali na uzalishaji sukari pia shirika hilo kupitia viwanda vyake vya sukari wanazalisha vyakula vya mifugo, asali ambayo inatumika katika viwanda vya kutengeneza vinywaji vikali pamoja nishati ya umeme.

  Alisema miwa ya kuzalishia sukari katika viwanda vyao wanaipata kutoka kwenye vikundi vya ushirika wa kulima wa miwa vilivyoko katika mikoa yote nchi nzima kasoro mkoa wa Havana na Pañar del Rio na kwa mkulima mmoja mmoja ambao kwa pamoja hukusanya miwa katika vituo ambavyo hupeleka kiwandani.

  Hata hivyo alisema kuwa viwanda vyao vinanunua miwa kwa bei tofauti kulingana na ubora wa miwa na kwamba shirika lao linawasaidia wakulima kwa kuwaelimisha namna bora ya kulima pamoja na kuwaazima mashine za kuvunia wakati wa mavuno. Miwa yote nchini Cuba inavunwa kwa kutumia mashine.

  IMETOLEWA NA: 

  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  IJUMAAA, AGOSTI 25, 2017.

  0 0

   Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Khamadu Kitunzi akielezea teknolojia inayotumika kujenga jengo la kituo cha mafunzo cha mahakama leo jijini dar es salaam.
   Kaimu jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa na Mwakilishi wa Benki ya dunia nchini, Bella Bird (kulia) na kulia ni jaji kiongozi wa mahakama kuu ya Tanznaia Mhe. Ferdinand Wambali walipotembelea ujenzi wa kituo cha mafunzo cha Mahakama leo jijini Dar es salaam
  Picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo.

  Na Mohamed Ali-Mahakama.
  MAHAKAMA ya Tanzania inakusudia kuanzisha kituo cha Mafunzo kwa ajili ya watumishi wake pamoja na wadau ili kuwaongezea ujuzi utakaosaidia kuboresha huduma zinazotolewa na Mahakama. 

  Kituo hicho kinachojengwa katika eneo la Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam kitawaunganisha watumishi wa Mahakama na wadau katika mafunzo kwa njia ya video (video conferencing).

  Akizungumzia Kituo hicho, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Hamis Juma amesema ujenzi wa kituo hicho ni sehemu ya Maboresho ya huduma za Mahakama ambacho pia wadau wa Mahakama watakuwa ni sehemu ya mafunzo yatakayokuwa yakitolewa.

  Amesema badala ya Majaji, Mahakimu, watumishi na wadau wa Mahakama kwenda kupata baadhi ya mafunzo kwenye chuo cha Uongozi wa Mahakama- Lushoto (IJA), baadhi ya mafunzo watakuwa wakiyapata katika kituo hicho.

  Naye Mratibu wa Mpango Mkakati wa Mahakama pamoja na maboresho ya Huduma za Mahakama Mhe. Zahara Maruma alisema ujenzi wa kituo hicho ni utekelezaji wa nguzo ya tatu ya mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania ambapo kupitia nguzo ya pili ya Mpango huo, Majaji na Mahakimu hupatiwa mafunzo mbalimbali ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wakati.

  Akizungumzia nguzo ya tatu ya Mpango huo, Mhe. Maruma alisema nguzo hiyo inahusiana na urejeshaji wa imani ya wananchi kwa Mahakama na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za Mahakama ambapo kupitia kituo hicho wadau wa Mahakama watahusishwa kwenye Mafunzo mbalimbali ili kurahisisha suala la upatikanaji wa Haki.

  Kuhusu suala la matumizi ya Teknolojia ndani ya Mahakama, Mratibu huyo alisema hivi sasa Mahakama inao mpango wa kujenga vituo vya aina hiyo kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuunganisha Mahakama zote nchini kwa njia ya video (video conferencing).

  Ujenzi wa kituo cha Mafunzo cha Mahakama ulioanza hivi karibuni kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Benki ya Dunia unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 78. Aidha, Jengo la kituo hicho cha mafunzo linajengwa kwa kutumia teknolojia ya gharama nafuu iitwayo Moladi na linatarajiwa kukamilika ndani ya wiki nane.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na  waandishi wa habari katika hafla ya kupokea Pikipiki za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa pikipiki ya TONGBA ya China.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akikagua kwa kujaribu kuziendesha Pikipiki  hizo za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa pikipiki ya TONGBA ya China.
  .Muonekano wa pikipiki hizo.
   Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amepokea Pikipiki za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa Pikipiki ya TONGBA ya China.

  Hatua hiyo inakuja baada ya RC Makonda kutafuta kampuni hiyo na kuwasilisha ombi la kupatiwa Pikipiki za kisasa kwaajili ya kuongoza Misafara ya Viongozi, Misiba na kuwahisha Wagonjwa waliozidiwa Hospitalini ambapo kampuni hiyo ilipokea kwa mikono miwili ombi hilo kwa kutoa Pikipiki hizo.

  Makonda amesema lengo lake ni kuboresha Mazingira ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na vifaa vya kutosha ambapo hadi sasa amefanikiwa kupata Baiskeli 500, Pikipiki za kawaida 200 Computer 100 , Pikipiki za Trafic 10 na kufanya maboresho ya Magari ya Jeshi hilo yaliyokuwa yameharibika.

  Aidha Makonda amemuagiza aliekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam kuwakamata Askari wote waliobainika kushirikiana na wauzaji wa Dawa za kulevya na wale wanaobambikizia Wananchi kesi kukamatwa ndani ya masaa Masaa matano.

  Agizo hilo limekuja baada ya hivi juzi msamariamwema kutoa taarifa za uwepo wa muhusika wa dawa za kulevya na Askari walipofika kwenye Hotel wakamkamata na kupewa Rushwa baada ya muda mtuhumiwa akaachiliwa na kurudi kwenye Hotel na kufanya fujo kumtafuta alietoa taarifa na baada ya Makonda kufika na kuangalia Camera za CCTV wakawabainu Askari hao.

  Pamoja na hayo amesema wapo Askari waliomkamata Mwananchi akiwa Mpenzi wake kwenye Gari kisha kuwapiga Picha za Utupu na kuwalazimisha watoe kiasi cha Million Tano iliwasisambaze picha hizo kitendo ambacho ni kinyume Sheria ambapo Makonda awezi kuruhusu vitendo hivyo votendeke kwenye Mkoa wake na kueleza kuwa anataka Sheria na Haki vitendeke.

  Makonda kubaini uwepo wa Askari wa Uwanja wa Ndege wanaoshirikiana na Raia wa China kusafirisha Kobe na Wanyamapori na Askari wanawabambikia kesi wananchi ikiwemo wale wanaowakamata watu kwenye sehemu za mapumziko.

  Amesema hatokubali kuona Askari wachache wanaotumia Magwanda kuwanyanyasa Wananchi na kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi na kufanya Wananchi kushindwa kutoa ushirikiano.

  0 0

  Meneja Ufadhili Miradi ya Elimu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Anne Mlimuka akiongea na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na malengo ya mradi wa ukarabati wa shule kongwe 10 za Serikali. Kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TEA, Sylvia Lupembe.
   Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Sylvia Lupembe (kulia) akiongea na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na kukamilika kwa ukarabati wa shule kongwe 10 za Serikali. Kushoto ni Meneja Ufadhili Miradi ya Elimu, Anne Mlimuka.(Picha na Fatma Salum-MAELEZO)

   Na. Neema Mathias-MAELEZO
  MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imekamilisha awamu ya kwanza ya ukarabati wa shule 10 kongwe za Serikali ili kusaidia kuwepo kwa miundombinu bora ya kujifunzia na kufundishia pamoja na kuongeza nafasi za wanafunzi kupata elimu.

  Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa mamlaka hiyo Bi. Sylvia Lupembe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Shule Kongwe za Sekondari, ambao  unatekelezwa na Serikali kupitia TEA na Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na wadau wengine.

  “TEA inakarabati takriban shule kongwe 17 kati ya 87 na tumeanza ukarabati wa shule 10 katika awamu ya kwanza unaogharimu shilingi bilioni 10, mpaka sasa ukarabati huo umefikia asilimia 80 na ifikapo mwezi Oktoba utakuwa umekamilika. Shule nyingine 7 zitakarabatiwa katika awamu ya pili,” alifafanua Bi. Lupembe.

  Alizitaja shule zinazokarabatiwa kuwa ni Mzumbe na Kilakala - Morogoro, Shule ya Sekondari ya wasichana Msalato-Dodoma, Shule ya Sekondari Mwenge - Singida, Shule ya Sekondari Pugu - Dar es Salaam, Shule ya Sekondari Ilboru –Arusha, Shule ya Sekondari Same-Kilimanjaro, Shule ya Sekondari Tabora Wavulana na Tabora Wasichana na Shule ya Sekondari ya Wasichana Nganza iliyopo Mwanza.

  Aidha Bi. Lupembe aliongeza kuwa awamu ya kwanza ya ukarabati umehusisha miundombinu ya majengo ikiwemo mabweni, madarasa, majengo ya utawala, kuboresha mifumo ya maji safi na maji taka, mifumo ya umeme pamoja na mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

  “Tayari makabidhiano ya awali yamefanyika kwa baadhi ya majengo hususan mabweni na madarasa katika shule za Msalato, Mwenge na Mzumbe,” alieleza Bi. Lupembe.
  Bi. Lupembe alibainisha kuwa mafanikio kutokana na mradi huo yameanza kuonekana kwani ari ya wanafunzi kusoma imeongezeka na idadi ya usajili wa wanafunzi imeongezeka katika shule ya Mwenge na nyingine zilizokarabatiwa.

  Kwa upande wake Meneja Ufadhili Miradi ya Elimu Bi. Anne Mlimuka alieleza malengo mbalimbali ya mradi huo ikiwa ni pamoja na kuhifadhi ubora wa miundombinu ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora katika mazingira bora, kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi katika shule za Serikali na kuboresha miundombinu ya maabara kwaajili ya wanafunzi wa masomo ya Sayansi ili kuendana na Sera ya Viwanda inayohitaji wataalam wengi wa Sayansi.

  “Mradi huu wa kukarabati shule kongwe utakapokamilika utaendelea kwenye shule za Kata ili kuirudisha elimu katika hadhi yake na kuzifanya shule zote za serikali nchini zitoe elimu bora, wataalam bora katika mazingira bora kama ilivyokuwa hapo awali,” alisema Bi. Mlimuka.

  Mamlaka ya Elimu Tanzania kupitia mradi wake wa kukarabati  shule kongwe za Sekondari za Serikali unalenga kuimarisha Sekta ya Elimu nchini hasa kwa Shule za Serikali ambazo zilipoteza hadhi yake iliyokuwa hapo awali pamoja na kufadhili miradi mbalimbali ya elimu katika ngazi za Sekondari na Elimu ya Msingi.


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akichukua Tiketi zake pamoja na chenchi mara baada ya kulipia huduma ya Kivuko wakati akielekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana pamoja na kuzungumza na abiria mbalimbali wakati akisubiri kuvuka kwa kutumia usafiri wa Pantoni kuelekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Yusuph Ndemango ambaye ni mlemavu wakati alipomkuta ndani ya jengo la abiria lililopo upande wa Magogoni kabla ya kuvuka na Pantoni kuelekea  katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiingia katika kivuko cha MV Kigamboni pamoja na abiria wengine  wakati akivuka kuelekea upande wa pili wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya Kivuko cha MV Kigamboni pamoja na abiria wengine wakati akivuka kuelekea upande wa pili wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili upande wa Kigamboni mara baada ya kushuka pamoja na abiria wengine kwenye pantoni la MV Kigamboni.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama mmoja mara baada ya kuvuka upande wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akinunua chapati mara baada ya kuvuka upande wa Kigamboni wakati wa asubuhi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Kigamboni mara baada ya kuvuka kwa kutumia usafiri wa Pantoni wakati katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minazini Kigamboni jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiimba pamoja na wanachama wa CCM waliopo katika kambi ya mafunzo ya vijana iliyoandaliwa na Umoja wa vijana wa vyuo na Vyuo vikuu(CCM) katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Wanachama hao wakiimba mara baada ya Mwenyekiti wa CCM Taifa kuwasili ukumbini hapo.
   Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachama wa CCM waliopo katika kambi ya mafunzo ya vijana iliyoandaliwa na Umoja wa vijana wa vyuo na Vyuo vikuu(CCM) katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

   PICHA NA IKULU


  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, wakati alipofika ofisini kwake kujitambulisha na kuzungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo tangu alipoteuliwa kuliongoza Jeshi hilo, IGP Sirro, yupo mkoani Arusha, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao. Picha na Jeshi la Polisi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa katika picha na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo wakati alipofika ofisini kwake kujitambulisha, , IGP Sirro, yupo mkoani humo, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani katika mkoa wa Arusha, baada ya kukagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili katika mkoa huo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao. Picha na Jeshi la Polisi.
  Baadhi ya askari wa kikosi maalum cha kupambana na uhalifu wa kutumia silaha wakiwa tayari kwa kutoa heshima ya kijeshi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, alipowasili katika mkoa wa Arusha, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao. 

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro (kulia), akizungumza na baadhi ya askari wa Jeshi hilo katika mkoa wa Arusha, wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili, ambapo aliwataka askari kufanyakazi kwa kufuata misingi ya sheria na taratibu za nchi wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za kipolisi. Picha na Jeshi la Polisi.

  0 0

  Baadhi ya nyumba zinaendelea kubomolewa na wenye nyumba wakikusanya mabati, mbao na wengine Kimara Stop Over barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam. 

  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

  0 0


  0 0

  Na Lawrence Raphaely - Bunge.

  Balozi wa China nchini LU Youqing amefika Ofisini kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai  Jijini Dar es Salaam mapema leo kumuaga baada ya muda wake wa kukaa Tanzania kwisha.

  Akizungumza na Spika Ndugai, Balozi huyo alisema kuwa muda wake wa kutumikia kama Balozi wa China hapa nchini umekwisha hivyo hana budi kuondoka ingawa angetamani kuendelea kubaki.Balozi huyo aliongeza kuwa amefurahi kuona kuwa katika kipindi chake chote akiwa hapa nchini uhusiano baina ya Tanzania na China umezidi kukua.

  “Ninafuraha kubwa wakati ninaporejea China kuona kuwa uhusiano wetu wa kihistoria umezidi kukua na kwamba kuna ongezeko kubwa la uwekezaji wa China hapa Tanzania na pia tumesaidia katika utekelezaji wa miradi mingi,” alieleza Balozi huyo.

  Balozi huyo ambaye amesema kuwa Tanzania ni nchi yake ya mwisho kuhudumu kama Balozi aliongeza kuwa kwa sasa anarejea nchini China na akiwa huko ataendelea kujitikita katika shughuli za kudumisha uhusiano baina ya Tanzania na China.

  “Tanzania ndiyo nchi yangu ya mwisho  kuhudumu kama Balozi na nitakaporejea nyumbani (China) nitaendelea kufanya shughuli nyingine ambazo zinalenga kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na China,”  alisema Balozi Youqing.

  Kutokana na hilo Balozi Youqing alisema kuwa ingawa  anarejea nchini China lakini yupo tayari kwa Tanzania kuendelea kumtumia kama Balozi wake katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali zitakozosaidia katika kudumisha ushirikiano baina wa nchi zote mbili.

  “Nipo tayari kwa Tanzania kuendelea kunitumia kama Balozi wake aliyepo Nchini China, ninawakaribisha kwa mikono yote miwili tuendelee kufanya kazi kwa pamoja,” alisema Balozi huyo.

  Kwa upande wake Spika Ndugai alimshukuru  Balozi huyo kwa kazi kubwa ambayo ameifanya akiwa hapa nchini na kumueleza kuwa daima Watanzania wataendelea kumkumbuka kwa kazi nzuri aliyoifanya.

  “Mimi binafsi katika kipindi chako ukiwa kama Balozi nimeshuhudia ongezeko kubwa la watanzania wengi tena wa hali ya chini wakisaifiri kwenda China kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kibiashara,” alisema Spika Ndugai na kuonegeza kuwa; kupitia fursa hiyo Watanzania wengi wameweza kujiajiri kupitia biashara ya kununua bidhaa toka China na kuja kuuza hapa nchini.

  Mhe Spika pia alimshukuru Balozi Youqing kwa uchakapakazi wake katika kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia wataalamu kutoka nchini China.

  “Unaondoka lakini utakapojisikia kurudi, sisi kama Bunge na Serikali kwa ujumla tupo tayari kukupokea kwa mikono miwili na kuendelea kufanya kazi na wewe,” alisema Spika Ndugai.

  Mbali na hayo Spika Ndugai pia alimuomba Balozi Youqing kuendelea kuwa Balozi wa Tanzania atakaporejea nchini China kwa kuendelea kufanya shughuli ambazo zitasaidia katika kuimarisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini LU Youqing  anayemaliza muda wake alipofika kumuaga  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa masuala ya  Diplomasia na Vyombo ya Habari- Ubalozi wa China Bi. Wang Fang.
  Balozi wa China nchini LU Youqing  anayemaliza muda wake akimueleza jambo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai alipofika kumuaga  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa masuala ya  Diplomasia na Vyombo ya Habari- Ubalozi wa China Bi. Wang Fang.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimkabidhi zawadi  Balozi wa China nchini LU Youqing  anayemaliza muda wake alipofika kumuaga  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa China nchini LU Youqing  anayemaliza muda wake akimkabidhi  zawadi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai alipofika kumuaga  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Spika Bw. Said Yakubu
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) katika picha ya pamoja  na Balozi wa China nchini LU Youqing  anayemaliza muda wake alipofika kumuaga  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai akiagana  na Balozi wa China nchini LU Youqing  anayemaliza muda wake mara baada ya kuzungumza nae  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Picha na Ofisi ya Bunge

  0 0


older | 1 | .... | 1350 | 1351 | (Page 1352) | 1353 | 1354 | .... | 1897 | newer