Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

SIMBA MABINGWA WA NGAO YA HISANI 2017

$
0
0
 Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallance Karia na Makamu wake, Michael Wambura wakiwa pamoja na Wachezaji wa Timu ya Simba baada ya kuwakabidhi Ngao ya Jamii waliyoitwaa leo baada ya kuwashinda watani wao wa jadi Yanga kwa changamoto ya mikwaju ya penati ya 4-3, katika mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.


Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima akiwania mpira wa mshambuliaji wa Yanga Donald ngoma katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Ngao ya Jamii unaoendelea hivi Uwanja wa Taifa.

Kiungo wa Yanga Rafael Daud akimruka beki wa Simba Method Mwanjali katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Ngao ya Jamii unaoendelea hivi sasa Uwanja wa Taifa
Beki wa kati wa Yanga Kelvin Yondani na mshabuliaji wa Simba Laudit Mavugo wakigombania mpira katika mchezo wa ufunguzi wa ligi wa Ngao ya Jamii unaoendelea hivi sasa Uwanja wa Taifa.
Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma akimruka beki wa Simba Method Mwanjali katika mchezo wa ufunguzi wa ligi wa Ngao ya Jamii unaoendelea sasa hivi Uwanja wa Taifa
Golikipa Rostand Youthe akiruka juu na  kudaka mpira akiwa sambamba na mshabuliaji wa Simba Emanuel Okwi.
Kiungo wa Simba Haruna Niyonzima akipiga pigo la adhabu nje ya kumi na nane
Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma akipambana na beki wa kati wa Simba Salim Mbonde katika mchezo wa ufunguzi wa ligi Ngao ya Jamii.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

VIJUSO VYA MAGAZETI YA ALHAMIS LEO AGOSTI 24,2017

TaGEDO YAPATA UGENI KUTOKA UJERUMANI, WAFANYA SHUGHULI MBALIMBALI IKIWEMO USAFI WA MAZINGIRA

$
0
0
Vijana wa Kituo cha ubunivu na ushonaji nguo cha Taasisi ya Kijamii ya TaGEDO, wakimwelekeza jinsi ya kutumia cherehani, kijana Astrid Naundorf kutoka Chuo Kikuu Cha Munister, wakati vijana wa Chuo hicho walipotembelea Kituo hicho, Kigamboni Dar es Salaam, leo.
---------------------------------------


KIGAMBONI, DAR ES SALAAM.

Vijana kutoka Chuo Cha  Munister nchini Ujerumani, leo wametembelea Kituo cha Taasisi ya Kijamii ya kuelendeleza Vijana na Kinamama katika Ujasiriamali hapa nchini (TaGEDO) kilichopo Kigamboni Dar es Salaam, na kushiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo kusafisha mazingira.

Vijana hao zaidi ya 20 walishirikiana na vijana wenzao kutoka TaGEDO na kufanya usafi kwenye eneo la Ofisi ya Mtaa wa  Kisiwani na baadaye kushiriki katika mafunzo ya ushonaji nguo kwenye mradi wa ushonaji nguo wa kituo hicho na baadaye ulifanyika mjadala wa kubadilishana uzoefu katika mafanikio na changamoto zinazokabili vijana na kinamama.

Kituo hicho cha Taasisi ya TaDEDO hadi sasa kina vijana 83 ambao kwa namna mojawapo walikosa fursa  ikiwemo ya kutoendelea na masomo ambao sasa wanapatiwa mafunzo ya ujasiriamali wa kubuni na kushona nguo ambapo baadhi yao tayari ni mafundi.

Akizungumzia kituo hicho, Kiongozi wa TaGEDO Venance Kalumanga, amesema lengo la kuanzisha mafunzo hayo ya kubuni na kushona mavazi ni kutaka baadaye waanzishe kiwanda kikubwa cha ushonaji kitakachoweza kutoa ajira kwa kina mama na vijana ikiwa ni moja ya hatua ya kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli katika azma yake ya kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa Viwanda.

"Hadi sasa kwenye kituo chetu tunazo cherehani kumi ambazo baadhi tulijitolewa sisi waanzilishi ambao tunatoka Chuo Cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni na nyingine tulipewa na mfadhili kutoka Chuo Kikuu cha Munster cha Ujerumani, Dk. Reinhold Hemker. Sasa kwa kuwa mafunzo tunaoa bure kwa vijana na kina mama wanaokuja hapa changamoto ni namna ya kukidhi mahitaji, hivyo tunawaomba wadau wote wa maendeleo wajitolee kutusaidia ili tulisaidie taifa letu kwa ufanisi", alisema Kalumanga.

Kalumanga ambaye ni Mhadhiri katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, katika Idara ya Jinsia na Maendeleo, alisema, baadhi ya wadau ambao pia wametoa mchango mkubwa kuanzishwa TaGEDO ni pamoja na wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na UDOM.
 Taasisi ya Kijamii ya kuelendeleza Vijana na Kinamama katika Ujasiriamali hapa nchini (TaGEDO) Venance Kalumanga akichoma taka, wakati yeye na wenzake wa Taasisi hiyo, walipoungana na Vijana kutoka Chuo Cha  Munister nchini Ujerumani, kufanya usafi kwenye eneo la Ofisi ya Mtaa wa Kisiwani, Kigamboni, dar es Salaam, leo
 Vijana wa TaGEDO wakishirikiana na Vijana hao kutoka Ujerumani kukusanya taka wakati wakifanya usafi kwenye ofisi ya Mtaa wa Kisiwani, Kigamboni Dar es Salaam, leo.
ZIFUATAZO NI PICHA TAGEDO NA VIJANA HAO KUTOKA UJERUMANI WAKISHIRIKI KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI WAKATI WA ZIARA HIYO, LEO
🔻
 MSAFARA KUTOKA MTAA WA KISIWANI KWENDA OFISI YA TaGEDO
🔻
 MAANDALIZI YA CHAKULA CHA WENYEJI NA WAGENI
🔻
MAFUNZO YA USHONAJI
🔻
 MAFUNZO YA USHONAJI
🔻
 CHAKULA CHA MCHANA
🔻
 PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

PROF. BRIAN VAN ARKADIE ATOA SOMO MAPINDUZI YA KILIMO MHADHARA WA ESRF

$
0
0
TAASISI ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imefanya mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara. 

 Katika mhadhara huo msemaji Mkuu alikuwa Prof. Brian Van Arkadie, majadiliano yalitanguliwa Prof Samuel Wangwe na Aloyce Hepelwa Akiwasilisha mada yake aliwataka wataalamu kubadilika katika namna ya kusaidia kuongeza tija katika kilimo na kuachana na dhana za zamani kwamba wakulima wameshindwa kubadilika na kukwamisha maendeleo. 

 Amesema katika mjadala huo wa hadhara kuhusu maendeleo ya kilimo kutoka wakati wa uhuru hadi sasa katika jengo la mikutano la ESRF mjini hapa alisema kwamba tafiti nyingi zimekuwa zikishutumu wakulima kwa kuwa na muono mdogo na kubisha mabadiliko yanayohitaji kuongeza uzalishaji. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

 Aidha alisema kwamba kumekuwepo na tafiti zinazoonesha kwamba kilimo kimekwama katika uasili wake na kuhitajika tafiti za kuona namna bora ya kukikwamua. Hata hivyo alisema profesa huyo, kumekuwepo na mabadiliko ya maana katika uchumi wa vijijini, hasa kwa kuangalia uhalisia wa uchumi kwa kuzingatia fursa za kiuchumi na masoko katika maisha ya wanakijiji. 

 Alisema kutokana na mabadiliko hayo ni dhahiri kusema kwamba wakulima hawabadiliki ni kushindwa kwa wataalamu ambao ndio walibuni na kupanga mipango ambayo haikuweza kuwanufaisha wakulima. Profesa Brian Van Arkadie ambaye pia alishawahi kuwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam na miongoni mwa watafiti ESRF anasema kuna hatua mbalimbali zilizofikiwa na wakulima wa Tanzania tangu uhuru na kwamba kuna uhusiano kati ya kilimo na maendeleo yaliyopo sasa. 

 Alisema katika mkutano huo wa hadhara ulilenga kuchambua masuala muhimu yanayojitokeza katika kilimo cha Tanzania na kuona namna bora ya kukabiliana na changamoto hizo kwa maendeleo ya taifa, kuwa kuanzia miaka ya 1970 mazao kwa ajili ya masoko ya nje yaliporomoka sana na kusababisha taifa kutafuta njia nyingine ya kurekebisha hali hiyo ikiwamo kuanzishwa kwa mradi wa kubadili kilimo wa SAGCOT. Prof. Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara mkubwa ulishirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara akiwasilisha utafiti wake katika mkutano huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.

 Ingawa mazao hayo ya kilimo yameonakana kuporomoka kutoka miaka hiyo, kumekuwepo na ongezeko kubwa la pengo la kipato kati ya watu wa mijini na vijijini huku ukuaji wa vijijini ukikumbwa na udumavu. Pamoja na ukweli huo amesema profesa huyo, kuna mabadiliko ya kutosha katika maeneo ya vijijini na katika kilimo kwamba kusema hakuna maendeleo si kitu sahihi.

 Alisema zipo sababu za kupungua kwa uzalishaji wa mazao makuu kama kahawa, tumbaku, mkonge na hilo linatokana na serikali kuingilia kati mfumo wa masoko ambao haukuwa unaswihi. Profesa huyo alisema hata hivyo, kwa miaka 50 kilimo cha Tanzania kimefanikiwa kulisha taifa kwa kuwezesha watu wa mijini na vijijini kupata vyakula hasa vile vya msingi ingawa wakati mwingine ukame ulileta usumbufu. 

 Huku Tanzania ikiwa na ongezeko la watu kutoka milioni 12.3 kwa mwaka 1967 hadi milioni 44.9 kwa mwaka 2012 ni dhahiri ukuaji wa kilimo umesaidia kuiweka nchi katika hali bora zaidi ya upatikanaji wa chakula ingawa ifikapo mwaka 2030 watu wa mijini watakuwa wameongezeka kwa asilimia 37 na kuweka shinikizo ambalo kwa namna nyingine linaweza kuwa na maana kwa kuwa mazao ya chakula yatakuwa ndiyo ya biashara na hivyo kuacha kutegemea yale ya asili kama kahawa na tumbaku.  Mtafiti mshiriki mwandamizi wa ESRF Prof Samuel Wangwe akijadili mada iliyowasilishwa na Prof Brian Van wakati wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Katika utafiti mwaka 2007, imeonekana kwamba nusu ya mapato ya watu wa Dar es salaam yamekuwa yakitumika kwa ajili ya kununua chakula na kufanya kiasi kikubwa cha kazi za kilimo katika mazao ya chakula kuwa biashara nzuri kwa wakulima.Katika mada yake profesa huyo alisititiza kwamba hakuna shaka maendeleo nchini katika kilimo yapo lakini tafiti nyingi zimeshindwa kuelekeza kisahihi maendeleo hayo na ukweli wa kutoneemeka kwa wakulima. 

Akijadili mada hiyo ya Prof. Brian Van Arkadie, Mtafiti mshiriki mwandamizi wa ESRF Prof Samuel Wangwe ameshauri serikali kutonakili mikakati na sera za nchi zilizoendelea wakati wa utekelezaji wa mikakati ya kugeuza nchi kuwa taifa la uchumi wa kati linalotegemea viwanda. Alisema hayo katika mhadhara kuhusu kilimo nchini kwamba si sawa kunakili sera na mikakati ya nchi zilizoendelea kama Uingereza, Asia ama Marekani katika kutekeleza sera ya viwanda bali ibuni yenyewe kwa kuzingatia hali iliyopo. Mhadhiri mwandamizi kitengo cha kilimo uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Aloyce Hepelwa akijadili mada iliyowasilishwa na Prof Brian Van wakati wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati akijadili mada iliyowasilishwa na Prof Brian Van Arkadie kutoka Uingereza kuhusu mazao ya chakula kama ndio mazao ya biashara katika mikakati ya muda mrefu ya kubadili kilimo cha Tanzania na athari za kisera, Prof Samuel Wangwe alisema kila nchi ina njia yake ya kufikia ustawi na neema ya viwanda na hivyo Tanzania lazima ifuate njia yake na sio kunakili. “Hatuwezi kupita njia ambayo nchi kama Uingereza, Japan, au nchi za Ulaya zimepita wakati wakikua kiviwanda, lakini tuwe na njia yetu katika kuelekea uchumi wa viwanda . 

Kama hatutakuwa makini hatutafanikiwa,” alisema. Prof Wangwe pia alisema kwamba mapinduzi ya Kilimo lazima yapewe kipaumbele kama taifa linataka kuwa na uchumi wa viwanda. Akikaribisha wadau kushiriki katika mhadhara huo Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kwamba mhadhara huo ulikuwa ni njia muafaka ya kubadilisha maarifa ili kuboresha kilimo cha Tanzania kwa kukipatia kilimo hicho mkakati wa muda mrefu wa kubadilika. Picha juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wanazuoni mbalimbali wakiwasilisha maoni yao wakati wa mhadhara wa kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliondaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema katika kuimarisha kilimo hicho ni vyema masuala yanayogusa mazao ya chakula na yale ya kupeleka nje na sera kuangaliwa kwani masuala hayo yana athari za muda mrefu katika ukuaji wa kilimo. Katika hadhira hiyo aliwataka washiriki kuangalia kwa makini historia ya kilimo nchini, sera na kuona athari za muda mrefu na fupi za sera zilizopo na kama kweli wataalamu wametekeleza wajibu wao katika kutafuta suluhu ya wakulima au kuendelea kudai kwamba wakulima hawako tayari kubadilika. 

 Dk. Kida alisema kwa kuangalia historia ya kilimo Tanzania wataalamu hao watakuwa na nafasi kubwa ya kuchangia katika kuendeleza kilimo ambacho ni msingi mkubwa wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kwani wapo asilimia 80 wakitegemea kilimo na taifa ambalo linataka kwenda katika uchumi wa viwanda ambavyo mali ghafi zinategemewa kutoka katika sekta ya kilimo.Aidha alimshukuru Prof. Brain Van Arkadie ambaye ndiye alikuwa msemaji mkuu kwa utafiti alioufanya ambao aliuwasilisha mbele ya mkutano wa wasomi mbalimbali. Prof. Van Arkadie ambaye ni veteran ambaye alishawahi kushiriki katika mpango wa miaka mitano wa kwanza wa maendeleo mwaka 1963. Na kufanyakazi katika maeneo mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki na Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Mwenyekiti wa mhadhara huo Profesa wa Kilimo Uchumi kitengo cha Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Lucian Msambichaka akiendesha mhadhara huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida na kushoto ni Prof. Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara huo. Prof. Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara huo akifafanua jambo wakati wa kipindi cha maswali na majibu. Pichani juu na chini ni sehemu ya wanazuoni na wadau kutoka taasisi mbalimbali walioshiriki kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara katika mhadhara huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam. Picha ya pamoja ya washiriki wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara ambao uliandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akibadilishana mawazo na wageni waalikwa baada ya kumalizika kwa mhadhara huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam

AFISA MTENDAJI MKUU WA STANDARD CHARTERED BANK-TANZANIA, ABADILISHANA UZOEFU WA KAZI NA WAFAYAKAZI WA AIRTEL LEO

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso, (kushoto), akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao (Network), Bw. Emmanuel Luanda, Mkurugenzi wa IT, Bw. Frank Filman, na Mkurugenzi wa Masoko, Bw.Isack Nchunda. kampuni ya Airtel ilitembelewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Standard Charted bank ili kubadilishana uzoefu katika kuhudumia wateja wao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso, (kulia), na Afisa Mtendaji Mkuu, wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Bw. Anjay Rughani, wakizunhuzma kabla ya kuanza kwa semina hiyo. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso, akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati akimkaribisha Afisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, kutoa semina ya kuhamasisha (motivation), makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam. kampuni ya Airtel ilitembelewa na Afisa Mtendaji Mkuu huyo kutoka Standard Charted Bank ili kubadilishana uzoefu katika kuhudumia wateja wao.
Afisa Mtendaji Mkuu, wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Bw. Anjay Rughani, ambaye ni mmoja kati wa watanzania wachache wanaoshikilia nafasi hiyo ya juu kwenye taasisi za kimataifa, akizungumza wakati wa semina ya kuwahamasisha (motivation), wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi, Airtel, makao makuu, jijini Dar es Salaam.

IGP SIRRO ATEUA KAIMU KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR NA KAMANDA WA KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM

$
0
0


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Nyakoro Sirro amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Juma Yusuf Ally kuwa Kaimu Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Uteuzi huo unafuatia kustaafu kwa aliyekuwa kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdani Omari Makame kwa mujibu wa sheria baada ya kutimiza umri wa miaka sitini (60).

Kabla ya uteuzi huo DCP Juma alikuwa ni Mkuu wa Utawala na Fedha Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.

IGP Sirro pia amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi  (SACP) Lazaro Mambosasa kuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam. Kabla ya uteuzi huo, SACP Mambosasa alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa MtwaraKamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi  (SACP) Neema Mwalimu Mwanga anakwenda Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.

IGP Sirro pia amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Gilles Bilabaye Mroto kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na  Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Emmanuel Lukula kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke.

Kabla ya uteuzi huo, ACP Lukula alikuwa Afisa Mnadhimu wa Polisi mkoa wa Mbeya.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote kuendela kushirikiana na Jeshi hilo kwa kufichua taarifa za uhalifu na wahalifu ili kwa pamoja tuendelee kuiweka Tanzania salama.


Imetolewa na:
Barnabas David Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.
S.L.P 9141
Dar es Salaam

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA ATEMBELEA TAASISI YA MAFUNZO YA UANASHERIA KWA VITENDO TANZANIA (LAW SCHOOL OF TANZANIA

$
0
0

Na Scholastica Njozi – Law School of Tanzania

Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi amewataka watumishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) kutambua kuwa wamebeba dhamana kubwa kwa Taifa. 

Waziri Kabudi ametoa wito huo leo alipotembelea Taasisi hiyo wakati akiwa katika ziara ya kutembela taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo ili kujionea  namna Taasisi hiyo inavyotoa mafunzo.

“Nataka niwahakikishie kuwa mmebeba jukumu kubwa sana kwa Taifa hivyo mnapotekeleza majukumu yenu zingatieni sana kuhakikisha wahitimu wanakuwa na maadili, wasiopenda rushwa na kubwa zaidi watambue wanakwenda kuwatumikia watanzania maskini”, alisema Mhe. Waziri.”  Prof. Kabudi aliongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Taasisi Dkt. Zakayo Lukumay, amesema watahakikisha wahitimu wote wanakuwa na uzalendo kwa nchi yao kwa kupitia mafunzo wanayoyapata. 
Prof. Palamagamba Kabudi mwenye tai nyekundu akiwa na viongozi wa Taasisi alipotembelea majengo.
Prof. Palamagamba Kabudi, akimsaidia mwanafunzi  Bi. Jesca Mbawala namna ya kutafuta vitabu kupitia mtandao, alipotembelea maktaba ya Taasisi.
Waziri wa Katiba na Sheria, Prof.Palamagamba Kabudi akitia saini kitabu cha wageni

RAIS DKT MAGUFULI AMUAPISHA NAIBU KAMISHNA MKUU WA TAKUKURU IKULU DAR ES SALAA LEO

$
0
0
 Brigedia Jenerali John Julius Mbungo aliyeapishwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi  Brigedia Jenerali John Julius Mbungo baada ya kumuapisha kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Brigedia Jenerali John Julius Mbungo akila kiapo cha maadili ya Viongozi wa serikali baada ya kumuapisha kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Brigedia Jenerali John Julius Mbungo wakati akiongea machache  baada ya kumuapisha kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Brigedia Jenerali John Julius Mbungo baada ya kuongea machache  baada ya kumuapisha kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Mhe. Angela Kairuki  baada ya kuongea machache  baada ya kumuapisha  kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela baada ya kumuapisha Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Bw. Alex Mfungo akiongea machache  baada ya kuapishwa kwa  Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea machache baada ya kumuapisha Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Mhe. Angela Kairuki, Waziri wa sheria na Katiba Profesa palamagamba Kabudi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju, katibu Mkuu Kiongozi Balozi  John Kijazi, wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Brigedia Jenerali John Julius Mbungo baada ya kuapishwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.

PICHA NA IKULU


Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika biashara mbioni kukamilishwa

$
0
0
Na MbarakaKambona,

Wadau wa haki za binadamu kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za serikali, taasisi binafsi na wafanyabiashara wamekuta na kupitia rasimu ya kwanza ya mapendekezo ya Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika biashara.

Wadau hao walikutana Agosti 23, 2017 katika kikao kilichofanyika katika ofisi zaTume ya Haki za Binadamu jijini Dar es Salaam kujadili rasimu hiyo kufuatia utafiti uliofanywa na wataalamu na maoni yaliyokusanywa kutoka katika maeneo mbalimbali ya biashara.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Mhe.Iddi Ramadhani Mapuri alisema kuwa kuanzishwa kwa mpango huo kumelenga katika kuhakikisha kuwa mifumo yote ya kitaifa na kimataifa ya sera na sheria inazingatia na ulinzi na utetezi haki za binadamu wakati wote wa utekelezaji wa majukumu ya kibiashara na kuweka mifumo ya utatuzi wa migogoro ya waathirika pale itakapojitokeza.

Utafiti huo ambao ulifanyika Mei, 2017 ulihusisha wadau mbalimbali wakiongozwa na Tume, zikiwemo taasisi za serikali, taasisi binafsi, wafanyabiashara na wananchi ulifanyika katika maeneo maalum yaliyochaguliwa ikiwemo maeneo ya kilimo katika Mkoa wa Mbeya- Mbarali, Maeneo ya viwanda Mkoani Dodoma na Singida na maeneo yaUtalii upande wa Zanzibar uliofanyika.

Utafiti huo unafuatia tamko la Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lilitolewa mwaka 2011 linalotaka nchi wanachama kuanzisha Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika maeneo ya biashara ili kutoa muongozo wa kulinda uvunjifu wa haki za binadamu katika maeneo hayo.

Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Francis Nzuki wakati akiongea na waandishi wa habari katika mkutano huo alitoa mifano kadhaa waliyoiona wakati wa utafiti huo moja wapo ni katika maeneo ya Kilimo ambapo wakulima walio wengi wanatumia dawa mbalimbali katika kuzalisha mazao yao kitu ambacho kwa namna moja au nyingine inahatarisha maisha ya watu na mazingira yao, hivyo ni vyema shughuli hizo zikawekewa miongozo ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza baadae.

Aidha, Mhe. Iddi Ramadhani Mapuri alitumia nafasi hiyo ya mkutano kuwakumbusha wadau na wananchi kwa ujumla kwamba utetezi na ulinzi wa haki za binadamu sio wa serikali, taasisi binafsi wala wafanyabiashara peke yao, bali ni jukumu la watu wote.

Pia aliwakumbusha wadau kuwa kazi iliyo mbele yao ya kuandaa mpango huo ni kubwa hivyo ufanisi wao katika maandalizi ya mpango huo utasaidia na kurahisisha utekelezaji wake kitaifa na kimataifa.

Mchakato wa maandalizi ya mpango huo unatokana na ahadi ya Serikali iliyoiweka katika Mpango kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu (NHRAP) wa mwaka 2013-2017 ambapo Serikali ilifunga ahadi ya kuanza kuandaa mpango endelevu wa Haki za Binadamu katika maeneo la biashara.

Mchakato huo unafadhiliwa na taasisi ya Denmark, Danish Institute for Human Rights (DIHR) na Centre for Research on Multinational Corporation (SOMO).

 Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe.Iddi Ramadhani Mapuri akiongea na washiriki wa kikao cha wadau wa haki za binadamu wakati akifungua mkutano huo uliofanyika katika ofisi za Tume zilizopo  jijini Dar es Salaam Agosti 23, 2017. Kulia kwake ni Kamishna Mkaazi wa Tume Zanzibar, Mhe. Mohamed Hassan na Kushoto kwake ni  Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Bwn. Francis Nzuki
 Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Bwn. Francis Nzuki akiongea katika kikao cha wadau wa haki za binadamu mara baada ya Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe.Iddi Ramadhani Mapuri (katikati) kufungua rasmi mkutano huo.
 Mmoja wa watoa mada ya haki za binadamu na biashara, Bi. Nora Gotzmann akiwasilisha mada yake iliyohusu masuala ya Biashara na Haki za Binadamu, jinsi ya kulinda, kuheshimu na namna ya kupata utatuzi wa migogoro inapojitokeza.
 Mratibu wa Mradi wa kuandaa Mpango kazi wa Haki za Binadamu na Biashara kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jovina Muchunguzi akiongea na washiriki wa kikao hicho cha wadau wa haki za binadamu wakati akiwasilisha mada.
 Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakijadiliana namna ya kuboresha Mpangokazi huo.
Mmoja wa washiriki katika mkutano huo, Bwn. Constantine Mugusi akifafanua jambo kwa wana kikundi wenzake wakati wa majadiliano ya kuboresha Mpangokazi huo.

JANUARY MAKAMBA AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR

$
0
0
Na Mathias Canal, Zanzibar

Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) limefunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 kwa kuwashirikisha washiriki wapatao 350, ambapo miongoni mwao wanadiaspora wamehudhuria zaidi ya 200 na watendaji kutoka taasisi za Serikali zote mbili wakiwa ni 150.

Diaspora wametakiwa kutumia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini katika sekta ya kuimarisha na kuanzisha viwanda ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa dhamira yake ya kuifanyaTanzania kuwa nchi ya viwanda.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB)  alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi litakalodumu kwa siku mbili Agosti 23 na 24, 2017 katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel uliopo katika kijiji cha Kama Wilaya ya Magharibi A.

Mhe Makamba alisema kuwa kwa sasa Demokrasia imeimarika nchini kutokana na serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kukubaliana kwa kauli moja kuimarisha usalama wa wananchi ili kurahisisha uimara wa uwajibikaji wa ujenzi wa Taifa.

Alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kuwa kuna changamoto nyingi zinazowakabili Diaspora ikiwemo ucheleweshwaji wa uwekezaji sambamba na kutokuwepo sera ya utambuzi dhidi yao lakini changamoto hizo zinaendelea kutatuliwa na hatimaye kumalizika kabisa.

Changamoto zingine ilikuwa ni pamoja na kuwepo kwa uraia wa nchi mbili ambapo Mhe Makamba alisema kuwa serikali inalifanyia kazi jambo hilo kwani halipo katika uhalisia kwa sasa kwa kutokuwepo kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili Diaspora waweze kutumia fursa ya uwekezaji nchini kwa urahisi huku akiwasihi kutumia fursa muhimu za uwekezaji katika Nyanja zote kwani faida itakuwa kwa Diaspora wenyewe, watanzania waishio nchini na Taifa kwa ujumla wake.

Alisema kuwa Diaspora ni kiungo muhimu katika kuchangia sehemu kubwa ya maendeleo endelevu katika nchi zao za asili kwa kuchangia katika uhamishaji wa rasilimali, ujuzi na mawazo na hatimaye kupelekea nchi yao kunufaika na uchumi wa kidunia unaoonekana kukua siku hadi siku.

Alisema kuwa fedha zinazotumiwa na Diaspora katika nchi wanazoishi ni miongoni mwa vyanzo vinavyosababisha ukuaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, fedha hizo zitakapotumika vizuri kwa uwekezaji katika biashara na vitega uchumi ndio huwa chanzo na kichocheo cha ukuaji jadidifu wa pato na uchumi wa nchi zinazopokea fedha hizo.

Aidha, Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imeweka msisitizo na juhudi za kukusanya mapato ili kukuza uchumi wa Tanzania na uwezo wa serikali kujiendesha.
Mhe Mkamba aliwasihi Diaspora kufuata kanuni,taratibu na sheria katika nchi wanazoishi ili kuendelea kuiweka Tanzania katika sifa nzuri ya kuwa na wananchi wenye kufuata sheria na taratibu.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeratibu Kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) kwa minajili ya kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna ya kutumia fursa za uwekezaji.
Kongamano hilo ni mwendelezo wa makongamano matatu ya awali yaliyofanyika mwaka 2014 na 2015 Jijini Dar es Salam na mwaka 2016 lililofanyika Mjini Zanzibar.

Lengo kuu la makongamano hayo ni kwa Serikali na wanadiaspora kukutana, kubadilishana mawazo na kuwashajihisha wanadiaspora kuwekeza nchini kwao kwa maslahi yao na kwa ustawi wa uchumi wa taifa lao.

Kongamano hili la nne la Diaspora limebebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao”

Katika hatua nyingine washiriki wote wamepata fursa ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuboresha umoja huo wa watanzania waishio nje ya nchi sambamba na kutoa maoni yao kwa serikali kwa dhamira ya kuwa na Umoja na ushirikiano bora kati yao na serikali.

Pia walitembelea shamba la BIG BODY SPICE linalolima mazao mbalimbali ya

viungo ikiwemo mazao ya Pilipilimanga, Mdalasini, Kahawa, Hiliki, Vanila,


Mdoriani, Kakao, Karafuu, Tangawizi, Mrangirangi na Mkungumanga.



Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Mkurugenzi Mpya wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Ndg Geofrey Mwambe akizungumza wakati wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni linalofanyika Sea Cleaf Hotel Mjini Zanzibar
Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo 
Dkt Hamed Hikmany (Katikati) akiongoza mada kuhusu Ushauri wa uwekezaji kwa siku zijazo mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Mhe Hassan Khamis (Katikati) akiongoza mada kuhusu Jukumu la jumuiya ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi katika uwekezaji sambamba na Diaspora na nchi yao katika maendeleo endelevu mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni wakimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni wakifatilia kwa makini Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar
Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni wakimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar.
Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakitembelea shamba la BIG BODY SPICE kujionea kilimo cha mazao ya viuongo
Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu kilimo cha mazao ya viuongo mara baada ya kutembelea shamba la BIG BODY SPICE
Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu kilimo cha mazao ya viuongo mara baada ya kutembelea shamba la BIG BODY SPICE
Mkwezi akionyesha umahiri wa kukwea mnazi mbele ya Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) walipotembelea shamba la BIG BODY SPICE
Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Kisasa Fumba Town Development mara baada ya kutembelea katika eneo hilo.

Tigo yakabidhi zawadi kwa washindi 113 wa Promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi

$
0
0

Meneja Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama akimkabidhi simu aina ya Tecno S1, Ally Mwaisemba, mmoja kati ya washindi 113 wa promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi jijini Dar Es Salaam leo. Jumla ya washindi 219 wamejishindia simu hizo nchi nzima.

Meneja Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama akimkabidhi simu aina ya Tecno S1, Ally Mwaisemba, mmoja kati ya washindi 113 wa promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi jijini Dar Es Salaam leo. Jumla ya washindi 219 wamejishindia simu hizo nchi nzima.

Meneja Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama akimkabidhi simu aina ya Tecno S1, Godfather Masawe, mmoja kati ya washindi 113 wa promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi jijini Dar Es Salaam leo. Jumla ya washindi 219 wamejishindia simu hizo nchi nzima.
Meneja Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama akimkabidhi simu aina ya Tecno S1, Justina Lyimo, mmoja kati ya washindi 113 wa promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi jijini Dar Es Salaam leo. Jumla ya washindi 219 wamejishindia simu hizo nchi nzima.
Meneja Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama akimkabidhi simu aina ya Tecno S1, Zawadi Koli, mmoja kati ya washindi 113 wa promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi jijini Dar Es Salaam leo. Jumla ya washindi 219 wamejishindia simu hizo nchi nzima.
Meneja Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama akimkabidhi simu aina ya Tecno S1, Zawadi Koli, mmoja kati ya washindi 113 wa promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi jijini Dar Es Salaam leo. Jumla ya washindi 219 wamejishindia simu hizo nchi nzima.
Washindi wa promesheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao za simu aina ya Tecno S1. Jumla ya washindi 219 wamejishindia simu hizo nchi nzima.

KAMPUNI YA ZIPLINE WASAINI MKATABA NA WIZARA YA AFYA NA MSD KWAAJILI YA KUSAMBAZA DAWA KWA DRONE

$
0
0
WIZARA  ya afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto na Bohari ya Dawa Tanzania(MSD) wamesaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya Zipline jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya kuanza kujenga vituo vya kurushia Drone za kusafirishia dawa kataka maeneo mbalimbali hapa nchini wakianzia na Mkoa wa Dodoma na Mwanza.

 akizungumza wakati wa kusaini na kubadilishana mikataba ya makubaliano, Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa  mradi huo umekuja wakati muafaka kutokana na ukuaji wa Teknolojia Bohari ya Dawa Tazania itapata urahisi wa kusambaza zawa katika vituo mbalimbali vya Afya.

Amesema kuwa  kwa kuanza mradi huo utaanza kwa kusambaza dawa ambazo zinaubaridi kama Damu katika vituo 200 vya mkoa wa Dodoma ambapo baada ya hapo watandelea na mikoa ya Kanda ya ziwa na baadae nchi nzima.

 Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Zipline, Keller Rinaudo,amesema kuwa Mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa nchini Rwanda na hapa nchini utaenda vyema zaidi pia amesema kuwa utatoa ajira nyingi kwa vijana wa kitanzania ambao watakuwa na mawazo mazuri ya ubunifu kwaajili ya kuendeleza kuenea mradi huo hapa nchini.
  
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa kusaini Mkataba kati ya wizara ya Afya, Bohari ya Dawa Taznania(MSD) na Kampuni ya Zipline kwaajili ya kuanza kufanya utafiti wa maeneo yatakayojengwa kwaajili ya sehemu ambapo Kampuni ya Zipline itakuwa ikirushia vifaa maalum ambazo ni Drone zitatumika kusambaza dawa katika mikoa maeneo ambayo ni ngumu kufikika kwa urahisi kutokana na umbali wake.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Zipline, Keller Rinaudo, akizungumza wakati wa kusaini Mkataba wa Makubaliano kuanza kujenga vituo kwaajili ya kurushia Drone ambazo zitakuwa zikisafirisa dawa kwenye maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi ikiwa mradi huo utaanza katika mikoa ya Dodoma na Mwanza. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt. Mpoki Ulisubisya, Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Zipline, Keller Rinaudo wakisaini mkataba wa kuanza kujenga vituo vya kurushia Drone zitakazo kuwa zikisafirisha dawa kwenye maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Bakari Kambi.
Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu wakibadilishana mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Zipline, Keller Rinaudo wakibadilishana kwaajili ya kuanza kujenga vituo vya kurushia drone zitakazo kuwa zikisafirisha dawa katika maeneo mbalimbali ya nchi. Ktikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya akisuhudia wanavyobadilishana mikataba hiyo jijini Dar es Salaam leo.

MKAZI WA LINDI ALAMBA KITITA CHA ZAIDI YA MIL 118/- M-BET

$
0
0
 Mshindi wa kitita cha zaidi ya shilingi milioni wa zaidi 118/- Erick Matey ambaye ni mkazi wa mkoa wa Lindi(kushoto)akikabidhiwa hundi yake na Afisa habari wa M-BET,David Malley(kulia)anaeshuhudia katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa  Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, James Mbalwe.
 Kaimu Mkurugenzi wa  Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, James Mbalwe(kulia) na Afisa habari wa M-BET,David Malley(katikati)wakimsikiliza mshindi waM-BET aliyejishindia zaidi ya shilingi milioni  118/- Erick Matey,Ambaye ni mkazi wa mkoa wa Lindi,Wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ya kumkabidhi mshindi huyo hundi yake aliyojishindia  kupitia mchezo wa kubahatisha Supper 12 unaoendeshwa na M-bet.
  Kaimu Mkurugenzi wa  Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, James Mbalwe(wapili kushoto) na Afisa habari wa M-BET,David Malley(kulia)wakimpongeza kwa kumpigia makofi mshindi wa zaidi ya shilingi milioni wa zaidi 118/- Erick Matey ambaye ni mkazi wa mkoa wa Lindi,Wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ya kumkabidhi mshindi huyo hundi yake aliyojishindia  kupitia mchezo wa kubahatisha Supper 12 unaoendeshwa na M-bet.
 Mshindi wa kitita cha zaidi ya shilingi milioni wa zaidi 118/- Erick Matey ambaye ni mkazi wa mkoa wa Lindi(kushoto)akiwaonesha hundi yake waandishi wa habari(hawapo pichani) Wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ya kumkabidhi mshindi hiyo aliyojishindia  kupitia mchezo wa kubahatisha Supper 12 unaoendeshwa na M-bet,Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa  Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, James Mbalwe na Afisa habari wa M-BET,David Malley.
 Mshindi wa kitita cha zaidi ya shilingi milioni wa zaidi 118/- Erick Matey ambaye ni mkazi wa mkoa wa Lindi,akiwa ameshikilia hundi yake mara baada ya kukabidhiwa rasmi leo wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ya kumkabidhi mshindi hiyo aliyojishindia  kupitia mchezo wa kubahatisha Supper 12 unaoendeshwa na M-bet.

Na Mwandishi wetu
MKAZI wa mkoa wa Lindi Mjini, Erick Matey mwenye umri wa miaka 26 ameibuka mshindi baada ya kubashiri vyema matokeo ya mechi kupitia Kampuni ya m-Bet na kujishindia zaidi ya Shilingi Milioni 118/-.

Matey amekabidhiwa fedha zake leo katika hafla  fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana

Kwa upande wake, Afisa habari wa  M-Bet, David Malley alisema kuwa Matey alifanikiwa kuzoa kitita hicho baada ya kufanikiwa kutabiri matokeo ya mechi 12 za ligi ya Ulaya kwa mtindo wa kucheza kawaida yaani super 12.

“Tunafarijika kumkabidhi Matey kitita hicho cha aidi ya Sh milioni 118/- akiwa ndiye mshindi wa m-Bet ambapo atapata Sh milioni 97/- baada ya makato ya kodi,” alisema Malley.

Aliwataka watanzania kuchangamkia kutumia mtandao wa intaneti kuonyesha ushabiki halisi wa soka akisema kuwa Perfect 12 ni mchezo wa ziada unaoruhusu kutabiri mechi 12 kwa Tsh 1,000 tu ambapo ukipatia zote  unaondoka na kitita chako mchana kweupe.

Naye Mshindi huyo, Erick Matey amewashauri watanzania wote wenye umri unaoruhusiwa kisheria kujitokeza kubashiri matokeo ya mechi mbalimbali kupitia Kampuni ya m-Bet .

"Nashukuru sana m-Bet kwa kuniwezesha kujikwamua kimaisha, nitatumia fedha hizi kutimiza ndoto yangu ya kununua kiwanja na kuanza ujenzi", alisema Matey

Kuhusu m-Bet, ni Kampuni iliyosajiliwa chini ya Sheria za Tanzania na kupewa leseni na Bodi ya Michezo ya kubahatisha tanzania kwa lengo la kufanya upatikanaji rahisi na mwingiliano wa huduma ya mchezo wa kubahatisha (Sim Betting) nchi nzima

“Kushiriki, ingia www.m-bet.co.tz, chagua kucheza kawaida au Perfect 12 ambapo kwa Shilingi 1000, unachagua matokeo 12. Ukipata yote sawa, unanyakua kikapu cha m-Bet,” alisema Malley.

IGP SIRRO AWASILI MKOANI TANGA KWA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima ya kijeshi baada ya kuwasili mkoani Tanga, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo, IGP Sirro amewataka askari kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akikagua kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) baada ya kuwasili mkoani Tanga, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo na kuwataka kufanyakazi kwa weledi na kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.

 Baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi katika mkoa wa Tanga, wakiwa kwenye gwaride la kumpokea Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, ambaye amewasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo ili kujua changamoto wanazokutana nazo wakati wakitekeleza majukumu yao ya kazi za Kipolisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto), akipokea taarifa kutoka kwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, SACP Benedict Wakulyamba (aliyesimama), mara alipowasili katika mkoa huo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo ili kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao ya kazi za Kipolisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto), akizungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo katika mkoa wa Tanga, wakati alipowasili mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kujua changamoto mbalimbali wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao ya kazi za kipolisi. 
Picha na Jeshi la Polisi.

WAZIRI KAIRUKI AZINDUA MPANGO WA ELIMU YA RUSHWA KUTUMIA MABASI YA UDART LEO.

$
0
0
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais MeneJementi ya Utumishi wa Umma na Uongozi Bora, Angelah Kairuki akikata utepe kuashiria uznduzi wa mpango elimu ya ruswa utakaornezwa na mabasi takribani 60 ya UDART. Pmoja naye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando na viongozi mbalimbali. 
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menegementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angelah Kairuki akipata uzoefu wa matumizi ya moja ya basi la UDART. 
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menegementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angelah Kairuki akimshukuru Msanii Mrisho Mpoto kwa kazi nzuri ya kufikisha ujumbe kwa jamii katika hafla ya uzinduzi huo. 
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menegementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angelah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa meza kuu pamoja na viongozi mbalimbali.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menegementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angelah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa meza kuu.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menegementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angelah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wa mapambano ya rushwa.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menegementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angelah Kairuki akibadilishana mawazo na Afisa Mtendaji mkuu wa UDART, Mhandisi Ronald Lwakatare.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menegementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angelah Kairuki akiaga baada ya kuhitimisha shughuli ya uzinduzi huo. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogspot)
Msanii Mrisho Mpoto kiongozi Mrisho Band akiotumbuiza na wasanii wake wakati wa uzinduzi wa mpango huo jijini Dar es Salaam leo.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Uongozi Bora, Angelah Kairuki (katikati) wageni wa meza kuu wakifuatilia ujumbe uliokuwa ukitolewa na wasanii katika uzinduzi huo. 
Wageni wakifuatilia ujumbe uliokuwa ukitolewa na wasanii katika uzinduzi huo.
Wageni wa wakifuatilia uzinduzi huo.
Wasanii wa kundi la Amani na Upendo wakiburudisha katika uzinduzi huo.



KINANA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI TANO ZA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA, LEO, JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akiwa katika mazungumzo na Mabalozi wa nchi tano za Ukombozi Kusini mwa Afrika, wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini, alipokutana nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mabalozi hao ni wa nchi za Zimbambwe, Zambia, Namibia, Msumbiji na Afrika Kusini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati), akiwa na Mabalozi wa nchi tano za Ukombozi Kusini mwa Afrika, wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini, baada ya mazungumzo nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mabalozi hao ni wa nchi za Zimbambwe, Zambia, Namibia, Msumbiji na Afrika Kusini. 
PICHA: BASHIR NKOROMO. KWA PICHA ZAIDI ZA KIKAO HICHO/>BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MZEE WASIRA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Stephen Wasira leo ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WAHALIFU MTANDAONI

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliokutanisha Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kupata elimu juu ya Sheria ya Usalama wa Mitandao, Utekelezaji wake na namna ya kuchukua tahadhari, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Hamza Juma (wa pili kulia), akizungumza na wajumbe wa Kamati na watendaji wa TCRA katika ziara ya kikazi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani.
Mwanasheria Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Philip Filikunjombe akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar inayohusu Sheria ya Usalama wa Mitandao. Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam ulikuwa na lengo la kutoa elimu juu ya Sheria ya Usalama wa Mitandao, utekelezaji wake na namna ya kuchukua tahadhari .
Wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakisikiliza mada iliyokuwa inawasilishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Barnabas Mwakalukwa (hayupo pichani), wakati wa ziara ya kikazi katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam.

…………………………………………………………………..

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, ametoa onyo kali kwa wale wanaofanya uhalifu kwa njia ya mtandao kuchukua tahadhari kwani hawapo salama na kuahidi kuwashughulikia kwa mujibu wa Sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, katika mkutano uliokutanisha uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Naibu Waziri Ngonyani amesisitiza kuwa serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini wamendelea kufanya doria katika mitandao ili kubaini watu ambao wanatumia vibaya mitandao.

“Tutumie mitandao kwa ajili ya kuleta maendeleo na si kinyume chake kwani ukifanya uhalifu wowote kwa njia ya mtandao tutakukamata popote ulipo na kukuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria”, amesema Eng. Ngonyani.

Aidha, Naibu Waziri Ngonyani amewataka wananchi kutumia kikoa cha Tanzania (.tz), na Kituo Mahiri cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC), kwa ajili ya kuhifadhi taarifa zao ili zisiingiliwe kwa urahisi na kuweza kuibiwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Hamza Juma, ameitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa jamii kuhusu masuala ya matumizi ya mtandao kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.

“Nawaomba TCRA na vyombo vya habari nchini msaidie kusambaza elimu hii kwa wanachi ili waweze kupata uelewa wa masuala ya matumizi salama ya mtandao na changamoto zake”, amesisitiza Mhe. Juma.

Kwa upande wake Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Barnabas Mwakalukwa, ametoa onyo kali kwa wale wanaotumia mitandao vibaya katika kuleta uchochezi wa kidini, kisiasa na kutumia majina ya viongozi na watu maarufu kwa ajili ya kufanya utapeli kuacha mara moja kwani Jeshi la Polisi litahakikisha linachukua hatua kali za kisheria dhidi yao.

Amewataka wananchi kuwa tayari kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zinazohusu uhalifu wa kimtandao ili kuweza kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kwani suala la ulinzi na usalama ni letu sote.

Tangu kuanzishwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 kumewezesha Jeshi la Polisi nchini kufuatilia kwa karibu na kushughulikia uhalifu mtandaoni ambapo kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Juni, 2017 Jeshi la Polisi limeweza kukamata watuhumiwa 315, kufikisha mahakamani kesi 153, kesi 19 zilipatikana na hatia na zingine zipo chini ya upelelezi.

DKT. ALOYCE NZUKI AFUNGUA WARSHA YA KUKUSANYA MAONI YA WADAU WA KANDA YA KATI KWA AJILI YA KUPITIA UPYA SERA YA TAIFA YA UTALII YA MWAKA 1999 MJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii Tanzania mjini Dodoma leo. 

Dkt. Nzuki amesema ipo haja sasa kwa Sekta za Umma kuona umuhimu wa kuwekeza moja kwa moja katika biashara ya utalii nchini hususani katika huduma za malazi na usafiri ili kuiwezesha Serikali kupata mapato ya moja kwa moja na kuongeza zaidi kwenye pato la taifa. 

Alisema kwa kuimarisha usafiri wa anga kutawezesha usafiri wa watalii moja kwa moja kutoka kwenye soko na kuwaleta nchini huku wakilipia gharama zote hapa nchini tofauti na hivi sasa ambapo baadhi ya makampuni ya nje hulipwa fedha kiasi nje ya nchi na hivyo kuikosesha Serikali mapato kupitia ushuru unaotozwa na TRA. 

Alisema sio lazima Serikali iwe inasimamia moja kwa moja utoaji wa huduma hizo kwa kuwa upo uwezekano wa kutumia makampuni makubwa hata ya nje ya nchi kuja kuendesha huduma hizo kwa ufanisi zaidi hapa nchini.  
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) na wadau wengine wa sekta ya utalii wakimsikiliza Prof. Raphael Mwalyosi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kulia) wakati akiwasilisha mada kuhusu Hoja ya Marekebisho ya Sera ya Utalii ya Mwaka 1999 katika warsha ya kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya kupitia upya Sera hiyo iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii mjini Dodoma leo.
Kamu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deograsias Mdamu akizungumza katika warsha ya siku moja ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii Tanzania mjini Dodoma leo. 
Picha ya pamoja ya Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (katikati waliokaa) na wadau wa sekta ya utalii katika warsha ya siku moja ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii Tanzania mjini Dodoma leo.
Baadhi ya wadau wa sekta ya utalii wakisikiliza moja ya mada katika warsha ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta hiyo kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii Tanzania mjini Dodoma leo. 
 Baadhi ya wawezeshaji wa hafla hiyo ambao ni Maafisa Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakisikiliza moja ya mada katika warsha hiyo. 
Baadhi ya wadau wa warsha hiyo wakisikiliza hotuba ya ufunguzi ya Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki. 
 Baadhi ya wadau wa warsha hiyo.
Baadhi ya Washiriki wa warsha hiyo kutoka Mikoa ya Kanda ya Kati iliyofanyika mjini Dodoma. (NA HAMZA TEMBA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)
HOTUBA YA UFUNGUZI YA NAIBU KATIBU MKUU, WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, DKT. ALOYCE NZUKI

HOTUBA YA KAIMU MKURUGENZI IDARA YA UTALII, DEOGRASIAS MDAMU

NEEMA YA UPATIKANAJI WA MAJI YA KUTOSHA DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amefanya ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa Maji ya kutosha kwa Wakazi wa Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo Makonda ametembelea Ujenzi wa Vituo vya Usambazaji wa Maji, Visima pamoja na maeneo yatakayojengwa mifumo ya kisasa ya kusafirisha na kutibu Maji taka.

Makonda amesema lengo la Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli ni kumtua Mama Ndoo kichwani na kuhakikisha huduma ya Maji inawafikia Wananchi wote.

Amesema kukamilika kwa miradi ya Ujenzi wa Vituo Vinne vikubwa vya usambazaji wa Maji vinavyojengwa maeneo ya Changanyikeni, Makongo, Wazo na Bunju*vitasaidia kuzalisha Maji ya kutosha na kutatua kero kwa Wananchi.

Katika ziara hiyo pia Makonda ametembelea Visima 10 ambavyo aliahidi kwenye Ziara ya Dar Mpya ambavyo Ujenzi wake umekamilika vikiwa na uwezo wa kuzalisha Lita 16,000 kwa kila kisima ambavyo vitahudumia wakazi wa Wilaya ya Ubungo.

Aidha Makonda ametembelea eneo la Jangwani ambapo 
kutajengwa Mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha Bilion 200 na eneo la Kilongawima Mbezi Beach kunakojengwa mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha Bilion 135 chini ya ufadhili wa Bank ya Dunia na Serikali ya Japan.

Hata hivyo amesema bado Serikali inaendelea kufanya jitiada za kuhakikisha Wakazi wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke wanapata maji ya kutosha kupitia miradi mbalimbali inayoendelea.

Amewataka Wananchi ambao bado hawajaunganishwa na huduma ya Maji kufika Ofisi za DAWASCO ili waunganishiwe Maji bila malipo ambapo baada ya hapo watawekewa utaratibu wa malipo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama  Ujenzi wa moja ya Vituo vya Usambazaji wa Maji, Visima pamoja na maeneo yatakayojengwa mifumo ya kisasa ya kusafirisha na kutibu Maji taka.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama mambo ya kupitishia maji ikiwa ni pia sehemu ya miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo mafupi juu ya muundo mzma mzima wa miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akishiriki kuchimba mtaro wa kupitisha bomba la maji ikiwa ni sehemu ya miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images