Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

RAZA AMWAGA ZAWADI MICHEZO YA MASKULI MIKOA

0
0
Mwenyekiti wa ZAT ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe. Mohammedraza Hassanali akimkabidhi kalkuleta Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Omar Ali Bhai kwa ajili ya washindi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa skuli za mikoa yote ya Unguja na Pemba inayotarajiwa kuanza Septemba 12, 2017 katika uwanja wa Amaan Mjni Unguja. 
Mkurugenzi Idara ya Michezo na Utamaduni Hassan Khairalla Tawakal akitoa shukurani kwa Mhe. Raza kwa msaada alioutoa kuwazawadia washindi wa michuano ya mpira wa miguu kwa skuli za mikoa ya Zanzibar itakayofanyika mwezi ujao mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.
Mkurugenzi Idara ya Michezo na Utamaduni katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Hassan Khairalla Tawakal, akimtambulisha Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa wizara hiyo Omar Ali Bhai kwa Mwenyekiti wa kampuni ya ZAT Mhe. Mohammedraza Hassanali.

Na Salum Vuai, MAELEZO

MKURUGENZI wa kampuni ya usafiri wa anga na huduma za viwanja vya ndege Zanzibar (ZAT) Mohammedraza Hassanali, ametoa wito kwa kampuni na taasisi mbalimbali kuunga mkono juhudi za serikali kuimarisha michezo maskulini.

Akizungungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vitu mbalimbali kwa ajili ya zawadi za washindi kwenye mashindano ya mpira wa miguu mikoa ya Unguja na Pemba iliyofanyika nyumbani kwake Kibweni, Raza alisema ni wajibu wa kila Mzanzibari kusaidia sekta ya michezo.

Alifahamisha kuwa, iwapo wafanyabiashara wa Zanzibar wataunganisha nguvu kwa lengo la kuinua michezo kuanzia ngazi ya skuli ambako ndiko kwenye msingi wa vipaji vizuri, nchi hii itafika mbali kimichezo na kulitangaza vyema jina la Zanzibar. 

“Hii ninchi yetu sote, tuna wajibu kusaidia juhudi za serikali, na nimpongeze Mhe. Rais kwa kuteua Mkurugenzi makini na mwenye jitihada kuongoza Idara ya Michezo na Utamaduni,” alieleza Raza.

Raza ambaye pia ni Mwakilishi wa jimbo la Uzini, alisema hatachoka kutoa msukumo katika sekta ya michezo na misaada mingine ya kijamii, na vitu hivyo alivyotoa ni kutimiza ahadi yake aliyoitoa kabla mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Katika hafla hiyo, Mkurugenzi huyo alikabidhi vityu mbalimbali kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Omar Ali Bai kwa ajili ya zawadi za washindi na washirikiwenmgine wa mashndano hayo yaliyopangwa kuanza Septemba 12, 2017 katika uwanja wa Amaan.

Mkurugenzi Bai aliyemuwakilisha Katibu Mkuu wa wizara yake Bi. Khadija Bakari Juma, akimshukuru Mhe. Raza, alisema kuwekeza katika michezo maskulini ni jambo muhimu kwa kuinua ufahamu wa wanafunzi masomoni.

Alisema dhana za watu wanaodhani mchezo inarejesha nyuma maendeleo ya masomo sio sahihi, kwani ushahidi duniani unaonesha wanafunzi wengine mahodari wamekuwa wakijikita kucheza michezo mbalimbali.

“Akili nzuri hutoka kwenye mwili wenye afya ambao kujengeka kwake kunatokana na mtu kujishughulisha katika michezo ambayo wataalamu wanasema ni sehemu bora kwa makuzi ya watoto”, alieleza.

Alimuahidi mfadhili huyo kwamba vitu vyote alivyovitoa vitafika kwa walengwa, huku akiwaomba wananchi wengine wenye uwezo, makampuni na wafanyabsiahara mbalimbali kushirikiana ili Zanzibar irejeshe hadhi yake michezoni ambayo kwa miaka ya karibuni imeonekana kutetereka.

Mapema, Mkurugenzi wa Idara ya Michezo na Utamaduni katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, alimshukuru Raza kwa moyo wake wa uzalendo, na kuwa tayari kutumia mali zake katika kujenga ustawi wa nchi.

Alisema kuwa Rais Dk. Shein amepania kwa dhati kuendeleza michezo kama anavyofanya katika mambo mengine, na akamsifu Raza kwa kuwa kiungo kizuri kati ya idara yake wanafunzi na watu wengine katika kuhakikisha michezo nchini inapiga hatua. 

Katika hafla hiyo, Raza alikabidhi kalkuleta za kisasa, madishi ya kuhifadhia chakula na kalamu huku akiahidi kufanya mambo mengine makubwa kwa ajili ya kuwashajiisha washiriki wa mashindano hayo ya mikoa sita ya Unguja na Pemba.

DKT. PALLANGYO AONGOZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI ZIARA KATIKA MIRADI YA GESI LINDI

0
0
Msimamizi wa Uzalishaji na Ujenzi katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Said Ngongoki akielezea jinsi uzalishaji unavyofanyika kiwandani hapo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti mara walipofanya ziara kiwandani hapo
Meneja Rasilimaliwatu kutoka katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Msafiri Figa ( wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika eneo la uzalishaji la kiwanda hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akibadilishana mawazo na mwakilishi kutoka Idara ya Biashara katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Emily Wu (kulia) katika eneo la uzalishaji la kiwanda hicho.
Mtaalam kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Dominick Ngunyali (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya jinsi gesi inavyopokelewa katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika eneo la kupokelea gesi hiyo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele kulia) akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye ziara katika eneo la Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.
Meneja Rasilimaliwatu kutoka katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Msafiri Figa (kushoto) akielezea jinsi udongo wa aina mbalimbali unavyochanganywa katika hatua za awali za maandalizi ya utengenezaji wa vigae (tiles) kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa Mitambo katika Kituo za Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi cha Somangafungu kilichopo mkoani Lindi, Edwin Konyani katika ziara hiyo.
Msimamizi wa Bomba la Gesi Upande wa Umeme katika Kituo cha Kupokea Gesi kutoka Songosongo na Madimba Joseph Msafiri (katikati) akielezea jinsi  gesi inavyopokelewa katika kituo hicho kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika ziara hiyo.
Sehemu ya Kituo cha Kupokea Gesi kutoka Songosongo na Madimba kilichopo Somangafungu mkoani Lindi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ameongoza Kamati y Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika maeneo mbalimbali yenye miradi ya gesi katika mkoa wa Lindi lengo likiwa ni kuona utekelezaji wa miradi hiyo. 

Kati ya maeneo waliyotembelea ni pamoja na Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia cha Somangafungu, Makutano ya Bomba la Gesi Asilia (Somangafungu) mkoani Lindi pamoja na eneo linalotarajiwa kujengwa Mitambo ya Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) lililoko katika Manispaa ya Lindi.

MAHUJAJI WA TANZANIA WAANZA KUWASILI SAUDI ARABIA

0
0
Na Mwandishi Maalum, Riyadh, Saudi Arabia.
Mahujaji kutoka Tanzania wameanza kuwasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza nguzo ya tano ya dini ya kiislamu ya kuhiji Makkah inayofanywa na watu mbalimbali duniani, wakiwamo Waislamu kutoka Tanzania.
Baadhi ya mahujaji wakionekana Uwanja wa Ndege baada ya kuwasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya swala ya Hija.
Mahujaji kutoka Tanzania wakiwa wamewasili nchini Saudi Arabia.
Baadhi ya Waislamu wanaoendelea kuwasili nchini hapa wakionekana pichani.
Ibada ya Hijja mwaka huu inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti hadi mwanzoni mwa mwezi Septemba, huku jumla ya mahujaji 977 kutoka Tanzania wameshawasili katika miji ya Madina na Jeddah. Mahujaji hao waliwasili katika viwanja vya ndege vya Madina na Jeddah na kupokelewa na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania.

Tanzania kwa mwaka huu inataraijiwa kupeleka mahujaji wapatao 2,700. Indonesia ndiyo nchi inayoongoza kwa kupeleka mahujaji wengi mwaka huu inatarajiwa kuwa na mahujaji wapatao 168,000. Mwaka huu Saudi Arabia inatarajiwa kupokea mahujaji zaidi ya 2,000,000 kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni.

KHERI YA SIKU YA KUZALIWA MDAU MC BARAKA

0
0
Leo Aug 23 ni siku ya kuzaliwa kwake Blogger Mc Baraka #Bukobawadau napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mola kwa kuendelea kunijalia mpaka kufika hapa nilipo.

Shukrani kwa Wazazi/Walezi kwa yote.Nathamini na kukumbuka mengi sana hasa Maneno yenu/Wosia,Upendo ,Ukarimu na Faraja zenu ...Sina lakusema zaidi ya Asanteni na nawaombea kila jema,Inshallam Mwenyezi Mungu azidi kuwajalia afya njema

Shukrani za dhati kwa Ndugu,Jamaa,Marafiki, kwani kwenye Safari ya Maisha yangu nimekutana Ndugu wengi ambao si wakuzaliwa nao kutoka Tumbo Moja /Ukoo mmoja,Lakini kwangu nawathamini sana natambua sana uwepo wenu ,Ni vigumu kutaja kila mmoja lakini wenyewe mnajijua kwa pamoja nasema Nawapenda sanaaa.!Na namshukuru Mungu kwa kunipa watu...!!

WAZIRI MAHIGA AMPOKEA WAZIRI WA NCHI WA UINGEREZA AMBAYE YUPO ZIARANI NCHINI

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza, Mhe. Stewart Rory alipofika Wizarani tarehe 22 Agosti, 2017 kwa ajili ya mazungumzo rasmi na Waziri Mahiga. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Uingereza. Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lale la Kimataifa la Maendeleo (DFID) inaisadia Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Maji, Elimu, Nishati Mbadala na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya. Mhe. Stewart yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 22 na 23 Agosti, 2017. 
Sehemu ya ujumbe ulioambatana na Mhe. Stewart. Kulia ni Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Sarah Cooke, Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID), Bi. Beth Arthy na Afisa kutoka Ubalozini. 
Sehemu ya ujumbe wa Wizara wakati wa mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Waziri Stewart kutoka Uingereza (hawapo pichani). Kushoto ni Bw. Salvatory Mbilinyi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Bw. Joseph Kapinga, Afisa Mambo ya Nje. 
Waziri Mahiga akiagana na mgeni wake Mhe. Stewart mara baada ya kumaliza mazungumzo yao .
Picha ya pamoja 
Waziri Mahiga kwa pamoja na Mhe. Stewart wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu lengo la ziara ya Mhe. Stewart nchini.

ETIHAD AVIATION GROUP RECOGNISES PARTNERSHIP WITH WOMEN FOR EMIRATI WOMEN’S DAY

0
0
  •    Women account for 51 per cent of Etihad Airways’ 13,000 employees
  •    51 per cent of all UAE nationals in Etihad Aviation Group are female
Etihad Aviation Group (EAG) is celebrating the third annual Emirati Women’s Day with a series of events to highlight this year’s theme, Women are partners in giving, in line with the UAE’s 2017 Year of Giving initiative.
Women comprise 36 per cent of EAG’s nearly 26,000-strong workforce, working alongside men in what are traditionally regarded as male professions such as engineering, the flight deck and cargo. Emirati women are also well represented in these functions, with several of them sharing their experiences at panel discussions held at the Etihad Airways Headquarters today.
Technical Engineer Mariam Al Obaidli’s talent and passion were identified by the company four years ago when she was offered the opportunity to join the Etihad Airways Technical Engineer Programme, as part of the airline’s investment in the development of UAE national capabilities.
Today, she is one of 42 Emirati women completing their two-year, on-the-job training in order to obtain their GCAA Aircraft Engineering Licenses.
Nowadays Mariam wakes up at 4am to be at Etihad Airways Engineering for the daily meeting at 5.30am and she couldn’t be happier. “You should see the engineers’ expressions when they see local women working hard in such extreme conditions, and knowing that we want to be here – they’re amazed by it,” she recounted for the audience.
Mariam was joined on the panel by an Etihad lawyer, pilot, and airport manager, who shared their own experiences of partnership with the audience.
“Our constitution declares that men and women are equal in their rights and obligations. It provides equal access to education, healthcare and jobs. Her Highness, the mother of our nation, is the champion of our success, securing our indispensable role as an active driving force in the nation’s sustainable development,” Amina Taher, Vice President of Corporate Affairs, Etihad Aviation Group said.
“As a company, we foster the talents of our women and men; we encourage them to work together to promote innovation, to mentor their junior colleagues, to volunteer in the community and to give to charity. In a corporate environment, it is also important we stand together to develop not just our company, but the UAE and our society.”
Guest speaker Dr. Khawla al-Saadi, Chairwoman of the Emirates Autism Society, will address staff at a special workshop on 29 August. This workshop will explore the notion of giving through showcasing successful female leaders and managers, both within the company and outside, who, despite the challenges of balancing career and family, also devote time to mentoring young women as they embark on their careers.
Speaking about Emirati Women’s Day, Dr. Khawla al-Saadi said: "The women of our beloved country have delivered remarkable successes under the leadership and support of Her Highness Shaikha Fatima Bint Mubarak, Chairwoman of the UAE General Women’s Union, Supreme Chairwoman of the Family Development Foundation and Chairperson of the Supreme Council for Motherhood and Childhood, for women’s issues and aspirations.
“Women are Partners in Giving’ is not just a slogan. It conforms with our capacity to implement the directives of our leadership in the past and today. Our role is not only to take part in building our nation, but to play a vital role in its evolution too. We will always promote giving around the nation and abroad, and to reach out to people who need help wherever they are.”
Etihad Aviation Group employs 2,859 Emiratis – 1,462 women and 1,394 men – in the UAE and around the world.

 Emirati Women come together at Etihad Aviation Group’s  Head Quarter in Abu Dhabi to celebrate Emirati  Women’s Day by hosting a special event at the EAG in Abu Dhabi.


SERIKALI KUANZA KUTOA LESENI MPYA KWA MAGAZETI NA MAJARIDA NCHINI

0
0

SERIKALI imesema inaanza kutoa leseni mpya za machapisho mbalimbali ikiwemo magazeti na majarida yote nchini ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kifungu cha 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 unaokwenda pamoja na Kanuni ya 7 ya Kanuni za Sheria ya Huduma za Habari za mwaka 2017 zilizochapishwa kwa mujibu wa tangazo la Serikali na 18 la Februari 3, 2017.

Akizungumza katika Mkutano na Wanaandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema kuwa utoaji huo wa leseni kwa machapisho yote umeanza rasmi leo Agosti 23, 2017 na utafikia tamati Octoba 15, 2017 na magazeti yote yahakikishe yanakamilisha taratibu ya kupatia leseni mpya kwa kipindi hicho, na baada ya muda huo hawataruhusiwa kuyachapisha kwani watakuwa wanatenda kosa kisheria.


Dkt. Abbas amesema, kwa mujibu wa sheria, utaratibu huu wa sasa unafuta mfumo wa awali wa utoaji wa Hati za Usajili wa magazeti na majarida uliokuwa ukitumika kwa mujibu awali kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.

Fomu za maombi, akaunti ya kulipia pamoja na orodha ya nyaraka zinazohitajika kwa ajili ya usajili huo, vinapatikana kuanzia saa katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO za jijini Dar es salaam na Dodoma au katika sehemu ya "Huduma Zetu" katika tovuti ya Idara hiyo BOFYA HAPA.
Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas akizungumza katika Mkutano na Wanaandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo.

PROF. ELISANTE AWATAKA MAAFISA UTAMADUNI KUTANGAZA VIVUTIO VYA KIUTAMADUNI VILIVYOPO KATIKA MIKOA YAO

0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro jana wakati wa ziara yake ya kikazi ambapo aliwataka watumishi wawe na utamaduni wa kufanya kazi  kwa kushirikiana na wananchi.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo akieleza umuhimu wa filam katika kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ukumla wakati wa kikao na Maafisa Utamaduni na watendaji wa Mkoa wa Morogoro. 
 Wajumbe wa kikao wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (Hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi jana mkoani Morogoro.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na baadhi ya Wazee wa kimila wa Mkoa wa Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi jana Mkoani hapo. 
Baadhi ya wazee wa kimila wa Mkoani Morogoro wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel          (Hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi jana mkoani hapo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (Kulia) akimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Utawala na Fedha Dkt. Yonika Ngaga (kushoto) alipotembelea makaburi ya Wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini yaliyopo Mazimbu Morogoro wakati wa ziara yake ya kazi jana mkoani hapo.  
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa fundi bombo Idara ya Matengenezo Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Bw. Ally Mkopi alipotembelea makaburi ya Wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini yaliyopo Mazimbu mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kazi jana mkoani hapo.

(Picha na Lorietha Laurence –WHUSM).

SERIKALI KUONDOA KABISA MFUMO WA ZAMANI WA MALIPO YA KODI YA ARDHI NCHI NZIMA

0
0
 Afisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bwana Haruna Kiyungi akieleza jinsi ya kutumia Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi/kielektroniki
 Afisa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi Bwana David Malisa (katikati) akitoa mafunzo kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya Ziwa jinsi ya kutumia Mfumo wa GePG
 Afisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Joines Mhalila akielekeza jinsi ya kutumia simu katika kufanya malipo ya kodi ya ardhi.
  Afisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bwana Haruna Kiyungi akionesha kwa vitendo jinsi ya kutumia Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi/kielektroniki.


Na. Hassan Mabuye
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishirikiana na Wizara ya Fedha, imesambaza maafisa wake katika halmashauri 169 kote nchini.

Maafisa hawa wanaotoa mafunzo katika vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi na tozo nyingine kwa kutumia simu ya mkononi ili kuondoa kabisa mfumo wa zamani wa malipo.

Zaidi ya maafisa 170 kutoka makao makuu ya Wizara ya Ardhi, Wizara ya Fedha na kutoka kanda nane za ardhi wameanza kutoa elimu hiyo katika halmashauri na vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi ili kurahisisha ulipaji kodi ya ardhi kwa wananchi kwa kutumia simu zao na kuondoa usumbufu.

Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi ni mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi ambao utamrahisishia mwananchi kulipia popote walipo kwa kutumia simu zao kwa urahisi zaidi.

Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kupatiwa hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Ili kujua unadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi kwa kutumia simu ya mkononi bonyeza *152*00# au kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi yaani sms halafu unatuma kwenda namba 15200 na baada hapo unaweza kulipia kwa njia ya Mpesa, Tigo Pesa au kulipia tawi lolote la benki ya NMB na CRDB.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo huu wa kielektroniki wa GePG katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini na kuondoa kabisa mfumo wa zamani.

Mfumo huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Mmiliki wa kipande cha ardhi ataweza kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.

Kwa majaribio ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na baada ya mafanikio makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa mikoani.

Kwa zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika daftari la msajili (official search), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.

Kwa sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini.

DKT. PHILIP MPANGO ATEMBELEA KIWANDA CHA KUUNGANISHA MATREKTA YA URSUS-KIBAHA

0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (katikati) akiwasili katika kiwanda cha kuunganisha Matrekta ya URSUS-TAMCO, kilichoko Kibaha mkoani Pwani kuangalia kazi ya uunganishaji matrekta zaidi ya 200 pamoja na kusikiliza changamoto zinazoukabili mradi huo.

Na. Benny Mwaipaja-Kibaha

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametembelea mradi wa kuunganisha matrekta ya Ursus, uliopo Kibaha mkoani Pwani na kusisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuendeleza kilimo nchini ili kukuza sekta ya viwanda.

Tayari Matrekta 204 yenye uwezo wa HorsePower 50 yamekwisha unganishwa yakisubiri kuuzwa kwa watumiaji hatua ambayo Dkt. Mpango amesema itaongeza tija katika kilimo na kukuza ajira hususan kwa kundi kubwa la vijana.

Ameahidi pia kuwa Serikali itayafanyiakazi haraka maombi ya Shirika la Maendeleo la Taifa NDC la kutaka kupata kibali cha kuajiri zaidi ya wafanyakazi 90 watakaohusika na mradi huo pamoja na kutoa shehena ya Matrekta 267 yaliyokwama katika Bandari ya Dar es Salaam ili yaweze kuuzwa kwa wananchi kuendeleza kilimo.

 Kwa upande wake, Meneja wa Mradi huo kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa-NDC, Mhandisi Adam Mbura, amesema mradi huo utahusisha pia uanzishwaji wa vituo vinane katika kanda mbalimbali kwa ajili kuuza matrekta, zana na vifaa vingine pamoja na  kutoa huduma kwa wateja.

Amesema kuwa kukwamuliwa kwa makontena 64 yaliyokwama bandarini yakiwa na matrekta hayo 267 pamoja na vipuri vya kuunganisha Matrekta hayo pamoja na baadhi yaliyopo katika eneo la Mradi la TAMCO, Kibaha mkoani Pwani, kutawezesha kukamilisha haraka kwa kazi hiyo.

Baadhi ya vijana wanaofanyakazi katika mradi huo wamesema kuwa wamenufaika na ujuzi wanaoupata kutoka kwa wataalamu wa ufundi kutoka nchini Poland na kuahidi kuuendeleza ujuzi huo kwa vijana wenzao ili mradi huo uweze kuwa na manfaa kwa kutatua changamoto mbalimbali za kiufunsi zitakazokuwa zikiwakabili wakulima

Mradi wa kuunganisha Matrekta ya URSUS-TAMCO, Kibaha Mkoani Pwani unafadhiliwa na Serikali ya Poland ambapo kiwanda kikubwa cha kuunganisha matrekta kinatarajiwa kujengwa katika eneo hilo na yatauzwa kwa gharama nafuu, kati ya shilingi milioni 38 hadi milioni 42 kulingana na ukubwa na uwezo wa trekta.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango akiwasha moja ya matrekta yaliyounganishwa katika Mradi wa Kuunganisa Matrekta ya URSUS-TAMCO, uliopo katika eneo la Kibaha mkoani Pwani, alipotembelea mradi huo.
Meneja Mradi wa Kuunganisha Matrekta ya URSUS, Kibaha mkoani Pwani, Mhandisi Adam Mbura, akimweleza Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, moja ya majembe yaliyounganishwa kupitia mradi huo.
Mafundi pekee wa kike katika Mradi wa Kuunganisha Matrekta ya URSUS katika eneo la Kibaha Mkoani Pwani, Bi. Fatma Abbass (kulia) na Rahabu Japhet wakisikiliza wosia na maelekezo kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, (hayupo pichani) alipotembelea Mradi huo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (aliyevaa tai) akiwa katika picha ya pamoja na vijana mafundi wanaounganisha matrekta katika Mradi wa kuunganisha Matrekta ya URSUS, kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, (kushoto) akizungumza na Meneja Mradi wa kuunganisha Matrekta ya URSUS, Mhandisi Adam Mbura, (katikati) katika eneo la mradi huo uliopo Kibaha mkoani Pwani ambapo tayari matrekta 204 yameunganishwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo ambapo zaidi ya matrekta 2,400 na zana zake yanatarajiwa kuunganishwa, wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alipofanya ziara kwenye mradi huo.
Sehemu ya matrekta 204 yaliyounganishwa katika Mradi wa Kuunganisha Matrekta ya URSUS-TAMCO, katika eneo la Kibaha mkoani Pwani.

WAJUMBE WA CPA TAWI LA TANZANIA WAKUTANA NA WAJUMBE WA CPA TAWI LA CANADA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
   Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya  Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania Dkt Raphael Chegeni (katikati) akiongoza kikao wakati Wajumbe wa Kamati hiyo walipokutana na Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada  katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo.
 Mwenyekiti  wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada  Mhe. Yasmin Ratansi (wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo wakati Wajumbe wa Chama hicho kutoka Canada walipokutana na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya  Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Mhe. Yasmin Ratansi akimkabidhi  zawadi Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya  Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania Dkt Raphael Chegeni mara baada ya Wajumbe wa pande zote mbili kuzungumza mapema leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati Tendaji ya  Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania katika picha ya pamoja na Wajumbe wa   Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada mara baada ya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
        (Picha na Ofisi ya Bunge)

Tanzania yapata Msaada wa Shilingi Trilioni 1 kutoka Uingereza

0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe. Rory Stewart alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu   Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID) nchini  Bi. Elizabeth Arthy  aliyeongozana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe. Rory Stewart pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke walipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mazungumzo na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe. Rory Stewart pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke walipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana  na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe. Rory Stewart akiwa na Mkuu   Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID) nchini Bi. Elizabeth Arthy pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana  na akiwa na Mkuu   Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID) nchini Bi. Elizabeth Arthy aliyeongozana na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe. Rory Stewart pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari baada ya kufanya mazungumzo  Waziri wa Mambo ya Nje wa uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe. Rory Stewart akiwa na Mkuu   Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID) nchini Bi. Elizabeth Arthy pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017.Picha na IKULU

Rais Magufuli amteua Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi kuwa Kamishna wa Operation wa Mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya

0
0

WAZIRI MKUU AWAKARIBISHA WACUBA KUJENGA VIWANDA TANZANIA

0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Balozi Lucas Domingo Polledo, ambapo amewakaribisha wafanyabiashara wa Cuba kuja kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa. 

Amesema kwa sasa Serikali ya Tanzania inaagiza dawa kutoka nje ya nchi jambo ambalo linasababisha kutumia fedha nyingi, hivyo uwepo wa kiwanda utasaidia katika kupunguza gharama. Pia wawekezaji watakuwa na uhakika wa soko la bidhaa zao. 

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumanne, Agosti 22, 2017) wakati akizungumza na Balozi Polledo mjini Havana. Waziri Mkuu yuko nchini Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. 

Alisema Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda nchini kama mkakati wa kukuza uchumi na kufikia uchumi wa kati, hivyo wafanyabiashara kutoka nchini Cuba wanakaribishwa kuja kuwekeza nchini, hususani katika viwanda vya dawa na sukari. 

Waziri Mkuu alisema licha ya Tanzania kuwa ni nchi ya amani na yenye utulivu wa kisiasa, pia imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji jambo ambalo litawawezesha watakaokuja kuwekeza nchini kupata tija. 

Pia alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Cuba kwa ushirikiano mzuri na Serikali ya Tanzania kwa sababu Cuba ni mojawapo kati ya nchi zenye ushirikano wa muda mrefu na Tanzania hususani katika masuala ya Kisiasa, Kijamii, Kielimu na Kiuchumi. 

“Tanzania na Cuba zina historia ya kutosha. Tunatambua mahusiano mazuri yaliyopo kati nchi zote mbili, ambayo yalikuwepo kuanzia Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere.” 

Kwa upande wake, Balozi Polledo alisema Serikali ya Cuba itahakikisha uhusiano wake na Serikali ya Tanzania unaendelea kuimarishwa. Pia alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo pamoja na kukuza uchumi. 

Alisema licha ya kuwahi kufanya kazi kama Balozi katika nchi mbalimbali za Afrika, baada ya kufika Tanzania amefurahishwa na kasi ya ukuaji wa uchumi pamoja na kuimarika kwa hali ya siasa na amani.”Hali hii ni tofauti na mataifa mengine ya Afrika.” 

Pia Balozi Polledo alisema kwamba Serikali ya Cuba itaendelea kushirikiana na Tanzania katika uboreshaji wa Sekta za Afya na Elimu, ambapo alisema jumla ya madaktari 50 wa Cuba wakiwemo maprofesa 11 wako nchini wakihudumia wananchi katika mikoa mbalimbali. 


IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMATANO, AGOSTI 23, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akisalimiana na Balozi wa Cuba Nnchini Tanzania Bwana Lucas Domingo Polledo walipo kutana kwa mazungumzo ya kikazi jana August 22/2017 akiwa katika ziara ya kikazi Havana Cuba. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

SERIKALI YARIDHIA WAATHIRIWA WA JANGA LA MOTO SOKO LA SIDO KUENDELEA KUBAKI KATIKA ENEO LAO,NAIBU SPIKA ACHANGIA MILIONI KUMI

0
0
Baada ya Soko la Sido kuteketea kwa moto,hatimaye Serikali Mkoani Mbeya imeridhia Waathirika wa janga la Moto katika soko hilo kuendelea kubaki katika maeneo yao ya awali na kuagizwa kujenga  vyumba vya kudumu ili kukabilina na majanga ya moto yanapojitokeza.

Akitoa maelekezo ya serikali,Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewaagiza watendaji wa halmashauri kupiga kambi katika eneo la soko la Sido haraka kuanzia siku ya kesho kwa ajili ya kubuni michoro na mpangilio wa soko hilo ili wafanyabiashara waanze ujenzi na hatimae kuendelea na biashara zaoa kama kawaida.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Mbeya Mjini,Mkoa ikiwa ni pamoja na mbunge wa Jimbo  Mbeya Mjini Mh.Joseph Mbilinyi pamoja na Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson ambaye ametoa msaada wa shilingi milioni 10 kwa wathirika hao.Aidha baada ya kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha ,Mkutano huo ukaridhiwa kuwa fedha hiyo ibaki kwa Mkuu wa Mkoa huku uongozi wa soko ukipanga matumizi ya fedha hiyo.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Makala ameliagiza Jeshi la Zimamoto kuendelea kutoa elimu ya zimamoto,kusambaza vifaa vya kuzuia moto na kuchimba visima vya maji vya ziada katika masoko huku akiwataka viongozi wa ngazi zote za mkoa kuchukua tahadhari za moto kwenye masoko kutokana na ripoti kuonesha chanzo cha janga hilo ni mabaki ya moto uliotokea kwenye moja ya vibanda vya mamalishe waliokuwa ndani ya soko hilo.

 Naibu Spika ,Mhe.Dkt Tulia Ackson akimuonesha jambo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Amos Makalla mara baada ya kufanya mkutano na Wanyabiashara wa Soko la Sido-Mwanjelwa jijini Mbeya mapema leo.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, waandishi wa habari, wanasiasa pamoja na jeshi la polisi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa mbeya Mh.Amos Makalla wakitembelea eneo la soko la Sido lililoteketea Kwa Moto hivi karibuni Jijini Mbeya.


Baadhi ya Wananchi wakiwa sambamba na Wafanyabiashara wa soko la Sido-Mwanjelwa,wakifurahia uamuzi uliotoewa na Serikali ya Mkoa wa Mbeya,kuwa Wafanyabiasha hao wabaki katika soko hilo badala ya kuhamishwa katika soko lingine.

Baadhi ya Wananchi wakiwa sambamba na Wafanyabiashara wa soko la Sido,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Amos Makalla alipokuwa akizungumza nao kwenye mkutano wa pamoja katika kutoa maamuzi ya kuwa Wafanyabiasha hao wabaki katika soko hilo badala ya kuhamishwa katika soko lingine huku utaratibu wa ujenzi ukiendelea kuwekwa sawa.

PICHA ZOTE NA FADHIL ATICK MR.PENGO MBEYA.


MSHINDI WA MZUKA JACKPOT AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA SHILINGI MILIONI 80 JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
 Balozi wa Mchezo wa Bahati Nasibu wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya thamani ya shilingi milioni 80 Mshimdi Mkuu wa Mchezo huo, Rashid Ally katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Regence Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed.
Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Lumuliko Mengele, akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni mama wa mshindi huyo, Fatma Kavila. Katikati ni mshindi, Rashid Ally.
Wapiga picha kutoka vyombo vya habari wakichukua tukio hilo.
Meza kuu. Kutoka kulia ni Maneja Masoko kutoka  Commercial Bank Of Africa (CBA), Solomon Kawiche. Baba wa mshindi huyo, Kamba Kavila, Meneja Masoko wa Kampuni ya The Network Product Tatu Mzuka, Lumuliko Mengele, Rashid Ally na mama yake Fatma Kavila.
Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed, akizungumza katika hafla hiyo ya kumkabidhi mshindi huyo kitita hicho.
 Rashid Ally akizungumza na wanahabari kuhusu ushindi wake.
Maneja Masoko kutoka  Commercial Bank Of Africa (CBA), Solomon Kawiche, akizungumza jinsi watakavyomsaidia mshindi huyo jinsi ya kutumia fedha hizo.
Baba, mama na mwana wakiwa wameshika mfano wa hundi wa kiasi hicho cha fedha alichoshinda mtoto wao.

MSHINDI  Mkuu wa mchezo wa bahati nasibu ya Tatu Mzuka , Rashid Ally, leo amekabidhiwa sh.milinoni 80 alizojishindia katika droo kubwa  iliyochezwa Jumapili.

Rashid ambaye alijishindia kiasi hicho cha fedha katika mchezo huo wa Tatu Mzuka, alionyesha kutoamini, huku akiwa na furaha na shukrani baada ya ushindi huo wa kihistoria. Rashid, ambaye ana umri wa miaka 21 tu, anaishi na familia yake maeneo ya Temeke, Dar es Salaam. 

Akizungumzia ushindi wake, Rashid ambaye amemaliza kidato cha nne hivi  karibuni, alisema kuwa alikuwa anacheza angalau mara 4 hadi 6 kwa wiki kwa kutumia pesa aliyokuwa anaipata katika  shughuli zake za kila siku.
'Ndoto yangu ni kujenga nyumba, na kuwekeza katika kilimo,  kitu ambacho nitafanya kwa kushirikiana na mama pamoja na Baba yangu. Nia yangu ni kuikuza iwe ni biashara kubwa ' alisema Rashid.

Pia alisema ana mpango wa kuendelea kucheza mchezo na kuwa balozi wa Tatu Mzuka, ili kuwasaidia watu kufurahia mchezo huo na kuuamini. 

"Watu wengine ni wagumu kuamini kwamba unaweza kushinda kiwango hiki kikubwa cha fedha kupitia shilingi 500 tu. Ninafurahi kuwa miongoni mwa watu wa kwanza  kuthibitisha hili"

Balozi wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein, alisema Tatu Mzuka ina nia ya kuendelea kutengeneza washindi zaidi wa zawadi ambazo zitabadilisha maisha ya watu na familia zao.

 "Kama Tatu Mzuka, tunafurahi kuona kwamba mchezo huu unabadilisha maisha ya Watanzania. Mbali na kiwango kikubwa cha pesa tunachokitoa katika droo kubwa ya kila Jumapili, tumeishalipa zaidi ya  milioni 350  kama ushindi wa kila siku kwa wachezaji mbalimbali wa mchezo wetu. Kwa wastani mtu mmoja anakuwa mshindi wa Tatu Mzuka kila sekunde 10, masaa 24 kwa siku, na siku 7 kwa wiki "alisema Mussa.

Pia akizungumza katika tukio la kukabidhi ushindi huo, Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed alimpongeza Rashid kwa ushindi huo na akamwomba kuwekeza fedha kwa makini ili abadilishe maisha ya watu wengine. Hemed aliipongeza Kampuni ya The Network Product  Tatu Mzuka kwa kuendesha mchezo kwa uaminifu na kwa haki na kutimiza ahadi yake  kwa umma.

UBALOZI WA KUWAIT WAANZISHA MRADI “KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU”

0
0
Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania umeanzisha mradi uitwao ““KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU” ambapo umezindua kituo cha computer katika Taasisi ya Taaluma za Maendeleo – Chuo Kikuu cha Dar es Salam.
Hafla ya uzinduzi wa kituo hicho ambacho ni cha kwanza  ilihudhuriwa na Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Ester Dugumaro, Mkuu wa Uwekezaji na Mipango wa UDSM Dr. Bujuluru   pamoja na baadhi ya waalimu chuoni hapo.
Katika hotuba yake Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem alisisitiza kuwa Mradi Mpya unaolenga kuanzisha chumba cha Kompyuta katika taasisi za elimu ya juu ni muitikio wa wito uliotolewa na viongozi mbali mbali nchini  kuhusiana na kuweka mkazo katika kuinua elimu na kuunga mkono juhudi za Raisi John Magufuli aliyetangaza kutoa elimu bure kwa wananchi wote.
Balozi Al-Najem aliongeza kuwa mradi huu un
a lengo la kuanzisha idadi kubwa zaidi ya vituo vya Kompyuta katika vyuo mbalimbali nchini kote kwa kushirikiana na Asasi na Jumuiya za misaada za Kuwait na Tanzania, na hii ni kutokana na umuhimu  wa elimu kwa njia ya mtandao, Al-Najem aliongeza kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma kitakua ndio kituo cha pili kufaidika na mradi huuu mkubwa, kikifuatiwa na  chuo kikuu cha Zanzibar (SUZA).
Kwa upande wake Profesa Ester Dugumaro alitoa shukurani za dhati kwa Nchi ya kuwait kwa niaba ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa misaada mbali mbali inayotolewa kwa Tanzania katika sekta ya elimu, huku akielezea matumaini yake ya kutiwa saini kwa makubaliano ya kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kuwait  na vyuo vyengine nchini humo katika nyanja zote.
Bi. Dogomaro aliongeza kuwa wanafunzi wa Uzamili na Uzamifu ndio watakaofaidika zaidi na kituo cha kompyuta kilichoanzishwa na Ubalozi wa Kuwait   ambapo wataweza kutumia mitandao kutafuta taarifa na maelezo kwa madhumuni ya utafiti.
Yafaa kuweka wazi kuwa Ubalozi wa Kuwaiti hapa Tanzania umeanzisha miradi mbalimbali  katika kipindi cha hivi karibuni kama “Kisima cha Maji kwa Kila Shule” na “Maabara ya sayansi kwa kila shule” yenye lngo la kuisaidia Tanzania katika sekta ya elimu.   
 Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem kwakushirikiana na  Mkuu wa taasisi ya taaluma ya maendeleo Profesa  Esta  Dugumaro, Mkuu wa Mipango Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Pancras Bujuw  wakikata utepe kuashiria  umezindua wa  kituo cha computer katika Taasisi ya Taaluma za Maendeleo  Chuo Kikuu cha Dar es Salam.
 Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem   (alieekaa)   akifafanua jambo mara baada ya uzinduzi huo.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

MTANANGE WA YANGA NA SIMBA NGOMA BADO NGUMU MPAKA SASA

0
0
Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima akiwania mpira wa mshambuliaji wa Yanga Donald ngoma katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Ngao ya Jamii unaoendelea hivi Uwanja wa Taifa.
Kiungo wa Yanga Rafael Daud akimruka beki wa Simba Method Mwanjali katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Ngao ya Jamii unaoendelea hivi sasa Uwanja wa Taifa
Beki wa kati wa Yanga Kelvin Yondani na mshabuliaji wa Simba Laudit Mavugo wakigombania mpira katika mchezo wa ufunguzi wa ligi wa Ngao ya Jamii unaoendelea hivi sasa Uwanja wa Taifa.
Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma akimruka beki wa Simba Method Mwanjali katika mchezo wa ufunguzi wa ligi wa Ngao ya Jamii unaoendelea sasa hivi Uwanja wa Taifa
Golikipa Rostand Youthe akiruka juu na  kudaka mpira akiwa sambamba na mshabuliaji wa Simba Emanuel Okwi.
Kiungo wa Simba Haruna Niyonzima akipiga pigo la adhabu nje ya kumi na nane
Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma akipambana na beki wa kati wa Simba Salim Mbonde katika mchezo wa ufunguzi wa ligi Ngao ya Jamii.
Mashabiki wa timu ya Simba
Mashabiki wa timu ya Yanga
Kikosi cha timu ya Simba
Kikosi cha timu ya Yanga

SIMIYU KUFANYA MAPINDUZI YA KILIMO KUPITIA UMWAGILIAJI

0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu.

Mkoa wa Simiyu umejipanga kufanya mapinduzi ya Kilimo kupitia skimu kubwa ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni, kwa lengo la kuwainua wananchi Kiuchumi na kukabiliana na upungufu wa chakula.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika kikao kilichofanyika kati ya Viongozi na Wataalam ngazi ya Mkoa,Wilaya na wananchi wa vijiji vya Kata ya Mwamanyili Wilayani Busega kujadili juu ya mipango ya utekelezaji wa skimu hiyo.

Amesema katika Skimu hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Busega itaingia mkataba na kukopa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) ambayo tayari imekubali kutoa mkopo huo, ili kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya maji kutoka Ziwa Victoria kwenda kwenye mashamba, kuwawezesha wananchi kununua mbegu bora, mbolea, na zana bora za kilimo.

Aidha, ameeleza kuwa wananchi katika skimu hiyo watazalisha mpunga kwa misimu miwili kwa mwaka na kupanda mazao mengine mbadala hususani ya jamii ya mikunde mara baada ya kuvuna mpunga, kwa ajili ya kurutubisha Ardhi.

Mtaka amefafanua kuwa Uongozi wa Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi wenye mashamba katika Skimu ya Umwagiliaji ya Mwamanyili watakaa kupanga namna bora ya urejeshaji wa mkopo huo, ambapo amewataka wananchi kuwa waaminifu kutekeleza utaratibu watakaokubaliana.

Ameongeza kuwa kutokana na uwepo wa Maji ya Uhakika ya Ziwa Victoria mkoa umekusudia kufanya mapinduzi katika Sekta ya Kilimo na kujenga jamii ya watu wanaoishi kijasiriamali ili waweze kulima kisasa na kibiashara na  kuongeza tija katika uzalishaji.

“Tungehitaji tufanye mapinduzi ya Kilimo ili hata siku Mhe.Rais atakapofanya ziara ya kikazi, anakuja kuliona shamba la ekari 2050 za wale walioitwa maskini; tunataka Wilaya ya Busega iwe ya mfano hapa Tanzania ambayo wananchi wake wanalima bila kutegemea mvua” amesema Mtaka.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mwamanyili Mhe.Charles Luhenze ametoa wito kwa wananchi wa kata hiyo kuchangamkia fursa hiyo na kuwataka kutoa ushirikiano kwa watalaam wanaoendelea na kazi mbalimbali za kitaalam katika eneo la Skimu hiyo kila watakapohitajika.

Naye Malibe Misalaba Sitta mkazi Kijiji cha Nasa Ginnery kata ya Mwamanyili amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka kwa juhudi alizozionesha katika kuhakikisha wananchi wa wilaya ya Busega wanafanya Kilimo cha Umwagiliaji, hivyo akaomba mipango iliyobaki ikamilike haraka ili Skimu hiyo ianze kutekelezwa mara moja
Paulo Buchenja mkazi wa Kijiji cha Mwanangi kata ya Mwamanyili amesema vijana wengi wamehamasika kulima kilimo cha Umwagiliaji wakiamini kuwa kupitia skimu hiyo watalima kisasa ambapo wataongeza uzalishaji hali itakayopelekea kujikomboa kiuchumi.  

Skimu ya Umwagiliaji Mwamanyili Busega itatekelezwa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 2050, wananchi watalima kisasa(kitaalam) na kibiashara ambapo mavuno yanatarajiwa kuanzia magunia 30 hadi 40 kwa ekari.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya Skimu ya Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
 Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera  akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya Skimu ya  Umwagiliaji inaotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Busega Tano Mwera wakifurahia jambo kabla ya kuanza kikao na wananchi wa Kata ya Mwamanyili kujadiliana juu ya  Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
 Diwani wa Kata ya Mwamanyili Mhe. Charles Luhenze akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya Skimu ya Umwagiliaji inaotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwamanyili wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao cha kujadiliana juu ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
 Ndg.Shadrack Yohana Mkazi wa Kijiji cha Nasa Ginnery Kata ya Mwamanyili,akichangia jambo katika kikao cha Viongozi wa Mkoa, Wilaya ya Busega na wananchi kilichofanyika katika Kijiji cha Mwamanyili,  kwa lengo la kujadili juu ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
  Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwamanyili wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika kikao cha kujadiliana juu ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya maandalizi ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.

TTCL YAPEWA CHANGAMOTO KUFIKA VIJIJINI

0
0
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Mhandisi Edwin Ngonyani, ameitaka Kampuni ya Simu Tanzania TTCL kuongeza juhudi za kutoa huduma kwa Wananchi hasa waliopo katika maeneo ya Vijijini ili kuwawezesha Wananchi kupata Mawasiliano ya uhakika kutoka katika Kampuni yao Umma.

Mhe Ngonyani ametoa maelekezo hayo alipofanya ziara fupi ya kutembelea Makao Makuu ya TTCL ambapo amepata fursa ya kuzungumza na Bodi na Menejimenti ya TTCL ambapo alitumia hadhatra hiyo kutoa mrejesho wa ziara yake ya kutembelea maeneo mbali mbali ya Tanzania Bara na Visiwani kukagua huduma za Taasisi zilizo chini ya Wizara yake.

Mhe Ngonyani amesema, pamoja na mafanikio makubwa ambayo TTCL imeyapata katika Viwango vya ubora wa huduma, kuongeza idadi ya Wateja, usimamizi na uendeshaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) na Kituo cha Kutunzia Kumbukumbu za Kimtandao( NIDC) bado TTCL inakabiliwa na changamoto kubwa ya kufikisha huduma ya Mawasiliano Vijini hasa katika maeneo ambayo kwa sasa hayana Mawasiliano kabisa baada ya kuzimwa mwa mitambo ya Mawasiliano iliyokuwa ikitumia teknolojia ya CDMA.

Aidha, Mhe Ngonyani ameiagiza Bodi na Menejimenti ya TTCL kuongeza kasi ya kusambaza huduma za TTCL 4G pamoja na kufanyia kazi kilio cha muda mrefu cha Watumishi wa TTCL kuomba kuboreshewa Maslahi yao.

“Pote nilipopita Bara na Visiwani, Watumishi wa TTCL wameniomba nifikishe kilio chao kwenu, wamekaa kipindi kirefu sana bila kuboreshewa maslahi yao huku gharama za maisha zikiwa juu. Ninashauri msikie kilio hiki ili pamoja na kuboresha huduma zenu, mazingira ya kazi na maslahi ya Watumishi pia yapewe kipaumbele,”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mhe Mhandisi Omari Rashid Nundu amesema, Bodi na Menejimenti ya TTCL zimepokea maelekezo ya Mhe Naibu Waziri na kwamba mpango mkakati wa muda mfupi uliowekwa na Kampuni hiyo, changamoto hizo zitafanyiwa kazi.

“Mhe Naibu Waziri, tunayo nia ya dhati ya kuibadilisha TTCL na kuifanya iwe kweli Kampuni ya Umma inayowaunganisha Watanzania. Tumedhamiria kuwafikia Wananchi wote kwa huduma za kiwango cha juu na unafuu sana wa gharama sambamba na kuimarisha vitendea kazi na maslahi ya Watumishi. Tunaomba Serikali iendelee kutuunga mkono na kutuwezesha kutimiza mipango hii,” amesema Mhandisi Nundu.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Waziri Kindamba amesema, TTCL mpya imejipanga kikamilifu kujiendesha kibishara na kufikia lengo la kutoa gawio Serikalini. Bw Kindamba ameongeza kuwa, TTCL kupitia kauli mbiu yake ya Rudi Nyumbani imekusudia kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata huduma za Mawasiliano kwa Teknolojia za 2G/3G na 4G LTE sambamba na huduma za kifedha za TTCL PESA ambayo imezinduliwa hivi karibuni.

Mapema mwezi ulipita, TTCL ilizindua huduma za kifedha kwa njia ya Mtandao ijulikanayo kama TTCL PESA. TTCL PESA itawawezesha Wananchi kupata huduma mbali mbali kama Kutuma Fedha, Kulipia Ankara za huduma kama vile Maji, Umeme (LUKU), Ving’amuzi na Kununua vifurushi vya TTCL huku huduma nyingine zikiendelea kuongezwa.

Aidha,TTCL PESA itasaidia katika kufanya makusanyo ya tozo za Serikali pamoja na kuongeza usalama na kupunguza hatari ya kupotea kwa fedha kupitia vitendo vya uhalifu kama ujambazi wanavyofanyiwa Wananchi (Wakulima na Wafugaji) wanaotembea na fedha nyingi katika maeneo mbali mbali wanapofanya biashara zao za mazao na mifugo.


Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Waziri Kindamba (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) mara baada ya kuwasili katika ofisi yake kusaini kitabu cha wageni.
Sehemu ya menejimenti ya kampuni ya TTCL ikiwa katika kikao hicho na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Mhandisi Edwin Ngonyani alipowatembelea.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) leo Makao Makuu ya kampuni hiyo alipotembelea na kuzungumza na Bodi hiyo katika ziara yake ya kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omar Nundu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mhandisi Omar Nundu (kushoto) akitoa maelezo mafupi kuhusiana na utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) alipotembelea na kuzungumza na Bodi ya TTCL leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw Waziri Waziri Kindamba akiwa katika kikao hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mhandisi Omar Nundu (kushoto) akitoa maelezo mafupi kuhusiana na utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) alipotembelea na kuzungumza na Bodi ya TTCL leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam.

Viewing all 46206 articles
Browse latest View live


Latest Images